Search This Blog

THE RETURN OF THE AMBROSY - 5

 





    Simulizi : The Return Of The Ambrosy

    Sehemu Ya Tano (5)





    Dolin alimuogopa mwanamke huyo aliyefanana naye kila kitu mpaka mavazi, lakini wakati yupo katika taharuki hiyo ghafla huyo mwanamke alipotea. Hapo ndipo alipoamua kujiandaa haraka haraka kisha akatoka chumbani mbio akaelekea kwenye mishe mishe kwani siku hiyo alikuwa na mtoko yeye na mchumba wake.

    Habari hiyo Dolin alimueleza mchumba wake, ukweli ilikuwa ni habari ambayo ilimshangaza sana mchumba wake huyo na hata asiyaamini maneno ya Dolin.

    "Nasema kweli David, hivi tangu lini mimi nikakudangaya?.." Alisisitiza Dolin akimuasa mchumba wake wa kuitwa David. David aliangua kicheko kisha akasema "Bado siwezi kukuamini Dolin,usitake kuniambia nikuhamishe pale sababu kwa sasa sina pesa. Hebu tafuta uongo mwingine wa kuweza kunishawishi na sio kuniambia kwamba nyumba ile inamauza uza" Alisema hivyo David, ni baada Dolin kumuomba amuhamishe pale anapoishi shauri ya mauza uza kadhaa aliyokumbana nayo. Lakini David hakutaka kukubaliana na maneno hayo ya Dolin, alijua kuwa Dolin anadanganya.

    "Sina maana hiyo mpenzi wangu, ama kama nakudanganya naomba usiku wa leo tukalale wote. Nadhani utayaamini maneno yangu" Aliongezea kusema Dolin kwa sauti ya upole iliyojaa taharuki ndani yake. Muda huo ilikuwa yapata saa moja kasoro, ndio muda ambao kumbi ya starehe ulikuwa umenoga. Hivyo Dolin na David walikunywa na kula huku mioyoni mwao tayari wakiwa na nadhiri kuwa usiku wa siku hiyo watalala wote sababu David alitaka kuamini kama kweli maneno aliyoambiwa na mpenzi wake. Muda wa kuondoka ulipowadia wapenzi hao walikodi taxi ambapo iliwapeleka mpaka nyumbani anapoishi Dolin,mtu wa kwanza kutelemka alikuwa ni Dolin huku akionekana kulewa tila lila ilihali wa mwisho akiwa ni David naye vile vile likuwa amelewa kama ilivyo kwa Dolin.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Bei gani?.." Aliuliza David akimuuliza dereva taxi.

    "Elfu kumi na tano tu brother" Dereva huyo alimjibu David, muda huo Dolin aliposikia bei aliyotamka dereva taxi aligeuka kumtazama akishangazwa na bei aliyotajiwa mpenzi wake,ni bei kubwa ambayo haikulingana na umbali wa safari. Lakini Dolin wakati anataka kuongea neno kwa dereva huyo ajabu alimuona Ambrosy, Dolin alishtuka hata asiamini macho yake ilihali Ambrosy alimkonyeza kisha akaondosha gari kwa kasi kwani tayari alikuwa ameshapewa pesa yake, huku nyuma Dolin alibaki kuisindikiza kwa macho gari ile kitendo ambacho kilimfanya kuduwaa kwa muda mpaka pale David alipomgusa na kisha kuingia naye ndani. Wawili hao walipoingia ndani, bado Dolin alikuwa na taharuki ya aina yake, ghafla pombe ilimruka. Ndani ya nafsi yake alijiuliza "Hivi ni macho yangu ama ni ndoto?.." Ni swali ambalo alijiuliza Dolin, swali ambalo mwishowe aliishia kujifyonya. David alikuwa pembeni yake, hivyo alistushwa na kitendo hicho cha mpenzi wake kujisonya mara kwa mara. Ndipo kwa sauti ya kilevi alimuuliza "Mbona upo hivyo?.. Kuna nini?.." Dolin alimgeukia David akamtazama kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani bila kumjibu. Alipofika alijitupa chali kitandani ilihali ubongo wake bado ukitafakari kile alichokuona. Akiwa na wasi wasi alichukua simu yake akatafauta namba ya Walemi kisha akampigia. Simu ya Walemi iliita bila kupokelewa, ila bado Dolin hakukata tamaa alirudia kupiga mara mbili mfululizo na hatimae siku ilipokelewa. Hapo Dolin akasema "Walemi shoga yangu,tayari mambo yamekuwa magumu. Awali nilimuona akivuka barabara lakini safari hii kanibeba kwenye taxi kanileta nyumbani na shemeji yako"

    "Kwahiyo? Ni kusaidie nini Dolin!? Si nyie ndio mlio nishauri nimuue? Ajabu leo hii baada mambo kuharibika narudi kwenu kuwaomba msaada kila mmoja ananikimbia. Dolin naomba unisikilize kwa umakini! Mimi ndio Walemi na kwa hili hii kila mmoja ajue lake.." Maneno hayo yalisikika kwa njia ya simu, maneno ambayo Walemi aliyaongea kwa jazba sana. Dolin alijihisi kuchoka, alitupa simu kando akashusha pumzi ndefu kisha akajinyanyua pale kitandani akarejea sebuleni alipomuacha David. Alipofika Alistaajabu kumkuta mwendawazimu sebuleni huku akila makombo ya vyakula kwa pupa. Akiwa na woga Dolin alipasa sauti kumuita David "Davi.. David.. We Davi.. Uko wapi baby!?.." Aliita Dolin punde si punde yule mwandawazimu aligeuka David. "Ahahahahah hahahaha hahaha" Alicheka sana David halafu akanyanyuka kutoka kwenye sofa akazipiga hatua kusogea pale aliposimama Dolin. Dolin aliogopa sana alirudia nyuma akimuhofia David. Na mara baada kuona David anazidi kumkaribia aligeuka ili akimbilie chumbani, ni zoezi ambalo alifanikiwa ambapo aliweza kujifungia chumbani na kisha kuegemea mlango huku akihema haraka haraka. "Mungu nisaidie!.." Alijisemea hivyo Dolin huku macho yake yakitazama juuu, na pole pole aliushusha uso wake ambapo hapo alipata kumuona David amelala kitandani. David alicheka kidogo kisha akasema "UJUE wewe sio mzima hata kidogo. Dolin mpenzi wangu dishi limeyumba,amini hata kichaa anaafadhali. Yani haiwezekani unaingia ndani halafu unajifungia mlango kana kwamba unakimbizwa". Alisema David akimwambia Dolin. Muda huo Dolin yeye alionekana kupagawa zaidi,hali ambayo ilimpelekea kupoteza fahamu. Alipozinduka alijikuta yupo chini ya mti mkubwa aina ya msufi...ilikuwa yapata saa tano asubuhi. Mithili ya kichaa Dolin alikurupuka pale chini ya mti, huku akipiga mayowe alitimua mbio huku na kule hata asielewe namna gani alivyofika msufini. Hiyo hali iliweza kumpelekea kifo Dolin ni baada kuvuka barabara kwa pupa ambapo aligongwa na gari, habari yake ikawa imeishia hapo. Jumbe kadhaa wa kadhaa zilizagaa kuhusu kifo cha Dolin,hakika ilikuwa ni taarifa ambayo iliwastua wengi waliomfahamu binti huyo hasa kutokana na urembo malidhawa aliojaliwa achilia mbali makalio mkubwa yavutiayo machoni pa wanaume wapenda wezele. Kifo cha Dolin kilimstua sana Walemi, hofu ikazidi mara mbili moyoni mwake kwani alijua chanzo cha kifo hicho ni Ambrosy marehemu aliyerejea. "Dani mpenzi wangu.. Rafiki yangu Dolin kafariki.." Alisika akasema hivyo Walemi. Maneno hayo alikuwa akimwambia Daniel. Daniel alishtuka kisha akasema "Mmh! Dolin? Si jana tu umeongea nae?.."

    "Haswaaa! Lakini chanzo cha kifo hiki mimi nakijua..." Aliongeza kusema Walemi. Muda huo ilikuwa yapata saa tano usiku. Wapenzi hao waliokuwa wamelala.

    "Mmh kivip sasa mbona sikuekewi?.."

    "Utanielewa tu Dani. Unajua Dolin alikuwa ni moja ya marafiki walio nishauri nimuue Ambrosy ili nibaki na wewe. Na kabla ya kifo chake aliniambia kuwa Ambrosy anamtokea mara kwa mara.. Kwahiyo mpaka hapo dhahili dhahili Ambrosy ndio atakuwa amemuaa. Huyu mtu amekuja kulipa kisasi " Alisema Walemi. Daniel alikaa kimya huku akitafakari, aliona tayari kaingia katika vita isiyo muhusu maswali mengi alijiuliza ndani ya kichwa chake. Alijiuliza." Naam! Hapa sasa tayari balaa linakaribia. Leo kaondoka Dolin, kesho kutwa mara zake mmoja baada ya mwingine kisha mwisho inakuwa zamu yangu. Kwanini nisiende mbali na Walemi? Je, niendelee kuishi naye ili nikate tiketi ya umauti?.." Pumzi alishusha kwanza Daniel baada kujiuliza maswali hayo. Mwishowe akajisemea." Laah lazima nimkimbie huyu mtu, kila mmoja atabeba mzigo wake wa dhambi. Walemi.. Walemi.. Nakupenda sana lakini katika hili utanisamehe ". Dan ilipokwisha kujiseema hivyo alimtaka Walemi walale huku akisisitiza kuacha mara moja kumzungumizia Ambrosy marehemu aliyerejea duniani.

    Wakati Daniel akiwaza kumsaliti Walemi, usiku huo huo Penina alionekana akiwa ndani ya taxi akiwa na mpenzi wake aliyemfuata nchini KENYA. Wawili hao waliokuwa katika jiji la Nairobi wakitembea huku na kule. Penina liitembezwa huku na kule, lakini mwisho wawili hao waliingia kwenye kumbi moja ya starehe kuponda raha ilihali muda huo huo alionekana Dolin na David wakiingia katika kumbi hiyo,na kwa kuwa Penina na Dolin walifahamiana vema hivyo walipeana salamu ya juu juu kisha kila mmoja akaketi sehemu husika na mwenza wake.

    "Daah Dolin nae sio wa mchezo mpaka huku?.." Alisema Penina huku akichomoa simu yake maana muda mrefu alikuwa hajaishika. Jambo la kwanza aliingia mtandaoni, habari ambayo ilivuma ni juu ya kifo cha Dolin. "Dolin amefariki?.." Alishtuka Penina wakati huo huo akatazama kule walipokaa Dolin na David,ajabu hakuwaona. Aliporudisha uso wake kwenye kiti alichoketi mpenzi wake, alikutana uso kwa uso na Ambrosy..



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Penina alitaharuki kumuona Ambrosy, aliogopa sana kwani alifahamu fika Ambrosy ameshafariki miaka kadhaa nyuma iweje leo hii aonekane. Lakini wakati Penina akiwa na taharuki hiyo, Ambrosy alipotea akaonekana mpenzi wake. "Vipi mbona upo hivyo" Aliuliza bwana huyo ambaye ndio mpenzi wake Penina. Alimuuliza swali hilo baada kumuona Penina akiwa na hofu usoni mwake.

    "Hapana.. Hapana siwezi kuamini.." Alisema Penina huku akinyanyuka kwenye kiti. Mpenzi wake alimzuia asiondoke akihitaji kujua ni nini kinacho msibu ila bado Penina hakutaka kukaa sehemu hiyo. Ndipo kwa sauti ya juu akasema "Baby tuondoke, tuondoke bwana". Wawili hao waliondoka haraka haraka kwenye kumbi hiyo ya starehe. Walipofika hotiin Penina alijitupa kitandani huku akionekana kuwa na mawazo mengi kichwani mwake. Pumzi ndefu alishusha mara kwa mara, na punde akasema "Baby, unajua kituko nilichokiona bado kinaumiza ubongo wangu?.."

    "KIPI hicho mpenzi wangu?.."

    "Ni ngumu sana kuniamini ila ukweli ni kwamba marehemu aliyekuoa mume ww rafiki yangu nimemuona,na kingine kilicho nishangaza zaidi ni baada kumuona rafiki yangu aliyefariki siku ya jana.. Ukweli nimechanganyikiwa sana nahisi huyu mtu amekuja kulipa kisasi "

    "Aamh! Kwanini alipe kisasi? Na wewe unahusika vipi kwenye kisasi hicho?.." swali hilo lilimfanya Penina kumsimulia mpenzi wake mkasa wote ulivyokuwa mpaka kufikia hatua ya Walemi kumuua Ambrosy. Ulikuwa mkasa ambao ilimshangaza sana jamaa huyo, mpenzi wake Penina na mwisho wa yote alimtaka aende kwa mganga ili aweze kumsaidia. Ushauri huo Penina aliona wa maana sana, hivyo alihitaji kurejea Nchini Tanzania ili akamuone mganga ambaye aliamini anaweza kumsaidia.

    "Ni kweli la sivyo nitakufa siku si zangu! Haiwezekani kabisa dhambi ya mtu mwingine inighalimu na mimi" Alisema Penina kisha akajinyanyua kitandani akaelekea bafuni kuoga ndipo alale. Zoezi hilo alilifanya kwa dakika tano tu akawa ametoka bafuni, ajabu hakumkuta mpenzi wake. Alistaajabu sana hasa baada kuona mkoba wake umefunguliwa. Alipotazama hakukuta fedha alizokuwa nazo wala simu yake. Hapo ndipo toka ndani ya chumba akaelekea falanda lilokuwa kando ya chumba hicho ambapo baada kufikia alimuona mpenzi wake akiingia ndani ya gari na kisha kuishia zake. Penina alijiuliza maswali mengi juu ya uamuzi aliochukua mpenzi wake, lakini yote kwa yote alirejea chumbani kulala akingojea kesho papambazuke ili ajue atafanya nini ndani ya jiji la Nairobi nchini Kenya.

    Ilikuwa shughuli pevu Penina kupata usingizi hasa baada kufikiria ujio wa Ambrosy, hivyo alijipindua huku na kule kitandani ilihali akishusha pumzi mara kwa mara. Peni alienda mbali kabisa kushindwa kuelewa kwanini mpenzi wake kamkimbia pasipo kufahamu chanzo. Habari anakuja kuipata asubuhi kabisa ambapo aliambiwa kuwa jamaa huyo ni tapeli, na pia ni mwizi maarufu jiji humo.

    "Pole sana, hata hivyo mshukuru Mungu. Huyu mtu hafai hata kidogo. Ni tapeli na ni mwizi sio mchezi. Kwanza hana sehemu maalumu. Leo akionekana kiwanja hiki, kesho ataonekana kiwanja kile. Nani asiyemjua Dominic?.." Alisema mtu huyo. Kijana mfanya usafi katika hotel aliyolala Penina siku hiyo. Penina alishangazwa na maneno hayo. Ukweli hakuzania kama mpenzi wake amebadilika kiasi hicho.

    Alishusha pumzi ndefu na hata asijue aelekee wapi,hakuwa hata na senti...aliona Dominic amemuachia msala mkubwa sana ambao ni ngumu kuutatua katika jiji hilo ambalo hana mazoea nalo tofauti na Dar es salaam. Penina alijiuliza ataishi maisha gani katika jiji hilo hali ya kuwa hana pakuanzia, lakini kipindi anajiuliza maswali hayo upande wa pili alionekana Penina mwingine akiwa kwenye moja ya mitaa jijini humo. Penina huyo alipokuwa anatembea, punde kwenye moja ya uchochoro alikutana na mtoto mdogo mwenyewe umri yapata miaka mitano. Mtoto huyo alikuwa akiangua kilio. Penina baada kumuona mtoto huyo alichuchumaa kisha akamuuliza kipi kimemsibu, ila mtoto huyo aliendelea kulia na hata asiseme kinacho mliza. Lakini wakati Penina akiendelea kumdadisi, punde alionekana mzee wa makamo. Mzee huyo aliyeonekana kupendeza ndani ya kanzu alisema "We Binti! Hebu mbebe mtoto wako uondoke naye.."

    "Nakwambia mbebe kabla sijakujazia watu mshenzi wewe" Hayo maneno yalimuogopesha sana Penina, hivyo haraka sana alimbeba mtoto japo si wake. Na pindi alipokuwa naye, kelele zilisikika kutoka mtaa wa pili. Kelele hizo zilikuw zikisema "Mwiziiii.. Mwiziiii.. Jamani mwizi wa mtoto..". Mazingira yalikuwa ni uswahili. Zogo hiyo iliweza kupelekea kila kila mtu aliyesikia kelele hiyo kutoka kwenye nyumba yake akiwa na siraha kwa dhumuni la kumkabiri mwizi huyo. Muda huo Penina alipotea akimuachia mtoto aliyekuwa naye, punde si punde akaonekana Penina mwenyewe akikatiza sehemu hiyo alipo mtoto ikiwa muda huo huo japo la wananchi wenye hasira kali walifika na kisha kuanzakumpiga. Pindi Penina alipokuwa akicheza kipigo, Ambrosy alikuwa kando kwani shughuli yake ya kutafuta sababu ya kifo cha Penina ilikuwa imekamilika.

    "Hii ndio dawa yao! Haiwezekani kila siku watoto kupotea kinyemela. Tumechoshwa na matukio haya" Alisikika akisema mama mmoja mnene ambaye alionyesha kuchoshwa na matukio kadhaa wa kadhaa ya kupotea kwa watoto. Penina anakufa namna hiyo baada kupokea kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

    Siku zilisonga Ambrosy bado akiendelea kiwatokea Walemi na Daniel,na kisha kuwafanyia kila aina ya mauzauza. Mwishowe kabisa Daniel alijihisi kuchoka, hivyo aliona hamna budi kuyafanyia kazi mawazo yake ya kumkimbia Walemi. Rasmi Daniel anaamua kupiga mnada baadhi ya makampuni pasipo kumshirikisha Walemi. Aliuza magari na maduka miradi mbali mbali iliyokuwa ya marehemu Ambrosy. Baada kujihakikishia kuwa tayari pesa anayo ya kutosha, aliona heri aonyeshe ufahari kwanza wa kutumia pesa na ndipo aondoke moja kwa maoja na hata asitie maguu Nchini. Kwenye kumbi mbali mbali za starehe Daniel aliponda raha, alitumia pesa namna ajisikiavyo kwani alijua kabisa hiyo ni pesa ambayo hakuivujia jasho.

    "Raha jipe mwenyewe. Tumia pesa ikuzoee..Nyinyi ni masikini kunyweni kuleni mapaka mtosheke. Kibopa hapa tajiri kijana nipo nitaghalamia" Yalikuwa ni maneno ya Daniel. Maneno ambayo aliyaongea akiwa amelewa akiwaambiaa marafiki zake ambao alifahamiana nao punde baada kufanikiwa kupata fedha nyingi. Jamaa hao walipo yasikia maneno ya Daniel walifurahia sana, sifa kedekede walimmwagia huku wengine wakifanya jitihada za kumpepea.

    "Yani Daniel wewe, haki ya Mungu naapia. Kwa moyo wako huu usipoenda peponi basi kutakuwa na mkono wa mtu sio bure.." Alisema jamaa mmoja kati ya hao marafiki aliokuwa nao Daniel. Dani alicheka sana kisha akasema "Ulisemalo ni kweli. Tena ni kweli kabisa hebu agiza kinywaji mjinga wewe. Hakuna kuzubaa, Dani pochi imetuna, natumia pesa nitakavyo hakuna mbwa wa kunizuia.." Aliongea kwa kujiamini Daniel huku meza aliyoketi na marafiki zake ikionekana kuchafuliwa na chupa za bia zenye majina mbali mabli. Lakini wakati Daniel akifurahi na marafiki zake, ghafla alikuja kijana ambaye alikuwa akiishi nae maisha ya gheto uswahili kwa Tandale kwa mtogole. Kijana huyo alikatiza mahali hapo baada kumuona Daniel akiponda raha Bar Rumba. Kwa tabasamu bashasha kijana huyo akasema "Daah! Daniel kaka ni wewe?. Ama kweli milima haikutani ila bindamu hukutakana".

    "Kijana hebu kuwa na adabu acha kushobokea watu wakati unaona tunapunguza msongo wa mawazo. We masikini umenijuaje mimi?.." Alijibu Daniel kwa sauti ya juu kabisa kisasi kwamba watu wote waliokuwa ndani ya kumbi hiyo waligeuka kutazama upande huo. "Dani.. Inamana hunijui?.. Acha utani bwana. Mimi naitwa Madina kakaaa" Aliongezea kusema kijana huyo ambaye alifahamika kwa jina Madina. Lakini licha ya kijana huyo kutaja jina lake, Daniel bado hakutaka kuendelea kumsikiliza na hivyo aliwaaambia marafiki zake wamtoe nje kijana huyo. "Sijawahi kufahamiana na mtu masikini kama wewe?.." Alisisitiza Daniel akimwambia Madina wakati huo Madina akasema kwa sauti ya huzuni "Daniel? Ni wewe leo hii unanikataa? Umesahau wema wangu wote niliokufanyia?.. Dani umekuja Dar huna pakuishi unatangatanga nimekusaidia lakini leo hii umefanikiwa unanisahau?.". Alisikika akisema hivyo Madina muda huo akisukumwa kupelekwa nje. Hapo Daniel hakuongeza neno lolote alikaa kimya ingawa baada ya dakika kadhaa alivunja ukimya kisha akasema." Oya! Siku yangu tayari imeharibika. Huyu kiumbe kaniharibia siku yangu kabisa"

    "Ni kweli pole sana ila ndio changamoto, unajua watu kama hawa wakati wa shida hawajitokezi lakini wakati wa mafanikio hujitokeza" Alidakia kwa kusema hivyo moja ya marafiki zake Daniel.

    "Kwa sababu hii basi niacheni nikapumzike ila kesho tutawasilina tukutane kumbi nyingine tofauti na hii..". Daniel alipokwisha kusema hivyo alizipiga hatua kuifuata gari yake tayari kwa safari kurudi nyumbani. Baada kulifikia gari alifungua mlango lakini kabla hajaingia ndani ghafla alisikia mtu nyuma yake akimsabahi." Habari yako bro."

    " Nikusaidie nini?..". Alihoji Daniel pasipo kuitikia salamu hiyo. Mtu huyo alikaa kimya kidogo kisha muda mfupi baadaye alikivunja kimya hicho na kisha kusema "Jina langu naitwa Ditto maarufu kwa kazi ya kupiga picha hapa mjini. BILA Shaka wewe ndio Daniel mume wa Walemi.." Alisama mtu huyo, hakuwa mwingine bali ni yule yule kijana aliyekuwa akimsumbua Walemi miaka kadhaa nyuma. Daniel baada kuyasikia maneno akaongeza kuhoji." Ndio kwahiyo unataka nini? Au umesikia nataka kupiga picha na mke wangu au unataka Nikusaidie nini?.. ".

    "Lahasha brother! Kwanza mimi sihitaji msaada wako ila wewe ndio utahitaji nikusaidie kwa sababu nina siri nzito kuhusu Walemi, awali wa yote tangu uingie nae katika mahusiano ulishawahi kwenda kupima VVU?..". Alisema Ditto huku akiacha na swali. Swali ambalo lilimfanya Daniel kustuka na kisha kushushusa pumzi ndefu wakati huo huo akionyesha utulivu wa aina yake!



    Daniel alipowa mithili ya maji ya mtungini, swali la Ditto lilimfanya kuwa na bumbuwazi la muda mfupi ingawa baadaye hakuweza kujali aliingia ndani ya gari akaondoka zake huku nyuma akimuacha Ditto akiangua kicheko. Usiku huo Daniel hakwenda nyumbani kwake, alikatisha sehemu wanapojiuza wanawake akamchukua mmoja akaenda kulala naye kwenye moja ya hotel ya kifahari Jijini Dar es salaam. Sophie hotel ndipo Daniel alipoingia kufurahi na mwanamke huyo aliyemnunua kwa niaba ya kukukesha naye. Hayo sasa yakawa ndio maisha ya Daniel, alilewa namna awezavyo ilihali mwanamke huyo aliyemchukuwa mwanzo akifurahi naye kwa nyakati tofauti tofauti. Aliitwa Sesilia mwanamke malaya ambaye alionekana kuvutia machoni hasa kwa jinsi umbika sura mpaka kiuno. Hapo Daniel alijikuta akishindwa kujing'atua kwani mbali na maumbile hayo lakini pia Sesilia alikuwa fundi haswaa kitandani, mambo ya pwani yote aliyamudu vema vitendo ambavyo viliweza kumpelekea Daniel kuzama katika penzi la mwanadada huyo akamsahau Walemi. Hatua hiyo ilimshangaza sana Walemi, hapo sasa akaanza kuingiwa na hofu juu ya Daniel wake kwa sababu tayari ilikatika miezi miwili pasipo kuonana naye na hata akimpigia simu hapatikani.

    "Daniel? Hivi kweli wa kunifanyia haya?.." Alijuliza Walemi, muda huo akiwa sebuleni ameketi kwenye sofa akiwaza na kuwazua mambo chungu nzima yanayo kabili ubongo wake. Wakati huo Walemi akiwa katika hiyo hali, upande wa pili alionekana Daniel akiwa na Sesilia kwenye moja ya kumbi ya starehe. Wawili hao waliokuwa wakila na kunywa huku tabasamu bashasha zikitamalaki katika nyuso zao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mrembo Sesi.." Alisikika akisema Daniel.

    "Abe Mr Dani.." Sesilia aliitikia.

    "Nimekuleta sehemu hii ili niweze kuzungumza na wewe mambo mawili matatu..."

    "Mambo gani hayo Daniel?.." Alihoji Sesilia huku akionyesha utulivu wa aina yake. Daniel alishusha pumzi kwanza kisha kaongeza kusema "Maisha ni matamu sana kama unaishi kwa furaha na kuponda raha kama hivi. Lakini katika maisha ili furaha izidi zaidi na zaidi inatakiwa uwe na mwenza wako pembeni ili uweze kufurahia huu ulimwengu. Ammmh! Sesilia amini tangu sikuile mara ya kwanza nilipolala na wewe ghafla moyo wangu ukatokea kukupend sana na ndio maana imekuwa ngumu kukuacha. Kwahiyo basi nipenda uwe mpenzi wangu kabisa ikiwezekana siku moja tufunge ndoa.. ". Alisema hivyo Daniel kwa sauti ya chini huku akimuonea haibu Sesi. Yalikuwa ni maneno ambayo yalimstua kidogo Sesilia ambapo alikaa kimya kidogo kisha baadaye akakivunja kimya hicho kwa kusema." Sio vibaya Daniel ingawa naona kama bado haraka sana hivi! Lakini pia ningependa kujua huna mke wewe?.."

    "Ukweli nilikuwa naye ila tuliachana.." Alidanganya Daniel.

    "Sababu ipi iliyowafanya kubwagana?.."

    "Nilimfumania, kwa hiyo nikaona hakuna haja ya kuendelea kuishi naye. Kwa kipindi kirefu nimekaa peke yangu lakini sasa naona moyo wangu unataka mke. Na nimekuona wewe ndio unanifaa.."

    "Dani unajua mimi nimeshazoea kushika pesa, je utaweza kweli kuniendo?.."

    "Ahahha Hahaha" Daniel aliangua kicheko kwanza baada kusikia swali hilo la Sesilia. Alipokwisha kukatisha kicheko hicho akasema "Pesa hapa ipo, tena nyingi sana ya kutosha. Nipe nafasi tafadhali Sesi.."

    "Oky! Hakuna neno" Alikubali Sesilia. Jibu ambalo lilimfurahisha sana Daniel ambapo aliweza kumkumbatia huku wakipeana mabusu moto moto. Naam! Mahusiano ya Daniel na Sesilia yanaanzia hapo. Kwingeneko Walemi alionekana kuwa mpweke baada kupiga simu ya Daniel bila mafanikio ya kumpata. Hofu ilimjaa moyoni mwake kwani ni kitambo sana hajamuona wala hana taarifa yoyote juu yake. Alihisi labda kauwawa lakini hakutaka kutulia maanani suala hilo, alimaini kwamba Daniel atarejea sababu anampenda sana pasipo kujua kuwa Daniel yule aliyemdhania sio huyu wa sasa. Pesa imembadilisha mara mbili ya alivyokuwa mwanzo, kiburi dharau vyote vilimuandama.

    "Sesilia unajua kuwa siku hizi sikuelewi?.." Alisikika akisema hivyo Madina. Ni yule kijana aliyekanwa na Daniel ambapo awali alikuwa akiishi naye gheto uswahili mitaaa ya Tandale kwa mtogole. Siku hiyo Madina aliamua kumtolea uvivu mpenzi wake kwa kumuhoji swali hilo baada kuona Sesilia wa sasa sio yule wa zamaani.

    "Hunielewi?. Na bado utaendelea kutonielewa. Labda leo ni kwambie ukweli we mwanaume usiye na mbele wala nyuma ili hata siku nyingine unielewe. Nimeipata mwanaume mwingine mwenye pesa ya kunihudumia, kwahiyo naweza kusema mimi na wewe basi.." Aliongea Sesilia kwa jazba. Madina hakuamini maneno hayo, aliona kama utani lakini Sesilia hakuwa katika masihara na zaidi aliongeza kusema." Mwanaume niliyempata ni tajiri sana,uwepo wake yeye utanifanya niache kazi ya ukahaba.. ".

    " Ukahaba?.. "Alihoji Madina.

    " Ndio.. Hahahahah kwahiyo miaka yote ulikuwa hujui kazi iliyoniweka mjini? Pole sana Madina kweli leo ndio siku ya kujua mengi. Pesa zote nilizokuwa nakupatia, kazi ya kujiuza ndio ilikuwa ikiniingizia... Na pia ukae ukijua kuwa.... "Kabla Sesilia hajamaliza kuongea alichotaka kukisema punde Ilisikika honi ya gari. Ni Daniel alikuwa amekuja kumchukuwa, hivyo Sesilia alizipiga hatua kuifuata gari hiyo kisha akaingia ndani wakati huo huo Daniel aliachia tabasamu akampungia mkono Madina. Madina hakuyaamini macho yake, kwa mara nyingine tena anapata kuonana na Daniel. Achilia mbali siku ile aliyomkana kwenye kumbi ya starehe, sasa anashuhudia akimchukuwa mpenzi wake. Alilia sana Madina ilihali muda huo huo asiamini kama Sesilia alikuwa Dada poa.

    "Mungu wangu.. Nitakuwa nimepona kweli? Na kama Sesi atakuwa ameniambukiza nitafanyaje mimi wakati mama yangu ananitegemea mimi mtoto wake pekee?..".

    "Na kwanini Daniel kabadirika kiasi hiki? Inamana amesahau fadhila zangu zote? Loh! Ama kweli pesa humbadilisha mtu. Dani huyu huyu mchafu kuoga leo hii hanijui mimi?..". Yote hayo yalikuwa ni maswali aliyokuwa akijiuliza Madina. Lakini mwisho wa yote alishusha pumzi ndefu akarejea ndani kujilaza kitandani sababu siku hiyo aliona sio siku njema kwake.

    Upande wa pili Daniel na Sesilia walikuwa ndani ya gari wakipiga zogo mbali mbali. "Kuna jambo nataka nikwambie siku ya leo, na hapa tulipo tunaelekea moja kwa shopping ukanunue nguo na viatu utakavyo sababu kesho tunaelekea Zanzibar kuanza maisha mapya"

    "Waoow! Daniel unasema kweli?..". Alihoji Sesilia kwa tabasamu bashasha asiamini kile asemacho Daniel. Dan alicheka kidogo kisha akajibu "Nilisha kwambia hapa pesa ipo nyingi ya kutosha. Shaka ondoa". Ni jibu ambalo lilimfanya Sesi kufurahi. Maandalizi yalipokamilika ilibaki kungojea siku waliyopanga kuelekea Zanzibar iweze kuwadia. Hatimaye siku hiyo iliwadia ambapo wapenz hao waliondoka zoa kwenda kuanza maisha mapya huko. Lakini wakati Daniel na Sesilia wakiwa ndani ya ndani ya boti, upande mwingine alionekana Daniel akiingia nyumbani kwake. Walemi alipomuona alipandisha munkali akitaka Daniel amueleze wapi alipokuwa siku zote hizo. "Leo nataka uniambie ulikuwa wapi Daniel, sitaki univuruge akili yangu..."Alisema Walemi kwa hasira akimwambia Daniel. Daniel kwa sauti ya chini akajibu." Suala dogo sana hili Walemi hupaswi kubwabwaja. Tulia kwanza nikabadilishe nguo kisha nije tuzungumze vizur.. Sawa Sawa?.. ". Daniel alipokwisha kumjibu hivyo Walemi alizipiga hatua kuelekea chumbani ilihali muda huo huo simu ya Walemi iliita. Ilikuwa namba mpya imempigia, hima alipokea ikasikika sauti ikisema." Habari yako Walemi,,naitwa Martha Benedicto bila shaka waanifahamu. Ammmh Napenda kukupa habari kuwa Daniel tayari yupo ndani ya boti muda huu anaelekea Zanzibar kuanza maisha mapya na mwanamke mwingine ambaye sijamfahamu kwa jina..". Ilisema sauti hiyo. Martha alikuwa moja ya watumishi wa kampuni za marehemu Ambrosy kabla kampuni hizo hazijataifishwa zikiwa chini ya Daniel. Hivyo Martha alipokwisha kusema hayo alikata simu huku akimuacha Walemi akiwa na taharuki. " Daniel anaeleke Zanzibar? Na huyu aliyeingia chumbani ni nani?..."







    Alijiuliza Walemi baada kuambiwa kuwa Daniel kaonekana akielekea Zanzibar wakati muda huo alimuona akiingia chumbani. Alichachawa Walemi, kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku akiogopa. Taarifa hiyo ilimuogopesha sana alitamani kuelekea chumbani kumuona Daniel huyo lakini alihofia uhai wake na hapo akabaki sebuleni hofu dhufo lihali ikizidi kumjaa. Punde nje ya nyumba hiyo walionekana watu wakitembea kila pande wakikagua mazingira, Walemi aliwaona watu hao kupita dirishani jambo ambalo lilimfanya kutoka ndani hima kwenda kuwahoji watu hao wanatafuta nini kwenye mji wake. Alipofika nje, mmoja wa watu hao alisema "Bila shaka huyu ndiye mfanyakazi anayeishi ndani ya nyumba hii.."

    "Naam! Lakini nadhani mmelidhika na muonekano jinsi ilivyo, kwahiyo kilichobaki hapa ni kunadisha. Mtu atakaye toa pesa inayolidhisha basi mjengo atamiliki huu mjengo" Alidakia mtu wa pili, mtu ambaye kimuonekano alionekana mzee wa makamo huku mkono akiwa na makashablaka. Idadi ya watu walikuwa wasiopungua sita. Walemi aliishia kuwatazama watu hao wala asiseme neno lolote. Ndipo mtu mmoja kati ya hao sita aliongeza kusema "Ingekuwa vizur endapo kama tutaingia ndani kutazama maadhali jinsi yalivyo"

    "Ni kweli kabisa" Mtu mwingine aliunga mkono suala hilo. Hivyo walizipiga hatua kuelekea ndani lakini walipofika geteni Walemi aliwauliza "Nyinyi ni akina nani na mnataka nini kwenye nyumba yangu?..". Watu hao walimshangaa sana Walemi, kwa pamoja walitazamana kisha wakacheka huku mmoja akiongeza kusema "Alaah kumbe hawa watumishi wa ndani wanatabu?.. Mama a hii nyumba tayari ipo sokoni, mmliki anaiuza kwahiyo kinachotakiwa ni wewe kuanza kuchukua kilicho chako na uondoke. Unamasaa sita tu".

    "Unasemaje wewe?.." Walemi alishtuka akauliza hivyo kwa taharuki ya hali ya juu. Pumzi ndefu alishusha kisha akasema "Ni nani aliyewaambia kuwa hii nyumba inauzwa?..".

    "Hatubishani. Una hati miliki?.." Alihoji mmoja kati ya watu hao.

    "Ndio ipo, subirini hapo hapo nikawaletee sitaki minivuruge" Alijibu Walemi. Haraka sana aliingia ndani kutafuta hati miliki ya nyumba aliyonayo pasipo kuogopa kitu chochote, akili yake ni kama ilichachawa, katu hakuweza tena kuyakumbuka mauzauza yaliyotokea muda mchache uliopita. Alipofika chumbani alikagua kila sehemu kuitafuta hati miliki ya nyumba hiyo, alifungua droo, aliinua godoro alihaha kila kona chumbani humo ila hakufanikiwa kupita na cha ajabu zaidi yule Daniel aliyeingia chumbani muda mchache uliopita hakumkuta. Baada kuisaka pasipo mafanikio hatimaye alitoka nje akionekana kuchoka, kwa macho yake akapata kuiona hati miliki ikiwa kwenye mikono ya hao mabwana.

    "Ahahahah Hahaha.. Nadhani umepata jibu muafaka, ila usijali una muda wa kujipanga sababu masaa sita ni muda tosha sana kwako" Aliongea mmoja wao watu hao akimwambia Walemi. Muda huo Walemi hakuwa sawa tena kifikra. Tayari aliona maisha yake yale ya zamani yanarejea kwa kadi ya ajabu, alidodosha macho kwa uchungu, pumzi ndefu alishusha kisha akahoji kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake "Kwani mmilki alikuwa anaitwa nani jina lake halali?.."

    "Hilo hupaswi kujaji saana.. Lakini kwa kukusaidia tu. Bwana wa mali hii anaitw Daniel Misoji...". Alijibiwa Walemi.

    "Daniel? Yani Dani huyu huyu Dani wangu?.." Walemi alijiuliza maswali hayo mara mbili mfululizo ndani ya kichwa chake, maswali ambayo yaliambatana na mshtuko mkubwa uliompelekea kupoteza fahamu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alizinduka akiwa Hospitalini akipatiwa huduma,alishtuka kujikuta sehemu hiyo na hivyo alihitaji kujua amefikaje fikaje mahali hapo. Nesi aliyekuwa akimpatia huduma alimueleza kila kitu jinsi.

    "Umeletwa hapa na wasamalia wema, walikukuta katika mazingira tatanishi ukiwa umepoteza fahamu" Nesi aliyekuwa akimpatia huduma alimjibu. Walemi alilia kw uchungu akiwa katika kiti cha kulazia wagonjwa. Kumbuku ikamjia akakumbuka mara ya mwisho nyumba aliyokuwa akiishi ilikuwa ikipigwa mnada huku chanzo cha kuuzwa nyumba hiyo kikiwa ni Daniel baada kukopa pesa nyingine zaidi mbali na alizokuwa nazo huku dhamana akiweka nyumba. "Oooh Mungu wangu nitafanya nini mimi?.." Walemi alijiuliza mstakabali wa maisha yake. Dunia sasa anaiona chungu, hakuwa na pakulala, mlo aliupata kwa nadra sana. Walemi yule mwenye ngozi nyororo na mwenye uzuri wa kuvutia sio Walemi huyu wa sasa. Walemi huyu anaonekana kuwa zaidi ya mwenda wa zimu. Alichakaa mara mbili ya alivyokuwa hapo awali kabla hajaingia kwenye himaya ya tajiri Ambrosy. Kila alipokatiza watu walimtazama kwa macho ya mshangao huku kila mmoja akidiliki kuongea lake ilihali wengine wakithibutu kumzomea ikiwa kama kulipa kisasi kwa nyodo alizokuwa akionyesha kipindi alipokuwa na pesa.

    "Ooh Mungu wangu nisaidie" Alijisemea Walemi akiwa kando ya barabara jua kali la utosi huku njaa kali ikilindima tumboni mwake. Hakujua aende wapi, macho yake yaligota kwa omba omba waliokuwa wakipita gari kwa gari kuomba pesa. Alishusha pumzi ndefu Walemi, machozi yalimengalenga akayafuta kwa khanga yake kukuu aliyojifunga kiunoni. Baada ya hapo alivuka barabara kuelekea upande wa pili kisha akaendelea na safari yake isiyo na muelekeo maalumu. Wakati Walemi akiwa katika maisha hayo ya kutangatanga ndani ya jiji la Dar es salaam,upende wa Daniel maisha yalikuwa raha mstarehe ndani ya Zanzibar akifurahia na Sesilia. Wawili hao katu hawakuijua shida, na wala Daniel hakuweza kutafakari hali gani aliyomuacha nayo Walemi. Akasahau kabisa kuwa Walemi aliaua kwa ajili yake, na wale asiponda raha kama si yeye.

    "Laah! Nafurahi saana hali ya hewa ya Zanzibar, hikika ni nzuri sana" Alisikika akisema Daniel akimwambia mpenzi wake atwae Sesilia, muda huo walikuwa kwenye moja ya kumbi ya starehe wakila na kunywa. Hayo ndiyo yakawa maisha yao. Lakini baadaye hali ilikuwa tofauti kidogo baada pesa kupungua kwa kasi kwenye Account yake,jambo amablo lilimshtua Daniel. Aliogopa sana huku akitilia shaka mstakabali maisha yake. Hali hiyo ilimfanya kupowa kidogo, pole pole akapunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima. Hasa hasa kuhusu starehe. Ni hatua ambayo ilimshangaza Sesilia kwani tayari ilishazoea maisha ya starehe, hivyo jioni moja aliweza kukaa na Daniel kisha kusema naye jambo.

    "Daniel.."

    "Naam mke wangu"

    "Hivi unafahamu kuwa mimi ni mwanamke mzuri nahitaji matunzo?.. Lakini pia mbali na matunzo nahitaji kustarehe kwa jinsi nijisikiavyo. Sasa huu mfumo wako wa kisasa siulewi kabisa ama ndio unaishiwa? Nambie ukweli basi ili nijue ustarabu wangu..". Alisema Sesilia kwa sauti ya nyodo. Daniel alinyamanza kimya, hakusema neno lolote wakati huo akili yake ikishindwa kuamua cha kumwambia Sesilia. " Loh! Ni mwanamke mzuri sana, na moyo wangu tayari umemtunuku. Je, nikimueleza suala hili linalo endelea si ataona tayari Daniel naenda kuishiwa? Na kama sitomueleza si nitakuwa nazidi kujichimbia kaburi?..". Maswali yote hayo Daniel alikuwa akijiuliza ndani ya akili yake muda huo wawili hao wakiwa ndani saa ya jioni. Hivyo baada kukaa kimya kwa muda wa dakika kadhaa hatimaye alikivunja kimya hicho kwa kusema." Hapana. Hilo wazo ondoa kabisa mke wangu! Daniel bado nina pesa nyingi sana ila hapa kati kuna mpango niliufanya kwahiyo ukanighalimu pesa nyingi, jambo ambalo lilinipelekea kupunguza kidogo matumizi yasiyo ya lazima". Alisema hivyo Daniel akimwambia Sesilia.

    "Ni jambo gani hilo? Na kwanini ulifanye pasipo kunishirikisha?.." Aliuliza Walemi kwa sauti ya jazba.

    "Sesi kuwa pole utajua tu" Daniel alijibu

    "Sawa ila kaa ukijua wewe mwanaume huwezi kushindana na mimi mwanamke.." Aliongeza kusema Sesilia na punde si punde nje Ilisikika honi ya gari. Sesilia akionekana kupendeza alitoka ndani akaifuata gari hiyo huku nyuma Daniel akibaki kumuita Pasipo kuitikiwa. Daniel akaona haitoshi aliamfauata mpaka nje ambapo alipata kuona gari ya kifahari nje. Punde akatoka kijana mmoja mwenye asili ya kiarabu. Sesilia kwa mahaba mazito alimkumbatia na kisha kupeana mabusu moto moto. Hakika ni kitendo ambacho kilimuumiza mno Daniel, hakuweza kuyaamini macho yake. Kwa sauti ya juu akasema "Sesilia! Ni wewe wa kunifanyia haya?..". Sesi akaangua kicheko huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye kifua cha huyo mtu aliyemfuata kwa gari ya kifahari. Mara baada kukatisha kicheko chake akajibu "Ndio Dani.. Kwa sababu hujanifanyia yale yoote uliyoniahidi. Kwahiyo nakuona we mbabaishaji katika mapenzi. Hivyo niache nijue hamsini zangu na wewe jua hamsini zako.." Sesilia alipokwisha kujibu hivyo aliingia ndani ya gari. Jamaa huyo aliachia tabasamu kisha naye akaingia ndani ya gari akaondoka na Sesilia huku nyuma Daniel akibaki mikono kichwani ilihali akilia kama mtoto shauri ya maumivu anayo yapata ndani ya moyo wake juu ya mtu ampendae kwa dhati.

    Siku zilisonga Sesilia akikacha kurudi kwa Daniel,kila Daniel alipompigia simu hakupokea na mara nyingine alikata kabisa. Hali hiyo kamwe haikumfanya Dani kukata tamaa, aliendelea kumpigia mara kwa mara na kumtumia jumbe kadhaa za kumuhitaji. Ilikuwa kama bahati siku moja. Siku hiyo Daniel alipiga simu Sesilia akapokea. Furaha isiyokifani ilitamalaki moyoni mwa Daniel, kwani nafasi hiyo aliamua kuitumia kwa kumuuliza kiasi cha pesa anacho hitaji Sesilia ili warudiane na maisha yaendelee.

    "Million mia moja hamsini Daniel, nambie kama pesa hiyo ipo nirejee kwako..". Alisema Sesilia mwanamke aliyejikita kipesa zaidi kwa kijana Daniel. Daniel aliposikia kiasi hicho alicheka kwa dharau kisha akajibu "Ni dhambi kubwa sana kuutesa moyo wangu kisa pesa hiyo ya chapati. Naomba njoo utakuta pesa yako".

    "Sawa dakika tano nyingi, unabahati sana sababu nilikuwa namalizia jitihada za mwisho ili nielekee Paris.." Alijibu Sesilia kisha kakata simu. Muda aliotaja ndio alioufanyia kazi. Sesilia alifika akamkuta Daniel akizipanga pesa kitandani huku akizihesabu kwa tabasamu bashasha." Waoooow! Saaafi sana Daniel. Unajli sana hisia za moyo wako "Alisema Sesilia akimwambia Daniel.

    " Ahahaha hahaha "Daniel alicheka kwanza halafu akasema." Sesilia.. Sesilia.. Mimi ndio Daniel bwana achana na hao shombe shombe wa kiarabu wataishia kukuchezea na kisha kukuacha. Haya pesa hizi hapa unalo la kuongea?.. "

    " Hapa Daniel sina.. Kweli wewe ni kidume cha shoka" Alijibu Daniel. Lakini wakati wawili hao wakiwa ni watu wenye furaha, mara ghafla chumbani uliingia upepo wa mkali. Upepo huo ukiambatana na popo wengi wa ajabu ulipeperusha fedha zote. Daniel na Sesilia walijitahidi kuzizuia lakini hawakuweza kufua dafu, mpaka upepo huo unatoweka chumbani humo,mkono mwao kila mmoja alisalia na shilingi Elfu kumi moja...



    Daniel na Sesilia walistaajabu kujikuta wakiwa na shilingi Elfu kumi kila mmoja. million maia moja thelathini ilitoweka..

    "Siayaamini macho yangu kama leo Daniel narudi maisha ya kimaskini!.." Alisema hivyo Daniel kwa sauti ya kilio huku macho yake yakiitazama shilingi Elfu kumi aliyonayo ambayo haitoshi hata nauli ya kumrudisha Tanzania bara.

    "Daniel? Unataka kuniambia hii ndio pesa iliyokuwa umebaki nayo?.." Aliuliza Sesilia. Daniel hakujibu alinyamanza kimya huku akionekana kuduwaa. Maisha ni safari ndefu,yenye milima na mabonde. Kijana Daniel anajikuta akiingia kwenye maisha ya kawaida kwa siku moja tu baada pesa zake kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Hivyo hakuwa na pakuegea ndani ya Forodhani, nyumba aliyokuwa amepanga alifukuzwa na kujikuta sasa akijikita katika kazi ya kubeba mizigo (Kuli) ili apate pesa ya matumizi lakini pia pesa ya nauli itakayo mrudisha Tanzania bara. Watu waliomfahamu Daniel walistaajabu sana kumkuta katika hali hiyo, baadhi yao walimuonea huruma na vile vile kuna waliomcheka.

    "Yakheee.. Huyu si ndio yule mbala aliyekauwa akitamba kila kumbi ya starehe?.."

    "Kabisa Yakhe kumbe na wewe umemfahamu? Haki huyu mbala hana akili, aliendekeza starehe weee sasa matokeo yake ndio haya". Waliokuwa vijana wawili ambao nao pia ni makuli eneo hilo la Forodhani, vijana hao waliomfahamu fika Daniel kutokana na starehe mbali mbali alizokuwa akizifanya tangu aingia kisimani humo.

    Upande wa pili Sesilia anakujikuta uzuri wake unapokutika kila kukicha, kwani baada maisha kwenda mlama kwa Daniel aliamua kuvunja uhusiano naye kila mmoja akapambana kivyake. Sesilia akaona uzuri wake ni mtaji tosha, lakini akajikuta anatumika na kila mwanaume huku akiishia kuzurumiwa ambapo mwishowe aliamua kuachana na kazi hiyo ya ukahaba, na hivyo aliomba kazi kwenye moja ya mgahawa huku mshahara pekee aliopewa ni chakula. Lakini Sesilia hakutaka kukata tamaa ya maisha, aliendelea kufanya kazi kwa juhudi. Juhudi hiyo mwishowe ikawa faida kwake baada mwanamke aliyemuajili kumlipa mshahara. Nafasi hiyo Sesilia aliitumia vema, alijiwekea vijisenti mpaka pale alipofanikiwa kupata nauli ya kumrudisha Tanzania bara. Hakika hakuyaamini macho yake, yote yaliyotokea aliona kama ndoto. Machozi yalimtoka pindi alipojitazama mara mbili mbili. Pumzi alishusha na kisha kujiuliza "Hivi ndio mimi Sesilia kweli?..Ni shetani gani aliyenipitia. Nitaificha wapi sura yangu mimi" maswali yote hayo Sesilia alikuwa akijiuliza kichwani baada kufika Dar es salaam akitokea Zanzibar,alijihisi kukosa nguvu, kichwa kikawa na wingi wa usongo wa mawazo ulimpelekea kutembea barabani kiholela mithili ya kichaa, kitendo ambacho mwisho kikamsababishia umauti baada kugongwa na gari nyakati ya jioni. Siku iliyofuata, Daniel naye alifanikiwa kurejea Dar es salaam. Aliinua uso wake akitazama majengo marefu ambayo alitesa kwa starehe kisha baadaye akashusha uso wake na hata asiamini kama kweli maisha yamemuendea mlama.

    "Naam! Nimeamini Dania ni tambala bovu, Daniel nimeumbuka. Nitauficha wapi uso wangu kwa watu niliokuwa nawadharau? Na nitamueleza nini Walemi mwanamke aliyenipenda mpaka akathubutu kuua kwa sababu ya upendo wake kwangu?.." Alijisemea Daniel ndani ya moyo wake huku akiendelea kuzipiga hatua barabani ilihali akionekana kituko kwa watu waliomfahamu ambao Daniel baada kutajirika alikuwa akiwapandishia vioo. Lakini wakati Dani akitembea akiwa hana hili wala lile kwenye moja ya mitaa Masaki, ghafla gari Hilax ilimpita kisha ikasimama mbele yake. Daniel kichwa chini mkono nyuma aliendelea kutembea mpaka akalifikia gari hilo ambapo alitoka Madina katika gari hilo akiwa na taharuki juu ya Daniel "Daniel ni wewe my bro?.." Alisema Madina.

    "Ndio mimi Madina, hatimaye Mungu kanipiga kofi na haya ndio maisha niliyonayo kwa sasa. Hapa unaponiona sina hata senti. Nipo kama tiara sina muelekeo Madina" Alijibu Daniel kwa sauti ya chini huku akiona haibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Daah! Pole sana Daniel lakini haya ndio maisha. Si wewe tu ambaye umechezea maisha bali wapo wengi mno mtaani ambao waliokuwa matajiri kama wewe ila mwishowe pesa zikapotea. Cha kuzingatia ni kumuheshimu kila mmoja kwa sababu huwezi jua kesho yake ama wewe mwenyewe huwezi kujua kesho yako. Mr Daniel nadhani kwa kipindi kirefu sana niliishi na wewe kwenye gheto moja Tandale kwa mtogole ingawa mwenzangu baada kuzifuma ulikataa na ukadiliki kunichukulia mpenzi wangu. Mimi niliona ni hali ya kawaida katika maisha ya mwanadamu. Jambo ambalo hukulijua, wakati tunafanya kazi ya kuuza mazaga barabani mimi chini chini nilikuwa nafuatilia ajira. Hatimaye nafanya kazi kwenye moja ya kampuni hapa nchini. Inalipa vizur sana kwahiyo kwa sasa maisha yangu yapo Safi kabisa " Aliongea Madina kwa kirefu zaidi akimwambia Daniel. Daniel alijiinamia na wala asiseme neno lolote. Hapo Madina akaongeza kusema" Ehe yukowapi na Sesilia?.. ". Hilo ni swali ambalo lilimfanya Daniel kaungua kilio, hasa akikumbuka unyama alioufanya kwa Walemi. Daniel alilia sana huku Madina akimtia moyo. Aliponyamanza akamueleza hali harisi iliyotokea baina yake na Sesilia baada pesa kupotea kimazingara.

    " Daah pole sana Daniel.." Alisema Madina kisha akaingiza mkono mfukoni akatoa kiasi cha pesa shilingi Elfu tano akampa Dani halafu akaingia ndani ya gari akaondoka zake huku akimwambia "Itakusaidia kwa matumizi mbali mbali Dani".

    **********

    Kwingeneko alionekana Walemi akizulala bila muelekeo maalumu. Hayo ndio yalikuwa maisha yake. Punde wazo lilimjia kuwa aliwahi kuishi na mwanamke aliyeitwa Siwema, hivyo alielekea mahali anapoishi lakini akaaambiwa kuwa Siwema alihama nchini baada maisha kumnyookea.

    "Alihamia wapi! ?.." Aliuliza Walemi kwa mshangao wa hali ya juu. "Mara ya mwisho alituambia anahamia Uingereza" Alijibiwa Walemi na mmoja ya waliokuwa majirani zake Siwema. Hakika Alistaajabu sana. Hivyo ilibidi asafe kinyonge wala asijue mstakabali wa maisha yake. Akiwa na sintofahamu hiyo kwa mara nyingine tena anakutana na Ditto baada kupotezana kwa kipindi kirefu "Habari yako Walemi?..". Ditto alimsabahi Walemi. Walemi alishtuka aliposika sauti hiyo, haraka sana akageuka kisha akasema kwa sauti ya jazba "Unataka nini we mshenzi mbona unanufuatilia sana?.."

    "Ahahahah" Ditto alicheka kwanza kisha akasema "Mimi sio mshenzi, ila wewe ndio mshenzi. Walemi hupaswi kuilaumu nafsi yako bali huu ndio wakati wa kuweza kuudhuru kaburi la yule uliyedhurumu nafsi yake kisha mrudie Mungu wako.. Umefanya dhambi nyingi sana.. Na jambo usilo lijua hapo ulipo tayari ni muasirika wa Ukimwi. Unamkumbuka yule mzee uliyemuua nyumba ya wageni? Usitake kuniambia kwamba hukufanya naye tendo... "Alisema Ditto maneno hayo ambayo yalimchanganya Walemi. Kwa jazba akamuuliza Ditto" Wewe umejuaje yote haya.. "

    " Walemi mimi ni msaka tonge, amini Ambrosy hajakufahamu ukiwa katika kazi ya umama ntilie. Ambrosy alikujua kitambo sana akakupenda ila alihitaji japo kukufahaamu kwa ufupi akanipa kazi ya kukufuatilia kila hatua, namba yako ya simu alinipa yeye picha ambazo ulipigwa pasipo kujua pindi ulipokuwa ukimsaliti nilipiga mimi.. Kwahiyo sijakufuatilia kwa nia mbaya japo muonekano wako hauendani na matendo yako... Kwaheri Walemi umepoteza bahati, na siku zote bahati haiji mara mbili. Ditto nimeshamaliza kazi niliyopewa na Ambrosy. Sihitaji kiasi chochote cha pesa kutoka kwako japo nina ushahidi wa kutosha kuwa wewe ni muuaji wa.. Nitakuwa sijakutendea haki wakati uliyemuua naye alikuachia gonjwa lisilo na tiba. Mzee yule alikuwa kiwembe. Pole sana " Ditto alimjibu Walemi kwa kirefu zaidi. Jibu ambalo lilimshangaza Walemi, na hapo ndipo alipkumbuka maneno ya mwisho kutoka kwa yule mzee aliyemuua gest." Umeniua sawa lakini najua Walemi wa sasa sio wa miaka ijayo.. Hahaha Hahaha pole sanaaaa" Pumzi ndefu alishusha Walemi, machozi yalimtoka wakati baada kuyakumbuka maneno hayo ya mzee yule aliyemuua gest kwa kosa la kumlaghai kingono kwa kumuahidi atamtafutia kazi mwishowe baada kumaliza haja yake akamgeuka, kitendo ambacho kilimpelekea Walemi kuchukua uamuzi huo wa kumuua pasipo kujua kuwa tayari naye kaachiwa ugonjwa wa Ukimwi.

    Kwa hakika Walemi alijiona mkosefu sana kwa Ambrosy huku akijutia kumuua mwanaume aliyempenda kwa mapenzi yote. Akajikuta akijutia kumpenda kwa dhati mwanaume ambaye mwishowe alimkimbia. Si mwingine bali ni Daniel. Kwenye kaburi la Ambrosy Walemi alifika, huku akilia kwa uchungu aliomba msamaha juu ya kaburi hilo. Punde ilisika sauti ikisema "Walemi,ondoka kwa amani. Ambrosy hana kinyongo na wewe ila alirudishwa ilk apoteze mali ambazo zilipelekea yeye kuondolewa kwenye uso wa Dunia. Kumbuka Ambrosy ni mwanaume ambaye alikupenda kwa dhati kutoka ndani moyo wake, hata mara moja mpaka anaondoka Dunia hajaona hata umbile lako la ndani.. Hiyo alidhihilisha kuwa kufanya mapenzi sio maana kwamba ni ishara ya upendo. Ambrosy hakuwa muhuni, alipenda maendeleo yako na alikuheshimu pia.. "Ilisikika ikisema hivyo sauti hiyo ambayo iliweza kumshtua Walemi pale juu ya kaburi la Ambrosy.

    " Hebu simama.. "Sauti hiyo iliongeza kusema. Walemi alisimama, ghafla kufumba na kufumbua alijikuta yupo katika mavazi yake yale yale aliyotoka nayo kijijini kwao Dodoma. Maajabu hayo Walemi yalimpagawisha huku akijitazama kila upande wa mwili wake ihali muda huo huo amri ikatoka ikimtaka aondoke mahali hapo. Haraka sana Walemi alitimua mbio. Sasa wazo la kuendelea kuishi jijini ilitoweka, jiji la Dar es salaam aliliona chungu kabisa. Alifanya kila liwezekanalo akapata nauli ya kumrudisha kijijini kwao mkaoni Dodoma. Kila mwanakijiji alimshangaa Walemi kwani hakuwa na mabadilko, si mavazi wala muonekano. Walemi yule aliyetoroka akikwepa kuolewa na mwanaume ambaye hakumpenda, ndio huyo huyo aliyerejea kutoka Dar es salaam alikokwenda kumtafuta Dani wake,zaidi aliomgezeka umri na kurefuka.

    "Kipi ulichoambulia sasa Walemi?.." mama Walemi alimuuliza binti yake aliyerejea nyumbani tangu apotee miaka kadhaa nyumbani kwao. Walemi hakujibu ingawa alijua kitu alichorudi nacho kutoka Dar es salaam, hivyo aliishia kulia tu huku akiomba msamaha, alijiona ni mwana mpotevu.

    " Yuko wapi Daniel wako uliyemfuata?.." Aliongeza kuhoji mama Walemi wakati huo akidondosha machozi. Mwishowe wazazi walimsamehe ingawaje baada ya siku kuzidi kwenda afya yake ilimabidirika sababu tayari ilikuwa na virus vya Ukimwi. Hali hiyo iliwashtua wanakijiji achilia mbali wazazi wake, na hapo ilimpelekea kutengwa na baadhi ya marafiki zake ambao waliamini kuwa wanaepuka kuambukizwa. Hali hiyo ilimfanya Walemi kudhoofika zaidi na zaidi mpaka pale umauti ulipomkumba. Wakati huo huo mjini baada Daniel kupoteza utajiri wa hali ya juu, alichanganyikiwa kisaikolojia hasa hasa pindi alipojingundua kuwa ni muasirika. Alikata tamaa kabisa ya maisha,dunia akiona mbaya. Akaona hakuna haja ya kuendelea kuishi, hivyo aliamua kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kunywa sumu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    USIACHE AMBACHAO KWA MSALA UPITAO..



    ****MWISHO***

0 comments:

Post a Comment

Blog