Simulizi : Karibu Kuzimu
Sehemu Ya Nne (4)
Pilipili ikaniwasha mno usiku kucha. Mwili wangu ukawa na mikwaruzo kutokana na kujikuna kwa makucha maeneo ninayowashwa. Asubuhi ilipowasili japo muwasho umeacha lakini mikwaruzo ikajenga kwenye mwili kama mgonjwa wa lenge lenge, nikaona aibu kutoka nje nikajifungia chumbani tu mpaka wakati wa Mama Chodo alipokuja kunigongea twende kazini. Ndipo nikanyanyuka kitandani nikafungua mlango kisha nikamsalimu, lakini Mama Chodo hakujibu salamu baada ya kuona mikwaruzo mwilini mwangu. Akashtuka akaduwaa kwa kunitazama mwili, haraka akauliza.
“Nini tena hichi?,” Mama Chodo aliuliza huku macho kodo yakiendelea kunitazama kana kwamba kaona kitu cha ajabu machoni mwake.
“Mbu walikuwa wengi jana, waliniuma wakapelekea nijikune mpaka nikatoka mikwaruzo,” Nikaongopa.
“Sasa, kwanini ukuweka Chandarua?.”
“Nilipitiwa.”
“Acha uzembe Prisca.... Kuna ugonjwa wa Malaria uenezwao na Mbu aina ya Anofelesi. Ni hatari.”
“Ni leo tu mama, naamini haitojirudia tena.”
“Sawa.... Unaenda leo kazini?” aliuliza Mama Chodo huku akiwa kashika ndoo ya uwani, ili akaoge.
“Naenda,” Nikajibu kwa shauku ya kwenda kazini nikavishike viporoli.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi naona, usiende,” Mama Chodo akanizuia. Hakaikatisha shauku yangu yote ya kwenda mgahawani.
“Kwanini?,” Nikadadisi.
“Ukienda na hali hii, utastaajabisha wateja. Bora ubaki uende kesho,” Mama Chodo alieleza huku akishika bega langu, kwa ajili ya kunifariji.
“Sawa mama.... Ehe, Chodo kashakwenda shule?.”
“Itakuwa kashaenda, namjua mdogo wako. Kipindi cha mitihani anawahi mno.”
“Mh, basi ni sawa.”
“Haya. Acha nikaoge niondoke, nishachelewa,” Mama Chodo aliongea huku akitembea kuelekea bafuni kubafu mwili. Akaoga akarudi chumbani, akajiandaa mwishowe akaondoka kufungua mgahawa.
Nikabaki mwenyewe, nikafanya usafi wa ndani. Hatimaye nikatoa nguo chafu zote nje nifue, nikafua nikaanika baada ya kumaliza. Nikajipikia chai, kisha nikanywea na chapati nilizonunua mtaani. Nilipomaliza nikaosha vyombo nilivyonywea chai, baada ya kazi nikaenda kujilaza chumbani kwenye kitandani. Usingizi ukanizoa bila kutarajia, moja kwa moja nikazama kwenye njozi. Nikaota nipo kati kati ya msitu huku nimetapakaa damu kwenye vazi mpaka mwili, sababu yakutapakaa damu. Kando yangu punde tu yalitokea mauaji ya kinyama, mauaji ya mama mjamzito aliyepasuliwa tumbo kwa Shoka baada ya kufanywa kinyume na maumbile. Na vijana watatu, nikashtuka njozini huku nikiwa mtu wa wasi wasi. Utazani ilikuwa kweli, mapigo ya moyo yakaenda kasi. Nikakaa kitako kitandani nikafikiria njozi ile, lakini sikupata hitimisho. Nikataka kunyanyuka nitoke nje ghafla nikashtuka nilipoona damu kwenye shuka nililotandika kitandani, nikajisemeza.
“Ni nini kimetokea?. Damu hii imetoka wapi?, mbona hakuna nilipo na jeraha?,” Nikajiuliza lakini sikujipatia majibu, nikapuuza nikajua ni Chodo karudi. Ameanza hila.
Basi nikanyanyua mguu wa kushoto ili nitelemke kitandani. Mama! maumivu niliyoyapata sehemu ya siri ni makali mno, nikataharuki upesi nikapeleka mkono sehemu nyeti. Mara nikashtuka kukuta sijavaa kufuri angali wakati nalala nilivaa, hofu ikanikamata tu pale niliposhika sehemu nyeti na kukuta damu zikiendelea kuvujaa taratibu. Akili sasa ikafikiri na ikajua kama tayari nishatolewa bikra, na mtu nisiyemtambua. Nikaumia sana, sijaumia sababu ya maumivu. Bali nimeumia sababu nimetolewa usichana wangu bila idhini yangu, nitafanyaje sasa. Na maji yakimwagika hayazoleki ikabidi nikubali matokeo, nikajisafisha mwisho nikabadili nguo. Kisha nikatoka chumbani huku nikichechemea, nikaelekea kukaa sebuleni huku nikiugulia maumivu. Kufika sebuleni nilipokaa tu nywele zote zikasisimka baada ya kumuona jini Suleiman kalala sebuleni katika kiti kirefu, na ukiangalia mlango wa kuingilia ndani nimefunga. Sikuelewa Suleiman kapitaje hadi kuingia ndani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wewe,” Nikamuamsha jini Suleiman kwa ghadhabu huku nikimtingisha bega apate kunisikia upesi amke. Jini Suleiman akaamka akakaa kitako kitini kisha akaniangalia kwa jicho la kusinzia, akanitathimini. Kabla ajamaliza kunitathimini nikamtandika swali kwa ukali huku kwa mbali nikiwa na kauwoga.
“Suleiman umepita wapi?.... Na wewe ndiye uliyenifanyia upuuzi, si ndiyo?,” Suleiman hakujibu maswali, bali nae akauliza kwa hisia.
“Kuongea kwa ukali ni suluhisho.... Wewe kwasasa kaa chini tuzungumze. Au ujapenda ulivyonikuta hapa?,” Jini Suleiman aliuliza huku akijaribu kunitoa hofu kwa kunipalaza kichwani mara baada ya kuhama alipokuwa amekaa na kuja kukaa nilipokuwa nimekaa. Punde jini Suleiman nikaona amenyamaza kuongea anachezea ndevu zake zilizo ndefu ka waarabu wa Oman, kisha akameza mate akaendelea na mazungumzo.
“Inaelekea una hofu nami, acha nikutoe hofu. Usiogope, mie ni mtu mzuri tu kwako.... Pengine unajiuliza. Kwanini nakufuatilia?,” Jini Suleiman aliuliza mara baada ya kuona sikumjibu mwanzo.
“Sijajua,” Nikajibu huku nikimkata jicho la kuibia Suleiman.
“Acha niweke wazi hili, nakufuatilia sababu. Nimekupenda.”
“Unanipenda?.... Basi wewe, ndiye uliyenitoa usichana wangu. Si ndiyo?.”
“Naam, mimi ndiye.”
“Shiiiit. Na wewe ni kiumbe wa aina gani...maana nimefunga mlango lakini umeweza kuingia ndani, niambie. Umewezaje kuingia? na. Kwa nini unitoe usichana bila ya idhini?.”
“Kumbuka, awali nilishakuambia kuwa. Mimi nina uwezo mkubwa kushinda kiumbe yeyote duniani, hata wewe nilijua unaitwa Prisca.... Prisca, upendo wangu kwako ndiyo unaonifanya nikiuke sheria. Halafu viumbe kama sisi, tukimpenda mtu wasaa wowote tunapojisikia tunamuingilia.”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa basi nyie ni wa binafsi.... Halafu swali langu unajibu kwa mafumbo. Nilikuuliza, wewe ni kiumbe wa aina gani?. Niambie nikujue,” Jini Suleiman alicheka kidogo mara baada ya kuuliza swali lile kwa mara nyengine. Hakujibu papo kwa hapo bali, akaendeleza mafumbo ya kutafakari bila ya ufafanuzi sahihi. Akaacha kucheka, akatulia kidogo akinitazama kisha akauliza huku akitabasamu.
“Prisca, bado tu ujajua sirika langu?.”
“Sijajua.... Sirika lako ni lipi?, ni mchawi au?,” Nikauliza mfululizo huku kwa kuropoka bila kufikiri.
“Wewe unaona. Mimi ni nani?.”
“Naona ni kiumbe, wa ajabu,” Jini Suleiman alifurahi mno mara baada ya kusikia jibu langu lenye kubeba uhalisia kidogo.
**********
Jini Sulesh alipomaliza maongezi na nduguye akaelekea majini, akiwa yupo njiani kabla hajafika majini mkono wake ukaonekana kutingishika “vibrate”. Kwa maana simu inaita akanyanyua mkono akaangalia akagundua kama ni nani aliyepigia simu, akapokea.
“Eehe. Baba, kwema?” aliuliza jini Sulesh huku akisindikiza uchangamfu mara baada ya kusikia sauti ya mkwe wake Mzee Mahonge.
“Kwema tu,” Mzee Mahonge akajibu.
“Naona umenikumbuka kulikoni, mwenzangu kasharudi nini,” Jini Sulesh akaongea.
“Hajarudi...ila nimekupigia ili nikuombe umtafute mwenzako katika jiji hilo la Dar es salaam. Maana dada yake katuhabarisha kuwa kashampatia nauli arudi, lakini kagoma kurudi,” Mzee Mahonge alitoa agizo, akanyamaza kidogo punde akasikika akibanja kikohozi kizito.
“Sawa baba, nitamtafuta japo nahofia kuwa Dar es salaam ni jiji kubwa. Sidhani kama nitamuona kwa urahisi” aliongea jini Sulesh kana kwamba anakata tamaa kunitafuta.
“Mungu atakuwa pamoja nawe. Utamuona tu.... Muhimu ni wewe kuwa na juhudi ya kumtafuta.”
“Nitashukuru...basi ngoja nianze kumtafuta kitakachojiri nitakujulisha.”
“Sawa. Nakutegemea,” Mzee Mahonge alikata simu mara baada ya kumaliza maongezi na Sulesh.
Jini Sulesh akatoa mkono sikioni, akashusha mkono chini kisha akaendelea na safari ya kuzama majini. Alifika majini akakuta baadhi ya majini wapo vikundi huku huzuni ikiwajaa katika nyuso zao, sura za huzuni alizokutana nazo Sulesh zikamshangaza pole pole akajikongoja kufuata kundi moja aulize. Baada ya kufika katika kundi alilohitaji kuuliza akamchomoa binti mmoja aitwaye Zusia akamuulizia kwa pembeni.
“Zusia, kimetokea nini?.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Msiba umetukumba,” Zusia ambaye ni jini mlimbwende katika tawala yao akajibu.
“Aliyekufa ni, nani?,” Jini Sulesh akadadisi.
“Mzee Chandu. Ndiye aliyekufa.”
“Yule mzee, mwenye mkia wa farasi unaong'aa?.”
“Eeehe.”
“Alikuwa anaugua?.”
“Hapana, leo Mzee Chandu alitumwa na mfalme aende kwa majini wafu. Akasuluhishe mtafaruku tuliokuwa nao, baina yetu na wao. Lakini alipofika huko majini wafu hawakutaka suluhisho, wakahamua kumuua na maiti yake wakatupa kwenye fukwe ya bahari,” Zusia alieleza kwa mapana. Ili Sulesh apate kufahamu kifo cha Mzee Chandu kilivyokuwa.
“Aisee...taratibu za mazishi, vipi. Zishapangwa?,” Jini Sulesh akauliza huku katika uso wake akionyesha kuhuzunika kwa ajili ya kifo kilichomkuta mzee wao wa busara.
“Ndiyo.... Atazikwa usiku eneo la Giza, kule kwenye masinagogi,” Zusia akajibu.
“Nashukuru kufahamu, sasa ngoja nikuache nikapumzike kidogo baadae tutaonana. Huko Giza,” Jini Sulesh aliaga kisha akaelekea kwanza, kwenye kumbi ya kifalme kusalimu kabla ajaelekea kwenye pango kupumzika.
Kufika akawakuta wazazi wakibadilishana mawazo, akasalimu kwa haraka kisha akataka kuondoka. Lakini kabla hajafika mbali akazuiwa na baba yake, baada ya kuzuiwa mara mama yake akauliza swali huku taratibu akipata bilauri ya damu ya mnyama.
“Suleiman. Yupo wapi?.”
“Karejea, katika ulimwengu wa binadamu,” Sulesh akajibu.
“Kufanyaje?,” Binti Surya akazidi kuuliza.
“Kukamilisha, jambo lake.”
“Taarifa ya kifo cha Mzee Chandu, mmekisikia?” aliuliza Binti Surya huku akitupia fundo la damu taratibu kinywani.
“Mie taarifa ninazo, lakini Suleiman. Yeye hana.”
“Basi kama hana, naomba mtaarifu. Leo arudi mapema ili ahudhurie mazishi.”
“Sawa mama, nitamtaarifu,” Jini Sulesh alikubali. Hatimaye akaongoza moja kwa moja pangoni, kabla hajapumzika akampigia Suleiman simu ili amjulishe kilichotokea majini.
**********
Jini Suleiman kabla hajanijibu, akaniacha njia panda baada ya kupigiwa simu na nduguye. Nikabaki nimebutwaa tu pale sebuleni nikimtafakari Suleiman kuwa ni kiumbe wa aina gani, wakati nikiwa natafakari huku nimejiinamia kichwa mara nikasikia mlango ukibishwa hodi kwa ghadhabu. Nikakurupuka upesi nikanyanyuka kwenye kiti nikawahi kufungua mlango ili nijue aliyegonga mlango vile ni nani, kufungua mlango tu nikaandamwa na maswali lukuki yaliyoulizwa na Chodo ambaye ndiye aliyegonga mlango ule kwa ghadhabu.
“Muda wote, ulikuwa wapi?. Ulikuwa ndani, na mwanaume?.”
“Nauliza, ulikuwa ndani na. Mwanaume?. Nijibu, kama kweli ulikuwa ndani na mwanaume. Nikupe heko zako...nakosea?.”
“Unanikosea heshima Chodo, mdogo wangu.... Sikuwa ndani na mwanaume,” Nikajibu.
“Wee, usithubutu. Mdogo wako nani?, unaweza kuwa na mdogo ka mie.... Halafu ungejua kama nakuchukia usingethubutu kuniita mdogo wako. Kwanza unanitia kichefu chefu tu, hebu...nitokee,” Chodo aliongea kwa kejeli ya kubana pua kisha akanisukuma nitoke mlangoni apate nafasi ya kuingia ndani.
Sababu nilishajua Chodo ananichukia sikujisumbua kuongea nae nikakamata hamsini zangu nikaelekea chumbani, huku nikamuacha Chodo nae akiingia chumbani kwake kwa ajili ya kujibadili vazi kabla ya kula. Akajibadili mwishowe akatoka chumbani akarudi sebuleni kula chakula nilichoandaa, bado nikiwa chumbani nikakumbuka kutoa lile shuka ambalo lililochafuka kwa damu. Nikalikunja nikatoka nalo nje kulifua kabla ya Chodo na Mama Chodo kuliona, ikasababisha waniulize maswali ambayo http://deusdeditmahunda.blogspot.com/yangepatikana majibu ya kustaajabisha ufahamu. Nikalichukuchua na kulianika lile shuka mwisho nikarudi ndani baada ya kumaliza kudobi, ndani nikakuta Chodo kashamaliza kula kashatoa vyombo mezani sasa anasoma kitabu cha Riwaya kinachoitwa TAKADINI. Sikumbuguzi mie nilitulia nikiangalia tamthilia ya kihindi ya WAARIS kwenye runinga, katika kipindi cha Star Swahili. Nikaangalia tamthilia ile huku nikifurahi panapo na furaha na huku nikihuzunika panapo na huzuni, kifupi tamthilia ile niliipenda na nikaifuatilia kuanzia mwanzo mpaka hapo nilipofikia kipande cha kumi. Kweli sikutaka inipite hata kipande kimoja lakini! kwa hila za Chodo baadhi ya vipande vilinipita, nakumbuka. Vilinipita sababu Chodo alisema nizime runinga, nampigia kelele. Yeye anasoma, lakini huo ni uwongo tu. Eti, nampigia kelele wakati hata sauti sikupandisha juu ni ya wastani tu niliweka. Chuki zidi yangu ndiyo ikamtuma aniamuru vile, aliona kama nafaidi kumbe hakuna ninacho faidi chochote zaidi ya kufarijika tu. Basi nikazima runinga kama alivyotaka, na halafu si unajua mtu kwao. Kama ni kwao fuata taratibu, mimi nikafuata taratibu. Nikaachana na Chodo nikaingia chumbani kujilaza nikalala nusu saa kuja kuamka, kwa mbali nikamsikia Mama Chodo akiongea na mwanae sebuleni. Wazi nikajua Mama Chodo kasharudi kazini, ikabidi ninyanyuke kitandani nielekee sebuleni kwa ajili ya kumsalimu Mama Chodo. Kufika sebuleni nikasalimiana na Mama Chodo baada ya salamu nikatenga chakula alichorudi nacho kutoka mgahawani, tukala. Tulipomaliza kula kila mmoja akanyanyuka kwenye kiti akaelekea chumbani kulala, upande wangu usingizi ulikuwa ni mtamu sijapata ona. Kwanini?. Sababu nilikuwa naota ndoto tamu za mahaba, kwa kweli ulikuwa ni usiku mzuri kwangu kushinda usiku mingine. Nililala haswaa mpaka asubuhi ilipofika sina habari, na hata Chodo alivyoondoka shule sina habari. Habari ikanijia pale niliposikia jogoo akiwika jirani na dirisha langu, kukiwa kumepambazuka tayari. Haraka nikatoka chumbani ili nikamuamshe Mama Chodo nikijua bado hajaamka, lakini nilipotoka chumbani nikashangaa kumkuta Mama Chodo sebuleni akimalizia kujiandaa ili aende kufungua mgahawa. Mikwaruzo sababu imepungua upesi nami nikajiandaa ili niongozane na Mama Chodo, nikaongozana na Mama Chodo baada ya kujiandaa. Tulipofika kwenye mgahawa tukagawana kazi kama siku zote, tukafanya kazi kwa pamoja hadi usiku ulipowadia. Tukafunga mgahawa baada ya kumaliza kuuza chakula, na kwa kuwa chakula kiliisha chote ikabidi chakula chetu sisi tukapike nyumbani. Hivyo tukapita Luhanga kituoni kununua Samaki wa mafungu ili tukapike ugali nyumbani, baada ya kununua Samaki tukarudi nyumbani huku tukiwa tumechoka hoi. Kufika nyumbani tukamkuta Chodo kalala sebuleni kwenye kiti huku mlango wa sebuleni kaacha wazi, mlango ulipoachwa wazi Mama Chodo hakupenda basi ikamlazimu abwatuke kwa kosa ambalo ametenda mwanae. Ambaye mwanae huyo muda wote alikuwa amelala asijue kinachoendelea katika sayari.
“Una akili kweli?,” Mama Chodo aliuliza kwa kubwata mara baada ya kumuamsha na kumkalisha kitako mwanae.
“Kwanini?,” Chodo alijibu kana kwamba ajui mama'ake anachoongelea. Akajifikicha macho kwa ajili ya kuondoa usingizi apate kuelewa anachomaanisha mama'ake.
“Unaweza nipatia sababu ya kuacha mlango wazi?. Na sababu ya kulala sebuleni mbu wakutafune?,” Mama Chodo akang'aka.
“Aisee!!!, nisamehe mama.... Nilipitiwa tu na usingizi” alijibu Chodo kwa upole. Kufuata tamaduni za Afrika ya mtoto kumheshimu mzazi.
“Haya. Ila usirudie maana mtindo huu unakaribisha vibaka, na wewe mwenyewe utapatwa na Maralia sugu.”
“Sitothubutu kurudia, ujinga huu. Mama.”
“Sawa...ngoja niingie jikoni niandae chakula, tule. Kisha tukapumzishe miili kwa ajili ya kuondoa uchovu” aliongea Mama Chodo kisha akaelekea jikoni kupika ugali.
Dakika kadhaa ugali ukawa ushaivishwa, ukatengwa ukalika kisha wote tukaingia chumbani kulala. Tangu jini Suleiman anitoe usichana, usingizi wangu ukawa unaambatana na njozi mbalimbali. Hata usiku huo njozi ilifikia hatamu, nikaota nipo ziwani tukivua Samaki na Suleiman katika kuvua Samaki mara nikasikia kwa mbali nikiitwa. Nikajivika ujasiri nikaitika, ile kuitika tu ghafla nikashangaa kuona jini Suleiman akicheka huku akinirushia viulizo.
“Unaitika nini?.... Unajua maana ya kuitika sauti hiyo?.”
“Sijui,” Nikajibu huku nikionyesha kuwa jasiri kidogo.
“Ngoja ujue sasa. Kuitika sauti hiyo maana yake ni umekubali kukaribishwa katika jamii yetu na umekubali kufunga ndoa,” Jini Suleiman alieleza huku bila wasi wasi akishika maungo yangu.
Ghafla nikakurupuka kwenye njozi, nikaja kuangalia dirishani nikakuta kushapambazuka haraka nikajiandaa. Upesi nikaenda kumuamsha Mama Chodo nae ajiandae, Mama Chodo alipoamka nae akaelekea kumuamsha mwanae ili amke ajiandae. Baada ya wote kujiandaa tukaongozana, tukaja kuachana na Chodo njiani. Yeye kama siku zote akaelekea shule, kisha mimi na Mama Chodo tukaelekea mgahawani kwa ajili ya kutekeleza wajibu wetu wa kila siku.
**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jini Suleiman aliwasili majini akaungana na sirika lake kwa ajili ya maziko. Wakamzika Mzee Chandu, na wote wakatawanyika kwenda kujipumzisha. Kesho yake Suleiman na Sulesh wakadamka wakaelekea kwenye jukumu lao, Suleiman akaelekea Kigogo Jaba. Na Sulesh akaelekea Mabibo mwisho hawakuongozana waligawana maeneo, Suleiman akaja kutokea Kigogo Jaba eneo la kanisa la katoliki chini ya mti wa muembe. Akanusa magharibi, mashariki, kaskazini na kusini hatimaye akapotea eneo lile akaja kutokea nje ya mgahawa wetu. Huku akiwa kavalia kanzu ndefu nyekundu, bila kusita akaingia ndani ya mgahawa kama mteja. Wote tuliokuwepo tukamtumbulia macho bila kutambua kuwa tunayemtazama ni kiumbe gani, si mimi, si Mama Chodo na si Wateja ndio waliomtambua jini Suleiman. Wote hatukumtambua, na ukizungumzia mie. Mie namjua jini Suleiman kwa sura na jina tu, lakini ukiniuliza anatokea jamii gani. Kweli sijui cha kukujibu, sababu amekuja katika mgahawa wetu ka wateja wengine. Lazima nimfuate, nikamfuata alipo nikamchangamkia kwa kumhudumia. Nikamhudumia akala akamaliza akalipa pesa kabla hajaondoka akaniita nje ya mgahawa, nikatii wito nikaongoza kumsikiliza. Kufika nikataharuki jini Suleiman kanivuta mkono ghafla akanikumbatia, kumbatio la Suleiman mara likafanya niduwae na kujiona kama nipo peponi. Mwili wake ulijaa joto, marashi yake ni yakuvutia na mavazi yake ni nadhifu sana. Ukweli Suleiman ni kijana mtanashati na anajipenda, kuanzia mwili mpaka mavazi. Yaani kumbatio tu kashanimaliza, kwake sioni wala sisikii.
**********
Jini Sulesh nae baada ya kutokea na kuzunguka Mabibo mwisho kutwa bila mafanikio ya kuniona, akaona bora amtafute nduguye warudi majini. Alikuwa mtaa wa Msikitini kwenye nyumba moja yenye dirisha la kioo “Aluminium”, akakitazama kile kioo punde kwenye kile kioo akamuona kaka yake amenikumbatia. Ghafla akafura nyuso ikawa mfano wa Nyati, upesi akapotea eneo lile akatokea katika mgahawa wetu ambapo nimesimama na Suleiman. Akiwa amevaa mavazi yale yale kuu kuu, bila kufikiri akanyoosha mkono wa kuume punde tu likatokea kombora katika mkono. Kwa hasira akamtwanga nalo Suleiman kichwani, Suleiman ghafla akadondoka chini huku akigala gala akiugulia maumivu. Huruma ikanijia, nikamuonea huruma sana jini Suleiman haraka nikamsogelea alipodondoka. Nikamuinua kichwa chake nikakiweka mapajani mwangu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Binti umenikataa, sababu ya ndugu yangu.... Suleiman. Kwa nini umehamua kunisaliti?,” Bado nikiwa chini na Suleiman, mara nikamsikia Sulesh akinung'unika. Kunung'unika kwake ndipo akanifumbua macho ya kujua kuwa yeye na Suleiman ni ndugu na wao ni majini.
Suleiman swali la mdogo wake hakulijibu akabaki akimtazama tu na kuugulia maumivu. Ukimya ule Sulesh ukamkasirisha, alikasirika zaidi kwa jinsi alivyoona nilivyompakata Suleiman kimahaba. Wivu ukamshika, donge la uchungu likamkereketa kooni. Hakashindwa kujizuia jazba akachukua sheria mkononi, muda huo huo akanyoosha mkono wa kuume likatokea kombora lengine linalowaka waka mwanga mwekundu. Nikaogopa sana, hofu ikachukua nafasi baada ya kuona kombora lile naelekezewa mie. Kweli bwana safari hii kombora lile Sulesh akalituma kwangu, bahati nzuri wakati linakuja Suleiman akaliona upesi akanikinga. Kombora lile likamtwanga yeye na ghafla akapotea nami eneo lile, huku tukamuacha jini Sulesh akiingia mgahawani akiwa kwenye nyuso ya kupaniki baada ya kugundua Suleiman kamsaliti.
“Za. Saa hizi,” Jini Sulesh alitoa salamu kwa Mama Chodo, ambaye kwa wakati ule alikuwa bize na kuhudumia wateja. Mara baada ya kuingia mgahawani.
“Salama...nikusaidie nini. Chakula?,” Mama Chodo aliuliza mara baada ya kuhudumia baadhi ya wateja. Akamsikiliza kwanza Sulesh.
“Sihitaji chakula, nipo hapa kukutaarifu kuwa mimi na Prisca ni ndugu. Na yule kijana aliyetoka na Prisca ni kaka yetu, leo tumekuja kumchukua arudi nyumbani...hivyo basi naomba usimtafute,” Jini Sulesh aliongopa, kisha akamkazia macho Mama Chodo akimtathimini aone kama ataleta utata.
“Prisca, ni ndugu yenu?. Mh, sawa...lakini ningeomba nimuone mara mwisho, maana nimeishi nae vizuri sana kama mwanangu,” Mama Chodo akaomba ombi.
“Mama, haitowezekana. Sababu kaka yetu kashatangulia nae nyumbani,” Jini Sulesh alizidi kuongopa.
Mama Chodo hakupinga akajua kweli Sulesh na Suleiman ni ndugu zangu. Sababu ya yeye awali kunikuta kwenye mazingira ya utata, akakubali. Sulesh akatoka, kufika nje ya mgahawa akapotea nyuma akamuacha Mama Chodo katika mgahawa wake akiendelea kuhudumia wateja. Yeye alitokea majini akiwa mnyonge na mawazo kichwani mwake
Nikatokea na Suleiman kwenye mjengo wa kifahari, unaopatikana Mabibo hostel. Nikashangaa sikuamini wala sikutaraji kuwa katika mandhari ka yale, maana nyumba ilikuwa ni ya mfano. Ilikuwa ni ghorofa moja, ndani kulikuwepo na bustani nzuri ya maua. Sebuleni kulienea thamani tupu, kulikuwa kimya. Kwa maana katika mjengo ule hapaishi watu. Nikavutiwa na pahala pale, nikasahau matatizo yaliyopo duniani. Nikazubaa kabisa katika sofa, nikaja kushtushwa na Suleiman baada ya kunipiga busu shavuni. Sasa ndipo nikazinduka, akili ikarejea kama awali baada tu ya kumbukizi kuja katika mfumo wa ubongo. Hofu ikarejea nikajaribu kumkwepa Suleiman kwa kukaa mbali nae, nikijua saa yoyote atanidhuru.
“Prisca, sasa ushajua sirika langu. Usiogope...nizoee, ili nijiamini nishinde katika vita laumu,” Jini Suleiman alinitoa hofu huku akishika mabega yangu mara baada ya kusogea jirani yangu.
Kigugumizi kilinibana, sikuweza kutia neno nilibaki nikimtazama tu Suleiman nikimdadisi. Haraka akili yangu ikachanganua, ikaniambia kuwa. Suleiman ni jini mwema na ni mwanaume mzuri. Sababu yeye ndiye aliyenitoa bikra na baadhi ya mambo alinisaidia, basi nikamjengea ujasiri. Sikuthubutu kumuogopa, pole pole nikamzoea. Sulesh nilimuogopa na nikamchukia, sikumpenda hata kidogo. Yote sababu ya matendo machafu niliyoyashuhudia kwake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
Jini Sulesh akiwa amejipumzisha pangoni kwa kujilaza chali akiwaza, mara akapitiwa na usingizi akalala. Wasaa mwingiiine akaja kushtuka akamka baada ya kuhisi mguu wake wa kuume ukilambwa, akaangalia katika mguu akaliona Joka lenye upanga kichwani likiendelea kumlamba. Joka lile likalamba mguu mpaka yakatokea maandishi ya kustaajabu, maandishi yenyewe yakasomeka hivi;
“ñèñdá kwêñyê kumbï yå kifâlmë, üñæhîtäjíkà hàrækã ßàñæ,” Jini Sulesh maandishi yale aliyaelewa sana. Maandishi yalikuwa ni ya kijini, yanamueleza aende kwenye kumbi ya kifalme, wazazi wanamhitaji haraka sana. Kumbe hata Joka lile liliagizwa na baba yake.
Upesi Sulesh akapotea pale pangoni akatokea katika kumbi ya kifalme, akawakuta wazazi wote wawili wapo hoi. Wakigalagala huku wakizungukwa na baadhi ya majini wakiwaangalia, haraka Sulesh akawakimbilia wazazi akawainua vichwa vyao akavilaza mapajani. Mwishowe akapitisha macho katika miili ya wazazi labda ataona jeraha lakini hakuona jeraha, akashangazwa. Na moyo ukaumia kuona wazazi wakiteseka bila ya yeye kujua tatizo, akauliza.
“Eti!!, ni nini kimewapata?,” Jini Sulesh aliuliza baadhi ya majini waliokuwepo pahala pale, mara baada ya yeye kutogundua kilichowapata wazazi wake.
“Hatujui. Ila nahisi litakuwa gonjwa lao la kila siku,” Jini mmojawapo mwenye umbile la Majusi, mwenye jinsia ya kiume akajibu lile swali huku usoni akiwa na majonzi.
“Su Su Suleiman, umemuacha wapi?,” Binti Surya aliuliza kwa tabu, sababu ya maumivu makali anayoyapata kooni huku akiwa bado yupo mapajani.
“Yupo katika ulimwengu wa wanadamu, akitanga tanga tu,” Jini Sulesh alijibu huku akionyesha chuki, pindi akikumbuka usaliti aliofanyiwa na nduguye.
“Wanangu, sasa fanyeni haraka. Kamilisheni mambo, sisi wazazi wenu gonjwa hili la kurithi. Muda wowote litatuondoa,” Binti Surya alihasa huku akimkodolea macho mumewe aliyekuwa hoi nae mapajani. Mara akabanja mfululizo ghafla akatema kikohozi cha damu, kisha akaamuru.
“Sulesh, hebu.... Kalete ile dawa ya kututuliza.”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haraka Sulesh akapotea akatokea katika pango la wazazi, akachukua dawa hatimaye akarudi katika kumbi huku mkononi akiwa ameshika kichupa chenye rangi ya dhahabu “Gold” chenye dawa. Akawanywesha wazazi dawa papo hapo wazazi wakapata ahueni, akapotea nao akatokea nao katika pango lao ili wapumzike. Wazazi wakapumzika, yeye akarudi kwenye pango lake. Safari hii hakumkuta lile Joka, akaendelea kuchapa usingizi mpaka majira ya jioni. Ambacho kijua cha jioni kikiambaa ambaa, usiku uliopendeza kwa mwanga wa mbalamwezi, wenye mvua za rasha rasha. Wenye sauti za ndege mbalimbali, usiku ambao si tulivu. Usiku ambao uliopendezeshwa na nyota, usiku huo ni mzuri sana kwa majini kwa ajili ya matembezi. Usiku huo Sulesh hakuhofia akapotea majini akatokea ufukweni kwa ajili ya kupunga upepo, alipofika akajifikicha macho mara akatazama mawinguni. Akafumba macho muda si muda akafumbua, alipofumbua tu akategemea kumuona Suleiman alipo. Alimuona nduguye alipo baada ya kufumbua macho na kuangalia juu mawinguni.
**********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment