Search This Blog

MKE WANGU NUSU JINI, NUSU MTU - 4

 






Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu 
Sehemu Ya Nne (4)




?Mimi ni mtu. Kwani we hujui kwamba wanawake wote sisi ni watu nyiye wanaume ndiyo binadamu ingawa pia ni watu??

Kivipi Munil??



?Kwa sababu mnatokana na ubini wa Adamu. Ndiyo likapatikana jina la bin Adamu ambapo watu wamezoea kusema binadamu. Lakini neno lenyewe ni bin Adamu, kama watoto wa kiume wengi unavyoweza kukuta wanaitwa bin Hemed, bin Jumaa lakini sisi wanawake ni binti.?

?Sawa nimekuelewa sana Munil. Lakini Munil huoni kama mimi kuweka fedha zote hizo benki naweza kuulizwa na serikali nimezitoa wapi??

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

?Hakuna atakayekuuliza bwana, acha woga wako mume wangu.?

Siku hiyo tulilala wote na Munil mimi nikiwa kama mume wake kwa mara ya kwanza. Jambo moja ambalo lilinishangaza ni kwamba, wakati tunataka kulala baada ya kuongea kwa muda, nilimwambia Munil tuzime taa, akasema ataenda kuzima yeye.



Baada ya muda nilishtukia taa imezimwa lakini ninaamini hakuwa ametoka kitandani. Hiki kitendo ni cha pili kutokea kwake na kunishangaza.

?Ulikwenda kuzima taa?? nilimuuliza. ?Ndiyo,? alinijibu huku nikijua si kweli.

***



Asubuhi na mapema, Munil ndiye aliyetangulia kutoka kitandani. Mimi nilipoamka nilimkuta ameshaoga na amevaa nguo nyingine, ni gauni refu jeusi. Nilimuuliza umetoa wapi hilo gauni, akanijibu alifuata nguo zake nyumbani kwake, yakaisha.

Ilikuwa wakati napiga mswaki nje kabisa, mama mwenye nyumba ambaye anaishi kwenye upande mwingine alinifuata hadi karibu akaniuliza:

?Huyo binti ni nani??

?Mke wangu.?

?Umeoa lini??

?Siku nyingi kidogo ila alikuwa kwao.?

?Kwao wapi??

?Bagamoyo.?

?Uliwahi kufika??

?Ndiyo, sasa ningeoaje kama ningekuwa sijafika kwa wazazi wake??

?Sawa ila mimi nina??



Kabla hajamaliza kusema, Munil alitokea na yule mama mwenye nyumba akawa kama anaweweseka, kama anahisi kizunguzungu. Mara aniangalie kwa macho ya kulegea, mara amwangalie Munil na kumpa mkono kama anayemsalimia.

?Mama vipi kwani?? aliuliza Munil.



Lakini bado mama mwenye nyumba wangu akawa hasemi wala hafungui mdomo.

?Labda ana tatizo la ghafla, tumshike kichwani,? alisema Munil huku akifanya hivyo. Mara, mama akashtuka na kurudia katika hali yake ya kawaida, akaniangalia mimi, akamwangalia Munil kisha akasema anaomba msamaha kwa wote, akaondoka kurudi ndani kwake.



Munil aliniambia nipige mswaki haraka sana nirudi chumbani. Nikafanya hivyo.

?Hii nyumba tunatakiwa kuhama haraka sana mume wangu,? aliniambia.

?Kisa??

?Si nzuri. Unajua huyu mama amekuwa akikuchezea siku nyingi sana. Kila unapolala anakuja kukukalia juu ya mwili wako. We hujagundua kuwa ukiamka asubuhi unakuwa umechoka sana??

?Hilo ni kweli, ina maana yeye ndiyo kisa??

?Haswa, ndiyo sababu. Mimi usiku wa kuamkia leo nimemtimulia mlangoni, alitaka kuingia. tena nimemwambia akirudia kitampata kitu kibaya zaidi.?

?Munil, kwani wewe ni mganga??

?Aka! Mi si mganga ila huwa nasali sana kwa Mungu wangu.?

?Unan?tisha Munil.?

?Usitishike bwana.?



Tulikunywa chai, tulipomaliza nilimwambia Munil nikatafute nyumba nzuri, akasema kwa siku hiyo nitapata nyumba nzuri sana lakini haipangishwi, nikamuuliza amejuaje, akasema anaamini hivyo.

Nilimbishia, nikaondoka. Lakini akasema nichukue kiasi cha dola nikabadili ili niweze kupata za kuweka



mfukoni. Hata sehemu ya kubadilishia nilikuwa sizijui kwa hiyo nilichofanya niliwauliza watu.

Kwa kiasi cha dola alizonipa Munil kwenye kubadili nilipata shilingi laki mbili. Eti ndiyo za kushika.



Niliwapata madalali, wakanipeleka kwenye nyumba nzuri sana. Waliniambia nisubiri wakaenda kuniitia mwenye nyumba ambaye alifika baada ya kama dakika ishirini na tano hivi. Alinichangamkia, akaniingiza ndani. Hakukuwa na mtu lakini kulikuwa na kila kitu kwa maisha ya binadamu, akasema watoto wake wapo shuleni, mkewe amekwenda kazini mjini Dar es Salaam.



Aliniingiza kila chumba, nikakubaliana naye kwamba ni nyumba nzuri, nimeipenda nitailipia maana ilikuwa na maegesho ya magari pia.Basi, wakati tunatoka yule mwenye nyumba akaingia chumbani na kubadili shati, akatoka akiniuliza nitalipia lini. Nilimwomba anipe nusu saa tu nifike nyumbani kwa mke wangu kuchukua pesa.



Nilimkuta Munil amelala chumbani akisema anahisi uchovu.

?Vipi kwenye nyumba mume wangu?? aliniuliza.

?Nimepata, tofauti na ulivyosema nitapata lakini haipangishwi.?

?Ni shilingi ngapi??http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



?Kwa mwezi shilingi laki moja, vyumba vya kulala vitatu, sebule kubwa, stoo, choo, bafu. Kilichonifurahisha zaidi ni maegesho ya magari, wenyewe watahama baada ya sisi kulipa.?



Nikakumbuka kuwa, kumbe hata fedha niliyokuwa nayo ilitosha kulipia na kubaki salio zuri tu, nikamwambia nakwenda kulipia sasa, Munil akasema sawa lakini akaachia tabasamu.



Kufika, nilikuta mzee mmoja tofauti na yule anaingia ndani ya nyumba hiyo akiwa na mkewe. Alinikaribisha, akaniuliza shida yangu.







"Mzee mimi nimetokea kule juu, nilikuja awali hapa nikakutana na mwenye nyumba lengo ni kutaka kupanga nyumba hii, nilishafanya makubaliano naye, ila nilifuata pesa nyumbani."

Nilishangaa mimi kusema hivyo halafu yule mzee akamtazama mke wake kisha akanigeukia mimi.

"Huyo mtu alikuingiza ndani?"

"Ndiyo, alinitembeza kila chumba akasema atahama baada ya mimi kumlipa."

Wakati nayasema haya, kichwani nikaisikia sauti ya Munil ikisema…

"Utapata nyumba nzuri sana lakini haipangishwi."

"Mimi ndiyo mwenye nyumba hii na sipangishi, huyo mtu uliyesema aliingiaje na unaona mimi ndiyo nafungua hapa!"

"Mimi sijui mzee, ila niliingia humu ndani kwako."



Yule mzee alionekana kusinyaa kwa muda akiwa kama anayejiuliza ni nini kilitokea?

"Basi kijana umeliwa," alimalizia kwa kusema hivyo huku akiingia ndani na mke wake.



Moyoni nilisema hata kama ni kweli nimeliwa, lakini mbona mzee mwenyewe hakuonesha kushtuka kwa kitendo cha mimi kuingizwa ndani mwake na mmiliki hewa yeye akiwa amefunga nyumba?

Niliona kuna mchezo. Niliondoka na miguu ya kunyong'onyea kurudi kwangu. Kwa mbali nilimuona Munil akikatiza mtaa. Nikajua alikuwa akitoka nyumbani kwenda mahali lakini yeye hakuniona.



Kufika nyumbani nilimkuta Munil amelala chumbani.

"Ha! Mke wangu, mbona kama nimekuona mahali unakatiza mtaa?"

"Mimi?" aliuliza kwa kushtuka Munil."Wewe ndiyo, tena gauni hilohilo, nywele hivyohivyo ulivyo. Ni nini?"

"Utakuwa umeniona vibaya."



Nilimueleza Munil kilichotokea kwenye nyumba akasema si nilikwambia mimi!

Nilimuaga Munil kwamba nakwenda kwa rafiki yangu mmoja maeneo ya stendi, akanikubalia.

Nilitoka nyumbani lakini badala ya kwenda kwa huyo rafiki yangu, mimi nilikwenda kwingine kabisa baada ya kughairi njiani.



Nilikwenda kukutana na msichana mmoja ambaye ilikuwa nifunge naye ndoa.

Niliingia kwake ambapo nilimkuta anakunywa chai. Alinipokea kwa furaha sana na kunikaribisha chai.

"Nimeshakunywa, nimeshiba sana."

"Basi kaa," aliniambia.

Ile nakaa tu, akaniambia.

"Nasikia umefunga ndoa Bagamoyo?"



"Mh! Nani kakuambia?" nilimuuliza kwa mshtuko mkubwa.

"Jamani, mbona siyo siri. Mimi nimeambiwa jana na Hawa, yule rafiki yangu halafu leo nikamsikia Rufina."

"Siyo kweli bwana," nilimficha.

Baada ya mazungumzo mafupi, mlango ukagongwa na sauti ya kike ikabisha hodi.

"Karibu, nani?" yule mwenyeji wangu alisema.

"Mimi."



"Wewe nani sasa?" aliuliza mwenyeji huku akiuendea mlango. Alifungua huku mimi nikiwa namuangalia yeye nikiamini kwamba kama huyo aliyebisha hodi anamjua lazima uso wake utaonesha tabasamu.

"Khaa! Mbona hakuna mtu," alisema akigeuka kuniangalia.

"Hakuna mtu? Au kaondoka?"



"Aondoke mara hii, kwenda njia gani? Maana hapa kwangu mtu akitokea kule unamuona hadi anapofika," alisema huku akirudi kukaa na kufunga mlango.

"Hodi," ile sauti ilibisha tena. Safari hii ikiwa kwa juu zaidi. Kidogo nilihisi kama sauti ninayoifahamu na kuizoea.



Safari hii yule mwenyeji wangu hakuitika, alisimama taratibu na kuufuata mlango akiwa anakaribia kushika kitasa kwa ndani, hodi nyingine ilibishwa.

"Hodii."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alifungua mlango haraka, lakini pia hakuona mtu.

"Jamani, si bure kuna kitu. Mbona hakuna mtu?"

"Hodiii."



Safari hii sauti hiyo ilitokea mlango wa nyuma. Mwenyeji wangu akaenda, kabla hajafungua hodi ikapigwa usawa wa dirishani nilipokaa mimi, nikainuka haraka sana kuchungulia hakukuwa na mtu!

"Nahisi kuna kitu kinaendelea," nilimuambia mwenyeji wangu.

"Ni kweli," naye alisema huku akitetemeka.

"Au mimi nimekuja na balaa?"

"Sijui, utakuwa unajua mwenyewe."



Tukiwa tunaongea hivyo, mara tukasikia sauti ya ajabu kutokea nje mlango mkubwa ikisema:

"Haya wee! Haya wee! Haya wee! Ihaaa! Haya we! Haya wee! Haya wee! Ihaaaaaaa."

Nilisimama na kuaga kwamba naondoka kwa kupitia mlango wa nyuma. Cha ajabu sasa, niliposema tu mimi naondoka, napitia mlango wa nyuma sauti ya kicheko ilisikika mbele.

Nilitoka haraka sana na kutembea kwa kasi nilikiwa siangalii nyuma zaidi ya kulia na kushoto, nywele zilisisimka sana, damu mwilini ilikuwa ikitembea kwa kasi.

Niliamua kurudi nyumbani lakini sikupanga kumsimulia Munil kilichonipata.



Nilimkuta Munil amelala lakini aliponiona hakuonesha uchangamfu ninaojua na si kawaida yake tangu nianze kumfahamu.

"Baby, mbona kama huna raha?" nilimuuliza.

"Nipo kawaida mbona!"

"Hapana, hauko kawaida. Nakufahamu mke wangu."

"Mume wangu," aliniita.

"Naam."

"Hebu kaa hapa," aliniambia kisha nilipokaa akasema:

"Unadhani katika ndoa yetu kuna siku utanisaliti?







?

Haitatokea Munil, nakupenda sana.?

?Kweli!??Naamini uliwahi kuwa na wanawake kabla yangu! Je, unaweza kuachana nao??

Alivyosema hivyo tu, nikajua Munil alijua nilikwenda kwa mwanamke wangu wa mwanzo ndiyo maana akawa hana raha na kuniambia maneno hayo ya kuniapiza.

?Naweza mke wangu.?

?Basi naomba ufanye hivyo kuanza leo hii.?

?Nimekuelewa mke wangu.?



Hapo ndipo nikamwona Munil akichangamka kwa mbali. Lakini na mimi dhamira yangu ikanisuta sana. Sasa nikayarejesha mawazo kwa yule mwanamke nilikokwenda, kwamba yale maajabu yalikuwa ni nini!

***

Ilikuwa ni usiku wa kama saa tisa hivi, nilishtuka kutoka usingizini, nikahisi kama kitandani niko peke yangu. Nilipeleka mkono upande aliolala Munil kweli nikabaini nilikuwa peke yangu.

Nikiwa nawaza atakuwa amekwenda wapi? Chooni, mara nikasikia mlio nje ya dirisha.

?Haya weee! Haya wee! Haya wee! Ihaaaa! Haya we! Haya weee! Haya wee! Ihaaaaaaa!?

Nilikurupuka kitandani kutaka kukimbia lakini Munil akanishika mkono palepale kitandani na kunirudisha kulala.

?Nini kwani mume wangu??

?Kuna sauti za ajabu dirishani,? nilisema.

?Zikitokea wapi? Mbona mimi sizisikii??

?Kutokea nje mke wangu halafu hizo sauti kama nimewahi kuzisikia mahali.?

?Mahali gani??

?Sikumbuki. Lakini pia Munil hukuwepo kitandani wewe mke wangu!?

?Sasa kama sikuwepo kitandani nilikuwa wapi mume wangu??

?Mbona nilipapasa sana hukuwepo??



?Ulipapasa vibaya,? alisema Munil kwa sauti iliyoashiria kwamba hakuwa amelala kwa muda mrefu. Yaani si kwamba alitoka kuamka kama mimi.

Wakati tunaongea hayo, kulikuwa giza. Nilimjua ni Munil kwa sababu ya sauti tu na si kumwona sura.

?Sasa kama mume wangu wewe ndiyo unakuwa mwoga mimi itakuaje??



?Wewe umesema hujazisikia hizo sauti kwa hiyo huwezi kuogopa kitu,? nilimjibu Munil. Akaniomba tulale na kuachana na mambo hayo.Kweli, ndani ya dakika kama tano labda nilipitiwa na usingizi mzito. Lakini kwenye saa kumi na moja nikashtuka na kukuta taa inawaka, Munil hayupo kitandani.



Nilijua ametoka kwenda uani kwa sababu kulianza kukucha.

Ilipita nusu saa, Munil alikuwa hajarudi. Nikatoka kitandani kumfuata. Nilifika chooni hakuwepo, bafuni hakuwepo, nilipotaka kutoka nje niliachana na wazo hilo kwa sababu niliona mlango wenyewe ulifungwa kwa vitasa vya ndani.



Nilishangaa hali hiyo. Nikajiuliza Munil anaweza kuwa wapi kama huko hakuwepo?

Nilirudi chumbani, ile naingia tu, nilimkuta Munil amelala chali kitandani akiangalia godoro.

?Munil,? niliita kwa mshtuko.

?Vipi, ulikwenda chooni??

?Noo! Munil hunitendei haki. Mimi ni mume wako lakini wewe una vitu vyako unafanya kwa siri.?

?Kama vitu gani na kwa nini umeniambia hivyo??

?Ulikuwa wapi Munil??

?Kha! Kwani wewe umeniacha wapi??

?Hukuwepo kitandani Munil.?

?Nilikuwepo, sasa ningetoka kwenda wapi??



Sikuendelea na Munil, nilipanda kitandani kulala. Lakini sikupitiwa na usingizi tena. Wakati najiulizauliza kuhusu Munil, nikasikia taa ikizima tap! Nilichungulia kwa mbali na kubaini kwamba taa ilizima ndiyo lakini mzimaji ambaye naamini alikuwa Munil hakutoka kitandani kuifuata swichi ukutani.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

?Unajua mume wangu sijui una matatizo gani, sijui nikupeleke kwa mganga wa kienyeji? Umekuwa mtu wa kuweweseka sana kuliko kawaida.?

?Mimi nahisi wewe una mambo ya maajabu sana. Si useme tujue moja.?

?Kama lipi mojawapo??



?Hilo la kutokatoka halafu baadaye unasema eti ulikuwepo kitandani wakati mimi nimejua kitandani hakuna mtu.Eti Munil alikuja juu akidai nimemdhalilisha sana kwa kule kumwambia ana mambo yake ya ajabuajabu, aseme nijue moja.

?Unajua unamkasirisha na kumfedhehesha ambaye wewe humjui.?



?Kama nani zaidi ya baba yako na mama yako??

Munil alicheka kicheko cha kejeli huku akionekana kama nasema nisichokijua.

?Unacheka nini sasa??



?Sijacheka,? alisema akikaa kitandani. Uso wake ulikabiliana na mimi ana kwa ana, kidogo nikashtuka kwani nilimwona amekuwa na sura kama ya paka mweusi tiii!

?Haa! Munil,? nilihamaki.

Halafu yeye kwa upole akasema



?Natamani nihame hapa kwa muda lakini nitashindwa kwa sababu ya wewe mume wangu.?

?Uhame kwa sababu gani mke wangu??

?Naamini uchawi wa huyo mama mwenyewe nyumba unakusumbua hadi sasa.

?Haniwezi yule hata iweje!?Nilihisi Munil anataka kukwepana na ukweli na kuhamisha mada kwa kuitumbukiza yakwake.









?Mimi sisumbuliwi mke wangu ila nasema kwa ukweli kabisa kwamba huwa sikuelewi.?

?Mbona mimi ni salama sana mume wangu kwa nini jamani ushindwe kunielewa mimi??

?Ina maana mimi sina akili sana kichwani mwangu au??

?Unazo, ila nahisi unachanganyikiwa.?



Nakumbuka siku hiyo mvua ilinyesha sana kiasi kwamba mtu akitoka nje kuingia ndani lazima ajifute au asipojifuta aweke alama za miguu yenye matope.

Nilitoka kwenda kuoga ndipo nikakutana na kisa kingine cha ajabu na cha kutisha sana. Kule bafuni nilikuta alama za miguu ya ng?ombe, yaani kwato. Nikakumbuka kwamba siku moja niliwahi kusikia



kuhusu mwanamke kama ni jini anaweza kujibadilisha sehemu zote za mwili kasoro miguu tu kwamba lazima iwe kwato za ng?ombe.

Niliziangalia zile alama nikagundua baada ya kutoka bafuni zilitoka kwenda chumbani. Nilizifuata hadi zikawa zinapotelea jirani na mlango. Wakati nashangaa, Munil alifungua mlango kama vile mtu aliyesikia dalili za mtu kutembea.

Tulikutana uso kwa uso, mwenzangu alionekana amekasirika sana.

?Vipi?? aliniuliza.?Poa,? nilimjibu huku macho yangu yakikimbilia kwenye miguu yake lakini gauni refu alilovaa halikutoa nafasi ya mimi kumwona miguu yake.



Pale ndipo nilipobaini kwamba, tangu nimeanza kumjua Munil sijawahi kumwona miguu yake wala kujua anapenda viatu vya aina gani! Hilo lilkuwa halina ubishi. Hata nguo zilizokuwemo ndani ni nyingi lakini hakuwa na viatu, nikasema moyoni nitamuuliza baadaye sana.



Ghafla nilihisi joto la ajabu, mwili uliishiwa nguvu nikaanguka. Watu warefu, waliovalia nguo nyeupe wakiwa na mapembe mawili kichwani, kasoro mmoja tu alikuwa na pembe moja kwenye paji la uso walisimama pembeni yangu, wakainama na kunishika mkono kama wanataka kuniamsha.



Nilikataa, wakaniamsha kwa nguvu huku wakicheka. Walinibeba juu kwa juu hadi ufukweni na kunitishia kunitosa ndani ya bahari. Nilipopiga kelele walicheka kwa furaha lakini pia hawakuniacha, wakanirusha majini.



Nilisema mama nakufaa huku nikiwa hewani kwenda majini, akatokea Munil na kunidaka. Nikafurahi sana kugundua ni yeye.

?Huwezi kufa mume wangu wakati mimi mkeo nipo,? alisema Munil kwa sauti tamu kama mwanamke.

?Je, ikitokea ukatangulia kufa wewe hawa watu si wataniua mke wangu?? nilimwambia.

?Haitatokea mimi nikafa kabla yako wala mimi kufa. Mimi nipo tu mume wangu.?

?Una maana gani??

?Mimi bado sana si wa kufa leo wale kesho.?

?Nimekuelwa sana lakini una maana gani kusema hivyo??

?Mimi ni jini!?



Nilishtuka, nikajikuta nimelala kitandani huku Munil akinipungia kunipepea na feni ikipuliza kwa sana ili nipate hewa.?Pole sana,? aliniambia.

?Asante kwani ilikuaje Munil??

?Ulianguka ghafla.?

?Halafu??

?Nikakubeba kukuingiza chumbani.?

?Halafu???Halafu nini sasa si ndiyo umeshtuka sana hivi.?

?Mbona nilibebwa na watu wakaenda kunitupa baharini??

?Halafu??

?Halafu wewe ukanidaka.?

?Halafu??

?Halafu ukasema wewe hutakufa, nitaanza kufa mimi nikakuuliza sababu ukasema sababu wewe ni jini, ni kweli mke wangu??

?Ni kweli kwamba??

?Wewe ni jini??



?Hivi mume wangu ningekuwa jini ungeweza kuishi na mimi? Kuna binadamu amewahi kuishi na jini chumba kimoja, kitandani kimoja? Hebu kaulize wenzako watakwambia kama iliwahi kutokea.?

Nilipowaza sana nikaamini ikwamba wapo watu niliwahi kuwasikia wakisema kwamba binadamu anapokutana na jini anauguza au anapatwa maradhi ya ajabu, sasa iweje mimi niwe nalala naye kabisa halafu niendelee kuwa hai, si ningekufa?



Niliachana na mawazo hayo, Munil alionekana kuufuatilia sana uso wangu ili kujua unaongea nini lakini sijui aliuonaje, akaniuliza:

?Vipi kwa sasa, uko swa??

?Niko sawa mke wangu.?

?Basi na wewe usiwe unaniwazia sana jamani,? alisema Munil huku akunisogelea na kunibusu. Mwili wangu ulisisimka, nikamwambia, akaniuliza nataka nini?

?Ah! Swali gani hilo mke wangu??



Munil alivutia kwake akaniweka kwenye kifua na kuniletea kinywa chake, akatoa ulimi akiashiria kwamba na mimi nimpe wa kwangu Nilitoa ulimi, nikauingiza kwenye kinywa cha Munil, ukatalii humo kwa dakika kadhaa, nikamwona Munil akianza kunung?unika kimahaba.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilisema moyoni kwamba nitumie nafasi ile ya kukutana naye kimwili ili kubaini Munil alikuwa na miguu ya aina gani! Ni kweli ya kwato za ng?ombe au la!Huo ulikuwa usiku sasa na wakati nawaza hayo nikasikia taa! Giza!



?Umezima taa Munil?? nilimuuliza kwa mshtuko mkubwa maana ilipo swichi ya taa na kitandani tulipokuwepo sisi ni mbali, ni lazima mtu atoke kabisa kitandani kuifuata swichi.

?Nimezima mimi ndiyo.?

?Umezimaje??

?Nilikwenda.?

?Siyo kweli, Munil usinifanye mimi ni mtoto mdogo aisee.?







?Khaaa! Sasa nikudanganyie nini jamani??

?Umenidanganya Munil kwa sababu hujatoka kitandani na taa iko mbali lakini unadai umeizima kwa kutoka!?



?Ee, siyo kwamba nilitoka mzima, nilisogea pale mwisho wa kitanda ndipo nikapeleka mkono na kuzima swichi.

Kwa maelezo hayo ya Munil nilizidi kumshangaa na kumwogopa kwani hata ukisimama hapo aliposema bado ilikuwa huwezi kunyoosha mkono na kuifikia swichi.

?Munil,? niliita.

?Abee mume wangu.?



?Bado umenidanganya. We hapo hata ufanyaje huwezi kwenda pale kwenye ukingo wa kitanda ukanyoosha mkono na kuifikia ile swichi, iko mbali sana.?

Nilimwona Munil akiamka kitandani, akasogea hadi kwenye ukingo wa kitanda. Alinyoosha mkono na kuifikia swichi, akawasha ile taa! Tap!



Kusema ule ukweli nilishangaa sana, pia nilishtuka kwani nilichobaini ni kwamba wakati ananyoosha mkono kuanzia kiunoni kwake kwenda shingoni alirefuka sana na ndiyo maana aliweza kufika kwenye swichi.

?Oke, oke!? nilisema nikijifanya nimemwelewa lakini huku na mimi nikishikilia msimamo wangu kwamba alirefuka sehemu ya kati ya mwili wake.

***



Asubuhi ya siku iliyofuata, mimi niliamka nikiwa nimechoka sana, tena nilichoka kupita kiasi kwa hiyo sikuwa najisikia kutoka nyumbani.

Sikumbuki ni muda gani Munil aliamka lakini nilibaini tu kwamba alikuwa nje akiosha vyombo na kushughulikia mambo mengine.



Nilipoamka ilikuwa yapata saa nne asubuhi, nikaenda kwanza chooni kabla ya mambo yote. Niliweza kuona alama za kwato za wazi kabisa kutokea nje ya mlango wa kuingia kwangu kwenda chooni, bafuni na kutoka nje.



?Hivi inawezekana kweli hizi kwato ninazoziona ni za Munil mke wangu?? nilijiuliza mwenyewe lakini sikupata jibu lolote zaidi ya kuendelea kuhisi tu.

Moyoni nilijielekeza jambo moja kwamba, nikishaoga na kunywa chai niondoke kwenda kwa shemeji kumwambia hali halisi ya mke wangu Munil.



?Lazima niende na lazima nikamwambie anipe ushauri, huyu si mwanamke mzuri,? nilisema moyoni.

Basi, sasa wakati wa kunywa chai nilimwambia Munil nilipenda zaidi mayai kuliko mkate na siagi. Akasema anakwenda dukani kununua mayai.



Alipotoka tu, nikakumbuka tukio la jana yake la yeye kwenda kwenye ukingo wa kitanda na kunyoosha mkono mpaka kuifikia swichi ukutani na kuwasha taa.



Nilijaribu kufanya hilo zoezi, nilikwenda kwenye ukingo wa kitanda hicho nikajiegemeza na kunyoosha mkono ili kuifikia swichi lakini sikuweza hata kufikia robo!

?Mh! Si nilisema mimi!? nilijikuta nikitoa sauti hiyo mi mwenyewe.

Nilirejea kukaa kwenye kiti ili Munil asije akanikuta nafanya lile jaribio.

Alipoingia, Munil alionekana kuwa na wasiwasi na mimi na kile chumba. Aliangalia kitanda akaniangalia mimi kisha akaguna na baadaye kucheka sana.

?Unacheka nini sasa?? nilimuuliza kwa woga.



?Hamna kitu.?

?Hamna kitu wakati umecheka sana??

?Jamani, kwani mtu akifurahi hacheki mume wangu??

?Kwa hiyo wewe umefurahi siyo??

?Nimefurahi ndiyo. Kama mume ninaye, maisha ndiyo haya, kuna nini tena??

?Kifo je?? nilimuuliza kwa kumtega.

?Kifo sikijui mimi wala sijawahi kuona mtu amekufa wala kusikia kuna mtu amekufa japokuwa najua kuna kufa kwa watu.?

?Kuna kufa kwa watu? Una maana gani??

?Nasema nasikia watu huwa wanakufa!?

?Ina maana wewe si mtu??

?Jamani hilo si tulishawahi kulimaliza.?



Niliachana na mazungumzo na Munil nikawa nawaza tu jinsi nitakavyomshibisha shemeji na matukio ya Munil ambayo yalishaanza kunichosha sasa.

?Mume wangu,? aliita Munil wakati mimi nikiwa kwenye dimbwi la mawazo kuhusu vitendo vyake.

?Niambie.?

?Hivi unadhani kutoniamini mimi ni dawa ya kumwamini mtu mwingine??

?Una maana gani??



?Mi najua huniamini hata kidogo lakini sasa ungejaribu kuniamini. Unajua mnasema wenyewe kwamba kuku ukimchunguza sana huwezi kumla, si ndiyo??

?Ndiyo.?

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

?Ndivyo kwangu na hata kwako pia, mimi nikitaka kukuchunguza sana siwezi kukufurahia. Pia nikwambie jambo moja mume wangu katika mambo ambayo siyapendi katika ndoa ni matatizo yetu kuwaambia au kuyaombea ushauri kwa watu wengine.?

Aliposema kauli hiyo nilishtuka sana nikamtumbulia macho.



?Una maana gani?? nilimuuliza haraka. Mimi nilichojua ni kwamba alishatambua mpango wangu wa kwenda kumwambia shemeji matukio yake.

?Natoa tu angalizo lakini sina maana yoyote mbaya au nzuri, mimi nipo tu. Ninapokuwa na ushauri kwako nakupa wakati wowote kama mume wangu, sikukatazi lakini kuamua ya kwako kwani wewe ni mume.



?Ukiona kama kwenda kwa shemeji yako na kumwambia mawazo yako kwangu atakusaidia sawa lakini ungejaribu kuwa makini kwanza kabla ya hiyo hatua.



?Pia sidhani kama kuna umuhimu wowote wa wewe kuendelea kuchunguza mambo yangu hadi kufikia hatua ya kujaribu kuwasha taa ya chumbani humu kwa kukaa kwenye ukingo wa kitanda kama nilivyofanya mimi, japokuwa najua lengo lako ni kuona wewe utaweza kama nilivyoweza mimi??







Nilishtuka sana, kwani hayo yote, Munil aliyasema nikiamini hakuna alichokuwa akikijua kwani sikumwambia kwamba nitakwenda kwa shemeji.

?Munil nadhani hayo tuyaache.?

?Hapana mume wangu tunatakiwa kuyaongea ili tuyamalize.?

?Mimi nimeamua tuyaache.?

?Kama umeamua kwa dhati sawa.?



Nilimuaga Munil kwamba nakwenda kuonana na rafiki yangu mmoja halafu nitakwenda gereji ambako ni kazini kwangu akasema sawa ila nisichelewe kurudi.

Nilipotoka nyumbani niliamini namfuata rafiki yangu mmoja anaitwa Chamanilili lakini kabla sijafika kwa Chamanilili niliamua kupitia kwa demu wangu mmoja anaitwa Mayinu ambaye naweza kusema



tangu niwe na Munil ndiyo nilikata naye mawasiliano. Yaani Munil alichangia mimi kumwacha demu huyo.

Nilipofika kwenye nyumba aliyokuwa akiishi nilikuta pameota majani mengi, nikashtuka kwani hata kwa muda nilioachana naye hakukuwa na sababu ya nyumba kubomolewa kiasi cha kuota majani.

Nilijaribu kuangalia nyumba za jirani zote zilikuwa zimefungwa na wenyewe hawapo.



?Mh! Nini kimetokea? Halafu hata kama nyumba ilibomolewa mbona za majirani hakuna hata moja yenye watu au walihamishwa?? nilifikiria mwenyewe kichwani.

Nilitoka kuendelea na safari zangu, mbele nikakutana na Mayinu, uso wake ulipooza licha ya kuniona jambo ambalo sikulitegemea.



?Mayinu mbona umesinyaa hivyo?? nilimuuliza.

?Mbona kawaida tu.?

?Aaah! Si kawaida yako yaani hujaniona siku nyingi halafu leo kuniona unakuwa kama tulionana asubuhi tu!?

?Mimi nipo kawaida,? alisisitiza Mayinu akiwa amenifikia maana baada ya mimi kumuona nilisimama.

?Nyumba ilivunjwa?? nilimuuliza.

?Ipi??

?Uliyokuwa unaishi??

?Jamani, ivunje na nani sasa??

?Mayinu mimi nimetokea pale.?



?Mimi nilitoka nusu saa iliyopita na ndiyo narudi. Sasa ivunjwe na nani na kwa ajili gani? Tena wakati natoka nyumba ya jirani kwa mama Ally walikuwa wanapika chakula kwa ajili ya genge lake.?

?Mimi sijaona nyumba, nimeona majani na jirani sijaona mtu yeyote zaidi ya nyumba kufungwa.?

?Pameota majani?! Au umekosea nyumba wewe??

?Unadhani naweza kukosea nyumba yako??

?Ndiyo nashangaa.?



Palepale nilianza kuhisi kuwa huenda Munil ana mkono katika tukio lile kwani niliwahi kuhisi siku za nyuma nilipokwenda kwa dada wa demu wangu mmoja yalitokea mauzauza.

?Kwa hiyo?? aliniuliza Mayinu lakini bado hakuwa na uso wenye nuru. Alionekana kama anaumwa.

?Basi ngoja turudi,? nilimjibu nikigeuka naye.



Tulitembea huku nikiwa na shauku kubwa ya kujua kama kweli nilipotea nikaenda sehemu nyingine au kuna kitu cha zaidi ya ninavyojua mimi.



Kila hatua tano mbele iliashiria kuwa nilikuwa nimekwenda kwenye nyumba sahihi kabisa na wala sikupotea kama ilivyodaiwa na Mayinu.

?Ulipita hapa?? aliniuliza Mayinu.

?Ndiyo.?

?Hapa je??

?Kote huku jamani, mimi nitapasahau nyumbani kwako kweli??

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ghafla tulitokea kwenye nyumba yake, ikiwa ipo vilevile ninavyoijua, nikashangaa. Hata nyumba za majirani zilikuwepo na huyo mama Ally aliyesema alikuwa anapika chakula nje kwa ajili ya genge lake nilimuona akashtuka kuniona, akasema:

?Hee! Mwana mpotevu huyo.?



Nilimsalimia, akasema nimepotea hadi nimekuwa mweupe tofauti na zamani, akanikaribisha.

Mayinu aliniingiza ndani kwake, nikakaribia, akafunga mlango huku akisema:

?Umekuja kunipa penzi au kunisanifu nikoje kwa sasa?? Mayinu aliniuliza kama kwa ukali kidogo.

Ilikuwa kumuweka sawa nikaamua kumwambia nimekuja kukupa penzi.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog