Simulizi : Tropea Mji Wa Wafu
Sehemu Ya Pili (2)
Ilikuwa ni kisa kifupi mzee Ndole alichokuwa akiwasimulia vijana wale pale kijiweni, kisa ambacho kiliwaacha midomo wazi vijana hao.
"Sawa mzee lakini bado hatujaona sababu inayotufanya tusimsaidie kijana mwenzetu" Alisema kijana mmoja. Mzee Ndole alishusha pumzi huku akionekana anataka kusema jambo, lakini kabla hajasema chochote kijana wa pili aliongeza kusema "Na je, hayo mambo ya Tropea umeyajuaje? Ama na wewe ulikuwa huko?.."
"Naam! Kabisa maswali yenu mazuri." Alisema mzee Ndole kisha akaendelea kusimulia kisa hicho cha kusisimua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada kumalizika kwa tendo hilo,tayari upande wa pili Duniani kila kitu kilikuwa kimeshakamilika, na mwili wa Noela ulikuwa kwenye machela ukipelekwa kuzikwa. Lakini kabla haujafikishwa kwenye kaburini, ghafla Noela akawa amekohoa. Ni jambo ambalo liliwashangaza watu, kwa maana hiyo Noela alikuwa ameshatoka Tropea, hivyo nafsi yake ukauvaa mwili wake, kitendo ambacho kilipelekea kuzinduka. Ila endapo kama angelizidi kukataa kufanya jambo lile, basi Noela angelikuwa marehemu mpaka sasa.
Siku zilisonga miezi ikasogea, hatimaye Noela akapata ujauzito na akajifungua mtoto ambaye ndio Bingo. Bingo sio damu ya mzee Abacha, Bingo ni mtoto wa sultani wa Tropea mumiliki wa ngome ya Abid huko Tropea. Na ndio maana mtoto yule begani ana muhuri. Na vile vile kuhusu mimi kufahamu hayo ni sababu nilikuwa na ukaribu sana mama Bingo, hivyo aliniambia yote yaliyotokea huko. Noela hakunificha kitu, na magonjwa hayo anayoumwa ni shauri ya kukaidi masharti aliyopewa Tropea. Aliambiwa pindi mtoto atakapo zaliwa arudi tena Tropea, lakini Noela hakufanya hivyo japo hapo awali ndoa yake ilitulia kabla haijaharibika tena baada mzee Abacha kuchoshwa na maradhi yaliyomkuta Noela. Maradhi ambayo yalisababishwa kwa kuyakaidi masharti.
"Laah kweli Dunia ina mambo" Alisema moja wa vijana pale kilingeni. Muda huo huo mzee Ndole aliongeza kusema "Kwa hiyo basi, vijana wangu chonde chonde msije mkaivalia Shera harusi isiyo wahusu. Nina mengi sana ya kuhumusu mama Bingo ila sitotaka kuwaeleza yote" Kwisha kusema hayo, mzee Ndole aliondoka zake. Kimuonekano ni mzee ambaye alikuwa hovyo sana, katu mtu asingeliweza kukaa naye na kuzungumza jambo lolote. Lakini leo hii vijana hao wanajikuta wakipata mkasa mfupi unao muhusu mama Bingo. Na sio hao tu walioweza kufahamu hayo mambo, bali Bingo naye alijua ukweli. Kwan wakati mzee Ndole anayasimulia masuala hayo Bingo alikuwa kajificha nyuma ya kibanda,muda huo alikuwa amefuata chai ya tangawizi ili achachue mdomo lakini baada kukuta Ndole akiyasema maneno hayo ilimbidi ajifiche kando ili afahamu ukweli.
Naam! Hatimaye Bingo anapata kufahamu ukweli, alipojitazama kwenye bega akaona ile Alama aliyosema mzee Ndelo. "Mungu wangu" Alijisemea Bingo hata asiamini macho yake. Wakati huo akiwa katika hali ya taharuki mara ghafla nyuma yake aliguswa bega,bega lile lenye Alama. Bingo alishtuka kisha akageuka kumtazama mtu aliyemgusa,akakutana uso kwa uso na yule msichana aliyeitwa Roya. Kwa mara ya pili Roya anamtokea Bingo, jambo hilo kilimtia mashaka Bingo. Hapo ndipo kwa sauti kali akamuuliza "Wewe ni nani na unataka nini?.." Roya akacheka sana kisha akajibu "Mimi ni Roya,nipo hapa kwa nia njema. Nayo ni kukupa muongozo wa Kufika Tropea ili ufike mahali ilipo dawa ya kumtibia mama yako" Alisema Roya, na punde si punde akaangua kicheko kisha akapotea..
Kitendo hicho kilimuogopesha sana Bingo, haraka sana akatimua mbio kurudi nyumbani kwao. Alipofika alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwa mama yake, huko aliketi kando yake kisha akasema "Mama, mimi ni mtoto wa wa nani? Nataka uniambie ukweli pasipo kunificha" Alitaka kujua ukweli Bingo. Maneno hayo aliyoyasema yalimfanya mama yake kumgeukia akiwa pale pale kitandani kisha akamuuliza "Kwanini unasema hivyo? Ama kwa kuwa baba yako ameamua kututelekeza?.."
"Si hivyo mama, Hivi Tropea ni wapi?.." Aliongezea kuhoji Bingo, swali hilo lilimuweka katika wakati mgumu mama yake, kiasi kwamba akashindwa kujua mwanaye maneno hayo kayatoa wapi. Kwa sauti ya chini kabisa mama huyo alisema "Bingo mwanangu, ni safari ndefu sana lakini kwa sasa bado mapema kufahamu ukweli ila siku yoyote nitakukwambia"
"Nini? Sio vizuri mama. Ni vile hujui tu ni tabu gani mwanao naipata, ila laiti kama ungeijua basi ungeniambia ukweli ili nikachukua mamuuzi yaliyo sahihi" Alifoka Bingo.
"Mamuuzi gani? Na tabu gani ambayo unaipata? Na jina hilo umelisikia wapi? Bingo hali yangu yenyewe hii lakini bado unataka kuniweka roho juu, kwanini lakini?.." Alisema mama Bingo akimuasa mwanaye ambaye alionekana kughazibishwa na jambo hilo la siri aliyonayo. Hapo Bingo hakusema jambo lolote, zaidi alinyanyuka na kisha kuondoka zake. Na kwa kuwa tayari usiku ulikuwa umeingia, hivyo alifanya maandalizi kwa niaba ya chakula cha usiku. Muda wa kula ulipowadia Bingo alikuwa kimya,aliongea tu wakati anaelekea chumbani kwake kulala. Usiku wakati yupo usingizini kwa mara nyingine tena alitoa ndoto ya ajabu sana, aliota kuwa yupo makaburini saa za usiku. Ghafla aliona jeneza likiwa juu likiletwa mahali alipokuwa amesimama huku akiwa na hofu kali,mwili wake ukitetemeka hali ya kuwa kijasho chembamba nacho kikimtoka.
Watu wale waliolibeba jeneza walizidi kumsogelea Bingo, ajabu walipomkaribia wakapotea na punde si punde mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi za hapa na pale ilianza kunyesha. Bingo alizidi kuogopa, muda huo hajui wapi pa kukimbilia, hivyo alibaki kusimama akisubiri nini hatma yake. Mbele yake lilionekana kaburi, kaburi ambalo lilionyesha kuwa ni lazamani sana. Kaburi hilo ghafla likaanza kutikisika, muda mchache baadaye ulitokea mkono hivyo hivyo mpaka mwili wote ukawa kwenye uso wa dunia.
"Mungu wangu" Alisema Bingo huku akirudi nyuma akimuogopa yule mtu aliyefufuka. Lakini wakati anarudi nyuma, bado mambo yakawa ni yale yale, wafu waliendelea kufufuka. Ndani ya nusu saa mamia ya wafu walionekana pale makaburini. "Bingo.." Ilisikika sauti nzito ya ajabu ambayo ilijirudia mara mbili mbili. Sauti hiyo ilimuita Bingo. Bingo kutokana na woga pia na hofu aliyokuwa nayo aliogopa kuitika. Alibaki kurudi nyuma tu ilihali wale wafu nao wakimfuata, punde hatua zake zilifika ukingoni. Kuna kitu alikigusa nyuma kwa kisigino, hivyo akageuka nyuma ili atazame kitu hicho, aliona jeneza lile ambalo hapo awali aliliona likiwa limebebwa na watu kabla hawajapotea katika mazingira tatanishi. Na ndani ya jeneza hilo Bingo aliuona mwili wake, kitu hicho kilizidi kumuogopesha Bingo akajikuta akakimbia huku na kule kama mwenda wazimu. Lakini mwishowe alijikuta akiwa katikati ya kundi lile la wafu, ajabu katika wafu wale alikuwemo na mfu ambaye alifanana naye kila kitu achilia mwili ule alioona kwenye jeneza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bingo, wewe ndio mrithi wa ngome ya Abdy. Hivyo jiandae wakati kuelekea Tropea sababu wewe ni damu yetu" Maneno hayo aliyasema yule mfu ambaye alifanana na Bingo, ambapo alipokwisha kusema hivyo wafu wale wengine walipotea akabaki mwenye. Aliongeza kusema "Sifikirii kama utakwepa njia hii ya Kufika Tropea, lakini pia Kufika kwako huko sio kama ndio utakuwa mwisho wa maisha yako hapa duniani. Tambua hata sisi tulikuwa kama wewe" Alisema mtu huyo aliyefanana na Bingo.
"Kwanini mnanifuatilia sana? Na hiyo ngome ya Abdy inanihusu nini mimi?.." Aliuliza Bingo kwa sauti ya woga. Ajabu mtu huyo aliangua kicheko, cheko ambalo lilisikika likijirudia mara mbili mbili. Baada kuhitimisha kicheko hicho akasema "Abdy, hii ni ngome tata sana iishio Tropea. Tropea huu ni mji ambao watu wake ni wafu. Hivyo basi kuna mgongano baina ya ngome hiyo na ngome ya Buda. Hizi ni ngome mbili tofauti ingawa zote wafuasi wake ni wafu,. Mtoto wa Sultan Starlon anataka kumiliki ngome zote mbili ikiwemo ya baba yake lakini pia ngome ya baba yako Sultan Abatish ambaye tayari ni mzee. Kupitia hilo Batish ameamua kutuma watu wake waje kukutafuta wewe binadamu mwenye asiri ya Abdy ili ukaiokomboe ngome ya baba yako.. "
" Je, hakuna mtu mwingine mpaka mimi?.. "Aliuliza tena Bingo kwa taharuki kubwa akitishwa na maneno hayo aliyoyasema mtu huyo aliyefanana naye. Kabla mtu huyo hajamjibu, Bingo aliongeza kusema" Hamuoni kama mimi nipo katika harakati za kumlea mama yangu kipenzi ambaye yapata miaka mingi akiwa mgonjwa?.. "
" Ahahahahaha "Alicheka mtu huyo kwa mara nyingine tena. Kwisha kuhitimisha kicheko chake akasema" Unataka mama yako arudi katika hali yake?.. Basi Kama utamani iwe hivyo karibu Tropea, njoo uokoe ngome ya Abatish ili mama yako awe huru sasa.. "Alisisitiza mtu huyo kisha akanyong'onyea na punde si punde akageuka nyoka akaishia zake. Hapo Bingo akashtuka kutoka usingizini huku akihema juu juu wakati huo huo maneno yale alivyoambiwa na yule mtu kwenye ndoto yalijirudia.
" Unataka mama yako arudi katika hali yake?.. Basi Kama utamani iwe hivyo karibu Tropea, njoo uokoe ngome ya Abatish kisha mama yako awe huru sasa.. " Maneno hayo yalijirudia mara mbili mbili kichwani mwake. Akakumbuka pia maneno yale aliyoambiwa na yule ajuza wa ajabu kwenye ndoto mara baada kumuelezea habari kuhusu upatikanaji wa dawa itakayo mfanya mama yake kupona. Na hivyo ajuza huyo akawa amemjibu
"Ipo Tropea! Mji uishio wafu itakulazimu ufe ili Kufika huko"
Punde usingizi ulimpotea kijana Bingo, ndoto hiyo aliyoota kwa mara nyingine tena ilimuogopesha. Akajikuta anashindwa kuelewa afuate kipi, na ninani mkweli kwa maana Ajuza yule wa ajabu alimwambia afuate dawa Tropea hali ya kuwa mtu yule aleyemtokea ndotoni alimwambia aende Tropea kuokoa ngome ya Abdy, ngome ambayo mtoto wa Sultan Starlon anataka kujimilikisha zote. Ngome ya baba yake ambayo ni Buda, lakini pia ngome ya Sultan Abatish. Abatishi aliona tayari anakwenda kupoteza umwamba wake katika mji huo, nguvu za kupigana zilikuwa zimeshamtupa mkono kwa sababu uzee ulikuwa umeshashika kasi katika mwili wake na ndio sababu ya kutuma watu wake waje duniani kuitafuta damu yake ili akakomboe ngome hiyo ili Zama zisipotee. Pumzi ndefu alishusha kijana Bingo, katu usingizi haikuweza kumjia kwa haraka zaidi ya kutafakari mara mbili mbili safari hiyo ya Tropea. Lakini baadaye kidogo alijilaza kitandani kwa mara nyingine tena na punde si punde usingizi uliweza kumpitia. Kesho yake asubuhi Bingo alifanya shughuli zake kama afanyavyo kila siku kabla ya kwenda kwenye mihangaiko, baada kuhakikisha kila kitu kipo sawa alifunga safari kuelekea nyumbani kwa mzee Ndelo. Mzee ambaye alionyesha anavitu vingi sana anavyovifahamu mama yake lakini pia Bingo alihisi kuwa mzee huyo anaweza kumpa mambo mawili na tatu yanayohusu Tropea.
"Habari mzee" Alisema Bingo mara baada kufika nyumbani kwa mzee Ndelo. Muda huo alimkuta mzee huyo akilisha mifugo yake. Ndelo aliposikia sauti hiyo aligeuka nyuma akawa amekutana uso kwa uso na kijana Bingo, ajabu kilichomshangaza mzee Ndelo ni kumuona Bingo akiwa emedhoofu ilihali uso wake ukionyesha kuwa ni mtu mwenye matatizo chungunzima.
"Aah Bingo?.." Aliachia tabasamu mzee Ndelo kisha akaongeza kusema "Karibu sana"
"Asante sana babu, lakini ujio wangu huu unajambo.."
"Ni kweli hata mimi nafahamu hilo lakini subiri nimalize shughuli yangu hii kisha tuketi ili tuweze kuongea kwa kina zaidi"
"Sawa"
Baada ya shughuli nzima kukamlika hatimaye Bingo na mzee Ndelo waliketi chini, wakaanza kuteta mambo mbali mbali hasa kuhusu mji wa Tropea ambapo Bingo alianza kwa kumueleza Ndelo juu ya ndoto za ajabu anazoota.
"Pole sana kijana, lakini ukweli utabaki kuwa huo. Ni siri nzito uliyonayo Bingo na nilitegemea hapo baadaye utakuja kukusumbua tangu pale mama yako akosee masharti aliyopewa Tropea.." alisema Ndelo. Bingo alishtuka kwa taharuki ya hali ya juu akauliza "Unamaana gani mzee?.." Ndelo aliangua kicheko kidogo halafu akajibu "Nitakwambia Bingo, lakini pindi utakapo jua huu ukweli haraka sana fanya mamuuzi yaliyo sahihi. Bingo, tazama kwenye bega lako" Bingo alitazama, aliiona halama kwenye bega lake. Bado alionyesha kutokuwa na sintofahamu na hivyo alirudia kuhoji "Hii ni nini?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndelo akasema "Huu ni muhuri kutoka Tropea, katu chata hii haitoweza kufutika sababu wewe ni mtoto kutoka ngome ya Abdy.."Alipokwisha kusema hivyo alimsimulia moja kwa moja na kisa kile kilichomkuta mama yake mpaka Kufika hali hiyo, kwa mara nyingine tena Bingo akaisikia simulizi hiyo ukiachilia mbali ile aliyosikia mwanzo akiwa mafichoni. Hakika ilimshtua sana Bingo, hofu ilimjaa huku maswali kibao akijiuliza kichwani mwake.
"Kwahiyo nifanye nini sasa mzee wangu, sababu ndoto hizi zinanikosesha amani kabisa. Sipati usingizi, na hata nikipata sisinzii kwa muda unatakiwa. Nisaidie tafadhali" Akionekana kuwa na majonzi usoni mwake alisema maneno hayo kijana Bingo. Hapo mzee Ndelo alikaa kimya, lakini punde si punde akasema "Njia pekee ya wewe kuepuka mauza uza haya ni kujitoa muhanga wa kuelekea Tropea basi. Eeh tofauti na hivyo utaendelea kusumbuliwa na mwisho wa siku utaangukia pabaya" Alisema mzee Ndelo. Hapo Bingo alikaa kimya katu hakutaka kuongeza neno lolote zaidi ya kujiinamia huku akitafakari safari hiyo nzito ya kuelekea mji wa wafu kwenda kuikomboa ngome ya baba yake lakini vile vile kwa dhumuni la kufuata dawa ya kumtibia mama yake. Mwisho wa yote Bingo alinyanyuka akaondoka zake kichwa chini mikono nyuma akirejea nyumbani, lakini kabla hajafika mbali mzee Ndelo alipasa sauti kumuita Bingo. Bingo aliposikia sauti ya mzee huyo aligeuka nyuma kumtazama. Mzee Ndelo akasema "Nenda Tropea kijana" Kwisha kusema hivyo mzee huyo alizama ndani huku akimuacha Bingo akiambaa na njia ya kuelekea nyumbani kwao.
Akiwa njiani bado akili yake aliipa mzigo mizito sana wa kuifikiria safari ya Tropea, kijana aliona shida kuu si Kufika huko bali ugumu upo katika njia ya Kufika huko. Njia ngumu sana, ni njia ambayo ilimuogopesha Bingo.
"Nife? Mmh mbona kibarua kizito?.." Alijikuta akijisemea hivyo Bingo mara baada kutafakari kwa kina safari hiyo wakati huo akiwa njiani akirudi nyumbani. Ajabu alipokwisha kujisemea hivyo ilisikika sauti nyuma yake ikiangua kicheko "Ahahah ah hahaha" Bingo alishtuka, haraka sana akageuka. Akakutana uso kwa uso na mama yake. "Khaa mama?.." Alitaharuki Bingo huku akirudi nyuma kwa woga. Wakati huo huo mama yake alisema "Bingo mwanangu kwanini hutaki kwenda kuikomboa ngome ya baba yako ambayo ipo shakani? Ama kwanini hutaki kufuata dawa ili mama yako nipone? Bingo mwanangu Bingo tafadhali nenda Tropea" Alisema mama Bingo, Bingo alishtuka, asiamini kile akionacho. Kwa sauti ya mshangao akasema "Mamaaa? Ni wewe?.."
"Ahahahahaha hah hah" Aliangua kicheko mama Bingo kisha akapotea. Hapo sasa Bingo alitimua mbio huku akipiga mayowe. Alipofika ndani alifungua mlango kwa nguvu moja kwa moja mpaka chumbani kwake,huko akapata kukaa na kutuliza hofu. Na wakati yupo katika hali hiyo ya hofu, punde alimsikia mama yake akikoroma chumbani kwake. Hapo Bingo alisimama akiwa ameshika kiuno, mwili nao ukiwa umchoka dhofulihali huku akijiuliza juu ya yule mtu aliyechukua taswira ya mama yake na kisha kumuelezea maneno yale. Mwishowe alishusha pumzi ndefu kisha akazipiga kuingia chumbani kwa mama yake ambapo alimkuta akihema kwa nguvu, jasho nalo lilimtoka kwa wingi. Bingo aliogopa alitoka ndani mbio akaelekea nyumbani kwa mzee Ndelo kuomba msaada.
"Babu mama hali yake ni mbaya sana, tafadhali twende ukanisaidie. Nampenda sana mama yangu" Alisema Bingo kiasi kwa sauti ya juu juu. Mzee Ndelo akajibu "Sawa tangulia nakuja"
"Usikose mzee wangu nipo chini ya miguu yako" Alisisitiza Bingo. Mzee Ndelo aliahdi Kufika bila kukosa.
Ujio wa mzee huyo alifanya kila jitihada walau kupoza hali ile iliyokuwa imemuibukia mama Bingo, hivyo baada kuwa sawa mzee Ndelo alimuita Bingo nje. Bingo alitii wito, na hapo ndipo Ndelo alipomwambia "Bingo, hii hali inaweza kumuondoa dunia mama yako siku yoyote ile endapo kama hutokubali matakwa ya kutakiwa Kufika Tropea. Kijana piga moyo konde, wewe ni mwanaume nenda Tropea, lakini pia nakuhakikishi kuwa kuna mafuta utayapaka mwili mwako, hayo yatakusaidia pindi utakapo wasili mji ule wa wafu.. "
" Mafuta? Mafuta gani hayo?.. "Alihoji Bingo. Mzee Ndelo akaongeza kusema" Niambie kwanza upo tayari?.. "Alikaa kimya kidogo kijana Bingo ila mwishowe alijibu" Ndio nipo tayari.. " Hakika jibu hilo lilimfanya mzee Ndelo kuachia tabasamu bashasha kisha akasema kwa sauti ya upole" Bingo, nakuhakikishi utaenda salama, na utarudi salama pia. Vile vile nakuasa ukirudi kutoka Tropea, basi hautoishi maisha haya. Tropea huu ni mji wa wafu lakini pia unamali nyingi sana. Muhimu usivunje masharti ya huko. Bingo kijana shupavu kesho Tropea...
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jioni sana, yapata saa moja kasoro robo. Kijana BINGO kwa mara nyingine tena anakutakana na mzee Ndelo katika mapanda njia.
"Bingo.."
"Naam! Mzee"
"Kwanza napenda kukupa hongera ya kukubali takwa hili la kuelekea Tropea, vile vile ukiachilia mbali hongera hiyo nataka nikuthibitidhie kuwa tupo pamoja katika safari yako hii ngumu. Hivyo basi chukua mafuta haya. Haya mafuta jipake mwili kabla hujalala, pia chukua maji haya ambayo nayo utakunywa mara tatu. Yani bunda la kwanza bunda la pili mpaka la tatu. Hii ni safari ngumu sana kwako Bingo lakini hupaswi kuogopa sababu woga wako utaweza kukughalimu, yapaswa kupiga moyo konde. "
" Huko maisha utakayo ishi katu usithubutu kufanya mapenzi na mwanamke yoyote, wala usikate chakula utakacho letewa. Pia Bingo kuwa makini, pindi utakapo muona mtu yoyote uliyewahi kumuona Dunia usimpapalikie kujifanya unamfahamu. Kuwa mtu tofauti kabisa na watu utakao wakuta huko ingawa najua kwa vyovyote vile lazima utausudiwa ukiwa kama mtoto wa Sultan"Aliongeza kusema mzee Ndelo wakati huo Bingo akiwa ameshikilia vitu vile aliyopewa ambavyo ni mafuta na maji maalumu aliyoyatengeneza mzee huyo ambaye ni mganga wa jadi.
"Sawa nimekuelewa, na napend kukuahidi kuwa nitafanya kama ulivyo nielekeze" Alisema Bingo.
"Sawa safari njema kijana"
"Ammh vipi Kuhusu mama yangu? Ni nani atamuhudumia?" Kabla Bingo hajaondoka alimuuliza swali hilo mzee Ndelo. Ambapo mzee huyo alijibu kuwa atamsaidia bila tabu yoyote. Bingo alifurahi sana kisha akarejea nyumbani huku akili yake ikifikiria safari ya Tropea. Alipo fika nyumbani alimkuta bibi yake kafika, ujio huo ulimfurahisha sana Bingo kwani alijua tayari kapitakana mtu wa kumlea vilivyo mama yake kwa kipindi hicho atakachokuwa yupo mji wa wafu.
"Karibu sana bibi, habari za siku nyingi" Alisema Bingo akimsabahi bibi yake.
"Ni nzuri, ingawa nimepotea njia mara nyingi ila hatimaye leo nimefika. Umekuwa mkubwa Bingo" Alijibu bibi huyo huku akitupia na utani kidogo, utani ambao ulimpelekea Bingo kuangua kicheko.
Huyo ni Bibi yake Bingo, bibi mzee mama yake. Baada miaka gedegede kupita hatimaye bibi huyo anakuja kumuona mwanaye ambaye ni mama yake Bingo. Alikuwa ni mzee sana, alipata tabu sana kutembea lakini siku hiyo alidhamilia Kufika pasipo kukosa.
"Naam! Safari hii sasa inaonekana itakuwa ya neema kwangu.. Tayari kapatikana mtu wa kubali na mama yangu. Najua hawezi kupata shida pindi bibi atakaposhirikiana na mzee Ndelo. Mungu nitie nguvu" Alijisemea Bingo, muda huo tayari ulikuwa muda wa kulala. Alifanya kama mzee Ndelo aliyomwambia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*********
"Basi nilipojipaka mafua yale, kiukweli mwili uliniwasha. Nikajikuna kila sehemu ya mwili wangu mpaka nikajiuliza ama mzee Ndelo kaniingiza mkenge? Wakati huo najiuliza swali hilo, mikono yangu nilikuwa nikiipeleka kila kona mwili wangu kwa namna mwili ulivyokuwa unawasha. Lakini baadaye kidogo hali hiyo ilipotea ila mwili wangu ulionekana kuvimba manundu. Kitendo hicho sasa kikanifanya kuhofia kuinywa ile dawa, ingawa baadaye nikakata kauli nikajitoa ufahamu nikainjwa dawa hiyo. Baada ya hapo sikujua kilicho endeelea. Muda mchache baadaye niliamka kutoka kitandani,tayari palikuwa pamekucha. Hivyo nilikurupuka nikavaa nguo zangu haraka haraka kisha nikazipiga hatua kuelekea chumbani kwa mama kumjulia hali, ajabu sebuleni nilikutana na jopo la kina mama wakiaonyesha nyuso za huzuni. Nilizidi kupagawa, maswali kibao nikajiuliza kichwani mwangu "Mungu wangu ama mama kafariki?.." Hilo ndilo swali ambalo lilichukua nafasi kubwa ndani ya ubongo wangu, lakini hofu zaidi ilinijaa baada wale wakina mama kutonitazama licha ya kwamba nilikatiza katikati yao, pia mbali na hilo nilisimama kwenye kizingiti cha mlango wa kutoka na kuingilia ndani ambapo Mzee mmoja hivi alifika eneo hilo nililo simama nikamuamkia wala hakuitikia na vile vile alioneakana kuwa busy na hata asijishughulishe na salamu yangu. Ndipo nilipoamua kutoka ndani,nje niliona jeneza, haraka sana nikalisogelea jeneza hilo ili nijue ndani ya jeneza hilo kuna mwili wa nani. Lahaulla. Ni mwili wangu. Millander mke wangu nilishtuka sana kuona mwili wangu ndani ya lile jeneza, na hapo ndipo nilipohisi kuwa sionekani machoni mwa watu.. "
" Enhee baada ya hapo?.. Aliuliza Millander, mkewe Bingo. Akionyesha utulivu wa hali ya juu kusikiliza mkasa huo ambao unampelekea Bingo kila siku usiku wa manane kutoka ndani na kuelekea makaburini huku anaporejea huja akiwa na damu sehemu mbali mbali za mwili wake lakini pia akinukia harufu ya ubani.. Hiyo ni hali ambayo ilimchosha Millander na ndio maana siku hiyo alihitaji kujua kipi hasa kinachomfanya bwana huyo kutenda kitendo hicho? Na kwa kuwa Bingo alimpenda sana mkewe katu hakuweka pangamizi kumpa ukweli harisi. Bingo aliendelea kusimulia.
********
Baada kuona mwili wake ndani ya jeneza alizidi kuogopa, lakini punde tu mzee Ndelo alionekana mbele yake. Mzee huyo alikuwa ameshika koti kubwa jeusi lenye kofia yake, vile vile alikuwa na upanga mkubwa kiasi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Bingo.." mzee Ndelo alipasa sauti kumuita Bingo. Bingo akaitika kwa sauti ya woga wakati huo mzee Ndelo alisema "Usiwe na hofu juu ya haya maombolezo,japo huu ni msiba wako lakini usiwe na tabu yoyote kwani hapo ulipo tayari upo katika mazingira ya kwenda Tropea. Wewe ni nafsi na ule kwenye jeneza ni mwili wako"
"Mzee unamaana gani sasa? Mbona kama sikuelewi?.." Aliuliza Bingo. Mzee Ndelo aliangua kicheko. Alicheka sana kisha kisha akajibu "Ndio. Kwa sasa huwezi kunielewa ila utakapo toka Tropea nafikiri utanielewa. Mwili huu nitahakikisha hauzikwi,nitajua kipi cha kuwa ya ilimladi mwili wako uwepo duniani. Ukisharudi kutoka Tropea, utauvaa na maisha kama kawaida yataendelea"
"Je, unataka kuniambia kwamba kuna madhala endapo kama mwili wangu utazikwa?.."
"Madhala yapo"
"Ni yapi hayo"
"Ni mwanzo na mwisho wa maisha yako" Alijibu Mzee Ndelo, ni jibu ambalo lilimshtua Bingo ilihali muda huo huo mzee huyo aliweza kukumbushia kijana mambo kadhaa ambayo hatakiwi kuyafanya pindi atakapo kanyaga ardhi ya mji wa wafu. Ndelo alisema "Bingo, na kukumbushia kwa mara nyingine tena na tena. Tropea huu ni mji wenye mitego ya kila aina, unavishawishi vya hapa na pale ambavyo usipokuwa navyo makini utajikuta unaishia huko huko. Hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kuwa makini, acha tamaa za wanawake. Usikatae chakula wala kinywaji haijalishi vyakula hivyo ni vya aina gani,aidha vinywaji hivyo ni vyaina gani. We kula, we kunywa tu ili usije ukaonekana tofauti sana na watu wa kule. Ni hayo tu mengine utayajulia huko kwani inavyosemekana ule mji kila baada ya miaka miwili hubadilishwa tamaduni ya namna ya kuishi... "
" Asante sana Babu, hakika sitokuangusha. Nitafika kwenye ngome nitafanya kile kinachotakiwa mpaka pale nitakapo rejea duniani. Ila muhimu tu. Utunze mwili wangu "Mzee Ndelo aliposikia maneno hayo ya Bingo aliachia tabasamu pana kisha akilikunjua koti hilo jeusi akamvisha Bingo lakini pia alimkabidhi na upanga.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Upanga huu ni mahususi kwa kuutumia pindi utakapo kabiliwa na maadui wabaya, najua itakuwa moja ya changamoto kubwa kwako ila pambana usikubali kushindwa kirahisi" Aliongezea kusema mzee Ndelo. Bingo aliukamata upanga huo kimalifu,upanga ambao ulionekana kumelemeta vilivyo. Punde mzee Ndelo alinyoosha mkono juu kisha akashusha, ikatokea wingu jeusi la ajabu likamfunika usoni Bingo, baada ya dakika kadhaa wingu hilo lilitoweka usoni mwa Bingo ambapo alijikuta yupo katika msitu mnene, usitu tulivu pasipo kusikika sauti ya ndege wala mnyama yoyote. Bingo alishtuka sana akashindwa sasa aelekee wapi ndani ya msitu huo. "Ooh Mungu wangu" Alijisemea Bingo akianza kwa kushusha pumzi ilihali muda huo mbele yake anapata kuona watu wanne. Wanaume wenye miili milaba mine. Watu hao walionekana kutisha sana kwa namna walivyoumbika. Kila mmoja alikuwa na masikio makubwa huku macho yao nayo yakishabiliana vema kabisa na macho ya simba. Vile vile, kucha zao za vidole zilikuwa ndefu. Bingo aliogopa sana, pole pole akarudisha mkono wa kulia nyuma ya mgongo wake akitaka kuchomoa upanga uliokuwa kwenye Kala alilolivaa. Lakini kabla hajafanya kitendo hicho, ghafla alisikia sauti nzito. Sauti ambayo ilikuwa ikijirudia mara mbili mbili, sauti hiyo ilisema "Bingooo. Kwa hapo ulipo huwezi kukabiliana na hao viumbe. Tambua hao sio binadamu, hivyo haraka sana kimbia" Bingo aliposikia sauti hiyo alishtuka kisha akainua uso wake kutazama huku na kule na punde si punde akapasa sauti akauliza "Nikimbilie wapi?.." Sauti hiyo ya Bingo iliwafanya wale watu kugeuka upende ule aliokuwa amesimama. Hapo sasa ndipo Bingo alipoogopa zaidi, haraka sana akatimua mbio akipita ndani ya huo msitu huku nyuma wale watu wa ajabu nao walufukuzia nyuma..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bingo alitimua mbio, na kila alipogeuka aliwaona watu wale wakimfuata, hapo sasa purugushani ya maana ikazuka ndani ya msitu huo. Ajabu wale watu baada kukimbia kwa muda mrefu pasipo kufanikiwa hatimaye wakatumia njia ya kuruka mti mmoja baada ya mwingine na sio kukimbia ardhini kama waliyokuwa wakifanya awali.. Waliruka mti mmoja baada ya mwingine wakati huo huo Bingo baada kukimbia kwa muda mrefu hatimaye mbio zake zinaishia ukingoni, mbele alikutana na mporomoko mkubwa wa maji huko chini ikionekana miamba mbali mbali hali ya kuwa nyuma yake wale watu walionekana kuja kwa kasi ya ajabu...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment