Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu
Sehemu Ya Pili (2)
Nilifika msibani asubuhi ya saa kumi na mbili na nusu baada ya kaka kunipigia sana simu kunitaka tukaungane. Macho yangu yalicheza kumtafuta Munil. Sikuwa na mtu wa kumuuliza zaidi ya kumtumia meseji.
"Uko wapi baby, mbona sikuoni?" niliandika kwenye meseji.
Meseji hiyo ilijibiwa kwa maneno haya:
"Mxwakabamshhaka."
Niliguna kwanza baada ya kukutana na meseji hiyo ya ajabu. Nilijiuliza amekosea au? Na kama amekosea alitaka kuandika nini maana hata pale nilipojaribu kuunganisha maneno sikupata maana hata moja.
Nikatuma meseji nyingine ya kumwambia kwamba amekosea kuandika, akanijibu hivi:
"Pkamahsdioaha***---."
Niliamua kwenda pembeni ili nimpigie, simu iliita mpaka ikakatika. Nikapiga tena, akapokea.
"Baby vipi? aliniuliza Munil.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mbona unakosea kuandika meseji wewe? nilimpelekea swali moja kwa moja.
Nalikosea kuandika meseji kivipi jamani?
Si unaandika mambo yasiyojulikana, sijui ni maandishi gani yale!
Mbona nimeandika sawa. Halafu hii simu ninayo mwaka wa kumi sasa sijawahi kuambiwa na mtu hata siku moja kwamba nimeandika meseji vibaya.
Kwanza nilishtuka kumsikia akisema simu ile anayo kwa mwaka wa kumi kwani ni mpya halafu si rahisi kwa msichana kama yeye akae na simu miaka kumi, pia Munil aliniambia ana miaka ishirini na nne, ina maana alianza kumiliki simu akiwa na miaka kumi na nne?
Nilitamani kumuuliza kuhusu hilo lakini kila nilipotaka kuuliza nilijikuta nashindwa na midomo kuwa mizito huku akili ikiniambia wasichana wa siku hizi wanaweza, wala si ajabu.
"Ina maana mimi nimeona vibaya?" Maana sijafuta meseji zako ujue.
Umeona vibaya mume wangu, we soma vizuri au simu yako ndiyo inachanganya herufi.
"Oke ngoja niangalie, nitakwambia.
"Uko wapi?" nilimuuliza mwisho, akasema yumo ndani kwenye msiba huo.
Nilirudi na kukaa, nikafungua meseji, ya kwanza iliandikwa:
Nipo msibani baby, wewe je umeshafika kwenye msiba?
Nilishtuka sana kukutana na maneno hayo badala ya yale ya mwanzo. Nikasoma meseji ya pili, ilisema hivi:
"Nimekoseaje baby, mbona nimeandika sawa tu, labda simu yako.
"Noo, si kweli, nilisema na kumshangaza kaka, akaniuliza.
"Si kweli nini wewe?
"Ah! Kuna meseji hapa imenishangaza sana.
"Sasa meseji ikushangaze wewe halafu kusema useme na sisi, wewe vipi bwana?!
"Kaka we acha tu.
***
Gari la kusafirishia mwili wa marehemu lilifika, watu tukatangaziwa kwamba, kwa vile gari hilo ni dogo, watakwenda watu wa karibu zaidi na marehemu. Mtangazaji akaanza kutaja majina ya watakaosafiri.
Nilitega sikio kusikiliza jina la Munil lakini matokeo yake nikasikia jina la kaka. Nikamtumia meseji.
We huendi baby?
Akajibu:
"Nakwenda."
"Mbona sijasikia jina lako."
"Limeitwa mbona baby."
"Limeitwaje?"
"Si Munil. Tena wamesema Munil Rashid Sultan el Said."
Moyo ulinikatalia kwamba jina hilo halijatajwa lakini pia nikasema moyoni kwamba, kama lilitajwa kweli nitamuona kwenye kuingia kwenye basi hilo la Coaster.
Watu walikunywa chai, maiti ikafuatwa hospitalini, watu wakajipanga kwa safari. Nilikuwa mbele sana ili nimuone Munil akiingia kwenye basi lakini mpaka mtu wa mwisho anapanda sikumuona.
Palepale nikamtumia meseji kumuuliza:
"Mbona sijakuona ukipanda kwenye basi baby?"
Nilisimama jirani na dirisha, nikashtuka kuguswa kichwani. Nilipoangalia, alikuwa Munil:
"Vipi?" aliniuliza.
"Poa, sikukuona."
Tukaagana akaondoka zake. Dakika tano mbele baada ya basi kuondoka, kaka akanitumia meseji:
"Huyu dada uliyesemezana naye ni nani?"
Nikamwambia ndiyo yule aliyenipa taarifa za msiba. Kaka akaguna tu! Mh!
Saa sita mchana, kaka akanitumia meseji akaniuliza hivi:
"Unakumbuka yule dada alivaa nguo gani?"
Nikamjibu gauni jeusi. Akasema hata mimi nilimuona hivyo lakini nashangaa hapa namuona amevaa jekundu sijui amebadilishia wapi wakati basi halijasimama popote! Na mimi nikaguna tu!
***
Usiku wa siku hiyo, nilikuwa kwenye baa moja napata bia mbili tatu kabla ya kwenda kulala. Meseji ikaingia kwenye simu yangu, ilitoka kwa Munil na aliiandika hivi:
"Mimi sipendi tabia yako ya kukaa baa usiku kama huu."
Nilipomaliza kuisoma niliangalia kulia na kushoto nikiamini nitamuona. Nilishtuka kwamba amesafiri nikamuuliza:
"Umejuaje niko baa?"
"Nimeambiwa na mtu."
Hapo pia nikawa na utata napo, nani amwambie mimi niko baa wakati hakuna mtu hata mmoja anayejua kama mimi na yeye tuna ukaribu au ni wapenzi?
Munil, kuna mtu anajua mimi na wewe ni wapenzi mapema hii? nilimuuliza kwenye meseji, naye akajibu hivi:
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wengi mbona, hata rafiki yako Saleh wa kioski cha stendi anajua.
Palepale nilichukua simu na kumpigia Saleh.
"Sema ndugu yangu," Saleh alisema baada ya kupokea simu yangu.
"Eti Saleh, wewe unajua kwamba nina msichana anaitwa Munil ni mpenzi wangu?
Aaa! Munil yule msichana mweupe mzuri sana?
Huyohuyo ndiyo.
Najua.
"Ulijuaje?"
"Si juzi kama sikosei ulikaa naye pale baa!"
"Kwani uliniona?"
"Nilikuona nikakupigia simu lakini sikukupata."
"Kwani Saleh, yule msichana anaishi wapi?"
"Kule mitaa ya juu jirani na kwako tena."
"Kwa nani?"
"Sijui ni kwa nani!"
"Unamjua siku nyingi?"
"Sana tu."
Nilikata simu lakini huku nikiwa najiuliza bado kwamba ni kweli Munil ni msichana anayejulikana na Saleh kwa muda mrefu bila mimi kujua?
Niliazimia kwenda kwa Saleh kwenye kioski chake ili kumuuliza kwa mapana na pia kumsimulia hali fulani ambayo mimi naitilia shaka akilini mwangu.
**************
Ilikuwa saa kumi na mbili jioni ambapo nilitoka kuwasiliana na Munil nikaenda kwa Saleh. Nilimkuta akaachia tabasamu nikajua anataka kuanza kuniambia kuhusu Munil.
Lakini kabla hajasema chochote, mteja mmoja alifika na kutaka huduma. Alipotoka mteja huyo
akaja mwingine, akaja mwingine na mwingine mwishowe mimi nikaamua kuondoka maana nilikuwa na safari nyingine.
Basi nitakupigia ili kuongea na wewe, aliniambia Saleh wakati namuaga.
Niliondoka na akili kwamba, ni kweli Saleh anamjua vizuri Munil kwa jinsi alivyoanza kusema naye.
***
Usiku wa saa mbili, nilikuwa nimekaa kwenye baa moja napata bia mbili tatu huku nikitaka kuwasiliana na Munil kuhusu msiba na mazishi kwa ujumla.
Kabla sijampigia au kumtumia meseji, Munil akanitumia meseji yeye
Naamini wewe pia upo kwenye wazo la kunitumia meseji lakini nimekuwahi. Je, mzima mpenzi wangu?
Nilishtuka sana kusoma ujumbe huo wa Munil maana sikuutegemea hata kidogo. Nikamjibu niko poa mpenzi sijui wewe, naye akanijibu:
Mimi mzima ila sipendi tabia yako ya kukaa baa mpenzi wangu.
Nikamjibu:
"Leo sijakaa baa mpenzi labda jana."
"He! Yaani unanidanganya hata mimi?"
Sikudanganyi mpenzi wangu niko nyumbani, kama unaweza kuruka angani ruka uje. Mimi nasema niko nyumbani hapa nakunywa soda tu.
Sawa mume wangu lakini kuna siku utajua nini maana ya kauli yangu. Niko makini sana na watu wanaojua uhusiano wetu, kama vile Saleh. Wewe si ulikwenda kwa Saleh amesemaje?
Nilishtuka kuisoma meseji hiyo kwani sikuitegemea kwa maana kwamba, imekuaje Saleh akamwambia Munil kwamba mimi nilikwenda kwake baada ya kuzungumza naye kuhusu yeye? Sikupenda kwa kweli!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimtumia meseji Saleh nikiwa nimeiandika hivi:
"Saleh na wewe, kwani ilikuwa lazima umwambie Munil kwamba niliongea na wewe na nilikuja kwako leo?
Meseji ile mpaka leo nikiikumbuka bado nasema ndani ya utawala wa viumbe wa ajabu kuna
ufahamu wa hali ya juu sana. Wakati nimetuma meseji hiyo, ile bado inasachi pa kwenda, Saleh alishaipokea na kunijibu hivi:
"Kwani tatizo liko wapi ndugu yangu?"
Wakati meseji inasema imedeliva kwa Saleh, mimi nilikuwa naandika meseji ya pili ya kumwambia sijapenda, lakini kabla sijaituma ikaingia meseji ya Saleh ya kujibu hiyo akiniuliza, hujapenda nini sasa ndugu yangu?
Hebu fikiria hapo. Lakini naomba ijulikane kwamba kumbe Saleh huyo hakuwa Saleh ninayejuana naye mimi licha ya kwamba kweli nilimkuta kwenye kioski chake. Hapo mbele nitasimulia ilivyokuwa ndiyo maana nasema mke wangu alikuwa nusu jini nusu mtu.
Basi, kwa wakati huo nilipoona Saleh anajibu meseji zangu hata kabla sijamtumia au ikiwa yangu bado inasachi niliamua kuachana naye nikiamini labda ni tatizo la mtandao.
***
Baada ya siku mbili, Munil alirudi Kibaha, kaka pia alirudi. Walifika jioni ya saa kumi na moja. Kaka akanitumia meseji kuniambia nifanye nifanyavyo lazima nikutane naye siku hiyo. Ile namalizia kusoma meseji ya kaka, meseji ya Munil nayo ikaingia, akitaka kuonana na mimi kabla jua halijachwa!
Sawa kwa nini wametuma meseji wote kwa muda huohuo kama wapo pamoja? nilijiuliza.
Mara ikaingia meseji nyingine ya Munil akisema: Najua utakuwa una ahadi ya kukutana na watu au mtu lakini ukimalizana naye niambie ili utakapokuwa nije nikuone, iwe nyumbani kwako au popote pengine.
Nilimjibu poa mke wangu. Baadaye nikaenda kukutana na kaka nyumbani kwake. Alinikaribisha huku akiniangalia sana siku hiyo kuliko siku nyingine yoyote.
Baada ya salamu kaka alikaa kimya kidogo kisha akaanza kwa kusema:
"Mdogo wangu, nataka kukuuliza swali moja tu!"
"Niulize kaka."
Mara ikaingia meseji ya Munil, kaka akaniambia soma kwanza hiyo meseji.
"Nukuu ya leo: Ukitaka kujibu maswali ya mwenye kiu, fikiria kwanza ndipo ujibu ili kuepuka kumpoteza."
Nilishtuka lakini bila kumuonesha kaka kwamba nimeshtuka. Meseji hiyo ya Munil ilionesha kwamba alijua nakutana na kaka ndiyo maana akafanya vile. Nilipomaliza kuisoma, nikamwangalia kaka kwa macho ya endelea nakusikiliza.
"Umemaliza?" aliniuliza kaka.
"Ndiyo."
"Enhe? Nilitaka kukuuliza mdogo wangu, yule msichana ni nani kwako?"
"Yupi?"
"Niliyesafiri naye msibani."
"Kaka kama nilivyokwambia, kukutana naye kwa mara ya kwanza ni siku ile ya kutoa mahari kaka. Baada ya pale akaja kunipigia simu ya kunijulisha kifo cha mchumba wa binti yetu."
"Oke, hujaulizia ni nani?"
"Hapana kaka."
"Kweli?"
"Kweli kaka."
"Sasa cha kushangaza mdogo wangu, mimi niliwauliza ndugu kule msibani wanasema yule binti wao hawamjui na wala hawajawahi kumuona.
"Niliwauliza ni kwa nini ameambatana na wao msibani mbali vile wakasema hawajui na hakuna aliyemuuliza. Cha ajabu baada ya mazishi usiku, nilimuota vibaya. Nilimuota amesimama mbele yangu akiwa amenishikia kisu akitaka kunichoma nacho."
"Kweli kaka?"
"Kabisa kabisa. Nikamuuliza kwa nini unataka kunichoma kwa kisu? Akajibu anataka kuniua kwa sababu mimi ni kikwazo katika maisha yake, nikamuuliza sikufahamu, nakuwaje kikwazo katika maisha yako? Akakasirika na kunifuata na kisu nikashtuka kwa kupiga kelele."
"Mh! Kaka bwana, naamini ni ndoto tu kwa sababu wewe mwenyewe umekuwa ukimweka akilini kwa muda mrefu."
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hata kama, mimi nilichotaka kukwambia…"
Kaka alitaka kuniambia kitu lakini akajishika koo ghafla huku akisema anahisi kama kuna vumbi ndani ya koo lake.
"Ni nini tena?"
"Sijui," alijibu kaka.
Hali ya kaka ilizidi kuwa mbaya sana, akawa hawezi kusema wala kuniangalia. Alikuwa amefumba macho.
"Kaka," nilimuita.
Nilimfuata shemeji nikamwambia, akaja mbio akaniuliza ni nini?
"Sijui shemeji, ni ghafla tu."
"Tumkimbize hospitali," alisema shemeji.
Kwa kuwa nilikuwa nina namba ya simu ya dereva teksi mmoja aliyekuwa rafiki yangu, nilimpigia simu ili aje pale nyumbani haraka lakini sikumpata hewani.
Nilikimbia kuchukua gari, bahati nzuri ile naingia barabara kuu nikaliona gari dogo nikalisimamisha na kukubaliana bei kisha tulikwenda nyumbani, tukampakia kaka na kumkimbiza Hospitali ya Tumbi lakini tukiwa njiani alikata roho tena akiwa mikononi mwangu.
Ilikuwa pigo kubwa sana kwetu, kwangu na kwa familia maana kaka ndiye aliyeniita Kibaha na kuishi kwake baadaye nikaanza kupanga chumba changu, polepole nikajijenga hadi kufungua gereji yangu mwenyewe.
Tuliufikisha mwili wa marehemu hospitali kwa ajili ya kuuhifadhi, nilipotoka tu Munil alinipigia simu.
"Haloo," aliita kwa sauti ya upole tofauti na siku zote.
"Haloo, Munil."
"E! Pole na msiba, nimepata taarifa kaka yako amefariki dunia."
"Kweli Munil, kaka amefariki dunia." Palepale nilianza kulia.
"Da! Ilikuwaje?"
Nilimsimulia ilivyokuwa, ikafika mahali Munil naye akaanza kulia akisema anamkumbuka walivyosafiri wote kwenda msibani. Akasema alitamani sana kumzoea kama shemeji lakini ilishindikana. Tukaungana wote katika kilio cha kifo cha kaka.
"Sasa mipango ya mazishi ikoje?" aliniuliza Munil.
"Sijajua, mpaka nifike kwake na kukaa na familia nzima ndiyo nitajua."
"Oke basi utaniambia mume wangu, pole sana," alisema Munil na kukata simu.
Alipokata simu tu, palepale akili ikanijia kwamba, Munil aliambiwa na nani kwamba kaka yangu alifariki dunia wakati kafia mikononi mwangu na sikuwa nimempigia simu mtu mwingine yeyote yule kumjulisha kuhusu kifo hicho cha ghafla.
Nilijikuta nampigia simu ili kumuuliza nani alimwambia kama kaka amefariki dunia!
"Haloo mke wangu unajua umenishangaza sana tena sana?" nilimuuliza Munil alipopokea simu yangu.
"Kukushangaza nini mume wangu?" Munil aliniuliza.
Aliponieleza hivyo, nilimuuliza ni nani alimpa taarifa za kifo cha kaka yangu wakati alipokata roho tulikuwa mimi na shemeji na hakuna kati yetu aliyempigia simu mtu yeyote kumfahamisha juu ya msiba huo.
Nilijikuta nampigia simu ili kumuuliza nani alimwambia kama kaka amefariki dunia.
Lakini cha kushangaza sasa, badala ya kumuuliza nani alimwambiwa habari zile nikamuuliza kama atakuja msibani.
Ndiyo niko njiani nakuja, alinijibu Munil, nikamwambia sawa kisha nikakata simu.
Lakini akili nyingine ikaniuliza kwamba, Munil amesema anakuja, anakuja wapi sasa! Maana sikumwambia kama tupo Tumbi. Ilibidi nimpigie simu tena.
"Umesema unakuja?" nilimuuliza.
"Ndiyo."
"Wapi?"
"Si mpo Tumbi Hospitali?"
"Ndiyo, nilikubali nikakata simu."
Lakini pia akili ikaniuliza Munil alijuaje kuwa tupo Tumbi? Nilijiuliza sana kuhusu Munil, ni mwanamke wa aina gani. Anaweza kuwa jini? Lakini hapo nilipingana napo kwani wanasemaga ukikutana na jini
unaweza kuugua au kufa ghafla, sasa yeye ni jini gani hadi nalala naye, naongea naye, anajichanganya na watu wengine kama kawaida na anaishi mtaani.
Wakati nawaza hayo, yale mazungumzo yangu na kaka yalinirudia kichwani yakiwa hivi:
"Enhe? Nilitaka kukuuliza mdogo wangu, yule msichana ni nani kwako?
"Yupi?"
"Niliyesafiri naye msibani."
"Kaka kama nilivyokwambia, kukutana naye kwa mara ya kwanza ni siku ile ya kutoa mahari kaka. Baada ya pale akaja kunipigia simu ya kunijulisha kifo cha mchumba wa binti yetu."
"Oke, hujaulizia ni nani?"
"Hapana kaka."
"Kweli?"
"Kweli kaka."
"Sasa cha kushangaza mdogo wangu, mimi niliwauliza ndugu kule msibani wanasema yule binti wao hawamjui na wala hawajawahi kumuona.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Niliwauliza ni kwa nini ameambatana na wao msibani mbali vile wakasema hawajui na hakuna aliyemuuliza. Cha ajabu baada ya mazishi usiku, nilimuota vibaya. Nilimuota amesimama mbele yangu akiwa amenishikia kisu akitaka kunichoma nacho."
"Kweli kaka?"
"Kabisa kabisa. Nikamuuliza kwa nini unataka kunichoma kwa kisu? Akajibu anataka kuniua kwa sababu mimi ni kikwazo katika maisha yake, nikamuuliza sikufahamu, nakuwaje kikwazo katika maisha yako? Akakasirika na kunifuata na kisu nikashtuka kwa kupiga kelele."
"Mh! Kaka bwana, naamini ni ndoto tu kwa sababu wewe mwenyewe umekuwa ukimweka akilini kwa muda mrefu."
"Hata kama, mimi nilichotaka kukwambia."
Mazungumzo yale yalipofikia hapo, nilishtuka kama vile nilikuwa naota na tayari mwili ulishahifadhiwa mochwari baada ya madaktari kuthibitisha kwamba kweli alifariki dunia, nikatoka sasa ili kukutana na shemeji ambaye muda wote alikuwa akilia sana mahali.
Nilimchukua shemeji hadi nyumbani kwa kaka. Nikakumbuka kwamba, Munil alisema anakuja hospitali na sijamwambia kwamba tunakwenda nyumbani. Nilitoa simu ili kumpigia nimjulishe maana hata kwa kaka napo, watu walishaanza kujaa wakishangaa kilichotokea, hasa majirani.
Ghafla nilimuona Munil akiwasili akiwa ndani ya teksi. Alishuka akaja na kunikumbatia kisha akalia sana kwenye kifua changu. Teksi ilimsubiri.
Siku hiyo alivaa kama baibui na kichwani alijifunga kitambaa cheusi na miwani ya jua usoni. Alipendeza, pia alivutia sana machoni kwa kumtazama tu.
Baada ya pole nyingi, Munil alizama ndani kwa akina mama. Lakini akaniachia maswali. Kwamba, alijuaje tupo kwa kaka? Oke, labda alituona njiani kwenye gari wakati yeye akienda Tumbi. Je, alipajueje nyumbani kwa kaka?
Kusema ukweli maswali kuhusu Munil nilikuwa nayo mengi sana lakini sikujua kwa nini nilikuwa nayapuuza kuyafuatilia kwa karibu.Kwa kaka kulikuwa na msiba sasa na niliwajulisha ndugu zangu wote nilioweza. Kazi ikawa moja kuusimamia msiba kwa maana ya chakula kwani hata kama kaka alikuwa na pesa benki isingekuwa rahisi kuzitoa haraka na pia nilishindwa kumuita shemeji pembeni kumuuliza chochote kuhusu fedha kwani alikuwa hajitambui.
Cha ajabu sasa, nikiwa nawaza hivyo, Munil alinitumia meseji akisema tutoke nje tuongee mara moja, nikamwambia poa.Nilitangulia mimi kutoka, akafuata. Tulisimama chini ya mti mmoja wa jirani.
"Najua mambo yaliyotokea ni ya ghafla sana naamini hamjajipanga kifedha. Sasa mimi nakwenda kuchukua pesa narudi muda si mrefu."
"Da! Nashukuru sana Munil mke wangu, sijui ulijuaje?!"
"Mbona ni suala liko wazi mume wangu, jambo lolote zito la ghafla watu huwa hawana pesa mfukoni," alisema Munil huku akienda kwenye teksi aliyokuja nayo.
Nilijiuliza sana, Munil anafuata pesa hizo wapi? Benki, nyumbani kwake au kwa mtu? Pia nikajiuliza kwani anafanya kazi gani mpaka awe na pesa za kukaa mahali. Pia nikajiuliza sijui anakwenda kuleta kiasi gani cha pesa? Moyoni nilisema akija na shilingi laki tano tu zitatosha kwa kubana matumizi.
Baada ya nusu saa, Munil alirudi, akashuka kwenye teksi akiwa ameshika mfuko wa karatasi ulioshiba vizuri. Aliniita palepale chini ya mti, akanikabidhi kisha yeye akaenda ndani na teksi ikaondoka.
Ghafla, akili yangu ikaniambia niangalie namba za ile teksi, nikashtuka. Tofauti na mazoea ya namba zetu nchini, zenyewe ziliandikwa JIN 000 KIF!
Nilishangaa sana kiasi kwamba nilikazia macho ile teksi mpaka ilipotoweka kabisa. Nikaenda nyuma ya nyumba ya kaka ambako hakuna watu, nikafungua mfuko na kuangalia zile pesa! Zilikuwa noti mpyaaa!
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikaa mahali na kuanza kuzihesabu moja baada ya nyingine kwa muda mrefu, nikapata shilingi milioni tatu na laki tano! Kwanza niliangalia kulia na kushoto nikiwa siamini macho na akili zangu.
"Hivi huyu Munil amezipata wapi hizi pesa zote? Tena mpya! Kwanza anafanya kazi gani?" nilijiuliza moyoni. Ghafla nikasikia harufu ya manukato anayojipulizia Munil nikashtuka kuangalia nyuma usawa ambao mtu anaweza kutokea, sikumuona Munil wala dalili ya mtu kuja eneo lile. Nikasimama, ile harufu ya manukato ikazidi kukolea.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment