Search This Blog

NILIWAROGA WALIMU MPAKA BASI - 4

 






Simulizi : Niliwaroga Walimu Mpaka Basi
Sehemu Ya Nne (4)




 … “Ni huku mama, mahesabu yanasema hivyo,” nilimwambia mama naye akaniambia niende, nishughulike naye halafu mimi nimkute palepale aliposimama. Nilifanya mambo yangu, kufumba na kufumbua nilijikuta nipo kwenye kijumba kimoja cha ajabuajabu sana, mwanamke mmoja mtu mzima alisimama nje huku akisemasema maneno ambayo yaliashiria hakuwa na akili timamu. Nilimwamkia akawa anacheka ndipo nilipobaini ni kichaa. Nikajigeuza kurudi katika hali ya uchawi kwani mpaka namwamkia nilikuwa nimejibadili kuwa binadamu kama yeye. Niliingia ndani ya nyumba hiyo kwa ujasiri nikiamini ningemkuta Mwalimu Paschal. Nilipofika kwenye chumba kimoja nilikuta mtoto mdogo amelala, lakini pia dira yangu ya kichawi ikaonesha kwamba, Mwalimu Paschal hakuwepo ndani ya ile nyumba. Niliwaza kwenda kugombeshwa na mama kwa kushindwa kumpata mwalimu huyo. Nilitoka hadi kwenye mti mmoja, nikasimama hapo. Giza lilikuwa nene, hakukuwa na mlio wowote zaidi ya vijidudu vya usiku ambavyo milio yao huashiria eneo hilo kuna msitu jirani. Niliinua mkono juu, nikaita Mwalimu Paschal. Mwalimu Paschal. Nilitumbua macho nikitaraji kumwona mwalimu huyo akija juu angani na kutua miguuni pangu lakini wapi. Niliendelea kuita kwa zaidi ya mara sita, ya saba Mwalimu Paschal alitua miguu pangu akiwa amevaa bukta tu. Sikujua alitokea kwake au ndani ya nyumba ile lakini kama ni ndani ya nyumba ile mbona dira ilinikatalia hakuwepo! Nilinyoosha tena mkono juu nikaziita fimbo ambazo zilitua kwenye kiganja cha mkono wangu wa kulia. Palepale nilianza kumchapa mwalimu huyo kwa nguvu zangu zote huku nikimwambia: “Ni kwa nini unashabikia mambo yasiyokuhusu, ni kwa nini lakini na wewe ni mwalimu?” Mwalimu Paschal hakuwa akinijibu wala kujitetea kwa njia nyingine yoyote ile zaidi ya kujishika zile sehemu ambazo nilikuwa namchapa na fimbo. Nadhani alifanya vile kuondoa maumivu kidogo. Fimbo moja ilipokaribia kwisha na mwalimu wa watu alionesha kuchoka kupita kiasi ndipo nilipoamua kumwachia huku nikimwonea huruma. Nilisimama, nikanyoosha mkono wa kulia kuelekea juu, nikasema maneno yangu ya kichawi, Mwalimu Paschal akayeyuka kama barafu. Hapo ina maana alirudi nyumbani kwake, kama ni chumbani haya, kama ni sebuleni sawa. Nilirudi alipo mama, nikamkuta. Aliponiona tu aliangua kicheko cha nguvu huku akinyoosha mkono kunipa ili anipongeze. Na mimi nilimpa mkono wangu, mama akaniambia: “Wewe ni jasiri kuliko wanaume wachawi wanaojiita majasiri. Ulimpomkosa mwalimu nyumbani naona ukaamua kumleta palepale ulipokaa.” Hapa niseme kidogo. Kwa kawaida, wachawi hata wanapokuwa majumbani wamekaa, huwa wanaona mambo ya kichawi yanayofanywa na wenzao. Mfano, mchawi amekaa mahali akiendelea na shughuli zake nje ya uchawi, sasa kama kuna wachawi wanapita kwenda kuwanga mahali yeye anawaona na anajua ni wachawi, ila mwiko mkubwa kabisa hataweza kusema. Basi, baada ya hapo mimi na mama tulirejea nyumbani. Mama akasema nikalale yeye anakwenda kukutana na wenzake wachawi kwa ajili ya kwenda kuwanga au kuroga mahali kwingine. *** Ilikuwa asubuhi yenye wasiwasi mkubwa sana kwani ndani ya nafsi kama nilisikia nikijiambia mwenyewe kwamba Mwalimu Paschal alijua kila kitu. Kwamba alijua niliyempiga ni mimi. Nikataka nisiende shuleni ikabidi nimshirikishe mama, akaniambia nimuondolee ujinga wangu, akasema: “Toka lini umesikia hayo, mchawi amempiga mtu usiku halafu akamjua ni nani? Ikitokea hivyo labda huyo aliyepigwa pia ni mchawi na kama ni hivyo hataweza kupigwa.” Kidogo nilijisikia nafuu na amani ilirejea moyoni, nikajiandaa na kwenda shuleni. Nilikuta walimu wote, hadi mwalimu mkuu wamesimama nje ya ofisi, walionekana walikuwa katika mazungumzo mazito maana hata muda wa mstarini ulipofika, hakuna mwalimu aliyekuja kusema lolote na kwa kawaida lazima mwalimu mmoja aje na kusema kisha sisi wanafunzi tuingie madarasani. “Kiranja ingiza wanafunzi madarasani,” alisema mwalimu mkuu huku walimu wengine wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao. Tulikaa madarasani kwa saa tatu hakuna mwalimu aliyejitokeza kufundisha ndipo nilipoanza kuingiwa na wasiwasi kwamba huenda bomu la Mwalimu Paschal lilifika shuleni kwa walimu wenzake, moyoni nilijipa ujeuri na kusema kwamba endapo atatokea mwalimu wa kuchongachonga naye nitamfanyia stahiki yake kama Mwalimu Paschal. Siku hiyo pia Mwalimu Cecilia hakutokea shuleni na haikujulikana alikuwa akiendeleaje huko kwake. Mara kengele ya dharura iligongwa. Nasema ya dharura kwa sababu iligongwa kabla ya saa nne muda wa mapumziko. Wanafunzi wote tulikwenda mstarini. Cha ajabu, tuliwakuta walimu wote wameshasimama wakitusubiri sisi wanafunzi. Mwalimu mkuu alionesha ana hamu ya kutaka kuzungumza. “Nyamazeni kidogo,” alisema mwalimu mkuu maana wanafunzi tulikuwa tunaongeaongea sana. “Tumewaiteni kwa ajili ya dharura kubwa, Mwalimu Cecilia alipata matatizo ya kishirikina juzi usiku, aliingiliwa na wachawi, wakamtesa sana, wakampiga sana hivi tunavyoongea hali yake imekuwa mbaya zaidi amekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi. Lakini kabla la Mwalimu Cecilia halijakaa sawasawa, usiku wa kuamkia leo, Mwalimu Paschal naye...



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

 Amekumbwa na tatizo kama hilo, ameingiliwa, akapigwa sana huku akionywa eti aache tabia ya kimbelembele. Bahati nzuri, Mwalimu Paschal yeye anasema aliyemfanyia kitendo hicho kama anamjua ni mwanafunzi wa hapahapa tena ni wa kike ila ameomba apewe muda ili amkumbuke sawasawa.” Palepale niliinama kidogo nikashika tumbo, nikajibadili kuwa kiumbe mwingine, lakini mstarini nilibaki mimi kama mimi, nikatoka hadi nyumbani kwa njia ya kichawi. Nilimsimulia mama kinachoendelea shuleni. Mama bila kuchelewa, akanishika mkono tukafutika na kutua shuleni, mbele ya mwalimu mkuu, mama akamwekea mkono kwenye kichwa, mara mwalimu mkuu akabadili maneno, akasema: “Lakini hata hivyo mimi binafsi siamini uchawi. Nitamwambia Mwalimu Paschal aachane na mawazo hayo, kwani anaweza kusema ni mwanafunzi Fulani kumbe siye, ni ibilisi tu anataka kumgombanisha.” Niliwaona walimu wengine wakimkazia macho huku wakitingisha vichwa maana ilionesha mwalimu mkuu ametoa kauli ya kuwageuka. Baada ya hapo, mimi na mama tulifutika na kutua nyumbani kwa Mwalimu Paschal. Tulimkuta amekaa nje ya nyumba yake huku akijikanda kwa maji ya moto sehemu mbalimbali za mwili wake zilizokuwa zimevimba. Nilimwangalia mama ambaye naye aliniangalia mimi. Kwa pale, Mwalimu Paschal hakujua kama kuna ugeni umefika kwake. Mama alimshika kichwa na kukigeuzia juu, yaani akawa anaangalia juu bila ridhaa yake lakini haikuwa rahisi kwa yeye kujua kama anafanya kitendo hicho. Baada ya hapo, mama alimshika mkono na kumsimamisha, mwalimu akasimama wima kama mwanajeshi, lakini uso wake ulionesha anajisikia maumivu makali sana. Baada ya hapo alimshika na kumkalisha kwenye kiti, mwalimu akaa bila kupenda, ndipo alipoanza kusomewa mashitaka yake na mama. Alimwambia hivi: “Kama umekuja kwa lengo la kufundisha wanafunzi pale shuleni basi fuata hayo, kama umekuja kwa ajili ya kupambana utaondoka bado kijana mdogo. Wewe ni mtu wa kusema unamjua aliyekuchapa usiku? Unamjua ni nani? Hebu nitajie.” Mwalimu Paschal akiwa amekaa kwa unyonge alijishika kifuani na kusema: “Mimi kama nilimwona mwanafunzi wa shule ninayofundisha!” “Ulimwona wa kike au wa kiume?” “Wa kike.” “We mjinga nini? Sema ulimwona mwanafunzi wa kiume.” “Nilimwona mwanafunzi wa kiume.” “Ndiyo, ukiulizwa ujibu hivyohivyo, ulimwona mwanafunzi wa kiume.” “Nilimwona mwanafunzi wa kiume.” “Sawasawa.” Mara kwa mbali, watu wawili walikuwa wakija uelekeo wa pale kwa mwalimu. Mama akamshika kichwa Mwalimu Paschal kisha mkono mmoja akawanyooshea wale watu. Kidole kimoja ndicho kilichokuwa kimewanyookea zaidi wale watu, hivyo walitembea kwa kufuata maagizo ya kile kidole, yaani walikuwa wakienda jinsi kidole kinavyotaka. Walipita mbali na pale tulipokuwa tumesimama. Wakaingia kwenye uchochoro mmoja na kuendelea na safari lakini kiukweli haja yao ilikuwa kuja pale kwa mwalimu. Ghafla tena kwa mbali tuliwaona walimu, akiwemo mwalimu mkuu. Walikuwa wakija pale, mama akamwacha kumshika mwalimu, akanishika mimi na kusimama pembeni jirani kabisa na mlango mkubwa wa kuingilia ndani. Walimu walipofika walimsalimia mwenzao huku wakimpa pole. Wengine walimuuliza kama anawezahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kutembea, akasema anaweza ila si kama ilivyokuwa kabla hajapigwa. “Eti nasikia aliyekuchapa ni mwanafunzi, ni kweli?” mwalimu mkuu alimuuliza. “Ni kweli.” “Wa palepale shuleni kwetu?” “Ndiyo.” “Mwanamke mwanaume?” “Mimi niliyemwona ni mwanaume.” “Pole sana.” “Asante sana.” Aliposema aliyemwona ni mwanaume, nilimwangalia mama, akawa anatingisha kichwa kukubaliana na kauli ya mwalimu yule. Hapa napenda sana kusema machache kuhusu tabia hiyo. Wapo wachawi wana uwezo huo, wanaweza kukupa maelekezo ya cha kusema mahali na ukafanya hivyo bila ridhaa yako. Na unaweza kukuta mtu anatoa jibu fulani na watu wanashangaa, halafu baada ya hapo hata yeye mwenyewe anashangaa. Mambo haya hutumika zaidi katika mahakama. Wapo watu wana kesi mbaya na wanakwenda kwa waganga wakubwa wakifika kule wanapewa dawa ambazo zitamfanya aliyemshitaki kusema maneno ya kumshangaza hakimu na wasikilizaji wengine. Basi, wale walimu waliendelea kuwepo pale mpaka mimi nikakasirika. Nikawasogelea na kusimama usawa wao kisha nikawanyooshea kidole na kukielekeza kwingine, palepale waliaga na kuondoka. Mimi na mama tukamrudia Mwalimu Paschal. Safari hii mama aliniangalia mimi tu. Nilimwambia mwalimu kama atadiriki kwenda kwa waganga ili kuturoga sisi ataanza kufa yeye na ukoo wake wote. “Tena nakwambia, ulisikie vizuri, kama utakwenda kwa waganga, wewe na ukoo wako wote mtateketea.” “Sitakwenda kwa waganga.” “Niangalie vizuri.” Mwalimu Paschal alinitumbulia macho kuniangalia vizuri. “Mimi nani?” “Wewe?” “Mimi ndiyo.” “Weweee. Wewe sikujui.” Nilimgeukia mama huku nikihema kwa nguvu

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilijua angenitaja jina. Na kama ingetokea hivyo palepale ningempachika gonjwa baya ile afe na kupoteza ushahidi wa siku za baadaye. Baada ya hapo mimi na mama tulirudi nyumbani kwa njia ya kichawi. Lakini tulichofanya kabla ya kuondoka ni kumshika kichwa Mwalimu Paschal na kusema maneno ya kichawi kisha tulipomwachia alirejea katika hali yake ya kawaida na alionesha dalili kama aliyezinduka kutoka kwenye hali ambayo kwake hakuitambua. Nyumbani mimi sikukaa, nilikwenda shuleni ambapo nilikuta wenzangu wote wapo madarasani. Na mimi nilikwenda darasani kwangu, nikaenda kwenye kiti changu, nilimgusa yule mtu aliyenibadili naye akapotea nikakaa mimi. Hakuna aliyejua kama kulikuwa na binadamu feki ndani ya darasa kwani kila jambo lilikuwa likienda kama kawaida sanasana labda watu waliniona nimekuwa mpole sana siku hiyo kabla ya kurudi mimi mwenyewe. Mwalimu wa kipindi siku hiyo alikuwa mkali sana, sijui kwa nini. Na alikuwa miongoni mwa wale waliokuja kwa Mwalimu Paschal. “Sasa ni muda wa kujibu maswali kwa kila mwanafunzi mmoja mmoja atakayeshindwa nitamchapa viboko viwili, sawa?” Wanafunzi tukaitikia sawa. Alimsimamisha mwanafunzi wa kwanza, akapatia, akaja wa pili, akapatia, mimi nikawa wa saba na walionitangulia wote walipatia. Swali nililoulizwa mimi lilikuwa gumu sana, nikajua nitakosa, kabla ya kujibu nikapuliza upepo hewani. Mwalimu akawa kama anaweweseka. “Ngoja nikubadilishie swali wewe, ngoja kidogo. Halafu wewe! Lakini nadhani tuwe tumefikia mwisho wa maswali,” alisema yule mwalimu. Nilinyoosha mkono chini kwa chini, nikanyoosha kidole changu cha kulia na kuanza kukitembeza kutokea usawa wa pale aliposimama mwalimu na kuelekea mlangoni. Palepale mwalimu akachukua vitabu vyake na kuanza kuondoka. Wanafunzi wote walisimama, wengine wakawa wanacheza, wengine wanarukaruka, wako walionifuata na kuniuliza nilimfanya nini mwalimu yule mpaka akaamua kuondoka ghafla, sikuwajibu. Hatimaye darasa likawa kimya, kila mtu alikuwa amerudi kukaa akijisomea. Darasa nililokuwa nasoma mimi wanafunzi tulikuwa na uwezo wa kuwaona walimu wakiwa nje ya ofisi yao, hivyo nilikuwa nachungulia upande ule kila wakati kama nitaona jambo jipya. Mara mwalimu mkuu alitoka, akasimama akiwa amejishika kiuno. Alikuwa akiangalia upande wa darasani kwetu huku kama anazungumza. Ilionekana alikuwa akizungumza na walimu ambao walikuwa ndani ya ofisi yao. Mara walimu wengine watatu walitoka, wakasimama na mwalimu mkuu. Hapo mapigo ya moyo wangu yalianza kwenda kwa kasi, nilijua kuna jambo walimu wamelipata kutoka kwa walimu wenzao. Ghafla tena akatoka yule mwalimu aliyefungasha virago vyake, akasimama na wenzake, na yeye akawa anaongea. Sikujua nini kilikuwa kikiendelea, ghafla nikamwona mwalimu mkuu akianza kutembea kuja upande wa darasani kwetu, wenzake wakamfuata kwa nyuma, nikajua tatizo lipo kubwa sana, nilijiinamia kwa kuweka mikono kwenye dawati na kusema maneno fulani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Nyie walimu wanakuja, walimu wanakuja tulieni,” mwanafunzi mmoja anayeitwa Simon alisema kwa sauti ya chini kidogo. Na mimi nikainua uso. Mwalimu mkuu alizama ndani, walimu wengine na wao wakaingia huku wakiwa na nyuzo za hasira. Kilichonishangaza zaidi ni kwamba, walimu wote wakanitupia macho mimi jambo ambalo lilinikera sana, nikakielekeza kidole changu kimoja chini, halafu nikawa nakichezesha kama mkia wa ng’ombe vile, walimu wakatulia. “Lakini walimu wenzangu, hili jambo tuliangalie kwa umakini zaidi, mimi nadhani twendeni tukakae ofisini kwangu na kuzungumza kwa kirefu zaidi,” alisema mwalimu mkuu. Walimu wengine wakasikika wakiunga mkono huku yule aliyetoka darasani mwanzo kabisa akiwa ametangulia. Nilizama chini ya dawati, nikafumba macho kwa muda nilipofumbua nilibadilika na kuwa mtu mwingine mchawi, lakini pale kwenye dawati langu alibaki mimi wa asili ambapo hata wanafunzi wenzangu walijua mimi nipo. Nilitoka kwa mwendo wa polepole kuelekea mlango mkubwa huku miguu nikiirusha kwa juu. Kama wanafunzi wenzangu wangeniona nilivyokuwa kwa wakati ule wote wangekimbia nje kupitia madirishani. Nilitembea kichawi hadi ofisini kwa walimu. Walimu wote, hata wale ambao hawakuwa wamekuja na wenzao darasani walikuwa kwa mwalimu mkuu. Na mimi niliingia na kusimama pembeni wao wakiwa hawanioni. “Sasa walimu ni hivi, kinachoonekana ni kweli yule mwanafunzi anaweza kuwa na nguvu za kishirikina, lakini nina wasiwasi kwamba hata yeye mwenyewe hajui,” huyo aliyesema hayo alikuwa mwalimu mkuu. “Anajua bwana, huwezi kuwa mchawi au mshirikina halafu usijue kitu,” alidakia mwalimu mwingine. Yule mwalimu aliyedakia nilimnyooshea mkono lakini sikumgusa halafu nikafanya kama namkaba koo lake kwa nguvu. Alianza kujishika koo na kutaka kuongea lakini akawa anashindwa na maneno yakamtoka kama mtu aliyekabwa. Kila alipojitahidi kusema ndipo na mimi nilipozidisha kukaba hewa lakini kwake ilikuwa kazi, akatoa macho. Lengo langu ilikuwa nimtoe roho lakini nikasita, nilijua nitasababisha balaa kubwa shuleni na hata kwenye kile kitongoji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



… “Jamani ni nini hii?” aliuliza mwalimu mkuu huku akiwa anasimama na kumshika yule mwalimu niliyemtenda makuu. Alishindwa kusema, akabaki amejishika koo. Walimu wengine walisimama wakiwa wanamwangalia wasijue cha kufanya. “Mimi naona tumpelekeni hospitali,” alisema mwalimu mkuu. Hakuna mwalimu aliyeunga mkono wazo hilo zaidi ya mmoja wao kusema: “Hili kwa mtazamo wangu si tatizo la hospitali, labda tumpeleke tu kwa sababu sisi ni walimu.” “Sasa tumpeleke wapi akapate msaada?” mwalimu mkuu alihoji. Nilimtumbulia macho yule mwalimu niliyemtenda, tukawa kama tunaonana, yaani yeye alifanikiwa kuniona kwa macho yake mawili, akanyoosha mkono kama aliyetaka kusema: “Jamani huyu hapa ndiye mbaya wangu,” lakini nikampulizia upepo, akapitiwa na uwezo wa kuniona ukapotea. Niliamua kumsamehe kwa kushusha mkono na kuacha lile tendo la kama kumkaba. Mwalimu akarejea katika hali ya kawaida na kutulia, alijiachia, akakohoa sana na kupiga chafya. “Pole sana,” mwalimu mkuu alimwambia. Walimu wengine walimpa pole pia, akaitika asante huku akijishikashika sehemu mbalimbali za mwili kama anayelalamikia kwamba sehemu hizo ndizo zinazomuuma. “Kwa sasa unajisikiaje?” mwalimu mmoja aliuliza. “Kama nafuu, lakini nashangaa sana mwenzenu.” “Unashangaa nini?” “Kama nimemwona…” kabla hajamalizia kusema nilimpulizia tena upepo, akanyamaza. “Kama umemuona nani?” mwalimu mkuu alimuuliza tena. Palepale nilimnyooshea kidole mwalimu mkuu kama ninayemwonya kutojihusisha na masuala ya watu wengine, nikafanya kama namkaba koo, akakohoa ghafla, nikamwachia na yeye akatulia kimya. Mama alinifundisha kwamba ukitaka mtu unayemwangia asikukumbuke kabisa hata kama alikuona kwa bahati mbaya mfute uso kwa kiganja cha mkono wa kushoto. Na mimi nilifanya hivyohivyo, nilimfuata yule mwalimu nikamfuta uso kwa kiganja cha mkono wa kushoto. Wakati namfuta, alihisi anazibwa macho hivyo alishtuka na kupeleka mkono wake usoni kisha akafikicha macho. Nilipotoka kwa huyo nikamfuta mwalimu mkuu pia japokuwa yeye hakuwa ameniona hata mara moja, naye akapeleka mkono usoni kwa mshtuko na akasema:http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Khaa! Mbona kama macho hayaoni sawasawa?” “Ooo, kumbe yanaona bwana,” alisema akiwa amekaa. Ofisi ilikuwa kimya, walimu walikuwepo lakini hakuna aliyesema lolote, walikuwa wakimwangalia mwalimu niliyemtenda. Ilionekana kila mmoja amekuwa mwoga kutoa sauti akiamini atapata matatizo kama mwenzao na ndiyo maana mwalimu mmoja alisema tatizo la yule si la kulipeleka hospitalini. Nilitoka polepole huku nikiwasonya lakini hawakusikia. Nilirudi darasani, nikapita mpaka kwenye dawati langu na kujirudishia ubinadamu kisha nikakaa. Nilipokaa tu na yule niliyemwacha akiwa ameshapotea, mwanafunzi mmoja aliniuliza: “Hivi leo una nini wewe?” “Kwani vipi?” nilimuuliza kabla sijamjibu. “Umekuwa mpole muda mrefu.” Hapa nataka kuzungumza jambo moja ili watu wajue. Katika jamii tunamoishi haya mambo yapo, tena makubwa sana. Unaweza kukaa hata kwenye siti ya daladala na binadamu wa ajabu lakini ukawa hujui. Kinachotokea ni kwamba, mtu huyo anakuwa kama boya, mwenyewe halisi anakuwa katika kuwanga. Mfano mzuri kwenye daladala, mchawi anaweza akakaa na wewe siti moja, ghafla akataka kufanya mambo yake ndani ya daladala hilohilo ndipo anapoamua kumuweka binadamu wa uongo na yeye kuanza kuwanga. Sasa, mara nyingi kama mchawi huyo utakuwa unamfahamu, atabadili tabia. Atakuwa na hali ya kinyume na ile unayoijua, hasahasa wengi huwa wapole, wasiotaka kutoa sauti au kujisogezasogeza kutoka pale walipokaa. Basi, nilimjibu yule mwanafunzi kwamba, sikuwa najisikia vizuri lakini kwa wakati huu kidogo najihisi nafuu. Ghafla mwalimu mmoja anaitwa Msafiri aliingia na kusema: “Hamjambo wote?” “Hatujambo, shikamoo mwalimu,” tulimsalimia tukiwa tunasimama. “Marhaba, nimekuja badala ya mwalimu aliyetoka kwani hajisikii sawasawa. Pale alipoishia mimi nitaanzia pale, sawa?” “Sawa.” “Haya, kaeni.” Moyoni nilijiuliza, mwalimu huyo anamaanisha ataanza kwa kuuliza maswali kama mwalimu mwenzake au? “Nina maswali hapa, hata kama yalijibiwa lakini kwa mimi yataanza upya bila kujali yaliyopita.” Huyu mwalimu alionekana kuongea kwa ujasiri kama vile alishaambiwa kilichomtokea mwenzake yeye akasema hakitamtokea, maana alikuwa akitoa sauti nzito tofauti na kawaida yake. Kingine kilichonipa mawazo zaidi ni kwamba, wakati nilipoingia kule kwenye ofisi za walimu na kuwakuta wenzake wote, yeye hakuwepo. Wengine wote walikuwepo isipokuwa wale niliowachapa usiku, yaani Mwalimu Paschal na Mwalimu Cecilia ndiyo hawakuwepo. “Lakini tukubaliane, ukikosea swali viboko, hilo sitaki mtu abishe wala apinge, sihitaji mtu aseme sawasawa au si sawasawa.”
ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog