Search This Blog

JINI MAUTI - 5

 







    Simulizi : Jini Mauti
    Sehemu Ya Tano ()




    Michael hakutaka kuniuliza maswali zaidi, alichokifanya ni kuondoka kuelekea katika uwanja wa kucheza na kuanza kucheza. Muda mwingi macho yake yalikuwa kwangu, alionekana kama mtu ambaye muda wote alitamani niwe namwangalia jinsi alivyocheza.



    Ilipofika saa 12:30 jioni, tayari giza lilianza kuingia. Nilimwambia Michael kwamba nilitakiwa kuondoka lakini hakutaka kukubaliana nami, aliniambia kwamba tuendelee kukaa kwani kama kuondoka tungeondoka tu.



    Sikuwa na sababu ya kukataa, tuliendelea mpaka ilipofika saa moja usiku. Tayari giza lilikuwa limeingia ndipo aliponiambia kwamba alichoka kucheza, hivyo alitaka twende kutembea.

    “Wapi?”



    “Kule kwenye mawemawe.”

    “Ila si unaona giza!”

    “Kwani unaogopa giza? Wewe twende tu, mlinzi wako nipo hapa,” aliniambia.

    Nilijua nini kingetokea, nilijaribu kumwambia Michael kwamba sikutaka kwenda kule lakini akaning’ang’aniza sana, sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye.



    Alionekana kubanwa, kuna kitu alitaka kukifanya, alitaka kufanya mapenzi na mimi kitu ambacho hakikuwa kikikubalika moyoni mwangu. Tulitembea ufukweni mpaka sehemu iliyokuwa na kilima fulani ambapo kulikuwa na miamba kadhaa.



    Hakukuwa na mtu yeyote aliyetuona, tulichokifanya ni kusogea mbele ni sauti za mawimbi tu ndizo zilizokuwa zikisikika mahali hapo. Tukaelekea sehemu ya chini iliyokuwa na mwamba uliokuwa na uwazi mkubwa, akaniambia tukae hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Kuna nini?” nilimuuliza huku nikiwa na hofu.

    “Davina…”

    “Abeee.”

    Akanisogelea zaidi, akausogeza uso wake karibu yangu, nikaanza kuzisikia pumzi zake nzito, akabaki akiniangalia tu kwa macho yaliyojaa matamanio. Hakuzungumza kitu, alichokifanya ni kuipandisha juu sketi yangu.



    “Unataka kufanya nini?”

    “Subiri kwanza.”

    “Hapana Michael, siwezi kufanya hivyo,” nilisema huku nikijitahidi kumzuia.



    “Unaogopa nini? Kuna nani anatuona? Mbona unakuwa hivyo? Davina, sisi ni wapenzi na si marafiki, wewe si dada yangu na mimi si kaka yako, tatizo lipo wapi?” aliuliza Michael.

    “Michael! Sitaki ufe!”

    “Nife? Nife kivipi?”



    “Ukifanya mapenzi na mimi, utakufa.”

    “Hahah! Sasa ajabu ipo wapi hapo? Kama kufa kila mtu atakufa,” aliniambia huku mikono yake ikifungua vifungo vya blauzi yangu.



    Kwa kweli niliogopa, kichwa changu kilikumbuka matukio yaliyotokea, niliwakumbuka wanaume watatu waliokufa mara baada ya kufanya nao mapenzi hivyo nilijua hata kwa Michael ingetokea hivyo.

    Nilimuonya kwamba hakutakiwa kufanya mapenzi na mimi kwa sababu angekufa lakini hakutaka kusikia hata kidogo, tena ndiyo kwanza aliniambia kama kufa kila mtu atakufa.



    Sikupenda kuona Michael akifa, nilijitahidi kumzuia lakini ilishindikana kabisa, mwisho wa siku nakuja kushtuka, blauzi haikuwa mwilini mwangu na hata sketi ilitupwa chini na hivyo kuanza kufanya mapenzi nami huku akiwa amenilaza chini.



    Sikusikia raha yoyote zaidi ya kulia kwa uchungu kwani niliamini ilikuwa ni lazima Michael afariki dunia palepale. Hivyo ndivyo ilivyotokea, nikahisi joto likianza kupanda mwilini mwake, alianza kutetemeka na mara nikamuona akianza kukakamaa.



    Hakuchukua muda mrefu katika hali hiyo, mara nikayaona macho yake yakianza kubadilika rangi, yakaanza kuwa mekundu huku meno yake yakianza kugonganagongana, ndiyo alikuwa ameanza kuwa katika hali ya mwanzo ya kukata pumzi.



    Niliogopa, nilitetemeka, nikamshika vilivyo Michael huku nikimuita, asiniache peke yangu, asife pale tulipokuwa. Aliendelea kuwa kwenye hali ileile, alikuwa chini, mapovu yakaanza kumtoka na mwili kuanza kubadilika rangi.



    Niliogopa sana, sikutaka kubaki mahali hapo, nilichokifanya ni kuvaa haraka na kukimbia. Sikurudi kule walipokuwa wanafunzi, nilikimbia na kurudi nyumbani huku nikionekana kuchanganyikiwa.

    *****

    Kama kawaida yetu wachawi tulijazana katika uwanja wa kukutania, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kusherehekea, siku ya kula nyama na kunywa damu tu. Kama kiongozi wa wachawi mahali hapo, kila mtu aliniheshimu, niliogopeka na kila mchawi niliyekuwa nikizungumza naye, alinioneshea heshima kubwa.



    Nyama za binadamu zilikuwa mezani, hazikuwa zimepikwa, zilikuwa mbichi ambazo nyingine zilikuwa na damu.

    Nililetewa bakuli kubwa lililojaa nyama nyingi, nilipoletewa, nikaliweka juu ya meza na kuanza kuchukua kipande kimoja baada ya kingine.





    Hapa naomba niwaambie kitu, unapokuwa katika uwanja wa wachawi na kuletewa nyama za watu, usifikiri kwamba utaiona chungu au kugundua mara moja kwamba nyama unayokula si ya mnyama, kwako itakuwa tamu kama unakula nyama ya ng’ombe.

    Nilikula sana nyama huku wachawi wengine wakinifuata na kunipongeza, kazi niliyoifanya ya kumpeleka Michael pale uwanjani ilikuwa kubwa na ilinijengea heshima zaidi. Michael na watu wengine niliowaua walikuwa ndani ya banda moja kubwa ambalo ndilo tulilohifadhia misukule mingine.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila wakati nilikwenda kule na kuwaangalia, hawakuwa wakinifahamu, waliniona lakini kwao nilionekana mgeni kabisa. Wanaume niliowapenda sana walikuwa ndani ya chumba kimoja, nilipowaangalia nilijisikia vibaya ila sikuwa na jinsi, ilitakiwa iwe kama ilivyokuwa.



    Siku hiyo tulitakiwa kuondoka mapema uwanjani hapo kwa kuwa kesho yake tulikuwa na mkutano mkubwa wa kitaifa hivyo tulihitajika kujiandaa.

    Asubuhi ilipofika, nilikwenda shuleni. Kwa mbali nilianza kusikia vilio, sikutaka kujiuliza kwamba nini kiliendelea, nilijua fika kwamba taarifa za msiba wa Michael zilisambazwa shuleni hapo.

    Moyo wangu uliumia mno, nikajikuta nikibubujikwa na machozi mashavuni mwangu, niliumia kwa kile kilichotokea. Wanafunzi walibembelezana tu, nikajifanya sijui kilichotokea, nilichofanya ni kuwasogelea baadhi ya wanafunzi na kuwauliza.



    “Michael amekufa, alikutana na jini jana usiku kule Coco Beach,” aliniambia mwanafunzi mmoja, uso wake ulikuwa na majonzi tele.

    “Michael amekufa?” nilijifanya kuuliza kwa mshtuko.

    “Ndiyo! Jini amemuua,” aliniambia mwanafunzi mwingine.

    Hawakujua nilijisikiaje, niliumia moyoni mwangu lakini sikuwa na jinsi. Siku hiyo shuleni hapo hata walimu hawakufundisha, walibaki ofisini mwao tu. Mchana ulipofika ndipo tetesi zikaanza kusambaa kwamba jinsi Michael alivyokufa, kifo cha aina ileile ndicho alichokufa Hemedi wiki chache zilizopita.

    “Kwa hiyo jini aliyemuua dereva bodaboda ndiye aliyemuua Michael?” alihoji mwanafunzi mmoja.

    Wanafunzi tukajiandaa na kuelekea msibani. Hatukuwa wanafunzi wengi ila tulichaguliwa baadhi. Wakati tukiwa njiani ndipo nilipogundua kitu. Sifael, mvulana aliyenipenda sana ambaye mara kwa mara alikuwa akiniangalia, alionekana kubadilika.



    Aliniangalia kwa macho yaliyojaa hofu, alionekana kama mtu aliyeniogopa mno. Sikujua kitu gani kiliendelea, nikajifanya kutokujali, niliendelea na safari. Tulipofika msibani, tukawapa pole wafiwa na baada ya dakika chache, Sifael akaniita, japokuwa aliniogopa, siku hiyo alionekana tofauti.

    “Unajua ukweli,” aliniambia.

    “Ukweli upi?”

    “Juu ya kifo cha Michael.”

    “Hapana! Sijui chochote.”

    “Davina, utakuwa unajua tu ukweli. Kama hukumuona huyo jini, basi wewe ndiye jini mwenyewe,” aliniambia Sifael.

    “Mimi jini?”

    “Ndiyo! Jana usiku nilikuona unaondoka na Michael kuelekea kule kwenye miamba, tena kulikuwa na giza,” aliniambia Sifael, nikashtuka japokuwa sikutaka kumuonesha mshtuko wangu.

    “Mimi?”

    “Ndiyo!”

    “Hapana! Utakuwa umenifananisha.”

    “Yaani mimi nikufananishe wewe?”

    “Inawezekana!”

    “Haiwezekani! Ni wewe. Davina, umemuua Michael,” aliniambia huku akionekana kuanza kuogopa.

    “Nimemuua Michael?”

    “Ndiyo.”

    Sifael hakutaka kuzungumza sana, kila aliponiangalia, alizidi kuwa na hofu.





    Nahisi aliona akiwa amesimama na mtu asiyekuwa wa kawaida hata kidogo, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo huku akionekana kuchanganyikiwa.

    Alikwenda katika kundi la wanafunzi na kutulia katikati, alionekana kuogopa sana, kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Niliingiwa na wasiwasi kwa kuona kwamba kama nisingefanya jambo fulani basi Sifael angeweza kuwaambia watu wengine kwamba jana aliniona nikiondoka na Michael kwenda kule kwenye miamba.

    Nilichokifanya ni kuondoka kuelekea chooni, huku, nilisimama na kisha kuanza kuzungumza maneno ya kichawi, hapohapo nikapotea na kutoka chooni. Hakukuwa na mtu aliyeniona, nilikuwa nikitembea kuelekea kule kulipokuwa na kundi la wanafunzi ambapo Sifael alikuwa mmojawao.

    Nilipofika, nikamnyooshea kidole, hapohapo akadondoka chini. Hakukuwa na mtu aliyeniona, walimuona Sifael akidondoka peke yake tu. Pale chini alipokuwa, akaanza kukakamaa mwili, wanafunzi wakakimbia, wazee wakakusanyika kumwangalia, hawakujua nini kiliendelea, mapovu yakaanza kumtoka.

    Nilifanya hivi kwa kuwa sikutaka Sifael atoe siri ya kile kilichotokea jana. Hapo nikarudi chooni ambapo nilijitoa kwenye hali ya kichawi na kuwa kawaida. Nikatoka chooni na kuelekea kule watu walipomzunguka Sifael.



    *****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuanzia siku hiyo sikutaka kujihusisha na wanaume, niliogopa kwa kuwa nilijua kwamba endapo ningefanya mapenzi na mwanaume yeyote yule ilikuwa ni lazima afe kama ilivyotokea kwa wengine.

    Katika kipindi chote hicho mama hakuwa amejua kwamba nilikuwa mchawi, sikuonyesha dalili zozote zile, nilikuwa mkimya na mpole. Wanaume wengine walikuwa wakinifuata nyumbani, wengi walinitongoza lakini msimamo wangu ulikuwa uleule kwamba sikuhitaji mwanaume yeyote yule.

    Nilisoma mpaka kidato cha nne na matokeo yalipotoka, nilifanya vizuri na hivyo kwenda kujiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamini iliyokuwa jijini Dar .

    Hapo shuleni nikamuona mvulana mmoja, mvulana mwenye sura nzuri ambaye kwa kumwangalia, kuna kitu nilichohisi kwamba hakuwa sawa, Nitakueleza kwa nini hapo baadaye.

    Mvulana huyu aliitwa John. Alikuwa kidato cha tano, hakuwa muongeaji sana, maisha yake yalitawaliwa na upole



    mkubwa, hakuwa mzungumzaji sana.

    Endelea…



    Kwa kumwangalia John, nilitokea kumpenda, sikujua ningemwambia nini ili apate kunielewa.

    Hakukuwa na mtu aliyewahi kuzungumza na John kwa zaidi ya dakika tano, alipenda kukaa peke yake lakini kitu kingine kilichowashangaza watu, huyu John alikuwa na akili sana darasani.



    Kwa kumwangalia, alikuwa na mwili wa kawaida lakini kama kulikuwa na kazi ya kufanya, iwe ya kubeba vitu au kazi nyingine, John alifanya kwa nguvu zote, kitu cha kubeba watu wawili, tena kwa shida, yeye alikibeba peke yake.

    Kama John akiwa mbele yako, kisha wewe ukiwa nyuma na kumuita, alivyokuwa akigeuka, hakuweza kugeuka shingo tu kukuangalia, alikuwa akigeuka mwili mzima kama roboti.



    Maisha yake yalimshangaza watu wengi, wengine wakahisi kwamba alikuwa na tatizo, kumbe mbali na hilo, kulikuwa na kitu kingine kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake ambacho watu hawakuwa wakikifahamu, hata mimi pia sikukifahamu katika kipindi hicho, ila baadaye nilijua kila kitu.

    “John,” nilimuita, alikuwa mbele yangu akitoka darasani, kama kawaida yake, akageuka mwili mzima.

    “Niambie Davina.”

    “Unakwenda wapi?”

    “Nyumbani.”

    “Hivi unaishi wapi?”

    “Sinza Mori.”

    “Nashukuru kukufahamu.”

    Nilichokihitaji ni mazoea na John, hakukuwa na kitu kingine zaidi ya hicho. Nilimpenda, kiukweli niliwahi kupenda lakini kwa John nilipenda mpaka nikawa sili, sinywi wala sioni.

    Nilijua kwamba kila nilipofanya mapenzi na mwanaume, ilikuwa ni lazima afe lakini kwa John, nikashindwa kujizuia kabisa, mapenzi yake yaliukimbiza moyo wangu vilivyo.

    Kila nilipofika shule ilikuwa ni lazima nionane na John, nizungumze naye hata kwa dakika chache ndipo niendelee na ratiba yangu.



    Kulazimisha ukaribu namna ile, mwisho wa siku nikajikuta nikiwa karibu sana na John ambaye hakuwa mzungumzaji sana.

    Ukaribu ule ukasababisha mimi na yeye kuanza kutambulishana nyumbani. Kwangu, niliendelea kuwa na furaha mno, baada ya siku kadhaa ndipo nilipoona kwamba kulikuwa na jambo moja tulitakiwa kufanya, jambo hilo ni mapenzi.

    “Kufanya mapenzi?” aliniuliza.

    “Ndiyo!”

    “Hapana! Haiwezekani, kwani sisi wapenzi?”

    “John! Yaani hisia zote hizi, mambo yote tunayofanya bado unataka nikutongoze? Tena mimi msichana nikutongoze!” niliuliza na kumuonesha hisia kali za kimapenzi kupitia macho yangu.

    “Hukuniambia.”

    “Sawa. Basi ndiyo nakwambia kwamba ninakupenda,” nilimwambia.

    “Nashukuru.”

    “John! Kwa nini unanifanyia hivi?”

    “Kukufanyia nini?”

    “Kuniumiza! Kwani ukiniambia kwamba unanipenda pia, utaumia?”

    “Hapana! Okey! Nakupenda pia.”

    “Sasa inakuwaje?”

    “Kuhusu nini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuionesha dunia kwamba sisi ni wapenzi.”

    “Usiwe na hofu! Tuvutevute muda kwanza,” aliniambia na kuleta stori nyingine kabisa.

    Nilimpenda sana na kila nilipomwambia tufanye mapenzi, alinizungusha tu. Kuna siku alisema kwamba tutafanya kesho, ilipofika, aligeuka na kusema siku nyingine. Nilikuwa simuelewi, wakati mwingine nilidhani alishtukia kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.



    Kutokana na kuwa wapenzi, shule nzima wakalifahamu hilo, wakajua kwamba ninatoka kimapenzi na John. Kila siku ilikuwa ni lazima tuonane shuleni, nilipokuwa nikiumwa, ilikuwa ni lazima aje nyumbani kuniangalia.

    Wanaume wengi walikasirika kwa kuwa walinitamani sana, walitamani kuwa na msichana aliyekuwa na umbo zuri kama langu. Hawakupata nafasi, kile walichokuwa wakikitaka hawakukipata, mwisho wa siku wakajikuta nikiangukia kwenye mikono ya John.



    Kwa wasichana walinichukia sana, walimpenda John, kila mmoja alitaka kuwa naye kutokana na upole wake, uzuri wake na hata akili zake. Wengi walijigongesha kwake lakini mwisho wa siku mvulana huyo akaamua kuwa na mimi.

    Kwa hiyo shuleni tukazungukwa na maadui na miongoni mwa wasichana waliokuwa wakinichukia alikuwepo mmoja aliyeitwa Asha. Alikuwa msichana mrembo ambaye pale shuleni walimpa jina la Beyonce, alipenda kupendwa, kitendo cha kuwaona wanaume wengi wakimpapatikia kilimpa raha.



    Alitembea na wavulana kadhaa, hakuchuja, mwisho wa siku kabisa akataka kutembea na John.

    Alianza kumtafuta kijana huyo, alijitahidi kuweka mitego ya kila aina lakini John hakuingia mkenge, alikasirika mno, baada ya siku kadhaa, akashtukia John akiwa nami.

    Hilo ndilo lililomuumiza mno, hakuamini, akaniwekea kinyongo lakini sikutaka kujali. Alitangaza vita lakini hakujua alikuwa akitangaza vita na mtu wa aina gani. Aliwaambia marafiki zake kwamba alinichukia na ilikuwa ama zake ama zangu, ilikuwa ni lazima kunikomesha.



    Kwa kuwa John alikuwa wangu, sikutaka kujali sana, nikamsikiliza na kukubaliana naye kwamba tulitakiwa kusubiri.

    Kila siku nilishikwa na mhemko, mwili ulinisisimka kila siku, nilishindwa kabisa kuvumilia, nikajiona kwamba ule uvumilivu niliokuwa nao ulikuwa ukienda mwishoni kabisa.

    Baada ya kukaa kwa kipindi cha miezi miwili ndipo aliponiambia kwamba kile nilichokuwa nikikitaka basi kilitakiwa kufanyika. Nilifurahi moyoni, sikuamini kama kweli hatimaye John alikubaliana nami.

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Mbona hauamini mpenzi?” aliniuliza.

    “Basi tu. Tufanyie wapi?”

    “Wewe unataka wapi?”

    “Popote tu.”

    “Basi nitakushtua, twende Bagamoyo, kuna hoteli nzuri tu. Ila kuna kitu,” aliniambia.

    “Kitu gani?” nilimuuliza, akashusha pumzi.

    “Nadhani huo ndiyo utakuwa mwisho wa mimi na wewe kuonana,” aliniambia maneno yaliyonishtua.

    “Kivipi?”

    “Kwani haujaelewa?”

    “Yaani ndiyo utakuwa mwisho wa mimi na wewe kuwa pamoja?”



    “Nimesema mwisho wa mimi na wewe kuonana, yaani baada ya hapo, hautoniona tena,” aliniambia huku akiniangalia machoni.

    Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nikagundua kwamba mboni za macho ya John hazikuwa zikicheza.

    “John…” nilimuita.

    “Unasemaje?”

    “Wewe ni nani?”

    “Kivipi tena?”

    “Sikueleweelewi mpenzi,” nilimwambia.

    “Hahaha! Eti mimi ni nani! Binadamu kama wewe.”

    “Hapana! Unaonekana wa ajabu sana.”

    “Najua. Ila mimi siyo jini, naomba usiogope,” aliniambia.

    “Mmmh!”

    “Tatizo nini? Mbona unakuwa na hofu.”

    “Hakuna kitu.”

    Hata nilipoagana naye nilikuwa na maswali mengi kichwani mwangu, nilibaki nikijiuliza kuhusu John lakini sikupata jibu. Usiku wa siku hiyo nilipokutana na wachawi wenzangu nikawaambia kwamba kulikuwa na sehemu tuliyotakiwa kwenda, ila tusingeweza kwenda wote, ilikuwa ni lazima tujigawe, yaani twende wachache, kama watatu hivi.



    Nilitaka kujua ukweli juu ya John, alikuwa nani? Jini au binadamu. Baada ya kumaliza kikao tukaondoka na nyungo zetu mpaka alipokuwa akiishi John. Kama ilivyokuwa, tukapitia katika pembe ya nyumba na kuingia ndani.



    John alikuwa amelala kitandani, nikamsogelea mahali pale na kumwangalia, nilikuwa nikimchunguza, wachawi wenzangu waliokuwa mle ndani wakaanza kuniangalia kwa mshangao.

    Hawakuelewa sababu ya mimi kufanya vile, yaani kumchunguza sana John kama mtu niliyekuwa nikitafuta kitu fulani. John alikuwa binadamu wa kawaida, si jini kama nilivyohisi, sasa kwa nini mboni za macho yake hazikuwa zikicheza? Kila nilipojiuliza, nilikosa jibu, nilipomaliza tukaondoka zetu.



    Bado maneno yake kwamba siku hiyo ingekuwa mwisho wa yeye kuonana nami yalinitia hofu, sikujua alimaanisha nini na kwa nini aliniambia maneno hayo tena katika kipindi kigumu kama hicho, nilibaki na mawazo hayo mpaka siku ambayo tulianza safari ya kwenda Bagamoyo.



    Njiani, nikaanza kujiwa na mawazo juu ya mauti ambayo ingeweza kumkuta John baada ya kufanyanaye mapenzi, moyo wangu uliogopa lakini sikuwa na jinsi, nilitakiwa kukubaliana na hali iliyokuwepo kwamba iwe isiwe ni lazima nifanye mapenzi na John.



    Tukaenda kwenye loji moja, ilikuwa ni ya gharama kidogo, John alilipia na kuingia ndani. Kila nilipokuwa nikimwangalia moyo wangu ulidunda sana, nilimpenda na nilifikiria kwamba huo ndiyo ungekuwa muda wangu wa mwisho kuonana na John kwani baada ya kufanya mapenzi, angefariki dunia.



    Upole wa John ulikuwa mpaka chumbani, mimi ndiye niliyemsogelea na kuanza kumvua nguo zake, nilijitahidi kupitisha mikono yangu huku na kule, nikimshika hapa na pale ilimradi mwisho wa siku tufanye kile kilichotupeleka ndani ya chumba kile.



    Nilimfanyia hivyo kwa dakika kumi, ikawa zamu yake ambapo akaanza kufanya vilevile. Ilichukua muda wa dakika thelathini, akaja kifuani kwangu na kuanza kufanya mchezo ule.



    Nilishikwa na hofu, nikajua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa John, kilichonishangaza ni kwamba hakufa, aliendelea kushughulika nami kwa muda wa dakika arobaini na tano, alipomaliza, akasogea pembeni na kupumzika.

    “Vipi?” nilimuuliza huku nikishangaa.

    “Poa.”

    “Upo salama?”

    “Ndiyo! Kwani vipi?”

    Kwa kweli nilishtuka mno, sikuamini kilichokuwa kimetokea, ilikuwaje John awe salama na wakati alitakiwa kufa kama ilivyokuwa kwa wanaume wengine, kila nilipojiuliza, nikakosa jibu. Hapo nikaanza kupata jibu kwamba inawezekana sikuwa na uwezo wa kuua tena, yaani mwanaume yeyote ambaye angefanya mapenzi nami, asingekufa kama ilivyokuwa zamani. Nikamshukuru Mungu katika hilo pasipo kujua kwamba huyu John alikuwa nani.

    “Davina…” aliniita.

    “Abeee…”

    “Ni muda wa kuondoka.”

    “Yeah! Ngoja nijiandae tuondoke.”

    “Simaanishi kwenda Dar.”

    “Kumbe kwenda wapi?”

    “Si nilikwambia kwamba hatutoonana baada ya hapa?”

    “Ndiyo!”

    “Basi huu ndiyo muda.”

    Aliniambia, akainuka kitandani, akaanza kuvaa nguo zake haraka, alipomaliza, akaanza kuufuata mlango. Akaushika na kuufungua na mimi nikamfuata, alipotoka nje na kuubamiza mlango, sekunde mbili tu nami nikaufungua, kilichonishtua, sikuweza kumuona John. Nikaogopa.

    *****

    Nilichanganyikiwa mno, sikujua ni kitu gani kilichotokea mpaka John kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Nilichokifanya ni kutoka nje, nikaanza kumtafuta John lakini sikuweza kumuona, kila nilipoangalia, palikuwa peupe.

    Sikutaka kukaa Bagamoyo, siku hiyohiyo nikarudi nyumbani huku nikiwa na mawazo sana juu yake. Nilipofika nikajifungia chumbani na kuanza kufikiria juu ya kile kilichokuwa kimetokea Bagamoyo.



    Bado nilijiuliza juu ya John, alikuwa nani. Jambo lililotokea lilinishangaza, kila nilichokuwa nikijiuliza nilikosa jibu kwani kichwa changu kilichanganyikiwa mno. Kwa sababu nilikuwa nimechoka sana, usiku wa siku hiyo sikwenda kuroga kama zilivyokuwa siku nyingine.



    Asubuhi ilipofika nikaamka na kwenda shule. Nilipofika huko, sikutaka kuliweka wazi suala la John, nilibaki kimya kabisa. Macho yangu hayakutulia, nilidhani kwamba John angeweza kuibuka shuleni lakini sikufanikiwa kumuona.



    Mpaka tunaingia darasani, nilipoangalia kiti chake, hakuwepo jambo lililowafanya wengi kuuliza alikuwa wapi lakini hakukuwa na aliyekuwa na majibu. John hakuwahi kutega shule, kila siku alifika shuleni, hakuwahi kuwa mgonjwa, kila siku alionekana kuwa mzima wa afya, sasa siku hiyo alikuwa wapi? Kila aliyejiuliza, alikosa jibu.



    Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, wengine walikuja kuniuliza, majibu yangu yalikuwa mawili tu, sikumuona kwa kipindi chote na sikujua alikuwa wapi.





    Sikuwa na furaha hata kidogo, kichwa changu kilikuwa na mawazo tele juu ya John, nilichanganyikiwa mno, sikujua alikuwa wapi na kama kupotea alipotelea wapi. Kitendo kile alichokifanya, kile cha kupotea kilionesha dhahiri kwamba inawezekana alikuwa mchawi, lakini ilikuwaje siku ile tulipokwenda kwake hakukuwa na dalili zozote za kuonesha kwamba alikuwa mchawi? Je, kama hakuwa mchawi wala jini, alikuwa nani? Kila nilichojiuliza, sikupata jibu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi wa kwanza ukapita, John hakuonekana, mwezi wa pili nao ukaingia, hakuonekana na mpaka tunamaliza kidato cha tano na kuingia cha sita, bado John hakuonekana. Katika kipindi chote hicho nilikuwa na mawazo tele, kutokuwepo kwa John kulinisikitisha mno, sikuamini kama hakuwa nami tena.



    Baada ya kufunga shule kwa likizo ndefu, sikutaka kukaa Dar es Salaam, nikamwambia mama kwamba ninataka kwenda kumtembelea bibi mkoani Tanga, hakuwa na kipingamizi, akaniruhusu hivyo kwenda huko.

    “Ila utapafahamu?” aliniuliza.



    “Hakuna tatizo, nitafika tu, si umesema Lushoto? Wala usijali, nitafika tu,” nilimwambia mama.



    Sikuwahi kufika kijijini kabla, sikuwahi kumuona bibi yangu katika hali ya kawaida zaidi ya ile hali ya kichawi ambayo kila siku ilitufanya kuonana. Niliondoka nyumbani siku iliyofuata na kuanza safari ya kuelekea Lushoto.

    Ndani ya basi nilikuwa na uhakika wa kufika huko, nilikuwa na nguvu ya kichawi ambayo ilikuwa na kazi ya kuniongoza kila sehemu na ndiyo maana lisingekuwa jambo rahisi kupotea huko.



    Ndani ya basi nililokuwemo nilikaa kitini na mvulana mmoja, kiukweli alikuwa mweupe mno, alikuwa na mchanganyiko wa rangi iliyoonesha mmoja wa wazazi wake alikuwa Mwarabu.



    Kijana yule alikuwa mchangamfu mno, kila wakati aliyatawala mazungumzo, sikuwa muongeaji sana lakini kutokana na uchangamfu wake, naye akanifanya niwe muongeaji mkubwa.

    “Lushoto kwa nani?”

    “Bibi yangu!”

    “Waoo! Kumbe tupo safari moja.”

    “Na wewe unakwenda Lushoto?”

    “Ndiyo!”

    “Ni kwa nani?”

    “Babu yangu!”

    “Sawa! Nashukuru kuwa nawe safari moja.”

    “Usijali! Inawezekana tukawa ndugu bila kujua,” aliniambia na wote kuanza kucheka.

    “Inawezekana.”

    “Yeah! Hivi unaitwa nani?”

    “Davina. Na wewe?”

    “Naitwa Karim.”

    Safari ikaendelea huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale. Tulipofika Mombo, tukateremka kisha kuchukua mabasi madogo yaliyokuwa yakienda Lushoto. Tukaanza safari nyingine tukiwa pamoja, cha kushangaza, mpaka nilipokuwa nikiteremka, naye alikuwa akiteremka hapohapo.



    “Eeh! Kumbe bado tupo pamoja!”

    “Ndiyo maana nilikwambia isije kuwa babu yako ndiye babu yangu!” aliniambia Karim huku akitabasamu.

    Alipokuwa akielekea Karim ilikuwa jirani na alipokuwa akiishi bibi. Nyumba ya bibi ilikuwa hapa na nyumba ya babu yake ni kama ya tatu kutoka tulipokuwa tukiishi. Bibi alifurahi kuniona, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kunipongeza kwa kazi kubwa niliyokuwa nikiifanya ambayo wachawi wengine waliona kuwa juu sana.



    Kwa kawaida inapofika usiku, hasa kwa sehemu kama Lushoto ambapo kunakuwa na baridi kali, huwa watu wanatoka nje usiku na kuwasha kuni kisha kuanza kuota moto. Siku hiyo na mimi nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa nje kwa ajili ya kuota moto.



    Tulikusanyika watu wote kutoka katika nyumba ya bibi, tulikuwa kama kumi na moja kisha kuwasha moto. Bibi alikuwa na kazi kubwa ya kutuhadithia mambo ya zamani huku wakati mwingine akituhusia kumcha Mungu kana kwamba yeye alifanya alichotuambia.



    Wakati tukiendelea kuota moto, kwa mbali nikamuona Karim akiwa amesimama, sikutaka kukaa hapo, nilichokifanya ni kusimama na kuanza kumfuata. Aliponiona, aliachia tabasamu pana. Akanivuta pembeni.

    “Vipi?” nilimuuliza.

    “Poa! Nataka twende sehemu tukazungumze kidogo.”

    “Wapi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapo mbele.”

    “Usiku wote huu!”

    “Kwani unaogopa nini? Upo na mimi komandoo,” aliniambia Karim huku akionekana kujiamini.

    Sikuhofia kitu chochote, aliponiambia kwamba twende pembeni kidogo, nikakubaliana naye. Tukaelekea huko, kulikuwa na giza totoro.



    Nilijua kile ambacho kingekwenda kutokea, nilijua fika kwamba Karim alitaka kufanya mapenzi na mimi, sikutaka kukataa, mimi mwenyewe nilishampenda hivyo kusingekuwa na tatizo lolote.

    Sura yake nzuri, uchotara wake ulinichanganya mno, sikuona kama kungekuwa na sababu ya kumkatalia mwanaume kama Karim, tena alikuwa amekuja yeye mwenyewe.





    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog