Search This Blog

NILIVYOKUTANA NA MZIMU FACEBOOK - 4

 






Simulizi : Nilivyokutana Na Mzimu Facebook

Sehemu Ya Nne (4)





Nilianza mahusiano ya kimapenzi na Farida ambaye alizidi kuonekana msichana mwenye mvuto kwangu kupita kawaida.

Sikutaka mahusiano yangu na Farida yajulikane chuoni hapo kutokana na wanachuo wengi kufahamu kwamba nilikuwa mvulana mpole ambaye niliogopa wasichana kupita kawaida, sikuwa miongoni kati ya wale wavulana ambao walikuwa wakiwahusudu wasichana kuliko kitu kingine chochote.

Mahusiano yalikuwa ya siri mno, tena mara kwa mara nilikuwa pamoja naye lakini sikutaka mtu yeyote afahamu uhusiano uliyokuwa ukiendelea kati yetu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mpaka kufikia katika kipindi hicho hatukuwa tumefanya mapenzi kabisa, ingawa Farida alionekana kuwa tayari kwa kila kitu lakini nilikuwa nikimwambia kwamba alitakiwa asubiri kwani nilikuwa nikiweka mambo yangu sawa.

Kwa wakati huo sikutaka kufanya vitu kwa kukurupuka, nilijua fika kwamba nilikuwa nina mahusiano ya kimapenzi na Farhia, msichana ambaye nilifahamiana naye facebook na ndiye aliyenipa utajiri hivyo kitendo cha kumsaliti na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na msichana mwingine, Farida kwangu nilikiona kuwa ni zaidi ya ukatili mkubwa ambao nilikuwa nikienda kumfanyia, ukizingatia hakuwa amekosea wala kunifanyia jambo lolote lile baya.

Muda wote alinionyesha ni kwa jinsi gani ambavyo alikuwa akinipenda na kunijali zaidi ya kitu kingine chochote katika hii dunia japokuwa katika kipindi chote hicho hatukuwa tumefanikiwa kuonana ana kwa ana. Hilo kwangu lilikuwa ni zaidi ya tatizo.

Mapenzi yangu na Farida yalizidi kupamba moto siku hadi siku, naweza kusema kwamba yalinichanganya kupita kawaida.

Katika hali ya kushangaza nilionekana kusahau kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yangu na Farhia. Sikumkumbuka na wala sikutaka kukumbuka kitu chochote alichowahi kunifanyia katika maisha yangu.

Katika kipindi hicho wala sikuwa na hofu hata kidogo moyoni mwangu, uhusiano wangu na Farida ulizidi kuniteka vilivyo na kuota mizizi mpaka kufikia hatua ambayo baadhi ya wanachuo walianza kufahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea kati yetu.

Ni hapa ambapo hata washikaji zangu sikutaka kuwaficha kitu, ilibidi niwaeleze ukweli kuhusu Farida.

“Na Farhia je?” aliniuliza Deo huku akinishangaa, lilikuwa ni swali ambalo nilitegemea kuulizwa hasa kwa mtu kama yeye ambaye alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu na msichana huyo.

“Amefanyaje?” nilimuuliza swali lililoashiria wazi kwamba sikuwa na hofu hata kidogo.

“Akijua unafkiri itakuwaje?”

“Sidhani kama nitaweza kumwambia, hii itabaki kuwa siri yangu.”

“Kuwa makini lakini mzee baba.”

“Usijali, hilo limepita kuna lingine?”

“Hakuna.”

“Basi fresh,” nilimwambia huku nikiachia tabasamu pana.

Kutokana na kuwa na mahusiano na Farida, nikajikuta nikizidi kupata usumbufu kwa wasichana ambao niliwakataa na mwisho wa siku kutengeneza uadui mkubwa. Hakukuwa kuna msichana ambaye alitaka kuona nikiendelea kuwa na mahusiano na Farida.

Ukumbuke mpaka kufikia hapo wasichana walikuwa wakichanganyikiwa na utajiri niliokuwa nao, ulikuwa ni utajiri uliokuwa unaongezeka siku hadi siku.

Wanachuo ambao nilikuwa nikisoma nao walionekana kunishangaa, hawakuamini kama kwa wakati huo nilikuwa na biashara ambayo iliniingizia kiasi kikubwa sana cha fedha.

Hakukuwa kuna mwanachuo ambaye alifahamu kile ambacho kilikuwa kikiendelea nyuma ya pazia zaidi ya washikaji zangu, Deo na Nickson. Hakukuwa kuna mwanchuo ambaye alijua kwamba utajiri niliokuwa nao ulitokana na Farhia, msichana ambaye nilikutana naye facebook na kuanzisha uhusiano naye wa kimapenzi.

Japokuwa nilikuwa nikipata kila kitu nilichokuwa nikikihitaji katika maisha yangu kwa wakati huo lakini Farhia aliamua kunipa sharti moja ambalo lilionekana kubeba uzito wa mambo mengi ambayo kiukweli katika kipindi hicho sikuyafahamu, pengine labda kutokana na uchache wa kushindwa kufikiria mara mbilimbili kabla ya kukubaliana naye.

Sharti kubwa ambalo alinipa, lilikuwa ni kutotaka kuniona nikiwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana yeyote yule na hii ilitokana na sababu ambayo ilikuwa imejenga wivu mkubwa moyoni mwake, hilo kwangu halikuonekana kuwa tatizo hata kidogo.

Nilijua fika kwamba Farhia alikuwa msichana mrembo ambaye nilikuwa nikimpenda na hivyo lingekuwa ni jambo gumu sana la kumsaliti.

Tangu nilipopata utajiri na kuanza kusumbuliwa na wasichana ambao walionekana kunipenda hapo ndipo ambapo nikaona sharti lake kuwa gumu sana lakini kwa sababu niliamini alikuwa akinipenda, nilimsaliti huku nikiamini kama angejua basi ningemuomba msamaha na mambo yote yangeisha.

***

Siku ziliendelea kukatika huku uhusiano wangu na Farida ukiendelea kupamba moto kama kawaida. Mwezi mmoja ulipita huku nikiwa bado sijafanya naye mapenzi kabisa. Mwezi wa pili ukafika, hapo ndipo ambapo uvumilivu ulimshinda.

Siku moja majira ya usiku kama saa tatu hivi alinipigia simu na kuniuliza kama nilikuwa nyumbani kwa wakati huo au nilitoka.

“Nipo nyumbani kwani kuna nini?” nilimjibu huku nikimuuliza kwa mshangao.

“Hakuna kitu mpenzi wangu ila nipo njiani nakuja,” alinijibu.

“Unakuja wapi?”

“Nyumbani kwako.”

“Saa hizi?”

“Ndiyo kwani kuna tatizo gani?”

“Hakuna ila mbona usiku sana?”

“Nimekumisi mpenzi wangu.”

“Mmh! Ila nyumbani wanajua?”

“Wanajua kuhusu nini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kwamba umetoka unakuja kwangu?”

“Abdul mimi ni mtu mzima, naishi maisha yangu. Usiwe na wasiwasi wowote kuhusu familia yangu.”

“Lazima niwe na wasiwasi, kumbuka unaishi na wazazi wako.”

“Ndiyo wanajua.”

“Wanajua unaenda wapi?”

“Nimewadanganya kwamba naenda kwenye birthday ya rafiki yangu, Martha hivyo leo sitarudi mpaka kesho.”

“Sawa kwahiyo umefika wapi?”

“Nimefika Karume, kuna foleni kidogo.”

“Okay, ukifika utaniambia basi.”

“Sawa mpenzi,” aliniambia kisha nikakata simu.

Akili yangu ilichanganyikiwa muda huo, sikutaka kuamini kama Farida alikuwa akija nyumbani kwangu tena katika usiku huo.

Wakati nilipokuwa nimejilaza kitandani huku akili yangu ikimfikiria msichana huyo mara simu yangu iliingia ujumbe mfupi. Nilipoutazama ujumbe huo, ulikuwa ni wa Farida na aliniambia kwamba tayari alikuwa amefika, yupo nje.

“Umepaa au?” nilimuuliza baada ya kumkaribisha ndani kwangu.

“Hahaha! Niliona foleni ni ndefu hivyo ikabidi nishuke nikachukua pikipiki,” alinijibu huku akiendelea kujichekesha.

“Pole.”

“Ahsante.”

“Unatumia kinywaji gani?”

“Ahsante nimeshiba.”

“Umeshiba kinywaji?”

“Ndiyo.”

“Mmh!”

“Mbona umeguna?”

“Hakuna kitu,” nilimwambia huku nikimtazama usoni.

Kwa muda wa dakika kadhaa ambazo nilikaa naye mule ndani huku tukipiga stori za hapa na pale nilishangaa kumuona akianza kukaa mikao ya ajabu huku akijipapasa mapaja yake yaliyokuwa wazi kutokana na sketi fupi aliyokuwa ameivaa.

Kwa picha iliyokuwa ikiendelea mahali hapo haikuhitaji uwe na elimu kiasi gani ili uweze kuelewa ni kitu gani ambacho Farida alikuwa akikihitaji.

Akili yangu ilichanganyikiwa kabisa mahali hapo, kwa jinsi nilivyokuwa nikimwangalia Farida ndiyo kabisa nilizidi kuchanganyikiwa. Ingawa sikupanga kufanya naye mapenzi kwa kuhofia kumkosea Farhia lakini siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti kabisa.

Kwa kasi ya ajabu Farida alinirukia na kuanza kunipapasa mwilini mwangu taratibu kwa kutumia viganja vyake, kila kiungo alichokuwa akinishika nilikumbwa na msisimko wa ajabu. Mpaka kufikia hapo sikuonyesha ugumu wowote na nilikuwa tayari kufanya naye mapenzi.

Ni ndani ya dakika chache nikajikuta nipo kitandani tena kifuani mwa Farida nikifanya naye mapenzi. Tulistarehe kwa dakika chache lakini kabla sijamaliza tendo lenyewe ndipo hapo ambapo nikamuona Farida akitapatapa kama mtu aliyezidiwa na maji. Ni katika hali hiyo ghafla! Nikamuona akitokwa na mapovu mdomoni huku akiwa amekakamaa mwili mzima kama vile alikuwa amepigwa na shoti. Nilishangaa.





Kiukweli nilichanganyikiwa vibaya mno. Farida alikuwa kimya, hakuwa akitapatapa tena kama vile mwanzo, ni katika kipindi hicho ambapo alikuwa amelala usingizi tena kwa jinsi alivyokuwa amelala ni kama vile alikuwa amelala kwa muda na muda wowote angeweza kuamka.

Haikuwa hivyo kama nilivyokuwa nikiwaza kichwani mwangu kwani hata pale ambapo nilimuita na kujaribu kumtingisha mwili wake, hakuweza kuniitikia wala kufumbua macho yake japo kunitazama.

“Farida! Farida!” niliendelea kumuita kwa sauti kubwa huku nikimtingisha mwili wake, cha ajabu hakuniitikia, aliendelea kubaki kimya huku mapovu yakizidi kumtoka mdomoni.

Ni hapa ambapo niliyapeleka masikio yangu upande wa kushoto mwa kifua chake na kuanza kuyasikiliza mapigo yake ya moyo. Muda huo kitu nilichokuwa nikikihitaji ni kuyasikia kama yalikuwa yakidunda ama la.

Nilipofanya hivyo ajabu sikusikia kama yalikuwa yakidunda, kulitawa ukimya wa hali ya juu. Ukimya huo uilizidi kunishangaza, macho yalinitoka mithili ya mtu ambaye alikuwa amekabwa, roba.

“Farida acha utani wako bhana, hebu amka, unajua sipendi masihara,” nilijikuta nikimwambia maneno haya huku nikitabasamu. Muda huo nilionekana kama mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa.

Kiukweli mpaka kufikia hapo sikuwa sawa hata kidogo, kila nilipokuwa nikimuona Farida jinsi alivyokuwa amelala kitandani kwangu, akili yangu ilichanganyikiwa vibaya mno.

Baada ya kupita dakika kadhaa ndipo hapo ambapo akili yangu ilipata wazo la haraka. Kutokana na hali aliyokuwa nayo Farida muda huo, nilijiwa na wazo la kumpeleka hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Sikutaka kupoteza muda, haraka sana nilimbeba Farida na kwenda kumuingiza ndani ya gari kisha nikaondoka naye kuelekea hospitali ya Temeke.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Japokuwa kwa wakati huo nilikuwa barabarani nikiendesha gari lakini akili yangu haikuwa barabarani humo kabisa. Sikumbuki niliendesha gari kwa mwendo gani ila nakumbuka muda wote nilikuwa nikiwaza kufika haraka hospitalini.

Baada ya kupita dakika kumi nilikuwa tayari nimeshafika katika hospitali hiyo. Nilishuka kwenye gari na kisha kwenda kuomba msaada kwa nesi niliyekutana naye. Baada ya kumuelezea hali aliyokuwa nayo mgonjwa wangu haraka alienda kuwaita wenzake wawili, wakaja kunisaidia kumtoa Farida na kumpeleka moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha matibabu. Muda huo nilibaki nje kusubiria majibu.

Hapo kwenye benchi sikutulia hata kidogo, nilisimama na kuanza kuzunguka huku na kule kama mwendawazimu. Nilichokuwa nikikihitaji ni kuona Farida akipona na kuwa sawa kwani hiyo ndiyo ingekuwa salama ya maisha yangu.

Baada ya kupita dakika kadhaa daktari aliyeingia chumba hicho cha matibabu alitoka, haraka nilimkimbilia na kumuuliza hali ya mgonjwa wangu ilikuwa inaendeleaje.

Daktari huyo hakunijibu kitu, isipokuwa aliniambia kwamba niongozane naye mpaka ofisini kwake, nilifanya hivyo kama alivyoniambia.

“Naam dokta,” nilisema huku nikimtazama usoni. Kwa jinsi nilivyokuwa nikimtazama, uso wake uliashiria kuwa na tatizo.

“Una uhusiano gani na huyu mgonjwa?” aliniuliza.

“Ni ndugu yangu,” nilimjibu.

“Una uhakika?”

“Ndiyo dokta.”

“Ndugu yako kivipi?”

“Mdogo wangu.”

“Kweli?”

“Ndiyo dokta kwani kuna nini? anaendeleaje?”

“Usijali nitakwambia lakini kabla sijakwambia kuna kitu nitahitaji uwe nacho.”

“Kitu gani hicho?”

“Ujasiri.”

“Dokta mbona sikuelewi?”

“Kijana nafahamu fika kuwa wewe ni mwanaume na nikikuambia jambo hili utalipokea kwa ujasiri mkubwa, hutoogopa kwani binadamu wote safari yetu ni moja. Nasikitika kukwambia kwamba mdogo wako hatunaye tena duniani. Tumejitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake lakini tumeshindwa. Mungu amempenda zaidi,” aliniambia daktari maneno yaliyonivuruga akili yangu.

Nilishikwa na bumbuwazi, sikuamini kile alichokuwa akiniambia daktari huyo. Nilihisi kama alikuwa akinitania lakini swali lililojijenga kichwani mwangu ni kwamba nilikuwa na ukaribu naye upi ambao mpaka ukafikia hatua ya kuanza kujenga mazoea ya kutaniana kiasi hicho?

Jibu lilikuwa ni HAPANA kwamba hatukuwa na mazoea ya aina yoyote yale na hivyo kile alichokuwa akinieleza kilikuwa ni ukweli mtupu.

“Farida amekufa?” nilimuuliza daktari swali hilo kwa kukurupuka, alikwisha nieleza kila kitu lakini nilihitaji kupata uthibitisho wa kauli yake.

“Pole sana kijana, ni hali ya kawaida ambayo itamkumba binadamu yeyote hapa duniani,” aliniambia daktari huku akinipa pole kutokana na msiba huo mzito uliyonikumba katika maisha yangu.

Katika kipindi hicho sikujua nilitakiwa kuanzia wapi? wala kumalizia wapi? Kwa sababu kila kitu kilionekana kuwa kigumu kwangu.

Japokuwa nilimdanganya daktari kwamba Farida alikuwa ni mdogo wangu wa damu lakini ukweli ulibaki kuwa moyoni mwangu. Nilikuwa kwenye uhusiano naye wa kimapenzi na kibaya zaidi wazazi wake sikuwa nikiwafahamu, huo ulikuwa ni zaidi ya msala.

Baada ya kumaliza mazungumzo na daktari na kuniambia kwamba mwili wa marehemu ulipelekwa mochwari, niliondoka huku nikimuahidi kurudi siku inayofuata kwa ajili ya kwenda nyumbani kuwaeleza kile kilichokuwa kimetokea.

Kiukweli nilichanganyikiwa vibaya mno, usiku huo niliondoka hospitalini hapo huku nikiwa nimetawaliwa na mawazo lukuki.

Sikumbuki ni kitu gani kilitokea lakini cha ajabu nilipofika maeneo ya usalama nilishangaa polisi wakinisimamisha na kuniweka chini ya ulinzi.

“Kijana kuanzia sasa hivi upo chini ya ulinzi,” aliniambia polisi mmoja ambaye mkononi alikuwa ameshika pingu huku mwingine akiwa ameshika bunduki.

“Kwa kosa gani jamani?” nilimuuliza.

“Umeua.”

“Nimeua?”

“Ndiyo.”

“Nimemuua nani?”

“Unajifanya hujui, yule msichana uliyemtelekeza hospitalini ni nani ambaye unahisi amehusika na kifo chake kama sio wewe, una kesi ya kwenda kujibu. Muuaji mkubwa wewe,” aliniambia polisi huyo huku akinifunga pingu.

“Afande hiri rijamaa litakuwa ni riuaji sugu kabisa tena rijeuri, si unaliona jinsi linavyoangalia na macho yake makubwa,” alisema yule polisi mwingine kwa lafudhi ya watu wa kanda ya ziwa, huku akinipiga na kitako cha bunduki.

“Jamani afande mimi sijaua,” nilisema huku nikijaribu kujitetea.

“Utaenda kujielezea mahakamani, muuaji mkubwa wewe,” aliniambia yule polisi aliyenifunga pingu kisha tukaongoza moja kwa moja mpaka kituoni.

Hicho ndicho kilikuwa kipindi ambacho nilijutia mambo mengi sana katika maisha yangu. Nilijuta kumfahamu Farida mpaka kufikia hatua ya kuanzisha uhusiano naye wa kimapenzi.

Bila uhusiano huo sidhani kama ningeweza kukumbwa na mambo yote hayo. Katika hali ya kushangaza machozi yalianza kunitoka na kutiririka mashavuni mwangu.

”Unaria nini? unaria wakati umeua. Subiri ukatumikie kifungo cha maisha jela tena kwa jinsi unavyoriaria hivyo huko jela utaenda kuolewa,” aliniambia yule polisi huku akizidi kunipiga na kitako cha bunduki.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





Usiku huo nilipelekwa sero kisha nikaambiwa kwamba ningekaa huko kwa siku kadhaa mpaka pale ambapo uchunguzi wa jeshi la polisi ungekamilika na kama ningekutwa na hatia yoyote ile ya kusababisha mauaji basi ningepelekwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu ya uraiani, ningeenda kuozea jela.

Nilipoambiwa hivyo nilishtuka sana, hapo hapo nilihisi kama tumbo langu likinguruma kwa fujo hali iliyoashiria kwamba muda wowote ule ningeweza kujisaidia haja kubwa. Haikuwa hivyo isipokuwa uoga ndiyo ambao uliokuwa umenitawala.

Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu, wakati mwingine nilijiuliza maswali lukuki ambayo yalikosa mtu wa kunijibu kwa wakati huo.

Nilijiuliza kwamba ilikuwaje mpaka polisi hao wakafahamu kwamba kweli kulikuwa kuna msichana alikufa, tena nilimuacha hospitalini?

“Au ni yule daktari aliwaambia? Lakini kama ni yeye kwanini sasa amewaambia kwamba nimeua? Amedhamiria nini?” nilijiuliza maswali mfululizo yaliyokosa majibu.

Nilikaa sero kwa muda wa siku mbili. Siku ya tatu iliyofuata majira ya asubuhi ndipo hapo ambapo nikashangazwa na kitendo cha kuachiwa huru.

Niliambiwa kwamba baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi kukamilika, ilionekana kwamba sikuwa na hatia yoyote ile hivyo kuanzia siku hiyo nilikuwa huru kuendelea na maisha ya uraiani.

“Ila kijana kuwa makini sana, jichunge usije siku ukajichanganya ukaingia tena mikononi mwa jeshi la polisi, utapotea. Usione kuna watu wamefungwa jela vifungo mbalimbali ukadhani wote wamefanya makosa, wengine wamejitakia,” aliniambia polisi mmoja ambaye alikuwa akinikabidhi vitu vyangu nilivyoviacha kipindi nilipokuwa naingizwa sero.

“Sawa afande nimekuelewa,” nilimwambia.

“Ok vipi utaweza kwenda nyumbani mwenyewe au tukupe ulinzi?” aliniuliza wakati ambao alikuwa akinikabidhi funguo ya gari.

“Nitaweza kwenda mwenyewe wala usijali afande.”

“Sawa ila kuwa makini,” aliniambia.

Siku hiyo sikuamini hata kidogo kwa kile kilichokuwa kimetokea, kitendo cha kuachiwa huru na jeshi la polisi niliona ni sawa na swala kuachwa na simba hali ya kuwa simba alikuwa na njaa ya siku saba. Hakika ilikuwa ni ajabu mno tena yenye kustajabisha.

Niliondoka kituoni hapo kurejea nyumbani kwangu kwani ni siku mbili zilikuwa zimepita tangu nilipokamatwa na kuwekwe sero. Barabarani bado sikuonekana kuwa sawa, muda wote nilikuwa nikifikiria kile kilichokuwa kimetokea.

Mpaka kufikia muda huo sikujua kama mwili wa Farida ulichukuliwa na ndugu zake mochwari kwa ajili ya mazishi.

“Ila na mimi nawaza vitu vya ajabu sana, watawezaje kwenda kuuchukua mwili mochwari na wakati hawajui kama amekufa?” nilijiuliza swali hili ambalo lilinifanya nizidi kujiona kuchanganyikiwa kupita kawaida. Akili haikuwa yangu muda huo.

Nilipowaza kuhusu Farida nilihisi kusisimka mwili. Nilikumbuka siku ile alipokuja nyumbani kwangu usiku na mambo yote yaliyotokea mpaka kusababisha kifo chake.

Niliumia sana kumpoteza Farida na kila nilipokuwa nikikifikiria kifo chake jinsi kilivyotokea sio siri, niliona fika kuwa kulikuwa kuna kitu nyuma ya pazia. Kifo chake hakikiwa bure hivi hivi.

Baada ya kupita nusu saa niliweza kufika nyumbani kwangu. Niliingia bafuni kuoga, nilipomaliza nilirudi kisha nikajilaza kitandani. Japokuwa nilihisi njaa lakini sikutamani chakula kwa muda huo.

Akili yangu ilikuwa ikimfikiria Farida tu ambaye katika kipindi hicho alikuwa amefariki dunia. Kifo chake kilitokea katika mazingira yakutatanisha sana.

Nilikumbuka kwamba sikuwa nimeiwasha simu yangu muda, hapohapo nikaiwasha na kuitupa upande wa pili huku nikiendelea kujilaza.

Kitendo cha simu yangu kuwaka tu, haikuchukua sekunde kadhaa ikaanza kuita. Nilipoangalia kwenye kioo niliona jina la Farhia. Nikapokea.

“Abdul kwanini ulizima simu siku zote hizo?” lilikuwa ni swali aliloniuliza mara baada ya kupokea na kuweka simu sikioni.

“Jamani hata salamu mpenzi?” nilimuuliza kwa sauti ya upole.

“Kama unapenda salamu usingezima simu.”

“Mpenzi hebu punguza moto kwanza, mwenzio nilipata matatizo.”

“Matatizo?”

“Ndiyo.”

“Matatizo gani?”

“Nilikamatwa na polisi.”

“Ulikamatwa na polisi?”

“Ndiyo.”

“Kwa kosa gani?” aliniuliza kisha nikanyamaza kwa muda, nilikuwa nikifikiria uongo ambao nilitakiwa kumdanganya kwani sikutaka afahamu ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea.

“Niambie polisi walikukamata kwa kosa gani?” aliendelea kuniuliza huku sauti yake ikiashiria wazi kwamba taarifa hiyo ilimshtua kupita kawaida.

“Ni matatizo tu,” nilimwambia huku nikiendelea kutunga uongo kichwani.

“Matatizo gani?” aliniuliza.

“Farhia mpenzi wangu lakini shukuru nimetoka salama, sijafungwa. Sioni kama kuna haja ya kukwambia kilichotokea.”

“Nataka uniambie.”

“Lakini mpenzi.”

“Sitaki mpaka uniambie ulikamatwa kwa kosa gani? au umejiingiza kwenye biashara haramu?”

“Hapana.”

“Kama siyo sasa polisi walikukamata kwa kosa gani?”

“Kuna uhalifu ulitokea hapa jirani na ninapoishi.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Enhe! Ikawaje?”

“Wahusika waliofanyiwa huo uhalifu walinihisi mimi nilikuwa nimekula njama na hao watu hivyo wakaniweka ndani.”

“Halafu ikawaje?”

“Baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi kukamilika, ilionekana kwamba sina hatia yoyote hivyo wakaamua kuniachia huru na ndiyo sababu leo hii umenipata. Ingekuwa siyo hivyo muda huu tungekuwa tunazungumza mambo mengine.”

“Pole sana mpenzi wangu pia utanisamehe kwa kukuhisi vibaya.”

“Usijali mpenzi wangu, naelewa kila kitu hivyo kuwa na amani.”

“Jamani sasa umekula nini?”

“Bado sijala.”

“Kwanini?”

“Hata hivyo sina njaa.”

“Mmh! Usiniambia hivyo hebu fanya mpango ule.”

“Sina njaa lakini.”

“Utaniudhi unajua.”

“Sawa basi ngoja niende nikapike.”

“Unapika nini?”

“Tambi.”

“Tambi na nini?”

“Na chai.”

“Sawa basi fanya hivyo kwanza, ukimaliza uniambie ili nikupigie.”

“Sawa,” nilimwambia kisha nikaenda jikoni kuandaa chakula hicho.

Mpaka kufikia hapo ilikuwa ni vigumu sana kuamini kwamba Farhia ndiye ambaye alikuwa akifanya mambo yote hayo yaliyokuwa yakitokea katika maisha yangu. Katika kipindi hicho kama angetokea mtu akaniambia kwamba kifo cha Farida kilisababishwa na Farhia hakika ningemuona mtu huyo kuchanganyikiwa.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu, kilikuwa ni siri tena ambayo mpenzi wangu, Farhia hakuifahamu.

Nilimuamini sana Farhia na hii ndiyo sababu ambayo ilinifanya nisiwe mwepesi wa kumuhisi chochote kile kibaya. Naweza kusema kwangu nilimfananisha na malaika, hakuwa na dhambi yoyote ile, alikamilika kwa kila kitu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku hiyo sikuishia kuwasiliana na Farhia tu bali nilianza kupokea meseji nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo marafiki zangu ambao walikuwa wakinipa pole kutokana na kile kilichokuwa kimetokea katika maisha yangu.

“Unajua siamini kama Farida amefariki dunia? Ila yote ni mipango ya Mungu,” aliniambia Deo ambapo hakuishia hapo tu, isipokuwa aliendelea kuniambia kwamba Farida tayari alikuwa amezikwa tena alizikiwa makaburi ya Temeke.

“Amezikwa?” nilimuuliza huku nikionekana kushangaa.

“Ndiyo mzee baba si unajua waislamu nyie hamcheleweshi, kazikwa jana,” aliniambia.

“Inamaana ndugu zake walienda kumchukua?” nilimuuliza swali la kukurupuka.

“Walienda kumchukua wapi?” alinihoji swali ambalo jibu lake nilishindwa namna ya kulielezea.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog