Search This Blog

THE RETURN OF THE AMBROSY - 2

 






Simulizi : The Return Of The Ambrosy

Sehemu Ya Pili (2)







"Nimefikaje mahali hapa?.." Aliuliza Walemi mara baada kuzinduka na kujikuta akiwa hospital. Doctor aliyekuwa akiendelea na shughuli ya kumtibia alimtazama kisha akamjibu "Pole sana binti ila soon utakuwa sawa na kila kitu utajua sawa?.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Lakini Doctor ningehitaji kujua kwanza, tafadhali niambie" Aliongezea kusema Walemi, maneno ambayo aliyaongea kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimtiririka wakati huo akihisi maumivu makari kichwani alipokuwa ameumia. Hivyo Doctor mara baada kuona hali hiyo aliyokuwa nayo Walemi ilimbidi amueleze kila kitu "Uligingongwa na gari wakati upo katika harakati zako, ila bahati nzuri aliyekugonga hakutaka kukimbia kwahiyo aliamua kukufikisha hapa ili upatiwe matibabu" Alisema Doctor, maneno hayo yalizidi kumtoa machozi Walemi ambapo kwa sauti iliyoambatana na kilio alisema "Kwanini kila siku mimi? Hivi nina mkosi gani hapa duniani? Maisha yangu yenyewe yatabu nikila leo kesho sijui nitakula nini. Mkosi huu utanitoka lini jamani Walemi mimi?.." Alipokwisha kusema hayo aliendelea kulia kwa uchungu wakati huo Doctor alishaondoka humo Wodini. Muda mchache baadaye aliingia mwanamama akiwa na mkoba wake begani, mkoba wa ghalama. Kimuonekano mama huyo maisha yake yalikuwa si haba.

" Habari yako binti, pole sana" Alisema mama huyo kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake wakati huo akiketi kando ya kitanda alicholazwa Walemi. Walemi bado aliendelea kulia, ndipo huyo mama alipoambembeleza na hatimaye Walemi akawa amenyamamza kitendo ambacho kilizua ukimya kidogo huku mama huyo akifikiria namna ya kumuelezea Walemi kuwa yeye ndio aliyemgonga. Lakini baada ya kimya hicho, mwisho alisema "Samahani sana, kwanza mimi naitwa Emakulata. Napenda kutanguliza samahani kwa sababu mimi ndio niliyekugonga kwa bahati mbaya ila.." Kabla mama huyo hajaendelea kuongea Walemi alidakia akasema "Stop, Shetani mkubwa wewe. Maisha yangu yenyewe hayana mbele wala nyuma. Bado umeona unite majeraha ili nishindwe kujitafutia riziki, bora ungeniua tu. Ungenimalizia kuliko kuniingizia kwenye maisha ya shida zaidi" Alisema Walemi kwa sauti ya juu huku akiangua kilio. Alipokwisha kusema hayo alishika kichwa chake wakati huo bado akiendelea kulia kwa uchungu bila kukomaa. Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina Emakulata alishusha pumzi ndefu mara baada kuyasikia maneno hayo ya Walemi aliyoyaongea kwa jazba. Alikaa kimya kidogo huku akiwa amejiinamia,lakini punde ukimya huo aliuvunja na kusema "Binti mimi sio mtu mbaya bali ile ilikuwa bahati mbaya tu, laiti kama ningekuwa mtu mbaya basi pale pale ningeandoka zangu. Sawa? Usijali nipo tayari kukusaidia kwa vyovyote vile, ujue ni ajabu sana binti mzuri mrembo kama wewe kufanya kazi ile ya kuombaomba. Nadhani Mungu kanituma nije kukusaidia, nina pesa za kutosha hivyo utakapo pata ahueni utaenda kuishi kwangu saw!?.. "Alisema Emakulata huku akiachia tabasamu na kisha kumsogelea Walemi, kwa sauti ya chini kabisa akaongeza kusema" Amini neema imekaribia kwako" Walemi aliachia tabasamu pana, maneno hayo yalimfurahisha mno wakati huo huo humo wodini aliingia mwadada akiwa na mavazi ya hotelini,dada hiyo mkononi alikuwa ameshika kikapu ambacho ndani kulikuwa na chakula. Emakulata alipomuona alimkaribisha kwa tabasamu bashasha kisha akasema "Mgonjwa wangu ni huyu hapa, kwahiyo kinachotakiwa kila siku uwe unamletea chakula. Asubuhi mchana na usiku, bili yote niorodheshee nitalipa mimi".

"Anhaa sawa dada" Aliitika dada huyo aliyeleta chakula muda huo huo akamtazama Walemi kisha akampa pole. Baada ya hapo alimuamdalia chakula Walemi akaanza kula. Alipomaliza Emakulata alimuuliza ufupi wa maisha yake,simulizi ambayo Walemi hakuta kuificha, alieleza kila kitu ambapo katika magumu yote aliyopitia ni moja tu ambalo lilimgusa Emakulata, nalo ni lile alilonusurika guest.

"Mungu wangu kweli dunia hii inamambo, pole sana Walemi kwa magumu yote. Lakini pia kumbe bado kuna baadhi ya maeneo kuna utamaduni wa kuchaguliwa wachumba?..Loh ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni" Alisema Emakulata kisha akakaa kimya kidogo akilainisha koo kwa maji aliyokuwa nayo katika mkoba wake. Baada ya hapo aliongeza kusema "Basi ngoja nikaendelee na majukumu yangu ya kiofisi ila jioni nitakuja kukusabahi"

"Sawa mama asante sana kwa ukarimu wako" Alijibu Walemi.

**********

Baada ya siku kadhaa mbele Walemi anapata nafuu, aliruhusiwa kurudi nyumbani huku akiambiwa dozi anaweza kuimalizia nyumbani. Walemi anakaribishwa nyumbani kwa Emakulata,mwanamama asiye na mwana hata mmoja. Maisha yake ni yakihafari sana, aliishia Mikocheni B. Nyumba yake ni nzuri kupita maelezo, nje uwani zilipaki gari mbili za kifahari. Hilux,Bmw X5. Mbali na kuwa na vitu hivyo vya kifahari, vile vile Emakulata aliishi na mwanaume ambaye ni raina wa Paris ingawa maisha ya mwanaume huyo yalitegemea pande mbili tofauti. Tanzania na Paris.

"Karibu sana Walemi hapa ndio nyumbani kwangu, jisikia upo nyumbani" Ilisikika sauti ya Emakulata akimkaribisha Walemi nyumbani kwake. Muda huo Walemi hakujibu bali alikuwa angavu akitazama huku na kule maanzali ya nyumba namna ilivyo ndani. Lilikuwa jambo la ajabu sana kwa Walemi,kitendo ambacho kilimfanya kimoyomoyo kujisemea "Ama kweli tembea uone, yani nyumba kama upo pepeni?.." Kwisha kujisemea hayo aliketi chini sakafuni akihofia kuchafua masofa ya ndani humo, kitendo hicho kilimshangaza sana Emakulata kwa sauti ya upole akasema "Sio vizuri Walemi, hebu simama ukae kwenye kiti usihofu jisikie kama upo nyumbani"

Walemi alinyanyuka kwa wasi wasi alizitazama nguo zake alizovaa kisha akatupia macho kwenye masofa yaliyokuwepo hapo sebuleni, nafsi ikamsuta kuwa asikie huku akili ikimuaminisha kuwa anaweza kuchafua kutokana na nguo zake zilizochakaa. Lakini mwishowe aliketi. Punde si punde Emakulata akamletea chakula kizuri pamoja na juice ya matunda.

"Walemi,mimi hapa naishi na mume wangu tu. Sina mtoto wala ndugu.."

"Doh! Pole sana Anti, na kivip unasema huna ndugu?.."

"Kwanza suala nzima la mimi kutokuwa na watoto ni tatizo tu la ugumba ambalo ambalo lilitokea kipindi nipo shule, nilipata mimba nikaitoa ili nipate kuendelea na masomo. Kitendo hicho kikawa kimeghalimu uwezo wangu wa kutunga mimba,na suala la mimi kutokuwa na ndugu. Ukoo wa baba ulikuwa mfupi, hivyo walipokufa kwenye ajari yeye pamoja na mama pia mdogo wangu, habari ikawa imeisha hapo "

" Pole sana Anti, lakini ilikuwaje wewe ukapona?.. "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Ni Mungu tu Walemi, sababu siku hiyo wanasafiri mimi nilibaki ili nimalizie mtihani shule. Ukweli lilikuwa pigo kubwa kwangu na kibaya zaidi marehemu baba wala mama hawakuwahi kutoenyesha watoto wao ndugu zetu walipo. Sababu ambayo nilisikia kuwa wazee wetu wakati wanaoana wazazi wao pande mbili walikuwa hawajaliafiki, na hata hiyo ajari ilisemekana kuna mkono wa mtu " Yalikuwa mazungumzo ambayo Emakulata alikuwa akizungumza na Walemi wakati huo wakila chakula. Emakulata alimueleza Walemi kwa ufupi kuhusu maisha yake, mkasa ambao ulimuacha mdomo wazi Walemi.

Maisha sasa yakawa yenye furaha kwa Walemi, alinunuliwa nguo za kisasa na viatu vya kisasa pia. Uzuri ambao ulikuwa umepotezwa na shida dhahili ukaoneoana machoni pa watu. Lakini furaha hiyo ya Walemi haikuwa ya kudumu,ilitoweka mfano wa mshumaa uzimikapo baada asubuhi moja kuamka na kukuta Emakulata amekufa kwa kunyongwa..

"Mungu wangu Emakulata!.." Alistuka Walemi huku hofu ya kuishiwa kuua ikimtawala moyoni mwake.





Ilikuwa ni asubuhi ya bahati mbaya sana kwake, ni pale alipoamka na kufanya usafi wa nyumba mpaka anamaliza pasipo kumuona Emakulata na sio kawaida yake. Hilo suala lilimshtua kidogo Walemi istoshe usiku wa jana mumewe alirejea kutoka Paris ambapo kati yao walikuwa na mgogoro wa chini chini,jambo ambalo lilimfanya Walemi kuamini kuwa huwenda Emakulata bado anahasira za jana, hivyo aliendelea na shughuli nyinginezo ndogo ndogo. Lakini baadaye nafsi ilimsuta, kwani muda ulizidi kutokomea pasipo Emakulata kutoka chumbani. Hapo ndipo Walemi alipoamua kwenda kuchungulia kwenye upenyo wa mlango ili atazame chumbani aone kama bado Emakulata bado u kitandani kalala ama la! Ajabu alipokuwa ikihaha kuchungulia mlango ulifunguka, kitendo ambacho kilimshtua.

"Kumbe mlango upo wazi?.." Alijikuta akijisemea hivyo huku pole pole akichungulia chumbani. Ghafla alipiga mayowe huku akifunga mlango kwa haraka haraka. Kwa macho yake aliushuhudia mwili wa Emakulata ukining'inia,hapo ndipo alipokumbuka ushapu aliokuwa nao yule mwanaume wa Emakulata asubuhi alipoamka.

"Walemi karibu sana jisikie upo nyumbani. Aamh! Mimi nafika kwa rafiki yangu mara moja ila sio muda mrefu nitarudi sawa mama?.." Yalikuwa ni maneno ya huyo mwanaume ambaye Walemi hakumfahamu kwa jina, maneno hayo aliyasema huku akiwa na hofu fulani wakati huo mkononi akiwa na begi ndogo ilihali akionekana kupendeza kama mtu anayesafiri. Pumzi ndefu alishusha Walemi baada kukumbuka maneno hayo, hofu dhofu lihali ilimjaa moyoni mwake wakati huo akifikiria ni namna gani ya kuukwepa huo msala, kwani hatakama hatohusishwa na mauaji ila lazima atasota lumande.

"Mungu wangu, mbona kila nguzo ninayopata inavunjika? Nikimbilie wapi?.." Alijiuliza Walemi huku machozi yakimtoka, hakika alijihisi kama mtu aliyezaliwa na bahati mbaya hapa Duniani,alienda mbali kufikiria maisha ya kurudi katika hali ya kuombaomba wakati tayari tabu hiyo alikwisha isahau. Hivyo mara baada ya kufikiria kwa kina mwishowe aliona hana cha kupoteza aliondoka humo ndani, nje akamkuta kijana mfungua geti. Kwa sauti yenye hofu na woga ndani yake Walemi alimwambia "Una habari kama Emakulata kanyongwa?.."

"Kanyongwa?.." Alihoji kijana huyo huku akionyesha kutoyaamini maneno ya Walemi kwani aliamua kuingia ndani ili athibitishe. Nafasi hiyo Walemi akaitumia, akaondoka zake nyuma akimuachia balaa mfungua geti. Muda mchache alisikia ving'ora vya police, kitendo hicho kilimfanya aongeze kasi ya kukimbia. Hakutaka kuendelea kuonekana maeneo hayo ya maisha ya bei ghali, bali alikimbilia uswahilini maeneo ya Mwananyamala. Alilia sana Walemi, bado hakujua kwanini yanamtokeaa yote hayo? Sasa akakumbuka nyumbani kwao,alitamani siku yoyote arudi kuliko tabu anazozipata katika jiji la Dar es salaam. Tabu hizo zilimfanya kuziyeyusha pole pole ndoto za kuonana na Lameki kw mara nyingine tena,alijihisi mkosefu kwa wazazi wake na hivyo anahitaji kurudi ili akaombe msamaha. Yote hayo Walemi alikuwa akiyawaza akiwa amejibanza kando ya nyumba iliyopo moja ya mitaa ya Mwananyamala,ilikuwa ni jioni jua likitokomea.

Tabu hizo zilimfanya Walemi kukumbuka kidogo maisha ya nyuma, ni zamani kidogo jioni moja ambayo alikutana na Daniel.

"Walemi,kuna jambo moja nataka nikueleze" Alisema Danie kisha akakaa kimya.

"Jambo gani hilo mpenzi?.."

"Ni kuhusu mstakali wa penzi langu mimi na wewe, naelewa umenipenda lakini siku zote mapenzi pasipo pesa ni ngumu sana kuaminiana" Aliongezea kusema Daniel.

"Mmh" Walemi aliguna kisha akamuuliza "Unamaana gani Dani?.."

"Maana yangu ni kwamba ili penzi letu liote mizizi migumu? Basi yanipasa kutafuta pesa kwanza"

"Anhaa hapo nimekuelewa lakini tambua mimi sijakupendea pesa bali nimekupenda mwenyewe na istoshe wewe ndio mwanaume wangu wa kwanza kabisa"

"Ahahah ah hahaha" Aliangua kicheko Daniel kisha akasema "Naam! Hapo tu ndio umenikosha. Unajua siku hizi wasichana kujitunza ni vigumu sana ila kwa wewe nimekuelewa. Aamh tuachane na hayo, lengo na nia kuu ya kukuita hapa jioni hii ni kukutaarifu kwamba kesho nasafiri naelekea Dar es salaam kutafuta maisha" Walemi alishtuka baada kuyasikia maneno hayo ya Daniel. Kwa taharuki kubwa akasema "Unasemaje Dani? Yaani unataka kuondoka uniache mimi peke yangu? Hapana suala hilo ni ngumu sana kukubaliana nalo, lazima tuondoke wote.."

"Walemi mpenzi jaribu kuwa mstaarabu basi, mimi mwenyewe naenda huko nikitegemea nitafikia kwa rafiki yangu. Je, chumba kimoja tutalalaje? Cha msingi vuta subira mambo yakikaa sawa nitakuita uje tuishi wote sawa mpenzi?.." Walemi hakusema jambo,alikaa kimya huku akionyesha kughadhibika. Hakika taarifa hiyo ilimchefua kwani aliamini kuwa huwenda Daniel akapata mwanamke mwingine na ikampelekea kulowea. Lakini mwisho wa yote alikubaliana na uamuzi wa Daniel japo kwa shingo upande ila hakusita kumpa baraka zote hali ya kuwa wote kwa pamoja wakiwekeana nadhiri ya dhati kwamba ipo siku watakuwa mke na mume, jambo ambalo lilikwenda tofauti kabisa. Daniel alilowea mpaka kupelekea wazazi wa Walemi kumtafutia mchumba mwingine ambaye Walemi hakupendezwa naye ambapo sababu hiyo ikampelekea kukimbilia jijini Dar es salaam, uamuzi ambao mwishowe alijikuta ukimuweka matatani kwa kukumbana na magumu ya hapa na pale.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walemi alipokwisha kukumbuka hayo alishusha pumzi ndefu huku machozi yakimtiririka kisha punde si punde akili yake kwa mara nyingine tena akairudisha kwenye kisiwa cha kumbukumbuku. Safari hiyo alikumbuka siku ile aliyomuona Daniel wake, kumbu kumbu hiyo ilimtoa chozi alilia sana asiamini kama ni kweli Daniel ameondoka katika mazingira ya kutatanisha.

Kesho yake asubuhi Walemi alianza kutembea huku na kule kutafuta kibarua mitaa ya Mwananyamala, alifanya hivyo ili aweze kupata chochote cha kutupia tumboni mwake na kazi aliyoiona pekee inamfaa ni kupika chakula mgahawani (Mama ntilie) alichagua kazi hiyo kutoka na ufinyu wa Elimu yake. Lakini napo kupata kwake kazi hiyo ilimuwea vigumu, sababu kila mgahawa aliofika kuomba kazi aliambiwa nafasi zimejaa. Hali ambayo ilimchosha Walemi ila hakukata tamaa. Kabla giza totoro halijalivaa jiji la Dar es salaam, mara ghafla alikutana na mzee mmoja wa makamo. Mzee huyo alikuwa amevaa kanzu safi na barakashia kichwani huku mkononi akiwa na mikataba baadhi ya nyumba. Mzee huyo alikuwa dalali maeneo hayo. Walemi alimsimamisha mzee huyo kisha akampa salamu yake, mzee akajibu "Aaah mtoto mzuri kama wewe unaniamkiaje mimi? Mjini hapa hakuna mzee wote vijana tena tunapambana mpaka tonya la mwisho" Walemi alishangazwa na maneno hayo lakini hakutaka kujaji sana zaidi alieleza shida yake ili aone kama mzee huyo ataweza kumsaidia.

"Baba natafuta kazi.."

"Unatafuta kazi!! Haya kazi gani?.."

"Hata kazi ya ndani ama kazi ya mama ntilie mimi nafanya tu" Alijibu Walemi. Mzee huyo alikaa kimya kidogo huku akionekana kutafakari jambo fulani, punde alivunja ukimya huo kisha akasema "Kazi zipo nyingi sana, ila tu ni wewe kukubalina na matakwa yangu"

"Matakwa matakwa gani hayo tena?.." Aliuliza Walemi kwa taharuki kubwa.

"Kwanza upo tayari au unanipotezea muda tu hapa?.."

"Nipo tayari ila ndingependa uniambie matakwa hayo?.." Alijibu Walemi. Mzee huyo akamtazama Walemi kuanzia juu mpaka chini, akaachia tabasamu kisha akamwambia "Nihitaji kwanza penzi lako"





Ni suala ambalo lilimshtua sana Walemi, hakuamini masikio yake kile alichokisikia kutoka kwa mzee huyo aliye hitaji penzi lake.

"Vipi umeshindwa niondoke zangu?.." Aliuliza mzee huyo. Walemi hakujibu alibaki kujiinamia tu na hata asiseme jambo lolote. Na ndipo mzee huyo alipoamua kuondoka zake huku nyuma akimuacha Walemi akiwa bado analitafakari suala hilo. "Eeh Mungu wangu, ni nini hatma ya maisha yangu katika jiji hili? Mbona kila niangukiapo kuna vikwazo?" Alijiuliza Walemi ndani ya nafsi yake huku akikuna kisogo chake, iliona ni maswahibu makubwa mno anayokumbana nayo tangu afike jiji hapo.

"Ni kweli leo napata kuona maana ya ule msemo usemao mjini cha bure salamu tu, nitaishije bila kazi mtoto wa kike mimi?.." Aliongezea kujiuliza Walemi, na mwishowe alikata kauli akatimua mbio kumfuata mzee huyo aliyehitaji penzi lake ili amtafutie kazi.

"Unasemaje?" Alihamaki mzee huyo mara baada kusikia sauti ya Walemi ikimuita.

"Nimekubali ila usinidanganye sawa?.." Alisema Walemi huku tabasamu fake likitamalaki usoni mwake. Mzee huyo aliposikia maneno hayo ya Walemi aliangua kicheko,jibu hilo lilimfanya kufurahi mara dufu moyoni mwake, na ndipo mkakati wa kutafuta nyumba ya wageni ulifanyika ili avunje jungu namna iwezekanavyo.

************

"Hakika sikutegemea kama ningeonja penzi lako, mtoto mzuri umejazia kila pande. Na kwa mautundu yako nahisi wewe umezaliwa Tanga" Ilikuwa ni sauti ya mzee aliyetimiza azma yake ya kufanya mapenzi ya Walemi. Maneno hayo aliyasema mara baada kumalizika kwa tendo. Walemi alicheka kidogo, punde akaishusha pumzi yake ndeefu kisha akasema "Hapana mimi sio mtu wa Tanga, nimezaliwa Dodoma na nimekulia Dodoma.."

"Laah! Kumbe? Kiukweli sikutegemea wasichana wa Dodoma kama nao ni mafundi kiasi hiki. Hongera sana mrembo. Na jina lako unaitwa nani?.."

"Naitwa Walemi"Alijibu kwa mkato Walemi huku akishuka kitandani. Aliposimama sakafuni akasema" Naona tayari kumekucha, vipi kuhusu ule mpango?.. "

" Mpango? Mpango gani sasa?.. "Alihamaki mzee huyo. Walemi alishtuka, uso wake ukionyesha taharuki fulani aliongeza kusema." Kwa maana hiyo umesahau makubaliano yetu?.. "

" Ahahah ah hahaha "Aliangua kicheko mzee huyo kisha akajibu" Binti hapa mjini unatakiwa kujiongeza katika jambo la faida kama hili.. " Alipokwisha kusema hayo aliendelea kucheka huku Walemi akimtazama tu wakati huo akihisi kuchanganyikiwa juu ya kile anacho kisikia.

" Walemi, mimi ni dalali wa nyumba na viwanja vile vile magari. Mimi sio dalali wa kumtafutia mtu kazi,lakini pia bado hakijaharibika kitu. Unanafasi ya kujiingizia kipato hapa mjini na maisha yakasonga kwa upande wako. Wewe ni mwanamke mzuri sana, uzuri wako unafaida kubwa sana " Alisema mzee huyo.

" Unamaana gani?.. "Walemi Aliuliza, kabla huyo mzee hajamjibu akaongeza kusema." Na kwanini unakuwa katili namna hii, umenilaghai, nimevua utu wangu nikakupa penzi kwa dhumuni la kupata kazi lakini mara hii wanigeuka?.. "

" Sio kukugeuka, ndio maana nimekwambia kuwa uzuri wako huo ni dili hapa mjini. Hivyo kwa kuwa umekutana na mimi mtu wa mjini, basi nitakuonyesha njia sahihi ya kujiingizia kipato kupitia uzuri wako. "Alisema mzee huyo kisha akacheka. Alipokatisha kicheko hicho akaongeza kusema." Uza mwili wako upate hela mama,mimi siwezi kukutafutia kazi ila nimekupa mbinu ambayo inaweza kukusaidia"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Uanasemaje?.. "Alihamaki Walemi, alistushwa na maneo hayo ya huyo mzee. Ni kejeri na dharau kubwa aliyoonyesha mbele yake na yote sababu alishamaliza hitaji lake. Walemi aliumia sana,hasira zilimjaa kiasi kwamba midomo yake ikawa inatetemeka kwa hasira. Alijihisi kukosa nguvu, akajitupa kitandani huku akishusha pumzi yake ndefu hali yakuwa mzee huyo naye pembeni alikuwa akiangua kicheko wakati huo akitelemka kitandani na kisha kuzipiga hatua kuelekea bafuni kuoga huku akiongea maneno chungunzima,maneno ambayo yalizidi kumkwaza Walemi ambapo mwishowe aliamua kutoka humo chumbuni akaelekea jikoni, huko akamkuta mpishi akiandaa chakula mahususi kwa wageni wafikao katika nyumba hiyo ya wageni.

"Habari yako dada" Walemi alimsalimu mwanadada aliyemkuta humo jikoni.

"Salama kwema?.." Mwandada huyo alijibu kwa mashaka,akistushwa na ujio huo wa Walemi mpaka jikoni. Walemi aliachia tabasamu pana kisha akaongeza kusema "Chai bado? Maana nasikia njaa ndio sababu iliyonifanya nikufuate jikoni"

"Ndio naanda hapa ila nafikiri ndani ya nusu saa itakuwa tayari hadi supu pia" Alijibu dada huyo saa safari hiyo akiitazama jiko akimpa kisogo Walemi. Nafasi hiyo ilimpelekea Walemi kuchukua kisu akakificha nyuma, na punde si punde akaaga akaondoka zake moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba alicholala na yule mzee aliyejionyesha kuwa ni dalali wa nyumba na viwanja. Hapo alimkuta akiwa ndio ametoka bafuni muda mchache uliopita, hivyo alikuwa akijifuta maji maji sehemu mbali mbali za mwili wake.

"Umerudi? Mimi nakadhani umeondoka kwenda kulifanyia kazi suala hilo nililokushauri" Alisema mzee huyo. Akaongeza kusema. "Ama ushauri wangu mbaya? Basi Kama unaona mbaya fanya kile ambacho moyo wako unapenda" Alikomea hapo kisha akaangua kicheko kama kawaida yake. Muda wote anayasema hayo Walemi alikuwa amesimama mikono nyuma huku akimtazama tu. Mzee huyo hakujali aliendelea kujifuta maji maji na punde si punde akaanza kuvaa kanzu lake. Alipomaliza alichukuwa makashablasha yake, tayari kwa safari ya kuelekea katika mihangaiko yake. Lakini kabla hajaondoka, Walemi alisimama mlango, kwa hasira kali akasema "Maneno yote umemaliza ila bado sijajua lengo lako ni nini?.."

"Khaa unataka nini sasa? Kama ni raha tumepata wote kwahiyo kipi tena unataka kutoka kwangu?.." Aliuliza mzee huyo kwa hasira naye vile vile.

"Hayo ndio makubaliano yetu?.." Alirudi kuhoji Walemi. Ni kama maswali hayo yalionyesha kumkera dalali huyo. Na ndipo kwa jazba kali akajibu "Sina muda wa kujibizana na wewe malaya wa kuja hapa mjini, huu ni muda wa kusaka shilingi na si vinginevyo. Hebu nipishe niondoke zangu"

"Kamwe huwezi kuondoka humu ndani, ni unyama ulionifanyia wewe mzee..." Alilia Walemi.

"Kwahiyo? Nikusaidie nini tena zaidi ya ushauri niliokupa? Ama kama haufai basi nenda ukaombe ombe barabarani sindio nyendo zenu nyie watu wa Dodo.." Kabla mzee huyo hajamaliza kusema alichotoka kukiongea, haraka sana Walemi alimchoma kisu kisha akakichomoa muda huo huo alimchoma kwa mara nyingine tena kitendo ambacho kilimpelekea mzee huyo dalali kuanguka chini huku akisafa ilihali damu kama maji ikitambaa kwenye sakafu mule chumbani. Walemi Alistaajabu, alikodoa macho na hata asiamini kile anachokiona. Kwa sauti ya juu huku akihema haraka haraka alijikuta akisema "Khaa nimeua.. Nimeua mimi" Alisema hivyo Walemi wakati huo akitazama mikono yake iliyotapakaa damu. Punde si punde alitoka mbio chumbani humo lakini kabla hajafika nje ghafla...



Ghafla alikutana na yule Mwandada mpishi aliyemuona kule jikoni,hima alijibanza kwenye moja ya koldo ambayo ilimpelekea dada huyo kutomuona. Alipo jihakikishia kuwa yupo salama kuondoka katika nyuma hiyo ya wageni alitimua mbio huku bado wasi wasi ukiendelea kutamalaki moyoni mwake. Hatamaye anabahatika kuondoka eneo hilo la tukio,ilikuwa ni maeno ya Kinondoni. Mfano wa mwendawazimu Walemi alikimbia huku na kule, alivuka barabara pasipo kutazama kulia na kushoto. Watembea kwa miguu walimtazama kwa mishango lakini pia abiria mbali mbali waliokuwemo kwenye daladala hasa zilizokuwa foreni, nao walipigiwa na butwaa kumuona Walemi akihaha kana kwamba anakimbizwa na mtu asiyeonekana.

Honi kali na bleki ya hapo kwa papo ilisikika, kwa mara nyingine tena Walemi anajikuta kunusurika kugongwa na gari.

"We kichaa nini?.." Ilisikika sauti ikihamaki, sauti ambayo ilitokea ndani ya gari hiyo iliyomnusuru Walemi kugongwa. Ilikuwa ni sauti ya mama mmoja mnene na mwaupe mfano wa papai la kizungu. Walemi akapiga magoti chini kuomba msamaha, hakuishia tu kuomba msamaha bali aliomba asaidiwe kwani alihisi nyuma kutakuwa na watu wanamfuatilia shauri ya lile tukio alilolifanya muda mchache uliopita.

"Nisaidie mama yangu tafadhali nisaidie, kuna watu wananifuata wanataka kuniua" Alisema Walemi huku akiangua kilio. Mama yule hakusita alimfungulia mlango wa nyuma, haraka sana Walemi akaingia kisha gari ikaondoka.

Kwa mara nyingine tena Walemi anajikuta yupo katika mikono ya mwanamama mashughuli mwenye pesa zake mjini. Ukiachilia mbali msaada ule alioupata kipindi kwa Emakulata ambaye mwisho wa siku alinyongwa na mumewe, Walemi anadondokea kwa mwanamama mwingine. Huyo aliishi Makongo, eneo tulivu kabisa lisilo na fujo.

"Karibu sana binti, hapa ndio nyumbani kwangu sijui ungependa nikusaidie kinywaji gani?.." Alisema mama huyo, akimkaribisha Walemi nyumbani kwake kwa tabasamu bashasha kabisa. Walemi alishusha pumzi kwanza kisha akajibu "Hapana sihitaji kinywaji chochote mama yangu?.."

"Mmh kwanini? Sio vizuri ujue. Halafu istoshe pale nilipokuona unaonyesha ulikimbia muda mrefu kwahiyo lipoze koo hata kwa soda tu" Aliongezea kusema mama huyo. Maneno hayo yalimfanya Walemi kuachia tabasamu kisha akasema "Basi nisaidie maji tu"

"Mambo si hayo?.." Aliunga mkono mwanamama huyo na papo hapo akaambaa kuelekea mahali lilipo freji. Kwa muda wa dakika kadhaa tayari walionekana mezani, Walemi akiwa na grasi yenye maji, huku mwanamama huyo naye akiwa na grasi iliyojaa juice. Hapo zogo mbili tatu zilifuatia, mama huyo akianza kwa kujitambulisha jina lake.

"Naitwa Pendo, sijui mwenzangu unaitwa nani?.."

"Naitwa Walemi.." Alijibu Walemi kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake huku uso wake ukitandabaisha kuwa ni mtu mwenye mashaka na wasi wasi. Jambo hilo Pendo aliligundua kwa kumtazama usoni na ndipo alipomuondoa hofu huku akitamani kujua ni kitu gani sana kimemsibu mpaka kuwa katika hali hiyo.

"Basi tu mama yangu, kuna wahuni walitaka kunibaka. Istoshe walinitishia kuniua" Alidanganya Walemi, safari hiyo uso wake akiwa ameinamisha chini.

"Pole sana Walemi, wazazi wako wapo wapi?.."

"Wapo mkoani Dodoma, nimetoroka nyumbani baada wazee wangu kunilazimisha kuolewa na mwanaume nisiyempenda"

"Mmh pole Sana, Enhee na hapa mjini unajihughulisha na kazi gani?.." Walemi alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Nilikuwa nafanya kazi Bar lakini nimefukuzwa baada wateja kunigombanisha na boss wangu kwa madai madai kuwa nawauzia pombe ikiwa mimi sinywi"

"Sawa, yote hiyo ni mtihani ya maisha. Nakupa pole kwa mara nyingine tena ila nipo tayari kukusaidia. Nitakupa kazi ambayo nitakuwa nakulipa mwisho wa mwezi, cha kuzingatia ni nidhamu ya kazi na sio kuwadharau wateja. Utaisha hapa hapa nyumbani kwangu sawa?.. "

" Sawa, pia nashkuru kwa msaada wako. Lakini ningependa kufahamu kazi hiyo ni kazi gani?.. "

" Usiwe na haraka utajua tu "Alijibu Pendo kisha akainuka akaelekea chumbani kwake wakati huo huku sebuleni Walemi alibaki na sintofahamu kuhusu kazi hiyo.

" Mmh kazi gani hiyo? Mbona ananiambia niweke nidhamu kwa wateja?.. "Alijiuliza Walemi. Kabla hajapata jibu la swali lake hilo Pendo alirejea akaketi sebuleni kisha zogo mbili tatu zikiendelea.

Pundo ni mwanamke mnene na mweupe sana, alikuwa ni mama mkubwa wa makamo. Aliishia peke yake tu licha ya utajiri aliokuwa nao mwanamke huyo, ambapo pia mbali na hayo alijishugulisha na biashara mbali mbali kwani alikuwa na maduka ndani na nje ya nchi. Maisha ya Pendo yalikuwa ya raha sana, pesa alikuwa nazo nyingi mno hivyo aliweza kusomesha watoto wake shule za ghalama lakini pia aliwafungulia bank kila mmoja. Alikuwa na watoto wawili tu wakike na wa kiume.

"Basi Kama nilivyokwisha kukueleza Walemi,ili upate kuishi na watu lazima heshima ifuate mkondo" Alihitimisha Pendo mara baada ya zogo la muda mrefu.

"Sawa mama nimekuelewa" Alijibu Walemi, lakini ajabu Pendo alikana kuitwa mama, kwa sauti ya chini kabisa akamwambia "Usiniite mama,niite Anti tu inatosha" Aliachia tabasamu Pendo mara baada kusema maneno hayo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku iliyofuata Walemi akiwa chumbani kwake huku akingojea kuelekezwa kazi anayotakiwa kufanya, mara ghafla alisikia kwa mbali mazungumzo sebuleni. Mazungumzo hayo yalikuwa baina ya Pendo na mwanaume ambaye hakumfahamu. Mwanaume huyo alikuwa ni mwenye mwili mkubwa, alivalia suti nyeusi na viatu vyeusi huku mkononi akiwa amevalia saa ya ghalama.

"Umekuja kwa muda muafaka kabisa" Alisema Pendo.

"Yes unajua mimi ni kama mzungu ingawa nimwafrika. Haya nipe mambo mbona chombo sikioni?.." Alijibu mwanaume huyo.

"Usiwe na haraka, taratibu. Tuliza presha bwana. Tena leo unatakiwa upande dau kidogo maana mtoto mtoto kweli?.." Alisifu Pendo,

"Pesa? Pesa kwangu sio tatizo Pendo,kinachotakiwa sasa ni kumuita mtoto mwenyewe ili akanipe vitu adimu maana nina uchupa sana. Ahahah ha hahahahaha" Aliongezea kusema mwanaume huyo kisha kumaliza kwa kichoko cha kibosi. Yote hayo Walemi alikuwa akiyasikia, hakika hakuyaamini masikio yake,alijikuta akihema juujuu baada kuona yupo katika himaya ya mwanamama mshenzi anayejihusisha na biashara ya kuuza mabinti.

"Eeh Mungu nisaidie" Alisema Walemi huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio. Na wakati yupo katika hali hiyo, ghafla alisikia sauti ya Pendo ikimuita.

"Walemi.. Walemi.. Walemi"

"Abee Anti nakuja" Aliitika Walemi na mara moja akatii wito.

"Kama nilivyo kwambia hapo awali, sitaki uniangushe" Alisema Pendo na punde akamgeukia yule mwanaume aliyekuwa akiongea naye kisha akaongeza kusema "Chombo hicho, dondosha pesa KWANZA kisha ukafanye yako. Dakika kumi tu ukizidisha utaongeza pesa.."







"Ahahaha hahaha ha! Pendo, kuhusu hilo wala usijali. Pesa kwangu sio tatizo, muhimu binti anikoshe tu" Alisema mwanaume huyo huku akimpapasa mabega Walemi ambaye alikuwa karibu yake kwa muda huo. Walemi hakufurahishwa na kitendo hicho, hivyo aliutoa mkono wa mwanaume huyo kwenye mabega yake ambapo Pendo aliweza kumkea huku akimtishia kumpiga.

"Binti twende, istoshe kuna fungu lako nitakupatia" Aliongezea kusema mwanaume huyo huku akimvuta Walemi chumbani.

******

Mchezo ulipokwisha Walemi alilia sana, hakuamini kama kweli Pendo ni mshenzi kiasi hicho. Uchungu mkubwa ulimkumba moyoni mwake, alijiuliza kipi ameikosea duniani maana kila kukicha heri ya jana. Kila nguzo anayoegemea inavunjika, maisha ya tabu furaha haidumu.

"Kwanini kila siku mimi?" Alijiuliza Walemi akiwa ameketi kitandani huku akiwa amejiinamia kilio nacho kikichukuwa nafasi. Muda huo huo mwanaume huyo aliyemaliza naye tendo alimgusa mgongo,kitendo ambacho kilimchefua akamgeukia nakisha kumpiga kofi shavuni. Ghafla mwanaume huyo aliwaka, alikasirika akashuka kitandani akavaa nguo zake wakati huo akiongea maneno chungunzima "We malaya unathubutu kunipiga mimi? Sio rahisi kihivyo, umenivunjia heshima mshenzi wewe. Kwa uzuri gani ulionao mpaka unipige?.." Alisema huyo mwanaume. Walemi aliogopa, haraka sana aliomba msamaha kwani alijua atabaki katika wakati mgumu pindi Pendo atakapo fahamu jambo hilo.

" Siwezi kukusamehe ila cha moto mtakiona wewe na bosi wako "Aliongezea kusema hivyo mwanaume huyo kisha akatoka chumbani. Alipofika sebuleni alimkuta Pendo kasimama kuashiria kuwa muda wote alikuwa anayasikiliza malumbano yaliyokuwa yakiendelea chumbani baina ya mteja wake na Walemi.

" Kunani Mr?.. "Aliuliza Pendo kwa taharuki.

" Sina haja ya kuendelea na wewe, umeamua kuniletea mtu ili anidhalilishe sio? Ok asante bwana ila mguu huu ndio mwanzo na mwisho kukanyaga hapa nyumbani kwako. Mimi sio wa kupigwa na huyo malaya asiyejua hata kufua nguo za ndani" Alifoka mwanaume huyo. Bado Pendo alionyesha kuchachawa, maneno ya mteja wake yalimfanya kuwa roho juu kwani ndio biashara ambayo ilikuwa ikimuingizia kipato kikubwa kuachilia mbali maduka aliyokuwa nayo nje na ndani ya nchi.

"Kaa chini tuzungumze, unavyotaka kufanya hivyo sio vizuri Mr" Alisema Pendo kwa sauti ya upole kabisa.

"Nani akae? Mimi? No.. No... No sitaki inatosha utanitafuta kwa muda wako" Alijibu mwanaume huyo kisha akaondoka zake huku nyuma akimuacha Pendo ameshika kichwa chake kana kwamba a nakaribia kuchanganyikiwa. Baada ya hapo alipasa sauti kumuita Walemi kwa sauti kali iliyosheheni hasira kuu "Walemi.. Walemi"

"Abee Anti?.."

"Njoo hapa, naona sasa unataka kunipanda kichwani" Alifoka Pendo wakati huo mara moja Walemi alitii wito huku mboni zake zikionyesha kuvuja machozi.

"Kwanini umekwenda kinyume na maelekezo niliyokupa?.." Alifoka Pendo. Walemi aliogopa, alifuta machozi yake wakati huo huo machozi yakiendelea kumtoka. Lakini licha ya Walemi kuonyesha hofu usoni mwake ila bado Pendo hakuweza kumuhurumia, alizidi kumuuliza kwa msisitizo.

" Nisamehe Anti, nisamehe sana sitorudia tena" Aliongea Walemi kwa sauti ya upole kabisa iliyojaa huzuni nzito ndani yake. Na wakati anaomba msamaha mara ghafla ujumbe mfupi uliingia kwenye simu ya Pendo, haraka sana Pendo aliichukuwa simu hiyo na kisha kuutazama ujumbe huo. Aliusoma, akasthuka akakunja sura kisha akampa Walemi simu ili naye ausome ujumbe huo.

"Mimi ndio Mr Daud nafikiri unanijua vizuri hasira zangu pindi ninapo chafukwa na roho. Hautuniona tena hapo kwako mpaka kinyago chako ukitimue" Ulisomeka hivyo huo ujumbe. Ni ujumbe ambao ulizidi kumchefua Pendo ilihali muda huo Walemi akionekana kukosa cha kuongea. Punde si punde Pendo akamwambia "Sipo tayari kuendelea kukaa na wewe hapa, utakwamisha mambo yangu mengi sana. Kilichobaki hapa ondoka hivyo hivyo ulivyokuja"

"Anti! Niende wapi mimi?.." Aliuliza Walemi kwa sauti ya kilio. Pendo akajibu "Kwani mwanzo nilikutoa wapi? Ondoka kabla sijakufanyia kitendo kibaya"

"Kweli Anti umeamua kunifukuza? Sawa basi naomba hata pesa kidogo ya kuanzia maisha mapya. Tafadhali nisaidie"

"Walemi? Nitakufanya kitendo kibaya ambacho hutokuja kusahau maishani mwako, ondokaa mjinga wewe" Alitishia Pendo, kitendo ambacho kilimuogopesha Walemi, haraka sana akatoka ndani ya nyumba hiyo na kisha kurudi mtaani kwa mara nyingine huku moyoni akiwa na hofu kubwa kutokana na mauaji aliyoyafanya siku mbili nyuma. Mbali na hilo, pia Walemi alihofia kusakwa na jeshi la police juu ya kifo kile cha Emakulata.

"Mungu nisaidie" Alijisemea Walemi huku akiambaa na moja ya mitaa ndani ya jiji la Dar es salaam.

Akiwa katika pitapita yake, ghafla anaguswa bega. Ni saa ya jioni sasa. Walemi alishtuka, haraka sana akageuka nyuma kumtazama mtu huyo aliyemgusa.

"Ahahah ah hahaha" Aliangua kicheko mtu huyo, bado Walemi alipigwa na butwaa na kushindwa kumuelewa huyo mtu.

"Ananifahamu ama?.." Alijiuliza Walemi huku akihema juujuu. Lakini kabla hajapata jibu la swali hilo alilojouliza, punde mtu huyo akasema "Habari yako dada, nina jambo moja tu nataka nikueleze na itabidi uwe makini sana.."

"Jambo gani? Na wewe ni nani?.." Alirudia kuhoji Walemi kwa hofu kubwa moyoni.

"Naitwa Dito, mpiga picha maarufu kitaa hiki hapa" Alisema mtu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina Dito. Dito alikuwa amevaa begi ndogo mkongoni,wakati huo camera yake ikining'inia shingoni.

"Enhee kwahiyo? Je, umesikia mimi nataka kupiga picha?." Aliuliza Walemi. Dito kwa mara nyingine alicheka kisha akasema "Sina maana hiyo na ndio maana nimekwambia unahitaji uturivu ili uweze kunielewa kipi najitaji"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kitu gani? Hebu achana na mimi" Alijibu Walemi kwa hasira huku akiendelea kuambaa na uchochoro. Ukweli alionekana kuchanganyikiwa hasa juu ya maswahibu yanayo mkumba, vile vile istoshe siku hiyo hakuwa na uhakika wapi atalala hali ya kuwa yeye ni mwanamke. Hivyo mpiga picha huyo ni kama alizidi kumchanganya zaidi. Lakini wakati Walemi anazipiga hatua za kuondoka ilihali akiwa amemkacha Dito, ghafla alisikia sauti ya Dito ikimuita "We dada?.." Walemi akaguka. Muda huo huo Dito alifungua zipu ya begi lake akachomoa picha kisha akamuonyesha.

"Hii ni picha yako dada bila shaka yoyote,na unajua ulichokifanya kule kwenye nyumba ya wageni.. Hivyo basi kaa ukijua wakati wowote picha hizi naweza kuzisambaza na kutoa taarifa juu ya kifo kile ulicho sababisha" Alisema Dito kijana mpiga picha. Walemi alishtuka sana, ghafla kijasho kikaanza kumtoka huku akishindikizwa kabisa kuelewa jamaa huyo alimpigaje picha pasipo yeye kujua, na ni kwanini aliamua kufanya hivyo pasipo idhini yake. Yote hayo Walemi alikuwa akiyafikiria ndani ya ubongo wake,ambapo mwishowe alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Kwanini umeamua kufanya kitendo hicho? Na ni nani aliyekwambia kuwa nimefanya mauaji"

"Hahahahaaa hahaha" Dito alicheka kwa kebehi kisha akasema "Sina muda wa kujibizana na wewe. Kila kitu kipo wazi, najua unafahamu unachotakiwa kufanya ili kunusuru maisha yako. Sababu tayari dau nono limetangazwa kwa mtu atakaye kuona"

"Watanijuaje? Kwani umeshawaonyesha picha yangu?.." Aliuliza Walemi kwa sauti ya woga. Dito akajibu "Lah! Sijawaonyesha ila mpishi wa pale kaelezea muonekano wako namna ulivyo. Na kama hii picha nitawaonyesha basi itakuwa rahisi sana kutiwa hatiani"

"Mungu wangu, sasa unanisaidiaje kaka yangu?.. :" Aliuliza Walemi huku akitetemeka mwili mzima. Kijana Dito bila hata kutafakari namna ya kumsaidia alisema "Milioni sita nipatie ili picha hizi niweze kuzifuta"

Milioni sita ni pesa ambayo mlima mrefu kwa Walemi hasa kulinganisha na maisha anyoishi. "Kwanini lakini unanifanyia hivyo? Hapa nilipo Sina hata mahali pa kuishi. Je, pesa yote hiyo nitaitoa wapi mimi?..Samahani kaka yangu hebu fikiria namna nyingine ya kunisaidia nipo chini ya miguu yako tafadhali " Alilia Walemi. Lakini Dito wala hakujali kilio chake,aliamua kuondoka huku nyuma akimuacha Walemi akiendelea kububujika machozi. Kwa mbali ilisikika sauti ya mwanamama akilalama. Sauti hiyo ilikuwa ikisema" Binti unakuwa mchafu mchafu tu, mara unasahau kudai pesa. Hivi unafikiri huu mtaji nimekupata kwa kuhongwa? Sasa nasema hivi kesho nisikuone hapa kwenye mgahawa wangu. Haiwezekani kila siku unanitia hasara, kwanza huna uchungu na maisha na ndio maana jambo hili unalichukulia kawaida " Ilisema sauti hiyo. Ilikuwa ni sauti ya mama mmoja ambaye alikuwa akijishughulisha na kazi ya mama ntilie,siku hiyo huyo mama alikuwa amechafukwa na roho baada msaidizi wake kutoonyesha umakini katika kazi. Hivyo siku hiyo aliamua kumwambia ukweli huku akimuachisha kazi mara moja ikionyesha kuwa msaidizi wake huyo amekuwa sikio la kufa. Walemi mara baada kusikia mzozo huo alizipiga hatua kuelekea mahali hapo huku akiachana na yule mpiga picha aliyetaka pesa nyingi kuliko maisha yake. "Liwalo na liwe, kama dunia tambala bovu basi sina budi kulidekia kwa shida. Mungu nisaidie" Alijisemea Walemi ndani ya moyo wake wakati huo akizidi kujongea mahala pale palipokuwa na mzozo. Alipofika alimaliza mama huyo kwa sauti ya chini kabisa "Malakhabaa mwanangu hujambo?.." Alijibu mama huyo kwa sauti ya ukarimu kabisa iliyomfanya Walemi kushusha pumzi kwanza na hata asiamini kama kweli huyo ndio yule aliyekuwa akifoka muda mchache uliopita.

"Sijambo, amh samahani mama.."

"Bila samahani"

"Eti naweza kupata kazi?.."

"Kazi? Kazi gani sasa ambayo unahitaji?.."

"Kazi yoyote tu hapa, hata kuosha vyombo aidha kupika. Yani kazi yoyote tu mama maana ninashida sana. Nipo chini ya miguu yako tafadhali"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Basi huna sababu ya kunisujudia binti, sababu hii ni kazi ambayo isiyo hitaji Elimu kubwa sana,muhimu kujitambua na kutambua nini wateja wanataka,vile vile uaminifu katika kazi. Muda mchache uliopita nimemtimu binti mmoja hivi alikuwa ananisaidia saidia hapa. Sababu anakiburi sana, unamwambia hivi yeye anafanya vile. Ukweli nimemvumilia sana ila mwishowe nimenyoosha mikono juu. Kwahiyo wewe utashika nafasi yake sawa?.. ". Alisema mama huyo. Hakika Walemi alifurahi sana ambapo kwa mara nyingine tena akapiga magoti chini kumshukuru mama huyo. Lakini huyo mama alimuinua kisha akamuuliza" Unaishi wapi?.. ". Walemi alishusha kwanza pumzi ndefu kisha akajibu" Ukweli sina mahali pa kuishi. Yani maisha yangu yamekumbwa na mitihani mizito sana " Alilia Walemi kwisha kusema hivyo.

" Pole sana, usijali utakaa kwangu. Naishi na mtoto wangu lakini pia na mdogo wangu ila yeye ni mwanafunzi. Pole sana mdogo wangu " Alisema mama huyo. Kwa mara nyingine tena Walemi anapata msaada. Furaha isiyokifani ilitawala ndani ya moyo wake lakini furaha hiyo hiyo ilitoweka pindi alipofikiria juu ya suala la zile picha ila mwishowe alichukulia kawaida tu liwalo na liwe ndilo neno shina alilokuwa akitembea nalo.

**********





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog