Search This Blog

NILIVYOKUTANA NA MZIMU FACEBOOK - 5

 





    Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Facebook

    Sehemu Ya Tano (5)







    Ni kama vile nilikuwa nimepigwa na ganzi muda huo, nilishindwa kujua nilitakiwa kumjibu vipi mshikaji wangu, Deo ili aweze kunielewa mantiki yangu.

    “Unasema kwamba walienda kumchukua wapi?” alirudia kuniuliza huku akihitaji ufafanuzi wa kauli yangu iliyompa utata kwa kiasi fulani, hakujua mantiki yangu ilikuwa ni ipi hasa.

    Niliamini hata kama ningemwambia kwamba walienda kumchukua mochwari na walijuaje kwamba alikuwepo huko? Bado maswali yangekuwa ni mengi yasiyokuwa na kikomo.

    Nilichokifanya ni kumpotezea mada na kuanza kumwambia habari nyingine tofauti na hiyo tuliyokuwa tunazungumza muda huo.

    ***

    Tangu nilipokishuhudia kifo cha Farida kwa macho yangu, kwa kweli niliogopa sana, moyoni mwangu nilitawaliwa na hofu kubwa. Niliishi maisha yaliyojaa wasiwasi kwa muda mrefu, wakati mwingine majira ya usiku nilipokuwa nikilala, nilimuota ndoto nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zinanitisha.

    Hicho kilikuwa kipindi ambacho nilitamani kuhama katika nyumba hiyo niliyopanga. Niliiona kuwa chungu kutokana na mauzauza ambayo yalikuwa yakiendelea kunitokea.

    ***

    Baada ya kupita kipindi fulani ndipo hapo nilionekana kusahau kila kitu, yale yote yaliyokuwa yametokea yalibakia kuwa historia kwangu tena ambayo sikutaka kuikumbuka hata kidogo.

    Niliendelea na masomo chuo huku biashara yangu ya mgahawa nayo ikiendelea kama kawaida.

    Katika kipindi hicho tayari ulikuwa umepita mwaka mmoja tangu uhusiano wetu wa kimapenzi na Farhia ulipoanza lakini mpaka kufikia hapo nilionekana kukata tamaa kabisa ya kuonana naye.

    Hii ilitokana na kipindi chote ambacho nilihitaji kuonana naye, mara zote alikuwa ni mtu wa kuniwekea vikwazo lukuki, wakati mwingine alikuwa akinidanganya kwamba kuna siku ningeonana naye lakini kitu cha ajabu siku hiyo haikuweza kufika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo lilinifanya nishindwe kuelewa kwamba kulikuwa kuna kitu gani hasa kilichokuwa kikisababisha mpaka nishindwe kuonana naye, ingawa yeye ndiye aliyenipa utajiri lakini hakuonekana kuwa na haraka ya kutaka kuniona. Hilo lilizidi kunishangaza na kuanza kujiuliza alikuwa ni msichana wa aina gani? inamaana hakuwa na hisia zozote na mimi? Na kama alikuwa nazo je, alikuwa akizikidhi wapi?

    Kwa kweli majibu ya maswali hayo sikuwa nayo wala hakukuwa kuna mtu yeyote yule wa kunijibu.



    “Kwa nini hutaki tuonane? Kila siku umekuwa ni mtu wa kunidanganya? Hivi tutaendelea kuishi maisha haya mpaka lini?” nilimuuliza siku moja nilipokuwa nikizungumza naye kwenye simu kama ilivyokuwa kawaida yetu.

    “Usijali ipo siku tutaonana ila unakumbuka tulikubaliana nini?” aliniambia kisha akaniuliza swali.

    “Kuhusu nini?” nilimuuliza huku nikionekana kusahau kwa wakati huo.

    “Nilikwambia kwamba sitaki unichanganye na wasichana wengine, nataka unipende mimi tu,” aliniambia kwa kunikumbusha.

    “Ndiyo nakumbuka kwani kuna nini?”

    “Basi naomba iwe hivyo sitaki kuumia kwa sababu ya mapenzi, nimekukabidhi moyo wangu, sitaki uumize.”

    “Lakini….” Nilisema lakini kabla sijamalizia sentensi yangu akanikata kauli.

    “Najua unachotaka kuniambia ila usijali ipo siku utaniona, kwa wakati huu naomba usivunje makubaliano yetu kwani utakuwa umenikosea sana, sipendi unikosee mpenzi,” aliniambia huku akionyesha msisitizo katika hilo.

    Ingawa Farhia aliyazungumza maneno hayo huku akionekana kuwa msichana ambaye alionyesha kunipenda kwa dhati lakini kasoro yake ilikuwa sehemu moja tu. Tangu uhusiano wetu wa kimapenzi ulipoanza mpaka kufikia katika kipindi hicho hatukuwa bado tumeonana na hilo liliendelea kuwa tatizo.

    ***

    Kutokana na mkasa ambao ulinisibu siku chache zilizopita wa kutembea na msichana, Farida mpaka kufikia hatua ya kunifia mikononi mwangu na kunusurika kufungwa kifungo cha maisha jela. Kwa kweli nilionekana kujifunza kutokana na makosa.

    Ni kama vile Mwenyezi Mungu alikuwa akinionyesha malipo ya usaliti jinsi yalivyokuwa hapa duniani, yaani kwa yote yale ambayo nilikuwa nikiyafanya kwamba sikutakiwa kuyafanya hata kidogo.

    Labda niseme huo haukuwa ndiyo mwisho wa kumsumbua Farhia juu ya kuonana naye. Niliendelea kumsumbua kila siku huku nikiamini kwamba kwa kuendelea kuishi naye mbalimbali bila kuonana ndiyo ilikuwa sababu ambayo ingenifanya niendelee kumsaliti ilihali moyo wangu ulisita kufanya hivyo.

    “Kwahiyo unataka kuniona tu?” aliniuliza baada ya kuona usumbufu umekuwa ni mkubwa.

    “Ndiyo,” nilimjibu.

    “Halafu ukishaniona utafanyaje?”

    “Nitakubusu, nitakukumbatia, nitakwambia maneno mazuri, kingine tutakwenda beach kupunga upepo wa bahari.”

    “Kwahiyo ni hayo tu ambayo unatamani kuyafanya ukiniona?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yapo mengi sana.”

    “Kama?”

    “Kufanya mapenzi na mengine mengi ambayo siwezi kuyataja yote.”

    “Uko serious kwamba unataka kuniona?”

    “Ndiyo.”

    “Kweli, hutoogopa?”

    “Farhia mbona sikuelewi? Unanichanganya unajua, nimekwambia ndiyo nahitaji kukuona hata leo,” nilimwambia kwa sauti ya ukali kisha nikashangaa simu ikikatwa upande wa pili. Nilihisi labda aliishiwa salio na hivyo niliamua kumpigia lakini ajabu simu yake ilikuwa haipatikani.

    Nilishangaa na kuanza kujiuliza au simu ilizima chaji? Wakati nikijiuliza kuhusu simu yake labda ilizima chaji ghafla! nikaanza kusikia harufu kali ya manukato chumbani kwangu, yalikuwa ni manukato ambayo harufu yake haikuwa ngeni, niliwahi kuyasikia kipindi fulani chumbani kwangu lakini sikuyatilia maanani, nilizidi kuchanganyikiwa mno.

    Nilianza kuweweseka, sikuwa na amani hata kidogo. Mawazo yangu yalikuwa kwa Farhia ambaye alinishangaza na kuanza kuhisi labda alikuwa ni jini.

    Ndugu yangu, huwezi kuamini, usiku mzima nilikesha, asubuhi iliyofuata ilikuwa siku ya jumanne, sikuwa na kipindi cha asubuhi chuo hivyo nilitulia chumbani. Kichwa changu kilikuwa kikimfikiria Farhia tu.

    Wakati nikiwa humo chumbani, nikaanza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana, pumzi zikaanza kutoka mfululizo kana kwamba nilikuwa nikikimbizwa ama kukimbia mwenyewe.

    Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi sana. Ghafla! nikasikia sauti ya msichana ambaye alikuwa akiniita. Kwa kweli nilihisi kufa.





    Sauti ya msichana huyo ambaye alikuwa akiniita ilikuwa ikijirudia masikioni mwangu mara mbilimbili kama vile sauti ya mwang’wi.

    Niliogopa sana, nikaanza kuangalia huku na kule kwenye kila kona ya chumba changu lakini kitu cha ajabu sikumuona msichana huyo. Mapigo ya moyo wangu yakazidi kuongezeka kasi.

    Kitendo cha kuendelea kubaki ndani ya chumba hicho ambacho nilikiona kuwa na kila dalili za kuhatarisha uhai wangu, niliona ni kosa kubwa tena la jinai, nilichokifanya muda huo ni kutoka ndani na kuelekea sebuleni kwa ajili ya kutoka nje maana uoga ulinijaa mpaka kwenye unyayo.

    Nilifanya hivyo lakini nilipofika sebuleni na kuukaribia mlango mkubwa kwa lengo la kuufungua na kutoka nje, nilishangaa kuona ukiwa umefungwa kwa ufunguo. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, kwa kuwa kulikuwa kuna ufunguo, nilifungua.

    Hapo ndipo nilikutana na majaabu mengine. Mlango uligoma kufunguka na katika kipindi chote ambacho nilikuwa nikiufungua ni kama vile nilikuwa nikicheza kwani uligoma kabisa kufunguka.

    Nilishindwa kuvumilia maajabu yaliyokuwa yakiendelea kunitokea mule ndani, nikataka kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani waliokuwa karibu. Nilipoanza kupiga kelele kabla sijamalizia sentensi yangu, nilikumbwa na kigugumizi cha ghafla!

    Nilishangaa sana, haikuwa ni hali ya kawaida kutokea katika maisha yangu. Sikuwahi kuwa na kigugumizi kabisa, sasa ilikuweje nikawa nacho?

    Wakati nikiendelea kujiuliza swali hilo, mara nikaanza kusikia harufu ya manukato yale niliyotoka kuyasikia chumbani.

    Nilibaki nikitetemeke mno, kijasho chembamba kikaanza kunitoka. Mara katika hali ya kushangaza nilishangaa nikianguka chini na kutulia hapo kwa muda. Ingawa nilijitahidi kusimama lakini nishindwa kabisa, juu yangu kulikuwa kama kuna kitu kizito ambacho kilikuwa kikinigandamiza kwa nguvu.

    Hapo chini nilipokuwa nimeanguka, mara nikaanza kuhisi macho yangu yakiwa mazito, usingizi mzito ukaanza kuninyemelea. Nilijitahidi kuyakaza macho yangu lakini wapi, yalizidi kulegea, hapohapo nikapatwa na usingizi mzito.

    ***

    Nilishangaa nikiwa ndani ya nyumba moja kubwa sana, nilibaki nikiyaangaza macho yangu huku na kule, nikitaka kufahamu nilikuwa wapi kwani hata ile nyumba kwa jinsi ilivyokuwa nzuri, sikuamini kama duniani kulikuwa kuna nyumba kama hiyo.

    Wakati nikiendelea kushangaa nyumba hiyo, pembeni yangu alisimama msichana mmoja ambaye nilipomtazama niliweza kumfahamu, alikuwa ni Farhia. Alibaki akiniangalia huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana na kuufanya uzuri wake kuongezeka mara dufu.

    Swali la kwanza kabisa ambalo nilijiuliza, pale nilifikaje?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ya mwisho nakumbuka nilikuwa nyumbani kwangu, sebuleni. Sasa nani alinileta katika nyumba hiyo kubwa? Wakati nikijiuliza hayo, Farhia akanisogelea na kusimama karibu yangu kabisa.

    “Nakupenda sana Abdul,” aliniambia kisha akanibusu kwenye paji la uso.

    “Farhia la….” Nilisema lakini kabla sijamalizia sentensi yangu, nilishangaa akanikata kauli.

    “Shiiiiiiiiii! Usipige kelele wazazi wangu watasikia,” aliniambia kwa sauti ya chini kabisa.

    “Nimefikaje hapa, naomba unirudishe nyumbani.”

    Nilipomwambia hivyo sikutaka kusubiri jibu lake, nilisimama na kutaka kuondoka zangu mahali hapo. Nilipoufikia mlango na kuufungua, cha ajabu hakukuwa kuna nje.

    Ndugu yangu, najua unaweza ukanishangaa ni kwa jinsi gani ambavyo sikupaona nje. Nilichokiona ni mimi mwenyewe, yaani sijui nielezee vipi unielewe. Ni kama vile nyuma yangu kulikuwa kuna mlango ambao niliufungua na kujiona mimi yule nikiwa nimeufungua mlango, hivyo ndivyo nilivyoona kwa wakati huo.

    “Nipo wapi hapa?” nilimuuliza Farhia mara baada ya kumgeukia na kumkuta akitabasamu.

    “Mpenzi wangu jamani nimekwambia usipige kelele wazazi wangu watasikia,” aliniambia huku nikimuona akifanya masihara, ni kama vile alikuwa akinitania na kwamba hakukuwa kuna wazazi wake ambao ningeweza kuwasumbua.

    “Hebu kwanza niambie hapa ni wapi? Mbona huniambii?” nilimuuliza kwa ghadhabu.

    “Hapa ni nyumbani kwetu mpenzi wangu.”

    “Nyumbani kwenu?”

    “Ndiyo.”

    “Sasa kwanini hipo hapa?”

    “Kwa sababu wazazi wangu wanataka kukufahamu.”

    “Wazazi wako?”

    “Ndiyo.”

    “Wanifahamu mimi?”

    “Ndiyo tena leo nataka nikutambulishe rasmi,” alinijibu.

    Kwa kweli ndugu msomaji, nilizidi kuchanganyikiwa mno, yaani mpaka kufikia hapo sikujua nilitakiwa kutoka vipi mule ndani. Niliyaona mauzauza yakiwa yameshamiri.







    Kile alichokuwa ameniambia Farhia kuhusu wazazi wake kiukweli kilinichanganya mno. Nilikumbuka kama kuna siku ambayo niliwahi kumwambia kwamba nilitaka anitambulishe kwa wazazi wake.

    Kwa kweli sikuwahi kuzungumza wala kupanga naye jambo lolote lile. Sasa ilikuweje akaamua kunipeleka kwa wazazi wake bila hata ya kunishirikisha mimi mwanaume wake?

    Hilo lilizidi kunishangaza mno, nikashindwa kuelewa mantiki yake ilikuwa ni ipi hasa kwa wakati huo.

    Muda huo aliniambia kwamba nilitakiwa kusubiri kwani wazazi wake walikuwa ndani na baada ya dakika kadhaa wangeweza kuja kuniona.

    “Kwa nini lakini umenileta hapa nyumbani kwenu bila kunishirikisha?” nilimuuliza huku nikimlaumu kwa kosa hilo alilokuwa amelifanya. Yaani kwa jinsi nilivyokuwa nikizungumza muda huo ni kama vile nilikuwa siogopi na kwamba niliyazoea mazingira hayo.

    “Mpenzi subiri basi nitakueleza kila kitu,” aliniambia huku akinituliza munkari niliokuwa nao.

    Aliponiambia hivyo mara upepo mkali ukaanza kuvuma, nikazidi kushangaa upepo huo ulitoka wapi muda huo na wakati ndani ya nyumba hiyo madirisha yalifungwa. Hiko kilikuwa ni kioja kingine.

    Wakati nikiendelea kushangaa maajabu ya upepo huo uliokuwa ukivuma kwa kasi, nikamtazama Farhia usoni. Alikuwa akitabasamu kama ilivyokuwa kawaida yake. Ile hali ya upepo iliyokuwa imetokea mule ndani ni kama vile alionekana kuizoea na kwamba ilikuwa ni hali ya kawaida kutokea katika maisha yake ya kila siku.

    “Kuna nini?” nilivunja ukimya na kuamua kumuuliza, kwa sababu kile kilichokuwa kikiendelea kilizidi kuniogopesha na kunitisha mno.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usiogope wazazi wangu ndiyo wanakuja,” alinijibu.

    Baada ya Farhia kuniambia hivyo, nikashangaa kuwaona watu wawili wakiwa wamesima mbele yangu. Mmoja alikuwa ni mwanaume na mwingine alikuwa ni mwanamke. Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wakionekana, hawakuoneakana kuwa kama binadamu wa kawaida. Muonekano wao tu, ulitisha kutazama.

    Walikuwa na kwato miguuni na kitu kingine cha kuogopesha zaidi walionekana kuwa na manyoya mwili mzima kama sokwe.

    Ndugu msomaji kuna vitu vingine vinashangaza na kuogopesha mno. Huwezi kuamini muda huo nilipokuwa nikiwashuhudia watu hao waliokuwa wamesimama mbele yangu huku nikitazamana nao uso kwa uso, nilitamani kukimbia lakini miguu yangu ilikuwa mizito hivyo nilishindwa kukimbia na badala yake nilibaki nikiwatazama watu hao kwa uoga.

    Nilimtazama Farhia ambaye muda huo alikuwa akikauka kwa kucheka.

    “Mbona unaogopa sana, usiogope hawa ni wazazi wangu. Huyu ni baba yangu na huyu ni mama yangu,” aliniambia huku akinitambulisha kwa wazazi wake hao ambao walikuwa wakitisha kutazama.

    “Karibu sana mwanangu, jisikie upo nyumbani,” aliniambia mama yake huku akinipa mkono uliokuwa umejaa manyonya. Nilibaki nikitetemeka mno. Kutokana na uoga niliokuwa nao nikamtazama tena Farhia.

    “Farhia inamaana kumbe wewe ni….” Nilimwambia lakini kabla sijamalizia sentensi yangu nilishangaa kujiona nikiwa sebuleni kwangu. Nilikuwa nimelala chini.

    Sijui niwaeleze vipi ili muweze kujua hali ambayo nilikuwa nayo muda huo. Unajua hapa duniani kuna vitu vingine vikikutokea unaweza ukahisi labda ni mauzauza na pengine labda unaota lakini kumbe ndiyo ukweli halisi, yaani kile unachokiona kimekutokea kwenye ndoto ama mawazo yako ndicho hicho kimekutokea kweli katika maisha halisi.

    Kwa nini nayasema haya yote ni kwa sababu nataka kukufundisha somo kubwa sana katika maisha yako. Dunia ya sasa imetawaliwa na utandawazi, kila kona mitandao ya kijamii ndiyo imeshika hatamu.

    Kumekuwa kuna wimbi kubwa sana la vijana ambao wanaitumia mitandao ya kijamii kutafuta kazi, marafiki na hata wapenzi.

    Miongoni kati ya watu hao, wapo ambao wamefanikiwa na mpaka leo ninapokusimulia mkasa huu wanayafurahia maisha, lakini nisikufiche kitu ndugu yangu, hii mitandao ya kijamii hususani mtandao huu wa facebook uone kama ulivyo.

    Sote tunaamini kwamba mtandao huu upo kwa lengo la watu kufahamina na kuchati kama ilivyozoeleka na wengi wetu, ipo hivyo lakini huwezi kuamini mtandao huu huu wa facebook ndiyo uliyonikutanisha na mzimu ulionitafuna nusu ya maisha yangu.





    Hapo sebuleni nilipokuwa nimelala chini, kwanza nilishtuka sana, sikujua nilirudi vipi mahali hapo. Nilikumbuka mara ya mwisho nilikuwepo nyumbani kwa akina Farhia. Sasa ilikuweje nikawa tena sebuleni kwangu?

    Nilipigwa na butwaa, hofu ilikuwa imenitawala moyoni mwangu, kile kilichokuwa kimetokea, nilikiona kuwa zaidi ya maruweruwe.

    Nadhani hakukuwa kuna siku ambayo nilichanganyikiwa kama siku hiyo. Hiyo ilikuwa ni siku nyingine ambayo nilikumbwa na mauzauza yalionifanya nizidi kuogopa kila nilipokuwa nikikumbuka.

    Niliogopa sana, sikutaka kuendelea kukaa hapo kwani nilihisi Farhia alikuwa jini na muda wowote angeweza kunitokea. Nilichokifanya niliamka pale chini na kwenda chumbani ambapo moja kwa moja niliingia bafuni kuoga, nilipomaliza nilijiandaa haraka na kisha kuondoka kuelekea chuo ambapo baadaye nilikutana na washikaji zangu.

    “Una nini wewe?” aliniuliza Deo, hapa ni baada ya kuiona tofauti niliyokuwa nayo muda huo. Sikuwa na furaha hata kidogo, nilionekana kutawaliwa na wasiwasi.

    “Kitu gani?” nilimuuliza.

    “Mbona upo hivyo?”

    “Nipoje yaani?”

    “Huna raha kabisa, hebu tuambie kuna nini?”

    “Au mademu wameshaanza kukuchanganya nini?” aliniuliza Nickson.

    “Hapana washikaji sio hivyo,” niliwaambia.

    “Siyo hivyo kitu gani sasa? hebu sema nini kinachokusumbua mzee baba?” aliniuliza Deo.

    Kwa kweli sikutaka kuwaambia washikaji zangu kuhusu kile kilichokuwa kimenitokea, nilibaki kimya kwa muda huku nikionekana kutafakari juu ya jambo fulani lililokuwa linanitatiza. Kwa wakati huo nilikuwa nikijiuliza kama nilitakiwa kuwaambia ukweli ama la, niendelee kuficha ibaki kuwa siri yangu?

    Baada ya kupita dakika kadhaa niliamua kuwaambia ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea, kwanza wao wenyewe walibaki wakishangaa, hawakutaka kuniamini hata kidogo, kile nilichowaambia kuhusu Farhia waliona kama ni utani, wakaniambia kwamba nilikuwa nawadanganya na kwamba sikumuona msichana huyo ana kwa ana.

    “Au ulikuwa unaota?” aliniuliza Nick.

    “Jamani washikaji nimemuona kweli Farhia kwa macho yangu, amenipeleka mpaka nyumbani kwao,” nilimwaambia huku nikijaribu kuwaaminisha.

    “Acha masihara yako, yaani amekupeleka mpaka kwao?” aliuliza Deo.

    “Ndiyo.”

    “Mh! Mimi siamini,” alidakia Nick.

    “Nimeenda nyumbani kwao mpaka nikaonana na wazazi wake.”

    “Umeenda lini?”

    “Leo asubuhi,” nilijibu jibu lililowafanya wakaanza kunicheka.

    Ndugu yangu hata kama ungekuwa ni wewe muda huo lazima ungecheka na kunishangaa sana, hebu tuchukulie mfano jana tuwe wote kutwa nzima halafu leo asubuhi tusionane, halafu mchana wake nikwambie kwamba nilienda Zanzibar asubuhi. Jambo hilo lisingeweza kukuingia akilini hata kidogo.

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa washikaji zangu, ingawa nilijitahidi kuwaelezea ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea lakini hawakuniamini zaidi waliniona kama mzushi fulani hivi.

    Kwa kweli nilichanganyikiwa sana, siku hiyo majira ya jioni nilipomaliza kipindi chuo sikutaka kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani, nilienda kwenye baa moja iliyokuwepo maeneo ya Temeke.

    Nilipofika katika baa hiyo, nilitulia kwenye meza moja ambapo niliagiza pombe kwa mhudumu na kuanza kunywa kwa kuamini kwamba zingenipunguzia mawazo niliokuwa nayo kichwani kwa wakati huo.

    Hali hiyo haikuweza kubadilika hata theluthi, japokuwa nilipokunywa nililewa lakini katika hali ya kushangaza mawazo bado hayakufutika kichwani mwangu. Niliendelea kumuwaza farhia tu.

    Wakati mwingine sikutaka kuamini kama alikuwa jini hivyo kila kitu kibaya ambacho nilikuwa nikikifikiria kwa wakati huo kuhusu yeye nilikipuuzia huku nikijiona kumkosea sana, sikutakiwa kumuhisi hivyo hata kidogo.

    Katika kipindi hicho chote cha mawazo nilikuwa baa huku nikiendelea kuiangalia chupa ya bia ya Safari ambayo ilikuwa mezani. Kwa wakati huo nilikuwa nimeinywa nusu japokuwa nilikuwa nimekaa mahali hapo kwa takribani saa mbili nzima lakini mawazo juu ya Farhia yalikuwa mengi, nikashindwa kuendelea kukaa mahali hapo tena, nilichokifanya ni kuondoka huku ikiwa imetimia saa mbili za usiku.

    Nikaingia kwenye gari na moja kwa moja kuondoka mahali hapo kuelekea nyumbani. Kichwani niliendelea kuwa na mawazo tele. Kwa kuwa sikuwa mzoefu sana wa pombe, nikaanza kuona mawenge japokuwa nilikuwa nikiendelea kuendesha gari langu kama kawaida.

    Nilipofika nyumbani na kuingia chumbani, nikavua nguo na kwenda bafuni kuoga ili kuondoa uchovu niliokuwa nao siku hiyo. Nilipotoka bafuni, nikajilaza kitandani, nikajaribu kuutafuta usingizi lakini haukuweza kupatikana kwa urahisi kwa sababu kichwa changu kilitawaliwa na mawazo mazito kwa wakati huo.

    Kila nilipojaribu kuutafuta usingizi ndivyo ambavyo macho yangu yaliendelea kutazama huku na kule mule chumbani bila kuchoka.

    Nilijilaza kitandani kwa muda wa dakika thelathini, mara nikasikia simu yangu ikiwa inaita, nikaichukua na kisha kuangalia kioo. Namba ilikuwa ngeni.

    “Hello,” nilisema huku nikitulia kuisikiliza sauti ya mtu huyo aliyenipigia.

    “Hello, mambo vipi? Uko poa?” ilikuwa sauti ya msichana ambaye alinisalimia.

    “Niko poa, samahani naongea na nani?” nilimwambia kisha nikamuuliza.

    “Leila,” alijitambulisha msichana huyo.

    “Leila?” nilirudia kumuita huku nikishangaa.

    “Ndiyo.”

    “Leila yupi? Na namba yangu umeitoa wapi?”

    “Mh! Inamaana umenisahau mimi Leila tunasoma wote chuo?”

    “Ooh! Cr?”

    “Ndiyo.”

    “Ah! Kumbe ni wewe, niambie.”

    “Safi, unaonekana una mawazo sana.”

    “Yeah! Lakini ni mambo madogo tu.”

    “Sio kawaida yako lakini.”

    “Kivipi?”

    “Kukuona ukinywa pombe.”

    “Pombe? Inamaana kumbe uliniona?”

    “Ndiyo nilikuona lakini vipi upo sawa kweli?”

    “Yeah…nipo sawa kabisa.”

    Mazungumzo hayakuishia hapo, tuliendelea kuzungumza na jinsi ambayo mazungumzo yalipokuwa yakipamba moto ndivyo ambavyo ukaribu ukazidi kujengeka.

    “Naomba kesho tuonane,” siku moja alinitumia ujumbe WhatsApp, muda huo nilikuwa nikichati naye.

    “Kesho sidhani kama itawezekana,” niliandika na kumtumia huku nikisindikiza na emoji ya kutafakari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pleasee nakuomba Abdul tena nakuomba sana. Ningependa kuonana nawe kesho. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuonana nawe na kuongea. Kuna kitu nataka kukwambia ambacho kimenitesa kwa muda mrefu sana, sikutaka kukwambia mwanzo ila kesho naona ndiyo siku muafaka ya kukwambia.”

    “Unataka kuniambia nini Leila?”

    “Nitakwambia kesho endapo utanikubalia nionane nawe.”

    “Na kama nisipokukubalia je?”

    “Utakuwa umeuumiza sana moyo wangu.”

    “Kivipi?”

    “Kwa sababu utanikatilia nikuone.”

    “Okay! Kwahiyo tutaonana wapi? Na ni muda gani?”

    “Sijui unapendelea kwenda sehemu gani?”

    “Popote kuzuri.”

    “Okay! Nadhani pale Liquid pako vizuri sana, tunaweza kwenda?”

    “Sawa haina noma.”

    “Tena itakuwa vizuri sana kwa sababu kesho ni siku ya karaoke.”

    “Kumbe unapenda kwenda mara kwa mara hapo?”

    “Siku moja moja tu.”

    “Sawa tutakwenda,” nilimwambia.





    .



    Siku hiyo ilipita, siku iliyofuata ilipofika majira ya usiku nilitoka na kuanza kuelekea katika baa hiyo tulioahidiana kuonana huku nikiwa ndani ya gari langu.

    Sikuchukua muda mrefu sana nikawa tayari nimekwishafika mahali hapo. Nikateremka na kisha kuingia ndani ambapo nilichukua kiti na kutulia kwenye meza moja ambayo ilikuwa tupu.

    Muda huo nilikuwa nikimsubiria Leila ambaye aliniambia kwamba alikaribia kufika kwani mahali alipokuwepo kwa wakati huo kulikuwa kuna foleni kidogo. Kwa upande wangu hilo halikuwa tatizo, niliendelea kumsubiri huku macho yangu yakibaki kuangalia huku na kule mule ndani, hata pale ambapo alinifuata mhudumu na kunisikiliza hitaji langu nilimwambia asubiri mpaka mgeni wangu atakapofika eneo hilo ndipo nitamuita na kumuagizia.

    Baada ya kupita dakika kama kumi hivi ghafla! macho yangu yakatua katika uso wa msichana mrembo, Leila ambaye alikuwa amevaa sketi fupi ya rangi nyeusi ambayo iliyaacha nje mapaja yake yaliyokuwa yamenona.

    Nilibaki nikimwangalia huku nikionekana kutoamini kama kweli msichana huyo ndiye yule ambaye nilikuwa nikisoma naye chuo. Alionekana kuwa mrembo sana na kadiri ambavyo niliendelea kumuangalia jinsi alivyokuwa ameumbika kiukweli nilizidi kukiri kwamba Mungu hakukosea katika uumbaji wake.

    Nilisimama kwa lengo la kusalimiana naye, sikuishia hapo tu! nikamkumbatiana kwa muda na kisha nikamkaribisha, akachukua kiti na kukaa pembeni yangu

    Watu walikuwa ni wengi sana mahali hapo, kila mtu alionekana kuwa bize na mambo yake. Kuna wale ambao walikuwa wakiongea kama wapenzi, kuna wengine walionekana kutokuwa na habari yoyote ile, yaani wao muda wote walikuwa wakinywa pombe kupindukia.

    Wakati yote hayo yakiendelea kulikuwa kuna msichana mmoja ambaye alikuwa amesimama jukwaani na kwa wakati huo alikuwa akiimba wimbo wa ‘To love you more’ ulioimbwa na mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani, Celine Dion. Nilifurahi sana kwani sehemu hiyo haikuonekana kuchosha, kila mmoja alikuwa amechangamka.

    “Utanisamehe kwa kuchelewe kufika,” aliniambia kwa kujitetea mara baada ya kukaa kitini.

    “Usijali,” nilimwambia kisha hapohapo nikamuita mhudumu na kumuagizia kinywaji.

    “Khee! Unaagiza juisi jamani?” aliniuliza Leila huku akinishangaa.

    “Ndiyo unajua mimi sio mzoefu sana wa pombe nadhani juisi inatosha.”

    “Sawa na mimi niletee juisi basi,” aliniambia kisha akamuagiza mhudumu ambapo ndani ya dakika kama tano hivi tukahudumiwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo ndipo tulipoanza mazungumzo yetu huku wimbo kutoka kwa msichana ambaye alikuwa akiendelea kuimba jukwaani (karaoke) ukituburudisha mahali hapo.

    “Jana uliniambia kuna kitu leo unataka kuniambia,” nilimwambia huku nikiwa na shahuku ya kutaka kufahamu.

    “Ndiyo Abdul nakumbuka?”

    “Niambie sasa.”

    Nilipomwambia hivyo akanyamaza kwa muda, alionekana kama mtu aliyekuwa akitafakari jambo fulani ambalo hakujua ni kwa jinsi gani ambavyo angeweza kuliwasilisha.

    “Leila nakusikiliza, niambie,” nilimwambia maneno yaliyomshtua kutoka katika dimbwi la mawazo.

    Akatanitazama usoni, ni hapa ambapo akatabasamu na kila alipokuwa akiendelea kunitazama basi mchezo ukawa ndiyo huo.

    “Kuna nini? hebu niambie basi,” nilimuuliza huku nikionekana kuwa na shahuku.

    Ingawa Leila alionekana kushindwa kuniambia kile kilichomfanya mpaka akaniita mahali hapo lakini niliendelea kumlazimisha mpaka pale ambapo akaamua kunieleza ukweli huku akionekana kunionea aibu.

    “Kama nitakuwa nakosea kukwambia yote haya naomba unisamehe sana ila najua ulikuwa unatembea na Farida lakini kwa sasa ni marehemu. Najua ni maumivu kiasi gani uliokuwa nayo moyoni mwako hasa kwa kuondokewa na mtu uliyekuwa unampenda. Abdul lengo kubwa la mimi kukuita hapa ni kutaka kukwambia kwamba wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu, kila siku nimekuwa nikikufikiria sana, nimeona leo nikwambie ukweli ila kama nitakuwa nimekosea naomba unisamehe,” aliniambia huku akitokwa na machozi. Nilishtuka sana, sikutegemea kama angeweza kuniambia maneno kama hayo ambayo yangeuumiza moyo wangu kiasi hicho.

    “Mbona imekuwa mapema sana kiasi hicho?” nilimuuliza.

    “Hapana Abdul nahisi huu ndiyo muda sahihi wa kukwambia kama nikichelewa wengine watakuwahi halafu na mimi sitaki nikukose kabisa, nakupenda sana,” alinijibu.

    Mpaka kufika hapo sikujua nilitakiwa kumjibu vipi Leila. Aliponiambia maneno hayo huku akitokwa na machozi katika hali iliyonishangaza nilishangaa kuona sura yake ikibadilika na kuwa sura ya Farhia.

    Nilishtuka sana nisijue ni nini ambacho nilitakiwa kukifanya, wakati nikiwa katika hali hiyo mara nikashangaa kuona sura ya Farhia ikibadilika tena na kuwa sura ya Leila kama vile mwanzo.

    Nilibaki nimepigwa na bumbuwazi kwa kushuhudia maajabu hayo mpaka pale ambapo sauti ya Leila iliponigutua kutoka katika hali hiyo.

    “Hey…” Aliniambia huku akinishika bega la upande a kulia, nikashtuka.





    “Hapana Abdul nahisi huu ndiyo muda sahihi wa kukwambia kama nikichelewa wengine watakuwahi halafu na mimi sitaki nikukose kabisa, nakupenda sana,” alinijibu.

    Mpaka kufika hapo sikujua nilitakiwa kumjibu vipi Leila. Aliponiambia maneno hayo huku akitokwa na machozi katika hali iliyonishangaza nilishangaa kuona sura yake ikibadilika na kuwa sura ya Farhia.

    Nilishtuka sana nisijue ni nini ambacho nilitakiwa kukifanya, wakati nikiwa katika hali hiyo mara nikashangaa kuona sura ya Farhia ikibadilika tena na kuwa sura ya Leila kama vile mwanzo.

    Nilibaki nimepigwa na bumbuwazi kwa kushuhudia maajabu hayo mpaka pale ambapo sauti ya Leila iliponigutua kutoka katika hali hiyo.

    “Hey…” Aliniambia huku akinishika bega la upande a kulia, nikashtuka!

    “Una nini?” aliniuliza mara baada ya kuniona nimeshtuka.

    “Hakuna kitu,” nilimwambia huku nikijiweka sawa.

    “Mbona umeshtuka sasa? Upo sawa kweli?”

    “Hakuna kitu Leila, tuondoke.”

    “Tuondoke twende wapi sasa? Mbona sikuelewi?”

    “Nimekwambia Leila tuondoke, sitaki tena kukaa hapa.”

    “Umechoka? Au nilichokwambia nimekuudhi basi nisamehe, sikujua kama nitakukosea,” aliniambia huku akiniomba msamaha huo.

    Nikaona kama ananipotezea muda wangu, nilichokifanya nikasimama na kuondoka mahali hapo huku nikimuacha akinishangaa! Kitendo hicho cha kuondoka kwa ghafla! hakika kilimuacha na maswali yaliyokosa majibu.

    Nilipoingia ndani ya gari sikutaka kumsubiri, nikawasha gari na kuondoka mahali hapo huku nisijue ni nini kilichoendelea kwa Leila.

    Nilipofika nyumbani kwangu, sikutaka kuingia chumbani. Nilikaa sebuleni kwa muda huku nikijaribu kukumbuka kile kilichokuwa kimetokea kule baa. Iliwezekanaje Leila akabadilika na kuwa Farhia halafu hapohapo akabadilika tena na kuwa Leila yule yule wa mwanzo?

    Kwa kweli hilo lilinishangaza, wakati mwingine nikaanza kumuona Leila kuwa kiumbe cha ajabu.

    “Jamani au ni mawazo yangu? Lakini nimeona sura yake ikibadilika na kuwa sura ya Farhia?” nilijiuliza huku nisijue jibu la swali langu hilo.

    Nilipagawa, kile kilichokuwa kimetokea kikaonekana kunitisha mno. Naweza kusema huo ulikuwa ni muendelezo wa kuyaona mauzauza ambayo mpaka kufikia muda huo sikujua ni kwa nini yalikuwa yakinitokea mimi tu!

    Hofu kubwa ilikuwa imenitawala moyoni mwangu, wakati nikiendelea kuwa katika hali hiyo ni hapa ambapo nikapigiwa simu na Farhia. Nilipoliona jina lake, nilihisi kuchanganyikiwa. Nikaogopa kupokea.

    Simu iliendelea kuita, mara ya kwanza, ya pili, ya tatu mpaka ya nne. Katika kipindi chote hicho sikutaka kupokea. Nilikwishafahamu kwamba Farhia hakuwa binadamu wa kawaida, alikuwa ni jini.

    Baada ya kupiga simu mara nne ndipo hapo akanitumia ujumbe mfupi ulionitaarifu kwamba nipokee simu yake kwani kulikuwa kuna kitu ambacho alitaka kuniambia. Nilipousoma ujumbe huo, haikuchukua dakika chache, akanipigia nami nikapokea.

    “Kwa nini hutaki kupokea simu yangu?” aliniuliza.

    “Nilikuwa mbali na simu,” nilimjibu kwa kumdanganya huku hofu ikiwa bado imenitawala moyoni mwangu.

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo.”

    “Na umetoka wapi usiku huu?”

    “Kutoka wapi, kivipi yaani?”

    “Ulikuwa wapi?”

    “Mbona leo sijatoka kabisa, nilikuwepo nyumbani tu.”

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo nina uhakika.”

    “Na yule aliyekuwepo baa na mwanamke alikuwa ni nani?”

    “Baa?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo inamaana unajifanya hujui?”

    “Farhia mbona sikuelewi?”

    “Hunielewi au unajitoa ufahamu tu! Nimekuuliza yule aliyekuwepo baa na mwanamke alikuwa ni nani kama siyo wewe?”

    “Baa ipi?”

    “Abdul halafu usinifanye mtoto mdogo unajua.”

    “Farhia mpenzi wangu.”

    “Niambie ulikuwa unafanya nini kule baa? Na tulikubaliana nini na umefanya nini?” aliniuliza maswali ambayo yalinifanya nihakikishe kwamba Farhia hakuwa binadamu wa kawaida.

    Aliwezaje kujua kwamba nilikuwa baa na mwanamke? Hilo lilinishangaza sana, nikashindwa kumjibu kwa wakati huo. Nikabaki namumunya maneno kama mtoto mdogo.

    “Labda nikwambie kuwa najua kila kitu unachokifanya katika maisha yako. Najua muda huu kwamba upo sebuleni unaongea na simu, umetoka baa tena umeondoka baada ya kuniona katika mazingira ya kutatanisha,” aliniambia kisha akanyamaza kidogo halafu akaendelea kuzungumza.

    “Sasa sikia, sitaki kumwaga damu za binadamu zisizokuwa na hatia, nilizozimwaga zinatosha. Nimekutahadharisha na bado naendelea kukukumbusha kuwa sitaki unichanganye na mwanamke mwingine tofauti na mimi. Umeamua kunipenda mimi basi nipende mimi tu, hiyo ndiyo shida yangu kwako na wala sihitaji kitu kingine kutoka kwako,” aliniambia kisha hakutaka kusubiri jibu langu, akaamua kukata simu.

    Hapo ndipo nilipogundua kwamba Farhia alikuwa sio binadamu wa kawaida, kulikuwa kuna kitu cha ziada ndani yake maana kama angekuwa ni binadamu kama walivyokuwa binadamu wengine asingeweza kujua mambo yote hayo, mengine yalikuwa ya siri.

    Hilo likazidi kuniogopesha mno, huwezi kuamini muda huo niliogopa mpaka kuingia chumbani kwangu, nilibaki nimekaa pale sebuleni kuwa uwoga mpaka pale ambapo usingizi ukanipitia.

    ***

    Siku iliyofuata niliamka na kujikuta nimelala kwenye kochi, nikashangaa sana lakini nilipokumbuka usiku wa siku hiyo kilitokea nini? na kupata majibu sahihi, sikuhitaji tena muda wa kushangaa.

    Nilichokifanya niliamka na kuingia chumbani kwangu, ingawa uwoga bado nilikuwa nao lakini kwa wakati huo ulinipungua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaingia bafua kuoga haraka haraka tofauti na siku nyingine. Sikumbuki kama nilitakata ama la, isipokuwa nilipomaliza, nilivaa nguo na kutoka kuelekea chuo kama ilivyokuwa kawaida yangu.

    Siku hiyo nakumbuka ilikuwa ni siku ya Ijumaa. Kutokana na maswahibu yaliyokuwa yakiendelea kunitokea katika maisha yangu huku nisijue ni nini ambacho nilitakiwa kukifanya.

    Katika hali iliyowashangaza washikaji zangu, ilipofika majira ya saa sita mchana, wakati ilipoadhiniwa adhana ya kwanza, nikawaaga kwa kuwaambia kwamba nilikuwa nikienda msikitini kuswali.

    Hilo likaonekana kuwashangaza sana, kwani tangu waliponifahamu mpaka kufikia katika kipindi hicho sikuwa na utaratibu wa kuwaaga kwenda msikitini.





    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog