Search This Blog

MKE WANGU NUSU JINI, NUSU MTU - 5

 





    Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu 
    Sehemu Ya Tano (5)




    ?Kama umekuja kunipa penzi sawa, twende chumbani my dear, nimekumisije??

    Tuliongozana hadi chumbani, Mayinu akasimama, akanikumbatia na kuanza kunipa ulimi kwa muda wa dakika kadhaa mpaka nikawa nimepata moto.



    Alinivua nguo, alipomaliza na mimi nikamvua nguo yeye kisha wote tukapanda kitandani.

    Tuliendelea kuchezeana hapa na pale ili kuzidi kuchajishana. Mwishowe tukafikia kipindi cha kuanza



    kwa mchezo. Mchezo ulikuwa mzuri, Mayinu alinikumbusha mbali sana huku na yeye akidai alinimisi kama mimi pia nilivyommisi.



    Yeye ndiye aliyetangulia kumaliza hamu yake akaendelea kuniburudisha mimi ambapo pia nikawa nakaribia kumaliza hamu yangu. Nilipomaliza nilimwegemea kifuani kidogo nilipoinua uso baadaye ili nimbusu nikashangaa kumuona ni Munil.

    ?Ha! Munil,? nilisema kwa mshtuko mkubwa.



    ?Unajua wewe mwanaume hutosheki? Nakushangaa sana,? alisema Munil akinisukumia huko nikadondokea upande wa pili kwenye godoro.

    ?Munil mke wangu,? nilimwita kwa sauti yenye mtetemeko wa ajabu.



    ?Kwenda huko, hivi unajua kama mimi Munil nina uwezo wa kukutoa roho ndani ya dakika moja tu ukawa umesahaulika hapa duniani kwenu? Au unataka niseme nini kwako ili unielewe we mwanaume usiyekuwa na haya wala soni?



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ?Basi mke wangu, kwanza nimegundua kwamba hakuna cha siri nitakachokifanya halafu wewe usikijue.?

    ?Kwa hiyo kama ungefanya mimi nikashindwa kukijua ungekuwa unanisaliti kila kukicha siyo??

    ?Hapana mke wangu.?

    ?Sasa nini? Nilishakuonesha ishara kama mara moja kwamba uachane na wanawake wengine nikajua umejua lakini sasa nahisi kuwa kumbe hukujua au ulijua bali ulipuuza.

    ?Uliwahi kufika motoni??

    ?Sijawahi.?

    ?Kuna aliyewahi kufika akakusimulia kulivyo??

    ?Hakuna.?



    ?Basi naomba uwe unatulia sana mume wangu. Najua wewe unasakamwa na shetani tu lakini usinifanyie hivyo mume wangu, kama ni utajiri tunao mkubwa sana mpaka unashindwa jinsi ya kuutumia maana tangu baba yangu amekupa zile pesa sijakusikia ukisema unataka kufanya biashara yoyote.



    ?Kwanza mimi naona hata mpango wa kupangisha nyumba ungekufa tukanunua kiwanja tujenge jumba la kifahari mbona fedha inatosha.?

    ?Ni kweli mke wangu.?

    ?Haya, twende nyumbani sasa.?



    Tulivaa nguo na Munil, tukaondoka. Wakati tunatoka niliamini kwamba, nje nitamuona yule mwanamke aliyekuwa akipika chakula cha gengeni aliyenichangamkia lakini hakuwepo na mazingira ya nyumba yalikuwa yale ya mwanzo ya kuwepo kwa nyasi nyingi na nyumba kubomolewa.



    Nilishindwa kumuuliza chochote Munil, nikaamua kumfuata kwa nyuma kama mbwa anayetembea na bosi wake kwenda mahali.

    Nilitegemea maajabu kutoka kwa Munil njiani sikuyaona hadi tunaingia ndani. Nilipokaa tu akasema:

    ?Mume wangu najua kama una mipango mingi sana, nakuruhusu uende lakini akilini mwako ondoa suala la kunisaliti, sipendi hata wewe huwezi kupenda.?



    ?Ni kweli mke wangu, siwezi kupenda na nimefurahi sana kunisamehe kwako. Ila nakwenda kwa yuleyule rafiki yangu.?

    ?Nenda salama mume wangu, nakupenda sana,? alisema Munil akasimama na kunikumbatia kwa nguvu zake zote.



    Niliondoka, nilitembea kwa kuinamisha kichwa chini kwani kitendo alichonifanyia Munil ni cha ajabu sana sijawahi kukisikia kwa watu wengine.

    Kufika Kibaha mjini nilipata wazo la badala ya kwenda kwa rafiki yangu huyo niliamua kwenda kwa rafiki yangu mwingine anaitwa Isaya.



    Isaya ni rafiki kaka kwani amekuwa akinisaidia mawazo na amenizidi umri. Kwa hiyo niliamini niende kwake kwa ajili ya kumwomba ushauri kwamba ni biashara gani nifanye na kiasi kile cha pesa nilichopewa ukweni kwangu.

    Nilimkuta Isaya amekaa sebuleni na mke wake. Watoto walikuwa nje na ndiyo walionipokea.

    ?Eee bwana vipi, mbona umepotea namna hii rafiki yangu?? Isaya alisema akinishangaa. Akaendelea:



    ?Kwanza nakuona kama umenawiri sana, umepata pesa nini??

    Mimi nilicheka tu, nikakaa kwenye kochi huku mkewe akinikaribisha kwa furaha naye akidai hajaniona siku nyingi sana.

    ?Mimi nipo sana ila sema tu mambo yalikuwa mengi. Lakini katika yote naomba samahani kwenu kwamba nilioa bila kuwaambia.?

    Walishtuka, wakatazamana. Isaya akauliza:

    ?Umemuoa nani??

    ?Kuna dada mmoja anaitwa Munil.?

    ?Munil?? aliuliza haraka mke wake.

    ?Ndiyo shemeji, unamfahamu nini??



    ?Hapana, ila kuna habari zimesambaa hapa Kibaha kwamba kuna kijana amefunga ndoa na jini. Sasa watu wanasema huyo msichana ni jini kwa sababu hajulikani alikotokea na ana mwonekano tofauti kabisa na wasichana wetu wengine hapa Kibaha.



    ?Nasikia anaonekana mara mojamoja sana akitembea mitaani. Na huwa anapendelea kuvaa magauni mpaka chini kabisa kwa vile hana miguu ya binadamu ana kwato kama za ng?ombe.?

    Wakati mke wa Isaya anasimulia hayo, mimi mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda kwa kasi nikijua



    msichana anayesema hapo lazima atakuwa Munil. Kwa sababu gani? Hata mimi niliwahi kujiuliza kwamba tangu nimeishi Kibaha sijawahi kumwona Munil. Pia, sijawahi kumwona akiwa amevaa nguo nyingine mbali na magauni.

    ?Da! Shemeji si huyo,? nilisema kwa sauti iliyotoka kwa uvivu sana.

    ?Kwani huyo uliyemuoa wewe ni mtoto wa nani hapa Kibaha au ametokea mkoa?? aliuliza Isaya.

    Itaendelea wiki ijayo.



    ?Hapana, kwao ni mkoa huuhuu wa Pwani ila wazazi wake wanaishi Bagamoyo.?

    Niliposema hivyo wakatazamana tena, lakini Isaya kama akayumbisha mazungumzo kwa kusema:

    ?Mimi bwana kwa muda tulioachana niliamua kukata shauri na kuokoka. Kwa hiyo mimi na nyumba yangu tumeokoka na tunamtumikia Bwana!?



    ?Ooh! Ni vyema sana Isaya. Sasa mimi bwana nimekuja nina shida. Shida yangu nimepata vijisenti kidogo sasa ishu iko kwenye biashara. Je, nifanye biashara gani??

    ?Mh! Labda kwanza ungesema umepata kiasi gani ndipo nikushauri.?

    ?Kama shilingi bilioni mbili hivi.?







    Isaya na mkewe walishtuka sana. Wakatazamana kwa macho ya wasiwasi. Ilionekana kama hawakuamini maneno yangu.

    ?Shilingi ngapi?? aliuliza Isaya huku akikaa sawasawa.

    ?Kama bilioni mbili hivi.?

    ?Haiwezekani!?

    ?Ndiyo nakwambia sasa.?

    ?Wewe, pesa yote hiyo umeitoa wapi? Umeiba??

    ?Hapana, nimepewa na baba mkwe wangu.?

    ?Baba wa mkeo huyo uliyemuoa??

    ?Ndiyo.?



    ?Mh! Shemeji hongera sana. Kumbe umeoa kwenye ukoo wenye uwezo mkubwa sana.?

    ?Ni kweli, mbona nimepewa na gari la kisasa, jipya, lipo nyumbani.?

    ?Kweli? Mbona huendeshi sasa?? aliuliza Isaya.



    ?Siendeshi kwa sababu zangu lakini kuna siku nitaanza kuingia nalo mitaani, si unanijua.?

    Isaya aliniangalia kwa muda kisha akasema kwa kiasi hicho cha pesa hana biashara ya kunishauri kichwani. Alisema ni vizuri kama nitawaona wataalam wa uchumi wakanishauri nifanye biashara gani!



    Tuliendelea na mazungumzo lakini nilipotaka kuaga, Isaya akasema tusali kwanza ili Mungu anibariki!

    ?Sawa,? nilijibu huku Isaya akisimama na mimi pia nikasimama sambamba na mkewe.

    Alipoanza kusema Bwana tunakushukuru palepale nilijikuta chini. Nikaanza kutokwa na povu



    kinywani huku nikirusharusha miguu huku najiona.Wale wenyeji walisogelea na kuanza kuniombea kwa kelele lakini baada ya hapo kilichoendelea sikukijua.

    Nilipokuja kuzinduka, nilijikuta nipo kitandani, tena hospitalini.

    Niliangaza pembeni yangu nikamwona Munil amesimama lakini uso wake ukiwa umekasirika sana. Hakukuwa na mtu mwingine zaidi yake.



    ?Pole,? aliniambia kwa mkato.

    ?Asante. Nini kilitokea??

    ?Unaniuliza mimi! Mimi ndiyo nikuulize wewe nini kilikutokea.?

    ?Nani kanileta hapa??

    ?Mimi sijui.?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ?We ulijuaje kuwa nipo hapa??



    ?Nilijua ninavyojua mimi mwenyewe.?

    Kwa mbali nilianza kupata picha kwamba nilikuwa kwa Isaya, wakati nataka kuondoka akasema tusali, nikakubali na kusimama ndipo nikaanguka.

    ?Isaya yuko wapi??

    ?Isaya ni nani??

    ?Nilikuwa kwake.?

    ?Mimi sijamwona.?

    ?Simu yangu iko wapi??



    Munil alinipa simu yangu, nikaangalia namba ya Isaya, nikaipata na kumpigia.



    ?Haloo.?

    ?Halo Isaya, vipi bwana??

    ?Sasa wewe mbona ulikimbia wakati wa maombi?? aliniuliza Isaya.

    ?Nilikimbia??



    ?Ulikimbia. Mimi nadhani kuna kitu cha kujiangalia sana ndugu yangu, unakimbiaje maombi ya Bwana Yesu??

    Kabla sijamjibu, Munil alinipokonya simu, akaiweka loud speaker, akaanza kuongea yeye.

    ?Haloo.?

    ?Haloo, nani shemeji??



    ?Mimi naitwa Munil na ndiye niliyemkimbiza mume wangu hapo nyumbani kwako. Wala usiwe na wasiwasi kuhusu yeye, ila nakuonya kuhusu mpango wako wa kutaka kufuatilia maisha yangu.

    ?Mimi najua mambo mengi tu kuhusu wewe. Mfano, wewe si umeokoka unasema? Lakini mbona una mwanamke kule stendi??



    Nilisikia simu ya Isaya ikikatwa ikalia tii tii tii! Munil alinirudishia simu huku akisema:

    ?Kwa hili mimi sina tatizo na wewe mume wangu kwani najua ulikwenda kwa Isaya kwa nia njema tu ila wao wanataka kunijua mimi ni nani ndiyo maana niliamua kukukimbiza pale walipoanza kuomba kwa sababu mimi sipatani na maombi.



    ?Na wala hapa si hospitali kama unavyojua, hapa tupo nyumbani, angalia.?

    Kufumba na kufumbua, kweli nikaona nimelala kitandani kwangu, chumbani.

    ?Ha! Munil, haya mambo yakoje??



    ?Haya mambo ni madogo sana mume wangu. Mimi ni binadamu mwenye uwezo mkubwa katika maisha. Hebu nyoosha mkono wako juu,? aliniambia Munil. Nikanyoosha mkono juu.

    ?Nyoosha tu.?Nilinyoosha tu, nikashangaa mkono wangu unarefuka hadi kushika paa la nyumba.?







    "Si unaona maajabu hayo mume wangu? Rudisha mkono halafu fanya kama kuna mtu unampepea hewani.?

    Nilifanya alivyoniambia Munil, palepale paa la nyumba likahama kutoka sehemu yake, nikaweza kuona anga na nyota zake mpaka mwezi.

    Mbaya zaidi niliona hata vitu vikubwa vikikatiza angani mchana kweupe pee!

    ?Vile vitu ni nini??

    ?Vile si vitu mume wangu. Ni binadamu wabaya ambao wakati wenzao wanafanya kazi za kutafuta maisha mchana kutwa wao wanapita angani kuwaroga ili maisha yao yaharibike.?

    ?Kwa hiyo wale ni wachawi??

    ?Ni wachawi mume wangu.?

    ?Na wewe ni nani? Maana umesema ni binadamu mwenye uwezo mkubwa.?

    ?Kumbe jibu unalo. Mimi ni mwanadamu mwenye uwezo mkubwa sana. Hebu pepea mkono hewani tena ili kufunika paa.?

    Nilipepea mkono hewani paa likajiziba kama kawaida. Lakini bado nilikuwa na maswali kuhusu Munil na dalili zote za kijini alizokuwa akinionesha. Moyoni nikasema:

    ?Kuna siku mambo yote yatakuwa hadharani.?

    ?Haiwezekani mume wangu,? alisema Munil kama aliyekuwa akijibu mawazo yangu.

    ?Unasemaje mke wangu, mbona sikuelewi??

    ?Ah! Nimejikuta nimesema tu. Na mimi bwana, sijui nawazaga nini wakati mwingine,? aliniambia Munil lakini mimi nikakataa kwamba lazima atakuwa alitambua mawazo yangu.

    *****

    Usiku wa siku hiyo ukawa wa ajabu tena kwangu, nikiwa nimelala usingizi wa fofofo, niliota ndoto kwa wakati ule. Nasema kwa wakati ule kwa sababu baadaye nilikuja kubaini kwamba haikuwa ndoto uhalisia.



    Niliota mimi na Munil tunashuka ndani ya gari pembeni mwa bahari maeneo ya Bagamoyo. Munil ambaye nilikuwa nikimwendesha, alinishika mkono na kuanza kutembea akiwa mbele yangu.

    Cha ajabu mbele tulikokuwa tunakwenda ni kwenye maji ya bahari na Munil hakuwa akionesha wasiwasi kuhusu uelekeo ule.[/COLOR]



    ?Munil,? nilimwita.

    ?Abee mume wangu,? aliitika bila kugeuka kuniangalia.

    ?Sasa kwenye bahari tunakwenda kufuata nini mke wangu??

    ?Kusalimia.?

    ?Kumsalimia nani??

    ?Wazazi wangu.?

    ?Lakini wazazi wako si wanaishi kule kwenye ile nyumba, kwenye maji wamehamia lini??

    ?Ndiko wanakoishi miaka yote.?

    ?Mh! Labda wewe, lakini sitaweza kuingia kwenye maji kwa sababu sijui kuogelea na pia nitashindwa kuhema.?

    ?Hutashindwa kuhema wala kutembea ndani ya maji.?



    Wakati Munil anamalizia kusema neno, wala kutembea ndani ya maji, tayari tulishayaingia maji.

    Cha ajabu sasa. Wakati tunaingia kwenye yale maji, mwanzomwanzo sikuona dalili ya maji kunipiga miguuni kama inavyokuwa, badala yake ilikuwa kama napita kwenye njia ya kawaida.



    Nikiwa namfuata Munil nyumanyuma tulitembea hadi kufikia eneo la maji marefu ili tuzame. Nilijua ujanja wetu wote ungeishia pale. Lakini wapi! Tulianza kuzama polepole tukiendelea kutembea. Munil alitangulia kuzama mzimamzima kwa sababu alikuwa mfupi kwangu.

    Huku akiendelea kunishika mkono, mimi nikazama polepole huku nikijiona hadi kufikia hatua ya maji kufikia kidevuni sasa yanaelekea midomoni!

    ?Munil,? nilianza kuita kwa tahadhari.

    ?Abee.?

    ?Nakufa.?



    Wakati nasema nakufa ndiyo maji yalikuwa yakigusa midomo lakini cha ajabu sikuona bughudha kwamba nashindwa kupumua kwa sababu maji yapo midomoni.

    Wote sasa tulizama ndani ya maji ya bahari tukaacha kutembea na kuanza kuelea mimi nikiwa nyuma yake. Tulielea kwa umbali mrefu hadi tukafika nje ya jumba moja kubwa likiwa mlemle ndani ya maji. Kwa haraka tu, nikakumbuka kuwa ni nyumbani kwa Munil. Ndiko tulikofika siku ile japokuwa mimi niliona ni nje nchi kavu.



    Kwa macho yangu niliweza kuona nyumba hiyo iko ndani ya maji tena yenye kina kirefu lakini maji yake kila nilipokuwa nikiyashika yaliteleza mkononi. Nilipoangalia juu nilishindwa kuona mawingu au anga.



    Munil alibonyeza kengele iliyokuwa ukutani kwa juu, geti kubwa likafunguka lenyewe, tukaingia humo. Cha ajabu kingine hata sebuleni mwa nyumba hiyo, vitu vilikuwa ndani ya maji. Hapo sasa tulikuwa tukitembea kawaida.



    ?Karibuni jamani karibuni,? yule mama wa Munil wa siku zile alitukaribisha akitokea chumbani. Alimkumbatia Munilw, akanifuata na kunikumbatia pia.[/COLOR]

    ?Poleni na safari.?

    ?Tunashukuru sana mama.?

    ?Shikamoo mama,? mimi nilisalimia nikiwa nakaa baada ya kuoneshwa kiti.

    ?Marhaba, karibu sana.?



    Munil alipitiliza, mama yake akamfuata. Hapo nikapata nafasi ya kutafakari na kuangalia mambo mengine zaidi. Pale sebuleni ni maji pande zote, juu yangu, chini, kulia, kushoto, mbele yangu na nyuma pia.

    Lakini nilikuwa nahema kama kawaida kama vile nipo nchi kavu. Nje ya madirisha makubwa ya vioo niliweza kuona samaki wakubwa kwa wadogo wakipita katika maisha yao ya kila siku.

    Mara nikasikia mlio wa kama wa mtu anayenitisha kutokea mlango mkubwa halafu nikaona maji yanasukumwa.



    ?Welelelewelelele,? sauti nzito ilisema. Jitu nene, refu likasimama mbele yangu, jicho lake moja tu lilikuwa kwenye paji la uso.

    Masikio yalisimama kama ya paka, ulimi wake ulikuwa nje muda wote huku meno yakiashiria kwamba yalichongoka kama misumari.









    Mapigo ya moyo yalikuwa yakinidunda, nilivyokuwa nikiliangalia lile jini, nilibaki nikitetemeka pale nilipokuwa nimekaa. Ni kweli kwamba nilizoea kuona vitu vya ajabu mbele yangu lakini kwa muonekano wa lile jini, nilitamani kukimbia.



    Lilikuwa limeingia ndani kwa kishindo kikubwa, mle ndani nikabaki nikiliangalia kwa hofu kubwa kwani kwa muonekano wake, endapo ningekutana naye katika ulimwengu huu, hakika ningekimbia.



    ?Karibu mume wangu,? alisema mama yake Munil.

    Hapo nikagundua kwamba lile jini kubwa lililokuwa limeingia alikuwa baba yake Munil.

    Halikuendelea kubaki kwenye hali ile kwani lilikuwa kubwa sana, ghafla katika hali ambayo sikujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, likaanza kupungua ukubwa huku likijitahidi kujirudisha katika hali ya kawaida.



    Ni ndani ya sekunde thelathini tu, likawa na muonekano kama binadamu wa kawaida.

    Toka nimezaliwa, niliwahi kupita katika vipindi vilivyonitia hofu kubwa, vilivyonifanya mpaka usiku kutokulala kwa raha au kuota njozi mbaya, lakini katika vipindi vyote hivyo, kipindi hiki kilikuwa kibaya zaidi.



    Leo hii ninaposikia mtu anawazungumzia majini, tena kwa lugha nyepesi kabisa ya kuona kwamba jini ni kiumbe wa kawaida huwa ninamshangaa, jini si kiumbe cha kawaida hata kidogo, ni kiumbe kinachotisha mno na kinaweza kukufanya kitu chochote kwa wakati wowote ule.



    Muonekano wa baba yake Munil haukuwa wa kawaida, kuna muda alionekana kuwa kawaida lakini kuna muda alikuwa akionekana kuwa mwenye hasira kali mpaka kufanya macho yake kuwa mekundu kama yalikuwa yakiwaka moto.



    Mabadiliko yake yalinishangaza lakini nikaupiga moyo konde kwa kujiambia kwamba hata iweje mahali pale, sikutakiwa kuonyesha hofu yoyote ile.?Mbona unataka kumuumiza mwenzako?? aliniuliza baba yake Munil, kwa hapa naomba nimpe jina la mzee.



    ?kivipi mzee?? nilimuuliza japokuwa kwa mbali nilikuwa na jibu la kile alichoniuliza.

    ?Kwa nini ulikwenda kwa watu wanaofanya maombi??

    ?Mimi??

    ?Kwani hapa naongea na nani??

    ?Nilikwishaongea naye nyumbani, nilimuomba msamaha kwani sikuwa nikijua hilo kwamba lingemuumiza,? nilimwambia huku nikionyesha hofu usoni mwangu.



    Kuna vitu vingi sana nilikuwa najifunza kupitia viumbe hawa waliojifanya kuwa na maumbo ya kibinadamu kumbe ni shetani wakubwa.



    Nilimuona mke wangu akiwa na nguvu kubwa, yaani ya kupotea hapa na kuibukia sehemu nyingine au kujibadilisha na kufanana na mtu mwingine kabisa. Sasa kitu nilichokuwa nikijiuliza, kama yeye alikuwa na nguvu nyingi, kwa nini alikuwa akihofia maombi? Je, maombi yalikuwa na nguvu kubwa kuliko yeye? Sikupata jibu.



    ?Acha kujiuliza maswali ya kipumbavu, hakuna kitu chenye nguvu zaidi yetu.?

    Bado walitaka kunionyeshea kwamba walikuwa na nguvu za juu sana, kila nilichokuwa nikijiuliza kichwani mwangu walikuwa wakinipa majibu kwa haraka sana.



    Siku hiyo nilishindwa kuwa na amani ndani ya nyumba ile, baada ya kukaa kwa dakika tano, Munil akakohoa na kuanza kuzungumza.?Nimemleta nyumbani hapa kwa sababu kuna mambo nataka tuzungumze,? alisema Munil.?Mambo gani?? aliuliza mama yake.



    ?Mmemgawia kiasi kikubwa cha fedha na hajui atafanyia biashara gani. Kichwa chake kimejijenga zaidi kwenye biashara ndogondogo na hajui ipi ni biashara ambayo inastahili kuanzishwa na mtu



    mwenye hela nyingi kama yeye,? alisema Munil.

    ?Hilo si tatizo. Kuna jingine?? aliuliza baba yake Munil.

    ?Hapana,? nikadakia.?Simama twende sehemu,? aliniambia baba yake.

    ?Twende wapi??

    ?Usiulize maswali, wewe twende.?

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka kuzungumza kitu chochote kile, nikasimama na kuanza kumfuata. Naomba niseme kitu kimoja, kule kuzimu nilipokuwa hakukuwa na utofauti na huku duniani, kila kitu unachokiona huku, na kule kipo.



    Kuna barabara nzuri za lami, kuna shule ambayo kila siku wanafunzi walikuwa wakienda kusoma, kuna kumbi za starehe, kuna pombe na vitu vyote vya anasa isipokuwa makanisa na misikiti.

    Tulitembea katika barabara moja, ilikuwa ni mchana wa kawaida sana. Njiani tulikuwa tukipishana na viumbe vya ajabu, vipo vilivyokuwa na sura za paka, ng?ombe, mbuzi na sura nyingine za kutisha.



    Hakukuwa na aliyekuwa na habari na mimi, kila mmoja alionekana kuwa bize na mambo yake, tulipotembea kwa umbali fulani, tukafika katika nyumba moja kubwa, nje kulikuwa na fimbo moja kubwa iliyosimikwa kwa nje,



    juu ya fimbo ile kulikuwa na chungu kikubwa kilichokuwa na michirizi ya damu pembeni, kwa jinsi akili yangu ilivyoniambia, chungu kile kilikuwa na kazi ya kuweka damu, maswali yaliyonijia kichwani, je mtu huyu alikuwa nani? Na nani alikuwa akiweka damu hizo kwenye chungu kile, sikuwa na majibu. Tukaingia ndani.









    Muonekano uliokuwa ndani ya nyumba ile ulinitisha, mapigo ya moyo wangu yalikuwa yakidunda kwa nguvu kana kwamba moyo ulitaka kuchomoka. Nyumba ile ilikuwa na mwanga hafifu ambao uliifanya hofu yangu kuongezeka zaidi.Sakafu ilikuwa nzuri yenye kung?aa lakini katika kila pembe ya



    nyumba ile kulikuwa kumesimikwa mti huku kukiwa na mafuvu ya watu yaliyowekwa juu ya miti ile.

    Nyumba haikuwa kimya, kulikuwa na sauti za ajabu zilizokuwa zikisikika kila sehemu, sauti zile hazikuwa



    za kawaida, kila zilipokuwa zikisikika, moyoni mwangu kuliongezeka hofu kubwa.Tukapiga hatua mpaka mbele ya mlango mmoja uliokuwa unaturuhusu kuingia ndani ya chumba kimoja, mlango huu uliandikwa namba zilizosomeka 666 ambazo kwa imani ya dini zilimaanisha kuwa namba hizo ni ujio wa shetani katika utawala wake mpya.



    Naomba nikwambie kitu kimoja. Japokuwa kipindi hiki nilikuwa na mke wangu ambaye nusu alikuwa jini na nusu mtu lakini nilifahamu sana kuhusu mambo ya dini, nilipewa uwezo huo kwa sababu majini yote kule kuzimu huwa yanafahamu maandiko kwa kuwa nayo wakati mwingine huyatumia hayohayo kuwapotosha watu.



    Mimi kama mtu mchafu niliyetawaliwa na jini ambaye niliishi naye ndani ya nyumba yangu, nilipewa uwezo wa kufahamu mambo mengi kuhusu dini zote na huku nikiyajua maandiko mengi kutoka katika Biblia au Koran. Huwa ni lazima majini au wachawi wafahamu mambo mengi kutoka katika vitabu hivyo kwa kuwa wao wenyewe wanatamani kuwateka watu wa Mungu kupitia vitabu hivyohivyo wanavyoviamini.



    Mara baada ya kusimama kwa sekunde kadhaa nje ya mlango ule, baba yake Munil akaufungua na tukaingia ndani. Hakikuwa chumba cha kawaida kama nilivyokuwa nikidhani, kilikuwa chumba kikubwa sana ambacho kwa ukubwa wake ningekifananisha na nusu ya uwanja wa kuchezea mpira wa miguu.



    Chumba kile kilitawaliwa na moshi uliokuwa ukifuka, kulikuwa na milio ya ajabu iliyokuwa ikisikika chumbani humo. Mbali na vitu vyote vya ajabu, kulikuwa na meza kubwa iliyokuwa imesheheni vikombe vya dhahabu, vikombe vile vilijazwa damu na sikujua ni nani aliyekuwa akitakiwa kunywa kwani hakukuwa na mtu yeyote tuliyemuona mahali pale.



    ?Karibuni sana,? nilisikia sauti ikitukaribisha.

    Haikuwa sauti ya kawaida kama binadamu wengine, sauti ile iliusisimua mwili wangu, nikahisi kijasho chembamba kikinitoka huku kwa mbali nikianza kutetemeka.

    Ilikuwa inatisha sana, nahisi kama ingekuwa katika ulimwengu huu wa kawaida, ningeweza kukimbia



    na kumuacha baba Munil peke yake.Ghafla tukafika katika sehemu iliyokuwa na kiti kikubwa kilichokuwa na kichwa cha ng?ombe kwa juu, kiti hicho kilipambwa kwa dhahabu huku pembeni, kwa chini, kuliwekwa ngozi ya binadamu na pale mbele yake kukiwa na meza iliyotengenezwa kwa mfano wa mgongo wa binadamu.



    Kiti kilikuwa wazi na baada ya sekunde chache, mwanaume mmoja akatokea mahali pale na kukaa. Sikuweza kuuona uso wake, ulikuwa umefunikwa na nguo moja kubwa mfano wa shuka jeusi, alipokaa kwenye kile kiti, akaikutanisha mikono yake.



    Mikono yake haikuwa ya kawaida, ilikuwa imejaa manyoya huku viganja vyake vikiwa na vidole zaidi ya kumi katika kila kiganja. Sura yake haikuwa ya binadamu, alikuwa na muonekano wa panya huku kichwani akiwa na mapembe matatu makubwa.



    Alichokifanya ni kulitoa lile shuka alilokuwa amejifunika, nilichokiona, kifua chake kilikuwa na tundu kubwa mithili ya kifuu. Macho yake yalikuwa makubwa yaliyoonekana kutisha mno, japokuwa nilikuwa nimeona viumbe vya ajabu na vyenye kutisha, naweza kusema kwamba huyu naye alinitisha sana.



    Alichokifanya baba Munil ni kukiinamisha kichwa chake kisha akapiga magoti na kumsujudia kiumbe huyo. Sikutaka kubaki kama nilivyokuwa, na mimi nilichokifanya ni kuinamisha kichwa changu na kupiga magoti chini.



    Mara nikasikia mshindo wa mtu, nikajua kwamba lile jitu la ajabu lilikuwa limetoka katika kiti kile na kuja kule tulipokuwa kwani nilikuwa nakiona kivuli chake kikianza kusogea tulipokuwa.

    ?Mnataka niwasaidie nini?? lilikuwa swali lake la kwanza kwetu.

    ?Tumekuja kuchukua ushauri wa kibiashara kutoka kwako,? alisema baba Munil.

    ?Mmekuja na sadaka??

    ?Hapana, ila tutakuja nayo baada ya kutupa ushauri.?

    ?Mnahitaji ushauri upi??

    ?Ushauri wa kibiashara.?



    Baada ya kiumbe yule kusikia hiyo, akapotea ghafla huku akituacha tukiwa tumeinamisha vichwa vyetu chini. Baada ya sekunde kadhaa likatokea tena na kututaka tuviinue vichwa vyetu.

    Alikuwa kwenye muonekano mwingine kabisa, hakuwa katika vazi lile kubwa lililoonekana kuwa shuka bali alikuwa amekuja huku akiwa kavaa joho kubwa kama wanalovaa wanachuo katika siku ya mahafali yao.





    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilipomuona, nilishangaa sana lakini baba Munil akaniambia kwamba kiumbe yule alikuwa amevaa vile kwa sababu alikuwa akiingia kwenye kazi ambayo mara nyingi hufanywa na watu wenye elimu ya juu hasa duniani.



    ?Kwa hiyo wanaamini ushauri hutolewa na wasomi tu?? nilimuuliza baba Munil kwa sauti ya chini.??Ndiyo, tena ushauri wa kibiashara wa matumizi makubwa ya fedha kiasi hicho ulichokuwa nacho,? aliniambia baba Munil.

    Kiukweli nikashangaa!

    ****

    Sikuacha kuogopa, bado niliendelea kuwa na hofu moyoni mwangu, mwili wangu ulinitetemeka huku kijasho chembamba kikiendelea kunitoka. Nilikuwa binadamu kamili, binadamu ambaye sikuzoea kuona majini, hata kama ningeishi kwa miaka mingi, bado ningeendelea kuogopa kila siku.



    Mungu ametupa uwezo mkubwa wa kuviona vitu vingi, majini huwa ni roho chafu, hivyo unavyoweza kuviona sehemu yoyote ile, kwa sababu macho yako hayana uwezo wa kuona roho chafu, hivyo unavyowaona tu, ni lazima utatishika.



    Mwanaume yule ambaye kwao alikuwa mshauri alikuwa akituangalia, sikuweza kumkazia macho kwa kuwa alikuwa na umbo baya na la ajabu, nilibaki nikimwangalia tu huku nikijifanya kutokuogopa chochote kile.

    ?Ni lazima mtoe sadaka,? alituambia mtu yule.

    ?Sadaka! Sadaka gani?? niliuliza.

    ?Ni lazima ipatikane sadaka ya damu, ushauri nitakaokupa, utakusaidia kuziendeleza fedha zako katika misingi mingi ya kupata faida,? aliniambia mtu yule.

    ?Anaposema sadaka ya damu, hata mbuzi au ng?ombe?? nilimuuliza baba Munil.

    ?Hapana, ni lazima awe binadamu, tunakupa silaha za kuweza kuwamaliza, utazitumia katika kutuletea hiyo sadaka,? aliniambia kiumbe yule.



    Sikuwahi kuua, nilisikia tu kwamba watu walikuwa wakitolewa kafara lakini kwangu, sikuwahi kufanya kitu cha kikatili namna hiyo. Baada ya sekunde chache, kiumbe kile kikaanza kuzungumza maneno ambayo sikuyaelewa, ndani ya muda mchache tu, kitu kama kisu kikatokea mkoni mwake na kisha kunigawia.



    ?Utatumia hiki kutolea sadaka,? aliniambia kiumbe kile. Tukaondoka zetu.

    Sikutaka kuendelea kukaa huko kuzimu, nilichokifanya ni kumfuata mke wangu na kumwambia kwamba ilitupasa kuondoka mahali hapo, tukaaga na kuelekea kule tulipoingilia, baada ya hapo, ghafla tukajikuta tukiibukia kutoka baharini, japokuwa tulikuwa ndani ya maji, hatukuweza kulowa.

    ****



    Kuna vitu vingi sana vilikuwa vikinitatiza, nilikuwa nikimfikiria mke wangu na uwezo wake aliokuwa nao. Mimi nilikuwa binadamu, nilikuwa na uwezo wa kibinadamu, sasa inakuwaje leo hii nikubali kuoana na jini?



    Ukweli toka moyoni mwangu, sikuwa mtu huru, kila nilichokuwa nikikifanya, niliamini kwamba mke wangu alikuwa akiniangalia kwani matukio kadhaa ya nyuma yaliyokuwa yametokea yalidhihirisha hilo.



    ?Nitaishi hivi mpaka lini? Lini nitakuwa binadamu mwenye uhuru na maisha yangu?? nilijiuliza maswali mfululizo lakini sikupata jibu.



    Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu, kuanzia siku ile ambayo tulitoka kuzimu niliendelea kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu. Sawa, mke wangu Munil alinifanya nipate fedha nyingi ambazo sikuwahi kuota hata siku moja kwamba ningezipata, lakini bado sikuwa na amani katika kufanya matumizi ya fedha zile.



    Upande huu ulikuwa na mapenzi na upande mwingine ulikuwa na utajiri. Pande zote hizo nilikuwa nikizitumikia lakini kulikuwa na upande mwingine ambao ulikuwa wa muhimu sana, upande ambao haukuonekana na mtu yeyote zaidi yangu, uhuru.



    Nilihitaji kuwa huru, nipendwe lakini na binadamu wa kawaida na hata kama siku nikipata utajiri basi uwe ule usiokuwa na masharti. Nilihitaji uhuru, sikutaka kuendelea kuishi katika maisha yale tena.

    Kuwa na fedha, ukapendwa vinaweza kuwa si vitu bora kama ukikosa amani na uhuru. Kuna watu



    wana ngapi wana fedha lakini wamekosa uhuru? Wamepata fedha nyingi na kuambiwa walale chini? Utajiri gani sasa? Kwangu, sikutaka nipate utajiri wa namna ile kwani japokuwa vitu hivyo havijaanza, niliamini kwamba naweza kutoka na kujiweka huru.



    ?Haiwezekani, siwezi kuendelea kuwa mfungwa wa nafsi yangu!? nilijisemea, kipindi hiki, kauli yangu hiyo ilikuwa ni yenye kumaanisha, nilitaka kuwa huru, niwe kama binadamu wengine.







    MOYONI nilidhamiria kwa asilimia mia moja kwamba ilikuwa ni lazima nirudi katika maisha niliyokuwa nikiishi awali, hata kama nilikuwa na fedha, kwangu hazikuonekana kuwa na umuhimu wowote ule kama ningeendelea kuishi maisha na mke ambaye alikuwa nusu jini nusu mtu.



    Mimi kama binadamu, nilijua fika kwamba Mungu aliniumba ili nimuabudu na alijisikia wivu sana kumuona mwanadamu aliyemuumba akimuabudu mtu mwingine tofautu na yeye, hivyo nilitaka kubadilika.



    Nilikuwa radhi kupoteza kila kitu maishani mwangu, sikujali sana kuhusu fedha wala utajiri wa jumba la kifahari nililokuwa nalo. Hakuna aliyezaliwa na fedha, wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu lakini kadiri tulivyoendelea kukua, watu wakajipanga na kupata mafanikio, hivyo na mimi nilitakiwa kufanya hivyo.



    ?Maisha ya huku yanatesa, mambo ya kusafiri na kwenda kuzimu, siyataki tena, ni bora nipoteze kila kitu, lakini si kuendelea kuishi katika maisha haya,? nilijisemea moyoni mwangu.

    Niliendelea kujifikiria mengi chumbani nilipokuwa, nilikuwa na mawazo mengi kwani kitu nilichoamua



    kwenda kukifanya kilikuwa ni hatari sana katika maisha yangu. Nilijua kwamba kuna mambo mawili yanaweza kutokea endapo tu ningeamua kuyabadilisha maisha yangu na kumuabudu Mungu wa kweli.



    Jambo la kwanza nilijua fika kwamba ningepoteza kila kitu, kuanzia nyumba, fedha, magari na vitu vingine lakini jambo la pili ambalo lilianza kunitisha ni kwamba endapo mke wangu angejua kile nilichokuwa ninataka kukifanya, basi angeweza kuniua.



    ?Mume wangu! Mbona una mawazo sana, tatizo nini?? aliniuliza Munil, alikuwa ameingia chumbani hapo akitokea sokoni.

    ?Hakuna tatizo, bado nazifikiria hizi fedha ni nyingi mno, lazima nitoe kafara kwani haiwezekani nikakosa matumizi ya fedha hizi,? nilimwambia Munil.



    ?Kama ulivyoambiwa, fanya hivyo, nakuahidi kwamba utakwenda kuwa na fedha nyingi kuliko kawaida na watu wote watakushangaa, utajiri wako utaongezeka maradufu,? aliniambia.

    ?Mke wangu! Asante sana kwa kunisaidia, hakika umeyabadilisha maisha yangu kutoka katika umaskini na kufikia hapa nilipo,? nilimwambia.

    ?Usijali, tupo pamoja mume wangu! Hakika siwezi kukuacha ukiteseka,? aliniambia.



    Hapa kuna swali nilikuwa nikijiuliza ambalo lilikuwa likijirudia mno kichwani mwangu. Nakumbuka kipindi cha nyuma, kwa nilichokuwa nikikiwaza, mke wangu alikuwa akikijua na aliniambia kwamba nilikuwa nikiwaza nini, cha kunishangaza katika kipindi ambacho nilichukua uamuzi wa kuyabadili maisha yangu na kumuabudu Mungu, hakuweza kuligundua hilo.



    Hapo ndipo nilipopata jibu kwamba Mungu alitenda miujiza kwa nafasi yake, hakutaka mke wangu ajue kile nilichokuwa nikikifikiria kwa wakati huo kwani endapo angejua ilikuwa ni lazima aniue.

    Siku iliyofuata kwa miguu yangu nikaanza kutafuta kanisa lilipokuwa. Nilikuwa nikitetemeka sana,



    kijasho chembamba kikinitoka huku kila wakati nikiwa na hofu kubwa. Sikuchukua muda mrefu, nikafika katika kanisa moja lililoandikwa Praise And Worship, nilisikia sauti za watu wakiimba, nilichokifanya, nikaingia ndani.



    Nilipokanyaga ndani ya kanisa lile, sikujua ni kitu gani kiliendelea. Ila nilipopata fahamu, nilikuta watu wakiwa wamenizunguka kila mmoja akikemea.

    Nilibaki nikiwa na mshangao hali iliyonifanya niulize.

    ?Ulikuwa na mapepo ila Mungu ameyatoa, jina lake lihimidiwe,? alisema mchungaji wa kanisa hilo.

    ?Nilikuwa na mapepo?? niliuliza kwa mshtuko.

    ?Ndiyo! Nini kilitokea maishani mwako mpaka kuwa na mapepo mengi kiasi kile??



    Hapo ndipo nilipoanza kusimulia historia ya maisha yangu. Wengi walishtuka kwani hawakuamini kama binadamu wa kawaida ningeweza kumuoa jini na kuishi naye kipindi hicho bila kunidhuru.

    Kuanzia siku hiyo, nikayabadili maisha yangu, niliporudi nyumbani, sikulikuta gari langu na hata

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nilipoingia chumbani na kulifungua kabati langu lililokuwa na fedha, lilikuwa tupu kabisa ila nilifurahia kwani hata mke wangu, hakuwepo.



    Sikujali, japokuwa nilikuwa nimepoteza vitu vingi maishani mwangu, ila nilifurahi kwa sababu nilikuwa huru, nikaanza kuwa mtu wa kwenda kanisani na kushiriki katika vipindi vyote vya maombezi.



    Mke wangu Munil hakurudi tena, sikuwa kama nilivyokuwa, nilikuwa mtu mwenye nguvu za Mungu zilizojengwa na maombi mazito niliyoomba kila siku.

    Katika maisha yangu, nilimshukuru Mungu kwa kuniokoa kutoka kwa mke wangu ambaye alikuwa Nusu Mtu, Nusu Jini.



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog