Search This Blog

MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI - 1







IMEANDIKWA NA : SADARI KISESA



*********************************************************************************



Simulizi : Mama Usinifundishe Uchawi

Sehemu Ya Kwanza (1)



UTANGULIZI...

“Uchawi upo japo serikali haiamini kama upo. Uchawi huleta utata kwa raia na serikali. Raia wanaamini uchawi sababu unawakuta, serikali haiamini uchawi sababu ya katiba yao. Raia wanaona uchawi ni mateso, sababu ya kufanyishwa kazi pasipo kujijua wenyewe pia wanaona mateso sababu ya kurudishwa nyuma maendeleo. Kwa kiasi kikubwa uchawi hauna nafasi serikalini tena hausikilizwi unaonekana kama ukakasi.

Uchawi ni tishio kwa binadamu uonekanapo. Humkosesha amani na humjengea hofu. Uchawi hauna faida yoyote zaidi ya mateso. Ijapokuwa wachawi wanaona kuna faida. Ukweli wanashangaza mtu anatumikia uchawi toka utoto mpaka uzee, lakini mafanikio hana! badala yake anaambulia fedheha. Hayo yote ya nini ebu...tumpe Mungu nafasi ya kubariki maisha yetu.”



SONGA NAYO....

Mkoani Morogoro, wilaya ya Mvomero, kata ya Kibaoni, na kijiji cha Maharaka. Anga yote ilikuwa imetanda kuashilia mvua saa yoyote inanyesha. Hali ya hewa si shwari baridi lilikuwa kali kupita maelezo. Ardhi baada ya muda ukali wa jua ulipoa ikaacha shamrashamra za wanakijiji zikilindima. Ndege nao walifurahia ujio wa mvua. Shorwe kwa makundi wakawa wanarukaruka na kukimbizana huku wakionyesha furaha kwa ajili ya ujio wa mvua. Yange yange hawakuachwa nyuma walikuwa kipaumbele kupendezesha anga kwa rangi zao nyeupe na kuruka kwa madaha, “Kwaa kwaaa kwaaaa”.

Alaah! Kunguru nae anafurahia ujio wa mvua kwa kurukaruka huku akitoa sauti angavu angani. Anga kikweli siku ya leo ilipendeza ama kweli Mungu hakukosea kuumba viumbe vyake. Ameumba na sasa wanamtumikia. Yaani ni kazi kwelikweli, nakuambia ujio wa mvua ulileta hekaheka hadi kwa wanakijiji. Wanakijiji walitimua mbio na kurudi majumbani wakijua mvua itanyesha kumbe lahasha!!!. Lakini katika pilikapilika za wanakijiji kujihami na mvua, alionekana kijana wa kiume chini ya mwembe akiwa kajiinamia huku mkono wake wa kuume ukiwa umeshika tama. Kijana hakuonyesha dalili ya kuhofia ujio wa mvua. Alijikatia tamaa kabisa na ndipo alipoamua kutulia chini ya mwembe. Kichwa chake kilionekana kimejaa msongo mkubwa wa mawazo huku asijue kinachoendelea angani. Alikuja kushtuliwa na mama yake mara baada ya kuitwa kwa muda mrefu na mama yake kwa kutingishwa mabega.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Naam!!!,” Kijana yule aliitika kwa mshangao na kukurupuka toka kwenye lindi la mawazo mara baada ya kusikia mama yake akimuita.



“Mbona unaonekana una mawazo sana...nini kinachokutatiza?” aliuliza mama yule huku akiangalia juu ya anga na kuhofia ujio wa mvua.



“Unajua fika mwanao ninavyoteseka kwa kulima, lakini hata mwaka mmoja sijafanikiwa kupata mafanikio” alieleza kijana yule mambo yanayomsumbua.



“Hayo mambo ndiyo yanakufanya ujikatie tamaa mapema?.”



“Sio mapema unavyodhani...ebu wewe fikiria miaka mingapi imepita lakini mimi nipo vile vile.”



“Miaka mitano si mingi, nakusihi zidi kupambana tu ipo siku utafanikiwa.”



“Lini sasa?...kama kupambana nimepambana sana hadi nimechoka.”



“Eeh...nyanyuka tukazungumzie nyumbani hapa tusije nyeshewa na mvua. Unaona hali ya hewa ilivyobadilika mvua itanyesha sasa hivi” aliongea mama yule huku akimvuta mwanae mkono wa kuume upesi anyanyuke waondoke.



Kabla kuondoka wakaficha majembe kisha wakaongoza njia kuelekea nyumbani na kufika jioni. Kijana yule akaenda chumbani kwake akamwacha mama yake akiandaa chakula cha usiku jikoni.



**********

Kijana huyu alibahatika kuishi na mama yake pekee kutokana na baba yake kufariki akiwa mdogo katika mazingira ya kutatanisha. Hakubahatika kusoma alikuwa ni mtoto wa kulima bustani na kufanya kazi za nyumbani.

Zao kubwa alilopendelea kulima hasahasa ni nyanya. Alilima Nyanya kwa uchungu huku akijipa matumaini ya kuwa ipo siku atafanikiwa. Kijana huyo na mama yake waliishi katika nyumba ya urithi iliyoachwa na marehemu baba yake aliyejulikana kwa majina ya Iddy Ramadhan Mbawala. Walisongesha maisha katika nyumba iliyojengwa kwa matofali ya kuchoma. Njaa upande wao waliizoea huku kejeli za majirani zikishamiri juu yao kwa kuwatupia vijembe vya chinichini wakisema. Wanajifanya maskini tajiri, wacha wafe na njaa.

Lakini kijana yule na mama yake waliziba masikio hawakutaka kabisa kusikiliza maneno yanayosemwa na majirani. Kipindi cha mavuno kijiji cha Maharaka huwa kinakuwa na ahueni kwa wanakijiji kwa sababu ya mavuno kupatikana kwa wingi msimu huo. Mama yake kijana yule anayefahamika kwa jina la Binti Mngane mama wa mtoto mmoja anayetambulika kwa jina la Sharifu. Kijana aliyejikatia tamaa mapema, msimu wa mavuno upande wao wanafurahia kuwa unakuwa ahueni. Binti Mngane ameishi na mwanae muda mrefu lakini hakuweza kumweleza siri iliyo ndani ya moyo aliyoficha kwa kila mtu asitambue, atakaetambua kifo kina mhusu. Usiku huo Binti Mngane aliivisha chakula hatimaye akamuita mwanae waje kula achana na kula tu bali kulikuwa na jambo analohitaji amwambie mwanae.



“Sharifuuu” aliita Binti Mngane kwa kupaza sauti.



“Naam” aliitika Sharifu kutoka kwenye chumba chake chenye mwanga hafifu wa Koroboi.



“Unafanya, nini?” aliuliza Binti Mngane huku akitenga chakula ukumbini.



“Nakunja nguo, siunajua ndani humu kulivyo na panya” alijibu Sharifu huku akitokwa na jasho usoni na pia machozi yakimtoka machoni kutokana na moshi wa Koroboi.



“Achia...ugali tayari.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Sawa, nakuja anzaga kula.”



Sharifu kukunja nguo ilimchukua dakika akamaliza akatoka chumbani akasogea hadi kilipo chakula. Alishangaa kumkuta mama yake akimsubiri wakati alimwambia aanze kula





“Si nilikuambia uanze kula, mbona unanisubiri tena ?,” Sharifu aliuliza huku akishangaa kumuona mama yake mikono jinsi ilivyokauka kutokana na kunawa muda mrefu.



“Mwanangu, sijazoea kula peke yangu,” Binti Mngane alijibu huku akiachilia tabasamu.



“Sawa ... lakini mboga ya leo, sijapenda,” Sharifu alisema mara tu baada ya kuona na kuila mboga ile.



“Nitafanyaje? ... muda ulikwenda nikaona mboga nyepesi ni hii.”



“Mboga nyepesi ni mrenda peke yake ... kuna mchicha, matembele kwa nini hujapika hizo ?.”



“Hizo zina utaratibu wake nazo kama vile kuchambua na kuosha lazima zingenichelewesha ... tule, tena huu leo ??nimeupika vizuri,” Binti Mngane alijibu huku akionyesha tabasamu kufurahia mrenda aliokaangiza.



Sharifu hakupendezwa nao mrenda, akala kwa kujilazimisha kwa kuwa palikuwa hakuna mboga nyingine, hivyo hakuna budi kula. Akala kwaajili ya kutuliza njaa tu, walipomaliza kula akatoa vyombo na kuvipeleka mahali koridoni.



“Ukishaweka vyombo njoo, kuna mazungumzo kidogo” alisema Binti Mngane kwa kumhabarisha mwanae.



“Kiukweli, umetahabika sana” alizungumza Binti Mngane mara baada ya mwanae kurudi ukumbini mara baada ya kuweka vyombo.



“Sanaaa ... mpaka sasa nishachoshwa na hayo matahabiko.”



“Kama ulishachoshwa mimi leo kuna kitu nahitaji nikuambie ... upo tayari ?.”



“Kitu gani hicho mama ?.”



“Si unahitaji mafanikio, sasa presha yako ya nini ?.”



“Lazima niwe na presha, kwa kuwa kitu chenyewe sikijui unachotaka kuniambia.”



“Ondoa shaka ... nitakuambia.”



“Sawa nakusikiliza, niambie nipate kujua hicho kitu.”



“Lakini si unania kweli ya kufanikiwa ?.”



“Ndiyo ... nahitaji kufanikiwa leo hata kesho.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kwasasa ushakua mkubwa na hali ya kijijini ushaiona ... vijana wengi hapa kijijini wamepata mafanikio kwa haraka wewe hushangai hilo.”



“Naliona hilo na nashangaa ... ila bado sijakuelewa unamaanisha nini?” aliuliza Sharifu ili apate kuelewa mama yake anataka kuzungumza nini.



“Ninachomaanisha, nitakuambia,” Binti Mngane alimeza mate kidogo kisha akauliza.



“Ila una moyo ?.”



“Moyo ninao ... niambie.”



“Kama una moyo vizuri, sasa nisikilize kwa makini.”



“Eeeeh !.”



“Vijana wenzako hapa kijijini, wanafanikiwa kwa kitu hiki kimoja tu ambacho ni ...,” Binti Mngane kabla ya kuendelea kuongea akapaliwa akakohoa mfululizo hatimaye akaendelea kuongea.



“Ambacho ni uchawi, sasa wewe upo tayari kujiunga na uchawi ?.”



Sharifu alichoambiwa na mama yake kilimshangaza sana, hakuamini akafikiri kuwa labda ni mzaha hivyo akabaki akicheka sana.



“Unacheka nini ?,” Binti Mngane aliuliza huku akikunja ndita kwa hasira.



“Nimefurahi tu.”



“Kilichokufurahisha ni nini eti ?.”



“Ujue sijakuelewa ... hivi unatania au unaniambia kweli ?.”



“Kuna muda wa matani na usio wa matani, haya ninayokuambia hapa ni kweli hakuna utani wowote.”



“Kabisa!?.”



“Eeenh !.”



“Ujue mama unanichanganya kiukweli.”



“Kivipi ?.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mimi na uchawi wapi na wapi ?.”



“Kwa hiyo unataka kusema unataka kuendelea kuteseka ... si ndiyo ?.”



“Sihitaji.”



“Kumbe ?.”



“Sio mzoefu pia naogopa mno kuwa mchawi, kwa sababu ni aibu kubwa katika jamii kujihusisha na masuala kama hayo.”



“Sijaona hapo kinachokuogopesha ... unajitakia kuteseka kumbe mwenyewe.”



“Lakini mama mbona naona kama unaning'ang'aniza unaona huko kuzuri. MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI ...... sitaki kabisa kama mafanikio yenyewe yanapatikana hivyo, bora nife nikiwa maskini tu. ”



“Nani alikuambia huko ni kubaya ?, kuwa mjinga ... utabaki kuwasindikiza vijana wenzako hadi mwisho wa dunia,” Binti Mngane alisema kwa hasira huku akinyanyuka kwenye mkeka kama ugomvi na mashavu kutunisha kama Panya buku akaingia chumbani.



Sharifu naye akaingia chumbani kwake kwa kuona mama yake kaondoka kakasirika na kumwacha peke yake ukumbini. Alipofika kitandani usingizi haukuja kabisa alikuwa bado anafikiria maneno aliyoambiwa na mama yake. Akawaza na kuwazua mara mbili mbili ndipo akagundua anayosema mama yake yana ukweli mtupu baada ya kukumbuka baadhi ya vijana wenzake waliofanikiwa pale kijijini. Sharifu kadri anavyozidi kukumbuka wivu unamshika anatamani leo kesho aweze kufanikiwa.



“Bora, nikubali tu,” Sharifu alijiwazia moyoni huku akipinduka pinduka kitandani kwa kukosa hata lepe la usingizi.



“Lakini hata nikikubali ... uchawi huo nitaupata wapi?” alijiuliza Sharifu kwa kutokujua mama yake kama yupo kwenye chama cha uchawi.



“Lakini potelea pote ............ Mama nahisi atakuwa anapajua. Ngoja nitamuuliza, ikiwezekana nijiunge. ”



Unaambiwa hakuna mkate mgumu mbele ya chai na hakuna Bausa yeyote mbele ya usingizi. Sharifu usingizi ukamnyong'onyesha akawa mpole hatimaye akapitiwa na usingizi. Kesho yake akaamka mapema akatoka nje alipofika nje akakutana na mama yake ukumbini akamsalimu lakini cha ajabu mama yake hakujibu ile salamu.



“Ina maana mama, yaani kitu kidogo tu umeninunia hivyo ?,” Sharifu akauliza.



“Umenishangaza sana yaani nafanya kwa faida yako, lakini wewe unaniona kama hayawani .... Sasa endelea kutahabika maana ndiyo hali uliyoichagua” aliongea Binti Mngane kwa sauti iliyojaa ukali.





“Mimi na wewe hatuna ugomvi ... vitu hivi ni vya kueleweshana tu.”



“Nikueleweshe mara ngapi ... wewe kama umeamua kukataa mpango wako.”



“Jana mimi sikufikiri vizuri ... ila kwasasa nishafikiria na nishaona umuhimu wa kujiunga.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sijakuelewa bado ... unataka kusema nini?” aliuliza Binti Mngane kwa kujifanya aelewi anachotaka kusema mwanae.



“Nimekubali, kuingia katika uchawi.”



“Vizuri sana ... sasa ushakua mkubwa yakupasa uwe mjasiri sio unakuwa mbabaishaji.”



“Lakini mama, huo uchawi nitaupata wapi ?,” Sharifu akauliza.



“Kwa kuupata usijali, niachie mimi nitashughulikia kila kitu.”



“Bado sijakuelewa hapo, unasema nikuachie wewe ... je wewe utaupataje ?.”



“Ondoa shaka ... leo usiku jiandae nitakuja kukuchukua.”



“Tunaenda, wapi ?.”



“Unapopatikana, uchawi.”



“Wewe, unapajua ulipo ?.”



“Nimekuambia ondoa shaka ... wewe si nia yako kupata uchawi sasa tatizo lako ni nini ?.”



“Sawa,” Sharifu alikubali kwa kuona jinsi na yeye lengo lake la kupata mafanikio ataweza kulifikia.



Sharifu baada ya mazungumzo na mama yake akatoka nje kufagia banda la kuku. Akafagia na hatimaye akarudi ndani kuandaa chai kisha wakanywa kwa pamoja na mama yake. Walipomaliza kunywa chai Sharifu akaaga anakwenda shamba akashika njia ya kuelekea shamba. Alipofika shamba akachukua jembe akaanza kulima akalipiga jembe mpaka kijua cha saa kumi kilipoanza kuzama ndipo naye akarejea nyumbani. Aliporudi nyumbani akamkuta mama yake anaunga mbaazi akatoa salamu kisha akaingia chumbani kujibadili akaoge, akatoka amevaa taulo na mkononi kashika ndoo ya uani. Sharifu akateka maji na kwenda kuoga wakati alipomaliza kuoga akaingia chumbani kujibadili mavazi, alijibadili kisha akaenda kuketi ukumbini kwenye mkeka akisubiri chakula cha usiku ili ale apumzike. Masaa matatu yalipita chakula kikaivishwa na tayari kwa kuliwa. Walipomaliza kula Sharifu akatoa vyombo akaingia ndani kujipumzisha. Binti Mngane akaosha vyombo na kuingia chumbani naye kulala, yapata saa nane ya usiku Binti Mngane kama alivyoahidi akanyanyuka kitandani papo hapo akabadilika sura ikawa na unga mweupe. Kwa upande wa mavazi akabadilika akawa amejifunga kiremba cheusi kichwani, kifuani na kiunoni kwaajili ya kumstili maeneo nyeti. Alipohakikisha yupo tayari akatoka chumbani akaelekea kwenye chumba cha mwanae. Alipofika akamkuta mwanae bado kalala, akachukua roho ya mwanae na mwili akabakisha pale pale kitandani. Baadaye akatokea kimiujiza kwenye mbuyu mkubwa uliokuwa na aina mbalimbali ya vitisho. Binti Mngane akashika roho ya mwanae kwa ngangari mara baada ya kuliangalia lile eneo kwa undani. Hazikupita dakika nyingi akaona baadhi ya wachawi wenzake wakiwa kwenye nyuso za kutisha, akafumbua macho ya mwanae apate kuona wanachama wenzake. Sharifu akafumbua macho aliogopa sana akapepesa macho yake kwa hofu kubwa kwa kuangalia na kuvuta picha ya kila mahali kama ataweza kupafahamu pale. Kumbukumbu zikapotea, akazidi kupitisha macho kwa kila mchawi labda ataweza kumjua yoyote lakini wapi. Hakuweza kuwatambua wale wachawi zaidi ya mama yake tu, wakati akiwa anashangaa shangaa hovyo kwa hofu ikasikika sauti ya mama yake ikisema;



“Usiogope, hapa ndipo pahala sahihi kwako.”



“Naona Binti Mngane, leo umetuletea mwanao ... sijakuelewa umemleta mwanao ili iweje atolewe kafara au laah ?,” Mzee Damanda ambaye ni mkuu wa wachawi kama inavyojulikana kwa shirika la kichawi akaingilia mazungumzo ya Binti Mnguli nawan



“Hapana, sijaja kumtoa kafara ila nimekuja ili ajiunge nasi,” Binti Mngane akajibu.



“Una uhakika mwanao ataweza kuungana nasi ?,” Mzee Damanda aliuliza kwa kutoamini kama Sharifu ataweza uchawi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kuweza naamini anaweza, naomba tumsaidie ili aweze kuwa mwanachama imara,” Binti Mngane aliomba kwa unyenyekevu ili mtoto wake aweze kupata kibali cha kukubaliwa.



“Mimi kama Mzee Damanda nimekuelewa .... Wanachama wenzangu nanyi mnasemaje ?,” Mzee Damanda alisema akageuka kwa wanachama wenzake na akawauliza.



“Sisi kama wanachama wenzake tunapenda kusikia hivyo, maana vijana ndiyo wanahitajika haswaa kwenye chama chetu,” Mama Kitenya ambaye ni miongoni wa mmoja wa wachawi akasema.



Mzee Damanda alipoona wachawi wamekubaliana kujiunga kwa Sharifu katika chama chao. Akamkabidhi mavazi na zana za kichawi Sharifu ukiwemo usongo mweusi, kaniki nyeusi, pembe la ng'ombe na usinga kisha akachanjwa chale maeneo husika kama kwenye paji la uso kifuani na mgongoni.



“Ushakuwa mwenzetu ni vyema ukazijua sheria zetu ... sheria zetu ni hizi yakupasa uzishike hutakiwi kusaliti chama, kutoa siri za chama na kumjaribu mwanachama mwenzako pia yakupasa uhudhurie kila siku ya kilinge,” Mzee Awaka kacha lake.



Mzee Damanda baada ya kumwapisha Sharifu kuwa mwanachama rasmi akahitimisha kikao. Sharifu tokea siku hiyo akawa mchawi aliyekubuu, siku inayofuata usiku wa saa sita Sharifu akaelekea shambani kufukia kichwa cha paka kwaajili ya kukinga shamba kama alivyoagizwa. Msomaji tatizo hili watu linawakuta katika maisha unakuta unafanya kazi kwa bidii lakini unaona mambo hayaendi. Mara nyingi huwa kuna watu wasiopenda maendeleo ya wengine hao hufanya juu chini ili waweke vipingamizi watu wasifanikiwe. Upande wa Sharifu kinga ikamsaidia kiasi zilipita siku kadhaa akatokea mzee mmoja akaenda kwenye shamba la Sharifu kutenda uchawi hakujua kama Sharifu ameweka kinga.



“Huyu mtoto, kumbe ni mshenzi ... mbona sioni shamba lake,” Mzee yule alijiongelea moyoni huku akitafuta njia ya kuondoka mara baada ya kushindwa kufanya jambo lililomleta.



Alipobahatika kuona njia akapotea kimiujiza mashambani. Asubuhi Sharifu akaagizwa na mama yake sukari akapita njia iliyokaribu na nyumba ya mzee yule aliyeshindwa kutenda uchawi shamba lake. Mzee yule alimkuta nje ya nyumba yake akipunga upepo Sharifu hakusita kutoa salamu.



“Shikamoo” alitoa salamu Sharifu kisha akasimama njiani kusubiri ajibiwe salamu.



“Ingekuwa mali, ungeenda kumpa baba yako,” Mzee yule aliongea akanyamaza kidogo kuongea akafikicha macho yaliyokuwa yakifukuta kwa kuwasha kisha akaendelea kuzungumza.



“Yaani nusu uniue, ebu ... nitokee mbele yangu” alifoka Mzee yule kwa hasira.



Sharifu hakuelewa alichozungumza mzee yule akaamua kuondoka huku akitabasamu. Alipofika dukani akanunua sukari akarudi nyumbani na kumkuta mama yake yupo jikoni akingojea sukari. Binti Mngane akakabidhiwa kifuko cha sukari na mwanae. Alipokea akaweka kiasi kwenye uji na nyingine akamtuma mwanae aweke kwenye bobo. Sharifu akaweka sukari ndani ya bobo kisha akaketi kwenye mlango wa jikoni akisubiri kifungua kinywa ndipo hapo uvumilivu ukamshinda japo hakutaka kusema ikabidi tu amweleze mama yake.



“Mzee Kaoneka ananishangaza.”



“Anakushangaza na nini ?,” Binti Mngane akauliza.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Wakati naenda dukani nilimkuta yupo nje ya nyumba yake amekaa akipunga upepo.”



“Kakufanyaje?” aliuliza Binti Mngane kwa kutaka kujua kwa kina.



“Si nilitoa salamu, alichonijibu sikutegemea kabisa.”



“Kajibuje ?,” Binti Mngane akauliza.



“Kaniambia salamu yangu ingekuwa mali, ningeenda kumpa baba yangu.”



“Kwanini, kasema hivyo ?.”



“Mimi mwenyewe, sijamwelewa kwa nini kanijibu vile.”



“Kuna kitu kibaya umemfanyia au uliwahi kumfanyia ?,” Binti Mngane alizidi kuuliza.



“Hapana ... sijawahi hata siku moja kumjibu vibaya,” Sharifu alijibu akanyamaza kidogo kwa kuona mama yake yupo bize na kukoroga uji.



“Mbona umenyamaza? ... endelea nakusikiliza,” Binti Mngane akauliza na kusema.



“Mzee yule hakuishia hapo, aliniambia kuwa jana nusu nimuue na akanifurumusha nitoke,” Sharifu aliendelea kuongea mara baada ya kupewa ruhusa na mama yake.



“Mzee Kaoneka, itakuwa ni adui yako namba moja haiwezekani akuambie maneno kama hayo angali hujamfanya chochote” alisema Binti Mngane kwa msisitizo.



Sharifu akaumia sana moyoni kusikia vile na akajiwekea nadhiri ya kumuonyesha Mzee Kaoneka kuwa naye anazo nguvu za giza. Nyakati za mchana akatimiza dhamira yake akaenda kimiujiza kwa Mzee Kaoneka akamkuta Mzee Kaoneka ukumbini akisoma gazeti lake la MWANANCHI.



“Mzee ulijua siku hizi mimi wakujaribiwa?” aliuliza Sharifu kwa hasira.



“Hapana mjukuu wangu ... kwani kuna nini ?,” Mzee Kaoneka kwa kujifanya kama hajui chochote akauliza.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sharifu hakumsikiliza wala hakumjibu Mzee Kaoneka akaona kama anacheleweshwa muda. Akajiwekea asilimia mia kuwa Mzee Kaoneka ndiye adui yake namba moja hivyo hakumuonea huruma hata kidogo. Roho mbaya ikamwingia akamsotea kichwani Mzee Kaoneka kwa makalio akainua mikono yake juu kikatokea kisu na kuku mweusi mikononi mwake. Akamchinja Kuku yule na Kuku papo hapo alivyomalizwa kuchinjwa Mzee Kaoneka akakata roho na kuaga dunia. Sharifu mara baada ya kumaliza tukio la mauaji akapotea ghafla kimiujiza. ”







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog