Search This Blog

THE RETURN OF THE AMBROSY - 3

 






Simulizi : The Return Of The Ambrosy

Sehemu Ya Tatu (3)







"Naitwa Siwema,mtoto wangu anaitwa Rachel na mdogo wangu anaitwa Mary"

"Nikefurahi kuwa fahamu, mimi jina langu Walemi"

"Jina nzuri sana mdogo wangu. Basi na hapa ndipo ninapo ishi. Nimepanga chumba kimoja na sebule" Aliongezea kusema mama huyo ambaye alijitambulisha kwa jina Siwema. Aliongea maneno hayo huku akijivunga. Yote hayo ni baada ya kumfikisha Walemi nyumbani kwake.

"Mary unasoma kidato cha ngapi?.." Aliuliza Walemi. Mary alicheka kidogo kisha akajibu "Kidato cha tatu dada Walemi"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Safi sana kazana mdogo wangu maana maisha ya sasa hivi bila Elimu ni shida sana"

"Ni kweli nakazana pia hata dada yangu hapo nadhani anaelewa" Alisema Mary, maneno ambayo yalipelekea furaha isiyo kifani kutawala maeneo hayo. Hakika Walemi alifurahia ukarimu na unyenyekevu alionyeshewa na Walemi pamoja na mdogo wake.

Siku zilisonga Walemi akiendelea kufanya kazi na Siwema, kazi ya umamantilie huku akilipwa kutwa shilingi elfu mbili tu,pesa ambayo waliokubaliana kulipata mwisho wa mwezi. Kazi hiyo ilimfanya Walemi kupoteza ule uzuri aliokuwa nao hapo awali kipindi kile yupo kwenye himaya ya marehemu Emakulata. Walemi akawa hatamaniki, mfuke wa moto ulimchakaza maradufu lakini hakuwa na budi kuvumilia kwani hakuwa na mbinu nyingine ya kuishi jiji humo.

Siku moja jioni sana, alionekana Walemi akizozana na mteja wake.

"Naomba pesa yangu naomba pesa yangu. Sitaki uniharibia kibalua changu" Alisema Walemi akimwambia moja ya mtaje wake fundi makenika.

"Acha ujinga. Nimeshakwambia pesa yako kesho ila bado unaleta ujinga wako,sitaki unipande kichwani sawa? Nitakuvunja miguu" Alisema kwa hasira kijana huyo fundi makenika. Lakini maneno yake hayo katu hayakuweza kumtisha Walemi kwani alijua atakatwa pesa yake pindi atakapo muachia pesa hiyo huyo kijana, hivyo alizidi kumganda ili ampe pesa yake. Ugomvi ulizuka sasa, kijana huyo akampiga kofi Walemi, Walemi alilia sana ila bado alidai haki yake jambo ambalo liliweza kuzua vuta nikuvute. Ila wakati ugomvi huo unaendelea punde ilisikika sauti ikisema "Fundi unapigana saa hii je gari yangu umemaliza kutengeneza? Na kwanini umpige mtu anayedai haki yake, hujui kama unajisababishia matatizo?.."

"Hapana bro, dem huyu anazingua sana. Nimemwambia leo hela sina lakini Kawa mgumu kunielewa. Mbona yule dada wa mwanzo alikuwa muelewa? Aachane na mimi sitaki mazoea naye" Alifoka kijana huyo.

"Vipi Kuhusu gari yangu?.."

"Gari ipo sawa"

"Sawa kesho nitamtuma kijana aje kuchukua, unadai bei gani" Kijana huyo alitamka kiasi anachodai, alipewa kisha akaondoka zake huku akiwa amefura hasira na hata asimpe Walemi pesa yake. Walemi alimtazama mwishowe akaishia kusikitika kisha akaambaa na njia kurudi mgahawani kwake. Lakini kabla hajafika mbali alisikia sauti ikimuita. Haraka sana akageuka nyuma akamuona yule jamaa aliyemlipa ujira fudi makenika akimuita kwa ishara ya mkono. Walemi alitii wito. "Habari yako" Alisema jamaa huyo ambaye alishika bakora yake nzuri ya kutembelea ilihali kuanzia kofia mpaka suruali ikiwa za vitambaa huku viatu navyo vikonyesha dhahili shahili ni viatu vya ghalama, kando yake ikionekana gari aina ya Hulux. Jamaa huyo alioneakana mtanashati na mtu nadhifu kabisa asiye na njaa ya pesa.

"Nzuri tu" Alijibu Walemi kwa sauti ya unyonge huku akijifuta machozi.

"Unamdai shilingi ngapi yule jamaa?.." Walemi alitaja kiasi cha pesa anayomdai yule fudi makenika.

"Pole sana dada hizi ndio changamoto zenyewe ila usikate tamaa hakikisha unapambana mpaka unafikia malengo yako. Naitwa Ambrosy" Alisema jamaa huyo ambaye alijitambulisha jina hilo. Na alipokwisha kusema hivyo alizama mfukoni akachomoa kitita cha pesa akahesabu kiasi shilingi elfu thalathini akamkabidhi Walemi. Walemi alishtuka, alishangaa sana asiamini kama pesa yote ile ni yake. "Asante sana. Je, pesa yote hii yangu?.."

"Ahahaha hahaha ha ndio mbona ndogo sana hiyo?..." Alijibu Ambrosy wakati huo akiingia ndani ya gari yake. Na kabla hajaondoka Walemi aliisogelea gari yake kisha akamuuliza jina.

"Naitwa Ambrosy" Kwisha kusema hivyo Ambrosy aliondoka zake huku nyuma akimuacha Walemi akiwa amepigwa na butwaa.





Alistaajabu sana Walemi kupewa pesa yote ile na mwanaume ambaye hakumfahamu wala kumuona mahala popote, lakini yote kwa yote alishusha pumzi kisha akarejea kule mgahawani ili warudi nyumbani kwani alisubiriwa yeye tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mbona umechelewa?.." Aliuliza Siwema. Walemi akajibu "Kuna mteja mmoja hivi alitaka kunizungusha kuhusu hela yangu, basi nimemkaba mpaka kaitoa"

"Safi sana. Eeh hivyo ndivyo inavyotakiwa sasa. Siku zote hawenga wanasema ukicheka na nyani utavuna mabua.." Aliongezea kusema Siwema. Maneno hayo yalimfanya Walemi kuachia tabasamu kisha wakafungua mgahawa tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani.

Hayo ndio yakawa maisha ya Walemi pamoja na Siwema. Walemi alimchukulia Siwema kama dada yake, vile vile Siwema alimchukulia Walemi kama mdogo wake. Amani utani pia masihala yalitawala kati yao, abadani asilani huwezi kukuta Walimi hao wakikwaruzana zaidi ya kuelekezana pindi mmoja anapokwenda kombo. Na kwa kuwa Siwama alifahamu vema mji wa Dar es salaam kamwe hakusita kumuelekeza Walemi kasumba mbali mbali za jiji hilo, Walemi naye alimuelewa huku akimuahidi kuyatekeleza yote anayomuelekeza.

"Machoni ni kama watu lakini moyoni mwao ni chatu, na sio kila atakaye kwambia nitakusaidia jambo fulani basi kadhamilia kweli kukusaidia. La hasha Walemi mdogo wangu, hili jiji lina mambo mengi sana. Anaweza kukwambia hivyo kwa manufaa yake mwenyewe, hivyo wewe ukawa kama daraja kwake ambalo Litamfanya yeye afike kwenye kilele cha mafanikio. Walemi, wakati mimi naanza maisha ya kujitegemea kiukweli nilipata shida sana. Vishawishi vya kingono, kuna baadhi ya wanaume waliishia kunilaghai wakivunja ahadi waliyo niahidi pindi nitakapo wakamilishia matakwa yao. Ilinilazimu kukubaliana na hali harisi sababu kipindi hicho sikuwa na hili wala lile kulinganisha na ukiwa nilio nao wa kufiwa na wazazi wangu huku wakiniachia mdogo wangu wakati huo mali zote za wazee wanandugu waligombania na kutuacha mikono mitupu tukiwa hatuna pa kuanzia. Hakika lilikuwa pogo kubwa sana, lakini nilijitahidi kufanya kile ninacho kiweze ilimladi tu mdogo wangu asiache shule. Japo tuliishia maisha ya kifukara tulikilala mahali pachafu na kula mlo mmoja kwa siku ila katu sikuweza kukata tamaa mbali na kukutana na majaribu ya magumu. Nilifanya kazi bar, kazi ambayo ndiyo hiyo nilirubuniwa na kuchezewa kwa udanganyifu wa kusaidiwa, lakini bado sikukata tamaa mpaka pale Mungu aliponionyesha mlango wa mafanikio ambapo mshahara wangu wa miezi sita nilinunua matunda nakisha kuuza kando ya barabara. Mdogo mdogo mtaji ukakua, na bahati nzuri nikapata mwanaume ambaye alinijali na kunithamini,sababu alikuwa ni mtu wa kumcha Mungu, hivyo na mimi nikafuata nyendo zake sababu hapo awali sikuwa mtu wa kusari mara kwa mara. Hapo sasa nikawa na furaha, ila furaha hiyo haikudumu sana baada mume wangu huyo kufariki kwa kugongwa na gari huku akiniacha na mimba miezi sita. Nilijifungua salama na ndio huyo Richel.. Hivyo basi mdogo wangu Walemi nimeamua kumwambia haya ili ujue kabisa namna jiji hili lilivyo lakini pia utambue kwamba kila jaribu lipitalo mbele yako Mungu anamakusudi nalo. Ndingependa uwe mcha Mungu, usali bila kukoma naimani ipo siku atakunyooshea mkono wa baraka hata pindi utakapokuwa na maisha yako basi wema wa Mungu uweze kukuongoza sababu maandiko yanasema kumcha Mungu ndicho chanzo cha maarifa.. " Alisema Siwema maneno ambayo alikuwa akimuasa Walemi nyakati za usiku mara baada kumaliza kula. Walemi alishusha punzi ndefu kisha naye akasema" Usijali dada yangu, yote hayo nitayafanyia kazi. Omba tulale ili kesho tuwahi kazini?.. ". Alipokwisha kusema hivyo Walemi punde si punde Siwema aliomba maombi ya kulindwa usiku kama afanyavyo kila siku, maombi hayo yalichukua muda mchache kisha wakaingia chumbani kulala tayari kwa kuupumzisha mwili kwa niaba ya kesho.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku zilisonga, zilipita wiki mbili sasa tangu siku ile ambayo Walemi apewe pesa na Ambrosy. Lakini hatimaye kwa mara nyingine tena wawili hao wanakutana, Walemi alikuwa amebeba vyakula vya oda akiwapelekea mafundi ujenzi waliokuwa wakijenga gholofa mbali kidogo na mahali ulipo mgahawa wao, ilihali Ambrosy naye akiwa ndani ya gari akielekea katika mihangaiko yake.

"Walemiiiii.." Alipasa sauti Ambrosy kumuita Walemi ambaye naye alionekana kuwa shap kuzipiga hatua,ila aliposikia sauti hiyo alisimama akageuka kule ilipotokea sauti akawa amaekutana na tabasamu bashasha kutoka kwa kijana Ambrosy.

"Khaa Ambrosy mambo?.." Alitaharuki Walemi na wala hakusita kumsabahi. Muda huo huo Ambrosy alitoka ndani ya gari akazipiga hatua kumfuata Walemi mahala alipokuwa amesimama,alipomkaribia alisema "Pole na kazi Walemi" Walemi kabla hajamjibu Ambrosy alitabasamu kisha akajibu "Asante pole pia na wewe!.."

"Asante pia, aamh! Wapi unaelekea sasa?.."

"Naelekea hapo kuna mafundi wanawapelekea chakula"

"ooh! Hongera, na ndivyo inavyotakiwa binti kuchakarika sio kukaa nyumbani tu kama boga kila shida mpaka ulie lie. Basi kama hutojali twende upande ndani ya gari nikupeleke haraka sana iwezekanavyo"

"Aah wala usijali Ambrosy, kwanza sehemu yenyewe sio mbali hatua kadhaa tu nimefika"

"OK najua uniogopa. Je, naruhusiwa kukusindikiza?.." Walemi aliposikia swali hilo alikaa kimya kidogo wakati huo akishindwa kuelewa nini lengo hasa kijana Ambrosy ambaye anaonekana kumshobokea sana. Lakini mwishowe aliona haina haja ya kukataa ombi lake hali ya kuwa hapo awali alimasidia.

"Ndio unaruhusiwa" Alisema Walemi,ambapo Ambrosy alishusha pumzi kisha akaongozana naye.

Muda mfupi baadaye walionekana wakirudia huku wakionyesha kucheka na kutabasamu, maongezi nayo yalichukuwa nafasi kana kwamba ni watu ambao wamezoeana kitambo sana. Kitendo hicho cha wawili hao kufurahi hakika kiliwaacha midomo wazi baadhi ya watu waliowafahamu Ambrosy na Walemi. Walemi alifahamika kwa kazi yake ya mama ntilie ilihali Ambrosy naye alifahamika kwa umaridani na utajiri wa makapuni aliyonayo jiji humo.

"Mbona watu wanatutazama sana?.." Aliuliza Ambrosy. Walemi aliangua kicheko kisha akajibu "Kwetu uswahili bwana, hatupitwi na jambo. Unajua Ambrosy jinsi ulivyo wewe wanaoona kabisa mimi sina hadhi ya kuongozana nawe"

"Unamaana gani Walemi?.."

"Nina maana kwamba wewe tajiri, iweje uongozane na mama ntilie?.." Alijibu Walemi. Hapo Ambrosy hakuongeza neno lingine, na kwa kuwa tayari alikaribia gari yake, hivyo alihitaji kuendelea na safari yake. Aliingiza mkono mfukoni akachomoa kiasi kadhaa cha akamkabidhi Walemi kisha akaingia kwenye gari akaondoka zake wakati huo akiwa amepiga Walemi busu la hewani lilimfanya Walemi kuwa na sintofahamu kuhusu jambo hilo na hata usiku Walemi alipolala ghafla akajikuta akimuwaza sana kijana Ambrosy, hali hiyo ilimpelekea kuchelewa kupata lepe la usingizi kwani Ambrosy aliutawala vema ubongo wake na pole pole akajikuta akitamani walau siku moja awe naye karibu kwa siku nzima.

**********

Walemi aliachia tabasamu,baada kuyakumbuka mambo hayo kwa ufupi muda huo akiwa nje. Na hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kuanza kuvutiwa na Ambrosy mwanaume ambaye mwishowe alimpenda na kumthamini ingawa baadaye Walemi aliamua kumuua ili afurahie mapenzi na mwanaume aliyempenda kwa kipindi kirefu. Lakini punde tabasamu hilo lilipotea baada kukumbuka kuwa yupo katika wakati mgumu baada kutambua kuwa marehemu Ambrosy yupo hai..



Hakika Walemi aliogopa sana baada kutambua jambo hilo, hofu dhofu lihali ilitamalaki moyoni mwake sababu ujio wa Ambrosy duniani alijua sio wa kawaida zaidi ya kulipa kisasi juu ya dhuluma kubwa aliyofanyiwa.

"Ooh Mungu wangu nisaidie" Alijisemea Walemi akianza kwa kushusha pumzi ndefu wakati huo akilini akiendelea kuyakumbuka masuala mbali mbali aliyowahi kufanyiwa na marehemu Ambrosy, kijana ambaye alimtoa kwenye maisha ya chini mpaka Kufika maisha ya kubadilisha magari kama nguo, kula chakula anachokitaka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

********

Siku zilikatika takribani nne Walemi akiwa hajaonana na Ambrosy, lakini siku moja saa ya jioni Walemi akiwa katika harakati za kuosha vyombo ghafla alipokea wito kutoka kwa mvulana ambaye alimfahamu kwa jina Derrick. Derrick huku akihema juujuu kana kwamba alikuwa akikimbizwa alisema "Dada Walemi kuna jamaa anakuita" Walemi aliposikia maneno hayo alistisha kwanza zoezi la kuosha vyombo kisha akamuuliza Derrick "Ni nani huyo?.."

"Hata simfahamu ila ni jamaa fulani hivi mwembamba kiasi halafu kavaa shati ya kitenge na..." Kabla Derrick hsajamalizia kusema muonekano wa huyo mtu aliyemuhitaji Walemi, Walemi alimkatisha kwa kusema "Basi nimeshamfahamu, twende unielekeze mahali alipo"

Hapo hatimaye wawili hao waliongozana kuelekea kule alipo Ambrosy, walipofika Derrick alipewa pesa shilingi elfu kumi kisha akaondoka zake akiwaacha wawili hao wakiteta yao.

"Mmh habari yako Walemi" Ambrosy alimsabahi Walemi kwa sauti ya upole iliyojaa tabasamu bashasha ndani yake. Tabasamu hilo Walemi aliweza kilijibu huku akisema "Ni nzuri sijui kwako Ambrosy"

"Kwangu pia nzuri. Ammh Walemi, ni siku mbili tatu hivi zimepita mimi na wewe hatujaonana. Yote ni shauri ya harakati za hapa na pale lakini bado tupo pamoja. Vile vile kama unavuojua, wahenga waliwahi kusema kuwa kimya kingi huja na kishindo ama ukiona kobe ameinama basi ujue anatunga sheria.." Aliongezea kusema Ambrosy kisha akamalizia kwa kicheko.

" Yani wewe? Haya niambie unamaana gani sasa?.. "Aliuliza Walemi. Ambrosy hakujibu, zaidi aliingia ndani ya gari yake akatoa mfuko ambao ndani yake ulionyesha kuwa na vitu. Mfuko huo akamkabidhi Walemi halafu akasema" Pokea mzigo huu, nafikiri utaufungua pindi utakapo fika nyumbani kwanu "

" Asante sana Ambrosy, hakika siamini kama mtu wenye wadhifa huu unaweza kunijali kiasi hiki. Narudia tena kusema asante sana kaka yangu " Alifurahi Walemi. Baada ya hapo Ambrosy alizama mfukoni akachomoa kiasi cha fedha shilingi elfu hamisini akamkabidhi, kitendo ambacho kilizidi kumchanganya Walemi. Mbali na hayo Ambrosy alimwambia" Siku ukiwa na tatizo tafadhali usisite kuniambia sawa Walemi?.. " Walemi alisita kidogo lakini mwishowe alikubalina na matakwa hayo kisha Ambrosy akaondoka zake huku nyuma akimuacha Walemi akiisindikiza gari yake kwa macho,na mwishowe alishusha pumzi ndefu wakati huo akirejea mgahawani kuendelea na usafi. Lakini alipofika alishtuka kumuona Siwema akiwa katika hali ya majonzi,kitendo hicho kilimshtua sana Walemi na ndipo alipomsogelea kisha akamwambia "Dada mbona uko hivyo? Kuna tatizo? Ama nimekukosea?.."

"Wala hujanikosea mdogo wangu, ila nahisi kama hii duniani inawenyewe. Pia nafikiri katika duniani hii kuna watu wameumbiwa furaha mpaka kufa kwao" Alisema Siwema, maneno ambayo yalimuweka njia panda Walemi. Hivyo kwa taharuki alichuchumaa kisha akamuuliza "Unamaana gani dada?.." Siwema alikaa kimya kidogo lakini punde si punde alikivunja kimya hicho akasema "Nimepoteza pesa nyingi, naweza sema huu ndio mwanzo wa kuishi maisha ya kuunga unga baada mjumbe wa vikoba kuondoka na pesa yetu yote. Yani hapa nilipo nimechanganyikiwaa,wiki ijayo nitakiwa kulipa kodi bado ada ya mdogo wangu. Daah! Siwema mimi jamani" Alisema hivyo Siwema huku akitiririsha machozi.

"Pole sana dawa, lakini hupaswi kulia bali ni kumuomba Mungu aone namna gani ya kutusaidia. Nina pesa kidogo nafikiri tutaweza kumpoza mwenye nyumba halafu mengine tutajua cha kufanya. Nyamanza basi" Alisema Walemi kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake ambapo Siwema aliyafuta machozi kisha wakarejea nyumbani,na walipofika Walemi alimueleza Siwema ukaribu alioupata na kijana Ambrosy mpaka inafikia hatua ya kumpa pesa na kumnunulia zawadi. Ilikuwa ni gaoni nzuri sana, pia mikufu ya ghalama na viatu vizuri vya kike. Hakika Walemi hakuamini machoni mwake, sio yeye tu hata Siwema naye pia hakuamini ambapo kwa taharuki kubwa alisema "Ni kisema kuwa mtu huyu anania ya kukuchezea basi nitakuwa muongo, sababu asilimia kubwa wanaume wenye pesa zao huwafuata warembo na wale wasichana wenye kazi nzuri. Lakini ajabu mtu huyu kakuona wewe mpaka inafikia hatua anakununulia vitu hivi vya ghalama. Hongera sana mdogo wangu, lakini vipi ameshakwambia kuwa anakupenda?.. "

" Hapana bado ingawa machoni naona kabisa mtu yule ananipenda ila anashindwa kuniambia "Alijibu Walemi.

" Basi usijipendekeze sana kwake, ukiwa naye tulia kabisa maana siku zote wanaume wanasema mwanamke imara hajilengeshi.. "

Ukaribu wa Walemi na Ambrosy sasa ukashika kasi ingawa kila mmoja hakuweza kueleza kile kilicho ndani ya moyo wake japo Walemi alimchukulia Ambrosy kama kaka yake huku Ambrosy yeye akishindwa kutandabaisha ukweli wake kwa binti huyo mama ntilie aliyeonekana rafu kila idara. Ingawa Ambrosy licha ya kuwa kijana mtanashati katu hakuweza kujuta kupoteza muda wake akiwa naye.

Na jioni moja Ambrosy alimnunulia simu ili awe akiwasiliana pindi atakapo mkumbuka, hakika ni kitendo ambacho kilimvutia sana Walemi na baada ya siku kadhaa kupita tangu Walemi amiliki simu hatimaye Ambrosy anapata kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa njia ya simu kwani alishindwa uso kwa uso. Kijana huyo aliumbwa na uso wa haibu. Ni mazungumzo ambayo yalichukuwa muda mrefu sana, na mwisho wa yote Walemi alimtaka Ambrosy ampe siku kadhaa ili amfikirie.

"Hilo ondoa shaka Walemi, nipo tayari kukaa hata mwaka kungojea jawabu lako" Alisema Ambrosy akianza kwa kushusha pumzi ndefu.

Kweli baada wiki mbili kukatika Walemi anapata kumtumia ujumbe Ambrosy kuwa amemkubalia ombi lake, lakini wakati ujumbe huo unamfikia Ambrosy muda huo huo simu ya Walemi akaita. Ilikuwa ni namba mpya. Haraka sana Walemi alibonyeza kitufe cha kupokelea kisha akasema "Hello nani mwenzangu?.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mimi ndio yule kijana mpiga picha, kama umenisahau naitwa Dito. Nilitaka kujua vipi ile pesa niliyokwambia umeshaipata ama umeamua kukataa? Jibu moja ili nijue cha kufanya sababu mpaka sasa wanandugu wa yule mzee uliye muua kule guest wanakutafuta kwa udi na uvumba. Picha zako ninazo na tayari namba yako nayo nimeipata kwahiyo dau litaongezeka sasa. Ukizubaa naharibu kila kitu "







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog