Search This Blog

MKUFU WA MALKIA WA GOSHEN - 5

 





    Simulizi : Mkufu Wa Malkia Wa Gosheni

    Sehemu Ya Tano (5)





    “Sasa nilihangaika sana kutafuta bashara itakayoweza kusimama kwa haraka maana mimi sina muda mrefu tena hapa duniani … kwenye uchambuzi wangu nikaona biashara ya cedar itanifaa.”

    .

    .

    Melkizedek akatoa macho ya mshangao.

    .

    .

    “Ndiyo maana nikasema ni siri,” Mzee akasema kwa sauti ya chini. Melkizedek akatazama kushoto na kulia, akasema:

    .

    .

    “Ndiyo cedar?”





    “Ndio.”

    .

    .

    “Si unajua ni hatari kubwa ikigundulikana? Kifungo miaka minne na kazi ngumu?”

    .

    .

    “Najua kila kitu, Melkizedek. Mimi pia nilihusika kwenye kutengeneza na kupitisha sharia hiyo. najua kila kitu, ila nimeona hamna namna na huo ndiyo mlango pekee wa mimi kutokea, kwa haraka.



    Naomba uwe unanisaidia kusafirisha mzigo huo huko nje ya Goshen.”

    .

    .

    Melkizedek akakosa cha kusema. Alikunja ngumi na kuing’ata akitafakari. Alikuwa kama vile ametoka kupigwa na kupumbazwa na shoti ya umeme. Kizuri gharama.

    .

    .

    “Tattiana akiwa malkia, mizigo yako haitakuwa tu haitozwi kodi bali pia itakuwa haikaguliwi. Usihofu sana, bwana Melkizedek.”

    .

    .

    “Mzee, naomba uniwie radhi. Nipatie muda wa kulitafuna hilo jambo lako.”

    Mzee akashusha pumzi na kupandisha mabega.

    .

    .

    “Sawa. Ila naomba unitaarifu mapema kama umeshindwa kumeza.”

    .

    .

    Kabla hawajaagana, Mzee akahitaji kuonana na Tattiana. Binti akaitwa wakapewa faragha ya kuongea. Melkizedek aliwapisha sebuleni akirejea chumbani.

    .

    .

    “Kuna uwezekano ukawa unafuatiliwa na watu toka makaoni. Hakikisha mienendo yako inakuwa safi na stadi. Umesikia?”

    .

    .

    Tattiana akatikisa kichwa. “Ndio, nimesikia.”

    .

    .

    Mzee akaendaze.

    .

    .

    . ***

    .

    .

    .

    .

    “Mama anaendeleaje?” Malkia aliuliza punde tu alipompokea Fluffy toka kwenye farasiwe.



    Yalikuwa ni majira ya saa tatu usiku kama wangelikuwa wanatumia mfumo wa masaa wa sasa. Kulikuwa ni tulivu na penye baridi lililowavesha watu nguo nzito. Wanajeshi walikuwa wametanda eneo hili la Malkia kuhakikisha usalama.





    Malkia alikuwa amevalia gauni rangi ya fedha, lililobana kiuno chake na kujimwaga huko chini. Nywele zake ndefu zilikuwa zimesukwa kwenye njia pana pana na kumfanya aonekane kama kabinti cha shule ya msingi.

    .

    .

    Mkononi alikuwa amevalia bangili za kuvutia zinazong’aa, shingoni mkufu ulioonekana vema kutokana na gauni lake kutelekeza mabega.

    .

    .

    Fluffy alikuwa amevalia suruali yenye mkanda mkubwa uliononing’iza mfuko wa jambia lake refu. Viatu virefu vilivyokomea magotini. Blauzi ya kumbana, mikononi akiwa amejifunga riboni za ngozi ngumu.

    .

    .

    “Anaendelea vizuri tu, amesema nikusalimu,” Fluffy alimwambia Malkia akitabasamu.

    .

    .

    “Ahsante sana. Mbona hujaja naye?”

    .

    .

    “Amegoma kuja pasipo kujali nimembeleza namna gani. Amesema tukienda kumsalimia inatosha, hamna shida.”

    .

    .

    Malkia akafadhaika.

    .

    .

    “Nilijua nitamuona ukija naye. Nilifanya makosa kutoenda nawe.”

    .

    .

    “Usijali, Malkia wangu. Tutakuwa tunaenda kumsalimu.”

    .

    .

    “Lini? Itachukua muda kwenda na kupata nafasi hizo. Ningejua ningekupatia zawadi zangu uende nazo.”

    .

    .

    “Usiwaze sana, Malkia.”

    .

    .

    “Lazima niwaze, Fluffy. Alinitendea wema sana, sina budi kumrejeshea fadhila.”

    .

    .

    “Mama anaelewa yote hayo. Usijipe shida ya mawazo .”

    .

    .

    Walifika sebuleni walipoketi na kuongea kwa dakika kadhaa kabla Fluffy hajaaga anaenda kupumzika. Malkia akamsindikiza akaenda zake. Ilikuwa ni safari ya hatua thelathini za mtu mzima toka kwenye himaya ya Malkia.





    Nyumba kubwa yenye walinzi ishirini na mbili waliobebelea silaha mbalimbali. Waliinamisha vichwa kumpokea jenerali wao. Fluffy akawarejeshea salamu na kuzama ndani



    Akavua nguoze na kuzitupia chini kupumzisha mwili, kisha akaenda kuoga, huduma aliyokosa kwa muda wote aliokuwa safarini. Alitoka bafuni na nguo nzito akijifutia maji.

    Ndani kulikuwa kuna joto kwasababu ya kufungwa madirisha na milango.

    Aliokota nguo zake alizozitupia chini, na mara akaona karatasi imedondoka toka nguoni. Akainyanyua na kuitazama. Ilikuwa ni ile mama yake aliyompatia.



    Alikuwa ameisahau. Kuiona kwake kukamkumbusha maneno ya mama yake. Na hata kukamtia hamu ya kutaka kujua karatasi hiyo ina taarifa gani.

    Akaketi kitandani na kuanza kuiperuzi. Alikunja ndita akiwa makini, macho yake yalienda kila kona ya karatasi, lakini hakuambulia kitu.



    Karatasi ilikuwa imeandikwa kwa lugha ngeni asiyoijua. Michoro na alama zilizokuwepo karatasini zilikuwa vitendawili alivyoshindwa kuvitegua.

    .

    .

    “Sasa mama amenipaje kitu anachojua siwezi kukifahamu?” akalalama.



    Akajaribu kusoma tena lakini hola! Akawaza namna ya kufanya kwa sekunde kadhaa, akapata wazo.

    .

    .

    Akajivesha nguo kisha akamuita mwanajeshi mmoja na kumuagiza.

    .

    .

    “Niitie Seth haraka!”

    .

    .

    Mwanajeshi akatimiza agizo ndani ya muda mfupi, Seth akawa amefika mbele ya Fluffy. Wakaketi sebuleni wakisindikizwa na vikombe vya kahawa.





    “Nimekuita hapa nataka unisaidie jambo moja, lakini uufunge mdomo wako maana ni siri,” alisema Fluffy. Seth akatikisa kichwa pasipo kusema jambo. Alikuwa amejitanda tambara kubwa zito jeusi lililokomea kidevuni kuacha mdomo unywe kahawa.



    Fluffy akatoa karatasi lake na kumkabidhi Seth. Seth akapitisha macho yake upesi, haraka akauliza:

    .

    .

    “Umetoa wapi hii?” .

    .

    “Ni siri,” Fluffy akajibu, kisha akauliza: “Ina nini?”

    .

    .

    “Ina siri,” Seth akajibu.

    .

    .

    “Siri gani?”

    .

    .

    “Siri ya giza.”

    .

    .

    “Giza?”

    .

    .

    “Ndio!”

    .

    .

    “Giza lipi?”

    .

    .

    “Yani eneo la giza lililopo huko Misri!”

    .

    .

    “Misri kule kwa wakina Farao?”

    .

    .

    “Ndio. Kule kuna piramidi ya Giza.”

    .

    .

    “Hiyo piramidi ina nini? Yani kuna siri gani kwenye hiyo piramidi?”

    .

    .

    “Ndiyo nataka kusoma sasa, maana hicho ni kichwa cha habari tu.”

    .

    .

    “Sasa mbona ulishtuka?”

    .

    .

    “Hili eneo si la kawaida, jenerali. Panatisha na panaogofya. Si watu wengi wana habari nalo, linatunza siri muhimu za watawala wakubwa, mafarao, na mojawapo ya himaya kubwa kuwahi kutokea duniani, Misri!”

    .

    .

    Kwa maelezo hayo ya Seth, Fluffy akaanza kujenga hofu. Kwanini mama yake amempa habari hizo? Ina maana hajui kuhusu eneo hilo? Alipumbazwa na mawazo.

    .

    .

    “Tunaweza tukasoma kwa pamoja?” Seth akamshtua kwa swali. Fluffy akatikisa kichwa.

    .

    .

    “Ndiyo, tunaweza.”

    .

    .

    Taratibu Seth akaanza kusoma na kumfafanulia Fluffy yale yaliyokuwepo kwenye karatasi. Fluffy akapata vipele vya msisimko kwenye ngozi.





    Kadiri karatasi ilivyokuwa inasomwa, vinyweleo vikamsimama, na mwili ukaanza kumtetema. Mpaka Seth anamaliza, moyo wake ulikuwa unaenda mbio kana kwamba umechoka kukaa ndani na sasa unataka kwenda nje kupunga hewa.





    Seth akamaliza kusoma. Akamtazama Fluffy na kumuona amejawa na hofu pana. Alitabasamu kabla hajamuuliza:



    “Upo sawa?”



    Fluffy akatikisa kichwa kisha akaichukua karatasi yake.



    “Nashukuru sana, Seth. Unaweza ukaenda.”



    Seth akanyanyuka.



    “Utakaponihitaji nipo radhi kukusaidia, jenerali.”



    “Nashukuru,” akajibu Fluffy. Hakuwa sawa, na uso wake ulikuwa kielelezo. Seth alipokaribia mlango, alimuita akamwambia:



    “Hakikisha unafunga mdomo wako.”



    Seth akatikisa kichwa chake kabla hajafungua mlango na kujiendea. Alimwacha Fluffy akipambana kupata usingizi kutokana na mawazo, ila kwa kuwa uchovu wake ulikuwa mzito zaidi, akapitiwa na usingizi pasipo fahamu.





    ***





    Usiku ulikuwa unazidi kuwa mzito na mwanga wa mwezi pia ukizidi kuwa finyu na kufanya giza liwe totoro.



    Kulikuwa tulivu sana, hata kitu kidogo kilikuwa kinasikika vema hivyo basi sauti za wadudu, upepo, miti na matawi ndivyo vilikuwa vinapiga kelele.



    Ndani ya kasri ya Sultan napo kulikuwa kimya, ila tu kwenye chumba cha kiongozi huyo ambapo sauti ya muziki ilikuwa inasikika. Muziki huo laini uliokuwa unaimbwa kwa lugha la kiarabu ulikuwa unatoka kwenye santuri iliyokuwa imekaa kando ya kitanda cha Sultan.



    Santuri hiyo ya kitambo ilikuwa ni moja na pekee ndani ya himaya nzima. Na si tu kwenye himaya hii, bali kwenye himaya lukuki. Kumiliki santuri ilikuwa anasa, tena ya juu haswa.



    Sultan alikuwa amelala kitandani akisikiliza muziki huu mtamu uliokuwa unanguruma. Mwimbaji alikuwa mwanamke mwenye sauti nyembamba ya mawimbi. Aliimba taratibu. Hata kama hujui lugha atumiayo, muziki huu ungekugusa.



    Sultan alikuwa mbali kimawazo. Wimbo huu ulikuwa unazidi kumpaisha kwenda mbali zaidi.



    Kichwani mwake alikuwa na mamb0 kadhaa aliyokuwa anayatatua. Macho yake yalikuwa mekundu na lips zake zilikuwa kavu. Alikuwa anamuwaza Karim. Alikuwa anamuwaza mkewe mkubwa.



    Alijikuta ana hamu ya kufanya jambo fulani kubwa kwa Karim. Kitendo cha mwanaume huyo kutoroka jela na kuua askari wake, tena ndani ya kasri, kwake ilikuwa ni dharau kubwa ambayo haitakiwi kuonyeshwa kwa mkuu wa himaya.



    Alitaka kumfunza adabu.



    Tangu alipopewa habari zake alikuwa anawaza atamuwajibisha vipi, kila njia aipatayo akiiona si sahihi au haitafaa.



    Lakini ndani ya mawazo hayo pia akamuwaza na mkewe. Vipi kama akimteketeza Karim, atampata tena mkewe? Je aamue kuwa mpole tu kwa Karim ili amsaidie kumtafutia mkewe?



    Hapana! Akasema na roho yake akitikisa kichwa. Siwezi kumlamba miguu mtu yeyote ndani ya himaya yangu. Sasa nimlazimishe?



    Aliwaza na kuwaza. Jeshi lake lilikuwa tayari likingoja tu amri yake, ila sasa anabanwa na kigugumizi baada ya kufikiria pande zote mbili za shilingi.



    Mara akiwa anaendelea na mawazo yake, anasikia hodi inagongwa. Kwa mara ya kwanza hakuisikia, kwa mara ya pili akaipuuzia, kwa mara ya tatu akaitikia kwa sauti kali.



    Ndani akaingia askari: mwanaume mfupi mwekundu, mkakamavu ndani ya sare. Alisimama kama sanamu. Sultan hakumtazama, bali alisimamisha tu masikio apate kumsikia. Askari akasema:



    “Sultan wangu, Sultana amerejea.”



    Sultan akashtuka. Akamtazama askari kama mtoto aliyemwaga sukari.



    “Unasemaje?” akauliza.



    “Sultana amerejea,” askari akarudia tena. Mara mlango ukafunguliwa na Sultana, bi mkubwa, akazama ndani. Nyuma yake alikuwa anafuatwa na askari ambaye alikuwa anajaribu kumzuia.



    Sultan aliwapa askari zake ishara ya kichwa, wakatoka ndani na kuwaacha peke yao, yeye na mkewe.



    Sultana alipiga magoti akimimina machozi, akamwomba radhi mumewe kwa aliyoyatenda.



    Kwa muda Sultan akawa amekaa kimya akimtazama mkewe. Hakuamini anachokiona, ni kweli ama ndoto? Alikosa cha kusema akabakia amekodoa. Alifuta uso na kiganja chake kisha akashusha pumzi ndefu.



    “Ulikuwa wapi?” akauliza kwa sauti ya chini isiyo na jazba. Sultana akashindwa kujibu kwa kubanwa na kwikiwi za kilio.



    Sultan akamuonea huruma mkewe. Akamfuata na kumnyanyua, akamketisha kitandani.



    Alimngoja mpaka pale kilio kilipokoma, mwanamke akasema:



    “Nisamehe mume wangu, nimekukosea.”



    “Nimeshakusamehe,” akasema Sultan. “Bali nataka kujua ulikuwepo wapi?”



    “Nilikuwepo kwa kaka yangu, Karim.”



    “Mbona nilikuja nikakukosa?”



    “Kwasababu Karim alinigeuza upepo usipate kuniona. Tulijua endapo ungenikuta pale basi ingelikuwa tabu, ungeghafirika mno.”



    “Huoni umeniudhi zaidi?”



    “Najua mume wangu. Nisamehe sana maana sikushirikisha kichwa changu kwenye kufanya maaumzi. Hofu ya wewe kunikuta pale ilhali sikukuaga iliniponza.”



    “Karim yupo wapi?”



    “Yupo kwake … Naomba umsamehe maana amefanya yote haya kwasababu yangu ili apate kunirejesha tena duniani. Ni mimi ndimi mwenye makosa.”



    “Hakuna,” Sultan akatikisa kichwa. “Karim amenikosea sana. Kwanini hakunieleza haya mpaka avunje kasri yangu? Hakuna himaya yoyote inayodiriki kugusa kasri yangu, iweje huyu mtu mmoja?”



    “Kwa moyo wote namuombea msamaha.”



    “Hapana! Lazima ajue mimi ni nani. Mimi ni Sultan.”



    Japokuwa Sultana hakuchoka kumwombea msamaha Karim, Sultan hakuelewa. Kiburi cha madaraka kilimlevya na alitaka kuonyesha nguvu yake. Aliona kumwacha Karim ni kama vile kutangaza kushindwa mbele ya wananchi wake.



    Ilimradi sasa ameshampata mkewe, Karim hana tija.



    Kisasi cha mganga huyo kushindwa kumsaidia kuupata mkufu, kilikuwa kinamtafuna.



    Alimkarimu vema mkewe, akamtaka akaoge aje kupumzika maana amechoshwa na safari ndefu toka kwa Karim. Mke akamtii mumewe na kwenda bafuni, Sultan akanyanyuka haraka na kwenda nje.



    Akamuita kiongozi wa jeshi lake, na kumpa agizo.



    “Kaharibu mji wote wa Karim. Namtaka akiwa amekufa!”



    Kiongozi akaitikia kabla ya kutwaa vikosi vyake vitatu vya wapambanaji tayari kwa ajili ya kwenda kwa Karim kufanya kile wallichoagizwa.



    Sultan alipotoa agizo hilo sasa akajihisi ametua mzigo kifuani. Alitabasamu akijirudisha ndani alipojilaza kitandani, akaongeza na sauti ya muziki kwenye santuri.





    ***







    Asubuhi palikucha na Rhoda. Aliamka upesi akanywa kahawa kupasha tumbo kisha akakamata kitabu cha mahesabu ya mapato na matumizi ya mgahawa na kukipitia kwa muda.



    Hakuwa amevaa vema. Alipoamka tu alinawa uso wake kisha akajiweka mezani kufanya kazi.



    Alipopata walakini alimuita mfanyakazi wake amueleweshe, alipomaliza akakiweka kitabu kando na kupitia mazingira ya mgahawa wake kuhakikisha kila kitu kipo sawa.



    Aliongozana na mfanyakazi wake mkuu, mwanamke mzee wa miaka hamsini na kitu aitwaye Abella.



    "Mauzo yameshuka, nini shida Abella?" Rhoda aliuliza wakiwa wanatembea.



    "Sijajua nini shida madam," Abella akajibu. "Hatukubadilisha chochote tangu umeondoka, ila bado wateja walipungua tu!"



    Rhoda hakusema kitu, wakamaliza kuzunguka kisha wakaketi.



    “Naomba chakula kidogo,” Rhoda alimwambia Abella. Punde chakula kikaletwa kwenye kisosi Rhoda akakabidhiwa.



    Akala tonge moja tu kabla hajakiweka kisosi chini, akasema:



    “Abella, chakula ni kibaya.”



    Alitema chakula hicho na kukisogezea mbali.



    “Samahani sana, madam,” Abella aliwahi kuomba msamaha.



    “Kwanini mnapika chakula kibaya hivyo?”



    “Ni bahati mbaya tu.”



    “Bahati mbaya? Alafu mnalalamika wateja wanapungua! Wateja watakujaje kwa aina ya chakula kama hicho?”



    Abella hakujibu kitu, alikuwa anatazama chini akishikashika mikono yake.



    “Abella, kama kazi imekushinda ni bora ukaniambia. Ina maana lazima mimi niwepo ndiyo biashara iende?”



    “Hapana, madam. Nisamehe halitajirudia.”



    Maongezi yao yalikatishwa na sauti toka nje. Ilikuwa ni sauti ya farasi ambayo ilimshtua Rhoda na kumfanya anyanyuke haraka. Aliachana na Abella akachunggulia kutazama nje.



    Akamuona Bonas akiwa ameongozana na mwanaume mmoja, wote wakiwa juu ya farasi wa kahawia. Haraka akapandisha juu akimwambia Abella awakarimu wageni yeye atarejea punde.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikoga na kujivesha vema, akarejea chini kukutana na Bonas. Wakasalimiana na kujuliana hali.



    “Nimekuja sasa,” Bonas alisema akitanua mikono yake. “Niko tayari kwa ajili ya kazi.”



    Rhoda akatabasamu.



    “Umewahi, Bonas.”



    “Nimewahi?” Bonas akatahamaki. “Si kama tulivyoahidiana au?”



    “Yeah, ni kama tulivyoahidiana ila bado sijaongea na mfalme. Baadae ndiyo nitaenda kumjulia hali.”



    “Sawa, ila umejiandaaje na hiyo safari?”



    “Bonas, siwezi kutoa majibu mazuri mpaka pale nitakapoongea na mfalme.”



    “Sasa madam, tutaweza kwenda huko kesho kweli kama tulivyopanga? Huoni tutakuwa na muda mfinyu sana wa kujipanga?”



    “Ni kweli. Inabidi tusogeze muda mbele kidogo kwa ajili ya maandalizi, kama siku mbili hivi. Tuachane na hayo, eti umesikia habari za kuonekana kwa Malkia Sandarus?”



    “Yah! Nimesikia.”



    “Umesikia wapi?”



    Bonas akatabasamu.



    “Mimi mtu mpana hapa himayani, habari kama hizo haziwezi kunipita.”



    “Unadhani hizo habari zina ukweli ama porojo tu?”



    “Zina ukweli kabisa!”



    “Una uhakika gani?”



    “Ndugu yangu alimshuhudia kwa macho yake na si mlevi.”



    “Alimshuhudia akifanya nini?”



    “Alikuwa anatembea tembea. Huku na huko.”



    “Bonas, unajua hizi si habari njema kwangu.”



    “Kivipi?”



    “We jua si habari njema kwangu. Na ninapata maswali kweli, atakuwepo wapi? Na anafanya nini?”



    “Ubaya hakuna anayejua. Kama lingetokea kabla ya kwenda kwa Venin, huenda angetusaidia kujua.”



    “Lakini kuna mtu anaweza kutuonyesha njia,” mwanaume aliyeongozana na Bonas alisema. Wote wakamtazama.



    “Nani huyo?” Rhoda akauliza upesi.



    “Kuna mzee mmoja yupo kule ng’ambo ya mto. Yeye huwa ananasibu ana maono japo si maarufu sana kwa walio wengi,” akajibu rafikiye Bonas, Loki kwa jina.



    “Una uhakika?” Rhoda akauliza. Macho yalikuwa yamemtoka akiachama mdomo kuonyesha namna gani alivyobamwa na habari hizo.



    “Ndiyo, nina uhakika. Hata ninaweza kuwapeleka mkihitaji.”



    Rhoda akamtazama Bonas, mwanaume huyo akampandishia nyusi, akarudisha macho yake kwa Loki akisimama na kusema:



    “Ngoja, twende!”



    Akapandisha zake juu na kuwaacha wanaume peke yao.



    “Loki, una uhakika na unachokisema?” Bonas aliuliza. “Unajua hizi habari ni kubwa sana kwa huyu mama na endapo akijua umemlaghai inaweza ikapelekea ngoma nzito na ngumu kuicheza.”



    “Sijamdanganya, nimesema kweli tupu, Bonas. Ya nini nidanganye?”



    “Ni mzee gani huyo unayemuongelea?”



    “Mzee Tretho.”



    “Tretho wa kule mambugani? – mchunga ng’ombe?”



    “Ndio, unamdharau enh? Mimi namjua maana nilishawahi kukumbana naye mahali.”



    “Mbona hukuwahi nambia? Sijawahi kusikia kama ana lolote!”



    “Kwasababu Tretho ni msiri na si mjivuni.”



    Mara wakasikia mlango unafunguliwa, Rhoda akachomoza toka chumba chake cha juu.



    “Tuombe Mungu unachosema kikawe kweli,” Bonas alisema akipachika kiganja chake juu ya bega la Loki. Rhoda aliwakaribia, akawatazama kwa macho yenye bashasha.



    “Tunaweza tukaenda!” akasema akitangulia kwenda nje.



    Walipanda farasi zao, pasipo kuwa na ulinzi wowote, wakaanza safari ya kuelekea ng’ambo kukutana na Trethro. Ndani ya kama dakiaka ishirini na kitu hivi wakawa wameufikia mto.



    Wakavuka na kuchukua mwendo wa robo saa kabla ya kujikuta mbele ya nyumba ndogo chakavu. Fupi na isiyo na mahadhi ya kuvutia. Madirisha yake yalikuwa madogo, na paa lake likiezekwa na nyasi zilizooza.



    “Ndiyo hapa,” Loki akamwambia Rhoda. Rhoda akapekua kwanza mazingira kabla hajauliza:



    “Kunaonekana kimya, kutakuwa kuna watu kweli?”



    “Anaishi mwenyewe,” Bonas akadakia. “Ni yeye na ng’ombe zake tu!”



    Loki akashuka na kuusogelea mlango, akagonga na kuita pasipo majibu. Akazunguka nyuma ya nyumba mpaka zizini, hakumuona Loki wala ng’ombe.



    “Hayupo!” Loki alimwambia Rhoda aliyekuwa bado yupo juu ya farasi. “Anaweza akawa yupo malishoni.”



    “Muda huu?” Bonas akatahamaki kwa swali.



    “Hana mahala pengine pa kwenda zaidi ya huko,” Loki akajibu upesi.



    “Lakini malisho hufanya nyakati za jioni! Pengine kamuangaze kwa majirani,” Bonas alishauri. Loki akaenenda upesi huko kumtazama na kumuulizia Tretho.



    Muda mfupi baadae akarejea. Akamtazama Rhoda na kumwambia:



    “Hayupo!”



    Rhoda akakunja sura kwa hasira.



    “Wamesema amechukuliwa na wanajeshi,” Loki akajazia taarifa. “Ilikuwa ni leo asubuhi wakati anawapatia maji mifugo yake.”



    Rhoda akastaajabu.



    “Wamekwambia amechukuliwa kwa kosa gani?”



    “Hapana!” Loki akatikisa kichwa. Rhoda akashusha pumzi ndefu.



    Aliona sasa njia imekuwa ndefu zaidi.



    Kama Tretho amekamatwa ina maana atakuwapo lokapu kule karibia na milki ya mfalme. Kumpata mzee huyo maana yake ni kumtoa lokapu, na kumtoa ni mpaka kuwepo na maelezo ya kueleweka, ama amri toka kwa mfalme.



    Akimwomba mfalme, ataulizwa kwanini anataka msaidia mzee huyo. Ataweza kusema sababu ni Malkia? Hatompatia tembe za mashaka mfalme juu ya kusumbuka huko na Malkia Sandarus?



    Au hataonekana ni mtu mwenye kuamini ulozi kupita kiasi?



    Aliguna.





    ***





    Baada ya kuangaza huku na huko na kuhakikisha kwamba yupo mwenyewe tu, Seth akatoa kijidaftari chake na peni ndani ya mfuko akaanza kuandika maneno fulani yenye alfabeti za ishara.



    Alfabeti hizi hazikuwa na mpangilio maalum, kuna ambazo aliziandika kwa juu, zingine chini na katikati! Alikuwa makini akiziandika, na fika alikuwa anajua anachokifanya.



    Aliandika ukurasa wa kwanza kisha akafungua wa pili na wa tatu, kuna muda aliacha kuandika akawa anafikiria, kisha akaendelea kuandika na kuandika.



    Alikuwa amejitenga kabisa na ulimwengu akiwa ameketi juu kabisa mwa jengo kubwa la kijamaa. Pembeni kidogo kulikuwa kuna kachumba kadogo chenye kengele kubwa nyeusi iliyokuwa imetulia tuli.



    Hapa ndipo mahala anapopapenda Seth, patulivu na pasipo na bughdha. Kila anapohitaji muda wa kuwa mwenyewe, basi huja huku juu ya paa, huketi na kufanya mambo yake.



    Anatazama himaya nzima akiwaza na kuwazua kwa kadiri atakavyo. Ni watu wachache tu ndiyo walikuwa wanajua makazi haya ya Seth. Na hata hao wanaojua huwa wanampatia muda wa yeye kuwa peke yake kwa utambuzi.



    Tangu apande huko juu, sasa alikuwa ameshakula takribani dakika ishirini hivi. Ila utulivu wake ulikuja kupotezwa na ujio wa mgeni ambaye hakumtarajia. Kwasababu alikuwa amemezwa na karatasi ya kijidaftari chake, hakugundua kama kuna mtu amemjongea.



    “Seth!” Sauti ikamshtua. Haraka akafunga kijidaftari chake na kukirejesha ndani ya mfuko, na peni yake pia.



    Akageuka nyuma kumtazama mgeni. Alikuwa bwana Bozi: mzee wa baraza la Sawaridi mwenye heshima zake.



    Mzee huyu ndiye aliyempendekeza Seth na Dummy kwa Malkia, kwamba wanaweza kutumiwa na kuleta tija.



    “Pole kwa kukushtua!” Alisema Bozi kwa tabasamu akiweka mkono wake begani mwa Seth. Seth akatabasamu lisilotoka moyoni.



    “Karibu.”



    “Ahsante sana, Seth. Najua haukutarajia ujio wangu, na pengine nitakuaribia mipango yako. Naomba uniwie radhi.”



    “Usijali, karibu.”



    Bozi akaketi. Alijetengenezea na majoho yake asijiweke uchi.



    “Kumbe huku ni pazuri kiasi hiki!”



    “Yah! Kuna upepo wa kutosha.”



    “Na muono bora kabisa. Ukiwa hapa waweza kuona kila jambo linaloendelea himayani. Si bure wapenda kukaa huku.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Seth akatabasamu pasipo majibu. Kichwani alikuwa anawaza ni nini kimemleta Bozi pale, na kama ameona kile alichokuwa anaandika na kukielewa.



    “Nimekutafuta sana huko chini kabla ya kufikiria kwamba utakuwepo huku,” Bozi aliendelea kulonga kwa bashasha. “Tokea asubuhi sijakuona, ina maana ulikuwepo huku?”



    “Hapana,” Seth akajibu kifupi.



    “Sawa, nisikupotezee sana muda wako, kuna jambo fulani nilikuwa nataka kuongea na wewe, na jambo hili ningependa liwe siri kati yangu na wewe.”



    Siri tena? Seth aliongelea kifuani. Alikuwa tayari ana siri ya Fluffy, na sasa nyingine ilikuwa inataka kuongezwa!



    “Vipi, naweza nikaendelea?” Bozi aliuliza. Seth akatikisa kichwa.



    “Nakuskiza.”



    “Seth, bila shaka unajua mimi ndiye nilikusogeza karibu na Malkia.”



    “Najua.”



    “Safi sana. Unajua nafasi hiyo ni kubwa sana, na sikuwahi kukuomba fadhila yoyote ile.”



    Seth kimya. Alishajua sasa mchezo upi unataka kuchezeka, ila bado hakujua nini kilikuwa nyuma ya mchezo huo. Akawa mpole asikie japo moyo wake tayari ulishachagua kutoshirikiana na Bozi.



    “Na sijalenga kupata fadhila yoyote ile toka kwako, Seth. Lakini naona kuna jambo mbele yetu, jambo muhimu na nyeti.”



    Seth kimya, anaskiza.



    “Seth, naona tunastahili zaidi ya hiki tulicho nacho sasa.”



    “Ukimaanisha nini?” Seth akafungua mdomo kuuliza. Alitazama macho ya Bozi yaliyokuwa yamejaa uchu, Bozi akatabasamu.



    “Usiwe na haraka, Seth. Taratibu taratibu tutaelewana. Mimi nataka mema kwa ajili yako, yangu na himaya nzima. Naona ni vema sasa tukaanza mipango ya kurejesha himaya yetu mikononi toka kwa hawa wanawake.”



    Seth akamtazama Bozi kwa mshangao. Alikosa cha kusema.



    “Najua unaweza kudhani ni ngumu, ila hakuna kisichowezekana. Kwa hali na mali inabidi turejeshe himaya yetu mikononi, hatuwezi tukawa tayari kutawaliwa na mgeni, tena mwanamke!



    Najua endapo tukiunganisha nguvu, tutalifanikisha hili kwa wepesi pasipo hata kumwaga damu.”



    “Ni kweli, lakini mimi si miongoni mwenu. Nashukuru kwa kunishirikisha.”



    “Seth …”



    “Nimesema nashukuru, sina haja ya kujiunga na upande wowote ule kwa lengo lolote lile! Bila shaka nimeeleweka, na unaweza ukaenda.”



    Bozi akabaki ameduwaa. Alishusha pumzi ndefu akanyanyuka.



    “Pengine haupo kwenye hali nzuri kihisia. Nitakupatia muda.”



    “Hata kama ukinipatia milele, jibu langu litakuwa hilo hilo! Sina nyendo, uroho, wala hitaji lolote la kisiasa.”



    Bozi akaguna.



    “Hujui usemalo, na hakika utakuwa kujuta.”



    “Baada ya kwanza kujuta wewe,” Seth akasema kwa kujiamini. Bozi asitie neno, akaenda zake baada ya kumkata Seth jicho kali na kutabasamu kwa kebehi.



    Seth akaendelea na kazi yake ya awali, ila sasa asiifanye vema sababu ya mawazo.



    Alikaa kama dakika tano tu, mara wanaume watatu waliovalia magwanda ya jeshi wakawaja na kusimama kandokando yake. Mmoja akamwamuru:



    “Simama!”



    Kabla hajasema jambo, akanyanyuliwa na kubebwa kama kiroba. Hakujua anapelekwa wapi.

    “Kuna mzee mmoja yupo kule ng’ambo ya mto. Yeye huwa ananasibu ana maono japo si maarufu sana kwa walio wengi,” akajibu rafikiye Bonas, Loki kwa jina.



    “Una uhakika?” Rhoda akauliza. Macho yalikuwa yamemtoka akiachama mdomo kuonyesha namna gani alivyobamwa na habari hizo.



    “Ndiyo, nina uhakika. Hata ninaweza kuwapeleka mkihitaji.”



    Rhoda akamtazama Bonas, mwanaume huyo akampandishia nyusi, akarudisha macho yake kwa Loki akisimama na kusema:



    “Ngoja, twende!”



    Akapandisha zake juu na kuwaacha wanaume peke yao.



    “Loki, una uhakika na unachokisema?” Bonas aliuliza. “Unajua hizi habari ni kubwa sana kwa huyu mama na endapo akijua umemlaghai inaweza ikapelekea ngoma nzito na ngumu kuicheza.”



    “Sijamdanganya, nimesema kweli tupu, Bonas. Ya nini nidanganye?”



    “Ni mzee gani huyo unayemuongelea?”



    “Mzee Tretho.”



    “Tretho wa kule mambugani? – mchunga ng’ombe?”



    “Ndio, unamdharau enh? Mimi namjua maana nilishawahi kukumbana naye mahali.”



    “Mbona hukuwahi nambia? Sijawahi kusikia kama ana lolote!”



    “Kwasababu Tretho ni msiri na si mjivuni.”



    Mara wakasikia mlango unafunguliwa, Rhoda akachomoza toka chumba chake cha juu.



    “Tuombe Mungu unachosema kikawe kweli,” Bonas alisema akipachika kiganja chake juu ya bega la Loki. Rhoda aliwakaribia, akawatazama kwa macho yenye bashasha.



    “Tunaweza tukaenda!” akasema akitangulia kwenda nje.



    Walipanda farasi zao, pasipo kuwa na ulinzi wowote, wakaanza safari ya kuelekea ng’ambo kukutana na Trethro. Ndani ya kama dakiaka ishirini na kitu hivi wakawa wameufikia mto.



    Wakavuka na kuchukua mwendo wa robo saa kabla ya kujikuta mbele ya nyumba ndogo chakavu. Fupi na isiyo na mahadhi ya kuvutia. Madirisha yake yalikuwa madogo, na paa lake likiezekwa na nyasi zilizooza.



    “Ndiyo hapa,” Loki akamwambia Rhoda. Rhoda akapekua kwanza mazingira kabla hajauliza:



    “Kunaonekana kimya, kutakuwa kuna watu kweli?”



    “Anaishi mwenyewe,” Bonas akadakia. “Ni yeye na ng’ombe zake tu!”



    Loki akashuka na kuusogelea mlango, akagonga na kuita pasipo majibu. Akazunguka nyuma ya nyumba mpaka zizini, hakumuona Loki wala ng’ombe.



    “Hayupo!” Loki alimwambia Rhoda aliyekuwa bado yupo juu ya farasi. “Anaweza akawa yupo malishoni.”



    “Muda huu?” Bonas akatahamaki kwa swali.



    “Hana mahala pengine pa kwenda zaidi ya huko,” Loki akajibu upesi.



    “Lakini malisho hufanya nyakati za jioni! Pengine kamuangaze kwa majirani,” Bonas alishauri. Loki akaenenda upesi huko kumtazama na kumuulizia Tretho.



    Muda mfupi baadae akarejea. Akamtazama Rhoda na kumwambia:



    “Hayupo!”



    Rhoda akakunja sura kwa hasira.



    “Wamesema amechukuliwa na wanajeshi,” Loki akajazia taarifa. “Ilikuwa ni leo asubuhi wakati anawapatia maji mifugo yake.”



    Rhoda akastaajabu.



    “Wamekwambia amechukuliwa kwa kosa gani?”



    “Hapana!” Loki akatikisa kichwa. Rhoda akashusha pumzi ndefu.



    Aliona sasa njia imekuwa ndefu zaidi.



    Kama Tretho amekamatwa ina maana atakuwapo lokapu kule karibia na milki ya mfalme. Kumpata mzee huyo maana yake ni kumtoa lokapu, na kumtoa ni mpaka kuwepo na maelezo ya kueleweka, ama amri toka kwa mfalme.



    Akimwomba mfalme, ataulizwa kwanini anataka msaidia mzee huyo. Ataweza kusema sababu ni Malkia? Hatompatia tembe za mashaka mfalme juu ya kusumbuka huko na Malkia Sandarus?



    Au hataonekana ni mtu mwenye kuamini ulozi kupita kiasi?



    Aliguna.





    ***





    Baada ya kuangaza huku na huko na kuhakikisha kwamba yupo mwenyewe tu, Seth akatoa kijidaftari chake na peni ndani ya mfuko akaanza kuandika maneno fulani yenye alfabeti za ishara.



    Alfabeti hizi hazikuwa na mpangilio maalum, kuna ambazo aliziandika kwa juu, zingine chini na katikati! Alikuwa makini akiziandika, na fika alikuwa anajua anachokifanya.



    Aliandika ukurasa wa kwanza kisha akafungua wa pili na wa tatu, kuna muda aliacha kuandika akawa anafikiria, kisha akaendelea kuandika na kuandika.



    Alikuwa amejitenga kabisa na ulimwengu akiwa ameketi juu kabisa mwa jengo kubwa la kijamaa. Pembeni kidogo kulikuwa kuna kachumba kadogo chenye kengele kubwa nyeusi iliyokuwa imetulia tuli.



    Hapa ndipo mahala anapopapenda Seth, patulivu na pasipo na bughdha. Kila anapohitaji muda wa kuwa mwenyewe, basi huja huku juu ya paa, huketi na kufanya mambo yake.



    Anatazama himaya nzima akiwaza na kuwazua kwa kadiri atakavyo. Ni watu wachache tu ndiyo walikuwa wanajua makazi haya ya Seth. Na hata hao wanaojua huwa wanampatia muda wa yeye kuwa peke yake kwa utambuzi.



    Tangu apande huko juu, sasa alikuwa ameshakula takribani dakika ishirini hivi. Ila utulivu wake ulikuja kupotezwa na ujio wa mgeni ambaye hakumtarajia. Kwasababu alikuwa amemezwa na karatasi ya kijidaftari chake, hakugundua kama kuna mtu amemjongea.



    “Seth!” Sauti ikamshtua. Haraka akafunga kijidaftari chake na kukirejesha ndani ya mfuko, na peni yake pia.



    Akageuka nyuma kumtazama mgeni. Alikuwa bwana Bozi: mzee wa baraza la Sawaridi mwenye heshima zake.



    Mzee huyu ndiye aliyempendekeza Seth na Dummy kwa Malkia, kwamba wanaweza kutumiwa na kuleta tija.



    “Pole kwa kukushtua!” Alisema Bozi kwa tabasamu akiweka mkono wake begani mwa Seth. Seth akatabasamu lisilotoka moyoni.



    “Karibu.”



    “Ahsante sana, Seth. Najua haukutarajia ujio wangu, na pengine nitakuaribia mipango yako. Naomba uniwie radhi.”



    “Usijali, karibu.”



    Bozi akaketi. Alijetengenezea na majoho yake asijiweke uchi.



    “Kumbe huku ni pazuri kiasi hiki!”



    “Yah! Kuna upepo wa kutosha.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Na muono bora kabisa. Ukiwa hapa waweza kuona kila jambo linaloendelea himayani. Si bure wapenda kukaa huku.”



    Seth akatabasamu pasipo majibu. Kichwani alikuwa anawaza ni nini kimemleta Bozi pale, na kama ameona kile alichokuwa anaandika na kukielewa.



    “Nimekutafuta sana huko chini kabla ya kufikiria kwamba utakuwepo huku,” Bozi aliendelea kulonga kwa bashasha. “Tokea asubuhi sijakuona, ina maana ulikuwepo huku?”



    “Hapana,” Seth akajibu kifupi.



    “Sawa, nisikupotezee sana muda wako, kuna jambo fulani nilikuwa nataka kuongea na wewe, na jambo hili ningependa liwe siri kati yangu na wewe.”



    Siri tena? Seth aliongelea kifuani. Alikuwa tayari ana siri ya Fluffy, na sasa nyingine ilikuwa inataka kuongezwa!



    “Vipi, naweza nikaendelea?” Bozi aliuliza. Seth akatikisa kichwa.



    “Nakuskiza.”



    “Seth, bila shaka unajua mimi ndiye nilikusogeza karibu na Malkia.”



    “Najua.”



    “Safi sana. Unajua nafasi hiyo ni kubwa sana, na sikuwahi kukuomba fadhila yoyote ile.”



    Seth kimya. Alishajua sasa mchezo upi unataka kuchezeka, ila bado hakujua nini kilikuwa nyuma ya mchezo huo. Akawa mpole asikie japo moyo wake tayari ulishachagua kutoshirikiana na Bozi.



    “Na sijalenga kupata fadhila yoyote ile toka kwako, Seth. Lakini naona kuna jambo mbele yetu, jambo muhimu na nyeti.”



    Seth kimya, anaskiza.



    “Seth, naona tunastahili zaidi ya hiki tulicho nacho sasa.”



    “Ukimaanisha nini?” Seth akafungua mdomo kuuliza. Alitazama macho ya Bozi yaliyokuwa yamejaa uchu, Bozi akatabasamu.



    “Usiwe na haraka, Seth. Taratibu taratibu tutaelewana. Mimi nataka mema kwa ajili yako, yangu na himaya nzima. Naona ni vema sasa tukaanza mipango ya kurejesha himaya yetu mikononi toka kwa hawa wanawake.”



    Seth akamtazama Bozi kwa mshangao. Alikosa cha kusema.



    “Najua unaweza kudhani ni ngumu, ila hakuna kisichowezekana. Kwa hali na mali inabidi turejeshe himaya yetu mikononi, hatuwezi tukawa tayari kutawaliwa na mgeni, tena mwanamke!



    Najua endapo tukiunganisha nguvu, tutalifanikisha hili kwa wepesi pasipo hata kumwaga damu.”



    “Ni kweli, lakini mimi si miongoni mwenu. Nashukuru kwa kunishirikisha.”



    “Seth …”



    “Nimesema nashukuru, sina haja ya kujiunga na upande wowote ule kwa lengo lolote lile! Bila shaka nimeeleweka, na unaweza ukaenda.”



    Bozi akabaki ameduwaa. Alishusha pumzi ndefu akanyanyuka.



    “Pengine haupo kwenye hali nzuri kihisia. Nitakupatia muda.”



    “Hata kama ukinipatia milele, jibu langu litakuwa hilo hilo! Sina nyendo, uroho, wala hitaji lolote la kisiasa.”



    Bozi akaguna.



    “Hujui usemalo, na hakika utakuwa kujuta.”



    “Baada ya kwanza kujuta wewe,” Seth akasema kwa kujiamini. Bozi asitie neno, akaenda zake baada ya kumkata Seth jicho kali na kutabasamu kwa kebehi.



    Seth akaendelea na kazi yake ya awali, ila sasa asiifanye vema sababu ya mawazo.



    Alikaa kama dakika tano tu, mara wanaume watatu waliovalia magwanda ya jeshi wakawaja na kusimama kandokando yake. Mmoja akamwamuru:



    “Simama!”



    Kabla hajasema jambo, akanyanyuliwa na kubebwa kama kiroba. Hakujua anapelekwa wapi.



    Alihofia uhai wake.





    Aliingizwa kwenye chumba fulani cha giza, akafungiwa humo. Aliuliza yupo wapi na nani anamfanyia hilo tukio ila hakuna aliyemjibu zaidi ya kurudiwa na mwangwi wa sauti yake.



    Chumbani alikuwa mwenyewe na hakuna mtu nje aliyekuwa anamsikia, pasipo kujali ni kelele namna gani alipiga.



    “Huyu ni kwanza, na tutawamaliza wale wote watakaokaidi mpango wetu.” Sauti ya kiume ilisikika gizani.



    “Lazima mpango wetu ufaulu, lazima turudishe himaya mikononi mwetu.”



    “Ndio!” wengine wakaitikia. Ilikuwa sauti ya watu wawili, zote za kiume.





    ***





    Hodi ilibishwa mara moja kabla mlango haujafunguliwa. Alikuwa ni bibi yake Sultana mdogo akiongozana na mlinzi, mwanaume mrefu jabali.



    Bibi alikuwa amejitundika kikoi kipana kilichofichama shingo na mabega yake. Gauni refu jeusi na mkoba wa rangi nyekundu mkono wake wa kuume.



    Nywele zake ndefu zenye mvi alikuwa ameziviringita na kuzibania vizuri upande wa kushoto. Usoni hakuwa ametia kipodozi chochote hivyo uso wake ukaonyesha umri wake pasipo matatizo.



    Hakuonyesha kujali, hakuwa na sababu ya kufichama umri ilhali ni majaliwa ya muumba.



    ‘umri ni maji ya mto, yakienda hayageuzi shingo’ waenenda vema walishawahi kusema.



    Bibi alitazama huku na huko, hakumwona mjuu wake. Akaita akiketi kitini na mlinzi akienda zake baada ya kumaliza kazi.



    Baada ya muda kidogo, akatokea msichana, yani mjukuu, akiwa amelewa usingizi. Alipomuona bibiye akatabasamu, akamkumbatia na kuketi karibu yake.



    “Mbona kuchelewa hivi?” Sultana akauliza.



    “Unajua kulivyo mbali huku kwenu, alafu mimi ni mzee si kama wewe!”



    Sultana akapiga makofi mara tatu na mara kijakazi akaja upesi, akamwagiza alete kikombe cha kahawa upesi kwa ajili ya bibi yake.



    “Bibi, ulipata barua yangu?” Sultana hakuwa na subra.



    “Ndiyo, niliipata na ndiyo hiyo imenileta hapa.”



    “Sasa bibi unanisaidiaje?”



    “Mjukuu wangu, humwachi mgeni aheme?”



    Sultana akajikuta anatabasamu. Kijakazi alifika akamiminia kahawa kwenye kikombe na kumpatia bibi aliyekinyaka na kukipeleka mdomoni kunywa mafundo mawili.



    “Sasa mjukuu wangu wataka nini?” Bibi akauliza. “Kama maji tayari yameshamwagika, unataka kuyachota?”



    “Kama inawezekana bibi!” Sultana akalipuka kwa hamu.



    “Hapana,” Bibi akasema. “Maji yakishamwagika hayawezi kuzoleka kamwe.”



    “Basi tufanye mpango wa kuyachota mengine!” Sultana akapendekeza.



    Bibi akanywa kwanza mafundo mawili ya kahawa, kisha akatazama kando.



    “Mjukuu wangu, nadhani umesahau jambo, na si mbaya nikakukumbusha. Sina ulozi wa kumdhuru mtu, sijawahi kumdhuru yeyote, bali tu kusaidia.”



    “Lakini bibi …”



    “Hapana! … siwezi nikamuumiza yeyote.”



    “Basi naomba unisaidie.”



    “Nitakusaidia ila si kwa kudhuru wengine.”



    “Inawezekana hilo?”



    “Ndio, hakuna lisilowezekana!”



    “Lakini bibi, vipi kama sisi tukidhuriwa kwa mioyo yetu ya maua?”



    Bibi akamshika mjukuu wake shavu akimtazama machoni.



    “Unanikumbusha mbali sana, kipindi kile ulivyokuwa mtoto. Ulikuwa mbishi na mkorofi. Sababu hiyo ukawa unapigana na wenzako kila uchwao … mabaya mawili hayatengenezi jema moja.”



    Sultana akatazama chini. Alinywea kana kwamba amemwagiwa maji ya baridi. Bibi akafungua mkoba wake na kutoa chupa moja ndefu yenye mfuniko mweusi, ndani yake kulikuwa kuna unga mzito wa kahawia.



    Akaiweka mezani.



    Akatoa tena chupa nyingine, ndogo kwa umbo yenye mfuniko mpana mweupe, nayo akaiweka mezani kisha akaufunga mkoba wake.



    “Hili ndilo jaribio letu la mwisho,” akasema bibi akishika chupa ile ndefu. Akamwonyeshea mjukuu wake.



    “Umeona hii?”



    “Ndio, bibi!”



    “Utaitia kwenye njia atakayokatiza mumeo.”



    Sultana akatikisa kichwa kuafiki.



    “Na hii,” Bibi akaonyeshea chupa ndogo. “Utaiweka nguoni mwake.”



    “Ahsante bibi.”



    “Tahadhari, inabidi uyafanye haya mumeo asijue.”



    “Sasa bibi nitawekaje akiwa ananiona?”



    “Na inabidi uiweke siku ya tatu baada ya mwezi kuwa mzima.”



    “Je kama asipokuja siku hiyo?”



    “Basi itakulazimu usubirie tena mpaka utakapopata wasaa huo. Ukiiweka siku tofauti na hiyo, hakuna mabadiliko yoyote yatakayojiri.”



    Sultana akazikusanya chupa zake akizijaza kiganjani.



    “Hizo hazitamfanya Sultan akupende zaidi,” Bibi akasema. “Bali zitamfanya akumbuke nyumba yako atakapokuwa mbali.”



    “Kivipi?” Sultana akauliza.



    “Dawa itakayokuwa nguoni mwake, itamfanya asikie harufu yako muda wote. Na dawa atakayoikanyaga kwa mguu wake, itamfanya azunguke koote ila arejee hapa hapa. Kiu ya miguu yake itakuwa hapa.”



    Sultana akatabasamu. Akamkumbatia bibi yake kwanguvu.



    “Ahsante sana bibi.”



    “Lakini mjukuu wangu, kama bwana akirejea kwako mara kadhaa, na akahisi harufu yako mara kede, kama hujampatia cha kumfanya akukumbuke, na hicho kipo kichwani, basi ni kazi bure.”



    “Kwa hilo ntajitahidi sana,” akaahidi Sultana.



    “Sasa naona utanipa muda wa kumpumzika.”



    Sultana akacheka.





    ***





    “Kwahiyo?” Sauti ya mwanamke iliuliza ikitokea ndani ya chumba.



    “Sijajua cha kufanya mpaka sasa,” sauti ya kiume ikajibu.



    Ni ndani ya nyumba yenye ulinzi wa kutosha, ya mfanyabiashara Melkizedek. Sebuleni walikuwa wameketi watoto: Fanty na Tattiana wakila cha usiku. Walikuwa wakipiga soga na kukenua.



    Huko nje walinzi wawili walikuwa wamesimama getini wakibebelea mikuki. Mwingine mmoja alikuwa anazunguka huku na kule kuhakikisha usalama.



    Mazingira yalikuwa ya kimya na joto, upepo ukipuliza kwa maringo.



    “Una maanisha nini kusema hujajua cha kufanya mpaka sasa?” aliuliza mwanamke, mke wa Melkizedek. Alikuwa amejilaza kitandani pamoja na mumewe.



    Alikuwa amevalia gauni jepesi jeupe la kulalia. Nywele zake ndefu rangi nyekundu zilikuwa zimetapakaa kitandani. Uso wake mwembamba mrefu wenye kidevu chenye ncha ulikuwa unatazama dari.



    Macho na mdomo wake vilikuwa vinafanana na vya mwanae Tattiana. Mwili wake ulikuwa mwembamba ukiingia kama mara mbili na nusu ya mumewe ambaye alikuwa amejlaza chali , tumbo lake kama kiroba likitazama juu kama kichuguu.



    “Unajua uzito wa hilo ombi?”



    “Najua, lakini ni zito kuliko mwanao kuwa malkia?”



    Kukawa kimya kidogo.



    “Mzee wa watu amekupigania, na kuna uwezekano mkubwa wa mtoto wetu kuwa malkia. Nini unataka zaidi ya hicho?”



    “Tatizo mke wangu, Cedar si haramu kuuzwa tu kwetu bali kwenye himaya nyingi. Vipi kama mzigo ukikamatwa huko na kuharibu taswira yangu?”



    “Kumbuka tayari mtoto wako atakuwa malkia, atakusaidia!”



    “Atanisaidia kwenye himaya zingine? Kuficha uhalifu wangu?”



    “Melkizedek, nimechoka sasa kuongelea hili jambo karibia kila siku. Fanya utakavyoona wewe ni sahihi!”



    “Kwahiyo umesusa?”



    “Si kwamba nimesusa, bali nimeona sina msaada wowote, na tayari umeshafanya maamuzi yako binafsi. Mchango wangu ni nini tena kwako?”



    Kukawa kimya. Kama dakika moja ikapita, hodi ikagongwa mlangoni.



    “Baba, mzee amekuja!” Sauti ya Fanty ilisikika. Melkizedek akamtazama mkewe.



    “Ameshakuja!”



    “Ndio, si alikwambia atakuja?”



    “Sasa nimjibu nini?”



    Mwanamke akatikisa kichwa.



    “Unavyoona wewe,” akajibu.



    “Ebu acha basi kisirani. Mimi namwambia anipatie muda zaidi.”



    Mke hakujibu, akanyanyuka na kujivesha gauni lake jekundu maridadi kisha akamtaka mumewe waende kumpokea mgeni. Melkizedek akavalia shati kubwa, akaongozana na mkewe mpaka chini.



    Walimkuta mzee akiwa ameketi na watoto. Watoto wakapisha kuwapa faragha.



    “Nimekuja kama vile tulivyoahidiana,” alisema Mzee akitabasamu.



    “Karibu sana,” Melkizedek na mkewe wakamkarimu.



    “Samahani, sitakuwa na muda mwingi wa kukaa na nyie. Kuna mahali natakiwa kupitia nikitoka hapa. Sema niliona nikatize mara moja kupata majibu yangu.”



    Melkizedek akatabasamu na kumtazama mkewe. Macho yake yalionyesha yu njia panda.



    “Nataka nipate majibu yenu ili basi nijue namna ya kuenenda katika jitihada zangu za kumfanya Tattiana awe malkia.”



    “Tumekubali!” akasema mke wa Melkizedek. “Tumekubali, tumejadiliana na mume wangu na tumeona inawezekana.”



    Mzee akatabasamu na kutikisa kichwa.



    “Nilijua hilo halitakuwa tatizo kubwa kwenu. Mtoto kuwa malkia si jambo dogo!”



    Mzee na mke wakatabasamu, Melkizedek akaigiza. Moyoni bado alikuwa na ukakasi.



    Mzee hakukaa, akasimama na kuaga.



    “Sasa niachieni kazi mimi. Najua vile n’takavyofanya,” alisema kabla hajashika mlango na kuyoyoma.



    “Mke wangu u …”



    “Nini? Tumeshamaliza majadiliano. Twende ule tulale.”



    Mke akatangulia kwenda akimwacha mumewe nyuma akisita na roho.



    ***



    “Nimemkuta mfalme? Rhoda alimuuliza mlinzi getini. Alikuwa amekuja hapo makaoni akiwa mwenyewe. Alikuwa amevalia gauni rangi nyeupe iliyofifia likipambwa na maua maua madogomadogo.



    Ulikuwa ni usiku, kwa majira ya sasa tungesema ni mishale ya saa nne. Kuja hapo mwenyewe njia nzima ilikuwa si jambo la kawaida, ila kwake wala halikumwia vigumu. Dhamira ndani ya nafsi yake ilikuwa kubwa.



    “Ndiyo yupo, ila huwezi kumwona muda huu,” alisema mlinzi.



    “Siwezi kumwona? Unaniambia kama nani?”



    “Mam, muda sasa umeenda. Mfalme atakuwa amepumzika na ahitaji bughdha. Rhoda akasonya, akamsukumia mlinzi kando kisha akazama ndani. Mlinzi hakusumbuka naye tena, akabaki anamshuhudia tu mwanamke huyo akizama ndani.



    Rhoda akaita mara mbili, na mara mfalme akatoka tokea chumbani. Alikuwa amevalia nguo za kulalia, shati na suruali nyepesi. Alikutana na Rhoda wakaketi sebuleni.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna shida gani Rhoda?” Phares akauliza.



    “Nina ombi dogo kwako, mfalme,” Rhoda akasema akifinyanga vidole vyake.



    “Rhoda, tafadhali niite Phares. Una ombi gani hilo lililoshindwa kungoja?”



    “Phares, kuna mtu ambaye anaweza kutusaidia kujua wapi Malkia alipo!”



    “Malkia?”



    “Ndio, namaanisha Sandarus!”



    Phares akatabasamu.



    “Rhoda, kuna jambo ulilowahi kuliacha likakupita kwa jema?”



    “Phares, hili jambo kwako ni dogo?”



    “Hapana si dogo, ila juhudi zako ni za kushangaza. Tuachane na hayo, nani huyo anaweza kutusaidia?”



    “Kuna mzee anaitwa Tretho.”



    “Ndiyo nani huyo?”



    “Ni mfugaji fulani hivi anaishi ng’ambo ya mto.”



    “Umeshindwa kumalizana naye? – au shida ni nini?”



    “Sijashindwa kumalizana naye, tatizo hayupo. Askari wako walimkamata na kumtia ndani.”



    “Askari wangu? Bila shaka ana makosa?”



    “Ndio, na sijaja hapa kumwombea msamaha ila kukuomba niweze kuongea naye na tumsikilize nini anachoweza kutupatia.”



    Phares akashusha pumzi. Alifikiria kwa muda wa dakika moja kabla hajakata shauri la kumuita askari wake na kumwagiza amlete Tretho mbele yake. Asakri akatii na punde Tretho akaletwa.



    Akasimamishwa mbele ya mfalme.



    Alikuwa ni mzee mfupi mwenye ndevu nyingi nyeupe. Alikuwa amevalia joho la kaki linalomfikia chini kidogo ya magoti.



    Hakuwa na viatu, na mikono yake ilikuwa imefungwa kamba maalum wanazofungiwa wafungwa. Alikuwa ananuka ng’ombe, yeye pekee akionekana kutokujali harufu hiyo.



    Aliinamisha kichwa chake kumsalimu mfalme kabla hajatazama kinyenyekevu.



    “Unaweza ukaongea naye,” Phares akamwambia Rhoda akimwonyeshea mkono mzee Tretho. Rhoda akatabasamu na kuinamisha kichwa chake kutoa shukrani kisha akamgeukia mlengwa.



    “Tretho, unaweza kunisaidia kumtafuta mtu ambaye sijui yupo wapi?”



    Tretho akatikisa kichwa.



    “Hapana, siwezi,” alijibu kwa sauti yake kavu ya chini.



    “Tretho hakuna mtu anayetaka kukujeruhi. Nataka tu kufahamu ili unisaidie. Ninashida kubwa sana na nimeambiwa wewe unaweza kunisaidia.”



    Tretho kimya.



    “Unaweza ukanisaidia tafadhali?”



    “Siwezi kufanya hicho kitu. Aliyekwambia amekudanganya.”



    Rhoda akasaga meno kwa ghafira. Alimtazama Phares, Phares akamtikisia kichwa na kumnong’oneza:



    “Tumia busara,”



    Rhoda akahema kwanza kupunguza fukuto la hasira kifuani, alafu akamrudia Tretho na tabasamu.



    “Nitakupa chochote unachotaka endapo ukinisaidia. Unataka nini?”



    Tretho kimya. Alitazama chini.



    “Usiogope, sema wataka nini?”



    “Nataka mnitoe lupango,” hatimaye Tretho akanena. Rhoda akatabasamu.



    “Siyo hilo tu, bali pia msinitoze tena kodi kwa wanyama wangu. Sina kodi ya kulipa mara kwa mara. Ninafuga ng’ombe wale kwasababu ndiyo familia yangu pekee iliyobakia.”



    Wakati akisema hayo, macho yake yakawa mekundu. Rhoda akamtazama Phares na kumshika mkono. Akamnong’oneza:



    “Naomba umsikilize.”



    “Kutokulipa kodi?”



    “Tafadhali nakuomba. Ni huyu mmoja tu.”



    “Endapo wengine wakijua unadhani italeta picha gani? Vipi nao wakigoma?”



    “Haitatokea, tafadhali naomba,” alisema Rhoda akilegeza macho na kuuminya minya mkono wa Phares.



    Phares akatikisa kichwa mara moja. Rhoda akatabasamu, akamwambia Tretho kwamba amekubaliwa ombi lake. Tretho akawa radhi sasa kumsaidia.



    “Ili kufanikisha shughuli, kunahitajika vitu kadhaa: Majina matatu ya mlengwa anayetafutwa, na kitu chake chochote kile, aidha nguo, nywele ama kiatu.”



    Hili tena likawa jaribio kwa Rhoda. Atavitolea wapi hivyo vitu?



    “Kama hivyo vitu havipo?” akauliza.



    “Kazi inakuwa ngumu zaidi. Mahitaji mengine ni makubwa na yanagharimu,” akasema Tretho.



    Kabla Rhoda hajasema jambo, akamtazama kwanza Phares. Kuna vuguvugu la hofu lilikuwepo kati yao.





    ***





    “Una uhakika ndiyo hapa?” aliuliza mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa Sultan. Walikuwa tayari wamewasili eneo la Karim lakini hawakuona chochote hapo.



    Kulikuwa ni msitu wa miti na vichaka virefu. Hakukuonekana kama kuna dalili yoyote ya makazi ya watu, labda wanyama tu.



    Giza lilikuwa limeshamiri na sauti za wadudu zikitambaa kujaza anga.



    “Ndiyo hapa hapa mkuu!” akajibu mwanajeshi aliyeulizwa. “Huwa natumwa kuja hapa, napafahamu. Hapa ndiyo penyewe!”



    “Sasa Karim anaishi msituni?”



    “Hapana, mkuu! Kulikuwa kuna nyumba hapa.”



    “Sasa ipo wapi?”



    “Nashindwa kuelewa ipo wapi! Ila ni hapa.”



    Mkuu wa vikosi akaamrisha wanajeshi wake wapekue eneo zima la tukio. Zoezi likaenda kwa takribani dakika ishirini pasipo mafanikio. Hakuna kilichoonekana.



    “Hatujaona kitu, mkuu! Hamna mtu.”



    “Inawezekanaje?” mkuu wa vikosi akauliza.



    “Karim ni mlozi, mkuu. Atakuwa ametumia ulozi wake kujikinga,” akasema mwanajeshi mmoja. Hilo jambo likaonekana lina mantiki ndani yake.



    “Sasa tunafanyaje?” mkuu akauliza. “Sultan hawezi kutuelewa tukienda kumweleza haya. Kuna yeyote mwenye wazo?”



    Mwanajeshi mmoja akanyoosha mkono. Kabla hajasema alichonacho, mara akakakamaa kama mti. Macho yalimtoka na mishipa ya damu ikamsimama.



    Alianza kutikisika kama simu iliyowekwa mfumo wa kutetemesha. Mdomo ukatoa mapovu na macho yakatoa damu. Akadondoka chini na kufa!



    Wote wakapata hofu. Kilikuwa ni kitu cha ajabu kutukia!



    Kama haitoshi, akafuatia mwingine na mwingine kutengeneza idadi ya watu watatu. Wote wakafa kifo cha aina moja. Wakikakamaa na kutoa mapovu na damu. Kisha wakidondoka kama migomba.



    Wanajeshi wakatazama huku na huko. Hakukuwa na mtu waliyemuona. Sasa nani anawaua? Ila swali kubwa lilikuwa nani anafuatia kufa baada ya hao watatu?



    Mioyo iliwakimbia wakatota woga. Japokuwa walikuwa wameshikilia silaha zao mkononi, hazikuwa na faida wala kazi. Utapambanaje na kitu usichokijua wala kukiona?



    Akafuatia mwanajeshi mwingine … mwingine pia kwa kasi ya ajabu! Wengine wakaanza kukimbia kuokoa roho zao.



    Na wao hawakufika mbali, mara udongo ukaanza kutitia! Kila walipokanyaga palimomonyoka na kutengeneza shimo. Hakuna hata mmoja aliyebaki, wote wakamezwa shimoni.



    Wakajikuta mahala pa giza. Walikanyagana na kusukumana maana walikuwa hawaonani. Hawakujua wapi pa kwenda wala pa kutokea.



    Ilikuwa kizungumkuti!



    Wakiwa humo mara kwa mbali ukaonekana mwanga mdogo wa ginga la moto. Mwanga huo ulikimbia na kupotea. Haikujulikana wapi ulielekea.



    Ukapita muda mchache, ukaonekana tena mwanga wa ginga la moto ukiwa karibu tofauti na mwanzoni kana kwamba mtu aliyekua ameubebelea moto huo alikuwa amejongea karibu.



    Mara ukapotea!



    Ulivyokuja kuonekana tena, ukawa upo karibu zaidi ya mara iliyopita. Mara sauti ya panga ikasikika, sauti za watu kadhaa zikalalama kwa maumivu. Mwanga ulipoonyesha walikuwa ni wanajeshi watano wameuawa.



    Walikuwa wamelala wanavuja damu za kutosha.



    Kufumba na kufumbua mwanga wa ginga la moto ukapotelea mbali kana kwamba aliyeubebelea anakimbia kwa kasi! Pumzi za watu zikaanza kusikika zikihema hofu.



    “Mbeba moto ni muuaji!” ikafoka sauti moja.



    Haukupita muda mrefu, mara ginga la moto likaonekana tena kwa mbali! Likawa linapotea na kuibuka tena. Linapotea na kuibuka tena.



    Pasipo mashaka wanajeshi wakajiandaa kupambana.



    Lakini ajabu ginga hilo la moto lilipotea na kuja kutokea karibu na wanajeshi hao likiwa upande tofauti kabisa na ule uliotokea. Hivyo likawa limewapoteza wale waliokuwa wamejipanga.



    Likazima na mara sauti za watu wakilalama maumivu zikasikika. Watu wanne wakaenda. Walikuwa chini wakimwaga damu, tayari wamekufa.



    Ginga la moto likaonekana layoyoma.



    Haukupita tena muda mwingi, yakaonekana maginga mawili ya moto kwa mbali.





    La haula! Ina maana wauaji wameongezeka. Sasa watu wakashindwa kustahimili na kila mtu akakimbilia anapopajua yeye kuokoa maisha yake.



    Wakakanyagana na kusukumana. Kila mtu alikuwa anataka kuokoa roho yake hivyo wa mbele ni nani?



    Hawakujua wapi wanapoelekea na hawakujali ilimradi tu wajiweke mbali na ginga la moto la muuaji.



    Eneo walilomo lilikuwa ni kama bomba pembeni palikuwa hapapitiki na panateleza. Njia pekee iliyokuwa katikati ndiyo ilikuwa kavu na yenye ahueni.



    Malighafi yake ilikuwa ya mchanga. Tena wa kiasi kikubwa ambao ulikuwa unameza miguu ya wakimbiaji na kuwachosha kwa kuwapokonya pumzi.



    Wengi waliokimbia wakaanguka. Hawakuonekana ila vishindo vyao vilisikika na wenzao wakawakanyaga kwa juu.



    Vilio vyao vilivuma huku na kule wakilalama.



    Wale walioachwa na wenzao wakiwa wamepigwa na bumbuwazi na mchezo ule wa maginga ya moto, wote wakamalizwa.



    Haikubaki hata pumzi ya mmojawapo. Kwa mwanga wa maginga ya moto wakaonekana wakiwa wamelala chini wakimimina mito ya damu.



    Ajabu ni kwamba wale waliobebelea maginga hayo ya moto hawakuwa wanaonekana. Maginga haya yalikuwa yalikuwa yanaelea hewani!



    Kitu pekee kilichokuwa kinajulisha kwamba kuna mtu, ni kishindo cha miguu. Ama basi jambia lililokuwa linatumika kunyofolea roho za watu.



    Baada ya kazi ya mauaji kumalizika, sasa maginga hayo yakayoyoma. Haikujulikana yameenda wapi kwani yalizima kama taa zinavyozima umeme ukatikapo.





    **





    "Tuko wapi humu?" Sauti ya mwanajeshi mmoja wa Sultan ikauliza. Hawakuwa wanaonekana ila vishindo vyao vilikuwa vinasikika.



    Ukitulia na kuvisikiliza vishindo hivyo kwa umakini basi utabaini watu hawa walikuwa wachache, hata kumi hawafiki.



    Walikuwa wanaelekea upande mmoja wakiswagana kama mbuzi.



    "Hakuna anayejua wapi tulipo. Na hakuna mwenye uhakika kama tutatoka hai," alijibu mmoja kwa sauti ya huzuni.



    "Kama nikitoka humu, hii kazi siitaki tena!"



    "Kama ukitoka."



    "Ndio kama nikitoka. Najua nitatoka."



    Kukawa kimya. Baada ya muda mmoja akalipuka kwa sauti kuu:



    "Ona! Kuna mwanga kule."



    Kweli umbali wa kama hatua hamsini za mtu mzima kulikuwa kuna kama katundu kalichokuwa kanapitisha mwanga.



    Wanajeshi wakafurahia. Sauti za vicheko zilisikika wakiamini sasa wamefanikiwa kupata mlango wa kutoka humo shimoni.



    Wakaongeza mwendo. Wakakimbia zaidi na zaidi. Punde wakafikia hilo tundu na kuangaza juu.



    Kweli kulikuwa kuna uwazi na dunia nyingine yenye mwanga ikionekana. Ila kabla hawajafanya jitihada za kupanda huko, mmoja akasikika akiuliza:



    "Huu ni muda wa usiku, huu mwanga umetokea wapi?"



    Mwingine akasonya.



    "Nawe! Unadhani tuna muda wa kuulizana na kujadiliana tena humu?"



    Wawili wakamuunga mkono.



    "Kweli hatuna muda. Tupande na mengine tutayajua huko huko juu!"



    Watu hawa watatu wakafanya jitihada na kupanda huko juu. Wengine wakasita, wakangoja waone kama kuna lolote litakalojiri.



    Waliogopa kujitoa chambo.



    Basi wakangoja macho yao yakitazama juu, na masikio yakiwa makini kumeza kila taarifa itayakayoletwa.



    Wale waliopanda wajuu, watatu kwa idadi, wakaangaza huku na huko. Walikuwa wamechafuka na matope na nguo zao zina mabaki ya damu ambazo pasipo shaka zilikuwa za wale wenzao waliouawa.



    Hawakuona kitu chochote isipokuwa jangwa la michanga mekundu. Hapakuonekama wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia.



    Wapi pa kutokea na wapi pa kwendea.



    Anga lilikuwa la bluu na angavu ila jua halikuonekana wala mwezi.



    "Tunaelekea wapi?" Mmoja akauliza.



    "Twende huku!" Mwingine akajibu akinyooshea kidole upande wake wa kaskazini.



    "Huko ndo wapi?" Mwingine akauliza.



    "Sijui!" Akajibu yule aliyeonyeshea kidole chake huko kaskazini, akaongezea: "Ila naamini siku zote kaskazini ndiyo njia."



    Basi wenzake wakaamua kumwamini na kuongozana naye kuelekea huko kaskazini.



    Zikapita kama dakika kumi na tano.



    Wale walioachwa kule chini kwenye giza walivyoona kimya, basi nao wakashauriana kukwea kwenda kuungana na wenzao, pengine wamefaidika na uthubutu wao.



    Wakasaidiana na kukwea. Walikuwa watano kwa idadi. Nao pia walikuwa wamechafuka kwa matope na damu.



    Wakashangazwa sana na jangwa. Wakaangaza wapi waelekee.



    "Tufuate nyayo hizi!" Mmoja akashauri akinyooshea kidole nyayo za wenzao waliotangulia hapo kabla.



    Wote wakapendezwa na hilo wazo na basi wakaanza kuzifuata hizo nyayo.



    Wakatembea kwa mwendo mchache, kama dakika nane, wakakutana na damu mchangani.



    Wakashtuka sana na kujiuliza ni za nani. Kadiri walivyosonga mbele basi na damu zikaongezeka. Nyayo zikisambaa.



    Muda si mrefu mbele wakaona miili ya wenzao ikiwa imelala chini. Vichwa vimelala pembeni!



    "Mungu wangu! Tumeisha," akalia mwanajeshi mmoja.



    "Mimi sikutaka kuja huku. Ona sasa!" Akalalama mwingine.



    Wote wakajazwa na hofu. Wakatazama huku na huko hawakumwona muuaji. Yupo wapi?



    "Turudini jamani!" Akashauri mmoja. Na kabla hajawangoja wenzake akaanza kutimua.



    Wengine nao wakipelekeshwa na woga wakaanza kukimbia kurudi shimoni.



    Wakafika ila hawakulikuta shimo. Hawakujua limeenda wapi!



    "Kweli ni hapa?" Akauliza mmoja.



    "Huoni hapa ndipo nyayo zilipoanzia?" Akajibu mwingine kwa jazba.



    Kufumba na kufumbua wakashangaa wakiwa wamezingirwa na kikundi cha watu waliovalia majoho mekundu.



    Watu hawa walikuwa wameziba nyuso zao wakiacha macho tu. Mikononi mwao walikuwa wamebebelea majambia makali.



    Walikuwa wanalingana kimo na maumbo ya mwili kana kwamba mapacha wa mfuko mmoja wa uzazi.



    Pasipo kuuliza watu hawa wakaanza kushusha majambia yao kuwakata kata wanajeshi wa Sultan.



    Wakambakiza mmoja tu akiwa hai kisha wakapotea kama walivyokuja. Mwanajeshi yule mbakizi asiamini kama amebakizwa.



    Aliwatazama wenzake walivyokuwa wanaelekea kuwa wa baridi. Akajihisi amepoteza nguvu.



    Jangwa lilipotea usiku ukarejea kama kawaida. Na mwanajeshi huyu akajikuta palepale alipokuwa kabla udongo haujatitia kutengeneza shimo.



    Hakujua amefikaje. Aliondoka kwa mbio kali moyo ukimkita kama ngoma.



    Ila kama kuna swali ambalo lilikuwa linamsumbua kichwani ni kwanini aliachwa hai ingali wenzake wameuawa?



    Lengo lilikuwa ni moja tu; kwenda kumpasha habari Sultan. Ya kwamba Karim ni mtu wa aina gani.



    Ya kwamba Karim ana uwezo gani.





    ***





    "Naweza nikampata wapi?" Fluffy alimuuliza mlinzi mmojawapo aliyekuwa amesimama kumsikiliza.



    Mwanamke huyo alikuwa amevalia nguo zake za kazi. Ila siku hiyo hakuwa amebana nywele zake. Aliziacha huru zifanye vile zinapenda.



    Mlinzi alitikisa kichwa chake akasema:



    "Sijamwona kabisa."



    "Tangu lini?" Fluffy akauliza.



    Mlinzi akajaribu kuwaza, Fluffy asingoje jibu akaenda zake.



    Alikuwa anawaza wapi alipo Seth. Haikuwa kawaida kwake kumsaka hivyo. Mara moja tu anapomhitaji huwa anampata. Tena kwa kuagiza tu.



    Sasa aliagiza tokea jana, siku ikaenda. Na leo anamsaka hamwoni!



    Ameenda wapi?



    Hakutaka kukata tamaa akaendelea kuulizia. Mtu mmoja angalau akampatia mwanga. Alimwambia:



    "Mara yangu ya mwisho kumwona alikuwa maskani mwake."



    "Maskani mwake ndiyo wapi?" Fluffy akauliza.



    "Kulee juu ya paa!" Akanyooshea mwelekezaji, basi Fluffy asipoteze muda akaenda huko juu.



    Akatazama lakini hakuona kitu. Ila wakati anapekua pekua akaona kijikaratasi fulani. Alikifuata akakiokota na kukitazama.



    Kilikuwa kimeandikwa kwa alama na lugha ngeni. Hakuweza kukielewa kina ujumbe gani na kinamaanisha nini.



    Ila akakiweka mfukoni kisha kwa muda kidogo akajiuliza kwanini Seth hupenda huko juu. Neno 'maskani yake' inaonyesha ni eneo lake pendwa.



    Hakutaka kujichosha kutafuta majibu, akatoka huko na kwenda mpaka kwenye makazi ya Dummy.



    "Unajua lolote kuhusu hii karatasi?" Akauliza.



    Dummy akachukua muda kwanza kuitazama.



    "Umeitoa wapi?" Akauliza.



    "Inaweza kusaidia kumpata Seth?" Fluffy naye akauliza. Dummy akatikisa kichwa na kujibu:



    "Hapana. Ni taarifa tu ya mambo fulani."



    "Kwahiyo haiweza ikasaidia kumpata Seth?"



    "Ndio, haiwezi."



    Kukawa kimya kidogo.



    "Lakini jenerali, unamhitaji Seth kiasi hiki?" Dummy akauliza.



    "Kwani wewe haumhitaji?" Fluffy naye akauliza. Dummy akatabasamu kwa mbali.



    "Namhitaji."



    "Sasa mbona waniuliza?"



    "Si kwa ubaya. Nilidhani pengine naweza nikajazia nafasi yake kama hutojali."



    "Usijali, shida yangu ilikuwa ni yeye tu."



    "Sawa jenerali."



    Fluffy akachukua karatasi na kwenda zake nyumbani. Dummy akahakikisha mwanamke huyu amepotea kabla hajatoka ndani akienda upande wa magharibi.



    Baada ya punde akawa ndani ya nyumba ya Bozi. Wakapena salamu na kujiweka mezani. Dummy akamweleza Bozi juu ya Fluffy.



    "Hatoweza kumpata," Bozi akasema akitabasamu. "Seth yupo mahali salama zaidi."



    "Lakini mkuu, kwanini anahangaika kumtafuta hivyo? Hudhani kwamba wana agano?" Dummy akauliza.



    "Huwezi jua, ila kwakuwa Seth tunaye sisi basi hamna haja ya shaka,"Bozi akajibu akitabasamu, akaongezea: "Lakini huenda jenerali wana mahusiano na Seth. Na sasa anamtafuta mpenzi wake."



    Akacheka.



    "Ila Mkuu, vipi kuhusu ile karatasi?" Dummy akauliza.



    "Usijali. Hakuna atakayeweza kumtafsiria. Hakuna himaya hii nzima. Mwache abaki nayo kama kumbukumbu ya mpenzi wake."



    Kisha akacheka tena.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Waliteta na kuteta kwa siri mafichoni, wakatikisiana vichwa kabla ya kupeana mikono ya kheri na matabasamu. Wakaachana.



    Kila mmoja akashika lake ila wakiwa na moja linalofanana kwenye vichwa vyao – nalo ni mapinduzi mapinduzi. Mapinduzi ya kumwondoa Malkia ili waitie himaya mikononi mwao.



    Walipeana miadi ya kukutana baadae kwa ajili ya kuelezana mambo kadhaa.



    Jambo hili lilikuwa ni la siri, ila tena si la siri maana wahenga walishawahi nena kwamba hakuna siri ya watu wawili duniani.





    **





    “Umekamilisha kila kitu?” Aliuliza Tretho. Macho yake yalikuwa mekundu na nguo zake za kigagula. Alikuwa ndani ya kijengo chake cha mbavu za mbwa.



    Alikuwa anaongea na Rhoda ambaye alikuwa amevalia kimaridadi. Hadhi yake haikuendana na mazingira ya pale alipokuwepo. Mkono wake wa kuume ulikuwa umeshikilie kakibuyu kadogo kapya.



    Alikuwa hapo kwa madhumuni ya kuja kufanya ulozi. Alikuwa mshida na hivyo basi hakuwa na budi kuendana na mahitaji.



    “Nimekamilisha ndio,” akajibu Rhoda akitikisa kichwa. Akazama ndani na kuketi kwenye kigoda kidogo kikuukuu.



    Ndani kulikuwa kuna joto na harufu yake haikuwa ya kupendeza. Jiko lilikuwa humo humo na kadirisha kadogo kalichokuwepo kalikuwa kamegeukia zizini.



    Rhoda alihisi anakosa pumzi, ila akavumilia na kuupiga moyo konde. Tretho alikuwa kando yake akichemsha majani fulani ya kambakamba. Majani hayo yalikuwa yanatoa harufu ya mlonge.



    Tretho akakoroga majani hayo kisha akamtazama Rhoda.



    “Umepata ya nani?”



    “Ya mwanaume mmoja mkulima wa huko Kondeni.”



    “Naomba niione.”



    Rhoda akamkabidhi Tretho kibuyu kile. Tretho akakifungua na kisha akamiminia kidogo kiganjani mwake.



    Ilikuwa ni damu!



    Akatabasamu kabla hajailamba damu hiyo na kuisikilizia tamu yake.



    “Ni sawa. Ni ya mkulima.”



    Rhoda akastaajabu na kujiulizia ndani ya kifua chake. Ina maana kama asingeleta ya mkulima wa huko Kondeni ingegundulikana?



    Mara Tretho akamtazama na akimnyooshea mkono. Alikuwa anataka na mchanga. Rhoda akapenyeza mkono wake ndani ya mfuko kisha akatoa kifuko kidogo cheusi, akamkabidhi Tretho ambaye alikifungua upesi na kuuliza.



    “Una uhakika lakini?”



    Rhoda akatikisa kichwa chake.



    “Ndio, babu.”



    Mchanga huo ulikuwa ni wa nyayo za mtu anayeaminika kuwa Malkia. Waliupata baada ya mwanajeshi yule aliyetoa taarifa kuwapeleka eneo alilodai alimwona Malkia, huko wakaona nyayo na kuzichota.



    Moja ya sharti la Tretho ilikuwa ni damu ya mkulima na mchanga wa nyayo za mtu anayetafutwa. Na hayo yalikuja baada ya Rhoda kushindwa kutoa taarifa za Malkia zilizokuwa zinahitajika.



    “Una uhakika huu mchanga ndiyo wenyewe?”



    Rhoda akatikisa kichwa kukubali. Basi Tretho akachanganya majani yake na damu ile ya mkulima wa kondeni, kisha mchanga ule wa nyayo za Malkia akajipangusia mikononi mwake, viganjani.



    Baada ya muda kidogo akaepua sufuria yake ya dawa na kuchukua kaniki ya kijani. Akampatia maelekezo Rhoda.



    “Utanifunika gubi gubi na hii kaniki. Hakikisha hewa haipiti. Alafu uwe msikivu sana kunisikiliza japokuwa nitaongea lugha usiyoifahamu.”



    “Sasa babu nitashikaje na kuelewa lugha nisiyoifahamu?” Rhoda akauliza. Tretho akamwambia jukumu la kuelewa lugha hiyo si la mteja, bali lake. Ni yeye ndiye atakuja kumtafsiria.



    “Utanakili maneno machache utakayokuja kunambia pindi nivuapo hii kaniki.”



    Baada ya maelezo hayo, utekelezaji ukaanza ambapo Tretho alichovya kidole chake kwenye damu na kutia ndonya kwenye paji la uso. Akainamia sufuria iliyokuwa inafuka moshi wa majani, Rhoda akamfunika.



    Zikapita kama dakika mbili, wakati huo Tretho alikuwa anahangaika ndani ya kaniki, mara akaanza kunguruma kama simba. Akafoka foka kama mtu anayekabwa, mara akatulia tuli.



    Mara akaanza kuhororoja kwa lugha za sayari zingine. Rhoda kwa umakini akajitahidi kunasa machache machache. Zoezi lilipokwisha, akamtajia Tretho yale aliyobahatika kuyatunza kichwani.



    Tretho kabla hajaongea, akatikisa kichwa.



    “Yupo mbali sana!”



    “Wapi?” Rhoda akawahi kuuliza. Tretho akajaribu kumweleza kwa kutumia uwezo wake wote. Rhoda akafadhaishwa na majibu.



    “Kama yupo huko mbali kote, hapa anafikaje? Na ana mkufu?”



    “Bila shaka haji kwa miguu wala farasi kwa maana ni safari ya miezi. Na kuhusu mkufu, sijauona. Pengine kwakuwa amevalia gauni la kuficha kifua.” Tretho akajibu kwa kujiamini.



    Rhoda akatekwa na mawazo kichwani kwa muda akibung’aa kabla hajalipuka kuuliza:

    “Unaweza kujua anakujaje hapa na kama kuna namna za kumzuia?”



    Tretho akashusha pumzi ndefu. Macho yake yalibeba hofu.



    “Unajua hili la kutambua mahali, ndilo huwa nalifanya mara kwa mara kwasababu ni jepesi na lisilodai makubwa. sijawahi kuhangaika na hayo mengine maana njia zake zina madai makubwa.”



    Kitu ambacho Tretho hakuwa anajua ni kwamba Rhoda anaweza akafanya lolote lile ilimradi malengo yake yatimie. Si mtu wa kujiuliza mara mbilimbili punde linapokuja swala la kupata anachokitaka.



    Ila alipuuza, alikuwa ana mambo kadhaa ya kufanya na kujadili kichwani mwake. Haswa kuhusu mkufu. Kama Malkia yupo hai, je atakuwa na mkufu?



    Ana historia ya kuzamia ndani ya Tanashe, alitoka na mkufu? Akili yake ikajibu ndio na ndiyo maana amepata nafasi hata huko alipoenda. Ila akabishana na hili. Bado hakuamini kama inaweza kuwa rahisi kwa mtu kutoka hai Tanashe.



    Pengine Malkia amekuwa mlozi! Na ndiyo maana anaweza kuja huku Goshen na kurudi huko alipo.



    Malumbano ya hoja yakazuka kichwani mwake, lakini bado akaona ana haja ya kwenda Tanashe. Kule kuna jambo atalipata, kule kuna kitu muhimu atang’amua ambacho kitamsogeza hatua moja mbele.



    Ila akapata wazo.



    “Tunaweza kwenda wote Tanashe?” akamuuliza Tretho.



    “Hapana, nashukuru,” Tretho akajibu akikunja kaniki yake. Rhoda akambembeleza sana na kumuahidi kumpatia donge nono ambalo hatalisahau endapo akiambatana naye kwenda huko.



    “Ni lini waenda?”



    “Sina sababu ya kungoja tena, kesho mapema.”





    ***





    Ndani ya nyumba ya pembezoni majira ya usiku mwepesi.



    “Umehakikisha kila mtu muhimu yupo?” Aliuliza Bozi akimtazama Dummy. Dummy kabla ya kujibu akageuza kwanza shingo yake na kuwatazama wanaume fulani watano.



    “Wote wapo.”



    Wakaketi na Bozi akawamiminia mivinyo ndani ya glasi zao kubwa. Ulikuwa ni muda murua kwao. Walikutana kwa ajili ya kuyapanga mambo muhimu kwenye mlengo wao wa mapinduzi.



    Mbali na Bozi na Dummy, wanaume wengine watatu walikuwa ni wanajeshi, na wawili waliobakia wakiwa wananchi wa kawaida, haswa wakijishughulisha na vijibiashara.



    Wakiwa wanaonyeshana nyuso za furaha, wakateta na kuyapanga mambo yao ya kidhalimu. Kila mtu alitoa wazo lake juu ya nini kifanyike ili barabara ya kufikia lengo iwe sawa.



    Katika kila njia ambayo ilipendekezwa, basi na umwagaji damu haukukwepeka. Mawazo ya wote yalisikizwa na kupewa uzito unaostahili na mratibu wa kikao bwana Bozi – mwenyeji.



    “Hili jambo ni nyeti. Tuhakikishe linakuwa hivyo mpaka pale litakapotimia. Hata huko mnapolisambaza, hakikisheni halivuki juu ya meza,” Bozi alitoa angalizo kabla ya kuendeleza soga.



    Akayarejelea makubaliano yao ya kikao kabla naye hajatia neno.



    “Kuna watu wa kuuawa, kuna watu wa kubakiziwa uhai. Mimi nina wazo pia, kwanini mapinduzi haya yasiwe ya kimya? Hata wale watakaouawa ibakie kama simulizi tu isiyojulikana nani mtunzi?



    Kumbuka ni watu wasiozidi watano ndiyo ambao labda wanaweza kaa mbele ya njia. Sasa ya nini tuhatarishe makubwa?”



    Wazo likaungwa mkono, lakini litatekelezwaje? Bozi akatoa tena ufafanuzi.



    “Kwenye hii kamati yetu tutahitaji tena watu kama watatu hivi, na basi kazi hii itakuwa nyepesi kama unyoya kwenye pepo.”



    Na kwa kufanya kazi iwe nadhifu, basi Bozi akasema ataifanya kwa mikono yake. Ndani ya siku mbili tu atakuwa ameshaikamilisha na atawaita tena kuelezana hatua inayofuata.



    “Kwa sasa tulizeni makoo na midomo yenu tusije tia kitumbua mchanga.”



    Wakanywa na kunywa. Kama tulivyosema hapo awali, huu ulikuwa ni muda murua kwao.





    ***





    Akiwa anahema kama mbwa, akadondoka mbele ya Sultan. Mwanajeshi huyu pekee msalia wa janga la Karim alikuwa amechoka mno. Alikuwa anavuja jasho jingi, macho yakiwa yamemlegea kwa kukosa nguvu.



    Ni usiku mzito sasa akiwadia hapa, alitaka kuonana na Sultan asilale kabisa mpaka atomize hiyo haja. Japo ilikuwa ni usiku, ilibid Sultan ataarifiwe. Na kwasababu za uzito wa kazi waliyoenda kuifanya, Sultan hakujivuta kwenda kupokea ripoti.



    Ila alifanya kwa siri maana mkewe hakuwa anajua kama aliagiza kikosi huko kwa nduguye. Kwa akili yake alijua mumewe amesamehe na kusahau.



    “Vipi huko utokako?” Akauliza Sultan aliyekuwa amekabwa na hamu ya taarifa. “Wenzako wako wapi?”



    “Wote wamekufa!” akajibu askari jeshi huyu wa Sultan kisha akaendelea na zoezi lake la kutafuta oksijeni.



    “Wamekufa!” Sultan akastaajabu. “Nani ameuwaua?”



    “Karim! – Karim amewaua wote!”



    Mwanajeshi huyu alipopata ahueni ya hewa, akamweleza Sultan yale yote yaliyotokea kwenye uwanja wa vita, vimbwanga na maajabu yake.



    “Wala hatukumwona tunayepambana naye ila tuliisha!”



    Mpaka anamaliza kutoa mkanda mzima, akawa ameshamjengea hofu Sultan.



    “Ameniambia nije nikupe salamu zake. Na amesema kama wewe umetuma wa kwako, basi ujiandae kwani naye atatuma wake.”



    Sultan akahisi tetemeko la moyo. Alimruhusu askari yule aende kisha akarejea ndani ambapo hakukaa kwa amani bali mawazo. Alimtazama mkewe pembeni yake akiwa amelala, akajiuliza kama ana haja ya kumwamsha watete.





    Alijazwa na hofu. Kwanza ya kitisho cha yale yaliyotukia huko kwa Karim, na pili kumshirikisha mkewe kwa jambo ambalo alimkataza kulifanya.

    Akabaki akiwaza na kuwazua. Akanyoosha mkono kabisa kumwamsha mkewe, ila akasita na kuamua tu alale kwani kesho yake wataongea vema. Roho yake ikakubali.

    Akalala na asubuhi ya mapema akaamka na kumweleza mkewe yale yote yaliyotokea. Na kufanya maelezo yajitosheleze, akamwalika na yule mwanajeshi pekee aliyenusurika kifo ahadithie yale aliyokumbana nayo kwa Karim.

    “Sasa tunafanyaje mke wangu?” Sultan akamuuliza. Uso wake ulikuwa kielelezo cha namna ya woga ulivyo.

    Mke wake akatikisa kichwa kwa masikitiko. Hakutaka kumlaumu mumewe kwa yaliyotukia tayari, hivyo akaamua kumtafutia namna ya kumsaidia.

    “Nitaenda kuongea naye, usijali.”

    Japokuwa Sultan hakutaka kuonekana mwoga mbele ya mkewe, akaigiza mwenye ujasiri, mkewe akawa mwerevu kuliona hilo. Kwani kama asingelikuwa mwoga, asingelimsirikisha jambo hilo kama vile ambavyo hamshirikishi kwenye mambo yake mengine.

    “Utaenda kumwambia nini?” Sultan akauliza.

    “Najua mwenyewe. We niachie hiyo kazi.”

    Sultan akamuuliza mkewe kama atahitaji ulinzi. Mke akasema yupo sawa, atahitaji mmoja tu ambaye atamsindikiza safarini. Sultan akaafiki, japo kishingo upande.



    ***



    “Tayari, tunaweza kwenda,” alisema Rhoda. Mwanamama huyu aliyekuwa amevalia suruali ya ngozi na viatu virefu pamoja na blauzi nyeusi iliyokuwa imekaba mwili.

    Kwenye nyonga yake alikuwa amesimamisha panga. Nywele zake alikuwa amezibana vema, na alionekana yupo tayari kwa ajili ya vita.

    Pamoja naye alikuwa ameongozana na wanajeshi thelathini. Wote walikuwa na farasi wao. wamejiandaa kivita. Macho yao yalikuwa yanawatazama Rhoda na Phares waliokuwa wamesimama malangoni mwa hekalu za mfalme.

    “Kwahiyo upo radhi kabisa, kwamba haunihitaji?” aliuliza Phares akiwa ameshika mikono ya Rhoda.

    “Usijali, Phares. Goshen inakuhitaji zaidi. Watabakiaje pasipo mfalme?”

    Wakakumbatiana kabla ya Rhoda kwenda moja kwa moja upande wake wa kushoto, kukutana na Tretho. Mzee huyu naye alikuwa amevalia vema siku hiyo, si yale matambara yake.

    Alikuwa amevamia suruali nyeusi na shati pana la kaki. Vyote alipewa na Rhoda. Mgongoni mwake alikuwa amebebelea kifurushi kikubwa cha madawa.

    Alimtazama Rhoda akampokea kwa tabasamu.

    “Twende,” Rhoda akamwambia akimwelekezea na shingo yake. Tretho akamfuata farasi wake na kupanda. Wakaanza safari ya kwenda Tanashe.

    Rhoda alikuwa na amani moyoni mwake kwani hakuwa amesahau dawa aliyopewa na Venin. Dawa ya kumkinga na walozi wote waliopo huko Tanashe.

    Baada ya masaa kadhaa tu wakawa wamezama ndani ya Tanashe. Kuingia ndani ya himaya hii ilikuwa ni rahisi sana ila kutoka ilikuwa ni sadaka. Ilikuwa ni jasho na damu.

    Kutoka kilema ndani ya himaya hii ilikuwa ni ushindi, tena mkubwa mno.

    Kuzama tu ndani ya himaya, ikawachukua kama dakika nane tu, kukaanza kuwa kiza. Ni mawingu meusi yalikuwa yamefunga anga na kutengeneza giza totoro. Giza ambalo waweza kusema ni la saa moja, na watu wazima wakaamini.

    Basi ikawalazimu wanajeshi wawashe maginga yao ya moto kutengeneza mwanga. Wakasonga mbele na mbele. Kumbuka hawajui wanapoelekea. Ni mkufu ndiyo unaotafutwa ila hawaujui wapi pa kuanzia.

    Basi mara njiani wakakutana na kundi kubwa la mbwa. Mbwa hawa walikuwa weusi kama vile rangi iliyokuwepo muda huo. Macho yao yalikuwa mekundu yakiwaka kama moto.

    Walikuwa ni wakubwa kama ndama. Walionekana ni wenye nguvu kwa ujazo wa misuli yao na walikuwa wana njaa. Njaa ya nyama, tena ya moto.

    “Hawa wote ni mtu mmoja,” akasema Tretho.

    “Umejuaje? Wanataka nini?” Rhoda akawahi kuuliza huku macho yake yakitazama mbwa wale.

    “Najua, na wala tusihangaike nao. Waambie wanajeshi wako wasifanye jambo lolote baya kwani hawa ni wapofu.”

    Rhoda akamtazama kwanza dereva wake, Bonas, kisha akapaza sauti kwa kuwataka wanajeshi wake wasifanye jambo lolote. Wote wakatii amri. Wakapita salama tena katikati ya msitu huo wa mbwa ambao uligeuka kuwa moshi.

    “Huyo ni mlozi mwepesi,” alisema Tretho. “Yupo mmoja tu na siyo wale wenye nguvu.”

    Safari ikadumu kwa muda wa kama lisaa ndipo wakaona nyumba kubwa mno. Nyumba hiyo ilikuwa ni ndefu na yenye umbo la moja. Lilionekana dirisha moja tu, tena kwa juu ambalo ndilo hilo lililokuwa lina mwanga pekee.

    Rhoda akamuuliza Tretho kama wanaenda hapo na anajua lolote kuhusiana na hapo. Tretho akatikisa kichwa chake kabla hajajibu:

    “Sina ujuzi mkubwa wa walozi isipokuwa wale wadogo na wa kawaida. Ila kwakuwa una kinga twaweza kwenda.”

    Rhoda akakata shauri na kusonga eneo hilo. Shida yake ilikuwa ni kupata tu mwelekeo. Ama mtu ambaye anaweza kumuulizia.

    Walipofika hapo wakaita lakini kulikuwa kimya. Mara wakiwa wanangoja bado, ile taa iliyokuwa inawaka kule juu ikazima. Na jengo zima likawa kimya.

    Ndani ya giza la nyumba, sauti ya mtu anayenusa ikasikika, na kisha ikafuatia sauti iliyoshangaa.

    “Binadamu?”

    Baada ya sauti hiyo kukaendelea kuwa kimya. Rhoda na wenzake wakabashiri kwamba hamna kitu hapo. Wakapanga kuondoka. Ila kabla hawajahepa, upepo mkubwa ukavuma!

    Rhoda akahangaika sana kujishkiza. Baada ya punde wakakaa vema. Ila laiti kama angelikuwa hana kinga basi wote wangekuwa wameenda mpaka muda huo.

    Upepo uliokuwa umepuliza, haukuwa wa kawaida. Ulikuwa ni ule wa kufanya watu wageuke kuwa majivu kufumba na kufumbua. Ulikuwa ni upepo wenye dawa ila haukufua dafu. Na basi hapo mwenyeji, baada ya kutoona hajafanikiwa, akajitokeza.

    Alikuwa ni mwanaume mrefu mwembamba mwenye nywele ndefu nyeusi. Alikuwa mweupe pe mwenye macho ya paka. Alikuwa amevalia suti zile za zamani zikiwa zimemfiti vizuri mwili wake.

    “Nyie wakina nani na mnataka nini hapa kwenye himaya yangu?” akauliza. Rhoda akajitambulisha yeye ni mwanamke toka Goshen mwenye shida ya kusaidiwa. Basi mwanaume yule mwenyeji akamtaka aingie ndani kuteta.

    Rhoda akataka kuingia na Tretho, kama msindikizaji, mwenyeji akamkatalia.

    “Utaingia wewe peke yako.”

    Japokuwa alikuwa na kinga, bado Rhoda alikuwa anahofia. Alizama ndani ambapo hakuona chochote zaidi ya giza totoro. Hakukuwa na chanzo chochote cha mwanga humo ndani.

    “Karibu sana,” sauti ya mwenyeji ilisema pasi na mashaka. Lakini Rhoda hakuona wapi pa kukaribia. Pote palikuwa giza!

    “Ooooh hauoni!” alisema mwenyeji. Na punde akasnap vidole vyake, na punde mwanga ukawaka nyumba nzima!

    Nyumba ilikuwa kubwa na yenye kupendeza. Rhoda akaketi na kujadili kidogo na yule mwenyeji wake, akamdanganya kwamba amepoteza mkufu wake, na mtu aliyemuibia alizama ndani ya himaya hiyo.

    Mwenyeji akasema hamfahamu, ila anaweza akamsaidia endapo tu akimwambia kwanini ameamua kuhatarisha maisha yake kuja kuutafuta mkufu huo.

    Rhoda akasita kumwambia. Akamsisitiza tu amasaidie. Lakini mwenyeji hakuelewa na akataka kumdhuru Rhoda. Akageuka kuwa mnyama mkubwa mweusi mithili ya ng’ombe. Kabla hajafanya kitu, mara mwanga wa jua ukarejea kwenye hali yake.

    Na yule mnyama akanywea wakati Rhoda akifanya jitihada za kutoka humo ndani. Akampanda farasiwe na kutimka.

    Lakini wakati Rhoda anaendelea kuzunguka, kuna mtu alikuwa anamtazama kwenye rada zake. Alikuwa anamwona kila anachofanya, kila anapoenda.



    ***



    Sauti ya kokoro kokoro .... kokoro kokoro ... kokoro kokoro ikarudia tena na mara mlango ukafunguka!

    Hatimaye zoezi lake la kujiokoa lililokuwa linafanyika kila siku pasipo mafanikio, leo likazaa matunda.

    Mkononi mwake alikuwa ameshikilia pini nyembamba aliyoinyofoa toka kwenye nguo yake. Pini ambayo amekuwa akihangaika nayo kufungulia kufuli tangu siku ya kwanza alipotupiwa ndani ya chumba hicho cha giza.

    Seth akatazama huku na kule. Palikuwa shwari. Hakujua kwanini walinzi hawakuwepo hapo. Pengine hawakuwa wanategemea kama anaweza kuchoropoka humo.

    Akatoka upesi na kukimbia kwa tahadhari. Akauficha uso wake usionekane na wengineo ambao labda wanaweza kuwa maadui.

    Hakwenda kwake, akanyookea moja kwa moja mpaka nyumbani mwa Fluffy, jenerali. Hapo akaomba ruhusa walinzi aonane na mkuu huyo.

    Jambo hilo likawa si jepesi. Ila Fluffy alibahatika kumwona hivyo akaagiza aruhusiwe. Akazama ndani.

    Seth alikuwa na uso wa uoga. Hata wakati anaingia ndani alikuwa anatazama nyuma yake kila saa akidhani kuna mtu anamfuata. Alipoketi akamwambia Fluffy kwamba mazingira si salama.

    "Kwanza ulikuwepo wapi?" Fluffy akauliza. Seth akamwambia alikuwa ametekwa, Bozi akihusika na tukio hilo.

    "Kivipi? Mbona nilimuuliza kuhusu wewe. Hakuwa na taarifa! Kwanini akuteke?"

    Seth akamweka bayana Fluffy ya kwamba Bozi anataka kupindua madaraka. Fluffy akashangazwa sana. Ilimuwia vigumu kuamini.

    "Kwanini afanye hivyo? Kuna lolote ambalo halipo sawa?" Akauliza.

    Seth akamwambia watu hao hawahitaji kutafuta lisilo sawa, bali utawala. Na watafanya lolote lile kuhakikisha wanaupata.

    Habari hizo zikamstaajabisha sana Fluffy. Hakuwahi kutaraji kama jambo kama hilo laweza kutokea.

    Akaona hizo taarifa zinabidi zimfikie Malkia haraka iwezekanavyo kwa usalama wake. Haraka akamtaka Seth waende huko.

    Akaenda chumbani na kuchukua ile karatasi yake ya siri. Wakatoka nje na Seth. Hapo tu mlangoni wakakutana na Bozi akiwa ameambatana na kikosi cha wanaume watano.

    Wanaume hao walikuwa wamebelea silaha na kujivesha sura za ghadhabu.



    Haikuwa rahisi kwa Fluffy kupambana na watu hao. Alistaajabu wengine walikuwa ni walinzi wake wa karibu. Akawekwa chini ya ulinzi na kuchukuliwa kimya kimya kwa siri wakipita njia panya mpaka kwenye jengo lao walilomfungia Fluffy ndani.



    Mbaya zaidi watu hawa walikuwa wamekwapua karatasi ile ya siri ya Fluffy. Karatasi ambayo ilikuwa inaeleza mambo ya siri ya kule Misri. Karatasi ambayo Fluffy alikuwa ameificha asimwambie mtu kuhusu, isipokuwa tu Seth.



    Japokuwa alipambana kunusuru karatasi yake, hakufua dafu kwenye mikono ya wanaume watano, ukitazama Seth hakuwa mtu mwenye ujuzi wowote kwenye maswala ya kujilinda. Kweli hupewei vyote.



    “Sasa mtakaa humo wapenzi. Bila shaka mlikumbukana sana,” Bozi akasema kwa kebehi kisha akaangua kicheko. Ingawa Fluffy alimtishia na kumwahidi atammaliza kwa mikono yake, Bozi hakuonekana kujali.



    Zaidi akampungia mkono na kuufunga mlango akiwaacha wafungwa gizani.



    “Bado na yule mwenzenu!” Sauti ya Bozi iliwafikia Fluffy na Seth waliokuwa ndani, gizani. Kisha ikafuatia kicheko kilichokuwa kinaishilia kadiri na muda.



    “Sasa tunafanyaje, Seth,” Fluffy akauliza kwa hofu. Sauti yake ilikuwa ina ashiria anguko, huzuni.



    Lakini kinyume chake, Seth akamwambia kuna tumaini. Alikuwa anaamini watatoka mule, na wataikomboa Sawaridi kwa mara nyingine tena.



    “Maadui hawakuisha. Ni bora adui wa nje kuliko yule wa ndani unayeshirikiana naye sahani na kijuiko,” Seth alisema kwa sauti ya chini.





    ***





    Baada ya hatua nzito, mlango wa nyumba ya mfanyabiashara Melkizedek unagongwa mara tatu, kisha mgongaji anatulia. Alikuwa ni mwanajeshi, yule aliyepewa kazi na mfalme ya kumfuatilia Tattiana katika mienendo yake yote.



    Tattiana, binti wa Melkizedek ambaye alitokea kukamata jicho la mfalme. Binti mwenye macho mazuri, uso wa kistaarabu na nywele kama unyoya wa sufi.



    Punde mlango ukafunguliwa na Fanty, kaka yake Tattiana, akauliza amsaidie nini mlinzi yule ambaye alisema anataka kuonana na baba yake kama yupo.



    Haraka Fanty akaenda kumfikishia baba yake ujumbe, ndani ya muda mfupi akashuka kukutana na mwanajeshi.



    “Karibu.”



    Uso wa Melkizedek ulikuwa na wasiwasi. Siku zote ukiwa unajua kuna jambo baya umelifanya, basi ukutanapo na mhusika ama mtendwa, basi waanza kujitunuku mashaka.



    Akili ya Melkizedek ilikimbia haraka na kuwaza kwamba ukute makubaliano yake na yule mzee wa baraza kuhusu biashara ya Cedar yamebumburuka, na sasa amefuatwa kukamatwa.



    “Ahsante, sikaribii. Nina ujumbe toka kwa mfalme.” Mwanajeshi akamkambidhi Mlekizedek barua iliiyokuwa imefungwa na kamba ya madini ya fedha, ikichapwa na mhuri wa mfalme.



    Mwanajeshi akaenda zake akimwacha Melkizedek anaikagua barua ile. Akazama ndani na kumwita mkewe kumjulisha kuhusu barua toka kwa mfalme.



    “Itakuwa inamhusu binti yetu,” mama akasema upesi. Alikuwa amevalia gauni lake la thamani. Mkono wake ulinyaka barua toka mikononi mwa mumewe, haraka akafungua ujumbe huo na kuusoma.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ulikuwa ni ujumbe wa mfalme akiomba kukutana na Tattiana.



    “Si nilikuambia!” mama akalipuka. “Hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea ndoa. Endapo binti yetu akimkarimu vizuri mfalme, basi tutakuwa wakwe.”



    Mama pasipo kupoteza muda akamwita mwanae na kwenda naye chumbani. Akamwandaa vema kwa kumkwatua na kumchagulia nguo iliyopendeza macho yake. Lakini zaidi akamhusia asimwangushe kwani hiyo ni nafasi adhimu sana kwake.



    “Unaweza ukageuza familia na ukoo wetu kuwa wa kifalme. Tukaheshimika zaidi, na tukafanikiwa zaidi.”



    Kisha akamfunda namna ya kuenenda.



    “Mtazame mfalme kwa uso wa haya. Usimnyime tabasamu wala mkono wako. Hakikisha anakuwa wa moto kila anapokuwa karibu na wewe. Usiwe na papara, tulia na uzingatie kama paka mwitu awapo mawindoni.”



    Likapita kama nusu saa hivi, mara farasi wawili toka kwenye kasri ya mfalme wakawasili nyumbani kwa Mlekizedek. Kwenye mgongo wa farasi mmoja alikuwa ameketi mwanajeshi, na mwingine alikuwa hana mtu mgongoni.



    Huyu ambaye hakuwa na kitu mgongoni, alikuwa ni mweupe. Kamba yake iliyomshika shingo ilikuwa imeshikiliwa na mwanajeshi aliyekuja nao.



    Mwanajeshi huyo akasema amekuja kumtwaa Tattiana. Tattiana akatoka ndani na kumwea farasi, wakatimka kwenda kasrini kwa mfalme.



    Ni muda mchache ukapita, na mara akatokea kijana fulani hapo nyumbani kwa wakina Tattiana. Kijana huyu alikuwa mwembamba mwenye nywele ndefu rangi ya kahawia na ndevu zilizojaa kwenye taya.



    Akamuulizia Fanty kwa walinzi, Fanty akaitwa na kuja kujumuika naye hapo nje ya uzio.



    “Nimemwona Tattiana akiongozana na mwanajeshi. Kuna nini?” akauliza mwanaume huyu ambaye kwa mujibu wa maongezi ya Fanty, alikuwa anaitwa Roboth. Macho yake yalikuwa madogo yanayong’aa.



    Fanty akamwambia kwamba Tattiana amepelekwa kasrini kukutana na mfalme na kama mambo yakiwa vema basi ataolewa na mkuu huyo wa nchi. Roboth akastaajabu sana. akaishiwa na nguvu akiuliza:



    “Kuolewa? Na vipi husumu mimi?”



    Fanty akamsikitikia. Japokuwa Roboth alikuwa ni rafiki yake, na anajua fika alikuwa ana mahusiano na Tattiana, ambaye ni dada yake, hakuwa na fursa ya kumzidi mfalme.



    Akamwambia amsahau Tattiana, kwani atajiumiza tu. hata familia yake haiwezi kumwelewa. Roboth akapinga hilo jambo kwa nguvu zake zote. Fanty asimjalli, akarudi zake ndani.



    Na kumbe mama yake alikuwa anaushuhudia mchezo wote huo. Akamfuata Fanty na kumuonya.



    “Sitaki yule kifaranga akanyage tena hapa kwangu, wala amsogelee Tatty. Sawa?”



    Fanty akaitikia, kisha akaenda zake.





    ---





    “Karibu,” Akasema Phares akimpatia mkono Tattiana. Tattiana akashuka wakaenda zao ndani.



    Walifikia sebuleni wakakaketi katika umbali wa kunyoosha mkono kumfikia mwenzako. Mfalme akamsifia Tattiana amapendeza. Tattiana akiwa ameinamisha uso wake akashukuru.



    Wakakaa kwa muda wa kama dakika mbili pasipo kuongea. Tattiana alikuwa anafinyaga vidole vyake wakati Phares akifurahia kutazama uso wa binti huyo mrembo akiwa anatabasamu mwenyewe.



    Mwishowe Phares akamtaka Tattiana amwandalie chakula cha usiku. Angependa kula mkono wake. Na zaidi akataka abaki naye kwa siku hiyo.



    “Sawa, mfalme wangu,” Tattiana akaitikia.





    ***





    Farasi alipolia, Bonas akamwambia Rhoda:



    “Ni muda mrefu sasa twatembea. Huoni kama itakuwa vema tukipumzika.”



    Walikuwa wametimiza kama masaa sita hivi wakitembea. Watu wote walionekana kuchoka isipokuwa Rhoda mwenyewe. Bado macho yake yalikuwa makavu na mwenye nguvu.



    Alikuwa anaangaza angaza huku na kule japo haoni jambo isipokuwa giza.



    Wakapumzika. Na wale wenye chakula wakatoa kula.



    “Unaweza ukaona lolote tukiwa hapa?” Rhoda akamuuliza Tretho.



    “Sijajua,” Tretho akamjibu. “Ni mpaka tufanye huo msako.”



    Basi Rhoda akasogea kidogo kando apate kumaliza haja yake ndogo. Alipomaliza, kabla hajajirejesha kule walipo wenzake, akaangaza kushoto na kulia kwake. Akaona taa moja kwa mbali upande wake wa kaskazini.



    Aliporejea akamwambia Tretho na Bonas.



    “Kwahiyo tutaelekea huko?” Bonas akauliza.



    “Ndio,” Rhoda akajibu. “Ila ni sisi wenyewe siyo na kikosi kizima.”



    Bonas na Tretho walipomaliza kula, basi wakatoka na Rhoda kwenda kule walipoona taa. Baada ya mwendo wa dakika ishirini na, wakawa wamekaribia kufika. Ilikuwa ni nyumba ya wale wabibi walozi watatu.



    Ila punde, wakaanza kuona maajabu!



    Kwanza walisikia sauti ya popo na mvumo wa upepo tokea kushoto mwao. Kutazama wakaona rundo kubwa la popo wakubwa. Popo hao walikuwa wanakuja upande waliopo.



    Wakawavamia katika mtindo wa kuwazunguka. Japokuwa Rhoda alishikilia kizingiti chake alichopewa na Venin kama kinga. Hakikumsaidia. Wakajikuta wananyanyuliwa na kimbunga kile cha popo na kusafirishwa wakielekea wasipopajua.



    Ndani ya hekalu kubwa, kubwa mno, popo wakaingiza watu hao ndani na kuwamwaga kwenye ukumbi. Ndani ya ukumbi huo wakawakuta wenzao, yaani kile kikosi cha watu waliokuja nao wakiwa tayari wameuawa!



    Kila waliyemwamsha, hakusikia wala kufurukuta. Walikuwa wamekauka ngozi yao ikiwa nyeupe pe!



    “Wamenyonywa damu,” akasema Tretho. “Hawajabakiziwa hata tone moja.”



    Wakiwa hapo wanabung’aa. Hawaoni pa kuingilia wala kutokea. Yule mtu aliyekuwa anamtazama Rhoda kwenye rada, akaangua kicheko kisha akatia kidole chake kwenye rada na kukoroga.



    Mara Rhoda na wenzake wakaanguka chini kwa kizunguzungu. Wakapoteza fahamu.





    ***





    “Malkia, hakuna aliyemwona,” askari alifikisha ripoti kwa ukakamavu.



    “Umeulizia vizuri lakini?”



    “Ndio, nimeuliza kila eneo na kila mtu. Hakuna aliyesema amemwona jenerali kamanda.”



    Malkia akanywea. Aliminya mdomo wake akitazama kushoto. Akafikiri kwa muda kidogo kabla hajauliza:



    “Na kaimu?”



    “Yu njiani yuaja,” akajibu mwanajeshi na kisha akaondoka. Malkia akarejea sebuleni kukutana na Zura aliyekuwa ameketi kwenye kiti akifuma kitambaa kikubwa kizito.



    “Hamna anayejua wapi alipo,” Malkia akamwambia Zura huku akinyanyua gauni lake zito lililofumwa na nyuzi za dhahabu apate kukaa kochini.



    “Sasa atakuwa ameenda wapi?”



    “Sijui. Tangu aliporejea toka kwa mama yake, nilionana na kuongea naye kwa muda mchache sana. Sijui amekumbwa na nini.”



    Punde si nyingi, akaja mwanaume mrefu mwenye mwili mpana, Benadi. Mwanaume huyu alikuwa makamu wa Fluffy. Malkia akamuuliza kama amemwona Fluffy ama ana taarifa zozote kuhusiana naye.



    “Hapana, sijui alipo,” akajibu Benadi akitikisa kichwa.



    “Umeongea naye karibuni?”



    “Hapana, sijaongea naye.”



    “Unadhani atakuwa wapi?”



    Benadi akatikisa kichwa chake. Basi Malkia akamruhusu aende zake.



    Benadi alipotoka nje, akatembea kwa umbali mfupi kabla hajasikia jina lake linaitwa na sauti tokea nyuma. Alikuwa ni Bozi akiwa amejiveka shuka moja kubwa jekundu.



    “Naweza nikapata wasaa wa kuongea na wewe?”



    “Kwa sasa, hapana. Malkia amenituma kumtafuta Jenerali.”



    “Oooh, huwezi jua labda naweza nikasaidia,” akasema Bozi kwa tabasamu.



    Basi wakasogea kando, mahali ambapo hamna watu, wakateta ambapo Bozi akamshirikisha Benadi juu ya mpango wao wa siri. Benadi akashtuka sana. Akahofia mwanzoni. Ila Bozi akamwambia kwamba wapo wengi nyuma yao.



    “Kuna wenzako ambao tayari wameshajiunga nasi. Tuna jeshi kubwa na watu wenye ushawishi.” Bozi akasema na kuwataja watu kadhaa. Kidogo, Benadi akapooza. Ila bado tu alikuwa na chembe za mashaka kwani jambo aliloambiwa halikuwa dogo hata kidogo.



    “Hakikisha inakuwa siri. Hili ni jambo ambalo linafanyika chini kwa chini.”



    Benadi akaomba apewe muda. Akaenda zake akisindikizwa na macho ya Bozi mpaka ndani, kisha Bozi akaenda zake. Akaenda kukutana na wanajeshi fulani ambao aliwapa kazi ya kumtazama Benadi.



    Ilitakiwa wajue sasa harakati zote za Benadi asije akamwaga mchele kwenye kuku wengi. Kama akikataa, basi amalizwe mapema.



    “Hakikisha mnajua wanaoingia na wanaotoka ndani ya nyumba yake. Kila mtu anayeongea naye na kuwasiliana naye. Sawa?”



    “Sawa,” wakaitikia wanajeshi na kwenda zao kutekeleza agizo.





    ***





    Usiku ukazidi kujongea na kuwa mzito. Kwa majira ya sasa, tungesema ni saa nne ya usiku. Na ilikuwa ndani ya Kasri ya mfalme wa Phares.



    Kila kitu kilikuwa mezani kikiwa kimepangiliwa vema. Mabakuli yaliyobebelea vyakula vya kila aina na vinywaji, ambavyo vingi vilikuwa ni mvinyo mwekundu. Basi Tattiana akamwita mfalme na kumwambia kwamba chakula tayari na hivyo ajongee.



    Lakini wakati huo si kwamba Mfalme alikuwa tumbo tupu, lah! Alikuwa tayari ameshapewa ka chakula ka kusogezea muda. Kale cha kumfanya asipige mihayo.



    Akanyanyuka na kujongea mezani. Siku hiyo hakukuwa na kijakazi yoyote yule wa kumhudumia mfalme isipokuwa Tattiana peke yake. Mwanamke huyo aliwaonba vijakazi wote wapumzike na ni yeye ndiye atahusika na kila kitu.



    Akampakulia chakula mfalme kisha kabla hajaketi akabakia kusimama apate majibu yake. Mfalme akang’ata na kutafuna. Na akanywa pia. Hakika akapenda chakula kile. Kilikuwa kitamu haswa.



    Akatabasamu akimtazama Tattiana.



    “Unaweza ukakaa?”



    Tattiana akaketi akiweka mikono yake mapajani. Mfalme akamsifia kwa chakula chake kitamu na amekifurahia sana.



    “Ni nani aliyekufundisha kupika hivi?”



    “Mama yangu.”



    “Ni ajabu kuona binti wa familia kama ya kwako akijua kupika hivi.”



    Tattiana akatabasamu pasipo kusema kitu. Alitazama tu chini. Basi mfalme akala chakula mpaka akashiba. Akafurahia sana maana hakuwahi kula chakula kitamu vile.



    Huenda na sura ya Tattiana ilichangia kwake kuona chakula kitamu. Uso wa binti huyo ulikuwa ni kielelezo tosha cha namna gani Mungu alivyo hodari wa kuumba.



    Mpaka anamaliza chakula, mfalme alikuwa anamtazama tu Tattiana. Huku naye binti huyo akitazama chini na kutabasamu mwanana.



    Binti akatoa vyombo ambavyo mfalme amekula navyo kisha akareja na kuketi na mfalme. Akamuuliza:



    “Kuna kingine ambacho ningeweza kukuhudumia mfalme wangu?”



    Mfalme asiwe na kauli, akatikisa kichwa chake. Kabla muda mfupi hawajaenda kupumzika wote. Huko mfalme akapata kujua mwili wa Tattiana. Alikuwa ni msichana ambaye hakumjua mwanaume hapo kabla.



    Baada ya kumaliza tendo, mfalme akapitiwa na usingizi mzito akimwacha Tattiana mkavu asiye hata na lepe.



    Alikuwa anatafakari siku nzima ilivyoenda. Namna ambavyo alivyokuwa anachakarika na hatimaye akafanikiwa kumfurahisha mfalme. Akajiuliza sana, vipi kama akija kuwa malkia itakuaje? Atafanya nini?



    Hakujua. Ni kitu ambacho hakuwahi kukitarajia maishani mwake. Kulala na mfalme, tena ndani ya chumba cha kasri! Haikuwa kawaida.



    Basi akanyanyuka na kwenda mpaka dirishani mwa chumba. Akafungua dirisha na kutazama nje. Kama haitoshi akatoka chumbani na kwenda kuzurura kasri nzima.

    Alifurahia sana mazingira ya mule.



    Ila akiwa anazurura zurura, akajikuta anamkumbuka Roboth, mpenzi wake wa enzi. Alienenda dirishani upande ule ambao makazi ya Roboth yalikuwepo, akatazama kana kwamba anamwona.



    Alijitahidi kumpuuzia maana alikuwa anaelekea maisha mapya. Maisha ambayo yangewafanya wazazi wake wajivunie. Maisha ambayo yangempatia heshima tele kwenye uso wa himaya ya Goshen.



    Kukosa huko usingizi kukamfanya awaze mawazo mengi sana, yenye tija na yasiyo na tija. Alirejea chumbani kwa mfalme akaendelea kutafakari, lakini haikupita muda mrefu sana, akataka sasa kulala.



    Akalaza mgongo wake kitandani na kumwekea mkono mfalme. Akagundua mwanaume huyo ni wa baridi kupitiliza. Akashangaa sana maana haikuwa kawaida. Ndani kulikuwa kuna joto, na hata blanketi walilokuwa wamejifunika lilikuwa zito.



    Sasa baridi limetokea wapi? Ama mfalme anaumwa?



    Tattiana akamtazama mfalme, mbona haonekani kama anayeumwa! Mbona hakumwona kama ana dalili zozote za kuumwa?



    Akaondoa mkono wake mwilini mwa mwanaume huyo maana kadiri alivyokuwa anauweka hapo ndivyo na yeye akawa anahisi baridi mwili mzima. Alijigeuzia kando alale.





    ***





    “Sasa tunafanyaje? Ndiyo hatutatoka humu?” sauti ya kike iliuliza ndani ya lupango.



    “Unajua kwa mara ya kwanza, hawakuwa wameweka ulinzi maradufu kiasi hiki. Sasa hata mlango wameufunga huko nje kwa komeo si chini ya tatu,” sauti ya kiume ikajibu.



    “Endapo tusipotoka humu, basi Malkia ataisha. Hakuna mtu mwingine wa kumwamini huko nje.”



    “Basi inabidi tufikirie namna ya kujichoropoa humu.”



    “Lakini kivipi? Mawazo yangu yamegoma kabisa. Au una wazo lolote?”



    “Hapana, ila ntalipata tu tena karibuni.”



    Mara wakasikia sauti za watu wakiingia chumbani. Basi wakakaa kimya kusikiliza. Lupango waliyomo iliwaruhusu wao kufanya hivyo maana ilikuwa inapakana na sehemu ambapo wakina Bozi walikuwa wanapenda kukutana kufanyia majadiliano.



    Wakasikia sauti ya mwanaume mmoja, na punde ikakaribishwa na ya Bozi kuketi chini.



    Kadiri sauti hiyo mpya masikioni mwao ilivyokuwa inaongea, basi Fluffy akaitambua. Ilikuwa ni ya Benadi. Akamnong’oneza Seth, sauti hiyo anaijua. Wakasikiliza na kugundua kuwa Benadi alikuwa naye amesilimu na kujiunga na wakina Bozi.



    “Lakini mtanipangia nyadhifa gani?” Sauti ya Benadi ikauliza.



    “Usijali,” Seth akajibu. “Wewe sasa hivi ni kaimu, ila kwenye serikali mpya, wewe ndiye utakuwa jenerali.”



    Sauti ya Benadi akicheka ikavuma. Kisha sauti ya meza ikikitwa. Bila shaka kicheko kilikuwa kipana.



    “Basi tupo pamoja. Hilo halina wasi kabisa,” Benadi akasema.



    “Sawa sawa. Basi kuna kazi moja ambayo tunataka uitekeleze. Kazi hiyo itakapokwisha, basi na filimbi ya kuhitimisha mchezo itakuwa imepuluziwa papo.”



    “Ipi hiyo?”



    “Kummaliza Malkia.”



    Sauti ya mguno ikaita. Kisha Benadi akasema:



    “Ila si rahisi.”



    “Kwako ni rahisi kuliko kwetu,” Bozi akasema. Kukawa kimya kwa muda. Kisha sauti ya mtu akishusha pumzi ndefu.



    “Vipi, kuna shida yoyote? Kama kuna tatizo ama mahali umekwama tunaweza kusaidiana.”



    “Vipi lakini haitasababisha namna yoyote ya kuwatia watu hofu, na pengine nikaonekana msaliti?”



    “Benadi, hakuna namna ya kukimbia maneno ya watu siku zote. Ila labda cha kukuarifu ni kwamba, tunataka mambo haya yafanyike kimya kimya. Hatutaki mtu yeyote afahamu mpaka pale tutakapokuwa tumekamilisha kila jambo. hivyo tungeshauri ukatumia sumu kummaliza. Na ni bora ikawa chakulani.”



    “Sumu?”



    “Ndio. Tayari ipo, ni swala la kutiwa tu kwenye chakula.”



    “Sawa, ntajitahidi.”



    Sauti ya makofi mawili ikasikika, na mara vishindo vya miguu vya mtu vikasikika. Punde kidogo.



    “Hii hapa. Utatia kidogo tu. itammaliza chini ya siku tatu.”



    “Sawa. Naweza nikaenda sasa.”



    “Ndio. Utatupa mrejesho.”



    Zikasikika vishindo vya miguu na kisha ikafuatiwa na sauti ya mlango kufungwa. Mara ikasikika tena sauti ya makofi na vishindo vya watu wasiopungua wawili.



    “Kaendeleeni kutekeleza kazi yenu,” sauti ya Bozi ikasema. “Hakikisheni mnajua kila nyendo zake. Kila anapotoka na kurudi asije akatuchoma.”



    Baada ya hiyo kauli, vikasikika vishindo vya miguu vikipotelea. Kisha kukawa kimya kabisa. Basi sauti ndani ya lupango zikadakia.



    “Seth, wanaenda kumuua Malkia.”



    Kimya kidogo. Mara sauti ikauliza:



    “Unaweza kuchimba?”



    Hakukuwa na majibu. Ila mara sauti ya mtu akifukua gizani ikaanza kusikika. Na ilikuwa inaongezeka kadiri na muda.



    “Tusaidiane, tufanye upesi. Hii ndiyo njia pekee ya kututoa nje.”





    ***





    Walipokuja kuzinduka, wakajikuta mbele ya kiti kikubwa cha rangi nyekundu. Hakuna aliyeelewa hapo wamefikaje, wakabak kutazamana: Rhoda, Tretho na Bonas.



    Vichwa vilikuwa vinawauma vikiwagonga haswa. Walitazama huku na huko hawakuona kitu isipokuwa giza. Ni pale tu walipokuwa wamejilaza, na mbele kidogo penye kiti ndipo palikuwa na mwanga. Huko kwengine kote macho hayakuweza kuona jambo.



    Na pale kwenye kiti kile chekundu palikuwa patupu. Hawakujua nani alikuwa amekaa pale. Na ameenda wapi. Wakatazamana. Na pengine wakaulizana maswali ambayo hakuna kati yao aliyekuwa na majibu.



    Ila haikupita muda mrefu, wakasikia sauti ikitokea pale kitini. Ikiwaambia:

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimewapa muda ili mnipe sababu za kuwaachia uhai wenu.”



    Hawakujua anayenena ni nani. Wakauliza ila hawakujibiwa. Walitawaliwa na hofu kubwa. Ukapita kama dakika tatu, na mara popo wakavamia eneo hilo. Wakatanda kiti na mara akatokea mtu hapo!



    Popo wale wote walipotelea ndani ya mwili wa huyo mtu. Yaani yeye ndiye aliyekuwa popo hao wote.



    MWISHO WA SEASON ONE





    ***TUKUTANE WEEK END HII KWENYE MUENDELEZO WA MSIMU WA PILI MBARIKIWE SANA KWA KUWA WOTE PAMOJA


0 comments:

Post a Comment

Blog