Search This Blog

OSAKA MJI ULIO POTEA - 2

 






Simulizi : Osaka Mji Ulio Potea 
Sehemu Ya Pili (2)




"Muda mrefu nimefanya kazi na nyinyi pasipo kujua mimi ni nani, mimi sio mtu wa kawaida" aliongeza kusema Inspekta Jeff, lakini kamanda yule aliye muweka chini ya ulinzi hakutaka kusikia ngonjera hizo alikataa kuamini na ndipo alipo mwambia kwa sauti kali "Nitakupasua ubongo" maneno hayo yalimfanya Inspekta Jeff kuangua kicheko alicheka sana kisha akapotea mule chumbani. Kamanda yule aliyekuwa amemuweka chini ya ulinzi alitoka mbio, hakuamini kile alicho kiona "Hatimaye yametimia, yule hakuwa binadamu wa kawaida" aliongea kamanda yule.



Wote walishtuka, kila mmoja alipigwa na bumbuwazi ndipo walipo fungua albamu ya picha ili kutazama picha walizo piga naye ikiwa kumbikumbi. Lakini Inspekta Jeff hakuonekana kwenye yoyote ile, walichoka vibaya sasa wakaamini kuwa hakuwa binadamu wa kawaida. Kimya kilitawala, katika pekua pekua wakabahitika kuona kitambulisho cha Inspekta Jeff, walikiweka kwenye meza na kuanza kukitazama kwa umakini. Wakaona kuwa ni binadamu aliye zaliwa miaka takribani mia sita iliyo pita,

"Hii kali ya mwaka kamanda" kamanda mmoja aliongea. Upande wa pili alionekana Jeff akiwa amesimama katikati ya barabara usiku ule ule. Alingojea safari ya kurejea Osaka iwadie. Alionekana kuwa na furaha, alitabasamu kwani aliamini ile kazi aliyo tumwa na mfalme wa Osaka amesha ikamilisha, kwa kuwa aliambiwa kuwa pindi atakapo kamilisha mpango wa kumuua Saigon atarudishwa Osaka, sasa alingojea kwa shauku kubwa alitewe njia ya kurudi mji huo ulio potea.

"Mfalme tayari nimekamilisha kazi yako, sasa mbona muda unazidi kwenda sioni chochote" alisema Jeff alikuwa na uchu wa kurudi nyumbani Osaka. Alipokwisha kusema hayo Jeff, ghafla hali ya hewa ikabadilika, radi ikapiga na giza zaidi kutanda sanjari na umeme kukatika jiji lote.

"Jeff, najua fika una uchu wa kupata madaraka Osaka, ila sio rahisi kuyapata mpaka utakapo hakikisha Saigon umepoteza kwenye uso wa Dunia" sauti nzito iliyo ambatana na mwangwi iliongea. Inspekta Jeff alisthushwa na maneno hayo kwani yeye alijua fika Saigon ameuawa kwenye ajari ile mbaya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mbona sielewi, inamaana hamjaona kile kilicho tokea?" alihoji Kwa taharuki kubwa.

"Ahahaha hahaha" mtu huyo aliyekuwa akiongea na Jeff aliangua kicheko, cheko la kutisha ambalo alipo hitimisha akasema "Katika ajali ile wamekufa watu wamesalia watu wawili tu, Saigon hajafa lakini pia kuna binadamu wa kawaida naye kanusurika kifo, na zaidi ile Pete uliyo takiwa kuirudisha Osaka ipo chini ya mwanadamu. Siku zote binadamu ni kiumbe dhaifu nenda, rudi mahali pale ilipo tokea ajali, kachukue pete ile kabla yule mwanadamu hajatoweka nayo " hapo Inspekta Jeff akakumbuka kitu, mbali na kumuua Saigon lakini pia alitakiwa achukue pete aliyo kimbia nayo Saigon. Hivyo basi, pasipo kilemba mwandika, alikimbia kuelekea kule ilipo tokea ajari, kama ilivyo ada alipotea kila hatua moja. Alipo fika sehemu ile alimuona Alexandra akichemea akiishia zake huku nyuma Saigon akimfuata "Itunze pete hiyo, ni pete yenye bahati sana. Inaweza kuyabadilisha maisha yako sawa sawa Alex" aliongea Saigon huku akivuja damu sehemu mbalimbali ya mwili wake. Lakini muda mchache baada kusema hayo, ghafla akasikia upepo mkali mithili ya kimbunga, upesi Saigon akageuka akamuona yule yule adui yake wa kuitwa Jeff akimjia kwa kasi, kwa uwezo wake wa ajabu akajua dhamira ya Jeff kuwa amejia pete, na sasa akajiandaa kumkabili ili Alex afike mbali na atoweke na pete ile yenye miujiza..

"Alex kimbia brotheee!" alipaza sauti Saigon na kisha kunyoosha mkono juu, ghafla kwenye kiganja ukatokea upanga.. Upanga mkali uliotapaa nembo za MAFUVU.



Kwa kuwa Jeff alikuja kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, aliona ipo haja ya kuanza na kuitwaa Pete kisha amuue Saigon, lakini mambo yakawa si mambo Saigon alimtia vikwazo na ndipo naye alipo amuwa omba siraha kabambe kutoka Osaka ikiwa muda huo Alexandra akizidi kutokomea na pete kutoka Osaka, lakini punde si punde nguvu zilimuishia kijana huyo akashindwa kuendelea na safari hali ya kuwa pambano likipamba moto baina ya Saigon na Inspekta Jeff. Jeff aliihitaji Pete kwa vyovyote vile..



Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, ugomvi ule wa Saigon na Inspekta Jeff uliendelea wakati huo Alexandra naye alianguka chini na kushindwa kuendelea na safari. Alianguka kando ya barabara, alikata tamaa kabisa huku moyoni akijua fika kifo ni halali yake. Lakini wakati yupo hoi bin'taabani ghafla kwa mbali aliona tochi mbili zikimfuata mahali alipo angukia, tochi zile hatimaye zilimfikia na kumuacha hatua kadhaa mbele zikasimama ilikuwa ni gari ndogo Toyata yenye tela nyuma, punde akashuka mtu akiwa amevaa koti kubwa jeusi, mtu yule akajongea pale alipo angukia Alexandra. Alipo mkaribia akachomoa tochi kwenye koti alilovaa akaiwasha na kummulika akapata kumuona Alexandra akiwa na majeraha mbali mbali usoni na sehemu nyingine ya mwili wake zikiwa zimetapakaa damu, damu nyekundu na damu ya kijani pia. Mwanaume huyo alishtuka, akatazama kulia na kushoto huku akiwa na wingi wa wasi wasi wakati huo Alexandra akiomba msaada kwa sauti ya chini kabisa.

Mwanaume huyo alikuwa ni bubu yaani hawezi kuongea, roho ya huruma ikamtanda akachuchumaa akamshika mkono kisha akanyanyuka moja kwa moja mpaka kwenye gari lake. Akawasha gari na kuondoka naye.



Mlipuko mkubwa ulisikika, mwanga mkali ukapaa angani. Gari lile lililopinduka likateketea na vijana wale walio nasa mule ndani, huku upande wa pili nako mambo yalikuwa si mambo baina ya Saigon na Inspekta Jeff binadamu wa ajabu waliopo kwenye uso wa dunia wakitokea Osaka.

Walipigana kwa siraha za ajabu ajabu, kila mmoja alionyesha umahiri lakini Jeff alionekana kukata pumzi jambo ambalo lilipelekea Saigon kumudu pambano kwa umahiri mkubwa.



"Jeff sio rahisi kupigana na mimi, hili ni funzo tosha kwako na wale walio kutuma uje kunifuatilia hapa duniani" alisema Saigon kwa sauti yenye uchovu iliyojaa ushujaa ndani yake, naye alikuwa hoi bin'taabani shauri ya kuvuja damu nyingi sehemu aliyo pigwa risasi.



"Ahahaha hahaha" Inspekta Jeff aliangua kicheko akiwa chini hata asiwe kunyanyuka. Alicheka sana, cheko la ajabu ambalo lilizua hali ya taharuki katika jiji lile la Arusha usiku ule wa manane. Tetemeko lilizuka, manyunyu ya mvua kwa mbali yakaanza kushuka sanjari na Ngurumo nzito kupaza mara mbili zaidi ya awali.



Kwenye kiganja chake cha mkono wa kulia alikuwa ameshika kitu, kitu hicho kilimpa ujasiri wa kujiamini jambo ambalo lilipelekea kuangua kicheko.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sitokufa Saigon bali wewe ndio utakufa, zaidi umemponza yule binadamu uliye mkabidhi pete" alisema Jeff sambamba na kunyanyua mkono wake ule ule ulioshika kitu. Ilikuwa ni sindano yenye dawa ya kuongeza nguvu. Saigon alipo iona sindano ile alishtuka, upesi akatazama upande wa kulia kwenye kifua mahali kuwa ameihifadhi.

"Mshenzi sana wewe, umejua kunihadaa lakini Jeff tambueni kuwa ipo siku Osaka itapotea moja kwa moja" alisema Saigon baada kuona ile sindano ya kuongezea nguvu aliyo kuwa nayo ipo kwenye mikono ya Jeff.

Inspekta Jeff akajichoma sindano ile, akagugumia maumivu akapiga yowe kisha akasema "Muda wako umekwisha, duniani haupo wa Osaka hutokuwepo, kazi nyepesi niliyo baki nayo" kwisha kusema hayo, radi ikamlarua Saigon, akasambalatika vipande viwili. Baada ya jambo hilo, Jeff akacheka punde si punde akapotea mahali hapo. Sasa hali ya hewa ikawa shwari kabisa, umeme ukarejea kwa mara nyingine tena sambamba na tetemeko lile kuyeyuka.



Palipo pambazuka karibu vyombo vyote vya habari viliripoti kuhusu maajabu yaliyo tokea usiku ulio pita, kilicho washangaza zaidi ni kuona damu ya kijani iliyo thubutu kupausha eneo ilipo dondokea.

Wakati jambo hilo likiacha watu midomo wazi, kwingineko katika nyumba moja katikati ya jiji lile palikuwa na mzozo mkubwa ukiendelea.

"Huu ni upuuzi kabisa, mtu huyu tukiendelea kumfuga ataweza kutuletea matatizo, nakuomba jioni ya leo kamtelekeze sehemu yoyote ile la sivyo nitakufukuza kazi" aliongea mtu huyo kwa sauti ya juu, alikuwa ni mwanamke wa makamo, maneno hayo alikuwa akimwambia jamaa yule asiye weza kuongea japo kusikia alisikia vizuri, jamaa huyo alijikuta akiingia kwenye mgogoro na bosi wake baada kumpa msaada Alexandra, aliitwa Bula.



Bula akatikisa kichwa ishara ya kukubaliana na matakwa yake.

"Jifunze sio kila mtu lazima kumpa msaada, ipo siku msaada wako utakutia matatani. Je, kama mtu huyu amekuja kutupepeleza tutaishi wapi? " aliongeza kusema mwanamke huyo na kisha kuingia chumbani kwake, moyoni alikuwa na mashaka juu ya Alexandra, alidhani kijana huyo huwenda kuna kitu amekuja kukifanya kwenye nyumba yake, na hivyo akafikiria kumpoteza kabla muda ule alio mwambia Bula akamtekelekeze haujawadia. Upesi akampigia simu Don Dominic kwa dhumuni la kumtaka atume vijana wake ili waje wammalize Alexandra ambaye hali yake ipo mahututi, mwanamke huyo nguli wa kusambaza madawa ya kulevya hakujua kama kundi lile tata la Don Dominic limeangamia amesalia Alexandra peke yake, lakini pia hakujua kama Alex naye ni moja ya watu waliokuwa chini ya Dominic.



Simu ya Dominic iliita mpaka ikakata, mwanamke huyo hakukata tamaa kwa mara nyingine teka akampigia huku moyoni akiwa na shauku kubwa ya kutaka kuwasiliana naye ili ampe kazi hiyo ambayo ipo nje na biashara wanayo ifanya. Hatimaye simu ilipokelewa "Hello"



"Dominic kuna kazi hapa" baada simu kupokelewa mwanamke huyo aliongea kwa ujasiri mkubwa. Aliye pokea simu hiyo hakuwa Dominic kama mwanamke huyo alivyo dhania bali alikuwa ni yule yule binadamu wa ajabu kutoka Osaka Inspekta Jeff, ila sauti aliyo sikia mwanamke huyo ilikuwa ni sauti ya Dominic. Wakati mwanamke huyo anamueleezea hali halisi namna ambavyo muajiriwa wake alivyo msaidia mtu asiye mtambua, upande wa pili Bula alipo itazama Pete aliyovaa Alexandra, ghafla kwa mbaali akakumbuka jambo la miaka takribani mia tatu iliyo pita.. Zamani sana!



Alikumbuka namna gani alivyo kuwa akiishi Osaka, moyoni alitamani arudi kule lakini hakuwa na uwezo kwani aliletwa duniani kwa dhumuni la kufanya kazi ya mwanamke huyo aliye kuwa akimfuga. Aliitwa Madamu Maklina. Mwanamke ambaye alikuwa akijishughulisha na kazi ya kuuza madawa ya kulevya, mwanamke huyo aliishi na Bula pasipo kujua kuwa ni mtu wa ajabu aliye toka Osaka.

Bula akatikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, moyoni alijua Pete hiyo imetoka kwa nani, hivyo akahitaji kujua wapi alipo mtu yule aliye mpa Pete kwani alimfahamu fika. Lakini wakati Bula anawaza jambo hilo, ghafla nje ya nyumba akasikia pikipiki ikiwasili mahali hapo. Punde si punde ikazimwa, kupitia kioo cha dirisha akamuona mtu akipita, machale yakamcheza upesi upesi akamfunika shuka Alexandra pale kitandani kisha akambeba begani akapitia mlango wa nyuma kwa dhumuni la kutoroka naye.



Kwenye gari lile analo tumia kusambazia madawa ya kulevya akamuweka, akaliwasha kisha akaondoka naye mahali hapo ikiwa upande wa pili Inspekta Jeff aliingia kuonana na Madamu Maklina, muda huo Jeff alikuwa kwenye taswira ya Don Dominic. Ghafla maongezi yao yalistishwa na sauti ya gari, kwa sauti ya juu Maklina akasema "Ndio huyo anamtorosha, kama umejizatiti maliza kazi mwenyewe Dominic" Madamu Maklina alisema huku akinyanyuka kwenye kiti akalisogelea dirisha akamuona Bula akiondoka na mtu yule aliyetaka amuue upesi akiamini kuwa uwepo wake unaweza kuharibu mikakati yake.

Kufumba na kufumbua Jeff alionekana nje, akawasha pikipiki yake ikagoma kuwaka, akarudia tena na tena. Safari hiyo ikakubali, hima akamkimbiza Bula. Nia yake ni kuipata pete ile aliyo kuwa nayo Alexandra, patashika nguo kuchanika ikazuka. Bula aliendesha gari kwa kasi ya ajabu huku Jeff naye akionekana kuongeza gia moja baada ya nyingine sanjari na kuacha hofu upande wa watu walio kuwa wakishuhudia kwa macho, mioyoni mwao wakahisi huwenda ni Senema inaigizwa.

Kupitia kioo cha pembeni cha gari (Side mirro) Bula akapata kumtambua mtu yule anaye mfuatilia. Akatikisa Kichw ishara ya kukubali jambo fulani kisha akakakunja kona kuingia barabara za uchochoroni, hivyo hivyo Jeff naye akaunga, hatimaye Bula akatokea barabara kuu kwa mwendo ule ule wa kasi, Jeff naye akatokea vilivyo wakati huo kwa mbali vikasikika ving'ora vya jeshi la polisi.



Mbele zaidi lilipita kundi la watu likimkimbiza mwizi muda ule, Bula hakuona hatari ya kuwagonga, alipita upesi lakini upande wa Jeff juhudi zake ziliota mbawa kwani jopo lile la watu lilikuwa limeshaivagaa barabara hivyo akashindwa kupenya.

"Nitawapata washenzi wakubwa nyinyi" alisema Jeff baada juhudi zake kuota mbawa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ndani ya hospital ya M. Meru, Bula akaingia na gari lake. Jopo la wauguzi likaleta kitanda maalumu cha wagonjwa chenye magurudumu manne. Akachukuliwa Alexandra akalazwa kwenye kitanda kile na kukimbizwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi (ICU). Bula alibaki nje akitazama usalama. Alikuwa na wasiwasi tele akidhania kuwa Jeff anaweza kuvamia wakati wowote. Wakati anawaza jambo hilo kutokea wakati wowote, ghafla akamuona mtu mtu kwa mbali akiambatana na nesi aliyekuwa ametoka kwenye moja ya wodi, mtu yule alionekana kuwa na mashaka, alitembea haraka haraka ikiwa muda huo huo Bula akafuata vile machale yalivyokuwa yakimcheza. Akamfuatilia ili amjue ni nani.



Naam! Alikuwa ni yule yule, kiumbe wa ajabu anaye jiita Inspekta Jeff. Baada ya tafuta tafuta ya hapa na pale hatimaye aligundua mahali alipo Bula na Alexandra.

Jambo la kwanza alimuua moja ya wauguzi kisha akachukuwa vazi lile alilokuwa amelivaa muuguzi yule akalivaa, kufumba na kufumbua akamuona muuguzi mwingine, akavuta akamkaba na kisha kumpa onyo.

"Kwanza lazima ujue mimi sio binadamu wa kawaida, nipo hapa kwa lengo moja tu" alisema Jeff, sauti aliyokuwa akiitoa ilikuwa nzito tofauti na ile aliyokuwa akiongea siku zote. "Wewe ni nani kwani, na unataka nini?" aliuliza muuguzi huyo ambaye yupo katika himaya ya Jeff.

"Utanijua tu lakini kwa sasa sihitaji maswali yoyote, fuata kile nitakacho kisema. Nenda kwenye wodi namba sita kuna mgonjwa, katika kidole chake kuna pete, nenda kumvue pete ile kisha niletee" alisema Jeff na kisha kumuachia muuguzi huyo ambaye alionekana kujawa na woga shauri ya sauti aliyokuwa akiitoa. Pasipo na kupoteza muda muuguzi yule alitii agizo, akaelekea kwenye wodi ile lakini alipo fika tu akakuta jambo lipo tofauti. Hakumuona mgonjwa, upesi akapanda ghorofa ya tatu akatazama chini kuiona ile gari iliyo mleta ikiisha zake.

Haraka akarudi kumpasha habari Jeff, naye akatoka upesi akadandia pikipiki yake, mambo yakawa ni yale yale. Baada ya mbio ndefu mwishowe gari la Bula likaishiwa mafuta, sasa akashuka ili akabiliane naye ana kwa ana.

"Bulaaa pole sana bro, mbio za sakafuni huishia ukingoni, mlishindwa kutambua kuwa kukimbilia dunia sio suruhisho. Afadhali nimekupata na wewe japo hukuwa kwenye lengo langu ila sitokuacha salama kama nilivyo shindwa kumuacha salama Saigon"



"Ahahahah hahahaha" aliangua kicheko Jeff mara baada kusema maneno hayo, alipo katisha cheko lake akachomoa siraha kali yenye miyonzi mikali tayari kwa dhumuni kumyeyusha Bula. Alitumia siraha ile kali akiamini kuwa ndio inayo weza kuamua Bula kwa kuwa sio binadamu wa kawaida. Alifanya hivyo kisha akamfuata Alexandra kwa dhumuni la kuchukuwa Pete ile, kabla hajamfikia Alexandra akazinduka kutoka usi.

Alihema haraka haraka, mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio.

"Osaka!" ndani ya akili yake akajisemea alistaajabu ndoto aliyoota, ndoto ambayo ilishamili mambo ya ajabu kutoka Osaka jina ambalo hakuwa kulisikia hata mara moja maishani mwake.



Ndoto hiyo iliupeperusha usingizi wake, kwa kuwa ilikuwa alfajiri hakuona haja ya kuendelea kuuchapa usingizi aliamka na kuingia mtaani kuendelea kusaka vibarua baada kufukuzwa kibarua alicho kuipata siku nne nyuma toka aingie jijini Arusha, kilikuwa kibarua cha kubeba zege, ugumu wa kazi hiyo ukampelekea kochoka hoi akalala usingizi mzito ambao ulipelekea siku iliyo fuata kuchelewa kibaruani, huo ndio ukawa mwanzo na mwisho wa kuendelea kufanya kazi hiyo, alifukuzwa, hata siku iliyo fuata alilala usingizi mnono ambao ulimfanya kuota ndoto mbalimbali, moja ya ndoto tata aliyoota ni hiyo ya kukutana na watu kutoka Osaka, jina ambalo hajawahi kulisikia.

Alfajiri ile angavu kabisa Alexandra alitoka kwenye moja ya kibanda alicho kuwa akipendelea kulala, akaingia mtaani kusaka kibarua kipya huku kichwani akiwaza ndoto ile ya aina yake.

Mpaka jua linazama hakuambulia chochote, alikosa kazi. Kazi ile ambayo ingeendana na elimu duni aliyo kuwa nayo. Lakini licha ya kuambulia patupu aliendelea kusaka, ndipo usiku mmoja wakati anarudi maskani kupumzika aliona kundi la vijana wasio pungua saba wakiwa wamesimama kando ya gari la kifahari. Pole pole Alexandra alijongea mahala pale ili ajue ujue kuna agenda gani inayo fanyika.

"Hakuna mafanikio yanayo kuja kirahisi mabraza, nipo hapa kuwapa maisha. Inataka moyoni lakini, vile vile unatakiwa uwe msiri na mjanja wa kukwepa mitego ya kipuuzi. Hii ni faida kwenu na kwa familia zenu. Je, mpo tayari?" wakati Alexandra akikaribia mahala pale, alisikia sauti ikisema maneno hayo, sauti hiyo ilitokea ndani ya gari lile la kifahari.

Maneno hayo yaliwatisha baadhi ya vijana wale, mmoja baada ya mwingine aliondoka kati ya vijana wale saba walibaki wawwili tu, Alexandra naye akajiunga jumla wakawa vijana watatu. Waliingia ndani ya gari lile kisha wakaondoka moja kwa moja mpaka kwenye moja ya jumba la kifahari, kazi kubwa waliyo kutana nayo ilikuwa kazi ya kuuza madawa ya kulevya. Kazi hatari. Kila mmoja akaogopa kufanya kazi hiyo, Alexandra akawa mstari wa mbele kuipinga kwa sababu alihofia kifo ikiwa wadogo zake wanamtegemea. Hivyo basi baada vijana hao kupinga kufanya kazi hiyo hatari, wakaambiwa hawawezi kuchomoka ndani ya jengo jumba hilo wakiwa hai...



"Sio jambo la kawaida kuondoka humu ndani, kila mmoja anatakiwa kufanya kile kinacho takiwa" moja ya watu waliokuwemo mahali hapo alisema sambamba na kuiweka sawa bastora yake.

Woga uliwajaa vijana hao, ili kulinda mioyo yao wakakubaliana na matakwa ya wanaume wale. Onyo kali wakatoa kwa yule atakaye kwenda kinyume na matakwa yao, kwa pamoja wakaapa kutofanya hivyo. Walifundishwa kazi namna inavyo takiwa kufanya, donge nono la pesa walipewa. Hapo ndipo vijana hao walipo shawishika, wakaamini hiyo ndio dili kabambe ambayo inaweza kuwatajirisha.



Naam! Baada ya miezi sita Alexandra yule sio huyu tena, alibadilika mbali na kuwa mlevi lakini pia alikuwa ni mtu mwenye roho ya aina yake. Kazi iliyokuwa akifanya ilimlazimu aingie kwenye maisha hayo, kwa kuwa pesa alikuwa nayo ya kutosha alipenda starehe, alitumia pesa kwa Malaya na kulewa ipasavyo. Alisahau kuwa kijijini kwao kuna watu wanao mtegemea, akasahau mpango wa kurejea japo kuwajulia hali.

Juhudi yake katika kazi hiyo ya kusambaza madawa ya kulevya, ikamfanya bosi wake kumpenda na kumuamini. Alimuona ni mtu sahihi wa kufanya naye kazi zaidi ipasavyo achilia mbali yule ambaye alishughulikia kazi ya kuwasaka vijana wa kufanya kazi hiyo. Ndipo jioni moja tulivu, Mr Jordan alimuita mezani Alexandra.



"Nafurahi kuona juhudi zako za kazi Alexandra, safi sana. Nakupongeza kwa hilo, ila kuna kazi kubwa nataka nikupatie" alianza kwa kusema hivyo Jordan.

"Ndio ahsante sana bosi, na pia nipo tayari kwenye hilo" aliitikia Alexandra. Jordan akampigia makofi, akatabusamu kidogo kisha akaongeza kusema "Nataka nikutumie nje ya nchi, kuna mzigo utatakiwa ukauchukue huko"

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Wapi huko bosi?" aliuliza Alexandra.



"Nchini Uturuki, kila kitu kipo sawa. Kuna watu wangu wengine kule watakupokea, utakaa kidogo ili ung'arishe macho kabla hujaanza safari ya kurejea Tanzania" alisema Jordan akiingiza na utani ndani yake. Wawili hao kwa pamoja waliangua vicheko.

Ilikuwa ni habari njema kwa kijana Alexandra, na sasa alingoja taratibu zote zikamilike kisha aanze safari ya kuelekea nchini Uturuki.

Hatimaye ile siku ya kuanza safari iliwadia, ilikuwa ni siku njema kwake wala hakuwa kuifikiria katika maisha yake, watu walio kuwa walimzunguka wakamtakia kila laheri.

Alifika salama salimini alipokelewa vizuri kabisa, alilala malazi mazuri huko Nchini Uturuki. Wakati wa kurejea alikabidhiwa mzigo wa madawa arudi nao nchini Tanzania. Lakini safari yake ilota mbawa baada kunaswa kabla hata hajakanyaga Airport. Na huo ndio ukawa mwisho wa kijana Alexandra, kijana aliye badirika upesi baada kuzama ndani ya jiji la Arusha kwa dhumuni la kutafuta maisha. Ufinyu wa elimu yake na uchu wa kusaka mafanikio ili aweze kuwasaidia wadogo zake inapelekea kumdumbukiza kwenye kazi ya kusambaza madawa ya kulevya, kazi hatari duniani ingawa ilimpa pesa ya kutosha ambayo nayo iliyeyuka kwa kuponda raha huku akidiliki kuwasahau kilicho msababisha kwenda jijini kusaka shilingi.



Mwisho wa yote anaishia jela, nje ya nchi yake. Alifungwa kwenye Gereza la Diyarbakir, Gereza linalopatikana nchini Uturuki, ni Gereza lenye mazingira ya ya kinyama. Wafungwa huuwana wao kwa wao, ukiwa mnyonge utalawitiwa bila kupenda, maisha magumu na yakishezi ndani ya Gereza lile ilimpelekea Alexandra kulia na kusaga meno, majuto yakawa mjukuu upande wake, kuna wakati alikata tamaa ya kuishi kabisa kabla ya hukumu haijafika, nayo ilikuwa ni siku ile ya kunyongwa. Alifungwa miaka sita sanjari na kunyongwa mpaka kufa, hivyo alingojea kifo tu. Lakini alipo kumbuka kuwa kuna damu aliyokuwa ameitenga inamtegemea alitamani kutoroka. Jambo ambalo ngumu sana ndani ya Diyarbakir kwani ni Gereza lenye ulinzi mkali.





Maisha ya Gereza yalimfanya Alexandra kupoteza furaha, aliwakumbuka wadogo zake, lakini pia alimkumbuka mpenzi wake. Kila siku alizidi kunyong'onyea, alimlaani Mr Jordan moyoni aliamini kuwa yeye ndio chanzo cha matatizo yote hayo.



Baada kuishi Gerezani kwa muda mrefu, hatimaye alipata rafiki ambaye naye alikuwa ni mfungwa, Mtanzania mwenzake aliyehukumiwa kifungo cha maisha. Kutokana na kuishi kwa muda mrefu ndani ya Gereza hilo alipewa cheo kikubwa cha kuwahubiria injili njema wafungwa wenye imani ya kikristo lakini pia mfungwa huyo alipewa jukumu la kuzika wafungwa hasa hasa wale wanao kufa kutokana na mauaji yanayo tokea katika Gereza hilo. Aliitwa Devis. Mzee wa Makambo, mwanaume anaye ishi jela kwa miaka mingi sana.

"Sioni haja ya kuendelea kuwa mnyonge kijana" siku moja jioni Devis alimwambia Alexandra, ilikuwa wasaa ambao wafungwa wote ndani ya Gereza walikuwa wamepumzika. Alexandra alionekana kujitenga, muda wote alionekana kuwa mnyonge. Alipo sikia sauti hiyo aligeuka nyuma yake akakutana uso kwa uso na Devis swahiba wake wa karibu ndani ya Gereza.

Kabla Alexandra hajasema neno lolote, mzee yule aliketi kando yake. Akaachia tabasamu kisha akaongeza kusema "Ni lini moyo wako utakuwa na furaha? Achia tabasamu japo la kinafiki, hesabu haya kama moja ya mapito yanayo kukabili maishani mwako"



Alexandra aliposikia maneno hayo alishusha pumzi ndefu kwanza kisha akasema "Sikudhania kama ningeishi maisha haya Devis, nahisi haya ni machozi ya wadogo zangu ambao niliwaacha mazingira magumu. Sijui wapo katika hali gani, lakini pia sitoweza kuwaona shauri ya hukumu hii niliyo pewa. Alaaniwe Jordan kwa kunileta huku mimi" alimaliza kwa kuangua kilio, moyoni mwake akahisi kumchukia maradufu Jordan lakini pia aliuchukia umasikini wake. Chozi na maneno yake ilimfanya Devis kujisikia tofauti, alimuonea huruma hasa kulingana na umri mdogo kabisa aliokuwa nao.

"Kama utaweza nisaidie ndugu yangu, nisaidie tafadhali ili nikiepuke kitanzi, nirudi salama nikaishi na wadogo zangu kwenye hali yoyote ile ya kimaisha" aliongeza kusema Alexandra huku kilio nacho kisikome.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Waooh! Nafikiri huu ndio muda muafaka wa kutimiza malengo yangu niliyo kuwa nayo miaka dahari iliyo pita, kwa kuwa nguvu ya kupambana kukamilisha lengo sina, basi huyu mtu atabeba jukumu hili" aliwaza kwanza Devis kabla hajamjibu Alexander juu ya kumpa msaada alio uhitaji.

Ndipo kwa sauti ya chini iliyo jaa simanzi ndani yake Devis akasema "Nipo tayari kukusaidia kama sio kusaidiana. Unanifahamu kwa jina la Devis, jukumu langu ni kuendeleza neno la Mungu ndani ya Gereza hili lakini pia nashughulika na mambo ya uzikaji. Ila mbali na hayo, awali nilikuwa mtumishi wa Mungu moja ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam zamani sana, nilipo fungua kanisa nilihitaji kupata waumini wengi ili niweze kunufaika, kupiga pesa ili kurejesha heshima yangu iliyo toweka uoesi baada kufukuzwa kazi kwenye moja ya kampuni ya kuuza na kununua magari. Maisha yangu yaliyumba kwa kasi, nilibaki kapuku maskini wa kutupwa, ndugu jamaa hata marafiki walinitenga, kuna wakati nilifikiria kujiua ili kukwepa husuda za watu, hata mke wangu alinikimbia shauri ya umaskini wangu. Kosoro mama yangu tu, mama yangu alinishika mkono akanitia moyo, baadaye akanishauri nifungue kanisa niombe kwa imani tena bila kukoma ili Mungu anifanyie wepesi kwa kila jambo" alisema kwa uchungu Devis, chozi likamtoka, hima akalifuta kisha akaendelea kusema, alikuwa akisimulia ufupi wa yale yaliyotokea miaka kadhaa nyuma "Lilikuwa zoezi gumu sana, niliambulia waumini wachache, jambo hilo likanikatisha tamaa kabisa, niliingiwa na wivu pindi nilipoona baadhi ya makanisa yakijaza watu, nikatamani kujua siri kubwa inayo tumika. Ndipo mchungaji mmoja alipo nidokeze kuwa pasipo kuwa na miujiza kamwe sitoweza kupata waumini, akaongeza kusema kuwa binadamu wa leo wanavutiwa na miujiza na sio kupayuka payuka hovyo Kanisani. Kwa hamu kubwa nilimuuliza mahala gani naweza kupata uwezo wa kuwa na miujiza hiyo, mchungaji yule akanijibu kuwa wapo baadhi wanatumia nguvu za giza kwa kumtegemea Alminat, lakini mwisho wao huwa mbaya sana, lakini kwa upande wako nakushauri nenda Osaka, kaibe pete, pete ile ina kila aina ya miujiza. Kama utafanikiwa kuipata pete hiyo dunia nzima itakujua na itakuheshimu " alisimulia Devis.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog