Search This Blog

TROPEA MJI WA WAFU - 3

 






Simulizi : Tropea Mji Wa Wafu
Sehemu Ya Tatu (3)




Bingo alijikuta yupo roho juu, aliutazama ule mporomoko roho ikasita kujitupa lakini alipogeuka nyuma akahofia wale watu na hivyo akapata ujasiri wa kujitosa. Wale watu hawakuweza kubaki kumtazama tu, vile vile nao walijitupa katika mporomoko huo. Ama hakika walipania kumpata Bingo sababu kwao binadamu ni chakula, tena chakula pendwa hasa. Akiwa na hofu dhofu lihali kijana Bingo aliweza kuogelea kwa mita kadhaa kutoka kwenye ule mporomoko, na mwishowe alifanikiwa Kufika nchi kavu ambapo alionekana kusafa kwa maumivu huku akiwa ameshika goti wakati huo akihema haraka haraka. Lakini wakati yupo katika hali hiyo, ghafla mtu moja aliinuka ndani ya maji. Mtu huyo alipotazama upande ule aliokaa Bingo walikutana uso kwa uso na Bingo. Bingo alishtuka ilahali mtu huyo alipiga mbizi,janja ambayo Bingo aliishtukia na hivyo akatoka mahali hapo akazama ndani ya msitu mwingine ambao wenyewe ulisheheni viumbe hai. Walikuwemo ndege, wanyama na wadudu pia. Bingo alitimua mbio kwa kasi ya kawaida akiwakimbia wale watu waliompania. Na mara baada kukimbia kwa dakika kadhaa hatimaye kijana aliishiwa nguvu alianguka chini wakati huo nyuma yake vikisikika vishindo vikisogea mahali alipoangukia, dhahili shahili Bingo alijua ni wale wale watu. Hivyo hofu ilimjaa lakini baadaye kidogo alijikuta akipata nguvu za kuendelea na harakati za kuwakimbia watu wale ambapo mbele kidogo aliona pango, humo humo Bingo alijitosa kitendo ambacho kiliwafanya wale watu kupitiliza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bingo alishusha pumzi, hata asiamini watu wale wamepitiliza. Hivyo alipumzika na punde usingizi ulimpitia alilala fo fo fo, alipozinduka hakujua ni saa ngapi sababu hali ya hewa ya msitu huo ilikuwa tofauti kabisa na hali ya hewa ya kawaida. Muda wote ilikuwa hali ya mawingu, hakuna jua wala mwezi.

"Inamaana Tropea bado sijafika?.." Ndio swali ambalo Bingo alijiuliza mara baada ya kuamka, lakini kabla hajapata jibu alishtuka kuona karatasi mbele yake. Karatasi hiyo ilikuwa imetapaka damu. 'Hiyo ni Ramani, ichukue ili ipate kukuongoza "Wakati Bingo anastaajbu kuona taratasi hiyo ilisikika sauti ukimwambia hivyo. Mtu aliyesema maneno hayo hakuonekana zaidi ya kusikika sauti tu. Hivyo Bingo hakuweza kukaidi maneno hayo, pole pole alipeleka mkono wake kuichukua hiyo karatasi, hatimaye akaitwaa mkono akaifungia kuitazama. All shangaa baada kuona bado hajafika hata robo ya safari yake, kitendo hicho kilimfanya kutoka mule ndani ya pango kwa kutumia Ramani hiyo aliendelea na safari.

Akiwa njiani, ghafla aliguswa bega. Hapo Bingo alisimama kisha akageuka nyuma kumtazama mtu aliyemgusa. Lakini hakuona mtu yoyote,hivyo aliendelea na safari yake ndani ya msitu huo mnene huku Ramani ikimuongoza vema. Bingo aliambaa katika msitu huo, alitembea bila kuchoka, ajabu alikuwa hasikii njaa wala kiu. Ila pindi safari hiyo ikiwa imekolea punde si punde alisikia ngurumo ya simba. Hapo Bingo alisimama akachomoa upanga wake kisha akatulia kusikiliza wapi inapotokea sauti hiyo. Ghafla mbele yake alimuona simba akimjia kwa kasi ya ajabu.. Hima Bingo naye alitimua mbio kumfuata huku akiwa amenyanyua juu upanga wake. Alipomkaribia alikunja magoti yake kisha akalaza mwili wake ilihali Simba naye akiwa tayari ameruka kwa niaba ya kumkwaruza Bingo kifuani lakini mpango wake ukawa umeenda kinyume sababu Bingo alionyesha umahilli wa kumkwepa. Hapo Bingo alisimama, kwa mara nyingine tena Simba huyo naye akajitayalisha kumkabili binadamu huyo ambaye aliona yupo vizuri kwa namna alivyomkwepa hapo mwanzo.

"Bingo fanya ulicho kifuata" Wakati Bingo anajiandaa kumkabili simba, alisikia sauti ikimuasa namna hiyo. Hivyo Bingo aliamua kutimua mbio, kitendo ambacho kilimfanya yule simba kumkimbiza. Punde mshale ulipita nyuma yake ukaenda kumpata simba kisha vicheko vikasikika. Si wengine bali ni watu jamii ya wale ambao walikuwa wakimkimbiza Bingo, watu hao walikuwa katika mawindo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Basi watu hao walikusanya pale alipofia simba, na mara moja shughuli ya kumuandaa ilianza wakati huo Bingo akishuhudia kwa macho yake akiwa amejificha ili asionekane.

Shughuli nzima ilipokamilika walimteaua mtu mmoja abebe mzigo wa nyama, ni kijana mdogo ndio aliyepewa jukumu hilo. Safari ya kurejea kwenye makazi yao ikaanza, na mahali alipokuwa amejificha Bingo ndipo walipopita. Hivyo Bingo akajikuta amekamatwa na hao watu.

********

Ni katika kijiji kidogo kabisa, watu hao walifika. Na ndio makazi yao na familia zao. Wake wakiwapokea waume zao ilihali watoto nao walishangilia urejeo wa wazee wao. Lakini kituko na jambo la kushangaza ni baada jamii hiyo yenye watu wa ajabu kumuona Bingo. Watu hao walimzunguka kijana Bingo huku wakishangaa kwa namna alivyokuwa, mtu mmoja alimgusa ajabu haraka sana alirudisha mkono nyuma wakati huo akilalama maumivu. Hali hiyo iliwashangaza watu hao, ndipo mmoja alimsogelea ili naye amguse. Hivyo hivyo alisafa na maumivu.. Amri ilitoka, ni sauti kubwa na nzito iliyopenya vema kwenye masikio ya Bingo ingawa hakujua watu hao wanaongea Lugha gani zaidi ya kuona watu wanasambalatika akajikuta yupo pake yake katikati ya uwanja. Muda mchache baadaye alimuona ajuza akijikongoja kuja mahali hapo aliposimama, na kabla hajamkaribia ajuza huyo alimuuliza Bingo "Unaitwa nani?.."

"Naitwa Bingo.."

"Nani aliyekuleta huku wakati hustahili kukanyaga mahali hapa? Je, ukijitazama ulivyo, unaendana na sisi?.." Alirudia kuhoji ajuza huyo kwa lugha ambayo Bingo alielewa, ni ajuza ambaye alionekana kuzeeka sana huku ngozi yake ikiwa mfano wa gamba la nyoka, macho yake nayo yakishabiliana mno na macho ya simba. Bingo alikosa jibu ilihali muda huo huo alisikia sauti ikimwambia" Hapo ndipo utaweza kujihami kutumia panga lako "Sauti hiyo ilipokwisha kumwambia hivyo Bingo, Ajuza yule alipotea kufumba na kufumbua Bingo akajikuta yupo sehemu tofauti kabisa. Ni kwenye jengo kubwa na la zamani, juu ya jengo hilo aliona ubao ulioandikwa Spiritual prison(Jela la kiroho)

"Wapi hapa?.." Alijiuliza Bingo baada kuliona jengo hilo ilahali mlango mkubwa wa hilo jengo ulifunguliwa, nguvu ya ajabu ilivuta mpaka ndani kisha mlango ukajifunga. Humo ndani Bingo alipata kuona ulingo mkubwa huku watu wakipigana, sio watu wakawaida sababu walionekana kutumia nguvu za kichawi.. "Hapo Bingo utakiwa kuwa makini, chini ya ulingo kuna mikuki ya sumu, Chunga usidondokee huko. Lakini pia vile vile mtu utakaye pigana naye hakikisha asikuguse hata kidogo,miili ya watu hao inasumu kubwa sana.. Hiyo ni hatua ya kwanza, bado unasafari ndefu ya Kufika Tropea.. "Ilisema sauti hiyo, sauti ambayo ilimfanya Bingo kushusha pumzi wakati huo akijiandaa kuchukuwa upanga wake ili akabiliane na mtu atakaye tunukiwa ajabu upanga haukuwepo!



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Bingo alishtuka baada kuona upanga wake haupo kwenye kala, hofu ilimuingia akiwaza ni namna gani ataweza kulimudu pambano pasipokuwa na upanga kwake. Na wakati yupo katika hali hiyo ya hofu, kule ndani ya ulingo ule uliozungushiwa nyavu za chuma ilihali chini ya ulingo huo pakiwa na utitiri wa simba na chui, mpambano ulikuwa ukiendelea kwa wale watu wa ajabu. Wote kwa pamoja walikuwa wakitumia panga za kichawi ambazo zilipambwa na nembo mbali mbali za mafuvu. Bingo alishusha pumzi ndefu, bado hofu dhofu lihali ilizidi kutawala moyo wake lakini mwishowe alishusha pumzi ndefu kisha akainamisha uso wake kuzitazama zile ndondi. Shangwe za hapa na pale zililipuka, mtu yule ambaye alionekana kuutawala vema ulingo alishangiliwa kwa nguvu zote. "Eeh Mungu nisaidie" Alisema Bingo ndani ya nafsi yake, ajabu maneno hayo aliyojisemea yalipelekea ngumi zilizokuwa zikiendelea kustishwa mara moja na kisha mkuu wa mapigano hayo alimuamuru mpiga ngoma maalumu aliyekuwa akiruhusu mapigano kutuliza ghasia iliyokuwa imetokea. Ndipo ngoma ikapigwa halafu mkuu huyo akaongea maneno ambayo Bingo hakuweza kuyaelewa zaidi ya kujikuta amekamatwa na watu ambao walikuwa binadamu wa kawaida kama alivyo yeye. Watu hao walimpeleka Bingo kwenye chumba maalumu ambacho kilikuwa bucha kwani chumba hicho kilikuwa na ndoano kubwa za kutundukia nyama vile vile kilitapakaa damu mbali mbali huku baadhi ya viungo vya binadamu vikiwaa vimezagaa kila kona.. Bingo alizidi kuogopa wakati huo huo mtu mmoja kati ya wale walimfikisha ndani ya chumba hicho alimuuliza "Unajua upo wapi hapa?.."

"Hapana sijui" Alijibu Bingo kwa sauti ya upole iliyojaa woga ndani yake. Ajabu watu hao waliangua kicheko. Walicheka sana kisha mtu wa pili akaongeza kusema "Hapa haupo Duniani, huu ni utawala mwingine na sio utawala wa kiungu muumba mbingu na nchi.. Hivyo basi unapofika Maeneo haya hustahili kabisa kumtaja Mungu wako.."

"Kwanza umefuata nini huku?.." Mtu wa tatu alihoji ilihali muda huo kijana Bingo akionekana kuwa na sintofahamu fahamu juu ya mambo hayo yanayomkabiri.

"Hapa nimepita tu, safari yangu mimi ni kuelekea Tropea.." Alisema Bingo.

"Tropea?.." Mtu wa nne alitaharuki. Kwa kujiamini kabisa Bingo akajibu "Naam!.."

Jibu hilo la Bingo liliwafanya wale watu wanne kutazamana wakakonyezana kisha mmoja wao akamwambia Bingo "Safari bado unayo ndefu kijana, lakini kutokana na kuvunja taratibu za himaya hii nafikiri safari yako imekomea hapa.." Maneno hayo yalims Bingo, ghafla kijasho chembamba kikaaza kumtoka lakini muda mchache baadae akauliza "Kwanini sasa ndugu zangu?.."

"Ukiwa huku hutakiwi kumtaja Mungu, nadhani uliona namna mkuu alivyositisha mapigano sababu yako wewe. Lakini pia mbali na hilo, umetia hasara baadhi ya rasili mali za huku, kuna baadhi ya vitu vimeteketea kwa moto vile vile umesababisha maafa makubwa..na ndio maana umeletwa katika chumba hiki cha mateso. Utakatwa kiungo kimoja kimoja mpaka unakufa "

" Hapana msinifanyie hivyo, nyinyi ni binadamu wenzangu.. Tafadhalini nisaidieni jamani nipo chini ya miguu yenu " Hapo Bingo alipiga magoti chini akiomba msaada kwa watu hao ambao aliona wanaweza kumsaidia juu ya kile alichokosea. Watu hao walicheka kwa mara nyingine tena kisha mtu wa pili akamwambia" Usajili lakini utatakiwa kufanya kile tunacho kitaka. Je, upo tayari?.. "

" Ndio nipo tayari ".

" Ahahah hahaha hahahaha. Vizuri sana kijana. Tulikuja na mtu wetu kwa niaba ya kupigania pesa katika kitongoji hiki. Lakini mtu watu kauliwa, kwahiyo basi wewe itabidi ushike nafasi yake ili turudi Duniani na mali za kutosha kama yalivyokuwa malengo yetu. Ila, chunga sana usirudie kosa.. " Aliambiwa hivyo Bingo,ambapo alishusha pumzi ndefu akasimama akanyoosha mkono kuwapa shukrani watu hao lakini ajabu hao watu walikataa na mmoja akamwambia" Haturuhusiwi kushikana mikono,nyota zatu zipo katikati ya viganja vyetu "

" Sawa naitwa Bingo.. "Alijibu Bingo..

" Vizuri sana karibu ujumuike nasi.. "

********

Hapo sasa mke wangu Millander nikapata nafasi ya kuungana na wale watu ambao walikuwa binadamu wenzangu, lakini moyoni bado nilikuwa na hofu sababu nilijuliza nitapigana vipi kwenye ulingo hali ya kuwa upanga wangu umepotea kimaajabu. Na vile vile jambo lingine ambalo lilinipa hofu na kujikuta nikiwa na wingi wa woga ni baada kuambiwa kwamba nifanye kile watakacho kitaka. Basi niliambatana nao, tukatoka ndani ya chumba kile ambacho kilionyesha dhahili shahili kweli kweli ni chumba cha mateso, tena mateso yenyewe sio ya kawaida. Ni mateso ya kukatwa viungo mbali mbali.

"Daah! Pole sana mpenzi wangu, hivi unaweza kuniambia baadhi ya viungo ulivyoviona" Aliuliza Millander, mkewe Bingo ambaye muda wote alikuwa makini kumsikiliza mumewe akimsimulia mkasa ambao ulimpeleka Tropea mji uishio wafu. Na hiyo yote ilitokea baada Millander kumtilia wasi wasi mumewe kutokana na nyakati za usiku Bingo hutoweka nyumbani, akirudi hurudi akiwa ametapakaa damu baadhi ya sehemu ya mwili wake huku akinukia ubani.

"Ahahah ah" Alicheka kwanza Bingo, akifurahishwa na swali la mkewe. Baada kukatisha kicheko chake akasema "Viungo vingi tu, kuna sehemu nyeti za kike na kiume,viganja na nyao mara vichwa. Yani viungo vingi tu"

"Laah! Ama kweli Dunia inamambo. Enhe ikawaje sasa?.." Alihoji Millander. Bingo naye akaendelea kusimulia.

**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Waliambatana moja kwa moja mpaka kwenye chumba kingine ambacho huko napo palikuwa na watu wengine, binadamu wa kawaida. Bingo alijikuta akitabasamu wakati huo huo watu hao walimkaribisha kwa bashasha huku kila mmoja akijtambulisha jina lake.

"Mimi jina langu Bingo" Alisema Bingo baada watu hao kumaliza kujitambulisha kwake.

Hatimaye siku ambayo Bingo anatakiwa kupigana ikawaidia, mashabik wengi walijaza ukumbi ule wenye ulingo wa kutisha. Ndondi za ufunguzi ziliendela mahala pale, watu hao ambao hawakuwa binadamu wa kawaida walichapana kama hawana akili vuzuri. Na pambano lilipoonekana kupamba ubabe na ubishi wa hapa na pale, Bingo alijikuta akiwa roho juu akihofia uhai wake akilinganisha na hali tete aliyomuacha nayo mama yake duniani. Punde ngoma nzito ilipigwa,mpambano wa ufunguzi ukamalizika na hivyo nafasi ifuatayo ni kwaniaba Bingo na mpiganaji mwingine ambaye hakumfahamu. Kwa mara nyingine tena ngoma hiyo ilipigwa, ndipo shangwe zilipolipuka, muda mfupi baadae akajitokeza Jitu kubwa linye milaba minne, macho ya Jitu hilo yalishabiana vema na macho ya simba huku baadhi ya sehemu ya mwili wake akiwa na magamba ya nyoka. "Ahahaha hahaha ha!.." Jitu hilo lilicheka, kicheko ambacho kilizua tetemo fulani, na kila lilipopiga hatua kishindo kizito kilisikika. Lilipofika katika ya ulingo lilinyanyua mkono wake juu, ghafla katika kiganja chake ulitokea upanga mkubwa wenye nembo za ajabu ajabu.. Hapo sasa lilimsubiri mtu anayepigana naye siku hiyo.. "Bingo.." Mtu mmoja ambaye ni binadamu,alimuita Bingo. Bingo akaacha kulitazama Jitu lile la kutisha akamgeukia mtu yule aliyemuita. Ndipo huyo mtu akamwambia "Kazi kwako sasa..."

"Unamanisha nikapigane naye?.." Alihoji bingo kwa taharuki kubwa.

"Ndio.. Na sio kupigana naye tu, bali unatakiwa kushinda ili safari yako ya kwenda Tropea iweze kuendelea.." Alijibiwa Bingo, maneno ambayo yalimshangaza wakati huo akijiuliza atakabiliana vipi na Jitu hilo kubwa la ajabu..



Bingo alishtuka sana baada kuambiwa apigane na lile Jitu la ajabu, akawaza ni namna gani ataweza kulimudu pasipokuwa na upanga wake. Pumzi ndefu alishusha kisha akafunga zipu ya koti lake ambayo hapo awali alikuwa ameifungua upande wa kifuani,ilihali muda huo shangwe ziliendelea kulipuka katika ulingo ule, watu wale wa ajabu walikuwa wakilishangilia lile Jitu ambalo lilionyesha kuwa na uchu wa kupambana. Hapo sasa Bingo alishuka kwenye ngazi inayoelekea ulingoni, punde si punde alifika kitendo ambacho kilionyesha kama kituko katika ulingo huo. Vicheko mbali mbali vilisikika wakimcheka Bingo, bila shaka walionekana kumdharau kijana huyo kutokana na umbile lake lilivyo ndogo wakati huo akitegemea kupigana na Jitu lenye miraba minne. Ngoma ilitumbuizwa kuashiria pambano kuanza,ndipo hapo patashika lilipoanza. Jitu lile lilirusha upanga wake kwa nguvu na umakini wa hali ya juu lakini Bingo alichokuwa akikifanya ni kukwepa kwa kuruka kwenye uzio wa nyavu zile za chuma huku akipata upenyo anarusha mateke kadha wa kadha, mateke ambayo si chochote si lolote kwa hilo Jitu.

Mwendo ukawa huo huo, hatimae mzunguko wa kwanza ukafikia tamati, bila mshindi kupatikana.

"Bingo unatakiwa kukaza buti, sababu sheria ya huu ulingo hamatakiwi kutoka wote mkiwa hai. Lazima mmoja afe ndipo apatikane bingwa. Hivyo pambana kwa nguvu zote kijana sawa sawa?.." Alisisitiza mmoja ya wale watu waliomtuma Bingo kupigana. Jamaa huyo aliongea kwa sauti ya juu sana sababu ya fujo zilizokuwa zikiendelea mle ndani. Bingo alikubali kwa kutikisa kichwa kisha ngoma kwa mara nyingine tena ikalia kuashiria kwamba mzunguko wa pili unatarajia kuanza. Kama ilivyo ada kwa watazamaji waliweza kushangilia kwa nguvu zote, muda huo huo Jitu lile lilikuwa tayari lipo katika ya ulingo, safari hiyo halikuwa na upanga bali mkononi mwake lilishika rungu lenye misumari. Punde mpambano ukaendelea, hatari kwa kijana Bingo. Lile Jitu lilitembeza rungu lake kwa ustadi wa hali ya juu kiasi kwamba Bingo akizubaa basi habari yake itakuwa imekomea hapo. Lakini Bingo aliweza kukwepa, ila mwishowe alijihisi kuchoka kwani ikumbukwe alikuwa akipigana na mtu wa ajabu yani sio mtu ambaye sio wa kawaida.

Hivyo hali hiyo ilimpelekea Bingo kuishiwa nguvu, hatimaye alianguka chini kitendo ambacho kililifanya lile Jitu kucheka sana wakati huo likinyanyua juu rungu lake ili limalize mchezo. Pale alipo angukia Bingo, kumbukumbu zake zikarudi nyuma.akakumbuka kuwa hapo alipo yeye ni nafsi ingawa yupo katika hali ya kibinadamu. Sio mfu wala sio kiumbe cha ajabu kama ilivyo hao aliowakuta katika kitongoji hicho. Mwili wake upo duniani na pia unafanyiwa maandalizi ya kuzikwa ingawa mzee Ndelo alimwambia kuwa atafanya juu chini ili kuhakikisha mwili huo hauzikwi mpaka pale atakapo rejea kutoka Tropea. Pia mbali na hayo, Bingo alikumbuka kuwa bado anakazi ngumu na nzito ya kuhakikisha anakanyaga mji wa wafu ili kuikomboa ngome ya baba yake, zoezi ambalo litampelekea kupata dawa ya kumponyesha mama yake, hivyo basi ni wajibu wake kupigana ipasavyo ili safari yake iweze kuwa safari ya matumaini. Matukio hayo Bingo aliyakumbuka kwa haraka haraka ndani ya kichwa chake, ghafla akafumbua macho yake akajihisi kupata nguvu ilihali muda huo huo lile Jitu tayari lilikuwa limeshanyanyua rungu juu likingojea nusu sekunde tu limalize mchezo. Kweli punde tu kwa nguvu lilishusha rungu hilo ambapo Bingo aligaagaa pembeni, rungu hilo likawa limepiga sakafu, kitendo ambacho lilipelekea sakafu kupasuka na punde si punde tetemeko la ajabu lilizuka, kwenye upenyo wa nyufa, Bingo alibahatika kupenya ambapo alidondokea kwenye tope. Muda huo sasa bado baadhi ya majengo yaliendelea kubomoka huku vifo navyo vikiendelea kuzuka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

**********

Hapo sasa mke wangu Millander nikawa nimepotezana na wale watu ambao walinitaka nifanye kile wanacho kitaka. Niliendelea kukaa kwenye lile tope ambalo liliishia usawa wa kiuno changu, na jambo ambalo nilikuwa nalo makini ni kuilinda ramani ya kunifikisha mji ule wa wafu. Lakini wakati nipo ndani tope hilo mara ghafla nikawekwa chini ya ulinzi na watu wengine tofauti na wale niliokuwa nao hapo mwanzo kuacha wale binadamu wenzangu. Watu hao walikuwa na mapembe, miguu mikubwa ingawa kimaumbile ni wafupi sana. Ajabu masikio yao yalikuwa marefu sana. Walikuwa wanne. Basi walitoa kwenye tope lile wakanipeleka kwa mkuu wao ambaye naye alifanana nao kila kitu,lakini pia lugha waliyoongea sikuweza kuielewa ila tu jambo la kwanza walinivua koti langu halafu wakanipeleka kwenye chumba mahususi ambacho ndani palikuwa na giza nene. Daah! Millander we acha tu, nilipagawa sana sababu koti walibaki nalo halafu kwenye mfuko wa koti lile kuna ramani yangu ambayo itanifikisha Tropea. Niliwaza nitafikaje sasa kwenye ule mji wa wafu? Mungu si Athumani, muda mchache baadaye nilitolewa ndani kile chumba, nikapelekwa kwenye mbuga kubwa sana mfano wa jangwa. Nilishangaa sana sababu eneo hilo lipo tofauti kabisa na lile la mwanzo,lakini yote kwa yote sikutaka kujaji saana kwa sababu nilijua kwanza sipo duniani kwahiyo mambo hayo inabidi tu niyachululie kawaida. Hivyo pumzi ndefu nilishusha baada kumaliza kuvaa koti langu, punde mwanadada mmoja hivi alinisogelea halafu akaniambia "Unaona hii mbuga! Unatakiwa ukimbie kwa namna uwezavyo, huu ni mchezo mepesi sana unatakiwa kushinda ili utetee uhai wako" Sauti hiyo ya huyo mwanadada ilipenya vema masikioni mwangu lakini si kama nilikuwa nasikia sauti ya kike bali sauti niliyokuwa nasikia ilikuwa ya kiume, nene na nzito.

"Enhee ikawaje sasa maana daah! Mtihani kweli kweli.." Alihoji Millander. Hapo Bingo alishusha pumzi kwanza kisha akaendelea kusimulia.

*********

Filimbi ilipigwa, hapo Bingo akaanza kutimua mbio, ajabu nyuma yake jangwa lile lilikuwa likimomonyoka. Bingo aliposimama aligeuka nyuma, alishtuka kuona jangwa likimomonyoka huku moto nao ukizuka katika shimo hilo. Hapo sasa Bingo akaendelea na safari yake ya kukimbia kwa kasi ya ajabu, lakini siku zote mbio za sakafuni huishia ukingoni.. Ndivyo ilivyokuwa kwa kijana Bingo, kwani baada kukimbia kwa muda mrefu hatimaye mbele yake njia mbili tofauti. Njia moja ilielekea kulia na nyingine ilielekea kushoto. Hivyo basi Bingo akaona hapo ndipo pa kuongozwa na ramani, lakini alipoingiza mkono mfukoni hakuikuta ramani yake..





"Ramani yangu imepotelea wapi?.." Alijiuliza kijana Bingo baada kujikuta ramani haiko kwenye himaya yake. Muda huo lile jangwa liliendelea kumomonyoka kuelekea pale aliposimama Bingo hali ya kuwa naye akishindwa kuchagua njia ya kwenda sababu palikuwa na njia mbili. Njia moja ilielekea kulia na nyingine ilielekea kushoto, hivyo akawaza endapo kama ramani angelikuwa nayo basi ingemuwea rahisi sana kuamua pakwenda.

"Hapa liwalo na liwe" Alijisemea Bingo ndani ya nafsi yake kisha akatimua mbio kuelekea njia ya kulia, njia ambayo mbele zaidi ilitokomea kwenye msitu mzito wenye miti iliyosheheni miba, wadudu wakali pasipo kusahau wanyama mbali mbali wa mwitu. Hapo sasa Bingo alishusha pumzi ndefu, akakaa kwanza chini wakati huo akitafakari namna ya kufika Tropea ihali akiwa hana ramani ambayo ingempa muongozo. Lakini wakati yupo chini mara ghafla aliguswa bega,ambapo alishtuka sana akatoka kwenye dimbwi la mawazo akamgeukia mtu huyo aliyemgusa. Ni mtoto mdogo, mwenyewe umri wa miaka kumi na mbili. Mtoto huyo alimshika Bingo mkono kisha akamvuta pasipo kusema naye neno lolote. Wawili hao waliambaa msitu kwa msitu mpaka kwenye kilele cha mlima, ambako huko Bingo alipata kuona mtu mkubwa mbele yake, na katika mto huo ilionekana boti ndogo ikiwa na watu ndani yake. Bingo aliitazama boti ile kwa dakika kadhaa kisha akarudisha uso wake kumtazama yule bwana mdogo aliyemleta kwenye kilele hicho cha mlima. Hapo sasa huyo mtoto alimuonyesha Bingo kiganja chake, ambapo Bingo akapata kuwaona wale watu waliomo ndani ya boti huku mmoja wao akiwa makini kuitazama ramani ya kuelekea Tropea..

"Alaah! Kumbe ramani walibaki nayo pindi waliponivua koti langu? Hapa hakuna kuogopa tena liwalo na liwe" Alijikuta akijisemea hayo Bingo ndani ya nafsi yake mara baada kugundua kuwa ramani ilibaki kwa wale watu waliomuamuru akimbie kwenye jangwa. Lakini nao vile vile hawakuwa watu wa kawaida.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Hahaha hahahaha" Aliangua kicheko bwana mdogo huyo kisha akapotea, Bingo alishtuka ila hakuona haja ya kupoteza muda, haraka sana alishuka kwenye kilele kile cha mlima, kwa kasi ya ajabu akaifuata ile boti ili apate kuichukua ramani yake. Haikuwa kazi nyepesi, lakini mwishowe alipata Kufika kwenye huo mto ambapo boti hiyo ilikuwa imesimama huku ndani sherehe mbali mbali iliendelea. Hapo sasa Bingo akaizunguka boti, akapita nyuma moja kwa moja akazama mpaka ndani ambapo aliliona sanduku la dhahabu likiwa wazi, na ndani ya sanduku hilo ilikuwemo ramani yake. Hakika pumzi ndefu alishusha kijana kisha pasipo kupoteza muda alichukuwa ramani yake akatoka ndani ya boti hilo huku akiwatazama jicho upande watu wale waliokuwa wakisherehekea.. lakini kabla Bingo hajatokwa kabisa,alijigonga kwenye uzio wa boti, kitendo ambacho mkuu wa msafara aliweza kupasa sauti akiwataka watu wake wakae kimya.. Muda huo huo Bingo alijitupa ndani ya maji na kisha kuanza kuogelea.. Watu hao waliomuona, mmoja aliingia chumba kile kilicho kuwa na ramani, alishtuka baada kuikosa, akajua dhahili imechukuliwa na yule mtu aliyeonekana ndani ya maji ambaye ndio Bingo. Hivyo haraka sana akarudi kwa mkuu wake akamueleza hali harisi. Mkuu huyo akiwa na wingi wa hasira alichomoa upanga wake akamfyekelea kibaraka wake halafu amri ikatoka kwa watu wengine waliosalia. Punde si punde walijitupa ndani ya maji hali ya kuwa muda huo Bingo alizidi kuogelea kuufuata mto maji yanako elekea ili apate wepesi wa kuwakimbia wale watu. Bingo aliogelea kwa nguvu zake zote huku nyuma akifuatiwa na wingi wa maadui. Hatimaye alifika kwenye mporomoko mkubwa wa maji, hakuona haja ya kuogopa alijitosa mzima mzima ilihali watu wale wa waliokuwa wakikimbia waliogopa kutosa katika mporomoko huo lakini nguvu ya maji iliweza kuwavuta wakajikuta nao wakiungana na Bingo ndani ya mporomoko huo,vile vile boti nayo iliavutwa hali. Mkuu wa msafara pamoja na vibaraka wake wakateketea ndani namna hiyo ikiwa muda huo Bingo yeye alipoteza fahamu akasombwa na maji ingawa alikwama kwenye mti ambao uliangukia mtoni.

*******


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog