Search This Blog

MKUFU WA MALKIA WA GOSHEN - 4

 






Simulizi : Mkufu Wa Malkia Wa Gosheni

Sehemu Ya Nne (4)





.

"Utakuwa na mimi kwa siku tatu hapa. Kaa, tule, tuongee, tupange."

.

.

.

Rhoda akageuza uso wake na kumtazama Venin. Kwa kugeuka huko akawa amempoka Venin nywele zake.

.

.

.

"Nashukuru sana, Venin," akasema kwa uso mkakamavu. Akajitoa karibu na mwanaume huyo na kuelekea kwa Bonas.

.

.

.

"Natumai siku zangu tatu hapa, zitakuwa za kheri na za kazi."

.

.

.

Venin akatabasamu kipembeni. Akapandisha mabega yake juu akibinua mdomo.

.

.

.

"Nitahakikisha hilo, Rhoda."

.

.

.

Baada ya muda mfupi karamu ikawa imeandaliwa kwa ajili ya wageni. Wanawake wazuri wasiojulikana wametokea wapi, wakaandaa chakula kitamu na kinono.

.

.

.

Vinywaji vikajazwa mezani na hata ala za muziki zikapamba.

.

.

.

Venin akamkarimu Rhoda, pamoja na wote aliokuja nao waje wale wafurahi. Rhoda na walinzi wake wakajumuika kula na kunywa.

.

.

.

"Mam, hii si kawaida," Bonas akamnong'oneza Rhoda. "Venin hajawahi kukaa na vijakazi meza moja. Sijawahi kuona mara zote nilizowahi tia miguu hapa."

.

.

.

Rhoda akazipokea taarifa hizo kwa tabasamu. Ila halikudumu sana usoni baada ya Bonas kumwambia:

"Kuna jambo atakuwa amelipanga, kuna jambo anataka kulifanya."





Taarifa hiyo ikampa tafakuri Rhoda.

Akamtazama Venin aliyekaa upande wake wa pili, Venin akatabasamu na kumuonyeshea kikombe cha mvinyo.

.

.

.

"Kuna taabu, Rhoda?" Akauliza.

.

.

.

Rhoda akatikisa kichwa pasipo kusema jambo.

.

.

.

Macho ya Venin yakamtazama Rhoda anavyokula na hata anavyomeza. Yalikuwa yanawaka tamaa na hamu. Alijikuta anapenda kumtazama mwanamke huyo kila nyendo aliyokuwa anafanya.

.

.

.

Ilikuwa ni ombwe sasa, nini ataenda kulifanya muda wa usoni.

.

.

.

Jambo hili likamfikirisha pia Rhoda, na kwa kiasi fulani likamnyima raha. Ila alikuwa mtaka cha uvunguni, ilibidi ajiandae kuupinda mgongo.

.

.

.

. ***

***

.

.

.

.

.

.

Jua lasimama na kumkuta Sultana mdogo akiwa yu macho na mwenye nguvu. Alikuwa amevalia sketi ndefu rangi ya zambarau iliyokaba kiuno chake na kukomea chini ya magoti.

.

.

.

Kifuache kilifunikwa na blauzi nyeusi nyepesi iliyokaba shingo na kuacha huko kwingine. Mikono yake, kama kawaida, haikukosa bangili zilizometameta na kuvutia. .

.

.

Kichwa chake alikifunga kiremba cheusi kilichokatizwa na kamba kamba kadhaa mithili ya mikufu yenye vidani vya kung'aa.

.

.

.

Hapo alikuwa amevaa kawaida. Yaani siku yake ilikuwa ya kazi, la sivyo angejikwatua ipasavyo. Lakini mbali na yote bado akapendeza mwanamwali huyu. .

.

.

Hakuwa na haja ya kujieleza kwamba yeye ni mke wa Sultan. Macho yako yangetosha kukupatia majibu, tena ya haja. Ni kama vile nguo ziliumbiwa mwili wake.

.

.

.

Hata akijezeka magunia, la haula anapendeza!

.

.

.

Asubuhi nzima hii alikuwa anaambatana na vijakazi wake kufanya usafi wa nyumba. Kila kona ya dari akaigusa na fyagio na sakafu ikang'azwa zaidi.





Japokuwa ni hulka yake kutenda hivi kila mwisho wa juma, yaani kufanya usafi wa jumla, ila wa siku hii ulikuwa kabambe.

.

.

.

Aliusindikiza yeye mwenyewe, alielekeza na kupendekeza baadhi ya mabadiliko. Nyumba ikang'aa na kunawiri. Mwishowe akaifukiza marashi kwa kumalizia.

.

.

.

Akajipata bafuni, akasuguliwa mwili na kijakaziwe. Kisha akajikwatua yeye mwenyewe, hapa hakumwamini kijakazi zaidi tu ya kioo na mkono wake.

.

.

.

Akajifukiza marashi na kuketi sebuleni akijipatia sharubati ya matufaha matamu toka Uajemi.

.

.

.

Mwili wake ulituama vema ndani ya gauni maridadi la kahawia, jembamba na refu, likiacha mgongo wake mwekundu wazi. Huku nywele zake ndefu, nyeusi ti, zikiwaka mafuta na kusongwasongwa vizuri ndani ya banio jeusi la ishara ya mapenzi.

.

.

.

Loh! Mwanamke alinoga. Harufu yake ilitamba sebule nzima. Kama ni bustani, basi hili halikuwa jingine bali uwaridi. .

.

.

Alikuwa mbichi zaidi. Kama vile msichana wa miaka kumi na misaba. Ama yule ambaye hata ungo haujui sembuse kuuvunja.

.

.

.

Hapa kama mume huaja kwa msongo wa kazi, akifika hapa lazima akunjue sura. Na hilo ndilo lilikuwa lengo la mwanamama huyu.

.

.

.

Alijua fika Sultan atakuja nyumbani kwake, hakujua muda, ila alijua lazima atakuja. Na mwanaume huyu atakapokuja, hatakuwa na furaha.

.

.

.

Ana mawazo juu ya mkewe mkubwa. Ana mawazo juu ya mkufu. Haya matatizo, kwa namna ya lazima, yatamfanya aghafirike.

.

.

.

Na hapa ndiyo mkono wa mwanamke utaonekana. Mkono wa Bi mdogo. Kumpokea, kumbembeleza na kumtuliza mume.





Kwa Sultana huyu, haya matatizo yalikuwa mtaji na fursa kwake. Alitaka kucheza nayo aushinde moyo wa Sultan ambayo nusura aupoteze kwa blanda ya dawa ya bibiye aliyoipoteza njiani.

.

.

.

Sasa anataka ajitahidi acheze karata kuu. Karata ya kutengeneza kasri ya Sultan katika mji wake.

.

.

.

Alifungua pazia la dirisha akatazama nje, bado muda ulikuwa mchanga. Akaagiza glasi nyingine ya sharubati hii aipendayo na kuendelea kujipatia mafundo ya kusogezea muda.

.

.

.

Akanywa nusu ya glasi, na mara kijakazi wake akaja upesi kumkuta.

.

.

.

"Sultana, pasipo shaka Sultan anakuja. Msafara wake unaoneka kwa mbali unakuja."

.

.

.

Sultana akatabasamu. Akapandisha kichwa chake kumpa ishara kijakazi wake aliyetimka kwenda nje.

.

.

.

"Karibu Sultan kwenye mikono yangu," akajikuta anasema kabla hajamalizia sharubati yake na kwenda nje ya geti kumlaki mgeni.

.

.

.

Alimjaza Sultan kifuani mwake, akamteka mkono mpaka sebuleni alipomkalisha na kuketi pembeni yake.

.

.

.

Mkono wake wa kuume ulichezea ndevu za Sultan, mguu wake wa kulia akiuweka juu ya paja la mwanaume huyo.

.

.

.

Macho alilegeza na sauti yake ilikuwa kavu lakini nyororo. kichwa chake akilikilaza kifuani mwa Sultan akisikiliza mapigo ya moyo.

.

.

.

"Ungependa nikuandalie nini, Sultan wangu?" Sultana akauliza.

"Nashukuru sana, sina hamu ya kula kitu," akajibu Sultan akitikisa kichwa.

"Hapana, Sultan. Huwezi kuja kwa mpenzi wako, tena ambaye hujamuona muda mrefu, ukakataa kula," akasema Sultana kwa sauti shinikizi.





"Si kwamba nakataa, bali sina hamu."

"Sultan, angalau sunna. Sitajisikia vema hakika. Najua haujala hata jana."

"Umejuaje?"

"Mie si mgeni kwako. Natambua yote hayo nikikutazama usoni, laaziz."

.

.

.

Sultan akavuta na kushusha pumzi ndefu. Kweli hakuwa amekula. Ila pia mwili wake haukuwa na hitaji la kula. Mawazo yalijaza mpaka tumbo.

.

.

.

Sultana alinyanyuka akamtazama mumewe.

.

.

."Najua una mawazo, mengi yanakutatiza. Sipendi ukinyong'onyea na ukiwa mhaba wa furaha. Acha nkufanyie jambo."

.

.

.

Akaenda jikoni yeye mwenyewe. Akawatoa vijakazi wake wote ndani. Akahudumu sharubati ya ukwaju mzito kwa ajili ya kupalilia hamu ya chakula kwa Sultan.

.

.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

.

Akavua nguoze na kubakiza fupi iliyoacha maungo yake tamanishi wazi. Sultan akanywa sharubati kisha mwanamke akamtaka waende kupata maji pamoja.

.

.

.

Sultana akamkogesha mume na kumpeleka chumbani alipomlaza kifudifudi na kummiminia mafuta ya mzeituni kumkanda mwili mzima kumuondolea uchovu.

Pasipo kuomba ruhusa, Sultana akalala usingizi mzito. Akakoroma akiachama kabisa mdomo wazi.

.

.

.

Mpaka hapo Sultana akawa ameshinda pambano moja; kumpa pumziko mume. Pumziko ambalo hakupata kwa takribani siku mbili.

.

.

.

Akijua wazi mumewe akiamka atahitaji chakula, akajivesha nguo na kuwapa kazi hiyo vijakazi, kisha yeye akaenda kujilaza kando na Sultan.

.

.

.

Baadae yakiwa majira ya jua kupooza wakawa wapo mezani, yeye na mumewe, wakipata biriani, viazi, ndizi na nyama ya ngamia. Nyama aipendayo Sultan. Akishushia pia na sharubati yake pendwa, dhabibu.





Hapo sasa Sultan akaanza kutoa yaliyobana kifua. Akaeleza juu ya mkewe na ya Karim. Mbali na mkufu ambao tayari ameshaanza kuukatia tamaa.

.

.

.

Sultana akamsikiliza mumewe mpaka mwisho. Akashusha pumzi yake ndefu kabla hajaanza kuuliza maswali utadhani hajui kinachoendelea.

.

.

.

"Ina mana mpaka leo hujapata kumuona?"

"Sijamuona na sijui wapi alipo!"

"Umeenda na kuulizia kwa nduguze?"

"Kote huko. Hakuna anayejua!"

"Pole sana, Sultan. Ila usijali, mkeo ni mtu mzima. Anajua anachokifanya. Cha muhimu ni kumuombea salama tu."

"Lakini ..." Sultan akachombeza. "Nina mashaka sana na Karim. Na usiri wake unanipa mashaka zaidi. Nilikuta farasi wa mke wangu kwake. Pamoja na vijakazi wake hapo. Najua alikuwapo pale, lakini sikumuona abadani!

Nahisi kuchanyikiwa."

.

.

.

Kweli ilikuwa inakanganya. Na Sultan alichanganyikiwa kwasababu hakufikirisha akili yake zaidi ya ubinadamu. .

.

.

Alisahau Karim ni nani, na ana uwezo gani. Alimuweka Karim kwenye kategoria moja na binadamu wengine hivyo basi akaishia kustaajabishwa.

.

.

.

Wakaendelea kula mpaka walipomaliza kabla hawajajipumzisha Sultan asionekane mwenye dalili ya kuondoka leo, kesho ama mtondogoo.

.

.

.

Wakati huku ikiwa hivi, watu wakifanya jitihada za kutafuta furaha na amani, huko upande mwingine wa dunia, kwenye kasri ya Sultan ndani ya lupango palikuwa kisima cha huzuni na majuto kwa Karim.

.

.

.

Alikuwa amejilaza juu ya sakafu akiwa amejikunyata kwa baridi. Akihangaika mara kwa mara kupambana na wadudu waliokuwa wanamtambalia.





Alikuwa amevalia bukta tu, tena fupi. Mwili wake uliojaa nywele ukibakia wazi kukaribishwa wadudu kadhaa kusaka kitoweo.

.

.

.

Yalikuwa tayari ni majira ya usiku. Mataa yakawashwa kasrini na walinzi kuanza kuzunguka huku na kule.

.

.

.

Mlinzi mmoja akasogelea selo ya Karim akiwa kabebelea sahani ya chakula baridi. Akafungua mlango na kuiweka sahani chini. Akaisukumia kwa Karim kwa mguu kisha akatoka ndani na kufunga.

.

.

.

Akaenda zake. Punde Karim akaamka na kula. Alikula matonge mawili tu, akaacha. Chakula kilikuwa kibovu. Alikula tu apate jikomboa dhidi ya kifo.

.

.

.

Akajikunyata na kujilaza. Akatazama dari la chumba kwa muda kabla kope zake hazijafunga kwa usingizi.

.

.

.

Akiwa usingizini, mara akasikia sauti ya dada yake yamuita. Yamlilia.

.

.

.

"Kaka, nirudishe duniani!"

.

.

.

Akashtuka kweli. Akatazama kushoto na kulia asione mtu. Akafikicha macho yake mara tatu akihema kwanguvu.

.

.

.

Hakukaa punde, sauti ikarudia tena. Mara hii akiwa macho hajalala. Aliisikia kwenye sikio lake la kushoto.

.

.

.

Sauti yamlilia.

.

.

.

"Kaka, kaka, nirudishe duniani!"

.

.

.



Karim alichanganyikiwa. Alibana masikio yake asisikie. Alihangaika huku na kule akipiga kelele lakini sauti bado ilikuwa inajirudia!

.

.

.

Sauti ilikuwa inamlilia. Iliongezeka kadiri muda ulivyokuwa unaenda. Ilikuwa inadai uhai. Ilikuwa inadai kurudishwa duniani.

.

.

.

Haikukoma mpaka pale askari wa Kasri alipokuja upesi. Alikuwa amebebelea jambia lake refu uso wake ukitambaliwa na mashaka.

.

.

.

"Kuna nini?" Akauliza akishikilia nondo za lupango.

"Kuna mtu!" Akajibu Karim. Alikuwa ametota jasho na ingali baridi. Alikuwa anakodoakodoa akitazama huku na huko.

.

.

.

Askari akatazama tazama asione jambo. Akatahamaki.

.

.

.

"Acha kunisumbua!"

.

.

.

Alitoa macho ya ukali akimnyooshea kidole Karim, kisha akaondoka zake.

.

.

.

Karim akasimama upesi na kwenda nondoni. Akamuita sana Askari asiondoke zake, ila haikusaidia. Askari alienda.

.

.

.

Kishingo upande, akaamua kurejea alipokuwa na kuketi. Hakupata usingizi kabisa. Alidhani sauti itarudi tena masikioni na kumghasi. Alidhani pengine atamuona anayeongea.

.

.

.

Ila haikuwa tena hivyo. Hakusikia chochote mpaka asubuhi inakuja. Jua liliposimama ndipo akalala kujipumzisha.

.

.

.

.

. ***

***

.

.

.

.

.

.

.

"Malkia, tayari watu wanakungojea." Sauti ya Fluffy iliita.

.

.

.

Malkia alikuwa ndani ya chumba akijitazama kwenye kioo. Kichwani alikuwa amevalia krauni ya Malkia inayometameta. Kofia hii ilikuwa ya dhahabu.





Gauni lake lilikuwa linaumiza macho kwa kuwaka. Uso wake ulikuwa umepambwa maridadi kabisa. Alikuwa ananukia marashi ya ghali na matamu puani.

.

.

.

Alijikuta anatabasamu mwenyewe. Haki alivutiwa na kile alichokiona kiooni. Alitazama mkufu wake kifuani kama mtu anayewaza jambo. Kisha taratibu akajikusanya na kunyanyuka.

.

.

.

"Tunaweza kwenda!" Akasema akimtazama Fluffy.

.

.

.

Fluffy alikuwa amevalia suruali ya ngozi iliyombana, blauzi nyeusi yenye kauzibe kagumu kifuani. .

.

.

Begani blauzi hiyo ilikuwa na medali kadhaa, na vyeo pia. Mikono yake ilikuwa imefungwa glovu za ngozi na kubebelea jambia refu.

.

.

.

Alivalia pia buti ndefu. .

.

.

Alionekana kama mtu aendaye vitani. Ndio, alikuwa ni jemedari. Na hizo ndizo zilikuwa nguoze za sherehe.

.

.

.

Shavuni alikuwa na kovu lakini bado halikutosha kumnyang'anya uzuri. Alipendeza sana. Ungeweza kuona ushupavu wake kwa kumtazama.

.

.

.

Mwendo wake pia ulikuwa wa kikakamavu.

.

.

.

Alimuongoza Malkia mpaka mahali fulani aliposimama na kuwatazama watu kwa chini. Mahali hapo palikuwa ni sakafu iliyojishkiza ghorofani. .

.

.

Mtu angesimama hapo basi angeliona watu wote, na watu wote wangelimuona. Haya yalikuwa makazi ya Kuhani mkuu wa mwisho ambaye naye alienda na maji kuwafuata wenzake baada ya kulambishwa ncha ya panga la Malkia.

.

.

.

Malkia sasa alikuwa na jeshi kubwa. Jeshi la kutosha. Jeshi la kutisha.





Jeshi hili lingeweza kumpa kiburi mtu yeyote yule: kiongozi yoyote yule kwenye uso wa dunia. Wanaume hawa walikuwa maelfu, tena wenye afya na silaha.

.

.

.

Malkia alitabasamu na kupunga mkono, watu wakalipuka na furaha. Walinyoosha juu silaha zao wakipiga nduru.

.

.

.

"Maisha marefu Malkia!" Fluffy akapaza sauti.

"Maisha marefu Malkia!"wakaitikia wafuasi. "Maisha marefu Malkia! Maisha marefu Malkia!"

.

.

.

Malkia alipaliwa na furaha. Alihisi kifua chake chataka kupasuka. Macho yake yalilenga machozi. Mdomo wake ulitafuta cha kunena.

.

.

.

"Leo hii imekuwa siku ya furaha sana kwangu," akasema. "Sikuwahi kujua kama nilipewa talanta hii hapa ulimwenguni. Sina cha kusema zaidi ya kuwarudishia shukrani zote kwenu. .

.

.

Mlitaka haya, na ndiyo maana yakatukia. Tumetengeneza familia mpya sasa. Familia yenye nguvu na upendo ndani yake.

.

.

.

Familia ya Samaridi. Hakuna familia itakayokuja kutokea kama hii. Samaridi ni mimi; Samaridi ni wewe. Samaridi ni sisi!"

.

.

.

Yowe zikaita tena uwanjani.

.

.

.Ilipulizwa tarumbeta kuu, bendera mpya ya Samaridi ikapandishwa juu na Malkia.

.

.

.

Ilikuwa bendera yenye rangi tatu: nyekundu, kijani na njano. Juuze kukiwa na ua kubwa la Samaridi. Ua lijishkizalo pembezoni mwa mto.

.

.

.

Nyekundu rangi ya damu na moto. Ilikuwa kiashiria cha namna gani Samaridi ilivyopatikana.

.

.

.

Damu za makuhani zilimwagika, ili watu wapate kuwa huru. Ililazimika baadhi ya watu wauawe ili Samaridi ipate kutokea.





Kijani rangi ya ustawi na ukuaji. Rangi hii iliwekwa kuonyesha imani, mategemeo na dhamira ya Samaridi. Kukua.

.

.

.

Kijani ni upya, ni mbolea. .

.

.

Samaridi haitaishia pale, bali itazidi kuchanua. Na majani yake mapana yataingilia mpaka kwenye himaya nyingine.

.

.

.

Njano rangi ya mwanga na furaha. Samaridi itakuwa mwanga kwa himaya zingine, kwa matendo ya haki na usawa.

.

.

.

Siku zote lengo lake mbele itakuwa ni kuwafanya watu wajazwe na furaha. Wawe na nguvu na wenye hekima.

.

.

.

Lakini zaidi ya yote hayo, bendera ikatiwa nakshi ya kofia ama krauni ya Malkia juu ya ua. Krauni hii ilikuwa haionekani ukiitazama upesi bali kwa kina.

.

.

.

Ilikuwa ni ishara ya utawala wa Malkia. Muasisi wa himaya. .

.

.

Ilikuwa ni ukumbusho wa milele, watu wote wakajua kwamba himaya hiyo ilifumwa na mkono stadi wa mwanamke.

.

.

.

Si tu mwanamke, bali mwanamke shupavu. Mwanamke wa nguvu. Mwanamke wa shoka!

.

.

.

Baada ya Malkia kupandisha bendera, akazunguka kuweka alama kwenye mipaka yake. Kisha akaketi na wanaume watatu walioteuliwa kwa ajili ya majadiliano kadhaa muhimu kwa himaya.

.

.

.Kalikuwa kajikao kadogo, kwa ujumla wakiwa watu sita: wanaume hao watatu pamoja na Malkia, Fluffy na Zura.

.

.

.Wakajadiliana kuhusu mambo ya chakula, ulinzi wa himaya na hata malengo pia.

.

.

.Chakula kilichokuwepo hakikuwa kingi kutosheleza mwaka. Hivyo ilibidi jambo lifanyike upesi kabla njaa haijaja.





Wakakubaliana milango ifunguliwe sasa kwa watu kujishughulisha na shughuli za maendeleo huku serikali ikiwaunga mkono kwa kiasi kikubwa.

.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

.

.

Wenye kujuzi wa kulima, walime. Wafanyabiashara nao wafanye. Wafua vyuma na wawindaji pia.

.

.

.Kwa muda wa mwaka mmoja mzima, serikali haitatoza kodi wala makato yoyote. Yote hayo yakiwa yamelenga kukomaza kwanza uchumi wa watu binafsi.

.

.

.Kuhusu jeshi la ulinzi wa himaya, wakakubaliana kufanya usahili, si watu wote watachukuliwa ingawa jukumu la kulinda himaya ni la wote.

.

.

.

Wale watakaofuzu watatengwa na kuitwa wanajeshi. Watalipwa na kutengenezewa sare.

.

.

.

Zoezi hilo la usahili atalisimamia Fluffy mwenyewe. Shughuli za uzalishaji na mambo ya biashara akakabidhiwa Zura pamoja na wasaidizi.

.

.

.Angalau mambo yalienda sawa sasa. Kikao kikavunjwa kwa miadi ya kuitishwa muda wowote jambo muhimu litakapozuka.

.

.



Lakini kabla ya kutawanyika, mwanaume mmoja mjumbe wa kikao, akijulikana kwa jina la Bozi, alisafisha koo lake kudai kusikilizwa. .

.

.

Watu wote wakamtazama na kumpa masikio.

.

.

.

"Malkia, kuna jambo," akasema.

"Lipi hilo?" Malkia akauliza.

"Ni pendekezo tu," akasema Bozi."Kuna watu wana talanta huko nje. Mmoja ni mvumbuzi na mjuzi wa historia. Mwengine ana nguvu za kumbukumbu za mambo ya karne.

.

.

.

Watu hawa walikuwa wanatumiwa na Makuhani kwenye shughuli zao na wakawapa msaada mkubwa.





Vipi, hawawezi wakatoa msaada wowote kwenye himaya yetu changa?"

.

.

.

Malkia akapendezwa sana na hizo habari. Akaomba kukutana na watu hao upesi apate kuwatazama na kuwatathmini.

.

.

.

Kutii agizo la Malkia, upesi watu hao wakaitwa. Na Malkia akapata nao faragha.

.

.

.

"Unaweza kunambia ni nini unakumbuka ambacho ni wazi kitanisisimua?" Malkia akamuuliza mtunza kumbukumbu.

.

.

.

Katika hali ya kustaajabisha, mtunza kumbukumbu akaelezea mapambano yote kati ya Malkia na Makuhani.

.

.

.

Hakuacha hata tukio moja nyuma. Hakuacha hata neno moja nyuma. Ni kana kwamba aliyarekodi matukio hayo kwa mkanda wa filamu.

.

.

.

Maneno yake na namna alivyoyatamka kwa umakini, kulimstaajabisha Malkia. Alibakia mdomo wazi akimtazama mtu huyo anavyomiminika.

Mpaka anamaliza, Malkia alikuwa ameziba mdomo wake kwa kustaajabu.

.

.

.

Aliwezaje kukumbuka yote haya? Alijiuliz akilini.

.

.

.

Kweli akakiri mtu huyu alikuwa na talanta. Anafaa kumtumia kwa ajili ya kutunza rekodi zote muhimu. Ila alimtaka pia awe anaziweka kwenye maandishi.

.

.

.

"Samahani Malkia, siwezi kusoma wala kuandika," akasema mwanaume huyo.

"Unaitwa nani?"Malkia akauliza.

"Naitwa Dummy," akajibu mwanaume.

"Dummy, unamjua Zura?"

"Ndiyo, namjua."

"Mfuate yeye. Mwambie Malkia amenielekeza unifundishe kusoma na kuandika."

.

.

.

Malkia akamkabidhi Dummy mwanajeshi mmoja amsaidie kumuongoza kwenda kwa Zura. Sasa Malkia akabakia na mwanaume mmoja.





Yule aliyenadiwa kuwa mjuvi wa historia.

.

.

.

Malkia akataka pia kuyasikia yake.

.

.

.

"Una kipi cha kunambia?"

"Malkia, najua wapi asili ya mkufu huo uliovaa," akajibu mwanaume huyo.

.

.

.

Jibu hilo likamfanya Malkia abandue mgongo wake kitini na kukaa vema. Habari hizi zilimshtua. Alizunguka mahali na sehemu nyingi lakini hakuwahi kukutana na mtu aliyesema hili.

.

.

.

Tena kwa kujiamini kiasi hiki.

.

.

.

Alijikuta anapata kiu kali ya kufahamu. Kabla hajatia neno, mwanaume akaongezea:

"Najua pia wapi ulipotokea."

.

.

.

Malkia akakunja sura akitoa macho.

.

.

.

.

.

.

.

***

***

.

.

.

.

.

.

.

.

Ulikuwa ni usiku wa pili sasa Rhoda akiwa ndani ya himaya na Venin. .

.

Ndani ya usiku huu, akikuwa amejilaza chumbani akihesabu vidole vyake. Kichwani akitatua mambo kadhaa.

.

.

.

Chumba kilikuwa kikubwa mno. Kitanda kipana cheusi chenye godoro na shuka jekundu.

.

.

.

Kwenye kuta za chumba kulikuwa kuna picha picha kadhaa za wanyama zinazovutia. Picha hizi ziliwekwa baada ya Rhoda kushinikiza.

.

.

.

Hapo awali, kulikuwa kumebandikwa midoli ya kutisha. Mifupa na mabaki ya binadamu. .

.

.

Kwa binadamu wa kawaida asingeweza kulala.

.

.

.

Hadi marashi ilibidi yabadilishwe kwa kupuliziwa mapya, kwani harufu ya damu na miozo ndiyo ilikuwa imeshikilia chumba.

.

.

.

Rhoda aliona kama kesho yachelewa apate kwenda. Alishachoka kuishi ndani ya himaya hii ya kutisha.







Alitamani asogeze masaa mbele. Alikuwa anachukia kila mara anapomuona Venin anamtazama kwa macho ya uchu.

.

.

.

Alijihisi hayupo salama kabisa. Na lolote laweza kutukia ndani ya muda wowote.

.

.

.

Na kweli, kama vile alivyowaza, mara akasikia sauti ya mlango unagongwa. Moyo wake ukalipuka kama umeangushiwa bomu!

.

.

.

Alitoa macho akatazama mlangoni. Kabla hajasema wala kufanya lolote alishajua ni nani yupo mlangoni. .

.

.

Alijiuliza nini afanye. Aliamua kukaa kimya, ila hodi haikukoma. Iliendelea kuita na kuita. Na mwishowe jina likatajwa:

"Rhodaa!" .

.

.

Ilikuwa ni sauti ya Venin. Bado Rhoda aliamua kunyamaza akiigiza amelala.

.

.

.

"Najua upo macho Rhoda," sauti ikasema. "Naomba niingie nina maongezi na wewe."

"Tutaongea kesho," akajibu Rhoda kwa kunong'oneza. Sauti ambayo haitoki hata nje ya kitanda.

"Nenda bana. Sitaki kuongea na mtu!" Rhoda aliendelea kunong'oneza. Ni kama tu vile alikuwa anajiongelesha mwenyewe maana sauti ilikuwa ndogo mno!

"Rhodaa!" Sauti ikaendelea kuita mlangoni.

Rhoda akajifunika shuka gubigubi.

"Nimesema sitaki," akasema kwa kunong'ona. Mara sauti ikamjibu.

.

.

.

"Sitakaa sana."

.

.

.

Akashtuka. Aliisikia sauti hiyo karibu kabisa na yeye. .

.

.

Alifunua shuka akatazama. Mara akamuona Venin amesimama kando na kitanda!

.

.

.

.

. ***







Moyo wake ulipiga sana. Karibia unyofokee nje. Alijikuta mwili unapigwa na baridi lililoanzia kichwani mpaka miguuni.

.

.

.

Mwanaume huyu amefikaje hapa na mlango umefungwa? Ni kama vile alisahau uwezo wa Venin. Kwamba ni mlozi wa tabaka la juu.

.

.

.

Kwamba mtu huyu ni maarufu kwa hilo na hata yeye amemfuata kwasababu hiyo akifunga safari ndefu tokea Goshen.

.

.

.

Kwa muda akakosa cha kusema akihema tu. Alipopata oksijeni ya kutosha kumshusha angalau robo ya presha, ndipo akaongea. .

.

.

Wakati huo Venin akiwa anatabasamu asijue kwamba anaendelea kuchukiza na kutisha.

.

.

.

"Venin, nini wataka kwangu?" Rhoda akauliza.

"Nataka tu kuongea nawe. Samahani naonekana kukushtua mno."

"Usijali," Rhoda akasema pasipo kumaanisha. "Ila muda mwingine usiwe unaingia kama sijakuruhusu. Vipi kama ungenikuta nipo uchi?"

"Tatizo haukutaka kunijibu, Rhoda."

"Nilikuwa nimelala. Ningekujibuje?"

"Haukuwa umelala. Nilinusa harufu ya hasira zako, pia ulikuwa unaongea kwa sauti nikasikia."

.

.

.

Kukawa kimya kidogo. Rhoda alikosa cha kusema.

.

.

.

"Usijali, sijaja kwa hilo bali jambo moja," akasema Venin

"Jambo gani?"

.

.

.

Venin akasafisha koo kwanza.

.

.

.

"Unajua ni kwa muda mrefu sana nimekuwa mpweke. Nyumba hii ni kubwa na huchosha. Siwezi nikaendelea kuishi hivi milele.

.

.

.

Ningependa nipate mtu wa karibu. Atakayewajibika na furaha yangu, kujaza pale nilipopungukiwa.





Nimeona wewe wastahili kwa hilo. Ningependa kukupatia hiyo nafasi," akahitimisha Venin.

.

.

.

Alisema kana kwamba Rhoda ndiye mwenye shida ilhali ni yeye. Haki madaraka yalimlevya, hakuzoea kuomba wala kubembeleza.

.

.

.

Hata hayo maneno machache aliyoyasema hapo, aliambiwa na kijakazi wake akayajaribu pengine yangeweza kumsaidia.

.

.

.

"Una maanisha nini Venin?" Rhoda akauliza. Alishajua nini Venin anataka, na akili yake ilikuwa inachakata cha kumjibu wakati akimzubaisha kwa swali lisilo na tija.

"Nimesema, nataka nikupe hiyo nafasi ya kuwa nami karibu."

"Kuwa nawe karibu kivipi?"

.

.

.

Venin akasaka jibu. Kidogo kidogo alikuwa anapoteza uwezo wa kumudu hisia zake za hasira.

.

.

.

"Uwe mke wangu," akajibu. Jibu hili lilikuwa lina tembe za ukali ndaniye.

.

.

.

Rhoda alijua fika hawezi akakataa ombi la mwanaume huyo, ni hatari kwa usalama wake. Tena ukizingatia yupo ndani ya himaya yake.

.

.

.

Aliwaza atatokaje kwenye mtego huo na uhai wake. Alihofia kwenda kuning'inzwa kule msituni.

.

.

.

"Sawa, nimekuelewa Venin," akajibu. "Ila imekuwa ghafla sana, nimeshtuka na sikutaraji.

.

.

.

Naomba ungenipatia wasaa wa kufikiria na kuchambua maamuzi yangu."

"Sawa," akajibu Venin. .

.

.

Rhoda akategemea kwa jibu hilo atakuwa amefanikiwa. Moyo wake angalau ukapoa. Ila ajabu akashangaa Venin bado ameendelea kuketi.

.

.

.

"Nisubirie mpaka saa ngapi?" Venin akauliza. Kabla Rhoda hajajibu, akamvunja moyo akisema:

"Siwezi toka hapa pasipo jibu hilo."





Rhoda akaishiwa nguvu. Kitumbua kiliingia mchanga. Mchezo haukuwa umekwisha na hakuwa ameshinda.

.

.

.

Akafikiria upesi. .

.

.

Hii ndiyo ilikuwa nguvu yake inayomuokoa kila mara. Kufikiria na kuibuka na mawazo kwa haraka.

.

.

.

Alipata cha kusema. Lakini pia ili lieleweke ilibidi ajikaze kisabuni. Ameze tikiti zima.

.

.

.

Akanyanyuka na kujitengenezea vema akiketi. Akautwaa mkono wa Venin na kuuweka kiganjani mwake.

.

.

.

Ulikuwa wa baridi mno kama vile ametoka ndani ya jokofu. Rhoda alitamani kuutupia mbali, ila akavumilia.

.

.

.

"Venin, kipi utanipa endapo nikikukubalia kuwa mke wako?" Akauliza.

.

.

.

Venin akatabasamu meno yote yakionekana. Aliona sasa mambo yake yaenda kuwa shwari.

.

.

.

"Nitakupa nusu ya himaya yangu," akajibu upesi.

.

.

.

Rhoda akatabasamu.

.

.

.

"Au wewe wataka nini?" Venin akauliza baada ya kuona hilo jambo halikukuna sana moyo wa Rhoda.

"Nataka jambo fulani. Hili litakuwa mtihani kwako na endapo utalifaulu basi mimi niko radhi, kwa moyo wote, niwe wako milele."

"Jambo gani hilo Venin afanye upesi? Unataka kichwa cha Mfalme gani? Malkia gani?" Venin akauliza haraka.

"Sitaki jambo kubwa sana, bali tu unisaidie kupata ninachoenda kutafuta huko Tanashe.

.

.

.

Nitakapopata kitu hicho na kurejea salama, hakika nitakupa chochote unachotaka."

.

.

.

Rhoda alisema kwa kujiamini akimtazama Venin machoni. Alijua fika mpango huo ni mtego mmoja mkubwa sana wa kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.





Kwanza ataupata mkufu, pili atautumia kummaliza Venin. Aliamini hili ndilo wazo takatifu kwake kwa muda huo.

.

.

.

"Kitu gani hicho waenda kutafuta? Hukuniambia zaidi ya kuomba kinga," akasema Venin.

"Ni mkufu tu wa thamani niupendao."

"Mkufu?"

"Ndio."

"Mkufu tu? - Siwezi nikakutafutia mwingine mzuri zaidi?"

"Hapana, nautaka huo tu."

.

.

.

Hapo Venin akanywea. Hakika alikamatwa. Alikumbuka namna alivyomwambia kaka yake kuhusu ujio wa watu fulani Tanashe - kwamba watakuja na yeye inabidi awamalize ili apate damu ya kumtia nguvu.

.

.

.

Sasa mipango yake ilikuwa inaelekea kuharibika. .

.

.

Alidhani angeweza kumshawishi Rhoda asiende huko, lakini sasa maji yalionekana kuzidi unga. Asingeweza.

.

.

.

"Sawa, nimekusikia," akajibu na kuongezea; "Kesho tutaweka agano."

.

.

.

Hakuongea tena. Akanyanyuka na kuondoka zake akimwacha Rhoda na tabasamu pomoni.

.

.

.

Alielekezea kichwa chini akienenda. Akanyookea chumbani kwake mlango ulipojifungua kumpokea kisha ukajifunga na komeo alipozama.

.

.

.

.

.

.

***

.

.

.

.

.

Askari wa Kasri alikuwa anatembea akiwa amebebelea sahani ya chakula mithili ya uji mchanganyiko na makande.

.

.

.

Chakula hichi kilikuwa kinatoa mvuke mzito. Na kwa macho tu hakikuonekana kizuri wala kitamu.

.

.

.

Askari huyu alikuwa anakwepa mvuke wa chakula hicho kana kwamba anakwepa harufu ya kinyesi. Bila shaka chakula kilikuwa kina harufu isiyopendeza.

.

.

.

Alikomea mbele ya chumba lupango, cha tatu tokea mlangoni, chumba chenye giza alipohifadhiwa Karim. Akagonga vyuma vya mlango.





Kang! Kang!

.

.

.

Kisha akainama na kukipitisha chakula kwenye uwazi akikisukumia mbali.

.

.

.

"Chakula hicho!" Alisema kwa amri.

.

.

.

Yalikuwa ni majira ya jioni, kama saa kumi na moja ya mapema tu, lakini humu ndani palikuwa giza kana kwamba saa nne usiku. .

.

.

Hakukuwa na mwanga. .

.

.

Kumuona Askari kulihitaji utumbue macho. Kumuona Karim ndiyo kabisaa ilibidi ukodoe kiasi cha kutaka kunyofolea macho nje.

.

.

.

Askari alisimama akitazama kwa muda kidogo kama Karim atachukua chakula. Hakuona wala kuhisi chochote. .

.

.

Akapaza sauti;

"Hutaki kula enh?"

Kimya.

"Sema kama hutaki kula nikampelekee mbwa wangu ale!" Akafoka.

.

.

.

Bado kukawa kimya.

.

.

.

Bwana Karim hakuwa amekula kwa siku nzima. Askari alitegemea kama angeona chakula hicho basi angekiparamia, ila ikawa kinyume.

.

.

.

Alihisi labda Karim amekufa, ama hayupo ndani. Haraka akachomoa kurunzi yake kiunoni na kumulika.

.

.

.

Alikuwepo! .

.

.

Alikuwa amejikusanyia kwenye kona ya lupango akiwa amekunja magoti yake na kulaza kichwa juu yake.

.

.

.

Askari akahakikisha kama anahema. Ndiyo alikuwa anahema, akathibitisha. Akazima kurunzi yake ya kale.

.

.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

.

"Nitarejea hapa baada ya muda mchache. Kama hautakuwa umekula hicho chakula nitampeleka mbwa!" Akatishia Askari.

"Chukua uende nacho!" Karim akajibu kwa sauti ya chini.

"Ooooh hutaki kula, sio?" Askari akauliza kwa kebehi.

"Si kwamba sitaki kula," akajibu Karim. "Ila hicho chakula ni cha mbwa."

.

.

.

Askari akakohoa kwa kicheko.





"Kwani wewe una utofauti gani na mbwa hivi sasa?" Akauliza.

.

.

.

Kimya kidogo, akaongezea:

.

.

.

"Karim, majira yako yamekwisha. Hii ndiyo hatma yako. Kama wajitia wewe ni mlozi mkubwa, jikomboe humu wote tuone."

.

.

.

Akangojea majibu. Kulikuwa bado kimya. Akaamua kuondoka zake asichukue hata kile chakula alichokuwa anatishia.

.

.

.

Akatoka zake nje kwenda kusimama mbali kidogo na jela. Akatoa tumbaku mfukoni na kuanza kuvuta akifurahia uhuru.

.

.

.

Kutokana na mwanga akawa sasa anaonekana vema. Alikuwa ni yule yule Askari anayemtembelea na kumpa Karim chakula kila siku.

.

.

.

Alikuwa amevalia shati na bukta fupi ya kaki. Kichwani alikuwa na kofia nyekundu, baghalasia, yenye kamfyagio cheusi.

.

.

.

Alikuwa ndiye anayehusika na kazi hiyo, na jela nzima kwa ujumla. .

.

.

Jela hii haikuwa na wafungwa wengi, watano tu, hivyo haikuhitaji kusimamiwa na lukuki ya watu.

.

.

.

Askari huyo akiwa hapo anatazama tazama huku na huko ya Kasri, akivuta tumbaku, mara akaona mtu mmoja kwa mbali. Karibu na geti.

.

.

.

Mtu huyo alikuwa anaongea na askari mwingine, na mara askari huyo akanyooshea kidole kwake.

.

.

.

Mara mtu huyo akaanza kujongea kumfuata. Hatua zake zilikuwa ndefu hivyo punde akawa amemfikia.

.

.

.

Alikuwa ni mwanaume mwenye wingi wa ndevu. Alivalia kanzu yenye mistari mistari na viatu vya wazi. Kichwa chake alikifunga na kiremba.

.

.

.

Mkononi alikuwa amebebelea kifurushi kidogo cheusi.





Akasalimia kisha akajitambulisha kama mfanyakazi wa Karim.

.

.

.

"Nimekuja kumuona na kumjulia hali."

.

.

.

Askari akamtazama kwa macho ya upekuzi na kebehi.

.

.

.

"Oooh kwahiyo na wewe ni mlozi mwenzake?"

.

.

.

Kijakazi yule wa Karim akanyamaza asijibu.

.

.

.

"Hicho nini umebeba?" Askari akauliza akitazama kifurushi alichokikumbatia mgeni.

"Ni chakula tu nimemletea." "Fungua nione!" Akaamuru. .

.

.

Kijakazi wa Karim akafungua na kuonyeshea. Alikuwa amebeba matunda, nyama na vyakula vikavu. Pia kinywaji ndani ya chupa.

.

.

.

Askari akasonya.

.

.

.

"Ndiyo umemletea vitu vyote hivyo?"

"Ndio."

.

.

.

Akachukua matunda na nyama mpaka pale mkono wake ulipojaa, kisha ndiyo akampeleka mgeni huyo ndani ya jela akitafuna chakula alicholetewa Karim.

.

.

.

"Hata mimi sili chakula cha aina hii!" Alisema akitafuna. Mpaka walipofika, alikuwa amekula robo kama siyo nusu.

.

.

.

"Wewe una mgeni wako hapa!" Akapaza mbele ya lupango ya Karim. .

.

.

Akachukua chakula chake, maana hakikuwa kimeguswa, kisha akaondoka akimsisitizia mgeni ana muda mchache mno wa kuongea.

.

.

.

Karim akasimama kukutana na kijakazi wake. Akapokea mzigo na kuuweka chini.

.

.

.

"Amekula chakula chako kingi," akasema kijakazi. "Hakikuwa hivyo."

"Usijali," akasema Karim. "Nilikuwa na shida na wewe kuliko hata hicho chakula."

"Nisamehe, mkuu, kwa kutokuja mapema. Nilikuwa nahofia."

"Ilimradi umeshakuja, usijali."





Kukawa kimya kidogo.

.

.

.

"Kuna mtu hapo?" Akauliza Karim. Kijakazi akatazama kushoto na kulia.

"Bila shaka tuko peke yetu."

"Sawa sawa, sasa sikia," akasema Karim akimshika mkono Kijakazi.

"Kuna kitu nataka ufanye, nataka unitoe humu. Umesikia?"

"Ndio, mkuu."

.

.

.

Akamuelekeza Kiajakazi wake namna ya kufanya. Alimuelekeza dawa fulani kule kwenye makazi yake aiteke na kuja nayo ampatie.

.

.

.

Ahakikishe hakuna mtu yeyote atakayeiona.

.

.

.

"Unaweza?" Karim akauliza.

"Ndio, naweza mkuu. Nitarejea hapa kesho."

"Sawa, umenielewa lakini?"

"Nimekuelewa kila kitu."

"Ufanye upesi kabla Sultan hajaja. Usisahau. Uje unitoe humu!"

.

.

.

Kijakazi akatikisa kichwa kisha akaondoka. Karim sasa akaketi na kula akiwa na ahueni moyoni.

.

.

.

Alijua sasa muda si mrefu atakuwa huru. Na pengine hata kulipiza kisasi. Ila kwanza amrejeshe dada yake duniani.

.

.

Ikiwa ni majira ya asubuhi ambayo bado ilikuwa na giza, Malkia aliamka.



Alikuwa ndani ya chumba kikubwa mno, akiwa amelala juu ya kitanda kipana kilichokuwa kimetandikwa vema, kimejaa mito ya kila muundo; pembe nne, pembe tatu na kifilimbi.



Samani za chumba zilikuwa za kuvutia na kuhamasisha kupumzika. Chumba kilikuwa kimepambwa vema kwa maua, urembo, picha na kadhalika.



Kweli kilikuwa chumba cha Malkia.



Malkia alikuwa amevalia nguo nyepesi ya kulalia ikiwa imedariziwa kwa nyuzi za dhahabu na fedha.



Nywele zake ndefu alikuwa amezilazia huko mgongoni. Alikuwa ananukia marashi ya uwaridi, ngozi yake ikimeta na mafuta ya nazi.



Alinyanyuka akaendea dirisha kubwa lililojipachika chumbani na kulifungua. Akatazama himaya yake kwa muda.



Akawaza mambo kadhaa kuihusu. Akaitazama kila kona kwa uwezo wa macho yake. Ila haikupita punde akaikumbuka Goshen.



Alijiona yupo juu ya himaya ya Goshen, kwenye kile chumba chake, akiitazama himaya hiyo kama apendavyo kufanya kila asubuhi.



Aliona kila jambo vilevile kama alivyokuwa anaona. Aliona wakulima wakidamka asubuhi kwenda mashambani.



Aliona taa zikiwashwa, farasi wakipasha miguu yao kwa ajili ya safari.



Aliona malango ya makazi ya mfalme yakifunguliwa na askari wakitoka kwenda nje. Aliona watoto wakirandaranda huku na kule wakifukuzana kwa matabasamu.





Hakika ilipendeza na kugusa moyo wake. Akajikuta anatoa chozi.



Alijihisi amekuwa wa baridi, vinyweleo vyamsisimka. Aliikumbuka Goshen. Alitamani ingekuwepo mbele yake.

Aliwakumbuka watu wake. Alijiuliza wapo katika hali gani. Alitamani kuwaona hata kwa sekunde ajue wanaishije, ila hakuwa na huo uwezo.



Hilo likamuuma zaidi. Akajikuta anadondosha tena chozi.



Macho yake yalikuwa mekundu. Na pua yake pia. Alisikia mtu anagonga mlangoni haraka akafuta machozi kabla hajasema: "Karibu!" Akaingia Zura akiwa amebebelea chakula cha asubuhi. Alikuwa amevalia gauni na kofia yake kichwani, vyote rangi ya zambarau. "Bila shaka utakuwa umeamka mapema sana, Malkia," akasema Zura akiweka vitu mezani. "Najua ukiwa umesimama dirishani; ulikuwa unatazama himaya yako?" Akauliza kwa tabasamu.



Muda wote huo Malkia alikuwa amempa mgongo. Alijitahidi kutabasamu kisha akageuka, akitazama chini. "Ahsante sana kwa chakula," akasema. "Mbona hukumwachia kijakazi aniletee?" "Tangu lini ukahudumiwa na mtu mwingine mie nikiwepo? Tena mwenye nguvu tele?" Akauliza Zura, tena akitabasamu.



Malkia akaketi juu ya kitanda akitabasamu na kutazama chini. Zura akahisi kuna jambo halipo sawa. "Malkia," akaita. "Nini shida?" Akauliza akijongea kitandani.



Malkia hakusema jambo. Bado alikuwa kimya akitazama chini.



Zura akaunyanyua uso wake na kumtazama machoni. Akaona macho mekundu.





Akamshika mikono yake yote miwili kama daktari apimaye ugonjwa. "Nini kinakusumbua, mwanangu?" Akauliza kwa sauti ya ukarimu. "Niko sawa, ni hali tu ya kupita," akajibu Malkia. "Haupo sawa, mwanangu. Huwezi nidanganya chochote kuhusu wewe. Nimekua nawe tokea ukiwa mdogo kabisa, najua unapokuwa sawa na unapokuwa na itilafu.



Naomba unishirikishe maana sitakaa kwa amani." Malkia akavuta kamasi na kufikicha pua yake nyekundu. Alihofia kumwambia Zura juu ya kinachomsumbua kwakuwa kingeweza kumnyima amani.



Ama kingemkumbusha jambo ambalo amelisahau na tayari kalizika moyoni. Lakini ilikuwa ngumu kumlaghai Zura, ilibidi awe mjanja zaidi ya sungura. "Sijiskii vizuri, inaweza ikawa homa," akajibu. Zura akanyanyua mkono wake upesi na kuuweka mgongo wa kiganja kwenye paji la uso wa Malkia.



Hakukuwa na joto.



Akavuta na kushusha pumzi ndefu. "Ilianza usiku?" Akauliza. "Hapana," akajibu Malkia. "Ni punde tu nilipoamka." Zura akatikisa kichwa chake kama mtu aliyekubali. Akanyanyuka na kwenda dirishani.

Akatazama nje kwa sekunde kadhaa, kisha akageuka kumtazama Malkia. "Malkia, umekumbuka Goshen?" Akauliza. Malkia kimya. Alikuwa anatazama chini, na haikuchukua muda mrefu chozi likamshuka.



Zura akajua nini tatizo.



Akamsogelea Malkia na kumkumbatia akilaza kichwa chake juu ya kifuache.





Akawa anachezea nywele za Malkia kama bwana achezeaye manyoya ya paka, pasipo kusema jambo lolote.

Malkia akawa analia. Mafua yake yakaongezeka na hata kwikwi zikazidi.

Zura akahamishia kiganja chake mgongoni mwa Malkia akawa anambembeleza kwa kumpigapiga.



Bado hakusema kitu. Ni kama vile alikosa cha kusema kwa muda huo. Alichokifanya ni kumbembeleza tu Malkia huku akitazama dirishani. "Nimepakumbuka nyumbani," akasema Malkia kwa sauti ya kilio. "Nimepakumbuka nyumbani, mama. Nimepakumbuka mno." "Usijali, mwanangu. Kule ni nyumbani na patakuwa nyumbani siku zote. Hauwezi ukapatoa moyoni.



Lakini vipi kuhusu hawa watoto wako wa sasa? Utawaacha yatima?" Malkia hakujibu. Akaendelea kulia kwa muda. Alipokuja kutulia sasa kifua kikiwa chepesi, akasema: "Siwezi nikawaacha. Wameweka maisha yao mikononi mwangu. Wameniamini na roho zao. Wananitumikia kwa nguvu na damu.



Nitakuwa mtu wa aina gani kuvipa kisogo vyote hivyo?" Akajichoropoa kifuani mwa Zura na kushika tama. Hakika alikuwa njia panda.

Zura aliumia kumuona katika hiyo hali. "Malkia," akaita. "Nashindwa kukushauri lile lililo jema. Fuata moyo wako, mimi nitakuwa upande wako daima." Kisha akasimama. "Naona nikuache utafakari." "Hapana!" Akapaza Malkia. Alimtazama Zura akamshika mkono. "Tafadhali, usiende. Keti kuna jambo nataka kukwambia."





Zura akaketi. "Jana nilikutana na mtu mmoja, punde tulipomaliza kikao, akaniambia mambo ya kustaajabisha. Mambo makubwa kuhusu huu mkufu wangu." "Bila shaka ni Seth," Zura akadakia. "Umejuaje? "Hamna mwingine zaidi yake. Seth anajua mambo mengi ya kushangaza, ukizingatia umri wake ni mdogo mno." "Unamuamini?" Malkia akauliza. "Ndio, namwamini," akajibu Zura, kisha akaongezea: "Nilishawahi kukutana naye siku fulani. Akaniambia mambo ya kweli, ya kale haswa." "Kuhusu nini?" "Kuhusu himaya zote, haswa Goshen." "Goshen!" "Ndiyo. Anajua historia yake yote. Anajua ilipochimbukia, kuanzia kipindi kile cha vita za koo kati ya Geepas na Oethopas.



Kiufupi anajua juu ya historia za himaya zote. Hata pia akimtazama mtu anaweza jua ni wa himaya ipi." "Mbona hukuniambia?" "Sikuona haja ya kuharakisha hivyo, nilijua muda utafika mkakutana." "Amekwambia kuhusu mkufu wangu?" "Hapana, hajaniambia." Malkia akashusha pumzi ndefu. "Ni nini amekwambia?" Zura akauliza. "Ameniambia wapi mkufu huu unatokea. Huko katika himaya ya wasioonekana, chini ya bahari ya Sham.



Kama ukitazama vema nyuma ya kidani cha mkufu huu, kuna chapa ya maji. Lakini pia tarakimu ziliondikwa katika lugha watumiayo watu toka kwenye hiyo himaya.



Tarakimu hizo huonyesha huu mkufu ni wa ngapi katika utengenezwaji wake."





"Ni wa ngapi?" Zura akalipuka. "Ni wa kwanza!" Malkia akajibu. "Ina maana kutakuwa kuna mingine?" "Pasipo shaka, kutakuwa kuna mingine. Ila haijulikani wapi ilipo na nani anaimiliki. Vilevile kama uwezo wake utakuwa sawa na huu ama zaidi.



Mikufu hii hutolewa kila baada ya karne moja. Na unakuwa umemlenga mtu mmoja tu aumiliki. Na dunia haiwi shwari mpaka pale mtu huyo, anayestahili, atakapokuwa nao." "Sasa mkufu huo humtafutaje anayetakiwa kuumiliki?" "Kwa njia yoyote ile, ndivyo alivyoniambia. Lakini kwa mkufu huu kuonyesha ama kufanya jambo ni lazima uwe kwa anayestahili kuwa nao.



Ila haimaanishi kwamba asiyestahili hawezi kuutumia, la hasha! Anaweza pia, ilimradi tu arandane damu na mkufu huo.

Lakini hataweza kuutumia kama yule anayeumiliki. Na pia mkufu huo waweza kumpeleka mrama na kumlevya kiburi cha madaraka." "Sasa unajuaje kama mkufu huo upo kwa anayestahili?" Zura akauliza. "Mtu anayestahili anaweza kuamsha mkufu ukiwa karibu yake, hata kama haupo kifuani.



Na yeye ndiye anaweza kuushika na kuuficha mkufu huo mkononi, akanuwia." Kukawa kimya kidogo. "Ameniambia kuna muda itafikia, watu hao wa himaya ya wasioonekana watakuja kudai mikufu yao yote.



Wataambatana na jeshi zito kuja kudai mali zao." Hapo Malkia akawa ametatizwa kidogo. Alijitahidi kuvuta fikra itakuaje pindi atakapoona jeshi hilo la watu wasioonekana.





Watakuaje na ilhali hawaonekani. Watapambana vipi na watu na ingali hawaonekani?



Zura akamng'amua toka kwenye fikra hizo kwa kumuuliza swali: "Amekuambia lolote kuhusu nguvu za ziada ambazo hauzijui?" "Ndio, kuna jipya," akasema Malkia. "Ni kuhusu agano na mkufu. Waweza agano na mkufu huu, lakini yahitaji damu.



Unapoweka agano hilo unaweza ukasafiri kimwili kwenda mahali pengine mbali na hapo ulipo na kisha ukarejea.



Lakini pia unaweza ukaubadili mkufu kuwa lolote unalolitaka. Hata nyumba! Au mnyama yeyote vilevile." Zura akashangazwa haswa. Ni wazi mambo haya yalikuwa mapya na yenye kustaajabisha.

Alikosa sasa swali akabaki ameduwaa. "Ila Seth amejuaje yote haya?" Malkia akauliza. "Aliniambia babaye alikuwa akimfunda kuhusu historia kwa muda mrefu sana," akajibu Zura. "Alikuwa akisafiri naye kwenda mahala mbalimbali, akimfundisha lugha nyingi na kumsomesha vitabu vingi." "Baba yake alikuwa nani juu ya uso huu wa dunia mwenye uwezo huo?" Akastaajabu Malkia. "Alikuwa mtaalamu mkufunzi wa historia za kale, akiwa mshauri wa pili wa himaya ya Sedon ipatikanayo mbali mno na hapa." "Ilikuaje akafikia kwenye himaya ya wanyang'anyi?" "Alikuwa safarini yeye na baba yake kwenda himaya fulani ambapo baba yake aliitwa. Wakavamiwa na kukwapuliwa kila kitu.



Baba yake akauawa, ila yeye akabakizwa hai na kuletwa kwa Kuhani."





Walipomaliza kukata kiu za taarifa, Zura sasa akaaga akimwacha Malkia peke yake.



Malkia akaenda kuoga na kujiweka safi kabla hajaketi na kuanza kula chakula chake cha asubuhi.

Alikula akitafakari, na ungeweza kuliona hilo usoni mwake. Kuna jambo alikuwa alitafutia ufumbuzi, na aliendelea kulijadili hata alipomaliza kula na kujilaza kitandani akitazama dari.



Baada ya masaa mawili Zura akarejea kutazama kama Malkia amemaliza kula. Akakuta hola! Malkia hakuwepo.



Alitafuta kila kona ya chumba. Alipoenda dirishani akaona kisu chini. Alikinyayua akakitazama. Kisu kilikuwa kina damu!



Akajikuta ameachama. "Malkiaa!" Akapaza sauti akikunja ndita.

.

.

.

.

.

Farasi walishaandaliwa kwa ajili ya safari. Wanaume wakiongozwa na Bonas walikuwa wamesimama kando ya farasi hao wakimngojea Rhoda atoke ndani ya jengo wapate kuanza safari ya kurudi Goshen.



Ilikuwa ni majira ya asubuhi ya unyevu unyevu. Upepo ulikuwa unapuliza kwa nadra na jua liligoma kutoka kabisa kusalimia uso wa ulimwengu.



Bonas alitazama juu ya jengo, kati na chini, hakumuona Rhoda wala Venin. Shaka likaanza kujengeka ndani yake.



Mbona hatoki?



Alitaka kwenda ndani ila miguu ikagoma. Acha ajipe muda kwanza. Akaendelea kungoja. Alisema moyoni kama zikikatiza dakika kadhaa, basi atakata shauri na kwenda.



Pengine Rhoda amepata shida na anahitaji msaada, akili yake ilimwambia hivyo. Japokuwa alifahamu fika hawezi kupambana na Venin, ila angalau atakuwa amefanya jambo na si kukaa tu.



Aliendelea kungoja na kungoja. Akawatuma walinzi wazunguke nyuma ya jengo kutazama kama watamuona Rhoda, wakatii na baada ya muda mfupi wakarejea. "Hayupo!" Walifikisha habari.



Bonas akaamua kuzama ndani. Alitazama sebuleni asione jambo. Ghafla, akasikia mkono mkubwa begani mwake. Alishtuka akatazama. "Yagh namivezi vendredi?"sauti nzito iliuliza.

Alikuwa ni mwanaume mrefu mpana mwenye ngozi ngumu kama ya mamba. Rangi yake ilikuwa ya njano. Hakuwa amevaa shati bali bukta fupi nyeusi.



Macho yake yalikuwa mekundu. Nywele moja. Mdomo mpana na macho makubwa mekundu huku pua ikibakia matundu tu!





Alikuwa amemuuliza Bonas nani aliyemruhusu kuingia ndani.



Bonas akatabasamu kwanza. Haki alikuwa anafikiria cha kujibu. "Njhene fu sikkingh me ramshen," akasema. Yani anamtafuta mwenzake.



Kabla hajaulizwa swali lingine, wakasikia sauti ya vishindo vya miguu na maongezi. Wakatazama juu ngazini.

Wakamuona Venin akiwa anashuka na Rhoda wakishikana mikono na kupeana matabasamu.

Punde Venin akarusha macho yake kwa Bonas na mwanaume aliyekuwa pembeni yake. Akatoa ishara ya kichwa, mwanaume yule wa ajabu akaenda zake pasipo kusema jambo.



Venin na Rhoda wakashuka ngazi taratibu, bado wakiteta na kushikana mikono. Walipofika kwenye mwisho wa ngazi wakageukiana na kutazamana. "Sina hofu, najua kila kitaenda sawa," Rhoda alisema kwa tabasamu pomoni.



Venin akashusha pumzi ndefu. "Nitajitahidi kadiri ya nguvu zangu," alisema, kisha akaongezea: "Najua penye nia pana njia." Wote wakatabasamu. Wakakumbatiana na kupeana mabusu ya mashavuni. "Tutaonana hivi karibuni," Venin akanong'oneza. Macho yake yalikuwa yamelegea, uso wake mweupe ukimshuka kwa hisia.



Rhoda akajibu kwa tabasamu kabla hajashusha mguu wake akiwa amenyanyua gauni lake refu na kumuendea Bonas. "Tuondoke!" Akamnong'oneza Bonas huku akichanganyia mwendo. Alikwea ndani ya kijumba cha farasi wakaanza safari ya kuitafuta Goshen.





Safari ambayo ingechukua siku kadhaa kuitimiza. Kama vile tatu, nne ama tano kabisa. Inategemea na nini wanachokumbana nacho njiani.



Walipoacha jengo la Venin kwa mbali, Rhoda akapaza sauti akiamrisha farasi wasimame. Haraka akashuka na kwenda mbali kidogo.



Akaanza kutapika haswa!



Wanaume wakastaajabu. Mwanamke huyu alikuwa amatapika kama ugomvi ama mashindano. Atakuwa amekula nini? Walijiuliza.



Rhoda akatapika mpaka alipomaliza. Alipewa maji akasukutua mdomo kisha akasimama apate hewa huku akiwa anahema kwanguvu. "Ni nini maam?" Akauliza Bonas. Alimjongea Rhoda karibu akiwa ameweka mikono yake kiunoni.



Rhoda akavuta kwanza hewa ya kumtosha kabla hajaanza kunena. "Harufu!" Alisema akikunja uso. "Harufu imefanyaje?" Bonas akauliza. "Harufu ya Venin!" Rhoda akalipuka. "Yani mzoga si mzoga, maiti si maiti, mfu si mfu!" "Maam, mbona nilikuwa nakuona watabasamu? Hata mkakumbatiana na kupeana mabusu!" Rhoda akatikisa kichwa akibinua mdomo. Alimtazama Bonas kwa macho ya kilevi, akamshika bega. "Bonas, lazima ujue kula na vipofu. Ukitaka ufanikiwe maishani, ujue kula na vipofu. Usimshike mkono!" "Hakika wewe ni bingwa wa kuigiza!" Bonas akacheka. Rhoda alipotaka kuangua cheko tumbo likagoma. Lilikuwa tupu. Alitapika vyote.



Akaomba chakula upesi. Akafakamia matonge matatu makubwa kisha sasa ndiyo akacheka akiketi.





"Mpumbavu sana yule! Bonas, bora ukanyimwa kila kitu na Mungu ila si akili. Usipokuwa na akili, vyote ni bure! - uchawi, pesa, madaraka." "Kwanini wasema hivyo, maam?" "Kwasababu nimeshuhudia namna gani akili inavyozidi nguvu. Tena nguvu kubwa zisizo mithili." Kabla hajaendelea, akatia tena tonge mdomoni. Akiwa anatafuna akamuona mtu kwa mbali ndani ya msitu.



Akashtuka nusura amwage chakula.



Upesi, Bonas akaangaza, kweli akamuona mtu. Ila alikuwa tayari amekufa. Alikuwa ananing'inia akishikiliwa na kamba. "Ameshakufa yule!" Bonas alisema pasi na hofu. Rhoda akasimama haraka. "Tuondoke!" Akaagiza. Alikwea ndani ya kitoroli cha farasi na kufunga mlango kabisa. -- Huku nyuma, Venin hakubakia na amani hata punje. Tabasamu lake lilipotea mara tu Rhoda alipoyoyoma.



Aliachiwa mzigo mkubwa wa kuutatua. Aliachiwa mtihani uliomla akili pasipo majibu. Alijiuliza ni namna gani anaweza akasogeza mlima mbele yake, akakosa majibu.



Aliagiza damu ya kondoo, akaletewa glasini. Akanywa taratibu akiendelea kuzurisha akili.



Pale moyo wake ulipomwambia akome na mpango wake kwa Rhoda, picha ya mwanamke huyo mrembo ikakatiza kichwani kwake na kuua hilo wazo.



Hakutaka kumpoteza Rhoda kabisa. Ni mwanamke mzuri ambaye hajawahi kumuona maisha yake yote.



Labda ni kwasababu hakuwa anazunguka na huko duniani mara kwa mara, ila la hasha! Hata kama angezunguka huko, basi Rhoda angekuwa ni miongoni mwa wanawake wazuri tu ambao angewaona.





Alimuhitaji zaidi hivyo akakata shauri kusimama upande wake. Alimaliza kunywa damu glasini akajilamba, kisha akanyanyuka na kwenda chumbani.



Alivaa joho jeusi pamoja na kofia kubwa pana yenye pembe ndefu. Alishusha mapazia meusi ndani kukawa giza kana kwamba usiku wa manane.



Akawasha mishumaa mitatu tu, tena iliyokuwa kwenye kona.

Mwanga ulikuwa hafifu sana kwasababu chumba kilikuwa kikubwa. Ila Venin hakuhangaika na giza hilo, alikuwa anaona tu barabara.



Ni kama vile bundi ndani ya giza kubwa la msitu.



Alisogelea kioo kikubwa kilichomo ndani ya chumba chake, akakipaka unga mweupe kisha akatamka maneno kadhaa mageni.



Baada ya muda kioo kikaanza kutetemeka. Kiliruruma kwa sekunde kadhaa kisha kikakoma. Venin akarudia tena kutamka maneno akiongeza sauti.



Kioo kikaanza tena kururuma, mara hii kilichukua muda mrefu, ila kikaacha.



Venin hakukoma, akarudia tena maneno yake ya kigeni. Sauti ilikuwa kubwa kuliko ya mwanzoni, na hata ile ya pili.



Kioo kikaruruma kwanguvu. Kikapiga nyufa kubwa kikitoa sauti. Bado kidogo kivunjike chote mpaka pale taswira ya mtu ilipoonekana.



Alikuwa ni mwanaume yule aliyeonekana ile siku, juzi. Alikuwa ni mwanaume afananaye na Venin. Alikuwa ni kaka yake wa damu! "Unasemaje Venin?" Taswira ikauliza. "Ni nini unataka kuniambia saa hii?" Venin akashusha kwanza pumzi. Macho yake yalijawa na uoga. Mdomo ulikuwa mzito kufunguka. "Kuna shida?" Taswira ikauliza tena. "Ndio!" Akajibi Venin akijaribu kujiamini.





"Kuna jambo limetokea, kaka." "Lipi hilo?" "Ni mabadiliko tu ya mipango." Taswira ikaguna kisha ikanyamaza. Ilimwachia uwanja Venin apate kunena na kuteta. "Naomba usiwaue wale watu niliokuambia watakuja huko Tanashe," alisema Venin kisha akakaa kimya kusikiliza. Kukawa kimya kwa sekunde. Hamna mtu aliyeongea.



Venin akateka tena zamu. "Najua nitakua nimekukwaza sana, ila kama mdogo wako, naomba unisamehe sana kwa hilo. Nitatafuta njia nyingine ya kukutoa huko. Naomba unipatie muda." Taswira ikatabasamu. Mara ikaanza kuangua kicheko. Kicheko kikakua na kukua, sasa kikawa kinaumiza masikio!



Venin alijua fika kicheko hicho si cha shwari bali shari. Alikunja sura yake akiminya lips. Alikuwa anangojea neno toka kwa kaka yake.



Ila kabla taswira haijaanza kuongea, kioo kikaanza kupiga na kuongeza nyufa kwa kasi! Mwishowe kikaanza kumegeka kwa vipande kuangukia chini.



"Venin!" Taswira ikaita kwanguvu."Siku nitakayokutia mikononi mwangu, nitakuvunjavunja vipande! Vipande vipande!"



Kioo kikamalizika kupasuka chote. Hakikubakia hata kipande moja. Venin alijifunika uso wake usidhurike. Alipokuja kutazama akasikia sauti kwa mbali ikiyoyoma: "Nitawamaliza hao watu wako. Nitakumaliza na wewe!" Kisha sauti ikakoma.



Venin akatikisa kichwa akitazama chini. Akatoka ndani ya chumba na kwenda nje kibarazani alipoketi na kuanza kuwaza.





Sasa atakuwa amefanya nini kama watu hao wakimalizwa na kaka yake huko Tanashe? Endapo kama wakimalizwa ina maana atakuwa amempoteza Rhoda, si ndio!



Sasa afanye nini kuepusha hicho kikombe?



Alijua fika kaka yake anahitaji kunywa damu nyingi za binadamu ili awe na nguvu na kutoka ndani ya Tanashe. Na alijua pia, kinga aliyowapa wakina Rhoda haiwezi kuwasaidia kuwakinga dhidi ya kaka yake.



Sasa? Alihisi kuchanganyikiwa!



Aliona anazidi kupandikiza chuki aliyoijenga kwa kaka yake tangu muda mrefu. Chuki iliyodumu kwa miaka saba sasa.



Chuki ya kuwa kiungo kikuu kwa kaka yake kutupiwa ndani ya Tanashe baada ya makosa yake kumfanya atiwe nguvuni na wananchi waliokuwa na hasira kali baada ya kaka yake kuua watoto wao takribani hamsini na kuwanywa damu!



Siku hiyo hataisahau maishani. Kwani si tu kwamba ni siku iliyompa majuto, bali ni siku iliyobadili kabisa maisha yake na kumpa upweke mkuu.



Upweke uliomtesa sana.



Aliishi kwa roho ya manung'uniko na majonzi tele. Aliishi akijiuliza kila siku kwanini alipasua pazia lile kuu lililopo sebuleni.



Japo ni kwa bahati mbaya, liliruhusu mwanga mkali wa jua na kumpiga kaka yake aliyeshindwa kuhimili. Akadondoka chini na kuungua.



Akapoteza fahamu na nguvu. Akaokotwa na wananchi waliomtia ndani ya kitoroli cha chuma na kwenda kumwagia ndani ya Tanashe.



Hakutoka tena tangu siku hiyo! .

.



Siku haikuwa imeisha. Na kwa Karim ilikuwa ndefu mno. Alichoka kuishi ndani ya lupango. Alichoka kuishi kama mbuzi ndani ya zizi ilhali ana madaraka na maisha mazuri.



Alitamani kuona jua na kuendelea kufanya ulozi wake. Alitamani angekuwa ndani ya nyumba yake kubwa akibarizi kwa kutembea huku na huko.



Pia akiwa anakula na kunywa anachotaka.



Kweli nyimwa vyote ila si uhuru, aliamini. Urafiki aliounda na vyuma vya lupango hakuwa anaupenda na siku atakapouvunja, kwake itakuwa ni tafrija.



Ila alikuwa na kinyongo rohoni. Alikuwa na kinyongo dhidi ya Sultan. Kinyongo dhidi ya Askari. Japokuwa aliwaza kwa muda mrefu ni nini atawafanya akitoka, hakika alikosa jibu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ni Mungu pekee ndiye alijua ni kwa namna gani atakawashikisha adabu.



Kwa siku hii nzima mpaka sasa ni jioni, alikuwa akisikia tu kishindo cha miguu ananyanyuka na kuangaza. Pengine anaweza akawa kijakazi wake amekuja kumkomboa.



Hali hii ikamfanya kila saa akae karibu na vyuma vya lupango. Kila saa achomoze kichwa kuangaza.



Japokuwa alifanya hivyo, haikumsaidia. Kwani kijakazi bado hakufika. Siku nzima alikuwa yu njiani akija. Akitembea na kukimbia na farasi wake pasipo kupumzika.



Jua likiwa linaelekea kupotea, giza kuu linameza lupango baada ya kusaidiwa na giza la mchana mzima, ndipo kijakazi wa Karim anafika Kasrini.





Hakika alikuwa amechoka mno kwa safari za kwenda na kurudi pasipo kupumzika. Alikuwa amebebelea kikapu cha ukubwa wa kati ndani yake tusijue ameweka nini.



Alishuka akamsalimu mlinzi na kuomba aingie ndani. "Wewe si umetoka hapa jana, na leo nini wafuata?" Akauliza mlinzi wa getini. Macho yake yalikuwa makubwa na makali. Alikuwa mfupi kwa umbo ndani ya sare. "Nimemletea mkuu wangu shuka apate kujifunika ajikinge na baridi. Pia nimemletea baadhi ya mahitaji aliyoyaomba.



Sidhani kama lina ubaya?" Mlinzi akamtazama kijakazi kwa uso wa mashaka. Akampekua farasi wake na yeye pia kisha akamruhusu aingie ndani. "Nadhani unajua pa kwenda," akasema Mlinzi akifunga geti. Kijakazi akajiuma. "Samahani, nitamkutia wapi msimamizi maana sik..." "Nenda huko huko we kamtafute!" Mlinzi akafoka. Kijakazi asirudie tena kuuliza akamwacha farasi wake getini na kuelekea gerezani.



Mkononi akiwa na kikapu chake akaangaza kumtafuta msimamizi wa gereza. Wakati anahangaika kumbe msimamizi huyo alikuwa amamtazama.



Alikuwa ametulia gizani akivuta zake tumbaku na kutoa moshi kana kwamba chombo cha moto.



Kijakazi alipokaribia gerezani, akapaza sauti kumuita na kumuamrisha amfuate. "Habari ya siku?" Kijakazi akasalimia. "Kumbe ni wewe!" Askari akafoka. "Ndio, ni mimi." "Unafuata nini tena hapa?"





"Kuna vitu vichache nime..." "Hivi, unadhani huyo mkuu wako yupo nyumbani kwake hapa enh?"



"Hapana, si hivyo, Askari..."



"Unamuita nani Askari wewe kijakazi?" Kimya. Askari akatoka gizani na kumjongea Kijakazi.



"Una madaraka gani ya kuniita Askari wewe?" Akauliza akimtazama Kijakazi usoni. Kijakazi akatazama chini kwa uso wa pole.



"Si nakuuliza wewe? Hivi unajua madaraka yangu hapa? Au kwakuwa unanikuta tu hapa gerezani unadhani tupo sawa?" Bado kijakazi hakujibu. Alitazama chini. Askari akafyonza tumbaku yake na kumtemea moshi usoni.



Kijakazi akakohoa mara tatu kabla hajalalama: "Nisamehe mkuu. Sina tatizo na yeyote, nimekuja tu kumletea baadhi ya vitu mkuu wangu. Aliniagiza."



"Vitu gani hivyo? Umemletea ndumba?" Akauliza Askari kisha akaangua kicheko kikavu.



"Hapana, sijaleta hivyo vitu," akajitetea Kijakazi.



"Mkuu alilalama anang'atwa sana na mbu na wadudu wengine. Akaniagiza nimletee angalau shuka."



"Shuka tu? Na mbona kikapu kimejaa?" "Haya mengine ni chakula tu na kinywaji, pia dawa maana anaumwa."



"Embu lete!" Askari akakwapua kikapu na kuanza kukipekua kwa kutupia vitu nje. Kulikuwa kuna shuka jepesi rangi ya kijivu, makopo mawili ya bati pamoja na vifungashio vitatu.



"Nini hivi?" Askari aliuliza akinusa vikopo.



"Dawa, mkuu."



"Dawa gani?" "Ya mapafu. Mkuu alinambia anapata shida kuhema, haswa nyakati za usiku pindi baridi inaposhika."





Askari akanusanusa vikopo hivyo vyote, harufu yake haikumvutia. Akafungua vifungashio na kuvipekua. Kulikuwa kuna viazi vikavu, akachukua vitatu na kuvibugia vyote kwa pamoja, pasipo ruhusa. "Haya nenda!" Akasema akitafuna. Mdomo wake ulikuwa umejaa mashavu yakiumuka.



Kijakazi akaokota vitu vyake vilivyomwaga chini akavirejesha kwenye kapu. "Nashukuru sana, mkuu," akasema akiinamisha kichwa chake chini. "Si unajua huo mzoga wako ulipo?" Askari akauliza. Bado alikuwa anatafuna. Kijakazi akamuitikia: "Ndio, mkuu." "Haya, potea!" Kijakazi akaenda akiwa amekumbatia kikapu chake. Tabasamu lilimjaa usoni baada ya kuona ametimiza adhma.



Alitembea kwa haraka asije akasikia ameitwa. Alishika njia ya gereza akaenda kusimama mbele ya lupango, alipopaza sauti yake kuita.



Haraka Karim akasimama na kwenda kukutana naye. Wote walijikuta wana matabasamu mapana yenye matumaini tele. "Umefanikisha?" Karim akauliza kwa kunong'ona. "Ndio, mkuu. Nimefanikisha!" Akajibu Kijakazi akipekua kikapu chake.



Akatoa shuka na kumkabidhi Karim. Akatoa na vile vikopo pia akamkabidhi. Baada ya hapo akapandisha kanzu yake akatoa pakti fulani kwenye nyonga, akaikabidhi. "Bila shaka vimetimia, mkuu." Kulikuwa ni giza. Karim alikuwa anatumia mikono yake kutambua na kupembua. Mwanga mdogo uliokuwa unaingia kwa kupitia dirisha dogo lililopo juu kabisa, haukuwa wa kutosha.





"Vimetimia," sauti ya Karim ikasikika toka gizani, ikafuatiwa na kicheko.



"Vimetimia kabisa! Kabisa!" Akasisitizia Karim. Kisha akaangua kicheko cha haja.



"Sasa wewe nenda," akasema. "Sitaki kukuingiza matatizoni. Kazi yako imeshakwisha, pole sana. Nenda maana zawadi inakuja.



Nenda nitakukuta njiani." Kijakazi akainamisha kichwa chake kisha akaaga na kwenda.



Karim akasogelea mwanga mdogo unaingia kwenye dirisha akaweka vitu vyake chini. Akaketi kwa mtindo wa kusonga miguu kisha akafumba macho.



Kwa muda wa dakika tatu akawa anateta kwa lugha isiyojulikana ni ya himaya gani. Alipomaliza akafungua kopo moja, akatia vidole vyake viwili humo ndani na kutoa mafuta fulani mazito.



Akayapaka mikononi.



Akafungua kopo lingine, akatia vidole viwili na kuchota kilichomo, akapaka miguuni. Akafungua kingine cha mwisho, akachota pia kisha akapaka usoni.



Akaendelea na ibada yake hiyo huku nje msimamizi akiwa hana hili wala lile. Alikuwa anaendelea tu kuchoma mapafu kwa tumbaku zake zisizo na kikomo.



Alikuwa anazunguka huku na kule akipiga miluzi na kukobeka kitako cha tumbaku mdomoni kisha akifyonza.



Akiwa anawasha tumbaku mpya aendelee kujipa raha ya kukaribisha kifo kwa kansa ya mapafu, akasikia kishindo toka gerezani. Akatahamaki: "Nini hiko?" Macho yalimtoka. Alitoa jambia lake kwenye nyonga akalishikilia mkononi, kisha upesi akakimbilia gerezani kujua kinachoendelea.





Akatazama kila lupango, palikuwa sawa. Alipofika kwenye lupango la Karim, akakuta mlango umenyofolewa na kuwekwa pembeni.



Macho yakamtoka zaidi!



Akamulika ndani ya lupango, hakumkuta mtu zaidi ya mabaki ya makopo na vifungashio.



Karim alikuwa ametoroka! Ukweli huu ukatoboa moyo wake.

Upesi akanyanyua filimbi apulize kutoa tahadhari kwa Askari wenzake. Ila kabla filimbi haijafika mdomoni, akastaajabu mkono wake umekamatwa.



Kutazama, akamuona Karim. Macho yake yalikuwa mekundu yanayowaka kama moto. Uso wake ulikuwa unametameta kama umesakafiwa na nyota.



Askari akastaajabu sana kwa hofu.



Baada ya dakika mbili tu akawa ametundikwa juu ya mstimu mrefu hapo kasrini. Alikuwa tayari mfu, anamimina damu vibaya mno.

.

.

.

.

.

. *** .

.

.

.

.

.

"Ulikuwa wapi?" Aliuliza Zura punde tu baada ya Malkia kurejea chumbani. Mwanamke huyu hakutoka ndani ya hicho chumba tangu pale alipomkosa Malkia majira ya asubuhi.



Malkia hakuwa anajua kama Zura alikuwamo ndani. Alikuwa amedhamiria kurejea kwa siri, na alifanya hivyo baada ya kuhakikisha mazingira ni salama.



Kumbe Zura alikuwa amejikobeka kwenye kona ya mbali ya chumba. Na ndani kulikuwa giza hivyo hakuweza kumuona kiurahisi.



Alipotokeza tu, Zura naye akajichomoza akinena. "Oofh! Zura!" Malkia akastaajabu. Alijiona mjinga baada ya mchezo wake kutofaulu.





"Nilikuwa nimetoka kidogo kwenda kutembea," akajibaraguza.



"Umetoka Goshen, Malkia. Huwezi ukajikata mkono wako kwa sababu ya kwenda kutembea."



Malkia akaminya lips zake. Akaketi kitandani. Zura akawasha taa na kumjongea karibu.



"Kwanini umeamua kwenda pasipo kuniambia? Ni nini ulifuata huko?"



"Nilikuwa nimepakumbuka. Niliona haja ya kupaona. Kule ni nyumbani. Sikuweza kuhimili hitaji langu tena moyoni."



"Malkia, ni hatari! Vipi kama ukionekana huko? Vipi kama ungekumbwa na jambo lolote huko ilhali ulikuwa mwenyewe?"



"Isingeweza kutokea. Hamna mtu anayeweza kunidhuru. Hakuna mtu anayeweza kuniona nikiwa katika hii hali. Usijali sana, Zura!" Akasema Malkia kisha akasimama na kuanza kuvua nguo.



"Naenda kuoga, naomba uniletee chakula maana nina njaa sana." Zura akasimama na kuondoka kutimiza agizo. Ila hakuwa na furaha, hakupendezwa na namna Malkia alivyofanya.



Aliona ni hatari, na kweli ilikuwa hatari.

Pasipo kujua, Malkia akiwa huko Goshen anazunguka, mwanajeshi mmoja alimuona vema na sasa alikuwa njiani kwenda kwa mfalme kumtonya habari hizo.



Alimuona Malkia karibu na makazi ya zamani ya Zura. Japokuwa alikuwa amejifunika, alikuwa mwerevu kumtambua. Na akili yake ilisimama kidete kumwambia yupo sahihi.



Akafika kwa mfalme Phares na kupiga goti moja akiinamisha kichwa. Mfalme akamuuliza; "Kuna nini?"



"Nimemwona Malkia Sandarus!" Akasema mwanajeshi.



"Umemwona wapi?" Phares, mfalme, akauliza akisimama. .

.

.



"Nimemwona huko kusini karibu mwa himaya yako. Kwenye ile nyumba aliyokuwa anaishi Zura, mwanamke aliyemlelea na kumkuza!"

.

.

"Lakini una uhakika na si mawenge?" "Haki mfalme wangu, macho yangu yamemwona na kumtambua kabisa!" Punde likatumwa jeshi kwenda kumtafuta Malkia huko iliposemekana. Jeshi la wanaume sita na farasi zao wakafanya msako wa udi na uvumba, ila hawakutoka na jambo.

.

.

Hawakumuona Malkia kabisa ingali walimtafuta kwa masaa. Waljirejesha kwenye himaya ya mfalme, wakamtaarifu mfalme Phares. "Tumezunguka kote ewe mfalme, ila hakuna tulilopata!"

.

.

"Mmeuliza hata watu wanaoishi huko?" Mfalme akauliza. "Ndio, mfalme. Tuliuliza wote. Hakuna aliyemuona!" Mfalme Phares akashusha pumzi akishika kiuno. Alikosa cha kunena kwa muda.

.

.

"Mfalme, je tukamlete yule aliyekuongopea?" "La hasha! Mnaweza mkaenda." Wanajeshi wakaenda. Phares akabakia akiwaza na kuwazua. Alijiendea zake chumbani lakini bado akiwa ametingwa na mawazo.



Kutakuwa kuna namna! Alijisemea. Hii ni mara ya pili sasa anakumbana na hili jambo. Mara ya kwanza akiwa kwenye uwanja wa vita wakijiandaa, na mara ya pili hii sasa.



Ina maana yote hii ni mizengwe? Hapana!



Kuna mchezo gani hapa unaendelea? Huyu Malkia yupo wapi? Alitaka kujua zaidi. Aliadhimia kufanya jambo apate majibu ya maswali yake haya.





Akaona ni busara akimngojea Rhoda wapate kujadiliana. Pengine anaweza kumshauri kitu ukizingatia hana washauri wa karibu.



Alijituliza kabla ya muda kidogo hajatoka kwenda kupata chakula cha jioni. Aliandaliwa chakula kizuri na kingi na wajakazi wake.



Akiwa anakula, mwenyewe kwenye meza kubwa, mara anakuja kijakazi wake na kumwambia: "Mfalme una ugeni!" Akastaajabu. Alijaribu kufikirisha akili yake kama ana miadi, lah! Hakuwa nayo. Akauliza: "Ugeni wa nani?" "Wa mzee wa baraza!" Akajibiwa na kijakazi. Akatoa ishara ya kichwa kuruhusu ugeni huo.



Kijakazi akaenda na punde akarejea akiongozana na mzee wa baraza. Mzee huyu alikuwa ni mmojawapo wa waliomuunga mkono, ila baada ya kupewa presha na Rhoda.



Alikuwa amevalia joho refu rangi ya kahawia lenye kola ndefu lililosimama na kuziba kisogo chake.



Pembezoni mwa joho hilo kulikuwa kumedariziwa na nyuzi za madini ya silva. Joho lilikuwa la thamani, ila pia lililoonyesha hadhi yake ndani ya himaya kama mzee wa baraza.



Miongoni mwa watu wenye ushawishi wa maamuzi himayani. "Karibu." Phares alimkaribisha mzee. Mzee akainama kutoa heshima kwa mfalme.

.

.

"Nimekaribia mfalme," akasema kisha kuketi. "Umekuja na baraka za chakula. Karibu ule."

.

.

"Nimefurahi sana kukuta unakula. Huwa tunaamini mgeni amkutaye mwenyeji anakula, basi ameleta baraka." Mfalme Phares akatabasamu.





"Bila shaka utakuwa umekuja na falsafa ya mgeni njoo, mwenyeji apone." Mzee wa baraza akatanasamu akiyafinyanga mashavu yake yaliyokula chumvi za kutosha.

.

.

"Wala hujakosea mfalme, upo sahihi kabisa." Mfalme Phares akamminia kinywaji kwenye kombe, akamsogezea.

.

.

"Sikutarajia ugeni wako. Unastahili mapokezi zaidi ya haya."

.

.

"Usijali. Usihangaike na mzee anayeenda kufa hivi karibuni, mfalme wangu. Raha yangu ni kukuona ukiwa hai, na furaha pia."

.

.

"Nashukuru sana."

.

.

"Wa kushukuru ni mimi mfalme. Niliyetoka huko mbali kuja kukuhudumia mfalme wangu kwa kukupatia sababu ya kufurahi." Mfalme Phares akanywa kwanza mvinyo mafundo mawili kabla hajauliza;

.

.

"Sababu gani hiyo mzee wangu?" Uso wake ulishikwa na hamu ya kutaka kujua. Na yule mzee akiwa amelijua hilo, akanyanyua kombe la mvinyo na kugida huku mfalme Phares akingoja mzee amalize na kukata kiu yake.

.

.

"Huna haja ya kuwa na papara mfalme, nipo hapa kwa ajili yako," mzee akasema na kisha akatabasamu.

.

.

"Mfalme, utanisamehe kama nitakuwa nimekukwaza, ila inabidi ujue lengo langu ni kukufanya uwe na furaha." "Usijali. Karibu, waweza ukanieleza."

.

.

"Ni kwa muda sasa nimekuona ukiwa mpweke. Umekuwa ukiishi ndani ya jengo hili kuubwa mwenyewe ukizingirwa na wanajeshi, ama vijakazi.



Mfalme wangu, huoni kama ni wasaa wako sasa wa kuwapa wananchi wa Goshen malkia?"





Mfalme Phares akatabasamu. Hakujibu kwa haraka, akanywa kwanza mvinyo wake na kisha kuketisha kichwa chake juu ya tama akimtazama mzee wa baraza.

.

.

"Ni haramu kwa himaya yetu mfalme kutokuwa na malkia maana kasri itageuzwa kuwa pango la wahuni. Tulifanya makosa kutokukueleza hilo mwanzoni, lawama ni juu yetu."

.

.

"Usijali, mzee wangu," akasema mfalme. "Nitalifanyia kazi hilo uliloniambia." Mzee akatabasamu na kuinamisha kichwa chake kuonyesha ishara ya heshima.

.

.

"Sasa naweza nikaenda kwenye jambo langu la pili."

.

.

"Una lingine?"

.

.

"Ndio, mfalme. Siku zote unapoonyeshea tatizo, ni lazima pia uonyeshe suluhisho," akasema mzee kwa kujiamini kisha akapiga makofi mawili.



Punde wakatokea mabinti watatu warembo, wakaenda kusimama mbele ya meza ya mfalme.



Binti mmoja alikuwa mrefu kuliko wote, nywele ndefu nyeusi akivalia gauni rangi ya buluu iliyochoka. Uso wake ulikuwa mwembamba uliochongoka, kidevu chake kama ncha ya mkuki.



Mwingine wa pili alikuwa saizi ya wastani. Nywele zake zilikuwa ndefu nyeupe. Uso wake ulikuwa mfupi wenye mashavu na lips ndogo rangi ya pinki.



Alikuwa amevalia gauni jeupe, refu lililofunika miguu.

Wa tatu na wa mwisho alikuwa analingana kimo na wa pili, ila yeye mwili wake ulikuwa mwembamba zaidi. Shingo yake ndefu ilikuwa imepokelewa na mifupa.



Uso wake pia ulikuwa mwembamba wenye kidevu cha duara. Lips zake zilikuwa nyembamba zilizojichanua. Rangi nyeusi.





Wote waliinamisha vichwa vyao kumsalimu mfalme. Ila hakuna aliyediriki kuinua macho yake kumtazama. Wote walikuwa wanatazama chini kwa soni. "Mfalme wangu, hawa unaowaona hapa ni mabinti toka familia bora za wafanyabiashara waliojiwekeza na kulipa kodi serikalini.



Wana tabia njema na wanavuma kwa uzuri wao. Basi kwa macho yangu yaliyoona mengi nikaona pengine hapa kuna malkia wetu.



Pengine kuna atakayevutia macho na moyo wako mfalme, ukamfanya awe mama wa himaya." Mfalme alinyamaza kimya akiwatazama mabinti hao. Macho yake yalitembea kuwakagua, kushoto na kulia.



Ila yalikwama kwa binti mwenye nywele nyeupe. Alimvutia. Alitazama namna binti huyo anavyong'ata lips zake za pinki akitazama chini.



Namna anavyofinyanga vidole vyake kwa aibu. Akahisi moyo wake unapooza. Mzee wa baraza akaling'amua hilo, akajikuta ametabasamu.

Akauliza kwa sauti ya chini: "Vipi, je umempenda huyo?" Akaonyeshea kwa kichwa chake binti amuongeleaye.



Mfalme akahofia kutoa jibu la wepesi. Akasafisha koo lake akijilaza kwenye kiti. "Usiumize kichwa mfalme wangu. Ujio wangu huu ulikuwa wa kushtukiza. Ningependa kukupa muda wa kufikiri," akasema mzee wa baraza kisha akapiga tena makofi mawili, mabinti wakaondoka.

.

.

"Yule ni binti wa Melkizedeki, mfanyabiashara mkubwa wa chuma himayani. Anaitwa Tattiana. Ni mtaalamu wa mahesabu kama baba yake.



Ni mwerevu sana na mjuzi wa biashara pia."





"Nashukuru sana, mzee. Ningeomba unipe muda wa kufanya maamuzi kabla sijajitutumua kuchagua jambo." Mzee akasimama.

.

.

"Pasipo na shaka lolote, mfalme wangu. Kama nilivyosema hapo awali, ujio wangu ulikuwa wa ghafla. Naomba msamaha kwa usumbufu, lakini pia nikupe chumba upate kufikiria." Mzee akaaga na kumwacha mfalme Phares akibakiwa na mawazo zaidi. Sasa si tu juu ya taswira za Malkia Sandarus kwenye himaya yake, bali pia mwanamke wa kuoa.



Hakuwa na mawazo hayo ya mwanamke, ila sasa akawa amelewa kwa kuchambua.



Kitu kilichomfanya awe njia panda ni Rhoda. Aliwaza na kuwazua kama mwanamke huyo atakuwa tayari kuwa naye.

.

.

Lakini pia alihofia kujiingiza kichwa kichwa kwa mwanamke aliyeletwa na mzee wa baraza. Mbali na maneno ya mzee huyo kumhusu huyo mwanamke, yeye mwenyewe alihitaji kumjua kwa undani.



Basi akaamua kumuita mwanajeshi wake mmoja na kumpa maagizo: "Kamfuatilie yule binti wa Melkizedeki aitwaye Tattiana. Nataka kujua kila jambo kumhusu." Mwanajeshi akabeba agizo hilo na kutokomea kwenda kulitekeleza.

.

.

.

.

.

****

.

.

.

.

.

Sauti ya miguu ya farasi ilisikika nje ya nyumba. Punde mlango ukafunguliwa, akatoka mwanamke, alikuwa mama Fluffy.



Alikuwa amevalia kiremba kikubwa kichwani na gauni rangi ya udongo.

Mbele yake aliona farasi wanne wakiwa wamebebelea wanaume wanne wenye majambia marefu, na mwanamke mmoja aliyevalia kimapambano.





Alimtazama vema mwanamke huyu, akagundua ni mwanaye. Moyo ukamlipuka!



Haraka akamkimbilia akamkumbatia na kumpatia mabusu kedekede. Macho yake yalishikwa na maji ya machozi.

Tabasamu lake lilikuwa pana kuonyesha namna moyo wake ulivyoguswa. "Mwanangu, nilijua umeshakufa!" akasema akibubujikwa na machozi.



Waliingia ndani wakaketi, mama akiwa na kimuhemuhe cha furaha.



Fluffy akamueleza mama yake yale yote yaliyotukia. Kila jambo akamuweka wazi. Hakika hayo yakamshangaza mamaye.

.

.

"Uliwezaje kufanya yote hayo pasipo kuniambia?" "Nisamehe mama. Kila muda na kila wakati nilikuwa nahitajika kutimiza majukumu. Hivi sasa hali ilivyotulia nikaona nije sasa kukwambia."

.

.

"Nimefurahi sana kukuona mwanangu. Nilikuwa na donda kubwa sana moyoni. Nilikuwa nashindwa kulala kila usiku kwasababu ya kukuwaza wewe.



Sikujua kama upo hai. Hata nilipotaka kuja kukufuatilia, tukazuiwa maana vita zilikuwa zinaendelea huko. Himaya baada ya himaya!" Fluffy akatabasamu na kumshika mamaye mkono. "Nipo hai mama. Bado nipo hai." Wakakumbatiana.

.

.

"Ngoja nikakupikie chakula kitamu unachokipenda, mwanangu. Bila shaka usiku huu utakuwa nami. Tuna mengi ya kuongea," mama akasema akielekea zake jikoni.



Baadae, usiku ukiwa umeshika , wakiwa pamoja wanakula, wakawa wanaongea. "Sikudhania kama kuna siku itakuja kutokea himaya za wanyang'anyi zikafa," alisema mama. "Zilikuwa ni himaya zenye nguvu, zenye kuogopeka. Japokuwa zilikuwa ni za wahalifu, na kila mtu alijua, hakuna aliyediriki kuchukua hatua.





Nimefurahi sana mwanangu kuwa miongoni mwa walioziua himaya hizo. Pia mgeni wangu kuwa shujaa na hatimaye kuwa Malkia. Naona nyumba yangu imebarikiwa."

.

.

"Sasa mama ndiyo ufanye twende huko. Kule ndiyo nyumbani kwetu sasa!" Mama akatabasamu.

.

.

"Hapana mwanangu, siwezi kwenda huko. Usijali mie kwa sasa ni mzee, sihitaji kuhaha huku na kule tena na maisha. Kifo kitapata shida kunitafuta na kunipata.



Wewe endelea na majukumu yako, ila uwe unakuja kunipa salamu mama yako.



Na vipi? Umeshapata mchumba wa kukuoa?" Fluffy akacheka. "Hapana mama!"

.

.

"Unakawia nini? Au mmeadhimia himaya yenu kuwa vikongwe mkiwa mabinti?" Walitaniana na kufurahi. Kesho yake asubuhi na mapema, Fluffy akadamka na kumuaga mama yake anarejea Sawaridi.

.

.

Mama akamkabidhi karatasi fulani chakavu yenye rangi ya bati lenye kutu.

Alimminyia karatasi hiyo kiganjani na kisha akaificha kwa kuvifunga vidole vya binti yake. "Nimeihifadhi kwa muda mrefu sana hiyo karatasi. Niliipata mbali sana kipindi nikiwa binti kama wewe. Ila sikupata wasaa wa kufuatilia yale yaliyopo ndani.



Hivi sasa ni mzee, sina tena nguvu hizo. Nakukabidhi wewe. Na nakusihi usije ukawa kama mimi. Usipuuzie kilichomo humo ndani.



Abadani!"

.

.

.

Ni majira ya mchana. Jua lawaka na kuna mawingu mepesi mepesi kwenye anga kavu la bluu.



Ndani ya jengo kubwa la bwana Al Karim kulikuwa tulivu sana. Vibaraka walikuwa wamesimama huku na huko, wengine wakitembea na kuranda kule na kule aidha wakiwa wamebebelea vitu ama basi mikono mitupu.



Vibaraka hawa walikuwa wamevalia sare nadhifu na nyuso zao zikiwa zimejazwa na umakini wa kazi.



Siku hiyo ilikuwa 'bize' sana kwao. Tangu asubuhi walikuwa wakifanya marekebisho ama matengenezo yaliyoelekezwa na mkubwa wao - bwana Karim.



Punde bwana huyo, Al Karim, alipofika na kuitia ngome yake machoni, akaridhia na moyo wake kuwa anahitaji kufanya mabadiliko kadhaa mazingirani.



Aliona eneo hilo kama limechoka ama limepwaya. Pengine kwakuwa alikuwa mbali nalo kwa siku kadhaa. Alitamani rangi ibadilishwe baadhi ya maeneo na hata maua yapandwe.



Ila yote hayo yasingewezekana kwa mkupuo. Ilikuwa ni kiu tu ya ghafla ndiyo ilikuwa inamkereketa. Hamu ya kutaka tu kuona mabadiliko mbele ya macho yake.



Kiuhalisia kuna jambo fulani lilikuwa linamkereketa nafsini, na huku kuhangaika kulikuwa ni kama vile mfa maji anavyotapatapa.

.

.

Alishika hili, akaliacha na kulidaka lile. Aliekeza hili, akaacha na kuelekeza lile. Mwishowe alijikuta ameacha kila kitu na kujifungia ndani ya chumba chake.



Akatoa agizo ulinzi uwe imara na basi punde litakapoonekana la kutiliwa mashaka basi upesi ahabarishwe.



Hivyo basi kwa muda huu alikuwa ndani wakati bado vibaraka kadhaa wakihaha kutimiza moja ama mbili ya maagizo yake ambayo pengine hata aliyeyatoa aliyasahau.





Alifukiza udi chumba kizima kisha akawasha mishumaa mitatu, miwili meusi na mmoja mweupe uliokaa katikati.



Akachukua kitabu kimoja chenye jalada gumu rangi ya zambarau akafungua mpaka kurasa mia moja na nne, kisha akaketi chini kwa mtindo wa kupakata miguu.



Alifanya hivyo akiwa tayari ameshashusha mapazia na kutengeneza giza feki kana kwamba usiku. Pia akiwa amesogeza glasi ya maji karibu kabisa na mapaja yake.



Ni mwanga wa mshumaa tu ndiyo ulikuwa unamulika ukiwa karibu kabisa na kurasa ya kitabu ambacho amekifungua.



Alipitisha macho yake kwenye kurasa aliyoifungua kisha akaikodolea kwa sekunde kadhaa. Kuanzia juu kwenda chini, kisha tena akirudia zoezi.



Alifanya hivyo kwa takribani mara tatu na kisha akakifunga kitabu.



Akazungusha mikono yake juu ya kichwa cha moto wa mishumaa kama dereva azungushaye usukani wa gari kubwa alafu akajipangusia masizi usoni.



Alilirudia zoezi hilo mara tatu. Akafunga macho na kuyatamka maneno yale aliyopata kuyasoma toka kwenye kile kitabu na kuyahifadhi kichwani.

.

.

"Sabakittan sikol-utah yuzhetu fir-kau-n. Fey ghogu ishi, dhunyat fir-kau-n!" Alitamka maneno hayo mara tano. Kwa mara ya kwanza sauti ilikuwa juu ya kupaza, ila kadiri alivyokuwa anarudia ndivyo sauti ikawa inapungua.



Mwishowe ilikuwa ya kunong'oneza kana kwamba anamtonya mtu aliyeketi pembeni.



Alipomaliza akaudondosha mshumaa mmoja chini. Ulikuwa mweusi wa upande wa kushoto toka ulipo ule mweupe, alafu akarudia tena maneno yake na matendo.





Akaudondosha mshumaa wa pili mweusi. Ukabakia mshumaa mmoja, ule mweupe wa katikati.



Hapo akanywa kwanza maji yake glasini kisha akarejelea zoezi lake kama ada. Akaudondosha mshumaa mweupe chini.



Punde tu ulipoanguka na kuzima ukatokea upepo mkali ndani ya chumba. Sauti ya mwanamke ililia, na mara ghafla ikacheka kwanguvu.



Joto lilizidi ndani ya chumba mithili ya jangwa wakati wa mchana. Ndani ya muda mfupi Karim akatokwa na jasho. Si bure aliandaa maji yake ya kunywa.



Kufumba na kufumbua, akatokea mtu kwenye kona!



Alikuwa amejikunyata akificha kichwa chake katikati ya magoti. Nguoze zilikuwa nyeupe pe na hivyo basi akawa mwepesi kutambulika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Karim asitahamaki, akasema maneno fulani tofauti na yale ya mwanzoni, kisha akanyanyuka na kumfuata yule kiumbe.

Akamshika mkono na kumnyanyua. Alikuwa dhoofu lihali utadhani ametoka kutumika kupita kiasi. Karim aliongozana naye kwenda nje ya chumba akiwa anamsaidia kumpa balansi.



Alikuwa ni mke wa kwanza wa Sultan. Macho yake yalikuwa mekundu yaliyolegea. Mdomo wake ulikuwa mkavu, goigoi.



Karim alimketisha kwenye kiti kikubwa sebuleni alafu akaita kibaraka wake mmoja aliyekuja upesi kutii wito. "Kalete chakula kilicho bora pamoja na sharubati. Mpatie mama huyu!" Haraka kibaraka akaenda zake, muda si mrefu akarejea na sinia kubwa la chakula. Sultana akalinyaka na kuanza kufakamia kama vile mtu jangwa aliyeona chemichemi ya maji





Hakujali ustaarabu bali kuondoa kwanza njaa kali aliyokuwa nayo. Alipakia chakula mdomoni mpaka akawa anashindwa kutafuna. "Pole pole, dada. Utapaliwa," Karim alitahadhari ila Sultana hakujali.



Tumbo lake lilipopata ahueni ndipo akahema sasa. Alimtazama Karim kwa macho yake malegevu pasipo kusema jambo. "Pole, dada. Nisamehe sana, haikuwa dhamira yangu kukawia," Karim aliomba radhi.

.

.



Sultana akasema kwa uchovu: "Naomba nipumzike." Karim akaita kibaraka wake wa kike, akampa maagizo ya kumteka Sultana na kumsafisha kisha kumlaza kwenye chumba cha wageni.



Kibaraka akatii na kutekeleza maagizo. Karim akabaki mwenyewe sebuleni.

Baadae majira ya jioni akapata wasaa wa kuketi na dada yake kuongea mawili matatu. Akamweka bayana yale yote yaliyotukia tangu alimpotowesha duniani kwa makubaliano.



Sultana akashangazwa lakini pia akapata hofu. "Itakuaje Sultan atakaporejea kasrini, Karim? Huoni kama utakuwa umetangaza vita?"

.

.

"Sijali!" Karim akakoroma. "Kama ni vita na iwe vita, dada. Siwezi nikakubali kuishi jela ... kuishi kama mbwa!"

.

.

"Karim, inabidi niende kasrini tena upesi!" "Mbona unakuwa na hofu hivyo dada yangu? Utaenda tu wala usijali. Ila unajua nini Sultan atakufanya?"

.

.

"Potelea mbali, ilimradi tu niwepo, anione!" "Vipi kama akikuadhibu kama mimi?"

.

.

"Karim, sasa nitaogopa mpaka lini? Yule ni mume wangu, siwezi nikamkimbia!" Karim akanyamaza kwanza. Alifikiria jambo kabla hajauliza:

.

.

"Utamwambia Sultan ulikuwepo wapi?"





"Sijui! Sina hata la kusema. Sijui ntaanzia wapi!" Alijibu Sultana akitikisa kichwa, mjawa majuto.

.

.

"Punguza kwanza hofu, dada. Kwa hivyo hautapata majibu abadani. Tuliza kichwa."

.

.

"Nitatulizaje kichwa, Karim! Yani ... Mungu wangu! ... nahisi homa inanipanda."

.

.

"Usijali, dada. Mie nina namna ya kufanya."

.

.

"Namna ipi hiyo?"

.

.

"Kumuua Sultan!"

.

.

"Karim!"

.

.

"Ndio. Hata hivyo nilikuwa nimepanga hilo hata kabla sijakurejesha duniani. Nataka kumuua Sultan! Nataka kulipiza kisasi kwa yale aliyonitendea."

.

.

"Karim, hala hala kidole na jicho! Usije ukathubutu hata siku moja kumdhuru Sultan. Tafadhali nakuomba!"

.

.

"Ila yeye athubutu kunidhuru mimi, sio?" "Kwani amekuua?"

.

.

"Kwa yale aliyonifanyia si bora angeniua?"

.

.

"Karim, huu ni mwili tu na moyo wangu wote upo kwa Sultan. Endapo ukimuua basi ujue nami sitakuwa mzima. Sitakuwa na furaha.



Unajua wapi nimetoka na Sultan?" Karim hakusema jambo, akanyanyuka na kuondoka zake akiwa amefura. Alijiendea chumbani kwake akibamiza mlango.

.

.

.

.

.

***

.

.

.

.

.

"Mpenzi," sauti tamu ya mke mdogo ilipenya masikioni wa Sultan aliyekuwa amejilaza kitandani hoi bin taaban.

.

.

Mwanaume akagugumia kuitikia. "Amka mpenzi. Umelala kwa muda mrefu sasa, au hutaki kulala tena usiku?" Akauliza sultana huyu mdogo. Alikuwa kando tu ya Sultan akiwa amejifunga nguo nyepesi kifuani.



Nguo hii ilikuwa inaonyesha chuchu zake nyeusi pamoja na matiti yake yaliyojaa nyama.



Mkono wake mlaini ulikuwa unapapasapapasa mgongo mpana wa Sultan na kuukandakanda taratibu.





"Nimekuandalia chakula kizuri ukipendacho. Tayari kipo mezani, kitapoa. Amka tukaoge kisha tukale." Sultan akajikusanya na kuunyanyua mwili wake wa kiutu uzima. Aliketi kitako, mke akampokea kwa busu kabla hawajanyanyuka na kwenda kuoga.



Kisha wakajiweka mezani kwa ajili ya chakula.

Wote walikuwa wamevalia nguo nyepesi zenye kuupa mwili hewa ya kutosha.

.

.

"Nashukuru sana mke wangu maana wanipa faraja. Unajitahidi sana kunipa furaha ambayo naikosa huko nje ya nyumba yako." Sultana akatabasamu kiaibu.

.

.

"Ahsante, Sultan wangu."

.

.

"Sijui ingekuaje kama ningelikuwa naishi nawe kasrini. Bila shaka maisha yangu yangelikuwa mazuri kabisa. Ningeishi kwa amani." Kuna kitu kikamwambia Sultana, hii ndiyo fursa!

.

.

"Kwani kunashindikana nini, Sultan wangu?" Akauliza akimtazama mwanaume machoni. "Hamna kinachoshindikana ... ila."

.

.

"Nini Sultan? Bado unamuwaza mkeo mkubwa?" "La hasha."

.

.

"Bado sina nafasi yangu kasrini?"

.

.

"Hapana, mke wangu. Mambo haya hayapaswi kupelekwa haraka hivyo. Kila kitu kitaenda tu sawa. Huna haja ya kuhofia." Endapo nikikosa fursa hii basi haitakuja kutokea nyingine adhimu zaidi, Sultana alisema na moyo wake.



Kwenye huu muda wakati mwenzake akiwa hayupo ndiyo rasmi kwake kumaliza kazi. Hapa ndiyo pa kutokea na kukamata madaraka ya kuwa Sultana wa kwanza.



Hakutaka kuipoteza hii nafasi. Alijua fika Sultana wa kwanza atakaporejea kitini, zoezi litakuwa gumu.





"Sihofii, Sultan. Ila naona muda wangu umewadia sasa. Kwanini hautimizi haja yangu? Au sina sifa za kuwa kwenye kasri yako?"

.

.

"Unastahili, mke wangu. Una kila sifa. Najua pia kasri langu ni tupu halina mtu. Ila ningekuomba unipe muda kidogo. Siku hizi mbili zikipita, nitaita wazazi na kukuapisha kama wangu wa kwanza."

.

.

Sultana akakubali japo kwa shingo upande. Aliona siku mbili ni nyingi na hapa katikati laweza kutokea lolote likaharibu sherehe.



Hakuwa na furaha. Sultan akaligundua hilo. "Usinung'unike, Sultana wangu. Kila kitu kitakuwa sawa." Wakiwa hapo wanaendelea kula, kijakazi wa getini akaja na kuwasalimu, kisha akasema:

.

.

"Sultan, Sultana kuna mgeni wenu."

.

.

"Nani?" Sultana akawahi kuuliza. "Ni mlinzi wa kasri," kijakazi akajibu. Upesi akapewa agizo la kumruhusu mgeni huyo aingie ndani.



Akaingia na kusimama mbele ya Sultan. Alikuwa amevalia sare zake nadhifu akisimama kikakamavu.



Uso wake ulijawa na shaka. "Sultan, Karim ametoroka. Na ameua pia walinzi kadhaa!"

.

.

Sultan akanyanyuka akitoa macho na kukunja ndita. Alikunja ngumi yake pana nzito, akauliza:

.

.

“Unasemaje?” kana kwamba hakusikia.



Mlinzi akasita hata kurejea alichosema. Akiwa anatetemeka, na uso wake ukiwa mweusi kwa hofu, akasema: “Sultan, Karim ametoroka, na ameua walinzi kadhaa.”

.

.

Sultan akamzaba kofi zito mlinzi huyo kijumbe, kofi likammwaga chini na kumpachika alama nyekundu shavuni.

.

.

“Pumbavu!” Sultan akafoka. “Wazembe wakubwa nyie, wapuuzi msio na faida. Anatorokaje mtu aliye ndani ya lupango?”

.

.Mlinzi alinyanyuka upesi akasimama kiukakamavu akitazama chini. Jicho lake la upande uliozabwa lilikuwa limeiva kuwa jekundu mithili ya nyanya masalo.

.

.

“Tuwie radhi, Sultan. Wanaume waliokuwa zamu walishindwa kumzingatia kwa umakini.”

.

.

Sultan alisaga meno. Alipandwa na ghadhabu sana, hakutaka tena kumskiza mtu na badala yake akaondoka kwenda chumbani aliporejea akiwa amejisitiri na nguoze za thamani, akatoka ndani pasipo hata kuaga.



Akili yake haikuwa pale tena, bali Kasrini. Alikuwa anamuwaza Karim. Alikuwa anawaza namna ya kuenenda na mwanaume huyo aliyempanda kichwani.



Mke wake mdogo aliyeachwa kwenye bumbuwazi, akamsindikiza mumewe huyo ambaye hakuwa na habari juu yake kwa muda huo, akayoyoma na kundi lake la walinzi kuelekea kasrini.



Mwanamke akabaki malangoni akimtazama mume akipotea. Aliona ndoto ya kuelekea kasrini inayeyuka, na sasa amepata tena sababu rasmi ya kuhofia.





“Kama Karim ametoka, ina maana mwanamke yule naye atakuwa amerudishwa duniani?” alijiuliza.



Hakutoka hapo malangoni hata pale mumewe alipokuwa haonekani kabisa. Alikaa hapo akiwaza, macho yake yakionyesha ni namna gani alivyo mbali kifikra.



Alikosa raha kabisa. Alikuja kuokolewa toka kwenye bahari ya mawazo na kijakazi wake aliyeita na kumwambia:

.

.

“Sultana, malango yamekaa wazi sana, si njema kwa usalama.”

.

.

Basi akatoka na kwenda zake ndani. Akaenendea bilauri la mvinyo na kumiminia kwenye glasi akanywa. Glasi ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne … bilauri likakata.



Kabla hajaongeza bilauri lingine apoteze fahamu vizuri, akachukua peni yake ya kuchovya na karatasi akaandika ujumbe wenye aya tatu kisha akapaza sauti kumuita kijakazi wake.

Upesi kijakazi akaja.



Karatasi yake ya ujumbe akaikunja na kuitia bahashani. Ilikuwa ni bahasha yenye nembo ya kasri na nguvu ya Sultan. Akamkabidhi kijakazi.

.

.“Nimekuita hapa maana wewe wapajua kwa bibi yangu, haya upesi umfikishie ujumbe huu!”

.

.

Kijakazi asiulize jambo, akapotea machoni mwa Sultana wake kwenda kutimiza agizo.

.

.

.

.

***

.

.

.

.

Jioni wakati Jua larembua, limechoka na linaaga uso wa dunia, sauti kubwa ya tarumbeta inavuma ndani ya himaya ya Goshen.



Tarumbeta hii ilikuwa inapulizwa na mwanaume kiongozi aliyekuwa amepanda farasi wa mbele kabisa kwenye msafara wa bibie Rhoda uliokuwa ukirejea nyumbani.





Tarumbeta hii ilikuwa ni ishara, lakini pia shangwe ya wasafiri, wenye heshima na hadhi ndani ya himaya, kurejea wakiwa salama na kufanikisha kile walichokiendea.



Phares, aliyekuwa chumbani kwa muda huo, alijikuta anatabasamu baada ya kusikia tarumbeta hiyo. Zaidi akajikuta anacheka na kutikisa kichwa chake.

Rhoda alikuwa amerejea. Na pia alikuwa ametekeleza lile alilokuwa amelilenga!

.

.

Alitoka ndani akaenda kusimama nje akiwa ameambatana na wafuasi wengine pia na walinzi. Walikuwa wamebebelea maua kadhaa kwa ajili ya kumlaki na kumpongeza Rhoda.



Kama vile malkia, Rhoda akapokelewa kwa matabasamu na makumbato. Phares akaongozana naye kwenda ndani, kwenye sebule kubwa pana, walipojikuta wenyewe na tayari wakishahudumiwa vinywaji aghali.

.

.

“Pole sana kwa safari, Rhoda,” Phares alisema kwa macho yenye furaha. “Nimefurahi sana kukuona tena, lakini nimefurahi sana kwa maana kazi umeifanikisha.”

.

.

Rhoda akatabasamu kidogo na kutikisa mguu wake uliokuwa umebebwa na mwingine kutengeneza umbo namba nne.

.

.

“Nashukuru sana, Phares, japo haikuwa kazi ndogo.”

.

.

“Bila shaka, ila nilijua fika utafanikiwa.”

.

.

“Ulijuaje Phares?”

.

.

“Penye nia hapakosi njia. Ulikuwa na nia kubwa mno kiasi cha kutokushindwa na sababu yoyote mbele yako.”

.

.

Rhoda akatabasamu pasipo kuhangaika na kauli hiyo. Ndani ya moyo wake bado haja yake haikutimizwa. Haja yake itapoa pale atakapoutia mkufu ndani ya kiganja chake na kuivaa shingoni.





Kila alipokuwa anawaza kuhusu mkufu huo, hujikuta anapata nguvu mara mbili asiogope mlima wowote uliosimama mbele yake.

.

.

“Natamani sana kujua yaliyotokea huko kwa Venin,” Phares alichombeza. “Unaweza ukanambia kwa sasa au umechoka taabani ukitaka kupumzika?”

.

.

“Sijachoka kiasi hicho,” Rhoda akatikisa kichwa akimtazama Phares kwa macho yake yang’aayo urembo. Pasipo kusita akamwambia mwanaume huyo yale yote yaliyotukia. Mpaka kufika kikomo Phares akawa ameachwa na bumbuwazi.



Alijua safari hiyo ilikuwa ngumu ndio, ila hakujua kama ni kwa kiasi hicho. Akampongeza tena Rhoda na kumpa pole.

.

.

“Yameshapita sasa hayo, na sasa tutazamie yajayo Phares.”

.

.

“Ni kweli, ila sidhani kwa sasa kama ni muda muafaka. Ningependelea tuongelee hilo kesho.”

.

.

“Hamna shida, Phares. Kweli ni jambo kubwa na pana, na linahitaji tutulize vichwa … Je, kuna lolote jipya lililotukia hapa nikiwa huko mbali?”

.

.

Swali hilo likasafirisha akili ya Phares haraka kwenda kwenye lile tukio la mzee wa baraza na mabinti zake.

.

.

Alikumbuka mabinti wale na sauti ya mzee yule, ila mmh mmh hakuona kama hilo jambo Rhoda anatakiwa kulisikia, basi akalifichia kifuani na kuchakata akili yake upesi kuziba mwanya huo.



Akakumbuka tukio la taarifa ya kuonekana kwa Malkia ndani ya himaya. Hili akaona linastahili katika meza yao ya maongezi.

.

.

“Unasema kweli, Phares?” Rhoda alitahamaki kusikia.

.

.

“Ndiyo, ni kweli tupu.”

.

.

"Laki … lakini imewezekanaje?”





“Sijajua imewezekanaje? Nashindwa kuelewa mwanamke huyu yupo wapi na anafanya nini!” .

.

Rhoda akakosa cha kusema. Alibakia akiwanda wanda ndani ya mawazo yake asijue mlango wa kutokea.

.

.

“Tatizo hili swala si mara ya kwanza kutukia, ni mara ya pili sasa! Ina maana Sandarus yupo mazingira ya karibu? Na je mbona huonekana na kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha?”

.

.

Rhoda alihangaika kutafuta neno, akakosa kabisa. Alizidiwa mawazo. Aliona kweli sasa anahitaji kupumzika. Alinyanyuka akamuaga Phares kwamba anaenda nyumbani kwake kupumzika.

Phares alitamani kumwambia mwanamke huyo alale hapo makaoni, ila akakumbuka ni mwiko – hakuna mwanamke anayelala hapo isipokuwa malkia. Basi akashuhudia Rhoda akienda zake.



Mwanamke huyo hakupitia hata mahesabu ya biasharaze, akanyookea ndani ya chumba chake kabatini alipotia chupa ndogo yenye kimiminika rangi ya kahawia, akafunga kabati kwa komeo kubwa kabla hajaenda kuoga na kujilaza juu ya kitanda chake kipana maridadi.



Alijitahidi kuepuka mawazo alale kwa amani, lakini hola! Bahati kwake uchovu ulikuwa mwingi hivyo akajikuta analala, tena vema tu! .

.

Kwa siku kadhaa mwili wake ulikosa kitanda cha kumfanya anyooshe kila kiungo.

.

.

.

***

.

.

.

“Hodi!”

.

.

Kabla usiku haujazidi kuwa mnene, sauti kavu ya kizee inasikika toka kwenye mlango mkubwa, mpana na imara wa mbao.



Mlangoni alikuwa amesimama mzee wa baraza ndani ya joho lake jeusi na viatu vyake vya wazi rangi ya chumvi.





Alikuwa ndani ya eneo kubwa lenye nyumba kubwa kuukuu. Getini kulikuwa kuna wanaume wawili walinzi waliokuwa wamevalia sare na kushikilia mikuki mirefu mikali kwenye mikono yao ya kuume.



Walinzi hawa walikuwa wamemruhusu mzee huyu kupita na sasa alikuwa ana jukumu lingine la kugonga azame ndani ya jengo.



Hakurudia kubisha tena kabla hajasikia sauti ya mlango kufunguliwa kwa ndani, na mara mtu anachomoza kichwa kumtazama. Alikuwa ni kijana mwenye ndevu kiasi rangi ya kahawia sawia na nywele zake fupi.

.

.

Macho yake yalikuwa madogo yenye kiini cha paka. Kwa makadirio alikuwa ana miaka ishirini naa, haipiti ishirini na tano.



Alitabasamu alipomuona mgeni, akatabasamu na kuufungua mlango zaidi.

.

.

“Karibu sana.”

.

.

“Ahsante, nishafika.”

.

.

Mzee akaingia na kuketi kitini. .

.

Sebule ilikuwa ya wastani ila yenye kila kinachohitajika. Kwenye kuta zake kulikuwa kumening’inizwa dhana kadhaa zilizotengenezwa na chuma. Japokuwa dhana hizi zilikuwa za vita, zilivutia sebule.

.

.

“Karibu, mzee wangu. Nikuitie baba?” aliuliza kijana, jina lake Fanty, uso wake ukiwa na tabasamu.

.

.

“Hapana, Tattiana yupo?” Mzee akauliza.

.

.

“Ndio, yupo chumbani kwake.”

.

.

“Mwambie nahitaji kuonana naye.”

.

.

Fanty alipochukua hatua kwenda kumuita Tattiana, mara Mzee akamuita.

.

.

“Au achana naye, niitie kwanza baba, nina maongezi naye.”

.

.

“Sawa!” Fanty akajibu na kwenda zake. Punde akarejea akiwa ameongozana na mwanaume mfupi mnene mwenye nywele na ndevu za kutosha.







Mwanaume huyu alikuwa amevalia nguo za ngozi, mikono yake ikiwa na bangili kadhaa za chuma ila zinazovutia kwa maumbo yake mbalimbali. Macho yake yalikuwa madogo yakimezwa na ukubwa wa mashavu.



Kwa jina alifahamika kama Melkizedek. Mfanyabiashara na mfuaji mkubwa wa chuma.



Alifurahi kuonana na mzee wa baraza, walisalimiana na kujuliana hali kabla hajatesa kiti kwa kukalisha mzigo wake wa mwili.

.

.

“Sikutegemea kukuona hapa karibuni, mzee.”

.

.

“Hata mimi sikutegemea kurudi hapa karibuni.”

.

.

“Ni nini hicho kimekurejesha, tena usiku kama huu?”

.

.

“Ni habari njema, na si kingine.”

.

.

“Habari zipi hizo? Siku yangu leo haikuwa njema, naomba uibadilishe kwa ujumbe wako.”

.

.

Mzee wa baraza akatabasamu kwanza. Alimtazama mwenyeji wake akaona machoni namna gani alivyokuwa na kiu ya kujua.

.

.

“Unaweza ukawa mkwe wa mfalme,” akasema kwa ufupi.

.

.

“Ukimaanisha nini?” Melkizedek akalipuka kwa swali.





.

“Mfalme amempenda mwanao.”

.

.

“Tattiana?” Melkizedek akauliza kana kwamba ana binti kumi. Macho yalikuwa yamemtoka nje ya mashavu yake makubwa.

.

.

“Ndio, Tattiana wako huyo.”

.

.

Melkizedek akajikuta anaangua kicheko kizito tumbo lake likicheza kama ngoma. Akampatia mzee mkono wa kuume akitikisa kichwa.

.

.

“Nashukuru sana, mzee.”

.

.

“Huna haja ya kunishukuru mimi, ni uzuri wa binti yako ndiyo ambao umekamata macho ya mfalme.”

.

.

“Macho hayo yasingelimuona kama usingelimpeleka huko,” Melkizedek alidakia, Mzee akatabasamu.

.

.

“Hiyo ni kazi yangu tu nilikuwa natimiza. Lakini kwakuwa ni mwiko kukataa shukrani, acha niipokee.”

.

.

“Ahsante sana. Sijui ni namna gani ninavyoweza kulipa fadhila zako.”

.

.

Mzee akatabasamu tena. Hapa ndipo alipokuwa anapataka na kupangojea – kulipwa fadhila. Ila akaigiza kama mtu asiye na mhemko.

.

.

“Melkizedek, wewe ni mtu mkubwa na muhimu ndani ya himaya yetu. Kila mtu anajua namna unayoingizia serikali kodi rundo kutokana na biashara zako. Mimi ni mzee tu ambaye naelekea kufa sasa, usiumize sana kichwa chako.”

.

.

“Hapana, mzee wangu. Chungu kinachoivisha chakula mapema, hutunzwa vema. Ningependa kukuachia alama ya shukrani maishani mwako kama ambavyo waenda kuniachia mimi.





Unajua endapo mfalme akimuoa mwanangu Tattiana akawa malkia, hata biashara zangu zitapanuka sana. Kodi itapungua kama si kuondoshwa kabisa. Hata himaya zingine ambazo bado si wabia wangu kibiashara, naweza kuwateka.”

.

.

“Hakuna tone la uongo hapo,” Mzee akatia chumvi akitikisa kichwa.

.

.

“Sasa niambie ni nini naweza nikafanya kukushukuru, mzee wangu. Ningependa kujua mapema ili basi nipate nafasi ya kujipanga, kama itahitajika.”

.

.

Mzee akasafisha koo lake na kutulia. Akatazama chini na kuminya viganja vyake vya baridi.

.

.

“Melkizedek,” Mzee akaita, kisha akasema: “Hili jambo ni siri. Na ningependa libakie hivyo kati yangu na wewe.”

.

.

Melkizedek akaminya lips.

.

.

“Usijali. Nina kifua cha kutunza na mdomo wa kufumba.”

.

.

Mzee akashusha pumzi ndefu kwanza kabla hajasema:

.

.

“Nina biashara yangu fulani, naomba unisaidie kuikuza.”

.

.

“Biashara?”

.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

.

“Ndio. Si maarufu sana, jitihada na kutoka kwake ni hafifu … unajua nataka kuwaachia wajukuu zangu jambo la kufanya. Angalau hata nitakapoondoka, basi wasianguke. Sina cha kuwarithisha, vilivyopo havitoshi kukidhi hata robo ya hitaji lao.”

.

.

Melkizedek alikuwa kimya akisikiliza kwa umakini.

.

.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog