Search This Blog

KARIBU KUZIMU - 5

  





    Simulizi : Karibu Kuzimu

    Sehemu Ya Tano (5)





    Jini Suleiman akiwa amelala chumbani, huku nami nikiwa sebuleni nikiangalia runinga bila uwoga. Ghafla nikasikia mlango wa sebuleni ukigongwa, nikanyanyuka katika sofa kwa hofu nikaenda kufungua mlango. Ile kufungua nikakuta mgongaji hayupo, nikajipa moyo labda wenge langu sikusikia vizuri. Nikafunga mlango nikarudi tena kutazama runinga, kama nusu saa nikiwa makini na kutazama runinga mara nikasikia tena mlango ukigongwa. Sikusita kwenda kufungua, nikaelekea kufungua mlango lakini nilipofungua ikawa vile http://deusdeditmahunda.blogspot.com/vile kama awali. Sikumkuta mgongaji basi nikajisemea labda atakuwa ni jini Suleiman anafanya mauza uza pengine kwa kuniondoa upweke, hivyo nikafunga mlango huku kwa mbali nikilionyesha tabasamu langu. Nikaelekea chumbani nikamfuata Suleiman ili nimueleze huo mchezo alioanzisha sijapenda. Lakini kabla sijafika chumbani ile napiga hatua mbili tatu za kuelekea chumbani, nyuma yangu nikasikia kama mtu akitembea akinifuata. Haraka nikageuka nikashtuka, mapigo ya moyo yakaenda kasi. Maana nilichokiona niliogopa, sikuona mtu bali nikaona nyayo za binadamu zilizo na damu ambazo zimeanzia niliposimama mpaka sebuleni. Pima macho yakanitoka, nguvu zikaniishia nikanyong'onyea hata tabasamu likapotea. Mchaka mchaka nikajongea sebuleni, nawasili sebuleni sijaona chochote zaidi ya kuona zile nyayo zilizo na damu. Nikafikiria kuwa ni nani aliyeingia ndani huku ameumia, wakati milango yote nimefunga hata sikuambulia kudadavua kitu. Nikapiga moyo konde nikajirubuni kuwa labda jini Suleiman bado anaendeleza mauza uza ili niondokane na upweke, basi nikahamua kukimbilia chumbani nikaongee na Suleiman kuwa aache kunifanyia mauza uza, hata hivyo kabla sijafika tena chumbani. Nyuma nikasikia kicheko kikitokea sebuleni, kicheko kile kikanifanya niingiwe na uwoga. Punde mwili wangu ukafa ganzi, pole pole nikajongea sebuleni kwa ajili ya kuangalia ni nani anayecheka kicheko kile cha kujirudia mfano wa mwangwi. Kufika sikuona mtu wala sikusikia kile kicheko, nikashangazwa nikabaki nimeganda tu nikiduwaa na uwoga. Nikiwa nimeduwaa huku nimesimama tu mara nikashtuka niliposikia mkwenzi umepigwa, nikatumbua macho kule niliposikia mkwenzi. Ila sijaona mtu, upesi nikageuka ili nimfuate Suleiman. Lakini nikaonana ana kwa ana na jini Sulesh baada ya kugeuka.





    “Umefuata nini?,” Nikauliza japo kwa uwoga.



    “Unaniuliza nimefuata nini. Nimekufuata wewe,” Jini Sulesh alijibu huku akipalaza nywele zake taratibu kana kwamba hana uwoga.



    “Sitaki.”



    “Hutaki?. Utataka tu, ukumbuki kiasi nilichotoa. Halafu leo hii kirahisi ukatae, nani kasema,” Jini Sulesh aliongea huku akisogea niliposimama.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ah! nikakosa ujasiri. Uwoga ukatawala nikapiga ukunga, ule ukunga ukamuamsha Suleiman haraka akaamka akapotea chumbani akatokea tulipo. Akamkumta mdogo wake akisogea anibusu kilazima, Suleiman akapotea punde akatokea jirani zaidi. Akamsukuma Sulesh, Sulesh akadondokea sofani chali huku akicheka. Kicheko kile Suleiman akaigiza hajasiki, akageuka nilipo mwisho akaamuru niingie chumbani. Nikaingia.



    “Ha ha ha, te te te. Ndugu yaani ka umeomba lifti unataka kupiga na honi, ushasahau kama mke wa mtu ni sumu?,” Jini Sulesh akaongea. Maongezi yale japo nilikuwa chumbani lakini niliyasikia vema kabisa. Nikamsikia Sulesh akiongea kwa ukali na kaka yake.



    “Sulesh, mwanamke inaonyesha hakupendi. Kama hakupendi huna budi kumuachia kaka yako,” Jini Suleiman nae akaongea. Nilimsikia Suleiman akimjibu mdogo wake kwa upole sana.



    Ukimya! ukatawala. Kukawa zi zi ziiii, sikusikia maongezi tena. Dakika kadhaa ndipo nikaja kusikia ukunga wa maumivu uliopigwa na Suleiman. Hofu ikajaa, macho yakatoka pima. Nisijue kilichotokea huko sebuleni, nikiwa kwenye hali ile mara nikasikia vishindo vya miguu vikitembea kuja katika chumba changu. Akili ikaruka, upesi nikasogelea mlango nikafunga na funguo. Ndipo mtu yule aliposikia nafunga mlango, nikamsikia akiangua kicheko. Kicheko kile nilipokisikiliza nikatambua ni cha nani, ni kilikuwa cha Sulesh. Kicheko cha Sulesh kikazidi kunijaza hofu mara nikajikuta natetema tu, nilijaa na wasi wasi mpaka nikajihisi uso umeenea jasho. Kweli chumba nikakiona cha moto japo kulikuwa na ubaridi wa feni “Pangaboi”, ghafla kicheko sikukisikia tena nikajua Sulesh kashaondoka. Nikatoka chumbani taratibu huku nikijaribu kung'aza macho kila pahala labda nitaona chochote, lakini sikubahatika kuona chochote wakati ule. Nikaelekea sebuleni, ila nilipofika huko nikastaajabu na punde nikasikia mapigo ya moyo yakidunda. Sikuamini nilichokiona, nikaona Suleiman kalala sakafuni huku pale alipolala kukiwa kumetapakaa damu. Nikasogea jirani nichunguze, nilipochunguza nikagundua Suleiman tayari alikuwa kashafariki. Utumbo wote wa Suleiman nikaukuta upo nje mfano wa mzoga uliwapo na Kunguru, machozi yakanilenga. Mtoto wa kike kilio kikanitoka sio kama nalia sababu, Suleiman kafariki kifo butu. La hasha!, ninalia sababu nimejuana na nimependana nae Suleiman kwa muda mfupi sana. Naumia zaidi, nikikumbuka misaada aliyonisaidia lukuki.



    “Sasa ujanja upo wapi binti. Msaada ndio huo chini, ushakufa. Uamshe ukusaidia katika mazonge,” Jini Sulesh akasikika akiongea kwa kebehi. Aliongea huku akitomasa maungo yangu, kwa hasira nikamputa mkono asiendelee kunishika. Lakini Sulesh alionekana jeuri akaendelea kunishika, safari hii aliponishika kwa jazba nikamng'ata mkono. Cha ajabu badala ya kusikia maumivu akawa anacheka huku akifuata mwili wa nduguye, akaushika mwili hatimaye papo hapo akapotea na nduguye eneo lile.



    **********

    Usiku ule Sulesh akawasili majini na nduguye katika kumbi ya kifalme, akamlaza marehemu huku akiigiza kulia kana kwamba hausiki na kifo cha Suleiman. Akawaamsha majini wote, dakika tu wakakusanyika katika kumbi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Nini kimekukuta.... Nini kilichokuondoa duniani?,” Jini Sulesh aliigiza kulia zaidi, ili ajistili makucha katika sirika mara baada ya kuona majini wote wamewasili.



    “Sulesh. Suleiman umemkuta wapi?, na kapatwa na nini?,” Mzee Kadhir aliuliza mara baada ya kuona aelewi.



    “Alikuwa ufukweni, nikamkuta kakandamizwa na gogo la mbuyu,” Jini Sulesh alieleza huku bado akiwa anaigiza kulia.



    “Gogo la mbuyu!!, ndiyo limechukua uhai wake?,” Binti Surya aliuliza nae huku akihamaki mara baada ya kugundua mwanae mkubwa kaaga dunia.



    “Naam, nimeumia sana maana katika uzawa wetu. Tumezaliwa wawili tu ka dawa” alisema Sulesh huku akifuta machozi ya kuigiza.



    Baada ya majini wote kujua Suleiman kafariki mara sura zao zikabadilika zikawa na majonzi. Hakuna budi kufanya maziko, wakamzika Suleiman kwa hekima na heshima hatimaye majini wote wakatawanyika wakarudi majini kuendelea na majukumu uchwala.



    **********

    Usiku wa saa saba nikiwa chumbani nimelala kitandani, mara ghafla nje nikasikia upepo mkali ukipuliza. Na kupenya kwenye madirisha yangu ya chumbani, ukaleta baridi kali na kufanya nishindwe kujizuia. Nikajifunika gubi gubi ili baridi lisinipulize, lakini nikashangaa kuona upepo ule ukiwa bado unapenya kwenye maungo yangu. Ni wa ajabu, ulikuwa una nguvu balaa mpaka ukaweza kunifunua shuka kwa ghasia. Usingizi ukakata nikakaa kitako kitandani nikitafakari upepo ule wa namna gani, maana hata upepo wa kisuli suli sio vile. Nikashindwa kujua, nikabaki nikijikunyata ka kitoto cha Paka. Duh, upepo ulikuwa ni tishio nikakosa lepe la usingizi. Nikabaki nikikodoa macho tu pale kitandani, lisaa moja kupita upepo ghafla ukakata. Kukawa shwari ka awali, nikajaribu kujiegesha kitandani pengine nitapata usingizi tena. Kabla sijapata usingizi kupitia dirishani nikaona dalili ya mvua ikitaka kunyesha, niliona mweku mweku. Nikasikia mngurumo wa radi na punde nikaona mvua sasa ya rasha rasha ikinyesha, moyoni nafsi ikafurahi kwa maana mvua ilikuja wakati muafaka. Ilinibembeleza taratibu nikalala pono, muda mwingiiine kabisa nikiwa kwenye usingizi nikasikia nikiitwa kwa sauti ya juu. Mpaka kero ikanilazimu nijivute niamke, nikaamka kumuangalia aliyeniita lakini sikumuona bali niliona maajabu yakiendelea. Nikaona mlango upo wazi angali nilifunga, pia nikaona taa zote zikiwaka na kuzima ka kwenye kumbi ya starehe “Club”. Papo hapo hofu ikanitanda mwilini upesi nikajikuta nikibwata.





    “Wewe ni nani?, unayefanya hivi ni nani?...au ni Sulesh?,” Nilibwata huku nikiweweseka kwa uwoga.



    Hata maswali hayakupatiwa ufumbuzi bali yakachochea kicheko cha mwangwi kilipotoka sikujua wakati ule, hofu ikaongezeka maradufu. Ujasiri sikuwa nao hata thumni, ni uwoga tu ulionitawala. Nikatulia nikitetemeka mfano kitoto cha Paka kisikiapo baridi, mtetemo wa mwili ukachukua nafasi. Nilitetema mpaka nijajihisi kuishiwa nguvu, nikanyongea lakini ghafla kicheko kile kikafika ukomo kukawa tuli mfano umeme ukatikapo. Ujasiri ukarudi nikainuka kitandani, nikasimama ili nijaribu kupepesa macho chumbani nione ka kicheko kile kilitoka wapi. Hamadi! katikati ya mlango wa chumbani akatokea Sulesh baada ya kung'aza macho kwa muda, Uwoga ukarudi tena nilipoonana na Sulesh kwa mshtukizo. Nikabaki mpole na mara papo hapo nikazilai, fahamu nikaja kurudisha usiku wa saa kumi nikajikuta nipo kitandani nikaangaza macho kila kona ya chumba. Mtumee!! kuangalia kando nikamkuta. Jini Sulesh akiwa kando yangu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unataka nini?,” Nikapayuka.



    “Mapenzi. Nakupenda Prisca,” Jini Sulesh alijibu huku akikaza macho kwangu. Akionyesha kunitisha ili nije kusema neno lenye herufi nne kwa usahili.



    “Sasa sikupendi, pia sikuhitaji.... Naomba ondoka,” Nikaongea kwa sauti ya ukali, kisha nikateremka kitandani nikaelekea sebuleni kwa ajili ya kumkwepa Sulesh.



    Lakini kabla sijafika katika mlango wa chumbani, ile nanyanyua mguu tu nipige hatua ya kutoka chumbani nikaganda. Sikuweza kwenda mbele wala kurudi nyuma, kila nikijilazimisha nitembee wapi. Fadhaa ikanishika muda ule ikashikika, nikageuka nyuma kwa jazba nimuone Sulesh ka yupo kitandani au lah. Cha ajabu hakuwepo, nikageuka tena mbele nijaribu kwenda. Haraka nikashtuka baada tu ya kumuona Sulesh mbele yangu huku akitabasamu, mwili wote punde ukafa ganzi nikatamani nikimbie lakini sikuweza sababu ya kugandishwa bila kutaraji. Sikupanga yatokee ila yote ni njama za Sulesh. Niliendelea kusimama mfano sanamu, ndani ya nusu saa Sulesh nikaona akinibusu mdomoni na ghafla kumbukumbu zikapotea. Punde akanikumbatia tukapotea chumbani, tukaja kutokea chini ya bahari huku nikitembezwa kuelekea nisipopajua. Tuliendelea na matembezi mara ghafla tukapotea tena tukaja kutokea kwenye kumbi kubwa “Hall” naona ni la kifalme maana lilipendezeshwa na vito ghali, nilipofika kwenye kumbi ile nikajihisi nipo katika sayari nyingine kwa maana niliona. Viumbe ajabu ambavyo sijawahi kuviona maishani mwangu, niliona majini mbalimbali. Niliona majini Laadu, Shufaa na wengine wengi. Sababu kumbukumbu sikuwa nazo hivyo sikushangaa na wala sikuogopa sana, nikajiona jasiri tosha.



    “Baba, huyu ndiye atakayekuwa mke mtarajiwa. Anaitwa Prisca,” Jini Sulesh akatambulisha. Nami nikasikia akinitambulisha kwa mzee wa makamo, ambaye ndiye naona ni baba yake.



    “Vizuri. Mwanangu nimefurahi sana, leo kuonana na mkamwana,” Mzee Kadhir aliongea huku kweli akionyesha kufurahia ujio wangu.



    “Sasa leo nimekuja nae, ili nipate baraka,” Jini Sulesh akaongea.



    “Ni vema...lakini siunajua tumetoka kwenye pigo. Bora tuhailishe, hizo baraka tukupatie siku nyengine,” Mzee Kadhir akashauri.



    “Lakini. Baba Sulesh, kwanini tusimpatie mtoto baraka. Kama pigo tayari tushalipata hakuna kitakachobadilika, naona tumpe tu mtoto baraka, tena siunajua sisi muda wowote tutaonja umauti. Bila kumtengeneza mrithi mapema, tutakosea,” Binti Surya akaeleza.



    Mzee Kadhir akatafakari kwa muda, akaona ni ya kweli asemayo mkewe. Basi wakampatia mtoto wao baraka, Sulesh alipopatiwa baraka na wazazi akaaga kuwa anaondoka majini kwa kipindi kifupi. Ili aende nami ulimwenguni akanifunze hulka, hakukatazwa akaruhusiwa mara akapotea nami pale majini. Tukatokea sebuleni kwenye mjengo ule ule wa Mabibo hostel. Tukafikia kukaa sofani tuli huku tukitazamana, halikupita lisaa hatimaye nikamuona Sulesh kanyanyuka kwenye sofa akanifuata nilipoketi. Kisha akanibusu mdomoni na ghafla nikarudisha kumbukumbu upesi nikamkwepa nikataka kwenda chumbani, lakini akanizuia akanikalisha tena sofani kilazima. Nikachukia sana matendo mabovu ya Sulesh, yaani sikumpenda kabisa sema nitafanyaje. Wakati maji yashanifika shingoni, inabidi nikubali hali kishingo upande. Nikatulia tu nimsikilize.



    “Prisca, samahani sana. Najua kila nifanyalo na kuuzi, ila nami nitafanyaje napigania penzi langu. Nisamehe mama...nakupenda,” Jini Sulesh akajirudi.



    “Sitaki. Sikupendi, mbona unisikii...siwezi kuwa nawe. Kama imekuchoma niue tu kuliko kunitesa,” Nikapayuka.



    “Prisca....,” Jini Sulesh kabla hajamaliza kuongea. Nikamkatisha.



    “Ni nini?...au nirudie kwa herufi kubwa kuwaSIKUPENDI,” Nikagoma.



    “Ho ho ho. Shiiiiit, upuuzi huu,” Jini Sulesh aliongea kwa hasira. Hakupendezwa kabisa na matamshi niliyonena.



    Ghafla nikaona kabadilika akavimba uso mpaka uso ukawa mwekundu, dakika tu akanivaa kwa jazba na mara tukapotea sebuleni tukatokea chumbani. Ghafla akanisukuma kitandani akafunga mlango akanisogelea huku kafura.



    “Siutaki nikupende. Sasa kuanzia leo makazi yako yatakuwa humu, chochote kitakacho kutokea ni juu yako,” Jini Sulesh akaongea. Na mara akapotea akaniacha chumbani nikiwa gizani.





    Nikaishi kwenye chumba kwa tabu sana, mwanzo chumba kile kilikuwa wala hakitishi lakini hawamu hii. Chumba kilikuwa cha kutisha sana, kulikuwa na kila aina ya vitisho vya ajabu. Ikawa mara niamke nisikie sauti za kutisha, mara niamke nikute chumba kimetapakaa damu, mara niamke nikute kinyesi kitandani, mara niamke nikutane na Paka kitandani, mara siku nyengine nisikie watu wakiongea lakini nisiwaone. Basi kila siku nilikuwa nakutana na mambo ya ajabu katika chumba kile, japo nilikutana na magumu katika chumba kile lakini sikuwahi kubadili msimamo wangu. Nilisimama imara huku nikipiga moyo konde ili nishinde vikwazo, kweli nikavumilia. Nakumbuka ilikuwa ni Jumatano ya tarehe 18/03/2015 usiku, siku hii. Hali ya hewa ilikuwa nzuri wastani. Wingu zito likatanda, baridi kiasi likapuliza. Ujumla anga ilipendeza wastani, nikiwa bado katika chumba hatarishi. Sauti za chini nikazisikia sebuleni, watu wakiongea na kucheka. Mmojawapo wa watu hao akiwemo Sulesh. Nimetabiri Sulesh sababu sauti yake niliijua, na maongezi niliyoyasikia ni haya:-



    “Nduguze, nimewaita. Ili nipate ushauri wa jambo moja tu,” Nilisikia Sulesh akiongea, bila shaka alikuwa anaongea na majini wenzie.



    “Lipi?,” Nilisikia mwanamke akiuliza swali.



    “Prisca, hanipendi. Wazazi wanajua ananipenda, sasa wakijua ukweli si hatari. Hebu...nipeni ushauri, nifanye nini?,” Nilisikia Jini Sulesh akieleza kisha akauliza.



    “Mh, sasa sijui tukupe ushauri gani. Hebu...ngoja kwanza,” Safari hii nilisikia sauti ya mwanaume ikijibu, punde kimya kikatawala. Nahisi mwanaume yule alikuwa anafikiria kidogo, baada ya dakika nikasikia akiendelea kuongea huku akisindikiza kicheko.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haa haa haa, nishapata ushauri. Hivi wazazi wamekariri sura ya Prisca?,” Nilisikia mwanaume yule akiuliza mara baada ya kufikiri.



    “Ha hapana,” Jini Sulesh nilisikia akijibu huku akionyesha kusita.



    “Kama hawajaikariri sura ya Prisca. Ushauri wangu naona umuue Prisca.” Nilisikia mwanaume yule akitoa ushauri. Nikashtuka kisha nikatulia mara baada ya kusikia ushauri ule.



    “Eti nini?,” Jini Sulesh nilisikia akiuliza kwa kuhamaki.



    “Ehe, muue Prisca ili uchukue mwili wake. Uwekee roho nyengine ambayo itakayokupenda, kabla wazazi hawajajua,” Nilisikia mwanaume yule akieleza bila shaka yoyote.



    “Hiyo itakuwa poa. Kweli?,” Jini Sulesh nilisikia akiuliza kwa hofu kana kwamba hajawahi kuua.



    “Ndiyo. Itapendeza saana,” Nilisikia mwanaume yule akiunga mkono kwa furaha sana, lakini tangu mwanaume yule atoe ushauri ule sikusikia sauti ya mwanamke iunge mkono. Dhahiri inaonyesha mwanamke yule hakupendezwa na ule ushauri.



    “Sulesh, Prisca mwenyewe unaishi nae?,” Sasa nilisikia mwanamke yule akivunja ukimya kwa kuuliza swali.



    “Ninaishi nae, hapa ninavyoongea nimemfungia katika chumba kile,” Jini Sulesh nilisikia akieleza, nahisi alieleza huku akinyoosha kidole katika chumba nilipo. Ili wenzake wapate kuona chumba hicho kwa urahisi.



    “Kwa nini, sasa umemfungia?,” Nilisikia mwanamke yule akidadisi, kwa ajili ya shauku ya kutaka kujua.



    “Sababu hanipendi, na kama hanipendi. Bora akae huko...halafu muda ushakwenda ngoja niwatoe kidogo. Kuhusu ule ushauri nitaufanyia kazi kesho kutwa, baada ya kumaliza sherehe ya kuzaliwa kwa mfalme,” Jini Sulesh nilisikia akiongea. Mara kimya kikatawala, nahisi alikwenda kuwasindikiza majini wenzie kama ilivyo ada.



    Lisaa moja kupita nikamsikia Sulesh akifunga mlango huku akipuliza mruzi alikuwa katoka kuwasindikiza majini. Hakwenda kukaa, moja kwa moja akaongoza kwenye kabati dogo lenye vitabu. Akachukua kitabu kimojawapo kinachoitwa God Devil cha mwandishi wa Marekani anayeitwa Mos Cherl, akaelekea kuketi sofani tuli akisoma haya moja baada ya nyengine kwa makini. Alisoma kwa masaa mawili akaacha akajiegesha sofani akalala, usingizi bubu. Asubuhi ya alfajiri akaamka akahifadhi kitabu kabatini, hatimaye akaenda bafuni kuosha uso. Kabla hajamaliza kuosha uso akasikia nje mvumo mkali wa upepo. Haraka akajiosha uso akatoka bafuni, na wenge. Ile anatokeza sebuleni anaonana na Zusia akiwa ameketi sofani, Zusia ambaye ni jini mwenye jinsia ya kike. Ndiye jini mlimbwende ambaye makuzi ni sawa na marehemu Suleiman.



    “Ujio wako, nimesikia. Kulikoni?,” Jini Sulesh aliuliza huku pole pole akiambatana na Zusia sofani.



    “Nimerudi leo, sababu mazungumzo ya jana mie sikuyapenda. Kwa nini umuue Prisca, kisa mapenzi. Kama ni wanawake mbona wengi, tafuta mwanamke mwengine tu. Kumuua Prisca.... Si suluhu,” Jini Zusia akaeleza.



    “Lakini mie nampenda Prisca. Sitaki kumkosa kabisa,” Jini Sulesh akaongea.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe unampenda. Yeye hakupendi, hebu...acha ubishi, tafuta mwanamke mwengine.”



    “Hapana.”



    “Ila si lazima, lakini bora ujue kuwa jambo mlilopanga sijapenda,” Jini Zusia akaongea hatimaye akapotea, huku alimuacha Sulesh kabaki na msimamo.





    Kesho yake usiku wa saa sita. Jini Sulesh akafunga milango ya nyumba yote, kisha akapotea akatokea katika kumbi ya kifalme. Akajumuika na majini mbalimbali kwenye sherehe ya kuzaliwa baba yake, majini wote wakiwa kwenye shamra shamra za sherehe. Jini Zusia akang'aza jicho la wizi kwa Sulesh ghafla akapotea akatokea katika mjengo wa Mabibo hostel, akatalii kidogo ndani akiangalia usalama uliopo. Alipoona kupo shwari akapotea akaja kutokea katika chumba nilicho, akapuliza juu ya paa na mara taa ikawaka tukapata kuonana ana kwa ana nikashtuka.



    “Wewe ni nani?,” Nikauliza kwa kufoka.



    “Ni Zusia. Jini kutoka tawala anayotoka Sulesh,” Jini Zusia akajitambulisha.



    “Mbona mnaniandama. Na wewe umefuata nini kwangu?.”



    “Kwanza kaa ujue kuwa. Mimi si jini mbaya, bali ni jini mzuri niliyekuja kukusaidia...na Sulesh si jini mzuri kwako, yaani bila mimi kukusaidia. Utapotea.”



    “Sasa unanisaidiaje?.”



    “Sasa sikia, mie nitakutoa katika chumba hiki. Ila nikikutoa wewe inakupasa uondoke, usionekane eneo lolote la Dar es salaam. Umesikia?,” Jini Zusia akauliza kwa kukaza macho kwangu.



    “Ndiyo,” Nikakubali huku kwa mbali nikijilazimisha kuonyesha tabasamu mara baada ya kuona. Jini Zusia ndiye mkombozi wangu.



    Baada ya kukubali msaada, Zusia hakuchelewesha muda, mara akapiga jicho kali kwenye mlango ule wa kile chumba. ghafla mlango ukafunguka tukatoka mwishowe akafunga kupitia njia ile ile ya awali, kufika sebuleni akanishika mkono tukapotea pamoja. Tukaja kutokea nje ya mjengo kabisa, tulipofika hapo Zusia akaniangazia njia ya kuongoza. Nikaongoza, yeye akapotea akarudi kwenye tafrija baada ya kuona mie tayari nimetokomea. Niliongoza njia ile ya kuelekea kituo cha daladala cha Mabibo hostel, huku kwenye nguo na mwili nikiwa nimechafuka mno. Nilipofika kituo cha daladala cha Mabibo hostel, hapo ndipo nikakutana nawe nikakuomba msaada ukanisaidia.



    **********

    Prisca alimaliza kumhadithia Emmanuel simulizi ya maisha yake, ambayo iliyomfanya hii leo aonekane ka chizi kwa jinsi alivyokuwa rafu. Akajifuta machozi kisha akajiangalia mwili na mavazi, kwa huzuni. Mpaka Emmanuel alimuonea huruma sana, baada ya kugundua kuwa alipitia wakati mgumu. Emmanuel alisogea jirani ya Prisca akamfariji kwa kumkumbatia hatimaye wakaongozana kwenda kuonyeshana chumba atakacho pumzika baada ya Prisca kuonyesha uchangamfu.



    “Asante sana,” Prisca alishukuru mara baada ya kuonyeshwa chumba cha wageni, cha kupumzika.



    Kabla Emmanuel ajaongea chochote kwa wakati ule, mara simu yake ikawa inaita haraka akapokea kisha akatoka chumbani akaelekea sebuleni. Kwa ajili ya kuzungumza na simu vizuri, kwa kuwa simu ilitoka ofisini na alikuwa anahitajika haraka ofisini. Basi, Emmanuel simu ilipokata tu. Upesi akarudi chumbani kumuaga Prisca, aliaga mwisho akaondoka ofisini huko bandarini.



    **********

    Majini tafrija iliisha usiku wa saa kumi. Jini Sulesh aliaga akapotea akatokea sebuleni katika mjengo wa Mabibo hostel, alifikia kulala sababu alichoka sana. Hakukumbuka hata kukagua nyumba, wala kwenda kumtazama Prisca. Alfajiri akiwa amelala kwenye sofa akashtuka usingizini baada ya kusikia radi kali imepiga nje, akakaa kitako kwenye sofa kama nusu saa. Akanyanyuka akachungulia nje kupitia kwenye dirisha la sebuleni, akaona shwari. Akarudi tena kukaa sofani, alipokaa tu macho yake yakagongana na picha ya Suleiman iliyoko ukutani. Ghafla akamkumbuka Prisca haraka akapotea pale sebuleni akatokea chumbani, kufika huko chumbani. Macho yakamtoka pima baada ya kutomkuta Prisca kwenye kile chumba, upesi akajifikiria katika Medula Obulangata kuwa. Prisca ametokaje kwenye kile chumba. Lakini alikosa jibu stahiki, akajipa jawabu tu kuwa. Pengine Prisca ametoka labda sababu mlango hakukaza, hivyo akajaribu kung'aza macho kila dira pengine ataona alipo Prisca. Akang'aza Magharibi hakumuona, Kaskazini hakumuona, Kusini hakumuona. Lakini kuangalia Mashariki aliona Prisca jinsi alivyosaidiwa, alipofikia na mpaka alipo msamaria mwema wake. Hasira zikamshika, jazba ikampanda ghafla akajibadili kisha akapotea pale akaja kutokea bandarini eneo la mapokezi. Akiwa kwenye jinsia ya kike ya mwanamke wa kichina, ambaye anayeongea lafudhi ya kiswahili cha kubahatisha.



    “Daada, bosii wako nimeemkutaa?,” Mwanamke yule wa kichina aliuliza huku akionekana kukagua eneo lile la mapokezi kwa kupitisha macho kila kona mara baada ya kukutana na sekretari.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Umemkuta. Ila wewe ni nani?, ni mfanyabiara au ni mteja?,” Sekretari nae aliuliza mara baada ya kujibu swali la yule mwanamke wa kichina.



    “Ni mteeja.”



    “Ehee, una shida ipi?.”



    “Nataaka kuoonana nae. Anieelekeze mziigo wangu umefiikia wapi...maana hii ni siiku ya taatu sijaapata mziigo wangu.”



    “Ooh, lakini. Kwa sasa bosi ana mgeni....”



    “Usiijali nitaamsubiri,” Mwanamke yule wa kichina aliongea huku akitabasamu kwa mbali, mara baada ya kukaa katika sofa za mapokezi.



    Masaa mawili kupita, Emmanuel alitoka ofisini kwake akiwa na mgeni wake. Ambaye ni mzee wa makamo aliyepigilia suti nyekundu ya gharama, alimsindikiza mgeni yule mpaka sehemu ya kuegeshea magari “Parking”. Hapo ndipo akarudi ofisini baada ya kuhakikisha mzee yule kashapanda gari yake aina ya LANDCRUISER V8 na kuondoka, aliporudi mapokezi anataka kupita aelekee ofisini mara anasikia sekretari wake akimuita, hakuwaza akatii wito akajongea kumsikiliza sekretari.





    “Bosi, mwanamke yule wa kichina anahitaji kuonana na wewe. Bosi,” Sekretari aliongea huku akionyesha kidole kwa yule mwanamke, ili bosi apate kumuona. Ni kweli Emmanuel akageuka akamtazama yule mwanamke mara moja kisha aliongea huku akitafuna bazoka.



    “Mwambie, aje ofisini,” Emmanuel aliongea haraka na upesi akaongoza ofisini.



    Sekretari baada ya kupokea ruhusa. Akamruhusu yule mwanamke aingie ofisini kwa bosi akazungumze, nae yule mwanamke bila kuchelewa akaongoza katika ofisi. Cha ajabu kufika mlangoni kwenye kumbi ya kuingilia ofisini, yule mwanamke akajibadili akarudi kuwa. Jini Sulesh, akaingia ofisini. Ile anaingia tu wakagongana macho kwa macho na Emmanuel, mara Emmanuel akasisimka na akashtuka maana hakutegemea kukutana na Sulesh. Badala yake alitegemea kukutana na yule mwanamke wa kichina.



    “Ehe, mheshimiwa. Natumaini sina mihadi na wewe, hebu...nipishe kidogo niongee na mgeni wangu,” Emmanuel aliongea huku akikunja ndita asijue kuwa kama mwanamke yule anayehitaji kuongea nae ndiye aliye mbele kwasasa.



    “teh teh teh. Unasema huna mihadi na mie, kwani wewe una mihadi na nani?,” Jini Sulesh alianza kucheka kisha akauliza.



    “Nina mihadi na mwanamke fulani, mtu mweupe.”



    “Sasa, si ndiye mie.”



    “Hapana. Unasema ndiye wewe, kivipi?,” Emmanuel alipinga akijua yule si mhusika aliyeomba mihadi nae.



    “Ndiye mie. Ona,” Jini Sulesh alisema kisha akajibadili kuwa yule mwanamke wa kichina, na mara akarudi kwenye muonekano uliozoeleka.



    Emmanuel kuona vile akachanganyikiwa, aliona ofisi yote ndogo. Imejaa joto la ajabu japo ilikuwepo “AC” ya kutosha, ofisi yote akaiona chungu. Alitoka pale ofisini nduki akapita mapokezi upesi mpaka sekretari wake akashangaa akabaki kinywa wazi, alikwenda kwenye maegesho ya magari akapanda gari lake akatokomea nyumbani.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********

    “Dada, kulikoni. Bosi mbona kapita mapokezi akiwa resi?,” Sekretari aliuliza mara baada ya kufika katika ofisi ya bosi wake na kumkuta Sulesh kashajibadili tena kuwa muonekano wa mwanamke wa kichina.



    “Aah, boosi wako katooka viile sabaabu kapaata simu ya msiiba,” Mwanamke yule wa kichina aliongopa kwa kuongea lafudhi ile ile ya kiswahili cha kubahatisha, ili kuficha makucha kwa sekretari.



    Hatimaye. Jini Sulesh akaaga akaondoka bandarini bila ya kumaliza maongezi na sekretari, hata hivyo. Jini Sulesh kwa kuwa akutimiza dhima kuu, alichokifanya ni kupotea akaja kutokea kwenye gari ya Emmanuel. Katika viti vya nyuma huku Emmanuel mwenyewe akitingwa na msongo wa mawazo, na foleni ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi hasitambue chochote. Zile gari za upande wa barabara ya Ally Hassan Mwinyi ziliporuhusiwa na kuanza kutembea nae Emmanuel akakanyaga mafuta, ghafla Emmanuel akiwa kwenye mwendokasi akashtuka kusikia mtu nyuma ya kiti cha gari lake akijitambulisha bila hofu.



    “Kwa majina, naitwa Sulesh bin Kadhir. Ni jini ambaye aliyetokea kumpenda msichana mmoja tu, nae ni Prisca,” Jini Sulesh alijitambulisha huku akimpiga jicho kali Emmanuel, kupitia kwenye kioo cha mbele cha gari. Ili aone Emmanuel alivyo na hofu usoni.



    “Lakini mimi, sio Prisca. Sasa kwangu unataka nini?,” Emmanuel aliuliza huku akitetema kwa kugubikwa na uwoga kila pahala ya mwili.



    “Najua wewe sio Prisca. Ila najua unaishi nae kwa sasa, hivyo. Naomba nikabidhi Prisca kabla mambo hayajabadilika.”



    “Ila...,” Emmanuel kabla ajamaliza kuongea zaidi kwa wasaa ule, mara moshi mzito mweusi ukatanda ndani ya gari lake hadi yeye na. Jini Sulesh wakaogopa maana moshi ule ulikuwa si wa kawaida, ulikuwa ni wa ajabu sana.



    Na ghafla moshi ule ukaisha, kabla ya dakika tano kupita kwenye kiti cha nyuma ya gari alipokaa. Jini Sulesh, alitokea mzee mmoja aliyechakaa kichwani kwake na mvi. Halafu mwenye macho makali ka Paka, hakika ulikuwa ni mzimu. Mzimu wa babu yake Emmanuel, basi mzimu ule macho yake yalipogongana na macho ya. Jini Sulesh, ghafla ndani ya gari kukatokea shoti mfano wa radi. Kisha punde Sulesh akanyong'onyea haraka akapotea kwenye gari.



    “Emmanuel, Usiogope. Mjukuu wangu, nimekuja kufanya hitimisho. Unakumbuka kipindi cha nyuma kabla ya kifo changu, wewe ulipenda sana uje kujua. Umuhimu wa lile Ua la Uwaridi nililokukabidhi wakati upo na wazazi, sasa basi. Naona leo ni wakati sahihi wakujua umuhimu wa lile Ua,” Mzimu ule ulisema mara baada ya kuhakikisha. Jini Sulesh kweli amemkimbia na mjukuu wake hofu imemtoka anamsikiliza.



    “Babu, kweli nina shauku sana. Kwani Ua lile lina umuhimu gani?,” Emmanuel alidakia, akauliza kweli kwa shauku apate kujua umuhimu wa lile Ua. Ambalo babu yake amepewa na mizimu ya ukoo huko kipindi cha nyuma kwenye milima ya ajabu ya Uluguru.



    “Umuhimu wa lile Ua, ni kujilinda wewe na watu uwapendao msidhurike na kitu chochote cha hatarishi,” Mzimu ule ukaeleza.



    “Sasa, tangu unipatie lile Ua sijawahi kutumia na sijui kulitumia. Sasa Ua lile litanilindaje?,” Emmanuel akahoji. Kuhoji kwake kule ukamfanya mzimu ucheke, haukucheka kwa kuonyesha kebehi bali ulicheka kwa ajili ya swali lile lililoulizwa na mjukuu wake kwa kimue mue.



    “Sasa sikia, naona mapambano ya viumbe hatarishi yashaanza zidi yako. Kama yameanza ni kazi ndogo tu kwako, cha kufanya. Chukua lile Ua halafu kamkabidhi mtu yule unayempenda kutoka ndani ya moyo, yaani kivyovyote ile. Uwe unampenda kimapenzi au kirafiki, ukitenda hivyo. Utakuwa umemaliza mchezo wote, hamtofuatwa tena na kiumbe chochote hatarishi. Ng'o,” Mzimu ule ulielekeza mwishowe ukatokomea huko kuzimu, huku ukamuacha Emmanuel akiendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake Masaki.



    **********

    Zamu hii. Jini Sulesh alikuwa anatapatapa tu, zote ni juhudi za kumrudisha Prisca kwenye himaya yake. Safari hii alikuja kutokea sebuleni kwenye nyumba ya Emmanuel, alitokea nyuma ya sofa ambalo alilokaa Prisca huku. Prisca hasitambue chochote, yeye alikuwa makini tu na kusoma gazeti la MTANZANIA DAIMA. Jini Sulesh akachukua fursa ya kupotea pale nyuma ya sofa, akaja kutokea amekaa sofani jirani na Prisca huku. Prisca hasijue ka Sulesh kashawasili, wakatulia sofani ka lisaa bila Sulesh kumbuguzi Prisca. Lilipopita lisaa lile na kuwasili lisaa lengine, mara. Jini Sulesh ikaonyesha uvumilivu umemshinda, hakashindwa kujizuia akataka kumbusu Prisca ili apotee nae. Ghafla Emmanuel akaingia huku akiwa anahema kuonyesha kuwa ametoka kukimbia kwa ajili ya kuwahi kumsaidia Prisca, hali ile kidogo Prisca alishangaa akajua kwa wakati ule Emmanuel anahitaji faraja. Basi akataka kuweka gazeti kando ili akamfariji Emmanuel kwa kumlaki, la haula!.... Alimuona. Jini Sulesh jirani yake, hapo bila kutaka ajizi akakimbilia chumbani kwa ajili ya kumkwepa Sulesh. Hazikupita dakika Emmanuel nae upesi akaingia chumbani kwake akachukua lile Ua la Uwaridi alilohifadhi kwenye sanduku la nguo, haraka akaelekea chumbani kwa Prisca. Aligonga mlango akajitambulisha akafunguliwa, na mara akaingia chumbani na kufunga mlango. Na sababu Prisca ndiye mwanamke ampendaye Emmanuel tangu awali alipompatia msaada eneo la Mabibo hostel, hivyo hata lile Ua hakusita kumkabidhi yeye. Alimshawishi Prisca haweze kukubali kupokea lile Ua ili wawe salama, Prisca sababu ni muelewa na kwa kuwa alichoka kusumbuliwa na. Jini Sulesh basi bila ajizi akakubali kupokea lile Ua, pia bila shuruti akakubali kuwa mke wa Emmanuel baada ya Emmanuel mwenyewe kumuomba awe mkewe. Ua likiwa tayari lishapokelewa na Prisca, mara ghafla kule kule akatokea Sulesh tena kwa kishindo hadi likatokea tetemeko kwenye chumba kile. Takribani nusu saa imepita, ghafla Sulesh anaonyesha kunyong'onyea mara anadondoka sakafuni baada ya macho yake makali kuangalia lile Ua la Uwaridi alilolishika Prisca. Hakukaa sana ghafla akapotea akatokomea mazima eneo lile, huku akipiga ukunga wa maumivu. Na tangu siku hiyo Sulesh aliona ulimwenguni ka kituo cha polisi, hakuthubutu tena kuja ulimwenguni. Yote sababu ya lile Ua la Uwaridi lenye nguvu ya mizimu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********

    Ya nini?. Ulazimishe penzi, kwa ajili ya kujikonga nyoyo na kufurahisha moyo huku wengine wakiumia. Huo ni udhariri, iweje?. Unakubali kupoteza nguvu kwa ajili ya mtu mmoja ambaye asiyekupenda, kweli?. Hii inaingia akilini, hapana. Ni hapana sababu wapo wanaopenda, sasa kama wapo. Kwanini tusiwapende hao. Itakuwa nzuri sana, maana hao watatupenda, watatuthamini na watatuheshimu sana. Hebu...sasa hii leo sambaza upendo kwa watu kama hao, wala usijivunge. Wewe onyesha upendo kwa mtu kama huyo, naamini upendo wako hautopotea bali utakuletea makuu katika maisha.”



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog