IMEANDIKWA NA : SADARI KISESA
*********************************************************************************
Simulizi : Karibu Kuzimu
Sehemu Ya Kwanza (1)
UTANGULIZI...
“Katika maisha kuna kupata na kukosa. Basi usipende kutamani cha mtu vitatokea puani, Prisca alitamani. Tamaa ikamkamata akatamani maisha ya watu hatma akaambulia mateso, nini uteseke kwa ajili ya utajiri wa mtu angali ni mzima na una nguvu. Tafuta kwa jasho na usijaribu kukata tamaa kisa huyu anasema hiki, yule anasema kile. Jikwamue Mungu si Athuman, Mungu ni wa pekee jicho lake likutazamapo mwanga wa milele ung'aza katika maisha yako. Tenda walau siku moja ujitoe, maisha yako mkabidhi Mungu uone maisha yako yatakavyotendeka. Daima chochote hakitashindikana kwa Mungu mpe nafasi katika maisha yako ili akupe kalama duniani na mbinguni.
SONGA NAYO...
“Ilikuwa Jumamosi tulivu ni jioni katika barabara ya Mandela. Kituo cha daladala cha Mabibo hostel, anaonekana binti mmoja pembezoni mwa kituo cha daladala. Kachafuka na vumbi, macho yake yanaonekana kububujikwa na machozi halafu hasiweze kuyafuta. Mkono wake wa kulia anaonekana kupungia kila gari lipitalo lakini anagonga mwamba kusimamisha magari, bahati nzuri akatokea msamaria mwema wa kiume akapaki gari pembeni ya kituo cha daladala. Akashuka kumfuata binti yule ili azungumze nae.
“Binti, unakwenda wapi?,” Msamaria yule akauliza mara baada ya kumfikia yule binti.
“Naelekea Ubungo,” Binti yule nae akajibu swali aliloulizwa huku akiangalia chini kwa aibu akiogopa kwa jinsi alivyochafuka.
“Ubungo, ndipo unapoishi?” alizidi kudadisi yule msamaria mwema. Ili aone anzie wapi kumsaidia yule binti.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ubungo sio ninapoishi. Ubungo nakwenda katika kituo cha mabasi ya mkoa.”
“Oooh, lakini sasa mbona unalia halafu umechafuka?.”
“Kaka, ni stori ndefu.”
“Naona.... Ehe, unaitwa nani?.”
“Prisca,” Binti yule akajitambulisha kwa kifupi kana kwamba amechoshwa na maswali ya msamaria. Kilio akakiongezea maradufu.
”Prisca, sasa acha kulia,” Msamaria yule alisema huku akijaribu kupeleka mkono wake wa kuume kwenye shavu la Prisca, akasaidia kumfuta machozi Prisca kisha akaendeleza maongezi.
“Inaonekana, umepitia shida sana?,” Msamaria akauliza.
“Hakika, yaani mpaka nafika hapa ni lazima nimshukuru Mungu,” Prisca akajibu huku safari hii akijilazimisha kidogo kutabasamu, tabasamu lake hafifu likaonekana machoni mwa yule msamaria angalau msamaria akapata matumaini.
“Nitakusaidia...ila Ubungo katika kituo cha mabasi ya mkoa ulitaka kwenda kufanya nini?,” Msamaria akahoji.
“Nilitaka, nirudi nyumbani,” Prisca akajibu kisha akamkazia macho ya kudadisi yule msamaria. Ili ajue yule kijana alikuwa askari mpelelezi au lah maana si kwa maswali yale, anahoji kana kwamba anamhoji muuaji.
“Kwani nyumbani, ni wapi?,” Msamaria akazidi kudadisi maana akugutuka kama Prisca anafikiria nini moyoni mwake.
“Tanga.”
“Basi usirudi, maisha ya kijijini ni magumu sana. Mimi nitakusaidia ila nataka tukifika nyumbani unipe stori ya maisha yako. Nikufahamu zaidi.”
“Sawa. Nashukuru kwa msaada,” Prisca aliongea huku akijifunga vizuri kiremba kichwani kisiweze kuanguka.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Msamaria hakuhoji tena, wakaongozana na Prisca mpaka kwenye gari lake aina ya TOYOTA BMW wakapanda wakaondoka. Ndani ya lisaa wakawasili nyumbani wakafunguliwa geti na mlinzi hatimaye wakaingia ndani na gari, waliposhuka msamaria yule akamtambulisha Prisca kwa mlinzi wapate kujuana.
“Ngodongwe,” Msamaria yule akaita.
“Naam, Sir,” Ngodongwe akaitika kwa tahadhima.
“Nimekuita nikutambulishe mgeni.... Prisca huyu ni mlinzi hapa nyumbani anaitwa Ngodongwe” alitambulisha msamaria yule mara baada ya kuona wao na Ngodongwe wako pua na mdomo.
”Nashukuru kumfahamu” alishukuru Prisca kwa sauti ya upole.
“Ngodongwe, huyu anaitwa Prisca tutakuwa naye hapa nyumbani,” Msamaria yule akaendelea sasa na utambulisho. Wakati huu sasa akamtambulisha mlinzi.
“Sawa, Sir. Emmanuel.... Dada karibu sana jisikie upo nyumbani,” Ngodongwe akakaribisha.
“Asante,” Prisca akashukuru kwa dhati. Kwa ajili ya Mungu kumkutanisha na binadamu wema maana hakutaraji.
Utambulisho ukaisha Prisca na Emmanuel wakaelekea ndani, wakamuacha mlinzi nje akiendelea na windo. Kabla ya kufika ndani wakiwa wamesimama kwanza katika mlango wakuingilia sebuleni, Prisca akachombeza kautani kidogo.
“Kumbe, una jina zuri” aliongea Prisca kwa sauti ya chini kana kwamba ananong'ona.
“Mbona, hata lako zuri” alisema Emmanuel huku akionyesha kutabasamu kana kwamba amefurahia ujio wa mgeni.
“Mh, nashukuru,” Prisca alisema kisha yeye na mwenyeji wake kwa pamoja wakaingia ndani.
Prisca sababu alichafuka basi walipoingia ndani akaona aibu kuketi sofani akaketi sakafuni. Emmanuel alipoona mgeni kaketi sakafuni akacheka akasikitika kidogo kisha akamnyanyua Prisca akamkalisha sofani.
“Prisca, sofa zipo. Kwanini unakaa chini?,” Emmanuel akauliza kwa upole kabisa.
“Kaka, mie mchafu sistahili kukaa kwenye sofa zuri kama hili. Nitachafua,” Prisca akajibu kinyonge kiwango cha chini.
“Wewe kaa. Dada yupo atasafisha.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mh, lakini....”
“Lakini nini, nimekuambia kaa.”
Prisca akapokea ruhusa ya mwenyeji sasa ikambidi aketi sofani, akaketi lakini macho yote yakawa bize kutazama nyumba ile ilivyo nzuri. Akashangaa kwa kuduwaa mno mpaka akaja kushtushwa na swali la mwenyeji wake lililoulizwa zaidi ya mara tatu bila ya yeye kusikia.
“Prisca, unatumia kinywaji gani?,” Hilo ndilo swali lililokuwa likiulizwa na Emmanuel na ndilo swali lililomshtua Prisca wakati alipozama kwenye mshangao.
“Juisi itanitosha” alijibu Prisca kwa uchangamfu mara baada ya kushtushwa ghafla.
“Lakini umechukua muda kujibu, kuna tatizo?,” Emmanuel akauliza.
“Hamna, nipo sawa,” Prisca alijibu huku akikaa vema sofani. Akihofia ganzi isije kumkamata katika viungo vya mwili kwa ajili ya kuketi kwa muda mrefu sehemu moja.
“Basi ni sawa,” Emmanuel alisema, hatimaye akanyanyuka sofani akafuata glasi mbili pamoja na juisi sehemu husika.
Emmanuel ndani ya dakika kadhaa akarudi akiwa mkononi kashikilia glasi mbili za kioo zenye juisi ya Embe ndani yake. Alipofika jirani na Prisca akakabidhi glasi moja ya juisi kwa Prisca na kisha nae akaketi sofani tena, wakanywa juisi taratibu huku wakiendelea polepole na maongezi yao ya hadhira. Dakika kumi wote wakamaliza kunywa juisi Emmanuel akamuita dada aje kutoa glasi, haikupita nusu saa dada akawasili akachukua kile alichoitiwa mwishowe akata kuondoka. Lakini kabla ajafika kokote akaitwa tena na Emmanuel akatii wito akarudi kumsikiliza bosi.
“Jesca,” Emmanuel ikamlazimu kuita tena mara baada ya Jesca kurudi tena kwa mara ya pili. Ili kumhakikishia Jesca alikuwa anamuita yeye.
“Abeeh,” Jesca akaitika kitiifu. Kwa kumheshimu bosi pamoja na kazi yake.
“Nataka kukutambulisha kwa mgeni.... Mgeni huyu anaitwa Prisca tutakuwa nae hapa nyumbani,” Emmanuel akatambulisha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimeelewa, bosi,” Jesca akajibu kwa furaha na kinyenyekevu, kwa ajili ya kumuunga mkono bosi wake asijione kafanya makosa kumleta Prisca nyumbani.
“Prisca, huyu ni dada wa kazi hapa nyumbani. Anaitwa Jesca,” Emmanuel pia akamtambulisha Prisca kwa uweledi ili kati yao wafahamiane.
“Nashukuru kumfahamu,” Prisca alijibu huku akilionyesha tabasamu lake wazi kila mtu alione.
“Jesca, unaweza kwenda,” Emmanuel alitoa ruhusa mara baada ya utambulisho kuisha. Na bila kupoteza wasaa Jesca akaondoka nyuma akamuacha Emmanuel na Prisca wakiendelea kupiga soga binafsi.
“Eehe. Prisca, sasa simulia stori ya maisha yako” aliongea Emmanuel mara baada ya kuthibisha Jesca tayari kashaondoka machoni mwao.
“Nitasimulia.... Lakini wewe una muda wa kutosha?,” Prisca akauliza.
“Kwa sasa muda ninao, wewe simulia nitakusikiliza.”
“Sawa,” Prisca alikubaliana na Emmanuel kwanza akakohoa kwa kubanja kikohozi hafifu kisha ndipo akaianza kusimulia stori ya maisha yake iliyomfanya aonekane rafu leo.
“Ni mmoja wa watoto wa mwisho na watatu katika familia ya Mzee Mahonge na Binti Binge huko mkoani Tanga Muheza, wazazi wakanipenda sana lakini nikaja kuondoa upendo pale pindi nilipokataa kuolewa na mwanaume wampendao. Wakanilazimisha mno hatimaye wakatishia kuniachia hadi laana yote kwa ajili mie nikubali, usumbufu ukazidi kila kukicha wakiamka ikawa nyimbo hiyo hiyo ya kunishawishi niolewe na huyo mwanaume. Siku moja majira ya alfajiri nikaondoa kero nikatoroka kuja Dar es salaam kabla ya wazazi kuamka, nikapanga nifikie kwa Dada mkubwa ambaye ni wa kwanza kuzaliwa kwetu. Siku hiyo nikafungasha changu kisha nikaongoza moja kwa moja katika kituo cha mabasi kutafuta usafiri uelekeao Dar es salaam kabla hakujapambazuka, sababu sikuwa na nauli ya kutosha ikanibidi niombe lifti tu nilipofika pale kituoni. Mkosi ukaniandama siku hiyo maana kila gari niombalo lilikuwa linapita bila kusimama, huku madereva wakinionyesha ishara ya kujaza, sikukata tamaa nikajipa moyo kuwa nivumilie nikavumilia ndipo kama lisaa hivi nikaona gari aina ya FUSO lililobeba ndizi likiegesha kando ya kituo cha mabasi nilichopo. Hapo nikashusha pumzi nikajisemea moyoni.
“Nikizubaa itakula kwangu Fuso hili liking'oka tu ninalo, siwezi kukubali liniache.... Ukiangalia kuna karibia kupambazuka kukipambazuka tu sitoweza tena kupata hii nafasi.”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati najisemesha kwa mbali nikamsikia dereva wa fuso lile akimuamuru utingo kuwa apande haraka waondoke, papo hapo nami nikachukua nafasi ya kudandia lile gari kisiri haraka kabla halijaondoka. Nikajisweka kwenye mizigo ya ndizi bila ya wao kujua, gari lilipofika maeneo ya Mbezi mwili ukahisi kusisimka pindi gari liliposimama na mtu kushuka. Mtu yule aliposhuka nikasikia vishindo vya miguu vikija nilipo ili ajisaidia haja ndogo, moyo wangu ulikwenda mbio yule mtu alipofika nilipo na kuanza kujisaidia kwenye taili za nyuma huku jicho lake akikodoa kwenye mizigo ya ndizi kana kwamba ananikodolea mie. Nikazidi kujisweka kwenye gunia za ndizi nisipate kuonekana na yule jamaa, Mungu mkubwa nikashusha pumzi ndefu nilipoona yule jamaa baada ya kujisaidia amefunga komeo ya suruali na kurudi ndani ya gari waendelee na safari. Dakika si nyingi gari likawashwa tukaendelea na safari.
“Dah, Bwana Mgata safari yetu ya leo neema.... Mpaka tumefika Mbezi atujapata misukosuko nahisi leo basi hata sokoni kutakuwa shwari.”
“Kwanini, umesema hayo. Bwana Juma?.”
“Maana sio kawaida, kufika eneo hili bila kupata tatizo lolote.”
“Kweli, ila ni jambo la kumshukuru Mungu maana yeye ndiye mpangaji wa kila kitu,” Nikasikia maongezi ambayo yaliyokuwa yakiongelewa ndani ya gari baina ya dereva na utingo.
Saa mbili ya asubuhi gari likawasili Mabibo sokoni almaarufu kwa jina la MAHAKAMA YA NDIZI. Nikanyata sasa nitelemke kwenye gari ghafla nikasikia mtu anashuka ndani ya gari, kisha nikasikia vishindo vyake vya miguu vikija nilipo. Mwili wangu wote ukaisha nguvu kwa kujua nitaonekana na kupigiwa kelele za mwizi, lakini mara nikajikuta nikishusha pumzi ndefu pindi tu niliposikia yule mtu aliyekuwa akija kwangu anaitwa. Upesi nikashuka kwenye lile fuso nikapiga hatua kadhaa nikitoka kwenye lango kuu la soko, nilipotoka nje ya soko nikashangaa sana yote sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia katika jiji la Dar es salaam. Nikashangaa shangaa kwa muda hatimaye nikajikongoja taratibu huku zigo langu la begi likiwa kichwani likinimenya, nikafuata barabara kuu upande wangu wa mkono wa kuume kisha nikavuka ng'ambo polepole nikatembea kuelekea nisipopajua. Bahati nikamuona dada mmoja ambaye kiumri amenizidi kwa makadirio hata kuwa na miaka 30 au 32, nikaona akiuza njugu kando ya barabara nikamfuata nikamsalimu.
“Habari yako. Dada,” Nikamsalimu yule dada kwa ucheshi.
“Salama...nikuuzie karanga?,” Dada yule aliitika salamu kisha akaniuliza swali akijua nahitaji kumuungisha njugu.
“Hapana dada, nahitaji kuuliza tu.”
“Uliza.”
“Eti, huku ni wapi?,” Nikauliza huku nikionyesha kidole kule nielekeapo. Nikimuonyesha yule dada kama anapajua.
“Ooh, huku ni Mabibo mwisho.... Kwani wewe mgeni?,” Dada yule aliniuliza mara baada ya kugundua maelekezo yangu yanaonyesha kuwa mgeni wa jiji la Dar es salaam.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
”Ndiyo,” Nikamjibu.
“Kwani, unahitaji kwenda wapi?.”
“Nahitaji kwenda, sehemu moja inaitwa Kigogo Luhanga.”
“Oooh!!!, kama unakwenda Kigogo Luhanga fuatisha barabara hii moja kwa moja ukifika Mabibo mwisho. Hapo ndipo kuna daladala zinazoelekea Kigogo panda hizo daladala kisha mwambie Kondakta akushushe Luhanga,” Dada yule alinielekeza kwa uweledi fasaha.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa dada.... Asante,” Nikaongea. Nikamuaga yule dada kisha taratibu nikaendelea na safari, nikiwa bado njiani nikakumbuka maelekezo ya yule dada nikatabasamu kidogo.
“Oooh!!!, kama unakwenda Kigogo Luhanga fuatisha barabara hii moja kwa moja ukifika Mabibo mwisho. Hapo ndipo kuna daladala zinazoelekea Kigogo panda hizo daladala kisha mwambie Kondakta akushushe Luhanga,” Angejua kama nina pesa ya ngama asingesema nipande daladala, maana nimechalala hadi najionea mwenyewe uso wa aibu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment