Search This Blog

BINTI WA PILI WA MFALME - 3

 







    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alianza kuyafumbua macho yake kwa taratibu kabisa na hapo alikutana na sura ya Hancy.



    " Mozah, uko salama?? Unajisikiaje sasa???



    "Embu sogea" alizungumza Fancy na kumsogeza Hancy pembeni.



    "Embu inuka kama unaweza; alizungumza Fancy na Mozah alijitahid kuamka.



    " ammhhhh tumesharudi nyumbani, samahani kwa kuweza kuikatiza safari yenu " alizungumza Mozah.



    "Hivi wewe nimekuuliza Zaidi ya Mara ngapi kama unaumwa au lah na ukanijibu kuwa huumwi........ Kwanini lakini eti?? Aliuliza Hancy kwa hasira.



    "Samahani lakini" Alizungumza Mozah kwa sauti ya utaratibu.



    "Hiyo samahani yako inasaidia nini hivi unafikiri baba au mama yangu wangekuona katika halii hii si wangesema Mimi sikuwekei umakini......na kama ulikuwa mgonjwa kwanini nilivyoweza kukwambia twende wewe ukaja tu?? Aliendelea kufoka Hancy kwa hasira.



    " Samahani Hancy, nimeshakutaka radhi.... Naomba pia wote mnisamehe" alizungumza Mozah kwa sauti ya upole.



    "Hancy unaona unamfanya mpaka mtoto wa watu anaanza kulia?? Aliuliza Fancy kwa hasira na kusimama pale alipokuwa amekaa.



    "Sasa na wewe mbona Unataka kulia wakati wewe ndo umemgombeza mwenzako?? Aliyeweza Fancy na Hancy aliweza kutoka njee.



    "We Hancy si ninakusemesha...



    " Fancy.....nitaenda kuzungumza naye" aliongea Tom na kutoka njee katika kijumba walichoweza kufikia kwaajili ya kumtibu Mozah kabla ya kwenda nyumbani.



    Basi usilie mwaya alizungumza Fancy akimbembeleza Mozah huku Sarah na Sikitu wakiwa wanamtizama tu.



    "Hancy! Aliita Tom na Hancy aliweza kusimama huku akionekana kudondosha machozi.



    " Hancy...



    "Huyu Mwanamke ajui eti ananiumiza kiasi gani yeye anachukulia tu rahisi kwa kila jambo; hivi unajua alipodondoka nilishtuka sana nusura roho yangu initoke.. Nampenda sana Mozah sitaki kuona kitu chochote kibaya kikimtokea mbele yangu" alizungumza Hancy kwa hasira.



    "Sawa....sawa...nimekuelewa lakini punguza hasira kwanza..... Kisha tafuta muda mzuri uzungumze na Mozah kuhusu hili....... Sasa wewe unalia na yeye analia nani atambembeleza mwenzake?



    Muda ulienda na baadaye alionekana Mozah akiwa amepanda farasi mmoja na Hancy huku Hancy akiwa nyuma yake na kila mmoja akiwa kimya katika safari ile.



    " aaaaaahhhhhh me sijaipenda hii unafikiri tunaenda mazishini hata mazishini huwaga wanaimba nyimbo za mazishi alizungumza Fancy aliyeonekana kutopenda kabisa utulivu ule.



    "Mozah" aliita Fancy.



    "Abee"



    "Umeshamsemesha Hancy??



    Mozah hakujibu kitu zaidi ya kupandisha macho yake na kumtizama Hancy ambaye bado alionekana kuvimba kwa hasira.



    " aaaahhh kwani mnashida gani ninyi, si tumeshayamaliza" alizungumza Fancy



    "Kuna kitu nimesahau hivyo nitarudi nyie tangulieni alizungumza Hancy na kuanza kugeuka farasi.



    " Hancy si ungemtuma tu Tom" alishauri Sikitu.



    "Hapana nitafuata mwenyewe.



    " Sawa na Mozah na yeye?? Aliuliza Sarah aliyeonekana bado kuwa na wivu pindi awaonapo pamoja.



    "Nitapanda tu kwenye farasi wangu alizungumza Mozah na kutaka kushuka.



    " Unaenda wapi?? Aliuliza Hancy



    "Wewe si unarudi, sitaki kuwa mzigo kwako kwahiyo nitampanda farasi wangu hata hivyo naona Tom anapata shida kumuongoza.



    " Tom" aliita Hancy.



    "Wala sipati shida yoyote ile tena ninauwezo wa kuwaongoza farasi kumi nikiwa juu ya farasi wang" alizungumza na kucheka Tom



    Hancy alirudisha macho kwa Mozah ambaye alikosa cha kusema.



    "Haya sisi wengine twendeni Hancy anarudi na Mozah kule tulipoweza kutoka kasahau kitu kule....haya twendeni twendeni alizungumza na wote walianza kuvuta farasi zao kivivu kamba kwaajili ya Kuondoka.



    "Kaka aliita Fancy



    " Nini??



    "Ikumbukwe tu ya kuwa kitanda chenu kipo ngomeni" aliondoka kwa kuchka.



    "Mpuuzi huyu mtoto anadhubutuje kumwambia kaka yake maneno hayo" alizungumza Hancy na kuanza kumrudisha nyuma farasi.



    Alitembea kwa dakika Tatu kisha akasimamisha farasi.



    "Mbona umesimamisha hapa kwani haturudi tena?? Aliuliza Mozah na Ghafla alihisi mikono ya Hancy katika tumbo lake dogo.



    " Mozah......nahitaji unisamehe kwa kile nilichoweza kukifanya kwasiku ya Leo ila napenda utambue ya kuwa lile niliweza kulifanya kutokana na naumia sna pindi uwapo matatizoni na.......



    Kabla hajamaliza kuzungumza Mozah alimshika Mikono yake iliyokuwa katika tumbo lake kisha kukiegemeza kichwa chake katika kifua cha Hancy.



    "Haina haja ya kunitaka radhi Mimi pia ninamakosa katika hilo ila furaha sana baada ya kuona ya kuwa tumebaki wawili" alizungumza Mozah.



    "Nmhh alikohoa Hancy.



    " Kwanini kwani Kuna kitu ulitaka nipatia lakini ukashindwa kwasabab tuko wengi?? Aliuliza Hancy.



    "Ww unawaza nini wewe?? Aliuliza Mozah na kutoa kichwa chake katika kifua cha Hancy.



    " Hamna alijibu Hancy na kumkumbatia Mozah vizuri kabisa kisha kukilaza kichwa chake mgongoni mwake.



    "Twende basi tukachukue hicho kitu ulichoweza kukisahau.



    " Hmna nilichoweza kusahau, nilitaka tu tupate muda wetu wawili nikutake radhi" Alizungumza Hancy na kumfanya Mozah atabasamu kwa furaha na kuweza kuishika tena mikono ya Hancy kwa Mara nyingine.



    ***** katika kijiji cha Isambala *****CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nzanza na Nzenze nahitaji muende katika mji wa Isadora na chochote kinachoendelea baina ya binti yangu na mtoto wa Mfalme basi mnitaarifu" alizungumza Mfalme Nuhu



    "Na mtamtumia ndege huyu katika kurudisha taarifa na mkumbuke mnahitajika kwenda kwa Siri sana mtu yoyote asiweze kuutambua uwepo wenu katika mji ule.



    " Ndiyo Mfalme " waliitika wote kwa pamoja na kisha wakakabidhiwa ndege kisha wakaanza safari.



    "Mtabiri Tambitambi, unafikiri hii itasaidia??



    " Kwanza tufahamu maisha anayoishi alafu kisha tuta tafuta njia nyingine ya kumsaidia Mozah kama itawezekana, kwani mpaka sasa sijapata kuona damu zozote katika maono yangu" alizungumza Mtabiri Tambitambi na Bi Lunde aliweza tu kushusha pumzi ndefu pasina kuongezea neno.



    Katika upande wa pili alionekana Mganga Kipande na Malikia Samela.



    "Imekuwaje sasa??



    "Bado kazi ni ngumu sana ila nitamsaidia kwa kiasi kikubwa Sikitu akapate kuolewa na Hancy kwani kama hataolewa basi hatapata chochote.



    " siyo hata pata chochote, hatutapata chochote kwasababu..... ni mtoto wetu mtoto wangu Mimi na wewe, kwahiyo akikosa kule na huku akigundilika siyo mtoto wa mfalme basi hatutapata chochote, hivyo lazima tuhakilishe anafanikiwa" alizungumza Malikia Maua.



    Error iliyoweza kutokea Malikia Maua ni mama wa Hancy na Malikia Samela ni mama wa Sikitu hivyo ni Malikia Samela.



    Tulipoweza kuishia tunaendelea.



    **** Katika kijiji cha Isadora *****



    "Ahaaaaa kwahiyo umeweza kurudi tena??



    " Sawa tuone utaendelea kubaki hapa mpaka lini?? Ilisikika sauti ya kike ikizungumza huku akimtizama Mozah aliyekuwa akija na Hancy na kupokelewa na Tom.



    "Natumaini safari yenu ya kurejea katika ufalme imekuwa nzuri sana" alizungumza Tom akimtizama Hancy.



    "Nzuri sana" alijibu Hancy na kumtizama Mozah



    "Naweza kutembea" alizungumza na kuanza safari ya kutembea lakini alishindwa na kudondokea Mkononi mwa Hancy.



    "Siipendagi ubishi wako kabisa" alizungumza Hancy na kumuinua Mozah kwa kum beba kisha kuelekea naye ndani.



    Watumishi waliwapa heshima huku wengine walicheka na kumtazama Mozah kwa uwivu.



    Mbele walikutana na Fancy ambaye alikohoa na kumtizama Mozah aliyekuwa akimuonea aibu.



    "Nipishe" alizungumza Hancy na kumsukuma Fancy aliyeweza kudondoka chini.



    "We Hancy,wewe inamaana nilikuwa sipishi amah" alizungumza Fancy na kuwafuata nyuma.



    "Kwanini umenidondosha eti?? Aliuliza Fancy akionekana mwenye hasira.



    "Ulisimama mbele yangu kwanini?? Aliuliza Hancy na kumuweka mkewe kitandani.



    " Kwahiyo kwaajili ya Mozah, ukanidondosha Mimi??



    "Ndiyo kwaajili yake naweza kufanya chochote" alizungumza Hancy akitania na ghafla aliweza kuyaona machozi ya Fancy.



    "Fancy, nakutania tu, siyo kwamba nilimaanisha hapana" alizungumza Hancy.



    "Kwaajili ya mwanamke wako ndo unanidondosha Mimi?? Aliuliza tena Fancy.



    " Fancy, nimeshakwambia nilikuwa nakutania na haikuwa nia yangu kukudondosha" alizungumza Hancy na kumshika Mkono Fancy.



    "Fancy......aliita Mozah ila alikatishwa na sauti kali kutoka kwa Fancy.



    " Usiongee chochote wewe mwanamke, kwasabab yako Hancy amenidondosha mimi.. Unafikiri nitakusamehe kwahili?? Aliuliza Fancy na kuachia kicheko.



    "Mmeogopa eeeeeee?? Aliuliza Fancy.



    " Mjinga wewe, umenishtua eti?? Alizungumza Hancy na kumsukuma kichwa Fancy.



    "Umeogopa eeeee aliuliza Fancy na kumsogelea Mozah aliyekuwa ameshtuka.



    " Ndiyo" alizungumza Mozah na kumtizama kwa wasiwasi Fancy.



    "Usiogope Fancy ni mtu mwenye utani sana" Alizungumza Hancy.



    "Na Mara kadhaa utani huo ndo uwaga ukweli tu" alizungumza Fancy.



    "Kamletee wifi yako maji ya kunywa kwanza, ameshtuka sana eti, na wakati mwingine usifanye hichi ulichoweza kukifanya Leo"



    "Ndiyo kaka samahani, Wifi samahani.... Alizungumza Fancy kwa sauti ya upole.



    "Nimekusamehe ila umeniogopesha eti"



    "Kamlete kwanza maji ya kunywa"



    "Ndiyo" alijibu Fancy na kutoka njee.



    Wakati anatoka aliweza kupishana na Stela ambaye aliweza kumtizama kwa macho ya mashaka na kuingia ndani ya chumba kile.



    ****** *** ******



    Sarah akiwa amekaa katika chumba alichoweza andaliwa aliingia mtu na kukaa katika kiti chake.



    " Mbona umekaa tu pasina kufanya chochote kitu juu ya Hancy na Mozah??



    "Nitafanya nini ilihali Hancy tayari kwasasa ni mume wa mtu na tayari ameshaweza kuvunja ahadi tuliyoweza kuiweka tukiwa wadogo, laiti ningelijua hichi ndicho ulichoweza kuniitia ningebaki zangu kwetu"



    "Kwahiyo umeshakata tamaa mapema yote hii?? Basi humpendi Hancy hata kidogo, Mimi nakusaidia wewe katika hili"





    "Nimeshazungumza naye na tumeshaelewana ya kuwa tutabaki kuwa marafiki tu na hakuna kingine kitakachoweza kuendelea. alizungumza Sarah.



    "Watu weupe wenzako wakijua umeweza kuzidiwa kiakili na mtu mweusi basi watakudharau sana" alizungumza binti yule na kutoka njee.



    "Njoo" aliita Sarah na hatimaye alionekena Zawadi akigeuka.



    Mozah!! Ilisikika sauti ikiita



    "Abeeee mama"



    "Ammmhhhh hivi Fancy ni......... Au acha tu"



    "Kuna kitu unataka kuzungumza mama?? Aliuliza Mozah.



    " hapana achana nayo,ntachunguza mwenyewe " alizungumza Stela na kuendelea kuchana nywele za Mozah.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ila alionekana mtu mwenye wasiwasi na mashaka kidogo juu ya kitu fulani.



    "Hodi!! Ilikuwa sauti ya Hancy na Stela aliweza kucheka baada ya kumuona.



    "Karibu ndani mtoto wa Mfalme Kantala"



    Hancy alipiga hatua za kivivu na kuingia ndani ya chumba.



    "Hancy" aliita Mozah.



    "Mi nawapisha" alizungumza Stela na kutoka njee.



    "Mama sasa nani atanichana?? Aliuliza Mozah.



    Stela alimtizama Hancy na kutoka tu njee akiwa anatabasamu.



    " Kwanini ananitizama huku anacheka?? Aliuliza Hancy na kumfanya Mozah ageuke kumtizama.



    Baada ya Mozah kumuona Hancy na yeye alicheka.



    "Unanicheka kwanini?? Aliuliza Hancy na kumsogelea Mozah.



    Mozah alisimama na kumtizama usoni.



    " Kuna nini mbona unanitizama sana usoni?? Aliuliza Hancy na Mozah alimshika Mkono akampeleka kwenye kioo kisha akamkalisha.



    "Mama" alizungumza Hancy kwa kuogopa na kusimama juu.



    "Mpumbavu huyu ndo kanifanya Mimi hivi?? Alizungumza Hancy.



    " Nani huyo?? Aliuliza Mozah.



    "Hmna mtu alisema na kucheka tu Hancy kisha akamvuta Mozah katika mapaja yake



    " Nisafishe basi uso kwa mate yako" alizungumza Hancy.



    "Kwa mate yangu, kwanini mate yangu?? Aliuliza Mozah na kutaka kusimama lakini Hancy aliweza kumzuia.



    " Sawa basi Nisafishe kwa nguo yako" alizungumza Hancy na kumfanya Mozah amtizame usoni mwake kisha kucheka.



    "Nifute bana haya masinzi" alizungumza Hancy na Mozah alitoa kitambaa chake kisha akakiweka mdomoni mwake, na kuanza kumpangusa taratibu kabisa, aliweza kufika katika upande wa lipsi na Hancy alimshika Mkono.



    "Mozah naweza kukuomba kitu?



    Mozah alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo.



    " Kote umenifuta na kitambaa chako kwa mate yako je hapa mdomoni unaweza ukanifuta na lipsi zako kwa mate yako?? Aliuliza Hancy na kumfanya Mozah akiwa amebaki katika mshangao.



    "Unaongea nini wewe?? Aliuliza Mozah na kumtupia kitambaa chake Hancy.



    " Mozah....... Aliita kwa sauti ya upole na kusimama kwa kumfuata Mozah aliyekuwa amesimama.



    "Namaanisha eti, unaweza ukazifuta lipsi zangu kwa kutumia lipsi zako na mate yako??



    Mozah alibaki akimtizama Hancy usoni mwake na kujikuta akishindwa kuongea kutokana na Hancy kumshika mikono yake na pia kuziweka pumzi zake Karibu na Mozah.



    "Mi sijawahi" alizungumza Mozah.



    "Sawa kama huwezi" alizungumza Hancy na kutoka Mikono yake katika mikono ya Mozah kisha kurudi kwenye kiti na kuanza kufuta lipsi zake.



    Mozah alimzuia kisha akachukua rangi ya mdomo nyekundu kisha kumpaka Hancy mdomoni.



    "Nmekwambia sijawahi siyo kwamba siwezi, hivyo funga macho yako ili nisione aibu" alizungumza Mozah na Hancy alichukua rangi ya mdomo na kuikoleza Zaidi sehemu zake za lipsi.



    Kisha akayafumba macho yake.



    Mozah alianza kupeleka lipsi zake taratibu kabisa kwaajili ya kumbusu lakini katika mlango wao alionekana mtu akishuhudia kitendo kile na kushikwa na hasira kwa kukwangua mlango ule kisha kudondosha kitu ili tukio lile lisiweze kuendelea.



    Ilipoishia ni baada ya kuonekana mtu ambaye hakuweza kupend kile kilichokuwa kinaelekea kutokea baina ya Hancy na Mozah.



    Mozah alijitoa mapajani mwa Hancy ambaye aliweza kumrudisha na kumrukia mdomoni mwake.



    Mozah alijitahid kujitoa lakini baada ya muda sasa, yeye ndiye aliyeonekana kutokutaka kumuachia Hancy.



    "Kaka" aliita Fancy ambaye aliweza kuingia ndani na baada ya kukuta hali ile aliweza kufumba macho yake.



    "Samahani jamani, nilikuja kuleta taarifa..........Hancy baba anakuita" alizungumza Fancy.



    "Ammmhhhh tumeshamaliza alizungumza Mozah na kutaka kuondoka.



    " Bado.....alijibu Hancy na kumvuta Mkono Mozah.



    "Hancy......... Aliita Mozah.



    " Bado....rangi ya mdomo haijaisha" alizungumza Hancy na kumshika kiuno Mozah kisha kumuweka karibu kabisa na kifua chake.



    "Baba anakuita" alirudia kauli ile Fancy.



    "Mwambie hujaniona.....au mwambie yuko chumbani na mkewe Mozah" alizungumza Hancy na kujilaza mgongoni mwa Mozah.



    "Muone hata Mimi nitapata mume wangu, unaniringishia nini sasa, na ninaenda mwambia uko ndani lakini hutaki kutoka" alizungumza Fancy.



    "Kamwambie vyovyote utkavyo, lakini nisikukamate" alizungumza Hancy na kumbusu Mozah mgongoni ambaye alionekana kuona aibu.



    "Lione" alizungumza Fancy.



    "Linani?? Aliuliza Hancy na kuanza kumtoa njee Fancy



    "Hancy niache....niache wewe nimekwambia"



    "Alafu hakikisha hakuna mtu anakuja kugonga tena hapa ukae hapo....sawa"



    "Sitaki, alizungumza Fancy.



    " Utaona kama nitakupa ile Zawadi yako Leo" alizungumza Hancy.



    "Umeniletea!? Aliuliza Fancy kwa mshangao.



    " Ndiyo ila sikupi maana hunisikilizi"



    "Wewe......na kusikiliza umesema nikae hpa na hakuna mtu yoyote yule kuingia ndani....... Na ninakuhakikishia hakun mtu yoyote atakayeweza hata kujisogeza karibu na hapa; we rudi ndani .....ila mfanye polepole" alizungumza Fancy akimtania kaka Yake.



    "We mtoto wewe?? Alizungumza Hancy na kutaka kumpiga Fancy. Fancy alimsukuma na kumrudisha ndani ya chumba chake kisha akafunga mlango.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pembeni aliweza kuonekena Zawadi akishuhudia tukio hilo, hakuna na furah wala huzuni bali alionekana wa kawaida tu.



    "Hancy......aliita Mozah.



    " nini tena.....aliuliza Hancy aliyekuwa akimvua nguo ya juu Mozah aliyeweza kumzuia.



    "Tusifanye Leo bhna tufanye siku nyingine" alishauri Mozah.



    "Siku kama ipi?? Aliuliza Hancy aliyeonekana kuendelea kufungua vifungo vya nguo vya Mozah.



    " yoyote lakini siyo Leo. ......kwa maana Fancy anajua kile tunachokifanya" alizungumza Mozah.



    "Kwahiyo unaogopa??? Aliuliza Hancy aliyeweeza kuacha kufungua vifungo vingine zaidi.



    Mozah alitikisa kichwa ishara ya Ndiyo na Hancy alivirudishia vifungo vyake na kusema



    "Sawa samahani kwahili"



    Hancy alitoka njee na kumuacha Mozah ndani aliyebaki akimuita.



    Fancy alisimama pale alipokuwa amekaa



    "Heeeeeee mmeshamaliza haraka haraka hivi?? Aliuliza ila Hancy alimpita pasina kusema lolote lile.



    "We Hancy........ Aliita ila kabla hajaweza kumfuata Mozah aliweza kumfuata nyuma akimuita wakati hay yote yakiendelea bado pia Zawadi alionekana akiyatizama.



    " Hancy...... Aliita Sarah lakini Hancy aliweza kumpita.



    Sikitu akiwa njee aliweza kumuona Hancy akieleka kupanda farasi kisha akaondoka eneo lile.



    "Mbona kama ana hasira? Alijiuliza na kutazama upande ambao alihisi aliweza kumuona Nzenze



    Alitizama upande ule na kuamua kuelekea upande ambao Hancy aliweza kuondoka.



    Mozah alifika eneo lile lakini tayari Hancy alishaweza kuondoka.



    Alivuta pumzi ndefu kisha akampanda farasi kwaajili ya kumfuata Hancy nyuma.



    Muda ulienda na masaa yakapita alionekana Mozah akiwa anazunguka njee ya geti la ngome ya kifalme akimsubiri Hancy ambaye hakuweza kugundua wapi alipoweza kuelekea.



    Aliweza kumuona Hancy akija na aliweza kumsubiria ashuke kwenye Farasi alipiga hatua mbili kwaajili ya kumfuata lakini aliweza kuacha baada ya kumuona Sarah aliyeweza kufika pale.



    Hancy aliita Sarah na kumkumbatia Hancy ambaye alionekana kuwa mwingi wa mawazo.



    " Nimekutafuta sana,Kuna kitu nahitaji kukuonyesha alizungumza na kuanza kumvuta Hancy kumpeleka mahali ambako alihitaji kumpeleka.



    Mozah aliweza kujificha nyuma ya nguzo ya nyumba ili asiweze kuonekana. Hancy alipita eneo lile alihisi kama Kuna mtu mahali pale lakini alipoweza kugeuka hakuweza kuona mtu, wakati huo nao alionekana Zawad akiwa anamtizama Mozah aliyeweza kuliona tukio lile.



    Mozah alifuta machozi yake kisha kuelekea katika chumba chake kwa hali ya utaratibu kabisa.



    "Hancy........aliita Sarah na Hancy aliutoa Mkono wake.



    " Sarah nafikiri ulishanielewa...sitopenda tena tabia yako ya kunishika Mkono wala kunileta katika chumba chako, mke wangu akiliona hili hatoweza kupendezwa nalo. Hancy aliweza kutoka katika chumba cha Sarah na kuelekea ndani kwake.



    Wakati huo aliweza kuonekena mtu akicheke na kusema



    "Sarah, hivi unafikiri unauwezo wa kuwa na Hancy ; au Mimi nakusaidia wewe uwe na Hancy, hapana nahitaji uiharibu ndoa ya Hancy na Mozah kisha baada ya hapo Hancy ataniowa Mimi" kiliweza kuonekana kicheko tena cha kebehi kisha kumfuata Hancy nyuma akitaka kujua kipi kitaendelea baina yake na Mozah.



    Aligeuka nyuma na macho yake yaliweza kukutana na Zawadi ambaye alionekana kumfahamu vizuri sana na kwa kila tendo analoweza kulifanya juu ya ndoa ya Mozah na Hancy.



    Baada ya Zawadi kuweza kuonekana , alitoa heshima na kuondoka zake.



    Mozah ilisikika sauti ya kike ikiita kabla ya Mozah hajaingia katika chumba chake.



    "Abee mama" ilikuwa ni sauti ya Stela ambaye aliweza kumsogelea Mozah.



    "Una shida gani mbona unalia??



    " Hapana ...ni mdudu ameingia machoni" alizungumza Mozah.



    'Nimekuelea Mimi hivyo Naelewa....niambie mchana nilikuona wewe na Hancy mkiwa katika hali ya kutokuwa na maelewano .......Hancy ndo anakufanya unalia sindiyo?? Aliuliza Stela.



    "Hpana mama siyo Hancy" alidakia kw haraka haraka.



    Stela alimtizama bila kusema neno lolote.



    "Sawa nitamuuliza Hancy mwenyewe"



    "Hpana.... Nàfikiri ni matatizo kidogo baina yangu na yeye hivyo tutayamaliza tu; nisingependa umwambie" alizungumza Mozah.



    "Sawa twende ukale" alizungumza Stela na kumshika Mozah kisha Kuondoka naye wakati huo nao Hancy ndo alikuwa anakuja eneo lile.



    "Hancy' aliita Fancy.



    " chakula tayari twnde tukale"



    "Nimeshiba"



    "Umeshiba umekula wapi, twende tukale" alizungumza Fancy na kumshika Mkono Hancy kisha kumfikisha mpaka Katika meza ya chakula alimkuta Mozah akiwa tayari mezani alimtizama tu bila kusema neno na ndivyo ilivyokuwa kwa Mozah.



    "Mozah, kwanzia umekaa hapo hujagusa hata kijiko kwanini, vipi unajisikia kuumwa au?? Aliuliza Malikia Maua.



    " hapana Malikia Maua, nakula" alizungumza na kushuka kijiko kisha kuchukuwa chakula na kuanza kula.



    Sarah alikuja na kukaa pembeni ya Hancy ,Mozah alimtizama chini kwa chini pasina kusema chochote.



    "Jamani tuleni, alizungumza Sarah na kuanza kula.



    " Hancy huwa unapenda, ndizi kula na hii ya kwangu " alizungumza Sarah na kumuwekea ndizi mdomoni Hancy ambaye alibaki akiwa katika hali ya kutotaka kuipokea.



    "Mwenzko si anakupa ndizi" alizungumza Fancy na Hancy aliweza kuitumia ndizi ile kwa kulishwa na Sarah.



    "Mozah unashida gani mbona hulii?? Aliuliza Fancy.



    " Nimeshiba" alizungumza Mozah na kutoka katika meza ya chakula.



    Hancy alimtizama tu na kujikuta akishindwa kumeza ndizi ambayo tayari ameshaiweka mdomoni.



    Stela na yeye alisimama.



    "Unaenda wapi???



    "Naenda kumtizama binti yangu"



    "Lakini haujala chakula" alizungumza Fancy.



    "Nimeshiba" alijibu na kuondoka zake.



    "Sidhani kama ulivyoweza kufanya ni sahihi mbele ya mke wako....hata Mimi nimeshiba" alizungumza Malikia Maua na kuondoka zake.



    Mfalme Kantala na yeye aliweza kusimama na kusema



    "Mke wangu hana hamu ya kula hat mimi nimeshapoteza hamu"



    Hancy alisimama na kuondoka mezani huku Sarah akimfuata nyuma.



    Sikitu na yeye aliweza kusimama na kuondoka akifuatwa na Tom, mezani alibaki Fancy na Kipande.



    "We hujapoteza hamu ya kula??



    "Sijawahi kupoteza appetite kutoka na jambo ambalo hata halinihusu" alizungumza na kuendelea.



    "Na kutokana na. wewe ndo chanzo cha haya yote bado tu uko mezani; vipi unajisikia kula?? Aliuliza kipande

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Na utaishiaga kula tu katika falme hii kwani unajali sana tumbo lako" alizungumza Fancy na kusimama lakini macho yake yaliweza kugongana na Zawadi aliyekuwa akimtizama tu.



    "Na wewe unamtizama nan? Aliuliza Fancy kwa hasira na kuondoka.



    Mozah akiwa ameketi ndani kwake aliweza kuingia Stela.



    "Basi usilie alizungumza Stela na kwenda kumshika Mozah mabegani kisha kumtuliza kwa kumpiga piga mgongoni.



    " Basi mwanangu basi" alizungumza na kuendelea kum bembeleza.



    Huko nako alionekana Sarah akiwa nyuma ya Hancy aliyeweza kuonekana mwingi wa hasira.



    "Ngoja nikwambie kitu kimoja, Mozah ni mke wangu Mimi na nimeweza kumuowa kutokana na kuwa nampenda; hivyo sitopenda tena ukaribu wowote na wewe kwanzia sana siwzi kumliza mke wangu, kwaajili tu ya furaha yako.....Mozah akitoa machzo na Mimi huwa nayatoa moyoni mwangu, hivyo nakuomba Tafadhali rudi kwenu, kabla sijawa mtu mbya kwa upande wako". Alizungumza Hancy na kuondoka huku akimuacha Sarah ambaye alishindwa kuelewa baada ya kumuona Hancy akiwa na hasira kwa Mara ya kwanza toka aweze kumfahamu.



    " Sarah.....unashida gani mbona unalia?????? Aliuliza Fancy na Sarah aliendelea kulia zaidi



    Fancy alimkumbatia na kuanza kumcheka kwa nyuma Sarah ambaye hakuweza kuona.



    "Fancy kwanini ulinipigia simu na kuniambia Hancy anahitaji kuniona?? Aliuliza Sarah na Fancy alizidi kucheka tu kisha kuonyesha anachuki juu ya Sarah baada ya kumtoboa na pete aliyoweza kuivaa Mkononi mwake.



    " Fancy...... Aliita Sarah baada ya kuhisi maumivu.



    "Samahani" alisema Fancy na kumcheka pasina Sarah kujua hilo wakati huo nao alionekana Zawadi akimtizama Fancy kwa sura ambayo haikuweza kufahamika kama ni furaha au huzuni.



    ****** ****** ******



    Katika kijiji cha Isambala



    ******** ********** ********



    Mfalme Nuhu aliweza kupokea ujumbe ulioweza kutumwa kupitia ndege ambaye aliweza kumkabithi Nzanza na Nzenze.



    "atukuzwe Mfalme wa kijiji cha Isambala maisha kati ya Mozah na Hancy, yanaendelea vizuri na Mozah anaonekana kuwa na furaha huku aliko"



    Huo Ndiyo ujumbe ulivyokuwa ukisomeka.



    "Narizika baada ya kuona sasa Mozah anaishi vyema katika mji wa Isadora, ila vipi kuhusu Sikitu mbona hajamuelezea?? Aliendelea kuzungumza Mfalme Nuhu.



    " Kweli hajaongelea lolote kuhusu Sikitu" alizungumza Bi Lunde.



    "Naweza nitakufanya wewe, ukamuona Mozah" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    Aliweza kukaa chini na kutoa kitambaa chake chekundu kisha akakimwagia mwagia unga ambao aliweza kuunenea maneno kabla ya kuumwaga .



    Hatimaye aliweza kuonekena Mozah na Stela aliyekuwa akimbembeleza.



    "Kwanini mwanangu analia?? Kipi kimetokea?? Aliuliza Mfalme Nuhu baada ya kuona.



    ****** **** *****



    Hancy aliweza kugonga mlango kwaajili ya kuingia ndani na Stela baada ya kumuona aliweza kumuaga Mozah na kuondoka.



    Mozah aliyafuta machozi yake na kwenda kukaa kitandan, Stela alipoweza kutoka alimtizama Hancy na kumwambia maneno machache tu.



    "Baba yake akilitambua hili basi atakuja kumchukua binti yake"



    Hancy alienda karibu na Mozah na alipoweza kufika alikohoa kidogo kisha akakaa kitandani. Mozah alisogea kitandani na Hancy na yeye aliweza kumsogelea karibu kila alipozidi kusogea karibu na Mozah ndipo Mozah alipozidi kusogea.



    Hatimaye alifika mwisho wa kitanda na mozah aliamua kuinuka.



    "Mozah aliita Hancy na kumshika Mkono.



    Alitaka kuongea jambo lakini alijikuta anashindwa kuzungumza chochote na kuweza kupiga magoti mbele ya mke wake.



    " Hancy aliita Mozah kwa uwoga.



    "Unafanya nini?? Amka! Simama watumishi wako wakiona hili watafikiria vibaya, Hancy!!



    " Mozah Tafadhali naomba unisikilize kile ninachoweza kuzungumza" alizungumza Hancy.



    "Lakini si vyema kupiga magoti mbele yangu; simama kwanza kisha tuzungumze"



    "Hapana nisikilize kwanza" alizungumza Hancy na Mozah aliweza kupiga magoti akimuomba asimame.



    "Mozah.....alizungumza na kumshika mikono yote kisha kuiweka mbele ya uso wake.



    " Mimi sina mahusiano yoyote Yale na Sarah, na samahani kwa kuweza kuondoka mchana pasina kukuagaa ya kuwa ninaenda wapi?? Na.............'



    "Hancy........ Ni sawa tu Mimi nakuelewa lakini Tafadhali amka watu wakiona.......



    " haijalishi kwani nimepiga magoti mbele ya mke wangu, Mozah Tafadhali naomba msamaha wako'



    "Sawa amka kwanza" alizungumza Mozah akiinuka na kutaka kumuinua Hancy.



    "Nijibu kwanza, umenisamehe?? Aliuliza Hancy



    " Ndiyo simama basi" alizungumza Mozah na Hancy aliuliza tena.



    "Huwezi nisamehe kirahisi rahisi hivyo, pia siamini kama kweli umenisamehe" alizungumza Hancy na Mozah aliweza kumuinua.



    "Hancy.... Hata Mimi nina uhakika ya kuwa nilikukosea mchana wa Leo na Nahitaji pia msamaha kutoka kwako; Hancy ...... Aliita Mozah na Hancy aliweza kumpiga busu mdomoni.



    ***** katika kijiji cha Isambala******



    " huyu anamfanya nini binti yangu?? Aliuliza Mfalme Nuhu



    "Kwani wewe ulimfanya nini binti yangu aliuliza Bi Lunde na kuondoka zake



    " Nafikiri tumeangalia vya kutosha sasa" alizungumza Mtabiri Tambitambi na kutoa kitambaa chake.



    "Upumbavu gani huo unaendelea?? Alizungumza Malikia Samela



    " huyu mpumbavuuuuuu Sikitu ameenda kufanya nini huko huyo mjingaaaaa?? Alilalamika Malikia Samela.



    ***** **** katika mji wa Isadora **** ****



    "Hancy" aliita Mozah ambaye kwa sasa alishaweza kufika ukutani na Hancy akiendlea kumfungua nguo ya juu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hancy aliita tena Mozah na Hancy aliweza kuacha kufanya kile alichokuwa akikifanya na Mozah aliweza kupandisha nguo yake kisha kumuonyesha ishara ya mlangoni.



    Hancy aligeuka na aliweza kumuona Fancy.



    " Ni wewe tena?? Aliuliza Hancy akionyesha kuchoshwa na tabia ya Fancy.



    "Sikujua kama mnaweza mkafanya mapema nmna hii" alizungumza Fancy.



    "Kwani Kuna shida gani ikiwa tayari ni wana ndoa wanaruhusiwa kufanya hata kwa siku Mara 100 kwasababu Hancy ni halali ya Mozah na Mozah ni halali ya Hancy, tena kwasasa unatakiwa uwe na adabu na utambue ya kuwa sasa hivi kaka yako ameweza kuowa hivyo huna ruksa ya kuja tena katika chumba chake, na watumishi hakuna ruhusa ya mtu yoyote yule kuweza kufika katika chumba hichi au karibu na eneo hili kwanzia Leo na siku zote za mbeleni. Alizungumza Malikia Maua na akionyesha kuchukizwa na Fancy.



    "Mama....



    "Toka ndani ya hicho chumba" alizungumza Malikia Maua na kwenda kumtoa Fancy kisha akaufunga mlango.



    "Mama aliita Fancy lkini ghafla alipigwa kibao na Malikia Maua kisha akaanza kumkokota na kumpeleka ndani ya chumba chake.



    " Kwanini ulimpigia simu Sarah na kumwambia aje Isadora..... Kitu gani Unataka tena kutoka kwa mtoto wangu, kukubeba wewe na baba yako bado tu haikutoshi Unataka tena kuniletea tabia za baba yako kwa kumtaka mtoto wangu. Cheo cha kuitwa binti wa mfalme bado hujaridhika nacho Unataka tena kumpokonya Mozah mume wake, Kaa mbali kabisa na kijana wangu Kaa mbali naye " alizungumza Malikia Maua na kutoka hapo.



    Fancy alishikwa na hasira kuanza kutupa tupa vitu ndani.



    "Ww mwanamke wewe, unakuwa na kiburi kwa kuwa sasa wewe ni mke wa Mfalme, usijali kwani umebakiza miaka michache sana na nafasi hiyo itakuwa yangu Hancy ataniowa Mimi" Alizungumza Fancy kwa hasira.



    "Nilikwambia Mara ngapi ya kuwa hutakuwa na uwezo wa kufanya vile utakavyo pasina uwepo wa baba yako??? Aliuliza Kisude na kutabasamu.



    " Mimi pekee ndiye mwenye njia ya kukufanya wewe uwe Malikia.



    "Umeshindwa kumfanya yeye mke wako, utawezaje kumfanya mtoto wake mume wangu?? Nitapambana mwenyewe na sitaki unisaidie kwalolote, na huyu mwanamke nitamuonyesha ya kuwa Mimi ni nani?? Alizungumza Fancy na kumtizama Kisude ambaye ali pandisha mabega juu na kumtizama mwanaye.



    Njee alikuwapo Sikitu ambaye aliweza kusikia kila kitu.....



    " Mungu wngu hii ni nini hii aliuliza Sikitu akionyesha kutokuweza kuelewa kile kilichoweza kuzungumzwa.



    "Hancy.....mama anaonekana anahasira eeeeehhh"



    "Ndiyo, ila hawezi kumdhuru Fancy kwani ni mdogo wangu hivyo atamkemea tu" alizungumza Hancy aliyekuwa akipanda kitandani.



    "Malikia ameongea kwa ukali sana, au Kuna ugomvi katikati yao??



    "Sidhani alizungumza Hancy na kujifunika na shuka kwaajili ya kulala.



    " Hancy..... Naweza nikawa Mimi Ndiyo chanzo cha ugomvi wao?? Aliuliza Mozah



    "Hapana mama hajapendezwa na tabia yake ya kuingia tu ndani ya chumba changu bila kupiga hodi, ilihali kwasasa ninamke" alizungumza Hancy na kumtizama Mozah aliyekuwa akibinya binya vidole vyake



    "Mozah" aliita Hancy na kuinuka kitandani kisha kwenda kumchukua Mozah na kumketisha kitandani.



    "Huna lolote lile uliloweza kutenda juu yangu, na juu ya Fancy wala Mama yangu hivyo sipendi ujilaumu kwa makosa ambayo siyo ya kwako, hivyo acha kufikiria kile kilichoweza kutokea dakika chache zilizopita"



    "Hancy...........



    " Naomba tulale" alizungumza Hancy na kumpandisha kitandani kisha kumfunika na shuka yeye akapanda na kugeukia upande mwingine kisha akalala.



    "Hancy.....aliita Mozah na kumshika bega.



    " vipi wewe uko salama?? Aliuliza Mozah.



    Hancy alitabasamu na kumbusu Mozah katika paji la uso



    "Niko salama" alizungumza Hancy na kutabasamu.



    Mozah aliweza kumsogelea karibu na kukilaza kichwa chake katika kifua cha Hancy.



    "Hancy eeeeeeee" aliita Mozah



    "Naaam"



    "Najisikia Amani sana moyoni mwangu, kwani kwa Mara ya kwanza kabisa nimeweza kulala katika kifua chako" alizungumza Mozah



    Hancy aliweza kumkumbatia barabara na kumbusu zaidi katika nywele zake.



    "Hata Mimi najisikia vizuri sana kwani kwasiku ya Leo sihitaji hata shuka kwaajili ya joto, kwani joto la mwili wako linanitosha kwa siku ya Leo" alizungumza Hancy na Mozah aliweza kujilaza vizuri kifuani mwa Hancy.



    **** ***** *****



    "Tom" aliita Hancy na kwenda kumkumbatia



    "Ulikwenda wapi pasina kunitaarifu aise, nilikutafuta sana eti; ndipo nilipoweza kupata taarifa ya kuwa umepata safari; vipi kwanini ulienda mwenyewe kutafuta dawa!?



    " Kwasababu sitaki mazoea na mme wa mtu, untaka niongozane nawe alafu mkeo alale na nani?? Aliuliza Tom na kumfanya Hancy acheke



    "Alafu wewe"



    "Shika kwanza hii"



    "Dawa ya nini hii?? Aliuliza Hancy



    " Hii unachemsha kisha unachanganya na Supu ya samaki; ukiwa kitandani Mozah hawezi lalamika ya kuwa haumridhishi na ukinywa hii alafu ukalala naye hata kwa dakika moja tu; Mozah lazima awe mjamzito " alizungumza Tom.



    "Kwani bila hii siwezi mridhisha mke wangu, muone huyu" alizungumza Hancy.



    "Hpana lkini ni nzuri pia kwa afya yako na itakuongezea nguvu zaidi" alizungumza Tom.



    "Basi wacha nikaifanyie kazi alafu niifanyie majaribio leo usiku alizungumza Hancy na kuondoka zake eneo lile.



    Tom aliweza kukumbuka siku ambayo Hancy aliweza kumuomba ya kuwa asiweze kumpenda mwanamke ampendaye yeye.



    Pia akakumbuka siku ambayo Hancy alimuuliza anampenda nani kati ya Mozah na Sikitu.



    Anakumbuka ya kuwa kabla hajamjibu anampenda nani Hancy aliweza kumuwahi na kumwambia Mimi nampenda Mozah.



    Alirudisha kumbukumbu yake na kusema.



    " Hancy natumaini ya kuwa utamfanya Mozah awe mwanamke mwenye furaha kuliko wanawake wote duniani kwni ndiye mwanamke nimpendaye nami nitafanya njia zote za kuhakikisha ya kuwa unamfanya Mozah awe mwenye furaha " alizungumza Tom na alikuja Zawadi kwaajili ya kumpokea alichukua baadhi ya dawa na kuanza Kuondoka



    "Zawadi" aliita Tom na kumshika bega Zawadi ambaye aliweza kupata hisia kali sana.



    "Kwanini unakuwaga mkimya sana na huwa unaongea Mara moja moja sana kwani unashida gani?? Aliuliza Tom akiwa bado amemshika Zawadi aliwez kutoa Mkono wa Tom kwa kugeuka na kutaka kumjibu ila kabla hajamjibu aliweza kumuona Fancy katika chumba chake akiwa dirishani huku akimtizama Zawad aliweza kunyamaza na kuondoka zake. Tom alitizama juu na hakuweza kumuona mtu.



    " anashida gani mbona kama alikuwa anahitaji kusema jambo fulani lakini aliweza kuacha baadatu ya kutizama juu?? Alijiuliza lakini hakutilia maanani.



    Muda kidogo alionekana Zawadi akitembea katika kasiri ya kifalme aliweza kuvutwa na mtu asiyeweza kujulikana na baada ya hapo alionekana Fancy akiwa ameshikilia kisu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ulitaka kuzungumza nini juu ya Tom?? Aliuliza huku akiwa anampitishia kisu katika shingo yake.



    " hapana, hakuna chochote kile nilichkuwa nahitaji kukizungumza juu yake"



    "Nilishakwambia ya kuwa sihitaji uzungumze neno lolote lile kama sijakuruhusu, na kuwa makini sana au hutaki maisha ya mdogo wako"



    "Hpana muache mdogo wangu Tafadhali usimfanye chochote kile" alizungumza Zawadi akitokwa na machozi.



    "Basi kama unahitaji hilo; inabidi unisaidie kufanya kitu kimoja" alizungumza Fancy na kutabasamu.



    Wakati huo nao Mozah alikuwa ndani akivaa gauni lake na alikuwa akijitahidi kufunga zipu yake. Alivyoweza kusikia uwepo wa mtu ndani aliweza kumuomba amsaidie kufunga zipu huku yeye akiendelea kuvaa vaa bangili zake.



    Hancy alitizama nyuma yake na hakukuwa na mtu mwingine



    "Mbona unachukua muda mrefu hivyo; njoo nifunge nataka kutoka njee" alizungumza Mozah na Hancy aliweza kusogeza hatua kwaajili ya kwenda mbele na kufunga gauni la mkewe.



    Alishusha pumzi ndefu na kuanza kushika zipu kisha kuanza kufunga kwa kutetemeka bahati mbaya aliweza kumbana Mozah na zipu hali iliyoweza kumfanya Mozah apige kelele kidogo tu iliyopenya katikati ya ngome zake za masikio.



    "Umenibana" Alizungumza kwa sauti ndogo ilimfikia Hancy



    "Samahani" alizungumza Hancy na kumfanya Mozah ashtuke kisha ageuke na kumtizama Hancy.



    "Hancy ni wewe?? Aliuliza Mozah akijitahidi kujifunga zipu mwenyewe.



    " ammmhhhh samahani lakini nilitaka nikuulize kama utaniruhusu kufanya hivyo " alizungumza Hancy aliishika Mkono wake kwa wasiwasi.



    "Ha....ha....haina shida..... Nilidhani ni Fancy au Mama Stela ndo maana" alizungumza Mozah na kuendelea kujaribu kujifunga zipu.



    "Sawa me natoka njee nitarudi ukimaliza kuvaa" alizungumza Hancy na kuondoka kwa kuokota dawa zake alizoweza kupew na Tom.



    "Hancy.... Aliita Mozah.



    " Naomba unisaidie kufunga zipu kwamaana hakuna mtu mwingine hapa ndani" alizungumza Mozah na kuweza kumfuata Hancy kwa taratibu kabisa na baada ya kufika aliweza kugeuka nyuma na kutoa nywele zake hali iliyomfanya Hancy aweze kuuona mgongo wa Mozah vizur kabisa.



    Aliweza kuipeleka mikono yake katika nguo ya Mozah na taratibu kabisa akaanza kufunga nguo yake huku vidole vyake vingine vikiweza kuigusa ngozi ya mgongo wa Mozah ambaye aliweza kuweweseka kila alipoweza kuguswa na vidole vya Hancy.



    Baada ya kumaliza kumfunga aliweza kuzirudishia nywele za Mozah mgongoni mwake.



    "Mmhhhhh" aliguna Hancy Mozah na yeye aliweza kuguna.



    "Tayari" alisema Hancy na mlangoni alionekana Zawadi aliyeweza kuja na juice katika kikombe huku nyuma yake akiwa Fancy...



    "Wifi nimekuletea juice uweze kupata kabla ya kwenda kokote kule asubuhi hii" alizungumza Fancy na kuichukua juice ile kutoka kwa Zawad kisha kuanza kuipeleka kwa Mozah huku akitabasamu.





    Ilipoishia ni baada ya Fancy kuweza kuandaa juice na kwaajili ya kumpatia Mozah kupitia Zawadi.



    Sasa tuendelee



    "Ahsante alizungumza Mozah na kuipokea huku akimtizama Hancy.



    " ammmhhhh Me huwa naipendaga juice ya maembe kwahiyo naomba ninywe Mimi. Alizungumza Hancy na kuweza kuichukua juice kisha akainywa.



    "Hancy............ Aliita Fancy kwa mshangao mkubwa lakini tayari alishaweza kushindwa kumzuia Hancy kwani alishaweza kuimaliza.



    " Kuna shida gani, Zawdi anaweza kwenda kuiandaaa nyingine tu ila ukimuandalie mpe ya nanasi kama linapatikana alizungumza Hancy na kutoka njee



    Fancy alimtizama Mozah kwa hasira sana lakini aliishilia kucheka ili kumzubaisha na asiweze kutambua lolote lile linaloweza kuendelea katika moyo wake.



    "Siku nyingine nikikupatia kitu hakikisha ya kuwa unakunywa na kumaliza mwenyewe wala usimruhusu Hancy atie mdomo wake, Sawa wifi Mozah.



    " Ndiyo" alijibu Mozah akimtizama Zawadi ambaye alionekana mkimyaa sana na mwenye mawazo mengi sana.



    Fancy aliondoka akiwa ameikunja sura yake na mbele yake aliweza kugongana na Stela aliyekuwa akiongea katika chumba cha Mozah.



    "Anashida gani huyu?? Aliuliza Stela.



    " hamna'



    "Mimi huyu mtoto simpendi kabisa, na nahisi namchukia zaidi ya ninavyoweza kumchukia Sikitu.



    " Mama" aliita Mozah na Stela alimtizama.



    "Leo umependeza kweli" alizungumza Stela na kuweza kutoka ndani ya chumba kile na Mozah.



    ****** ****** *******



    "Sijisikii vizuri kabisa kwa siku ya Leo na nashindwa hata kutambua shida ni nini eti" alizungumza Mfalme Nuhu akimwambia Mtabiri Tambitambi.



    "Labd nimpigie Mtabibu aje akutizame" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Hapana sidhani kama shida itakuwa juu yangu, nawaza sana juu ya Mozah na nahisi Kuna jambo baya linaweza kumtokea kwa sasa" alizungumza Mfalme Nuhu.



    "Mara zote huwa unawaza kuhusu Mozah mbona sijawahi kukusikia unawaza kuhusu Sikitu?? Aliuliza Malikia Samela.



    " Tena yeye namuwaza sana kuliko Mozah, kama aliweza kutega nyoka ili aonekane mzuri kwa Malikia Maua vipi akiwa huko atamfanya nini binti yangu?? Aliuliza Mfalme Nuhu na kumfanya Malikia Samela aanze kuweweseka.



    "Au unafikiri sijui ya kuwa huo upumbavu uliweza kuufanya wewe na huyo mwanao mpumbavu?? Aliuliza Mfalme Nuhu kwa kugomba.



    " Hodi, hodi...... Atukuzwe Mfalme Nuhu wa kijiji hichi cha Isambala" alizungumza Mganga Kipande.



    Mfalme Nuhu aliweza kumtazama na kuzungumza



    "Unabahati ya kuwa hakumgusa Mozah laiti angaliweza kumgusa basi....kichwa chake kingekuwa halali ya ardhi ya Isambala. Alizungumza Mfalme na kutoka huku Mtabiri Tambitambi akitoka eneo lile lakini aliweza kusimama na kutizama juu ya anga baada ya kuhisi kitu alitizama kwa muda kisha akaondoka hata Mganga Kipande naye aliweza kufanya hivyo hivyo na kusema kama Kuna jambo baya linaenda kutokea juu ya Mozah.



    Malikia Samela alimtizama kisha akauliza " Jambo gani???



    Uliweza kuingia usiku na alionekana Mozah akiwa anaulizia kama Kuna mtu mahali alipoweza kuwepo yeye kwani kulikuwa giza sana.



    "Nani???.... We ni nani??? Hancy........Hancy...........ni wewe umenifuata huku?? Aliendelea kuuliza lakini kimya kiliendelea kutawala .



    Hatimaye viliweza kusikika vitu vikidondoka. Alishtuka na kutizama ghafla alisikia mlio wa paka na kuweza kumuona akitoka sehemu hiyo ya jiko.



    " haaaa nimeogopa sana" alizungumza na akimimina chai aliyoweza kumaliza kupika ghafla taa ziliweza kuzima na uliweza kuonekana Mkono wa mtu ukiwa umeshika kisu na ukiwa unamfuata nyuma Mozah aliyekuwa akipiga hatua za kutoka pale. Ghafla iliweza kusikika sauti ya Hancy ikimuita Mozah kwa shida na mtu yule aliweza kujificha maeneo yale.







    "Hancy.......mbona umekuja huku?? Aliuliza Mozah



    " Nilikusikia ukiniita na kuniomba msaada" alizungumza Hancy.



    "Hpana nilisikia michakacho jikoni nikahisi ni wewe kumbe alikuwa paka" alizungumza Mozah.



    "Unauhakika ni paka?? Aliuliza Hancy.



    " Ndiyo nimemuona akitoka" alizungumza Mozah.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa twende" alizungumza Hancy na kutizama upande ambao aliweza kujificha mtu ambaye alihitaji kumtoa uhai Mozah.



    Waliweza kufika ndani na Mozah aliweza kumkalisha Hancy kitandani.



    "Unauhakika lakini tofauti na paka hujaona kitu kingine?? Aliuliza Hancy.



    "Hapana, embu kunywaa kwnza hii chai unaweza jisikia vizuri na ukaacha kuelekea chooni kila Mara alizungumza Mozah na Hancy aliweza kukumbuka ya kuwa aliweza kuona kivuli cha mtu aliyekuwa ameshika kisu.



    Katika chumba kimoja aliweza kuonekena Fancy akitupa kisu chini kwa hasira.



    " upumbavu gani huu?? Nilikupa juice ili uweze kwenda chooni Mara kwa Mara nikuulie huko lakini ukampa Hancy, nataka kukuuwa bado tu unamuita Hancy......tutaona kama utaweza tena kukwepa mtego utakao fuatia" alizungumza Fancy na kutabasamu ila alihisi Kuna uwepo wa mtu nyuma yake alipoweza kutizama hakumuona mtu.





    Alielekea msalani kwake pamoja na kisu kile.



    Hakuwa amehisi vibaya ni kweli kulikuwa na mtu aliyeweza kumtizama na alikuwa Sikitu ambaye aliweza kutabasamu na kusema



    "Kazi hii itakuwa rahisi sana" alizungumza Sikitu na kutizma kama Kuna mtu aliyeweza kumuona kisha akaondoka pembeni ya moja kati ya nguzo zilizoweza kusimamisha Jumba lile la kifalme aliweza kutokeza Zawadi ambaye aliweza kujionea matokeo yote yanayoweza kuendelea katika Jumba lile la kifalme.



    Palikucha asubuhi na alionekana Mozah akiwa amelala katika Mkono wa Hancy.



    Hancy aliinuka na kuweza kumpandisha Mozah kitandani kisha akamfunika lakini aliweza kukumbuka kitendo cha kivuli kilichoweza kushika kisu kikiwa nyuma ya Mozah.



    "Ni nan huyo anayetaka kumuuwa Mozah; ni Mjomba Kisude au........hpna yeye amesafiri na bado hajaweza kurudi..... .sasa ni nani adui wa Mozah katika kasiri hii, au Sarah?? Sitamuacha huyu mwanamke hai alizungumza Hancy na kuinuka kutoka pale alipokuwa ameegema akimtizama Mozah.



    " Hancy aliweza kuita Mozah na kumshika Mkono



    "Vipi unaendleaje?! Aliuliza Mozah akijitahidi kuamka lakini alishindwa kufanya hivyo.



    " Naendelea Vizuri, kwanini Jana hukulala kitandani ukalala kwenye sakafu unaona sasa unavyo umwa sasa hivi?? Alizungumza Hancy na kumpima Mozah kwa kujishika kichwani na kumshika yeye.



    "Mwili wako ni wamoto zaidi, ngoja nikutafutie maji ya kuja kukukanda alitak kutoka njee lakini baada ya kukumbuka kile kivuli cha kisu alisita na kuanza kuita akiwa pale pale mlangoni kwa kupiga kelele na watumishi zaidi ya watatu waliweza kufika pale.



    Niletee maji ya baridi na kitambaa kisafi fanya haraka.



    " Ndiyo mtoto wa mfalme, ninyi wawili mtakaa mlangoni na wewe mmoja Kaa ndani na Mozah alafu msifunge mlango ili muweze kuonana" aliendelea kuzungumza Hncy na kuweza kutoka njee.



    "Mfalme mtaraji anatatizo gani?? Aliuliza moja kati ya wafanyakazi wale walioweza kupatiwa kazi baadye kidogo alionekana Tom akiwa ndani na Hancy huku Mozah akiwa amejipumzisha.



    " Hancy, unashida gani mbona kama una mawazo mengi hivyo "



    Hancy alimtizama Mozah kisha akamvuta Tom mbali kidogo na mahali alipo Mozah



    "Jana usiku niliweza kuona kivuli cha mtu kikiwa kimenshikia Mozah kisu kwa nyuma alipokwenda jikoni kunitengenezea chai.



    " una uhakika?? Aliuliza Tom.



    "Nina uhakika"



    "Lakini Mjomba Kisude bado hajarudi ndomaana nakuuliza una uhakika"



    "Nina uhakika bhna.... . na kivuli chenyewe nahisi ni cha mtoto wa kike "



    '"Wa kike??? Aliweza Kuuliza Tom kwa sauti ya juu



    "Kuna shida gani mbona umeshtuka?? Aliuliza Hancy



    " hapana" alijibu Tom



    "Me nahisi ni Sarah" alizungumza Hancy



    "Me na hisi ni Sikitu"



    Walitizamana wote kisha wakasema.



    "Fancy"



    "Na wewe unafikiri hichi ninachoweza kufikiria Mimi,?? Aliuliza Hancy na Tom alitikisa kichwa



    Ni baada ya Hancy na Tom kuweza kufikiria kitu juu ya Fancy.



    "Me nahisi ni rahisi kwa Fancy kuweza kumchunguza Sarah pamoja na Sikitu kwani ni wakike" alizungumza Tom na wote waliweza kukubaliana ila wakati wanaondoka na kuelekea kwa Fancy Zawadi alikuwa eneo lile na aliweza kuyasikia mazungumzo yale.

    Tom aliweza kumuona na kuendelea na safari zake huku akiwahi yeye pamoja na Hancy.



    "Hancy" aliita Mozah aliyekuwa amefika eneo lile.



    "Mozah" umefikaje.



    "Wewe......we..... Mbona umewahi kuamka mapema sana, vipi unaendleaje?? Aliuliza Mozah.



    " Naendelea vizuri kiasi" alizungumza Hancy na kumtazama Tom akimtaka aende kwa Fancy mwenyewe.



    Tom alitoa heshima na kuondoka zake.



    Tom aliendelea kwenda na mbele aliweza kukutana na Zawadi aliyekuwa amesimama mbele yake na kumtazama.



    "Zawadi, yuko wapi Fancy?? Umemuona wapi ?? Aliuliza Tom na kutaka kuelekea chumbani kwa Fancy Zawdi aliweza kumshika Mkono kabla hajamwambia kitu ulisikika mlango wa chumba cha Fancy ukifunguliwa.



    "Tom" aliita Fancy na kumuuliza.



    "Ulikuwa unazungumza na nani???



    " Na.....aligeuka na hakuweza kumuona tena Zawadi...... Hahahaha nilikuwa najiuliza kama uko ndani....vipi naweza kuingia aliuliza Tom.



    "Ndiyo karibu" alizungumza Fancy na kuingia ndani.



    Tom alitizama nyuma yake na hakuweza tena kumuona Zawadi.



    "Hii inastajabisha hii" alijizungumzia kimoyo moyo na kuingia ndani.





    ****** ******* ******



    "Nini nan huy aliyeweza kujaribu kutaka kumuuwa binti yangu?? Lazima niende huko lazima" alizungumza Mfalme Nuhu na kuweza kumuachia Ndege yule aliyeweeza kuleta ujumbe ule.



    "Lakini Mfalme Nuhu. Naamini yuko salama kwasababu Stela na Hancy wako upande wake watamkinga kwa kila jambo" alizungumza Bi Lunde.



    "Kama Sikitu yuko sehemu moja na Mozah siwezi kuwa na Amani nakwenda kumleta huyo mpumbavu huku kijijini nina uhakika ni kazi yake hii; kishoka....kishoka"



    "Ndiyo Mfalme Nuhu"



    "Andaaa farasi tunaelekea mji wa Isadora"



    "Ndiyo mfalme Nuhu" alijibu na Samela aliweza kuzisikia habari zile.



    "Kwanini anafanyaga ujinga huyu mtoto?? Alijiuliza Malikia Samela na kuingia katika chumba chake.



    ****** **** ******



    Alionekena Mozah akitembea huku akitizama nyuma yake na kuongeza mwendo zaidi huku akiendelea kutizama nyuma. Alisimama na kugeuka.



    " wa cheni kunifuata" alizungumza Mozah na Watumishi wale waliweza kusimama huku Mfalme Kantala na yeye akiwa amewasili eneo hilo.



    "Kuna shida gani binti wa mfalme Mozah?



    Wote waliweza kutoa heshima na kumsalimia Mfalme Kantal



    " Samahani mfalme wangu kama nimeweza kukusumbua kutokana na sauti yangu kupaa" alizungumza Mozah



    "Hapana nilikuwa napita maeneo haya ndipo nilipoweza kusikia sauti yako, kwanini mnamfuata mke wa mfalme mtaraji nyuma"



    "Samahani Mfalme lkini hii ni amri ya...........kabla hajaweza kutamka ya kuwa ni amri ya nani Tom aliweza kuyaingilia mazungumzo yale.



    " Mnaweza mkaenda"



    Wlitoa heshima kwa wote kisha wakaweza kuondoka zao.



    "Hii ni kazi yako na Hancy sindiyo, haya natoa amri kama mnahitaji kumlinda Mozah basi mlinde wewe au Hancy, ili asiweze kujisikia vibaya hata kidogo"



    "Ndiyo Mfalme wangu" alijibu Timo na Mfalme akaondoka huku Tom akimuonyesha Mozah njia ya kuelekea chumbani kwake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Fancy alikuwa nyuma yao na aliweza kutabasamu huku akisema.



    "Tayari nilishaweza kucheza mchezo wa kumuwekea Sarah kisu kile katika begi lake na Hancy aliweza kumfukuza sasa, amebaki huyu Mozah na nitamtumia Tom na Sikitu kwani nawaona wanaanza kuelekea katika njia zangu. Alicheka na kugeuka nyuma ambako alihisi Kuna mtu lakini baada ya kuona Hamna mtu aliweza kuondoka zake, Zawadi aliweza kutoka katika eneo aliloweza kajificha na kumtazama Fancy aliyekuwa akieleka chumbani huko huko.



    Mozah aliweza kuingia ndani na Tom.



    " Naelekea Msalani alizungumza na kumtaka Tom aweze kutoka njee.



    Tom alitoa heshima na kuweza kutoka njee huku akiwa amesimama mlangoni.



    "Najua kwa sabuni niliyoweza kuipaka katika sakafu lazima udondoke na utapiga kelele kisha Tom ataweza kukufuata huko ndani nami nitaingia na kuwafungia mlango huko kwa pamoja na Hancy ataweza kuwakuta basi mchezo wangu umekwisha na Mozah utarudi kwenu huku Tom akifukuzwa katika kasiri hii ya kifalme aliweza kucheka na kama alivyoweza kutabiri ndivyo ilivyoweza kutokea baada ya Mozah kupiga kelele Tom aliweza kwenda ndani na Fancy aliingia kisha akaufungua mlango.



    " we toka njee unawezaje kuingia ilihali niko Msalani?? Aliuliza Mozah.



    "Samahani samahani alizungumza na kutaka kufungua mlango lakini tayri ulishaweza kufungwa. Alisukuma na kusukuma lakini mlango haukuweza kufunguka.



    Wakati huo nao Hancy alikuwa akija baada ya kutoka katika kazi ya kifalme aliyoweza kupatiwa na bab yake.



    Fancy aliweza kuzisikia hatua za mtu na aliamini ni Hancy hivyo alitafuta sehemu ya kujificha asiweze kuonekana kisha akaufungua mlango huku nako ndani walishaweza kukata tamaa.



    "Mozah aliita Hancy na wote waliweza kushtuka.



    " Ha...Ha.... Hancy " aliita Mozah kwa wasiwasi.



    "Uko bafuni sawa fanya haraka utoke huko na Mimi niingie kwni nimechoka au Unataka niingie hivyo hivyo aliuliza Hancy akiwa anatania na akiwa anavua shati lake.



    " Hancy " aliita Tom na Hancy alikomea hapo kuendelea kufungua vifungo vya shati.



    "Tom" aliita na kwenda kusukuma mlango ambao uliweza kusukumika kwa urahisi wakati huo nao Fancy aliweza kujitokeza akiwa amebeba matunda. Hancy baada ya kufungua mlango alibaki akitizama tu kwani Mozah aliweza kuvaa taulo tuu na juu yake aliweza kufunikwa na shati la Tom huku Tom akibaki kifua wazi.



    Hancy aliingia ndani na kwenda kumtoa Mozah akiwa amemshikilia Mkono kwa nguvu sana.



    "Tom ..Tom.... Mozah mlikuwa mnafanya nini huko bafuni watu wawili na mbona huna shati??: aliuliza Fancy akajifanya haelewi kile kinachoweza kutokea.



    Hancy alitoa shati la Tom na kumpatia kisha akamfunika Mozah kwa shati lake.



    " Siyo hivyo unavyoweza kufikiria Hancy .........Mimi na Mozah"



    "Tom najua huwezi kufanya kitu kama hicho wala Mozah pia kwasababu nawaamini wote wawili na Mozah akinielezea vile ilivyoweza kuwa Mimi nitaamini hata asipoweza kunieleza pia. Alizungumza Hancy



    Mlango uligongwa na kijakzi aliweza kusema.



    " Mfalme Nuhu kutoka katika kijiji cha Isambala ameweza kuwasili hivyo amri ya Mfalme Kantala ni muwende mkampokee kabla hajaweza kuingia katika kasiri hii ya kifalme. alizungumza Zawadi na kuweza kuwatizama.



    "Mozah harakisha vaa nguo tuendee, Tom Tafadhali andaa farasi" Fancy alishikwa na hasira baada ya kuona ya kuwa mpango wake wote haujaweza kufanikiwa.



    Baadye walionekana wakienda kwa pamoja huku njia nzima ikiwa kimya si kweli ya kuwa Hancy hakuweza kufikiria vibaya juu yao alikuwa ni mwenye hasira sana pindi amuonapo Tom na Tom aliweza kugundua hilo baada ya kuona mikono ya Hancy inatetemeka.



    "Mozah hakikisha unatafuta muda mzuri na muelezee Hancy kila kitu ili asiweze kuweka mawazo potofu juu yangu"



    "Ndiyo" alijibu Mozah kisha akaenda kwa kasi kidogo na kuzungumza na Hancy.



    "Hancy"



    "Naam"



    "Nimechoka kumuelekeza farasi naweza kupanda farasi mmoja na wewe?? Aliuliza Mozah na Hancy aliweza kumruhusu bado mikono yake ilikuwa ikitetemeka kwa hasira na Mozah aliweza kuona hilo.



    Aliishika mikono ya Hancy ambayo iliweza kuachaa kucheza baada ya tu kuguswa na Mozah.



    " Nataka kuzungumza na wewe punguza mwendo wafarasi aliweza kuzungumza Mozah na Hancy alifanya hivyo huku Tom akisema tuongeze mwendi kidogo Fancy na Sikitu wote waliweza kufanya hivyo na Fancy aliweza kupandwa na hasira kwani mchezo wake wote uliweza kuvurugika kwa mbali alionekana Zawadi ambaye alitabasamu Sana, tena siku ya Leo aliweza hata kucheka na meno yake yakaweza kuonekena.



    "Unafikiri kila Mara utageuka mshindi, hapana Fancy siyo kila Mara" alizungumza na kuendelea kucheka .



    Ulifika usiku na wote walikuwa mezani wakipata chakula cha pamoja huku wakiendeleaa kupiga stori.



    "Siku ya kesho nitaondoka na Sikitu hivyo jiandae na Hancy kabla sijaondoka nataka kuzungumza nawe; hivyo itakubidi kesho uwahi kuamka. Alizungumza mfalme Nuhu na kucheka.



    " nimekuja katika nchi ya watu na ninaanza kupanga masharti yangu "



    Mfalme Kantala Alicheka na kusema



    "Leo umekuja ukweni bhna, ila ujio wake umetushtua kweli ungetoa tu taarifa tufanye maandalizi" alizungumza mfalme Kantala.



    Wakati huo nao Fancy aliweza kuwaza Sikitu akiondoka mpango wangu utafeli hivyo sitaweza kumruhusu mtu aweze kufanya hivyo alizungumza na hatimaye macho yake yaliweza kugongana na Malikia Maua.



    "Unawaza nini?? Aliuliza Malikia Maua.



    " Hamna"



    "Nani bora iww Hamna kuliko uwaze upumbavu, kauli ile aliyoweza kuisikia ni Tom tu kwani watu wengine walikuwa busy na mazungumzo yao.



    Tom aliweza kumtizama Fancy kisha akamtizama na Malikia na kuanza kuhisi kitu juu yao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda ule uliweza kupita na alionekana Sikitu katika chumba chake akiwaza sana.



    ITAENDELEA

BINTI WA PILI WA MFALME - 2

 







    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Pili (2)



    Harusi ilishaweza kuanza na ulikuwa ni wakati wa Mozah kuweza kuweka kauli yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtabiri Tambitambi: binti wa pili wa mfalme Nuhu wa kijiji hiki cha Isambala Mozah Nuhu, je upo tayari kuolewa na Hancy kijakazi kutoka katika kijiji cha Isadora....kumfanya mume wako katika shida na raha, tabu na furaha, huzuni na majonzi, njaa na shibe na ukienda tofauti na hivyo basi uadhibiwe na miungu wa Isambala? Kama ndiyo sema ndiyo kama hauko tayri sema hapana"





    Mozah alimtizama Hancy aliyekuwa akiisuburia kauli yake kwa hamu, akamtizama baba yake, akamtizama mama yake stelah akamtizama bibi Yake Lunde na kurudisha tena macho kwa Hancy.



    "Ndiyo" alijibu Mozah na hapo hapo ikisikika sauti ya kike ikisema hapana.



    "Mama" aliita Hancy kwa mshangao.



    "Hapana haiwezekani inawezekanaje ukamuoza binti yako kwa mtoto wa mfalme pasina taarifa zozote zile katika mji wao?? Aliuliza mama yake Hancy na Hancy akijaribu kumpotezea mama yake kile alichokuwa akizungumza.



    " Mfanyakazi mjinga sana wewe Tomimo " alizungumza mama yake Hancy na kwenda kumpiga kibao Tomimo ambaye alipiga magoti chini na kuomba msamaha.



    "Samahani malikia wangu ila nimefanya vile alivyoweza kupendekeza mtoto wa mfalme" alizungumza Tomimo.



    'M...m.....mtoto wa mfalme aliuliza malikia Samela na kuwa kama ambaye hajaelewa.



    "Nani mtoto wa mfalme wa Isadora kati ya wewe na wewe?? Aliuliza Samela.



    " Naitwa Malikia Maua kutoka katika kijiji cha Isadora, labda nimeingia kwa njia ambayo siyo nzuri lakini hata nyie mlichokifanya siyo vyema, kwani mmewezaje kumuozesha mwanangu binti yenu pasina kutoa taarifa yoyote katika mji wetu wa Isadora wala kumjulisha mmoja kati ya wazazi wake. Alizungumza Malikia Maua.



    "Ngoja.... Ngoja......ngoja.....alizungumza mfalme na kumsogelea Karibu Hancy ambaye alianza kutazama chini kwa aibu.



    "Wewe ninani??? Aliuliza mfalme Nuhu.



    " Hancy mtoto wa pekee na wa kwanza wa kiume katka familia ya Mzee Jongo, mmiliki wa mji wa Isadora " alizungumza Hancy.



    Mfalme Nuhu alimgeukia mtabiri tambitambi.



    "Kwani umeshamaliza shughuli zote za ndoa?? Aliuliza mfalme



    Kama bado naomba tuachie hapa hapa. Alizungumza Mfalme Nuhu.



    Kwa mila na desturi zetu ndoa hii tayari imeshaweza kutumia kwahiyo hatuna chaguo lingine. Alizungumza Mganga Kipande.



    "Eti wewe ni nani?? Aliuliza Mozah na kumsogelea karibu Hancy aliyekuwa akishindwa kumtazama na kuzungumza.



    Aliyeeonekana kuchoshwa kati ya wote Malikia Samela na mwanaye kwani wao Ndiyo waliyoweza kufanya mipango yote hiyo.



    ***** ****** *****



    " Mozah sikuwa nahitaji kukudanganya hapana, lakini nilihofia kukupoteza kama nitakwambia ukweli; najua hapo nitaonekana kuwa Mimi nimeijali sna nafsi yangu na kuizulumu nafsi yako, kwani nimetizama kile nafsi yangu inachokitaka na siyo kile nafsi yako ilichokuwa ikikitaka.



    "Hancy; kwanini ukaamua kuja kwa njia hii. Kwanini ukaamua kuja kama kijakazi?? Aliuliza Mozah.



    " Mozah,wasichana wengi hawanipendi Mimi kwa jinsi nilivyo bali wananipenda kulingana na cheo nilichoweza kuwa nacho, ona nilipofika katika kijiji hichi wote, waliweza kumkimbilia Tom, kwaajili ya nini kwa baba nilimpa cheo changu Mimi, lakini wewe........."



    "Hata kama lakini alitaka kuzungumza Mozah na Hancy alimuwahi.



    " Mozah me naamini umenipenda kwa jinsi nilivyo cyo kwa wadhifa nilionao, kwahiyo Tafadhali tayri sasa hivi tumeshakuwa mke na mume, nsamehe Mimi mume wako kwa kuweza kukudanganya wewe " alizungumza Hancy.



    "Nsamehe basi Mozah, alizungumza na kumshika Mkono Mozah.



    " mama yako siyo mkali?? Aliuliza Mozah na kumfanya Hancy atabasamu na kucheka.



    "Me nakuuliza wewe unacheka. Alizungumza Mozah na kutoa mikono yake mikononi mwa Hancy.



    " hapana sijakucheka wewe, alizungumza na kuchukua mikono tena ya Mozah, vipi unamuogopa?? Mama yangu hana shida japo mwanzo najua atakuletea shida ila kwa siku zinavyozidi kwenda atakuzoea na wewe, utaamini haya niyasemayo alizungumza Hancy na kusogea Karibu alipo Mozah kisha kumlaza kifuani mwake Mozah.



    "Alafu nilisahau kukwambia"



    "Nini aliuliza Mozah na kukitoa kichwa chake katika bega la Hancy.



    Hancy alirudisha kichwa kile kisha akamwambia.



    "Nina mdogo wangu wa kike jina lake Fancy, anamawenge kama wewe hivyo nahisi mtaendana.



    " Me sina mawenge alizungumza na kuinua kichwa chake tena.



    "Mozah, nimechoka nahitaji tulale" alizungumza Hancy na Mozah alijitoa kwenye bega la Hancy na kushika nguo zake za juu.



    "Saaa hizi,mbona mapema sana hata giza halijaingia vizuri tusubiri usiku usiku watu wakiwa wamelala" alizungumza Mozah na kuendelea kutengenezea gauni lake vizuri.



    "Hivi unafikiria hichi ninachoweza kufikiria Mimi; au unafikiri zaidi ya kile ninachoweza kukifikiria mimi?? Aliuliza Hancy na kumtazama Mozah kwa makini aliyekuwa akijichekesha chekesha.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Embu njoo tulale alizungumza na kumvutia Mozah upande wa ukutani kisha yeye akalala upande wa mwisho na kuweka mkono yake kiunoni mwa Mozah



    "Kama haujisikia vizuri basi natoa Mkono wangu alizungumza Hancy na kuanza kutoa Mkono wake.



    " hpana siyo hivyo, alizungumza Mozah na kuurudisha mkono wa Hancy kiunoni mwake.



    Hancy alipitisha Mkono wa pili katika kichwa cha Mozah na kutokea mbele ya uso wa Mozah huku Mozah akiushika Mkono ule kwa mikono yake miwili ; kisha kuyafunga macho yake na kuachia Tabasamu mwanana kabisa.



    Asubuhi kulipambazuka na alionekana Sikitu akinyatia maeneo ya karibu na pale waliloweza kulala Mozah na Hancy.



    Alitizama kulia na kushoto na baada ya kuona Hamna watu basi aliweza kuchungulia ndani kupitia vitundu vidogo vilivyoweza kuachia upenyo wa kuweza kuangalia ndani.



    Alipitisha macho yake na hatimaye aliweza kuwaona wakiwa wamelala kwa staili ya kukumbatiana.



    Ghafla alishikwa nyuma na mtu na kumfanya Ashtuke.



    "Hivi unafikiri ungekutwa pale na mama yake na Hancy, angekukubali sasa wewe kam mkwe kwake?? Aliweza kuuliza Malikia Samela na kumtazama mwanaye kwa hasira.



    " Lakini mama Mimi siwezi eti, na nilikwambia kabisa Mimi nampenda Hancy, wewe ukawa unang.ang.ania ya kuwa niwe na yule kijakzi, alafu na huu mpango wa kumuozesha Mozah kwa Hancy, ulikuwa mpango wako wewe , umeona sasa ilivyokuwa. alizungumza Sikitu kwa kumlalamikia mama yake.



    "Usijali kuhusu hilo, kwani nitafanya aonekane mtu asiyekuwa na bahati na Hancy, atakuowa wewe, ila utanipa ushirikiano kwa hilo" alizungumza Malikia Samela na kutazama chumba walichoweza Kulala Hancy na Mozah.



    ***** ***** *****



    Nahitaji kuelekea huko alikoweza kuelekea hyo mwanamke na Hancy " alizungumza mfalme wa kijiji cha Isadora na maandalizi yalianza kufanyika kwaajili ya safari.



    ****** ****** *****

    Hancy akiwa na Mozah katika mto mdogo huku wakiwa wamekaa chini na kuzungumza mambo yao. Aliweza kuja Samela na mwanaye Sikitu kwa nyuma kisha wakatoa kiboksi chenye nyoka na kumuachia nyoka aelekee uelekeo huo waliokuwapo huku wakicheka na kusubiri matokeo. Nyoka yule aliweza kwenda uelekeo waliokuwapo na kuanza kusogelea mguu wa Hancy aliyekuwa hana habari yeye pamoja na mkewe Mozah.



    "Mozah.... Aliita Hancy na ghafla alitulia.



    " Nini?? Aliuliza Mozah na kupandisha macho yake juu.



    "Hamna" alizungumza Hancy na kumtazama nyoka yule aliyekuwa akiishilia kwenye majani baada tu ya kumng.ata mguu wake.



    Waliendelea kukaa pale na ghafla alioweza kuonekena Malikia Samela akimleta Malikia Maua katika maeneo Yale yale aliyoweza kuwemo Hancy na Mozah.



    "Una shida gani mbona mwili wako unatoa jasho ghafla!! Aliuliza Mozah na kusimama pale alipoweza kukaa kwenye jabali mbele ya Hancy.



    " Hamna " alijitahidi kujibu Hancy ila sumu iliendelea kutembea katika mwili wake kidgo kidogo.



    "Unaumwa wapi?! Aliuliza na kuanza kumpapasa Hancy mwilini, mwili ambao tayari ulishalowa jasho.



    " Unaumwa wapi alizungumza na kutazama katika mguu ambao aliweza kuuwona unaalama ya kuumwa na nyoka.



    "Hancy" aliita kwa sauti ya juu iliyoweza kumfikia mama yake Hancy na kuanza mbio za kuelekea mahali alipoweza kuisikia kelele hiyo



    Aliweza kuchana gauni lake na kumfunga katika upande wa paja, na kukaza kwa kiasi kikubwa.



    Aliinama na kutaka kunyonya sumu kupitia mdomo wake, ila Hancy alimkataza kwa kusogeza mguu wake.



    Na hapo hapo aliweza kuingia Malikia Maua akiwa na Malikia Samela huku akihitaji msaada.



    "Hancy, Hancy, mwanangu..... Hancy.....jamani naomba msaada kwa mwanangu.



    Malikia Samela alitizama katika kichaka alichoweza kumuweka mwanaye Sikitu na hatimaye alimpa ishara ya aje pale alipo.



    Sikitu alitoka katika kichaka akiwa na Dawa tayari na alipofika alisema.



    " Niamini Malikia Mimi naweza kumtibu Hancy, alizungumza na kukitizama kidonda kile alichoweza kugongwa na nyoka.



    "Bila shaka huyu atakuwa ni nyoka wa kijani, nani hatari sana alizungumza na kutoa unga unga alioweza kuubeba katika kipoko chake na kumuwekea Hancy, huku akikamua majani aliyoweza kuwa nayo na kumiminia kwenye kidonda cha Hancy,



    Wakati huo nao alionekana Mozah aliyekuwa akija na majani aina ile ile aliyoweza kuwekewa Hancy akiwa nayo mdomoni huku akibeba magome ya mti ambao ndani ulikuwa na unga unga.



    " ahsante, ahsante sana kw kumsaidia mwenangu, alizungumza Malikia Maua na kumtaka Tom, amuinue Hancy, kisha Kuondoka naye eneo lile.



    Tom aliweza kumuona Mozah akiwa katika hali ya kuchuruzikwa na damu katika mwili wake kwni; aliweza kukimbilia kwa haraka sana na kwenda kuchukua dawa kwaajili ya Hancy aliweza kuitema na kumwaga magome Yale ya miti kisha akakaa chini huku kila mtu akiondoka eneo lile.



    Baada ya masaa kadhaa kupita.



    "Yani kama siyo mwanao huyu mkubwa sijui mwanangu angekuwa katika hali gni sasa hivi?? Alizungumza mama yake Hancy akimwambia Mfalme Nuhu ambaye alimtizama tu Sikitu na mama yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " unaendelea je Aliuliza Malikia Maua



    "Mama Mimi niko vizuri bhana alizungumza Hancy kwa kumtoa mashaka mama yake na kuingia katika chumba alichokuwa akikitumia yey na Mozah kwa siku ya Jana usiku.



    " Mozah ameenda wapi??? Aliweza kujiuliza pasina kupata majibu yoyote Yale.



    Alitoka njee na hapo aliweza kukutana uso kwa uso na Tom.



    "Mozah yuko wapi???



    " hata Mimi nashindwa kujua yuko wapi, ndani hayupo, au Kuna chochote kibaya kimeweza kumkuta Mozah? Aliuliza Hancy na kumtazama Tom.



    Wakati nakuleta nyumbani niliweza kumuona Mozah akitafuna Yale majani ya nyoka kwaajili ya kukuwekea katika kidonda chako, sasa kama hatapata dawa,majani Yale yanaweza kuwa sumu kwke, kwani aliyaweka kwenye kinywa chake.



    "Eeeeeehhhhhh alizungumza Hancy na kuanza kumtafuta Mozah huku akiita kwa sauti.



    " Kuna nini tena?? Aliuliza malikia Maua huku Samela na bintiye wakiwa wametoka njee katika kasiri ya kikao cha kifalme.



    "Aliweza kutafuna majani ya nyoka na likipita lisaa limoja hajapata dawa yoyote basi atapoteza maisha alizungumza Hancy na mama yake alishtuka sana.



    " Mbona Mimi sikutambua hilo" alizungumza na kuwapa kazi wafanyakazi wachache alioweza kuja nao wamtafute Mozah haraka sana .



    "Hancy.......ilisikika sauti ndogo na ya kuchoka ikitokea nyuma ya Hancy, Hancy aliweza kugeuka na hapo alikutana na sura ya Mozah iliyokuwa imelowa kwa jasho huku mdomo wake ukiwa umekauka sana na kuanza kupasuka hatua nazo hakuweza kuzisogeza mbele kwani mwili wake wote uliisha nguvu.



    " Mozah " aliita Hancy na kutaka kumfuata ila kabla hajafika eneo lile.



    Tayari Mozah alishaweza kudondoka chini na damu zilianza mtoka puani.



    'Mozah " aliita Hancy na kuweza kufika pale.



    Tayari damu zilishaanza kumtoka mdomoni.



    Tom alikuja na kumpatia dawa Hancy.



    Hancy aliweza kumsimamisha kichwa na kukiweka ktika mapaja yake huku akijitahidi kumnywesha mdomoni.



    Baadaye kidogo alionekana Hancy akiwa njee ya chumba kimoja huku akiwa anahangaika huku na huko, mama yake na yeye akiwa anaichezesha mikono yake...Tom akiwa amesimama sehemu moja na kukitizama chumba hicho, Mfalme Nuhu akiwa amekaa katika kiti chake cha kifalme huku akionekana kuwa na wasiwasi kwa kutingisha mguu wake huku Sikitu na mama yake wakitizamana tu kwa macho walioweza kuyafahamu wao.



    "Yuko wpi mjukuu wangu?? Aliuliza Bi Lunde aliyeonekana kuja na Stela katika eneo lile.



    " yupo ndani na Tabibu Mchome" alizungumza kijakazi Kibonge.



    "Anaendeleaje lakini?? Aliuliza Stela.



    " Anatoa damu nyingi sana hata baada ya kumpa dawa'



    "Hayo yote ni makosa yangu, kama ningeliweza kumtafuta kwa muda ule basi asingeweza kufikia hali hii" alizungumza mama yake Hancy akijilaumu.



    Tabibu Mchome aliweza kutoka njee.



    "Anaendeleaje aliuliza Mfalme Nuhu na kusimama alipokuwa amekaa.



    " Sumu haijaweza kufika katika moyo wake hivyo, dawa aliyoweza kupatiwa itamuondolea sumu yote katika mwili wake, ila atahitaji apate maziwa mengi kwaajili ya kuweza kusafisha kabisa sumu yote mwilini mwake pamoja na supu kila siku asubuhi ili mwili wake uweze kutengamaa" alizungumza Tabibu.



    "Kwahiyo tofauti na hilo, hmna tatizo lingine aliuliza Malikia Maua.



    " hpana Hamna"



    "Damu nyingi zimeweza kumtoka lakini kwnini sasa?? Aliuliza Maua.



    " Ni kwasababu sumu iliweza kujaa katika mwili wake" alijibu Tabibu Mchome.



    "Kama ndo hivyo mbona umesema haijafika katika moyo wake?? Inamaana gani tena unaposema Sumu imeshatembea katika mwili wake wote?? Aliuliza Malikia Maua.



    " Mama Tabibu amesema hayuko katika shida cha kufanya ni kutafuta hayo maziwa pamoja na supu aliyoweza kushauri" alizungumza Hancy akimshika mama yake.



    "Sawa" alijibu Malikia Maua.



    "Kisude na Pweza, mtaenda kutafuta mnyama yoyote yule mumlete hapa kwaajili ya supu ya binti yangu; alafu Tom tutaenda wote kutafuta maziwa lakini kabla ya hapo naenda ndani kumtazama anaendeleaje Alizungumza Malikia Maua na kuelekea katika chumba alichokuwa amelazwa Mozah aliingia na mwanaye Hancy.



    'Nzanza na Nzenze mtaongozana nao. Alafu Furaha na Zawadi harakisheni mkapate maziwa kutoka kwa ng.ombe sasa hivi, ...... Kishoka utaenda kupiga mbiu na kuwataarifu wanakijiji wote wenye maziwa kwmba mfalme anayahitaji kwa bei yoyote ile ili tukikosa katika kasiri yetu basi tukapate kutoka kwao. Alizungumza Mfalme Nuhu na kuingia ndani ya chumba kile.



    Akifuatwa na Tom, Stela pmoja na Bi Lunde.



    " Hivi mama naona au naota? Aliuliza Sikitu.



    "Sidhani kama hii ni ndoto, ila kupitia hapa bado tunanafasi kubwa San ya kumfanya Malikia Maua apendezwe nawe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Kivipi tena; wakati tayari umeona kabisa hilo limama linajali kuhusu Mozah wala hajui kuwa bila mimi mwanaye angeweza kufariki. Alizungumza Sikitu.



    "We fanya vile, ninavyoweza kukuagiza" alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa" alijibu na kuondoka zake.



    "We njoo hapa" alizungumza Malikia Samela.



    "Nini tena??



    "Tunatakiw tupate maziwa wa kwnza kabla ya mtu yoyote yule"



    "Nini?? Aliuliza Sikitu kwa kumshangaa mama yake.



    ***** ****** ****



    " Bi Lunde kama nilivyoweza kukwambia ya kuwa ukoo wenu una damu ya kifalme, kwhiyo hata tufanyaje hatuwezi kubadilisha utabiri huo. Alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Na kweli kwa maana tayri utabiri umeshatimia mjukuu wangu ameolewa na mtoto wa mfalme wa mji wa Isadora.



    " Vipi umeleta ile damu ya Mozah??



    "Ndiyo alizungumza Bi Lunde na kutoa kifuko cheusi kilichokuwa na damu iliyoweza kuchanganykana na udongo; bila Shaka ni damu iliyoweza kumtoka Mozah.



    Mtabiri Tambitambi aliipokea kifuko kile lakini ghafla aliweza kukidosha chini na kuweza kukitizama kwa makini sana.



    "Kuna nini tena?? Aliuliza Bi Lunde akijaribu kukitizama kile kifuko kama ataweza kuona kitu.



    " Kuna nini eti?? Aliuliza tena baada ya kutofanikiwa kuona chochote kile.



    "Damu, damu......damu itamwagika nyingi sana....siyo katika kijiji hichi tu hapana hata katika kijiji cha Isadora na vingine vingine" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Miungu wa Isambala itusaidie tuepukane na hili. Alizungumza Bi Lunde huku akionekana amejawa wasiwasi.



    ***** **** ****



    Alionekena Hancy akitizama sehemu moja.



    " Hancy unashida gani mbona unamtizama Shemeji yako hivyo?? Aliuliza Malikia Maua.



    Hancy aliguna tu na kurudisha Mkono wke katika uso wa Mozah aliyeonekana na yeye kumtazama Sikitu.



    "Mama...nafikiri Hancy pamoja na Mozah wamenielewa vibaya tu lakini Mimi siko hivyo wanavyofikiria wao, mimi ni mtu mzuri sana" Alizungumza Sikitu.



    "Kwanza nashangaa sana ulitokea wapi na Dawa ya sumu wa nyoka wa kijani, kama vile ulikuwa unatambua nitagongwana nyoka" alizungumza Hancy na kauli hiyo aliweza kuisikia Mfalme Nuhu alipotaka kuingia katika chumba kile na kumfanya asimame njee.



    "Ammmhh hamna lakini maeneo yale nilienda kuchuma dawa na kuitengeneza kwa kuwa kijakazi wangu pia aliweza kushambuliwa na sumu ya nyoka wa aina hiyo hiyo" alizungumza Sikitu kwa kujing.ata ng.ata



    Alionekana Mfalme Nuhu baadye akiwa na kijakzi wake Kibonge.



    "Mfalme Nuhu, kati ya Zawadi na Furaha hakuna hata mmoja aliyeweza kugongwana nyoka wa kijani, na kwa kipindi hiki nyoka wa kijani hawawezi kupatikana maeneo ya vyanzo vya maji, bali katikati ya misitu hivyo.......

    Na pia niliweza kuwahoji baadhi ya vijakazi wengine na Nzanza alisema aliweza kumuona Mganga Kipande akiingia na kimfuko cha kijani katika chumba cha Malikia Samela.



    " Kibonge....nataka uwende uka chunguze maeneo yote ambayo ni karibu na pale alipoweza kugongwa na nyoka Hancy na taarifa zote nilitee Mimi pia mwambie Nzanza aje hapa pamoja na zawadi na Furaha.



    "Ndiyo mfalme Nuhu" alijibu na kuondoka zake.



    Baadaye alirudi na majibu.



    "Mfalme nafikiri nyoka aliyeweza kumgonga Hancy ni nyoka aliyeweza kutumwa; kama Nzanza alivyoweza kusema yakuwa alimuona Mganga Kipande akija na kifuko cha kijani ni kweli kwani tumekuta kifuko hicho katika maeneo yale. Alizungumza Kibonge.



    " Nzanza aliita Mfalme.



    "Ndiyo mfalme"



    "Kifuko ulichoweza kukiona ndo hichi alichoweza kukileta Kibonge?? Aliuliza Mfalme.



    " Ndiyo Mfalme Nuhu na kama utakuwa unakumbukumbu vizuri, katika siku ya harusi yako na Malikia Samela aliweza kuja nacho na alitoa zawadi kupitia kifuko hichi" alizungumza Nzanza na kumfanya Mfalme akumbuke tukio hilo.



    "Inamaana Sikitu Ndiyo aliyeweza kupanga mipango yote hii, mpaka kuumia kwa Hancy, basi ntaka kujua lengo lake ni lipi; lakini kabla hajafanya kitu cha ujinga kama mama yake nataka akamatwe na apewe adhabu. Alizungumza MFALME Nuhu na ghafla alihisi Kuna mtu nyuma yake kisha akazungumza kwa sauti kubwa



    " Ni nani wewe unayedhubutu kukaa nyuma ya mfalme!?



    Ilisikika sauti ya juu ya kiume ikisema.



    "Utambulisho.



    " Mfalme wa Mji wa Isadora ameweza kufika katika ardhi ya Isambala "



    Mfalme Nuhu alisimama na kutoka katika kasiri yake na hapo aliweza kukutana macho kwa macho na Mfalme wa Isadora.



    "Baba aliita Hancy baada ya kutoka katika chumba alichokuwepo.



    " Mfalme " aliita Malikia Maua na kutazama chini.



    "Huyu ndo Mfalme wa Isador?? Alijikuta akiuliza na Malikia Samela.



    " Kumbe Hancy ni mzuri kama baba yake" alijikuta akizungumza Sikitu na kuachia Tabasamu.



    "Umefuata nini huku?? Aliuliza Hancy.



    "Nimekuj kukifuata kile ulichoweza kukifuata ww na mama yako huku" Alizungumza Mfalme na akimtizama mwanaye ghafla macho yake yaliweza kudondokea Mkononi mwa mwanaye.



    Alitembea hatua chache zilizoweza kubaki na kumshika Mkono ambao ulikuwa na kingozi.



    "Umeowa?? Aliuliza mfalme wa Isadora.



    "Baba... Ammmhhhh ......



    " Kwa ruhusa ya nani?? Aliuliza Mfalme.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kama hakuna ruhusa ya mtu yoyote yule kutoka katika ukoo wetu Mimi siitambui ndoa hii" alizungumza Mfalme



    Na alionekana Sikitu na mama yake wakishangilia kauli ile.



    Ni baada ya Mfalme wa Isadora kuonekana kuipinga ndoa aliyofunga Hancy na Mozah.



    "Baba, utanisamehe kwa hili lakini Mozah ni mke wangu, Mimi hivyo Haina haja ya ruhusa kutka kwa mtu yoyote yule wa ukoo wenu, kwani huyu ni mke wangu na siyo wa ukoo.

    Alizungumza Hancy.



    Mfalme wa Isadora alimtizama Hancy ambaye na yeye alimtizama baba yake.



    "Kwanzia leo nakunyang.anya cheo cha kuwa mfalme mtaraji wa mji wa Isadora na utabaki tu kuwa kama mtoto wa Mfalme kwni hilo ndo ambalo haliwezi kubadilika. Alizungumza Mfalme wa Isadora.



    "Sijali kuhusu kuwa Mfalme mtaraji wa mji wako,najali sana kuhusu mke wangu kwasasa kwani yeye ndiye furaha yangu" alizungumza Hancy na kucheka huku akimfuata baba yake na kumkumbatia.



    Hahahaha baba yake Alicheka na kumkumbatia mwanaye Hancy.



    "Ndo maana huwaga siupendi utani wao, mpaka nahisi miguu kuisha nguvu eti, alizungumza Malikia Maua.



    Na waliobaki wote walibaki wakishangaa kwani walishindwa kuelewa kipi kinaendelea.



    "Kwanini umeowa baba yngu bila kunipa taarifa ni kamsichana gani hako kamekufanya ukaowe upesi aliuliza Mfalme wa Isadora akiwa bado amekumbatiana na mwanaye.



    Hancy Alicheka tu na kumfanya Mfalme Nuhu apumue pamoja na watu wengine walioweza kubakia.



    " hivi hii ni sinema gani hii?? Aliuliza Malikia Samela na kumtazama mwanaye Sikitu aliyekuwa amebaki kinywa wazi.



    Usiku uliweza kuingia; wakiwa wamekaa wote kwa pamoja.



    Mfalme Isadora, Mfalme Nuhu, Malikia Samela, Malikia Maua, Tomimo, Mozah pamoja na Sikitu.



    "Utanisamehe Mfalme mwenzangu maana inaonekana nina kiherehere sana katika ngome za watu ila utanizoea tu, ammmhhhh kama nilivyoweza kukuta ndoa tayari imeshapita na siwezi kuipinga kutokana na kwamba anachoamua kijana wangu juu ya maisha yake basi Mimi huwa naweka Mkono wangu juu kukibariki kutokana na kwamba, ni maamuzi yake nani furaha yake; hivyo basi siwezi kulipinga hili kwani kwa mila na desturi zetu, mwanamke aliyeweza kuolewa katika koo za kifalme kisha akaachika basi mwanamke huyo hafai tena kuolewa na mtu yoyote yule hivyo siwezi kufanya hivyo kwa binti yako......... Na kingine, eti binti Mozah.



    " abeeee Mfalme wa Isadora.



    "Vipi mmeshalala??? Aliuliza Mfalme wa Isadora.



    "Sijakuelewa, Mfalme Tafadhali unaweza rudia"



    "Hancy; mmeshalala?? Aliuliza Mfalme Nuhu.



    " Mimi na...... Yani unamaanisha Mimi na Mozah?? Aliuliza Hancy.



    "Yani Mfalme kakuuliza hivi, umeshalala na mke wako??? Alizungumza Tom.



    " Eeeee tulilala jana; inamaana hamkutuona tukiingia ndani" alijibu Hancy.



    "Hakuna hata mmoja aliyeweza kuelewa hapo, ila bado hawajalala alizungumza Malikia Maua na Hancy pamoja na Mozah walitizama kisha wakajua maana ya swali waliloweza ulizwa.



    " Hapana " walijibu wote kw pamoja tena kwa sauti ya juu.



    "Sawa; ila hata mngenijibu kwa taratibu mbona ningesikia tu haikuwa na haja ya kuongea kwa nguvu hivyo" alizungumza mfalme wa Isadora jina lake Kantala.



    "Samahani Mfalme alizungumza Mozah kwa sauti ya chini.



    Huku Hancy akimtizama baba yake na kumwambia kama ulikuwa unatka kuniuliza basi ungeniuliza mwenyewe, c mpaka mbele yake" alizungumza Hancy akimtizama Mozah aliyekuwa aking.ata lipsi zake.



    Baadaye kidogo alionekana Tom akiwa nyuma ya Hancy huku akicheka



    Hancy aligeuka na kumtizama Tomimo ambaye aliacha kucheka.



    Hancy aligeuka tena mbele na Tomimo aliweza kucheka tena Hancy aligeuka kwa haraka na Tom aliweza kufunga mdomo wake.



    "Wewe.. Unanicheka Mimi eeee?? Aliuliza Hancy.



    Hapana alijibu Tom kwa kutikisa kichwa chake.



    Pouwa alijibu Hancy kwa ishara ya kidole na kugeuka mbele lakini aligeuka nyuma kwa speed na alikuta Tom akicheka.



    " Nilijua tu unanicheka alizungumza na kuanza kumkimbiza Tom huku akimpiga na vimawe vidongo alivyoweza kuviokota.



    Huku nako alionekana Mozah akiwa na Malikia Maua aliyekuwa akimcheka.



    Aligeuka na kumtizama malikia lakini alinyamaza alitabasamu tu na kugeuka mbele ila alihisi kama Malikia anamcheka Alitembea hatua tatu na kusimama alipogeuka nyuma Malikia Maua alikuwa akimtizama tu. Alitabasamu kisha akamuuliza



    "Malikia Maua eti unanicheka?? Aliuliza na kumfanya Maua acheke



    " hpn " alijibu na kumtangulia



    Hapana na anacheka alizungumza Mozah na kumtizama mama aliyeweza kumlea hata yeye alikuwa anacheka.



    Katika ufalme wa Isadora alionekana baba mmoja ambaye aliweza kuwa Mjomba wa Hancy aliyeweza kuridhishwa ufalme wa muda baada ya familia nzima ya Kifalme kuwa safarini.



    Alikitizama kiti cha Kifalme na kukisogelea kwa karibu huku akikishika na kukitizama kwa uchu wa madaraka.



    "Naamini ipo siku ipo siku tu lazima kasiri hii nitaimiliki mimi, itakuwa mikononi mwngu na nitampta tena Maua. Huyo walimuita Kisoda



    "Mjomba Kisoda unafanya nn hapo kwenye kiti cha kifalme?? Aliuliza Fancy baada ya kufika eneo lile.



    " Hamna nimemkumbuka tu baba yako ndo maana nakitizama kiti hichi" alipotezea kwa kuzungumza namna hiyo.



    "Hata na hivyo baba anakuja kesho, nasikia pia Hancy ameshaowa hivyo atakuja na wifi yangu" alizungumza Fancy na kuacha kutabasamu ghafla tu.



    Kisoda Alicheka na kushuka ngazi kadhaa zilizokuwa katika kufikia kiti cha kifalme.



    "Ahaaaa yani umesema Hancy kaowa?? Aliirudia kauli ile kwa kuwa kama anamuuliza lakini anatabasamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " ndiyo kaka yangu kaowa" alizungumza Fancy na kuibuka na kicheko kikubwa sana huku akiwaita wafanyakazi waandae nyumba vizuri kwaajili ya siku ya kesho kumkaribia mfalme Kantala pamoja na familia yake.



    Mjomba Kisoda alimtizama Fancy aliyekuwa akisherehekea sherehe ile ambayo alipanga kwnda kuiandaa yeye kwaajili ya kumkaribisha Mkwe katika familia hiyo ya kifalme.



    Kama Hancy ameshaowa inamaana siku yoyote ile atapewa ufalme,na siwezi kupambana naye akiwa tayari anacheo cha kifalme hivyo nahitajika kummalza akiwa na cheo hichi hichi cha mfalme mtaraji; na kama sitaweza kufanya hivyo basi siwezi mruhusu amuowe mwanamke mwingine tofauti na binti yangu " alizungumza Kisoda na kugeuza macho yake ambako mbele aliweza kumuona Fancy akifanya maandalizi Yale kwa furaha huku akimtizama na kumcheka.



    Usiku uliweza kuingia na Hancy alikuwa wa mwisho kuingia ndani na kumkuta mkewe Mozah akiwa ameka katika kitanda na kumsubiri yeye.



    Mozah aliweza kuinuka baada ya kumuona Hancy ameingia ndani.



    "Ww kaa tu alizungumza na kumfanya Mozah akae.



    "Umeshaandaa vitu vyote kwaajili ya safari?? Aliuliza Hancy.



    " Ndiyo tayari.



    "Sawa" alijibu Hancy na kukaa katika ncha ya pili ya kitanda kile alibaki tu akipiga piga miguu yake chini huku Mozah akipishanisha Mikono yake.



    "Hancy" aliita Mozah na kumfanya Hancy ashtuke hadi aainuke katika kitanda kile cha kamba.



    "Mimi nalala" alizungumza na Hancy alijibu Sawa lala.



    Mozah alipanda kitandani na kulala huku akiacha nafasi yamtu mmoja.



    "Mozah nahsi hutaweza kulala kwa Amani hivyo Mimi nitaenda kulala kwa Tomimo.



    Sawa alijibu Mozah na kujifunika vizuri.



    " Sawa lala salama" alizungumza Hancy na kutoka njee lakini baada ya sekunde kadhaa alirudi tena ndani na kumshtua Mozah aliyekuwa akivua nguo yake ya juu kwaajili ya Kulala.



    "Hancy" aliita kwa sauti ya uwoga na Hancy alimsogelea kwa ukaribu kabisa kisha akamshika mikono iliyokuwa imeshika nguo kifuani isidondoke na kuipandisha juu kidogo pamoja na nguo yake kwani kwa upande wa juu aliweza kupaacha wazi.



    Aliusogeza uso wa Mozah na kumpiga busu katika paji la uso huku akimfanya Mozah aishikilie kwa nguvu nguo aliyokuwa akijizuia isidondoke.



    "Mozah nakupenda mke wangu,na sitakufanya chochote kile bila ridhaa yako pia naomba uufikirie upendo wangu juu yako, Tafadhali na Mimi naomba unipende" alizungumza Hancy na kuteremsha lipsi zake mpaka puani mwa Mozah kisha akambusu na kutoka njee Mozah aliweza kuinua Mkono wake juu taratibu na kugusa paji la uso kisha akateremka mpka palipo na pua yake kisha kuigusa.



    "Hancy" aliita jina hilo kwa msisimko mkubwa huku akilisikilizia katika mwili wake.



    Hancy aliweza kusimama baada ya kufika mbali kidogo na chumba alichoweza kumuacha Mozah



    Mungu wangu kwanini moyo wangu unaenda mbio hivi?? Alijiuliza na kuugusa moyo wake.



    ****** ****** *****



    Ilionekana miguu ya kike ikielekea katika simu za Mkononi na kushika simu moja kisha akapiga na kuanza kuzungumza lugha ya kingereza



    "Hello; Sarah..... Hancy want to see u can't u come Tanzania??" ( habari Sarah Hancy anataka kukuona; vipi huwezi kuja Tanzania)



    Baada ya mazungumzo hayo alikata simu na Kuondoka eneo lile.



    Baada ya simu kukatwa aliweza kuondoka eneo lile.



    Huku nako kuliweza kukucha na alisikika jogoo akilia ishara ya kwamba tayari kumeshaweza kuwa alfajiri.



    Ndani ya chumba alichokuwa amelala Mozah alionekana akiwa bado yuko macho huku akiwa anafikiria busu aliloweza kupigwa na Hancy.



    "Mungu wangu, tayari jogoo ameshawika na kunaelekea kukucha sasa bado tu sijalala nawaza busu la Hancy inabidi nilale sasa alizungumza na kulala wakati akifanya hivyo alionekana Sikitu akiwa amesimama njee ya chumba chake na kukitizama huku akizungumza



    " hivi unafikiri nitakuachia Hancy kwa urahisi namna hii, hapana siwezi kukubali kuzidiwa na wewe hata Mara moja.....hivyo tutaongozana wote mpaka pale nitakapo hakikisha ya kuwa Hancy yuko mikononi mwangu na wewe utabaki kuitwa binti wa pili wa mfalme huku Mimi nikiitwa Malikia wa Isadora.



    Maandalizi ya kuweza kumkaribisha familia ya kifalme yaliweza kuandaliwa huku Mjomba Kisude akionyeshwa kutokupendezwa na maandalizi hayo na kubaki akimtizama Fancy ambaye alionekana akiyaendeleza maandalizi Yale.



    ****** ***** *****



    Sikitu unaelekea wapi?? Lilikuwa swali la Mfalme Nuhu.



    "Baba nataka kumsindikiza mdogo wangu nikapaone kwa wakwe zake kisha nitarejea baada ya mda kidogo alizungumza Sikitu.



    " Hapana hutaruhusiwa kwenda mahali popote pale" alizungumza Mfalme.



    "Na Kuna shida gani Sikitu akimsindikiza mdogo wake?? Aliuliza Malikia Samela.



    " Nimesema hata enda mahali popote pale.....namjua na kumtambua vizuri sana huyu hivy siwezi mruhusu akaenda mahali aendako Mozah. Alizungumza Mfalme Sikitu.



    Bi Lunde aliwatizama tu pamoja na Mtabiri Tambitambi.



    "Lakini Mfalme mwenzangu kama ameamua kumsindikiza ndugu yake ni vizuri, usimzuie mtoto kwahilo kama alivyoweza kusema ya kuwa atakaa kwa muda kisha atarudi" aliomba ruhusa Mfalme Kantala.



    "Lakini.......



    " Sijui kwanini unapendaga kumpinga mwanao Sikitu kwa kila kitu asemacho utafikiri si mtoto wako?? Alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa me nitafanya vile baba apendavyo sitaki kwenda kinyume na baba " alizungumza Sikitu na kuanza kurudi ndani.



    "Baba mi nafikiri ni vizuri kama nitaweza kwenda na dada Sikitu huko kisha atarudi baada ya muda kama alivyoweza kusema Alizungumza Mozah akimuombea Dada yake.



    "Lakini Mozah.......



    " Mfalme Nuhu Tafadhali mruhusu" aliongezea Hancy na Mfalme Nuhu hakuwa na kipingamizi tena juu yake.



    Alirudisha macho yake kwa Mtabiri Tambitambi ambaye aliweza kuyasikitikia maamuzi hayo lakini hakuwa na lakufanya.



    "Mfalme naomba nipewe ruksa ya kuongozana naye" aliomba ruhusu hiyo Stela mwanamke ambaye aliweza kumlelea Mozah



    Baada ya muda wote waliweza kupanda farasi na safari ilianza huku wakisindikizwa kwa makofi na vigelegele na wanakijiji wa Isambala huku wengine wakimwaga machozi ya furaha na mengine ya kuweza kuwakosa mabinti wote wa kifalme



    Waliweza kuondoka kwa mwendo wa haraka na baada ya muda kwenda sasa waliamua kuanza kutembea mwendo wa kawaida kabisa na farasi.



    Mozah alionekana kusinzia juu ya farasi wake na kuchoka.



    "Mozah tupumzike kwanza ndo tuendelee na safari, Unaonekana kuchoka na kusinzia juu ya farasi hiyo inaweza hatarisha maisha yako. Alizungumza Hancy.



    " hapana nimechoka kidogo tu lakini tunaweza tukaendelea na safari"



    "Lakini Mozah Hancy kasema kweli lolote laweza kutokea kama utasinzia juu ya farasi alizungumza Sikitu kwa kumuaffiki Hancy.



    " hpn Dada Sikitu wewe usijali Mimi bado ninauwezo wa kuvumilia kwa nusu saa nyingine alizungumza Mozah

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa kuwa makini basi wakati wa kuendesha farasi alizungumza Hancy na kutangulia mbele alipokuwapo Mama yake pamoja na watu wengine hivyo nyuma alibaki Mozah pamoja na Sikitu.



    Sikitu aliweza kutabasamu na kuweza kutazama kamba alizoweza kufungwa farasi aliyekuwa amepandwa na Mozah, alimtizama na Mozah kisha akacheka kidogo na kuweza kuacha kucheka alimvuta kamba farasi wake na kumfanya atembee kidogo sana zaidi ya farasi wa Mozah hivyo kumfanya Mozah awe mbele yake.



    Alitizama mbele na kuona maporomoko alimliga farasi yule teke na kumfanya aanze kasi huku akikumbuka ya kuwa kabla ya kupanda farasi huyo aliweza kwenda na kumkata kamba yake kidogo tu hivyo kila Mozah avutapo alama ile inazidi kuachia.



    Mozah alianza kupiga kelele na kuvuta kamba kwaajili ya kuweza kumsimamisha farasi lakini kamba ile iliweza kukatika na kujikuta hana cha kufanya kwaajili ya kumsaidia alibaki akipiga tu kelele huku akimshika yule farasi kwa kumkumbatia.



    Hancy aliweza muongeza farasi wake mbio kwaajili ya kwenda kumsaidia Mozah; huku Tomimo na yeye akifanya hivyo hivyo.



    Huku nyuma Mfalme Nuhu; Bi Lunde pamoja na Mtabiri Tambitambi walikuwa sehemu moja huku mtabiri akitizama vyombo vyake vya utabiri.



    "Tutafanyaje kubadilisha utabiri?? Aliuliza Mfalme Nuhu.



    "Laiti kungelikuwa na lakufanya kwaajili ya kuyazuia haya yote basi ningeyatekelezaga kabla hata hujaniuliza lakini kwasasa hakuna la kufanya kwasababu ufalme ulikuwa wa koo ya kina Bi Lunde ambaye aliweza kuingiliwa na mama yake Samela na kumfanya Mfalme wa mwanzo amuowe yeye, bado ufalme ukaendelea kuwa wa binti yake Bi Lunde lakini na yeye hakuweza kufanikiwa kwaajili ya Samela lakini kwasasa lazima Mozah afanikiwe kwaajili ya kuupata ufalme huu, na kama haitatokea hivyo basi kizazi cha Mozah lazima kiwe cha kifalme hivyo hatuwezi kubadilisha hili" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Na njia anayoweza kuitumia Sikitu ni njia mbaya sana, kwani anajifanya mwema mbele ya watu wote lakini ni nyoka mkubwa sana nyuma ya Mozah" alizungumza Bi Lunde huku akionyesha kuwa na mashaka Makubwa juu ya mjukuu wake Mozah.



    Baada ya muda alionekana Mozah akiwa amekaa chini huku Hancy akiwa amemfunika na nguo yake.



    "Unajisikiaje sasa?? Aliuliza Hancy.



    " vizuri "



    "Lakini kwanini unakuwa mbishi sana ww nilikwambia tupumzike lakini ukang.ang.ania safari, unaona sasa mpaka hata hujui saa ngapi ulimfanya Farasi aendee mbio hivi ungeenda kudondokea kule kwenye Yale maporomoko me ningenwambia nini baba yako! Alikuwa akigomba Hancy



    Hancy aliita Sikitu na kwenda kumshika mkono.



    " Inawezekana alipitiwa na usingizi lakini tayari ameshakutaka radhi si vizuri kumkaripia mbele ya watu wote hawa" alizungumza Sikitu.



    Stela alimtizama sana Sikitu na alikumbuka kabla ya safari aliweza kumuona Sikitu akiwa anamshika farasi aliyeweza kupandwa na Mozah lakini hakuweza kuwaza kitu chochote kile kibaya.



    "Ni sawa lakini Mimi pia sidhani kama hizi kamba za farasi zinaweza zikakatika zenyewe bila mtu kuzigusa alizungumza Stela na kumtizama Sikitu aliyeanza kuweweseka.



    Wtu wote walibaki wakimtizama Stela.



    " mama unaongea nini, samahani kwahichi kilichoweza kutokea ni kutokana na kutokuwa na umakini wakati naendesha ila sasa tumeshapumzika tunaweza tukaenda alizungumza na kusimama.



    "Wewe tutapanda farasi mmoja" alizungumza na kumvutia Mozah kwenye Farasi wake kisha kumpandisha na kukaa nyuma yake.



    "Safari inaweza ikaendelea" alizungumza Mfalme Kantala na wote waliweza kupanda farasi zao kisha safari ikaendelea huku nako.



    Tom alibaki akimtizama Sikitu ambaye alionyesha kumtazama kwa macho makali sana Hancy pamoja na Mozah.



    ***** ****** *****



    Jamani yamebaki masaa machache kabla ya Mfalme kuwasili ni vizuri kila mtu akaingia bafuni akaoge kisha mjipambe kwaajili ya kumpokea Mfalme mtaraji na mkewe



    Huyu alikuwa Fancy aliyeweeza kupendwa na vijakazi wote wa tawala ile kwa alikuwa mcheshi sana na mtu anayewapenda wote kwa pamoja bila kujali wadhifa wake.



    Pembeni alionekana Mjomba Kisude aliyekuwa akiwatizama wafanyakazi wakiondoka eneo lile pamoja na Fancy alielekea moja kwa moja hadi kwenye chakula ambacho kiliweza kuandaliwa kwaajili ya mke wa Hancy.



    "Cha kwanza ni kumuondoa huyu mwanamke kisha mambo mengine yatafuata" alizungumza na kutoa unga unga mweusi aliweza kuja nao katika kikaratasi kidogo alichoweza kuja nacho kisha akamiminia kwenye chakula kile na kuondoka.



    Hakufika mbali sana viliweza kuja viatu na kuweza kuonekana mikono ikikifunua kile chakula kilichoweza kutiliwa sumu.



    "Umekosea sana hii sumu yako haikupaswa kuwa hapa kwa siku ya Leo, hapana Huyo Mwanamke atakufa tena katika mikono yangu na siyo mikononi mwa watu wengine alizungumza na kutoa chakula kile kisha kukiweka kingine sampuli ile ile kisha akaita paka na kuwekea chakula kile chenye sumu na kuondoka.





    Hatimaye waliweza kufika katika kasiri ya kifalme japo ilikuwa usiku sana lakini waliweza kupokelewa kwa shangwe na vigelegele kutoka kwa wananchi wa mji huo wa Isadora.



    Mwanga hafifu ulioweza kutawala chumba cha kulia chakula uliweza kuwafanya baadhi ya watumishi katika nyumba ile wakiri kuwa Mozah ni binti mrembo sana.



    "Wifi yangu ni mrembo sana; sidhani kama Kuna mwanamke yoyote yule anayeweza kufikia uzuri wake" alizungumza Fancy na kutabasamu.



    Wakati huo wote alionekana Sikitu akimtizama Fancy ambaye naye alijikuta akimchukia kutokana na kwamba alikuwa akimsifia sana Mozah jambo amblo halikuweza kumpendeza.



    "Nafikiri ni muda mzuri wa kila mtu kuelekea ndani kwake na kulala na maswala mengine tutaweza kuzungumza kesho asubuhi tutakapokutana....Hivyo mkwe wangu naomba ukapumzike....... Ammmhhhh Zawadi!! Aliita Mfalme Kantala na Mozah alishngaa.



    " Ulivyotaja Zawadi nikajua ni yule wa kule katika kijiji chetu , kumbe ni majina tu yanafanana" alizungumza Mozah na kufanya watu wacheke.



    "Tayari umeshaweza kuandaa chumba atakacholala Hancy na mkewe?? Aliuliza Mfalme.



    "Ndiyo Mfalme Kantala" alijibu na fancy aliweza kusimama



    "Baba kwanini usiniulize .......Mimi Ndiyo nimefanya maandalizi yote juu ya kaka pamoja na wifi yangu natumaini watayapenda maandalizi yangu, twendeni nikawaonyeshe chumba chenu" alizungumza Fancy na kumshika mkono Mozah huku akimvuta kuelekea katika chumba alichoweza kukiandaa.



    Wafanyakazi wengine waliweza kuwa kuchukua Stela na Sikitu kisha kuwa peleka katika vyumba ambavyo walistahili kupumzikia huko kwa siku hiyo.



    ****** ****** ****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kulikucha asubuhi na Mjomba Kisude ambaye aliweza kufahamika kwa wadhifa wa Shemeji wa Mfalme katika falme ya Isadora.



    Aliweza kuamka akiwa mwingi wa furaha na aliweza kumuita kijakazi mmoja aliyekuwa akimfanyia usafi katika chumba chake



    "Wewe, mke wa Hancy Jana alikuja??



    " Ndiyo aliweza kuwasili"



    "Vipi kuhusu chakula alikula??



    " Ndiyo"



    "Chakula gani???



    " Kile kilichoweza kuandaliwa kwaajili yake"



    "Sawa unaweza ukaenda na sitohitaji mtu katika chumba changu kwa siku ya Leo" alizungumza Kisude na aliweza kuondoka kijakazi yule.



    Huku nyuma alitabasamu na kudai ila ikitokea ni habari za msiba juu ya mkwe wa familia hii basi asumbuliwe alitabasamu na kurudi katika kioo chake na kujitizama.



    Huku nako Hancy aliweza kuamka kutoka pale alipoweza kulala na kuelekea kitandani alipolala Mozah alimtizama kwa makini na kuanza kumpapasa nywele zake huku akitabasamu tu.



    Mozah aliweza kujigeuza na kumsogelea kwa karibu zaidi Hancy ambaye alivuta pumzi ndefu na kuanza kumsogeza Mozah taratibu kabisa akitaka kuondoka pale alipoweza kukaa ila Mozah alimsogelea karibu na kuweza kuweka Mkono wake katika kiuno cha Hancy hivyo kufanya uso wa Hancy ukutane na uso wake wakati huo bado akiwa usingizini.



    Hancy aliushika Mkono wa Mozah uliokuwa katika kiuno chake na kutaka kuutoa lakini ghafla aliweza kuingia Fancy na kumkuta katika hali ile.



    "Ooohhhh samahani nilisahau kugonga kabla sijaingia alizungumza Fancy na kumfanya Mozah ashtuke kutoka usingizini hapo ndipo macho yake yalipoweza kugongana na macho ya Hancy na wakati anaamka haraka haraka alijikuta amekutanisha lipsi zake naza Hancy pasina kutegemea, wote walijikuta wameshtuka na kushindwa kufanya kitu zaidi ya kubaki wakiwa wanatizamana.



    Fancy Alicheka na kutoka njee ya chumba kile



    Hancy alijitoa mdomoni mwa Mozah na wakati anasimama kwa haraka alijikuta anapamiana na uwa lililokuwa katika chumba hicho na kufanya tena adondoke kitandani na kuelekea moja kwa moj katika lipsi za Mozah aliyekuwa ameinuka kwaajili ya kutoka kitandani hapo na kujikuta wakiwa wamelaliana na lipsi zao zikiendana kwa Mara nyingine tena.



    *****Katika kijiji cha Isambala*****



    Alionekena Bi Lunde akiwa katika kaburi la binti yake Sarafinah na huku akiwa katika hali ya masikitiko.



    " Sarafinah uliweza kupoteza maisha na kumwacha mwanao katika dunia hii basi naomba ukapate kumlinda huko alikoweza kwenda, Tafadhali usimuache akapata matatizo uliyoweza kuyapata wewe, Mozah bado mdogo sana na hawafahamu binadamu wa njee kutokana na miaka yake mingi kuweza kuishi na mtu mmoja tu ambaye kwasasa anamfikiria kama mama, usimuache maadui zake wakautumia udhaifu wke katika kumteketeza na kumuharibia ndoa yake kwani baada ya miaka Mingi kupita Hatimaye nimeweza kuliona Tabasamu la ukweli katika uso wake; basi naomba umlinde na umtunzie mume wake.



    ****** katika kijiji cha Isadora*****



    Aliweza kutoka Kisoda na kukuta vijakazi wakiwa wamekaa sehemu moja huku wakionekana kuteta jambo fulani.... Aliweza kufika pale na waliweza kumpisha



    Alishtuka baada ya kuona paka watatu wakiwa wamekufa.



    "Ni nini kimetokea??



    " nini kimetokea hapa?? Aliuliza Mfalme Kantala na kuweza kupewa heshima na vijakazi wake.



    "Hii imekuwaje?? Aliuliza Mfalme Kantala.



    " Mfalme, Jana usiku niliweza kuona paka wakila chakula ambacho waliweza kuwekewa nahisi kilikuwa na sumu ndani yake" alizungumza Zawadi.



    "Na hicho chakula kilikuwa cha aina gani??



    "Ni chakula ambacho Fancy aliweza kuandaa kwaajili ya mke wa Hancy"



    "Na kwanini unazungumza sasa hivi?? Aliuliza Mfalme na kutaka vijakazi wake baadhi waweze kumfuata na wengine waweze kwenda kumleta Tabibu wa mji huo.



    " Ni nini hpa?? Aliweza kuuliza Maua na alipewa taarifa zile.



    "Mungu wangu binti wa watu" wote waliweza kumkimbilia katika chumba alichoweza kulala Hancy na Mozah.



    Sikitu aliweza kuyafikiria maneno Yake na kutabasamu.



    "Hivyo inamaanisha siyo Mimi mwenyewe, ninayehitaji kumuuwa Mozah bali Kuna mtu mwingine ambaye na yeye anahitaji kumuuwa, ila kwanini anahitaji kumuuwa Mozah?? Alijiuliza na kubaki akitabasamu tu.



    "Ila kabla ya kuyafahamu yote haya nahitajika kumjua ni nani ili niipate na sababu" Alicheka na kuelekea katika chumba alichoweza kufikia Mozah.



    Waliweza kuingia kwa mkupuo pasina kupiga hodi na waliweza kumkuta Hancy akizikausha nywele za Mozah kwa kuzifuta na taulo dogo.



    Aliweza kuacha na kumtizama mama yake ambaye aliweza kufika eneo lile.



    "Kuna shida gani?? Aliuliza Hancy na kumfanya Mozah afungue macho yake kisha kutizama sehemu aliyoweza kutazama Hancy.



    "Yuko wapi?? Aliuliza Mfalme Kantala na kuingia ndani akiwa na Tabibu.



    "Uko salama?? Aliuliza Mfalme na kuweza kumsukuma Hancy ambaye aliweza kudondoka chini.



    " Ndiyo Mfalme Kantala "



    "Tabibu ni huyu hapa" alizungumza na Tabibu aliweza kusogea mbele na kutoa baadhi ya vitu ambavyo aliweza kuja navyo.



    Mozah alikalishwa kitanda na Tabibu alimshika Mkono wake huku akiyafungua macho yake na kumtazama mdomoni



    "Kuna nini?? aliuliza Hancy aliyekuwa anashangaa watu walioweza kujaa katika chumba chake.



    Kuna nini?? Alimuuliza Mfanyakazi mmoja.



    " Amekula chakula chenye sumu" alizungumza na kumfanya Hancy aongee kwa sauti



    "Chakula chenye sumu?? Aliuliza kwa sauti na kumfuata Mozah ambaye alikuwa bado akipimwa na Tabibu.



    "Embu sogea" alimsogeza Tabibu na kuushika Mkono wa Mozah kisha kuyafumba macho yake.....akamfumbua mdomo na kumtazama kisha akayafumbua macho ya Mozah na kumtizama.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbona hana dalili zozote za sumu mwilini" alizungumza Hancy na baba yake alimwambia.



    "We unajua nini embu toka hapo Tabibu Zaramo ampime. Alizungumza Mfalme na Malikia Maua aliweza kumwambia mumewe.



    "Hata Hancy ni Tabibu pia; umesahau??



    " Imebaki njia moja tu ya kumtazama kama anasumu katika mwili wake au hana hivyo wote geukieni mlangoni" alizungumza Hancy na baba yake aliuliza.



    "Kwanini tutizame huko??



    "Kwasabab napomshika kwa sasa huna ruhusa ya kupaona" alizungumza Hancy.



    "Kwanini sina ruhusa ya kupaona na Mimi ni Mfalme??



    " Kwasababu wewe ni Mfalme na huyu ni mke wangu Mimi " alizungumza Hancy na Tabibu Zaramo alimtaka Mfalme ageuke.



    "Haya wote geukieni mlangoni" alitoa amri hiyo Mfalme na wote walifanya hivyo.



    Hancy alimtizama Mozah na kuanza kupeleka Mkono wake katika kifua cha Mozah huku akihema kwa nguvu sana na Mkono wake ukitetemeka Mozah alikohoa kidogo baada ya kuona Hancy anaelekezea wapi Mkono wake.



    Aliyafumba macho yake na Hancy aliweza kuusogeza Mkono wake hadi katika kifua cha Mozah kisha akafunga macho ya kuyasikilizia mapigo ya moyo.



    "Kwanini yanaenda kasi hivi?? Alijiuliza na kufumbua macho yake wakati huo nao Mozah alikuwa amelikamata shuka kwa nguvu zote huku akihema kwa kasi ya ajabu.



    Alianza kusogeza kichwa chake katika upande wa kifua cha Mozah kwa kuyasikilizia mapigo ya moyo wake na ghafla waliweza kusikia sauti ya Fancy.



    "Kuna nini mbona watu wote wapo katika chumba cha Hancy??



    Hancy aliweza kuacha kile alichokuwa akikifanya na kusema



    " Hana sumu "



    "Una uhakika?? Aliuliza Mfalme Kantala.



    " Ndiyo "



    "Sumu ya nini alizidi kuuliza Fancy ambaye alionekana kutokuelewa chochote kile.



    "Naenda kumuandalia Supu pamoja na maziwa Zawadi, Fancy na Sikitu ongozaneni nami" alitoa amri hiyo Malikia Maua na kutoka njee.



    "Wengine wote twendeni njee" alitoa kauli hiyo Mfalme Kantala na walianza kutoka njee



    "Hancy kama Kuna sehemu nyingine ambazo unapaswa kumtizama kama anasumu unaweza ukaendelea sisi tunatoka njee.



    Wote walitoka njee na alibaki Hancy pamoja na Mozah.



    Hancy alikaa chini na kuanza kumtizama sehemu za unyayo Mozah.



    " Hancy Kuna nini mbona Mimi sielew, wanasema sumu gani?? Aliuliza Mozah



    Hancy aliweza kuchukua panga lake na kutoka njee akiwa mwingi wa hasira huku Mozah akimfuata nyuma.



    Kisude aliita Hancy na kumfuata akiwa mwingi wa jazba alipomkaribia alichomoa upanga wake katika chombo alichoweza kuhifadhi.



    Ilipoishia ni baada ya Hancy kumfuata Kisude kwa Jazba akiwa amechomoa jambia lake.



    "Tunaweza tukaenda kuwinda wawili?? Aliuliza Hancy na kuachia Tabasamu ambalo hata Mozah alishindwa kuelewa kama ndicho kilichoweza kumtoa ndani kwa kasi hivyo.



    Alianza kuongoza safari na Kisude aliweza kuvuta pumzi ndefu kabla ya kumfuata tendo lile Tom aliweza kuliona na kugeuza macho yake kwa Mozah aliyeonekana kushikwa na butwaa.



    ***** katika kijiji cha Isambala ****



    " Mfalme Unaonekana kuwa mwingi wa mawazo alizungumza Malikia Samela na Mfalme Kantala alibaki akimtizama tu.



    "Endapo binti yako atamuumiza binti yangu kwa njia yoyote ile Mimi siwezi kumsamehe kwahilo" alizungumza na kumtazama.



    "Unachokiongea mimi sikuelewi" alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa, ila nahisi ujumbe utamfikishia alizungumza na kusimama ila kabla hajaondoka eneo lile alisimama na kuzungumza maneno kadhaa



    " Mkumbushe Mganga Kipande aje achukue hicho kikapu chake alichoweza kuletea nyoka "



    "Ki....Ki...kikapu gani?? Aliuliza kwa mgugumizo na Mfalme Nuhu aliondoka zake.



    *** Katika kijiji cha Isadora *****



    Wakiwa mezani wakipata chakula wote kwa pamoja huku meza ikionekana kuwa kimya.



    " Mimi nitaenda kula ndani alizungumza Mozah na kuinuka mezani.



    "Wewe Ndiye malikia mtaraji wa mji huu hupaswi kula sehemu tofauti na hapa tunapokula sisi" alizungumza Hancy akiwa ameushika Mkono wa Mozah na kumfanya akae tena.



    "Wifi usijali kuhusu kile kilichoweza kutokea siku ya Leo, nakuahidi ya kuwa haitajirudia tena kwani sitaweza kumruhusu mtu yoyote yule aweze kukuumiza tena" alizungumza Fancy akionekana mwingi wa furaha.



    "Ammmhh Mozah; kuhusu kile kilichoweza kutokea asubuhi embu tufanye kama hakijatokea kabisa na tuishi kwa Amani kwanza" alizungumza Mfalme Kantala.



    "Ndiyo tufanye kama hakijatokea kabisa na tusiwaze kuhusu hilo" alizungumza Malikia Maua na kuweza kumuongezea chakula Mozah.



    "Nashindwa kuelewa nimtu gani huyo ambaye alihitaji kumuuwa mdogo wangu katika siku ya kwanza kabisa ya ujio wake; hat Mimi naogopa sana na ninawaza kwanini alitaka kufanya hivyo?? Alizungumza Sikitu na kufanya Mozah asite kupeleka chakula chake mdomoni.



    "Sitaruhusu mtu yoyote yule amuumize tena Wifi yangu, na kile kilichoweza kutokea tumshukuru tu aliyeweza kuliona hilo na kuweza kuwapa paka chakula kile" alizungumza Fancy na Kisude alibaki tu akiwatizama huku akipeleka chakula chake mdomoni.



    Kisude alimtizama Fancy na kurudisha macho yake katika chakula chake.



    "Nimeshiba alizungumza Hancy na kutoka mezani.



    " Hancy aliita Mozah, Sikitu na Fancy.



    "Samahani alizungumza Fancy na kumfuata Hancy nyuma.



    " Hancy !! Aliita Fancy na ulisikika mlango ukifungwa Mozah aliinuka na kubeba chakula alichoweza kukiacha Hancy kisha akaondoka eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifika mpaka Katika chumba alichoweza kujifungia Hancy alisukuma na mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.



    "Hancy..... Hancy.......fungua basi mlango..... Hancy aliendelea kuita Mozah



    " kama amekataa kunifungulia mlango Mimi hawezi kukufungulia wewe, rudi tu mezani kula" alizungumza Fancy na kuanza safari ya kurudi mezani.



    "Aaaaahhhh nimeungua" alizungumza Mozah na kutoa sauti kwa nguvu iliyoweza kupenya hadi masikioni mwa Hancy na kumfanya aufungue mlango.



    "Umeungua wapi?? Aliuliza Hancy akitoa chakula Mkononi mwa Mozah.



    " Mkononi alisema Mozah na Hancy aliweza kuushika Mkono ule wa Mozah kisha kuanza kuupuliza taratibu kabisa.



    "Wapi umeungua?? Aliuliza Hancy akiutuzama Mkono wa Mozah.



    " nimeshikilia sahani muda mrefu ndo ikaanza kuniunguza.



    "Sasa kwnini ukiishikilia na unajua ya kuwa inaunguza?? Aliuliza Hancy kwa hasira.



    " Sasa si wewe haujala na nimekugongea mlango hujafungua alizungumza Mozah huku akionekana kutaka kulia.



    "Sasa mbona untaka kulia?? Aliuliza Hancy.



    "Wewe si umenigombeza" alizungumza Mozah machozi yakiwa yameshamdondoka.



    "Samahani sasa" alizungumza Hancy na kumfuta machozi Mozah kisha kubeba chakula na kuingia ndani ya chumba chake na Mozah.



    Wakiwa wameingia ndani huku Mozah akiwa anapooza chakula cha Hancy kabla ya Hancy hajakiweka mdomoni ulionekana Mkono wa kike ukiufungua mlango ule taratibu na kuushika mlango ule kwa hasira sana baada ya kuona kitendo kile.



    Huku nako alionekana Kisude akiwa nyuma ya Fancy na kurudia maneno Yake.



    "Kama Hancy amenifungia mlango Mimi hawezi kumfungulia mlango yoyote.......Eti Fancy umeona dunia inavyobadilika sasa....mwanzo wewe ndo ulikuwa mtu muhimu kwa Hancy lakini siyo kwasasa tena Kisude alimpita Fancy ambaye alimtizama kisha akamjibu.



    "Si shangi San kwasababu hata mwanzo ulikuwa mtu wa muhimu kwa Malikia Maua lakini siyo tena kwasasa, ila Mimi sina roho kama yako kama Hancy yuko na furaha na Mimi pia ninafuraha nisichokipenda ni kumuona kaka yangu akiwa na huzuni" alizungumza Fancy na kumpita Kisude



    Mfalme Kantala akiwa na mkewe Maua huku wakionekana kujadili jambo.



    "Unafikiri ni nani atakayekuwa amehusika na hili tena?? Alizungumza Mfalme Kantala



    "Hata Mimi nashindwa kuelewa ni mtu gani huyo ambaye ameweza kufanya hivyo, na Mozah ni binti wa kifalme endapo kitamkuta chochote juu yake basi ufalme wake hautaweza kutuelewa" alizungumza Maua.



    "Na cha muhimu kabisa ni kipenzi cha Mfalme Nuhu hivyo chochote kitakachotokea juu yake hata adhirika Nuhu tu hata Hancy na yeye kitamuadhiri" alizungumza Mfalme Kantala.



    "Na............... Kabla hajamalizia kauli yake alisita na kuita



    " Sarah........



    Malikia Maua aligeuka na kumuona Sarah.



    "Sarah!!! Na yeye pia aliita kwa mshangao.



    "Imekuwaje ukarudi hapa?? Aliuliza Maua.



    "Nilipigiwa simu na .......... Kabla hajamtaja aliyeweza kumpigia simu ilisikika sauti ya Fancy akija kwa makeleke ya furaha.



    " Sarah..........



    "Fancy" aliita Sarah na kwenda kukumbatiana kwa furaha.



    "Haaaaaaaaaa what a surprise" alizungumza Fancy na kumpokea Sarah.



    "Hancy..........Hancy.......... Toka njee uone nani kaja alizungumza Fancy na Hancy aliweza kutoka huku Mozah akimfuata kwa nyuma.



    " Sarah!! Aliita Hancy kwa mshangao na kwenda kumkumbatia.



    "Imekuwaje ukaja hapa?? Aliuliza Hancy



    " Nilipigiwa simu na ......... kabla hajamjibu aliweza kunyamaza baada ya kumuona Mozah.



    "Nani Huyo?? Aliuliza Sarah na kumtizama Mozah ambaye na yeye alibaki akimtizama.



    " ahaaaaa huyu ni.........."



    Kabla hajamtambulisha Mozah kwa Sarah Fancy alikatisha mazungumzo yale.



    "Sarah.......njoo huku nikuonyeshe kitu" alimtoa Sarah na kumtizama Hancy ambaye alionekana kupata shida kumjibu swali lile aliloweza kuulizwa.



    "Ni nani huyo?? Aliuliza Mozah na Hancy alimtizama Mozah tu bila kumjibu.



    " Tunafanyaje??? Alikuwa Fancy akiulizana na Hancy.



    "Kwanza nashindwa kuelewa imekuwaje akawa hapa" Alizungumza Hancy.



    "Mozah akigundua hili sijui itakuwaje?? Alizungumza Fancy.



    " Lakini me nafikiri zilikuwa ahadi za kitoto tu kama yeye alizichukua serious sina cha kumsaidia Mimi sasa hivi, nina mwanamke ninayeweza kumpenda.



    "Tatizo la watu weupe wakiweka ahadi hawawezi kuzivunja mpaka waweze kutimiza alizungumza Fancy.



    " Mimi nitaongea naye" alizungumza Hancy na ulioneka mdomo wa kike ukitabsamu baada tu ya kusikika maneno yale.



    Mozah akiwa ndani ya chumba chake aliweza kukumbuka Hancy alivyokuwa mzito kumjibu swali aliloweza kumuuliza juu ya Sarah.



    "Yule msichana ni nani kwnini Hancy, alishindwa kunijibu alijiuliza Mozah na kukumbuka jinsi alivyoweza kumuuliza Hancy na Hancy alivyokuwa akiweweseka.



    Ghafla alisikia vyombo vikiwa vimedondoka njee tu ya chumba alichokuwa akiishi yeye.



    " Ni nani huyo?? Alijiuliza na kutoka njee ambako alikuta bakuli likiwa limedndoka lakini hakukuwa na mtu.



    "Nani huyu kamwaga hapa chakula alafu kaondoka alijiuliza na kuokota bakuli ambalo tayari lilishaweza kupasuka.



    "Jikoni ni wapi tena? Alijiuliza na kuanza kutembea kuelekea katika njia ambayo alihisi ni jikoni nyuma yake ulioneka Mkono wa kike ukishika shika kuta za nyumba ile huku akimfuata kwa nyuma Mozah na kuachia Tabasamu katika mdomo wake.



    Aliweza kufika jikoni na hakuweza kupiga hatua kuelekea mbele zaidi baada ya kuweza kuona kitu ambacho kilimfanya ashindwe kufanya hivyo.



    Mbele ya macho yake aliweza kumuona Hancy akiwa amekumbatiana na Sarah.



    Alipomaliza kutazama alitoka jikoni pale akiwa amenywea kabisa hata hatua zake nazo ziliweza kupungua na alirudi akiwa na chombo kile kilichoweza kupasuka alirudi na kuingia mpaka chumbani huku nako alionekana Sarah akiwa ameachan na Hancy.



    " Sarah.....natumaini umenielewa na samahani kwa kuweza kuweka ahadi ambyo nimeshindwa kuitimiza natumaini hili kumbatio uliloweza kuliomba Leo ndo ombi la mwisho na utambue ya kuwa yule ni mke wangu na ninampenda sana"



    "Sawa kama hujaweza kunipenda siwezi kukulazimisha unipende ila kuna jambo moja la mwisho nahitaji kukuomba"



    "Jambo gani hilo??



    " Naomba tuendelee kuwa na uhusiano kama tulioweza kuwa nao mwanzo, ctopenda kuona ukikaa mbali na Mimi kwasababu tu tayari una mke wako" alizungumza Sarah na Hancy alitikisa kichwa ishara ya sawa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tuendelee kuwa marafiki" alizungumza Hancy na kutabasamu.



    Wakti huo nao ulionekana mdomo ukisikitikia maneno Yale.



    "Bahati mbay huyo mwanamke wako hajayasikia maneno haya" Alicheka baada tu ya kuzungumza maneno Yale.



    Wakati huo ndani alionekana Mozah akiwa amekaa kitandani na machozi yakiwa yanamtoka aliposikia mlango unafunguliwa aliyafuta machozi yake na kutizama mlangoni aliingia Zawadi akiwa na kibakuli ambacho aliweza kuleta chakula kile kile kilichoweza kudondoka njee ya chumba chake.



    "Ahsanteh alizungumza Mozah na kupokea chakula kile. Hapo hapo aliingia Hancy akiwa na Tabasamu huku akiamini ya kuwa amemaliza kila kitu juu yake na Sarah.



    " Zawadi unaweza ukaenda njee"



    Ndiyo Mfalme mtaraji. Zawadi alijibu na kutoka njee.



    Mozah alimtizama Hancy aliyeonekana kuwa mwingi wa furaha na kukumbuka kumbatio aliloweza kuliona.



    Alijikuta akila chakula kile kilichoweza kuletwa na kukiweka mdomoni pasina kutambua ya kuwa ni chamoto aliweza kuungua na kujikuta akisimama kwa kutafuta mahali ambako ataweza kutemea chakula kile.



    Mozah aliita Hancy na kumfuata Mozah aliyekuwa ameenda kutemea dirishani chakula kile.



    "Unashida gani wewe, kwanini unatema chakula ambacho mama yangu ameweza kutumia muda mwingi kukipika?? Aliuliza Hancy akionekana kutopendezwa na tabia aliyoweza kuifanya Mozah.



    " Samahni, nilikula pasina kutambua ni cha moto" alizungumza Mozah.



    "Ona sasa umemwaga chakula chote" alizungumza Hancy na kumuonyesha ya kuwa chakula kile chote kiliweza kumwagika.



    "Tafadhali usimwambie mama juu ya hili nitafanya usafi hapa" alizungumza Mozah na kutaka kuelekea kwaajili ya kusafish.



    "Wacha nitasafisha Mimi" alizungumza Hancy na kutaka kwenda kusafisha lakini ghafla aliitwa na Sarah.



    "Hancy, bado tu hujajiandaaa?? Aliuliza Sarah.



    " ahaaaa nilisahau kidogo Mozah nakuja" alizungumza na kutoka njee na Sarah ambaye aliweza kumfuata.



    Mozah alipiga hatua kwaajili ya kwenda kusafisha lakini alihisi maumivu katika mguu wake alipotizama aligundua ya kuwa chakula kile kiliweza kudondokea katika mguu wake.



    "Ahhhhhh alizungumza na kujitizama mguuni mwake ghafla aliingia Hancy na alijifunika.



    " twende mahali " alizungumza na kumuinua Mozah.



    "Hancy........aliita Mozah.



    " shshshshsh.......... Hupaswi kunikatalia twende pamoja' alizungumza na kuanza kumvuta Mozah ambaye alibaki akiguguma kimoyomoyo.



    "Mozah unashida gani mbona.......kama jasho linakutoka aliuliza Fancy na Sikitu pamoja na Sarah walimtizam huku Tom na yeye akionekana kuja eneo lile akiwa amebeba baadhi ya nguo.



    " Unaumwa?? Aliuliza Hancy na kumshika Mozah kichwani.



    "Hapana" alijibu Mozah na kuutoa Mkono wa Hancy



    Mozah aliweza kumpanda farasi na hatimaye walianza safari.



    Hancy alimpanda farasi mwingine kisha kumtazama Mozah.



    "Kuwa makini usimuendeshe kwa kasi"



    "Sawa" alijibu Mozah na safari iliweza kuanza.



    Waliweza kutembea kwa umbali mrefu kidogo huku Hancy akionekana kumtazama Mozah Mara kwa Mara.



    "Hancy njoo Mara moja" aliita Sarah na Hancy alimtizama Mozah kisha akaongeza mwendo wa farasi.



    "Wifi unajisikiaje?? Aliuliza tena Fancy aliyeweza kuonekana kuwa na mashaka juu ya Mozah.



    " Nipo salama" alijibu Mozah lakini hali yake haikuwa nzuri hata kidgo mdomo wake uliweza kumkauka na uso wake uliweza kuonekana kupauka huku jasho jingi likiwa linamtoka hii ni kutokana na kuungua na chakula katika sehemu ya mguu wake na kuutembeza mguu ule juani pasina kuupaka dawa yoyote.



    Fancy alipita na nyuma alibaki Tomimo.



    "Mozah......kama mguu wako unakuuma sana usijilazimishe naweza kukurudisha nyumbn na Hancy hataweza kukereka kwa kutoweza kuuona uwepo wako tayri Dada yake Fancy yuko hapa kwahiyo acha kuutesa mwili wako.



    "Hapana bado naweza nikamudi na sitaki kuwa chanzo cha huzuni katika safari ya watu wengi wenye furaha.



    " Lakini hali yako inazidi kuw mbaya alizungumza Tom na wakat huo nao Hancy aliweza kugeuka nyuma kwaajili ya kumtizama Mozah.



    "Bado niko......... Kabla hajamalizia sentensi yake nguvu zilimuishia na kujikuta anaiachia kamba ya faras na kuanza kuona giza huku akikosa muelekeo na kwa mbali akiisikia sauti ya Tom ikimuuliza kama yuko salama.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

Blog