IMEANDIKWA NA : ALEX WAMILLAZO
*********************************************************************************
Simulizi
: Sanda Ya Siwa
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilionekana gari ndogo aina ya Carina ikingia kwenye moja ya nyumba iliyowekewa uzio wa geti,punde si punde gari hiyo ilisimama. Ndani ya hiyo gari alishuka mwanaume. Mwanaume huyo anaitwa Joeli, Joeli alionekana kupendeza vizuri kwa mavazi yake alizipiga hatua kuingia ndani huku kichwa chini mikono nyuma. Alipofika ndani alimkuta mkewe akiwa kajilaza kwenye sofa,mwanamke huyo aliitwa Siwa. Siwa alitabasam baadakumuona mumewe karejea kutoka kazini,alikiweka kando kitabu cha riwaya alichokuwa akisoma,hima alinyanyuka na kuenda kumlaki. Lakini Joeli hakuonyesha uso wa furaha,alijisonya kisha akajongea mpaka chumbani ambapo huko alivua koti na tai na kisha akajitupa kitandani. Siwa akiwa subuleni alibaki amesimama,alijiuliza kwanini Joeli leo yupo tofauti na siku nyingine? Haijawahi tokea hata siku moja kumsonya ama kupuuza mapokezi yake. Kila Joeli alipokuwa akirudi kutoka kazini,nyuso ya furaha na bashasha ya kutosha ilikuwa ikimtawala usoni mwake lakini siku hiyo ilikuwa siku tofauti kabisa. Hakutaka kufurahi na mkewe,jambo ambalo lilimshtua sana Siwa akajihisi mkosefu mbele yake ila alipojaribu kuvuta kumbumbuku aligundua kuwa abadi hajamkosea. "Ama kazini leo mambo yamekuwa tofauti?..na kama sio,ni jambo gani limemsibu Joeli" alijiuliza Siwa bila kupata majibu ya maswali hayo aliyojiuliza,hivyo mwishowe aliamua kuzipiga hatua kumfuata Joeli chumbani. Alipofika chumbani alimkuta Joeli akiwa kajilaza kitandani,Siwa alimsogelea akaketi nae kitandani na kisha akasema "Mume wangu Joeli,pole na kazi. Lakini pia ningependa uniambie mbona leo upo tofauti kabisa na siku nyingine?.." alisema Siwa,kwa sauti ya chini kabisa iliyotamalaki heshima mbele ya mumewe. Joeli aliposikia maneno hayo ya mkewe, alimtazama kwa jicho la hasira kisha akageukia upande wa pili halafu akasema "Siwa, miaka kadhaa imepita sasa. Na sisi ni wanandoa,sioni dalili yoyote wewe kunasamba mimba. Sio kwamba tendo la ndoa hatufanyi,hapana tumefanya sana kwa nyakati tofauti tofauti ila bado sioni matokeo yoyote. Nadhani hujui ni jinsi gani naumia,naona wivu pindi niwaonapo wafanya kazi wenzangu wanavyotoka na familia zao siku za mapumziko kasoro mimi tu. Yani nimekuwa kama dume la njiwa!? Maisha gani haya siwa? Wakati siku zote raha ya ndoa lazima muwe na familia" alisema Joeli tena alionyesha kuhamaki kwa hasira. Siwa alimtazama kisha akatikisa kichwa,baadae akavuta pumzi na kisha akaishusha kwa nguvu halafu akamtaka Joeli amgeukia kwanza ili amjibu juu ya kile alicho maliza kuzungumza. Lakini Joeli alikataa akidai kwamba hana muda wa kujibizana nae,na hivyo punde si punde alinyanyuka akavua nguo alizokuwa amezivaa akavaa taulo na kisha akaelekea bafuni kuoga. Alipomaliza alivaa nguo nyingine tofauti na ile aliyovaa mwanzo,akachukua funguo ya gari akaondoka zake huku nyuma akimuacha Siwa akiwa kitandani amejiinamia asijue nini cha kufanya. Joeli aliekea kwenye kumbi ya starehe ili kupoteza japo mawazo juu ya kile alichokuwa akikiwaza muda wote,huko alikutana na rafiki yake kipenzi ambaye pia ni mfanya kazi mwenzake kwenye kampuni ya Quality Plaza. Rafiki yake huyo aliitwa Magesa. Magesa alifurahi kumuona Joeli,hivyo alipomuona alimuita ili waketi meza moja. Joeli alikubali,Na hapo ndipo walipoanza kuzungumza mambo mbalimbali hasa wakigusia mstakibali wa kampuni waliyokuwa wameajiliwa. Lakini mwishowe mada hiyo ilifinywa baada Joeli kuonekana kuwaza sana,kwani kuna wakati alionekana kuzubaa kabisa jambo ambalo lilimshtua Magesa ikabidi amuulize ni kitu gani kinacho msumbua Joeli. Ila Joeli hakutaka kusema ukweli wa jambo linalo msibu, aliishia kusonya huku akisindikizia kinywaji alichokua ameagiza. Kitendo hicho kilimuuzi sana Magesa lakini mwishowe akajiaminisha kwamba huwenda yakawa ni mambo ya familia ndiyo yanayo msumbua bwana huyo,na kama sivyo basi atakuwa na jambo lake mwenye moyoni ambalo anaona kama haliendi sawa. Hivyo Magesa hakutaka kujaji sana aliamua kukaa kimya. Mazungumzo mengineyo yalifuatia,lakini hayakuchukua muda mrefu yalikatishwa Mara baada mke na watoto wawili wa Magesa kufika. Magesa alinyanyuka akamuaga Joeli kisha akaondoka zake huku akimsihi Joeli apunguze mawazo. Joeli hakujibu neno lolote alikaa kimya wakati huo akimkodolea macho rafiki yake aliyeonekana kupendeza na familia yake,chozi lilimtoka Joeli ilihali moyoni akitamani nae siku moja aje kuwa kama Magesa.
Yote kwa yote alipotosheka na kiasi cha pombe aliyokunywa aliondoka zake kurudi nyumbani,muda huo tayali ilikuwa saa sita usiku. Siwa alikuwa bado hajalala alikuwa akimsubili mumewe ili aweze kuzungumza nae juu ya kile alichokisema jioni,ila bado Joeli hakutaka kusema na mkewe alienda mbali kutishia kumpiga kitendo ambacho kilimuogopesha Siwa. Alimuacha akiamini kuwa huwenda ule msemo wa wahenga waliosema kwamba siku hazifanani,unaweza kutimia hapo kesho panapo majaliwa kwani inawzekana Joeli akawa sawa tofauti na siku hiyo. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake asubhi,Siwa aliamka mapema akaanda chai kisha akaelekea chumbani kumwamsha Joeli ili anywe chai aende kazini. Joeli hakutaka kunywa chai ya mkewe,kwani baada kutoka bafuni kuoga aliondoka zake bila kusema jambo lolote na mkewe. Hakika Siwa aliumia sana ni jinsi gani anavyompenda Joeli na mambo anayomfanyia abadani hayaendani. Na hapo ndoa alipoanza kuiona chungu,hofu ilianza kumjaa hasa juu ya yeye kuhusu kubeba ujauzito. Alihofia huwenda akawa na amepata tatizo kwenye uzazi baada kukumbuka kitendo alichowahi kukifanya kipindi cha nyuma enzi yupo chuo. Ila suala hilo hakutaka liendelee kuutesa moyo wake,hivyo kupitia hilo alitamani siku moja akapime ili awe na uhakika juu ya uzazi wake. Wakati Siwa anawaza jambo hilo,kwingineko Joeli nae alipata ushauri nasaha kutoka kwa watu wake wa karibu. Hapo awali aliogopa kwenda kupima lakini mwishowe aliamua kupiga moyo konde aliona heri akapime na mkewe ili ajue ni nani kati yao mwenye tatizo,wakati huo Joeli moyoni akijiapia kuwa pindi atakapojikuta kuwa yupo sawa ilihali Siwa ndio mwenye tatizo,kamwe hatoendelea kuishi nae kwani hawezi kuishi na mti usio zaa matunda.
Hivyo jioni aliporudi nyumbani alikuja na taswira ya tofauti na jana mbele ya mkewe,alionyesha furaha huku moyoni akiwa na lake jambo. Habari njema ambayo iliweza kumfurahisha Siwa ni pale Joeli alipomwambia kuwa kesho wataenda hospital kupima ili wajue ni nani mwenye tatizo,huku Joeli akiongeza kusema kuwa pindi mmoja wao atakapo gundulika kuwa anatatizo basi haraka sana jitihada za kulitatua zitaanza. Aliongea hayo usoni lakini moyoni akiwa na siri yake ambayo Siwa hakuweza kuingundua. Kesho yake asubuhi baada ya kugungua kinywa wanandoa hao walielekea hospital kupima,na mwisho wa zoezi ikabainika kuwa Siwa ni mgumba(Hawezi kuzaa) Jambo hilo lilimshtua sana Siwa pia na Joeli. Siwa alijikuta akiangua kilio mbele ya doctor huku akiomba doctor arudi vipimo labda huwenda vipimo vya awali vikawa vimekosea,lakini Doctor alikataa katu katu huku akijinasibu kuwa yeye ni professional hivyo hana hofu na vipimo vya awali. Wanandoa hao walinyanyuka wakarudi nyumbani huku kila mmoja akiwa kimya,Joeli hakumsesha Siwa na wala Siwa hakumsemesha Joeli. Wote walikuwa na mawazo juu ya majibu waliyo yapata Hospital. Walipo fika nyumbani Joeli alitelemka kwenye gari kisha akazipiga hatua kuingia ndani wakati huo huo Siwa nae alishuka kwenye gari,alipomuona Joeli anaingia ndani alipasa sauti kumuita. Joeli aliposikia sauti ya Siwa, aligeuka nyuma kisha akasema "Unasemaje we mgumba?.." Maneno hayo yalimumiza sana Siwa akajikuta akishindwa kusema kile alichotaka kumwambia,aliishia kulia tu ilihali muda huo Joeli alionekana kuingia ndani bila kujali chozi la mkewe.
Hivyo baada kujihakikishia kuwa yeye ni mzima,haraka sana alirudi kwa watu ambao walimshawishi akapime. Safari hiyo Joeli aliomba ushauri kipi sasa cha kufanya,wapo walimshawishi kuwa amfukuze Siwa kisha aoe mwanamke mwingine. Vile vile wapo waliomshauri atafute tiba wakati huo wengine walimuaminisha kwamba ugumba hauna tiba zaidi ya ujanja unja. Hapo Joeli akajikuta yupo kati kwa kati,alishindwa achukue uamuzi gani. Kumfukuza Siwa aliogopa sana hasa akifikilia msaada aliompa tangu mwanzo wa elimu yake secondary mpaka anapata kazi. Wazazi wake Joeli hawakuwa na uwezo wa kumsomesha kijana wao,hivyo kilichomsaidia Joeli ni kuwa katika mahusiano na Siwa ambaye binti ambaye kwao walikuwa na pesa ya kutosha. Istoshe katika familia yao yeye ndio alikuwa mtoto pekee,Kwahiyo kila alichotaka alipewa. Alimlipia ada Joeli,pia alimpa pesa ya matumizi lakini kwa bahati mbaya kipindi Joeli anapata kazi taarifa mbaya ikatokea upande wa Siwa baada wazazi wake wote wawili kufariki kwa ajali, pesa na mali zote wanandugu walichukua huku wakimuacha Siwa mikono mitupu. Kwa maana hiyo Siwa akabaki hana sehem ya kutegemea za ya kumtegemea mchumba wake ambaye ni Joeli,uchumba huo mwishowe waliufuta baada kufunga ndoa ambayo ilileta furaha Kati kati yao ingawa baadae furaha hiyo imetoweka baada Siwa kugundulika kuwa ni tisa ilihali Joeli yeye anataka mtoto,jambo ambalo Joeli anawaza achukue uamuzi gani kwa Siwa tofauti na kumtimua.
Lakini wakati Joeli anaumiza kichwa kuhusu jambo hilo,upande wa pili Siwa aliona hana hatia kwa kilichotokea. Bado anampenda sana Joeli,na hayupo tayali kumpoteza. Hivyo kama ni mtoto basi atamuomba rafiki yake azae na mumewe ambaye ni Joeli ila kwa sharti moja ambalo atamuomba mumewe. Nalo ni kudumisha upendo kwake pasipo kumnyanyapaa kutokana na tatizo alilo nalo lakini pia asijiweke sana kwa rafiki yake huyo katika mazingira kana kwamba yule ndio mkewe. Aliwaza jambo hilo Siwa ambapo alijikuta akidondosha chozi kwani ni uamuzi mgumu hasa pindi utakapo wafikia walengwa. Lakini hakuwa na namna kwa sababu anampenda sana mapenzi wake..

Baada Siwa kuona jambo la mume wake kuzaa na rafiki yake linaeweza kunusuru penzi lao kwa sababu shida ya mumewe ilikuwa ni mtoto, ndipo jioni moja Siwa alimuita rafiki yake wa karibu sana. Anaitwa Naomi. Msichana mwenye urembo wa kuvutia kila kona,alijaliwa umbile zuri kuliko hata jina lenyewe. Nyuma alikuwa amejazia bila kitumia vidonge vya kukuzia makalio,ilihali rangi yake haikutegemea mkorogo wala kichwani hakutegemea wigi ama vidoleni kucha za bandia wala nachoni kope za kubandika. Naomi alikuwa na uzuri asilia ambao wanaume wengi hupendelea. Hivyo jioni hiyo Siwa alimuita Naomi ili aseme nae juu ya jambo lile aliloliwaza ambalo aliamini kwamba linaeweza kuendelea kumuweka kwenye ndoa yake na mumewe.
"Naomi,wewe ni rafiki yangu kipenzi wa kufa na kuzikana. Ila samahani kwa jambo hili nitakalo kwambia,lakini pia hata kama litakukwaza ila bado nitahitaji msaada wako rafiki yangu"
"Msaada gani shoga yangu? Halafu jaribu kuondoa hofu mimi ni rafiki yako hivyo kuwa huru sawa naweza kukusaidia wala usihofu.." alijibu Naomi baada kusikiliza kile alichokisema Siwa. Siwa kabla hajaanza kueleza shida yake alivuta pumzi ndefu kisha akaishusha kwa nguvu,moyo ulitaka aseme lakini akili ilikataa kitendo kilichofanya kuzua taharuki moyoni mwa Naomi ambapo alijiuliza ni jambo gani hilo ambalo Siwa anataka kumwambia mpaka impeleke kuogopa kusema? Naomi kabla hajapata jibu la swali alilojiuliza,Siwa alifungua kinywa chake na kisha akasema "Naomi rafiki yangu,siku za usoni amani imetoweka humu ndani kati yangu mimi na mume wangu. Chanzo cha yote hayo ni baada mume wangu kuona siku zinakwenda pasipo mimi kupata ujauzito,hivyo manyanyaso kila kukicha yakawa yananiandama. Nilitaka kumwambia tukapime ili tujue ni nani hasa mwenye tatizo,lakini niliogopa baada kuona akinionyesha uso wa hasira kila mara. Ila siku moja alijitosa,aliniambia tukapime. Na mwisho wa vipimo majibu yakaja kuwa mimi ndio mwenye tatizo. Naomi nimegundulika kuwa mimi ni mgumba sina uwezo wa kutunga mimba,Daah Siwa mimi" alisema Siwa huku akidondosha machozi yaliyomtoka baada kueleza kwa ufupi. Naomi alimsogelea,akamshika bega akapa pole ilihali muda huo huo Siwa aliyafuta machozi yake na kisha akaendelea kusema "Ni jambo ambalo limeniumiza sana,nahisi kama nampoteza Joeli wangu ambaye bado anaishi moyoni mwangu. Hivyo naomba Naomi unisaidie, nipo tayali kukupa ile gari yangu niliyozawadia siku ya sherehe yangu ya kuzaliwa lakini pia nitakupa pesa ambayo itafaa kuendesha maisha yako" Alisema Siwa,safari hiyo chozi lilikuwa limekata ingawa usoni alionyesha huzuni iliyotanda vema kutokana na mtihani alionao. "Sawa nipo tayali enhe nikusaidie nini?.." alihoji Naomi. Siwa kabla hajamjibu alishusha pumzi kwanza na kisha akajibu "Zaa na mume wangu,ila kwa sharti moja ukijifungua uachane nae ingawa ghalama ya malezi kwa mtoto atatoa. Sitotaka aendelee kulala na wewe ama kufanya starehe yoyote nae,kufanya hivyo ni kutaka kunusuru ndoa yangu Naomi ingawa nafaham fika Joeli atakuwa anatafuta mwanamke mwingine wa kumzalia mtoto ambaye pengine mwanamke huyo hatokua na mapenzi ya dhati kwake zaidi kumfilisi. Nisaidie kwa hilo Naomi nakuomba sana" alisema Siwa kwa sauti yachini iliyotamalaki unyonge. Naomi hakusema kitu chochote,alikaa kimya huku akijifanya kufikilia kile alichokisema Siwa kumbe moyoni akifurahi kwani kwa kipindi kirefu sana alitamani Joeli alowe na Joeli lakini bahati haikuwa yake. Joeli akawa amemuoa Siwa ambaye ndio huyo mwenye ugumba. Naomi alichekelea kimoyo moyo na kisha akajisema "Ama kweli kisicho riziki huwaga hakiliki abadani,nadhani huu ndio wakati wenyewe wa Siwa kumkosa Joeli kwa sababu utam wa asari ukichovya kidole kwenye kibuyu chake kisha akakilamba, ukihisi utam sio vyepesi kukiacha kibuyu hicho kilicho sheheni asari" Alijisemea maneno hayo Naomi moyoni mwake,baada ya hayo alimgeukia Siwa kisha akamwambia "Ni jambo gumu sana Siwa,ama naweza sema pia kwa upande wako suala hili umelifanyia maamuzi magumu. Najua jinsi mapenzi yalivyokuwa na nguvu kwenye sayari hii ya tatu,hutaki kumpoteza mumeo ila yote kwa yote naomba unipeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ nafasi nikalitafakari jambo hili kisha nikipata jibu nitakujuza kwani tayali nitakuwa nimeupoteza usichana wangu" Alisema Naomi.Siwa alioposiki maneno hayo alirudia kushusha pumzi kwa mara nyingine kisha akajibu "Nashukuru na nitashukuru zaidi kama utakubali ombi langu" Kwisha kusema hayo mazungumzo mengine yalifatia lakini hayakudumu sana kwani mwishowe Naomi aliomba kuondoka,hivyo Siwa alimsindikiza mgeni wake lakini kabla hajatoka kwenye uzio wa geti mara ghafla iliingia gari. Alikuwa ni Joeli amerejea kutoka kazini. Joeli alifungua mlango wa gari kisha akatoka ndani,kabla hajazipiga hatua kuelekea ndani ya nyumba. Alimtazama kwanza mkewe kisha akageuka nyuma yake kumtazama mwanamke aliyetoka ndani ya nyumba yake ambaye ni Naomi. Umbile la Naomi lilionyesha kumvutia sana Joeli kiasi kwamba alichukua sekunde kadhaa kumtazama binti huyo ambaye kwa muda huo hakuweza kumtambua kwani alikuwa amempa mgongo. Na wakati Joeli alipokuwa ametupia macho yake kumtazama Naomi,upande wa pili Siwa alionekana kusikitishwa na kitendo hicho cha Joeli aliamini Joeli wa zamani sio wa sasa. Jambo hilo lilimfanya Siwa kudondosha machozi huku akizipiga hatua kurudi ndani. Punde si punde Joeli nae alifatia,alimkuta mkewe akiwa kakaa kwenye sofa huku akiwa ameshika tama. Joeli hakujali wala hakuthubutu kumuuliza kipi kinacho msibu mkewe mpaka impelekee kushika tama,zaidi alihoji juu ya Naomi huku akihitaji kujua jina lake na sehem anapoishi huyo binti. Jambo hilo lilizidi kumuweka njia panda Siwa,maumivu makali aliyapata moyoni shahidi ni machozi aliyokuwa akiyatoa pasipo kuangua kilio. Alijikuta akijutia kile alichowahikufanya miaka ya nyuma,kwani laiti kama asingefanya vile basi maisha ya ndoa yake yangeliluwa na amani pia na furaha. Lakini majuto yakabaki kuwa mjukuu kwa Siwa,kwani matokeo alishapata hana budi kuugulia maumivu.
Siku zilisogea,Siwa alisubilia jibu kutoka kwa Naomi juu ya kile alicho mwambia ilihali upande wa Joeli nae alionyesha nia ya kumtaka mwanamke huyo pasipo kujua kwamba kuna kampeni nzito inafanyika kuhusu mwanamke huyo huyo vile vile Siwa nae asifaham ya kwamba rasmi anakwenda kumkabidhi fisi bucha. Lakini baada Siwa kungojea kwa muda mrefu,hatimae usiku mmoja Naomi alimpigia simu. Naomi alimueleza Siwa kuwa amekubali kumsaidia,Siwa alifurahi usoni ingawa moyoni aliumia ila hakuwa na jinsi ya kufanya. Hivyo jambo hilo wakapanga kuliendesha kwa mkataba baina yake na Naomi,na kwa kuwa maelezo walikuwa wakipeana kwa njia ya simu,Siwa aliamua kumuomba siku yoyote wakutane ili walimalize kwa makaratasi. Naomi hakukataa, alikubali kwa sababu alijua fika anakwenda kutajirika kupitia kivuri cha Siwa. Mbali na kutajirika,lakini pia anakwenda kumtwaa mikononi mwake mwanaume ambaye alikuwa akimtamani kwa muda mrefu.
Siku husika ilifika,siku hiyo Naomi alikuja akiwa amependeza kuliko siku ile ya kwanza aliyokuja nyumbani hapo kwa Siwa. Baada ya mazungumzo mawili matatu yaliyokuwa yakisukumwa na juisi ya matunda,hatimae Siwa alizibwaga mezani kalam na karatasi kisha wakaandikishiana kuhusu kile walichokipanga. Mkata wao ulieleza gari na kiasi cha pesa ambacho Siwa atamkabishi Naomi pindi atakapo jifungua mtoto,huku moja ya kipekele katika mkataba huo ukimtaka Naomi kuachana na mumewe Siwa pindi tayali atakapo kabidhiwa pesa na gari aliyoahidiwa. Suala hilo likawa limemalizika,na kilicho baki ni Siwa kumbariki mumewe kwa Naomi. Ila siri ikibaki kwao watu wawili, ambao ni Siwa na Naomi ingawa Naomi yeye alikuwa na siri yake nyingine tofauti na hiyo aliyonayo na Siwa. Hivyo mara baada kumalizika zoezi hilo Naomi aliaga akidai kuwa abataka kuondoka zake lakini kabla hajaanza safari, Joeli alifika. Siku hiyo alirudi nyumbani mapema sana kwa madai kwamba alikuwa anasumbuliwa na kichwa,ila ajabu alipomuona Naomi alijihisi kupona. Hisia zake ziligonga kwa Naomi,kupitia nafasi hiyo Siwa alinyanyuka kutoka kwenye sofa alimlaki mumewe kisha akasema huku akitabasam "Joel,huyu mtu bila shaka sio mgeni kwako. Anaitwa Naomi, alikuja mara moja kunitembelea. Naomba kabla hujaiweka funguo ya gari mfukoni,msindikize kwa gari" alisema Siwa huku akiumia moyoni ila hakuwa na jinsi. Joeli aliposikia maneno hayo ya mkewe alitabasam kisha akajibu "Hamna shida,Naomi twenzetu nikusindikize wala usijali " Hima Naomi alinyanyuka akaambatana na Joeli mpaka kwenye gari. Joeli alimfungulia mlango Naomi kisha akarudi upande wake akafungua mlango akaingia akapiga honi,mlinzi akafungua geti. Safari ikawa imeanza wakati huo huku nyuma Siwa akiisindikiza gari kwa macho mpaka pale mlinzi alipolifunga geti.. Siwa aliumia sana,alilia kwa uchungu.

Roho ilimuuma Siwa,mboni za macho yake zikashindwa kustahimili maumivu aliyokuwa akihisi moyoni hali iliyopelekea kutokwa na machozi huku akigeuka kurudi sebulen. Alipofika aliketi,akayafuta machozi yake na kisha kuanza kutafuta hitimisho la kutuliza akili yake iache kufikilia wakati mgumu anaopitia. Upande wa pili Naomi akiwa na Joeli ndani ya gari,walizungumza mambo mengi sana. Mambo ambayo yaliweza kuifanya kama safari yao kuiona fupi ingawa sehem anayoishi Siwa na mahali anapo ishi Naomi kuna umbali wa kilometa kadhaa ambazo kwa vyovyote itakulazimu kutumia nusu saa ama dakika arobaini na tano kufika mahali hapo anapoishi Naomi endapo utatokea nyumbani kwa Siwa. Hatimae Joeli alimfikisha Naomi anapoishi,Naomi alikuwa akiishi na marafiki zake watatu hivyo nae akiwemo jumla anakuwa wa nne. Hivyo baada kuona amefikishwa nyumbani alishuka kwenye gari ya Joeli,alitoa shukrani yake na kisha kuomba ruhusa ya kuondoka. Lakini Joeli hakutaka kumruhusu mwanamke huyo hasa kila alipomtazama umbile lake jinsi lilivyomkaa,alijikuta aking'ata maneno huku akirudia kuzungumza mambo ambayo alishakwisha kuyasema tangu walipokuwa ndani ya gari. Kupitia hilo ndipo akili na macho ya Naomi yakahisi kitu kutoka kwa Joeli,ila Naomi hakutaka kujilahisisha kwake na hivyo aliamua kuchukua uamuzi wa kuondoka pole pole huku nyuma akitikisa. Joeli alitoka ndani ya gari,alimuangalia Naomi kwa jicho la uchi lakini akaishia kutikisa kichwa huku akitamani siku moja aje awe mtu wake wa karibu kuliko hata mkewe wa ndoa ambaye ni Siwa.
Siku zilisonga,mawaelewano ndani kati ya Siwa na Joeli yakatoweka. Joeli alimdharau ipasavyo Siwa huku akimtusi na kumdhihaki juu ya tatizo alilokuwa nalo,Siwa aliumia sana akawa anajiuliza maswali mengi ambayo hakuyapata majibu yake ambapo mwishowe alijikuta akiangua kilio kwani hakua na jinsi kwa sababu alijua ni nini hasa kinachompelekea mumewe kumdharau na kumdhihaki. Ni ugumba alio nao ndio chanzo cha matatizo hayo,ambayo ilifikia hatua yakazidi mpaka akampigia Naomi simu ili ajue mpango wao umefikia wapi. Naomi alijibu "Siku zote mambo mazuri hayataki haraka Siwa,unafilili mimi sitaki hivyo vitu ulivyo niahidi? Nataka na nina ham navyo,kwahiyo punguza munkali rafiki yangu " Naomi alimjibu hivyo Siwa. Jibu ambalo lilimfanya Siwa kuwa mpole. Na wakati anakati simu kwa Naomi,punde si punde simu ya Naomi iliingia namba mpya. Haraka sana Naomi alipokea ambapo alijikuta akitabasam baada kusikia sauti ya Joeli. Naomi alisema "Joeli.."
"Ndio ni mimi,umenijuaje?.." alijibu Joeli. Naomi akaongeza kusema "Nimejua tu baada kusikia sauti yako,enhee niambie mzima wewe?.."
"Mimi niko sawa,ila Naomi nilikuwa naomba tukutane mara moja tafadhali kama utakuwa na nafasi" alijibu Joeli huku akiongezea na ombi hilo la kukutana,ombi ambalo halikutiwa pingamizi kwa Naomi. Zaidi walipanga sehem ya kukutana na kisha simu ikakatwa. Jioni baada Joeli kutoka kazini alirudia kumpgia simu Naomi,Naomi alimjibu kuwa tayali yupo mahali walipo kubaliana kukutana. Jambo hilo lilimfurahisha Joeli alirusha mikono juu kwa furaha,hima aliingia ndani ya gari yake. Kutokana na furaha aliyokuwa nayo alifungulia muziki mzito ndani ya gari wakati huo akiendesha gari kwa kasi kumuwahi Naomi. Haikuchukua muda mrefu alifika,ni Kwenye bar iliyoonekana kutulia kutoka na maadhali yake yalivyopambwa. Eneo hilo ndilo Joeli alilitumia kuzungumza mambo mengi na Naomi huku wakinywa vinywaji,na kwa kuwa Joeli alikuwa mdau mkubwa wa pombe,yeye aliagiza biya ilihali Naomi nae aliagiza soda na nyama choma. Hapo mazungumzo yalifuatia, mazungumzo ambayo yalidumu kwa masaa yasiyopungua manne kwa sababu Joeli alitumia muda mrefu sana kumueleza hisia zake Naomi huku akimmwagia sifa kidekede pia akimponda mkewe wa ndoa ambaye ni Siwa. Joeli alisema "Naomi,kwanza umeumbika. Unafaa kunizalia mtoto kwani yule mwanamke niliyemuweka ndani sina hamu nae tena,nitaishije na mwanamke asiyezaa? Wakati niwazi inafahamika kuwa raha ya ndoa ni familia " alisema Joeli kwa sauti ya ulevi, Naomi alijifanya kushtuka baada kusikia maneno hayo,alijiweka katika hali ya kutofaham kitu chochote kuhusu Siwa. Hivyo alihoji "Joeli,unataka kuniambia Siwa ni mgumba?.." Joeli aliposikia swali hilo kutoka kwa Naomi,alimkodolea macho. Macho ambayo yalionekana kulegea shauri ya kulewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kisha akamjibu "Kwani hajakwambia? Na iweje ashindwe kukwambia wakati nyinyi ni marafiki? Lakini nafikili hakijaharibika kitu,kwahiyo kuanzia sasa ukae ukijua kuwa Siwa ni mgumba hazai na pia hatozaa katika maisha yake. Na ndio maana nimekuwa nikikuhitaji kwa muda mrefu sana ili uje kuwa mama watoto wangu siku za usoni, mimi ni msomi lakini vile vile nina pesa. Kufanya kazi Quality Plaza sio mchezo istoshe nipo nyanja za juu, kwahiyo pesa nitakupa utavaa unachotaka na bila kusahau gari. Nitakupatia gari nzuri sana ya kutembelea" Joeli alimjibu hivyo Naomi. Ila Naomi hakutaka kujilahisisha kwa Joeli na ndipo alipomuuliza kuhusu Siwa. "Je, mimi nikishakuwa mama watoto wako. Na huyo Siwa itakuaje? Istoshe mimi na yeye ni marafiki!" Joeli alicheka baada kusikia swali hilo,na mara baada ya kukatisha kicheko hicho alijibu "Siwa atabaki kuwa kama Siwa,siwezi kumtimua kwa sababu alinisaidia sana miaka kadhaa nyuma Kwahiyo naishi nae kama kulipa fadhila lakini ukweli ukibaki kuwa sina hamu nae mimi. Zaidi ajichunge, asijenge wivu kwangu na jambo hili la mimi kutaka kuishi na wewe nitamwambia ili kama ataona nimemkosea aondoke mwenyewe sitotaka kumfukuza" alijibu Joeli,jibu ambalo Naomi alionyesha kulikubali kwani alionekana kutikisa kichwa.
Baada ya hayo kupita,hatimae walihitaji kurudi nyumbani. Joeli alimsindikiza Naomi mpaka nyumbani anapoishi,walipofika alimpatia kiasi cha fedha kisha akamkisi wakaagana ambapo Joeli nae alirejea nyumbani kwake muda huo tayali ilikuwa saa tano usiku. Alimkuta Siwa yupo kitandani kajilaza,Siwa alipomuona mumewe alifurahi sana ilihali Joeli hakutabasam wala kusema jambo lolote zaidi ya kubadilisha nguo na kisha kuelekea bafuni kuoga. Aliporudi hakuhitaji chakula alichopika mkewe,alidai ameshiba hivyo alilala. Lakini licha ya Joeli kuwa katika hali hiyo kama ilivyozoeleka ila siku hiyo Siwa alikuwa na jambo tofauti kabisa la kusema na mumewe,hivyo Siwa nae alilala kisha akamsogelea mumewe na kumwambia "Joeli mume wangu,najua mimi kwako sina thamani tena kutokana na tatizo nililo nalo. Lakini katika hili siwezi kukulaum sana bali nijutia nafsi yangu. Joeli naomba ukae ukijua kuwa Siwa nakupend sana sipo tayali nione ukiwa na huzuni muda wote na wala sitaki nikupoteze,hivyo basi kupitia hilo nakupa ruhusa utafute mwanamke mwingine atake kazilia mtoto ili roho yako ifurahi kwani furaha yako wewe ndio furaha yangu mimi kwani nakupenda sana ila katika hili sina namna.." alisema Siwa. Maneno hayo yalimshtua Joeli,akajiuliza ama tayali Siwa ameshajua kuwa natoka na rafiki yake? Na kabla hajapata jibu la swali hilo alilojiuliza,Siwa aliongeza kusema "Lakini pia mume wangu Joeli licha ya mimi mkeo kukupa hiyo nafasi,naomba nikuchagulie mwanamke utakae zaa naye wakati huo kwa upande wangu ukiendelea kunienzi kama zamani maana mimi ni mkeo halali na nitaendelea kuwa mkeo tu. Naomi,huyu ndiye mwanamke sahihi kwako kwa sababu wewe ni msomi,vile vile mzuri hufai kuchukua mwanamke yoyote tu ilimladi mwanamke. Ni hayo Joeli mume wangu" Aliongeza maneno hayo Siwa. Joeli alishtuka kwa mara nyingine ,akanyanyuka kutoka kitandani akamtazama Siwa pasipo kupepesa macho kisha akaachia tabasam lililoambatana na maneno matam. Joeli alisema huku akitabasam "Siwa,ama kweli kama ni tuzo ya mwanamke bora hapa duniani!basi wewe nakupa. Unafaa kwa sababu unajua hitaji la mume wako. Nasema Ahsante sana,umerejesha furaha yangu iliyokuwa imepotea,vile vile labda niseme nawe jambo moja,hakyamungu naapa mbele yako sito kusaliti kwani nafaham umuhimu wako kwangu. Sogea mpenzi wangu nikukumbatie" Alisema Joeli kwa sauti ya upole iliyotawala tabasam,na kwa kuwa alimuhitaji Siwa amkumbatie?nae hakufanya kosa alijisogeza akamkumbatia mume wake wakati huo akitabasam huku machozi yakimtoka kwa sababu alikuwa akiumia moyoni mwake.
Baada ya hapo Siwa alijing 'atua kidalini kwa Joeli alijifuta machozi kwanza na kisha akasema "Joeli,ni kweli utanilinda na kunipenda kama zamani?.. Joeli alishusha pumzi kwanza na kisha akajibu "Mke wangu Siwa ya nini kukudanganya? Nakupenda na nitazidi kukupenda"
"Sawa hamna shida ila leo nataka mechi na wewe ujue siku nyingi sijafanya" Aliongeza kusema maneno hayo Siwa,Joeli nae kutokana na furaha aliyokuwa nayo abadani hakusita kumpa kile mkewe alichokitaka.
Siku zilisogea, Joeli aliendelea kuweka ukaribu na Naomi lakini pia hakuweza kumsahau mkewe halali ambaye ni Siwa. Mapenzi ya Joeli na Naomi yalizidi kunoga,ikafikia hatua Siwa akawa ameyazoea mapenzi hayo kiasi kwamba kuna wakati Naomi alikuwa akija kulala na Joeli chumbani kwa Siwa wakati huo Siwa akiwapisha na kwenda kulala sebuleni mpaka asubuhi pindi Naomi anapo rejea nyumbani kwake.

Maisha hayo yalikuwa endelevu Naomi kuja kulala chumbani kwa Siwa na kisha asubuhi kuondoka zake,Siwa aliumia sana ila hakuwa na namna zaidi ya kukaa kimya. Alifanya hivyo akiamini kuwa pindi atakapo weka kinyongo huwenda mambo yakawamuwea tofauti kwa mara nyingine, ukimya ukawa ngao yake kulinda uhusiano wake na mumewe. Lakini kama wahenga walivyosema,vipo vitu vya kuchangia ila sio mapenzi. Na ndicho kilichotokea kwa Siwa kwani baada siku kusonga mbele zaidi mwishowe Naomi alizidi kumkamata vilivyo Joeli,na hivyo Naomi akamshauri Joeli kuwa amfukuze ama amuue Siwa ili aishi nae. Jambo hilo lilimshtua Joeli,ambapo alikataa katu katu. Kitendo hicho cha Joeli kumkatalia Naomi,Naomi alikasirika sana kwa sauti ya ukali akasema "Joeli unajua kama mimi nakupenda lakini pia na wewe unanipenda,nipo tayali kukuzalia hata watoto kumi ila kama hutotelekeza matakwa yangu basi mimi na wewe basi na hii mimba hii niliyonayo nitaitoa" Alisema Naomi,Joeli akajiuliza "anhaa kumbe tayali Naomi mjamzito? Jambo jema sana lakini kuhusu uamuzi huu? Mmmh acha nimuombe nafasi nikajifikilie kwanza nisije nikajutia maamuzi yangu " aliwaza na kujiuliza Joeli kisha akaishusha pumzi kwa nguvu,akamtazama Naomi wakati huo wakiwa kwenye moja ya kumbi ya starehe saa ya jioni. Na mara baada kumtazama alisema "Jambo hilo linahitaji muda kidogo kulifanyia kazi mpenzi wangu,kwanza nieleze furaha yangu baada kusikia we mjamzito pili nizungumzie suala la Siwa. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali kwamba hili jambo linahitaji muda kidogo hivyo tulia Naomi maana siku zote subira yavuta heri" alisema maneno hayo Joeli kisha akanywa soda aliyokuwa ameshaimimina kwenye grasi. Naomi bado alionekana kutolidhishwa na maneno ya Joeli, na hivyo akanyanyuka kutoka kwenye kiti huku akiwa amekasirika. Joeli baada kuona Naomi kanyanyuka akiwa na jazba alishangaa sana akamuuliza "Kulikoni mpenzi kwahiyo hujalizika na maelezo yangu?.." alihoji Joeli ila licha ya Naomi kuulizwa hivyo lakini hakujibu zaidi ya kuondoka na kutoka katika ule ukumbi. Upande wa pili watu wakiokuwemo ndani ukumbi ule walitupia macho yao kutazama kule alipokuwa ameketi Joeli na Naomi,baadhi ya watu hao waliokana kung'onona. Kwa sauti ya chini japo sio sana Joeli alisikia sauti ikisema kutoka kwa mmoja ya watu waliokuwemo mle ndani. Jamaa huyo ambaye alionekana kijana wa makamo mwenye utanashati wa aina yake alisikika akisema "Ebwanaee mtoto mrembo vile kamzingua mshkaji? Daah jamaa atakuwa kaishiwa nini? Alisema huyo jamaa wakati huo jamaa wa pili yake ambaye alikuwa nae meza moja,nae alijibu "Itakuwa;ingawa mshkaji mwenyewe anaonekana si haba" Lakini wakati huo jamaa hao wawili walipokuwa wakizungumzia juu ya varangati la Joeli na Naomi,kwingineko Joeli alionekana akimkimbilia Naomi ili ajue ni wapi mwanamke huyo anataka kwenda. Alipomfikia alimshika mkono na kisha akamuuliza"Naomi, nini sasa unafanya? Ama nimekosea kukwambia kuwa nahitaji muda kidogo kulifikilia jambo hilo utakalo wewe?.." alihoji Joeli ila Naomi hakujibu alitazama pembeni kitendo ambacho kilimpelekea Joeli kumuuliza kwa mara nyingine tena "Mbona unatazama pembeni? Nijibu basi ili nijue kama nimekukosea kukupa jibu lile " Hapo Naomi alimgeukia Joeli akamtazama akanying'atua kwenye mkono wa Joeli kisha akasema "Joeli Naomba uniachie kwa muda nafikilia kupumzika muda huu"
"Eti eeh sawa kama vipi panda ndani ya gari nikurudishe nyumbani kwako" alijibu Joeli wakati huo akimuonyeshea Naomi tabasam ambalo Naomi hakuweza kulijibu kwa sababu alikuwa amekasirika.
Walizipiga hatua kurudi mahali ilipokuwa gari yao,walipoifikia tu Joeli alimfungulia mlango Naomi kisha akarudi upande wake akafungua mlango akaingia ndani ilihali muda huo Naomi tayali alikuwa ameketi kwenye siti. "Daah Naomiiii.. unaniua kwa presha mamaa." Alisema Joeli huku akizungusha ufunguo wa gari ambapo punde si punde gari hiyo liliwaka. Wakati huo wale vijana waliokuwa waking'ona kuhusu lile vurumai la Joeli na Naomi lilokuwa limetokea muda mfupi uliopia nao walitoka ndani ya ule ukumbi wa starehe. Joeli alipowaona alishusha kioo cha upande wake na kisha akawanyooshe kidole gumba akiashiria kuwa mambo yamekwenda sawia. Jamaa wale walipomuona Joeli kawanyooshea kidole gumba, mmoja aliivunja shingo yake ili apate kutazama mtu wa pili aliyekaa nae Joeli wakagundua kuwa ni yule mwanamke aliyesusa muda mchache nyuma ambaye nae si mwingine bali ni Naomi. Hapo wale jamaa walimjibu kwa hiyo hiyo ishara, kisha Joeli akakunja kona tata akatembea zake wakati huo huku nyuma hao jamaa waliangua kicheko huku wakigongeana mikono. Na mara baada ya kicheko hicho mmoja alisema "Loh chezea sketi wewe? Hatari jamaa kabembeleza mpaka dem kaeleweka" CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kabisa aisee,Na nimeamini hawa wavaa sketi wana akili za kuku. Yani ubongo wao na ubongo wa kuku abadani hawapishani" kwisha kusema hayo maneno walirudia kuangua vicheko huku wakiambaa na barabara kutoka pale kwenye kumbi ya starehe.
Upande wa pili Joeli alimfikisha Naomi nyumbani kwake,ni nyumba aliyompangishia. Nyumba nzuri ya kifahari ambayo iliendana na hadhi aliyonayo Naomi. Na mara baada kumfikisha nyumbani, Joeli aliomba ruhusa ya kurudi nyumba kubwa yani kwa mkewe ambaye ni Siwa. Naomi alikubali lakini kabla Joeli hajaondoka,Naomi alimuuliza "Hivi Joeli kati ya mimi na Siwa ni nani bora?.." Swali hilo lilimfanya Joeli kucheka kidogo, na baada ya kuhutimisha kicheko chake alijibu "Me nafikili nyote bora ila mnazidiana. Wewe ni bora sana kwangu kwa sababu umenifanya niwe na furaha ya kutegemea kwamba miezi kadhaa mbele na mimi nitaitwa baba" alijibu Joeli. Muda huo huo Naomi aliongeza kusema tena safari hii alionyesha msisitizo. Naomi alisema "Basi kama umegundua kuwa mimi ni bora,ama unatamani kuitwa baba basi muue Siwa ili mahusiano yangu na wewe yazidi kudumu daima na tuwe baba bora kwa familia yetu"
"Daah Naomi kuua mtu sio kazi rahisi ujue? Alijubu Joeli. Naomi alishusha pumzi kwa nguvu na kisha akarudia kusema "Wewe ni mwanaume acha uoga, lakini pia ukae ukijua nipo tayali kushirikiana nawe. Je, upo tayali kulitekeleza jambo hili? Alihoji Naomi.
"Ndio nipo tayali" Joeli alijibu.
ITAENDELEA

0 comments:
Post a Comment