Simulizi : Joto La Mshumaa
Sehemu Ya Tatu (3)
Katika eneo moja anaonekana kijana akiwa na Baba yake wakiwa wanaongea, kijana huyo alikuwa anamueleza mzazi huyo kiuwa anahitaji kupata mwanamke wa kumuoa kabisa "baba ukweli siwezi kukuongopea namtafuta mwanamke popote pale alipo ambae ninaweza kumuoa laini siwezi kumchukua mwanamke wa hapa nyumbani kama wewe unavyohitaji". Ndipo mzee huyo alivuta pumzi za kutosha kisha akamshika mwanae bega na kumumbia jambo "Sawa mwanangu ngoja nikuambie kitu kimoja, fahamu kuwa ndani ya kijiji chetu hakuna mtu a,mbae tunamtarajia kuwa atachukua kiti hiki cha uongozi zaidi yako sasa lazima umchukue mwanamke wa hapa kwetu lakini si kwingine zaidi" Kijana huyo hakuweza kabisa kuelewa ndipo alinyanyuka na kuondoka zake pale alipo. Kijiji hiki kinajulikana kwa jina la CHAMLO ambacho kinapatikana umbali mrefu kidogo na vijiji vya KILIMALONDO. Kijna ambae alitarajiwa kuwa kiongozi baada ya mzazi wake kuwa na hali mbaya ya kiafya lakini hakuruhusiwa kuwa kupata nafasi ya uongozi mpaka pale atakapokuwa na mwanamke ambae atakuwa nae na kumsaidia katika kazi zake za uongozi. Alijulikana kwa jina la BAMUZI na baba yake ambae ndie kiongozi wa kijiji cha CHAMLO, alijulikana kwa jina la NGOLOLO, Ndipo kijiji kizima cha chamlo kila mwanamke alipata taarifa ya kuwa mtoto wa kiongozi Ngololo kuwa anatarajia kuwa na mwanamke wa kumuoa ili aruhusiwe kuwa kiongozi. Ndipo kila mwanamke ambae alijihisi kuwa ni mzuri zaidi alianza kujipitisha sehemu ambayo anapatikana kijana BAMUZI. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Majira ya mchana akiwa nyumbani kwake pamoja na vijana wake wa karibu sama aliweza kuwaeleza jambo moja muhimu sana ambalo linamfanya yeye akatae kuoa mwanamke wa pale kijijini kwao. "jamani mnafahamu kwa nini mimi sipendi kuwa na mwanamke yeyote hapa kijijini na nahitaji kwenda mbali ya kijiji hiki ili niweze kupata mwanamke ambae ataniheshimu?" Hawakuweza kumjibu zaidi ya kutikisa mabega kuonyesha kuwa hawafahamu chochote kabisa juu ya hilo na wanamshangaa kwa nini afanye hivyo, "Kiongozi hata mimi nashangaa kwa nini mana unamkataa mpaka msichana mzuri wa hapa kijijini kwetu yule binti wa mzee KILIMBI nani yule NAOMI". Alianza kucheka kwanza Bamuzi kisha ndipo akawaambia "mwanamke yeyote ambae utamuoa akiwa anatoka ndani ya kijiji chako elewa kuwa huyo mwanamke atakuwa msumbufu sana kwa sababu, akili yake yote hatoweza kunisaidia zaidi ya kujionyesha kaolewa na nani tu basi hiko ndiko nisichokifahamu lakini pia katika ndoto zangu sijawahi kumuota mwanamke wa hapa". aliwashangaza sana wenzake ambao walianza kwa kumcheka sana. Moja ya nyumba ndani ya kijiji hiko cha Chamlo alionekana binti mzuri sana akiwa na mama yake wakiongea huku akiwa anajisifia sana "Mama hakika Bamuzi mtoto wa kiongozi wetu mzee Ngololo hakika hana ujanja kabisa atanioa mimi tu au unanionaje mama yangu" Basi alikuwa anajigeuzageuza kama nyama choma au kuku aliyebanikwa na kugeuzwa huku na kule. "mwanangu hakika kwa uzuri uliuo nao Bamuzi hawezi kwenda mbali lakini jitahidi kufanya haya yafuatayo". Binti huyo alishtuka kwanza "yapi hayo tena mama". "Wewe kama mwanamke unabidi upendeze muda wowote na alafu uwe na adabu zaidi ya wanawake wengine pia ujifunze kuwasaidia kazi watu ikiwezekana ukimuona mzee Ngololo heshima yako iwe kubwa zaidi kwani yeye ndie atakayekufanyia mpango mwanae akuoe kwani hapa kijijini hakuna zaidi ya wewe NAOMI mwanagu". Basi Naomi alijikweza kwa uzuri alionao kwa kuamini kuwa mtoto wa Ngololo hatokwenda kokote zaidi ya kwake, na alifikia hatua ya kuwatambia wenzake ambao nao walikuwa wanawania nafasi ya kuwa na kijana huyo. Siku moja ilipofika wazee wapale kijijini Chamlo walikaa kama faragha na bwana Ngololo kumueleza jambo fulani. Swala kubwa amablo waliweza kugusia swala la mwanae amefikia wapi mpango wa yeye kuoa. "Haya kiongozi wetu tupatie habari mwanao kaamua nini kuhusu mwanamke?". Walitulia wakisubiria jawabu nzuri kutoka kwa mzee wa busara ambae huwa wanamtumia sana katika kutatua matatizo ya pale kijijini. "Nashukuru sana kwa kuniita na kuniuliza kwa maswali kama hayo, kwanza mwanangu nimemlea kwa mambo muhimu mengi sana ikiwemo na kutii amri ya mzazi pamoja na mtu aliyempita umri, kwa hiyo basi nimemuelza kanikubalia kuwa yuko tayari kumvchagua binti ambaye atakuwa mchumba wake na harakati za yeye kuwa kiongozi zitaanzia pale tu baada ya ndoa kupita". Walianza kufurahi kwa nguvu sana kwani jambo ambalo walilitarajia kuwa litafanikiwa basi limetimia vile watakavyo. "Basi itatakiwa iandaliwe siku maalumu sana ambayo itakuwa hatua nzuri ya yeye kuwaeleza wanawake wote na watu wote wa kijiji cha Chamlo kuwa fulani ndie atakaechaguliwa kuwa mchumba wake". Mzee Ngololo alikubali na aliomba aitwe kwanza Bamuzi ili athibitishe kama yuko tayari kwa jambo hilo. Bamuzi aliitwa na alifanikiwa kufika pale, alishangaa kuwaona wazee muhimu sana na ambao atakuwa nao endapo siku anakabidhiwa kuwa kiongozi rasmi wao ndio ambao watamsaidia sana katika kumuandalia mambo mengi na kumshauri zaidi. Jambo ambalo alielezwa pale lilimstaajabisha sana lakini alishindwa kukataa kutokana na heshima ya wao wazee, alifikilia sana kisha akasema yuko tayari na kamuandaa atamtaja siku hiyo, "Sawa wazee nimewaelewa lakini nataka kesho iandaliwe sherehe ambayo itakesha usiku mzima alafu kuamkia asubuhi ndipo watu wote wakusanywe na mimi nimchague huyo mwanamke". Jambo aliloliongea hapakuwa na mtu ambae alikaidi zaidi ya wao kukubaliana na hali ile kwani sio baya kwao na upande wa kijiji kizima kwani linaingiliana na furaha kubwa ambayo inakuja mbele yao. Taarifa zilifika na kijana mmoja maarufu sana katika utangazaji wa taarifa zozote zinazohitaji watu wazisikie na kuzifanyia kazi. ""Lmgambooooo....lamgambooo....likilia linajambo.. wanakijiji wooote wa CHAMLO mnahitajika leo mjiandae kwa vinywaji na ngoma kwa ajili ya kusherehekea kwa mtoto wa kiongozi kukubali kumchagua binti mmoja ambae atamiuoa ili na yeye akabidhiwe rasmi mikoba ya baba yake Ngololo, kesho utakuwepo mkesha pamoja wote na asubuhi mabinti wotee mjitokeze ili ajulikane nani ambae atapata nafasi hiyo tafadhali ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio" Wwatu walifurahi sana na wakaona kama bahati imewaangukia wao, kwa upande wa binti NAOMI hakuwa na tabu kabisa kwani alijitia imani kuwa hakuna zaidi yake. Majira hayo ya Asubuhi na map[ema ambapo maandalizi yanafanyika, huku upande wa kijiji cha KILIMALONDO mzee KAUZIBE kutokana na dhamira yake ya kumteka binti LYOTO bado iliendelea ndipo Lyoto alifanikiwa kumuonaakimnyemelea, alisimama na kuanza kukimbia sehemu ambako hapafahamu binti wa watu, Mzee Kauzibe alimsii sana asikimbie kwani atamuua kwa mshale alionao kwa muda ule, mzee hiuyo alizidi kumkimbiza lakini Lyoto alikimbia zaidi yake kwa bahati mbaya sana aliangukia kwenye korongo kubwa sana ambalo ni ngumu kuona chini zaidi ya mingurumo ya maji yaendayo kwa kasi kusikika yakisukumana. Mzee Kauzibe alishtuka baada ya kuona kuwa tayari kasababisha mauaji kwa binti wawatu, "jamani wewe binti si ungesimama tu jamani, mpaka unaangukia humo kwenye korongo, sikuwa na nia mbaya na wewe ooooh! pole sana binti Lyoto pumzika salama kabisa". Alirudi kidogokidogo huku akishika mikono yake na kuiweka kwenye kichwa chake huku akionyesha kuwa ana wasiwasi na lile swala ambalo limetokea kwa muda ule. Alikuwa anatetemeka mzee Kauzibe . Ndani ya kijiji hiko cha kilimalondo, kijana KATUNJE ana haha huku na kule baada ya kumkosa Lyoto alirudi kijijini na kumpa tyaarifa mama Mwaija na ndipo wakasaidiana kumtafuta ndani ya msitu ule mkubwa. Katika pitapita yao walifanikiwa kuona nyayo ambazo zilikuwa tofauti, Katunje akachuchumaa na kuzikagua kwa makini ndipo akasema "Mama huu ni mguu walyoto ila huu ungine ni wa mtu mzima kabisa lakini sijamfahamu" Ndipo mama mwaija akainama na yeye kuziangalia kwa makini "Haaa ni kweli sasa twende tuzifuatishe kwanza tujue mwisho wake wapi, alafu tujue tunafanya nini". Walizidi kuzifuatilia huku Katunje akiwa na hasira sana baada ya kumkosa binti wa karibu sana, hatimae mbio za sksfuni huishia ukingoni kwani walifika mpaka pale kwenye korongo na wakashuhudia kuna mikwaruzo ya miguu ambayo ilionyesha dhahiri kuwa mtu kadondokea mule. "Mama yangu binti wawatu katumbukia ndani humu jamani laaaah!". Mama mwaija alimtuliza aondoe kwanza zile fikra "Hapana usiseme hivyo mwanangu, twende kwanza nyumbani mana hapa sasa hivi tuko peke yetu tukifika nyumbani tutajua nini cha kufanya." wakiwa wanarejea Mama Mwaija akamuomba katunje achume ganda la mgomba ambalo ni nene sana, katunje alilileta baada ya kuligandua ganda hilo kwenye mgomba uliokaribu na hapo. mama huyo kwa ustadi usio wa kawaida akainama chini na kuanza kufanya mambo yake ambayo hata katunje yalimchanganya sana "Unafanya nini mama" Aliuliza katunje. "hapa mwanangu napima hii miguu naifananisha kisha tunakaa nalo hili siku moja litatusaidia kumjua huyu mtu aliyekuwa akimfukuza Lyoto" kwa wazo hilo hata lyoto alilikubalibila wasiwasi, waliendelea kutafuta njia ya kurudi pale ambapo walikuwa wanakaa zamani, katunje alikusanya kila kitu kwa kuwa hapakuwa na sababu yeyote ambayo ingemfanya aendelee kuishi pale ndipo wakawa wanarudi kijijini. kabla hawajarudi walifanikiwa kuiona mitego kadhaa "Mama hii mitego ya ndege na mnyama naifananisha zamani sana baba yangu alikuwa akiitega alafu ni mizuri sana yani". Alitaka kuitoa ile mitego ;lakini mama Mwaija akagoma kwanza " hapana mwanangu usiitoe kwa sababu aliyetega hapo aliwaona nyinyi mnaishi karibu sasa tuiache alafu siku ya kesho njoo ujifiche uangalie nani ambae anakuja kuangalia mitego hii labda anaweza kujua nani ambae kamkimbiza lyoto mpaka kuangukia mule korongoni". Katunje aliondoka na mama huyo wakiwa na huzuni kubwa, kijiji kizima taarifa ilimfikia na kwa upande wa mzee Swai alihuzunika kiasi kwani lengo lake halikutimia. Ilitimu majira ya saa nane za ,chana maji yenye nguvu za ajabu sana yalisukuma mizigo yote ambayo iliingia humo bila kujai kama kuna binaadamu ambae yupo mule ndani. Mungu hamtupi mja wake lyoto alikuwemo mule ndani ya maji akiwa hana habari yeyote baada ya kuzimia kutokana na ile hali iliyomkuta, maji yalishirikiana kumsukuma lyoto umbali mrefu sana ambao hauwezi kutabirika ila ilikuwa nje kabisa ya kijiji cha Kilimalondo. Upande wa kijiji cha Chamlo watu walikuwa na hamsha hamsha za hapa na pale ili wafanikishe swala lile la sherehe ambayo ni muhimu sana kwao. Wanawake walianza kwenda kuchukua maji mtoni na wengine walichukua nyavu ili kuvua samaki mtoni hapo ili wapate kuchemsha wale pamoja na pombe ambazo wanaziandaa "Hakika naamini NAOMI ndie atakae chaguliwa kuwa mke wa Bamuzi lakini sisi wengine hatuna uzuri zaidi yake" Binti mmoja ambae alikuwa akimueleza mwenzake huku wakielekea kuchukua maji, "wewe mbona unakata tamaa hivyo wewe pia mzuri ndugu cha kufanya hapa wakati wa mkesha basi tujikweze kwa Bamuzi na atatukubali baada ya kumfanya atukubalie kimapenzi sisi najua kesho tukivalishwa na kuandalia vyema atatukubali". walishauliana kwa kila jambo ili nafasi hiyo waipate. Majira ya jioni kijana Bamuzi alimuita mmoja wa kijana ambae yupo nae karibu sana na kumuambia jambo "sasa mambo ndio kama hayo, nakuomba ufanye jambo moja usiku ukifika mtafute NAOMI na umchunguze kila afanyalo alafu uje uniambie mana baada ya huyo hakuna mwingine naweza kumchagua". Kijana huyo alimsikiliza kwa makini na kumuahidi kuwa atalifanya kwa ukamilifu sana hilo jambo. Mama NAOMI alionekana kumsii sana mwanae huko aendako asidiriki kabisa kunywa pombe na alafu asikeshe arudi mapema sana ili aweze kumuandaa. Wakati huohuo Nomi akielekea kwa rafiki zake njiani alikutana na kijana mmoja ambae alimsimamisha na kuongea nae mawili matatu. "NAOMI samahani sana naomba unipe jibu langu kwani nakupenda sana". Kijana huyo ambae alijikakamua kuongea mbele ya mrembo wa kijiji. "Kha! weee mbona king`ang`anizi kama kupe kwenye mfugo, nimekuambia huna hadhi ya kuwa na mimi najiandaa hapa nataka kuwa mke halali wa BAMUZI sasa naomba usiniharibie". Baada ya kuongea hayo alinyoosha na njia kuondoka pale. Kijana huyo alibaki kuduwaa pale alipo ndipo muda mchache walifika wenzake na kumuuliza nini kimetokea, walimcheka sana kwani walimuambia kuwa Naomi ni mtu tofauti sana hawezi kuwa nae yule ndie mrembo wa kijiji hivyo ni ngumu sana kumkubalia yeye ni bora amuache aolewe na Bamuzi. "lakini kama kweli unampenda ngoja leo tumfanyie mchezo usiku na sisi tumharibie " Vijana hao walipanga njama za kumharibia NAOMI ili asipate nafasi ya kuwa na Banuzi na zaidi yake awe huyu kijana aliyemkataa. Majira ya usiku yamefika tayari Mzee NGOLOLO akiwa na washauri pamoja na BAMUZI walikuwa mahala husika ambako wameandaliwa kwa ajili yao, huku watu waklianza kupiga ngoma na kuanza kunywa pombe za kutosha. Wakisubilia asubuhi nani atatajwa, kijana ambae alipewa kazi na bwana http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Banuzi alijitahidi sana kumtafuta NAOMI mpaka akafanikiwa kumuona na akaanza kumchunguza. Wale vijnana ambao waliahidi kumharibia Naomi walifika na kuwa karibu sana na Naomi. "Sasa itabidi hii pombe utie ile dawa alafu ukampatie Naomi". Ndipo wakafanya hivyo na mmoja wa kijana akaenda kwa Naomi na kumuambia "Naomi tafadhali ebu pokea kinywaji hiki kutoka kwa mtoto wa Ngololo kijana Bamuzi kakutunuku kuwa mmoja wa watakaotajwa hapo kesho". NAOMI alishindwa kuamini kama kweli, alichukua na akakinywa chote bila kufahamu kuwa ulikuwa ni mtego tu. Kukataa alishindwa kwani jina la Banuzi ni kubwa sana pale kijijini na watu hawajawahi kulitumia vibaya jina hilo, ila hao vijana kwa kuwa walidhamilia kufanya hivyo walifanikiwa. Ngoma zilianza ndipo yule kijana ambae alikuwa anampenda sana Naomi alienda na kumshika mkono na kuanza kucheza nae wakati huo NAOMI hajielewi kutokana na kinywaji kilichochanganywa na dawa za usingizi. "nasikia usingizi nipeleke nyumbani" sauti za kilevi na uchovu alizozitoa NAOMI zilidhihilisha kuwa dawa inafanya kazi, na kijana huyo hakufanya makosa ndipo akamshika vyema na kumpitisha karibu na wale wazee na alipo BAMUZI, kijana aliyepewa kazi ya kumchunguza alifanikiwa kuona yote japo Bamuzi hakushuhudia zaidi. Safari hii ilifika hadi kwenye moja ya fumutu ambalo lipo mbali kidogo na pale kwenye shsrehe yao. Kijana alifanikiwa kufanya machafu aliyoyakusudia kwa kumuingilia kimwili mpaka alipotosheka na akamuacha palepale alipo huku akiwa hoi NAOMI. Baada ya hapo walishauliana kuwa wampeleke kwa mama yake, safari ilianza na kumfikisha hadi kwa mzazi wake na kumuambia kuwa kichwa kinamuuma ndipo alijisikia kizunguzungu na wao wakamsaidia kumleta pale, alimuingiza ndani na kulala mama akiwa hana hili wala lile juu ya mwanae. Asubuhi na mapema sanawatu wakiwa wanajiandaa ndipo Mzee mmoja ambae alijiimia kwenye mitego yake aliyoiweka kwenye maji ili apate kunasa samaki wakubwa sana. alifika na kuanza kuvuta kamba ya mtego ule aina ya dema lakini ajabu dema linatoka lakini anaushuhudia mkono wa mtu ukizama tena ndani. Ilimfanya aogope na kushangaa na kwa kuwa ni mzoefu sana aliamua kuingia ndani ya maji hayo na hatimae anamtoa binti Mzuri sana mpaka mzee akashangaa kwa nini awe mule ndani na anatokea wapi ni maswali ya haraka haraka ambayo alipata kujiuliza kwanza. Alimtoa nje na kumsukuma tumbo kwa kumminyaminya ili ayatoe majia mabayo kayanywa, yalitoka mengi sana lakini hakuzinduka, ilibidi afanye jitihada za hali ya juu kumfikisha nyumbani kwake na wakati huo watu wote wapo kwa mzee Ngololo ili kushuhudia tukio hilo la kumcgagua mchumba wa Bamuzi. Huduma zote za kiafya zinatolewa chini ya amri ya Banuzi ndipo alikimbia sana na kumfuata mmoja wa kijana na kumueleza ana shida ya kuonana na Bamuzi, hakika aliitwa na yeye akaitika wito kufika pale. "Vipi kijana tayari umeshamuona ni mwanamke gani?" aliuliza mzee huyo "Daah hapana kwani yule niliyemtarajia jana kafanya vitu vya ajabu sana, kwa hiyo itabidi niifuate ndoto yangu ilikonielekeza niende". "kijana banuzi nina shida nyumbani kwangu naomba tuongozane ukaone shida yangiu haraka sana". "sasa muda unafika sasa hivi wa kuchagua" "ndio najua ila mimi nina shida na wewe kama unakuja kuwa kiongozi wetu basi njoo unisaidie". Walionekana kukimbia kuelekea kwa bwana huyo. Shughuli ilianza kuwa na hofu baada ya kutoonekana kwa kijana Bamuzi na wanawake wamejipanga kwa kweli kumsubilia yeye. Wakiwa kwa mzee huyo ndipo Bamuzi anamshuhudia binti mrembo ambae hakuwahi kumuona ndani ya kijiji kile. Ndni ya kijiji cha SHISHIMO sasa mambo hayakuwa vizuli baada ya ugomvi mkubwa sana kuzuka baina ya Mama SIKITU na Baba SIKITU juu ya kile kinachomfanya mama sikitu kumtuhumu mkwewe kuwa ni mshirikina na baba sikitu kukataa katakata. "nakuambia ukweli baba yako mwanga yani mchawi" maneno hayo yalimfanya baba sikitu ambae ni mzee Chito kukasirika sana "hapana naona sasa umemchoka baba yangu hawezi kuwa mchawi baba yangu aliyenilea kwa muda mrefu sana". "Najua huwezi kuniamini kabisa ila unakumbuka ile siku ambayo ulikwenda shambani nini kilikutokea unataka kuniambia wewe shamba la baba yako hulijui wapi unaingilia na wapi unatokea?'" Mama sikitu aliuliza swali na wakati huo wakiwa mbali na nyumbani kwao. "Mh! kidogo inaleta utata kwani ukweli ile siku nilishindwa kuamini" Alithibitisha bwana Chito kuonyesha kuwa kweli siku hiyo haikuwa nzuri sana. "Kingine unaweza kuniambia maneno haya aliyokuwa akiongea baba yako kule shambani siku ile?" Chito alishangaa "Maneno gani hayo tena aliongea" Mama sikitu alianza kuigizia yale maneno kwani aliyakariri vyema sana """Nyamnyena Nyamyena, kulumbila kulumba. Mwanenu kulumbilolo Chito, kumchamba mwangu, kamililombile kulilima mpaka kujioni Nyamnyena Nyamnyena kulumbila kulumba......hayo ndio maneno ambayo alikuwa anayataja je unaweza kuniambia alikuwa ana maanisha nini" Ndipo chito alishika kichwa chake huku akiwa haamini kabisa. Mama sikitu aliendelea kumuambia kuwa yeye yuko tayari kukimbia pale na kurudi Kjiji ch BWAWANI lakini si kuendelea kukaa na mtu mchawi kama yule.
Baada ya maneno hayo na mkewe bwana Chito alionekana kuwa na mshangao mkubwa sana ambao hata mkewe nae alijikuta akimuangaklia kwa umakini sana na kutaka kujua kipi ambacho kinamfanya ashangae kwa vile. "Vipi unaniangalia tu wewe si unamtetea baba yako yani hata haukumbuki mwanzo tumefukuzwa kwa ajili gani yani sasa kama hauamini fanya uchunguzi utanielewa". "Mke wangu sawa lakini kumbuka kuwa yule ni baba yangu pia usijalibu kutamka maneno hayo asije akasikia alafu akatuachia laana hapa". Chito alijaribu kumtetea baba yake ambae alionekana kuwa na imani chafu ya kishirikina "Unaogopa laana basi nikuambie hakuna laana yeyote ambayo itatufika kutoka kwa mtu mchafu kama yule namheshimu lakini mkwe wangu ni mchawi". Walianza safari ya kurudi nyumbani lakini akili ya mama SIKITU yeye ni kuondoka pale na atajua mbele ya safari wapi ataelekea, wazo hilo lilipingwa sana na chito kwani hakutaka kuamini kweli baba yake anayo hayo mambo ambayo mkewe anamhisi. Walimkuta mzee Mambo sasa akiwa peke yake na huku uso wake ukiwa umefura kwa hasira. Ghafla aliaga na kuwaomba yeye anaondoka mara moja kwenda kwa rafiki yake. "Sasa baba vipi unaelekea wapi wakati usubiri mkweo hapa anataka kupika ugali" Japo na maneno hayo mzee huyo hakutaka kusikia aliondoka na mkongojo wake na kupotea machoni mwao. "Si unaona niliyokuambia yale " "Eeee weee mwanamke unataka kunikorofisha mimi na baba yangu ebu achana na habari hizo kabisa nisisikie". Mzee huyo safari yake ilifika hadi kwenye nyumba moja hivi ambapo aliingia moja kwa moja kabisa "Eeeh bwana NYANDU afadhali nimekukuta" Mzee ambae alimtaja kwa jina la nyandu alimkaribisha ndani na wakaanza faragha ya maongezi yao, "Haya niambie kipi kimejili" Nyandu aliuliza. "Bwana Nyandu sijajua nini nifanye kiukweli, kuhusu pale nyumbani" "Nini tena ebu niambie kwanza mana hata hivyo kuna kazi yako hukuimaliza kabisa" Nyandu alimueleza Mambo Sasa "Unajua kipindi kile cha nyuma zamu ya kutoa kafara ilikuwa kwangu sasa mtu mweneyewe mhusika ni kutakla mkwe wangu mtoto atakayemzaa basi ndio nimtoe kama nilivyoahidi" "Haswaaaa na ndivyo wengi tunavyojua" "Sasa, walivyokimbia mwanangu na mkwe wangu kutoka pale nyumbani basi kumbe walikoishi walishazaa mtoto wa kike na wakampa jina la sikitu sasa wamerudi pale nyumbani ila nahisi kama yule mwanamke kakomaa mana ananishtukia sana kwa mambo yangu mengi ninayoyafanya" Maongezi hayo yalikuwa ya siri sana ambayo yaliongelewa chumbani kwa bwana Nyandu ambae ni mshirika mwenzake. "Ngoja tutapiga ramli sasa hivi na tutajua kama kweli yupo hai au kafa na kama yuko hai hakuna kitu kitakachoshindikana kabisa atarudi yeye mwenyewe hadi hapa na wewe utafanikiwa kutoa kafara yako" Mzee Mambo Sasa alionekana kufurahi sana " Haya twende kwanza fanya hayo mambo" Ndipo Nyandu alitoka pale kitandani na kuchukua furushi kubwa la mambo yake, akachukua kaniki nyeusi mbili moja akampatia Mambo sasa na nyingine akawa nayo yeye na ndipo walipovaa lubega kama wamasai, Waliufukiza udi fulani hivi ambao ulianza kuenea taratibu mule ndani na akaanza kuongelea maneno kwenye moja ya kibuyu, baada ya hapo akapandisha mashetani ambayo yalisaidiwa na nyimbo maalufu sana kwao "Nyandu, nyandu nyandu leloooo, kulilolangula kumwana sikitu, kulilolangula kumwana sikitu, kulilohangaika kokote kuliliona sikitu, Nyamnyenaaa Nyamnyenaaaa" Baada ya kuongea maneno hayo ndipo akanyamaza kwa muda kisha akapaza sauti kama kumuuliza Mzee mambo sasa na akitoka kwenye ulimwengu wa kibinaadamu na kuingia ulimwengu wa kishetani kimaongezi baina ya Nyandu na Mambo sasa. "Mambo sasa sema najua una shida sana" "Nyamnyena nyamnyena kweli kabisa nina shida nataka kujua mtoto wangu chito na mkewe kweli walizaa mtoto wa kike?" Alimuuliza huyo jini au shetani lenye jina la NYAMNYENA, ndipo alipoanza kumcheka sana mara kadhaa kisha akamjibu "Ndio walizaa na pia mtoto wao alibakwa na mmoja wa kijiji hiko lakini akapona baada ya kumtupa polini, lakini kasaidiwa na mtu wa karibu yako sana": Alishtuka sana kasaidiwa na mtu wa karibu yangu kivipi na yupi huyo mtu wangu wa karibu ambae alimsaidia huyo sikitu "Mtu wangu wa karibu gani huyo Nyamnyena ambae alimsaidia na anaendeleaje?" alianza kucheka tena. "Siwezi kukutajia huyo mtu fahamu kuwa bado yuko mzima na yuko mbali sana na nyinyi kwa sasa sifahamu wapi kafikia lakini ni mzima haya kwa heri mana tumevuka milima na mabonde mpaka kufika hapa tunataka kurudi kwetu" palepale yalimtoka yale mashetani na Mzee Nyandu akarudi kwenye hali yake na kumuuliza nini aliambiwa na shetani wao. Alimhadithia kila jambo, mipango ilipangwa ili binti Sikitu afanyiwe mpango afuatwe. Kwa wakati huo sasa mzee Mambo sasa alirejea nyumbani na kuwakuta wakila ugali ndipo akaungana na kuanza soga za hapa na pale. "Mwanangu chito unajua kama mtoto wenu bado ni mzima" "mzima baba mbona unataka kutukumbusha mambo tuliyoyasahau mpaka sasa" "aminini hilo kuwa bado ni mzima mana nilikuwa sina amani kumkumbuka mjukuu wangu mana sina mjukuu kabisa nataka nifanye jitihada ya kumrudisha nina mganga wangu ambae aliniambia kuwa anaweza kumrejesha alipo" Kauli hiyo iliwafanya wawe na shauku kubwa sana ya kutaka kujua lini watafanya jitihada za kumrejesha Mtoto wao. Ndani ya kijiji cha CHAMLO wakati kijana BAMUZI akiendelea kumuangalia binti yule kutokana na uzuri wake kule wazee ambao walikuwa wanamsubiri waliamua kutumwa na kuja hadi kwenye nyumba ya huyu mzee ambako ilisemekana kuwa Bamuzi kaenda. Kweli walifanya hivyo na wakamkuta "Sasa mzee hakikisha kabla ya yote apone huyu na hali yake iwe nzuri sana kisha unipe taarifa pia asijue mtu yeyote kuwa uko na nani humu ndani" Mzee huyo alimuitikia na Bamuzi akatoka nje akakutana na wazee waliotumwa kuja kwake, aliongozana nao na kufika kule akisubiriwa achague nani ambae atamfaa. Akili ya Bamuzi ilihama kabisa na ikawa imefififa kwa NAOMI ambae alishaonekana mtu mchafu na kuzama zaidi kwa mgeni huyo ambaye hakufahamu katokea wapi na alionekana kumpenda sana. alijiuliza maswali kuwa ama ile ndoto yake iliyomuambia kuwa atasafiri kumtafuta ampendae na hatimae ndio yeye kafika mweneyewe?. Mtangazaji alisimama na kuanza kunadi kwa kutumia maneno mazuri sana ambayo kila mmoja yalimkosha lakini kwa kijana Banuzi haikuwa hivyo kabisa akili yake ilibaki kwa yule mgeni tu. Baba yake alimshangaa sana kuona mwanae kabadilika ghafla alimsogelea na akamhoji "Mwanagu vipi mbona uko na hali hiyo kipi kimekukuta huko ulikotokea". Bamuzi alikohoa kidogo kisha akasema "Baba hapa siwezi kuchagua mwanamke kwa sasa hivi kwani kichwa kinaniuma sana hapa nahisi kuumwa" baba yake akamshika kichwa kisha akatikisa kichwa kuashiria kweli ana homa kali. "Sawa mwanagu sasa ngoja tunyamazishe shughuli hii na ili wewe hali yako ikiwa nzuri basi tutawaita na utachagua". Aliitikia na mzee huyo akaomba nafasi ya kuongea, "Jamani hapa tunamkaribisha kiongozi wetu mzee Ngololo ili aseme kitu " Watu walifurahi sana kisha mzee huyo akasimama na kuwaomba kwanza wale mabinti wasimame kwanza kwa pamoja, waliposimama ndipo akawasifia sana kwa uzuri wao. "jamani wanawake wote hawa ni wazuri sana kwani leo hii wamejipamba sana lakini mwanangu kashindwa kumchagua yeyote kwani wote kawaona wazuri sasa tunasubili kesho mtatangaziwa lini afanye uchunguzi mzuri zaidi na sasa hali yake ni mbaya kidogo hivyo tunaomba mutawanyike" Iliwashangaza sana kauli hiyo lakini haikuwa na shida kwani aliyesema ni mtu mubwa pale kijijini. Baada ya siku tatu http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Bamuzi anaonekana kufuatilia sana kwenye ile nyumba ya mzee kujua hali ya yule dada. Mzee huyo ambae alimuokota binti huyo alijulikana kwa jina la MWALAMI alikuwa anaishi na kijana mmoja hivi wa makamo. Siku moja kijana huyo alimshuhudia binti huyo akitoka ndani humo na kukaa juani kwa kuwa ilikuwa ni asubuhi sana alimfuata babu yake na kumuuliza "babu hivi huyu mwanamke mzuri ni nani". Babu mwalami kwa hekima zake alijua kuwa kijana kamtamani binti huyo sasa itambidi atumie kauli nzuri kutengeneza heshima kwa Bamuzi. " kijana wangu huyu ni binti wa mbali huko aliletwa na mumewe kwa ajili ya matibabu na hivi karibuni ataondoka kwani watakuja kumchukua". Kijana hakuwa na neno, lakini taarifa ilianza kusambaa kuwa kuna binti mzuri sana yupo pale kijijini. Nyumbani kwa Mama Naomi na Naomi mwenyewe, walikuwa na mazungumzo ya hapa na pale "Mama mbona kama nimepoteza usichana wangu mama". Alimueleza mama yake jambo hilo baada ya kujigundua tofauti. "Unasemaje wewe umepoteza usichana wako kivipi tena" "Mama hata sijui ila nahisi ndio hivyo". Mama yake aliumia sana baada ya kusikia jambo hilo akawa anamsema sana kwa nini alimuambia asijalibu kukubali kunywa kinywaji chochote kile ili asije kukutwa na hali kama hiyo lakini Naomi hakusikia kabisa. Baada ya muda kupita ndipo alipomuambia kuwa asije kusema chochote na iwe siri yao wao wawili na ikiwezekana basi huyo kijana aliyemharibia usichana wake basi amuite siku moja ili aweze kumkanya kwa tabia yake hiyo mbaya. Naomi aliondoka na kuanza kumtafuta kijana huyo ambae mwanzo alikuwa anamtamkia kuwa anampenda lakini Naomi kutokana na kujiona kuwa yeye ni mzuri sana basi alikataa na kumtolea maneno ya kumkashifu kwa kufikilia kuwa ndoto yake ya kuolewa na Bamuzi itatimia. Moja ya mahali ambapo vijana wengi wa hapo hutulia baada ya kufanya kazi nyingi na kuchoka huja kupumzika hapo na kuanza kupiga stori za hapa na pale. "Jamani hivi Bamuzi anaoa lini maana ile siku sijaamini kama alikosa mwanamke wa kumchagua kwa jinsi walivyopendeza vile?" mmoja wa kijana alikuwa anauliza kwa kile ambacho anadai kuwa kilimchanganya kwa nini Mtoto wa kiongozi mkubwa sana pale CHAMLO kushindwa kuchagua jiko lake la kujidai nae nyumbani kwake, "Aaa hata mimi tena huwezi kuamini mpaka mrembo wa kijiji kizima hiki NAOMI hakumchagua kabisa yani". Ndipo kijana anayejulikana kwa jina la KIPEPE aliinuka pale alipoketi na kuwaambia kuwa "Nyinyi habari ya kumtaja Naomi sitaki kabisa Naomi ni mchumba wangu mimi na Bamuzi akamchague mwingine huko". Wakati wanaendelea kumcheka basi alitokea Naomi na akawafanya wote wakae kimya kabisa "Kipepe nakuomba njoo mara moja" kauli ile ilimfanya kipepe kushtuka na kujiuliza nini kitatokea lakini wenzake wakimzomea kwa ile hali aliyokuwa akiongea basi Naomi kasikia na anahitajika kusemea uhakika wa yale. "Kipepe kwa nini ulinifanyia vile?" Naomi aliuliza "kukufanyia nini tena mchumba wangu eti" "Unajifanya hujui yani umeniharibia usichana wangu juzi kwenye ngoma baada ya kunipa pombe yenye dawa ya usingizi kweli" Kipepe alikuna kichwa kutafuta nini amjibu "Kwa sababu nakupenda sana siwezi kukubali uolewe na Bamuzi wakati mimi ndio wa kwanza kukuhangaikia" "Sawa ila ni mapenzi gani ya kuniharibia usichana wangu hunipendi kabisa sasa hapa naenda kwa Mzee Ngololo naenda kumuambia kuwa umenilazimisha ". Kipepe kilianza kumshuka kwanza lakini kwa kuwa ni kijana wa kiume alikomaa kwanza "Poa nenda ila mimi mambo yangu nimepata na niko kwenye hatua ya kutangaza kijiji kizima na najua urembo wako utakuwa umeishia hapohapo na sijui kama utalinga tena ". "Sawa jigambe ila niko tayari kuaibika lakini wewe lazima ukione cha mtema kuni". Naomi aliondoka akiwa na huzuni kubwa sana. Kijana kipepe alienda kuwaeleza rafiki zake kisha akawaomba nini afanye. "Yani kaka hilo swala likifika kwa Bamuzi umekwisha si unamjua alivyo yule jamaa yani hacheleweshi kabisa nakuambia kama unakumbuka yule KIBO alichofanywa baada ya kumbaka yule mwanamke nani huyuuu.....NAMIO aaah! nilimuonea huruma sana kwa hiyo wewe sasa hivi nenda mtafute kabla hajaenda kusema usije ukafa". Baada ya siku ya pili watu wakisubilia sasa mambo yawe hadharani Bamuzi anaonekana na Mzee Mwalami wakiongea mawili matatu. "Bwana Mwalami nimekuambia jaribu kumdadisi anaitwa nani anatokea wapi na nini kilimtokea". Alisema Bamuzi "Nilishamuuliza anaitwa LYOTO, lakini sehemu anayotokea na kilichomkuta hafahamu kabisa ila anajua kuna mahali ambapo alikuwapo mwanzo kabla na anayemkumbuka ni mmoja tu anaitwa KATUNJE basi, ila vingine hajui kabisa" "umesema anaitwa nani?" alihoji kwa kuwa hakulikamata vyema lile jina "Anaitwa LYOTO pia ili iwe rahisi kumpa jina basi tumuite LYOTO KATUNJE" Bamuzi alifurahi sana kwa hilo jina ndipo akaweka vyakula pale kwa ajili ya huyo LYOTO ambae kutoka KILIMALONDO kusafirishwa na maji hadi kijiji cha CHAMLO. hakika MWENYEZI MUNGU NI MKUBWA SANA. Siku imefika na mapambo yaliendelea kutanda kila aina kwa mabinti wazuri sana wenye kupendeza akiwemo NAOMI ambae alikubaliana tayari na Kipepe kuwa watatunziana siri nzito hiyo. Mtangazaji wa habari za pale kijijini aliifanya kazi yake kwa umahiri mkubwa sana kiasi watu walipenda. wanawake walijaana wanaume pia na vijana rika za akina Kipepe walikuwa wengi sana kushuhudia mtoto wa kiongozi akichagua mwanamke ambae atamfanya achukue kiti cha baba yake amsaidie majukumu. "sasa naomba kumkaribisha BAMUZI aweze kuwatembelea kuwaangalia na atujuze kwa kumshika mkono ampendae aje nae mbele yake" Makofi yalikuwa mengi sana. Nyumbani kwa Mzee Mwalami basi alimchukua LYOTO na kwa kuwa hakuwa na nguo nzuri alikuja nae hivyohivyo kama kushuhudia tukio zima la kijana Bamuzi. Bamuzi alifika pale na kuangalia nje ya uwanja kwa watu ili amuone Lyoto lakini hakufanikiwa, watu wakawa wanamshangaa sana kwa nini sasa asichague na anawapita huku akiwaangalia wasio wahusika jamani. Ukimya ulitanda sana huku wakisubili. upande wa NAOMI alikuwa hoi kwani hakuamini kama klweli anampita tu bila hata kumshika mkono, mpaka dakika kadhaa Bamuzi anakata tamaa na akawa anamuendea Naomi ili amshike rasmi huku akijiuliza kwa nini huyu mzee Manuali anamfanyia mambo tofauti na walivyoelezana. Anapeleka mkono kwa Naomi na Naomi moyo wake unafurahi akiusindikiza ili aushike haraka, ndipo mzee Mwalami akasema "Bamuziiiiiiiii usifanye makosa" Baada ya neno hilo ndipo watu wakatazama kule ilikotokea sauti "LYOTO KATUNJEEEEE.....".alitamka neno hilo ndipo binti Lyoto akaitikia Bamuzi aliurejesha mkono kutoka kwa Naomi na akamkimbilia Lyoto na kumshika mkono. "Jamani huyu ndie mke ambae nilikuwa namuwaza kila siku atakuja kutokea" makofi hayakupigwa kwa kuwa walimuangalia mgeni huyo aliyewakosha kwa umbo dogo lililopendeza tena bado anaonekana kuwa mbichi kabisa. Watu waliruhusiwa baada ya kupata maelezo kamili kuhusiana na mwanamke yule. Siku iliyofuata Bamuzi,Lyoto na wazee akiwemo baba yake walienda kuwakogesha dawa za ulinzi na kuwakinga na maadui wowote ambao watajaribu kuutumia uchawi wa aina yeyote washindwe kwani Bamuzi anakuwa kiongozi akishikilia kiti cha baba yake. Ndani ya kijiji cha BWAWANI siku hiyo walionekana kukutana ili kuelezana jambo fulani, Ajabu kubwa ni juu ya kuonekana kwa SUSU akiwa kwenye hali mbaya sana na haijulikani nani ambae kayafanya hayo. Mzee Manuali alisimamia kesi hiyo huku akiwataka wajitokeze wao ambao wamefanya ujinga huo, pia ikishindikana basi yeye atamsubulia apone na akija kuwataja basi watamtambua. Bwana Mapato alimshauli ndugu yake kuwa sasa muda wa mapambano umefika kwani wajiandae kwa lolote na chochote, Hadi hapo wamemuuzia kesi Mzee Mambo sasa lakini walichokosea baada ya kumuonyesha susu. "Mapato tuachane na hayo ya Manuali sasa unajua kuwa kule bwawani kuna jambo ulilifanya vipi na ulitegemea kuwa sadaka hiyo itamuhusu bwana Mambo sasa vipii sasa." Sikujua aliuliza "kweli lakini ndio hivyo hayupo ila nahisi kama ile mizimu ya bwawani imeshakufa maana haijanilazimisha chochote mpaka sasa nafikilia kwenda kwa mtaalamu mpya ambaye atanisaidia kwa hilo". Majira ya usiku wa manane Mzee mapato akiwa kalala na mkewe basi upepo ulivuma na sauti za ajabu zikiendelea kutoka na wanyama wakiendelea kulia huko polini. Mapato alishangaa sana ndipo sauti ambayo ilikuwa ikijirudia rudia ikimpa taarifa ambayo ilimuogopesha "Mapatoo...kazi yetu hujaifanya...tunahitaji damu na kwa nini unatukabidhi ya mzeee sana klijana unatiutania?" Mapato alishindwa kuamini kwa zile kauli ambazo alikuwa akizipata "Sasa tutahitaji na mtoto wake Mambo sasa ndipo damu itimie na wewe utaifanya shughuli hiyo ya kuwaleta bwawaani muda wa siku tano". Mapato kashtuka sana na hakuamini kama atakuja kupata shughuli kama hiyo. Asubuhi na mapema anaenda kwa sikuja na kumuambia kuwa "Bwana weee mambo magumu". "Magumu kivipi tena" "Sikujua jana usiku sasa kuamkia leo, wameniletea vitisho kuwa Mambo sasa ni mzee sana sasa wanamhitaji na mtoto wake yani sikitu na mtoto mwenyewe hatujui kafia wapi mwaka huu unakaribia." Sikujua aliuma meno kwa mshangao na huku akiwa anafikilia sana. "Kweli jambo zito sasa hawajui kama mtoto wa mambo sasa kafa?" Walishindwa kujua mtoto gani wa mambo sasa anayezungumziwa na watamshawishi vipi bwana Mambo sasa aje Bwawani, ndipo mipango ikatengenezwa ya kumfanya mzee Mambo sasa arudi bwawani na wao wafanye yao. "Sasa itabidi mapato uondoke hadi kijiji cha SHISHIMO ukifika kule chunguza kwanza upajue kwao ukipajua mtafute mkewe alafu ujue wana matatizo gani ambayo utajua wewe pakuingilia". Mapato alikubali na akaanza kujiandaa kwa safari. Ndani ya kijiji cha SHISHIMO sasa Mzee Mambo sasa baba wa chito alienda kwa rafiki yake ili kuanza kufanya kazi ya kumtuma jini wao kwenda kumchukua SIKITU kokote aliko. "Sasa tuambizane hapa tunamtuma yupi?' aliuliza Mambo sasa " Nyamnyena ndie tunamtuma kazi na yeye atajua jini gani atamtumia kwenda kumchukua SIKITU kokote aliko" Basi walifanya kazi yao na hatimae wakafanikiwa Mizimu ya Nyamnyena ikakubali kumtuma jini wao ili kwenda kumchukua SIKITU. "Lakini Mambo sasa wewe rafiki yangu mpaka sasa nimeona kuna watu wanakutafuta wewe wakutoe sadaka kwa hilo jina lako Mambo sasa" Mzee huyo alishangaa mbona mageni hayo "Fahamu hivyo na wako mbioni tayari wamemtuma mmoja wao kuja hapa kijijini ili wapate kile wanachokihitaji sasa ni hatua ya kuchunguza kila mgeni anayeingia hapa tumkague kama mkubwa wa mambo basi tumjue anakuja kwa lengo gani na nani ambae anamtumikia". Kumbe harakati za mapato na sikujua zilishajulikana. Ndani ya KILIMALONDO majonzi kwa kijana KATUNJE kwa kupotelewa na Lyoto na hajui wapi ambako kapotelea, mama mwaija alikuwa karibu sana katika kuhakikisha kuwa anakuwa kwenye hali salama muda wowote ule "Katunje naomba hili ganda la mgomba tafuta viatu vya Mzee Kauzibe ufananishe kwa kuwa hawa wazee ndio wawindaji hodari hapa ukimaliza kwa huyo nenda kwa mzee UDEVU utafahamu ukubwa ukifanana njoo niambie nijue nakusaidiaje kumpata huyo binti yetu. Katunje alitulia huku akiwa na mipango yake ya chinichini kutaka kurudi basi nyumbani kwao maana hata hivyo aliona hakuna sababu kubwa ya kuishi mbali na kwake. "Lakini siwezi kumuacha huyu binti akiwa huko aliko na ni bora hata mwili wake niuone alafu nimrejeshe kule alikotokea na nikamkuta na naamini baada ya hapo najua baba mambo yake ya kichawi atakuwa kayaacha kabisa ".
Haikuwa kazi rahisi kwa Mzee Mapato kutaka kufanikisha lengo ambalo alilipangilia kulifanya kwa Mzee Mambo sasa ambae ndani ya kijiji cha SHISHIMO anajulikana kwa jina la CHITO. Jina hilila Mambo sasa ni la baba yake ikiwa kipindi ambacho bwana Chito yupo kijiji cha BWAWANI alitumia jina la baba yake na watu wote wa kijiji hiko wakamjua kwa jina hilo. Pia kwa upande wa Mzee Mambo sasa baada ya kupewa taarifa na rafiki yake kupitia mizimu yao ya NYAMNYENA alijiandaa vyema sana kuhakikisha kuwa hakuna mgeni yeyote ambae ataingia ndani ya kijiji chaobila wao kumtambua, hali hiyo ilipelekea kuwa makini sana pindi pale atakapohisi kuwa kuna mtu mgeni kaingia laziam wamfuate. Bwana Mapato aliona muda muafaka wa kuanza kuzoea pale kijijini umefika kwanza alifika kwa Mwenyekiti ambae alijulikana kwa jina la MASANJA huyu bwana alichaguliwa kuwa mweneyekiti wa pale kutokana na elimu ambayo aliyokuwa nayo na pia anatokea kijiji tofauti na Shishimo. Mzee mapato baada ya kuhakikisha kuwa kafika tayari ndani ya kijiji hiko ambacho kinasadikishwa kuwa mtu ambae anamtafuta anapatikana pale, ndipo aliulizia kwa mwenyekiti na kupelekwa. Hakika alijitambulisha vyema kabisa huku akiomba msaada wa kile ambacho alidai kuwa anakitafuta. "Mwenyekiti naitwa SUMAE natokea kijiji cha jirani hapo, shida yangu kubwa ni kumtafuta ndugu yangu ambae kanipotea kwa miaka mingi yani kulikuwa na ugomvi wa kifamilia sasa yeye akaondoka mpaka sasa namtafuta sijampta". Mzee Mapato aliamua kumuongopea bwana Masanja ambae alionekana kusikiliza kwa makini huku akionyesha sura ya huzuni. "Mh! pole sana ndugu yangu kwa jambo hilo lililokukuta, sasa ulihitaji msaada gani nikusaidie kwa sasa?" Mzee Masanja alimuuliza bwana Mapato ambae alijitambulisha kwa jina la Sumae. "Mwenyekiti nashukuru sana kwa ukarimu wako pili ninachoomba nipate hifadhi, pili sitaki taarifa ya kufika mimi hapa isambae kwani kama yupo hapa kijijini nina imani kubwa atakimbia na kutoweka". Mzee mapato alitumia nguvu ya ziada sana kumfanya mwenyekiti amuamini yeye kwa lile alisemalo. Alifanikiwa kupata nafasi ya kuishi pale baada ya kuonyeshwa kibanda ambacho ataishi pale, Mapato aliona moja ya mbinu zake zinaendelea vyema kutimia kwani atampata mzee Mambo sasa na kumshawishi kurudi kule kijijini na kumpeleka moja kwa moja kule bwawani ili iwe rahisi yeye kuuliwa na bwana mapato kufaidika kwa maisha yake na mikosi aliyo nayo. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku walilala, majira hayo ya usiku kwa upande wa Mama Sikitu hakupata usingizi kabisa, alisikia kelele za ajabu zikiendelea huko nje, ajabu zaidi akimuangalia mumewe hana hata habari alikuwa anakoroma sana kiasi ilikuwa inamchukiza sana Mama Sikitu. Aliondoka kwenye kitanda kisha akaanza kufungua mlango wa chumbani kwane ili atoke nje aende kushuhudia kile ambacho anakihisi kwa muda ule. Alifanikiwa kupiga hatua kadhaa mpaka kwenye sebule ya nyumba hiyo ambayo inatenganisha chumba chao na baba mkwe yani mzee Mambo sasa, "Mh! hizi sauti zinatokea chumbani kwa Mkwe kuna nini tena humu?". Alijiuliza maswali ambayo alishindwa kupata majibu yake, kadri sauti zinapozidi mshangao ulimzidi zaidi mama Sikitu huku akiwa na hofu kubwa sana pale alipo. Alisogea taraibu taratibu karibu na chumba cha mkwewe alipofika mlangoni akachungulia kwenye moja ya uwazi ambao upo kwenye mlango wa chumba hiko, alishika mdomo na palepale akadondoka chini na kuzimia. Anaonekana mzee Mambo sasa akiwa na kaniki nyekundu ambayo alikuwa kaivaa lubega mithili ya watu aina ya wamasai, alichungulia huku na kule ndani humo hapakuwa na mtu ndipo akamburuza na kumuingiza chumbani mwake. alitoka tena na kuufungua mlango wa kutokea nje kisha akauacha wazi na yeye akarudi chumbani kwake. Asubuhi na mapema sana CHITO kama kawaida yake aliamka lakini akipapasa wa ubavu wake hakuhisi kuwepo kwake. alishtuka kwani ndani ya nyumbaq hiyo chito ndie mfunguaji mlango na kumuamsha baba yake kisha huelekea shambani sasa kwa wakati huo ilikuwa kama ajabu kwake. Aliinuka na kutoka kuangalia mlango wa nje anashangaa kuona mlango ukiwa wazi. Ndipo akaenda kumgongea baba yake mlango ulikuwa umefungwa akajua baba yake alikuwa kalala. "Baba, umemuona mke wangu huku nje?" alimuuliza baba yake "Mh! mwanangu tangu lini mimi kuamka kisha nikaweza kutoka nje na baridi hili, kaenda wapi tena na yeye". Alikuwa anajibu huku akiwa anamjia pale mlangoni. "Yani nashangaa sio kawaida yake kutoka nje naona mlango umefunguliwa kama vile uko wazi pia mlango wangu chumbani ulikuwa wazi" Mzee Mambo sasa aliusogelea ule mlango wa nje akawa anasikitika sana ndipo akatoka nje na chito nae alimfuata baba yake kule nje "Aaaah! mwanagu hawa wanawake sio watu kabisa vichwa vyao vinafanana nadhani hata wana akili moja kama mama yako na yeye aliondoka hivihivi hapa nyumbani" Chito alichanganyikiwa sana baada ya kuambiwa kuwa na mama yake kapotea kwa mazingira yaleyale. Lakini ajabu iliyoje usiku wake mvua za rasharasha zilinyesha na asubuhi kuacha alama ambazo mtu angekuwa anapita basi angejulikana lakini hilo hapo halikuwepo. Mapato ambae kwa sasa alijiita kwa jina la Sumae alianza kukaa na mwenyekiti huyo ili aanze kumjuza kwa mambo fulanifulani, "Bwana mwenyekiti nina swali kidogo hapa?" alisema mapato " Sumae usihofu sema kile kitu ambacho unahisi kitakufaa kwenye uchunguzi wako" "Nilikotokea kuna ushirikina sana watu wanauliwa na wanagombanisha watu kupitia uchawi ndio maana mpaka sasa ndugu yangu kapotea kwa ajili ya hayo mambo vipi huku hayo mambo yapo?". Aliuliza swali ambalo alijua kuwa atapata makubwa ya kumsaidia sana. "Sumae kweli hapa pia yapo hayo mambo mfano kuna wazee kadhaa ambao wanasumbua sana hapa na nakutaka uwe makini sana na hawa watu" http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mzee Mapato akashuku huku akiwa na hamu ya kujua nani hao "Sawa hivi unaweza kunitajia ili nijilinde na hao watu nikiwasikia ili njiepushe nao". Mwenyekiti alipumzika kidogo na kusema "Kuna mzee mmoja hapa anaitwa MAMBO SASA....." "Anaitwa naniiii?" Ndani ya kijiji cha KILIMALONDO anaonekana kijana KATUNJE akiwa njiani kuelekea kwa bwana KAUZIBE alionekana kuwa na hasira sana ambazo zilikuwa zinamruhusu hata kujeruhi mtu, ghafla anatokea mama Mwaija ambae alikuwa anamshangaa sana. alimshika mkono na kumuomba asifanye jambo kwa hasira kwani atakuja kusababisha matatizo ambayo atashindwa kuyazuia "Ngoja nikuambie kitu kijana wangu, kila kitu kina mipango yake fanya mambo kwa utaratibu na utakuja kumjua mapema sana, nimegundua kuwa hilo ganda halitotusaidia kitu kwa sasa " Alisema mama mwaija na kumfanya Katunje amshangae kumuambia kuwa halina faida yeyote, "Kwa nini sasa useme halina faida yeyote kwa sasa?" Katunje aliuliza "Chakufanya nenda kijiji cha MPOLONI huko kuna mzee maarufu sana wa kuagua (kutambua) nyayo, huyu ukimuambia kuwa Mama Mwaija kaniagiza basi atakusaidia anaitwa Mzee UKELELE pia utakapo toka hapa mtu yeyote asikujue". Katunje alifikilia sana ndipo akalitupa lile ganda la mgomba ambalo lilitengenezwa kufananisha na nyayo za miguu ambayo ilionekana kule wakati wanamfuatilia LYOTO. Siku hiyohiyo kijana Katunje alijitolea kufa na kupona kwenda kijiji cha MPOLONI, safari yake ilianza kama masihara sana lakini kadri muda ulivyozidi ndipo safari ilikolea huku akiwa na kifaa ambacho alibebea maji. Majira ya usiku sana ndipo alikiona kijiji cha mpoloni na kumfanya afurahi sana kijiji hiko kilikuwa bondeni hivyo ilikuwa ni rahisi sana kuonekana. Hakuwahi kufika ndani ya kijiji hiki kwani ni mara yake ya kwanza na kwa kuelekezwa tu na Mama Mwaija. Akiwa njiani kukikaribia kijiji hiko ndipo alisikia sauti za vicheko vya watu ambao yeye hakuweza kuwaona, "Ahaaa kumbe na huku kuna upumbavu wa kichawi kama shishimo, nashukuru baba yangu alinikabidhi dawa ya kujilinda" Aliendelea kutembea bila wasiwasi hadi ndani ya kijiji hiko kikiwa na ukimya mkubwa sana. alifika kwenye nyumba moja ambayo aliona kuwa kuna watu wakizungumza mawili matetu kama familia, alifika na akawasalimia wote kwa pamoja "Shikamoni wakubwa zangu" katunje alitoa heshima " Malaaba abadi gadi gadi gijada" Wazee hao walikuwa wanaongea kama watu ambao wanaumwa mafua kwa muda mrefu maneno hayakai sawa yani yanapandanapandana. "Naitwa Katunje natokea KILIMALONDO nimekuja hapa kijijini kwa shida ya kutaka kumuona mzee UKELELE". walionekana kukaa kimya kwanza kisha mmoja wapo akasema "ugelele adabadigana mbali da hapa sasa bola ulale hapa kecho achubuhi tuguojeshe wabi anabadigana bwana ugelele" Ilimuia ngumu sana yeye kukubali kulala pale lakini akijiangalia kachoka na anashida ya kweli ya kumuona huyo mzee na kaambiwa ni mbali ambako anakopatikana, hatimae alifanikiwa kukubali kulala, Kabla ya yote aliandaliwa chakula chenye nyama nyingi ambazo hakuwahi kuamini kama atapatiwa kiasi kile, alianza kula na nyama ya kwanza hakuielewa ya pili, "Mh huyu mnyama gani" alijiuliza yeye mwenyewe bila hata kujibiwa akaendelea kula lakini ile nyama ilimshinda tabia kabisa. "Mgedi kalibu jisigie gama ugo jumbani kwako gilimalondo" Ndipo akaonyeshwa sehemu ya kulala, Katunje alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwani tumbo lilianza kumchefua huku usingizi hakuupata kwani alikuwa na dawa ambayo ilimsaidia kiasi fulani kutodhurika. Asubuhi aliwaaga baada ya kuelezwa na hatimae akafika hadi kwa mzee UKELELE. Alikaribishwa na baada ya kujitambulisha kuwa kaambiwa na nani aje pale " Aaah kumbe Mama Mwaija mimi ndio baba yake mzazi, na binti yake ninae mimi hapa ninaishi nae" lakini ghafla akawa anasumbuliwa na tumbo ndipo yule mzee akamshika vizuri tumboni akamuangalia kwa makini ndipo akachukua dawa fulani na kumkabidhi ainywe katunje alikunywa, alianza kutapika nyama zote na jinsi alivyokuwa akizivamia kwa fujo. aAliishika moja na kuanza kusikitika " Kijana ulikula wapi hizi nyama" Ukelele aliuliza " Mwanzo wa kijiji nilipofika na kuuliza" Katunje akajibu "Mwanangu umelishwa nyama ya mtu" Mzee ukelele akamueleza kuwa katunje kalishwa nyama ya mtu " Nyma ya mtuuuu......Mamaaaaa". Ndani ya kijiji cha CHAMLO, ilianza kuwa gumzo kubwa sana kwa LYOTO kuolewa na Kijana wa mzee kiongozi pale Chamlo bwana BAMUZI. Wanawake wa pale hasa NAOMI alishindwa kuamini kabisa kama Bamuzi kaamua kumuacha yeye na kumchukua mwanamke ambae hafahamiki wapi ambako anatokea, haikuwa kwa wasichana tu bali hata kwa watu wa kawaida ilikuwa ni ajabu sana kwao wao kufanya vile. Mzee Mwalami ndie ambae alimuokota yule mwanamke aliitwa kwenye moja ya kikao cha viongozi ili aulizwe maswali kadhaa kuhusiana na binti LYOTO KATUNJE, mzee huyo alifika siku hiyo ambayo aliambiwa kuwa anahitajika wazee kadhaa akiwemo mzee ngololo, pamoja na Bamuzi mwenyewe huku Lyoto aliachwa akiwa na wanawake ambao wanamtazama kwa umakini kama moja ya kazi yao kuhakikisha anakuwa salama muda wowote pale. "Jamani siku ambayo nilifanikiwa kuonana na huyu binti ilikuwa kama bahati kwani aliletwa na maji yaendayo kasi sana kupitia ule mto lakini pale alipo anafahamu jina lake pamoja na la baba yake ambae ni huyo KATUNJE hajui wapi anatokea ndipo nikaona vyema nimsaidie kwa kuwa kiongozi wetu anasaidia watu". Walifurahi kwa maelezo mazuri ya mzee yule japo wengine walikataa kabisa yale maelezo lakini BAMUZI alimaliza kwa kusema yule ndie chaguo lake watake wasitake. Mama Naomi pamoja na Naomi walisikitika sana kitendo cha Bamuzi kufanya vile " Hivi mwanangu anakasoro gani mpaka amchukue mwanamke wa kuja tu hapa?" Naomi na yeye alikuwa anamlilia mama yake amsaidie kwani anampenda sana Bamuzi kupita maelezo. "Mama...mmaaa...nisaidie mama yangu... nampenda sana unadhani nitaiweka wapi sura yangu na mimi najulikana kijiji kizima kuwa ni msichana mzuri sana jamani alafu anaamua kwenda kumchukua mwanamke asiejulikana... .Mama wewe kama kweli unanipenda fanya mpango wa kuharibu ndoa yao..." "Naomiiii...kuharibu ndoa ya mfalme mtarajiwa Bamuzi huoni kuwa ni laana hiyo mwanangu!" Naomi hakutaka kuelewa "Kama hivyo ni bora hata mimi njinyonge kuliko kuonekana nje nachekwa na watu" Naomi alifikia hatua ya kutaka kujinyonga "Basi mwanagu nitasafiri umbali japo mrefu hadi kwa mzee UKELELE kule MPOLONI nimuombe atusaidie ikiwezekana amuondoe huyu mwanamke kwani akiondoka yeye wewe ndie utatawala na kuwa na nafsi kubwa kwa BAMUZI. Muda mchache baada ya kumaliza kikao cha wazee wale ghafla mwanamke mmoja ambae ni mwangalizi wa binti mfalme mtarajiwa LYOTO alifika pale hukua akihema na kuonyesha kuwa ndani kuna tatizo, Bamuzi alikuwa wa kwanza kwenda kumuona mkewe alikuwa kazimia hana fahamu kabisa japo walihojiwa hakuna jibu sahihi zaidi ya lile walilosema kuwa walishtuka tu anaanguka chini na kuzimia. Aliitwa mzee ambae anahusika na matibabu katika jengo lile la Mzee Ngololo alimpima na kumuangalia kisha akasema " Jamani hapa kuna kazi kubwa, huyu mwanamke kakoswa na uchawi wa kijini kwa hiyo kuna madhara makubwa sana ambayo kayapata na hapa hawezi kuamka mpaka nikague uchawi gani na umetokea wapi mpaka umkusudie huyu, nikitambua kuwa ni aina gani ya uchawi basi nitajua dawa ya kumtibu na atakuwa vizuri", Alimaliza kwa kumfunika na nguo kama mtu aliyekata roho huku akijiandaa kufanya utaratibu wa kujua chanzo cha ugonjwa huo wa ghafla.........
Wakati LYOTO kalazwa kwenye moja ya kitanda pale ndani huku kijana BAMUZI alianza kuchanganyikiwa kwa kutoamini kwa lile jambo ambalo limemtokea mchumba wake mpya. Walikaa na kumsikiliza Mzee NGOLOLO atasema nini kuhusiana na matibabu ya Lyoto. Baadhi ya wanawake wa makamo ambao walichaguliwa kama wasaidizi katika nyumba ile ya Mzee Ngololo walianza kulia sana kwa kuhofia maisha ya yule mwanamke. Mzee mmoja alimfuata Kiongozi bwana Ngololo na kumuuliza swali "Mzee samahani hivi huyu mwanamke mnamjua kweli mpaka mmekubali kumuozesha mfalme wetu mtarajiwa?". Swali hilo lilikuwa kama kidonda kwa mzee huyo ambaye alikuwa na majonzi juu ya lile tukio lililomtokea pale kwake. "Ukweli ndani ya kijiji cha CHAMLO hakimtupi mtu kama sisi tusivyomtupa yeyote hapa kwetu, kwa hiyo huyu binti ilitulazimu kumkubali kwa sababu mwanangu kampenda pia maelezo ya mzee Mwalami yanadhihilisha kuwa anahitaji msaada mkubwa". Baada ya hapo hakuwa na swali lolote japo alionekana kuwa na maswali mengi baada ya kumuona kuwa kiongozi kakasirika kutokana na kuchanganyikiwa juu ya lile swala. Muda ulipita masaa yaliyoyoma kama sekunde, Mfalme wa pale Ngololo alimuita yule daktari aje kumpatia jawabu ambalo litamsaidia sana katika kumuokoa yule binti, kwa upande wa Bamuzi hakubali la kuambiwa kwa jinsi alivyotokea kumpenda sana Lyoto Katunje alikuwa yuko tayari kufanya jambo lolote ambalo hata kama litakuwa na madhara kwake lakini lengo afanikishe. Mzee daktari ambaye ni mahususi sana kwa kutibia watu wote ambao wanapatikana pale kwa mfalme Ngololo, pamoja na wanakijiji wote wa Chamlo. "Haya bwana KELEBU, nadhani sasa muda umewadia wa wewe kutupatia majawabu nini zaidi kimefanyika na nini kifanyike ili tufanikiwe kuokoa maisha ya mkwe wangu yani huyu binti". Aliuliza swali kwa bwana Kelebu ambaye anahusika na swala la utibabu wa Lyoto ambae mpaka mudas huo hajielewi kabisa yani kazimia kabisa hajitambui kwa masaa kadhaa baada ya kupigwa kwa uchawi ambao haujulikani wapi umetokea. "Mzee wa Chamlo pamoja na mtoto wako ambae ni mrithi wa Chamlo, ninachokisema mbele yako hakika ni ukweli mtupu, kwamba....Lyoto kapigwa na uchawi wa kijini na mizimu, iliyotumwa mbali ambako sijapafahamu". Ndipo Mzee MWALAMI alidakia kwa kuwa yeye ndie anamfahamu yule binti tangu siku ambayo alimuokota kutoka kwenye bwawa, " Sasa bwana Kelebu samahani umefahamu hiyo dawa ya kumponya?". Aliuliza mzee huyo ili apate kujua "Ndio ila inapatikana mbali na hapa kwani kuna Miti ya zamani sana ambayo inapatikana Msituni, huo ni mkubwa sana lakini kabla ya kuingia ndani ya msitu huo umezungukwa na miti hiyo mikubwa sana, sasa utomvu wake pamoja na majani yake ndiyo dawa sahihi katika kumtibu binti huyu". Baada ya kusikia vile kila mmoja alikaa kimya kabisa huku wakiwa wanawaza na wasijue nini wafanye, ndipo BAMUZI alifungua kinywa chake na kusema "Sasa, mganga wetu hakuna jinsi nyingine ya kumsaidia mke wangu?" Hapo waliinua vichwa vyao na kumuangalia muulizaji na anayetakiwa kujibu "Mkuu samahani kuwa hakuna njia rahisi zaidi ya hiyo kwani hayo majani ndio maalumu kwa kuponya hayo maradhi". Baada ya muda kupita majira ya jioni waliendelea kujadili mpaka walipokubaliana kuwa kuna umuhimu wa kumtafutia dawa hiyo kokote iliko, waliomba sasa nafasi ya kuwapata wale vijana ambao wakaojitolea kwenda umbali huo wote. Ndipo siku ya pili waliitwa wanakijiji wote wa Chamlo ili wapewe taarifa na wajue ni nani ambae atakubali kwenda msituni ili kutafuta dawa hiyo ya kumsaidia Lyoto. "Wanakijiji wa Chamlo tuna habari ya huzuni hapa tulipo, kwani mke wa ambae Kijana wangu alimchagua kwa bahati mbaya kapatwa na maradhi makubwa sana ambayo yamethibitishwa na Mganga wetu wa hapa kijijini bwana KELEBU, na akasema kuwa dawa yake haipatikani hapa bali inapatikana Ndani ya msitu mkubwa uliopo mbali kidogo na sisi hapa, sasa kilichoombwa kutoka kwetu ni vijana wajitokeze ambao watakuwa bega kwa bega na BAMUZI mpaka huko na kuchukua hiyo dawa ili kumsaidia mke wake...sasa tupo tayari kumpokea yeyote kwani mpaka sasa hivi mgonjwa anaharibika mwili wake". Waliendele kusubiliana pale huku wengine wakinong`onezana kimyakimya huku wengine wakitoa kama maneno ya kulaumu sana 'Tulisema sisi mnamchukua mwanamke ambae wa mbali matokeo yake ndio hayo, hamumju hata chembe ataenda mwenyewe huyo aliyekuwa nae` ni maneno ambayo yalikuwa yakisemwa na watu baadhi wakiwa kwenye kundi la watu kubwa wakijiamini kuwa sauti hiyo haitowafikia walengwa. Mpaka muda unapita hapakutokea yeyote pale. Upande wa nyumba ya mama NAOMI akiwa na mwanae, Naomi alimueleza mama yake kila kitu kwa kilichotokea kule " Mama kwani wewe ndio uliemuendea kwa mganga ?" Alimuuliza swali mama yake huku mama huyo akiwa kama anapumbazwa haelewi chochote "Unaongelea nini?" " Yani nasikia kuwa yule mwanamke, anaumwa na wanatakiwa wapatikane vijana kwenda na BAMUZI kuufikia msitu ambao dawa inapatikana" Naomi aliongezea. "Hapana mwanangu, mimi sijafanya hivyo mana nilikuambia kuwa nitaenda kwa mzee UKELELE kule MPOLONI ili niwaachanishe lakini si kumuua". Maneno mabaya yalipandikizwa kwa wanachi wa Chamlo kutohitikia wito wa mfalme wao na kupelekea Mzee Ngololo kuhuzunika sana "Hivi ni kweli mimi leo nitoe kauli na watu wasiifuate, ama kweli undugu kwenye raha na shida". Bamuzi yeye kama mwanaume alijitokeza na kumuambia baba yake japo alikuwa anamkataza " Baba naomba niruhusu mimi mwenyewe nielekee huko sitojali nani kanifuata nataka kumsaidia Mke wangu". Hakuna ambae aliweza kuamini kama Mtoto wa mfalme ambae anatarajiwa kuwa Mfalme ajitoe kwenda kutafuta dawa hiyo, Mzee Kelebu alimueleza kuwa anatakiwa ndani ya siku mbili kuanzia kesho yake awe tayari amesharudi, Kijana Bamuzi alijiandaa kwa ukamilifu huku machozi yakimtoka kwa wingi kutokana na machungu ya mtu wake wa karibu sana. Siku ya pili yake aliondoka na walinzi kama watatu hivi wakumsaidia chochote kibaya ambayo kitaweza kutokea mbele yao wakiwa safarini, Safari ilianza kwa kuagwa na watu kadhaa waliojitoa na kwa moyo japo hawakuwa na uwezo wa kwenda nao kwa pamoja, walionekana kupotea na njia ambayo iliwaonyesha kule ambako wanaelekea. Mzee UKELELE ndani ya kijiji cha MPOLONI alipomaliza kumueleza KATUNJE kuwa kalishwa nyama ya mtu hakuweza kuamini alianza kutema mate ovyoovyo kana kwamba mtu mwenye dini ya kiislamu anapolishwa nguruwe hali ya kuwa wao hawaruhusiwi kuila na akaambiwa kuwa umelishwa nyama ya nguruwe, laaah! kitakachotokea hapo Mwenyezimungu shahidi, Katunje alihamaki sana kwa kusema maneno mengi sana "Haaa! asalalee yani nikirudi pale watanitambua mbona watu wanakuwa na unyama hivi ina maana hapa mnakulana nyama wenyewe kwa wenyewe?". Hayo maneno yote aliyamaliza huku Mzee huyo akimuangalia tu, alimtuliza wakati Katunje akiwa na hamasa ya kutaka kulia kwa yale aliyofanyiwa na wanakijiji wa pale MPOLONI. "Kijana haya kabla ya yote ebu nieleze vyema sana shida yako ni nini mpaka mwanangu kakuelekeza kuja hapa". Mzee ukelele alimuuliza swali ili ajue kwanza shida ambayo ilimpeleka pale kwake kutoka kijiji cha KILIMALONDO ." " Baba samahani yani mpaka sasa yani sijielewi kabisa mimi natafunishwa nyama ya mtu aaaah jamani!, sawa ila shida yangu kubwa nimekuja pale kijijini naishi na binti mmoja ambae nilimuokota Ndani ya kijiji cha BWAWANI nikiwa na harakati za kumtafuta kaka yangu CHITO, nimeishi nae pale kwa muda mrefu huku mzee KAUZIBE aliyekuwa akinisaidia kumuuguza lakini mpaka sasa binti huyo kapotea kwa mazingira ya kutatanisha siyaelewi na baada ya kufuatilia naziona nyayo ambazo zilinipa akili kuwa alikuwa anafukuzwa, ndipo Mama Mwaija akanielekeza huku kwani wewe una agua nyayo za watu zilikopita." Mzee Ukelele alishusha pumzi nzito kisha akamuuliza swali kijana Katunje " Huyo mzee wa hapo kijijini kwenu anajihusisha na nini?" Mzee Ukelele alimuuliza katunje "Kuna wazee wawili pale nyumbani kuna KAUZIBE na UDEVU huyu Kauzibe ni mwindaji na Mganga wa miti shamba kwani ndie aliyemsaidia huyo binti mpaka akawa na hali nzuri, na huyu Mzee Udevu huyu ni mfugaji wa kuku na mbuzi wawili pale kijijini" Alimaliza kwa kutoa na kwikwi za hasira ya kulishwa na nyama ya mtu. "Kijana tulia usiwe na shaka kwani kazi uliyoingia hapa ni kubwa sana, kuna misaada miwili ambayo naweza kukusaidia mmoja wapo upo tayari?". Katunje alikuwa kachanganyikiwa kwani tangu afike hajapumzika na kapata habari mpya ya kulishwa nyama ya mtu pale kijijini wakati anafika hivyo alikuwa anajibu bila hata kufikilia majibu yake "Baba niko tayari" "Sasa msaada wa kwanza una vipengele vitatu ambavyo utahitaji nikusaidie kimoja wapo, la kwanza kumfuatilia huyo mtu ambae alikuwa anamkimbiza huyo binti kama madai yako, pili kumfuatilia huyo binti wapi kaishia tatu kukusaidia wewe uliyelishwa Nyama ya mtu ili usiendelee kulishwa na ukafanywa msukule hai bila kujijua Ipi nikusaidie?" Katunje alikodoa macho kama panya aliyebanwa kwenye mlango. "Baba, yani kumfuatilia mtu aliyemkimbiza Binti!, Kumfuatilia Binti aliko au kujisaidia mimi niliyelishwa nyama ya mtu ili nisifanywe msukule hai! Mh mbona ngumu baba basi na msaada wa pili upoje" Aliuliza Msaada wa pili ili auangalie kama utakuwa ni mwepesi aufanye, "Msaada wa njia ya pili utahitajika kusafiri kwenda msituni ambako kunapatikana Miti mikubwa iliyozunguka msitu huo mti huo una faida kadhaa kwanza kuondoa mikosi,nuksi na uchawi wowote ambao umekupata pia unaweza kutambua kitu kilichopotea endapo tukichanganya na dawa nilizo nazo hapa". Hapo ndipo kijana Katunje aliona hali imekua tete alijitahidi kudadisi kujua huo msitu uko mahali gani ili aweze kwenda kwani ni bora aufanye huu na yeye ajisaidie moja kwa moja na amsaidie binti LYOTO. Aliambiwa kuwa kesho ajiandae yani hakuna kupumzika." Utaondoka hapa usiku wakati unakaribia asubuhi safari yako itapita kijiji kimoja kinaitwa CHAMLO hapo utaulizia njia moja ambayo inaelekea huko ila ukishindwa kwa kuona kuwa umechoka utamuulizia Mzee MWALAMI na yeye atakuelekeza bila wasiwasi. Asubuhi na mapema kweli safari yake ilianza na Mzee Ukelele alimsindikiza huku akimsii awe makini sana katika safari yake. Katunje kwa kuwa ni mgeni alikwenda huku akiwa makini sana njiani huku akifuata maelekezo yale ambayo kapewa na Mzee Ukelele. Ndipo Mzee huyo aligeuza njia na kurudi nyumbani kwake huku akiwa na imani kubwa kuwa kijana huyo atafanikiwa kufika salama na kurudi na hiyo dawa ambayo kamuelekeza. Anaonekana Mzee KAUZIBE akirandaranda kwenye moja ya pori huku akiwa kama mwenye kutafuta kitu ambacho kilimpotea kwa muda mrefu sana. Baada ya dakika kadhaa alifika kwenye mtiu mmoja ambao alichuchumaa na kuanza kufukua kwenye mizizi ya mti huo, alikata moja ya mizizi na kutia kwenye kikoba chake muhimu ambacho alikuja nacho. Baada ya kumaliza hapo ndipo akaelekea kwenye yale maporomoko kisha akachuchumaa tena alitoa zile dawa zake na ile mizizi ambayo aliichimbua muda mfupi uliopita, alichukua jiwe na kuanza kusugua mzizi mmoja baada ya kumaliza alilamba huku akiugulia uchungu uliotokana na mzizi huo. baada ya kumaliza alisugua tena kisha akachukua unga ambao ulionekana una rangi ya nyeusi. Aliinuka na kwenda sehemu fulani ambako ulionekana kuna mti ambao uliokuwa unaungua akachukua kuni moja ulioshika moto vyema kisha akarudi pale alipokuwa mwanzo. akachukua unga mwingine ambao aliuweka kwenye moto na ukaanza kufuka moshi mzito sana alianza kuongea maneno ambaypo alikuwa anayafahamu yeye mwenyewe, baada ya kumaliza alinyanyuka na kurudi nyumbani kwake, wakati hayo yanafanyika Mama Mwaija alikiuwa anayashuhudia kwani hakuwa mbali na maeneo hayo "Ahaa kumbe huyu mzee ndio alivyo kha! ngoja arudi kwanza KATUNJE nimueleze".Mama huyo alifikilia kwanza ndipo akaenda kwa Mzee SWAI ambae alionekana kwa kipindi hiko hali yake kuwa si nzuri sana, Baada ya kufika pale alimueleza yote ambayo alihisi kuwa aliyaona kwa ufasaha akiyafanya mzee Kauzibe "Babu, niliyoyaona kweli nadhani huyu mzee atakuwa anahusika kabisa kwenye swala la kupotea kwa binti Lyoto". Mzee huyo wa makamo sasa akiwa anasimamiwa na kijana maarufu bwana KIMOLO, lakini hali ya mzee huyo ilikuwa ngumu sana kufanya chochote ndio maana hata swala la kumfuatilia binti LYOTO ilishindikana kabisa na aliweza kutamka kuwa asiendelee kufuatiliwa yeyote kuhusiana na huyu binti na baada ya kuambiwa na mama huyo kuhusiana na Mzee Kauzibe alishtuka kidogo na kuanza kutaka kusimama lakini alishindwa kutokana na hali yake "Mh! haya mambo sasa yanazidi kuchanganya kichwa changu, huyu bwana sijajua ana nia gani na mimi mpaka sasa wakati nilishaamua kuachana nayo sasa wewe nenda alafu alafu sisi tutakuja kukupa taarifa". Mama Mwaija aliondoka huku akiwa na imani kubwa sana kuwa mzee huyo atajulikana ile tabia yake. Huku mzee SWAI alimuita Kimolo na kumuambia kitu "Kijana hali yangu sio nzuri sana kwa sasa nakuomba umuagize yule kijana ambae huwa anauza mifugo aende kuuza tena ili ipatikane fedha za kuniuguzia na pia wewe mtafute kijana ambae nitamuelekeza akamtafute Mganga ambae atanihudumia kutokana na hali yangu". Kimolo aliitikia na mara moja alienda kumuita yule kijana na kumpatia maelekezo muhimu ambayo yalimfanya aelekee kufanya hilo jambo. Kijana huyo alienda kuchukua baiskeli yake na kumpakia mbuzi mkubwa kwenye tenga ambalo huwa analitumiaga kwa muda mrefu, Wakati akiwa njiani alifaniiwa kukutana na vijana wenzake ambao walimuuliza kuwa wapi ambako anaelekea ni maeneo gani, kwa kuwa yeye ni mmoja wa kijana wa pale aliwaeleza wapi anaelekea na anaenda kufanya nini. Ndani ya kijiji cha BWAWANI ambako kijana huyo anaelekea kuuza mbuzi huyo kwa kuwa mara ya kwanza alifanikiwa kuuza kwa muda mfupi, Mzee MANUALI akiwa nyumbani kwake akiwa anaendelea na kumuuguza mjukuu wake SUSU ambae alipigwa gongo la kichwani na kupoteza kumbukumbu, matibabu yalifanyika kwa muda mrefu huku akionyesha matumaini kwani susu aliweza kuongea lakini kumbukumbu zilikuwa zishapotea. Huku pia Mzee SIKUJUA ambae na yeye alikuwa nyumbani kwake akiwa na mawazo makubwa sana juu ya maisha ambayo aliyafanya kipindi cha nyuma na kusababisha kuishi kwa wasiwasi sana. "Haya maisha mpaka lini jamani, naishi kwa wasiwasi mang`amung`amu kila siku nikilala mala jana usiku MAMA MENGI namuotea kuwa anakuja kurejesha kuniua,mama Mengi anakuja na kisu kuja kuniua mimi mh! hapana kabisa itabidi nifanye jambo muhimu kwa sasa".Muda mchache ndipo anaingia yule kijana huku akinadi mbuzi kuuzwa kwa http://deusdeditmahunda.blogspot.com/bei rahisi "Mbuziiiiii, mbuziiiiiii kwa bei rahisi sana". alikuwa anaongea hayo maneno akiwa ndani ya kijiji akizunguka mitaa ya hapa na pale. Alifanikiwa kufika hadi kwenye nyumba ya mzee mwalami ndipo anamkuta kijana SUSU ambae alitokea kumkumbuka. Alishuka kwenye baiskeli yake na kwenda kumsalimia kijana huyo "Babu vipi rafiki yangu anaendeleaje na hali yake" aliuliza huyo kijana muuza mbuzi wa mzee swai. "Salama kabisa kijana umekuja kuuza mbuzi tena baada ya muda mrefu kupita," Mzee mwalami aliongea. "Mbona kama rafiki yangu hali yake si nzuri sana kimemtokea nini". Mzee mwalami alimueleza kila kitu na ndipo kijana huyo akendelea na kazi yake ya kutangaza mbuzi. Kwa ujasiri mkubwa sana bwana CHITO anaonekana kuwa na jazba kubwa sana juu ya baba yake pale nyumbani mzee MAMBO SASA, "Kwa hali kama hii baba lazima ataniambia mke wangu yuko wapi yani haiwezekani mke wangu kwa nini hamtaki naamini yeye ndie kampoteza" Upande wa bwana Mambo sasa akiwa na rafiki yake walionekana kufurahi sana katika kazi ambayo wameifanya " Sasa bwana Mambo sasa hapa tumemaliza kazi kabisa lile kombola ambalo tumelipeleka kule hakika litamrudisha kabisa hadi hapa" Aliongea bwana huyo ambaye ni rafiki wa mzee Mambo sasa. "Sasa una maana kuwa hii itamfanya popote alipo atarudi yeye mwenyewe kabisa". Mzee huyo aliuliza "Ndio kwani ule mzimu naufahamu kabisa yani muda hautofika kuwa siku nyingi majibu tutayaona hapahapa sasa wewe nenda nyumbani ila kumbuka kuwa usiku utaenda kumueleza mkuu kuwa mambo yanakaribia kuwa mazuriu kwani yule mtu uliyemuahidi anakuja ". Mzee mambo sasa alionyesha kufurahi "Lakini kuna yule mkwe wangu ambae nimemuweka kule ndani si nilikuambia?" "Ahaaah! kumbe, huyo nenda kamkate ulimi kabisa mapema alafu chukua hii dawa ambayo utamnywesha baada ya kumkata ulimi wake." Ndipo mzee huyo aliondoka kwenye nyumba ya rafiki yake na kuelekea nyumbani kwake. Wakatii huo kijana CHITO aliondoka nyumbani kwake na kwenda mtaani kumtafuta baba yake popote alipo, lakini kwa bahati iliyoje bwana MAPATO anafanikiwa kumuona Chito ambae yeye anamjua kwa jina la Mambo sasa bila kufahamu kuwa mzee mambo sasa ni baba wa chito ambae anamuona kwa muda huo. Mzee Mapato alimuuliza Mwenyekiti bwana MASANJA "Baba hivi yule mzee unamfahamu ambae anapita kule mbali". Mzee masanja aliangalia kwa makini sana kisha akamshika bega na kumuambia kuwa "Namfahamu vyema huyu mzee anaitwa bwana CHITO" mapato alishangaa kwanza "Naniii?" "Anaitwa chito aliondoka hapa kijijini kwa muda mrefu sana baada ya kugombana na baba yake ambae hakumtaka mke wake ndipo akaondoka kwa muda mrefu na sasa karudi tena" Baada ya kupata taarifa hiyo ndipo mzee Mapato akashtuka sana " Kama anaitwa chito na baba yake anaitwa nani?" Mzee Masanja alimshangaa sana kijana huyo "Nashangaa sana kijana kwani unamfahamu huyu?" " Hapana ila nimependezwa na habari yake ndio maana nataka nimfahamu baba yake pia". mzee masanja alifurahi sana "Ndio baba yake anaitwa Mzee MAMBO SASA na ni mmoja katika wale wazee ambao ni hatari sana katika wale wazee niliokutajia " Mzee MAPATO alishtuka sana ndipo akawa anashangaa mno " Ina maana kuwa ahadi niliyoweka kwenye ile mizimu Mzee Mambo sasa si huyu kabisa mamaaa itanibidi nirudi kabisa nyumbani kwanza au ngoja nimfuatilie nipajue anapoishi kwanza". Hapo ndipo alipojua kuwa kaingia sehemu siyo mtu aliyemkusudia ni tofauti na alivyokuja kuelezwa sifa yake ndipo aliamua kumfuatilia taratibu ili ajue wapi ambako anaishi yule mzee.. Mzee Mambo sasa alifika nyumbani huku akiwa na jukumu la kwenda kumkata ulimi mkwewe. lakini kabla ya hayo yote alifikilia kitu tofauti na hapo ambacho kinaweza kumfanya asijulikane na mwanae kuwa yeye ndie ana nia ya kumuweka msukule mkwewe, ghafla mwanae bwana Chito anaingia nyumbani hapo huku akiwa na panga lake mkononi "Baba nakuomba uniambie mke wangu siku ya pili hii haonekani umemuweka wapi?" Mzee mambo sasa alihamaki pia baada ya kumuona mtoto wake kaja kwa hasira " Nataka uniambie ukweli juu ya mke wangu hii ndio sababu hata katunje leo hatujui yuko wapi tuliondoka kwa mambo yako ya kijinga mama umemuua wewe nina uhakika utabadilika lini yani hapa nakuambia huniambii chochote nahitaji uniambie la sivyo nakuua na ni bora ufe huna faida mzee kama wewe" alimfuata kwa hasira huku akinyoosha mkono wake na kutaka kuushushia kwenye mwili wa baba yake ambae anamtuhumu kuwa kampoteza mkewe, ghafla mkono wake unashikwa nyuma na kufanya akose umakini wa kumshushia panga baba yake aligeuka nyuma anashangaa kabisa kumuona bwana MAPATO yupo pale na ndie ambae kamshika mkono akimsimamisha asifanye maamuzi magumu "Yani Mzee MAPATO umepajuaje hukuuu?"......
CHITO alishtuka na kustaajabu sana baada ya kuona mkono wake ukiwa umeshikwa na mtu ambae hakumtarajia kabisa kuwa atakuwa pale kwa muda ule, kama binaadamu wa kawaida lazima hali ya mshangao itakukuta kwa kuwa unakiona kitu ambacho hukutarajia kuwa kitakuja na kwa wakati gani hasa kwa bwana Mapato kuja ndani ya kijiji cha SHISHIMO bila hata yeye kujua kama takuja pale na kupafahamu nyumbani kwake, Alibaki kuduwa kwani neno lake la mwisho lilikuwa ni kumshangaa kwa kuja pale na kumzuia kufanya kile kitendo ndipo mkono wake ulipooza na kurudi chini na hatimae kuachia panga lake. Bila bwana mapato ilionyesha wazi kuwa Mzee Mambo sasa alikuwa anakula panga la mwili kabisa bila kujali kuwa ni baba yake, hayo yote alikuwa anayafanya kwa uchungu wa mkewe na kwa ajili ya kuyajua maovu ya baba yakle kuwa anajishirikisha na mabo ya kishirikina kwa muda mrefu hivyo hakuwa na imani juu ya baba yake na alimtuhumu kuwa moja kwa moja baba yyake chito na ndie ambae atakuwa anahusika kumfanyia vibaya mkewe kwani siku zote mchawi hana huruma hata mwanae atamtafuta. Mapato alichukua muda huo kuutumia udhaifu wa Chito na kwenda kumtoa baba yake chito na kumuweka pembeni kwanza huku akimuonyeshea huruma, mzee Mambo sasa nae alikuwa hamfahamu huyu kijana kwani kwake mzee mapato ni kama kijana tu japo uzee ulikuwa unamuanza, aliendelea kumuangalia kwa makini lakini akaona kuwa ni sura ngeni machoni mwake. "haya Mambo sasa twende nje kwanza tukaongee punguza jazba kwani hasira ni mbaya sana huyu baba yako bwana". Kitu kilichokuja kumshangaza sana bwana Mambo sasa wakati kijana huyo asiyemfahamu anakuja kumtoa Chito alimuita kwa jina la Mambo sasa, 'itakuwa hawa wanajuana hawa ila kwa nini amuite kwa jina langu'. Walitoka nje na kwenda mbali kidogo na nyumbani kwa baba yake Chito, lengo lilikuwa ni kumtiulioza jazba aliyonayo kwa muda ule kwanza asije kuharibu mazingira. Wakati wao wanaendelea huku nyumbani mzee Mambo sasa aliingia ndani mwake, hatimae mama sikitu anaonekana akiwa kwenye pembe ya chumba akiwa kafunikwa kaniki jeusi huku akitetemeka kama mtu ambae alikuwa anatetema baridi kali sana. Mzee huyo nbila huruma alitoka na kwenda kuchota makana ya Mahindi kwenye sebule ya nyumba hiyo ambayo yaliwekwa kwa nia ya kuuza kwa wale wanaopika pombe za kienyeji aina ya ULAKA unaotengenezwa kwa makana ya mahindi, lakini wakati anayafanya hayo alikuwa na wasiwasi wa kukutiwa na Chito hivyo ilimfanaya kumwagamwaga yale makana hadi kwenye chumba chake. Baada ya kufika kule alimpiga kidogo mdomoni ndipo akaachama na akamlisha makana yale kwa wingi baada ya hapo akaenda kuchukua maji na yaliendelea kumwagika vilevile mpaka kule chumbani na akamywesha. Hakika Mama sikitu kwa huruma sana alikuwa anatoa chozi tu bila kuongea chochote kabisa. "Yani kupona kwako wewe mpaka pale Mtoto wako atakapopatikana na mimi nikaenda kulipa nyama kwa wenzangu ndipo utatoka humu la sivyo milele utakuwa hivyohivyo nyooooooo". Maneno hayo yalionekana kama anayaelewa kwani alikuwa anatoa machozi kwa huruma kwa unyama ule ambao anafanyiwa. Ni mtu gani ambae anakosa hata huruma kabisa na mwanadamu mwenzake hadi kudiriki kumfanyia unyama kama anaofanyiwa mama Sikitu. Baada ya kumaliza kumfanyia yale aliyomfanyia akachukua dawa fulani na kunyunyuzia kwenye mlango wake huku akisema maneno kadhaa bila kusahau kumtaja kiongozi wao Nyamnyena kwani ndie anayewafanya kuwa wakubwa pale ndipo akaondoka. "Rafiki yangu nilitoka Bwawani kwa sababu moja tu pale, nilitumwa na Mzee SEMENI yule mwenyekiti nikutafute wewe popote ulipo ili wajue kwa nini umetoka kule kijijini wakati Mzee Mambo sasa ulionekana kuwa na msaada mkubwa pale kijijini" ni maneno ambayo alikuwa akliyaongea bwana Mapato kumuambia Chito. "Aaaah! kwanza ahsante kwa ushauri wako wa mwanzo ila kwa nza siitwi Mambo sasa hivyo nisingependa kuwepo kwako hapa uniite kwa jina hilo" Mapato alijifanya kushangaa japo taarifa ya jina lake analifahamu fika baada ya kuambiwa na mzee Masanja. "Aaaah! mbona unanichanganya sasa ehee jina lako nani " Aliuliza mapato. "Eheee! mimi ninaitwa CHITO nilitumia Mambo sasa baada ya kufika kijijini kwenu kwa sababu kama ile uliyonikutana nayo pale ukweli matatizo ya kifamilia na nilishawishika kurudi nyumbani hapa baada ya kule Bwani kupotelewa na mwanangu kipenzi SIKITU" Mapato alionekana kuhuzunika sana huku akimpa pole kubwa sana "Mh! pole hayo nayafahamu sana hata mimi niliagizwa kukuomba ufike kule lakini kwa hali hiyo ehee kuna habarii yule kijana SUSU unamjua " alihoji "Yeye tena namfahamu vyema mbona yani siku chache tu hizi niwe nimesahau jamani" walicheka kwa pamoja huku wakionyeshana vidole. "sasa yule kijana alikamatwa na watu ndipo mzee wake MANUALI akamtafuta kama unavyomjua akitoa kauli zake pale ajabu siku moja anaonekana lakini akiwa na matatizo ya kichwa yani hata jina lake sijui kama atakuwa analikumbuka pale alipo maana" Mzee chito alionekana kushangaa sana "Hivi kile kijiji chenu kina shetani gani jamani maana lakini huyu kijana naamini kama hakufanya mabaya maana nakumbuka alinifanya nikose haki yangu baada ya mimi na mzee SIKUJUA kwenda kwa mzee SEMENI kama mwenyekiti na shahidi yangu alikuwa yule lakini alinigeuka ila pole yake" Baada ya maongezi ya muda mrefuwaliagana na kila mmoja alielekea kwake. Mzee Chito alifika nyumbani kwake akiwa na imani kuwa baba yake atamkuta lakini haikuwa hivyo baada ya kufungua mlango na kutomkuta mtu, aliangalia chini akakuta makana na maji yaliyomwagika yakielekea chumbani kwa baba yake alishangaa sana huku akishika mdomo wake 'Aaah! haya makana na maji huku yanafuata nini' aliendelea kukagua akapata akili ya kufungua mlango wa baba yake lakini akapuuzia 'hivi inawezekana kuwa baba ana nia ya kumuweka mke wangu ndondocha au maan kama kuondoka Mama Sikitu namfahamu hawezi kuondoka bila hata kuniambia hata kama tumegombana kiasi gani'. Hapo ndipo alip[oanza kukumbuka maneno ya mkewe kabla kupotea nini alikisema 'baba yako ni mchawi....unaogopa laana kwa mtenda mambo mabaya hakika laana hiyo haitokufika....nyamnyena maana yake nini....hakika mimi nitaondoka siwezi kuishi na mtu mchawi' hayo yote aliweza kuyakumbuka kwa nyakati tofautitofauti. "Hamna baba kuna namna ambayo kaifanya na nitaigundua tu kwa nguvu maana nikimbembeleza hatosema kwanza kamuua mama, kamfanya ndugu yangu kupotea huko aliko". Ndipo alipoondoka na kuelekea kwa mwenyekiti bwana MASANJA ili aweze kumsaidia kwa mawazo kadhaa kwa mambo yale ambayo yanamsumbua sana. wakati anatembea akili yake inamtuma kuwa mkewe bado yumo mule ndani lakini akili hiyo ianamjia na kumpotea kwani alikuwa anaonekana kusimama kwa sekunde kadhaa na kuendelea na safari, alipofika alimkuta mwenyekiti lakini alishangaa zaidi kumuona bwana Mapato kwani alikuwa hafahamu kuwa mapato kafikia kwa mwenyekiti. "Oooh! kumbe umefikia kwa mwenyekiti wetu bwana MASANJA karibu bwana ila bwana masanja ningekuomba faragha kidogo kuna mambo tuje kuteta". Bwana huyo asiyekuwa na makuu alisimama na kumuomba radhi bwana Mapato kuwa atarejea muda mchache tu. Mapato nafsi yake ilimsuta sana kwani aliona uongo wake utajulikana pale aliomba sana mwenyekiti asije kugusia mambo yake, lakini ilikuwa tofauti sana na fikra zake. "Mwenyekiti samahani kwanza vipi mpango wako wa kuutoa ufalme na kuingiza uongozi mpya wa mwenyekiti na wajumbe unaendeleaje?''. alimuuliza bwana masanja ambae ana kampeni ya kuondoa uongozi ule wa kifalme na kuuweka wa kisasa ambao kila mmoja ana haki ya kuwa kiongpozi kwa kila kijiji, "Aaah! kuhusu hilo lipo mbioni kwani sasa ninahitaji kutembelea kila kijiji nijue uongozi wao unaongozwa vipi kama ni wa kifalme basi nitajitahidi mpaka unabadilishwa". Chito alionekana kufurahi sana "sawa ila nina shida kubwa iliyonileta hapa, najua nilishakuja hapa kukuambia kuwa mke wangu kapotea hii ni siku ya tano sijamuona lakini ninamshuku baba yangu mzazi kuwa anaweza kuwa ni mmoja wa waliomfanya jambo baya mke wangu sasa sijui unanisaidiaje" Mwenyekiti alishusha pumzi kwanza kabla ya kujibu, " Una vigezo gani ambavyo vimekufanya umtuhumu kuwa mzee Mambo sasa anahusika kwa hilo". mwenyekiti alihoji " Yani juzi nilikuta maji yamemwagwa lakini yakielekea kwake yani chumbani, jana makana ila leo nimeyaona maji pamoja na makana sasa nina wasiwasi isije kuwa anamlisha mke wangu hivyo vitu". Mwenyekiti alicheka sana ila alimtoa wasiwasi na kumuambia aende akapumzike kisha atamuita pale "Eti ulivyofika hapa ukanikuta nipo na mgeni alafu mkasalimiana kama mnajuana". Mzee chito akasita kisha akauliza " hapana kwani jina lake nani ?" "Anaitwa SUMAE kafikia hapa". Chito ilibidi aage tu maana hilo jina alilotajiwa ni tofauti ila hakuelewa kwa nini mapato na yeye kabadili jina. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mzee Mambo sasa anaonekana kwa rafiki yake NYANDU ambae ni mtu wake wa karibu sana kwa muda mrefu mno hata katika kazi zao huwa wanafanya pamoja, walionekana wawili hawa kutokuwa na furaha kabisa kwa hali ambayo walikuwa nayo kila mmoja alikuwa kimya akimtaka mwenzake aanzishe mazungumzo ndipo Nyandu akaanzisha mazungumzo "Bwana unajua kuwa Mkuu anatuta hata sijajua kuna nini huko maana wakati nipo hapa kuna ujumbe wa mizimu ulinipa baada ya dawa yangu ya hapa mkononi kukaza sana tena si kawaida" Ilionekana kuwa ni taarifa ya umuhimu sana kwao kuitekeleza kwa wakati huo bila hata kuchelewa "Sasa tunafanyaje" Baba yake chito alihoji " Tunafanyaje itabidi tuende na akatueleze hata ile kazi itabidi tukamuulize kama imefanikiwa" walikubaliana ndipo Mzee Nyandu kwa ustadi wake wa nguvu za giza walivaa makaniki na wakakumbatiana ghafla wakatoweka mithli spidi ya mwanga unavyosafiri. Safari yao iliwafikisha mahali fulani kama jangwani hivi palivyo baada ya kufika kwao ndipo watu kadhaa pia walitokea mbele yao hao walionekana kama walinzi kwani walikuwa na nguo sare huku wakiwa na umakini wa kutosha sana. Walionyeshwa njia ya kupita mahali fulani ambapo palionekana kuwa kama pango, waliingia humo kwa wao ni wenyeji kiasi fulani na hizo kazi hivyo hawakuwa na presha wala wasiwasi wowote. Hatimae walifika sehemu fulani ambako palikuwa na kiti kikubwa mbele yao, ghafla alitokea mtu ambae hakueleweka jinsi alivyo kwani ilisikika sauti na harufu kali sana ambayo Mzee Nyandu na Mambo sasa waliivumilia hivyohivyo, pia pale kwenye kiti palionekana kivuli tu kama moshimoshi hivi ambao una umbo la binaadamu. " Nyamnyenaaaaa.....Nyamnyenaaaaa kulumbila kululmbilolooooo" kwao ilikuwa kama salamu ambayo walianza nayo kumsalimia mkuu huyo. ndipo alipoanza kusema nini kawaitia pale, wakati huo wafuasi wake wako pembeni wengi sana. "'NDIO..NIMEWAITA HAPA KUWAPA TAARIFA KUWA NYAMNYENA KAFANYA KAZI NGUVU IMEPELEKWA LAKINI INAONEKANA HUYO BINTI ANA NGUVU ZA AJABU AMBAZO ZILISHINDANA NA NGUVU ZA NYAMNYENA, ILA ZIMEMJERUHI...T AARIFA ILIYORUDI KUTOKA KWA NYAMNYENA LAKINI INAONEKANA KWENYE MSITU KUNA KIJANA AMBAE ANAFANYA JITIHADA ZA KUCHUKUA DAWA KWENDA KUMTIBIA SASA NIMESHAMTUMA MZIMU ANAYETOKEA KWENYE MILIMA YA LYOTO ( Joto) ATAKWENDA KUMZUIA KINGINE NAMHITAJI YULE MAMA ULIYEMKAMATA BAADA YA SIKU MBILI,..." Maneno makali na yenye msisitizo yalitoka kwea kiongozi huyo na kuwafanya wao wawe na butwaa, walimsalimu tena kama njia ya kumuaga ndipo wakageuza kurudi hapo ndipo mzee Nyandu akamkumbatia tena mzee Mambo sasa na wakapotea kwa haraka zaidi. wakati huo huku CHITO anafika kwenye nyumba ya mzee Nyandu akiwa na Imani kuwa baba yake yupo pale kwa rafiki yake, aligonga mlango ghafla anasikia kishindo humo ndani """"Vuuuuuuupp!"""". Ndani ya msitu ambao umekaribia kijiji cha CHAMLO anaonekana kijana BAMUZI ambae alijitoa kutafuta hiyo dawa akiwa na vijana wake kadhaa kama watatu ambao alitoka nao, Walifika hadi karibu na miti ambayo waliambiwa kuwa iko mirefu sana, wakati huo pia kuna kijana alionekana akirandaranda kwa upande wake anafika kwenye kijiji cha Chamlo bila hata kufahamu kama hapo ndipo mwanzo wa safari yake kuanza. kwa bahati ambayo alikuwa nayo kwa siku hiyo alimkuta kijana mmoja ambae aliweza kumuuliza swali " Kijna samahani sana Nahitaji unielekeze kwa Mzee MWALAMI ". Yule kijana hakuwa na hiyana kabisa alianza kumuelekeza lakini kwa bahati nzuri alitokea NAOMI akiwa njiani kuelekea matembezi yake, "Dada Naomi samahani naomba umsindikize huyu jamaa kwa Mzee Mwalami kule'. Naomi alisimama akimsubiri mtu huyo. Kijana alikuwa makini sana kwa kila hatua.Naomi alikuwa anamuangalia sana Kijana huyo kwa kuwa alikuwa hamfahamu jinaaliendelea kumuibia ibia mwishowe akashindwa kuvumilia ndipo akamuuliza "Kaka unaitwa nani samahani" Naomi alitoa kibwagizo pale ili kijana huyo amalizie "Ahsante Naomi utanifahamu mapema sana ngoja nifike kwanza alafu nitakujuza yote utakayo siku tukionana kwani mimi nipo hapa kwa siku nyingi kidogo". Naomi hakuwa na neno zaidi ya kuendelea na safari hadi kwenye nyumba ya MWALAMI alimkuta ndipo Naomi akaondoka zake. Mzee mwalami alimkaribisha vyema sana ndipo akamuuliza kipi ambacho amekijia pale. " Mzee Natokea MPOLONI kwa bwana UKELELE mimi ni kijana wake ambae kaniagiza nipitie hapa ili wewe unielekeze kwenye msitu ambao unapatikana miti ya dawa kwani kuna dawa ambayo kaniagiza ikiwemo ni njia ya kunifundisha kazi za mitishamba" Kijna huyo alijieleza vyema sana mpaka mzee Mwalami akafurahi sana. "Kijana umefika na unahitaji kwenda lini huko?" Aliulizwa kijana " Nahitaji leo niianze safari kwani muda bado upo na kule kuna matatizo ambayo haitakiwi dawa hiyo kucheleweshwa." "Jambo zuri zaidi ni kuwa hapa mtoto wa mfalme kampata mke sasa huyo mwanamke kapata tatizo, ndipo huyo kijana wa mfalme akajitoa kwenda kufuata dawa kwenye huohuo msitu ambao wewe nakuelekeza hii ni siku ya pili inaanza itakuwa vyema mkienda kusaidiana au kama utahitaji ukamuone huyo mke wa kijana unaekwenda kukutana nae" Kijana huyo alimwambia mzee atakuja kumuona siku nyingine, ndipo akaelekezwa njia fupi sana ya kufika kwa siku hiyohiyo "Ila kumbuka kijana msaidie mfalme wetu huko ukimkuta, alafu wote murudi kwa pamoja sawa kijana ?" Mwalami alimsisitiza "Sawa mzee usijali". Wakati anakatiza kijiji kuielekea njia fupi hiyo anakutana na NAOMI ambae alimsubiria kwa hamu baada ya kumuoana moyoni mwake tayari donge la penzi lilisha anza kuingia 'Mh! huyu kijana sasa nikimuambia kuwa nampenda ataniona mimi sina adabu, sijiheshimu,sina thamani ila nampenda sana ngoja hata nimuulize jina'. Alijisemea hayo wakati yeye kijana anakuja Naomi alijiandaa kwa kumuuliza jambo. "Oooh! Naomi tumekutana tena " Naomi alitabasamu kwa kuona dalili zinajileta, " Kumbe ulitaka kuondoka bila hata kuniambia jina lako yako". Kwa kuwa Kijana huyo alionekana kuwa na haraka sana alimtamkia jina huku akiondoka " Usijali naitwa KATUNJE naelekea kwanza mahali fulani nikirejea tutaongea vyema sawa". Naomi moyoni mwake mlijaa furaha ya ajabu kwani tayari anaonekana kumpenda sana kijana Katunje. Baada ya muda kupita jioni sana alifika karibia na msitu lakini anashtuka anakamatwa na vijana watatu ambapo anageuzwa nyuma anakutana na BAMUZI kwa upande wake yeye hakumfahamu. walimhoji maswali kuna aliyoweza kujibu na mengine hakuweza kabisa "Mimi ni mmoja wa kijana wa mzee MWALAMI hivyo alinielekeza nije kukusaidia lakini mimi nilikuwa naishi kijiji cha mbali hivyo jana ndipo nilifika Chamlo" Uongo alioutumia ulimsaidia wao kumuelewa ndipo wakaungana na kuwa timu moja ya kutafuta huo mti. Jua sasa lilizama kabisa na giza likawa kinala kwa muda huo na kuwafanya wao waanze kuzoea mzingira ya giza, kumbuka ndani ya kijiji cha Shishimo kupitia Mzee Nyandu kutoka kwa mkuu wao tayari jini ambae atakuja kuwazuia hawa anatokea kwenye mazingira ya moto au joto kama maelezo ya mkuu wao alivyowaeleza kule pangoni, hivyo basi kwa upande wa Bamuzi pamoja na wale wengine akiwemo Katunje ambae hakujitambulisha jina pale, Walikuwa wamepumzika ghafla katunje anashtuka kwa pale alipo lala anashangaa kuona kizinga cha moto kikiwa kwa mbali kitu ambacho ni cha ajabu kwa mazingira kama hayo kutokea. Alimuamsha Bamuzi, "Hey hey amka kwanza uone hiki ni nini jamani" Bamuzi aliamka na wale vijana watatu nao wakaamka, walishuhudia kweli kizinga cha moto kikiwa kwa mbali kikiwaka, " Kijana itabidi tufike pale inaonesha kuwa kuna watu wanaishi wanaweza kutueleza kuwa hiyo miti iko wapi" Yalikuwa ni mawazo ya Bamuzi ambae alikuwa hana chochote anachokielewa. Alionekana kijana Katunje kutikisa kichwa huku akiangalia kwa makini ghafla akashangaa ile dawa ambayo kaifunga kwenye mkono wake kwa juu inamvuta sana mpaka anahisi maumivu, aliwaza akakumbuka kuwa 'Mjukuu wangu hii dawa ninayokufunga hata baba yako pamoja na mambo yake ya kichawi hatoweza kukudhuru sasa pindi ukihisi maumivu basi jua kuwa kuna hatari na unahitajika kuondoka haraka maeneo hayo usije kudharau....' alikuwa anakumbuka kauli kutoka kwa babau yake Katunje ambae bado hatujajua mpaka sasa yuko wapi, tunaweza kutambua mbele ya safari. Alisimama na kuwaambia "jamani hapa kuna hatari inatubidi kwa haraka sana tuondoke kabla haijatokea fanyeni haraka tuondoke jamani mniamini". Japo walikuwa wagumu kumuamini lakini iliwabidi ndipo wakatoka pale kwa haraka sana ghafla wanaona kabisa vizinga vya moto vikiwa pale walipotoka kwa wingi na vingine vikawa kama vinarushwa hivi kuwafukuza. Bamuzi hakuamini kwa kile ambacho anakiona mbele yake. Walitafuta mahali pengine ambako walihisi kuwa watafanikiwa kwa bahati [palikuwa salama kabisa, walilala mpaka asubuhi. Walianza kusaka mti huo ndani ya msitu huo lakini wakikumbana na vizngiti vya ajabu ajabu, hatimae wanafanikiwa kuifikia miti hiyo ndipo wakachimba mizizi yake na magome kadhaa pamoja na majani yake waliyachukua.Safari ya kurudi sasa ilikuwa ni kasheshe kwani kila wanakopita Katunje anawaambia ni hatari kila njia kwao ni hatari kabla hawajaendelea anajitokeza jitu lililooza sura mbele yao likitoa midenda huku akishikilia kijiti kinachotoa moto alikuwa anakilamba bila wao kuamini kuwa moto anavyouchezea, ndipo kijana mmoja kati ya wale watatu akajitokeza na kuwaambia " Mfalme huku ni porini tumekuja bila hata kutoa sadaka ya damu ili kama kuna mizimu kama hii basi ituache kutusumbua" kila mmoja alikubaliana na lile swala swali likaja tunafanyaje sasa. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/"Mfalme wangu wewe nenda kapeleke dawa kwa mkeo apone pia nawatakia maisha marefu acha mimi nijitoe muhanga kwa hili " walianza kumshangaa sana baada ya yule kijana kwenda kujitoa mbele ya yule kiumbe fasta sana akararuliwa kwa haraka bila huruma, Bila utata wao wakapata nafasi ya kupita kuelekea majumbani kwao, lakini majonzi mazito ya kumpoteza kijana wao mmoja wakiwa mbele Bamuzi ana angalia nyuma hawamuoni kijana yule ambae walikuwa nae yani KATUNJE. Bamuzi alishtuka sana akaanza kuangalia huku na kule lakini hawakufanikiwa kumuona kijana huyo. "Yani huyu jamaa kanisaidia sana sasa atakuwa wapi jamani". Walianza kumtafuta huku na kule lakini walishundwa kumuona kabisa, walisikitika wakajua kuwa lile jitu la ajabu litakuwa limemmeza. Basi waliondoka huku wakipita kukimbia ovyo hadi walipofika kwenye kijiji chao. Wanakijiji waliwaona wakiingia ndani ya kijiji kile na vijana ndipo walipoanza kuwa na aibu kubwa sana kwa kuwa mwanzo walikataa kabisa kuungana na Bamuzi kwenda kumsaidia kwenda kuchukua dawa na hatimae sasa Bamuzi anarudi akiwa na vijana wake wawili baada ya mmoja wao kujitoa sadaka. Baada ya kufika alipokelewa lakini hakuwa na furha kabisa kwa kupotelewa mtu muhimu sana kama Kijana yule ambae walikutana nae. Walifika baadhi ya vijana kama Mwalami na Mzee Kelebu ambae ni daktari wa pale kwao. Mzee Ngololo alimuendea mwanae Bamuzi akamuuliza "Mwanangu ehee habari za huko " Bamuzi alifuta chozi kwanza kisha akamshika mkono baba yake na kumuambia " Baba inatakiwa tumuombe radhi mzee mwalami pamoja na familia ya kijana ZWELI, "Kwa nini unasema hivo mwanangu?" "Kuna kijana alikuja kutusaidia kule polini ila hata jina lake hakuniambia kwa kuwa sikumuuliza ila alisema alitokea kwa mzee Mwalami sasa kafariki pamoja na kijana zweli kafariki lakini walijitolea muhanga kwa ajili yetu kabisa baba itatubidi tufanye hivyo" Walimuita mzee mwalami wakamueleza huku wakimpa pole lakini mzee huyo alishindwa kuelewa kabisa kwa nini anaombwa msamaha wakati yeye ahusiki na chochote kuhusiana na kijana huyo aliyekuja. " Yule kijana alikuja jana mapema sana hapa kasema anatokea kwa mzee mmoja rafiki yangu bwana Ukelele aliomba nimsaidie kumuelekeza kwenye uo msitu nikaona ni vyema sana akasaidiana na wewe sasa kama kafariki itabidi tupange siku tuende kwa mzee Ukelele kijiji cha MPOLONI ili tukamueleze kwa yaliyotokea.". Kijana Katunje ambae alipita kijiji cha Chamlo bila hata kujulikana kuwa yeye ni nani zaidi kwa binti Naomi ndie ambae kaacha taarifa zake lakini Katunje bila hata kufahamu kuwa ndani ya kile kijiji alichoshindwa kujitambulisha vizuri ndipo mahali husika ambako Lyoto yupo kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.................
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment