Search This Blog

MIMBA YA JINI - 1

 



    IMEANDIKWA NA : ALLY MBETU





    *********************************************************************************



    Simulizi : Mimba Ya Jini

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    SAA mbili kasorobo, Mustafa baada ya kufika ofisini, kabla ya kuanza kazi haja ilimshika na kuelekea msalani.

    Baada ya kumaliza kujisaidia alikwenda kwenye sinki la kusafishia mikono ili ajisafishe. Alivua pete ya ndoa na kuiweka juu ya sinki kisha alijimwagia sabuni ya maji mikononi na kuanza kunawa.




    Simu iliyokuwa mfukoni ilianza kuita, kwa vile hakuweka mlio ilitetemeka kuonesha ilikuwa inaita. Hakuipokea kwa vile bado alikuwa na sabuni mikononi, hivyo alinawa haraka na kufuta mikono kwa taulo dogo ili apokee simu. Lakini kabla hajaipokea ilikuwa tayari imekatika.

    Ingawa ilikuwa imekatika lakini aliitoa ili aangalie nani aliyekuwa akimpigia, kabla hajaangalia simu iliita tena, kwa vile ilikuwa mkononi aliangalia na kukuta jina la Shehna.

    Japokuwa alishtuka kuona jina lile ambalo kwake lilikuwa geni. Aliamini kuzungumza na aliyepiga angemjua kwa vile jina lilikuwa kwenye simu yake.

    Alibonyeza kitufe cha kupokelea na kusema:

    "Haloo."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haloo Mustafa, asalam aleiykum," ilikuwa sauti ya lafudhi ya kimwambao.

    "Waleiykum msalaam," Mustafa aliitikia huku akiifikiria sauti ile na kutaka kumjua aliyempigia ambaye jina na sauti yake vilikuwa vigeni akilini mwake.

    "Upo wapi?" sauti ilimuuliza.

    "Nipo ofisini."

    "Nipo ofisini kwako muda tu, lakini mwenyeji wangu sikuoni."

    "Nakuja basi."

    "Fanya haraka kuna sehemu nawahi, nilipita ofisini kwako mara moja."

    Mustafa alitoka haraka kumuwahi mgeni huyo, alimpita sekretari wake bila kumuuliza kitu japokuwa haikuwa utaratibu mzuri kumruhusu mgeni aingie ofisini bila mwenyewe kuwepo. Mara zote sekretari wake alikuwa akimruhusu mtu kuingia pale aliporuhusiwa kufanya hivyo.

    Lakini kwa kauli ya mgeni kuingia ofisini ilionesha ameruhusiwa bila ridhaa yake.

    Alipoingia ndani alishtuka alipokuta hakuna mtu ofisini, lakini harufu ya manukato mazuri ilisambaa kila kona.

    Alitoka haraka ili amuwahi kwa kuamini huenda aliamua kutoka baada ya kuchoka kumsubiri. Lakini aliamini hakutumia muda mrefu msalani.

    Alikwenda hadi getini kwa mlinzi na kumuulizia.

    "Eti kuna mgeni ametoka sasa hivi?"

    "Mgeni! mgeni gani?" mlinzi ilionesha kushtuka.

    "Mwanamke."

    "Bosi, toka uingie wewe hajaingia mtu yeyote."






    "Hapana, labda ulitoka eneo la kazi, mgeni alikuwa ofisini kwangu sasa hivi."

    "Bosi hakuna mgeni yeyote zaidi ya dada Sara ambaye alikutangulia kuingia kabla yako."

    "Mmh! Hebu ngoja."

    Mustafa alirudi hadi ofisini na kumuuliza Sara, sekretari wake akuyekuwa bize na kazi kwenye kompyuta.

    "Sasa mgeni ametoka?"

    "Mgeni gani?" Sara naye alionesha kushtuka.

    "Aliyekuwa ofisini kwangu sasa hivi?"

    "Bosi, hakuna mgeni yeyote aliyefika hapa, kwanza ilianza lini nimruhusu mgeni aingie ofisini kwako bila ruhusa yako?"

    "Sasa huyu mgeni kaingiaje na kapitia wapi?"

    "Bosi mgeni unayemsema umemuona wapi?"

    "Hebu njoo ofisini."

    Sara na Mustafa waliongozana hadi ofisini ambako harufu ya manukato makali ilikuwa bado ikinukia.

    "Bosi pafyumu nzuri kama hii umeitoa wapi?" Sara alisema huku akinyanyua pua zake kuivuta.

    "Sara, haya manukato nimeyakuta baada ya kurudi kutoka msalani."

    "Muongo!" Sara alishangaa.

    "Kweli kabisa, yanaonekana ni ya huyo mgeni aliyeingia ofisini kwangu."

    "Sasa kapitia wapi?"

    "Hebu subiri."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa alisema huku akichukua simu yake juu ya meza, aliangalia namba iliyoingia yenye jina la Shehna na kuipiga. Simu ilionekana kuwa bize inazungumza.

    "Simu yake inaongea."

    "Mmh! Si ulitoka nje, mlinzi anasema kuna mgeni aliingia?"

    "Hata yeye anasema hajamuona."

    "Mmh! Mtu gani tusimuone wote basi atakuwa jini."

    "Hapana si jini, nitampigia tena."

    Mustafa aliachana na mambo ya mgeni asiyeonekana, alikumbuka amesahau pete yake msalani wakati akimuwahi mgeni. Alikwenda hadi sehemu ya kunawia mkono, alishtuka kukutana tena na harufu ya manukato aliyokutana nayo ofisini kwake.

    Alipoangalia juu sinki hakuiona pete yake.

    Alishtuka na kuangalia chini labda imeanguka vilevile hakuiona, aliingia msalani kuitafuta pia huko hakuiona.

    Akili yake ilimweleza kuwa pete ile aliivua wakati akitaka kunawa mikono. Alitoka hadi kwa Sara kumuulizia.

    "Sara kuna mtu ameingia msalani wakati nlipoingia ofisini?"

    "Hakuna."

    "Unajua wakati nanawa niliweka pete yangu ya ndoa juu ya sinki, baada ya kuzungumza na simu niliwahi ofisini lakini ajabu nimerudi sijaikuta."

    "Mmh! Umeangalia vizuri?"

    "Nimeangalia, Sara au leo sikuja na pete?"

    "Umekuja nayo, si unakumbuka nilikutania siku ukiipoteza utamwambia nini mkeo."

    "Nakumbuka, sasa imekwenda wapi?"

    "Mmh! Mbona mauzauza leo."

    "Huwezi kuamini ile harufu ya manukato nimekutana nayo tena msalani."

    "Wewe!" Sara alishangaa.

    "Kweli Sara."

    "Bosi, hebu tulia kwanza inawezekana leo umeamka na mawazo mengi kutokana na ishu ya wifi. Nilikueleza mkienda Mbagala kila kitu kitakuwa sawa, yule mama kawasaidia wengi. Sema bosi tatizo ulilificha sasa hivi ungekuwa na mtoto."

    "Ni kweli, jana niliporudi nimemkuta wifi yako analia."

    "Tatizo?"

    "Lilelile la mtoto, anasema sijui kawasikia watu wakimsema kwa mafumbo kwamba yeye ni tasa."

    "Hukumweleza tuliyozungumza jana?"

    "Nimemweleza lakini anasema amechoka na uongo wa waganga, tangu tuanze kuhangaikia mtoto huu mwaka wa tano sasa."

    "Mwaka wa tano?" Sara alishtuka.

    "Ndiyo, na fedha tulizopoteza tungeweza kujenga nyumba kubwa na gari mbili."

    "Bosi yule mama kiboko wapo waliokata tamaa kama yeye lakini walipotumia dawa zake walipata watoto."

    "Mbona kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa hivyohivyo mpaka waliopata watoto tuliwaona, lakini alipotumia hakupata kitu."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hebu nendeni Mbagala tuone."

    "Alikubali kwa shingo upande, hivi namsubiri amesema atanipitia saa tano tuelekee huko Mbagala."

    "Basi bosi kapumzishe akili labda baadaye utakumbuka ulipoiweka pete."

    Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete.

    Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikutana na jina la Shehna. Aliipokea:




    Haloo."

    "Haloo Mustafa samahani, niliwahi kutoka kwa vile kuna sehemu nilitakiwa kuwahi."

    "Umepitia wapi?"

    "Jamani Mustafa kuna njia ngapi ya kuingia na kutokea ofisini kwako?"

    "Moja."

    "Basi ndiyo niliyopitia."

    "Mbona sekretari wangu hajakuona?"

    "Nimemkuta yupo bize ila sikutaka kumsumbua kwa vile mlango wako ulikuwa wazi."

    "Huyo hajakuona, na mlinzi?"

    "Sikumkuta inawezekana alikuwa msalani."

    "Mmh!"

    "Mustafa unaguna nini?"

    "Aah! Basi yaani bado ujio wako umekuwa kitendawili, pete yangu umechukua?"

    "Mustafaa! Niichukue ili iweje tuna uhusiano?"

    "Hapana."

    "Sasa pete yako niichukue vipi wakati hatuna uhusiano wa kimapenzi?"

    "Nashangaa."

    "Umemuuliza mkeo?"

    "Nimuulize nini ikiwa nimeondoka nikiwa nimeivaa?"

    "Mustafa acha ubishi, hebu muulize mkeo."

    "Nitamuuliza."

    "Muulize sasa hivi kisha nitakupigia," Shehna alisema na kukata simu.

    Mustafa hakutaka kuendelea kubisha aliamua kumpigia simu mkewe lakini alijua ni kuchochea matatizo kwa vile alikumbuka aliondoka nyumbani na pete kidoleni. Baada ya simu kupokelewa upande wa pili alimuuliza mkewe;

    "Samahani mke wangu eti pete nimeiacha nyumbani?"

    "Ndiyo, nashangaa kuiona kwenye sinki la kunawia mikono msalani."

    "Ooh! Afadhali," Mustafa alishusha pumzi ndefu.

    "Mbona umeshusha pumzi ndefu?" mkewe alimuuliza.

    "Yaani nimeitafuta kila kona ofisini nilidhania nimepoteza."

    "Una tabia ya kuvua pete?" mkewe alimuuliza.

    "Ninapotoka msalani sitaki ipate maji."

    "Basi pole mume wangu uliisahau, mi namalizia kazi nakuja."

    "Hakuna tatizo."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa alikata simu na kushusha tena pumzi na kuamini kabisa siku ile aliamka akiwa na mawazo mengi. Lakini kitu kingine kilichomshangaza harufu ya manukato aliyoyasikia ambayo hakuwahi kuyasikia maishani mwake. Simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna.

    Aliipokea:

    "Haloo."

    "Vipi, mkeo amesemaje?"

    "Amesema niliisahau nyumbani."

    "Sasa inakuwaje unanishushia lawama?"

    "Samahani nilichanganyikiwa."

    "Sasa kuna kitu muhimu kilinileta asubuhi ya leo ambacho kimekutesa kwa miaka mitano."

    "Kitu gani hicho?" Mustafa alishtuka.

    "Mtoto."

    "Umejuaje?"

    "Mustafa acha kujitoa akili, habari za mkeo kukosa mtoto kwa miaka mingi uliniambia mwenyewe na kuhangaika kwa waganga wa kila aina wa ndani na nje. Uliniambia umepoteza fedha nyingi lakini hakuna manufaa yoyote. Kutokana na kuhangaika sana imefikia hatua ya kukata tamaa japokuwa mnataka kwenda leo Mbagala kujaribu mara ya mwisho uongo kweli?"

    "Kweli, nilikuambia lini?"

    "Sasa inamaana ningejuaje bila wewe kuniambia?"

    "Basi nimechanganyikiwa kiasi cha kusahau kama niliwahi kuzungumza na wewe ishu hiyo."

    "Tuachane na hayo, Mustafa nataka nikusaidie mkeo kupata mtoto lakini naomba na wewe unisaidie shida yangu."

    "Shida gani?"

    "Kwanza nataka mkeo apate mtoto mengine yatafuata, ila naomba uniahidi mkeo akipata mtoto na mimi utanisaidia?"

    "Nakuahidi ukinisaidia mke wangu kupata mtoto unachokitaka kama kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia pia nitakupa zawadi kubwa sana."

    "Basi naomba msiende kwa mganga dawa nitampelekea mimi."

    "Nitaamini vipi kama utakayompa ni dawa?"

    "Utaamini mkeo akishika ujauzito mwezi huu."

    "Mmh! Sawa."

    Baada ya mazungumzo alikata simu na kutulia akiwaza huku akiamini matatizo ya mkewe kuchelewa kupata mtoto yamemchanganya sana hasa baada ya familia yake kuingilia kati na kumtaka aoe mwanamke mwingine kutokana na sheria ya dini yake.

    Siku zote hakutaka kuongeza mwanamke mwingine kwa kujua atakuwa hakumtendea haki mkewe pia kufanya vile ni kumnyanyapaa.

    Kibaya zaidi alijua angemuumiza mkewe kama mwanamke aliyemuoa angepata mtoto ungekuwa ukatili mkubwa kwa sababu wote hawakuwa na tatizo la kiafya zaidi ya kuchelewa tu kupata mtoto.

    Akiwa katika lindi la mawazo simu yake iliita, alipoangalia alikuwa mkewe, aliipokea:

    "Haloo mke wangu."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mume wangu pole na kazi."

    "Asante."

    "Eti kuna dada mmoja anaitwa Shehna amenipigia simu na kunieleza matatizo yangu kama niliwahi kumweleza na kunieleza kuwa amezungumza na wewe kuhusu dawa ya matatizo yangu na kuniambia nisiende tena kwa waganga dawa atakayonipa itatoa majibu mwisho wa mwezi huu?"

    "Hata mimi kaniambia hivyo... hebu subiri kuna mtu anagonga mlango."

    "Sawa."

    Baada ya dakika tatu mkewe alipiga tena simu ambayo aliipokea.

    "Ehe, mke wangu."

    "Kuna kijana kaleta kichupa kidogo chenye maandishi ya Kiarabu, kasema kapewa na dada mmoja ambaye hakumuona sura kutokana na kuvaa hijabu iliyomziba uso."

    "Kwa hiyo tusiende Mbagala?"

    "Hebu tuangalie na uongo wake."

    Mustafa alikubaliana na mkewe wasiende tena kwa mganga, alimpigia simu Shehna kutaka kumshukuru. Lakini simu haikuwa hewani, aliachana naye na kuendelea na kazi zake.

    ***

    Kutokana na wingi wa kazi, Mustafa alirudi nyumbani usiku na baada ya chakula walikwenda kuoga na kurudi kitandani.

    "Mume wangu Shehna alisema tukutane kimwili saa nne kamili ili yai la uzazi lisipotee," mke wa Mustafa alimweleza mumewe.

    "Alikupa maelekezo jinsi ya kutumia hii dawa?"

    "Ooh! Nilisahau kumuuliza."

    "Sasa tutafanyaje?"

    "Namba yake si unayo mpigie."

    Mustafa alinyanyuka kitandani na kwenda kuchukua simu, alitafuta jina la Shehna ili ampigie lakini ajabu halikuonekana.

    "Mbona jina lake silioni kwenye simu?"

    "Kwani alipokupigia hukusevu namba yake?"

    "Namba yake ilikuwemo kwenye simu."

    Mkewe naye alichukua simu yake kuangalia namba ya Shehna ambayo hakuiona.

    "Hata kwangu siioni."

    "Sasa tutafanyaje?"

    "Yaani najilaumu kutomuuliza maelekezo ya dawa, sasa hatujui tumywe au tujipake."

    "Heri maandishi yaliyoandikwa kwenye chupa yangekuwa ya Kingereza tungeweza kusoma maelekezo lakini Kiarabu siambui hata moja."

    "Sasa tutafanyaje na muda unakaribia?"

    "Hatuna jinsi kwa vile hakutupa maelekezo pia namba yake haipatikani,"

    Mustafa alinyamaza baada ya simu yake kuita, aliichukua na kuitazama na kujikuta akitamka kwa sauti.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Shehna."

    "Amepiga?" mkewe aliuliza huku akinyanyuka kutaka kuona kwenye simu.

    "Ndiyo."

    "Pokea haraka kabla hajakata."

    Mustafa alipokea simu.

    "Haloo Shehna."

    "Jamani mbona una pupa hivyo mwanaume wewe."

    "Lazima niwe na pupa kutokana na muda kusogea bila kuwa na maelezo ya matumizi ya dawa uliyotupa."

    "Ni kweli niligundua nilifanya kosa najua muda umekwenda sana, sasa chukua ndoo ya maji weka maji yaliyomo kwenye hicho kichupa nusu kisha mkaoge kwa vile muda utakuwa umekaribia baada ya kuoga jifuteni maji.

    Kabla ya tendo, kila mmoja ajipake mafuta hayo sehemu zake za siri ndipo muingiliane baada ya tendo kila mmoja anywe kidogo kisha muonge tena kwa kuweka mafuta yaliyobakia kwenye chupa na kulala."

    "Samahani Shehna."

    "Bila samahani."

    "Tunaweza kuoga na sabuni?"

    "Hapana, mnaoga hivyo hivyo."

    "Sawa nimekuelewa."

    "Mlikuwa mnataka mtoto gani?"

    "Ye yote."

    "Mbona moyoni wewe unataka mtoto wa kiume?"

    "Ni kweli lakini atakayepatikana nitampokea."

    "Na mkeo?"

    "Ye yote," alisema Mustafa.

    "Mbona unamsemea."

    "Yeyote tu ni mtoto," mke wa Mustafa alijibu kwa sauti.

    "Mbona uliweka nadhili mtoto wa kwanza akiwa mwanamke utampa jina la mama yako?"

    "Ni kweli, lakini atakayekuja nitampokea."

    "Sasa mnaweza kukubaliana mnataka mtoto gani atangulie, kama wa kike mtakunywa hayo mafuta kabla ya tendo kama wa kiume, mtakunywa baada ya tendo."

    "Tumekuelewa."

    "Mna swali?" Shehna aliuliza.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hatuna."

    "Haya usiku mwema."

    "Na kwako pia."

    Baada ya simu kukatika Mustafa alimgeukia mkewe na kumuuliza.

    "Nina imani umesikia, unataka tutangulize mtoto gani?"

    "Wa kike."

    "Kwa nini asianze wa kiume?"

    "Si umesema upo tayari kupokea mtoto yeyote."

    "Naomba mke wangu unipe upendeleo kwa huyu wa kwanza."

    "Umeshindwa vipi kunipa upendeleo mkeo wa pili awe wa kiume?"

    Walijikuta wakisahau muda ulikuwa umekwisha hivyo walitakiwa kutekeleza walichoelekezwa. Mpaka wanakubaliana muda walioelekezwa ulikuwa umevuka zaidi ya dakika kumi na tano.

    "Mke wangu tumevusha muda tulioambiwa tutafanyaje?"

    "Kwani saa nne imevuka?"

    "Lakini alisema saa nne juu ya alama."

    "Ilikuwa kutufanya tuwe makini zaidi, lakini muda haujapita sana."

    Walikwenda kuoga kwa kufuata maelekezo yote, baada ya kuoga walijipaka manukato na kunywa kwa vile walikubaliana kutanguliza mtoto wa kike. Baada ya hapo alikutana kimwili na baada ya tendo walikwenda kuoga na kurudi kitandani kulala.

    ***

    Usiku, Mustafa aliota akifanya mapenzi na mwanamke nzuri wa kiarabu ambaye alimweleza anataka kuzaa naye. Siku ya pili aliamka amechoka sana kutokana na kutumika mara mbili kwanza na mkewe pili katika njozi.

    Alipoamka hakumueleza mkewe alivyoota, alioga na kupata kifungua kinywa na kuwahi kazini. Mustafa akiwa kazini simu yake iliita, ilikuwa ya Shehna, aliipokea haraka.

    "Haloo Shehna!"

    "Aah! Mustafa, tanguliza asalamu aleykumu."

    "Ooh! Samahani, asalamu aleykumu."

    "Waleykumu salamu."

    "Haya bibie niambie?"

    "Nilitaka kukusalimia tu, pia kukueleza jinsi ulivyonifurahisha kwa kutunza siri zako."

    "Siri gani?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unajua wanaume wengi kila kinachotokea huwaeleza wake zao."

    "Mimi kimenitokea nini?"

    "Unakijua, lakini hukutaka kumwambia mkeo."

    "We' umejuaje?"

    "Mustafa tuachane na hayo, mbona jana umeniangusha?" Shehna alibadili mada.

    "Kivipi?"

    "Niliwaambia mfanye mapenzi saa ngapi?"

    "Saa nne."

    "Ndiyo muda uliofanya?"

    "Hapana lakini haikuvuka sana."

    "Mustafa niliwaeleza saa nne kamili lakini mmevuka muda, kwa nini umepuuza maagizo yangu?"

    "Samahani kwa hilo."




    Mmh! Sijui...halafu kwa nini hukufurahia uamuzi wa mkeo?”

    “Nimefurahi ndiyo maana tumekubaliana kutanguliza mtoto wa kike.”

    “Si kweli Mustafa, moyoni hujafurahia uamuzi wa mkeo kwa kulazimisha kutangulia mtoto wa kike kitu kitakachompa matatizo mtoto atakayezaliwa.”

    “Kwa nini?” Mustafa alishtuka.

    “Kuukunja moyo wako wakati wa tendo la ndoa tofauti na siku zote. Mimba iliyoingia umeitia sumu.”

    “Sumu?” Mustafa alishtuka.

    “Ndiyo, ili kuiondoa unatakiwa kuukunjua moyo wako bila hivyo mtoto atakuwa na matatizo.”

    “Nimekuelewa.”

    “Basi mi nikuache ufanye kazi.”

    “Nashukuru ila nilikuwa na hamu sana ya kuonana na wewe.”

    “Usiwe na wasi Mustafa utaniona mpaka utanichoka kwanza tumalize tatizo linalowakosesha raha kwa muda mrefu.”

    “Asante, nitakusuburi.”

    Mustafa alikata simu na kujikuta akiwa katika mawazo mengi juu ya mtu anayejiita Shehna. Alijiuliza ni nani mtu anayeyajua maisha yake kiundani pia kujua hata mambo yaliyojificha bila kumwambia.

    “Huyu mwanamke atakuwa nani...mmh! au...ha...hapana siyo lazima atakuwa mganga tu siyo jini.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa aliendelea kuwaza juu ya kauli tata za Shehna ambazo hakuelewa nini hatima yake. Alijiuliza alijuaje kama kitendo cha mkewe kulazimisha mtoto wa kike wakati yeye alitaka wa kiume kitu ambacho alimkubalia kwa shingo upande yeye alifanya siri lakini Shehna alitambua na kumtisha kuhusu ujauzito ambao yeye alisema uliingia siku ile usiku.

    Alijiuliza sumu hiyo ni sumu gani ambayo inaweza kuleta matatizo katika ujauzito ule na moyo wake ataunyoosha vipi. Kuingia kwa sekretari wake kulimkatisha mawazo yake.

    “Bosi vipi naona upo mbali?” Sara alisema akiwa ameshika faili mkononi.

    “Kawaida tu.”

    Sara alimpa kazi aliyomuagiza kuifanya, baada ya kumpa alimuuliza.

    “Jana nilisahau kukuuliza mlikwenda Mbagala?”

    “Sara tumetoka hapa saa ngapi?”

    “Kweli, jana kazi zilitushika, kwa hiyo wifi alienda peke yake?”

    “Hakwenda ila mwisho wa wiki atakwenda.”

    Sara alitoka na kumuacha Mustafa akiwaza na kuwazua aliyoelezwa na Shehna.

    ****

    Jioni wakati Mustafa anajiandaa kurudi nyumbani alipokea simu toka kwa mkewe.

    “Haloo mpenzi,” alipokea kwa madaha kama kawaida yake anapopigiwa na mkewe.

    “Mume wangu yupo wapi?” mkewe alizungumza sauti ya mtu anayeumwa sana.

    “Mke wangu mbona unaongea hivyo?” sauti ya mkewe ilimshtua.

    “Na...na...u...mwa.”

    “Nini?” Mustafa alitaharuki.

    “Na...na...,” sauti ilinyamaza ghafla na kusikia kishindo upande wa pili.

    Mustafa alijikuta akitaharuki na kutoka mbio ofisini kuelekea nje kwenye gari lake ili awahi nyumbani kujua mkewe alipatwa na nini. Alimpita sekretari wake aliyekuwa katika maandalizi ya kuzima vyombo vya umeme ili watoke na bosi wake.

    Alishangaa bosi wake akitoka mbio kuelekea nje bila kumsemesha, Sara aliacha kazi na kumfuata ili ajue kulikoni. Alimuona akielekea kwenye gari lake akiwa kama amechanganyikiwa, alimkimbilia na kumuuliza:

    “Bosi vipi?”

    “Sara hebu subiri,” alisema huku akiwasha gari.

    “Bosi kuna nini mbona mbiombio kwenye gari au kuna kitu cha kutisha kimetokea ofisini?” Sara alizidi kuhoji.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sara niache kwanza,” Mustafa alisema huku akiwasha gari na kuliondoa kwa kasi kuelekea getini na kumpigia kelele mlinzi afungue.

    Mlinzi alifungua haraka, Mustafa alilitoa gari kwa kasi kwa kuliingiza barabarani bila kuangalia na kuelekea nyumbani.

    Mlinzi alimfuata Sara na kumuuliza:

    “Vipi! Kuna nini?”

    “Hata najua! Nimemuona akitoka ofisini mbio hata sijui kapatwa na nini?” Sara naye alikuwa amepatwa na mshangao.

    “Hukumuuliza?”

    “Majibu yake hayaeleweki! Kila nilipomuuliza majibu anajua mwenyewe, kaacha vitu vyake vyote vya muhimu koti, lap top.”

    “Mmh! Basi kuna kitu kimempata si bure.”

    “Nina wasiwasi kuna kitu kimemtokea ofisini.”

    “Twende tukaangalie.”

    “Nani aingie ofisini? Toka juzi Bosi simwelewi mambo yake, nina wasiwasi bosi anataka kurukwa na akili,” Sara alisema.

    “Mmh! Hapana, asingeweza kuendesha gari vile.”

    Wakati wakijadiliana yaliyomtokea bosi wao, Mustafa alikuwa akiwaza nyumbani na kushindwa kuelewa nini kilimpata mkewe ambaye muda mfupi uliopita alizungumza naye akiwa katika afya njema.

    Alipofika nyumbani kwake alisimamisha gari lake nje ya nyumba yao na kukimbilia ndani bila kufunga mlango wa gari. Alipoingia ndani alishtuka kumkuta mkewe amelala chini akiwa amepoteza fahamu.

    Alijaribu kumwita lakini hakuitikia, alimbeba na kutoka naye nje ili amuwahishe hospitali, alimuweka siti ya nyuma ya gari na kufunga mlango.

    Naye alizunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari. Alipowasha gari liligoma kuwaka, alishangaa. Alipoangalia kwenye geji ya mafuta ilimshtua kuona mafuta yalikwisha.

    “Shit,” alisema kwa sauti huku akipaga ngumi kwenye gari.

    Mara simu yake iliitaka, huku akivuja jasho kutokana na tatizo la mkewe. Alijifuta kwa shati jasho lililokuwa likimvuja kama maji kisha aliitazama simu na kuona aliyepiga ni Shehna.

    “Haloo,” alipokea pumzi zikiwa juu.

    “Mbona hivyo?” sauti ya Shehna ilionesha kushtuka.

    “Nina tatizo.” 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tatizo gani tena Mustafa?”

    “Mke wangu yupo hoi hata sijui anaumwa nini?”

    “Mmh! Isiwe mimba?”

    “Mimba?” Mustafa alishtuka.

    “Eeeh, unashtuka nini?”

    “Mimba hiyo imeingia lini?”

    “Jana.”

    “Acha utani, hakuna mimba inayoweza kuingia mara moja na kuanza kumsumbua mtu.”

    “Mustafa kila mimba ina uingiaji wake.”

    “Basi yote nitayajua hospitali.”

    “Unampeleka hospitali ili iweje?”

    “Ana hali mbaya sana, kwanza sijui kama mzima.”

    Kauli ile ilimfanya Shehna aangue kicheko kitu kilichomshtua Mustafa na kuhoji.

    “Mbona unacheka?”

    “Nani alikuambia mimba ugonjwa?”

    “Shehna una uhakika gani kama ni mimba?”

    “Uhakika ninao, mrudishe mkeo ndani kwa vile haumwi.”

    “Hapana siwezi kufanya hivyo lazima nimpeleke hospitali.”

    “Haya fanya unavyotaka, lakini usinitafute wala tusilaumiane,” Shehna alitoa kauli ya kitisho.

    Kauli ile ilimshtua Mustafa na kumfanya ajiulize Shehna ana maana gani.

    “Shehna ulikuwa unataka nifanyeje?” ilibidi awe mpole.

    “Mrudishe kwanza ndani.”

    “Kisha?”

    “Mrudishe kwanza.”

    “Sawa.”

    Mustafa alimchukua mkewe na kumrudisha ndani akiwa katika hali ileile ya kupoteza fahamu. Baada ya kumlaza kwenye kochi alichukua simu ili kuwasiliana na Shehna.

    Alipochukua simu alikuta bado ipo hewani aliita.

    “Haloo Shehna.”

    “Abee Mustafa.”

    “Tayari.”

    “Kile kichupa cha manukato kipo?”

    “Sijui.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kiangalie kama kipo kisha chukua maji kwenye sahani ya bati nyeupe kiweke kisha mpake kichwani. Akiamka mpe anywe na mengine mpake tumboni.  
     




    Mustafa alikwenda chumbani na kukikuta kichupa juu ya meza ya kujipodolea. Alikichukua na kwenda kwenye kabati na kuchukua sahani ya bati nyeupe ambayo aliiweka maji na kukiweka kile kichupa na kufanya maji yale kunukia.

    Alifanya kama alivyoelekezwa kwa kumpa maji kichwani. Ghafla mkewe alifumbua macho.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Husna," alimwita kwa sauti ya chini.

    "Abee mume wangu," aliitika kwa sauti ya chini huku akipepesa macho.
    "Vipi?"

    "Safi," alijibu kwa sauti ya chini huku akikaa kitako.

    "Unajisikiaje?"

    "Mmh! Sijambo."

    "Kwani ilikuwaje?"
    "Yaani nilikuwa natoka chumbani ghafla nikaanza kujisikia vibaya..yaani vibaya sana. Nikapata wazo la kukupigia simu, nilijitahidi kukujulisha lakini ghafla kilikuja kiza kizito kilichoendelea sikujua."

    Mustafa alimpa maji anywe, lakini mkewe alihoji.

    "Ya nini?"

    "We kunywa."

    Mkewe alikunywa, yaliyobaki alimpaka tumboni.
    "Mume wangu mbona sikuelewi?"

    "Ndiyo tiba yako."

    "Kwa nini tusiende hospitali."

    "Shehna amekataa."

    "Alikuja."
    "Ndiyo," Mustafa alimdanganya mkewe.

    "Jamani mbona hakukaa ili nimuone, yaani yule dada anaonekana mwema sana. Kwani anasema hali hii inatokana na nini?"

    "Mimba."

    "Mimbaa!" Husna alishtuka.

    "Ndiyo, anasema imeingia kwa mtindo huo."
    "Ndiyo nasikia leo mimba ikiingia mara moja mtu unaona mabadiliko makali."

    "Basi mke wangu inaonekana mambo ya jana mimba imeingia."

    "Siwezi kuamini mpaka nikapime."

    "Duka la dawa lipo jirani kanunue kipimo."
    Snura alinyanyuka ili atoke nje, mara simu yake iliita. Alirudi kwenye kochi na kuichukua ilikuwa inatoka kwa Shehna.

    "Asalam aleykum," alipokea Husna.

    "Waleykumu salam," aliitikia Shehna kwa lafudhi ya mwambao.

    "Niambie shoga yangu, yaani umeniudhi kweli."

    "Kwa nini tena shoga?"
    "Yaani kumbe jana umekuja hata kusubiri tuonane?"

    "Nilikuwa na haraka, la muhimu afya mengine majaaliwa tutaonana tu."

    "Naona umenipigia simu una lipi shoga yangu?"

    "Vipi unaendeleaje?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh! Namshukuru Mungu."
    "Mambo ya kawaida, siku zote mimba zina ujaji wake kwa vile ni mara ya kwanza lazima imekusumbua."

    "Shoga hii siyo mimba, mimba gani ya siku moja?"

    "Husna acha ubishi, mimi ndiye najua."

    "Kwanza shoga, wewe ni nani mganga au ji.." Husna alikata maneno.

    "Malizia tu si ulitaka kusema mimi jini siyo?"

    "Hapana shoga."
    "Utanijua tu muda si mrefu kama mimi mtu, jini, mganga au mchawi," Shehna alisema kwa sauti kali kidogo.

    "Samahani shoga sikuwa na maana hiyo bali kukujua tu," Husna alijitetea.

    "Si nimekueleza utanijua wasiwasi wako nini."

    "Kuhusu ujauzito siwezi kuamini japokuwa nina dalili zote za ujauzito huenda ni malaria mi nataka kupima ili nihakikishe."

    "Husna naomba suala lako usichanganye na masuala ya kizungu," Shehna alimpa onyo mke wa Mustafa.




    "Sawa nimekuelewa shoga."

    "Najua majibu yako yamejaa unafiki sasa ukienda kinyume tusilaumiane."

    "Nimekuelewa shoga."

    "Nataka hili umweleze na mumeo, sawa?" Shehna alisema kwa sauti kali.

    "Sawa."

    Simu ilikatika na kumfanya Husna arudi kwenye kochi na kukaa, safari ya kwenda duka la dawa baridi ikakatika ghafla. Mustafa alishtuka na kumuuliza mkewe.

    "Vipi mbona huendi dukani?"

    "Shehna amekataa."

    "Amekataa nini?"

    "Nisiende kununua kipimo cha mimba wala nisikitumie."

    "Amejuaje unataka kwenda kununua?"

    "Nimemwambia nataka kuhakikisha kama kweli nina ujauzito nakwenda kununua kipimo cha mimba."

    "We unasemaje?"

    "Niseme nini? Mmh! Ipo kazi."

    "Kwa hiyo huendi?"

    "Amesema suala la ujauzito wangu tusichanganye na mambo ya Kizungu."

    "Kwa hiyo hata ukiumwa?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sijui muulize wewe."

    "Mmh! Sawa."

    Walikubaliana kutotumia dawa za Kizungu kipindi chote cha ujauzito japokuwa Husna moyoni hakuamini kama alikuwa mjamzito na kutaka kufanya kwa siri ili kupata uhakika.

    ***

    Sara baada ya bosi wake kuondoka katika mazingira tata alifunga ofisi na kuchukua vitu vya bosi wake ampelekee nyumbani ikiwa pamoja na kwenda kujua nini kilimsibu.

    Alikodi gari na kuelekea kwa bosi wake, akiwa njiani ghafla usingizi ulimpitia. Ajabu aliposhtuka alijikuta kitandani kwake akiwa amelala na mizigo ya bosi wake ameishikilia mkononi.

    Alipopepesa macho alishangaa kuona jua kama la asubuhi. Alinyanyuka kitandani na kushangaa kukuta mlango ukiwa wazi.

    Aliweka vitu kwenye kochi na kuangalia saa ya mkononi iliyomuonesha ni saa mbili asubuhi. Alishangaa kujiona akiwa nyumbani amelala na vitu alivyokuwa akimpelekea bosi wake.

    Alijawa na mawazo na kujiuliza alipotoka kazini na kukodi gari alimwambia dereva ampeleke kwa bosi wake au nyumbani kwake? Akakumbuka alimwambia ampeleke kwa bosi na si nyumbani.

    Alijiuliza kama alikwenda nyumbani kipi kilimsibu mpaka akalala na nguo zake bila kuvua viatu na mkoba wenye ‘laptop' na koti la bosi wake. Bado alikuwa njia panda kuhusiana na kurudi nyumbani na kulala bila kula wala kufunga mlango.

    Mara simu iliita ilikuwa ya bosi wake, aliipokea.

    "Haloo bosi."

    "Sara upo wapi?"

    "Nyumbani."

    "Unaumwa?"

    "Hata siumwi."

    "Mbona hujafika kazini?"

    "Bosi hata sijui niseme nini?"

    "Basi wahi ofisini huwezi kuamini nina nusu saa nipo nje ofisi imefungwa."

    "Mungu wangu, jana nilijisahau na kuondoka na funguo."

    "Basi wahi."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara alioga haraka na kubadili nguo kisha alikodi bodaboda kuwahi kazini huku akimuhimiza dereva akimbize pikipiki.

    Alifika ofisini baada ya dakika tano, Sara alimsalimia bosi wake na kufungua ofisi, Mustafa akaingia ndani.

    Alimkabidhi vitu vyake na kurudi kwenye eneo lake la kazi kumalizia kiporo ndipo amuuliza bosi wake jana ilikuwaje na kumweleza yaliyomtokea.

    ***

    Husna mke wa Mustafa akiwa nyumbani peke yake moyo ulimsukasuka juu ya hali aliyonayo ambayo alielezwa ni ujauzito lakini alikatazwa kutumia kipimo cha Kizungu kutambua kama ni mimba.

    Alijiuliza kama akikitumia nini kitakuwa, alimtuma mtoto dawa katika duka la dawa baridi akamletee kipimo kile. Baada ya kuletewa alikwenda msalani na kujisaidia haja ndogo na kuiweka kwenye kikopo kisafi na kurudi nacho chumbani.




    Alikiweka kile kikopo chini na kukichukua kipimo, alikifungua ili akitie kwenye kikopo chenye haja ndogo. Mara simu yake iliita alipoitazama ilikuwa inatoka kwa Shehna.

    Aliipuuza na kukiweka kile kipimo kwenye haja ndogo ili kuhakikisha kama ana mimba kweli. Kilipogusa tu kwenye haja ndogo, alihisi kama tumbo limechafuka ghafla. Ajabu nyingine haja ndogo iliyokuwemo kwenye kikopo iligeuka damu mbichi iliyotoa harufu kali. Alishtuka akiwa anashangaa hali ile, alizidi kushtuka kusikia hali ya majimaji ukimtoka chini kama ya kuziona siku zake. Alipoangalia alishtuka kuona nguo yote umetota kwa damu. Chini damu ilitengeneza michirizi aliyotapakaa sehemu kubwa kuonesha ametokwa na damu nyingi.

    Kizunguzungu kilikuwa kikali alijitahidi kunyanyuka kwa kujilazimisha na kufanikiwa kuishika simu yake. Aliitafuta namba ya mume wake kwa shida na kupiga na kupokelewa upande wa pili.

    "Haloo," Mustafa alipokea.

    "Mu..mu..me wangu na..na ..ku..fa," baada ya kusema vile simu ilimponyoka na yeye akajitupa chini kama mzigo na kupoteza fahamu.

    Mustafa alishtuka na kujiuliza mke wake amepatwa na nini tena. Hakutaka kutoka kama jana yake kwa kumshtua sekretari wake, alimuaga kwa sauti ya kawaida iliyoficha siri nzito ndani.

    "Sara nafika nyumbani mara moja."

    "Mbona hivyo kuna usalama?"

    "Kawada tu."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alitoka hadi kwenye gari lake na kuwasha kuwahi nyumbani huku akijiuliza mkewe amepatwa na nini. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi hadi nyumbani, baada ya kusimamisha gari alikimbilia ndani.

    Alipoingia ndani alishtuka kukuta damu imetapakaa chumba kizima. Alishtuka kuona kikopo kikiwa na damu na ndani yake kuna kipomo cha mimba.

    "Mungu wangu mke wangu kafanya nini?" Mustafa alishika mikono kichwani.

    Alimshika mkewe aliyekuwa amelala sakafuni ambaye alionekana kapoteza fahamu huku akiwa ametokwa damu nyingi. Alijikuta akishindwa afanye nini baada ya kujua mkewe kafanya kosa kwenda kinyume na maelekezo ya Shehna.

    Alimnyanyua na kumpeleka bafuni ambako alimfanyia usafi na kumrudisha kitandani, lakini wakati huo bado alikuwa amepoteza fahamu. Alibaki njia panda asijue ampeleke hospitali au afanye nini. Akiwa katika taharuki simu yake iliita, alipoangalia ilikuwa inatoka kwa Shehna, aliipokea haraka.

    "Haloo Shehna."

    "Haloo Mustafa, vipi mbona kama una tatizo?"

    "Ndiyo, mke wangu ana matatizo."

    "Matatizo gani tena?"

    "Yaani hata sijui, anatokwa damu."

    "Kwanza upo wapi?"

    "Nipo nyumbani."

    "Ha! Umeondoka sangapi wakati nimeingia nimeliona gari lako."

    "Sasa hivi."

    "Basi mi nipo ofisini kwako, utawahi kurudi?"

    "Shehna, yaani matatizo ya mke wangu unayaona madogo?"

    "Siyo madogo ya kujitakia."

    "Sasa unanishauri nini?"

    "Kuhusu nini?"

    "Tatizo la mke wangu."

    "Ulikuwa unahitaji msaada wangu ipi?"

    "Wa ushauri wako."

    "Mpeleke hospitali."

    "Si ulitukataza?"

    "Lakini mkafanya."

    "Siyo mimi ni mke wangu."

    "Basi mpeleke hospitali kwa hilo sina msaada wowote kwako lipo nje ya uwezo wangu."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Haina tatizo kwenda hospitali?"

    "Mustafa mi siyo mganga, wahi hospitali utampoteza mkeo," Shehna alisema kwa sauti kali kidogo.

    "Sawa nimekuelewa."

    "Sasa unarudi saa ngapi?"

    "Sijajua."

    "Ukimpeleka hospitali lazima atapata kitanda, nitakusubiri ukichelewa nitaondoka."

    "Sawa."

    Baada ya kukata simu Mustafa alimchukua mkewe na kumuwahisha hospitali. Alipofika alipokelewa na wauguzi na kukimbizwa wadini na kumuacha Mustafa nje akisuburi.

    Baada ya vipimo majibu yalionesha ujauzito umetoka. Mganga alimwita ofisini na kumweleza tatizo la mkewe.

    "Vipimo vinaonesha ujauzito umetoka."

    "He! Kweli alikuwa na mimba?" Mustafa alishtuka.

    "Ndiyo kwani ulikuwa hujui?"

    "Ha..ha....ndiyo."

    "Vipi Bwana Mustafa mbona unababaika?"

    "Kulikuwa na dalili lakini hatukuwa na uhakika."

    "Aah! Bwana Mustafa, unaniangusha siku hizi suala la ujauzito si la kusumbuka kwa vile mkiwa na wasiwasi mnakwenda duka la dawa baridi ambalo nina imani siku hizi lipo kila kona, unanunua kipimo na kupata uhakika."

    "Na..na sababu ya kutoka ujauzito?"

    "Inawezekana alianguka na kulilalia tumbo."

    "Duh! Sasa itakuaje?"

    "Atafanyiwa usafi na kuongezwa damu kutokana na kupoteza damu nyingi kisha tutaangalia hali yake kwa kesho, ikiendelea vizuri tutamruhusu."

    "Kwa hiyo naweza kumsubiri?"

    "Hapana kaendelee na majukumu ya ujenzi wa taifa ila acha namba yako ya simu tutakujulisha hali ya mkeo, yangu utaangalia katika business card yangu," Daktari alimkabidhi kadi Mustafa.

    "Nashukuru, lakini tatizo siyo kubwa?"

    "Siyo kubwa, damu ndiyo iliyopotea nyingi, lakini jioni ya leo atakuwa vizuri."

    "Nashukuru dokta."

    Mustafa alitoka na kurudi nyumbani kufanya usafi wa damu iliyomtoka mkewe. Lakini alishtuka kukuta nyumba ipo katika hali ya usafi hakuna hata na chembe ya damu sehemu.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     




    Hakutaka kuwaza sana aliwasha gari na kurudi kazini, alipofika alishtuka kukutana na manukato makali ambayo aliamini ni ya Shehna. Alipoingia tu Sara alimwambia.

    “Bosi hukupishana na mwanamke mwenye hijabu hapo mlangoni?”

    “Hapana.”

    “Mmh! Kapitia wapi? Sasa hivi katoka.”

    “Basi sijamuona.”

    “Yaani sasa hivi hata dakika haijafika, nina imani hata getini hajafika.”

    “Amesemaje?”

    “Anashida na wewe.”

    “Hakutaja jina lake?”

    “Amesema ukifika niseme sijui Shena.”

    “Shena au Shehna.”

    “Shehna, unajua tena lafudhi ya Kimwambao.”

    “Duh!” Mustafa alisema huku akigeuka na kukimbilia nje amuwahi mgeni wake.

    Mpaka anafika getini hakumuona mtu yeyote, alimfuata mlinzi na kumuuliza.

    “Shabani kuna mgeni amepita hapa?”

    “Ndiyo.”

    “Mwanamke au mwanaume?”

    “Mwanamke aliyevaa hijabu.”

    “Ameenda wapi?”

    “Baada ya kutoka nje lilipita gari ambalo lilimchukua.”

    “Duh! Yaani alipotoka tu gari lilipita?”

    “Amesimama barabarani kama dakika mbili hivi akisubiri, baada ya muda gari lilisimama na yeye kuondoka.”

    “Atakuwa ameenda wapi, kwa nini hakunisubiri?”

    “Kwani bosi hukuonana naye?”

    “Sikuonana naye.”

    “Yaani mmepishana, baada ya wewe kuingia na yeye akatoka.”

    “Mungu wangu sasa nimepishana naye wapi?” Mustafa alijilaumu kwani alikuwa ana hamu ya kumuona Shehna kwa macho baada ya kuvutiwa na sauti yake iliyomfanya aamini ni mwanamke mzuri.

    “Yupo vipi?”

    “Kwa kweli umbile kalificha na vazi alilovaa ni mweupe, kwa lafudhi yake anaonekana kama Mpemba vile. Ila yule mwana mke ana umbile la utata. ”

    “Kwa nini unasema hivyo?”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Toka anaingia na kutoka, upepo ulikuwa ukiisukuma nguo yake na kuonekana ramani ya umbile lake na kuonesha mwanamke mzuri sana. Kwani bosi hujawahi kuonana naye?”

    “Sijawahi.”

    “Mbona alivyokuuliza kama mnajuana sana?”

    “Kwenye simu si kwa kuonana.”

    “Labda atarudi.”

    “Mmh! Sidhani.”

    Mustafa aligeuka na kurudi ofisini, alipofika kwa msaidizi wake Sara alimuuliza.

    “Vipi bosi umemuona?”

    “Walaa.”

    “Anapaa?”

    “Hapana nimekuta ameisha panda gari na kuondoka.”

    “Bosi nilipokueleza ungetoka ungemuwahi.”

    “Labda atarudi.”

    “Nina imani atarudi amekusuburi sana.”

    “Sijui atarudi?”

    “Yaani unatoka tu yeye akaingia kama mmepishana mlangoni, nilimweleza akuwahi akasema atakusubiri. Baada ya kuchoka alitaka kuondoka nilimsihi akusubiri, akakubali. Nilikutafuta kwenye simu lakini haukuwa hewani.”

    “Mbona simu yangu sijazima?”

    “Yaani kila nikipiga inakata.”

    “Labda mawasiliano.”

    Mustafa alipotaka kuingia ofisini Sara alikumbuka kitu.

    “Bosi.”

    “Unasemaje?”

    “Ha...halafu mbona manukato ya yule mwanamke yanafanana na yale ya siku ile tuliyoyakuta ofisini kwako?”

    “Hata mimi nayasikia, yupo vipi?”

    “Kwa kweli sikumuona mwili mzima ila ni mrembo sana mrefu tena anayejijali sana.”

    “Poa, akirudi nitamuona,” Mustafa alijibu huku akienda ofisini kwake.

    Alipofika alikaa kwenye kiti na kutulia kwa muda kabla ya kuanza kazi, aliwaza kuhusu hali ya mke wake na yaliyomtokea. 




    Alishangaa kiburi cha mkewe kukaidi amri ya Shehna kwa kutumia kipimo cha mimba wakati alikatazwa. Alijikuta akimlaumu mkewe kwa ukaidi alioufanya kufikia hatua ya kupoteza ujauzito.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pia hali aliyoikuta nyumbani kwake ilimtisha sana na kushangazwa kukuta kumesafishwa, hakuna dalili za damu kumwagika. Alijikuta akijiuliza nani aliyefanya usafi ule wakati anaondoka nyumbani hakukuwa na mtu yeyote lakini aliporudi alikuta pamefasafishwa.

    Wazo lake lilikuwa labda shoga yake alipita kumsalimia na kukuta hali ile na kuamua kufanya usafi. Lakini kilichomshtua ni sehemu yenyewe ya tukio kuwa chumbani kwake na kushangaa kama shoga yake aliingia chumbani na kufanya usafi.

    Aliamini kama ni shoga yake lazima atapiga simu kuuliza kilichotokea. Mustafa akiwa katikati ya mawazo, Sara aliingia na faili la kazi na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye dimbwi la mawazo.

    "Bosi vipi?"

    "Poa," Mustafa alijibu huku akinyanyua uso kumtazama Sara.

    "Upo sawa?"

    "Kiasi."

    "Mmh! Bosi basi jana hata sielewi kilichonitokea!"

    "Kitu gani Sara?"

    Basi bosi baada ya wewe kuondoka, ghafla nilichukua vitu vyak..."

    Kabla Sara hajaendelea kumhadithia, alinyamaza baada ya kusikia sauti ya mtu mapokezi.

    Alitoka kwenda kumuangalia, alipofika alishtuka kutomkuta mtu. Lakini ghafla alishangaa kusikia kizunguzungu, alikwenda kwenye kiti chake na kukaa.

    Baada ya kukaa alisikia usingizi mzito, alipojaribu kujiepesha, usingizi ulimpitia. Sara aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kochi nyumbani kwake akiwa na nguo zake za kazini.

    Alishtuka na kujiuliza kinachomtokea ni kweli au anaota, alikumbuka tukio kama hilo lilimtokea jana yake wakati akimpelekea bosi wake vitu vyake baada ya kutoa mbio na kuviacha ofisini.

    Baada ya kukodi gari ambalo aliingia na kumweleza dereva ampeleke anapokaa Mustafa na kushangaa kujikuta amelala nyumbani akiwa na vitu vya bosi wake.

    Alijiuliza ni kitu gani huwa kinamtokea na kujikuta kwenye hali ile ambayo ilianza kumtisha.

    Kwa vile muda ulikuwa umekwenda baada ya kuangalia saa na kumuonesha ni saa mbili usiku, alikwenda kununua chipsi na soda kisha akapanda kitandani kuitafuta siku ya pili.

    ***


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa baada ya kutoka kazini, alipitia hospitali kuangalia hali ya mkewe inaendeleaje. Alimkuta hajambo kiasi ila mwili ndiyo haukuwa na nguvu hivyo kuendelea kuwepo hospitali mpaka siku ya pili.

    Hakutaka kumuulizia ilikuwaje mkewe akakaidi amri ya Shehna na kufanya aliyvotaka. Aliamini sehemu nzuri ya kulizungumza suala hilo ni nyumbani hasa baada ya kuhakikishiwa na daktari kuwa kesho yake angetoka.

    Hakutaka kumsumbua mkewe, alimuacha apumzike na yeye kurudi nyumbani. Alipita kwenye mgahawa na kuchukua chakula cha kubeba ili akalie nyumbani. Alipofika nyumbani, alioga na kupata chakula kisha alichukua ‘laptop' yake na kucheza gemu ya magari ili kuutafuta usingizi.

    Akiwa katikati ya mchezo, alisikia mlango ukigongwa huku akiitwa jina lake, aliacha kucheza gemu na kutoka sebuleni. Alitulia kabla ya kufungua mlango kusikilizia ni nani anayegonga usiku ule.

    "Nani?" aliuliza kwa sauti ya juu kidogo.

    "Mimi," sauti ya kike ilijibu ambayo haikuwa ngeni masikioni mwake lakini hakuikumbuka ni ya nani.

    "Wewe nani?"

    "Shehna."

    "Ka..ka..ribu," Mustafa alishtuka na kupata kigugumizi cha ghafla baada ya kusikia jina la Shehna.

    Alifungua mlango na kulakiwa na harufu nzurii ya manukato, ilikuwa tofauti na aliyoizoea siku zote, ilikuwa nzuri zaidi. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke mzuri sana aliyekuwa amevalia vazi refu la gauni la kumeremeta lililoacha mabega wazi na kufunikwa na mtandio.

    Chini alivaa viatu virefu, alipoangalia nje hakuona gari lolote lililopaki jirani. Kutokana na viatu vile venye kisigino kirefu, aliamini asingeweza kutembea kwa miguu umbali mrefu.

    "Karibu ndani."

    "Asante," Shehna alisema huku akiingia ndani na kulinyanyua juu gauni lake lililokuwa linaguza chini.

    Shehna alikwenda kukaa kwenye kochi na kutulia, Mustafa baada ya kufunga mlango alirudi kukaa kwenye kochi lingine.

    "Karibu sana," Mustafa alimkaribisha tena.

    "Asante za hapa?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh! Nzuri kiasi," Mustafa alijibu huku akimuibia Shehna kumtazama kutokana na uzuri wake, kitu alichokigundua Shehna na kusema huku akiondoa mtandio kichwani na kuziacha nywele zake ndefu nyeusi zionekane vizuri.

    Aliachia tabasamu kama ua la mchana linavyochanya, macho yake makubwa kidogo yaliyopakwa wanja yaliongeza uzuri wake. Yalioneka yameumbwa kwa mahaba tu.

    "Mustafa usipate shida ya kuhangaika kunitazama, una uhuru wa kunitazama upendavyo wala usiniogope."

    "Ha..ha..una..na," kutokana na kushindwa kujiamini maneno yalipandana.

    Mustafa kwa mara ya kwanza alimuona mwanamke mzuri katika maisha yake. Hakugundua kasoro yoyote kwa Shehna, kumbukumbu zake zilimkumbusha ndiye mwanamke aliyefanya naye mapenzi katika ndoto.

    "Mustafa mimi mtu wa kawaida najua uzuri wangu utakubabaisha, nione kama nyama yoyote isiyo na mfupa kwenye kisu kikali."

    "Unatu..tumia kinywaji gani?" Mustafa alijikaza na kumuuliza.

    "Kwa leo sihitaji kitu nataka tuzungumze kitu ili niondoke zangu."

    "Kitu gani?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mustafa unakumbuka nilikuahidi nini?"   




    ITAENDELEA

     

0 comments:

Post a Comment

Blog