Search This Blog

THE RETURN OF THE AMBROSY - 1

 




IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO



*********************************************************************************



Simulizi : The Return Of The Ambrosy

Sehemu Ya Kwanza (1)





 Walemi binti kutoka makao makuu ya Nchini, mkoani Dodoma. Anaondoka nyumbani kwao na kuingia jiji Dar es salaam kwa dhumuni la kutafuta maisha, anajikuta akipata tabu kwa kukosa makazi ya kuishi jiji humo. Jua lake mvua yake, Elimu yake ya darasa la saba ikawa kikwazo kwake kupata kazi, hali iliyompelekea kujikita katika kazi ya kuomba omba barabarani. Maisha hayo yalikuwa endelevu kwa Walemi, lakini baadaye alibahatika kupata kazi nyingine ya kuuza chakula kwenye moja ya mgawahawa mitaa ya Mwananyamala.(Mama ntilie) Upole na ukarimu wa binti huyo anajikuta unampelekea kupendwa na kijana mtana shati, kijana msomi na mwenye pesa za kutosha, kijana nadhifu ambaye alimuona Walemi mara moja tu wakati anakatiza na gari yake jirani na eneo ulipo mgahawa huo aliokuwa akihudumia binti huyo. Kijana huyo liitwa Ambrosy. Ambrosy alivutia mno na Walemi ni kama bahati aliyoipata Walemi kupendwa na kijana huyo asiye na kasumba hata lepe,kwani asilimia kubwa ya vijana wenye maisha mazuri hasa hasa vijana wa mjini hupendelea kuoa wanawake warembo wasio isha hamu kuwatazama. Lakini ajabu hali hiyo ikawa tofauti kabisa kwa kijana Ambrosy,alivutiwa na muonekano wa Walemi binti ambaye alionekana kuwa rafu kiasi kwamba hatamanishi kwa hali yoyote. Mwanamke matunzo, hatimaye Ambrosy anayabadirisha maisha ya Walemi,alimuendeleza kielimu lakini pia alimununua gari ya kutembelea bila kusahau kumfungulia duka la nguo eneo la kariakoo. Sasa Walemi uzuri nadhifu aliokuwa nao ukaaza kujidhilisha kwa macho ya umma akawa sio yule Walemi aliyekuwa akipita barabarani kuomba omba, akawa sio yule Walemi aliyekuwa mama ntilie, pesa sabuni ya roho dhahili shahili sabuni hiyo ikathubutu kumtakatisha Walemi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Lakini baada ya miaka kadhaa kupita, hatimaye Walemi anabahatika kukutana na mpenzi wake wa zamani sana wa kipindi hicho yupo mkoani kwao Dodoma. Mwanaume huyo ndiye aliyemtoa bikira huku wakiwekeana nadhiri kuwa katu hawatokuja kuachana maishani mwao. Ila mwishowe nadhiri hiyo ikaja kugeuka asidi mara baada mpenzi wake huyo kwenda DAR-ES-SALAAM kutafuta maisha na kisha kulowea. Walemi hakuamini machoni mwake kile akionacho, machozi ya furaha yalimtoka hasa walipokumbushana mambo kadhaa ya nyuma. Na hivyo Walemi akahitaji kujua anapoishi mwanaume huyo, alipopafahamu akawa anaenda kulala huko mara nyingine anafanya naye mapenzi huku akimuachia pesa nyingi ya matumizi pasipo Ambrosy kujua. Siku kadhaa mbele Walemi na huyo mwanaume walipanga mikakati ya kufanya mapinduzi juu Ambrosy ili wapate nafasi ya kufurahia penzi lao pasipo buguzi wala hofu yoyote. Walemi aliamini kufanya hivyo atabaki na amani na mpenzi wake huyo wa zamani, akasahau Ambrosy alipomtoa mpaka Kufika hapo alipo,wema Ambrosy ukawa kikwazo kwake na hatimaye Walemi alimuua Ambrosy kwa kumuwekea sumu kwenye chakula. Miradi yote sasa ikawa chini yake na mwanaume huyo, raha mstarehe wawili hao ikatamaraki mioyoni mwao. Ila baada miaka minne kupita tangu kifo chake Ambrosy, ajabu usiku mmoja Walemi alishtuka kusikia simu yake ikiita,alijikakamua akainuka na kisha akaichukua simu hiyo ili ajue ni nani aliyempigia. Namba ilikuwa mpya, hivyo kwa sauti iliyoonyesha bado anausingizi alibonyeza kitufe cha kijani kisha akaweka simu sikioni akasema "Hello nani mwenzangu? Na kisha kwanini unapiga simu usiku" Ajabu Walemi hakujibiwa, mtu huyo aliyempigia alikaa kimya kitendo ambacho kilimfanya Walemi kutoa simu sikioni na kisha kuitazama namba hiyo kwa mara nyingine tena. Ghafla alishtuka akaitupa simu chini, kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio mfano wa chura apumuapo. Namba ili ilimshtua sana, aliogopa Walemi akilini akajiuliza "Ambrosy? Si kasha kufa? Sasa iweje ten anipigie?.." Wakati Walemi akijiuliza maswali hayo punde si punde uliingia ujumbe mfupi (sms) Kwa mara nyingine Walemi alitaharuki ingawa mwishowe alipiga moyo konde akaichukua simu ili ajue ujumbe huo unasema nini. Alipofungua alikutana na jumbe iliyoandikwa THE RETURN OF THE AMBROSY... "

{Kurudi kwa Ambrosy}

"Mungu wangu marehemu karudi?.." Alijiuliza Walemi huku akihema juujuu asiamini kile alichokisisoma. Aligeuka kumtazama mumewe ambaye naye muda huo alikuwa amelala fo fo fo hata asiwe na habari kwamba mtu yule waliyedhurumu nafsi yake sasa karejea. Walemi aliogopa sana habari hiyo, maswali kibao akajiuliza pasipo kupata majibu.

"Ambrosy? No. Hapana sitaki kuamini kama kweli Ambrosy kafufuka,hii ni imani potofu kabisa na mambo haya hutokea kwenye senema na sio vinginevyo. Inawezekana vipi mtu aliyekufa akarudi tena duniani? Je, inamaana kwamba hakuna pepo ama jehanamu?.." maswali yote Walemi alikuwa akijiuliza kichwani mwake wakati huo mapigo ya moyo wake yakienda kasi,na punde si punde simu ile ikarudia kuita kwa namba ile ile aliyokuwa akitumia Ambrosy enzi ya uhai wake. Walemi kuona hivyo akafikiria heri kuizima simu hiyo, na sio kuizima tu bali alitenganisha kabisa betri na simu kisha akalala na kuanza upya kutafuta lepe la usingizi huku kiakili na kimwili akionekana kutokuwa sawa, Sula hilo la la kurudi kwa Ambrosy lilimchanganya mno.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada Walemi kusinzia, muda mchache baadaye mwanaume wake naye aliamka kwa dhumuni la kuelekea chooni kujisaidia. Mwanaume huyo ambaye aliitwa Daniel alijitahidi vema kushirikiana na Walemi kumuua Ambrosy ili wafurahie vizuri penzi lao kama zamani walipokuwa Dodoma. Hivyo Daniel alipoamka alijinyoosha kwanza kisha akainuka pale kitandani akatundua taulo yake kwenye enga tayari kwa safari ya kuelekea chooni. Lakini kabla hajafungua mlango wa kutokea chumbani alishtuka kuona simu ya mkewe imetenganishwa betri. "Mmh" Aliguna Daniel kisha akatikisa kichwa kama ishara ya kukataa jambo fulani halafu akazipiga hatua kuelekea chooni kujisaidia. Muda huo ulikuwa usiku wapata saa saba ikikimbilia saa nane. Daniel alizipiga hatua kuelekea chooni,ila kabla hajafika alistaajabu kutozikuta ndala maalumu za kuingia nazo chooni,hivyo kiashiria hicho kilimanisha kuwa chooni kuna mtu. Lakini ni nani wakati nyumba nzima anaishi yeye na mkewe tu? Kitendo hicho kilimfanya Daniel kupigwa na butwaa lakini mwishowe akaona hakuna haja ya kuogopa, aliusogelea mlango wa choo ili ausukume ajihakikishie kama kweli ndani kuna mtu ama lah! Ila kabla hajukaribia nafsi ilimsuta, haraka sana Daniel akarudi nyuma kisha akageuka akarudi chumbani kumuuliza Walemi kama kuna mahala ameziweka ndala hizo.

"Walemi, Walemi.. Walemi.." Daniel alimuamsha Walemi. Punde Walemi aliamka ndipo Daniel alipomuhoji suala hilo la ndala swali ambalo lilimshangaza sana Walemi ambapo kwa sauti yenye usingizi ndani yake akasema "Hivi ni ndoto ama? Dani unawezaje kuniamsha kisa ndala za chooni huku chumbani? Kuwa mstaarabu bwana niache nilela" Walemi alipokwisha kusema hivyo alijivutia shuka kuanzia miguuni mpaka kichwani kuonyesha kuwa hataki kubuguziwa. Hapo Daniel alishusha pumzi ndefu huku akiishia kumtazama Walemi pasipo kuongeza neno lolote, lakini mwishowe alirudi tena kule kule chooni. Safari hiyo aliziona zile ndala ila cha ajabu ndala hizo zilikuwa zimelowa maji kumanisha kuwa muda mchache uliopita kuna mtu alizitumia kuogea. "Mungu wangu" Alijisemea Daniel huku akizisogelea pole pole pale mlango,hali ya kuwa nyuma yake zilionekana nyao za maji zikiambaa kule alikotoka. Bado alizipiga hatua za woga kusogea pale kwenye mlango wa choo huku moyoni akiwa na woga wa hali ya juu uliompelekea kugeuka nyuma yake ambapo ndipo alipoziona zile nyao. Nyayo zile zilizidi kumchanganya Daniel, ghafla kijasho kikanza kumtoka na ile haja ndogo aliyokuwa nayo ikamshukia pasipo yeye kujua. Balaa lilizidi kuwa nzito upande wake pindi aliporudisha macho yake kule kwenye mlango wa choo, ghafla kwenye mlango akayaona maandishi yaliyo andikwa THE RETURN OF THE AMBROSY. Maandishi hayo makubwa yaliandikwa kwa michirizi ya damu. Muda huo huo akaonekana Ambrosy akiwa ndani ya mavazi meupe. Aliangua kicheko Ambrosy kisha akasema "Daniel.. Damu yangu haina hatia.. Mwambie Walemi kwamba mimi ni mgeni wenu.." Alipokwisha kusema hivyo akapotea..





"Mgeni wetu?" Alijiuliza Daniel, ndipo hofu ilipomjaa asiamini kama marehemu karejea. Hali hiyo ilimpelekea kuangua chini, aliamgukia kisogo kitendo kilimfanya kupoteza fahamu.

Alizinduka na kujikuta yupo hospital, pembeni yake alimuona mkewe ambaye alionyesha uso wa huzuni.

"Pole sana Daniel.." Alisema Walemi akimsabahi mumewe. Daniel alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Asante sana mke wangu, lakini nataka kujua kwanini niko hapa. Nimefikaje fikaje?.." Kabla Walemi hajaanza kumuelezea Daniel kisa hasa kilichopelekea Kufika hospital doctor aliingia humo wodini akamuomba Walemi aondoke ili mgonjwa apate muda wa kupumzika. Walemi alitoka humo wodini moja kwa moja alikwenda mpaka nje ambapo huko alitulia pamoja na watu mbali mbali waliokuwa wamefika hospitalini hapo kuona wagojwa wao. Hapo Walemi aliketi sehemu maalumu, alijiinamia huku akili yake yote ikifikiria suala lile lililotokea usiku. Habari hiyo ya kurejea kwa marehemu Ambrosy ilimchanganya sana, sasa alihisi maisha yake yatakuja kuwa ya tabu sana. Hofu dhofu lihali ilimjaa Walemi, hali ambayo ilimpelekea kushusha pumzi mara kwa mara huku uso wake ukionyesha dhahili shahili ni mtu mwenye maswahibu makubwa yanayomkumba.

"Dada, samahani muda mrefu tangu ufike hapa unaonekana ni mtu ambaye unamagumu sana yanakukabili. Je, unaweza kusema nasi ili tujue kama tunaweza kukusaidia hata mawazo labda ama ushauri" Ilikuwa ni sauti ya mwanamma mmoja wa makamo, mama huyo alisikika akisema hivyo baada kumtazama Walemi kwa muda mrefu ambapo aliweza kumuonea huruma namna Walemi alivyokuwa amekaa na kumruhusu akili yake kufikiria mbali, jambo ambalo lilimfanya kuwa tofauti na wale akina mama aliowakuta wakipiga zogo mbili tatu kuashiria kuwa wagojwa wao hali sio mbaya. Walemi aliinua uso wake kumtazama mama huyo aliyemsemesha, kwa mara nyingine tena alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Mama we acha tu, nimeamini ukisita ajabu ya Musa utayaona ya filauni"

"Unamaana gani?.." Aliuliza yule mama, wakati huo upande wa pili kule wodini alionekana Doctor akiendelea kumfanyia matibabu Daniel, lakini punde si punde Doctor alitoka humo wodini muda mchache baadaye alirejea kuendelea na matibabu. Muda huo Daniel alikuwa tayari ameshakaa sawa, aliweza kuelewa kila kitu tofauti na hapo awali alipomuuliza mkewe jinsi alivyo fika hapo hospital. Kumbukumbu zilimjia ambapo alikumbuka matukio yote yale ya usiku,tukio la kurudi Ambrosy lilimfanya aogope akihofia usalama wa maisha yake. Wakati Daniel anawaza hayo,Doctor alikuwa amegeukia nyuma akivua grovu mara baada kumaliza shughuli ya kusafisha kidonda cha Daniel ambaye muda huo alikuwa amepewa mgongo.

"Umesema unaitwa nani?.." Doctor alimuuliza Daniel. Daniel akataja jina lake. Doctor hiyo akiwa bado amempa mgongo Dani, aliongeza kusema "Safi sana, jina nzuri bwana Daniel sababu asilimia kubwa watu wenye majina kama haya huwa wapole wacheshi lakini wewe matendo yako kamwe hayaendani na jina jinsi lilivyo.."

"Unamaana gani?.." Aliuliza Daniel. Doctor akajibu

"Naam, kabla sijagusia huko naomba uniambie ukweli wako sababu tayari umesharejesha kumbukumbu, kwahiyo nafikiri kila kitu utakuweza kuikumbuka. Ni kipi kilicho kupelekea ukaangukia kisogo?.." Daniel alishtuka kusikia maneno hayo, aliogopa pia kujibu kwa sababu Doctor huyo alikuwa akiyasema maneno hayo huku akiwa amempa mgongo na hata asigeuka kumtazama. Wakati Daniel akiingiwa na wasi wasi kuhusu maswali hayo ya Doctor mara ghafla Doctor aliangua kicheko, na punde si punde nyuma kwenye mgongo koti alilovaa yalionekana maneno yaliyosemeka THE LETURN OF THE AMBROSY.. Daniel alishusha pale kitandani alipokuwa amelazwa, akajikuta kuelekea ukutani ilihali muda huo huo Doctor aligeuka safari hiyo akiwa na sura ya marehemu Ambrosy. Kwa sauti nzito na nene iliyokuwa ikijirudia Doctor akasema "The return of the Ambrosy. A hahaha hah" Kisha akapotaea. Nafasi hiyo ilimpelekea Daniel kupiga kelele, haraka sana alitoka humo wodini kama Mwendawazimu akatimua mbio kuelekea nje huku akipiga mayowe. Walemi alipomuona mumewe yupo katika hali ile alimkimbilia akamshika mkono na kisha kuingia naye ndani ya gari huku Daniel akionekana kupagawa. Walipofika nyumbani Walemi alimuuliza muwe ni kitu gani kilichomfanya atoke wodini mithili ya kichaa akiwaacha watu midomo wazi, Daniel kabla hajasema alishusha pumzi kwanza kisha akasema "Doctor"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Doctor? Amefanya nini?" Alihoji Walemi. Daniel alikaa kimya kidogo punde alivunja ukimya huo kwa kusema "Wakati nipo wodini doctor ananihudumia kuna muda alitoka lakini muda mchache baadaye alirejea kuendelea na huduma, alipomaliza aligeuka nyuma akivua grovu sehemu yake maalumu wakati tunapiga story mbili tatu. Katika maongezi hayo kuna maswali aliniuliza, maswali ambayo yalinishtua yakanipelekea nikae kimya. Hapo ghafla kwenye nguo yake mgongo nikaliona jina la Ambrosy, nilioga sana muda huo huo doctor akanigeukia ajabu alionekana akiwa na uso wa Ambrosy. Aliangua kicheko halafu akapotea. Si hilo tu mke wangu Walemi, hata jana usiku nilianguka na kupoteza fahamu baada kukumbana na mambo ya ajabu ajabu "Alisema Daniel, muda hao wapenzi hao walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa. Maneno hayo ya Daniel yalizidi kumchanga Walemi, hofu na woga vikatanda moyoni mwake aliwaza mbali sana hasa akifikiria mstakali wa maisha yake na mumewe. Kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake Walemi alimuuliza Dani "Kwahiyo ishara hiyo inamanisha kuwa Ambrosy hajafa? Yupo hai?.."

"Naam mke wangu, ndivyo hivyo.." Alijibu Daniel, jibu ambalo lilimfanya Walemi kunyanyuka pale kwenye kiti akazipiga hatua za pole pole kuelekea nje wakati huo moyoni ya akijisemea "Tayari mambo yameshaharibika, na kama kweli Ambrosy karudi nitaishije? Ooh Mungu wangu nisaidie.." Alipokwisha kujisemea hayo moyoni mwake alidondosha machozi chini huku mikono yake akiipeleka kwenye uzio wa kuta ambapo alipougusa akajiinamia wakati huo kichwani bado akiwaza mambo mengi hasa ujio wa marehemu Ambrosy,na hapo ndipo kumbu kumbu zilipo rudi nyuma kabisa. Alikumbuka siku ile alipoondoka nyumbani kwao Dodoma akaelekea jiji Dar es salaam ikiwa kama njia pekee ya kuwakimbia wazazi wake ambao walimtaka Walemi aolewe na mwanaume ambaye walimchangualia na sio Daniel ambaye alioneakana kulowea pasipo kurudi nyumbani,lakini mbali na hilo la kuchaguliwa mchumba Walemi pia aliamini jijini humo angeweza kupata kazi na hata ikatokea bahati ya kuonana na mwanaume wa ndoto yake ambaye sio mwingine bali Daniel. Ndani ya basi la Abood Walemi alikwea huku akiwa na kifurushi kidogo cha nguo ambazo alizifunga ipasavyo kwenye kitenge chake kukuu,akiwa na wasi wasi juu ya safari yake Walemi alitulia kwenye siti huku akiwa amejiinamia akiwaza ni namna gani atakavyo ishi ndani ya jiji la Dar ikiwa hana ndugu wala jamaa. "Mungu nisaidie" Alijisemea hivyo Walemi akianza kwa kushusha pumzi ni mara baada ya kuwaza kwa muda mrefu safari ya maisha yake.

Saa tisa alasiri gari liliwasiri Dar es salaam, abiria waliokuwemo katika gari hiyo walitelemka. Waliokuwa na wenyeji wao walipokelewa kwa shangwe, na wale ambao walionekana ni wenyeji waliambaa kuelekea getini ambapo Walemi akiwa na furushi lake aliwafuata watu hao. Hatimaye akawa nje ya stendi ya ubungo, alishngaa sana kuona wingi wa magari katika mji ule huku mjengo mrefu nayo ikimfanya kuamini kwamba duniani kuna mamb hali ambayo ilimpelekea Walemi kutazama huku na kule muonekano nao ukimtandabaisha ya kwamba ni mgeni wa jiji. Sauti za wapiga debe wakitaja vituo mbali mbali zilipenya vema katika masikio yake. Walemi alibaki kusimama kando ya barabara hata asijue aelekee wapi aende. Jua popole lilianza kutokomea, giza nalo likionekana kuivaa vema uso wa jiji la Dar es salaam huku mwanga wa mataa nayo yakilimurika jiji hilo. Bado Walemi alibaki kusimama, hofu dhofu lihali ikizidi kumtawala wakati huo mapigo ya moyo wake nayo yakimwenda kasi. Lakini wakati yupo katika hali hiyo ghafla mbele yake ilisimama gari ndogo taxi,kisha kioo cha gari hiyo kilifunguliwa. "Habari yako dada?.." Ilisika sauti ya mwanaume ikitokea ndani ya gari hiyo, sauti ambayo aliitoa kwa kumpa salamu Walemi ambaye muda huo alioneakana kukosa muelekeo. Walemi aliposikia sauti hiyo akatazama kule ilipotokea akakutana uso kwa uso na mwanaume yule ambaye kwa wakati huo alionyesha tabasamu kana kwamba anamfahamu Walemi. Kitendo hicho kilimfanya Walemi kushangaa ilihali muda huo yule mwanaume alimuita kwa ishara ya mkono,ambapo Walemi naye pasipo kutafakari alitii wito. Walizungumza mambo mawili matatu kisha Walemi akaingia ndani ya gari hiyo huku moyoni akiamini amepata msamaria mwema. Mpaka kwenye moja ya gesti maeneo ya kindoni Walemi aliingia na mwanaume huyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja Lameki.

"Karibu binti ondoa shaka kabisa, ngoja mimi nitoke nje mara moja nikutafutie chakula sawa?.." Alisema Lameki huku akinyanyuka kitandani na kumuacha Walemi akiwa amekaa. Lakini muda mchache baada Lameki kwenda kumchukulia Walemi chakula, punde si punde mlango wa chumba hicho uligongwa, Walemi akaenda kufungua akawa amekutana na mwanadada ambaye hakumfahamu ila alimuona mapokezi. Kwa sauti yenye wasi wasi yule dada alimuuliza Walemi kuhusu Lameki, Walemi akajibu "Ndio ndio namfahamu kwani vipi?.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kweli? Lakini mbona kama unaonekana wewe ni mgeni hapa Dar? Jaribu kuwa mkweli ili faida kwako" Aliongezea kusema yule mwanadada. Maneno hayo yalimtia hofu Walemi ambapo alikaa kimya kidogo kisha baadaye akasema "Ni kweli dada, huyu mbaba nimekutana naye stendi akaniomba kunisaidia sehemu ya kulala halafu kesho anitafutie kazi" Alisema hivyo Walemi. Yule mwanadada alimsikitikia Walemi, na mara baada kulihitimisha sikitiko hilo akamwambia "Kwa taarifa yako huyu kaka kazi yake ni kuchukuwa wale wadada wageni au wasio jiweze kisha anawanyofoa sehemu zao za siri na kisha kuzipeleka kwa watu wanao mtuma...





Yule mwanadada alipokwisha kumwambia habari Walemi aliondoka zake, lakini kabla hajafika mbali alisikia sauti ya Walemi ikimuita. Dada yule alisimama kumsikiliza ingawa moyoni akiwa na hofu ya kukutwa na Lameki. "Sema haraka usijenisababishia matatizo mimi" Alisema yule mwanadada. Walemi kwa sauti ya woga akajibu huku kijasho chembamba kikimtoka "Nisaidie basi, tafadhali dada usiniache mahali hapa"

"Nifanyeje sasa?.." Aliuliza yule mwanadada. Swali ambalo lilimpelekea Walemi kupiga magoti chini huku akizidi kuomba usaidizi kwa dada huyo kwani aliona tayari maisha yake yapo hatarini. Kitendo hicho kilimfanya yule dada kuingiwa na moyo wa huruma, ndipo alipoamua kuambatana naye mpaka stoo.

"Utalala hapa dada yangu lakini kesho utajua wapi pa kwenda maana kibalua changu kitakuwa hatarini pindi bosi atakaposhtukia mchezo huu. Stoo haruhusiwi mtu yoyote kuingia"

"Sawa dada asante sana kwa ukarimu wako, hakika Mungu atakulipa kwa wema wako sababu umenitoa kwenye shimo la mauti"

"Usijali, lakini pia inakubidi uwe makini sana na jiji hili. Hili ni jiji ambalo limejaza kila aina ya watu,ambapo utakuna na watu wenye roho nzuri vile vile utakutana na watu wenye roho mbaya. Hivyo basi kinacho takiwa ni akili kichwani mwako, la sivyo utakuja ghalimu maisha yako. Acha mimi nikaendelee na majukumu.. "Mwanadada huyo alihitimisha maongezi kati yake na Walemi kisha akaondoka zake kuendelea na majukum ya kupokea wageni waliokuwa wakija kulala.

" Loh! Ama kweli dunia inamambo "Maneno hayo alijisemea Walemi kule stoo, alijisemea hivyo mara baada kutoamini kile alicho ambiwa kwani alihisi ni kama ndoto. Mbali na hayo lakini pia pole pole joto la jiji likaanza kumpata, njaa kali ililindima tumboni mwake huku kiu ya maji nayo ikikausha kolomeo lake kwa kasi ya ajabu. Hakika Walemi alisafa lakini hakuwa na namna zaidi ya kumuomba Mungu amtie moyo wa uvumilivu ili kesho pambazuke akatafute hata upolo uliotupwa majalalani. Wakati Walemi anasafa na maumivu ya njaa na kiu, upande wa pili mapokezi walipita vijana watatu ambao walionekana kuvaa suti nyeusi na miwani meusi. Watu hao waliongozwa na Lameki kuelekea kule chumbani alikokokuwa ameachwa Walemi,lakini muda mfupi baadaye Lameki alirejea pale mapokezi akamuuliza yule mwanadada anayehusika kwenye kitengo hicho. "Dada vipi yule binti niliyeingia naye muda fulani hivi umemuona kapita hapa?.." Aliuliza Lameki kwa sauti ya hofu huku kijasho kikimtoka.

"Ndio kapita ila aliniaga kwamba anaenda kununua maji na punde tu atarejea lakini ajabu mpaka muda huu sijamuona. Kwani vipi unamfahamu? Ni mwenza wako?.." Alijibu Mwanadada huyo wakati huo akihoji na maswali mawili kadhaa ambayo pia Lameki hakuona haja ya kuyajibu zaidi ya kurudi upesi katika chumba kile.

Kesho yake asubuhi Walemi alidamka akamshukuru mwanadada yule aliyemstili kisha akaendelea na hamsini zake, ambapo alijikuta akitembea majalalani kutafuta vipolo vilivyo tupwa mithili ya Mwendawazimu. Hatimaye alibahatika kupata mkate, furaha isiyo kifani ilimjia Walemi kwani aliamimi kuwa tayari tatizo la njaa anakwenda kulimaliza.

Hayo ndio yakawa maisha ya Walemi, binti ambaye aliamua kuondoka nyumbani kwao kwa kutoroka akikwepa kuolewa na mwanaume ambaye hakumtaka. Mwanaume huyo alitafutiwa na wazazi wake baada kuona kuwa binti yao tayari amefikisha umri wa kuolewa, hivyo hakuna cha kupoteza muda zaidi ya kumuozesha kwa mwanaume ambaye waliona anamfaa huku wakitupilia mbali hitaji lake ambalo Walemi alikwisha eleza kuwa tayari anamchumba. Mchumba wake ambaye ameenda Dar es salaam kutafuta maisha wakati huo wakiwa wameshatia nadhiri mioyoni mwao kuwa pindi atakapo rejea wataoana. Lakini wazazi hao katu hawakutaka kumuelewa binti yao,walifika mbali na kumwambia kuwa asipotaka kuolewa na mwanaume waliomchangulai basi aondoke nyumbani hapo. Hivyo Walemi akaona bora aondoke kuliko avunje ahadi ya mpenzi wake aliyempenda kwa dhati, akaamua kutimkia jiji Dar es salaam kujitafutaia maisha lakini pia akiamini kuwa huwenda akapata bahati ya kumtia machoni mpenzi wake kwa mara nyingine tena baada kumuacha kijiji kwa kipindi kirefu pasipo mawasiliano yoyote. Aliitwa Daniel.

Jua lake mvua yake yake Walemi,mwishowe akajikita katika kazi ya kuombaomba huku malazi yake yakiwa ni kulala kando ya flem za maduka ya mjini kariakoo ilihali kazi hiyo mara nyingi aliifanyia mitaa ya posta kwenda mpaka feli.

Siku moja mvua kubwa ilinyesha jijini humo, mvua ambayo iliambatana na upepo mkali. Watembea kwa miguu walizipiga hatua za haraka haraka kuelekea kwenye maduka yaliyokuwa na ukingo wa kutosha, hali ya kuwa wenye magari yao nao wakipandisha vema vio huku wakati huo wakisubiri taa ya kijani iweze kuwaruhusu. Kwa mbali katika mvua hiyo alionekana Walemi akitembea kando ya magari hayo yaliyokuwa foleni, ambapo pasipo kuogopa wingi wa mvua hiyo Walemi alitembea gari hili mpaka gari lile akiomba pesa bila kufanikiwa kupata alicho hitaji kwani magari yote yalikuwa yamepandishwa vioo. Ila bado Walemi hakukata tamaa, bado alijongea kwenye magari mengine na hatimaye kuna gari ambalo lilikuwa karibu yake lilishusha kioo. Ndani ya gari hiyo Walemi alimuona Daniel, alistaajabu sana hakuyaamini macho yake wala Daniel naye hakuamini kama kweli anayemuona ni Walemi wake ama macho yake yaongopa. Lakini wakati wawili hao walipokuwa katika hali ya taharuki mara ghafla taa ya kijani ikawaka kuashiria kwamba magari yameruhusiwa,hivyo dareva wa gari aliyopenda Daniel aliwasha akaondoka huku nyuma wakimuacha Walemi akiwakimbiza wakati huo akilitaja jina la Daniel.

Siku zilisonga Walemi akiwa na tumaini la kukutana na Dani wake kwa mara nyingine tena ukiachilia mbali siku ile ambayo alimuona kwenye gari ambayo ilikuwa foleni, hivyo aliendelea kufanya kazi ile ya kuomba omba huku akiwa makini sana kuwatazama wale watu wanaompa pesa akijua atakutana na Daniel. Hakika ilikuwa ni kazi yenye changamoto kwake, kwani alitukanwa sana lakini pia alidharauliwa vilivyo ila hali hiyo katu haikuweza kumfanya Walemi kushindwa kuifanya kazi hiyo ambayo iliweza kumpatia kula vile vile mavazi ya kuustili mwili wake. Maneno ya dharau na kejeri aliyokuwa akimwambia aliyaweka kando, hivyo alifanya kazi kwa umakini wa hali ya juu kabisa kwa malengo mawili tofauti. Ambapo lengo moja ni kuhakikisha anampata Dani wake, vile vile pia lengo la pili asife njaa. Lakini mwishowe malengo hayo ya Walemi yalitoweka kama mawingu yatawanyikapo baada asubuhi moja kugongwa na gari pindi alipokuwa akivuka barabara kuelekea upande wa pili..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





Hatua iliyopita tuliishia pale Walemi alipogongwa na gari wakati anavuka barabara kuelekea upande wa pili. Ikumbukwe hapa Walemi anakumbuka namna ambavyo alivyofanya kukutana na Ambrosy mwanaume Tajiri aliyempenda kwa dhati, na mwisho binti huyo alichukuwa jukumu la kumuua baada kukutana na mpenzi wake wa zamani ambaye walipotezananae kwa muda mrefu. Dhumuni kuu la Walemi kumuua Ambrosy ni kutaka kufurahi penzi kwa amani na mpenzi wake huyo aliyempenda kwa DHATI ila baada ya miaka kadhaa Ambrosy anarejea duniani, je atafanya nini? HAPA WALEMI ANAENDELEA KUKUMBUKA MAMBO ALIYOFANYIWA NA MTU HUYO AMBAYE WALIDHURUMU NAFSI YAKE.

****



ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog