Search This Blog

MIMBA YA JINI - 2

 







    Simulizi : Mimba Ya Jini 

    Sehemu Ya Pili (2)







    "Vingi, sijui kipi kimoja wapo."

    "Kuhusu matatizo yako."

    "La kunipatia mtoto."

    "Umempata?"

    "Sijampata."
    "Kwa nini?"

    "Hatukufuata ushauri wako."

    "Toka muanze kuhangaika mkeo aliwahi kupata dalili za ujauzito?"

    "Hapana."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa hiyo kazi yangu nilimaliza?"
    "Bado kwa vile sijapata mtoto."

    "Utapata vipi na mkeo hataki mtoto?"

    "Sasa utanisaidiaje?"

    "Mustafa naomba sasa hivi unisaidie nilichokuomba."

    "Kama kitu kimo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia."
    "Nataka mtoto," Shehna alisema huku akimtazama kwa macho yake ya huruma yaliyojaa mahaba.

    "Mtoto!" Mustafa alishtuka.

    "Ndiyo."

    "Mimi nitampata wapi?"

    "Unawezaje kumpatia mkeo mtoto?"

    "Kwa kukutana kimwili."
    "Basi na mimi namuhitaji kwa njia hiyo."

    "Yaani mimi nifanye mapenzi na wewe?"

    "Ndiyo, kwani kuna ubaya?"

    "Si unajua mimi ni mume wa mtu?"

    "Mustafa hujawahi kutembea nje ya ndoa yako?"
    Swali lile lilimfanya apate kigugumizi kulijibu kwa vile alikuwa na mwanamke aliyempangia chumba na siku nyingine alikwenda kulala kule na kudanganya amekwenda safari ya kikazi.

    "Mustafa unaiheshimu sana pete ya ndoa kwa vile mkeo ni mkorofi na ana wivu sana, lakini huiheshimu ndoa yako. Au mimi kutaka kuzaa na wewe umeniona malaya?"

    "Ha...ha...pana Shehna sijakufikiria hivyo."

    "Sasa nipe jibu moja, utanipatia mtoto au hunipi?"
    "Nitakupatia."

    "Nimefurahi kusikia hivyo, nakuahidi kukupa zawadi kubwa sana katika maisha yako."

    "Nitafurahi sana."

    "Mustafa natoka mara moja nitarudi muda si mrefu."

    "Kwa hiyo nifunge mlango."

    "Usifunge narudi sasa hivi."
    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mustafa aliota akifanya mapenzi na Shehna huku akiahidiwa kuwa tajiri mkubwa duniani kama atampatia ujauzito. Aliposhtuka usiku alijikuta amelala sehemu ngeni machoni mwake. Ilikuwa sehemu nzuri sana ambayo hakuwahi kufika. Pembeni yake alikuwepo Shehna aliyepitiwa na usingizi.
    Wote walikuwa wamelala kwenye shuka moja bila ya nguo nyingine, Mustafa alishtuka na kujiuliza ile ni ndoto au kweli. Alijaribu kujifinya ili apate ukweli alihisi maumivu, alijiuliza alikuwa wapi na alifikaje.

    Ghafla alishikwa na usingizi na alipoamka alijikuta kitandani kwake akiwa amechoka sana. Alionesha alitumika usiku lakini bado alibakia njia panda kama alitumika Shehna alikuwa wapi.

    Alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga, nyumba nzima ilikuwa ikinukia manukato ya Shehna.

    "Mustafa," sauti ya Shehna ilimshtua.
    "Naam."

    "Chai tayari," Shehna aliingia chumbani akiwa amejifunga mtandio bila nguo nyingine na kuufanya mwili wake mantashau uonekane wazi. Alimshika mkono hadi mezani kulipokuwa na kifungua kinywa kitamu kilichomfanya Mustafa amsifie.

    "Hakika Mungu kakujalia kila kitu."

    "Kama nini?"

    "Mambo ya siri na bayana."
    "Asante, nioe basi niwe mke wa pili."

    "Itabidi nifanye hivyo."

    "Wewee! Mkeo atakufa kwa kihoro ana wivu sana."

    "Sasa itakuwaje?"
    "Shida yangu kwako mtoto tu nakuacha na mama wivu wako."

    Baada ya chai waliondoka pamoja kwa Mustafa kupitia hospitali na Shehna kushukia kwenye mataa ya barabarani.

    "Mustafa nishushie hapa."

    Mustafa alimshusha na Shehna alienda zake japo hakujua anakwenda wapi wala anakaa wapi. Alielekea moja kwa moja hospitali kumuona mkewe.




    Mustafa akiwa njiani kuelekea hospitali alikuwa mtu mwenye mawazo mengi kutokana na kila kitu kilichomtokea na kujiuliza Shehna ni kiumbe wa aina gani? Japokuwa alikuwa mwanadamu wa kawaida lakini matukio yake yalimchanganya sana na kujikuta akiingia hofu ya kila alichokiona ambacho hakikuwa cha kawaida.

    Aliushangaa uwezo wa Shehna wa kuelewa vitu vingi vinavyoonekana na vilivyojificha. Alikuwa amefanya siri ambayo hata mkewe na watu wengi hawakuijua kama ana nyumba ndogo. Lakini yeye aliijua bila kumwambia, alijiuliza ni nani kwenye uganga hayupo kwa vile alionekana mwanamke mrembo tena mwenye kujipenda.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tofauti na waganga wengi ambao wengi wao huwa hawajipendi, mavazi yao huwa ya kujiachia wala hawajui mapambo na manukato.

    "Sasa Shehna ni nani...au jini? Ha...hapana huko nimefika mbali," Mustafa alijiuliza na kukataa mwenyewe.

    "Mbona jana niliota nimelala naye sehemu nzuri lakini nilipoamka nilijikuta nipo nyumbani kwangu? Na Shehna alirudi saa ngapi na kwa nini hakuniamsha mpaka niliposhtuka asubuhi na kujikuta nimetumika kutokana na kufanya naye mapenzi ya ndotoni.

    "Mmh! Shehna mbona anataka kunipa mtihani mzito, anataka nizae naye kwa ahadi ya kumpatia mtoto kupitia kwa mke wangu. Sasa mbona ametaka azae yeye kwanza? Mmh! Kazi ipo."

    Alijikuta amefika hospitali bila kupata jibu kitu kinachomtatiza kuhusu Shehna. Aliingia hospitali na kwenda chumba alicholala mkewe, alimkuta akiwa amejiandaa kutoka baada ya kupewa ruhusa mapema.

    "Yaani mume wangu unajua naumwa unaniacha mpaka saa hizi?" Husna alimuuliza kwa hasira.

    "Tabia hii imeanza lini, hata salamu unafikia kunilaumu, ningekufa ungefurahi?" Mustafa alijibu kwa hasira.

    "Ufe na nini?"

    "Kwa vile hukutaka kujua haina muhimu, unaendeleaje?" Mustafa naye alikuwa mkali kwa mkewe.

    "Nisamehe mume wangu nilichanganyikiwa baada ya kuchelewa kukuona wivu uliniingia, ulipatwa na nini mume wangu?"

    "Ilitakiwa tusalimiane tujuliane hali kisha tuzungumze mambo mengine."

    "Ni kweli, nisamehe mume wangu nimekosa wivu wakati mwingine ugonjwa."

    "Nimekukataza mara ngapi sipendi wivu wa kijinga, kila siku umekuwa ukiniona akili yangu unawaza ujinga."

    Mustafa alimjia juu mkewe kwa vile alikuwa amepata nafasi, naye alikuwa amechoka na wivu wa kijinga wa mkewe ambao uligeuka kero kitu kilichosababisha kuanzisha uhusiano na mwanamke ambaye mkewe alimshtumu anatembea naye. Mwanamke huyo ilitokana na kushtumiwa na mkewe kwa hisia bila ukweli.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa hasira alifanya kweli kwa kutembea na yule mwanamke ambaye baadaye alimfanya nyumba ndogo na kumuhamisha mtaa ule na kwenda kumpangia sehemu nyingine na kuendeleza mapenzi kwa siri.

    Siri ile aliijua peke yake hata rafiki yake hakujua kama ana nyumba ndogo, lakini alishangaa Shehna kuijua.

    "Mume wangu huna dogo, nimekosa nisamehe."

    "Sawa, vipi unaendeleaje?"

    "Namshukuru Mungu sijambo japokuwa mwili hauna nguvu."

    "Pole mke wangu, wakati nakuja kuna mwendesha pikipiki alijigonga kwenye gari langu, watu wakajua nimemgonga wakataka kunipiga lakini askari wa barabarani alifika na kuniokoa," Mustafa alitengeneza uongo ili kumpoza mkewe.

    "Jamani pole mume wangu!" Husna alisema kwa sauti ya huruma.

    "Asante."

    Mustafa alimchukua mkewe na kurudi naye nyumbani, alipofika alijikuta akitaka kujua kipi kilimfanya akaidi amri ya Shehna. Baada ya kutulia kwa muda alimsemesha mkewe.

    "Mke wangu."

    "Abee, mume wangu."

    "Kipi kilichokufanya umuue mtoto wangu?"

    "Mume wangu kupima ujauzito ni kumuua mtoto?" Husna alishtuka.

    "Shehna alituambia nini?"

    "Mume wangu utaamini vipi una ujauzito bila kupima?" Husna alijitetea.

    "Si alitukataza?"

    "Ndiyo! Lakini bado nilishindwa kumuamini, mume wangu kwanza Shehna ni nani mbona masharti yake ya ajabuajabu?"

    "Mke wangu tumehangaika sehemu ngapi tumepewa masharti mangapi tuliyoyatekeleza, yaani hili ndilo umeliona gumu?"

    "Mi nimechoka kila siku masharti magumu."

    "Ha! Mke wangu umeweza kulala makaburini kutafuta mtoto, umeona kazi kutotumia dawa za kizungu ikiwa hali yako ilikuwa nzuri?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mume wangu mimi nina wasiwasi huyu mwanamke si mwanadamu!"

    "Mke wangu shida yetu mtoto au kujua Shehna ni mtu au jini?"

    "Mi simuelewielewi."

    "Mke wangu Shehna si jini ni mwanadamu pia si mganga."

    "Ni nani?"

    "Nimekuambia mtu."

    "Kama si jini wala mganga ni nani mbona unataka kutusaidia?"

    "Yule dada alipatwa na tatizo kama letu kuna siku nilimsikia akizungumza na mtu jinsi alivyohangaika kutafuta mtoto na kufanikiwa kupata. Nilivutiwa na habari zake na kumuomba anisaidie. Aliahidi kunisaidia na ndicho alichotusaidia, sasa mke wangu kipi kilichokutuma kuniulia mwanangu?" Mustafa alimuuliza akiwa amemkazia macho mkewe.

    "Mume wangu sikujua," Husna alikuwa mpole.

    "Sasa tutafanya nini? Lazima Shehna tumemuudhi tutafanyaje, kumbuka mke wangu tumehangaika sehemu ngapi hatukuona dalili za mimba hata siku moja. Lakini dawa ya Shehna siku moja na mimba juu."

    "Dah! Sijui itakuwaje ukimuona naomba uniombee msamaha, nipo radhi kufuata masharti yoyote atakayonipa."

    "Mmh! Sijui!"

    "Mume wangu tusitake kujihukumu, najua lazima atapiga simu, naomba umweleze aje nyumbani ili nimuombe msamaha au nimfuate popote."

    "Sawa nikimuona au kunipigia simu nitafanya hivyo."

    Mustafa alimuaga Husna na kwenda kazini kwa vile alichelewa kutokana na kumfuata mkewe hospitali.

    ***

    Mustafa baada ya kufika ofisini, alijawa na mawazo kuhusiana na matukio yote yaliyokuwa yakimtokea. Bado alikuwa njia panda kutokana na Shehna mwanamke mrembo aliyeonesha mapenzi mazito kwake. Lakini mambo yake yalionekana kama yana muujiza yaliyokuwa kila siku yanamstaajabisha.

    Alijiuliza alimjulia wapi mpaka kumpenda kiasi kile, kutokana na mavazi na vito vyote alivyovaa vilikuwa vya thamani kubwa sana. Ilionesha anatoka katika familia yenye uwezo mkubwa sana. Alipanga akikutana naye amuulize vizuri ajue alimuonea wapi na kipi kilichomfanya ampende na kupelekea kutaka kuzaa naye na si mwanaume mwingine.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sara akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, sekretari wake aliingia ofisini na kushangaa kumkuta bosi wake amezama kwenye mawazo. Toka aingie ilikuwa ilimeta saa moja bila kugusa kitu zaidi ya kuzama kwenye mawazo. Alimwita na kumfanya ashtuke.

    "Vipi bosi mbona upo mbali kimawazo?"

    "Wee acha tu, vipi unasemaje?" alijibu huku akifuta mikono usoni na kujinyoosha kama mtu mwenye usingizi au aliyechoka sana.

    "Nimekupigia simu ya mezani nashangaa inaita bila kupokelewa, naingia ndani naona upo kwenye dimbwi la mawazo. Unajua bosi siku hizi sikuelewi kabisa inaonekana hapo sawa."

    "Nipo sawa, ulikuwa unasemaje?" Mustafa alijibu huku akijiweka sawa kitini na kuiweka sawa Laptop iliyokuwa juu ya meza.

    "Kuna mgeni wako."

    "Duh! Akili yangu haijakaa sawa mwambie arudi baadaye," alijibu huku akifungua kazi kwenye desktop.

    "Lakini mgeni unamjua?"

    "Kwani nani?"

    "Yule dada mrembo."

    "Ooh! Kumbe Shehna mwambie apite."

    "Unaona!" Sara alisema huku akitabasamu na kutoka nje.

    Mustafa alishtuka na kushangaa kumfuata ofisini ikiwa walilala pamoja na kuachana muda mfupi. Akiwa ameinama alishtuliwa na harufu ya manukato na sauti tamu ya Shehna.

    "Asalamu aleykum Mustafa."

    "Waleykum salam Shehna."

    Alinyanyua uso na kukutana na Shehna akiwa katika vazi la hijabu iliyomziba mwili mzima. Baada ya kuketi aliiondoa nikabu iliyomziba uso na kufanya aonekane vizuri kisha alitikisa nywele zake nyingi nyeusi na kufanya zichanue kama ua huku tabasamu mwanana akilichanua na kumfanya Mustafa kujiona kama yupo ndotoni.

    Alitulia na kumtazama Mustafa aliyekuwa ametulia kama mtu aliyekuwa akitazama picha nzuri na kuitikia kama ameitwa.

    "Abee mpenzi," Shehna aliitikia bila kuitwa kitu kilichomshtua Mustafa na kumuuliza:

    "Shehna mbona unaitikia? Sijakuita."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mustafa uniite mara ngapi?"Shehna alimtazama Mustafa usomi huku macho yake makubwa kidogo ya kusinzia yaliyopakwa wanja na kufanya azidi kupendeza. Hakika Shehna alikuwa mrembo wa warembo.

    "Haki ya nani Shehna sijakuita," Mustafa alijitetea kwa kuamini toka aachane naye hajapiga simu wala kuonana naye.

    "Huna kitu unachotaka kuniuliza?" Shehna alimuuliza huku amemkazia macho ambayo yalizidisha uzuri wake.




    Ninacho lakini nilijua tutaonana jioni.”

    “Sawa angeniuliza jioni lakini toka ufike una muda gani?”

    “Zaidi ya saa nzima.”

    “Umeishafanya kazi gani?”

    “Bado sijaanza.”

    “Kwa nini?”

    “Sina kazi nyingi ningefanya wakati wowote.”

    “Kwa hiyo Mustafa unataka kunidanganya hata mimi?”

    “Kwa nini unasema hivyo?”

    “Mustafa toka uingie kuna vitu vinakutatiza na kujikuta muda mwingi ukijiuliza maswali mengi ambayo unaamini mwenye majibu yake ni mimi, uongo?”

    “Kweli.”

    “Haya niulize.”

    “Kwa nini tusizungumze jioni kwa vile huu ni muda wa kazi!”

    “Mustafa mi si mjinga kuacha kazi zangu na kuja kukusikiliza, najua leo huwezi kufanya kazi mpaka upatiwe majibu ya maswali yako.”

    “Umejuaje nataka kukuuliza?”

    “Mustafa muhimu kwa muda huu kujua nimejuaje au kukujibu maswali yako.”

    “Samahani Shehna.”

    “Mustafa kama nisingekuwa mimi usingemruhusu mtu kuingia ndani, uongo kweli?”

    “Kwa baadaye lazima ningewaruhusu.”

    “Kwa hiyo niondoke?”

    “Ha...hapana.”

    “Unajua kuna kitu kimenifurahisha sana leo ambacho nimepanga kukuzawadia, lakini unataka kuniudhi.”

    “Shehna samahani kama nitakukosea lakini naamini wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo maana nipo hapa.”

    “Kuna mengi ya kukuuliza nashindwa nianze na lipi.”

    “La mkeo.”

    “Umejuaje?”

    “Mustafa acha kuwa mgeni wa dunia kushtuka kila kitu, uliza ili ujibiwe si kujua nimejuaje.”

    Mustafa alizidi kumshangaa Shehna kuyajua yaliyojificha moyoni mwake, alijiuliza yeye ni kiumbe wa aina gani mwenye uwezo wa ajabu kama ule? Hakuwa na jinsi alimueleza aliyoelezwa na mkewe juu ya kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea.

    “Mustafa nimemsamehe kwa vile nakupenda lakini mkeo ana kiburi, masharti mengi amekuwa akiyavunja matokeo yake mnatumia fedha nyingi na nguvu nyingi bila mafanikio.”

    “Sasa utanisaidiaje?”

    “Unataka msaada wangu upi?”

    “Bado tunataka mtoto.”

    “Mmechelewa.”

    “Kivipi?’

    “Unakumbuka nilikuambia nini?”

    “Vitu vingi, kimoja wapo?”

    “Kuhusu kupata mtoto.”

    “Si ulisema utanipa mimi kwanza ndipo nikupe wewe.”

    “Ni kweli, lakini makosa ya mkeo yamefanya mambo yabadilike.”

    “Kivipi?”

    “Zoezi la mimi kupata mtoto nimelianza usiku wa leo.”



    Sasa tatizo nini?”

    “Tatizo hatuwezi kushea watu wawili kupata mtoto kwa vile wewe sasa hivi una mbegu moja baada ya mkeo kuiharibu ya kwanza iliyokuwa yake.”

    “Mmh! Kwa hiyo unataka kuniambia na wewe mjamzito sasa?”

    “Hapana.”

    “Kwa nini hukupata wakati dawa unaijua?”

    “Mimi ni tofauti na mkeo lazima nilale na wewe mwezi mzima mfululizo, tukiacha hata siku moja tumeharibu dozi na muda huo wote usikutane na mkeo.”

    “Dah! Itawezekanaje nilale mwezi mzima na mke wangu bila kukutana naye, akinitaka nitafanyaje?”


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wala usihofu hawezi kukugusa mpaka mwezi uishe.”

    “Mmh! Sawa.”

    “Nina imani swali moja nimekujibu uliza lingine.”

    “Nafikiri hili ndilo la muhimu mengine siyo muhimu sana.”

    “Mustafa yote muhimu, nipo hapa kukufanya uwe huru na kuondoa wasiwasi wote.”

     




    "Mmh! Anyway, hivi Shehna tulionana wapi kabla na kipi kilichokuvutia kwangu kupelekea kutaka kuzaa na mimi na kuwaacha wanaume wengi wasio na wanawake?"

    Shehna kabla ya kujibu alicheka kidogo kisha alitabasamu huku aibu ya kike ikimtawala na kuanza kuchezea kucha na kupeleka vidole mdomoni. Mustafa alitumia muda ule kuusanifu uzuri wa Shehna na kushangaa aibu iliyompata kutokana na swali lake.

    "Shehna kama swali langu limekuudhi naomba unisamehe, naweza kubadili swali," Mustafa alijihami.

    "Hapana, sivyo hivyo swali lako lazima nilijibu kwa vile nipo hapa kwa ajili ya kuondoa wasiwasi wa moyo wako. Mustafa huwezi kuamini nimekupenda muda mrefu sana hata kabla ya kuwa na Husna.

    "Mapenzi yangu hayajaanza leo ni muda mrefu nimekuwa nakupenda. Katika maisha yangu nilitamani uwe mume wangu lakini kuna vikwanzo ambavyo vilisababisha nichelewe kukueleza ukweli wa moyo wangu.

    "Bahati nilipata safari ya ghafla na kuondoka bila kukueleza dhamira yangu ungeweza kunisubiri. Niliporudi nilikuta tayari umeoa lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kutaka hata nipate angalau ukumbusho wa sura yako, ndiyo maana nikataka kuzaa na wewe.

    "Wakati napanga hivyo, niligundua una maumivu moyoni mwako kutokana na kuchelewa kupata mtoto. Baada ya kufanya uchunguzi, ilionesha umepoteza fedha nyingi kwenda kwa waganga bila mafanikio. Niliamini nikitatua tatizo ambalo limekunyima furaha, utakuwa tayari kunisikiliza na mimi shida yangu.

    "Ndipo nilipokutafuta kwa njia ya simu na kukupa maelekezo ambayo mwenyewe uliona maajabu lakini kiburi cha mkeo kikaharibu kila kitu.

    "Kwa vile nilipanga baada ya wewe kupata mtoto ndipo na mimi nipate wangu, basi baada ya mkeo kuvuruga ratiba, itabidi unipe kwanza mimi ujautito ndipo nikupe dawa ya kutafuta mtoto mwingine ambayo mkeo anatakiwa kuwa makini kosa lingine litamfanya awe tasa, hatazaa mpaka anakufa.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mustafa kama nilivyokueleza mapenzi yangu kwako hayakuanza leo bali muda mrefu, tumeonana sehemu nyingi lakini inaonesha umenisahau. Unakumbuka siku moja tulikutana ukitoka kufanya usaili ambapo ulikuwa mnyonge baada ya kujua amefanya vibaya.

    "Nilikueleza kuwa pamoja na kufanya vibaya lazima jina lako litachaguliwa kati ya matano na kubakishwa jijini Dar. Najua ulishangaa lakini baada ya muda, ilitokea kama nilivyokueleza. Unakumbuka ulikutana na nani akakueleza habari zile?"

    Maneno yale yalimfanya Mustafa ashtuke na kurudisha kumbukumbu nyuma miaka nane iliyopita. Siku aliyokwenda kufanya usaili wa kazi ambako walitakiwa watu watano katika watu mia moja waliokuwepo. Katika watu waliofanya vibaya katika usaili ule yeye alikuwa mmoja wapo, katika maswali kumi aliyoulizwa alijibu matatu hata nusu hakufika.

    Hata waliokuwa wakiwafanyia usaili, walimkatisha tamaa baada ya kumweleza hakuweza kufika nusu tofauti na wenzake zaidi ya sabini waliotangulia. Aliondoka akiwa hana matumaini.

    Lakini alipotoka nje ya ofisi ili aelekee nyumbani, aliitwa na msichana aliyekuwa amevaa hijabu iliyomziba mwili mzima na kuonekana macho.

    "Mustafa."

    "Naam," aligeuka kumtazama aliyeonekana anamfahamu, hakuweza kumuona uso zaidi ya macho.

    "Pole."

    "Ya nini?"

    "Ya kufanya vibaya.'

    ‘Umejuaje?"

    "Mbona umeniangusha kwa nini umeshindwa kujibu maswali yale mepesi?"

    "Yaani hata sijui."

    Yule msichana aliyarudia maswali yale na kumuuliza:

    "Sasa hapa swali gani gumu?"

    "Yaani hata mimi nashangaa, basi tena nitajaribu sehemu nyingine."

    "Mbona umekata tamaa mapema?"

    "Kama nimefanya vibaya huku zaidi ya watu sabini wamefanya vizuri huku nafasi tano tu zinatakiwa, kuna nini hapo?"

    "Usiwe na wasiwasi katika hizo nafasi tano, wewe utakuwemo na ndiye utakayebakia Dar."

    "Wewe nani?"

    "Mustafa shida yako kujua mimi nani au wewe kupata kazi na kuteuliwa kubakia Dar?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Shida yangu kupata kazi."

    "Basi subiri muda ufike."

    "Nitajuaje?"

    "Utapigiwa simu."

    "Wataijuaje namba yangu ya simu wakati hawakuchukua kwa vile ni mmoja ya watu waliofanya vibaya."

    "Namba yako nitawapa."

    "Namba yangu umeipata wapi?"

    "Mustafa hujawahi kuigawa namba yako?"

    "Nimegawa basi nitashukuru japokuwa najua hakuna kitu."

    "Siku tukikutana utaniambia."




    Mustafa aliagana na yule msichana mwenye lafudhi ya mwambao bila kumuuliza jina. Siku moja akiwa hana hili wala lile alipigiwa simu kujulishwa amefanikiwa kupita katika mchujo wa usaili na yeye ndiye aliyefanya vizuri kuliko wote anatakiwa kubakia Dar es Salaam.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alishtuka sana lakini hakuamini aliona kama watu wanamchezea akili, siku ya pili alikwenda ofisini kujaribu lakini alipotaja jina lake alikabirishwa na kujaza fomu ya kuajiliwa na wiki iliyofuata alianza kazi kwa kupewa ofisi na sekretari pamoja na mshahara mzuri.
    Lakini Mustafa alisahau kama kuna mtu alimweleza taarifa kuwa atapita kwenye usaili na atabakia jijini Dar japokuwa alikuwa amefanya vibaya sana.

    Furaha ya kupata kazi ilimfanya asitumie muda kuwaza ilikuwaje mpaka kupita na msichana yule alijuaje. Mustafa alitulia na kuvuta kumbukumbu kisha aliteremsha macho kumuangalia Shehna na kuamini kabisa ndiye yeye. Kwa lafudhi aliyoitumia japokuwa alimuona macho tu aliamini kabisa ndiye msichana aliyemtabilia mambo ya ajabu.

    "Dah! Kweli."
    "Kweli nini?" Shehna alimuuliza akiwa anamtazama usoni.

    "Nimekumbuka, hivi ulijuaje mi nitapita wakati nilikuwa najua nimefanya vibaya?"

    "Leo siyo siku yakeikifika nitakueleza, mpaka hapo nina imani baadhi ya vitu umevielewa kama una swali niulize."

    "Swali lingine nilitaka kujua wewe unakaa wapi katika familia yenu mpo wangapi, kwa sasa unajishughulisha na nini. Wewe ni mganga au nani?"
    "Ninapokaa si rahisi kukuelekeza mpaka twende pamoja, katika familia yetu tupo watatu wote wanawake mimi ni mtoto wa mwisho na swali la mwisho mimi si mganga wala mnajimu ila Mungu kanipa uwezo wa kuyajua matatizo ya mwenzangu."

    "Kwa nini huwezi kupata ujauzito kwa mara moja kama mke wangu?"

    "Dawa ya haraka nilikuwa nayo moja ambayo nilimpa mkeo hii inachelewa, kwa vile nami nina hamu ya mtoto sina jinsi lazima nitumie njia ya muda mrefu."
    "Kingine unajua sijawahi kulala nje ya nyumbani kwangu nitafanyaje?"

    "Mustafa nyumba ndogo huwa unalala nayo nyumbani kwako?"

    "Mmh!" Mustafa aliguna baada ya kujua ameumbuka.

    "Najua wasiwasi wako kulala nje ya nyumba yako mwezi mzima, nitalala na wewe mwezi huo mzima nyumbani kwako na kitandani kwako."

    "He! Na mke wangu atakuwa wapi?" Mustafa alioshtuka.
    "Atakuwepo ndani."

    "Siwezi kufanya mapenzi ndani na mke wangu akiwemo itakuwa kumdhalilisha."

    "Mustafa naomba unisikilize, wewe kila siku naomba ukilala usiku wakati mnataka kulala hakikisha wewe unakuchelewa kulala usikubali hata siku moja mkeo akukute kitandani. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mkeo akiisha lala utaingia bafuni kuoga na kujipaka mafuta nitakayokupa.

    Isipande kitandani hakikisha mlango wako umeurudisha bila kuufunga au dirisha ili nikija nisipate tabu ya kuingia.
    "Ukiishapanda kitandani usilale na nguo ya ndani kisha hakikisha mkeo analala ukutani wewe lala katikati ya kitanda mimi nikija nitalala mwanzoni mwa kitanda. Mpake mkeo mafuta kichwani kisha lala."

    "Mmh! Nitaweza kweli, mbona unanipa mtihani, kwa nini tusiwe tunakutana hotel na tukimaliza haja zetu, narudi nyumbani kulala?"
    "Mustafa kutafuta kwangu mtoto natakiwa kupata dozi ya mara tatu kwa usiku mmoja hivyo lazima nilale na wewe."

    "Una maanisha dozi ya kivipi."

    "Ya saa sita, saa tisa na kumi na moja alfajiri, unaweza kulala nje?"

    "Shehna mbona unanipa mtihani mgumu."
    "Mbona wako niliuweza wa kwenda kubadili matokeo ya usaili ili upite kama ningekamatwa ningekuwa wapi?" Shehna alimuuliza Mustafa akiwa amemkazia macho huku sura ya uzuri iligeuka kama mzee na kumtisha Mustafa.



    "Mustafa nimejitolea katika mambo yake mengi ambayo wewe huyajui, yaani kwa hili moja umeshindwa. Unakumbuka ulitaka kufukuzwa kazi mimi ndiye niliyerekebisha mahesabu ili ubakie kazini?

    Wewe ni mtu gani usiyejiuliza kila kosa lako halionekani?" Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka.

    Kauli ile ilimshtua sana Mustafa na kuzidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe wa aina gani. Alikumbuka baada ya kupata nyumba ndogo alijikuta akitaka kumfurahisha, alijikuta akifanya ubadhilifu wa fedha kazini kwake.

    Taarifa ilifika ofisi kuu na kufanya mahesabu ya ghafla huku akisimamishwa kazi kupisha wafanye mahesabu.

    Kitendo kile kilimshtua Mustafa na kujikuta akipandwa na presha na kulazwa hospitali kwa kujua hana kazi na lazima afungwe kwa vile alichota zaidi ya milioni kumi na tano.

    Siku ile akiwa hospitali majira ya usiku wa manane aliamshwa na daktari binti mrembo wa Kiarabu aliyekuwa amesimama pembeni ya kitanda chake.

    Alikuwa amevalia mavazi ya kidaktari na miwani myeupe nywele zake zilikuwa ndefu na nyeusi. Alikuwa binti mrembo sana, hakuwahi kumuona mwanamke mzuri kama yule katika maisha yake na kumwita jina lake. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mustafa."

    "Naam."

    "Pole sana."

    "Asante."

    "Tatizo nini?"

    "Wanadamu wabaya wamenisingizia nimekula fedha ya kampuni wakati sijala hata senti tano."

    "Mustafa kuwa mkweli, fedha umekula. Heri ungeijengea familia yako, wazazi wako wanaishi maisha ya kubahatisha kuliko ulichokifanya kumhonga hawara."

    Kauli ile ilimshtua Mustafa na kujiuliza yule daktari amejuaje au kuna mtu alimwambia, ilibidi amuulize amejuaje.

    "We umejuaje?"

    "Mustafa muhimu si kujua nimejuaje zaidi ya kukusaidia usifukuzwe kazi na kufungwa."

    "Utafanyaje?"

    "Kazi hiyo niachie mimi," Mustafa alizidi kumshangaa daktari atamsaidia vipi, daktari alitabasamu na kuzitikisa nywele zake ndefu nyeusi zilizoongeza uzuri wake.

    "Mustafa bai."

    Mustafa siku ya pili aliposhtuka alijua ile ilikuwa ni ndoto kwa vile pale hospitali hakukuwa na daktari wa vile. Lakini ajabu siku iliyofuata alielezwa arudi kazini kila kitu kimekutwa kipo sawa hakukuwa na hasara yoyote kwenye fedha ya kampuni. Japokuwa aliona kama ndoto iliyo na ukweli, hakutaka kushughulika nayo zaidi ya kushukuru kuponea tundu la sindano.

    "Mustafa unakumbuka siku hiyo?"

    Mustafa baada ya kuvuta kumbukumbu alijikuta akizidi kumshangaa Shehna na kujiuliza ni kiumbe gani aliyekuwa karibu ya matatizo yake muda wote na kujiuliza amekuwa akijuaje na kutokea kumsaidia. Alijiuliza alifanyaje mpaka hesabu zikakutwa zipo sawa wakati alijua tayari hana kazi na jela ilikuwa ikimwita.

    Shehna baada ya kumuona Mustafa amehama kimawazo, alimuuliza tena swali lake la awali.

    "Mustafa unakumbuka? Au umesahau maana akili yako ina ubongo wa samaki."

    "Nakumbuka."

    "Uliiba hela hukuiba?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Niliiba."

    "Unajua kwa nini ulibakia kazini?"

    "Sijui."

    "Hukujiuliza uliporudishwa kazini wakati ukijua umefanya makosa?"

    "Kwa kweli nilipitiwa kwa hilo."

    "Mustafa wewe ni mwanadamu gani usiyejiuliza unakwenda kama mnyama?"

    "Hata sijui nikuambie nini ili unielewe."

    "Inaoneka hata ukipewa kitu hujui kusema asante."

    "Shehna ukisema hivyo utanionea, kwa vile mazingira yake yalikuwa kama muujiza au kitu cha ndotoni. Hata wewe baada ya kunifanyia ulitakiwa kujitokeza na kunieleza ili nijue kwa kumshukuru."

    "Basi elewa yote hayo niliyafanya kwa ajili yako, kama nilivyokueleza nilipata safari ya ghafla, pia nilitaka kujitokeza muda muafaka kama huu."

    "Ulifanyaje?"

    "Leo siyo siku yake muhimu ni hili langu, kwa nini hili langu dogo hutaki kunisaidia hujiulizi kuna wanaume wangapi lakini nimekupenda wewe?" Shehna alimuuliza huku machozi yakimtoka na kuyafanya macho yake kuwa mekundu na kuongeza uzuri wake kama njiwa manga.

    "Basi nitajitahidi kufanya unavyotaka japokuwa unanipa mtihani mzito."

    "Si mtihani kama unavyoona, hebu jaribu leo utaniambia fanya yote niliyokuelekeza kama mkeo atajua basi mimi navunja mapenzi na wewe."

    "Shehna sitaki kukupoteza," Mustafa alichangwanywa na uzuri wa Shehna.

    "Basi fanya hivyo."

    "Nitafanya kwa ajili nakupenda."

    Shehna alifurahi na kwenda kumkumbatia Mustafa na kumpiga mabusu.




    "Katika siku uliyonifurahisha leo imezidi siku zote, Mustafa ukizaa na mimi nitakupa zawadi kubwa ambayo hukuwahi kuiota maishani mwako."

    "Nitashukuru."

    "Kingine ulichonifurahisha kutengeneza uongo kwa mkeo juu yangu, imenifanya nizidi kukupenda."

    "Lazima nifanye hivyo wewe ni mtu muhimu sana kwangu."

    "Basi acha nikuache uendelee na kazi tutaonana usiku."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hakuna tatizo."

    Shehna aliaga na kuondoka na kumuacha Mustafa akiendelea na kazi, baada ya muda Mustafa alitoka kufuata kitu kwenye gari. Alipofika mapokezi alishangaa kukuta rafiki yake kipenzi James akimsubiri.

    "Ooh! James umefika zamani?"

    "Kama nusu saa nimeambiwa una mgeni."

    "Mbona ametoka muda mrefu."

    "Bosi ametoka kapitia wapi?" Sara aliuliza.

    "Jamani si hapa au ulipitiwa na usingizi?"

    "Hatujamuona mtu, mgeni mwenyewe labda jini?"

    Sara alisema jina ambalo siku zote lilikaa mdomoni kwake na kumchefua sana Shehna na kupanga kumkomesha na tabia yake ya kumwita jini. Alipanga usiku kabla ya kwenda kwa Mustafa aanzie kwa Sara ili kumkomesha aachane na kufuatilia mambo yake.

    "Sara sitaki tena kusikia ukitamka jina hilo, siku hizi umenizoea sana eti eeh? Unasema lolote mdomoni mwako," Mustafa alimfokea Sara ilikuwa ni mara ya kwanza kukasirika toka aanze naye kazi miaka saba iliyopita.

    "Samahani sana bosi," Sara alishtuka huku woga ukimtawala.

    "Katika siku uliyoniudhi leo umeniudhi sana, una bahati nina mgeni ningekufukuza kazi sasa hivi," Mustafa alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni.

    "Bosi nisamehe, nilisema kwa utani sikujua kama nitakuudhi kiasi hiki," Sara alijitetea.

    "Nitamalizana na wewe baadaye ngoja nizungumze kwanza na mgeni wangu."

    "Kwani tatizo nini mpaka ukwazike hivyo?" James aliuliza.

    "James, tuzungumze yetu huyu nitamalizana naye."

    James ilibidi anyamaze kwa vile hakujua chanzo cha Mustafa kukasirika vile kilitokana na nini, siku zote alimjua ni mkimya na mpole. Waliingia ofisini huku Mustafa akiwa bado ana hasira, kabla ya kuzungumza aliinama kwa muda kuonesha Sara amemuudhi sana.

    "Kwani best kipi kimekukwaza hivyo?"

    "U...u...u na..," Musfata alinyamaza baada ya simu yake kuita, alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna aliipokea.

    "Haloo."

    "Mustafa."


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naam."

    "Mbona kama haupo sawa?"

    "Kwa nini?"

    "Sauti yako inajieleza."

    "Si huyu mshenzi leo atanitambua namfukuza kazi."

    "Kwa nini?"

    "Sikufurahia alivyokuita."

    "Ananiitaje?" Shehna alijifanya hajui kitu.

    "Eti anakufananisha na jini."

    "Hapana mpenzi usimfukuze kazi."

    "Kwa nini?"

    "Ameropoka kwa bahati mbaya, sitaki mimi kuwa na wewe tuongeze maadui."

    "Kwa hiyo?"

    "Mpe onyo tu, hawezi kurudia."

    "Ana bahati bila wewe ningemfukuza kazi sasa hivi."

    "Msamehe kuanzia sasa fungua moyo wako zungumza na mgeni kwa uchangamfu."

    "Sawa nitafanya hivyo."

    "Naomba ucheke kidogo basi," Shehna alisema kwa sauti tamu iliyofanya Mustafa acheke.

    "Haya mpenzi wangu kazi njema."

    "Asante nawe siku njema."

    Wakati huo Sara alikuwa kwenye hali mbaya kwa kujua siku ile ndiyo ya kufukuzwa, kazi ilimshinda, mapigo ya moyo yalimwenda mbio. Alijiinamia kwenye meza huku mkono mmoja ukiwa kifuani kuzuia mapigo ya moyo yaliyokuwa yakienda kwa kasi. Mustafa baada ya kuzungumza na mgeni wake alitoka kumsindikiza, alishangaa kumkuta Sara akiwa amejiinamia huku akilia kilio cha kwikwi.

    "Sara una nini?"

    "Sina kitu, nitafanya nini nawe hutaki kunisamehe?"

    "Yale yameisha ila siku nyingine kuwa makini na kauli zako kwa wageni wangu hasa Shehna."

    "A...a...sante bosi sirudii tena," Sara alitaka kumshika miguu, lakini Mustafa alimuwahi kumshika na kumnyanyua juu. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majira ya usiku Mustafa alikumbuka maelekezo aliyopewa na Shehna, alimuacha mkewe atangulie kitandani na yeye kubaki sebuleni akijifanya kuwa bize na lap top yake. Mkewe alimshangaa mumewe siku ile kuwa bize vile wakati alimwambia hawezi kufanya kazi za ofisini akishafika nyumbani.

    Baada ya kumsubiri mumewe kitandani kwa hamu kubwa, alishangaa kuona haji. Alitoka hadi sebuleni na kumkuta akijifanya yupo bize la Laptop yake.

    "Mume wangu imeanza lini muda wa kulala uanze kazi?"

    "Kuna kazi nilitakiwa lazima niifanye baada ya kufika, lakini nilisahau siwezi kulala bila kuifanya ili asubuhi nikifika kazini nifanye kazi nyingine," Mustafa alitengeneza uongo.

    "Lakini si ni wewe uliyesema baada ya kazi ni nafasi yangu?" Husna alimuuliza mumewe huku amemkazia macho.

    "Ni kweli mke wangu, lakini hii imetokea dharura."

    "Mmh! Sawa, sasa mimi nina hamu na wewe itakuwaje?"

    Kauli ile ilimchanganya sana Mustafa na kujiuliza itakuwaje kama mkewe atatangulia kukutana naye kimwili kabla ya Shehna, wakati alielezwa kukutana na mkewe mpaka mwezi upite. Alipata wazo la kumwambia asubiri ili avute muda wa kumfanya mkewe apitiwe na usingizi.

    "Mke wangu hebu nivumilie kwa muda huu."

    "Mmh! Sawa lakini kumbuka nilijiandaa leo kwa ajili yako."

    "Najua mke wangu, kuwa na subra namalizia nakuja sasa hivi."

    "Basi na mimi nitakaa hapa nikusubiri mpaka akimaliza tutakale," Husna alisema huku akikaa kwenye kochi.

    "Mke wangu imeanza lini kulindana kama kibaka na polisi?"

    "Yaani leo sijijui, natamani tukae pamoja mpaka umalize kufanya kazi zako, kitanda leo nimekiona kichungu bila wewe mume wangu."

    "Mmh! Sawa," Mustafa alikubali kwa shingo upande.

    Mkewe alijilaza kwenye kochi na kutazama mumewe aliyekuwa akijifanya yupo bize huku kichwa kikimuwanga kutokana mkewe kuonekana kama anajua nini kinatakiwa kufanyika. Muda ulikatika bila mkewe kuonesha dalili za kulala, alijiuliza atafanyaje ili mkewe alale na Shehna aje ndani.

    Alipoangalia saa ya ukutani ndiyo ulikuwa saa sita kasoro za usiku,alijikuta alikosa raha kabisa. Alijikuta akitamani kulala kwani na yeye kichwa kilianza kuwa kizito kwa usingizi. Wakati akiwaka yale mkewe macho yalikuwa makavu hakuonesha dalili zozote za kulala huku macho yakiwa kwenye Runinga.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Alijifanya kutoka nje kumtazama Shehna kama atakuja ili amuwahi na kumueleza kuwa siku ile hali ilikuwa mbaya wafanye kesho japokuwa alijua atakuwa amemuharibia dozi. Aliamini zoezi alilolitaka Shehna alilikuwa ngumu kutekelezeka hasa kulifanyia nyumbani kwake chumbani kwake na kitandani anapolala na mkewe na mkewe akiwepo kilikuwa kitu kisichowezekana kwa akili ya kawaida.

    Aliifunga Laptop yake na kunyanyuka huku akijinyoosha kidogo na kumfanya mkewe aseme.

    "Dah! Afadhali umemaliza yaani leo hata sijielewi jinsi nilivyo na hamu na wewe imekuwa kama siku ya fungate," Husna alisema huku akijiweka vizuri kwenye kochi ili anyanyuke.

    "Nakuja," Mustafa alisema huku akielekea nje.

    "Usiku wote huu unakwenda nje kufanya nini?"

    "Mke wangu maswali gani hayo?" Mustafa alisema kwa ukali kidogo.

    "Mume wangu kukuuliza ni ubaya gani mimi mkeo nina haki ya kukuuliza chochote."

    "Nakuja," Mustafa alisema huku akifungua mlango na kutoka nje na kumuacha mkewe akirudi kujilaza kwenye kochi kumsubiri mumewe.

    Mustafa siku ile alimshangaa mkewe kuwa vile na kujiuliza labda amejua nini kinaendelea usiku ule. Alitoka nje kwa kuamini lazima kwa muda ule Shehna atakuwa amefika nje.

    Wakati akiwaza hayo Shehna alikuwa amefika muda mrefu, aliyaona yote yaliyokuwa yakitendeka na jinsi Mustafa alivyokuwa akiteseka kwa jinsi mkewe alivyogoma kwenda kulala na jinsi ya kuyashinda masharti ya kukutana kimwili na mkewe ambaye siku ile alionesha kumtaka sana.

    Alijifikiria jinsi ya kumsaidia Mustafa kwa kumfanya mkewe alale kwa hiyari yake bila kulazimishwa. Shehna alifurahi baada ya kumuona Mustafa akitoka nje alijua ametoka kumtafuta ili kumpa hali halisi ya ndani. Alimuacha atoke nje kisha alimsogelea Husna mke wa Mustafa na kumpuliza usoni na kukaa pembeni.

    Husna alijikuta akisikia usingizi mkali bila kujielewa usingizi mzito ulimpitia. Mustafa baada ya kumtafuta Shehna kwa kuzunguka nyumba bila kumuona, alisogea mpaka mbele ya nyumba labda yupo barabarani lakini hakumuona. Baada ya kutomuona alisimama kwa muda kujiuliza atafanyaje ikiwa muda umekwenda na lazima akapande kitandani na ilikuwa lazima ampe mkewe haki yake ya ndoa kwa vile hakuwa na sababu ya kumnyima.

     


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliamua kurudi ndani akiwa amejikatia tamaa ya kutimiza masharti ya Shehna, alipofika sebuleni alishangaa kukuta hakuna mtu. Alijua labda amekwenda msalani, alibeba Laptop yake na kuingia chumbani, alishangaa kumkuta mkewe chumbani amelala hajitambui.

    Alishtuka usingizi wa dakika tano kumkuta mkewe amelala kama mtu aliyelala saa mbili zilizopita wakati anatoka alikuwa macho makavu. Hakuamini, aliona kama anamtania au alifanya vile ili kumtega. Alisogelea kitandani na kumwita mkewe kwa sauti lakini alionesha ana usingizi mwingi hata alivyomgeuza alionesha kweli amelala.

    Hakuamini zoezi lake kufanikiwa akiwa amekata tamaa kwa vile naye alikuwa na usingizi. Alichukua chupa ya manukato aliyopewa na Shehna, alikwenda bafuni kuoga na kujipaka nanukato yale.

    Kabla ya kupanda kitandani alihakikisha mlango amerudisha bila kufungwa, kisha alipanda kitandani na chupa yake ya manukato. Kwa vile mkewe alikuwa ameisha lala alimsogeza ukutani na yeye kulala katikati. Alifuata maelekezo ya kutolala na nguo ya ndani, alitoa nguo zote na kupanda kitandani akiwa mtupu. Alichukua mafuta kidogo na kumpaka kichwani mkewe ambaye alikuwa katikati ya usingizi mzito.

    Naye alijilaza pembeni ya mkewe, haikuchukua muda usingizi ulimpitia. Katikati ya usiku aliamshwa kwa kubembelezwa, alipofumbua macho alimuona Shehna amesimama pembeni ya kitanda akiwa amejifunga mtandio mwepesi ulioonesha mwili wake mzuri uliokuwa hauna kitu ndani.

    "Shehna," Mustafa alishtuka na kutaka kuongea kwa sauti.

    "Shiiii!" Shehna alimkataza asitoe sauti.

    Aliondoa mtandio aliojifunga na kuutupa pembeni kisha alipanda kitandani na kujilaza pembeni kwa Mustafa ambaye alikuwa akitetemeka huku jasho likimtoka, alijiuliza mkewe akiamka na kumkuta mwaname juu ya kitanda chake atamwambia nini. Hali ile Shehna aliiona.

    "Mustafa," alimwita kwa sauti ya chini.

    "Mmh!" Mustafa alishindwa kutoa sauti.

    ‘Wasiwasi wako nini?"

    "Shehna nakupenda lakini unanitia kwenye matatizo."

    "Naomba uniamini hakuna kitu chochote kitakachotokea, mkeo hawezi kuamka mpaka kesho asubuhi."

    "Umejuaje?"


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Niamini."

    "Sawa," Mustafa alikubali kumridhisha Shehna lakini alitetemeka mpaka utumbo.

    Shehna alipomuona Mustafa hayupo naye kimawazo alianza kumpapasa na kulifanya joto lisambae mwili mzima na kujikuta akijisahau kama yupo kwenye kitanda chake na mwisho kuzama kwenye penzi zito ambalo hakuwahi kulipata katika maisha yake.

    Shehna pamoja na kuwa mwanamke mrembo pia mapenzi aliyajua kwa kiwango cha hali ya juu. Kama kawaida, Shehna baada ya kupata dozi yake ya mara tatu, aliondoka na kumwacha Mustafa kwenye usingizi mzito.

    ***

    Sara baada ya kuponea tundu la sindano kufukuzwa kazi alijikuta akimchukia Shehna na kumuona ni kiumbe mbaya katika maisha yake. Kabla ya kuja kwake alikuwa akielewana na bosi wake ambaye siku zote alikuwa mpole na mwenye hekima, hakuwahi kumfokea hata siku moja. Lakini toka alipokuja yule mwanamke imekuwa kinyume kabisa.

    Alijikuta akikumbuka matukio ya kushangaza toka siku ya kwanza alipoitwa ofisini na Bosi wake kuulizia kama kuna mgeni ameingia ofisini. Tokea hapo amejikuta akikutana na matukio ya ajabu ya kupanda teksi na kujikuta nyumbani na lingine la kulala ofisini kitu ambacho siku za nyuma hakikuwahi kumtokea.

    Na tukio la siku ile la kutaka kufukuzwa kazi bila kosa lilizidi kumfanya amchukie sana. Siku ile aliporudi nyumbani alijikuta mwenye hasira nyingi, kila aliyemuona alijua siku ile hayupo vizuri.

    Shoga yake wa karibu Happy baada ya kufika nyumbani alimfuata chumbani kumsalimia. Alishangaa kumkuta amekaa kwenye kochi bila kuvua viatu na mkoba wake mkononi huku machozi yakimtoka.

    "Shoga vipi mbona hivyo?"

    Sara hakumjibu, alichukua kitambaa na kujifuta machozi, hali ile ilimfanya shoga yake adhanie labda amefiwa.







    "Shoga una msiba?"

    Alitikisa kichwa kukataa.

    "Sasa nini?"

    "Naomba kwanza maji," Sara alisema kwa sauti ya kukwaruza.

    Shoga yake alikwenda kwenye friji na kuchukua maji kwenye jagi na kumuwekea kwenye glasi. Baada ya kunywa maji kwa mkupuo yaliyopunguza hasira, alishusha pumzi ndefu na kusema.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Shoga kuna tukio moja leo linimeniudhi sana."

    "Tukio gani?"

    Sara alimweleza kilichomtokea na kutaka kufukuzwa kazi pamoja na matukio yote yaliyomtokea. Shoga yake alishtuka sana.

    "Sara unayosema ni kweli?"

    "Kweli kabisa, matukio ya yule mwanamke nina wasiwasi nayo, huenda yule ni jini si mwanamke wa kawaida."

    "Mmh! Huenda kweli, lakini si nasikia majini wana kwato kwa chini, uliziona?"

    "Yule ni mwanadamu wa kawaida lakini muonekano wake si wa kawaida hata manukato yake sijawahi kuyasikia sehemu yoyote!"

    "Mmh! Mungu wangu kama ni jini unafikiri itakuwaje?"

    "Dawa yake naijua, nakuapia kama ni jini atakimbia mwenyewe kuna vitu nitakwenda navyo kazini."

    "Vitu gani?"

    "Mifupa ya nguruwe au nyama yake, kama ni jini hawezi kuja tena ofisini na nitamwambia bosi kama yule si mtu ni jini."

    "Basi fanya hivyo."

    "Tena shoga nimejikuta nina hamu ya kiti moto, nakwenda kumchukua ili nimlie nyumbani."

    "Unachukua kiasi gani?"

    "Nusu na ndizi nne nikipiga na bia zangu mbili nalala vizuri."

    "Shoga nunua kilo moja maana hata mimi nina hamu nayo sana."

    "Poa nitakuchulia na ndizi mbili."

    "Hakuna tatizo."

    "Yaani kidogo kuzungumza na wewe hasira zimepungua, nakuapia nitamkomesha."

    "Kwa kufanya hivyo, utamuweza."

    Sara alijitapa huku akivua viatu kisha alibadili nguo na kuelekea bafuni kuoga.

    Alipanga akitoka kuoga aende kwenye baa ya Macha iliyokuwa ikiuza kitimoto ili akatimize adhima yake ili ajue kama Shehna ni jini au mtu.

    Alioga harakaharaka, alipotoka kuoga alijifuta maji na kujifunga upande wa khanga moja chini na nyingine alijitanda kwa juu. Alichukua noti ya elfu kumi na kutoka kuelekea kwenye baa hiyo.

    ***

    Mustafa aliposhtuka usingizini alijishangaa kujikuta kitandani na mkewe lakini Shehna hakuwepo. Alipoangalia saa ya ukutani ilimuonesha ni saa kumi na moja kasoro alfajiri. Wasiwasi wake ulikuwa labda ameamka na kwenda bafuni kuoga kabla ya kuondoka.

    Aliamka haraka kitandani huku akimtazama mkewe asiamke muda ule kabla hajajua Shehna yupo wapi. Alikwenda hadi bafuni lakini hakumkuta mtu akatazama msalani pia hakukuwa na mtu. Alikwenda mlangoni na kukuta umerudishiwa, alijua ameshatoka.


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa vile muda ulikuwa bado alirudi kitandani, alipojilaza usingizi ulimchukua mpaka aliposhtuliwa na mkewe kukiwa kumekucha. Alipofumbua macho kulikuwa kumekucha alinyanyuka kuelekea bafuni kuoga, alipotoka kuoga alikuta mkewe ameshamuandalia kifungua kinywa.

    Baada ya kufungua kinywa, alimshukuru mkewe kwa kumbusu shavuni na kutaka kuelekea nje lakini mkewe alikumbuka kitu na kumuuliza.

    "Mume wangu umefikia wapi?"

    "Kuhusu nini?"

    "Kuhusu Shehna, bado hujawasiliana naye?"

    "Alinipigia na kumueleza, alisema kiburi kimejaa na dharau ndicho chanzo cha kuharibikiwa mambo yako ameapa kama utaendelea na tabia zako chafu utakufa bila mtoto."

    "Muongo amejuaje mimi nina tabia chafu?"

    Alimweleza kila alichoelezwa na Shehna kilichosababisha ashindwe kushika ujauzito, Husna alichanganyikiwa siri zake zote kuwa nje na kujikuta akitaka kumjua Shehna ni nani, alijiuliza ni kiumbe gani anayejua mambo yake ya siri kiundani ambayo hakuna mtu mwingine aliyekuwa akiyajua. Akiwa bado yupo katika dimbwi la mawazo, Mustafa alimuuliza.

    "Lipi la uongo katika niliyokuambia?"

    "Mmh! Shehna kiboko, kayajuaje haya?"

    "Si kujua kwa nini anajua mambo yako, la muhimu kujua kwa nini natumia fedha na nguvu wakati mwenzangu huna ushirikiano?" Mustafa alizitoa hasira zake kwa mkewe baada ya kuonesha hakuwa na ushirikiano katika kutafuta mtoto.

    "La..lakini mume wangu unamuamini vipi Shehna, yule ni mgombanishi tu," Husna alijitetea.

    Mara simu ya Mustafa iliita alipoangalia aliiona inatoka kwa Shehna, aliipokea.

    "Asalam aleykum."

    "Waleykum Salamu, mmeamkaje?"

    "Salama."

    "Mbona hujatoka kwenda kazini?"

    "Si huyu mshe…"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/






    ITAENDELEA

     

0 comments:

Post a Comment

Blog