Search This Blog

KARIBU KUZIMU - 2

 






Simulizi : Karibu Kuzimu

Sehemu Ya Pili (2)





Nikakanyaga ngondi kuikaribia Mabibo mwisho, kufika Mabibo mwisho sikupanda daladala nikaendelea kukanyaga ngodi mpaka nilipofika Mabibo Loyola. Jirani na shule ya sekondari ya Loyola nikakutana na kijana mmoja wa makamo akiwa kavalia kanzu pamoja na balaghashe akienda msikitini kuswali, kwa uchangamfu nikamsimamisha yule kijana nikamsalimu kisha nikamhoji.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kaka, samahani eti...hapa ni wapi?,” Kaka yule akaniangalia kwa muda akionyesha kunidadisi kisha haraka akalijibu swali langu.



“Ni Mabibo Loyola,” Kaka yule alinijibu hima hima akaondoka huku hasijue kama kaniacha njia panda. Hata hivyo sikushindwa kuuliza akapita mtoto mmoja mwenye umri wa makadirio ya miaka kumi na miwili nikamsimamisha tena na nikamhoji.



“Eti, mtoto Kigogo Luhanga ni mbali sana?.”



“Sio mbali, ni kituo kinachofuata hapo mbele,” Mtoto yule alielekeza kisha akaomba aondoke, akaondoka. Hapo nikawa nishapata dira kutoka kwa yule mtoto basi nikaanza safari ya kuitafuta Luhanga. Nikafika Luhanga hapo nikamtafuta dada kwa njia ya simu ya mkononi aina ya Nokia Obama enzi hizo, nikampigia punde akapokea.



“Dada, nipo Luhanga,” Nikamhabarisha.



“Upo Luhanga!!!.... Nasikitika kuwa siwezi kuja,” Dada alinijibu kwa ukali. Akionesha dhahiri hakupenda uwepo wangu katika jiji la Dar es salaam.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kwanini, dada!!!?” Nikauliza kwa mshangao. Nisijue dada kimemkumba nini hadi amefikia kuzungumza vile.



”Mama kanipigia simu kaniambia umetoroka nyumbani, sababu hutaki kuolewa hivyo kaniambia ukija kwangu nisikupokee.... Kwa hiyo nakushauri mdogo wangu rudi tu nyumbani. Ujue siku hizi ndoa ni bahati sana” alitoa ushauri Dada wa kunishawishi nirudi Tanga nikakamilishe taratibu za ndoa.



“Dada, tegemeo langu lilikuwa ni wewe nikajua utanipokea vizuri. Lakini wewe unataka kunirudisha tena Muheza.... Sasa hiyo nauli ya kurudia ninayo?,” Nikaongea huku moyo ukisonona maana sikutaka kurudi tena Muheza.



“Nitakutumia nauli, tigopesa sasa hivi. Urudi,” Dada aliongea kisha akakata simu kabla sijamaliza maongezi nae.



Nikaganda katika kituo cha daladala cha Luhanga huku nikikumbata furushi langu lenye nguo, na nikibabaika nisijue kwa kwenda lakini nikiwa kwenye huzuni punde kwenye simu zikaingia jumbe mbili moja ikanijulisha kama dada tayari kanitumia pesa. Jumbe ya pili ilikuwa ni ya dada ikinitakia safari njema. Alinitumia kiasi cha elfu ishirini nauli ya kurudi Tanga, lakini haraka nikajifikiria ya nini nirudi Muheza nikaolewe na mtu nisiyempenda. Si bora nigande Dar es salaam nijue ni jinsi gani ya kujikwamua mwenyewe, wazo nikapuuza sikurudi Tanga tena bali nikakomaa katika jiji la Makonda. Nauli niliyopatiwa nikaweka kibindoni ije kunisaidia baadae, giza likaingia siku ikaisha nikatafuta kibanda umiza nijiegeshe mwili. Wakati nikitafuta kwa kulala mara nikaona kando yangu mgahawa akili ikanituma nilale mule nikalala, siku ya kesho yake ikanikuta pale nilichelewa kuamka kutokana na uchovu wa safari. Yapata saa moja kijua cha asubuhi kikiangaza kumekucha, sikujali nikachalaza usingizi wa kunoga mpaka pale niliposikia sauti ya kike ikiniita huku ikinitingisha mwili niamke. Nikaamka kwa kukurupuka mara baada ya kuitwa kwa muda mrefu na mama wa makamo.



“Usiogope binti,” Mama yule aliniondoa hofu mara baada ya kugundua kuwa nina hofu, akaninyanyua pale nilipokuwepo akanikalisha kwenye benchi kisha akauliza.



“Binti, unatokea wapi?. Halafu mbona umelala kwenye mgahawa wangu?.”



“Natokea Tanga Muheza, na nimelala katika mgahawa huu sababu sina kwa kijihifadhi,” Nikajibu.



“Sasa umetokea Tanga...ni nini malengo yako ya kuja Dar es salaam?, na hapa Dar es salaam una ndugu?.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Dar nimekuja kubadili maisha, na kuhusu ndugu hapa Dar ninao wachache.... Na isitoshe ndugu zangu hapa wanafamilia zao wameshindwa kunipa hifadhi,” Kiasi nikaongopa. Mama yule akanikodolea macho akiwa ananisikiliza kwa makini nilipokoma kueleza nikaona akicheka na kusikitika kisha akaendeleza maongezi.



“Binti, hili ni jiji la starehe. Pia nini jiji lenye ajira lakini kupata ajira nzuri ni ngumu.... Wewe ulitaka ajira gani?.”



“Yoyote tu.”



“Yoyote!!!.... Elimu yako ni ya nyanja gani?.”



“Elimu yangu, ni ya shule ya msingi.”



“Mh, kama ni ya shule ya msingi ajira zinazokufaa ni kama hizi zetu tu.”



“Hata hiyo inafaa tu”



“Kama ni hivyo, sawa.... Hifadhi umepata na kazi umepata.”



“Nimepata!!!. Wapi?,” Nikashangaa sikuelewa kinachomaanishwa.



“Kwangu. Nitakupa ajira na malazi,” Mama yule akanidadavulia, hapo ndipo nikaelewa sikusita kufurahi nikaonyesha tabasamu langu hata kama napitia wakati gani.



“Asante sana,” Nikashukuru.



“Usijali tutakuwa wote. Muhimu ni kuchapa kazi tu...unaitwa nani?,” Mama yule akahoji.



“Prisca.”



“Oooh, una jina zuri.... Mimi naitwa Mama Chodo nina mtoto mmoja mwanamke anasoma sekondari. Pia hata wewe nitaishi nawe kama mwanangu,” Mama Chodo nae alijitambulisha kwa ufasaha na uchangamfu.



“Nashukuru sana, mama,” Nikatoa shukrani huku nikimtazama Mama Chodo kwa jicho la kujivunia kuwa nae maana ni mwanamke wa kipekee sana. Ni mwanamke anayeonyesha kuwa na roho nzuri kwa kila mtu, kwa kweli nikampenda.



“Nyanyuka sasa, tufanye kazi,” Mama Chodo akaongea kisha akaninyanyua pale nilipokuwa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mimi na Mama Chodo haraka tukaanza pilika pilika za kuandaa vifungua kinywa vya wateja, siku hiyo wateja wakamiminika katika mgahawa wa Mama Chodo. Yote sababu ya uzuri wangu ulikuwa kivutio mno katika mgahawa wa Mama Chodo, wateja hawakuchoka kujaa nyomi kushinda mwanzo alivyokuwa akiuza Mama Chodo pekee. Sura yangu nzuri, macho ya kusinzia, umbo la umodo kiasi na rangi nyeupe ya wastani. Ndiyo ikaongeza chachu mgahawa wa Mama Chodo kupendwa, Prisca mie sikupendwa na wateja tu nikapendwa mpaka na Mama Chodo mwenyewe. Japo katika kazi sikuwa mzoefu lakini kwa muda mfupi tu nikawa bingwa nikawa mzoefu kushinda Mama Chodo, siku yangu ya kwanza nikachapa kazi balabala mpaka pale muda wakufunga mgahawa ulipofika tukafunga ofisi. Nikaongozana na Mama Chodo kuelekea nyumbani kwake anapoishi. Nyumba yake ilikuwa mbali kidogo na mgahawa ilikuwa ni Kigogo Jaba, ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu na sebule. Nyumba hiyo aliachiwa na marehemu mumewe kabla ya kufariki na ajali ya Meli pindi aendapo Zanzibar kikazi. Kigogo Jaba kwenye nyumba ya Mama Chodo tukafika usiku wa saa tatu tukamkuta Chodo kashalala kafunga hadi mlango, ikabidi Mama Chodo amgongee mwanae atufungulie tuingie ndani, tukaingia ndani mara baada ya Chodo kuamka na kutufungulia mlango tukaketi kwenye viti wote. Chodo akamwangalia mama yake kwa muda kisha akanitupia jicho la chuki mara akauliza swali lenye hila kidogo.



“Nani huyu?,” Chodo alimuuliza mama yake kwa kumtumbulia macho.



“Ni mgeni wetu, tutakuwa nae siku zote” alijibu Mama Chodo huku akijipiga mwili makofi kwa kuwafukuza mbu wamsumbuao mwilini.



“Una, undugu nae?,” Chodo akadadisi.



“Hapana...ni mtu tu asiye na hifadhi nikaona nimsaidie tuje tuishi nae,” Mama Chodo akajibu huku akinitupia mie jicho la aibu.



“Ushakuwa mama huruma.... Shauri yako siku utapoleta majini na majambazi utajuta” alizungumza Chodo huku akionyesha wazi hajapendezwa na maamuzi ya mama yake, hatimaye akaingia chumbani kwake kwa ghadhabu. Mama Chodo akajifiria kidogo akifikiria maneno ya mwanae kisha akapayuka kwa kupaza sauti.



“Sasa, unaingia ndani uli?.”



“Sili, endeleeni,” Chodo nae akapaza sauti akiwa chumbani, akamjibu mama yake. Mama Chodo akanigeukia akanitazama usoni kwa muda mrefu kidogo, naamini alikuwa anafanya utafiti kisiri kama maneno ya mwanae yana ukweli wowote lakini utafiti wake haukugundua chochote. Hivyo akatoa chakula kwenye mfuko mweusi wa malibolo ambacho tulichojiwekea wenyewe kutoka kazini, akanikaribisha ili tule tukawa tunakula. Mama Chodo akala kidogo akaacha akajisikia kuongea, akaongea kwa sauti ya kunong'ona.



“Mwanangu, naomba usijisikie vibaya kwa kauli aliyoiongea mdogo wako.... Naomba mzoee tu maana huyu mdogo wako ni mtu wa kuropoka ropoka.”



“Usijali mama, naamini ajanijua lakini punde atanijua tu. Atatambua uwepo wangu.... Ondoa shaka kabisa,” Nikamtoa hofu Mama Chodo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sawa mwanangu, basi kula ukaoge kisha nikakuonyeshe chumba cha kulala ujipumzishe. Najua umechoka sana sababu ni siku yako ya kwanza.”



“Kweli nimechoka sana mama. inanibidi leo nilale mapema niwahi kuamka kesho” nikaongea na Mama Chodo huku tukiendelea kutupia chakula kinywani.



Tulipomaliza kula Mama Chodo akatoa vyombo akapeleka jikoni kwa ajili ya kesho Chodo avioshe, akarudi sebuleni akaenda kuniandalia maji ya kuoga nikaoga nikarudi sebuleni nikamkuta mwenyeji akiwa ananisubiri ili anielekeze chumba cha kujipumzisha, akanielekeza nikaingia chumbani kupumzika. Mama Chodo nae akaingia chumbani kujipumzisha mara baada ya kunielekeza na kuhakikisha nimelala.



**********

Asubuhi na mapema Mzee Mahonge na Binti Binge wakatembelewa na ugeni. Mgeni mwenyewe si mwengine bali ni mwanaume Sulesh bin Kadhir wa kutoka Dar es salaam maeneo ya Mbezi Beach, ambaye ndiye waliotaka kuniozesha ila kutokana na mavazi kuu kuu aliyokuja nayo awali yakanifanya nimkatae na kumuona hafai.







“Habari, wazee wangu,” Sulesh alisalimu mara baada ya kukaribishwa sebuleni kwenye kigoda na wenyeji.



“Salama kijana.... Kwema?,” Mzee Mahonge aliuliza mara baada ya kumkaribisha mgeni kwa shamra shamra zote.



“Kwema.... Mwenzangu nimemkuta?,” Sulesh akauliza.



“Mh, baba. Mwenzako katoroka kaenda mjini,” Binti Binge alijibu swali la Sulesh huku akimtazama kwa haya.



“Kilichofanya atoroke, ni nini?,” Sulesh akazidi kuhoji.



“Ametoroka sababu hakukupenda.... Kasema licha ya kutokukupenda, kidini hamuendani. Wewe ni muislamu yeye mkristo. Nyie ni waarabu mnawatukuza masultani lakini sisi tunamtukuza Mungu,” Mzee Mahonge akafafanua. Akamuweka wazi Sulesh.



“Sasa yeye kasema hanipendi, lakini mimi nampenda mwanenu,” Sulesh akakiri.



“Najua baba,” Binti Binge alizungumza kisha akanyanyuka kwenye mkeka akaenda jikoni kuandaa kifungua kinywa.



“Kijana, usilaumu sana maana tulimpigia dada yake wa Dar simu. Tukaongea nae akatuambia kuwa Prisca yuko huko, ila kashampa nauli ya kurudi Tanga. Atakupenda tu,” Mzee Mahonge aliendeleza mazungumzo mara baada ya mkewe kuacha njiani.



“Kwa hiyo, kesho kutwa nikija nitamkuta.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Naamini utamkuta. Pia akirudi tutambembeleza akupende.”



“Nitashukuru.... Acha sasa niende tutaonana,” Sulesh akaaga. Ila kabla ya kuondoka Mzee Mahonge haraka akadakia kusema.



“Sasa kijana, unaondoka bila kula chochote kitu. Hebu.... Subiri mama yako huko anaandaa chai.”



“Mzee, ondoa shaka chai nitakuja kunywa siku nyengine. Acha leo niondoke.”



“Hakuna neno.... Najua ipo siku utakula tu, hapa kushakuwa kwako” aliongea Mzee Mahonge kimzaha mzaha.



“Kweli. Utaniagia mama, akitoka ngoja mimi sasa niende,” Sulesh akaaga tena. Akaondoka.



Sulesh akatoka nje akapanda gari lake aina ya ALLION nyekundu akakanyaga mafuta, Mzee Mahonge akamsubiri mkewe atoke jikoni na kifungua kinywa. Punde Binti Binge akatoka jikoni akiwa amebeba chupa ya chai na sahani iliyo na Magimbi, kufika sebuleni akashangaa kuona Sulesh hayupo wakati kabla ajaingia jikoni alimuacha pamoja na mumewe. Akauliza.



“Eti, Baba Dotinatha. Mgeni kaenda wapi?.”



“Kaondoka.”



“Kaondoka!!!, kaondoka bila kula?.”



“Kasema, atakula siku nyengine.”



“Eehe, sawa,” Binti Binge alikubaliana na matokeo, akatenga chai wenyewe wakanywa. Baada ya kumaliza kula wakaongoza porini na mumewe kwa ajili ya kutafuta kuni.



**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alfajiri ya saa kumi na moja nikamsikia Mama Chodo akigonga mlango wangu wa chumbani, nikaamka upesi nikaenda kumfungulia nimsikilize.



“Mwanangu, ume me meamka salama?,” Mama Chodo aliuliza kwa shida sababu ya mswaki uliokuwa kwenye kinywa chake.



“Nimeamka salama,” Nikajibu huku nikijifunga khanga kifuani vyema.



“Vizuri.... Muda tayari jiandae sasa tuondoke.”



“Sawa, naomba dakika nitakuwa tayari nishajiandaa,” Nikasema kisha nikaingia chumbani kujiandaa.



Mama Chodo aliponiamsha na kunihabarisha akaongoza kwenye chumba cha mwanae akagonga kidogo mlango, Chodo akaamka akaja kufungua mlango baada ya kusikia mlango ukigongwa. Akamkuta mama yake mlangoni akamsalimu kisha akatega sikio.



“Chodo, jiandae kwenda shule. Muda ushawasili” aliongea Mama Chodo kisha akarudi chumbani nae tayari kwa kujiandaa.



Chodo akatekeleza alichoambiwa akaenda kujiandaa. Ndani ya nusu saa sote tukawa tumeshajiandaa tukafunga milango tukaongozana mpaka Kigogo Jaba karibu na kanisa la Katoliki, pale tukaachana na Chodo. Chodo alikamata njia ya shuleni ya Kigogo Mapera, nasi. Mimi na Mama Chodo tukashika njia ya Luhanga kwenda kufungua mgahawa, yapata saa kumi na mbili kasoro tukafika mgahawani tukajibadili mavazi kisha tukaanza kazi. Tukagawana majukumu kila mmoja akafanya kazi kulingana na kazi tulizojiwekea, tukauza chakula na chakula kikaisha mapema. Jioni tu chakula kikaisha tukaosha vyombo kisha tukafunga mgahawa tukaongozana kurudi nyumbani, tukiwa njiani hatujafika nyumbani simu yangu ikaita nikaitoa kwenye sidiria hatimaye nikapokea baada ya kujua kuwa ni dada ndiye aliyepiga.



“Hallow,” Sauti ya Dada Dotinatha nikaisikia ikizungumza kwa usikivu.



“Hallow,” Nikachangamkia maongezi.



“Mdogo wangu, ndiyo umefanya nini?,” Dada Dotinatha akalaumu.



“Kuhusu nini?.”



“Si nimekupa nauli urudi nyumbani, sasa umerudi?.... Mbona Prisca unajitafutia laana za wazazi” alinung'unika Dada Dotinatha huku akinipa baadhi ya vitisho niogope.



“Dada, nisamehe sana. Kuhusu laana bora nipate kuliko kuolewa na mtu nisiyempenda wala kumtambua.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Shauri yako. Chezea bahati utakuja jutia.”



“Nijutie hiyo vepe. Kama bahati akose Sungura mtaka ndizi mbivu, sembuse mie mnuka kuvu.... Acha tu kwani kuolewa bongo.”



“Kauli yako ni ile ya kutokujua umuhimu wa ndoa.... Sasa basi kuanzia leo narudia tena, kuanzia leo hutoniona ninyanyue simu nikupigie. Mpaka nisikie umeridhia kuolewa,” Dada aliongea kwa ghadhabu kisha akakata simu. Wazi ikaonyesha amekasirika.



**********



ITAENDELEA
Pseudepigraphasnoreply@blogger.com
tag:blogger.com,1999:blog-7805201032262348818.post-28024131839285807882020-04-23T20:53:00.003+03:002020-04-23T20:56:37.124+03:00

0 comments:

Post a Comment

Blog