Search This Blog

TROPEA MJI WA WAFU - 1

 




IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO



*********************************************************************************



Simulizi : Tropea Mji Wa Wafu
Sehemu Ya Kwanza (1)




"Bingo mume wangu, tayari tumefikisha miezi takribani mitatu sasa tangu mimi na wewe tufunge pingu za maisha. Ukweli nafurahia sana uwepo wako katika maisha yangu na najivunia kuwa na mwanaume mzuri mkamirifu vile vile muaminifu, ukweli uko Sawa kwangu. Lakini licha ya kwamba maisha yetu ya ndoa kuwa yenye furaha na amani ila kuna suala moja huwa linanitatiza akilini mwangu na nashindwa kulielewe,hivyo natuamini leo utanipa uvumbuzi ili niweze kulielewe. Bingo nakupenda sana mume wangu tena zaidi ya sana, kwahiyo nakuomba unambie ukweli usinifiche mimi ni mkeo" Ilikuwa ni sauti ya mwanadada wa kuitwa Millander. Sauti hiyo ilisikika Millander akimbembeleza mumewe ambaye ni Bingo ili Bingo aseme ukweli wa siri nzito inayoendelea juu yake. Kwani kila siku ifikapo usiku wa saa nane Bingo alikuwa akiamka nakisha kujifunga mtandio mweusi kiunoni kwake baada kisha anatoka ndani na kuelekea makaburini. Jambo hilo mwishowe Millander alishindwa kulivumilia na hivyo usiku mmoja Bingo alipoamka alijiandaa kama afanyavyo kila siku na kisha kuelekea huko makaburini wakati huo huku nyuma yake Millander akimfuatilia bila mwenyewe kujua,ila kutokana na giza nene na woga aliokuwa nao Millander ulimfanya kurudi nyumbani bila kujua mwisho wa Bingo unakuwa wapi. Lakini pia jambo lingine ambalo lilimshtua Millander ni pindi Bingo arejeapo nyumbani hunukia harufu ya ubani huku sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwa zimetapakaa damu..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bingo aliposikia maneno hayo ya mkewe alishusha pumzi ndefu kidogo, akakaa sawa kitandani wakati huo Millander akimkodolea macho, uso wake ukionyesha dhahili siku hiyo kutaka kujua ukweli huo uliojificha juu ya mumewe. Hivyo Bingo kabla hajaanza kuongea hali harisi alikohoa kwanza kisha akasema "Millander mke wangu, kwanza asante sana kwa kutambua umuhimu wa ndoa yetu na vile vile kuniweka mimi kipaumbele kwa kunithamini kama mimi ni mumeo" Bingo alikaa kimya kidogo ambapo kwa mara nyingine tena akaishusha pumzi yake kisha akaendelea kueleza "Katika maisha yangu kuna mitihani mkubwa sana nimepitia, na ni changamoto ngumu ambazo nimekumbana nazo ambazo moja wapo ziliniladhimu kwenda TROPEA mji wa ajabu sana, mji uishio wafu mji ambao kuishi ni tabu hasa kwa wale wanadamu wenye hali ya kawaida yaani namanisha waliotunukiwa uhai. Nia na madhumuni iliyonipelekea huko ni kufuaata dawa ya kumtibia mama yangu mzazi ambaye kwa kipindi kirefu sana alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya hapa na pale,mama alisumbuliwa na miguu kuvimba na kutoa maji, mara nyingine kumtokea hali ya kushindwa kula kabisa chakula na kupoteza fahamu mara kwa mara. Millander mke wangu hayo ni magonjwa ambayo yalimtesa sana mama yangu hadi kupelekea kudhoofika huku kila dawa zikishindwa kutatua matatizo hayo. Ikafikia hatua mama akawa mtu wa kulala wakati wote,tayari alikataa tamaa ya kuendelea kuishi kwenye ulimwenguni akabaki kungojea siku ile ambayo Mungu atamtuma maraika aje kuchukua roho yake sababu alijiona hana tena thamani ya kuendelea kuishi kwani magonjwa hayo yalimfanya baba kumkimbia na kisha kuoa mwanamke mwingine ilihali ndugu baadhi nao wakionyesha kumtenga baada kuona mama hana dalili yoyote ya kupona" Alisema Bingo, makasa ambao ulimtoa machozi pindi alipo ukumbuka kwani ni zamani kidogo tangu mambo hayo yapite. Millander alipomuona mumewe amedondosha chozi alimgusa bega akamtuliza munkali kwa kumpa pole. Kijana Bingo aliyafuta machozi yake kisha akaendelea kueleza mkasa huo ambao ulimpelekea Kufika Tropea mji ambao huishi wafu, mbali na kwenda kuchukua dawa katika mji huo vile vile Millander alitaka kujua ni sababu ipi inayomfanya Bingo kila siku usiku wa manane kuamka na kisha kuelekea makaburini ilihali pindi anaporudi hunikia harufu ya ubani na pia sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwa zimetapaa damu.

***********

"Tumepoteza pesa nyingi, tumelala tongo macho kutafuta tiba yake lakini hakuna mafanikio yoyote. Nasema hivi mimi nimenyoosha mikono niacheni na maisha yangu" Ilikuwa ni sauti ya baba yake mkubwa Bingo. Maneno hayo aliyanena saa za jioni akiwa amelewa chakari,alipasa sauti juu ikiwa kama kutuma ujumbe malangoni kwa mama Bingo ambaye hali yake ni mahututi sana. Maneno hayo yalipenya vema kwenye masikio ya mama huyo hakika alisikitika sana, aliumia moyoni mwake lakini hakuwa na lakufanya zaidi tu alililia na maumivu yake.

Jioni moja Bingo alifunga safari kuelekea kule alipohamia baba yake,aliitwa Abacha. Ikawa siku nzuri kwake sababu alimkuta mzee Abacha akiwa nje akipiga zogo na mkewe wa pili. Safari hiyo ya Bingo ni kwa niaba ya kufuata matumizi lakini alijikuta akiambulia matusi na masimango kutoka kwa baba yake huku mzee huyo akidiriki kusema kwamba hana muda wa kumuhudumia mgonjwa asiyepona. Maneno hayo yalimuumiza sana Bingo, ndipo kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake akasema "Baba lakini kumbuka yule naye ni binadamu,na pia hakuzaliwa na yale matatizo ila ni mitihani tu ya dunia ambayo kila mtu inaweza kumpata. Hupaswi kumtupa, yule ni mkeo, hatakama umeoa mwanamke mwingine isiwe kigezo cha kumsahau mama yangu"

"Unanifundisha maisha?" Aliuliza mzee Abacha, swali ambalo lilimfanya Bingo kukaa kimya huku uso wake akiwa ameinamisha chini huku akitafakari jibu la kumrudishia mzee wake, lakini kabla Bingo hajasema chochote mzee Abacha akasema.

"Haya ondoka nyumbani kwangu,na ukamwambie mama yako mimi sipo tayari kusaidia chochote juu yake. Hapo nilipo fika basi inatosha" Bingo aliposikia maneno hayo aliinua uso wake akamtazama baba yake ambaye naye alionyesha uso uliofura hasira,chozi lilimtoka Bingo asiamini kama baba yake angeliweza kunena maneno hayo. Punzi alishusha kisha akaondoka zake bila kusema neno lolote. Akiwa njiani akirudi nyumbani aliyafikiria maisha ya mama yake lakini pia hakusahau upande wake.

"Naam! Kama ni jahazi tayari linaelekea kuzama kwani nahodha ameshabwaga manyanga huku safari ikiwa bado hajatia nanga. Ni dhahili shahili baba katutelekeza hivyo kinachotakiwaa ni mimi kucheka kichwa changu ili kujua kipi cha kufanya ili niweze kumsaidia mama yangu,ndugu wametutenga wamejitoa kabisa kuhusu kumuuguza mama. Ooh Mungu wangu nisaidie " Yote hayo Bingo alikuwa akiyafikiria akilini mwake, muda huo alikuwa akirejea nyumbani baada kutoka kwa baba yake ambaye alitimua kama mbwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hivyo kutokana na mtihani huo aliotunikiwa Bingo wa kususiwa mama yake ikabidi aachane na shule, ili aanze kusaka shilingi ya kutumia na mama yake. Alifanya vibarua vya kulima, alikata mkaa, yote ikiwa kusaka pesa akidiriki kuitupa kando Elimu yake akiwa darasa la sita. Maisha hayo ya kufanya vibarua yalikuwa endelevu kwa kijana Bingo, msimu wa kilimo ulikuwa faida kwake kwani aliweza kufanya kazi kwa bidii alitumia nguvu nyingi sana kulima bila kuchoka, alifanya hivyo huku akizingatia kununua mazao ya chukula na kisha kuyahifadhi ndani ili msimu wa njaa hapo kijijini kwao wasije wakapata tabu kwani hawakuwa na mashamba. Mzee Abacha alipoamua kuoa mwanamke mwingine aliuza mashamba yote ambayo alikuwa akiyatumia na mama Bingo kisha akanunua mashamba mengine kijiji cha pili. Haukuchi kuna kucha ndio maisha ya kijana Bingo na mama yake, alipambana Kadri awezavyo kuhakikisha mama yake anakula japo kwa utepe kutokana na hali aliyokuwa nayo. Siku zilisonga miezi ikasogea miaka nayo ikajongea, asubuhi moja yapata saa kumi na mbili wakati Bingo anajiandaa kuelekea shambani kumalizia kibarua alichopata siku kadhaa nyuma alisikia sauti ya mama yake ikimuita, sauti ambayo ilisikika kwa chini kabisa kiasi kwamba ilimshtua Bingo. Haraka sana Bingo alitupa jembe chini akarudi ndani kumsikiliza mama yake anakipi cha kusema.

"Bingo mwanangu"

"Naam mama nipo hapa mwanao" Aliitika Bingo.

"Najua unavyo hangaika kila siku,umediriki kuitupa kando Elimu yako ambayo ingekuwa msaada hapo baadaye. Naumizwa sana na suala hilo lakini natumaini ipo siku Mungu atakukumbuka nakupenda sana Bingo wangu" Bingo aliachia tabasamu mara baada kuyasikia maneno hayo ya mama yake, na mara baada kukatisha tabasamu hilo akasema "Wala usiwe na hofu mama,mimi ni mwanao. Tena mwanao pekee kwahiyo nitapambana mpaka tone la mwisho kuhakikisha wewe unafurahia maisha japo upo katika hali hiyo. Na vile vile.." Kabla Bingo hajamaliza kusema alichotoka kuongea mara ghafla nje ilisikika sauti kali ikisema" Bingo toka ndani mwanahidhaya mkubwa mkubwa wewe " Haraka sana Bingo alinyanyuka akatoka ndani kwenda kumsikiliza mtu huyo.

" Habari za asubuhi Bi Mandawa, shikamoo "Bingo alimsalimu mtu huyo aliyenena maneno yale yasiyo ya busara, sio mwingine bali ni Bi Mandawa.

" Sina haja ya salamu yako, ninachotaka hapa ni pesa yangu maana naona kazi imekushinda "

" Hapana bibi yangu kazi haijanishinda, muda niliamka kwanza kumnywesha uji mama. Baada kumaliza ndio nikawa najiandaa kuelekea shambani kwako,ila mama akawa ameniita kuna jambo alitaka kusema nami "Alijibu Bingo kwa sauti ya upole kabisa. Lakini Bi Mandawa licha ya kuambiwa maneno hayo bado aling'aka ila mwishowe alimtaka Bingo kumaliza kibarua hicho siku hiyo.

" Ni hurumie bibi yangu, nitapamaliza kweli leo?.. "Aliuliza Bingo. Bi Mandawa akajibu" Utajua mwenyewe ukishindwa basi ujue kabisa na pesa yangu unarudisha " Kwisha kusema hivyo aliondoka zake huku nyuma akimuacha Bingo akimsindikiza kwa macho.

******

Basi siku hiyo nililima sana, kuanzia asubuhi mpaka saa moja usiku. Haikuwa kawaida yangu kufanya kazi mpaka muda huo ila iliniladhimu kufanya hivyo ili kunusuru kurejesha pesa ya watu ambayo tayari nilikuwa nimeshakwisha itumia. Hivyo wakati narudi nyumbani, giza lilikuwa limeshatanda. Kijiji chote kimepoa ndege na wanyama wakipata nafasi ya kuzulula huku na kule huku sauti za wadudu nazo zikipasa vema kabisa kwenye masikio yangu. Mimi sikujali, jembe begani panga mkononi nilizipiga hatua za haraka haraka kurudi nyumbani lakini kabla sijafika mara ghafla njiani nilikutana na mtu ambaye siku mfahamu wala kuwahi kumuona mahali popote. Ajabu mtu huyo yeye alinifahamu, alikuwa ni ajuza japo kulikuwa giza totoro lakini nilimfahamu hiyo kwa sababu alikuwa na mkongojo.

"Wewe ni nani mbona mimi sikufahamu, na umetoka wapi pia unataka nini.." Nilimuuliza maswali hayo haraka haraka wakati huo nikiw a na woga, cha kustaajabisja ajuza yule aliangua kicheko huku sauti yake ikijirudia mara mbili mbili, vile vile sauti iliyotoka haikuwa yake ilisikika sauti ya kiume nzito..!







Niliogopa sana, nikataka kukimbia lakini miguu yangu ikawa mizito. Hapo sasa ikabidi nipige mayowe kuomba msaada kwa wanakijiji ili waje kunisaidia, kweli wanakijiji wakafungua milango yao lakini maajabu yakawa bado yanaendelea kwani wanakijiji waliotoka katika manyumba yao hawakuwa binadamu, dhahili shahili kwa macho yangu nilliwaona wakitoka damu midomo mwao huku wakijongea mahali nilipo simama kwa mwendo wa kusafa. Nilizidi kuogopa, kijasho chembamba kinanichwea wakati huo yule ajuza akiendelea kuangua kicheko japo sauti yake haikutandabaisha na muonekano aliokuwa nao. Punde si punde kicheko kile kilipotae na wale wanakijiji nao walipotea kimaajabu nikabaki sasa mimi na yule ajuza ambapo ajuza yule alifungua kinywa chake kisha akaniambia "Bingo najua tabu unazozipata wewe na mama yako, lakini tambua msaada umepatikana endapo kama utakubaliana na masharti nitakayo kwambia"

*****

Maneno hayo ya ajuza yalimshtua Bingo, kwa hamaki kubwa akamuuliza "Masharti gani na huo msaada unahusu nini?.."

"Ahahah aha" Kwa mara nyingine tena ajuza yule wa ajabu aliangua kicheko, baada ya kukatisha cheko lake hilo akasema "Dawa ipo, dawa ambayo itamrudisha mama yako katika hari yake ya kawaida, lakini kuipata kwake dawa hiyo inahitaji moyo ili Kufika huko ilipo..".

"Ipo wapi?.." Alirudi kuhoji Bingo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ipo Tropea! Mji uishio wafu itakulazimu ufe ili Kufika huko" Alisema ajuza huyo, maneno ambayo yalisikika kwa kujirudia mara mbili mbili mfano wa mwangwi.

"Nife? Halafu nikisha kufa?.." Aliuliza Bingo,lakini kabla ajuza hajajibu swali hilo la Bingo, ghafla ilisikika sauti ikimuita Bingo. Sauti hiyo ilipasa mara nne, mara ya tano Bingo aliitika kitendo kilicho mpelekea kutoka usingizini. Alistaajabu sana kujikuta yupo kitandani, kumbe yote hiyo ilikuwa ni ndoto. "Mungu wangu,kumbe ni ndoto? Inamaana gani ndoto hii?.." Alijiuliza Bingo wakati huo akiwa ameketi kitandani huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi mithili ya chura anayepumua. Kule nje sauti ile bado iliendelea kumuita na ndipo aliponyanyuka kutoka kitandani, akatundua kaptula yake iliyokatwa miguu kwa style ya kuzidiana, akavaa kisha akatoka ndani kwenda nje kutii wito. Alipofika mlangoni alikutana na uso wa Bi Mandawa. Bingo alishtuka sana akakumbuka kuwa kwenye ndoto ile aliyoota alikuwemo na Bi Mandawa.

" Habari za asubuhi Bi Mandawa, shikamoo "

" Sina haja ya salamu yako, ninachotaka hapa ni pesa yangu maana naona kazi imekushinda "

" Hapana bibi yangu kazi haijanishinda, muda niliamka kwanza kumnywesha uji mama. Baada kumaliza ndio nikawa najiandaa kuelekea shambani kwako,ila mama akawa ameniita kuna jambo alitaka kusema nami "

" Utajua mwenyewe ukishindwa basi ujue kabisa na pesa yangu unarudisha " Hayo ni maneno yaliyokuwa yakijirudia kichwani mwa Bingo, maneno aliyokuwa akijibizana na Bi Mandawa katika ndoto. Hali hiyo ilimfanya Bingo kuinamisha uso wake chini kitendo ambacho Bi Mandawa kilimpelekea kumuumiza Bingo kama yupo sawa.

" Nipo sawa bibi" Alijibu Bingo huku kwa mbali akiachia tabasamu hafifu lenye kitu fulani ndani yake.

"Mama anaendeleaje?.."

"Hivyo hivyo tunamshukuru Mungu"

"Sawa, basi mguu huu ni wako bwana Bingo" Aliongezea kusema Bi Mandawa. Bingo akakunjia mikono yake kwenye kifua akatega masikio yake vema kabisa kumsikiliza kikongwe huyo anakipi cha kumwambia.

"Ndio nipe maisha"

"Nina sehemu yapata nusu tu nataka unilimie,nimetumiwa pesa na mwanangu kwahiyo nimeona bora niweke mtu ili anisaidie" Alisema Bi Mandawa. Bingo alifurahi kusikia habari hiyo, kwani ndio yalikuwa maisha yake.

"Na ndingependa kesho uanze kwa maana siku yoyote mvua inaweza kunyesha" Aliongezea kusema Bi Mandawa, Bingo akajibu "Hilo ondoa shaka, umefika hapa kwa Bingo Alwatan kiboko wa ardhi. Kesho kesho kutwa nakukabidhi shamba lako" Maneno hayo ambayo Bingo aliyanena kwa kujiamini yalimfanya Bi Mandawa kuachia tabasamu pana kisha punde akaondoka zake huku akisisitiza Bingo afike shambani kwake bila kukosa.

"Usijali bibi" Alipasa sauti Bingo kumuhakikishia bibi huyo,kisha akarudi ndani moja kwa moja akamjulia hali mama yake kwani ndio utaratibu aliojiwekea tangu afikishe umri wa kujitambua. Baada ya hapo alirejea chumbuni kwake,hapo aliketi akashusha pumzi ndefu huku ubongo wake ukijaribu kuikumbuka ndoto ile aliyoota. Hakika ni ndoto ambayo ilimuacha mdomo wazi na kushindwa kufahamu ndoto hiyo ilimanisha nini. Lakini mwisho wa yote alifanya mchakato wa kumuandalia mama yake uji akamnywesha kisha akaelekea shambani kuendelea na kibarua alichoshika hapo awali.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya tofauti kwake, Bingo aliumiza kichwa juu ya kuwaza ile ndoto ya ajabu. Alishindwa kutambua inamaana gani kitendo ambacho kilimfanya kushusha pumzi mara kwa mara huku akisitisha kulima nakisha kupumzika kwa dakika kadhaa ilihali kichwa chake akikipa majukum ya kuidadavua ndoto ile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ipo Tropea! Mji uishio wafu itakulazimu ufe ili Kufika huko" Maneno yale ya ajuza aliyemtokea kwenye ndoto yalijirudia kichwani kwa Bingo,ndipo kwa mara nyingine tena akaishusha pumzi yake kisha akaendelea kulima. Lakini wakati Bingo yupo kwenye hali hiyo, mara ghafla alisikia sauti ikimuita. Sauti hiyo iliyokuwa ikimuita ilitokea nyuma yake,ni sauti ambayo ilimshtua sana kwani alifahamu fika sauti kabla hata hajageuka kule ilipokuwa ikitokea.

"Bingo Bingo Bingo.. Habari yako" Ilisema sauti hiyo, Bingo akiwa na hali ya taharuki aligeuka nyuma yake ili ajue kama ndio yeye mtu aliyemdhania ingawa mtu huyo miaka kadhaa imepita tangu afariki. Ajabu alikutana na mtu tofauti na yule aliyemfikiria, ni mwanadada mrembo mwenye umbile refu na mweupe mithili ya muarabu, nywere zake za singa wakati huo huo kifuani alikuwa amevaa mikufu ya dhahabu na mkononi akiwa na bangili. Hakiaak alikuwa mrembo sana ambaye alionyesha tabasamu muda wote. Bingo alishtuka akatupa jembe chini alionyesha kumuogopa mrembo huyo kwa woga na hofu kubwa moyoni alizipiga hatua kurudi nyuma huku akihema juujuu. "Wewe ni nani?.. 'Aliuliza Bingo kwa sauti ya woga kwani aliamini kabisa msichana mrembo kama yule ni nadra kuonekana vijijini, hivyo akahofia kuwa huwenda mwanadada huyo akawa jini.

"Ahahahahha" Alicheka mwandada huyo wakati huo huo akimsogelea Bingo kijana aliyeonekana kuhaha kwa woga. Mwanadada huyo alipomkaribia Bingo alimtazama usoni, akaachia tabasamu kisha akasema "Bingo, naitwa Roya. Tukutane Tropea" Alipokwisha kusema hayo mwadada huyo aliyejitambulisha kwa jina Roya alipotea ikasalia vumbi. Bingo alipiga mayowe akatimua mbio huku akipasa sauti ya kuomba msaada. Hapo sasa Bingo akaanza kuiamini ndoto ile aliyoiota,maneno ya mwanadada Roya yalimfanya kuamini kwamba ni kweli siku yoyote atafika Tropea mji uishio wafu, jambo ambalo lilimpelekea Bingo kupata tumbo joto hasa hasa baada kukumbuka ile ndoto ambayo ajuza alimueleza kuwa ili Kufika katika mji huo inamlazimu afe kwanza..



Suala hilo la kufa lilimchanganya sana Bingo kiasi kwamba akaanza kujiona ni mfu aliye hai,kwani mbali na lile tukio la kutokewa na Roya vile vile siku kadhaa mbele alitokewa na mtu wa ajabu ambaye alionekana sehemu mbali mbali za mwili wake ni nyoka ingawa miguu yake ikiwa kwato za mbuzi. Bingo alikuta na mtu huyo saa zile zile za jioni akiwa ametoka polini kukagua mitego yake,ambapo wakati yupo njia anarudi nyumbani huku alifurahi kumnasa kanga ghafla aliguswa bega nyuma kitendo ambacho kilimpelekea Bingo kushtuka na kisha kusimama ili amtazame mtu huyo aliyemgusa. Alishtuka kukutana na mtu wa aina hiyo, ajabu yule mtu aliangua kicheko wakati huo Bingo akimkodolea macho huku akemeza mabunda ya mate mara kwa mara kuashiria kumuhofia mtu yule. Punde si punde yule mtu alipotea kisha ikasikika sauti nzito ikisema "Bingo Bingo njoo Tropeaaaaa" Kwisha kusema hivyo sauti hiyo ilimalizia na kicheko kizito. Bingo aliogopa akatimua mbio huku akipiga mayowe "Nisaidieeni nakufaaaa nakufaaaa.." Sauti hiyo Bingo alipasa wakati huo akitimua mbio, hakusimama mpaka alipofika nyumbani kwao ambapo alipofika alihema haraka haraka huku mikono akiwa amegusa magoti yake. Pumzi yake ilipokaa sawa alizama ndani kumjulia hali mama yake,na wala hakuweza kumuelezea mamaye hali anayokumbana nayo kwa sasa. Bingo alionyesha moyo wa chuma. Lakini hali hiyo ya kukumbana na mauza uza kwa kukutana na watu wa ajabu ajabu katu haikuweza kupotea,bado Bingo aliandamwa na mauza uza hayo mpaka kupelekea kuonekana kituko kwa wanakijiji.

"Jamani hivi siku hizi Bingo mnamuelewa kweli?.." Ilikuwa sauti ya kijana mmoja akiwauliza wenzake wakiwa kijiweni saa ya jioni.

"Hapana hata simuelewi kiukweli, yani Bingo Kawa kama Mwendawazimu kila mara utamuona anakimbia kimbia mara utasikia anasema anaona watu wa ajabu ajabu. Hivi yupo sawa kweli yule?" Kijana wa pili alidakia kwa kusema hayo. Muda huo huo kijana watatu alisema"Bingo ni kijana mwenzetu ni mwanakijiji mwenzetu kinachotakiwa sisi kama vijana ni kumfuata tumuulize ni kipi kinacho mvuruga mpaka kupelekea aonekane kituko hapa kijijini"

"Kabisa, wewe umesema vizuri. Lakini mbali na hilo la kumdadisi ili kujua kinacho msibu, vile vile inatakiwa tumchangie pesa ili tumtafutie shamba. Bingo Kawa kama punda hapa kijijini, amekuwa mti wa kulima vibarua tu wakati kuna wanakijiji humu wanamiriki mashamba mengi kiasi kwamba mengine hawayafanyii kazi" Aliunga mkono na kisha naye kusema ya moyoni kijana wa nne ambaye kwa hapo kijiweni yeye ndio alikuwa muuza chai ya tangawizi pamoja na bagia. Yalikuwa ni mawazo mazuri mno waliyofikiria vijana hao lakini muda mfupi baadaye mawazo hayo yalionekana huwenda yataleta kigugumizi baada Mzee mmoja kusema nao jambo, mzee huyo aliitwa Ndole. Mzee Ndole kabla hajasema maneno hayo aliketi kwanza kwenye kiti kisha akaagiza chai na bagia mbili. Alipokabidhiwa alikunywa bunda moja la chai akasindikizia na kipisi cha bagia kisha akasema "Vijana wangu nimewasikia kila kitu mlicho kuwa mkikipanga kuhusu Bingo kijana wa mzee Abacha. Kiukweli ni mawazo mazuri lakini vile vile mawazo hayo yanaweza kughalimu maisha yenu mkajikuta manaingia matatani.." Alisema mzee Ndole kisha akakomea hapo kidogo huku akiwa nyai bunda la pili hali ya kuwa wale vijana nao wakionyesha utulivu wa aina yake ili kumsikiliza mzee huyo kwa umakini zaidi wajue anamaana gani kunena maneno hayo. Hivyo mara baada mzee Ndole kukirejesha chini kikombe hicho alikohoa kidogo halafu akaendelea kusema "Kuna siri kubwa katika familia ile. Hivi hata hamjiulizi ni kwanini mzee Abacha kaamua kumkacha mkewe na mwanaye? Mbali na mzee Abacha, hamunoni hata ndugu wengine nao wanalichukulia kawaida jambo hili wakati ni jambo la kumsaidia mwanamama yule? Nadhani mkijiuliza maswali hayo na mkajijibu vizuri basi mtaacha kufanya mlichokuwa mnakifikiria kukifanya"

"Mmh babu lakini umetuacha njia panda, kwa kuwa umeamua kusema basi ongea ukweli ili vijana wako tujue" Alisema moja ya vijana wale waliokuwepo mahali pale kijiweni. Mzee Ndole alikaa kimya kwanza hakutaka kumjibu kijana huyo. Ukimya huo wa mzee Ndole ulimfnaya kijana mwingine kuongeza kwa kusema "Maana tunasikia kuwa mzee Abacha aliamua kumuacha mkewe baada kubainika kuwa haponi ugonjwa alioa nao, kwahiyo akaona kwasababu nguvu bado anazo heri akaoe mwanamke mwingine"

"Mbona kama ni hivyo hataki kuhudumia nyumba kubwa?.." Alihoji mzee Ndole,na punde si punde akasema "Nyie bado watoto wadogo hamjui chochote, na kinacho waponza ni kujifanya kuwa kila kitu mnakijua. Kiujumla hamtaki kukaa na wazee ili mfahamishwe mambo msiyo yajua.. Mimi mzee Ndole nayajua mwanzo mpaka mwisho matatizo aliyonayo mama Bingo.. Anaitwa Noela, ndilo jina lake. Kipindi kile alipoana na Abacha walikaa kwa kipindi kirefu mno pasipo kupata mtoto. Jambo hilo Abacha hakufurahishwa nalo hali iliyopelekea amani kati yao kupotea..

**********

"Noela hivi unajua siku zote raha ya ndoa ni familia?.." Ilikuwa ni sauti ya Abacha akimwambia mkewe,muda huo ulikuwa usiku wapata saa tatu.

"Ndio mume wangu najua hilo.." Alijibu Noela. Abacha akaongeza kusema "Sasa kama unajua mbona sioni dalili yoyote ya wewe kunasa mimba? Mwaka wa ngapi huu?.." Maneno hayo Abacha aliyasema kwa hasira na ghabu, Noela hakujibu alikaa kimya huku akilia na Mungu wake. Furaha kati ya wawili hao ikayeyuka mfano wa mawingu angani, Abacha alihitaji mtoto hali yakuwa Noela uzazi wake kutunga mimba ni batili. Hivyo kila siku ukawa ugomvi,ingawa mara moja moja jirani yao Ndole alikuwa akiingilia kati kusuruhisha ugomvi huo.

Hali hiyo Noela ilimchosha na ndipo siku moja aliamua kufunga safari kuelekea nyumbani kwao kuomba mawazo kipi afanye ili ajenge mzizi thabiti kwenye ndoa yake.

"Ni heri umekuja mwanangu nafikiri tatizo hilo limekwisha" Alisema baba yake Noela baada binti yake kumuelezea matatizo aliyonayo. Yaliyokuwa ni maneno yaliyomfurahisha mno Noela, hivyo baba yake alimchukua moja kwa moja akaenda naye mpaka kwenye mti mkubwa ambapo hapo ndipo ilipokuwa mizimu yao. Mizimu ambayo ulikuwa ukiomba kitu inakupatia bila pingamizi lolote ingawa kuna masharti baadhi unakabidhiwa endapo kama utayatekeleza basi huwezi kudhurika lakini kama utakwenda nayo kinyume lazima madhara yatakupata.

Hapo Noela alieleza shida yake, mizimu hiyo ya ukoo wao ikamjibu ambapo chini ya ule mti kilitokea kibuyu ambacho lilionekana kupambwa na shanga mbali mbali. "Binti chukua hicho kibuyu hicho kibuyu" Ilisikika sauti ikimwambia hivyo Noela, sauti ya kiume ambayo ilijirudia mara mbili mbili. Noela aliogopa sana lakini mzee wake akamtoa hofu akamsisitiza akichukue hicho kibuyu. Hatimaye alikubali japo mikono yake ilikuwa ilitetemeka kwa woga. "Ahahhahaha. Hahahahaha.. Hahahahah" Vicheko vya ajabu vilisikika chini ya mti ule, na mara baada vicheko hivyo kutoweka ilisikika sauti ile kwa mara nyingine tena. Safari hiyo sauti ilisema "Noelaaaaaa.. Ndani ya kibuyu hicho kuna damu. Ondoka nacho hicho kibuyu mpaka nyumbani kwako hakikisha hakidondoki chini wala kulowana kwa kimiminika chochote. Kitunze vizuri kibiyu hicho kwani hakifai kuonwa na mtu wa ukoo mwingine. Ikifika saa sita usiku kunywa damu hiyo iliyomo ndani ya hicho kibiyu. Hali itakayo kutokea kubaliana nayo, vile vile hupaswi kupinga pindi utakapo hitajika kufanya jambo fulani. Sawaaaaaa "

" Sa.. Wa.. Sawa aa" Aliitikia Noela kwa woga kabisa huo ile sauti ikiwa imeshatoweka.

Baada ya hapo Noela aliambatana na baba yake kutoka pale kwenye ule mti wa mizimu ya ukoo. Hatua kadhaa mbele walisimama, baba akamtazama binti yake akatabasamu kisha akasema "Safari njema mwanangu, nafikiri tatizo lako limekwisha sasa"

"Asante baba na kweheri utamsalimia mama" Alijibu Noela ilihali naye pia akiachia tabasamu. Hivyo wakawa wameachana kila mmoja alirudi kwenye mji wake. Noela alifanya yote kama alivyoambiwa na mizimu,hakika ilikuonyesha kuwa amedhamilia kutuliza ndoa yake kwa kupata mtoto aliamka muda ule ule alioambiwa kule mizimuni,muda huo mumewe alikuwa amelala usingizi mzito asijue kinachoendelea. Noela aliimywa damu iliyokuwemo kwenye kile kibuyu, ajabu punde si punde tumbo likaanza kumuuma, hali hiyo ilidumu kwa muda wa dakika kadhaa kisha akaanguka chini akajikuta hajui kinachoendelea ingawa baadaye kidogo alisikia vishindo vya mtu anayetembea wakati huo kwa mbali zikisikika sauti za nafsi zikilalama..



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sauti hizo ambazo zilikuwa za ajabu zilimshtua Noela achilia mbali kishindo kile kilichokuwa kikimsogelea.

"Mungu wangu" Alisema Noela huku akitetemeka wakati huo punde si punde ulitokea mwanga mkali mwanga ambao haukudumu sana ukatoweka kisha ikatokea barabara ndefu ambayo pembeni ilipambwa na mafuvu. Bado Noela alitaharuki akashindwa kuelewa yupo wapi duniani ama kuzimu,lakini baadaye alijua kuwa hayupo duniani baada kusikia sauti za nyimbo zikiimba kwa kumkaribisha Tropea. Sauti hiyo ilipenya vema masikioni mwa Noela, ghafla kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku akiogopa.

"Noela Noela karibu katika himaya ya Abdi. Amini tatizo lako limekwisha endapo kama utakubaliana na matakwa yetu" Ni sauti ambayo aliisikia Noela, sauti hiyo ilikuwa ya Sultan katika mji ule wa Tropea, mji ambao wakazi wake ni wafu japo binadamu wa kawaida hufika huko ila kwa shida mbali mbali mfano mwenye shida kama ya Noela aidha utajiri.

"Matakwa? Matakwa gani hayo na wewe ni nani?.." Aliuliza Noela kwa sauti ya woga kabisa kwani sauti ile aliyoisikia ilimuogopesha sana kulingana na namna ilivyokuwa ikisikika.

"Ahahahahah Hahahahaha. Noela?.." Ilisema sauti hiyo huku ikijirudia mara mbili mbili. Punde Noela aliongozwa kwenye ile barabara iliyopambwa mafuvu, kitendo hicho ambacho kilimfanya Noela kupiga mayowe ya kuogopa. Muda mchache baadaye alijikuta yupo chumbani,chumba hicho kilionekana cha ajabu sana kwani kilipambwa kuliko kawaida. Pia katika chumba hicho ilisikika harufu ya marashi ambayo hayajawahi kusikika duniani. Noela alipagawa, muda huo huo Mlango wa chumba hicho ulifunguliwa akaingia mtu wa ajabu. Mtu huyo alioneakana sio binadamu wa kawaida, alikuwa na kichwa chenye mapembe, mwili mkubwa huku sehemu mbali mbali za mwili wake yakionekana magamba ya nyoka. Mbali na hayo, mtu huyo meno yake yalionyesha ni meno ya dhahabu lakini vile vile masikio yake yalikuwa yamepanda juu japo macho yake yalikuwa ya kibinadamu. 666,ndio namba zilizoandikwa kwenye paji la uso wa mtu huyo.

"Karibu Noela, mimi ndio mtu pekee nitakae kutatulia tatizo lako" Alisema mtu huyo huku akimsogelea Noela pale kitandani. Noela hakusema jambo zaidi ya kuogopa kutokana na namna alivyokuwa akitisha, hivyo alijinyanyua mpaka kitandani akakimbilia ukutani huku akionyesha ishara ya kukataa jambo hilo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Noela siku nzima umehitimisha, na hii ni siku ya pili tangu uingie Tropea. Tambua unamuda mchache sasa kuendelea kuwa huku sababu Duniani umeacha mwili wako na upo katika harakati za kuzikwa. Endapo kama hutouwahi mapema basi habari yako itakuwa imefika kikomo " Aliongezea kusema mtu huyo, maneno hayo yalimshtua Noela, hapo akajiuliza" Inamaana mimi hapa nilipo ni nafsi?.. " Kabla hajapata jawabu mbele yake ukutani ulitokea mwanga mfano wa TV, katika mwanga huo akaonyeshwa kinacho endelea Duniani. Hapo sasa Noela akapata kuona namna ndugu wanavyomlilia, umati wa watu ukiwa umehudhulia msiba, vile vile alipata kuuona mwili wake ukiwa katika harakati za kuhitimisha maandalizi ili ukazikwe. Alizidi kupagawa Noela ilihali muda huo mtu huyo wa ajabu alimfuata kitandani. "Noelaaaaaa.. Ndani ya kibuyu hicho kuna damu. Ondoka nacho hicho kibuyu mpaka nyumbani kwako hakikisha hakidondoki chini wala kulowana kwa kimiminika chochote. Kitunze vizuri kibiyu hicho kwani hakifai kuonwa na mtu wa ukoo mwingine. Ikifika saa sita usiku kunywa damu hiyo iliyomo ndani ya hicho kibiyu. Hali itakayo kutokea kubaliana nayo, vile vile hupaswi kupinga pindi utakapo hitajika kufanya jambo fulani. Sawaaaaaa" Maneno hayo yalijirudia kichwani mwa Noela,maneno ambayo aliambiwa na mizimu ya ukoo wao. Hivyo mara baada kuyakumbuka alitulia akisubiri huyo mtu atamfanya nini. Kilicho fuata hapo ni tendo la ndoa.

*******


ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog