Search This Blog

JINI MAUTI -1

 








IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI



*********************************************************************************



Simulizi : Jini Mauti
Sehemu Ya Kwanza (1)




Watu walikusanyika kwa wingi katika maduka ya vitabu na vibanda vya magazeti kwa ajili ya kununua kitabu kimoja cha kusisimua, kitabu chenye historia ya kweli aliyoisimulia msichana mwenye miaka ishirini tu, Davina Patrick Mosenya ambaye katika kipindi hicho alikuwa hoi hospitalini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mara ya kwanza waliposikia simulizi ya maisha yake katika Kituo cha Redio cha Global kwenye Kipindi cha True Story, wengi waliumia, wengi walisikitika mno, wengine walilia huku wengi wakionekana kutokuamini kama msichana mdogo kama Davina angeweza kupitia maisha hayo.

Kitabu hicho kiliitwa Jini Mauti, kilikuwa na simulizi ya kweli yenye kutisha na kusisimua mno, watu walikinunua mno mitaani, walitaka kusoma kile alichokuwa amekisimulia msichana huyo redioni.

Watu waliokuwa katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam, wakawaagiza ndugu na marafiki zao wawanunulie kitabu hicho kilichoanza kushika hisia za watu kutokana na simulizi yake aliyoisimulia redioni kumsikitisha na kumtisha kila mtu.

Mitaani kukawa gumzo, siku hiyo ambayo kitabu hicho kilitolewa, idadi kubwa ya watu walikusanyika katika hayo maeneo maalumu ya kuuzia vitabu, kila mmoja alihitaji kopi yake huku wengine wakiwa tayari hata kutoa mara mbili ya gharama iliyokuwa ikiuzwa.

Vitabu vipi kaka?? alisikika jamaa mmoja, alikuwa mbele ya meza ya muuza magazeti.

Vitabu vipi??

Jini Mauti!?

Duuh! Unakuja kuviulizia sasa hivi! Mbona vishakwisha kitambo,? alisema muuza magazeti.

Yaani saa nne asubuhi nimechelewa??

Ndiyo! Watu wamewahi asubuhi na mapema kana kwamba wamekuja kupiga kura, vyote nimemaliza, hebu nenda Kariakoo au Ubungo unaweza kuvikuta vingine,? alisema muuza magazeti.

Kila kona, hakukuwa na Kitabu cha Jini Mauti kilichokuwa mezani, vyote vilikwisha huku watu wakivihitaji sana. Kila aliyekuwa na kopi ya kitabu hicho, alijifungia chumbani na kuanza kukisoma, hata kumuazima mtu mwingine hakutaka.

Msichana Davina alikuwa hoi kitandani, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa usioonekana katika mashine za hospitali. Kitandani pale, mwili wake ulivimba mno, macho yalikuwa makubwa na hata kupumua kwake alipumua kwa shida mno, huku wakati mwingine mwili wake ukionekana kuwa na magamba kama mti, magamba yaliyokuja na kupotea mara kwa mara.

Madaktari waliingia kwa zamu, kila aliyeingia mle chumbani, alimuonea huruma, alionekana kuwa msichana mdogo, mrembo ambaye hakustahili kupitia maisha aliyokuwa akipitia.

Vipi? Anaumwa nini?? aliuliza Dk. Migiro, alikuwa akimwangalia Davina machoni.

Hatujui, tumempima lakini hatukukuta ugonjwa wowote ule,? alijibu daktari mmoja.

Kweli??

Ndiyo!?

Hawakutaka kujiuliza sana, walijua kwamba ugonjwa aliokuwa akiumwa Davina haukuwa ugonjwa wa kawaida, alirogwa, ulikuwa ni uchawi ambao kwa namna moja au nyingine ndiyo uliomfanya kuwa kitandani hapo.

Wakati akiteseka kitandani, wakati akilia, kitabu chake kilikuwa kikifanya vizuri sokoni, historia ya maisha yake aliyokuwa ameiandika katika kitabu kile ilimsikitisha kila mtu aliyeisoma, na hata jina la kitabu kile, kilimsisimua kila mtu, walitaka kujua zaidi kilichotokea kwani kwenye redio alisema kwamba asingeweza kusimulia kila kitu ila kitabuni angeandika yote.

Juu ya kifua chake kitandani pale alikuwa na kitabu chake, kitabu kilichoandikwa kwa mkono wake, kitabu chenye mvuto hata kukiangalia kwa nje. Watu kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakiingia kumuona, na kila aliyeingia, kitu cha kwanza kabisa alitaka kukiona kitabu kile, kitabu kilichoweka rekodi ya kuuzwa zaidi ya nakala laki moja, tena ndani ya masaa matatu tu, yaani saa moja asubuhi mpaka saa tatu.

Davina! aliita mwanaume mmoja mara baada ya kuingia ndani ya chumba kile, alikuwa mwanaume nadhifu, alivalia miwani, alichomekea vizuri.

Abeee, aliitikia Davina kwa shida.

Vitabu vimekwisha mitaani! Tutoe kopi nyingine?? aliuliza mwanaume huyo.

Hakuna tatizo, ila naomba unisomee hiki kitabu, nimekiandika mimi mwenyewe lakini ninapenda kila wakati nikisome au mtu anisomee, nimepitia mambo mengi Geofrey, wengi wamekufa kwa ajili yangu, Mungu, ninaomba unisamehe, nisamehe kwa yote niliyoyafanya,? alisema Davina huku akianza kukuhoa madonge ya damu, kwa shida, akachukua shuka na kujifuta.

Kwa hiyo nianze kukusomea??

Ndiyo! Ila wakati unakisoma, jua kwamba kuna mambo mengi nilisimuliwa na mama yangu na mengine kuyaona mwenyewe.?



Alipenda kwenda kanisani, alipenda kila anapokuwa, hasa mbele za macho ya watu anaimba nyimbo za dini, aliwahubiria watu wengi lakini yote hayo aliyokuwa akiyafanya yalikuwa ni kuficha ule uovu aliokuwa nao, kuficha mambo ya kishirikina aliyokuwa akiyafanya kila siku.

ENDELEAMara baada ya kijana mchangamfu, mkimya na mtanashati, Patrick Mosenya kumpenda mama yangu, hakutaka kutulia, alimfuata na kumwambia ukweli kwamba alimpenda na alikuwa tayari kwa kila kitu, hata kama babu angemfuata na kumpiga, ila kwa ajili yake tu, alikuwa tayari kwa kila kitu.

Wakakubaliana na kuwa wapenzi wa siri, walipendana mno. Kama unavyojua kwamba mapenzi hayana siri, watu mtaani wakajua kilichokuwa kikiendelea, babu na bibi walipoletewa taarifa, walikasirika, wakamuita mama na kumuonya juu ya uhusiano huo lakini kwa kipindi hicho walichelewa kwani tayari mama alikuwa mjauzito.

Ukiendelea naye, nitakuua wewe mtoto," alisema babu, alionekana kuwa na hasira mno, mama alinyamza, alibaki kimya huku akilia tu.

Nisamehe mama, sitarudia tena," alisema mama huku akilia kama mtoto.

Hili toto sijui limechukua akili za nani, yaani kuna siku nitalifunua hili," alisema babu, macho yalimtoka huku kila alipokuwa akizungumza chembechembe za mate zilikuwa zikimtoka.

Mama alimpenda mno Patrick, japokuwa babu na bibi walimuonya lakini hakuweza kusikia, kwa kuwa tayari waliambiwa kuhusu uhusiano wake na kijana huyo, wakaamua kufanya siri. Hakujua bibi alijuaje, kila alipokuwa akikutana na Patrick na kurudi nyumbani, bibi alimfuata na kumwambia ukweli kwamba alijua kila kitu kilichotokea, mama alishangaa mno kwani mpaka kipindi hicho hakujua kama bibi alikuwa mchawi, yaani kila alipokuwa akikutana na Patrick, alijigeuza katika umbo la paka na kusimama pembeni kisha kuwasikiliza.

Fanya ujinga wako wote ila siku ukipata mimba, utanikoma," alisema bibi, kwa kumwangalia, ungegundua kwamba alikuwa akimaanisha.

Baada ya mwezi mmoja kupita, mama akaanza kujisikia tofauti, akaanza kuhisi kizunguzungu huku wakati mwingine akisikia kichefuchefu na hivyo kutapika. Alionekana kuwa na wasiwasi, alichokifanya ni kwenda kupima hospitali na kugundua kwamba alikuwa mjamzito.

Aliogopa, aliwafahamu babu na bibi walivyokuwa wakali, kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kwenda nyumbani kwa kina Patrick na kumwambia ukweli, kijana huyo hakubisha, alikubali kwamba ilikuwa mimba yake, alichokisema mama ni kwamba ilikuwa lazima kuitoa mimba hiyo, Patrick akakataa.

Naomba usiitoe!

Siwezi kukaa na mimba, nyumbani wataniua, alisema mama huku akilia, mashavu yake yalilowanishwa na machozi.

Haiwezekani! Haiwezekani Stella! Ukitoa mimba, tutaonana wabaya, alisema Patrick huku akimwangalia mama usoni.

Nyumbani wataniua.

Hawawezi kukuua, niamini mimi, wakikufukuza, njoo kwetu, alisema baba huku akijiamini kana kwamba pale kwao kulikuwa salama.

Siku hiyo mama aliporudi nyumbani, bibi alionekana kuwa na hasira mno, ni kweli wakati mwingine mama alizoea kumuona bibi akiwa na hasira ila kwa siku hiyo alionekana kuwa na hasira mno, hakujua tatizo lilikuwa nini, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kimetokea, akamsogelea na kumuuliza tatizo lilikuwa nini,

akaanza kumkaripia.

Una mimba? Una mimba aliuliza bibi kwa sauti ya juu.

Hapana mama

Nasema una mimba! Sasa subiri, alisema bibi na kuondoka.

Mama alishtuka mno, hakukuwa na mtu mwingine aliyejua zaidi yake, Patrick na daktari aliyekuwa amempima, sasa bibi alijuaje kama alikuwa mjauzito? Aliogopa, hakutaka kukaa nyumbani hapo, alimfahamu bibi, hakuwa mtu wa masihara japokuwa alionekana kuwa mtu mcheshi muda wote, alichokifanya siku hiyo ni kuondoka na kuelekea nyumbani kwa akina Patrick.

Kwa hiyo tufanye nini?

Hata mimi sijui. Naogopa kurudi nyumbani

Usiogope, wewe rudi tu, alisema Patrick.

Siwezi.

Ni kweli alimaanisha alichokisema, hakutaka kurudi nyumbani, aliogopa, kila alipomkumbuka babu na ukali wake, hakutamani kurudi nyumbani hata mara moja. Akaondoka, alipoondoka, baba hakupafahamu, hakutaka kurudi tena, akapotea, japokuwa nyumbani waliamua kumtafuta, vijana wakatumwa na

kuahidiwa kiasi kikubwa cha fedha kama wangefanikiwa kumpata, mwisho wa siku wakarudi mikono mitupu, mama hakuonekana, hakurudi, alipotea, alitokomea huku akitaka kila mtu asahau kuhusu yeye.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mama alikuwa akikimbia kuelekea Lushoto Mjini, alionekana kuchoka lakini hakutaka kusimama, alikuwa akitafuta sehemu ambayo angeweza kukaa na kupata msaada wa aina yoyote ile.

Baada ya saa mbili, akafika mjini ambapo huko akaelekea katika kituo cha mabasi na kutulia hapo. Machozi yalikuwa yakimtoka, kile kilichokuwa kimetokea nyumbani kilimuumiza mno. Kufukuzwa na wazazi wake kilikuwa kitu kilichomuumiza mno.

Hakuwa na pa kwenda hapo mjini, alibaki kituoni hapo huku akiangalia magari yaliyokuwa yakiingia na kutoka. Hakuwa mzungumzaji sana, alionekana mpole mno lakini sura yake nzuri ilimchanganya kila mwanaume aliyemwangalia.

Wanaume wengi waliogopa kumfutana kwa sababu hawakutegemea kuona msichana mzuri kama mama kukosa

mwanaume maeneo hayo, wengi walihisi labda mwanaume wake alikuwa ametoka na kwenda sehemu.

Mama alikaa mahali hapo mpaka usiku, hakuondoka, aliendelea kukaa pale huku wengine wakifikiri labda alikuwa akisubiri magari ya kwenda nje ya nchi kama Kenya na sehemu nyingine.

Mpaka inaingia saa tano usiku alikuwa hapo kituoni. Aliniambia kwamba usiku huo ulikuwa ni usiku wa shida, baridi

lilimpiga sana, njaa ilimuuma na mbu walimng?ata lakini hakutaka kuondoka mahali hapo, aliendelea kung?ang?ania tu.

Ilipofika saa sita watu wote waliokuwa katika kituo kile walitakiwa kuondoka, hakuniambia kwa nini, nahisi ni utaratibu uliokuwa zamani, alichokifanya ni kutoka, hakujua angekwenda wapi, ilikuwa ni usiku mno lakini alichokifanya ni kusonga mbele, sehemu ambayo ilikuwa na vibanda vingi.

Alipofika katika vibanda vile, akakifuata kimoja kilichokuwa kimeandikwa kuwepo kwa huduma ya simu za mkononi, akachukua maboksi yaliyokuwa pembeni kisha kuyatandika. Alipanga usiku huo alale hapo kibandani, kutokana na baridi lililokuwepo likamfanya kujikunyata kabisa.

Ilipofika majira ya saa nane akaanza kuhisi usingizi mzito. Hali ilikuwa tofauti na kipindi cha nyuma kwani alijitahidi sana kuuvuta usingizi huo lakini haukuja kabisa. Baada ya saa kadhaa alisikia macho yake yakiwa mazito ghafla, akayafumba na usingizi kumpitia.

Ghafla akajikuta akiwa kwenye kundi la watu wengi, walikuwa wamesimama sehemu iliyoonekana kama uwanja mkubwa, idadi ya watu hao ilikuwa kubwa mno na isingekuwa kazi rahisi kuwahesabu mara moja.

Watu hao hawakuwa na nguo miilini mwao, walikuwa watupu kama walivyozaliwa. Mahali hapo hawakuwa kimya, walikuwa wakicheza ngoma za asili zilizopigwa pasipo mpangilio maalum.

Mbele ya watu wale kulikuwa na chungu kikubwa, chungu kilichokuwa na damu kwa juu, kilikuwa kimezungushiwa kitambaa chekundu huku pembeni yake kukiwa kumesimikwa mti mmoja mkubwa uliokuwa na fuvu la binadamu.

Ukiachana na vitu vyote hivyo, kulikuwa na meza kubwa, iliyoonekana kuwa chafu ambayo juu yake kulikuwa na vikombe na sahani chakavu ambazo ndani yake kulikuwa na nyama za binadamu. Kulikuwa na harufu mbaya mno mahali pale.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya Alhamisi, siku pekee ambayo wachawi wanaitumia kusherehekea, hakuna mchawi anayefanya kazi ya kuwanga siku hiyo, huwa wameitenga maalum kwa ajili ya kula nyama na damu za watu na kucheza ngoma, na hata wale watu waliotaka kujiunga na uchawi, walipelekwa katika uwanja wa kukutania kwa ajili ya kujiunga.

Ukiachana na wachawi hao, pia kulikuwa na kundi la watoto kuanzia miaka mitano kwenda juu, hawakuwa uchi kama wengine bali walikuwa na nguo zao, na waliletwa mahali hapo kwa ajili ya kutambulishwa na kuwa wachawi wapya.

Mama alitetemeka, moyo wake ulijawa na hofu kubwa, hakuwa akijua ni kwa nini alikuwa hapo, hakujua kama alikuwa akiota au kilikuwa ni kitu kilichokuwa kikiendelea mahali pale, alijaribu kuangalia huku na kule japo amuulize mtu lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa na habari naye.

Wakati akiwa amesimama tu, ghafla ngoma zikaachwa kupigwa, watu waliokuwa wakicheza wakaacha. Kwa mbali mbele yake akaonekana mwanamke mnene, alikuwa akitembea huku mkononi akiwa ameshika usinga.

mmoja mkubwa, alikuwa uchi kama wengine na kichwani alijifunga kitambaa kikubwa.

Japokuwa alikuwa mbali lakini alipomwangalia vizuri alimgundua mwanamke yule, alikuwa bibi yangu, yaani mama yake,

bi Mwamtumu. Kwanza mama hakuamini macho yake, alimwangalia vizuri mwanamke yule, alitaka kupata uhakika juu ya kile alichokuwa amekiona, hakuwa amemfananisha, alikuwa mama yake kweli.

?Mama!? alijikuta alisema huku akionekana kutokuamini.

Alimfahamu mama yake, alikuwa mtu wa dini, aliyeheshimika sana, kila wakati alikuwa mtu wa kutembea na Biblia huku akiimba nyimbo za dini, sasa ilikuwaje awe mahali pale, tena usiku kama ule? Kila alichojiuliza akakosa jibu.

Yaani mama yangu mchawi? Haiwezekani,? alisema mama huku akitetemeka mno kwani sehemu ile haikuwa na amani hata mara moja.





Bibi akanyoosha mikono juu, wachawi wote wakainamisha vichwa vyao, walionekana kufurahia sana uwepo wao mahali pale, walimheshimu bibi na hapo ndipo mama alipogundua kwamba bibi alikuwa mkubwa wa wachawi.

Leo ni siku ya kipekee, ni siku ambayo nitamkabidhi mtoto wangu huu mkoba wa kichawi ambao nilikabidhiwa na mama yangu, alisema bibi, aliongea kwa sauti ndogo lakini cha kushangaza ilisikika mahali pale pote.

Akamwangalia mama, alibaki akitetemeka mno, aliogopa, alitamani kukimbia lakini akashindwa kufanya hivyo, mahali pale alipokuwepo hakukuonekana kama kulikuwa na njia yoyote ya

kumfanya kukimbia.

Njoo binti yangu! Leo ni siku ya maana sana kwangu na kwako pia,? alisema bibi.

Mama hakutaka kusogea kule alipoitwa, aligoma lakini kitu kilichoshangaza alijikuta akianza kwenda. Alikuwa kama mtu aliyevutwa kwenda kule alipokuwa bibi ambapo alitaka kumkabidhi mkoba wa kichawi.

Siwezi, sitaki kuwa mchawi,? alisema mama kwa sauti, sauti iliyosikika sehemu yote mahali hapo, wachawi wote wakashtuka.

Unasemaje??

Sitaki kuwa mchawi, siwezi kuwa mchawi, mimi siyo mchawiii,? alipiga kelele mama.

Uchawi ule wa kule Lushoto haukuweza kukabidhiwa hata kama haukuutaka, ilikuwa ni lazima wewe mwenyewe uukubali, uuchukue kwa mikono yako. Wachawi walishtuka, bibi akakunja sura, alionekana kuwa mwingi wa hasira, kile kilichokuwa kikitokea, hakukitegemea kabisa,

hakutarajia kama mama angekataa kuchukua mkoba ule.

Stella! Ni lazima uchukue mkoba huu! Wewe ndiye malkia mpya wa kuliongoza kundi hili, alisema bibi yangu huku akimwangalia mama kwa hasira.

Sitakiii?? alisema mama kwa sauti kubwa.

Pumbavuuu?. alisema mama kwa hasira, hapohapo akaanza kutokwa na damu sehemu za siri kitu kilichomshangaza sana.

Mama akashtuka kutoka usingizini, ilikuwa usiku mwingi, akaanza kutetemeka kwa woga uliochanganyikana na hofu aliyokuwa nayo. Kile kilichokuwa kimetokea, alijua kwamba ilikuwa ndoto mbaya na bibi hakuwa mchawi kama alivyokuwa ameona.

Kitu kilichomshtua ni kwamba alihisi kuwa na unyevuunyevu chini ya kitovu chake, hapohapo akaamua kuangalia kuona alikuwa na tatizo gani kwani mara ya kwanza alihisi alijikojolea, alivyojiangalia, hakuamini, aliona amelowa damu.

Damu!? alisema kwa mshtuko.

Hali hiyo ilimshangaza sana, kile kilichokuwa kimetokea kilimfanya kuwa na hofu kubwa, alichokuwa akikikumbuka ni kwamba alikuwa akiota ndoto mbaya, ndoto kuhusu wachawi huku mama yake ambaye kila siku alimuona kuwa mtu wa dini akiwa kiongozi wa wachawi.

Kila kitu kilichotokea aliamini kwamba ilikuwa ndoto, sasa kwa nini damu ilimtoka kwenye ndoto ile ilimtoka katika maisha halisi? Kila alipojiuliza, alikosa jibu.

Alichokifanya ni kusimama na kuchukua kipande cha boksi kilichokuwa pembeni na kuanza

kujifuta, ni kweli hakutakiwa kufanya hivyo kwa kuwa kile kipande cha boksi kilikuwa kichafu lakini kutokana na maisha ya shida aliyokuwa nayo, hakuwa na jinsi.

Damu haikukata, iliendelea kutoka, hakuwa akisikia maumivu lakini damu ilitoka mfululizo hali iliyoonekana kumuongezea hofu kubwa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Damu hazikukata, ziliendelea kutoka, hakuwa akisikia maumivu yoyote yale lakini damu zilitoka mfululizo hali iliyoonekana kumuongezea hofu kubwa. Hakutulia, akatoka na kuelekea katika sehemu moja iliyokuwa na baa fulani ambayo mpaka muda huo haikuwa imefungwa, akaingia na moja kwa moja kuelekea msalani.

ENDELEA NAYO?

Unakwenda wapi huko?aliuliza msichana mmoja, alikuwa mhudumu katika baa hiyo.

Msalani? mama alijibu huku akionekana kuwa na wasiwasi.

Wewe ni mteja??

Hapana.?

Ila??

Nimepata tatizo! Nipo kwenye kipindi changu,? alijibu mama.

Mhudumu yule alimuelewa kwani hata na yeye alikuwa mwanamke, alichokifanya ni kumruhusu, alipofika mle ndani, akachukua maji na kujaribu kujiosha lakini kitu kilichoshangaza, damu hazikuweza kukatika, ziliendelea kutoka mfululizo kitu kilichomuongezea hofu kubwa.

Nitafanya nini?? alijiuliza.

Baada ya dakika kadhaa, damu zile zikakata lakini tumbo likaanza kuwa kwenye maumivu makali, mama alilia huku akilishika tumbo lake lakini hali iliendelea kuwa vilevile. Hakutaka kukaa mle msalani, alichokifanya ni kutoka huku akiugulia maumivu.

Mhudumu yule alipomuona akamsogelea na kumuuliza tatizo lilikuwa nini, mama akamwambia kwamba alisikia maumivu makali ya tumbo hivyo akamchukua na kuanza kumpeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.

Walipoanza kuondoka kuelekea huko hospitali, njiani mama alianza kuona mauzauza, kuna wakati alisikia sauti za paka wengi wakilia, tena kwa kuliita jina lake, wakati mwingine alikuwa akiwaona

wakipita karibu nao na kila alipomwambia mhudumu yule kuhusu wale paka alibaki akishangaa kwani hakuwa akiwaona.

Mama aliogopa, mauzauza yale yalimfanya kugundua kwamba ulikuwa ni uchawi uliokuwa ukifanywa na bibi. Hakutaka kuzungumza kitu chochote zaidi ya kuendelea na safari. Walipofika hospitalini, kitu cha ajabu kabisa ambacho hawakujua nini kilikuwa kikiendelea, hakukuwa na mtu yeyote hospitalini hapo.

Ilikuwa ni hali ya kushangaza mno, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Hiyo ilikuwa ni hospitali ya halmashauri iliyokuwa ikifanya kazi saa ishirini na nne, sasa kwa nini isiwe na mtu ndani? Madaktari walikwenda wapi? Yaani hata wagonjwa wasiwepo? Kila walipojiuliza, walishindwa kuelewa.

Mbona hakuna watu?? aliuliza yule mhudumu.

Hata mimi nashangaa kwa nini.?

Walijaribu kuingia ndani ya hospitali ile, hakukuwa na mtu yeyote, waliingia ndani ya kila chumba, hakukuwa na mtu yeyote yule. Walibaki wakishangaa, hawakuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mahali hapo.

Wakayafuata mabenchi yaliyokuwa kwenye moja ya korido zilizokuwa mle ndani wakaketi. Bado mama aliendelea kugumia kwa maumivu makali ya tumbo, alishindwa kusimama.

Akaanza kumwaga machozi pale kwenye benchi, mhudumu yule ndiye aliyekuwa akimpoza kwa kumtaka kunyamaza.

Wewe Stellah!? ilisikika sauti masikioni mwake, hapohapo akauinua uso wake na kuangalia mbele, bibi alisimama mbele yake huku mkononi akiwa na ule mkoba wa kichawi, mama akashtuka.

Mama!?

Chukua huu mkoba.?

Mama sitaki, sitaki kuwa mchawiiii?

Nimesema chukuaaa?

Sitakiii?

Mama alipiga kelele, hapohapo bibi akapotea na mkoba wake, kitendo cha kupotea tu, tayari yale maumivu ya tumbo aliyokuwanayo yakapotea ghafla na kuwa mzima kabisa. Mhudumu yule akabaki akimshangaa, kelele alizokuwa akizipiga alizisikia lakini suala la uchawi hakuwa akilijua.

Vipi?

Abeee.?

Umesema hutaki kuwa mchawi?

Ndiyo!?

Ulikuwa unamwambia nani?

Mama hakujibu swali hilo, alichokifanya ni kusimama na kuanza kukimbia kuelekea barabarani. Mhudumu yule alimshangaa, hakumuelewa mama, wakati mwingine alionekana kama chizi. Hakutaka kujali sana, kwa kuwa hakuwa akimfahamu, akaamua kumuacha.

Mama alikimbia mpaka alipofika sehemu iliyokuwa na giza, pembeni kulikuwa na miti mingi, alipofika hapo, akaufuata mti mmoja na kukaa chini yake. Alibaki akilia tu, hakuamini kama kweli mama yake alikuwa mchawi.

Hakulala usiku kucha, alikuwa mtu wa kulia tu. Sauti za paka zilikuwa zikisikika kila kona, aliogopa sana.

na sauti hizo ndizo zilizomfanya kutokulala kabisa. Hakukuwa na siku ambayo aliishi kwa hofu kubwa kama siku hiyo.

Mpaka inafika asubuhi, alikuwa machoz, akainuka na kuanza kuondoka mahali hapo. Lengo lake siku hiyo lilikuwa ni kwenda Dar es Salaam, hakutaka kuendelea kubaki Lushoto kwa kuamini kwamba kadiri ambavyo angeendelea kubaki huko basi bado angeendelea kufuatwafuatwa na bibi.





Siku hiyo mama alikuwa na mawazo mno, hakuamini kama tayari alikuwa amefika jijini Dar, sehemu aliyoipenda mno. Usiku ulipoingia, mama hakutaka kulala, aliogopa sana kwa kuwa alitishwa na uchawi aliokuwa nao bibi. Endelea sasa…Ilipofika saa sita usiku, ghafla akaona moshi mzito ukianza kuingia ndani ya chumba kile kutokea nje kupitia dirishani, hakujua ule moshi ulikuwa wa nini, hakujua ni nani alikuwa akiunguza kitu. Akaanza kukohoa, alichohisi ni kwamba, inawezekana kule nje kulikuwa na mtu aliyekuwa akiunguza kitu, alichokifanya ni kusimama kwa lengo la kutoka nje, alipokishika kitasa na kutaka kuufungua mlango, haukufunguka. Alichanganyikiwa, moshi ule ulizidi kuingia ndani ya chumba kile kiasi kwamba mpaka kitu kilichokuwa jirani hakuweza kukiona kutokana na wingi wa moshi huo. Ghafla, huku hali ikiwa hivyo, akaanza kusikia sauti za paka chumbani humo na sauti za watu waliokuwa wakitoa vicheko vya kejeli. Mama aliogopa mno, sauti za paka wale na vicheko vile viliendelea kusikika kwa juu zaidi. Huku akionekana kuchanganyikiwa kabisa, mara akasikia mtu akikohoa, alipoangalia, bibi alisimama mbele yake, japokuwa kulikuwa na moshi mkubwa lakini alishangaa ni kwa namna gani aliweza kumuona bibi, tena akiwa ameshika uleule mkoba. Chukua mkoba wangu Stellah,alisema bibi huku akimwangalia mama kwa macho yaliyojaa ghadhabu. Sitaki kuchukua, sitaweza kuuchukua, sitaki kuwa mchawiiiii, alipiga kelele mama. Nimesema chukuaaaaa Sichukuiiii, alipiga kelele mama. Bibi akapata ghadhabu zaidi, hapohapo akamshika mama mkono, ghafla akapotea naye. Walipotokea ni sehemu fulani iliyokuwa na mwanga hafifu, mbele yao kulikuwa na shimo kubwa lililokuwa likifoka moto mkubwa huku sauti za watu wakilia zikisikika, walikuwa wakiunguzwa katika moto ule. Akamchukua mama na kumsogeza karibu na shimo lile kubwa na kumwambia aangalie ndani. Kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakihangaika huku na kule, walikuwa wakipiga kelele huku wakiomba kutolewa ndani ya shimo lile lililoonekana kuwa na mateso makali. Mama aliogopa mno, akaanza kumuomba msamaha bibi japokuwa hakujua kama alifanya kosa lolote lile, alidhani kwamba naye angeingizwa ndani ya shimo lile. Bibi akamwangalia kwa dharau kisha kumchukua na kumpeleka sehemu moja iliyokuwa na vyumba vingi, akafungua mlango wa chumba kimoja na kumuingiza ndani. Mule kulikuwa na kiumbe kimoja cha ajabu sana, kilikuwa kikimchapa mtu fulani fimbo za mgongoni. Mgongo wote ulikuwa ukitoka damu, mtu yule alipiga kelele za maumivu lakini kiumbe kile cha ajabu hakikuacha, kiliendelea kumchapa mfululizo. Yule ********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ni kama wewe, alisema bibi na kuendelea: Alikataa kuchukua mikoba ya baba yake, sasa hivi anaiona joto ya jiw alisema bibi. Mama aliogopa zaidi, kila alipokuwa akimwangalia mtu yule kwa jinsi alivyokuwa akiteswa kwa kuchapwa fimbo, moyo wake ulimwambia ni lazima akubaliane na bibi kuchukua mikoba ile, yaani awe mchawi. Kweli awe mchawi? Aroge kama wachawi wengine? Apae na ungo? Akusanyike kwenye umati wa watu akiwa uchi wa mnyama? Aende kwenye makaburi usiku? Kila alipokuwa akijiuliza maswali hayo, jibu lake la mwisho ni kwamba isingewezekana kuwa mchawi. Bibi hakutaka kukaa naye sana, akamrudisha chumbani mule, mama akashtuka, akajiona akiwa kitandani, jasho lilimtoka, kilichomshangaza, moshi ule, sauti zile za paka na vicheko vya watu, vyote havikuwepo. Mzee yule alirudi katika chumba kile, alimkuta mama akiwa kwenye hali ya huzuni mno huku macho yake yakiwa mekundu sana. Alijaribu kumbembeleza na kumtaka anyamaze kwani alikuwa na mipango ya kumsaidia maishani mwake. Mama alikuwa msiri, hakutaka kumwambia mzee yule kilichokuwa kimetokea, alikubali kubembelezeka na mwisho wa siku kuanza kuongea mambo mengine kabisa. Mzee yule aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah alimwambia mama ukweli kwamba alimpenda mno na alitaka kuwa naye kimapenzi. Una mke? Ndiyo! Ila ninakupenda, nipo tayari kwa lolote,alijibu mzee Abdallah huku akionekana kumaanisha. Sawa! Nipangishie chumba na unifungulie biashara alisema mama. Hakuna tatizo. Mapenzi ni mapenzi tu, mzee Abdallah alitekwa sana na mama, akajikuta akifanya kama alivyoambiwa, baada ya siku tatu, mama akahamia katika chumba kimoja kilichokuwa Tandale kwa Mtogole huku akimfungulia biashara ya kuuza madela. Mama alifurahi mno, katika kipindi chote hicho hakuwa amemwambia kama alikuwa mjauzito na hicho ndicho kitu kilichomuumiza sana kichwa chake. Alihisi kwamba kama angemwambia basi huo ndiyo ungekuwa mwisho wake. Kitu kilichokuja akilini mwake ni kuitoa mimba ile. Hakutaka kujifikiria, akajipanga vilivyo, akapanga siku ya kwenda katika maabara ndogo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, siku hiyo ilipofika, akaelekea huko. Mimbahaiwezi kutolewa hii, alisema daktari. Kwa nini? Imekaa ndivyo sivyo, kama nikisema niitoe, utakufa. Unasemaje Huo ndiyo ukweli.





Mama alikuwa msiri, hakutaka kumwambia mzee yule kilichotokea, alikubali kubembelezeka na mwisho wa siku kuanza kuongea mambo mengine kabisa. Mzee yule aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah alimwambia mama ukweli kwamba alimpenda mno na alitaka kuwa naye kimapenzi.



ENDELEA NAYO



Una mke?

Ndiyo! Ila ninakupenda, nipo tayari kwa lolote, alijibu mzee Abdallah huku akionekana kumaanisha.

Sawa! Nipangishie chumba na unifungulie biashara, alisema mama.

Hakuna tatizo.



Mapenzi ni mapenzi tu, mzee Abdallah alitekwa sana na mama, akajikuta akifanya kama alivyoambiwa, baada ya siku tatu, mama akahamia katika chumba kimoja kilichokuwa Tandale kwa Mtogole huku akimfungulia biashara ya kuuza madera.



Mama alifurahi mno, katika kipindi chote hicho hakuwa amemwambia kama alikuwa mjamzito na hicho ndicho kitu kilichomuumiza sana kichwa chake. Alihisi kwamba kama angemwambia basi huo ndiyo ungekuwa mwisho wao.



Kitu kilichokuja akilini mwake ni kuitoa mimba ile. Hakutaka kujifikiria, akajipanga vilivyo, akapanga siku ya kwenda katika maabara ndogo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo, siku hiyo ilipofika, akaelekea huko.



Mimba haiwezi kutolewa hii alisema daktari.

Kwa nini?

Imekaa ndivyo sivyo, kama nikisema niitoe, utakufa.

Unasemaje?

Huo ndiyo ukweli.



Mama hakukaa sana mahali hapo, akaondoka na kuelekea katika maabara nyingine ambayo aliambiwa ilitumika sana kutoa mimba kwa wasichana, alipofika huko akaambiwa maneno yaleyale kwamba mimba isingeweza kutoka kutokana na namna ilivyokuwa tumboni, akakata



tamaa, hakuwa na la kufanya, alichokifanya ni kuamua kumwambia mzee Abdallah.

Hilo si tatizo, hata ungekuwa na watoto kumi, nimekupenda wewe, nalipenda boga, acha nipende na ua lake, alisema mzee Abdallah.



ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog