Search This Blog

OSAKA MJI ULIO POTEA - 3

 






Simulizi : Osaka Mji Ulio Potea 
Sehemu Ya Tatu (3)




"Osaka?" Alexandra akashtuka kusikia jina hilo, akakumbuka sio mara ya kwanza kulisikia kwa kuwa aliwahi kuota ndoto iliyo husu Osaka.

"Ndio mbona unashtuka kijana? Si unahitaji msaada, basi lazima tusaidiane, nitahitaji pete iliyopo Osaka kisha nikufanyie mpango kabambe wa kuondoka ndani ya Gereza hili kabla ile siku ya kuvishwa kitanzi haijawadia" aliongeza kusema Devis kwa msisitizo.



"Hapana Devis! Unania ya kunipoteza mazima, huo sio msaada ila ni kunitoa sadaka! Kweli kabisa upo tayari kunipeleka Osaka, kwanini juhudi hiyo usifanyike kuirudisha nyumbani"



"Ahahaha hahahah!" alicheka kwa madaha Devis, safari hiyo uso wake ulikuwa mkavu kabisa, alipo katisha cheko lake akasema "Njia ya kufika Osaka ipo tofauti kabisa na ile ya kukuweka huru"



"Unamaanisha nini?" aliuliza Alexandra kwa taharuki kubwa.



"Maana yangu ni kwamba njia ya kurudi nyumbani utahitaji chombo cha usafiri, lakini njia ya kwenda Osaka utahitaji kaburi, nikiwa na maana kuwa kifo ndio njia pekee ya kukanyaga ardhi ya Osaka. Hivyo basi nakupa nafasi ya kutafakari kijana kama kweli utahitaji msaada wangu, fikiria kutumikia kitanzi kwa maana kwamba kunyongwa mpaka kufa, au kwenda Osaka ambapo unakufa kwa siku zinazo hesabika na kisha unarudi kuwa hai na huru pia " alijibu Devis na kisha kuondoka karibu na Alexandra huku akimuacha akiwa amepigwa na butwaa!





"Osaka! Ni wapi huko? Na je, ile ndoto niliyoota wakati ule ilikuwa ina manisha kuwa itakuja kutokea?" Alexandra aliwaza ndani ya akili yake, ndoto ile aliyoota na maneno anayo ambiwa na Devis kwa pamoja vilimchanganya zaidi kuhusu pete anayo takiwa kuifuata huko, moyoni akahisi kuwa itakuwa ni pete ile ambayo alikabidhiwa na Saigon kwenye ulimwengu wa ndoto, pete ambayo ilileta kizaa zaa kilicho pelekea maafa makubwa.



Baada kuwaza kwa muda mrefu, mwishowe akashusha pumzi ndefu na kisha kusogea kwenye chumba mahususi cha kamali. Chumba kikubwa ambacho kilikuwa na ulingo wa ngumi mkubwa ulio wekewa uzio wa nyavu za chuma, ndani palikuwa na watu wakipigana pasipo na hata chembe ya huruma, mmoja tu ndio aliye takiwa kutoka katika ulingo ule. Ulingo wa kifo kama ambavyo ulivyo fahamika, ndondi hizo hutokea pale wanapo jitokeza wafungwa wawili wanao taka kuonyeshana utemi, na kila mmoja alikuwa na wafuasi wake walio mfuata nyuma.



Kupitia mapambano hayo vifo mbali vilizuka, lakini pia waliumizana vibaya sana.

Shangwe za hapa na pale zilizuka katika ulingo huo, vidume vya mbegu vilivyo jazia kimazoezi vilionekana kutunishiana misuri, kila mmoja alionyesha umahiri wa kukwepa ngumi na kushambulia huku kila mmoja akishangiliwa na wapambe wake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alexander alibaki kushangaa tu, alishindwa ashangilie upande gani, ila kwa jinsi vidume hivyo vilivyokuwa vikipigana bila kuoneana huruma, ile roho ya kushangilia ilimtoweka kabisa.

"Hii ni zaidi ya Jehanamu" alijisemea kimoyomoyo sanjari na kung'atuka mahali hapo, lakini kabla hajaondoka akaguswa bega, upesi upesi akageuka nyuma yake akakutana uso kwa uso na Devis, akamtazama kisha akamwambia "Hii nayo ni moja ya njia ya kukikwepa kitanzi, ingia kati kama unao uwezo wa kupigana hata dakika mbili. Ahahahaha" alimaliza kwa kicheko Devis kisha akaondoka zake, alikwenda kuketi sehemu ambayo engepata kuona mpambano vizuri.



Siku zilisogea, kila kukicha heri ya jana kwa kijana Alexandra kwani maisha katika Gereza lile yalizidi kumuwea magumu, ugomvi, chuki na kila aina ya takataka ulikuwemo Diyarbakir vilizidi kumchanganya na kibaya zaidi ni pale alipo sikia neno Osaka, hofu na woga mara dufu ilizidi kumjaaa.

Lakini pindi hayo yalipokuwa yakimtokea, Devis hakushindwa kumjia kwa nyakati tofauti kumuuliza maamuzi yake, amekubali au ameendelea na msimamo wake ule ule wa kukaidi kwenda Osaka. Majibu aliyo kutana nayo Devis yalimshtua kabisa na kuona kuwa kijana amedhamilia kunyongwa.

Ila hakuwa mwepesi kukata tamaa kwani naye alikuwa na nia thabiti ya kuimiliki pete kutoka Osaka, hivyo basi aliendelea kumuuliza na kujaribu kumshawishi ikiwa siku zinavyo zidi kwenda ndivyo siku ya hukumu nayo inavyo zidi kuongea.



Usiku mmoja Alexandra aliota ndoto kuwa mdogo wake wa kiume aliyeitwa Carols amegongwa na gari wakati akivuka barabara kwenda kununua dawa ya kumtibu dada yake aliye shikwa na homa kali, ndoto hiyo tata ilimtoa usingizini Alexandra, alihema haraka haraka. Mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio mithili ya saa mbovu, roho ilimuuma sana hasa baada kufikiria mazingira magumu aliyo waacha wadogo zake ikiwa yeye ndio nguzo kuu. Fikra za papo hapo akaichuja ndoto hiyo, akatafsiri akahisi kuwa nyumbani kwao kuna matatizo.

"Mmh! Hapa ipo namna, acha nikubali kwenda huko, huwenda huyu mzee akanikaniweka huru. Siku zote ndoto huwa imaanisha inawezekana wadogo zangu wanataabika" alijisemea ndani ya nafsi yake Alexandra baada kuitafakari ndoto ile. Na sasa akangojea aonane na Devis ampashe taarifa hiyo ya kukubali kwenda Osaka.

Alipo kutanaye alimueleza kukubali suala hilo, Devis alifurahi sana, alipompongeza kisha akasema "Utakwenda na utarudi, wakati usiku wa leo mafaili ya wafungwa wanao takiwa kunyongwa yanapitiwa, basi na wewe utatakiwa uanze safari ya kwenda Osaka"



"Osaka Osaka, huu ni mji ulio potea miaka mingi sana iliyo pita, fahamu kila baada miaka milioni mia nne, dunia hujisahihisha au naweza kusema inajisafisha. Kabla ya Nuhu na safina, yalitokea mabalaa makubwa kama yale yale kunyesha mvua kwa miaka arobaini na mwisho wa siku kuzuka matetemeko, chemimi kutoboka na bahari kuchafuka ilimladi kuhakikisha dunia inapoteza kila kitu kilicho kwenye uso wa dunia kinatoweka na kisha maisha kuanza upya " aliongeza kusema Devis wakati huo akitembea pole pole na Alexandra kuelekea kwenye chumba maalumu.



Hatimaye walifika katika chumba hicho, ndani palikuwa na majeneza mengi sana, Devis akamtoa hofu Alexandra kisha akaendelea kusema" Usidhani kwamba haya ninayo yaongea nayatoa kichwani kijana, la hasha nayatoa humu "akatoa kitabu kwenye kabati maalumu akaweka juu kwenye meza. Jela hapo. Kilikuwa ni kitabu kilicho fanana na Biblia, kilikuwa na kurasa nyingi sana.



" Hivyo basi ujio wa kizazi cha Nuhu ulikuja na vitu vingi sana, mali na viti mbali mbali. Osaka mjini huu ulikuwa na mali nyingi sana, lakini pia mali hizo kwa sasa zipo chini ya jitu kubwa linalo fahamika kwa jina Agu. Mwamba huyu alipotea na ghalika la nabii Nuhu kama ilivyo kuwa kwa miji na vizazi vingine " aliendelea kusema Devis.



" Nitafikaje huko" alihoji Alexandra.



"Ni rahisi sana, meza vidonge hivi kisha ingia ndani ya jeneza, utakaa kwa muda siku saba katika jeneza kabla hujarejea kuwa mwili ulio hai. La kuzingatia ukisha jiona upo sehemu nyingine tofauti, jiamini kwa kila utakacho kutana nacho, jitambumishe kwa jina Bravo na Alexandra tena" alijibu Devis na kisha kumpa vidonge hivyo Alexandra. Naye alipokea akameza na kisha kuingia katika jeneza tayari kwa safari ya kuelekea Osaka kukabiliana na mfalme Ogu ili achukue pete yenye miujiza amletee Devis kisha naye ampe njia ya kutoka katika Gereza hatari DIYARBAKIR ili akaishi na wadogo zake.



Alipo meza vidoge vile hali ikamuwea tofauti, kijasho kikimtoka kwa kasi sanjari na kupoteza fahamu mithili ya mtu aliye fariki, Devis akalifunika jeneza. Sasa yakawa majeneza mawili yaliyo takiwa kwenda kufukiwa kwa sababu kule ulingoni kuna mmoja alipoteza maisha.

Majeneza hayo yalifukiwa, wazikaji waliamini huo ndio mwisho wa kila mwanadamu, hata wasijue kuwa kuna binadamu mmoja atarejea amefukiwa kwa sababu maalumu, hivyo hatua ya kwanza ya kijana Alexandra ikawa imeanzia hapo kuelekea Osaka!



Koleo la mwisho lililo sheheni udongo wa kufikia kaburi ulipo tupa ule udongo hali ikawa tofauti kwa Alexandra, joto lilizidi mara dufu ndani ya jeneza lile lililo beba njia ya kuelekea Osaka, jambo ambalo lilipelekea kupoteza fahamu. Akashindwa kujua kipi kilicho endelea. Upepo mkali ulivuma, mithili ya kimondo jinsi kidondokavyo kutoka angani kushuka kwenye uso wa dunia ndivyo ilivyo kuwa. Lile jeneza lililo mbeba Alexandra lilitua sehemu ya ajabu tofauti na dunia ya kawaida, sehemu ile ilikuwa na kivuli hafifu mfano wa mawingu sanjari na kuwa tulivu huku upepo nao ukivuma kwa mbali kama pepo za fukwe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Vumbi kubwa ilipaa juu na kupelekea hofu kutanda kwa wakazi waishio ndani ya himaya ile, kila mmoja aliingiwa na hofu na kujiuliza ni kitu gani ambacho kimetokea sehemu ile. Baada vumbi kutoweka, kundi la watu wasio pungua sita liliwasiri mahala pale ilipo timka vumbi, walionesha kuwa ni askari wa jeshi fulani, walikuta jeneza. Walistaajabu sana, ni kitu ambacho hawajawahi kukiona maishani mwao. Mmoja baada ya mwingine akatelemka kwenye migongo ya farasi walio kuja nao na kisha kulizunguka jeneza lile sanjari na kulishangaa kisha kutazama juu lilipo tokea, wakati wanashangaa, upanga nao ukadondokea kando ya jeneza lile. Wakazidi kujawa na hofu, wakatazamana kisha mmoja wao akasema "Hii ni ishara mbaya, kuna jambo linatarajia kutokea lazima mfalme apewe taarifa haraka sana iwezekanavyo. Inawezekana kabisa maadui zetu wameanza kutuchokoza upya", wote kwa pamoja waliunga mkono kumpa taarifa mfalme wao kuhusu jeneza lile. Walihisi kuwa maadui zao wametuma ishara ya kuwa vita bado Itaendelea tena, vita kubwa iliyo zuka miaka kadhaa iliyo pita. Ni vita ambayo ilikuwa inakutanisha ngome mbili tofauti, vita hiyo hupelekea maafa makubwa hasa hasa kwa watoto na wanawake, hutumia panga kali mishale, mikuki na siraha nyingine mbalimbali.



"Lakini hawa watu wanataka nini kwetu?", aliongeza kusema yule mtu aliyetoa wazo la kumpa taarifa mfalme wao.

Alikohoa kidogo kisha akaendelea kusema "Lakini nina imani ipo siku yake tu, hatuwezi kushindwa miaka yote", alipokwisha kusema hayo akatoa amri kurudi kwenye ngome. Wakapanda farasi wao, lakini kabla hawajaanza safari, lile jeneza lenye mtu ndani likafunguka. Vumbi iliyotua kwenye mfuniko ikashuka chini, Alexandra akanyanyua kichwa huku mboni zake zisione vizuri mbele. Ila kadri muda ulivyozidi kusonga ndivyo alivyo pata uwezo wa kuona vizuri, hatimaye anapata kuona vizuri sasa. Alikohoa mara tatu sambamba na kupigwa butwaa baada kuwaona watu sita wakiwa wamemzunguka.

"Mkamateni tuondoke naye" aliendelea kusema mtu yule ambaye alionesha kuwa ndio mkuu wa msafara huo kwani mbali na kuonekana kutoa mawazo au amri kadha wa kadha lakini pia farasi wake alikuwa tofauti na farasi wengine. Farasi wake ikiwa mweupe.

Upesi walimnyanyua na kumuweka kwenye farasi kisha wakaondoka naye. MAZONA CITY Jina lililo andikwa kwa herufi kubwa kwenye ubao lilisomeka namna hiyo, ubao ulio bandikwa kwenye lango kubwa la mji ule ulio itwa Mazona. Wale watu waliingia na kisha lango likafungwa halafu yule farasi aliye mbeba Alexandra akaongoza mpaka kwenye uwanja mkubwa ambao ulikuwa jengo fulani kubwa, jengo ambalo halikuwa na dirisha bali mlango tu ambao nao ulionesha kuchakaa.



Alexandra alisimamishwa katikati pamoja na watu wengine, ambao walikuwa wamekamatwa kitambo hicho kilicho pita. Jumla walikuwa kumi, wanaume nane na wanawake wawili tu wote walikuwa wazungu kasoro Alexandra ambaye yeye pakee ndio alikuwa mtu mweusi jambo ambalo lilipelekea kuzua gumzo, walimshangaa na kuhisi kuwa ujio wake unaweza kuzua balaa lingine Mazona, mawazo ambayo yalikuwa tofauti na wale watu walio mkapata.

Mfalme alionekana juu ya jengo ndefu kabisa, ilikuwa na malikia wake pembeni. Umati mkubwa wa watu uliokuwa umekusanyika ukingoja kipi kinatarajia kutokea ulikaa kimya baada kengele kugongwa kuashiria kuwa ni muda wa kumsikiliza mfalme.

"Nadhani ule wakati muafaka umewadia, kutokana na vita vilivyo tokea miaka kadhaa iliyo pita haina budi kuwa makini na kiumbe yoyote atakaye aonekana kwenye mpaka wetu"



"Nowaondoe shaka watu wangu, hakuna wa kutikisa ngome yangu. Sisi sio wanyonge kama wengi mnavyo dhania, ulinzi imara uemongezwa. Hebu sasa tuache hili. Bila shaka mnatambua adhabu ambayo hupewa mtu anaye kamatwa na jeshi langu"



"Ndiooooo", umati mkubwa wa watu uliitikia, vifijo na ndelemo vilisikika. Nyuso zao zilichorwa alama mbali mbali, walitoboa masikio lakini pia mavazi yao ni ngozi za mnyama chui. Upande wa wanawake nao hivyo hivyo, waliyastili matiti yao na viuno vyao huku wakiacha wazi tumbo na mgongo. Walionekana kuwa warembo kweli kweli. Upande wa watoto ilikuwa tofauti, wao walivishwa nguo moja tu ya kustili sehemu nyeti.

Naam! Lango la jumba lile ulifunguliwa kisha mmoja baada ya mwingine alisukumwa kuingizwa ndani ya lile jengo ambapo humo ndani palikuwa na kisima kikubwa chenye maji, katika maji hayo palikuwa na viumbe wa ajabu ambao waliwekwa mahususi kwa ajili ya kuwatafuna vibaya wale watu wanao kamatwa au kuingia ndani ya ngome kinyemela.

Walipangwa mstari, vilio vilisikika pindi roho zao zilivyo kuwa zilitoka, damu ziliruka kila alipo tupwa mtu wakati huo shangwe zilisikika, watu wa Mazona walishangilia namna ambavyo mateka walivyo kuwa wakiteketea kinyemela.

Alexandra alitetemeka, hofu dhufo lihari ilimjaa, machozi yakamtiririka. "Devis Devis umeamua kunitoa sadaka, ni heri ungeniacha ninyongwe tu. Ona sasa nimeruka majivu nimekanyaga moto", aliyafuta machozi yake baada kuwaza wakati huo huo mtu aliye mtangulia alivutwa, akasukumwa na sasa akangojea zamu yake ya kutafunwa tafunwa vibaya na viumbe wale wa ajabu waliokuwa ndani ya kisima.

Lakini kabla hajatupwa ndani ya kile kisima, kule juu ghorofani binti wa mfalme wa kuitwa Rinda, binti huyo toka mwanzo alikuwa akimtazama Alexandra kwa jicho la aina yake na hata asipepese mboni zake, muda wote alikuwa akimuangalia tu. Ghafla alimsogelea baba yake, akalaza kichwa chake kwenye bega la baba yake kisha kwa huzuni akasema...



"Baba naomba huyu mwanadamu asifanyiwe unyama huu", Princess Rinda aliongea kwa sauti ya chini iliyojaa simanzi ndoto zake, kila alipo mtazama Alexandra roho yake ilimuuma kwani Alex wakati ule alionesha unyonge sambamba na kutetemeka, yote ikiwa shauri ya hofu kubwa iliyo kuwa imetanda moyoni mwake huku akili akijutia kukubali uamuzi wa mzikaji bwana Devis.

"Kwanini unasema hivyo? Unataka nivunje taratibu ya ngome ya Mazona?", mfalme aliuliza huku akimtazama binti yake kwa jicho pembe. Safari hiyo Rinda alidondosha chozi, chozi hilo lilimshtua mfalme yule, katu hakupenda kuona binti yake akidosha machozi, alimpenda sana na ndio mtoto wa pekee aliye bahati kumpata baada kukaa muda mrefu pasipo kupata mtoto, hivyo uwepo wa Rinda ulimfanya kuwa mwenye furaha muda wote na pia alimpenda, akathubutu kuteua walinzi watakao mlinda kila mahala ndani ya Mozana.



"Stoop", Sauti ya mfalme ikapasa akitaka zoezi hilo lisitishwe upesi, alikubali ombi la binti yake kisha akaingia ndani, aliketi kwenye meza akachukua karatasi pamoja na mwiba wa mnyama nungungu, akaandika maelezo haraka haraka halafu akaikunja kisha akarejea tena juu kwenye kilele cha jengo. Alitupa karatasi ile ya ujumbe, ikadakwa na mwanaume mmoja aliye itwa Josh, mtu hatari kweli kweli ndani ya mji ule Mazona.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Josh alikuwa na umbile ndefu na mwili mkubwa, sura yake ilijaa alama kadha wa kadha. Alionekana kutisha hasa pale anapo pandwa na hasira, hubadilika ngozi, anakuwa na ngozi ya nyoka huku macho yake nayo yaking'aa mithili ya macho ya Simba. Josh aliogopeka, na ni moja ya walinzi wanao mlinda Rinda, lakini pia mara nyingi alitumiwa na mfalme kutuliza ghasia pindi ugomvi unapo tokea wa wao kwa wao kwa watu waishio Mozana kwani mbali na vita kadhaa kuzuka kutoka kwenye ngome nyingine, hata wao kwa wao kuna muda hupigana. Vita vya ukoo.



"Josh waambie na wenzako, kuweni makini na huyu binadamu, hatujui nini dhamira yake. Lakini pia nahisi Rinda tayari ametokea kumpenda. Sitaki hili litokee", Akaachia tab hafifu Josh alipo maliza kusoma ujumbe ule alio andikiwa na mfalme, alitikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, akayainua macho yake kule juu kumtazama mfalme, wakagongana uso kwa uso na wote wakanyoosheana dole gumba. Kwa mahaba ya aina yake mfalme akampa busu binti yake na mkewe kisha akarejea ndani, akaketi kwenye kiti chake. Muda mfupi baadaye Rinda naye akafika mahala pale, kwa sauti ya unyonge akamwambia baba yake akitanguliza na neno samahani "Najua hujapenda yule binadamu kuwa hai mpaka sasa, lakini nikuondoe shaka baba, hakuna kitakacho haribika. Nina imani ndoto yangu itakwenda kutumia sasa", Alimaliza kusema kwa tabasamu bashasha Princess.



"Ndoto? Ndoto gani Rinda! Unataka huyu ndio akuoe wewe?", Mfalme alishtuka. Akamjia juu binti yake sambamba na kunyanyuka kwenye kiti chake.



"Punguza hasira baba, kila mmoja wetu anandoto. Hata wewe una ndoto na unatamani siku moja itimie, vile vile mimi pia nahitaji ndoto yangu itimie. Sasa basi ili itimie inanilazimu huyu binadamu awe hai. Samahani sana kwa hilo" aliongeza kusema Rinda na kisha kutoka mahala pale alipo baba yake, alilinga alijua fika baba yake anampenda sana ndio sababu pekee iliyo mfanya kujichukulia maamuzi kwa nyakati tofauti tofauti, naye mfalme yule kuna sekta alishindwa kuhukumu kwani hakupenda kumuudhi binti yake. Rinda msichana mrembo ndani ya Mozana, moja ya miji iliyo potea miaka dahari iliyo pita.



Baada kuponyoka kifo sasa Alexandra aliwekwa chini ya ulinzi mkali, alifungwa minyororo miguuni. Alifungiwa kwenye chumba chenye mwanga hafifu, chenye maji machafu yaliyo weza kufuga wadudu wakali, alivuliwa nguo zile alizo tua nazo Mazona akavishwa nguo za asiri wa mji ule. Nguo ambayo ilistili nyeti zake tu, huku sehemu nyingine zikiwa wazi.

Akiwa ndani ya chumba kile aliteseka sana, aling'atwa na wadudu wale, lakini harufu mbaya ya maji yale machafu yakamfanya kuwa vigumu kukimudu kikombe kile cha mateso, kwa mara nyingine tena akajikuta akitamani heri angepoteza uhai kabisa kama ilivyokuwa kwa mateka wale alio kamatwa nao kuliko mateso yale. Alexandra alilia sana, alikaa kwa muda ambao hakuufahamu ingawaje baadaye mlango ulifunguliwa na kisha kufungwa, ndani aliingia mtu ambapo Alexandra hakuweza kumtambua sababu ya giza lililo kuwemo mule ndani, mtu yule alitembea kwa madaha, alizipiga hatua moja baada ya nyingine kuzidi kumkaribia Alexandra.



Kwa kuwa tayari alikuwa amekata tamaa ya kuendelea kuishi, kamwe hakuwa na hofu moyoni mwake. Pingine akahitaji kifo kuliko kitu kingine kile kwa wakati ule ndani ya Mozana, mateso yaliuchosha vilivyo mwili wake.

Mtu yule hakusema neno lolote, alimsogelea na kusema "Hutakiwi kuwa muoga kiasi hicho, kwa kuwa umenusurika kifo basi unatakiwa kuwa na roho ya ujasiri. Kumbuka huu ni mwanzo wa safari yako, haujafika OSAKA, lakini hapa ndipo kilipo kitabu chenye sheria, ramani na taratibu zote zinazo patikana osaka, hivyo basi inakubidi ufanye mpango uaminike na Mfalme wa Mozana kwa kuwa Princess Rinda ameonekana kukupenda, sio mfalme tu bali fanya kila linalo wezekana uwaaminishe watu wa kaya hii kuwa Josh si lolote si chochote mdebwedo tu", Alisema mtu yule, sauti aliyo kuwa akisikia ilifanana na sauti yake.

"Nani wewe?", Aliuliza Alexandra kwa sauti ya juu.

"Ahahaha hahaha, Devis", Akianza kwa kuangua kicheko, mtu yule alijibu. Safari hiyo Alexandra alisikia sauti ya Devis yule aliyefanya mpango mzima wa yeye kuanza safari ile ya ajabu, safari ya kuelekea Osaka kuchukuwa pete yenye miujiza.

"Devis Devis Devis, mshanzi wewe umenitoa sadaka na bado unaniletea upuuzi?", Alexandra alifoka huku akiyumbisha mwili wake kana kwamba akitaka kujinasua kwenye minyororo aliyo fungwa, alipiga makelele ikiwa muda huo mtu yule aliye jitambulisha kwa jina Devis aliangua kicheko kwa mara nyingine tena kisha akaongeza kusema" Itabidi ufanye hivyo, ukipinga ujue kwako kitakuwa kiama fanya nilivyo kuelekeza uondoke Mozana uelekee Osaka, usitamani kifo kumbuka kuna damu inakutegemea huko duniani",Mtu yule alipokwisha kusema hivyo akapotea mule ndani hali ya kuwa sauti ile aliyotoa Alexandra hatimaye inagaonga ngoma ya masikio ya Princess Rinda. Rinda alishtuka, sauti ya Alexandra na sauti ya watu wa mji wa Mozana zilikuwa tofauti kabisa, hivyo mayowe yale yalitosha kumfanya Rinda kujua kuwa ile ni sauti ya mwanaume aliye mtetea, hivyo alifikiria kufanya utetezi mwingine tena. Lakini wakati Rinda anawaza kufanya msaada ule, mtu wa karibu yake bwana Josh tayari alikuwa amepewa jukumu la kummaliza kimya kimya Alexandra, hata Josh naye asijue kuwa kupitia yeye Alexandra anataka kujiaminisha kuwa yeye ni mwamba ikiwa ndio hatua nyingine ya kukikasaka kitabu kitakacho mpa mfumo mzima wa kufika mji wa Osaka.

"Josh! Hebu nenda kumuwekea huru yule mwanadamu", Kwa utashi na kujiamini, Rinda aliongea, mithili ya kimbunga Josh akafika ndani ya nyumba chumba kile, si kwa dhumuni la kutoa msaada la hasha bali kwa dhumuni la kumpoteza mazima Alexandra au ukipenda muite Bravo..





Alimkuta Alexandra amejiinamia, alimshika kichwa akimuinua ili kumuangalia usoni.

Aliongea lugha tata ambayo Alexandra hakuielewa zaidi alimuona Josh akichomoa kisu ili ammalize kabisa, lakini kabla Josh hajafanya kitendo hicho alipigwa ngumi ya tumbo iliyo pelekea kusukumwa mpaka nje, akiwa na minyororo ambayo alifanikiwa kuikata akasimama mbele Josh ambaye muda ule alikuwa akitweta maumivu. Binti mfalme pamoja na walinzi wengine ambao walikuwa wamesimama kwenye kilele cha jengo ndefu walistaajabu kuona Josh akiwa chini akigugumia maumivu. Alishindwa kuelewa ni jambo gani hasa ambalo limpelekea wawili hao kupigana.

Josh hakuwa tayari kupoteza heshima aliyo jiwekea muda mrefu hivyo upesi upesi alisimama na kuanza kukabiliana na Alexandra binadamu ambaye alionekana kuwa ni goi goi yaani hawezi jambo lolote, ila uwezo aliokuwa nao muda ule uliwaacha midomo wazi. Patashika nguo kuchanika ilizuka mahala pale, kila mmoja alionyesha ujuzi wa mkubwa. Lakini mwisho wa pambano Josh alipigika vibaya mno kwani Alexandra alikuwa na nguvu nyingi sana vile vile mwili wake ulikufa ganzi kiasi kwamba hakuhisi maumivu yoyote pindi Josh alipokuwa akimpiga.



Jopo la wananchi wa mji wa Mozana walio bahatika kushuhudia pambano lile lilishangilia sana anguko la Josh, mfalme naye alimshangaa sana Alexandra kwa kile alicho kionyesha, kijana wake kupokea kipigo lilikuwa jambo tata kuwa kulishihudia. Kimasihara tu Alexandra akajizolea umaarufu, mfalme wa himaya ya mji ule Mozana akamuamini, akampa cheo cha kuwa moja ya wanajeshi wake wa kulinda ngome huku akimshusha cheo Josh. Jambo hilo lilimuuma sana Josh moyoni aliamini kuwa kitendo cha Alexandra kuingia kikosini inaweza kumuwea shida kutimiza azma yake. Josh alimpenda sana Rinda binti mfalme ingawa alishindwa hisia zake kuziweka wazi kwa mrembo huyo, kwahiyo kwa namna ambayo aliona jinsi Rinda anavyo mthamini Alexandra, akahisi kuwa muda wowote wawili hao wanaweza kuanzisha mahusiano.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Heshima kubwa aliyo ipata kwa kumuadabisha Josh, alipewa sehemu nzuri ya kulala, sifa zake ziliambaa kwa kasi mji wote wa Mozana. Hakuwa mateka tena, aliaminika vilivyo. Baada kulala na kuamka alishtuka kujikuta yupo sehemu tofauti, alijiona yupo kwenye chumba kizuri chenye hadhi kubwa.

"Mmh nipo wapi?" Alijiuliza Alexandra wakati huo alinyanyuka kwenye kitanda akasogelea kabati ambalo lilikuwemo mule kwenye chumba, ni kabati la zamani sana. Lilipambwa na nembo mbali mbali za ajabu na kushangaza, nembo hizo zilitafsirika kuwa ni watu kuingiliana kinyume na maumbile. Kwenye mlango wa lile kabati aliona funguo ikining'inia, wala hakuona tabu wala woga kuikamata funguo ile na kisha kufungua mlango.

Alipo fungua akaona kuna vitabu kadhaa wa kadha vilonesha kujaa vumbi sanjari na bui bui kuweka makazi yao, akahitaji kujua kabisa undani wa kuhusu vitabu vile, lakini alipo peleka mkono wake ili achukue kimoja, alipigwa shoti, upesi akarudisha mkono nyuma sambamba na mlango kujifunga ikiwa muda huo huo binti mfalme aliingia chumbani mule akiwa na wingi wa tabasamu.



"Nje kuna shangwe, kuna mamia ya watu wanataka kukuona shujaa uliye weza kumuadabisha vilivyo Josh" Aliongea Rinda. Alexandra akageuka kumtazama, hakujua nini Rinda anamaanisha wakati huo huo nje zilisikika sauti zikimtaja kwa jina shujaa kwa nguvu zote, mbali na Josh kuaminika kwa mfalme wa Mazona vile vile alichukiwa karibu na watu wote waishio mji ule hasa hasa kutokana na ubabe aliokuwa nao, hakuwa na hata chembe ya huruma kwa kila iliye leta mzaha, mfalme imtumia kwa kazi kadha wa kadha hasa zile za mauaji kwa mtu atakaye kiuka taratibu na sheria za kuishi Mazona.

"Hebu toka ndani ukawaangalie uwapungie hata mkono", Aliongeza kusema Rinda. Alexandra bado alikuwa na sintofahamu kubwa moyoni mwake, alishindwa kujua alimpiga vipi Josh ilihali anaonekana ni mtu hatari.

Lakini wakati hayo yakiendelea, mara ghafla hali ya hewa ya Mozana ikaanza kubadilika, radi ikalarua mnara mkubwa uliokuwa kwenye mji ule, tetemeko la ardhi likazuka. Alexandra alishtuka, lakini Rinda akamtoa shaka akamwambia kuwa hiyo hali hutokea mara kwa mara na baadaye hutulia.

"Kwanini huwa inatokea, na nembo hizi za namna hii zinamaanisha nini?", aliuliza Alexandra. Princess Rinda akaangua kicheko cha madaha kisha akasema "Kuna mengi unatakiwa kuyafahamu ukiwa hapa Mozana lakini kwa sasa toka nje uone jinsi watu wa Mozana wanavyo kuhusudu". Alexandra akatii ombi, alitoka kwenye kile chumba, alifurahia kuona jinsi watu wa Mozana walivyo mkubali kwa kiasi kikubwa, lakini pia jopo la wanajeshi la mji huo hali kusita kumpa heshima kwa kuungama, jambo hilo lilimuuma sana Josh, na ndipo alipo amuwa kuchukuwa uamuzi wa kuondoka katika mji huo, alipotea kabisa ingawa aliacha ujumbe kuwa atarejea muda usio julikana kuja kuangusha utawala wote wa Mozana akianza na mfalme kisha Alexandra, alichukuwa farasi wake akaondoka kwa kasi ya ajabu na kuuacha mji wa Mozana Alexandra akiwa ndio habari kuu.



Lakini wakati Josh anatoweka upande wa Alexandra yeye alikuwa bado kwenye mabano, alishindwa kujua kama kweli aliweza kukubaliana na Josh. Pole pole moyoni akihisi wale wadudu waliokuwa wakimshambulia kwenye chumba kile cha mateso alicho fungwa huwenda wakawa wamechangia kumpa uwezo wa ajabu, aliamini hilo kwa asilimia kadhaa ila akahitaji kufanya utafiti mkubwa kwa kina. Alijishangaa safari hiyo kuelewa kile wakiongeacho watu wa mji ule, awali alikuwa haelewi lugha wanayo izungumza lakini sasa alielewa ingawa hakujua ni aina gani ya lugha waiongeayo.



Hatimaye aliishi kwa amani, alifuata taratibu zote za Mazona, akapata kujua mengi sana kuhusu mji ule, alipigwa muhuri ambao ulimtambulisha kuwa yeye ni moja ya watu walio potea na kuishi maisha mapya kwenye mji usio onekana kwa macho ya kawaida, moja ya mambo ambayo Alexandra aliyagundua ni mji huo uliwahi kuwepo kwenye uso wa Dunia lakini ulipotezwa kwa ghalika la moto baada Mungu kuchukizwa na maasi ambayo walikuwa wakiyafanya wakazi wa mji ule. Hawakutii agizo la Muumba wao, waliendekeza anasa za kila aina, hawakujali ibada. Zaidi zambi kuu iliyo mtia hasira Muumba ni ile ya kufanya mapenzi ya jinsia moja yaani Ushoga na kusagana upande wa wanawake. Mozana waliihusudu zambi hiyo, na hawakuwa tayari kuiacha ndipo Muumba akaupoteza mji huo kwa moto kwa dhumuni la kukiangamiza kizazi hicho hatari, zilitumika dakika tatu tu Mozana kupotezwa. Harufu ya damu ilitapakaa. Ni miaka dahari iliyo pita karne na karne.

Baada kukaa kwa muda mrefu Mozana, hatimaye Alexandra alijikuta akijisahau. Alisahau kuwa ana safari ndefu sana mpaka pale Devis alipo mtokea kwa njia ya ndoto na kisha kumkumbusha, tena aliongea kwa ukali na msisitizo mkubwa "Alexandra. Sifa na jina ulilo litengeneza hapa Mozana zinakulevya, najua kuwa tayari umeufahamu mji huu japo kwa asilimia ndogo sana, kumbuka jukumu lako. Tambua kuwa wewe ni mfungwa, unatakiwa kunyongwa Alexandra na vile vile unahitaji kuishi ili urudi nyumbani kwenu hai, hapa ulipo ni nusu mfu, uwezo ninao wa kukurejeasha duniani na udhabu yako ikawa ipo pale pale. Unakaa tu, na wala hujui kuwa mji huu wakati wowote utaangamia, hawa unao ishi nao sio watu kijana, hizi ni roho za watu walio angamia, nenda Osaka ondoka mahali hapa sio salama " Alifoka Devis wakati huo huo Alexandra alizinduka kutoka usingizini, alistaajabu kujikuta kuwa ilikuwa ni ndoto, mara nyingi aliziamini ndoto zake, hivyo hakutaka kulipinga suala hilo la mji huo kuendelea kupotea kwani tayari alikuwa ameshajua sababu za kuangamia kwa mji huo, ni laana na si vinginevyo. Mozana palikuwa tulivu, hapakuwa na usiku wala mchana, muda wote hali ya hewa ilikuwa aina moja, walilala kwa kufuata Kengere kubwa iliyo tundikwa kwenye mnara mrefu.

Ndoto ile aliyoota muda mfupi ulio pita ilimfanya asiendelee tena kuuchapa usingizi hivyo basi kwa mara nyingine akafungua kabiti lile lenye nembo mbalimbali za ajabu ajabu, kwa mara nyingine tena akaviona vile vitabu chakavu, vilikuwa ni vitabu zaidi ya vinne. Kwa hofu akakamata kitabu kimoja, ajabu safari hiyo hakupigwa shoti ilikuwa jambo jema upande wake, aliachia tabasamu bashasha kimoyo moyo akajisemea "Nafikiri huu ndio muda muafaka wa kuelekea Osaka, muhuri huu umenifumbua mengi. Nimewakumbuka wadogo zangu, lakini pia nimeikumbuka nchi yangu, ndugu jamaa na marafiki sioni haja ya kuendelea kuishi Mozana, naishi na roho ikiwa mimi ni nusu mfu?!"

"Hahahahah", Alipokwisha kujisema hayo akaangua kicheko cha madaha huku akiendelea kufunua kurasa za kitabu kile alicho kikamata. Lakini baadaye alikirejesha baada kuona kuwa kitabu hicho kinaeleza katiba, sheria na taratibu za Mozana. Sasa akachukuwa kitabu kingine, ndani ya kitabu hicho cha pili akapata kugundua kuwa kikielezea mji wa Osaka. Naam! Osaka, alifunua kurasa haraka, ghafla akaona ramani ya mji huo lakini pia una kila aina ya changamoto jinsi ya kupenya mpaka kukanyaga ardhi ya mji huo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Basi Alexandra hakuona haja ya kupoteza muda, upesi alichukuwa, karatasi akacharaza maneno kwa kutumia wino utokanao na mwiba wa mnyama Nungunugu kisha akaibandika kwenye kabati, aliacha ujumbe fulani, sasa akachukua kibegi chakavu kilicho kuwemo ndani ya kabati hilo, kila kitu kilipo kuwa tayari akasimama kwenye dirisha kutazama usalama wa Mozana. Hakika mji ulikuwa umetulia, ajabu hakuonekana hata mlinzi mmoja aliye kuwa akilanda labda.

Akiwa na kibegi chake mgongoni kilicho hifadhi kitabu chenye ramani ya kuingia Osaka, alitumia kamba kushuka chini ili atoweke kwa kutoroka, lakini kabla hajakanyaga ardhi, ghafla lilishwa panga ikaikata kamba ile, muda mfupi baadaye kengere ya kuashiria hatari ikagongwa.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog