Search This Blog

JOTO LA MSHUMAA - 5

 





    Simulizi : Joto La Mshumaa 
    Sehemu Ya Tano (5)






    Safari ya kijana KATUNJE iliendelea kuelekea ndani ya kijiji cha Bwawani kwa lengo la kuonana na bwana SIKUJUA kama mualiko wake ulivyo. Akiwa na imani kubwa kabisa kuwa kaka yake atafanikiwa kumuona bila wasiwasi Safari hii alienda akiwa na matumaini hayo.

    Kutokana na mwendo ambao alikuwa akiutembea haikumchukua muda mrefu sana aliweza kukiona kile klijiji cha Bwawani hapo aliona sasa muda umefika wa kumtafuta kwanza kaka yake kisha pindi akishindwa ndipo pale atakapomtafuta mzee Sikujua kwa lengo la kuonyeshwa kaka yake huyo. Aliweza kupita kila eneo kutokana na ile hali ya kutoonekana mbele ya mamcho ya binaadamu.

    Alifika mpaka pale kwenye ile nyumba ya Mwenyekiti bwana Semeni, aliikumbuka sana ile nyumba kwani siku ya kwanza anafika pale kijijini aliondolewa kama mbwa tena kwa kufukuzwa na vijana waliotumwa na Mwenyekiti huyo. 'Ahaa...hapa ndipo mara ya kwanza niliweza kufukuzwa baada ya kuulizia kaka yangu ngoja nianze na hapa.'

    Wakati anawaza hayo alimuona bwana mzee mmoja akiwa na kijana wa makamo mwenye umri unaokimbilia sawa na yeye, alishangaa hivyo ilimbidi awafuate kisha aweze kupata taarifa kuhusiana na yale ambayo wanataka kuongea zaidi na jambo gani ambalo wanataka kulisema na likamsaidia.

    Yule mzee alikuwa ni bwana MANUALI akiwa na kijana wake SUSU walifika wanafika kwa bwana Semeni ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Bwawani, Ujio wa watu hao ulionkena kuwa ni washida sana kwani walikuwa na haraka sana jambo hilo lilimfanya Katunje ahisi jambo ambalo lingeweza kumsaidia kwa mambo aliyokuja kuyafuata. Kwa upande wa katunje haikujulikana kwa nini anafanya jambo lile la siri japo hali yake inajulikana.

    Muelekeo wa Manuali na Susu ulifikia tamati kwenye ile nyumba ya mwenyekiti bwana Semeni na ndipo wakabisha hodi mara kadhaa na ndipo mlango ukafunguliwa ndipo mwenyekiti aliwakaribisha ndani na akarudisha mlango. Katunje alijiuliza maswali kadhaa.

    'Ina maana humu ndani ndipo pale kwa mwenyekiti, na kama ndio humu kuna swala gani linaendelea..ngoja nikasikilize kama nitafanikiwa kupata jambo lolote'

    Mawazo yake yalimtuma kwenda kusikiliza kipi ambacho wanazungumzia wale waliomo ndani, alihitaji kufungua mlango kwa kuamini kuwa yeye haonekani kwa macho ya kawaida ya mwanadamu, lakini kwa upande wa pili aliona kuwa ataharibu na akashindwa kupata kile ambacho alitaka kukipata kwa urahisi, hivyo aliamua kusikiliza kwa kupitia upenyo ambao ulionyesha yaliyomo ndani na waliomo ndani japo kwa nadra kuona kila kitu.

    waliomo ndani walikuwa watatu yani Mwenyekiti Semeni, Manuali na Susu. Hawa wote walionekana kuwa na mawazo ya pamoja kutokana na hali ya mihemko yao ya kutaka kujua la mwenzake. Mwenyekiti alianzisha mazungumzo ambayo yalimfanya kila mmoja kuwa tayari.

    "Manuali unajua kuwa muliahidi kuwa kijana wako atakuwa tayari kumsema yule ambae anasababisha mauaji na matatizo kama yale yaliyompata yeye siku kadhaa zilizopita...sasa mpaka sasa kimya" Aliongea mwenyekiti kwa sauti ya chini ambayo pia ilimpa shida katu je kusikia maneno yote ambayo yanazungumzwa.

    "Nafahamu lakini nilikuwa kwenye matiubabu yake, na hapa unaponiona yuko tayari kusema kila kitu kwani alihitaji aje kukuambia wewe kwanza kabla hata wanachi hawajapata taarifa hiyo..."

    "...lakini kwa taarifa ambayo niliyo nayo kuwa tayari mtu anayesababisha kaonekana na baadhi ya watu waliondoka hapa na kwenda kufuatilia huyo mtu kwa mahojiano zaidi na mmoja karudi nasubiri ripoti yake tu hapa..."

    Susu alionekana kuchanganyikiwa baada ya kuambiwa yale maneno, na kwa upande wa kijana Katunje hakuelewa chochote pale alihisi kama hayamuhusu kabisa ndipo akatoka pale akijinyoosha huku akijishikashika na kujitathmini kivipi yeye haonekani upande ungine alifurahi na ungine alikuwa na huzuni kwa kutojulikana wapi yeye alipo. Ghafla anakuja bwana Sikujua kwa mwenyekiti huyo jambo ambalo Katunje alimuangalia kwa makini na kumfananisha na mtu fulani hivi'

    "Huyu jamaa mbona kama nilishamuona kule nyumbani au ndio mzee Sikujua...ngoja nifuatilia nadhani kuna jambo nyeti limejificha"

    Alirudi pale sehemu ambayo alikuwa anachungulia, Mzee Sikujua alibisha hodi na kufanya mazungumzo ya ndani kughairishwa na kusikiliza huyo anayekuja ndani ni nani. Hatimae anakutana uso kwa uso na kijana Susu, moyo wake ulipwita mithli ya mpira udundao mara kadhaa baada ya kupigwa na mchezaji mahili. Moyo wake uliendelea kutokuwa na amani kwani alihgisi kila siri imevuja kwa mwenyekiti na kazi ambayo alikuwa anaifanya basi kuwa tupu na ukweli umevuja alijiona kuwa mtu mpumbavu ambaye anasafiria nyota ya bwana Chito kwa kumsingizia mauaji na matatizo ambayo yeye ndio msababishaji>

    "Bwana Sikujua samahani naomba tutoke hapo nje ili tuongee nije kumalizana na hawa wengine" Maneno ya mwenyekiti yalimpa faraja kubwa sana Sikujua kwa kuhisi kuwa kuna usalama kidogo, walisogea pembeni na hapo ndipo Kijana katunje na yeye aliwasogelea karibu kabisa ili apate kusikia kila kitu kinachoendelea.

    "Ehee habari ya safari huko ulikokwenda?"

    "Safari ilikuwa salama yenye matumaini na kile nilichokiendea...." Sikujua alikuwa anaongea huku akitetemeka kwa hofu kubwa aliyo nayo. "sasa....ulifanikisha ?"

    "..Ndio na nilifika mpaka kilimalondo na nikamkuta mke wa Katunje ndipo nikampa taarifa kuwa hapa afike mapema sana na nadhani siku ya leo yuko njiani". Aliongea hayo huku bila kufahamu kuwa kijana katunje mwenyewe anayasikia kila neno na nukta hakuiacha.

    "sasa...huyo mwenzako Mapato huko aliko atafanikiwa kumleta Chito maana ?" Mwenyekiti aliendelea kuhoji maswali ambayo yalikuwa yanamsaidia kijana Katunje kufahamu swala zima linaendeleaje pale.

    "Kuhusu Mapato kwenda Shishimo na kumfuata Chito halina ugumu japo nilikuja kwako kwa hofu maana siku ya leo imekuwa kubwa hajarudi kabisa sasa sijajua kipi ambacho kimempata huko...lakini mwenyekiti huyu Susu na mzee wake wamekuja kufanya nini huku kwako?"

    "Ooooh! hawa wamekuja kuulizia lile swala japo kwa maelezo yao wanasema tujitahidi na tukishindwa basi wao watachukua maamuzi mkononi kwani wanamfahamu". Sikujua aliona mambo magumu sana ndipo alimuomba kuwa awaruhusu kwa kuwaambia kuwa wanalishugulikia jambo lao. Katun je mpaka hapo aliweza kujua jambo muhimu na kumfahamu kuwa Sikujua na mwenyekiti si watu wazuri sana pale kijijini.

    Aliweza kujua pia kuwa kaka yake anapatikana kijijini kwao na inambidi afunge safari ya kwenda ndani ya kijiji hiko. Kabla hata hawajaachana yani wanaagana, Kijana mmoja maarufu kwa uuzaji wa mbuzi akiendelea kunadi karibu kwenye nyumba ya mwenyekiti.

    Sauti hiyo ilimfanya susu kutoka mule ndani na kuja nje ambako aliwakuta Semeni na Sikujua wkiendelea kuelezana baadhi ya mambo yao. Kijana huyo alifika pale na kupaki baiskeli yake pembeni na kuwasalimia, wakati huo Susu aliliona lile tenga ambalo lilimkumbusha mbali sana.

    "Baba...unaona hili tenga langu limekuja tena leo, " aliongea kwa sauti na kumfanya bwana Katunje kusogea pale na kuliona lile tenga ambalo na yeye analikumbuka vyema, haikutosha pia na ile nguo ambayo mara ya kwanza alimchukua Sikitu ambae yeye anamfahamu kwa jina la Lyoto kuiona ikiwa kwenye miguu ya mbuzi huyo"

    Kijana yule alistaajabu baada ya kumsikia susu akisema kuwa tenga lake "Susu unasema tenga lako hili kivipi?" Aliuliza kijana huyo ambaye ni kawaida kwake kuja pale baada ya muda kupita.

    "Hili tenga lina historia kubwa sana, hili tenga ndio chanzo ya mambo hapa kijijini bwana.." alikuwa anaongea kama mtu ambae kapandwa na mizuka.

    Waliweza kumshika huku hasa bwana Manuali na kuondoka nae, kijana Katunje alikuwa anamfahamu yule kijana kwani wote wanatoka kijiji kimoja ila ilikuwa ngumu kwake kuuliza chochote kutokana na hali yake ya kutoonekana. Tenga lile Katunje analikumbuka vyema sana alipiga mahesabu iweje lile tenga lizue yale mambo " Kijana yule anasema tenga lake lakini tenga hili mimi nililichukua hukuhuku nikambebea Lyoto hadi kilimalondo, nakumbukla Mfalme SWAI na kijana wake Kimolo walilichukua kwa nguvu lile tenga....leo lipo hapa basi mhusika atakuwa yule kijana anayedai tenga lake kwa nguvu zote"'

    Aliona kuwa Susu ndie muhusika mkubwa na yale yote lakini na huyu mzee Sikujua ana mambo gani ya siri na mwenyekiti kuhusiana na kaka yake Chito. Aliyawza mengi sana na upande mwingine aliona ile hali ya kutoonekana inamsaidia sana kwa baadhi ya vitu.

    Aliamua kuondoka na kuwafuata Susu na mzee Manuali. akiwa nao njiani Susu alikuwa anaropoka maneno ambayo yalionekana kuwa ni ya kweli ndani mwake. Njiani alikutana na kijana Ndunya ambae ni rafiki wa Susu ambae alimsaidia mzee Manuali kumkamata Susu vyema. Kuja kwa Katunje karibu kulimfanya Ndunya ashtuke na atoke pale jambo ambalo lilimshtua Katunje kwa kuhisi kuwa anaonekana na huyu jama.

    "Wee nani na mbona unawafuatilia hawa..."

    Laa haulaaa..kumbe kijana Ndunya anamuona vyema kabisa. Katunje aliishiwa pozi jambo ambalo lilimfanya atoweke maeneo yale kwa kukimbia. Wao walienda hadi kwa mzee Manuali na kumuweka susu ili kumpa matibabu kwa kuwa walihisi akili yake haiko sawa kwa nyakati zile.

    Baada ya muda kupita Ndunya na Manuali walikaa pamoja ndipo wakaanza kuongea baadhi ya vitu ambavyo walikuwa wanavishangaa pale kijijini.

    "Baba hivi haya maneno ambayo alikuwa anayaongea Susu unayachukuliaje..?" Aliuliza ndunya kumuuliza mzee Manuali. "Hata mimi ndugu yangu kwani kuna baadhi ya kauli na mambo yanaendana yani siamini kusema kuwa bwana Chito anayafanya haya hapana labisa". Wakati huo katunje tayari kafika nyuma ya nyumba hiyo huku akisikiliza kwa makini sana yale yote yanayoongelewa.

    "Baba labda nikuambie kitu kimoja, hawa wazee wawili nina wasiwasi kuwa wanahusika kabisa kutokana na matukio yanayoendelea" "Akina nani hao"

    "Hawaa...sikujua na mapato na si chito kama wanavyoongea mana mzee chito alivyopotelewa na mtoto wake Sikitu hakuwa na amani kabisa na alihitaji aondoke hapa kijijini...lakini kwa uwezo wa mzee Manyenye alimuambia atulie hapa kwa kuwa ni mzee Mzuri sana ila sikujua alimfanyia hujuma akishirikiana na mjukuu wako Susu, ila sijajua kuhusiana na hili tenga mana kila sehemu ukimkuta susu kipindi hiko anamuongelea sikujua atagusia tenga"

    Katunje aliushika usemi ambao ulisema kuwa "..Maana mzee chito alivyopotelewa na mtoto wake sikitu hakuwa na amani kabisa.." alipata kujiuliza swali " Ina maana kaka yangu alikuwa na mtoto ndani ya hiki kijiji, alafu kapotea kwa mazingira gani jamani mh...ila huyu kijana inabidi niwe karibu nae anipe mambo mengi sana" Katunje aliamua kujitokeza mbele yao na lolote liwe lengo aungane nao ili apate nafasi ya kuyajua mengi zaidi.

    Lakini hata kijana Ndunya hakuweza kumuona tena kama pale mara ya kwanza jambo ambalo lilimpa nafasi kubwa kijana katunje kujua mengi zaidi.

    Aliona vyema siku hiyo kupanga safari ya kwenda Kwao alikotokea yani Shishimo ili akamfuate kaka yake kama taarifa inavyosema.

    Ndani ya kijiji cha Kalulu anaonekana mwenyekiti wa kijiji hiko akiwa katikati ya wanakijiji wake baadhi hasa akiwemo mzee Uwesu ambae alikuwa anaonekana mwenye huzuni kubwa sana. hakika huzuni ilitawala kwani ilionyesha kuwa kuna taarifa ambayo ilifika pale ni ya kusikitisha kwa wote.

    "Mimi kama mwenyekiti, ambae nimeipata shutuma hii hakika sijafanya mauaji haya ambayo yamesemwa kuwa mimi muhusika...bwana Masanja hakunisindikiza japo alikuwa na nia ya kunisindikiza tuliachana ndani ya kijiji chake na mimi nikaelekea njia ya huku nyumbani kwangu..lakinijambo ambalo linaloonekana kuwa familia ya bwana chito wanataka kulificha jambo hili na Uwesu usimpate au usipate ukweli wowote kuhusiana na mwanao "

    Haikuwa siku nzuri kwao kwani mambo hayakuwa vyema, Ilimbidi bwana Uwesu na mwenyekiti pamoja na wazee kadhaa na vijana wa pale kijijini waanze safari ya kwenda kijiji cha Shishimo kwa ajili ya kujibia kesi ya mauaji ya mwenyekiti wa Shishimo.

    Muda huohuo Chito anarudi kutoka kwa Mzee UPENGO ndani ya kijiji cha MIPINGONI, huku akiwa na kazi ya kwenda kwa baba yake kuchukua Bangili ya mkewe ili apate kurudi tena kwa mzee huyo, Chito alidhamilia hata kumpoteza baba yake kwa jinsi hasira alizo nazo aliona kuwa ni mzazi ambae hana faida kwake kabisa kwa yale ambayo huwa anayafanya ndani ya familia yao.

    Aliweza kuingia ndani ya kijiji chao mapema jioni.

    Bwana Mambo sasa akiwa na Nyandu ambae ni rafiki wake wa karibu sana, walionekana kushtuliwa sana baada ya kuja taarifa kutoka kwa wakuu wao wanaojulikana kwa jina la Nyamnyena. "Mambo sasa hapa kuna taarifa imekuja ya kusikitisha na inatuhitaji kujipanga sana mana vita sasa imeanza". Mambo sasa alishangaa sana vita kuanza kwa yapi tena "Bwana unanichanganya vita hii kuwaje sasa ebu nieleze nipate kuelewa vyema"

    "Sawa yani...Nyamnyena wamesema kuwa lile mzimu wa Lyoto ambalo limepelekwa kumchukua Mjukuu wako SIKITU linahitaji nguvu ya ziada yani damu...mana anaonekana yule binti kupata nguvu za ziada ambazo zinashindana na nyamnyena...."

    Mambo sasa alishangaa sana

    "Sasa kwa nini usimuambie nyamnyena akasema wapi huyo binti alipo na akatuambia na sisi tukaenda kumaliza kazi hiyo?" "Sasa kama nyamnyena kashindwa kuingia ndani ya kijiji hiko utaweza wewe kweli hapa cha kufanya kwanza huyu uliyemshika ukamtupe kule kwao bwawani sasa hivi na umpotezee kumbukumbu ya kurudi huku ukirudi tuje kujua tunalifanyaje hili jambo".

    Kweli alijiandaa vyema mzee baba wa chito akaondoka nae mapato hadi kijiji cha Bwawani ambapo zamani walikuwa wanalifahamu kwa Songambele, alimuacha huko na kuchukua baadhi ya vitu ambavyo aliona kuwa vitamfaa kupitia bwawa lile na kuondoka navyo akimuacha Mapato akiwa usingizini.

    Anarudi nyumbani akiwa hoi baada ya kubadili mavazi yake ya usiku. Upande wa chito hakuwa mgumu sana alienda moja kwa moja hadi kwenye chumba cha baba yake akafungua vitu mpaka pale alipoikuta bangili ya mkewe na kuishika kwa umakini na kutoweka zake.

    Safari hii aliona vyema kwenda bwawani japo wanamchukulia kuwa muuaji lakini aliondoka akiwa na lengo la kumfuata bwana Manyenye ambae ana ushahidi tosha sana kuhusiana na zile bangili ajue zaidi kabla hata ajaenda kwa bwana Upengo kule Mipingoni.

    Mambo sasa anarejea nyumbani kwake lakini anakuta mambo hayako sawa baada ya kukuta mlango wa nyumba hukufungwa na ndani hakuna mtu. aakajua fika kuwa chito karudi alipiga mguu hadi ndani kabisa kwake lakini hakuisi chochote kabisa ndipo na yeye akaenda kwa rafiki yake Nyandu kumalizia kazi zao.

    Asubuhi na mapema sana Chito akiwa njiani kuelekea kijiji cha Bwawani na kwa kuwa alikuwa kajifunika miguo ambayo haikuwa rahisi kujulikana kwa lengo la kuwa salama zaidi, ilimfanya kupishana na ndugu yake bila kujuana Katunje ambae na yeye alikuwa anaelekea kijijini kwao kumtafuta kaka yake.

    Chito alifika moja kwa moja hadi kwa mzee Manyenye ambapo mzee huyo aliishiwa nguvu baada ya kumuona mzee mwenzake, kwa kuwa alikuwa na haraka sana kwa kuhitaji ukweli wa zile bangili na kama yeye mtengenezaji atataja ukweli wote.

    walisalimiana na wakapata muda wa kuanza maongezi yao. "Mzee manyenye najua muda mrefu sana mpaka sasa ila nina mambo yananitatiza nahitaji taarifa yake zaidi". "Usijali bwana Mambo sasa" alimuita lile jina ambalo alilitumia mara ya kwanza.

    "Mimi siitwi mambo sasa kama unavyofikilia ninaitwa CHITO...je unaweza kuniambia mzee MAMBO SASA wa shishimo unamfahamu vipi?" Manyenye aliona kama utani kwa yale maelezo ambayo wanapeana pale kwa kujua utani kumbe bwana Chito yuko makini sana kwa lile jambo alitakalo kujua ukizingatia mkewe na mtoto wake pamoja na ndugu yake hawaonekani na chanzo kinajulikana na huyu mzee manyenye naingia kundini.

    "Mbona unaniambia maneno ambayo siyaelewi ndugu yangu kuna shida kwani?"

    "Unaikumbuka hii Bangili niliyokuja kuchukua kwako?" Alimtolea bangili ambayo alimpatia bwana Manyenye. Mzee huyo aliikumbuka lakini maelezo yake yalionyesha kupinga ukweli jambo ambalo hakulifahamu kuwa anahatarisha maisha yake kwani Chito alichomoa kisu na kumuonyeshea mzee huyo

    "Mtoto wangu kapotea ndani ya hiki kijiji, haitoshi mke wangu kapotea kwa mazingira nisiyoyafahamu..haitoshi ndugu yangu kapotea mpaka sasa sijui wapi alipo, nipo radhi kukuua mzee endapo hukusema ukweli tupo wawili tu hapa sema ukweli wako wewe na mzee mambo sasa wa shishimo mna uhusiano gani kuhusiana na hizi bangili?"

    Manyenye hapo ndipo alipoamini kuhusiana na ukweli na umakini wa Chito kwa yale asemayo

    "Ngoja kwanza..ukweli ni kuwa baba yako najuana nae miaka mingi iliyopita kipindi ambacho nilikuwa mmoja wa kundi la wachawi la nyamnyena...niliondoka kwenye lile kundi nikiwa bado kijana ila walinitishia sana wakanipa kazi ya kutengeneza bangili za mauaji, pindi mtu avaapo iwe rahisi kwao kumuita na kumuua....nilitengeneza ya mama yako na nikatengeneza ya mkeo lakini niliacha hiyo kazi kabisa na hapa maisha yangi yako hatarini ndio maana ukaona kuwa nilikuwa mgumu kukupa mapema sana "

    "Ehee ikawaje sasa mpaka sasa hivi...."

    "Mpaka sasa nimejiondoa japo wananifuata...kwani baba yako jana kaja huku bwawani kumleta bwana Mapato ambae alikuwa anakufuatilia wewe huko kwenu alipitia hapa na kunipa kazi ya kutengeneza kingine japo sijajua kwa ajili ya nani kwa sasa ila siwezi ni bora hata kufa kuliko kusababisha mauaji"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maelezo hayo yalimsababisha kuelewa kila kitu kuwa baba yake kuwa muuaji mkubwa sana. alimpa mkwara kuwa asije kusema kwa yeyote ujipo wake yeye.

    "Lakini nimemuona ndugu yako alikuwa anakutafuta pia na wewe" Chito alirudi tena kwa mzee Manyenye "Ndugu yanguuuu......katunjeeeee"

    "Ndio japo hayuko kwenye hali ya kawaida sana nilimuelekeza kuwa afike kwenu ili iwe rahisi muungane kupambana na baba yenu aliyeamua kuwasaliti kwa kuhitaji ufalme wa kichawi kwa nguvu kwa kupoteza ndugu wa karibu zake">

    Chito aliondoka muda huohuo kurudi kwao shishimo.

    Katunje anafika kijijini kwao na kuona mazingira yamebadilika na hakuna hata wa kumuuliza kutokana na hali yake na ambayo ana amini kuwa inamsaidia sana, aliendelea kutembea huku na kule hadi nyumbani kwake lakini hakukuta mtu na hakupenda kumuona baba yake kutokana na ujinga wa mzee huyo.

    Chito alifanya juu chini kuondoka na baiskeli hadi kijijini hapo ambapo pia ilikuwa ngumu kumuona ndugu yake kulingana na hali aliyokuwa nayo ya kutoonekana na watu.

    Alichoamua akifika mahali anaita jina lake yeye mwenyewe ili kama yupo karibu ahisi ukaribu wake na kumuoan kuliko kuita jina la Katunje asije kumsababishia matatizo. "Chitooooooo....chitooooooooo"

    Sauti hiyo ilisafiri kwa kasi hadi kwenye ngoma ya masikio ya katunje na kuanza kuhaha huku na kule kumtafuta kaka yake kipenzi.

    Hatimae katunje anamuona kaka yake akiwa anapiga yowee la jina lake huku chozi likimtoka kwa wingi kutokana na uchungu alionao, mana mpaka muda huo alishajua kuwa mkewe kafariki na mtoto wake.

    katunje alienda kumziba mdomo kaka yake na kumuambia "Kakaaa mimi hapa katunje huwezi kuniona kwa hali niliyo nayo ila nakuhitaji kwanza uamini mimi ndugu yako niliyekutafuta kwa miaka yote hii nikipata matatizo ya dunia yanayosababishwa na baba yetu mzee Mambo sasa"

    Baada ya muda aliamini kuwa ndie yeye ambae alikuwa anamtafuta na walikaa mahali huku wakiongea "Hatuna muda wa kupoteza sasa imefika muda wa kwenda Mipingoni kwa mzee Upengo atakusaidia pia na tutalimaliza hili jambo kabisa......."

    Safari ya kwenda Mipingoni ilipangwa kuwa kesho yake kwani kwa siku hiyo pia ndio sikua mabyo kikao cha mwenyekiti wa Kalulu anakutana na wazee wa shishimo ambao wana hasira ya kupotelewa na Mwenyekiti wao wakihisi kuwa mwenyekiti wa Kalulu ndio msababishaji................



    Chito alikuwa haamini kabisa kama kweli yuko karibu na ndugu yake kipenzi ambae alikuwa anamtafuta kwa takribani miaka kadhaa iliyopita, Hali hiyo ilimfanya kumuangalia kwa ule upande ambao yupo ndugu yake Katunje japo hakuweza kumuona kabisa. Sauti ya kwikwi ambazo zilikuwa zikimtoka Katunje ziliendelea kutoka bila hata kuonekana kwa wakati huo Katunje alijihisi dhaifu sana kwa ile hali ambayo alitamani kumuona kaka yake na yeye akionekana.

    Lakini ilishindikana walibaki kuongea kwa sauti lakini kwa upande wa Katunje aliweza kumuona kabisa lakini ilikuwa tofauti kwa Chito ambae alikuwa anasikia sauti tu. "Ndugu yangu kipi ambacho kimekutokea mpaka uwe hivi sasa hivi?" "kaka ni historia ndefu sana mpaka sasa hivi bado furaha yangu haijaja mpaka pale utakaponiona japo mimi nakuona ". Chito alifikilia kwa makini sana kisha akamuambia jambo Katunje.

    "Katunje hakikisha huku tuendako usiongee kamwe kuna kikao ambacho nahitaji ukasikilize yale ambayo wanaongea alafu baadae tukutane hapa ili kuelekea kijiji cha Mipingoni kwa mzee Upengo sawa".

    "lakini kaka nitawezaje kujua mambo ambayo sijawahi hata kuyajua hata chanzo". Alihoji ili apate kufahamu zaidi. "Hapana ndugu yangu wewe nenda ili ukapate kujua yale ambayo yataongelewa kiufupi kuna kesi ya mauaji ya kiongozi wetu wa hapa kauliwa na kiongozi wa kijiji cha Kalulu kule aliko shemeji yako mengi utayafahamu muda ukifika".

    Basi kijana Katunje aliondoka pale alipoelekezwa na bwana Chito alielekea upande mwingine, pia hakutaka kabisa kukutana na baba yake kwani anafahamu yapi ambayo yanaendelea. Chito hakuwa mwenye kuamini kwa lile tukio lote ambalo limeendelea pale. Alishukuru sana kwa kila hali aliona kuwa muda sasa umefika wa kufanikisha yale ambayo kayapanga.

    Majira hayo ambayo yalikuwa yanaendelea na kikao cha viongozi wa pande mbili yani vijiji viwili walikutana kuzungumzia yale mambo ambayo yanamhusu kiongozi wa Kalulu. Katunje nae alifanikiwa kufika maeneo hayo akiwa na lengo la kupata habari zote ambazo zitakuwa zinahusu kikao kizima. Baada ya muda wa kikao chao kuisha ndipo katunje alirudi kumtafuta kaka yake.

    Alimkuta akiwa kajiinamia mahali fulani akiwa kashika tama. Alienda kumshika begani jambo ambalo lilisababisha Chito kushtuka kwa kuwa hakumuona aliyemshika ndipo alihaha lakini katunje alijieleza kumuambia kuwa yeye ni ndugu yake, "Haya vipi tayari umefanikiwa kujua hata kitu kimoja".

    "Ndio kaka kikubwa walikuwa wanapanga kumjua yule ambae alifanya yale mauaji kwa upande wa baadhi ya watu pale walisema kuna Mzee yule rafiki wa baba yani Nyandu anahusika sana kwa mauaji ya hapa na akishirikiana na baba kaka inaniuma kwa nini baba anakuwa katili hivi".

    "Basi ndugu yangu usilie mimi nimeshalia sana na nikapoa kwani kuna vingine nilivishuhudia mwenyewe lakini nimelia na nimenyamaza cha kufanya hapa tuongozane haraka sana yani tusipitie hata kwa mzee tuondoke moja kwa moja Mipingoni".

    Safari ilianza kabla hata hawajamaliza kijiji mke wa mwenyekiti ambae alishafariki dunia alimuona Chito akiwa anaongea peke yake. Alimuita "Chitooo....chito"

    "Oooh naaam...ndugu habari yako"

    "Safi mbona unaongea peke yako njiani kote huku tangu upo kule nakuona unaongea kama....au umechanganyikiwa shemeji yangu..."

    "Ni kweli....mambo yamekuwa magumu sasa.. vipi lakini lile swala limeendaje baada ya wao kuja ?" "Kwanza nilishangaa kwa nini hukuja pale..." Aliongea mke wa marehemu masanja.

    "Mhh! kweli ila ujue kuna kesi kubwa mii mwenyewe ninayo sasa ningekuja ingekuwa vurugu kubwa sana"

    "Kesi ipi tena hiyo..."

    "Si unajua kupotea kwa mke wangu mama sikitu mpaka leo sasa wazazi wake wanamhitaji na sijaenda kutoa taarifa mpaka pale nitakapopata uhakika "

    "Pole sana... lakini shemeji sikufichi muambie baba yako kuwa tabia hii aliyo nayo sisi tumemchoka kabisa kumbe mume wangu aliyemuua ni baba yako na rafiki yake Nyandu..imeniuma sana sijui kosa ni nini jamani wamenifanya kuwa mjane sasa hivi mimi hata umri wako bado unadai aaaah!".

    "Basi nyamaza fahamu hata mimi sifurahiki na jambo hili ambalo baba yangu analifanya nakuomba uvumilie haya yote yatakwisha kwa sasa nipo na mgeni naenda nae mahali fulani...."

    Aliongea Chito huku akimshika bega kumtoa wasiwasi. "Una mgeni gani tena?"

    "Niko na ndugu yangu ambae nilishakuambia kuwa kapotea kwa muda na leo nimeonana nae yulee KATUNJE..."

    "Yani chito unaniambia yuko kwa baba yako sasa hivi?"

    "Haaa haaa haa..hapana nipo nae ndio ambae nilikuwa napita kuongea nae sasa nikirudi nitakuja kukupa habari zaidi.. ila usije kutoa taarifa hii kwa mtu yeyote".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari yao iliendelea kama kawaida na hatimae walifika ndani ya kijiji cha Mipingoni na kuitafuta nyumba ya mzee Upengo kama kawaida yake. "Sasa katunje hapa tutaanza kumueleza kwanza shida yako ili kama ataweza kukusaidia basi akusaidie ndipo tufanye yale yaliyonileta huku" " sawa kaka".

    Kabla hata hawajafika hapo walikutana na mtu ambae bwana Chito alishakutana nae mara ya kwanza na akampa usafiri hadi ndani ya kijiji hiki, walisalimiana na akamueleza kuwa " Chito nimekukumbuka si ndio yule mara ya kwanza ukaniuliza kijiji hiki na nikakupa msaada!"

    "Haswaaaa ndio mimi kabisa ndugu haya hii safari ya wapi tena?" Chito aliuliza.

    "Hiii bwana namalizia shughuli za leo na nadhani kesho ukinielekeza wapi tukutane tutasalimiana mana mimi na wee tumekuwa kama ndugu sasa, baada ya hapo nitarudi nyumbani kwetu CHAMLO kupeleka taarifa japo nina habari nyeti sana za huko yani".

    "Aaaah nitafurahi sana sasa ngoja tufike na kesho tukutane hapahapa majira kama ya asubuhi ili tuongee zaidi unipe mambo mazuri ya kijijini kwenu labda naweza kushawishika kuhamia huko".

    Waliagana na wao wakelekea kwa bwana Upengo.

    Mzee upengo walimkuta na akawakaribisha vile ipasavyo na wote wakakaa lakini mZee huyo alimsalimia kila mmoja jambo ambalo hata chito ashangae alimjuaje kama kaja na mtu pale. "Usishangae uliyekuja nae mimi namfahamu na nadhani nilishakupaga habari zake kabla haya lete hizo bangili zote".

    Chito alizitoa na akampatia.

    Mzee upengo kwa ustadi wake mahili sana alichofanya ni kuiangalia na kuitambua ile ya Mke wa Chito alikaa kwa muda sana kisha akaaanza kusikitika kabisa. Sikitiko hilo lilimfanya chito awe na mshangao sana iweje afanye vile hakutaka kukawia ilibidi amuulize swali kwanza.

    "Baba mbona unasikitika baada ya kuiangalia hiyo bangili au sio yenyewe?"

    "Hapana ni yenyewe hii ya mama yenu tayari nyota yake imefifia ina maana kafariki na hii ya mkeo nyota zake zilizowekwa tayari nayo imefifia yani kafariki dunia..."

    Chito alipatwa na butwaa kubwa sana hakutaka kuamini kwa jambo ambalo anaambiwa kumbe muda wote ana hangaika kumbe mtu kafa tayari. walichukua muda mwingi sana mpaka anyamaze na bwana Upengo kuendelea. Maneno ambayo alikuwa anayatoa mzee huyo yalikuwa magumu na makavu yani maneno ambayo hafichi chochote kwa kupoza ukali wa maneno.

    "Si wafichi baba yako alimpeleka mkeo kwa mchawi wao mkuu na kule wakamchinja shingo, akapewa kisu baba yako akaambiwa atoe sehemu za siri zake zote pamoja na viungo vingine, sehemu za siri wamezificha mpaka pale zitakapokauka wamezianika na lengo lao baadae wasage zile nyama kisha achanjiwe baba yako na atawazwe kuwa mkuu wa wachawi hapa kijijini na vijiji vyote ambavyo vinazunguka....si hilo tu alipewa nyama kisha akaambiwa aje kukulisha wewe...kwa bahati nzuri madhara uliyoyapata ni madogo sana ambayo yatatoka kwa kuwa hukula nyama hata moja huo ndio usalama wako....."

    '"Ina maana baba yetu kamuua mke wa kaka yangu jamani aaah hivi huyu mzee huu ukatili kajifunza wapi jamani na sisi si ndio atatuua kabisa".

    Waliendelea kulia kwa pamoja pale, lakini kwa kuwa yameshatokea walikubaliana na hali halisi ambayo ipo pale. Walikabidhiwa baadhi ya dawa a,bazo zitawasaidia. lakini chito aliendelea kuulizia kuhusiana na katunje kupona itakuwaje "Katunje siwezi kumtibia mimi kwa kuwa yupo ambae kayafanya haya na yeye mwenyewe anamfahamu inambidi aende kijiji hiko na mtu huyo ataenda kumsaidia".

    Walizidi kumuomba sana mpaka pale alipowakubalia na ndipo akampa dawa na akaweka ndani ya maji kisha akaambiwa aende kuyaoga maji yale, baada ya kuyaoga hakika ilimsaidia na chito akamshuhudia jinsi ndugu yake alivyo jibaba.

    Hapo sasa furaha ilikuwa kubwa na kesho yake walijiandaa kama kawaida asubuhi walikutana na yule mtu ambae waliahidiana kukutana pale.

    "Sasa umesema unatokea kijiji cha Chamlo...." " kijiji cha Chamlo...?" Katunje alishangaa sana.

    Ndipo Chito na yule jamaa wakashangaa "Katunje una maana kuwa unakijua hiko kijiji ndugu yangu?' Aliuliza Chito

    "Kama nakifahamu hivi kuna kipindi fulani nilishawahi kwenda hapo yani nilipita sikukaa sana kwa mzee mmoja anaitwa MWALAMI niliendaga kutafuta dawa fulani lakini huko nilikutana na kijana mmoja anaitwa BAMUZI...."

    Alionekana kufurahi yule Mzee waliekutana nae pale

    "Hakika anapafahamu kwani hao wote ambao anawasema ndio wahusika wakuu wa pale kijijini "

    Chito aliona sasa ndio muda wa kubadilisha maisha na kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine. " Lkini uliniambia kuwa kuna habaari mpyanzuri ya kuvutia kule kwenu ipi hiyo?" Aliuliza chito

    "Ahaa kumbe yani habari nilizozipata kuwa kuna msichana mrembo sana ambae yupo kule na ambae kaolewa na mtoto wa mfalme Ngololo yani ana maajabu huyo mwanamke "

    "yapi haypo tena?"

    "Kwanza kaja pale hasikii vyema, haoni vizuri lakini sasa hivi kawa msaada mkubwa sana pale kijiini huwezi kuamini kabisa na pia kawa kivutio kwa kila mmoja "

    "Dah natamani kuja kuishi hapo kijijini kutokana na mshikamano mliokuwa nao na nakuahidi baada ya kumaliza mambo yangu nakuja huko na kwa kuwa huyu ndugu yangu anapafahamu nitakuja nae huyu anaitwa Katunje bwana ni ndugu yangu sana."

    Waliagana na wao wakaelekea kurudi kijiji cha Shishimo. TUkiwa upande wa mzee Mambo sasa ana haha hajui nini afanye anaelekea kwa mzee Nyandu baada ya kupata habari kuwa mambo yameanza kubadilika na wanahitajika kwenye kikao na mkuu wao.

    Walisafiri kwa usafiri wao wa kila siku na hatimae wanafika ndani ya pango hilo ambalo huwa wanakutana kila siku. Mkuu wa pale ambae anashirikiana na Mizimu ya NYAMNYENA, alikuwa amegadhbika sana kutokana na hali ambayo ipo mbele yao. Walitulizwa kwa kukaa kimya wote na ndipo yeye akasimama kutoka kwenye kiti chake cha ukuu na ndipo akaanza kusema.

    "SIDHANI KAMA MNAWEZA KUTUCHEZEA KWA NAMNA HII...MJUKUU WAKO SASA KAWA TISHIO KUBWA SANA KWETU...NA HII INATOKANA NA KUMUACHA KIJANA WAKO CHITO AJITAMBUE NA KUJUA NINI AFANYE ONA SASA ANAANZA KUTUGEUKA SASA NATAKA HUYU CHITO AULIWE MARA MOJA IWEZEKANAVYO SITAKI MAJADILIANO ZAIDI YA KUTENDA KAZI HIYO KWA MKONO WAKO...."

    baada ya kumaliza maneno hayo hakika waliruhusiwa kuondoka lakini mzee huyo hakutaka kabisa kufanya jambo hilo kwa mtoto wake ambae anampenda sana alikubali kufanya kwa wengine lakini si kumuangamiza Chito, lakini kutokana na ushawishi wa rafiki yake Nyandu hakuweza kukataa alikubali na ndipo mipango ya kumnasa Chito ikaanza kuwekwa.

    '"Lakini hapa kuna jambo ambalo nalihisi, mke wa Mwenyekiti anataka kurudisha kisasi sasa twende kumfuata ili tukamkomeshe..."

    Walisambaa kama radi kisha wakamfuata mke wa mwenyekiti na wakamkamata majira hayo ya mchana akiwa ndani kwake katulia, Mama huyo alishindwa afanye nini baada ya kushikwa na kuanza kutishiwa.

    "Naomba utuambie una mpango gani na sisi unataka kupindua maamuzi yetu hali ya kuwa wewe ni mgeni hapa kwetu, unatujua vyema sisi?..." Alizidi kutetemeka baada ya kujiwa mchana kweupe na wazee hao wakimtishia ndipo akajikuta anapata ujasiri wa kuropoka hata ambavyo hajaulizwa kabisa.

    "Nakuambiaje nyinyi hamtopona mtakufa kama mlivyomuua mume wangu...."

    Hawakutaka kuchelewa walimlisha vitu vya ajabu ndipo akaanza kulalama tumbo kuuma sana akaanguka chini huku akigaa gaa kwa maumivu neno lake la mwisho lilikuwa ni kuwaambia ukweli ambao aliona utawafanya kuamini kuwa yale wanayoyafanya yatakuja kuwaghalimu kwa hatua moja ama nyingine.

    "Chito na katunj,,ee wame..ku.t..na na wat..akuja kulipiza kisasi cha mambo yenu hayo mnayoyafanya". Pale pale alifariki dunia.

    Kama kawaida yao walichukua sehemu za siri za mama huyo na wakaondoka kabisa yale maeneo. Hawakuwa na huruma lakini jambo ambalo waliondoka nalo pale kuwa Chito na Katunje wameungana na watakuja kulipiza kisasi kwa mambo wanayoyafanya.

    "Mimi siamini kama katunje ni mzima yeye kamuona wapi ?" "Achana nae cha kufanya subiri siku watakayotangaza kuwa ile nyama imekauka na tayari kwa kusagwa na kufanyiwa utaratibu wako wa kuwa kiongozi na atakaeleta ujinga tunamaliza "

    Bila wao kujua kuwa hayo wanayoyafanya kuwa siku yake iko mwishoni kabisa.

    Katunje aliamua kumsimulia kaka yake wakati wako njiani historia yake na chito na yeye akamsimulia jinsi mtoto wake alivyopotea na mpaka sasa haonekani. "Kaka sasa sijaelewa huyo mtoto alikuwa ni wa kike?"

    "Ndio katunje"

    "Sasa, kuna watu nilipofika pale bwawani walikuwa wanagombania swala la tenga na ikaonyesha kuwa mzee SIKUJUA anahusika na upotevu wa tenga sijaelewa hapo?"

    "Ndugu yangu....baada ya kupotea kwa mwanangu kuna kijana anaitwa Susu, huyu alimuazimisha tenga sikujua la muda sana kwa jana anapotea sikitu na susu anadai tenga kwa sikujua na hakulipata kabisa... ajabu muda ulipita anakuja kijana kutoka kijiji cha Kilimalondo..." " Kaka kilimalondo ndiko mimi maisha yangu yaliko eheee..."

    "Kumbe ndo unakoishi....sasa alikuja na lile tenga tukashangaa kuona lile tenga ambalo susu lilikuwa lake na ajabu zaidi mbuzi ambae alikuwa kafungiwa mule alifungiwa na nguo ya sikitu ambayo aliivaa kwa mara ya mwisho niliumia sana nikajua mwanangu bado yupo...."

    "Kaka ebu subiri unajua mara ya kwanza kuja bwawani nilifika kwa mwenyekiti SEMENI nilijitambulisha kuwa namtafuta kaka yangu anaitwa Chito ila hawakukufahamu na hatimae wakanifukuza kabisaaa...." Alisema Katunje

    "Ni kweli ujue kwa nini nilikuwa natumia jina la baba yangu mzee Mambo sasa ndio maana ikawa ngumu kunipata......."

    "Unana sasa baada ya kukimbia nikajikuta nafika mahali ambapo nilipokuwa nakwenda waliogopa kunifuata na wakawa wanarudi cha kushangaza nilikuta damu zikiwa kwenye majani...mbele nikaona tenga lilee ambalo la susu tena vilevile...."

    "Weee katunje usiniambie hivyo...ehee"

    "Usiwe na wasiwasi...mbele nikaona nguo ambayo hata juzi ambapo yule kijana aliyekuja bwawani kuuza mbuzi wa SWAI namjua alikuja na kitambaa ya nguo hiyo...Nikaamua kurudi nikachukua tenga nikabeba na nguo nikaondoka navyo hadi sehemu moja kuna bwawa..."

    "Katunje ulidiriki kufika bwawani yaaa kuna hatari kubwa sana watu hawatoki salamaa eheee" Chito aliamua kukaa chini kabisa mana hii taarifa inampa mwangaza fulani na tukio la kupotea kwa mtoto wake.

    "sasa nikawa nahisi kiu na jasho usoni ndipo nikataka kunywa maji nataka kuanza tu ikanipata akili ya wasiwasi nikaangalia nyuma nikamkuta binti kakonda wadudu wamejaa mwilini yani utadhani ni mzoga....MPAKA SASA HUYO BINTI NAMTAFUTA SANA".

    'ndugu yangu huyo ni mwanangu anaitwa Sikitu nakushukuru sana kwa msaada wa kumhudumia mwanao tena nakushukuru sana itabidi tufanye juhudi kubwa sana kumsaka mpaka apatikane"

    "Kaka unaponiona hapa nimeshindwa ila itabidi tuende mahali fulani huko nadhani tutaanzia ". Waliondoka na wakiwa na nia kubwa ya kupitiliza kwenda kijiji cha Bwawani waelekee Kilimalondo hadi MPOLONI kwa mzee UKELELE. Hawakutaka kufika nyumbani kwani wanajua kuwa hakuna faida yeyote pale wanayoipata kukaa na mtu mkatili.

    Safari yao hakika ilifika hadi kijiji cha Bwawani walichofanya baada ya kugundua kuwa mzee sikujua kuwa ndie chanzo wa yale yote ndipo walifika kwenye nyumba yake wakapiga alama ya X na hadi kwenye nyumba ya Mapato napo wakapiga X mlangoni wakapiga alama ya muelekeo ambao ulionyesha njia ya kwenda kijiji cha Kilimalondo, kwa kuwa ilikuwa ni usiku walifanya hayo na hawakujulikana.

    Safari iliendelea moja kwa moja hadi kijiji cha Kilimalondo ambapo napo hawakutaka kusimama sana waliendelea kuelekea njia ya kijiji cha Mpoloni ambako kutwa mzima walitembea, kutokana na uchovu walipumzika mahali na ndipo wakaanza safari na asubuhi na mapema wanaingia kijiji cha Mpoloni. Mzee Ukelel alikuwa wa kwanza kuwaona kwani yeye huwa anajiimu mapema sana na kuanza kufanya kazi za utengenezaji wa dawa zake. Mzee huyo alifurahi sana kuwaona ndipo aliwakaribisha na wao wakakubali wito.

    Mwaija alikuwa na furaha sana baada ya kumuona katunje kwa macho yake kuwa karudi salama kama mwanzo.

    "Baba huyu ni kaka yangu anaitwa Chito tumezaliwa wawili tu, "

    "Sawa karibu sana kwetu lakini hii sura kama naifahamu haijanipotea sana machoni mwangu kama miaka mingi iliyopita "

    "Mh! ukelele unamjuaje huyu kama hivyo labda useme unamjua baba mana ndie aliyefanana nae. "

    "baba yenu anaitwa nani na anaishi wapi"

    "Anaitwa Mambo sasa na anaishi..."

    "Shishimoooo...." Alimalizia mzee ukelele. alionyesha kuwa anamfahamu sana huyo mzee. "Inaonekana mlikuwa mnajuana sana na baba yangu.

    "'Unajua baba yenu ni mtu mbaya sana, hata Katunje upotevu wa binti Lyoto na hali aliyo nayo anachangia kwa kiasi kikubwa baba yenu,,,mpaka sasa nimefahamu wapi anaishi...mimi kuna mzee mmoja anaitwa Upengo na baba yenu tulikuwa marafiki ambao tulikuwa na kazi za uganga lakini baba yenu akacha na akaamua kuwa mchawi kabisa na kipindi hiko alikuwa na nguvu alitufukuza pale tutafute mahali pa kuishi kwa hiyo sishangai sana kuhusu hilo"

    Muda ulipita siku zilipita Mzee Ukelel anapoteza maisha baada ya kupatwa na homa kali sana jambo ambalo lilikuwa na mshangao mkubwa sana kwa mwaija ambae anaishi peke yake pale, lakini Katunje anachukua jukumu la kuwa nae kama kawaida.

    PIa hali ya mwaija inaonyesha rasmi kuwa ni mjamzito ambae baada ya muda huko akawa mama mlezi. Walipanga safari ya kwemda kijiji cha CHAMLO ambako wanaenda kuanza maisha kwa kuwa yeye ana rafiki yake ambae amempa sifa tele ya huko kijijini kwao........





    Safari ilianza ya kusafiri kwa pamoja kwenda ndani ya kijiji cha CHAMLO, safari hiyo iliambatana na watu watatu ambao ni KATUNJE, CHITO na MWAIJA. waliiacha nyumba ya mzee ukelele ambae ni marehemu kwa wakati huo baada ya kuugua kwa maradhi yaliyotokana na uzee wake.

    Upande wa Mwaija hakuwa na furaha kabisa baada ya kupotelewa na babu yake pamoja na mama yake na kwa sasa yuko yeye tu lakini hakuna kitu ambacho kiliharibika zaidi kwani kijana Katunje alishashikilia majukumu yote ya kumhifadhi binti huyo pia ukizingatia ni mjamzito. Safari ilikuwa ndefu sana kwani katunje pekee ndie anapafahamu, waliamua kupumzika kwa muda kidogo kisha waendelee na safari yao.

    Njiani walikutana na vikwazo vingi hasa wanyama hatari lakini kilichowasaidia ni uwepo wa katunje ambae alikuwa anatumia dawa yake ambayo kafungwa mkononi kama irizi ambayo kwake aliamini kuwa inamsaidia kwa kiasi kikubwa sana. "Katunje unamuona yule nyoka anakuja upande wetu na hatuna njia ya kumkwepa joka kama hili ambao ni hatari sana!" Chito aliongea kumueleza ndugu yake katunje baada ya kuliona joka ambalo lilionekana kutishia maisha yao kwa wakati huo.

    Kiukweli lilikuwa kubwa sana kiasi hata mwaija alihofu kuuliwa mmoja wao ama wote kwa pamoja. "Hapana msiogope ngojeni kwanza lisogee nalikausha sasa hivi" aliyaongea hayo katunje huku akipandisha nguo yake yani shati lake la mikono mirefu kisha akaifikia ile kamba iliyozunguka mkono wake. alianza kuiteremsha taratibu na kadri ilivyozidi kuteremka ndipo nyoka yule alivyopoteza nguvu hatimae kupoteza fahamu kabisa. "haya twendeni huyu kalala tayari" hawakuamini kile kitendo kilichotokea kwa muda mfupi tu. "katunje yani ile dawa ambayo babu alikupatia tayari bado unayo tu?" Chito alimuuliza.

    "Ndio ninayo na ndio ambayo imenisaidia sana katika kumtafuta lyoto na wewe "Eti sijawahi kukuuliza hivi lyoto ni nani?" Chioto aliuliza "Lyoto ni yule binti ambae nilikuambiaga muda wa nyuma huko kuwa alikuwa na matatizo na nikaamua kumsaidia lakini kutokana na hila za wazee wa KILIMALONDO wakampoteza na sijui wapi ambako aliko mpaka sasa " Waliachana na hayo wakamshika mkono mwaija ambae alikuwa anaogopa kumtambuka joka lile na wakaongoza njia ya kuelekea Chamlo.

    Ndani ya safari yao ilifikia kikomo baada ya kuona dalili ya nyumba kuonekana na sauti za ngoma zikiendelea kurindima, hapo ndipo walipoamini kuwa wamefika tayari na kikubwa zaidi ni kujongea taratibu kwa madaha na kufika kule kisha kumtafuta yule jamaa ambae alijitambulisha ni mtu ambae anahusika na mambo ya kukusanya habari nje ya Chamlo na kumletea mzee Ngololo pamoja na mwanae Bamuzi. "Kaka unaona tumefika tayari sasa ni kuanza kumtafuta kwa kumuulizia yule mtu" Katunje alitoa kama maoni yake kwa kaka yake. "Ndio lakini hatuwezi kuanza kumtafuta mtu kwenye mji wa watu lazima tumtafute kiongozi wao yani mwenyekiti ndipo tujue tunampata vipi " Katunje alikumbuka jambo " hapana kaka huku hawana mwenyekiti bali wana mfalme lakini kuna mzee mmoja anaitwa nani nimemsahau ila kwake napafahamu nilipelekwa na binti mmoja wa hapa".

    Walifika ndani kabisa ya kijiji hiko kisha wakaanza kusambaa huku na kule kutafuta nyumba ya mzee ambae katunje alimsema.

    Kumbe Binti NAOMI hakuwa mbali na maeneo hayo alifanikiwa kumuona kijana Katunje hakika moyo wake ulikurupuka sana kiasi haamini kama ampendae kamjia yeye mwenyewe, aliamini kuwa mama yake kamsaidia kumleta kijana huyo kwa wakati maalum. 'haaa siamini kama huyu kijana kaja kwa ajili yangu, lakini ngoja niende kwa mama kumueleza kwanza'.

    Aliondoka kwa mwendo wa shida kubwa yani haraka sana kumfuata mama yake. Baada ya kumfikia kwanza alianza kukatika mauno yake mbele ya mama yake akimaanisha furaha na yeye kama binti nzuri kushinda wote pale kijijini na hakuna hata wa kumfananisha nae. "Mwanangu umechanganyikiwa sasa hivi...mbona unaonyesha uzuri wako mbele yangu wakati nafahamu kama wewe ni mzuri zaidi ya unavyojijua kuna nini?". Naomi alicheza ngoma yao ya kiasili akifuatisha ngoma ambayo muda mfupi katunje na chito waliisikia.

    "Mama...kweli naona kama mzee Ukelele kafanya kazi ya maana.." Mama ilimbidi aache kazi ambayo alikuwa anaifanya "kaifanya kazi gani mwanangu?" Naomi alimsogelea mama yake. "Mamaaaa....Yule kijana tayari kaja nimemuona kwa macho yangu tena anahangaika mtaani akiwa yeye baba yake na ndugu yake wananitafuta mama nahisi hivo" Mama yake naomi alicheka sana kisha akanyoosha mikono juu kisha akongea lugha fulani "Nyamnyenaaaa.....ahsante". Kumbe hata huyu mama ni mshirika wa lile kundi la mzee mambo sasa na Nyandu, hakika kazi ni kubwa sana kwa watu hawa wawili yani Chito na Katunje.

    Mama huyo aliingia ndani pamoja na katunje kisha akaonekana anabadilisha nguo zake na kuvaa nguo za kazi. walikaa kwenye mkao mama na mtoto.

    Naomi namuita Nyamnyena kisha umuulize maswali sawa usiogope" Naomi hakuwa na shida kwani yeye ndie anahitaji na mama yake ni mtu ambae yuko bega kwa bega kumsaidia " Ilo tu mama muite haraka". Alifukiza moshi fulani kwenye moja ya kifuu kisha mama huyo akajifunika kaniki. ndani ya dakika kadhaa mama huyo alibadili sauti kabisa na kuwa ya mwanaume ikiwa na maana tayari nyamnyena kama mzimu wao kafika mbele yake na yuko tayari kujua nini shida.

    "HAYA SEMA SHIDA YAKO HARAKA BINTIII" nyamnyena aliongea kwa njia ya mama Naomi "Nymanyena samahani naomba kuuliza leo kuna wageni wameingia hapa kijijini sasa sijajua kama wamekuja kwa jambo gani?" Nyamnyena alikaa kwa muda kisha akacheka sanaa " BINTI, NAKUSIKITIKIA SANA UNATAKA KUINGIA KESI AMBAYO HAIKUHUSU...WALE WAMEKUJA KWA KAZI MAALUM AMBAYO SISI TUNAPAMBANA WASIFANIKIWE KWA HARAKA IWEZEKANAVYO..PIA YULE KIJANA TAYARI ANA MCHUMBA YULE AMBAE UNAMUONA PIA HAYUKO KWENYE MAWAZO YAKO KABISA..." Naomi furaha ilipungua na huzuni ikatawala "Sasa wamekuja kufanya nini na utanisaidiaje kwani nampenda yule kijana" Nyamnyena alicheka tena na tena "BINTI, YULE MALKIA ALIYEOLEWA PALE NA BAMUZI NDIO FAMILIA YAKE HII ILIYOFIKA NA SISI TUNAMHITAJI YULE BINTI...CHA KUFANYA TUTAKUPATIA YULE KIJANA UMPENDAE NA SISI UTUFANYIE KAZI MOJA TU" Naomi alikaa vyema na kuuliza tena " Kazi gani hiyo Nyamnyena?" Alianza kunguruma kama simba mara paka mala sauti ya mwanamke kisha ikarudi tena ya kiume "TUNATAKA UMVUE ILE DAWA YULE KIJANA MKONONI, PIA TUNATAKA SIKU YA TANO WAO KUKAA HAPA UTAPATIWA DAWA NA KITI WETU UTAMPA YULE MWANAMKE ALIYEKUJA NAE MIMBA YAKE ITATOKA NA NJIA RAHISI YA KUIVUA HIYO DAWA...ILA TUMIA AKILI YA ZIADA".

    Hatimae aliondoka kwenye kichwa cha mama huyo na Naomi akamsimulia kila kitu. " Mwanangu mpaka sasa tumeingia kesi ambayo haituhusu kabisaaa ila kwa kupendapenda kwako huko kama wanaume wengine huwaoni si bora hata ukabaki na yule kijana aliyekutoa usichana wako" Mama aliongea kwa jazba huku akipanga njia ya kukabiliana na swala lile. "Sasa Naomi hakikisha unawafikia kabla hata hawajafika kwa mfalme mana akifika kule lazima tuwakose watapewa kinga kubwa ambayo tutashindwa hata kuwakaribia.

    Chito aliusoma ule mji akagundua jambo yeye kama mkubwa na aliyepewa kinga na mzee Upengo ndani ya kijiji cha cha MIPINGONI.

    Alimdokezea tu Mwaija na Katunje kuwa wawe makini ndani ya mji ule. Walifika hadi kwa mzee MWALAMI ambae mwanzo Katunje alifika, Mzee huyo alikuwa ndani na wao wakaanza kuhodika pale nje. Mwalami alitoka nje kama kawaida yake alidhani kuwa ni viongozi wake wanamhitaji. Kumbuka kuwa watu wa Chamlo hasa viongozi wanajua kuwa katunje kafariki japo jina hawakumjua ndio maana wakaongozana kwenda kutoa pole kwa mzee Ukelele kule MPOLONI, Alivyotoka tu nje alishtuka sana hata akatupa kisu ambacho alikuwa anakitumia ndani humo "Babu vipi mimi ni yule kijana wa Ukelele nimekuja tena?"

    "Hapana aaah umetoka kuzimu lini wewe kijana unakuja kunijaribu sio.."

    "Kukujaribu babu au umenisahau...babu umenisahau kweli mimi ni yule kijana nilikwenda kumsaidia Bamuzi kufuata dawa leo unanikana ". Katunje aliongea baada ya kuona kuwa mzee huyo anachanganyikiwa. "Ngoja nakuja kwanza....nisubiri " Aliingia ndani mwake kisha akatoka na maji fulani hivi na usinga hakuamini kama ndio yeye kwani taarifa yake kuwa kafa. alimpiga usinga na kumwagia maji kichwani hatimae katunje akadondoka chini. Chito na Mwaija walishangaa. "Mzee mwenzangu sikuelewi umemfanya nini ndugu yangu hali anakuambia ni yeye kama mwanzo mlikutana vipi ushindwe kumuelewa leo".

    "Si hivyo mwenzangu kweli alikuja hapa akitokea Mpoloni, alifikia kwangu nikamuelekeza huko alikotaka kwenda lakini wakati wenzake wanarudi yeye hakurudi na huko kuna mmoja alikufa, sasa taarifa iliyokuja ni kwamba yeye nae kafa kachukuliwa na mzimu wa moto, tulipanga safari ya kwenda mpoloni kutoa rambirambi...kwa ukelele sasa akatuambia kuwa kweli hajarudi mpaka muda huo nafahamu kuwa huyu kijana kafa sasa anapokuja leo ndio wasiwasi wangu kwani hapa kijijini tumeingiliwa baada ya kuondoka malkia wetu basi hatuna ulinzi tena...ila kama ni wakawaida atainuka mda mfupi tu ila kama mmekuja kunijaribu haki ya nani hainuki...."

    Yale maneno yaliwachoma sana ukifikilia chito furaha yake ni Katunje na mwaija ndio kabisa. Mwaija hakusita kuliamsha chozi alianguka kwa katunje na kuanza kulia huku akimuamsha.

    "bwana wangu amkaaa usiniache peke yangu ona babu Ukelele kafa mama yangu kafa na wewe tegemeo langu unadondoka nitabaki na nani?.....Katunjeeeeee amkaaaa". Lile neno la Katunje lilimzibua masikio Mwalami kwani sio geni kabisa kwake.

    "Weee binti katunjee unamjua weeweee!?" Mwalami aliuliza.

    "Sasa huypo katunje si ndio huyu uliyemfanyia hivyo ndugu yangu kabisa na huyu binti ni mchumba yake, huyo mzee ukelele unayemsema kafariki dunia tayari ndio kabaki huyu ambae ni nguzo yake sasa sijui unamsaidiaje?" Mwalami alitumbua jicho huku akikumbuka jambo.



    ""Binti nilikukuta kule mtoni ukiwa ndani ya maji ina maana maji yamekusafirisha mpaka sehemu salama..japo hatujui wapi ambako umetokea, yapi yamekupata pia jina lako nani'' Lyotooo..." Ahaaa unaona sasa jina lako zuri sasa lyoto ndio jina la baba yakoo "katunjeeee" Ahaa basi tutakuita Lyoto katunje".



    Hapo alipokumbuka akapata picha fulani hivi. "Jamani ngoja tumpe dawa hii atainuka sasa hivi mana hapa kuna mapya nimeyaona samahanini sana ila ni wasiwasi wa kujilinda tu". Walimnywesha dawa na hatimae akainuka toka usingizini. Walimsubiri kwa muda ndipo wote wakaingia ndani ili kuzuia watu walioko nje wasijue nini kinaendelea humo ndani na ukizingatia kuwa wao ni wageni pale.

    "Jamani ninataka kuuliza swali je mnamjua binti anaitwa Lyoto?" Katunje alishangaa huku akikodoa macho yenye furaha kubwa sana pia hakuamini kama atalisikia swali zuri zaidi ya fedha maishani mwake. " Babu mimi ni ndugu yangu wa karibu sana japo si wa familia lakini ni ndugu yanguambae kapotea miaka mingi sana namfahamu vyema "

    "haya anaitwa lyoto nani?". Mwalami aliuliza.

    "Jina la baba yake silifahamu ila nilikuwa natumia jina hilohilo na hata nahisi lyoto si jina lake kwani tulimpa kwa kuwa alikuwa hafahamu hata jina lake kabisa tukaona tumepe lyoto kwa kuwa changamoto tulizozipitia mpaka anakuwa salama". Katunje aliongea hilo swala wakati huo chito anavuta picha anahisi kama ndie mwanae wanaemzungumzia akianzia kwa katunje kusema kuwa kamkuta bwawani akiwa karibu na tenga, akikumbuka lile tenga lilivyozua mgogoro kule kijiji cha BWAWANI, akikumbuka mengi hadi hapa kuwa kapewa jina la lyoto lakini si lake asilia aliamua kuingilia kati' kabla ya kusema Mwalami aliuliza swali "Huyu binti ninayemfahamu mimi anaitwa LYOTO KATUNJE huyu dada alipokuamsha pale chini nje aliita jina la katunje ndio maana nauliza lakini pia binti huyo kwa mbali sikufichi kafanana na huyu bwana" Mwalami alisema huku akimnyooshea Chitohttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kweli mimi ndio katunje nadhani kasema hivyo kwa kuwa kanizoea sana kwa kufanana na kaka yangu siwezi kuthibitisha kwa sababu kaka yangu tulipoteana miaka mingi na huyu Lyoto kanipotea muda mrefu sana " hapo ndipo mzee Chito akashindwa kuvumilia na akaanza kuyasema yake yeye yaliyo moyoni na yanayomchanganya.

    "Mzee mwenzangu, ndugu yangu katunje pamoja na shemeji yangu Mwaija...nadhani kuwa ndugu yangu katunje anafahamu kama binti yangu anaitwa SIKITU kapotea toka kijiji cha Bwawani sasa ni bora tukamuone inawezekana akawa ni SIKITU au si yeye tukamsaidia Katunje kumpata binti huyo" Mwalami alilipata somo la kutosha sana mpaka akaamini kuwa cha kwako hakipotei.

    "Jamani kwanza inatakiwa tuwe kimya hapa tulipo humuhumu ndani tusitoke naenda kule kwenye uongozi mkubwa mana kuna yule mleta taarifa za kijiji amefika tunaenda kuchambua baadhi ya mambo kuhusiana na ubadilisho wa uongozi kutoka kwenye ufalme kuja kwenye ngazi ya mwenyekiti. nitajitahidi kuliweka hilo swala kisha tujue tunalitatuaje mana huyo binti analindwa sana hata mimi nina siku kadhaa sijamuona kabisa "

    Mwalami alikuwa anajiandaa kuondoka kama alivyosema "Sawa lakini ni bora ukamueleza huyo mleta habari kuwa rafiki zake aliokutana nao kule Mipingoni tumefika aje huku kutuona!" Mwalami aliwa ahidi kuwa atarudi na huyo mtu baada ya mazungumzo.

    Mzee Mwalami alifika kwenye kikao cha viongozi baada ya kuisha kwa ngoma ya furaha aliyopigiwa mfalme, ndipo wanenguaji wote waliambiwa wapumzike wakale na kubadilisha nguo zao kwa ajili ya kusherehekea kwa pamoja. Walikutana akiwemo na Mzee KELEBU pamoja na wengine waliohitajika pale. katika ajenda ambazo walizizungumzia ilikuwepo moja inayomhusu binti Lyoto kufanya harakati ya kujua wapi anatokea kabla ya kumpatia uongozi kupitia Bamuzi, jambo ambalo lilichukua muda sana ni baada ya matatizo ya kuingiliwa na uchawi mara kwa mara pale walipo. "Haya tumefahamu baada ya uchunguzi mrefu tunamkaribisha mpelelzi wa habari aliyefika jana atueleze yapi mapya yanayoendelea." Alikaribishwa

    "Kweli nimefika vijiji husika ambavyo tulivituhumu kuhusika na huu uchawi, nimegundua kuwa kuna kijiji kinaitwa Shishimo historia yake kuwa wapo wasumbufu sana ambao wanadiriki kuua watu ..sasa sisi vita vyetu ni kuwaendea moja kwa moja najua wanachojikingia hakina nguvu kama sisi tuliye nae huyu malkia mpya..pia nimegundua kuwa hapa kwetu wapo ambao wanashirikiana na kundi hili ambalo linajiita NYAMNYENA ni kundi la mizimu mikali sana endapo wakifanikiwa kujua kuitumia wanasambaratisha kila kitu...sasa ni kutuma jeshi letu kuwadhibiti.." walimuelewa kwa kila hatua aliyoisema. Muda wa mambo ya nyongeza ulifika ndipo mzee Mwalami aliomba nafasi ya kuongea kwa kirfu kidogo apate kueleweka.



    "Jamani mnajua kuwa malkia mimi ndie nilimleta baada ya kumuokoa......" Mara bamuzi akaingilia "Kwa hiyo unatakaje sasa...mzee nitakutoa kwenye cheo ulicho nacho unataka kunitenganisha mimi na huyu hakuna hata mmoja ambae ataweza mana tumemhudumia mpaka akafika hapa..." Aliyaongea ya kuyaongea mpaka wakastaajabu ndipo mzee ngololo akamtuliza "Kijana kumbuka wewe ni kiongozi wa baadae tumempa nafasi ya kuongea muache amalize..."

    "haya ahsante..kwanza sifa ya kiongozi lazima awe na BUSARA, awe na HEKIMA, awe na SUBIRA, hivi vitakusaidia sana nimekupa dondoo naomba uwe na hekima kwenye maongezi yako naomba uwe na busara kwenye maamuzi yako naomba uwe na subira katika kufanikisha mambo naomba niendelee kueleza jambo muhimu.....Kipindi namleta hapa binti tunamjua kwa jina la lyoto hatukujua jina la baba yake tukamsikia anataja jina la katunje na tukampachika jina la lyoto katunje si ndio?"

    "Ndiooo kabisa mwalami endelea tunakusikiliza"

    "Mnakumbuka kijana Bamuzi alienda polini kutafiuta dawa ya kumtibia Lyoto katunje mnakumbuka?"

    "Ndio mwalami tunakumbuka..."

    "Sawa, kuna kijana alienda kumsaidia kule je Bamuzi unamfahamu yule kijana kwa jina lake?" Mwalami alimuuliza

    "hapana simfahamu pia yule kijana alikufa tayari..."

    "Sawa najua hamfahamu, anaitwa yule ndie KATUNJE mwenyewe....kijana hakufa ila alichelewa kufika mpoloni alipatwa na vikwazo njiani..sasa yule katunje si baba yake ila alimsaidia tu huyu binti na msaada wake mkubwa sana kuliko wako wewe hapa hata punje haufiki...pia kuna wasiwasi ninaouona kuwa hata baba yake anajulikana munajua kwa nini?"

    "Mzee mwalami hizi habari ni mpya sana...lakini huyu katunje kama namfahamu nilipita kijiji kinaitwa MIPINGONI nikamkuta rafiki yangu anaitwa Chito akiwa na nduguye huyu " Hapo mwalami akamnyooshea mkono "Ewalaaah! kabisa na huyo chito unayemsema yupo mimi ndio wageni wangu wamekuja kukutafuta wewe uliwa ahidi kuwa utawapokea wapo nyumbani kwangu kule sasa ndio maana nikasema tuwe na busara kwenye maamuzi "

    Kila mmoja pale hakuamini kwa kile anachokisema mwalami,

    "haya maajabu kwelikweli, haya fanya haraka sana nenda kawaite uwalete hapa haraka mno kabla hata kabla Lyoto hajaamka ndani akajua kila kitu."

    Mzee Mwalami anajiandaa kwenda kuwaita kule alikowaacha na wakati huo tukumbuke tayari mama Naomi kamtuma mwanae kwenda kwa mzee Malami kufanya majambozi ya kuwanasa watu hao.





    Mzee Mwalami, alitoka kwenye kile kikao ili apate kwenda nyumbani kwake ambako aliwaacha wale watu. Pia Naomi nae akiwa kwenye harakati hizo hizo. aliondoka kutoka kwake yani kwa mama yake na kwenda moja kwa moja kwa mzee Mwalami ambako alikuwa na asilimia zote kuwa atawakuta. Alijua hivyo kwa kuwa kipindi ambacho kijana Katunje alikuja alimpokea yeye na ndie ambae alimuelekeza kwa mzee huyo.

    Umbali wa kutoka kwa mfalme Ngololo kwenda kwa mzee mwalami haukuwa mbali ukilinganisha na ule wa kutoka kwa mama Naomi. Utofauti kuwa Naomi aliwahi kwa kuwa ni kijana na mzee Mwalami pamoja na uzee wake ilikuwa ngumu kutembea kwa haraka sana. Naomi alipokaribia kwenye nyumba hiyo alisikia sauti za watu wakiongea akafahamu fika kuwa wao wako ndani alifungua furushi lake na kutoa kibuyu ambacho alikabidhiwa na mama yake, kwa bahati nzuri mzee Mwalami anakaribia na anafanikiwa kumuona yule binti akiyafanya madudu pale kwake. "Pumbavuu huyu binti hanijui vizuri na nilishamkanya mama yake hii tabia". Alitembea taratibu kisha alipomuona kuwa anataka kumwaga ule unga kwenye njia ya kupitia mlangoni kwake akamshtua.

    "Weee weee mwanaharamu...mkubwa wee huna hata aibu unafanya nini hapo toka harakaa khaaa!" Naomi alikurupuka kwa kukimbia na kuacha baadhi ya vitu ambavyo alikuja navyo pale. Mwalami alifika na kuviangalia na akagundua kuwa ni vya kichawi "Looh! yani mwanamke mdogo anajihusisha na mama yake kwenye uchawi sasa hivi navichoma moto hapa hapa".

    Aliingia ndani kwanza na kuwakuta wageni wake wakiwa kwenye harakati ambazo walikuwa wakizifanya hasa pale binti Mwaija alipokuwa akijisikia hali mbaya tumboni mwake. "Jamani kuna jambo gani tena hapa?" Mwalami aliuliza swali "Aaah tunashangaa tu anasema trumbo linamuuma sana hata hatufahamu nini hasa kimempata ". Mwalami ilimbidi aliache swala la kule kuwapeleka na ndipo akaanza kushugulika na binti huyo. Huku na kule waliendelea kutafuta dawa ambayo itamsaidia apone mapema sana.

    Naomi alifika nyumbani kwa mama yake akiwa hoi taabani. " Mamaaa mwalami kaniona" Naomi alimuelezea mama yake jinsi gani lile tukio lilitokea kule. "Kakuona haya mbona mimi nilishakurahisishia kazi nimeshapiga bao kwa yule binti sasa wewe unashindwa kumalizia!.." Mama huyo kumbe ndie kasababisha hali ya binti Mwaija kuwa mbaya sana akiwa na lengo la kumpoteza maishani mwake. "Hapana mama nimefika nataka kuanza tu kama ulivyonielekeza na yeye anatokea ndiopo nikakimbia na hata hivyo kibuyu na ile dawa nimeiacha..." Naomi alimhadithia mama yake kuhusiana na ile dawa na kibuyu kukiacha.

    "Mwanangu Naomii umeniuaaa tayarii haaa...haya nenda haraka ukachukue kabla hata hajaiharibu fanya haraka mjinga wee muone unakuwa lizembelizembe sana". Naomi alisafiri tena kurudi kule ambako anahisi kuwa atakipata au atakikuta mzee mwalami akiwa kamlindia jambo ambalo ni ndoto kwa mzee mwalami na watu kama hawa. Lile lengo lake alilitimiza mapema sana kwani alikichoma moto pamoja na ile Irizi. Naomi alipofika pale aliweka mikono kichwani huku akitoa machozi baada ya kuona vile vifaa vikiwaka moto mkubwa tu tena wa kutosha usiohitaji kuni wala kifuu ili kukoleza zaidi ya hapo.

    Alirudisha miguu yake kinyumenyume, huku akiwa haamini kabisa yale anayoyaona "Nitamuambia nini mama yangu jamani mamaaaaaa". Aligeuza shingo yake kwa mara ya mwisho kuusindikiza moshi ambao ulikuwa unafuka pale kisha akaelekeza uso wake njia ya kwenda kwa mama yake mzazi. Mama yake Naomi uso wake ulionekana kubadilika na kuwa rangi nyekundu uliovilia damu hii yote kutokana na ile hali ambayo imetokea haswa akihofia maisha yake kuwa mwisho kwa nyakati ambazo ni mapema sana.

    Naomi alifika nyumbani ndipo akapiga magoti ya kumuomba radhi mama yake huku akitoa chozi la hisia kujua kwa makosa yale ambayo kayafanya. "Mama yangu nisamehe kabisa mimi, mzee Mwalami kachoma morto vile vitu mamaaaa" Mama Naomi alimtumbulia jicho mwanae "Naomiiii nini etiii aaaah! nishakufa kabisa hapa ololooo". Baada ya muda mama huyo alitulia na kumtuliza mwanae kisha akamuambia "Mwanangu hapa hatuna jinsi nasubiri maelekezo ya wakuu wa Nyamnyena watakachokisema ndicho nitakifuata.".

    Upande wa Mwalami alipiga jitihada zake zote mpaka hali ya yule binti ikawa nafuu, " Jamani naombeni msitoke humu ndani, ngoja niende kuwaeleza kwanza kuwa imeshindikana na tutaenda kesho yake pia nitaenda kumuita daktari wa mfalme aje kumtibia zaidi".

    Walimuacha mzee huyo aondoke na wao wakabaki na mgonjwa wao. "Ndugu yangu katunje, hapa kijijini nina wasiwasi napo mana ila ngoja tukionana na huyo binti kama ndie yeye basi tunaondoka nae kama si yeye hapa sina muda wa kukaa hapa". Baada ya muda yani jioni sana ndipo mzee mwalami anafika na kufungua mlango kisha kuingia ndani na kuwakuta wakiwa wameshika tama wakimzunguka mwaija. Mzee huyo aliandaa chakula kilipokuwa tayari walikula wote kwa pamoja. "Jamani asubuhi tunadamkia kwa mfalme tayari nimeshamueleza lakini mzee Kelebu kashindwa kufika kwa sababu alikuwa na shughuli na mfalme".

    Majira ya usiku sana Mama Naomi na Naomi mwenyewe walifika kwa Mzee Mwalami nje ya nyumba hiyo. "Mwalami choonde sana tunakuomba uturejeshee vitu vyetu tutakufanyia kwa kila kitu ambacho utakitaka kwa sasa hivi tunaomba sanaaa chondeee..." Walikuja kuomba radhi kwa mze huyo ili waweze kurejeshewa vitu vyao. Mzee Mwalami aliona kuwa ni upuuzi ambao wanaongea aliwafukuza kwa kuwaambia kuwa ubishi wao utawafanya wasitoke salama pale la sivyo waondoke.Hawakuwa na ubishi waliondoka zao.

    Asubuhi na mapema sana katunje anaonekana kulia sana huku akitamka jina la mwaija, sauti hizo ziliendelea na kuwaamsha wengine walio lala ndipo kaka yake chito nae aliamka na kuangalia nini kimejili. Hakika kumbe mwaija alikuwa tayari kapoteza maisha. Walikuwa pamoja kutulizana kwani tayari mwaija ndio hivyo kawatoka, Mzee Mwalami nae aliwapa pole sana kwa lile tukio lililotokea.

    Waliamua kufanya utaratibu wa kuona nini wanakifanya lakini kwa muonekano wa bwana Mwalami alijua kuwa yule binti kauliwa kwa njia ya kishirikina "Jamani huyu mwanamke wako kafa kwa uchawi..na utaraibu wake lazima mapema hii azikwe ili kuwafanya wasimfanye mfu hai tena mana lilionekana kuwa ndio lengo lao..tukimzika hali kila mmoja anaona mnazika gogo haki ya nani.." Walifanya kila njia ndani humo walichimba kaburi kwa haraka sana na kumzika kimila zao za Chamlo. Baada ya pale waliombwa wasioneshe dalili zozote za kufiwa kwani pia ni aibu sana mgeni kufia kwenye eneo ambalo hata viongozi hawatambui na alifanya hivyo ili kuwapa kazi wale waliomfanyia ule unyama kwa makusudi ili wasifanikiwe.

    Aliwapanga Katunje na Chito kwa ajili ya kuelekea kwa mfalme huku akiwapa maneno ya kuwatia nguvu "Ninachohitaji huku mkifika muonyeshe hakuna kitu chochote ambacho kimetokea, pili nawa ahidi kuwa tukirudi huku naenda kuwaonyesha yule ambae kamuua mwaija". Japo maumivu walikuwa nayo lakini walikubali kuyaacha na kufuata yale ambayo yule mzee anayasema kwa kuwa wapo ugenini.

    Binti Lyoto akiwa kwenye chumba chake na binti Mwana ambae ni kaka wa Zweli. Aliambiwa kuwa amuandae vyema binti huyo ili akitoka nje onekane kama mwanamke wa mfalme Bamuzi. Pia lengo jingine ni kuonana na watu hao wambao wamenadi kuwa lyoto ni mtoto wao. Bamuzi akiwa na baba yake mzee ngololo "Baba unafahamu kama huyu binti anafaida sana hapa kwetu?" " Haswaa mwanangu ndio maana napenda sana asitoke hapa kwenda mahali popote. Ghafla anatokea kijana akiwa kwenye mwendo wa kasi sana, "Nini kijana wewe unachokimbia kuna uvamizi?" Aliuliza Bamuzi baada ya kumuona yule kijana akiwa hoi.

    "Mkuu kuna watu wameingia ndani ya mipaka yetu wapo wawili, wanakuja maeneo haya huku kwetu!.." Bamuzi pamoja na baba yake walisimama huku pia walinzi wakiwa tayari kwa amri ya kushambulia. "Kuna watu wawili wamekuja kushambulia....eti wana silaha hao wawili?" Aliuliza Bamuzi. "sifahamu kabisa ila wanapoonekana kuwa ni watu hatari sana mana wana mkuki...".

    "walinzi wote hakuna abaki mmoja akiwa na huyu Mwana akimuangalia Lyoto? na wewe binti hakikisha kama mzee Mwalami anakuja na hao watu msiruhusu kumtoa huyu binti mpaka tutakaporudi sawa?" Hivyo basi mambo yakawa yameiva mzee Ngololo akiongoza msafara pamoja na mwanae huku pembeni akiwa bwana Kelebu na matibabu yake. kwa wanajeshi watakao kuwa majeruhi." Walitoka pale na walibaki watatu tu akiwemo Mwana,Lyoto na mlinzi mmoja.. Wakati wao wanaelekea huko mzee mwalami na wale wawili wanafika pale wanakuta kimya "Mfalmeee wa Chamloooo" Ilikuwa kama salamu ambayo alikuwa anasalimia kama watakuwepo, ndipo mlinzi akaeleza kuwa hawapo na wameenda mahali.

    Walipata kuingia ndani humo. Mungu si Athumani, Lyoto anatoka ndani na uso kwa uso na Mzee Chito na Katunje kila mmoja walijikuta wanagongana majina "Lyootoooo..." Katunje alitamka jina hilo na chito nae " Sikitu mwananguuuu". Walitazamana wote na Sikitu au Lyoto nae alivuta kumbukumbu ndefu sana na kujua kuwa Sikitu ndio jina lake alinyanyua miguu yake kumfuata Katunje kwa kuwa ndie wa karibu kumjua mapema lakini Mzee Chito aliendelea kulitamka lile jina la Sikitu kwa nguvu zake zote ndipo sauti ya mzazi aliyepambana kwa udi na uvumba kuhakikisha mwanae anapatikana ilipenya barabara kwenye masikio ya binti huyo na kumgeukia mzee chito "Babaaaaa....babaaaaa mamaaa yuko wapi babaaa?". furaha yenye majonzi mazito sana ndani yake yaliwakutanisha wana ndugu hao. "Kaka chitoo huyu ndio huyo mwanao aliyepotea kwani?" Katunje aliuliza "Ndio ndugu yangu mwanangu huyuu mwanao huyuu uliyekuwa unamlinda damu yako hiii" Chito alimsogelea Katunje na kumuambia "Ndugu hapa tunaondoka hakuna kusubiri chochote hapa kama mtoto tumempata.." Mzee mwalami alishtukia hilo swala lakini aliona awape njia na yeye amzuge mlinzi kule aliko.

    Hatimae wanafanikiwa kutoroka watu wanne Katunje, chito, Sikitu, mwana na mwalami na yeye aliunga kuondoka kabisa kile kijiji kwani alihofia pia kufuatwa na wale wachawi sasa bora aondoke kabisa kile kijiji. Safari yao ilipita maporini sana kuogopa wakipita njia kuu watakuwa rahisi kuonekana. Uande wa huku kwenye ule msafara Walifanikiwa kuwakamata wazee wawili ambao hawakuwa wenye madhara sana kwani ndio wale wazee wa kijiji cha KILIMALONDO na si wengine bali ni KAUZIBE na UDEVU.

    Walikamatwa wale wazee hadi kupelekwa kijijini. Kwa bahati mbaya wanakuta mlinzi akiwa kalala fofofo kabisa hajitambui kabisa, Bamuzi humuambii chochote kuhusiana na Sikitu, alimtafuta kwa kumuita bila mafanikio ndipo alikuja kumuamsha mlinzi laaah! alikuwa mbali sana alipoamka anakutana na banzi la mgongoni na swali juu " Tumekuacha ulinde watu je wakuwapi hao watu?" Mlinzi alibahabahabuha hajui nini aseme "Wamekimbia baada ya kunipa maji nikanywa nashangaa napata usingizi..." Bamuzi alitaka kumchoma kisu palepale lakini baba yake alimkamata na kumtuliza apunguze jazba kwanza.

    Wale wazee walihojiwa "Mnatokea wapi na mmekuja kufanya nini huku?" Mzee Kauzibe kwa kuwa ni mzee mjanja sana alijibu kwa ufasaha "Ndugu zetu tunahitaji msaada wenu kwanza, tumekimbia kijiji cha Kilimalondo baada ya kutishiwa na kukoswa kuuliwa na kijana mmoja anaitwa KATUNJE...." Bamuzi na Mzee ngololo waliinuka "Katunjee?....unamjua wewe katunje?" "Ndio huyu kijana alibahatika kumpata binti mmoja ambae alimkuta akiwa na hali mbaya sana kijiji cha Bwawani kipindi anamtafuta kaka yake Chito. alivyofika pale huyo binti mimi nilimtibia mpaka hali yake ikawa njema na tukamuita jina la Lyoto..."

    Walizidi kuchanganyikiwa yale mambo kama yanapangwa litoke hili liingie hili. "Mzee ebu malizia kwanza hayo maelezo.." Mzee Kauzibe alihisi jambo. "Sasa pale tuna mfalme anaitwa SWAI akiwa na kijana wake KIMOLO kama mila zetu huwa Swai huchagua mwali wa kulala nae sasa ikaangukia kwa Binti Lyoto na mimi ndie niliyepewa kazi uya kumpeleka...hapo ndipo ndipo utata ulipoingia mpaka akatutaka sisi kutuua japo kweli tumekili makosa yetu na hapa anatutafuta ndio maana tukakimbilia huku..." Kila mmoja alikuwa hoi

    "Poleni sana hapa unamuona huyu kijana kapaniki kwa sababu ya binti mmoja ambae tulimuokota mto ule ambao unatokezea kwenu huko kilimalondo anaitwa lyoto katunje...." "Yani lyoto bado nzima haki ya nani anapona sana huyu binti...nakumbuka mimi kwa macho yangu anaangukia korongoni humo wakati nataka kumkamata...sasa akiniona si ataniua..."

    "Hapana pia huyo katunje na na Chito wapo hapa kijijini wamekimbia na Lyoto sasa walinzi tafuta mkiwakuta kamata leta hapa mapema sana tawanyika" .Walitawanyika na huku wazee hao waliposikia kuwa wale watu waliowakimbia kule bado wapo, waliama mapema sana na wao wakakimbia kurudi kijijini kwao kilimalondo. Mungu alisaidia wale na msafara wao majira ya usiku wanapata bahati ya kufika kijiji cha Kilimalondo kwa tena walijificha pamoja na wingi wote ule wanakaa kwenye nyumba ya zamani ya Katunje.

    "Haya karibuni poleni kwa safari ndefu..vipi kuna mtu kaumia jamani?" Aliuliza katunje akitaka kujua hali ya kila mmoja. Wale wazee walijitahidi asubuhi na mapema ndipo wanafika mana usiku mzima walikuwa safarini kurudi kijijini kwao kumkimbia Katunje. Asubuhi na mapema kwa kuwa walijiamini kuwa wako salama sana ndipo Mwana akakaa na Sikitu pamoja na wale wengine wakianza kukumbushiana na kupeana faraja. Ilionekana binti SIKITU ana waza kitu akivuta taswira avute lakini kama zinakataa. Walipanga siku ya pili yake ndipo waondoke, kumbuka tayari binti Sikitu ana nguvu zile alizopewa kama za umalkia ambazo kokote kule aliko lazima zitamrudisha kule alikopewa uongozi akaendelee kutawala. Majira ya usiku mzee Kauzibe na Udevu walilala nyumba moja tu. Huku Sikitu akili yake ikimtuma vibaya aliamka usiku usiku na kwenda kwenye nyumba ya mzee Kauzibe aliufungua mlango na kuwakuta wakiwa wamelala, Sikitu alikuwa katili sana kwa muda huo haikujulikana kwa nini anafanya hivyo mana Alimtumbukiza kisu mzee Kauzibe na mwenzake palepale wakaaga dunia na yeye akarejea nyumbani na kulala kisha wakaendeleza basi la usingizi lifike mji wa asubuhi,

    Kabla jogoo hajawika tayari waliamka wakitaka kujiandaa kuondoka wapite kijiji cha bwawani kwenda kumaliza mambo yote kule na akataje kama anamfahamu nani ambae kasababisha matatizo yake mpaka wao wanahangaika kwa kiasi kile kama mbwa walio kosa makazi.

    Lakini safari yao ilikatishwa na vilio ambavyo vilitoka mtaa wa pili. Katunje kwa kuwa ni mwenyeji pale aliomba yeye aende kutafuta na kujua nini tatizo ambalo limetokea huko au kuna tafrani gani ambayo imejitokeza, alishangaa kuona kwenye nyumba ya mzee Kauzibe mzee ambae alikuwa anamkubali sana lakini alijawa na tamaa watu wanalia huku akisikia sauti ya watu wakisema kachomwa kisu tena wote Kauzibe na Udevu yani hapa pamearibika cha kufanya tutafute wageni wa humu.

    Aliona litanuka muda si mrefu sana cha umuhimu ni kwenda kuwaeleza kuwa waondoke mapema kabla hata swala halijafika kwa mzee Swai. Alikimbia kwa spidi zote hadi nyumbani kwake "Mnasikia kuna wazee wawili wamefariki kwa kuchomwa na visu sasa wanawatafuta wageni....tunatakiwa kwenda Bwawani sasa hivi wasije kutukamata.....



    ...Waliungana watu wote yani mzee Chito, Mwalami, Katunje, Sikitu na Mwana kuondoka na kwa kuwa ilikuwa mapema sana ambapo kwa kijiji hiko ilikuwa ngumu watu kutembea ovyo na kukutana na watu, iliwawia ngumu wao kuonekana wakati wanaondoka pale. Safari ilianza mapema sana huku wakiangalia huku na kule kuhakikisha kuwa hakuna mtu ambae atakuwa anawatilia kiwingu, lakini huku nyuma kila mmoja akiwa na mashaka makubwa hasa yule Katunje kuhusiana na kifo cha watu wale. "Kaka unajua kuwa mpaka sasa sijaamini vifo vya wale watu wawili!". Katunje alikuwa anajiuliza kwa kumshirikisha kaka yake.

    "Kwani unawafahamu hao waliokufa?" "Haswaaa...nawajua vyema sana ndio mmoja wao alimsaidia sana Lyoto..aah skitu". "Binadamu tuna u yama sana haya tuwaachie wenyewe ngoja na sisi tuelekee nyumbani kwetu". Wakiwa njiani ndipo mzee Mwalami aliongeza katika hoja ile kwa kuonyesha kweli wako pamoja. Kwa mwendo waliokuwa wakitembea hakika sikitu na Mwana walichoka sana hivyo iliwabidi wapumzike mahali. Walitafuta mahali ambapo palikuwa kwenye mbuyu mkubwa sana ambao uliweka kivuli kikubwa sana.

    Wakati wanaendelea kupumzika alikuwa anafikilia sana mambo mengi sana mzee Mwalami kitu ambacho kila mmoja alikuwa na ulizo juu ya mzee yule. Lakini bwana Chito hakuwa mzembe aliona kukaa na kitu moyoni hawezi ilimbidi amuulize "Mzee Mwalami, mbona uko hivyo sasa jamani kama una mawazo huku ukimuangalia sikitu". Mzee mwalami ilibidi apindue shingo yake kisha akacheka kwanza "Hapana kuna swala nalikumbuka sana mpaka sasa limenikumbusha zaidi ya zamani".

    "Aaaakh bwana hapa sasa kama familia moja hamna cha kuogopa zaidi ebu ongea kwanza ili tujue tunakusaidia vipi" Hapo mzee mwalami alionekana akikaa vizuri kutokana na ile staili aliyokakaa mwanzo kuona inamchosha sana, kisha akameza mate yake kwa uchache wa kukosa maji ya kunywa.

    "yani maisha ambayo kapitia Binti yako Lyoto..mtanisamehe mana ndio jina nimelizoea sana maisha yake ndio ambayo nilikuwa naishi mimi nikiwa na miaka midogo sana.." Kila mmoja pale kasoro mwana na Sikitu ambao walikuwa wamelala kwa uchovu wa safari za kuunganisha. "Ehee mapya hayo haya tuambie yapi ambayo ulikuwa unaishi" Chito alihoji... "Nakumbuka sisi tulizaliwa watoto wawili, Tulilelewa kwa muda mrefu sana na wazazi wetu sasa baada ya mama yangu na baba yangu kuuliwa kwa moto kwa sababu ya ugomvi wa mashamba sisi tulianza kuishio kwa tabu sana...Kipindi ambacho ilitokea vita ya vijiji kugombea ufalme baada ya mfalme wetu kufa na hakuacha mtoto hata mmoja sasa haikujulikana nani ambae atachukua ule ufalme...watu walikufa sana mimi nilianza kumtafuta ndugu yangu nikiwa mdogo na huyo na alikuwa mdogo japo mimi ndie nilikuwa wa kwanza kuzaliwa..hakika sikumpata ndugu yangu na mimi nilibebwa na mzee mmoja ambae ni Mzee Ngololo akaniondoa pale na kukimbia na mimi akiwa kanibeba mpaka kijiji kile chake...sikujua mpaka hapo ndugu yangu wapi alipo na hata jina lake nimelisahau kwani tulikuwa wadogo sana na kikubwa zaidi sijui yuko hai au laah ndio maana nikikumbuka ya sikitu basi nalia sana mana nilishasahau". Walijikuta wote wanaungana kulia kiume.

    Hadithi ya maisha ya Chito na Katunje yalikuwa hivyo na yashatimia baada ya kuonana kwao. Maisha ya Sikitu na baba zake yalikuwa hivyo na yameshatimia, Walimpa imani kuwa ipo siku atafanikiwa kumuona kama yuko hai. Pia chito aliongea mambo mengi sana ambayo yalikuwa yanahusiana na kile kijiji ambacho kimetokea,vilevile walimuamsha Sikitu na kumkumbushia yale yaliyopita kama atakumbuka. Alionekana Sikitu kumkumbatia baba yake huku akilia kwa majonzi sana hali hiyo ilionyesha kuwa yuko tayari na kila kitu anakumbuka lakini hakutaka mzee chito amueleze swala la mama yake mana itakuwa swala lingine, lengo la mzee chito kufiuka ndani ya kijiji cha Bwawani. "haya jamani tuinuke twendeni huko mana si unajua kuwa muda tuwahi kufika na tujue tunaenda wapi sasa baada ya hapo". Walisimama na kila mmoja akiwa na nguvu nyingine ya kuendelea na safari.

    Waliongozana huku wakiwa kimya na kila mmoja akifikilia maisha baada ya kukimbia kule kijiji cha Chamlo yatakuwaje. Hatimae wanafanikiwa kukiona kijiji cha Bwawani na kila mmoja alifurahi ila wale wawili mzee mwalami na mwana walielekezwa kuwa safari yao iko pale na itakuwa inatimia na mambo yote yanaenda kufanyika pale na wale wazee waliotajwa kuwa ni wasumbufu wanapatikana pale.

    Mzee Mwalami kama mtu mkubwa aliyekula chumvi au munyu nyingi aliwasimamisha wote na kuwashauri jambo. "Nawaomba munisikilize kwa makini sana, nadhani kila mmoja ndani ya kijiji kile wanajua kuwa SIKITU kafariki si ndio...sikitu usijisikie huzuni tupo kukomesha upuuzi waliokufanyia kama unawajua sawa.." "Sawa baba.." Mzee mwalami aliendela kusema.

    "Kinachotakiwa hapa tuingia msituni huku...ili tujipange hata kutengeneza kitu cha kujihifadhi kwa siku kama tatu hivi wakati tunaangalia jinsi ya kuingia mana inahitajika kupasoma pale vizuri sawa..".Baada ya kusema hayo kila mmoja alikubaliana na ndipo wakageuza njia na kwenda ndani ya msitu huo uliokaribu na kijiji hiko.

    WAKATI wao wakifanya mipango hiyo. ndani ya kijiji cha Bwawani watu walionekana kuwa na furaha sana baada ya kuitwa na mwenyekiti SEMENI na wakishangilia kwa kupiga ngoma na wanawake wakicheza kwa furaha. Pale walionekana Mzee MAPATO na SIKUJUA, walikuwepo pale na wao wakishangilia sana. Haikujulikana furaha hiyo imewajia kwa njia gani.

    Baada ya muda kupita ngoma ilinyamazishwa na wote wakakaa kwenye viti vyao huku wengine wakilegea kwa ulevi wa pombe kali walizokuwa wanakunywa. "Hayaa nashukuru sana kwa hiki mlichoonyesha kuwa tuko pamoja sana sasa, nadhani uadui umejulikana kuwa ulikuwa ni kwa mzee Chito na ndugu yake katunje sasa tunatakiwa kuishi kwa raha na furaha sana hatutaki mauaji yoyote ambayo yalifanyika...sasa kabla sijamaliza na kuwaacha muendelee na furaha zenu nimkalibishe mzee Manyenye mzee mkubwa hapa nimpe nafasi ya kuongea kwanza" Hapo ndipo mzee wa makamo alijivuta kutoka kwenye kiti chake na kuja mbele za watu, na kwa kuwa sauti yake ilikuwa inakwaruza alafu pia ni ndogo sana iliwabidi watulie kumsikiliza wakitarajia mazuri kutoka kwa mzee huyo.

    "Mimi kama mzee wa hapa napenda kutoa maneno ambayo yatakayomuuma ajirekebishe mapema..." Kwa kauli hiyo tu iliwafanya watulie na pawe kimya kama wamemwagiwa maji ya baridi, ndipo mzee huyo alianza kuwaangalia sana watu yani hadhira ambayo anaiongelea ambao muda mfupi wametoka kwenye furaha na yeye anaonekana kubadilisha upepo wa furaha zao na kuwa huzuni.

    "Nawaomba mnisikilize..najua mmetoka kufurahi sana kwa neno kuwa hatutaki mauaji yaendelee mnajua kuwa mwanangu kauliwa...hatuwezi kufurahika na wauaji wakiwemo humuhumu kijijini.." samahani mzee ja..." Alikuja juu mwenyekiti kutaka kumsimamisha kwanza mana anaonekana kupeleka upepo mahali pengine. "Hapana....kijana usidiliki kunisimamisha wakati naongea mimi na wazee waliokufa ndio tulikubali wewe uwe kiongozi...sasa kuwa na adabu sawa..." Ilimbidi SEMENI awe mpole ili aishi na watu na kumuacha mzee huyo nuksi akiongea vitu vikavu.

    "Sasa...fahamu kuwa siku zinaisha hapa hakuna furaha zaidi ya kupumbazana tu...kama mnabisha mimi nawafahamu wote ambao walimuua sikitu mtoto wa chito na kumuua mwanangu mpaka sasa wamenibakishia mjukuu wangu basi...nitajeee?" Watu waliona kama maajabu ndipo wakasema kuwa " Mtajeeee?......"

    "Hapana siwezi kumtaja naamini wao wenyewe watajionea na watapata adhabu kubwa sana mbele..." Aliondoka na kuelekea nymbani kwake na kuwaacha pale wakiwa hoi hawafahamu nini kimekuwa ni nini?. siku ilikuwa imetimu kuisha na usiku ulishaanza kuingia wazee hao wawili walikuwa na mawazo kwa kila mmoja japo mipango yao ilionekana kufikia mwisho lakini inagonga mwamba baada ya mzee Manyenye ambae wanajua hawawezi hata kumuingia. Majira kama ya saa nane usiku anaonekana mwanamke akiwa anatembea kwa mwendo wa maringo sana huku akiwa kashika kitu ambacho hakikujulikana kwa haraka, mwendo wake ulionekana kuelekea kwenye nyumba ya mzee Sikujua, alipofika kwenye nyumba hiyo aliizunguka kama dakika kadhaa kisha akafika mlangoni, alionekana kutoa kitu ambacho kilifanana na kibuyu hivi alionekana akiingiza mkono ndani ya kibuyu hiko na kupaka kwenye mlango wa mzee huyo, Ilikuwa ni damu ambayo haikujulikana kaitoa wapi. Alama aliyoichora hapo ilikuwa ni X ambayo ilikuwa imekorezwa vyema sana, baada ya hapo aliweza kurudi kule ambako katokea. Pia kwa mzee Mapato akiwa kalala alishtuka sana na kuamka "Mh! hii ndoto mbona inanitishia hivi ngoja ifike asubuhi nikamueleze bwana sikujua ila mh! mbona yale maneno ya Manyenye yanaendana na hii ndoto?. Aliendelea kulala.

    Asubuhi na mapema sana mzee Sikujua aliamka kama kawaida yake alichukua kiti ili aende kuotea jua la asubuhi alipofungua mlango anataka kuufunga baada ya kugeuka nyuma anashtuka na stuli aliyoichukua ilimdondoka chini "Khaaa! hii si uchuro huu jamani watu wananitaka nini mimi eeeh! wakati tumeshatoka kwa mwenyekiti na kusema hatutaki hata kutishiana vifo damu hii imekuja fanya nini na nani kaiweka ?".Alipatwa na bumbuwazi la ghafla sana wakati huohuo mzee mapato anaingia pale anamkuta mwenzake akiwa haamini. " Vipi tena bwana sikujua?" Mapato aliuliza "Ahhh! bwana jionee nimeamka asubuhi nakuta hapa kuna damu sasa sijui hata nani kaweka na akiwa na nia gani!". "Yerewiiiiiiii.....haaa ndio hayahaya niliyoyaota usiku jamani tumekwisha kabisa"> Mapato na yeye alikuwa na yake hapo kwa kushangaa "Una maana gani kusema hivyo?"



    "Sikujua nimelala usiku nikaota kuwa tupo milimani ambako kuna maporomoko makubwa sana sasa tukashangaa maji wakati yanatoka milimani kama kawaida sasa yanaanza kurudi kutoka bondeni na yanapandisha mlima...kwa kuwa nina ujuzi wa kutabiri angalau ndoto...nikaona kuwa mambo yanatubadilikia tena sio kidogo makubwa kabisa yani...kuona hilo sio tabu nadhani uliyoyafanya kwa SIKITU yanakurudia na si wewe tu hata mimi....cha kufanya hapa kesho ni kukimbia tu hatuna jinsi tena."



    Maneno ambayo hayakuwa na kipingamizi kabisa. walikubaliana na swala la wao kesho yake ambayo ni siku ya pili kuondoka pale. Taarifa hiyo ilifika kwa mwenyekiti na kila mwanakijiji aliipata kwa huzuni sana kuwa yuko hatarini kuuliwa kwa wale ambao walitafsiri. Upande wa Sikitu na wengine walikuwa wamemkamata sungura kama watatu wakimfanyia utaraibu huku baba yake chito alimuuliza swali " Mwanangu, usiku jana muda flani sijakuona uliena wapi mana sikuwa na usingizi mkubwa nilikuwa nawaangalia nyinyi tu.." Chito aliuliza baada ya kuhisi kutowepo mwanae.

    "Hapana baba nilienda mbali kidogo kujisaidia haja kubwa" " Sawa lakini usijalibu kutoka peke yako mana usije kukamatwa na wanyama wakali.".

    Majira ya usiku kama kawaida, usingizi ulivyowachukua watu wa Bwawani alionekana binti yule tena asiyejulikana hata kwa jina. Alifikia kwenye ile nyumba alichoamua kushika kile kitasa kwa makini sana hatimae muda mchache sana mlango ulifunguka kumbuka kuwa Sikitu ana nguvu ambazo ziliweza kuwasaidia sana watu wa Chamlo kwa hiyo kwa hili kwake ilikuwa dogo sana.

    Aliingia ndani humo akamkuta mzee huyo akiwa kalala fofofo, alichoamua kutoa kibuyu chake na kutoa unga ambao alimpulizia puani ulikuwa kama madawa ya usingizi kwa Sikujua alionekana kuangusha kichwa kuonyesha hata kama alikuwa anaweza kuamka akishikwa kwa hapo hatoweza tena. Aalimfungua nguo ambazo alikuwa kavaa alimuacha uchi kabisa kama alivyozaliwa. Kwa binti huyo hakujali kumvunjia heshima mzee huyo haikujulikana kwa nini anafanya hivyo na ana nia gani baada ya hapo.

    Alichukua tena dawa kisha akampaka kwenye sehemu zake zote za siri kisha akamvalisha na yeye akaondoka zake. Kama kawaida bwana Mapato asubuhi mapema huwa anakuja kwa rafiki yake Alishangaa sana kuona mpaka muda ule bwana yule hajaamka na si kawaida yake kabisa. "Bwana huyu kanywa pombe nyingi sana jana mbona mpaka sasa ajaamka?" Aliingia ndani na kumkuta kweli akiwa kalala, alimuamsha kwa haraka ndipo na yeye akajikuta anakurupuka. "sikujua mbona mpaka sasa hivi nini unaumwa au". Sikujua anashangaa kama anahisi mabadiliko yametokea ndani ya mwili wake, aliingiza mkono wake huku akitoa macho kama panya kabanwa kwenye mlango "sikujua vipiwe mtu mzima bwana unashikaje huko..."

    "Mamaaaaaaa.....yanguuuu sio yangu hiiiii aah haaa sio yanguuu jamaniiii..." Mapato alishangaa sio yangu vipi tena kila akimtuliza sikujua haelewi kabisa sauti alizokuwa akizitoa zilikuwa kubwa sana sio yanguuuu... ilibidi ampige na kofi kali amtulize "Mzee mjinga wee sio yangu sio yangu nini mbona hueleweki eeeh". Watu waliokuwa wanapita walisikia hayo maneno waliyokuwa wanaongeailionekana kama ugomvi..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mapato ona sio yangu jamani yangu imekwenda wapi aaaah!..." Alivua nguo zake na kumuonyesha uchi wake na kuona uko wa jinsia ya kike tofauti na yake mwenyewe. "Mamaa yangu haya sasa mengine kabisa sikujua tumekwisha kabisa sasa hivi..".

    Ghafla watu walijaa kwa wingi na hakuwa mbishi aliwaonyesha watu jinsi ilivyo kwa hekma na busara mzee Manyenye aliomba asifanye hivyo kwa walio ona inatosha utakuwa unadhalilisha wengine. cha kufanya kutulia kujua nini kimefanyika. Walimuita Mzee Manuali ili asaidie kwani na yeye anayajua yale mambo kidogo. Baada ya kufika waliingia ndani alikuwa Mapato, susu,mwenyekiti, manyenye na sikujua mwenyewe wengine wakitaka kusubiri majibu hasa Ndunya, wakiwa ndani na muda huo jua likizama na sikitu wanasubiri siku ijayo waingie kijijini. "aaah katika kupiga mambo hapa naomba useme ukweli mana hili sio tatizo dogo dawa yake kusema yale uliyoyafanya inaonekana kama hii ni laana"> Mapato alimfinya sikujua asiseme chochote, Lakini sikujua aliona ni kitu cha kijinga kubaki vile basi alivyoamua kusema ukweli tu. walitoka nje hadi uwanjani na kusimama katikati ili aseme kile ambacho alikuwa nacho kutoka moyoni. Alikuja mwenyekiti na kusema haifai kwa wakti ule bado wakishindwa ndipo aseme.

    Ilishindikana kusema lolote,

    Usiku wa kuamkia siku nyingine Binti yuleyule alikwenda kwenye nyumba ya mzee Mapato na kwa mzee huyo alimfanyia yale ambayo kamfanyia mzee Sikujua. wakati anafanya juhudi ya kuondoka kwa bahati mbaya hali yake inakuwa mbaya anazidiwa na kuanguka chini, asubuhi watu walimshangaa kumuona binti aliyefanana na sikitu hakika walikimbia sana kwani walijua kama ni mzimu. Hatimae walimshika baada ya kuhakikisha kuwa ndie yeye. wakati huohuo Mwalami alifika kwa kuwa yeye hafahamiki akiwa na katunje wanashuhudia sikitu akipelekwa kwa mwenyekiti walirudi kwenda kuwaita wale waliokuwa kule polini. hakika walifika wote kwa pamoja na ndipo kila mwanakijiji alishindwa kuamini kama kweli sikitu mtoto wa chito au Mambo Sasa wapo pale. Ilibidi mambo yaghailishwe na wapewe nafasi baada ya kupewa na fasi iliyoombwa na mzee Chito. Haikujulikana hali ya Mapato ikoje mana mpaka muda ule hakuamka na sikujua kajifungia ndani kwa aibu aliyoipata. Kila mmoja pale alikuwa hoi na haamini iliwafanya kuambizana kila mmoja na eneo hilo walifurika watu shinda hata siku zote ambazo walikuwa wanaitwa na kuja pale.

    Sikitu alikuwa na hasira sana, huku mzee Manyenye alimuendea chito na kuongelea nae baadhi ya maneno fulani ambayo hayakusikika kwa baadhi ya watu.

    "Haya katika mambo ya maajabu ndani ya kijiji hiki pamoja na la leo hili, Huyu sikitu tulishajua kuwa kafariki na leo anaonekana....sina mengi mana leo najua yatatokea makubwa sana haya karibu mzee manyenye." Mwenyekiti alimkaribisha Mzee Manyenye.

    "Jamani msishangae kwani mwanzo nilishawaambia kuwa siku ipo kila kitu kitajulikana na niliongea jana tu ila leo hii tunaona sasa mzee Chito au Mzee MAMBO SASA karibu sanaa...". Kwa kuwa palikuwa na heshima zake walitulia na mzee chito akaenda mbele ya watu hao. wengi wao walikuwa wanamuangalia Sikitu hawaamini jinsi sasa alivyokuwa na kuwa mrembo sana.

    "Nashukuru sana Mzee wa kijiji Manyenye, nashukuru sana mwenyekiti Semeni, nashukuru sana Mzee MANUALI kama yupo.." "Hayupo kuna tatizo limejitokeza ila muda mfupi anakuja endelea" Manyenye alimuambia. "Sawa ...Mwenyekiti unakumbuka ulimfukuza kijana huyu mbele yako miaka michache iliyopita?...huyu ni KATUNJE..ndugu yangu mimi aliyenipotea kwa miaka mingi na tukaonana, nililalamika sana kuwa mwanangu kapotea hatukujua wapi kaenda kweli ama si kweli?"

    "kweliiiiiiiiii...iiiii.." "Nyamazeni sasa nampa nafasi mwanangu sikitu aseme kila kitu". Watu walizidi kunong`ona huku wakimsubiri sikitu akiwa anapanda pale alipoitwa. "Nawashabahi nyoote..Kabla hata sijaongea chochote nawataka wafuatao waje mbele yangu ambao ni SIKUJUA na MAPATO nawatakaa waje haraka sanaaa" Alikuwa analia sana huku akiwa analia kwa uchungu.

    Watu kama kawaida kwenye mambo kama hayo huwa hawachelewi, vijana kadhaa walitoka na kwenda kuwafuata hukohuko waliko, akiwemo na kijana Ndunya alikwenda kwa mzee Sikujua ambako anafika tu anakutana na sauti za vilio vya bwana huyo akiwa na bwana Manuali akiwa anamtuliza bila kujua kuwa yeye anahitajika sana. "Mzee sikujua fanya haraka sana unahitajika na mwenyekiti kuna mkutano wa ghafla kule". Alishtuka kidogo hata hivyo mzee manuali alimnyanyua huku akiendelea kumtuliza. Wengine walifika kwa mzee Mapato ambako walimkuta akitaka kujinyonga kwa ile hali aliyonayo kwani na yeye jinsia yake ilibadilika. Walimuondoa kwenye kitanzi na kuondoka nae hadi kule kwenye kikao. Sikujua alikuwa hoi na tumbo kuwa na joto baada ya kumuona Sikitu akiwa mbele yake. Sikitu aliendelea kusema. "Nashukuru kama mmefika hapa. "

    "Mzee sikujua nataka uje useme upuuzi wote uliofanya..je mzee huna mjukuu kama mimi unadiliki kutaka kuniua unanibaka sikujua kwa kudanganya utamsaidia baba yangu...mnashirikiana kumdhulumu baba yangu mnanitupa polini aaaah jamaniiiiii utu wako uko wapi jamani...hakika kama hukusema chochote nakuua sikujuaaaaaaa..." Alianguka chini kwa hasira ambazo zilimpelekea kuzimia..........

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    .Ndani ya kijiji cha SHISHIMO mambo hayakuwa mazuri sana wakati huohuo watu wamechanganyikiwa ndani ya kijiji cha BWAWANI. Watu walionekana kuwa na hasira sana kwa kuhisi jambo ambalo kila mmoja hakutaka kulisikia bila kumuadhibu kabisa yule msemaji. Wachache walienda kumpulizia SIKITU baada ya kupoteza fahamu, akili ya mzee chito ilihama kabisa pale na kuwaangalia sana wale wazee waliofika ambao nao walikuwa wanaficha sura zao kwa aibu ambazo walikuwa wanaziona.

    Mzee SIKUJUA alipanda kwa woga wote lakini vijana walimpeleka kwa nguvu zote hadi alipofika pale juu. Mzee huyo alibaki kulia kama mtoto mdogo mbele za wanakijiji ambao walikuwa tayari kumsubiri kwa hamu atoe kile ambacho kaambiwa aseme. Aliendelea kulia lakini njia ambayo aliiona kuwa itamsaidia basi alivua suruali yake na kubaki uchi wa unyama lengo aonyeshe zile nyeti zake ambazo zimebadilika. watu wakubwa kwa watoto walifumba macho kutohitaji kuona yale ambayo anayafanya bwana huyo.

    Njia hiyo ilimsaidia sana pamoja na rafiki yake MAPATO kwani walikimbia ovyo, walishindwa kuwakimbiza kwani walibaki kuwacheka japo ndani yake waligundua mambo fulani. Muda ulipita walikutana baadhi ya wazee wakiwemo bwana MANUALI, MWALAMI, CHITO, KATUNJE, SEMENI na MANYENYE. Wakati wanawake waliwaandaa wale wageni wawili yani Sikitu na Mwana mahala pa kupumzikia kutokana na hali ya sikitu. Huku wazee hao walizidi kuongea ndipo mambo mengine yaliibuka baada ya bwana Mwalami wa Chamlo kumgundua kuwa Manuali wa bwawani ni ndugu yake wa damu. jambo hilo lilikuja baada ya kueleza historia nzima ya chito na katunje, katunje na Sikitu, chito na sikitu ndipo mzee mwalami akaingizia yake hapo ndipo hata mzee Manuali alifahamu kuwa ndie kaka yake kabisa ambao waliachana miaka mingi iliyopita.

    Kila mmoja alifurahi sana walikumbatiana, kwa hiyo sasa ikawa mzee mwalami si mgeni tena pale na alichukua jukumu la kumlea Mwana ambae na yeye alikimbia pamoja nao, "Ndugu zangu nawashukuru sana kwa kunisaidia kumpata ndugu yangu..alafuuu yule binti kwa kuwa kijana hapa hana mtu anaweza akaelewanan nae akamuoa kabisa Mwana" walicheka baada ya kuingizia yale maswala. Majira ya usiku na wahenga wanasema kuwa usiku ni mrefu sana hivyo akili ya SIKITU haikuridhika kuwaacha wazima wale watu ndipo alipowalaza fofofo wale aliokuwa nao karibu na yeye akaelekea kumsaka mmoja hadi mwingine.

    Kwa bahati yake alifika kwenye nyumba ya mzee Sikujua alifungua mlango japo walijitahidi kuubana aliwakuta wakiwa wote wamelala, binti huyo mzuri wa moyo aliununua ukatili wa ghafla kabisa ndipo akamkata kisu cha shingo kila mmoja na hapohapo akasababisha vifo vyao, damu iliyomwagika kwa haraka zaidi ikiruka kutoka kwenye miili yao ilimfikia japo hakujali zaidi. Kwa unyama alioufanya ule mwili wake ulisisimka kuwaona wale watu awahemi tena, alijiuliza mara mbilimbili kuwa kama kweli wamekufa.

    Uoga aliokuwa nao alijishtukia jogoo linawika na yeye hajatoka mule ndani, wakati huohuo usiku walikuwa wanamtafuta baada ya kugundua kuwa SIKITU katoroka au kakamatwa kwa awamu nyingine kama mwanzo. juhudi zao zilizaa matunda baada ya kumuona asubuhi hiyo binti huyo kwenye nyumba ya Mzee sikujua, akiwa nje ya nyumba kwenye mlango akihema huku akiwa ameshikilia kisu chake na mkono ukitetemeka. Watu ilibidi wamuogope na wasimsogelee kabisa kwani alionekana si mtu wa kawaida. Baba yake na Katunje pia walikuja. CHITO ambae ni baba yake alishika kichwa chake kwa mikono miwili.

    "Mwanangu sikitu umefanya nini tena, mamaaa nini umefanya huko ndani..." Sikitu alianza kuangua kilio cha uchungu sana alianza kujongea pale walipo watu ndipo walianza kumkimbia, wengine wali[pata nafasi ya kwenda kuangalia ndani nini kakifanya. Ripoti ilifika kuonyesha kuwa wale wazee wakufa "Aaaah hakika huyu mwanamke ni muuaji kabisa kawachinja kabisa wote yani kwishaaaaaaa woteee.....". Kila mmoja alibaki na majonzi mazito, vijana walinda ulinzi kama sungusungu wa pale walimkamata kwa umaridadi mkubwa na kumpeleka eneo husika ambako huwa wanafungwa watu kama hao.

    Chito, Manuali, mwalami, katunje waliingilia kati lile swala kuwa wampe nafasi aseme kwanza "Hatuwezi kumkamata sawa hata kama kafanya mauaji, tumsikilize maelezo yake ndio ambayo yatamfunga au kumuacha huru huyu mtuhumwa.." Maelezo ya mzee Manuali yalitia moyo na kupunguza jazba ya watu waliokuwa pale. SIKITU alipandishwa kwenye eneo ambalo kila mmoja alikuwa anaweza kumuona lengo la kufanya hivyo ili aseme kwa nini kaua watu wale tena kwachinja kama kuku.

    "Haya mimi kama mwenyekiti, nakuomba utueleze hapa mana tuna kesi nyingi za mauaji na leo wewe umezifanya dhahiri kabisa tena mwanamke..." Sikitu hakuogopa jambo mana aliamua lolote liwe kwa muda ule ila dhamira yake imetimia."Sawa...nakumbuka kipindi baba yangu anataka kunisomesha, alinunua mikorosho kwa mzee Sikujua.lakini mzee huyo alimsaliti baba kwa kumuibia mikorosho akiwemo na huyu mwenyekiti..." Mwenyekiti aliposiikia katajwa aliruka kwanza toka pale alipo "Weeee....kwangu alikuja na ushahidi sikumdhurumu kabisa mimi tafadhali..alafu ongea vitu vyenye ushahidi..."

    "Pia..baada ya hapo...mzee sikujua alinitaka mimi niende kwake, ili nikachukue ujumbe ambao alitaka kumpa baba kwa kuwa waligombana...Baba na mama walienda kwa Mapato..mimi nikaenda kwa sikujua..mzee huyu aliniingiza ndani..akaniziba mdomo sikuweza kutoa sauti ndipo akaniingiliaaaa.....aaaah mamaaaaa..." Sikitu alianza kulia huku akiongea kwa kwikwi..watu walimsaidia kulia kwa kuwa iliwauma pia kwa yale ambayo kafanyiwa. Ndipo walimbembeleza ili aendelee.

    "..Nilipoteza fahamu kwa kuwa alihalibu usichana wangu nikiwa bado mdogo,...nilizimia sikujua nini kinaendelea..nakumbuka niliamka nilijikuta niko kwenye tenga ambapo mimi nimefunikwa na kiloba.nilijitahidi nikatoka..nguvu sikuwa nazo njaa ilinikuta, mwishowe nilizimia tena...Fahamu yangu ilirudi najikuta niko bwawani..sikujua nani ambae kanipeleka kule..lakini nikashukuru Mtu akaja kuniokoa akanitibia nikamfahamu kama Katunje..mika ilipita alipambana kuwazuia wale watu waliokuwa na nia kama Sikujua..hatimae nilipatwa na ajali mtu alinikimbiza kunifanyia mabaya nikakimbia nikaangukia korongoni...sikuumia..niliokotwa hadi kijiji kingine ambako wamenisaidia pia mpaka baba leo niko nae, sikuona umuhimu wa kuwaacha hawa wazee wawili wanaoshirikiana kuharibu ndoto za watu...."

    Maelezo hayo aliyoyatoa yaliwafungua bongo watu, kiasi kwamba hata mzee Manyenye alikuja kusema swala la SUSU na Mama MENGI yaliyowatokea. Mpaka hapo walimtuliza na wao wakazika wale watu. Baada ya siku kadhaa familia ya Chito akiwa na mwanae na nduguye walikaa pamoja, lakini tatizo lilikuja kwa Sikitu "Babaa...nimevumilia sana nimechoka.." "Nini tena mwanangu ulichochoka.." Baba aliuliza

    "Nataka kujua mama yangu yuko wapi la sivyo najiua kesho hutoniona mzima..." Aliongea kwa jazba mpaka katunje na Chito waliogopa, Ilibidi wamsimulie ukweli kabisa halisi ambao ulihitajika. Majonzi yaliendelea kutokatika na yalifanya kama ndio nyumbani kwake humo. "Baba asikubali aliyesababisha kupotea kwangu na maisha yangu kuwa magumu sikumuacha hai.. iweje huyu aliyempoteza mama yangu nimuache naomba kesho tuende hukohuko kwa babau la sivyo hutoniona ni bora na mimi akaniue na si kubaki hali mama yangu kafa".

    Hakika ilikuwa kasheshe yani SIKITU kachachamaa hataki ujinga tena. hali mama yake hamuoni.

    Ndani ya kijiji cha SHISHIMO, mambo yalicharuka baada ya kijiji kuwaka moto. ulionekana upepo mkubwa ukivuma maeneo karibia yote jambo ambalo lilifanya kila mwanakijiji ajiulize kulikoni kwa siku ya leo. Kwa bahati mbaya zaidi kuwa watu walionekana kufa baadhi yao miili yao ikiwa imeanza kutapakaa zaidi na zaidi. Nyumbani kwa mzee MAMBO SASA akiwa na NYANDU walikuwa wanaendelea kuimba nyimbo za kichawi, khafla alijitokeza mtu asiyejulikana wa aiana gani mana yuko mwenye shepu tofauti na binaadamu wa kawaida. Baada ya kukaribishwa ndipo akarudi kwenye umbo lake la kawaida.

    "VIJANA....NIMEWATUMA KAZI HAMTAKI KUFANIKISHA SASA NITAUA KILA MWANAKIJIJI WA HAPA.KAMA HAMUMLETI SIKITU NAUA KILA MMOJA..TAARIFA NAWAPENI FUNGENI SAFARI MKANILETEE SIKITU KABLA HAJAFIKA KWENYE ARDHI HII.." Jitu hilo lilondoka kimiujiza huku akiwaacha wale watu wawili wakiwa wanaduwaa hawajui nini waseme hata. "Umejua ana maanisha nini?" Nyandu aliuliza "Hapana" "Anamaanisha kuwa SIKITU huyo anayemuhitaji umtoe kafara..yuko njiani yani karibu kuja hapa sasa tujipange leoleo tuangaze anga lote tutazame anakuja kupitia wapi.

    Kweli Bila wao kufahamu kuwa sikitu sasa ni mtu mwingine kabisa kaja kwa njia ya kumaliza upuuzi wote, usiku kama walivyoahidiana walijipanga kutazama kila baadhi ya vijiji ambavyo walihisi kuwa atakuwa karibu, safari yao ilianza ndani ya kijiji cha KALULU, ambako hawakufanikiwa kuona kitu Waliongoza kwenye kijiji cha MIPINGONI ambako nako walikosa lakini kumbe mzee UPENGO alishawaona wakiwa kwenye rada hizo, alitikisa kichwa huku akionyesha kuwa ytuko tayari "Hawa wachawi wanapita anga zangu wananitafuta, huku kuna nini mpaka waje ngoja sasa niwaendee kulekule kesho pumbavu zao.."

    Walirudi wakasafiri ndani ya kijiji cha bwawani ambako waliona dalili nyingi za kuwepo sikitu, walirudi baada ya kujua kuwa kweli wanahitaji njia ya kumzuia kisha wamkamate akiwa nje ya kijiji hiko. Asubuhi ambayo ilisemwa familia ya watu watatu waliondoka Bwawani bila kutoa taarifa na kuja kwa baba yao, ambae kawaandalia chai ya asubuhi yenye maumivu. daaah kweli mchawi hana huruma. Wanaingia ndani ya kijiji hiko tu Sikitu anapata wasiwasi na katunje nae dawa yake inambana kuhashiria kuwa kuna hatari kubwa mbele yao.

    Sikitu hakuogopa alipita na kila alipopita ilionekana kuvunjwa kwa ngome ya kichawi iliyowekwa na babu yake. Mzee Mambo sasa alishtushwa kuona ugeni mkubwa hasa kijana Katunje kwa kuwa miaka mingi hakumuona. Mzee alikuwa mstaarabu wa usoni alivyoona kuwa mambo magumu alimkimbilia na kutaka kumkumbatia, katunje alimsukuma kama si baba yake wa kumzaa. "Mwanagu ulikuwa wapi mwenzako nilikuwa nakutafutaaa nilimtuma kaka yako aje kukufuata huyo kweli mnapendana eheee huyu ndio SIKITU..Sikituuu..sikituuuuuuu" Neno hilo lililtia shaka mpaka ilikuwa inasoma mara kwa mara kwenye vichwa vya watu.

    "Weee baba mnafiki, mchawi, muuaji hupaswi hata kuonekana...wee baba nimesikia umemuua mama yangu na ukatulisha nyama yake, hukutosheka ukamuua mkweo ukataka kumlisha nyama kaka ona sasa huyu mwanae analelewa na nani na anamtaka mama yake...mimi ndio maana niliondoka mapema sana sikutaka kuoan haya mambo yako..." "Wee keleleeee pumbavu huna adabu mmekuwa sasa hivi ngoja niwaonyeshe mana mnanipanda kichwani........." Alianza kuimba na kupuliza filimbi yake mla Nyandu akaja akawashika kiurahisia sana na wakaingizwa ndani mwake.

    "Mambo sasa haya tumewashika, tumuite Nyamnyena aje kumchukua sikitu...". Hakumaliza hata kusema lolote mshale ambao haukujulikana unatokea wapi, ulisiganisha mbavu za Nyandu kuanzia upoande wa kushoto hadi wa kulia., Palepale alidondoka. Mambo sasa alibaki kutoamini kabisa. alitaka kukimbia mara mzee upengo akamkamata "Unaenda wapi wakati nilimtuma mwanao aje kukupa taarifa kuwa siku yeyote nakuja kukusalimia sasa unataka kunikimbia jamani kweli urafiki gani huuu..."

    ".....Rafiki hawa si watoto wako kwa nini unadiriki kuwafanyia hivi huoni hata huruma kabisa ebu badilika najua rafiki yako alikuwa anakudanganya wewe ni mtu mzuri sana bwana....haya ebu kunywa hii dawa kwanza.." Alitoa kibuyu akampatia mzee huyo anywe.

    "Ukinywa hiyo inakuondoa ujinga wako wote sasa na hilo nyamnyena lenu nitalivunja sasa wewe kunywa. "

    "..Hata kama nikinywa niliyoyafanya sipaswi kusamehewa..ni bora ukaniua mape,a mana nahofia kuteseka na kuwaona watoto zangu wakiniona mbaya niliyebadilika..."

    "Babaaaa kunywa ile si akili yako baba kunywaaaa haraka..." Kipindi hiko mingurumo kama ya simba hivi ikiendelea ndani humo nayo ikisema "MAMBO SASA UNATAKA KUTUSALITI...HAKIKA USINYWE HIYO DAWA AHADI YETU WEWE NI KUWA MFALME WA DUNIA SASA UKINYWA UTAWAUA WENGI KAMA NILIVYOKUAHIDI MWANZO..."

    Mzee huyo, alichanganyikiwa akifanya mkono wake utetemeke kwa nguvu sana chozi lilimtoka kwa wingi hajui nini afanye watoto wake pia wakiendelea kumsii baba yao anywe ile dawa aliyopewa.

    "Mambo sasa hatuitaji kukulazimisha kunywa hiyo kwa ridhaa yako...ila kumbuka kuwa wewe na mimi tulikuwa kitu kimoja..nikakuacha wewe huko uliko sasa kama unataka kuwa mfalme wa kichawi wamalize watoto wako alafu tuone nani ambae atakuwekea maji ya moto wakati wa baridi au ukiumwa....fikilia sana mimi sikutaka kukuua kwa kuwa watoto wako walikuja kuniomba ndio maana nilimuua huyu anayekushauri ujinga..."

    Kwa ujasiri uliokuwa mkubwa sana alikunywa ile dawa. Ndipo sauti ya lile shetani la kichawi lilipotamka "UNANIUAAAAAAaaaaa". Mwili wa mzee huyo ulitokwa na jasho alianguka chini huku akipupa pupa kama kuku ambae aliyechinjwa na kuachwa mara moja.

    Mwili wake ulijaa mavumbi mengi kwa kuwa ilikuwa kazi kubwa sana baada ya kunywa mzee wa watu alihangaika sana mpaka pale alipotulia, Mzee Upengo alimtikisa kumbe alikuwa kapoteza fahamu "Msijali atakuwa sawa tu akirudisha fahamu atakuwa vyema kabisa.."

    Walimshukuru sana mzee huyo ambae kaja kujitoa kwa ajili ya kumsaidia baba yao.





    Mzee Upemgo alisea kuwa mzee huyo atakuwa sawa endapo akizinduka muda wa hapo baadae. Kila mmoja alikuwa kimya sana kutazamia zaidi majira gani ambayo ataamka. Mzee Upengo aliwasihi mambo kadhaa ya kuyafanya kabla ya kuondoka.

    "Sasa mnatakiwa kuwa makini sana maana mizimu ya Nyamnyena itakuwa bado haijaishiwa nguvu na endapo wakija mimi nitapata taarifa nitakuja mara moja kuimalizia mbali....alafu huyu akiamka hapa atakuwa hana nguvu mtampikia uji mwingi sana ambao mtachanganya na hii dawa muhakikishe anakunywa sawa?" Waliitikia kwa pamoja wote watatu na mzee huyo muhimu kwa wakati huo akaondoka zake. Huku nyuma wakiwa wamebaki watu watatu yani Katunje Chito na Sikitu, walikaa kwa pamoja na kupanga kujua wanamsaidiaje zaidi. "Babaa haya mimi nahitajika kurudi kule ambako yuko mume wangu Bamuzi siwezi kukaa huku kipindi chote". Walimshangaa sana baada ya kutoa ile kauli "Khaah! mwanangu kumbe kule ulikuwa umeolewa yani bila hata taarifa ila haina shida utakaa na sisi kwa muda na tutakupeleka huko".

    Muda mchache walimsikia mzee Mambo sasa akiomba maji ya kunywa, roho zao zilifurahi sana kwani kila kitu waliona sasa kipo sawa bin sawia. "Mpeni maji huyo haraka sana " Katunje alikwenda kumpa maji ya kunywa alikunywa yote huku wakimuandalia uji kama maelezo yalivyotakikana. Waliweza kutia na ile dawa baada ya kumnywesha uji wote alidai mwingine walifanya hivyo kama mara tatu, hakika alipoteza nguvu sana. Siku ya pili Alikuja mzee Upengo pale na kujua maendeleo ya mgonjwa huyo.

    Kufika kwa bwana huyo Mzee Mambo sasa alijihisi huzuni sana na aibu kubwa kwani hata akili yake ilirudi ile ya zamani na kukumbuka yapi kayatenda. Machozi yalianza kumbubujika kwa wingi huku akiwaangalia wanawe ambao nao pia walikuwa wanamuangalia. Mzee huyo Upengo alikuja karibu na kuchutama na kumsalimia "Habari yako bwana wewe". Alikuwa anaulizwa lakini alibaki kulia tu, alimfuta chozi kisha akarudia kumuuliza kwa mara ya pili "Habari yako mzee Mambo sasa wewe ni rafiki yangu bwanaaa yaache yaliyopita" Aliitikia kwa kichwa ndipo mzee huyo akawaita wote na kuwapa maelekezo.

    'Naomba mnisikilize jambo liliobaki ni la huyu mzee kwenda kule ambako alikuwa anachukulia kazi yani kwenye mizimu yao akiwa peke yake akachome yale ambayo yeye aliandaliwa ili baadae awe kiongozi " Chito alidakia kumuuliza swali "Sasa hapo mzee huko hakutokuwa na shida akienda peke yake ?" Mzee upengo alikaa kimya kwa sekunde kadhaa "Ndio shida ipo sio kubwa sana ila lazima afanye hivyo kuokoa maisha ya hawa wengine sawa jamani?" Waliitikia lakini Mzee upengo alimuita Chito pembeni na kumuambia jambo ambalo alishtuka kiasi lakini alitulizwa kwa maneno ya hekima.

    Hayakujulikana ni aina gani ya maneno ambayo yeye kapewa. Mzee huyo alimuendea Mambo sasa na kumuambia maelezo yale aliyokuwa anayatoa pale kuwa kesho yake ajiandae na afanye kila njia achome hiyo mizigo haraka kisha arudi pale na atakuwa salama kabisa. Mzee Upengo aliondoka na kuwaacha wale wakiwa pale lakini Chito alionekana kulia lakini haikujulikana kwa nini yeye analia. Maandalizi ya kesho yake yalianza walimuandalia kifungua kinywa kama mzazi wao ndipo asubuhi hiyo anataka kuondoka lakini aliwaita wote akakaa nao chini akawaeleza jambo moja ambalo alikuwa nalo kabla hajaenda.

    "Wanangiu samahani sana nawaombeni samahani kwa yote niliyoyafanya bila hata kujielewa yani kwa tamaa ambayo ilinikuta. lakini mmefanya jitihada sana kuniondoa kwenye upuuzi ule..pia mimi nakili kweli nilishilikiana na rafiki yangu Nyandu kuwauwa watu tulianzia kwa wazazi wake, kwa mkewe na mimi nikamuua mama yenu..mpaka mkwe wangu mama wa mjukuu wangu Sikitu pia nilitumwa kumuua mjukuu wangu sikitu lakini ikashindikana. nawaombeni samahani sana jamani na nawahidi naenda kujitoa lazima nikafanikishe haya yote na sasa nawaacha kama sitorudi muwe radhi na mimi".

    Alimaliza na kuinuka na kuelekea njia ambayo inaelekea shambani kwake. Walibaki kulia tu na kuhuzunika sana kwa yale ambayo wanayaona na waliyasikia kwa macho yao. Hawakuwa na jinsi walimuombea tu baba yao arudi salama. Mzee Chito alibaki akiwa hana hili wala lile ndipo akapata wazo ambalo lilikuwa zuri sana "Sikitu na Katunje nawaomba niwaambie kitu mnisindikize kijiji cha KALULUL nimpeleke Sikitu akawaona babu zake na Bibi pamoja na ndugu wa upande wa mama yake.

    Sikitu alifurahi mno, Safari ilianza kuelekea kwa Wazazi wa Mama wa Sikitu. Safari yao ilichukua muda mrefu kidogo ndipo wanafika ndani ya kijiji hiko cha Kalulu. Wanafiuka kwenye nyumba ya Mzee SUEDI ambapo wanakaribishwa lakini mzee huyo alipowaona tu alikunja sura na kutaka kuufunga mlango wake. Chito aliushikilia na kumuomba kwanza wasikilizwe yapi ambayo anayo yeye na anataka kumueleza, Alikubaliana na yote lakini kwa shingo upande, waliitwa familia nzima wakakaa tayari kusikiliza maelekezo kutoka kwa bwana Chito na jopo lake, kwa kuwa yeye aliolea pale hivyo kiasi anajulikana.

    Alianza kwa kusema. "Nawaombeni radhi kwa kutokuja kutoa taarifa yoyote kuhusiana na mtoto wenu..lakini bila kuficha mengi yametokea yalikuwa ya kifamilia na niliogopa kuja kutoa ushahidi bila kuwa na ukweli wowote ule. Naumia sana pindi ninapowaona nyinyi wazazi na ndugu wa mke wangu na kuwaambieni kuwa mke wangu kafariki duniaaaa...." Walishtuka kwa pamoja na ndipo ugomvi ulianza watu wakisema haiwezekani na wanamtaka mtoto wao, Mwenyekiti alikuta ugomvi huo na ndipo alipoingilia na kuweka mambo sawa na kila mmoja akawa anasikiliza nani anasema kwa utaratibu.

    Lakini sasa kaniachia mtoto huyu hamkumfahamu anaitwa Sikitu tumepitia mengi lakini yalisababishwa na baba yangu mpaka sasa tumefanikiwa kumbadilisha, nimekuja kutoa taarifa na kuwaonyesha mtoto huyu na saa kiongozi ndani ya kijiji cha Chamlo kwa mfalme Ngololo na mtoto wake Bamuzi ndie aliyemuoa huyu.Walimpokea na hapo walikaa siku mbili baada ya kila kitu kuishakazi ambayo ilibaki ni kumrudisha Sikitu ndani ya kijiji cha Chamlo. Safari yao ilianza.

    Upande wa mzee Mambo sasa anafanikiwa kulipata furushi ambalo alielekezwa kulifanyia kazi, na hatimae analiunguza moto palepale lakini sasa kwa bahati mbaya siku si nzuri kwake moshi wa vitu hivyo vinamuathiri na kumteketeza kama vumbi na kupoteza maisha yake kabisa. Maisha ya Mzee Mambo sasa na mambo yake yote yanaishia palepale alipokuwa anachoma na inabaki stori tu kuwa alikuwapo mzee mambo sasa mwenye mambo ya kizamani.

    Safari ya watu hawa sasa ilianza kwenda kuelekea ndani ya kijiji cha Bwawani, ambako walipofika walipokelewa vyema sana kwa vishindo, Wanakijiji walikusanyana kwa pamoja na kuwapongeza kwa ushujaa wa kuwavumbua wabaya na hatimae walikufa kwa ubaya wao kweli mwisho wa zambi mauti, Mwenyekiti akiwa na jopo la watu wengine kama Manyenye walimuomba mzee chito abaki pale kwani wanampenda bado. Alichokisema bwana Chito kuwa bado wanasafari ndefu ambayo wakisharudi watarejea pale kwa maisha yao yote, Bwana Manuali, Susu, Mwalami na Mwana waliungana kwenye safari hiyo ya kurudi Chamlo.

    Walisindikizwa kwa ngoma za ushujaa ambazo zilichezwa na wanawake wazuri sana. Waliondoka hadi ndani ya kijiji cha Kilimalondo ambako walikutana na Mfalme SWAI akiwa na mtu wake wa karibu sana bwana KIMOLO, Mzee Manuali alishangaa sana pale kuukuta ufalme alifanya jitihada za kuwaeleza wanakijiji kuwa hakuna uongozi wa ufalme ambao unaleta mafanikio zaidi ya unyaunyasaji na kiongozi ambae hafai basi wao humuweka kwa kuwa huenda kwa kurithishana.

    Wanakijiji wa pale wote waliitwa na mzee huyo kutoka bwawani alisimama na kuongea nao.



    wananchi nawaomba, haya munielewe

    Hakika hapa nimetimba, Mengi kuwaelezea

    Matatizo mwayachimba, maovu kujiwekea

    Usasa unatupita, uzamani kuendekeza

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa anatumia mashaii kama moja ya lugha ambayo aliona kuwa itafaa zaidi katika kuelimisha, lakini sehemu yoyote lazima wabishi na wanaotaka kuelewa zaidi hutokea ndipo akajitokeza mwana mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mwaija kama tunamkumbuka alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa mama Mwaija aliyefariki.



    Ni mzuri wa kupaza, sauti kubwa mbele yetu

    Mbali sisi tumeanza, na swai ndio kauli yetu

    Usijaribu kutubeza, kwa haya mafanikio yetu

    Huna kitu cha kusema, wewe ni nani kwetu.



    Mzee swai alivyoona kuwa watu ni wabishi alitaka kuwaeleza zaidi lakini sikitu aliingilia kati na kuyaongea ya kwake mbele za watu wakubwa yeye akiwa mdogo mbele yao.



    Akina mama sikieni, Na wengine wakubwa pia

    Yaliyosemwa sikieni, Mabaya nimepitia

    Huo ufalme ebu acheni, mwenyekiti bora pia

    Kiongozi asipowapeni, yale mliyoambiwa

    Huna budi mtoeni, chagueni mwingine pia



    Wanakijiji wa pale walikuwa na vigelele vingi na uongozi wa mzee swai uliishia pale na wakamuweka mwenyekiti palepale na akaanza kazi. safari yao iliendelea kuelekea kwenye kijiji cha Chamlo, ambako huko kulikuwa na mtafaruku mkubwa sana juu ya swala la Bamuzi kutokuwa na amani kwa kuondoka kwa Sikitu. Waliendelea kumtafuta na kuwa na amani ya kuwa sikitu atakuja kurudi tena.

    Mama Naomi hakuendelea kuishi kwani tayari alikufa kutokana na presha na kukosea masharti kutoka kwenye ngome yao ya Nyamnyena. Siku iliyofuata waliingia kwa pamoja wote na furaha ilikuwa kubwa sana kurudi kwao. Hawakufikilia yale yote yaliyopita bali waliganga yale yanayoendelea nao pia walifanya kazi ya kuwashawishi sana wale watu na kiukweli walikubali na mwenyekiti alipatiwa bwana Bamuzi. Maisha yalikuwa mazuri Sikitu alibaki na Bamuzi wake ndani ya kijiji cha Chamlo. Katunje alimuoa Mwana na Mzee chito aliondoka akiwa na Katunje na Mwana kuelekea Bwawani, pia Mzee mwalami manuali na Susu walirudi Bwawani.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ***MWISHO***


0 comments:

Post a Comment

Blog