Search This Blog

OSAKA MJI ULIO POTEA - 4

 






Simulizi : Osaka Mji Ulio Potea 
Sehemu Ya Nne (4)






Mlio wa kengere ile ulisikika mji wote wa Mozana, tayari jeshi lilikuwa kamili gado, aliye shuhudia mtu akishuka kwenye chumba alicho kuwa akikitumia Alexandra aliongoza jeshi lile kufika eneo la tukio. Akiwa na wingi wa maumivu sababu ya kudondoka chini Alexandra akajikakamua, mbele ya macho yake aliona farasi mashuhuri aliye kuwa akimtumia kipindi chote alicho kuwa Mozana, upesi pasipo kupoteza muda alimrukia juu kwenye mgongo na kisha kumpa uhuru wa farasi yule kuchanja mbuga kuondoka ndani ya ile ngome ya Mozana ikiwa ndio mwanzo wa safari yake ya kuelekea OSAKA baada kukukaa Mozana kwa kipindi kirefu.

Mlio wa kipyenga ukapasa, ishara hiyo ilitosha kuamuru lango kubwa la kuingia Mozana ufungwe, Alexandra alijua fika ishara hiyo iliashiria nini, hivyo alimchochea farasi wake aongeze kasi, naye alitii, nyuma aliacha vumbi ikiwa jopo la jeshi wasio pungua mia tano lilionekana kumfuata nyuma huku wakirusha mishale yao ambayo nayo haikuweza kumdhuru wala kumdhuru farasi wake.

Lango la Mozana lilikuwa zito sana, lilitegemewa kufunguliwa na kufungwa kwa kutumia kamba, wanaume wasio pungua themanini ndio hulifungua na kisha kulifunga, ni kama ilikuwa kama bahati kwa Alexandra siku ile, kwani lango lilifunguliwa mapema kabisa tofauti na utaratibu.



"Piga huyo asivuke lango", Amri ya moja ya mwanajeshi ilisikika, aliwamlisha wanajeshi wenzake waendelee kumshambulia Alexandra ambaye kwa muda ule alimfanya farasi wake kutii ya kuchanja mbuga vilivyo, kibegi chake chenye kitabu kitakacho muwezesha kufika Osaka kilikuwa mgongoni, kilipepea tu. Aligeuka kuangalia wapi lilipo fika jopo lile, lakini hakuweza kuwaona shauri ya vumbi kubwa kutamalaki kwenye aridhi ya mji ulie ulio jaa laana.

Lango lile pole pole likakalibia kufunga ikiwa Alexandra bado hajafanikiwa hata kulikalibia, mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio, aliogopa akahofia kupotezwa moja kwa moja pindi atakapo kamatwa na jeshi lile kwa sababu amesha onyesha usaliti.



Upande wa pili Rinda, binti mfalme aliingia kwenye chumba Alexandra hima hima, alishtuka baada kutomkuta, alijua fika ndio yule anaye kimbizwa na jopo la wanajeshi wa baba yake, aliumia alidindosha machozi kwani alimuhitaji, aliamini kuwa Alexandra anaweza kuwa mpenzi wake wakati wowote kwani alitokea kumpenda toka wakati ule alipo kamatwa akiwa kama mateka, na hiyo ikawa ndio chanzo cha kumuokoa kwenye himaya ya kifo sababu laiti kama asinge mtetea mbele ya baba yake Alexandra angepotezwa muda ule ule alio kanyaga Mozana akiwa kama mateka. Aliketi kitandani akajiinamia, alijihisi mkosefu mbele ya baba yake kwani yeye ndio aliye muaminisha mfalme kuwa Alexandra ni binadamu mwema anaweza kuwa msaada mkubwa siku za usoni.



"Binadamu hafadhiriki", Alijisemea kwa jazba Rinda, akayafuta machozi yake, macho yake yalitazama kwenye kabati lile linalo hifadhi vitabu mbalimbali, aliona ujumbe umebandikwa kwenye mlango wa kabati, kabla hajagungua mlango ule alibandua karatasi ile iliyo charazwa maandishi kisha akafungua mlango. Alipigwa na butwaa baada kuona utofauti, alipekua pekua akagundua kuwa kitabu kimoja hakipo, nacho ni kile ambacho kilihifadhi siri nzito tofauti tofauti ikijumuisha Mozana pamoja na Osaka.

"Mshenzi sana huyu, nitamwambia nini baba yangu?", Aliongeza kujisemea Rinda alipo gundua kuwa yule binadamu aliye mtetea, akamuamini, sasa amewaingiza matatizoni. Lakini wakati binti mfalme akilaani kitendo alicho kifanya Alexandra, mara ghafla baba yake aliingia, mfalme alikuwa amekasirika kitendo ambacho kilipelekea macho yake kubadilika, yaliwaka mithili ya macho ya paka pindi yatazamapo mwanga.

"Tazama Rinda umefanya nini sasa?", Mfalme alihamaki, Rinda akageuka kumtazama, aliogopa alitetemesha nyama za mdomo wake kwa woga huku machozi yake nayo yakishuka ado ado, sasa alifikiria kumuomba msamaha baba yake lakini akahofia zaidi pindi baba yake atagundua kuwa Alexandra ametoweka na kitu muhimu kwa maisha yao ndani mji huo, si kingine ni kitabu.



"Najua nimekosa kwako baba, naomba nisamehe nakuomba sana", Rinda alishuka chini akapiga magoti chini sambamba na kuomba msamaha, mfalme aliishia kumtazama tu hata asiseme jambo, alikuwa na hasira kuu. "Nilijua tu huyu sio mtu wa kuachwa, uliniaminisha ujinga Rinda, sio kirahisi hivyo, nimempoteza shujaa wangu Josh kisa mpuuzi wako, sasa basi omba jitahada za jeshi langu zifanikiwe, akamatwe yule kiumbe tofauti na hivyo, utatii adabu tu", Aling'aka mfalme, maneno hayo aliyasema kwa jazba akimtazama binti yake chini ya miguu yake, alimnyoshea kidole cha ghadhabu kisha akatoka mule chumbani haraka haraka huku akimuacha binti yake akiendelea kulia kwa uchungu. Punde si punde akanyanyuka akaichukua karatasi ile yenye maandishi aliyo yaacha Alexandra kisha akaisoma.



Upande ule wa Alexandra mambo yalikuwa yamefika hatamu, hatimaye alianza kulikaribia lango lile wakati huo huo ikisalia eneo ndogo sana lango lifungwe, alizidi kumchochea farasi wake, alionyesha umahiri wa hali ya juu. Lakini kabla hajatoweka kwenye ngome hiyo ghafla mikuki zaidi ya arobaini ilitua mbele yake, farasi akagoma kusonga, alilia huku akinyanyua miguu yake ishara tosha iliyo mfanya Alexandra kugundua kuwa mnyama huyo ameingiwa na woga hataki kusonga mbele ili kuliepuka jeshi lile ambalo lilimjia kwa ghadhabu.

"Twende bwana wewe", Aliongea Alexandra wakati huo akigauka kutazama nyuma, kutokana na vumbi kubwa lililokuwa nyuma yake hakupata nafasi hata ya kuwaona wanajeshi wale wapo walipo fika, alisikia vishindo tu. Alichoka, alishikwa na hasira ikiwa muda huo huo farasi yule akapigwa mshale wa mbavuni, alilia mara moja akaanguka chini papo hapo akapoteza maisha. Ajabu aliyeyuka farasi yule akawa majivu maeupe kama alivyo kuwa akifanana rangi yake.

"Waooh! Hapa liwalo naliwe, mimi ni Alexandra, kidume niliye jitoa kupambana kwa hali na mali, kamwe sitakiwi kukata tamaa. Acha iwe", huku akihema haraka haraka alijisemea maneno hayo, sasa alishusha pumzi ndefu kisha akatimua mbio kuliwahi lango.



Alikimbia sana, alianguka na kisha kunyanyuka safari ikaendelea, alikoswa koswa na mishale kadha wa kadha, lango liliendelea kusogea, sasa ilibaki sehemu ndogo saana kiasi kwamba mwili wake ungeliweza kupenya lakini endapo kama atachelewa kamwe hatoweza tena kupita.

Hatua za mtu mzima zipatazo tano ndizo zilizo salia, hapo Alexandra alijirusha mithili ya mzamiaji apigavyo mbizi kwenye kina kirefu cha maji, kishindo kikubwa kilisikika, vumbi kumbwa ikatimuka ngome ikatetemeka, yote hayo baada lango kufungwa. Alihama haraka haraka akiwa chini, vumbi ilimpa tabu, baada vumbi ile kutulia akapata kuona vizuri mahali alipo, aligundua kuwa tayari yupo nje ya Mozana ila akahisi kuwa jopo lile la wanajeshi huwenda likaendelea kumfuata hivyo hakuona haja ya kulaza damu, akataka kuanza kuisoma ramani ya kuelekea Osaka sasa kwani shughuli pevu ya kuchomoka Mozana ilikuwa imekwisha kwa asilimia kubwa sana, lakini alijikuta alitaharuki baada kujikuta hana ule mkoba wenye kitabu!



Hatua za mtu mzima zipatazo tano ndizo zilizo salia, hapo Alexandra alijirusha mithili ya mzamiaji apigavyo mbizi kwenye kina kirefu cha maji, kishindo kikubwa kilisikika, vumbi kumbwa ikatimuka ngome ikatetemeka, yote hayo baada lango kufungwa. Alihama haraka haraka akiwa chini, vumbi ilimpa tabu, baada vumbi ile kutulia akapata kuona vizuri mahali alipo, aligundua kuwa tayari yupo nje ya Mozana ila akahisi kuwa jopo lile la wanajeshi huwenda likaendelea kumfuata hivyo hakuona haja ya kulaza damu, akataka kuanza kuisoma ramani ya kuelekea Osaka sasa kwani shughuli pevu ya kuchomoka Mozana ilikuwa imekwisha kwa asilimia kubwa sana, lakini alijikuta alitaharuki baada kujikuta hana ule mkoba wenye kitabu!

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Endelea..



"Mambo bado magumu kudadeki", huku akitazama kila pande alijisemea maneno hayo, alikohoa mara tatu mfululizo, vumbi jepesi lakalivagaa koo lake, aliendelea kukohoa wakati huo bado akitazama kila sehemu akikitafuta kitabu chake.

Geti la Mozana lilitikisika, bila shaka lilikuwa likifunguliwa ili jeshi lile liendelee kumfuata Alexandra. Walikuwa na uchu, ilikuwa nadra sana kumuacha aondoke kwani walihofia huwenda ameondoka na kiti cha muhimu na ndio maana alipitia njia isiyo rasmi, hawakujua kama ameondoka na kitabu.



"Uko wapi kitabu? Sema uko wapi ili niondoke zangu", alipaza sauti huku akizunguka huku na kule mithili ya kichaa, alifukua fukua mchanga, alihaha kukisaka kitabu kile alicho toweka nacho pasipo mafanikio ya kukitia mkononi, muda huo anahangaika ndivyo geti lilivyo endelea Kufunguliwa wakati huo kelele za kuhamasisha zilisikika vilivyo masikioni mwa Alexandra. Jambo hilo lilizidi kumtia hofu, alizidi kukazana kukitafuta kitabu, hatimaye juhudi za zilionekana kuzaa matunda, ghafla aliona mkanda wa kike kibegi alicho bebea kitabu, upesi akasogea mahala pale, akaushika ule mkanda kisha akauvuta kutoka kwenye wingi wa mchanga uliokuwa umekifukia mkanda ule, ilikuwa ni kile kibegi chenye kitabu, ndani kitabu kikiwemo pia. Alexandra aliachia tabasamu, machozi ya furaha haya kuwa mbali kumtoka, zaidi aliachia kicheko. Alicheka sana, sauti yake ya kicheko ilijirudia mara mbili mbili mithili ya mwangwi, radi ikamulika, Ngurumo kubwa nayo ikapaza ikawa ishara tosha iliyo wafanya wale wanajeshi kutambua kuwa binadamu yule hayuko mbali, hivyo basi hamasa ya kulifungua geti ikaongezeka zaidi ikiwa muda huo huo Alexandra aliendelea na safari yake.



Alitimua mbio, alivaa mavazi ya asiri yavaliwayo na wakazi wa Mozana. Alikuwa kifua wazi huku akizistili sehemu yake nyeti tu. Nyuma kwenye bega lake alikuwa na chata maalumu ambayo alipigwa ikiwa kama ishara ya kuwa raia wa Mozana. Chata ya maajabu ambayo ilikuwa ya kiumbe, kiumbe cha ajabu kisicho patikana Duniani.

Hatimaye geti lile likifunguliwa, waliomuona kwa mbali sana Alexandra akiendelea kuikimbia. Alikimbia kwa tabu sana kutokana na wingi wa mchanga uliokuwepo mahali hapo, lilikuwa jangwa kubwa lenye urefu na mapana kiasi kwamba hata kitu kikiwa mbali mita ngapi kilionekana, hivyo baada geti kufunguka jeshi lile liliweza kumuona. Mkuu wa msafara akatelemka juu ya mgongo wa farasi akashusha pumzi ndefu kisha akasema "Huyu sio binadamu wa kawaida, anamapafu ya dubu sio bure, lakini licha ya kuwa yupo kamili gado, haiwezekani akatuacha. Bado atakuwa dhaifu upande wetu, akamatwe tu hakuna namna"



"Makamandaaa"



"Heiii, kamandaaaaa", jopo la jeshi liliitikia, waligonganisha siraha zao.



"Hakuna linalo shindikana, tupo pamoja?"



"Heii kamanda tuko tayari"



"Shukeni kwenye farasi wenu, mchanga huu ni mwingi mtachelewa, mkimbuzeni kwanza miguu yenu yule kiumbe lakini pia sisi wengine wachache tutabaki nyuma yenu tutamshambulia kwa siraha zetu, anatakiwa kukamatwa akiwa mzima, akasomeww hukumu. Sawa sawa", kiongozi alisitiza.



"Ndiooo kamanda", jopo hilo liliitikia, walikubali kile kiongozi wao alicho sema, upesi upesi uteuzi wa kuchagua wanajeshi watakao mfuata Alexandra ukafanyika, sasa kazi ikaanza huku wengine walio bakia walifanya kazi moja tu ya kumshambulia kwa mishale na mikuki. Kiongozi wa msafara alichomoa mkuki wenye sumu kutoka kwenye kara alilokuwa amefungasha mgongoni mwake, akaulaza kwenye bega lake la upande wa kulia sanjari na kuupima kwa jicho kabla hauruhusu. Alipo jihakikishia kuwa kipimo chake kipo sahihi akaurusha, ukapita pembeni kidogo ya sikio la Alexandra, upepo ulio tokana na kasi ya mkuki ule ukapelekea Alexandra kuanguka. Kiongozi yule aliangua kicheko, kwa furaha akagongeana viganja na wanajeshi wenzake, aliamini shughuli imemalizika.



"Umeua kabisa", moja ya wanajeshi alisema.



"Sio rahisi, lakini kama nitakuwa nimemuua hakuna shaka. Tutajua kupitia mkoba wake amebeba nini", alijibu kiongozi yule wa msafara.

"Uko makini sana, hakika unastahili pongezi wewe ni mdunguaji mahali", mwanajeshi mwingine alimsifu.



"Alinyanyuka basi kidume", waliendelea kujaji uwezo wa kiongozi wao wa msafara kwa kuweza kumdungua Alexandra, kwa umbali aliokuwa hawakuona pingamizi la kushindwa kumpongeza. Lakini wakati wanaendelea kutoa pongezi hizo, ghafla hali ikawa tofauti, udongo wa jangwa lile ukayumba yumba mithili ya uji unao tokota, punde si punde ukaanza kupotea, bonde kubwa lenye giza ndani lililo ambatana na moto likatokea, jeshi lile lililo bakia likarudi nyuma kwa kasi ya ajabu huku wakihofia kuwapoteza wingi wa wanajeshi walio mfuata Alexandra.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jangwa liliendelea kumomonyoka kuelekea kule alipo angukia Alexandra, moto nao ukazidi kukolea vilivyo. Jeshi lile liliteketea, moja baada ya mwingine alitumbukia kwenye bonde lile lenye moto. Baada kutulia chini kwa muda kadha hatimaye alinyanyuka, alisimama akageuka nyuma hakuamini alicho kuwa akikiona ikiwa muda huo kiongozi yule na wanajeshi walio bakia nyuma walipigwa na bumbuwazi kumuona Alexandra amenyanyuka, walistaajabu sana, wakachoka hata wasioamini kama kweli Alexandra bado ana pumua. Walizitupa siraha zao kwenye shimo lile, geti likafungwa. Waliondoka wengi wakarejea wachache ndani ya Mozana. Ikawa taharuki mpya Mozana kwani hata mfalme naye hakuamini kilicho tokea.



Upande wa Alexandra mambo yalikuwa sio mambo, aliendelea kukimbia kujiokoa na moto ule na sio wanajeshi wa Mozana tena. Mbele ya jangwa lile palikuwa na msitu mkubwa wenye kila aina ya miti, palikuwa na mti mkubwa umeanguka, moja ya matawi ya mti ule liligusa jangwa lile ambalo lilikuwa likimomonyoka na kuzuka moto. Kwa kasi ya kichovu Alexandra alikazana ili aliwahi tawi lile awe salama. Juhudi zake zilizaa matunda alifanikiwa kushika tawi la mti ule, alitabasamu akiamini kuwa yupo salama sasa, lakini tabasamu hilo likawa la muda mfupi tu kwani alipo shika tawi, mti ule ulinyanyuliwa juu na moja ya mijitu mikubwa inayo patikana ndani ya huo msitu.



Jitu lile liliunyanyua ule mti kwa dhumuni la kuutupa kwenye bonde lile lililokuwa likitoa moto, lakini kabla halijafanya kitendo hicho Alexandra akaruka pasipo kujali umbali aliokuwa nao. Jitu lilikuwa kubwa sana, umbile lake liliendana kabisa na Goriath, jitu lile lililo kabiliana na mfalme Daudi kama maandiko yasemavyo.



"Mshezi mkubwa wewe, siwezi kufa kizembe hivi", akiwa chini akigugumia maumivu, alijisemea maneno hayo ndani ya moyo wake, alihema haraka haraka huku akilitazama jitu lile, alistaajabu sana. Alitazama kibegi chake, akakuta bado kipo bavuni, aliachia tabasamu mwanana, sasa akanyanyuka kwa kudhumuni ya kufungua zipu ili achukue kitabu kile kisha aanze kuisoma ramani ya kumfikisha Osaka, lakini kabla hajafanya jambo hilo, ghafla akasikia kishindo nyuma yake. Upesi akageuka kutazama nini kilicho kuwa kikimnyemelea, akapigwa na butwaa kuliona Jitu lingine, safari hiyo lilikuwa Jitu la kike, Jitu lile lilitembea kwa madaha kuelekea mahali lilipo simama Jitu lile ambalo lilitupia mti kwenye bonde la moto na kisha kubaki likistaajabu namna mti ule ulivyo kuwa umiteketea.

Hapo Alexandra akajua yupo kwenye himaya ya mijitu hiyo, hakuona sababu ya kutazama ramani, hima kafanya jitahda ya kuyakwepa ili awe salama ndipo aisome ramani kwa umakini na utulivu wa kiwango cha juu.



Alilikwepa kwa kusogea kando kisha akajificha nyuma ya mti. Alifanya hivyo kwa umakini mkubwa ili asije akaonwa. Guu la kulia la Jitu lile lilikanyaga pembeni yake kidogo tu, woga ukazidi kumjaaa, mapigo ya moyo yakamuenda mbio lakini akajikaza kiume, hakupiga yowe kwani yowe lake lisingekuwa na manufaa upande wake, hivyo hata kupumua alipumua taratibu sana ilimladi tu asisikike. Hatimaye Jitu lile lilipita, hapo Alexandra akashusha pumzi ndefu, ghafla Jitu lile la kiume liligeuka nyuma, likajikuta walioungana macho na Alexandra, wakati huo huo Alex akatimua mbio jambo ambalo lilipe mijitu ile miwili la kike na kiume kumtimua. Hatua saba za Alexandra ilikuwa ni hatua moja tu ya mijitu ile, alicho kifanya Alexandra ni kukimbia zigzag kitendo ambacho kilipelekea kuwapata tabu mijitu ile kushindwa kumkamata. Miti ya msitu ule ilikuwa mirefu sana, lakini pia ilikuwa na kamba mbali mbali zilizo fanana na mizizi. Mithili ya Kima, Alexandra alinyanyukia moja ya kamba iliyo kuwa ikibembea. Hakujua urefu wa kamba ile wala hakujali uimara wake, alidandia nayo ikamsafirisha juu juu, akatoweka kwenye msitu ule wenye mijitu, mbele zaidi palikuwa na bonde kubwa lenye urefu na mapema, lilijaa ukungu lakini pia lilikuwa na msitu mwingine wa kawaida. Mwisho wa kamba ile iliyo msafirishaji ukawa ndio mwanzo wa kudodokea kwenye msitu mwingine wa pili.



Mithili ya kinyesi cha Kunguru kidondokavyo kutoka angani, ndivyo ilivyokuwa kwa Alexandra namna alivyo dokea kwenye msitu ule wa pili. Lakini kabla hajatua chini, alikoswa koswa na Joka lililo onekana kubwa sio kawaida, ni Joka ambalo liliunyanyua na kuamua kumuwahi kule kule juu lakini jitahada zake zikaota mbawa, liliambulia patupu.

Alikwama juu kwenye moja ya mti ya msitu ule, hali ya hewa ndani ya ule msitu ilikuwa shwari kwa asilimia chache iliendana na hali ya hewa ya Duniani. Walau Alexandra akajihisi yupo Duniani, hivyo ile nguvu na hali ya kuendelea na safari yake ikamjaa.

"Ngoja sasa nikutazme wewe ramani, maana naona kula dalili ya kukamilisha zoezi langu", akiwa bado kakwama juu kwenye mti aliongeza kujisemea. Sasa akavua mkanda wa kibegi chake akakipakata na kisha kufungua zipu. Kitabu kilikuwa na kava zenye picha za ajabu ajabu, hakika kilitisha. Alikigeuza mbele na nyuma akikichunguza vizuri halafu akahitaji kufunua kurasa ili aanze kujua yaliyomo huku kimoyo moyo akijishuku itakuache kama njia ya kuelekea Osaka atakuwa ameiacha Osaka!



"Itakua patashika", alishusha pumzi na kisha kujisemea maneno hayo ila kabla hajakifunua kitabu kile, ghafla alihisi kitu, machale yalimcheza, upesi akaanza kuangalia kila pande, alianza kutazama mbele kisha kulia na kushoto, alipo angalia nyuma yake akaliona Joka lile lililo mkosa muda mfupi ulio pita, Joka lile lilionekana likitambaa pole pole, liling'aa ni Joka lenye urefu na unene mkubwa. Alexandra aliogopa alitulia tuli kama maji ya mtungini, lilipo tokomea akafunua kurasa za kitabu kile pole pole na kwa machale makubwa, hakutaka kujua sheria za mji wa Osaka, alicho kifanya ni kujua yuko sehemu gani, yupo umbali gani na Osaka mji ulio potea. Lakini kabla hajaufikia ukurasa ule wenye ramani, Joka lile likapita tena na kutoweka. Hapo ndipo Alexandra alipoona kuwa hakuna haja ya kuendelea kusalia mahali hapo, alitelemka na kisha kutembea kwa wasi wasi kuongoza mbele eneo ambalo lipo tofauti na kule alipo liona Joka.

Alitembea umbali mrefu, hakubuguziwa na kiumbe chochote. Mbele zaidi aliona mifupa ya binadamu, kando ya mifupa ile palikuwa na bunduki na upanga. Vyote vilikuwa vimepigwa na kutu. Alifikiria kuachana na siraha hizo lakini roho ikamsuta akahisi kuwa huwenda siraha hizo zikawa na msaada mkubwa huko mbele ya safari yake. Alizichukua akazivaa mgoni, sasa safari ikaendelea. Mwili ulimuuma shauri ya mikimiki aliyokuwa akikutana nayo, safari hiyo kila kitu kilikuwa tofauti kabisa, alihisi njaa na kiu pia kitu ambacho kilimfanya kutembea kwa uchovu mkubwa, baadaye alipata kuona bwawa lenye maji mengi kiasi huku juu yakielea magugu. Alifurahi sana, pasipo kupoteza muda akalisogelea bwawa lile kwa dhumuni la kukata kiu yake, alichuchumaa ili anywe. Lakini wakati ana kunywa maji yale mara ghafla ndani ya maji kwa mbaali aliona majengo mengi na watu wakiendelea kufanya shughuli zao. Alishtuka Alexandra, hakuyaamini macho yake, na pindi akiwa katika taharuki hiyo ya kuona mji ndani ya yale maji, nyuma yake alihisi Joka lile linakuja mahali alipo...



Aliacha kuendelea kutazama mji ule aliouona ndani ya maji, sasa akageuka kutazama nyuma yake. Hakuliona Joka ambalo alilokuwa akilihisi, aliona watu wasio pungua saba, walikuwa wafupi mno, masikio yao yilikuwa marefu kiasi ila yalikuwa tofauti na masikio ya binadamu wa kawaida. Walivaa kiasiri pia.

Walionekana kuwa wapole, nyuso zao zilitia huzuni, Alexandra aligundua hilo jambo ambalo lilimpelekea kuwa mpole na kutowahofia kabisa watu wale. Alinyanyuka akasimama kidete, moja ya watu wale alitoa ishara ya kuashiria amani, alimtuliza Alexandra kwa ishara ya mikono, naye alionyesha utulivu ingawa hakuwaamini asilimia mia moja. Lakini wakati utulivu ukitawala mahali hapo, ghafla wakasikia Joka lile likija mahala pale walipo, upesi watu wale wafupi wakajitupa kando kidogo ya bwawa lile ambalo Alexandra aliona mji, wakajipaka matope, Alexandra naye alifanya hivyo upesi wakati huo huo Joka lile likatokea. Lilikuwa na hasira, lilitoa ndimi yake huku likiangaza kila pande. Halikuweza kuwaona watu wale walio jipakaa tope, mbali na kushindwa kufanya hivyo, upande wa Alexandra yeye alifanikiwa kuliona vizuri kabisa. Ni Joka kubwa, hakuwahi kuliona popote Dunia wala kwenye upande wa sinema.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Aaah! Kumbe tope hili ni daw? Maajabu mengine haya sio bure", akiwa bado amechakaa tope akajisemea maneno hayo, aliamini kuwa tope linaweza kumkinga vyema dhidi ya Joka lile.

Hatimaye liliondoka, walipo hakikisha limetoweka mahali hapo wakaoga miili yao ili kuliondoa tope lile. Alexandra yeye alioga huku akitazama kwa umakini ndani ya maji kwa dhumuni la kuuona mji ule kwa mara nyingine tena, lakini safari hiyo hakuuona. Alikereka ikiwa muda huo huo watu wale wafupi walimtaka aondoke ndani ya bwawa lile, alitii ingawa alitamani kuendelea kuuchunguza akidhania kuwa anaweza kuuona tena na zaidi akahisi kwamba huwend mji ule alio uona ndio mji wa Osaka wenyewe.

Watu wale wafupi waliambatana naye mpaka kwenye makazi yao, palikuwa na vijumba vidogo vilivyo endana na maumbile yao. Kilikuwa kijiji kidogo, walio ishi hapo wote walifanana maumbile yao. Lakini kamwe hakumshangaa Alexandra kutokana na umbile lake ambalo lilikuwa tofauti na maumbo yao, zaidi mtu mmoja kati yao aliingia kwenye moja nyumba yake akatoka na begi ndogo kiasi akafungua zipu akatoa nguo, lilikuwa ni koti kubwa la kikomando lakini pia zilionekana siraha mbali mbali za kisasa ambazo zinapatikana duniani. Vyote alikabidhiwa, akapokea na kisha kuvaa, muda mfupi tu muonekano wake ukabadilika hakuwa yule aliye toka Mozana, sasa akaonekana kuwa mtu mpya kabisa, mavazi yale yalimpendeza sana. Aliingiza kiganja chake kila mfuko wa koti lile, lilikuwa ni koti jeusi lenye urefu ulio endana na umbile lake. Kwenye moja ya mfuko alipata kuona picha, akaitazama picha ndogo (paspoti size)aliitazama kwa umakini picha ile lakini hakuitambua ile sura, moyoni akajisemea "Huwenda ndio mwenye mavazi haya, lakini alifikaje fikaje huku? Yaani nashindwa hata kuhoji maana wanaonekana kama hawasikii wala hawajui kuongea. Laah! Lakini koti hili limenikaa sawa kabisa, sasa ngoja nisikilizie kitajiri kipi hapa, na sitowez a kucheza mbali na mahali hapa maana iwe isiwe lile bwawa ndio utakuwa mlango wa kuingia Osaka", alipokwisha kuwaza hayo akashusha pumzi ndefu wakati huo huo akaletewa mchoro ulio chorwa kwenye bango ukionyesha sura mbali mbali huku kando pakiwa na Joka kubwa. Aliutazama kwa umakini hukua kuwa amezungukwa na jopo la watu wale wafupi, baada ya kuangalia kwa umakini akanyoosha dole gumba kuashiria kuwa tayari ametazama vya kutosha. Watu wale wakatabasamu, sasa wakampa siraha zile ambazo zilikuwa sambamba na mavazi aliyo yavaa. Yalikuwa mabomu matatu, upinde na panga. Lengo kuu la kukabidhiwa vitu hivyo ni kwenda kuliangamiza Joka lile kwani limeua ndugu zao na bado linaendelea kuua, hivyo halistahili kuishi.



Alexandra alipoelewa maana harisi alishtuka, aliogopa sana. Joka ni kubwa sana, na wala sio rahisi kufa kwa upinde wala bomu au upanga, Joka lilie liloonekana sio la kawaida na ndilo hilo anatakiwa kuliua.

Alivua mavazi yale akayabwaga chini, akakataa kufanya kazi hiyo, na sasa akachukuwa kitabu chake akafunua kurasa haraka haraka za, alipo ufikia ukarasa wenye mji wa Osaka akawaonyesha, kisha akasema "Nina safari zangu, sipo tayari kufanya kazi yenu. Mimi ni ni binadamu tu wakawaida tafadhali niacheni niondoke, natakiwa kufika hapa Osaka na si vinginevyo bwana, nyie mbilikimo vipi!? ", japo alijua watu wale hawasikii wala hawajui kuongea ila ilimlazimu kupaza sauti, aliongea maneno hayo kwa hasira, walimkera. Hakutaka kuendelea kuzungumza nao alikirudisha kitabu chake kwenye kibegi chake kisha akaanza safari ya kuondoka kulifuata bwawa lile alilo ona mji huku nyuma aliwaacha wale watu wafupi wakimsindikiza kwa macho tu, macho yaliwatoka waliamini kuwa siku zote binadamu ni mtu mwenye maarifa, anaweza kufanya jambo lolote la kushangaza kwa kutumia maarifa yake na ndio maana walijaribu kumshawishi kila mwanadamu aliye katiza eneo lao amuue Joka lile kwani liliteketeza ndugu zao, hivyo mwanadamu yule aliye jaribu kufanya jitahada hizo aliuawa. Joka likawa limejitengenezea utawala mkubwa huku wanyama wadogo wadogo pamoja na watu hao wafupi ikiwa ndioo chakula chao katika msitu ule.

Lakini wakati Alexandra alipokuwa akiendelea kutembea, moyo wake ulikuwa mzito sana. Roho ilimuuma sanjari na kumsuta kushindwa kutoa msaada huo kwa kisingizio kuwa anahofia kupotea mazima kwenye ulimwengu huo usio wa ajabu, alijiona amesha kuwa mfu, na kama asinge okolewa na watu hao hao aliogoma kuwasaidia basi Joka lile lingekuwa limeshammaliza pale pale kwenye bwawa alipokuwa akinywa maji lakini kitendo cha kupata mbinu kutoka kwa watu wale, mbinu ya kujipaka tope ikawa salama kwake.

Alikata shauri akarejea kwenye mkazi ya mbilikimo wale, alisikitika kuwakuta wakiwa wanyonge, akairejesha furaha yao kwa kukubali kufanya kazi hiyo ya kuliangamiza Joka, tena akawahakikkshia kuwa uwezo wa kuliua upo kwa asilimia kubwa.

Usiku uliingia, hakika mahali hapo palikuwa tofauti kabisa na Mozana. Usiku huo walikoka moto, walichoma nyama, Alexandra alikula pasipo kujali nyama anayo kula ya mnyama gani. Alizungumza nao kwa ishara lakini aliwaelewa. Moja siri aliyo ambiwa katika mazungumzo yao ni kuwa Joka hilo ifikapo usiku huwa halitembei hutulia ndani ya bwawa lile ambalo aliona mji, hapo sasa shauku ya kupambana nalo ikamjaa zaidi, lakini pia alihisi kuwa watu hao wana siri nzito kuhusu Osaka, na ili siri hizo azipate ni lazima awashawishi kwa kuliua Joka "Hakuna namna nyingine tena, japo kibarua kirefu ila maji ukisha yavulia nguo sharti uyaoge", alijisemea ndani ya nafsi yake kisha akalala akisubiri kesho yake kazi.

Lakini usingizi ulipo kolea, aliota ndoto kuwa Devis, mfungwa mzikaji ambaye ndiye aliye mtuma Osaka ameaga dunia! Ndoto hiyo ilimshtua na kumpelekea kuamka kutoka usingizini, aliamini ndoto zake. Alihema haraka haraka kwa hofu kubwa kwani Devis mbali na kumpeleka Osaka, vile vile ni msaada mkubwa kwa kuwa yeye ndio mwenye uwezo wa kumrejesha Duniani kwa kulifukua kaburi alilo mfukia.



"Nenda Osaka, ukisha rejea, ingia ndani ya jeneza mimi nitapata kukuona pindi utakapo ingia kwenye jeneza hili unalo zikwa nalo. Ndipo nitalifukua, utanipa pete ambayo ni hitaji langu kisha wewe nakurudisha nyumbani kwenu ili ukiepuke kifungo cha kunyongwa huku ughaibuni ", pindi alipokuwa akiitafakari ndoto yake ambazo mara nyingi hutumia, aliyakumbuka maneno hayo ya mwisho kutoka kwa mfungwa mzikaji Devis, mchungaji mwenye ndoto ya kuwa muhibiri mwenye miujiza itakayo wavuta waumini kwenye kanisa lake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Ilikuwa ni ndoto tata ambayo ilizunguka vyema kichwani mwa Alexandra, alipoa mithili ya maji ya mtungini huku usingizi nao ukimpaa kabisa. Alishusha pumzi ndefu, akatazama kiota cha moto chenye kuni ambacho kilionekana kupamba moto, moto uliwaka kwa hasira.

Muda mfupi baadaye usingizi ulimnyemelea, akajilaza. Baadaye tena aliamka kwa mara nyingine tena, safari hiyo aliota ndoto kuhusu mpenzi wake huko Duniani, nchini Tanzania mkoani Arusha kijiji cha Karatu. Ndoto hiyo ilimuonyesha kuwa mpenzi wake ambaye anampenda kwa dhati anakata tamaa ya kumngoja, na sasa anakubali kutii wazo la wazazi wake ambao walikuwa wakimlazimisha aolewe kuliko kumngoja mwanaume asiye na tumaini kurudi.

Mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio mithili ya saa mbovu, roho ilimuuma sana kwani anampenda saba mpenzi wake, wanamikakati mingi sana ambao wameipanga, hivyo basi ndoto ile iliweza kumtia shaka, shauku ya kutaka kurudi duniani kuzima mpango huo wa mpenzi wake kuolewa na mwanaume mwingine ilimjaa tele, lakini baada kukumbuka ndoto aliyoota kuhusu kifo cha Devis, alinyong'onyea.

"Lolote linaweza kutokea, ngoja nimalize zoezi hili upesi ili nijue cha kufanya, naam hakuna namna", alijisemea Alexandra baada kuzitafakari ndoto hizo kwa kina.



Usiku huo huo alianza mkakati wa kuandaa mitego ya kumnasa Joka lile analo takiwa kulia ili kuwaacha kwa amani jamii ile ya watu wafupi, watu wale waliamini binadamu wanamaarifa makubwa, kwa maarifa aliyo jaliwa Alexandra walijua ataweza kulimudu. Alivua kibegi chake chenye kitabu kile chenye ramani na taratibu husika za maisha ya Osaka, akazivaa siraha zake akachukua na mabomu kadhaa aliyo yakuta kwenye himaya ya mbilikimo wale, akazipiga hatua kuelekea kwenye bwawa lile mahali linapo patikana Joka lile, msitu ulikuwa tulivu mwanga hafifu kabisa ndio ulio tawala hata pasiwe na kelele zozote za mnyama wala mdudu. Bundiki mbili mgongoni pamoja na upinde sambamba na ghala lililo sheheni mishale huku mkononi akiwa na upanga makali aliendelea kutembea kwa hatua za kunyata kuelekea kwenye bwawa. Hatimaye alifika, aliliona Joka lile liking'aa kutokana na mwanga hafifu, lilikuwa limetulia tuli hata lisiwe na jambo kwani pindi giza liingiapo hupoteza ukali na uwezo wa kumuona adui. Udhaifu huo Alexandra alitaka kuutumia ili kabla hapajapambazuka Joka hilo liwe limepoteza maisha.



"Mshenzi mkubwa, na leo ndio utakuwa mwisho wako", huku akiwa na kila hali ya kujiamini, matumaini kibao yakiutawala moyo wake Alexandra alijisemea maneno hayo kisha akatazama ni wapi pa kuanza kutega mitego yake. Alitembea pole pole kando ya bwawa lile, ghafla aliguswa na kitu chenye ncha kali kwenye mguu wake, alipo shusha mkono wake ili kugundua gani kilicho mgusa akagundua kuwa waya wa sinyenge ndio uliogusa ugoko wake, akauvuta, ulikuwa mrefu ila ulikuwa na mwisho wake. Hiyo nayo ikawa siraha nyingine pia, Joka bado likazidi kuwa matatani kwani Alexandra alizidi kujidhatiti.



"Ama hakika kila lenye mwanzo lina mwisho wake, kwa kipindi kirefu umekuwa mfalme ndani ya pori hili. Umeua bila hatia, umetia vilema visivyo na msingi, ulilaaniwa utatembelea tumbo, huwezi kumfalme labda Simba aidha tembo na sio kiumbe wewe mtembelea tumbo. Sasa nakupoteza kwa mwendo huu, kwanza nitakukera kwa kukutupia bomu, najua utacharuka ndipo nami nitakapo washa moto kuelekea kwenye mtego wangu, najua utanifuata, hapo sasa ndipo utakapo kuwa mwisho wako. Kwani nitakuchachavya vibaya mno, kwa sababu najua nikikukosa utanimaliza, lazima ufe, hakuna namna", aliongea Alexandra akieleza namna atakavyo muua Joka, aliyasema hayo huku akitengeneza mitego wakati huo moyoni mwake ukiwa ndio mpango atakao ufanya baada kukamilisha mpango mzima.

Hatimaye zoezi hilo linakamilika, mtego ulikuwa tayari, alivua koti alilokuwa amelivaa akasalia ndani ya vazi lile alilo tokanalo mji wa Mozana. Alirudi tena mpaka pale kwenye bwawa, alikuta Joka bado limetulia hata lisiwe na habari yoyote. Sasa kazi ilitakiwa kuanza mara moja kabla hapajapambazuka, hivyo aliseti bomu lake na kisha kulirusha katika bwawa lile ikiwa nia na madhumuni kumkera Joka. Bomu lilipo tua likalipuka, moyowe ya Joka yakapaza, kupitia mwanga ule wa Bomu likapata kumuona mtu akiwa amesimama hatua kadha kutoka mahala lilipo lala. Tayari Alexandra alikuwa amewasha moto kwenye kijiti mfano wa mwenge, sasa alitimua mbio kuelekea mahali ulipo mtego, waya wa sinyenge alioutega vyema kwa kufunga mti wa kulia kwenda kushoto ukilenga kinywa cha Joka ulingojea kuuchana vibaya kinywa cha Joka lile.

Kwa ilikuwa ni giza, Joka lilikimbia kwa tabu huku likijigonga kwenye miti, lilifuata kijinga kile cha moto alicho kamata Alexandra ambaye kwa wakati ule alikuwa akikimbia mbio kuelekea kwenye mtego. Muda mfupi baadaye alifika, alipita chini kisha akasogea mbele zaidi ya mtego wake kisha akauvua upinde, akachukua mshale akajiandaa vyema kulishmabulia Joka lile pindi litakapo nasa kwenye waya ule. Naam! Hatimaye likayakanyaga, lilipo ugusa tu waya ule, kilele ziliongezeka maradufu, lilipigwa yowe ikiwa muda huo huo mvua kubwa iliyo ambatana na radi ikashuka, upepo nao ukalindima vilivyo na kupelekea miti yote ya msitu ule kuyumbishwa mfano wa Tr iliyo poteza muelekeo.



"Njoo.. Ahahahaha hahahaha njoo mwanaharamu mkubwa wewe", alisema Alexandra aliliambia Joka, alionekana sio Alexandra wa Dunian, huyu Alexandra alikuwa na roho ngumu iliyojaa ujasiri mkubwa, apesi akafyatua mshale wa kwanza, ulipo mpiga Joka, ajabu mshale ule ulidunda. Alirudia tena na tena kisha akachukua bundi yake na kisha kulishambulia risasi nyingi mfululizo, bahati mbaya waya ule ukamatika, Joka likawa huru na hata lisizuruke na risasi zile. Alishtuka Alexandra, akatupa bunduki chini akabaki na upinde tu pamoja na kara lililo sheheni mishale, akatimua mbio kujiokoa wakati huo huo nyuma akifuatwa na Joka lile ambalo lilionekana kuwa na hasira, mwanga ulio tokana na miale ya radi iliweza kumfanya kukuona wapo Alex anapo kimbilia.

Patashika nguo kuchanika ndani ya msitu, katika heka heka ya kujikomboa ghafla akaona kamba kama ile iliyo mtoa kwenye msitu wa mijitu mkubwa pindi alipo toka Mozana, kwake ilikuwa ni furaha tosha, aliirukia mithili ya mnyama Kima. Kamba ile ikatii, ilijivuta na kwenda kumtupa kwenye mto mkubwa uliokuwemo ndani ya msitu ule. Aliyajulia maji kajana, hivyo aliongelea upesi upesi mpaka kando ya mto ule kisha akajipakaa topo ili hata radi ikimulika asipate kuonekana.

Alipo maliza zoezi hilo, muda mfupi baadaye akaliona Joka lile likishuka ndani ya mto ule, liliogelea kwa kasi ya ajabu. Lilipo fika nchi kavu, likapunguza kasi, lilijikokota pole pole, lilipita kando ya Alexandra pasipo kumuona shauri ya tope alilo jipakaa. Pumzi alibana Alexandra huku akilitazama kwa ukaribu, alistaajabu sana namna Joka lile lilivyo kubwa. Punde si punde akapata wazo, nalo ni kumjeruhi tumboni baada kushindikana usoni zoezi lililo fanyika hapo awali. Alifanya hivyo, alifyatua mishale mitano mfululizo, ilipo mchoma upesi likageuka ili kujua ni kashi kashi gani iliyo tokea kwenye mwili wake, kitendo cha kugeuka kilizaa mkumbo mkubwa ambao ulimsukuma Alexandra ukapelekea kutupwa Mtoni. Tope lile lililo mficha ili asionekane likamtoka, giza nalo likatoweka angani jambo ambalo lilipelekea Joka lile kupata kumuona vizuri pasipo chenga yoyote.



Uso kwa uso wawili hao wakatazana, muonekano wa kutisha alionao Joka lile ulipelekea Alexandra kupiga mbizi kufuata mkondo wa maji. Alifanya hivyo ili kujinusuru dhidi ya Joka lile lenye hasira kali na ghadhabu ya hali ya juu.

Lakini licha ya Alexandra kufanya jitahada ile ya kishujaa, Joka lile halikulaza damu, lilimfuata ndani ya maji. Alex akainuka baada kuzama ndani ya maji kwa muda mrefu, wimbi kubwa likamkumba na kupelekea kumzamisha ndani ya maji kwa mara nyingine tena, wimbi kubwa lililo tokana na uzito wa Joka lile la kutisha, Joka kubwa lenye unene na mapana huku ngozi yake iking'aa vyema kabisa. Damu mchanganyiko na maji iliibuka, damu ile ilitoka kwenye jereha alilo jeruhiwa na Alexandra, jambo hilo lilimpa tabu sana Joka lile kwani pindi maji yalipo piga kwenye kidonda, yalimfuwasha sambamba na kukichimba kidonda hicho, na pole pole likaanza kuishiwa nguvu.

Kwa kuwa kasi ya kwenye maji maji ilikuwa ndogo upande wake iliweza kumpeleka Alexandra kuyachapa maji haraka haraka, aliongelea na kupiga mbizi huku mara kadhaa akigeuka nyuma kutazama umbali alio liacha Joka lile.



Lakini baadaye mbio zake zikafika ukingoni, mbele palikuwa na mporomoko mkubwa wa maji. Alishtuka baada kuhisi uwepo wa mporomoko huo, ndipo alipo anza kufanya jitihada ya kuyakata maji kuogelea kuelekea nchi kavu ili asidhurike. Juhudi zake ziliota mbawa, maji yalizidi kumvuta kwa kasi kwani tayari alikuwa ameukaribia mporomoko. Alipohisi kukwepa zahma hiyo hatari, alijilegeza, alikubali yaishie huku ndani ya moyo wake akiamini kuwa huwenda ile ndoto ya kifo cha Devis hiyo ndio maana yake.

"Huwenda hii ikawa ndio maana sahihi, jitihada yangu imeota mbawa, nakufa na huyu mwanaharamu mshenzi asiye faa. Itabaki kuwa katika pori hili kama historia niliyo iacha Mozana", aliachia tabasamu baada kuwaza ikiwa wakati akizidi kuukaribia mporomoko. Naam! Hatimaye aliukaribia, ulimtupa, Joka lile nalo likatupwa kama ilivyo kuwa kwa Alexandra. Kwa pamoja walipotea takribani dakika arobaini za kawaida hapa Duniani, lakini baadaye Alexandra aliibukaa akaelea juu, muda mfupi baadaye Joka lile nalo liilibuka likaelea juu huku damu zikiendelea kutapakaa.



MOZANA. Ghafla lango la mji ule lilipasuka vipande viwili, jeshi la mji wa Hanjari lilivamia na kisha kuua wanajeshi wa mji wa Mozana kwa fujo. Mfalme alitoka ndani upesi kwenye jengo ndefu, akapata kuona wingi wa wanajeshi wa mji wa Hanjari lilizidi kujongea. Kwa muda mrefu mji wa Hanjari umekuwa ukianzisha vita kwa lengo la kutaka kitabu cha kuelekea Osaka, mji wenye mali na kila aina ya vitu vya dhamani, kwani mbali na pete ile yenye maajabu, lakini pia Osaka palikuwa na kila miujiza na uwezo, uchawi na ulinzi makali utumikao kulinda mashirika au baadhi ya maraisi mbali mbali duniani. Mfalme wa Mozana ndiye aliyekuwa akilimiliki kitabu kile kabla Alexandra hajatoweka nacho, alikihifadhi kwa siri huku akiwa na nia ya kutafuta shujaa mmoja atakaye muamini ndipo amkabidhi kitabu hicho aelekee Osaka akamletee pete, lakini kabla mpango wake haijatimia Alexandra akatoweka na kitabu hicho ambacho kwa nyakati tofauti kimekuwa kikizaa vita kubwa mjini Mozana, wakati mchungaji na mzikaji mfungwa Devis akiitamani pete ile ya Osaka, huku kwenye miji iliyo toweka kwenye uso wa dunia karne kibao zilizo pita nayo ilikuwa ikiitamani pete ile.



"Sikiliza kwa umakini haya niyasemayo, nimekuja kwa dhumuni moja tu hapa kwenye mji wako. Sihitaji kelele. Ninacho kitaka ni kitabu", kiongozi aliyeongoza jeshi hilo la Hanjari alisema kwa msisitizo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sina kitabu cha Osaka, lakini pia hatakama ningekuwa nacho mngekuja kwa ustaarabu tukakaa meza moja tukajua jinsi gani ya kuchafanya kuliko kuua wanajeshi wangu", mfalme wa Mozana alijibu. Ajabu kiongozi yule wa jeshi la Hanjari aliangua kicheko huku akilitazama jeshi lake.



Alipo katisha cheko lake akaongeza kusema "Leo ndio unajifanya mwema, huna lolote na nidhamu yako ya woga. Sisi sio wa kukaa meza moja na wewe, uwezo tulio nao ni zaidi ya unavyo fikiria, ndio maana tumethubutu kupita kwenye jangwa la moto pasipo woga wowote. Leta kitabu tuondoke kabla hatujaipindua ardhi yako ndani ya dakika sifuri ", kwisha kusema hivyo shangwe kubwa lilisikika, wanajeshi wa Hanjari walishangilia namna kiongozi wao alivyokuwa akiongea kwa kujiamini, muda mafupi baadaye Josh akajitokeza. Ni yule kiongozi wa jeshi la Mozana hapo kabla hajatoweka baada kupokea kipigo kikali kutoka kwa Alexandra. Mfalme wa Mozana alipomuona ishtuka sana, alijua fika Josh atakuwa ametoa mbinu zote kwa maadui zao, alisikitika sana. Alipoa mithili ya maji ya mtungini wakati huo Josh na wenzake wakingojea kitabu.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog