IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO
*********************************************************************************
Simulizi : Osaka Mji Ulio Potea

Sehemu Ya Kwanza (1)
Dira ya maisha ilipoteza majira upande wake akiwa kijana mdogo kabisa mwenye umri wa miaka kumi na tano, ni baada wazazi wake wote wawili kufariki kwa nyakati tofauti tofauti baada kupata virusi vya ukimwi.
Alibaki na wadogo zake wawili, wa kike na wakiume. Maisha waliyo ishi yalikuwa magumu sana, ndugu jamaa hawakuwajali licha ya upweke walio kuwa nao. Lakini licha ya kuishi maisha hayo jambo moja ambalo Alexandra alizingatia ni kuwapenda vilivyo wadogo zake, na kuwatia moyo pindi walipo hisi huzuni. Lakini pia kijana huyo aligeuka kuwa mbogo alipoona au kusikia wadogo zake wameonewa.
Aliyafanya hayo kwa kutekeleza husia alioachiwa na marehemu mama yake. Kuwapenda kuwathamini na kuwalinda wadogo zake kwa kuzingatia kuwa sasa yeye ndiye pekee aliyebakia kuwa kama mama kama baba pia.
Alipo timiza miaka kumi na tisa, hapo sasa alikuwa kimawazo na kifikra. Siku moja alilipata wazo, wazo tata la kusafiri kuelekea jijini Arusha kutafuta maisha akiamini kuwa kule maisha yanaweza kumnyookea akapata kuishi maisha mazuri pamoja na wadogo zake.
" Wazo hili ni nzuri sana. Naweza kutusua maisha japo kuna ugumu mkubwa ndani yake. Lakini sitojali, ngoja nitajaribu kuwashirikisha wadogo zangu ili nisikilize watasema nini" aliwaza hilo suala akiwa kitandani akisaka lepe la usingizi baada shughuli za kutwa nzima. Fikra zanke zililenga kuwa mafanikio ya maisha yake hayapo kijijini bali yapo mjini pekee.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jambo hilo alipo lifikisha kwa wadogo zake liliwashtua, lakini aliwautiliza na kuwapa imani kuwa atarudi haijalishi atakuwa katika hali gani ya kimaisha.
Kwa shingo upande walikubaliana naye, kwahiyo akangoja ile siku aliyo pania kuelekea jijini kutafuta maisha.
Siku husika ilipo wadai, asubuhi moja alfajiri kabisa iliyo tawaliwa na mawingu mazito. Alexandera aliamka na kuweka mambo sawa kwa dhumuni la kuanza safari. Alichukuwa begi lake ambalo lilikuwa limechakaa, akatupia nguo mbili tu alizo kuwa nazo, suruali na flana ambazo nazo pia zilikuwa kuu kuu. Kila kitu kilipokuwa tayari akawamsha wadogo zake kwa dhumuni la kuwaga, walimtakia safari njema kwa masikitiko makubwa sana, walilia kabisa.
Rohoni alimuuma sana kuwaacha wadogo zake, lakini kwa kuwa mpenzi wake aliyeitwa Emakulata naye alifika kuja kumuaga ikabidi awaambie kuwa Emakulata yupo atakuwa akiwasaidia. "Mnapaswa kukunjua roho zenu basi. Maana endapo kama mtazikunja huwenda nisifanikiwe" aliongeza kusema.
"Wala halina shida, lakini cha kuzingatia usitusahau kumbuka umeacha wadogo zako, lakini pia umeniacha mimi mapenzi wako ambaye bado tuna ndoto ya kuwa mke na mume miaka kadhaa ijayo" alisema Emakulata kwa sauti ya chini iliyo jaa simanzi kubwa.
"Hilo haliwezi kotokea, nawapenda sana wadogo zangu. Lakini pia nakupenda sana mpenzi wangu, kamwe ndoto yetu haiwezi kutimia pasipo kuwa na kipato cha kutosha. Ngoja nikazisake ila nitarejea"
Kwa kuwa Emakulata alikuja kwa kutoroka, Alexandera akamwambia arudi nyumbani maana mzee wake alikuwa mkali kweli kweli. Ndipo wote kwa pamoja wakamkumbatia, walipo ng'atuka kwenye mwili wake kijana akaanza safari.
******
Usafiri wa magari kutoka kijijini kweo kwenda Arusha mjini ulikuwa ni nadra sana, ulikuwa wa kuvizia.
Wakati anatembea kuelekea barabarani kusubiri gari, kwa mbali alisikia sauti ya gari, lilikuwa lori, mlio wake ulidhilisha kabisa limebeba mzigo.
Allipofika barabani alipunga mkono ishara ya kulisimamisha, nalo likasimama.
"Nafika Arusha mjini kaka" alimwambia dereva.
Dereva yule akamjibu "Kama unashilingi buku tano panda juu ukazibe" pasipo kupoteza muda alizunguka nyuma akapanda juu kwenye mzigo uliokuwa umepakiwa kwenye lori lile na safari ikawa imeanza kuelekea jijini Arusha. Alipokuwa kwenye gari roho ilmuuma sana kukiacha kijiji chake na kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine, mahala asipokuwa na ndugu. Lakini pia mbali na hilo, alihuzunika kuwaacha wadogo zake peke yao, Angel mwenye umri wa miaka kumi na tano pamoja na Carlos mwenye umri wa miaka saba. Baada kuwaza sana hatimaye usingizi ulimpitia aliamshwa na tan'boy baada kufika jijini, ilikuwa yapata saa nane mchana.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Umefika, telemka ili mzigo ushushwe" alisema tan'boy. Alexandera alikurupuka akaangaza macho huku na kule, taswira ilikuwa tofauti kabisa na ile aliyo izoea. Majengo na wingi wa watu watanashati warembo, vyote hivyo alivyokuwa akivitazama akiwa amesimama kwenye nondo za gari vilimfanya kutaharuki.
"Unaonekana ndio mara yako ya kwanza kuja kwenye jiji hili" tan'boy aliongeza kusema, akacheka kidogo kisha akaendelea "Karibu sana, jipange kijana, maana wahenga wanasema, mjini njoo na akili yako tu vingine vyote utavikuta huku huku. Karibu unaweza kujumuika na vijana wenzako kushusha mzigo huu na kuingiza soko kubwa ili upate pesa ya kuanzia, lakini pia sio lazima. Ahahaha" alimaliza kwa kicheko tan'boy yule.
Maneno ya tan'boy yalimfanya Alexandera kujawa na sintofahamu kubwa kichwani mwake, lakini hakutaka kujaji sana. Upesi aliruka mpaka chini, akavaa begi lake ambalo lilionekana kuchakaa. Hakujua aanzie wapi wala aishie wapi, ni kama dira yake ilipoteza majira kabisa.
Alitulia pale pale sokoni mpaka jioni, ni muda ambao jiji la Arusha linakuwa limechangamka vilivyo. Taa za barabarani miundo mbinu ya hali ya juu namna jiji lilivyo jengeka, magari na watu wengi ilipelekea jiji kupendeza vyema.
Alijichomoa kwenye moja ya kibanda cha mgahawa pale sokoni, akaingia mtaani kutembea sehemu mbali mbali. Kulishangaa jiji. Ilipo timu mnamo saa saba, alihisi kuchoka, pia mboni zake zilihisi usingizi mkali sana. Kwa kuwa hakuna na mahala pa kulala, alitamani kuona sehemu yoyote iliyo jificha ili alaze mbavu akingoja kesho yake aanze rasmi kazi ya kusaka kibarua.
Akiwa amesimama barabarani, upande wa mkono wa kulia aliona uchochoro. Upesi akaelekea huko kuufuata uchochoro ule. Mbele zaidi alikutana na jumba bovu, ndani ya jumba lile palikuwa na vijana wasio pungua watatu, walikuwa wameuchapa usingizi.
Hakutaka kusema nao, alichukuwa kipande cha box akatandika sehemu akalala.
Ilikuwa ngumu kupata usingizi, ni maisha ambayo hakuyazoea, kulala mazingira yale ilimuwe vigumu sana hasa hali ya ubaridi iliyo kuwepo ndani ya jiji lile. Lakini baadaye usingizini ulimpitia, hapo alilala fo fo fo. Usingizi mzito ulio ambatana na njozi mbalimbali, lakini ghafla alikatishwa usingizi wake baada kuguswa makalio. Aliyafumbua macho yake upesi ili kumjua mtu anayetaka kumfanyia ushenzi ule. Macho yake yakakutana na uso wa mwanaume mmoja mwenye uso mgumu mithili ya kiatu cha baniani.
"Ahahaha hahahaha" Aliangua kicheko cha madaha mwanaume yule, akavuta sigara kisha moshi akampulizia usoni na kusema "Inaonyesha wewe ni mgeni mahala hapa, umevamia kambi kinyemela. Je, unaweza kusema umetumwa na nani kuja kutuchunguza?"
Maneno hayo na namna jamaa alivyokuwa akiongea ilimpelekea Alexandera kuogopa, isitoshe mbali na mwanaume huyo kumtilia shaka. Kando kando walionekana wanaume wengine wasio pungua saba, walionekana kuwa na miili iliyo jengeka kimazoezi vile vile walikuwa wakivuja jasho ikiwa chini ilionekana mizigo mbalimbali, mabaro ya nguo na tv kadhaa dhahiri shahili wanaume hao walikuwa wametoka kupora muda ule. Vile vile mbali na vidume hao vya mbegu, punde si punde wanaume wale wengine waliokuwa wamelala waliamka.
"Huu ni uzembe, mnashindwa kulinda kambi kwa umakini? Anaingia mtu kinyemela wala hamna habari" aliongeza kusema mwanaume yule akiwafokea vijana wake alio waacha kwa dhumuni la kulinda kambi.
Alexandera alijitetea, hakusita kuomba msamaha lakini pia akaahidi kuondoka usiku ule ule.
"Chifu, muda sio rafiki kwetu. Unajua Don Domic anasubiri simu yetu kabla hapajambazuka" mwanaume mmoja kati ya wale walio simama alisema, punde akachomoa upanga na kumkabidhi mwanaume yule aliyekuwa akimuhoji Alexandra kisha akaongeza kusema "Tenganisha kichwa na kiwili wili, ni kosa kubwa kumuacha mtu huyu akiwa hai kwani hatujui nini dhamira yake. Tusipo ziba ufa tutajenga ukuta. Adhabu kuu ya hawa wenzetu watatu walio fanya kosa la kizembe ni kwenda kuutupa mwili nje ya jiji"
Mwanaume yule aliupokea upanga, jina lake aliitwa Derrick, bonge la jitu la miraba minne. Kwa mkono wake wa kulia ulio shona misuli akaukamata upanga tayari kwa dhumuni la kumuua Alexandera kijana mtafutaji aliye kosea kambi kwa bahati mbaya. Lakini kabla Derrick hajafanya mauaji, ghafla akasikia sauti ikikemea "Hakuna kufanya ubaya kwa mtu huyu" alikuwa moja ya vijana wake kati ya wale alio toka nao kupora.
"Wewe kama nani unapingana na Derrick?" kijana yule aliye mkabidhi Derrick upanga alihoji wakati huo Mr. Derrick kiongozi mkuu wa kundi hilo akionekana kumtazama kijana wake kwa jicho kali lililo fifizwa na giza totoro.
"Naongea mimi kama Saigon, narudia tena kusema. Hauwawi mtu hapa" alijibu kwa msisitizo kijana huyo na kisha kumuamlisha Alexandera asimame.
"Ahahaha hahaha" aliangua kicheko cha dharau Derrick, akaimgiza mkono kwenye mfuko wa koti lake akatoa sigara akaitupia kwenye kinywa chake, njiti ikafyatuliwa njiti na kijana wake na kuupeleka moto kwenye sigara iliyopo kwenye kinywa cha Derrick, akavuta pafu tatu mfululizo kisha akamgeukia Saigon akampulizia moshi usoni kisha akasema "Naam! Sasa umekua., vijisenti tunavyo kupatia vinakupa jeuri. Lakini Saigon, siku zote yakupasa kujua kuwa kinyago ulicho kuchonga kamwe hakiwezi kukutisha. Maana yangu, wewe ni kama kinyago changu, hivyo basi huwezi kunitisha. Lazima nikutangulize kuzimu"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Pokea hii kwanza" aliongeza kusema Derrick sambamba na kumrushia ngumi Saigon, ngumi hiyo nzito kutoka kwa Derrick ililenga kifua chake mahali ulipo moyo. Lakini kabla haijamfikia, akaidaka. Ghafla macho yake yalibadilika, yaliwaka mwanga wa mwekundi. Kitendo hicho kikadhilisha kuwa Saigon sio binadamu wa kawaida, kwa maana hiyo Derrick ameingia choo cha kike..
Mkono wake ukahisi ganzi, mwili mzima ukajaa ubaridi. Alipoa mithili ya maji ya mtungini wakati huo vijana wengine walionekana kushangaa tu hata wasiwezi kufanya jambo lolote lile.
"Cheza na watu wengine usicheze na mimi, unapo jaribu kupewa heshima basi usimdharau yule anaye kupa heshima, nitakupoteza Derrick" Saigon aliongea wakati huo yale macho yake yaliyokuwa yamebadilika rangi yalikuwa tayari yamelejea kama awali. Ni kama Derrick aliduwaa, alikaa kimya kwa muda wa dakika mbili. Baada kurudi katika hali ya kawaida akamshika mkono Alexandra akamkumbatia, lakini pia akampa nafasi mbili za wazi kuondoka mahala pale au kujiunga nao.
"Jina langu naitwa Alexandra, nimekuja kutafuta maisha ili niwatunze wadogo zangu. Nipo tayari kuungana nanyi kusaka shilingi, nawaahidi sitowaangusha nitatoa ushirikiano mkubwa" Alisema Alexandra. Vidume vyote kwa pamoja vikampigia makofi, walishangilia kuona kijana mwenzao kakubali kuungana nao. Ila mbali na suala hilo, Derrick hakujua ni namna gani alivyo badilishwa mawazo na Saigon kwani dhumuni lake lilikuwa ni kumuua Alexandra wakiamini kuwa kijana huyo endapo kama ataruhusiwa kutoka katika kambi yao anaweza kutoa siri mwishowe ikawa patashika upande wao.
"Naitwa Duma karibu sana jisikie upo nyumbani"
"Jina langu Sam karibu sana mzee"
"Mimi ni Pablo"
"Naitwa Juva" vidume vyote viliendelea kujitambulisha kwa Alexandra, walikuwa ni zaidi ya wanaume kumi na mbili, shughuli yao kubwa ilikuwa ni kuvunja maduka na kupora lakini walifanya kazi za kusambaza madawa ya kulevya.
Muda mchache baada zogo kutulia, barabarani ilisimama gari aina ya Noah yenye rangi nyeusi wakati huo huo simu ya Derrick ikaita, upesi akaichomoa kwenye koti lake kubwa jeusi akaweka sikioni "Oky" alisema sambamba na kukata na kuirejesha mfukoni kisha akawaambia watu wake wabebe mizigo kuipeleka mahali ilipo gari lile.
Upesi upesi walifanya hivyo, zoezi lilipo kamilika gari ile ikaondoka ikiambatana na Derrick, Saigon pamoja na Alexandra ingizo jipya huku nyuma vijana wengine nao wakisambalatika kama ambavyo hufanya kila iitwayo leo. Taarifa ilipo mfikia Dominic aliwaka, alifoka na kumtupia lawama Derrick.
"Ni vigumu sana sana mtu kama wewe kumuamini mtu kwa usiku mmoja. Unafanya nini ndugu yangu?" alisema Don Dominic sanjari na kukunjua mguu aliokuwa amekunja mkao wa nne kwenye sofa huku walimbwende wawili wakichezea mabega yake.
"Inatubidi tujitasmini" aliongeza kusema, muda huo Derrick alikaa kimya, hakusema neno lolote.
"Lakini bosi anaonekana yuko fiti anaweza kuwa msaada siku za usoni" Saigon alidakia.
"Mpe nafasi atatufaa sana" aliongeza kusema. Dominic akamtazama kwa jicho pembe, akanywa bunda mbili ya bia iliyokuwa kwenye grasi aliyo shika mkononi. Alipo meza akasema "Sina ubaya na wala siwezi kupingana na mawazo yenu, huwenda ila nimeongea kwa tahadhari lakini pia lazima ajaribiwe kwanza kisha tusaini naye mikataba"
"Mruhusu aingie" aliongeza kusema Don Dominic au DD kama watu wake walivyo penda kumuita.
Dominic ni kijana nguli anaye jihusisha na masuala ya uporaji na uuzaji wa madawa ya kulevya. Aliajiri vijana wengi kwanye kila kitengo, kitengo cha uporaji aliajiri vijana na upande wa kusambaza madawa pia. Kitendo cha Derrick kijana aliye mteua kuwa kiongozi wa vijana wenzake kuamuwa kumleta kijana mwingine kilimtia shaka, lakini baada kutulizwa akahitaji kijana huyo amfanyie majaribio kwanza.
"Karibu katika himaya ya Don Dominic, jisikie upo nyumbani kijana" aliongea kwa tabasamu bashasha Dominic akimkaribisha Alexandra. Ilikuwa ni ndani ya jengo ndefu kiasi, kuta za jengo hilo zilionyesha kuchakaa kiasi kwamba ilibainisha kwamba jumba lile lilikuwa la kare. Lakini maandhali ya ndani yalionekana kupendeza, ndani jumba lilipambwa marashi mbali mbali sanjari na wale warembo waliokuwa wakimnyoosha nyoosha Dominic.
"Asante sana" aliitikia Alexandra akianza kwa kushusha pumzi ndefu.
"Aah.. Unaitwa nani wewe" aliuliza Dominic.
"Naitwa Alexandra" alijibu kijana.
"Ahahaha hahaha, safi jina nzuri sana, unaonekana shupavu pia licha ya jina konk ulilo nalo. Aaah, karibu. Na kukaribisha mara nyingine tena, najua umekuja kutafuta maisha hapa mjini, siku zote mwanaume hula kwa jasho. Ukiwa na mimi hesabu umesikini umekwisha utatembelea gari kali utakula chakula unacho kitaka endapo tu utajituma na kutekeleza maelekezo, vile vile kudumisha uaminifu "
" Karibu uketi "aliongeza kusema Don, kwa hofu na mashaka makubwa Alexandra akaketi mazungumzo kadha wa kadha yakafuatia yakisindikizwa na kinywaji baridi. Kwa kuwa hakuwa muumini wa kilevi chochote alikunywa soda.
Siku zilisogea, kila kundi la Dominic lilipokwenda kuiba akiambatana nao. Kijana alilidhia kufanya kazi ile wala hakujali au kuhofia kitakacho mtokea. Hatimaye alizoea, alitumia vilevi, hakusita kuchukuwa Malaya na kulala nao kama walivyokuwa wakifanya akina Derrick, Saigon na watu wengine waliokuwa kwenye kundi la Don Dominic.
Miezi mitatu ikakatika, hatimaye Alexandra alizoea uhalisia wa maisha hayo ya ujambazi. Usiku mmoja wakupumzika walipokuwa bar wakipata moja moto moja baridi baada ya mihangaiko ya hapa na pale, Derrick alimdokeza Alexandra kuwa usiku wa siku huo ndio wa kumpa mtihani baada hapo awali kutaka kumjaribu, lakini mpango ukawa umeota mbawa kwani hakuwa na uzoefu wowote katika mambo hayo. Hivyo basi baada kupata uzoefu, hatimaye ukafika ule muda wa kumjaribu.
"Unatikiwa kunywa kistaarabu" aliongeza kusema Derrick. Muda huo huo Derrick anamuasa Alexandra, ghafla Saigon akajihisi kusisimka. Kijana huyo mwenye maajabu ndani ya mwili wake akahisi balaa kubwa linatarajia kutokea. Ndani ya ubongo wake upesi upesi akapata wazo la kuwaasa wenzake waondoke. Nao walitii, walipanda gari lao, muda mfupi baadaye gari mbili za polisi zilifika mahala hapo. Zilikuwa zimesheheni polisi ambao walikuwa wamebeba bunduki aina mbalimbali mbavu mwao ni baada kupenyezewa taarifa kuwa kundi la Don Dominic lipo eneo hilo.
"Bahati yao, tungekula nao sahani moja mbweha hawa" inspekta aliyeitwa Egon alisema kwa hasira ikiwa muda huo huo inspekta Jeff naye alifika na pikipiki kubwa aina ya HONDA, ilikuwa ikitema mfuke huku ikilia mlio wa uchu.
"Wameondoka hivi punde tu" alisema Inspekta Egon alimwambia Jeff.
"Anhaa bila shaka tumepita njia tofauti ndio maana hatujaweza kukutana nao, lakini hilo lisikupe tabu kamanda hebu subiri" alijibu Inspekta Jeff sanjari na kuzipiga hatua kuingia ndani ya bar ile iliyoonekana kushueheni watu. Alitazama huku na kule, ndani ya ubongo wake akapata picha kamili namna ambavyo kundi lile la Don Dominic lilivyo ingia na kutoka na kutoka.
Alifuata picha harisi ya za fikra zake mpaka kwenye meza aliyokuwa ameketi Saigon, alipo kigusa kiti akahisi jambo fulani la ajabu. Upesi akatoa mkono wake kwenye kiti hicho na kuutazama kwa kina, ajabu akaachia tabasamu bashasha wakati huo, ghafla macho ya kamanda huyo yakageuka rangi yakaeaka mithili ya macho ya Simba ingawa hakuna mtu hata mmoja aliyegundua jambo hilo tata. Ndani ya ubongo wake akapata data kamili walipo watu hao. "Ahahahah ahahaha" akacheka kwa madaha Inspekta Jeff kisha akasema "Vizuri sana, kumbe upo huku! Mshenzi wewe kama ulifanikiwa kunikimbia OSAKA basi huku nitakula na wewe sahani moja" alipokwisha kusema hivyo upesi akatoka ndani bar ile, akapanda pikipiki akapiga kiki moja chombo ikawaka, kwa mbwembwe nyingi akaondoka mwendo wa ajabu kulifuata kundi lile la Don Dominic huku moyoni akiwa na shauku na hali mpya ya kulipata ili amkabili mtu yule aliye mkimbia Osaka mji ulio potea miaka mingi iliyo pita!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati Inspekta Jeff analifuata kundi lile la Don Dominic, upesi vijana hao walikata kona kuelekea kiwanja kingine kabla hawajampeleka Alexandra sehemu husika anapo takiwa kwenda kufanya jaribio lake.
Walionekana kufurahi wakati wote waliangua vicheko, muziki mkubwa ulisikika. Zilipigwa ngoma mbali mbali za America, hip hop, rnb na nyimbo nyingine kadha wa kadha. Hata hawakuwa na habari kama kuna mtu wa ajabu anawafuatilia. Hatimaye walifika eneo husika, ilikuwa sehemu yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, lakini mkusanyiko huo ulipungua pindi kundi hilo lilipo wasili eneo hilo.
Derrick aliketi kwenye meza yake, vijana nao waliketi kwenye meza zao kisha muhudumu aliyekuwa akihudumu kwenye bar ile akafika upesi kusikiliza mahitaji yao. Bosi alikuwa ni Derrick, hivyo akaongea pia vijana wao nao wakatoa hitaji lao ikiwa upande mwingine Inspekta Jeff alionekana kusimama huku pikipiki yake ikiendelea kutoa mlio, kichwani alikuwa akifikiria, aliwaza na kuwazua aende wapi kwani alikuwa panda njia.
Alitumia dakika tatu tu, alitumia uwezo wake wa ajabu kutazama wapi walipo elekea vijana wale wakati huo moyoni akiwa na shauku kubwa ya kukabiliana na adui yake aliyemkimbia Osaka. Alipo pata jawabu, akawafuata. Kama ilivyo kuwa ada, Saigon kijana mwenye maajabu alihisi jambo, safari hiyo nywere zilimsisimka kitendo kilicho pelekea akumbuke jambo lililo wahi kumkuta pindi alipo jihisi hali kama hiyohiyo ingawa aliipumzia. Jambo hilo lilitokea miaka takribani mia tatu iliyo pita, zamani sana huko Osaka.
"Derrick, acheni kufanya Upuuzi hapa sio salama yatupasa kuondoka upesi" alisema Saigon kwa sauti ya juu kabisa. Lakini jambo hilo Derrick hakukubaliana nalo. Alikataa katu katu, zaidi alinyanyuka kwenye kiti akamfuata na kumwambia "Unajifanya wewe una mashetani bro, kumbuka mimi ndio kiongozi wako baada ya DD. Hivyo basi unatakiwa kuwa mpole na uwe naheshima. Siku ya leo ni muhimu kwetu, usitupelekeshe"
Maneno hayo yalimfanya Saigon kushindwa kuongeza neno, alisimama tu wakati huo mwili ukizidi kumsisimka. Moyoni mwake alikosa amani kabisa, ndipo kwa mara nyingine tena akamwambia Derrick waondoke, kitendo hicho kilipelekea Derrick kumpiga chupa kichwani ila kabla chupa hiyo haijagusa kichwa chake, upesi alipotea akaibukia sehemu nyingine ikiwa muda huo huo Inspekta Jeff alifika eneo la tukio.
Alishuka kwenye pikipiki yake, akaizima sambamba na kuelekea ndani ya jengo lile walilo kuwemo Saigon na wenzake. Kila alipo kanyaga hatua moja, hatua iliyo fuata yaani ya pili alipotea. Hivyo hivyo mpaka akaingia ndani ya jengo, pasipo kuuliza alimpiga risasi moja ya vijana wa Dominic, mlio wa risasi ukapelekea kuzuka sokomoko. Waliogopa, kila mmoja alikimbia alipo pakua yeye ikiwa yote ni shauri ya kuokoa uhai.
Kwa kuwa jopo la watu lilikuwa wengi, ilimuwea vigumu Inspekta Jeff kumpata adui yake haswa haswa. Saigon alitoweka katika mazingira tatanishi, si yeye tu bali hata Derrick naye aliondoka pamoja na vijana wake kasoro yule aliye pigwa risasi.
Waliendesha gari lao kwa kasi ya ajabu wakati huo huo nyuma Inspekta Jeff alikuwa akiwafuatilia kwa mara nyingine tena.
Kamanda huyo alipiga risasi tatu mfululizo, mwisho likatokea jambo. Risasi moja ilipasua gurudumu huku risasi nyingine nayo ikienda kumpata Saigon kwenye bega, vurugu kali iliyopelekea gari kuyumba kulia na kushoto kutokana na kupasuliwa gurudumu mwishowe gari lilikwama kwenye mtalo, ilipinduka, moshi mzito ulipaa angani.
"Ahahaha hahaha" punde baada kusimama na pikipiki yake Inspekta Jeff aliangua kicheko. Cheko lake lilikuwa likijirudia mara mbili mbili mithili ya mwangwi, kwa namna gari lilivyokuwa limepinduka na kuharibika vibaya alijua fika genge la Don Dominic limetoweka lakini pia alijua fika kazi aliyo pewa ya kuja duniani kumuangamiza Saigon imetimia.
Alichomoa bastora kwenye koti lake kisha akapiga risasi mfululizo kwenye gari lile, akaangua tena kicheko kisha akainyooshea kidole pikipiki ile aliyokuwa akitumia kuwafuatilia wakina Derrick. Ilipotea kimaajabu, punde si punde naye alichuchumaa chini ghafla akapotea.
Lakini wakati Inspekta Jeff anafanya maajabu hayo, kuna watu walimshuhudia kwa macho yao. Nao walikuwa ni askari wenzake ambao walikula doria ili kujua mwisho wa Inspekta huyo na kundi lile la Don Dominic.
Inspekta Jeff alipo fika ofisini alieleza kila kitu kilicho jili, tena alieleza kwa furaha na tabasamu bashasha huku makamanda wenzake hata wasimpe hongera yoyote. Jambo hilo lilimtia shaka, machale yalimcheza ila hakujali. Moja kwa moja alizama mpaka kwenye chumba maalumu kwa dhumuni ya kuvua koti abaki na sare tu, lakini kabla hajafanya jambo lolote ghafla akasikia ubaridi kwenye kichwa chake na sauti ikimtaka anyooshe mikono juu.
"Inspekta Jeff, upo chini ya ulinzi kuanzia sasa" aliongea kamanda huyo baada kumuwekea bastora kwenye kichwa chake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Acha utani kamanda" alisema Inspekta Jeff huku akiendelea kuvua koti lake hata asitii amri ya kamanda yule aliye muweka chini ya ulinzi. Akalitupa juu kwenye meza kisha akamgeukia, akacheka kwa madaha na kusema "Tatizo liko wapi kamanda, mimi siogopi bundi yako kwa sababu najua haina madhara kwangu. Haupo makini na kazi yako"

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment