Simulizi : Sanda Ya Siwa
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa hakutokuwa na tatizo endapo kama tutashirikiana katika hili suala ili kama ni dhambi basi wote tukitumikie kikombe hiki" alijibu Joeli na kisha akaondoka zake kurudi nyumba kubwa wakati huo muda ulikuwa umeshataladadi kwa maana hiyo ilikuwa yapata saa tano usiku. Joeli alipoingia ndani alimkuta Siwa ameshalala,hakutaka kumuamsha zaidi aliingia bafuni kuoga na kisha akalala nae. Hapo Joeli akaanza kufikilia mstakibali wa Siwa,alijiuliza ni njia gani atayotumia kutimiza azma yake aliyopanga na Naomi. Hakuishia hayo tu,alizidi kuwaza mambo mengi sana hasa hasa akikumbuka miaka ya nyuma kidogo enzi ya uchumba wao. Hakika yalikuwa maisha yenye furaha sana kati yao,kipindi hicho Joeli alikuwa mtu asiye na hili wala lile kwa sababu maisha yao nyumbani alikuwa duni kiasi fulani ilihali upande wa pili Siwa maisha yao yalikuwa ya juu tofauti na maisha ya kina Joeli. Kwa maana hiyo Joeli aliishi kwa kumtegemea Siwa kuhusu shida ndogo ndogo,abadani Siwa nae hakuweza kusita kumsaidia mchumba wake. Kauli moja aliyopenda kumwambia Joeli ni kwamba hataki kumuona akilia shida hasa kwa shida ambayo angeliweza kumsaidia,ama hakika Joeli alifurahia uwepo wa Siwa binti wa kitajiri aliyetokea kumpenda wakati yeye hana kitu. Jambo ambalo lilimfanya Joeli kujiuliza maswali mengi rukuki kuhusu upendo huo,maswali ambayo aliyakosa majibu yake mpaka pale alipofunga nae ndoa na kutambua kweli Siwa kwake kafa kaoza. Yote hayo Joeli aliyakumbuka wakati huo akiwa amejilaza kitandani,alishusha pumzi kwanza ilihali muda huo huo akazama kwenye dimbwi la mawazo kwa mara nyingine. Safari hiyo alivuta taswira pindi Naomi atakapo mzalia mtoto,alijenga picha fulani kichwani mwake na kutambua kuwa itakuwa ni raha mstarehe lakini mara ghafla picha hiyo aliyokuwa ameijenga kichwani ilitoweka baada kukumbuka maneno ya Naomi. Maneno ambayo yalimshtua na kujikuta akiamini kuwa ili picha hiyo aliyojenga kichwani iweze kutimia basi inamlazimu kumuua Siwa. Jambo hilo lilimuweka Joeli kwenye wakati mgumu sana,ikawa ngumu kutema ngumu kumeza pia alijikuta akishusha pumzi mara kwa mara huku usingizi nao ukimtoweka mara dufu. Aliwaza na kujishauri uwezekano wa kulitekeleza hilo jambo,na kabla hajapata jibu muafa alikumbuka haya maneno ya Naomi aliyomwambia "Joeli unajua kama mimi nakupenda lakini pia na wewe unanipenda,nipo tayali kukuzalia hata watoto kumi ila kama hutotelekeza matakwa yangu basi mimi na wewe basi na hii mimba hii niliyonayo nitaitoa" Alikumbuka maneno hayo Joeli, kisha nae akajiuliza "Mmh kweliCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Naomi aue kiumbe changu? Aah wapi swala gumu hili,lakini nitamuuaje huyu mwanamke ili nisijikute naingia hatiaani?.." Baada kujiuliza swali hilo,alirudia kuyakumbuka maneno mengine aliyosema Naomi. Naomi alisema "Wewe ni mwanaume acha uoga, lakini pia ukae ukijua nipo tayali kushirikiana nawe. Je, upo tayali kulitekeleza jambo hili?.." Safari hii maneno hayo yalijirudia mara mbili mbili kichwani kwa Joeli. Hasa hasa neno ambalo lilimjia kwa sana kichwani mwake ni swali aliloulizwa kama yupo tayali kulitekeleza jambo hilo. Lakini mwisho wa yote Joeli alijijibu mwenyewe, ndani ya ubongo wake alijibu "Yeah nitakuwa tayali liwalo na liwe kwani Siwa ni sawa na mzabibu usio zaa, huu utang'olewa utatupwa mbali kabisa na shamba " kwisha kujijibu, alijifunika shuka. Safari ya kusaka usingizi ikawa imeanzia hapo.
Kesho yake asubuhi Joeli alihudhulia kazini kama kawaida,huku akiwa ametoka nyumbani bila hata kuonana na mkewe. Hivyo Siwa alipoamka jambo la kwanza alichukua simu yake na kisha kumpigia Joeli kwani ni siku mbili sasa walikuwa hawajaonana ingawa siku hizo mbili za hivi karibuni,Joeli alikuwa akilala nae. Simu ya Joeli iliita,kabla hajapokea alitazama kwanza ni nani aliyempigia. Akaona Siwa ndiye aliyempgia simu,hapo Joeli alikunja uso kuashiria kwamba ni kero kuona Siwa akimpigia lakini hakusita kupokea. Alipokea na kisha kusema "Hello"
"Hello Joeli mume wangu uko salama?.." alijibu Siwa kwa sauti ya mbali kabisa. Joeli nae aliposikia maneno hayo ya Siwa alishusha pumzi kidogo halafu akajibu "Ndio, kwani kuna tatizo?.." Siwa alishtuka kusikia jibu hilo ambalo liliambatana na swali ambalo anatakiwa kulijibu,lakini Siwa kabla hajalijibu swali hilo alikaa kimya kwanza huku kichwani akijiuliza "Mmh kulikoni mbona kawa mkali asubuhi yote hii mapema? Ama kazini mambo hayako sawa? Mmmh itakuwa lakini kama sivyo basi patakuwa na jambo hapa katikati limejificha" alijiuliza na kujiaminisha namna hiyo Siwa kisha akamjibu mumewe Joeli "Hapana hakuna tatizo ila nilita.." Kabla Siwa hajamaliza kusema alichotaka kumwambia Joel,mara ghafla Joeli alidakia akasema kwa sauti kali "Ila nini Siwa? Kwani hujui kama muda huu ni muda wa kazi? Ama nimekwambia leo siji nyumbani kwako? Aah embu tulia bwana usinichanganye asubuhi yote hii niache nifanye kazi kwanza ebo" kwisha kusema maneno hayo alikata ilihali hajapiga yeye. Siwa pumzi alishusha baada Joeli kumkatia simu,lengo la yeye kumpigia simu ilikuwa ni kumjulia hali tu kwa sababu ni siku mbili hajamtia machoni. Kwani Joeli anakuja nyumbani usiku sana wakati huo yeye amelala lakini pia anaondoka asubuhi mno wakati huo huo yeye akiwa amelala,na ndio maana siku hiyo asubuhi mapema alijisikia kumpigia simu ili ajue hali yake na sio kitu kingine,lakini mwishowe Siwa anajikuta akitolewa maneno makali ambayo yalimchoma ndani ya moyo wake na kujikuta akidondosha machozi bila kukata. Na muda huo sasa wakati Siwa alipokuwa anatokwa na machozi kwa uchungu,upande wa pili punde si punde simu ya Joeli ilirudia kuita. Jieli skasonya huku kimoyoni akijisemea "Mwanamke huyu kichwa nazi,sasa acha nimtukane kabisa ili atambue kwamba anachikifanya ni ujinga" Alijisemea Joeli huku akiwa makini kutazama kilichokuwa kikiendelea kwenye Computer ilihali mkono wake wa kushoto ukiifuata simu yake ya mkononi,hima alicha kutazama Computer aliitazama simu yake ambapo alijikuta akitabasam baada kuona safari hiyo kapigiwa na Naomi. Haraka sana bila kupoteza muda Joeli alipokea,ikisikika sauti ya Naomi ikisema "Joeli mpenzi umeondokaje kazini bila kujua mkeo nimeamkaje?.." Joeli aliposikia maneno hayo ya Naomi hakujibu,alikaa kimya kidogo na kisha akajibu "Siku huwa hazifanani malaika wangu,hivyo naomba kwa leo nisamehe" Alijibu Joeli akionekana kujishusha maradufu kwa Naomi,moyo wake ulitamalaki vyakutosha kwa Naomi alimsahau kabisa mwanamke anyeitwa Siwa kisa Naomi. Hasira zile alizozionyesha kwa Siwa mara tu alipompigia simu ili kumjulia hali zilitoweka,baada kupigiwa simu na Naomi ambaye alikuwa akilalama kwanini ameenda kazini pasipo kumjulia hali. Na kwa kuwa Naomi alitambua fika kwamba Katu Joeli hana ujanja kwake,hivyo alijifanya kususa msamaha wa Joeli.kitendo kilicho pelekea Joeli kusimamisha kazi aliyokuwa akifanya, akageukia kazi ya pili ya kumbembeleza Naomi. Lakini Naomi bado aliweka ugumu wa aina yake,hakutaka kuelewa kile akisemacho Joeli na ndipo Joeli alipojiongeza akamuuliza Naomi ni amfanyie ili amsamehe kwa kosa la kutokumpigia simu asubuhi.. Naomi haraka sana akajibu "Simtaki Siwa,na nataka uniambie sasa hivi lini tutatekeleza mipango tuliyopanga"
"Anhaa Kumbe hilo?.."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio"
"Basi acha kununa wiki hii tunamaliza mbona!?.." Alisema Joeli,hapo Naomi alisikika akicheka na punde si punde alimuimbia Joeli nyimbo nzuri ambapo wote kwa pamoja walifurahi wakati huo upande wa pili alionekana Siwa anayafuta machozi.
Na mara baada Joeli na Naomi kufikia muafaka,Waliagana na kisha Naomi akakata simu ambapo Joeli muda huo huo aliirudisha simu yake sehem maalum na kisha akaegemea kiti chake huku akiambatanisha na pumzi ndefu aliyoshusha wakati huo akijisemea moyoni "Siwa..Siwa..Siwa Utaniwia radhi kwa hatua hii"
Kwisha kujisema hayo maneno, alirudia kushusha pumzi kwa nguvu halafu akaendelea na kazi aliyokuwa akifanya muda huo kabla hajapigiwa na Naomi. Upande mwingine Siwa alionekana akiwa mezani kwa niaba ya kunywa chai ambayo tayali alikuwa amejiandalia,lakini ghafla alijikuta akishindwa kuinywa baada kukumbuka maneno aliyoambiwa na mumewe. Moyo ulimuuma sana,alijiuliza "kwanini Joeli anaamua kunifanyia haya? Kwa maana hiyo hajui kwamba mimi naumia? Aidha haoni thamani ya upendo wangu. Hivi dunia ya sasa kuna mwanamke mwenye kuweza kufanya maamuzi kama niliyoyafanya mimi? Ila bado tu Joeli haoni?.." alijiuliza Siwa huku akikitazama kikombe juu kwenye meza kilicho sheheni chai. Yote aliishia kuguna tu huku akivisogeza mbele yake chai na vitafunio maalum alivyokuwa amejiandalia asubuhi hiyo,na kwisha kufanya hivyo alinyanyuka akazipiga hatua kuingia chumbani kwake. Alipofika alikaa kitandani,mikono akaweka shavuni kana kwamba mama mjane aliyefiwa na mumewe. Alitulia dakika kadhaa kitandani hapo,lakini baadae alinyanyuka na kuisogelea droo ya kitanda ambapo ilikuwepo simu yake. Aliichukua haraka sana akanza kuitafuta namba ya Naomi,alipoipata alipiga. Punde si punde simu yake Naomi iliita,Naomi alitazama kioo cha simu yake akaona Siwa ndiye aliyempigia. Alipokea akasema "Rafiki kipenzi" Siwa akajibu "mmh wa kufa na kuzikana, habar za siku nyingi Naomi"
"Salama naona leo ndio umenikumbuka" alisema Naomi,Siwa alicheka kidogo na kisha akajibu "Ndio unajua siku nyingi hatujaonana wala kupigiana simu,hivyo leo nimeamua nikupigie maana mwenzangu upo kimya sana "
"Khaa? Lakini Siwa hakijaharibika kitu. Ammh bado tupo pamoja istoshe afadhali umenipigia,na hata kama usinge nipigia. Ningekupigia ili nikupe habari mpya " Alisema Naomi,hapo Siwa alishtuka na akakaa sawa kitandani huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua habari hiyo mpya aliyonayo Naomi "Enhee habari gani hiyo Naomi? Niambie tafadhali "
"Tayali nina mimba" Alisema Naomi kwa sauti ya kujiamini kabisa. Upande wa pili Siwa alishusha pumzi baada kusikia habari hiyo,wakati huo kichwani akijaribu kuunganisha matukio kadha wa kadha ya kiovu aliyokuwa akimfanyiwa na Joeli. Alipo pata picha kamili,akajisemea "Anhaa ndio maana Joeli ananiwea mkali siku za hivi karibuni,kwa maana hiyo ameshamuona Naomi ndio bora kuliko mimi? Lakini hata kama chanzo ni mimba ya Naomi lakini mbona aliniahidi kunipenda na kunienzi pindi nilipomruhusu kutoka kimahusiano na Naomi,kwahiyo tayali kavunja ahadi" alijisemea hayo maneno Siwa wakati huo huo Naomi alisikika akisema "Kulikoni Siwa mbona upo kimya? Kwani hujafurahishwa na hiyo taarifa?.." Siwa akajibu "Hapana sio kwamba sijafurahishwa,nimefurahi sana tena zaidi ya sana kwani tayali naona mume wangu anaenda kupata lile hitaji lake alilokuwa analitamani kwa muda mrefu. Ila tu jambo lilonifanya nikae kimya,ni baada kuwaza mambo anayonifanyia Joeli, nikahisi labda dharau anazoniletea ni kwa sababu ya wewe kumbebea mimba. Maana Joeli ananidharau sana,hataki kusema na mimi hata salam,sijui nifanyeje mimi kwa sababu kipindi hiki ndicho ambacho angenionyeshea furaha ingawa mimi sio mwenye mimba. Naomi,hivi unafikili dunia ya leo kuna mwanamke anaweza kumtoa sadaka mumewe kwa rafiki yake? Lakini mimi kama mimi baada kuona mume wangu anashida ya mtoto wakati mimi uwezekano wa kuzaa sina ikanibidi nimtoe sadaka kwa rafiki yangu ili amzalie nikiamini kwamba huwenda nitaishi kwa amani na yeye pia atajihisi mwenye furaha ila sasa ni kama sijafanya kitu,Joeli kila kukicha heli ya jana. Naomba rafiki yangu Naomi nisaidie na hili pia,nampenda sana Joeli wangu"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa usijali Siwa,pole kwanza kwa maswahibu hayo yanayo kukumba rafiki yangu lakini pia jaribu kupiga moyo konde yawakini tayali mimi mjamzito basi tambua bado miezi kadhaa tu nitajifungua. Nafikili hapo ndipo mkataba wangu utakapokuwa umefika tamati,kwahiyo nitajitahidi nimuweke sawa mumeo ili pindi atakapo achana na mimi rasmi akujali na kukuheshim kama awali. Wakati huo sasa nafanya jitihada hizi, wewe anza kuniandalia zawadi yangu tuliyokubaliana." Alisema Naomi. "Kila kitu kipo sawa usihofu kuhusu hilo,labda nikutakie siku njema Naomi" kwisha kusema hivyo alikata simu Siwa kisha akairejesha kwenye droo wakati huo upande wa pili Naomi aliitupia kitandani na kisha akaendelea na shughuli aliyokuwa akiifanya. Alikuwa akiziweka sawa nywere zake,kwani muda huo alikuwa ametoka bafuni kuoga. Lakini wakati Naomi anafanya hayo,moyoni alikuwa akijisemea mambo mengi kuhusu Siwa. Ambapo moja ya mambo aliyokuwa akijisemea ni kwamba Siwa ni asahau kuhusu Joeli,alienda mbali zaidi akidai kuwa kwa vyovyote Joeli hawezi kurudisha upendo wa dhati kwa Siwa kwani Joeli ni sawa na mtoto mdogo aliyechovya kidole kwenye kibuyu cha asali kwa hiyo sio rahisi kukiacha ilihali asali bado ipo nyingi kwenye kibuyu. Baada kujisemea hayo maneno aliguna,akainama akachukua mafuta akajipaka mwili na kisha akaongeza kujisema moyoni "Vipo vitu vya kuchangia ila sio mapenzi;katika hili Siwa utanisamehe. Sipo tayali kumuacha Joeli kwani laiti ungelijua usinge nikabidhi kwake,Joeli ni mwanaume niliyekuwa namtamani na kuwaza ni jinsi gani nitampata. Lakini mungu sio athumani,hatimae nimempata na mimba kanipa. Unafikili bado unachako?.." alijisemea Naomi kisha akaangua kicheko cha ndani kwa ndani.
Upande mwingine Siwa alitoka ndani akampelekea chai mlinzi wao wa getini, mlinzi huyo aliitwa Jerome. Alipokwisha kumkabidhi chai hiyo na vitafunio alizipiga hatua kurudi ndani lakini kabla hajaingia ndani, Jerome alimuita. "Bosi " Siwa aliposikia sauti ya Jerome aligeuka nyuma ambapo alikutana na ishara ya Jerome ikimuita kwa mkono. Hivyo ikabidi Siwa aahilishe safari ya kuingia ndani, alirudi nyuma kumsikiliza Jerome anakipi cha kumwambia. Alipomfikia,Jerome alisema " Samahani kwa kukusumbua bosi wangu, nia na dhumuni ya kukuita ni kutaka nataka kukushukuru kwa chai yako. Lakini pia kuna jambo nataka nikuulize "
"Jambo gani? .." alihoji Siwa.
"Unajua Bosi,kwanza naomba ufaham kwamba jina lako ni kama jina la mama yangu huko kijijini. Ila yeye anaitwa kwa kirefu;yani Siwa wazuri. Sijui lina maana gani lakini nahisi anamanisha binadam ama walimwengu siwazuri,Eeh kwahiyo bibi yangu akaona ni bora ampatie mwanae hilo jina baada kuona walimwengu siwazuri hata kidogo " Alicheka kidogo Jorome mara baada kusema maneno hayo,alipohitimisha kicheko chake aliendelea kusema "Kwahiyo basi,kwa kuwa wewe ni wajina wa mama yangu. Napenda nikuite mama yangu ingawa kiumri tunashabiana japo wanizidi miaka kadhaa. Hivyo mama!? Naomba leo uniambie ni jambo gani hasa linakusumbua kwani kimuonekano sura yako inaonyesha ubebea maswahibu mengi mno, niambie basi huwenda nikakupa hata ushauri. Amaa kwa kuwa mimi ndiyo hivyo tena na siwezi kukushauri?.." alisema Jerome,Hapo Siwa aliachia tabasam kidogo kisha akamjibu "Hapana Jerome ndiyo hivyo nini sasa? We ni binadam unanafasi yako pia na ndiyo maana tukakuamini na kukuweka hapa getini. Aamh tuachane na hayo Jorome,ila ukweli ni kwamba mwenzio napitia maswahibu mengi sana sana tena ya kusikitisha."
"Enhee mambo yapi hayo,au ni yakifamilia ambayo mimi sipaswi kujua?.." Alihoji Jerome huku akiikunja mikono yake kifuani kana kwamba anasikia baridi. Siwa kabla hajamjibu alishusha kwanza pumzi kwa nguvu kisha CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akasema akianza kwa kuguna "mmh,Jerome sioni sababu ya kuficha hili jambo. Kwa maana hata wahenga waliwahi kusema kwamba mficha maradhi kifo humuumbua,Kwahiyo mimi ni kama mgonjwa katu siwezi kuyaficha maradhi nitatakwambia kila kitu kwani huwenda ukawa na kitu cha kunishauri " alisema Siwa,mlinzi Jerome aliuendeleza uturivu wake. Wakati huo Siwa akaanza kumueleza kila kitu kuanzia hatua ya ugomvi kuhusu suala la upatikanaji wa mtoto mpaka kufikia ile hatua ya kumtoa sadaka Joeli kwa Naomi akiamini kwamba kufanya hivyo inaweza kumletea amani kati yake na mumewe ambaye ni Joeli,kitendo ambacho kilienda sawa hapo mwanzoni lakini kadili siku zilivyozidi kwenda ndivyo mambo yale yale ya zamani yakanza kujirudia mpaka kukomaa kabisa. Mlinzi Jerome iposikia mkasa huo wa Siwa,aliinamisha uso chini huku akisikitika. Baadae kidogo aliinua uso wake kisha akasema "Daah! Pole sana bosi wangu, kwani ukisikia majaribu ndiyo hayo. Kitu cha kwanza naweza kusema umefanya kitu kimoja cha busara sana ila mumeo ndio fala." Siwa alishtuka kusikia kauli hiyo ya mlinzi Jerome,kwa mshangao akahoji "We Jerome unamaana gani?.." Jerome alicheka kidogo halafu akamjibu "Nina maana kwamba mumeo ni fala,kwani haujui thamani yako ingawa pia na wewe ulikurupuka kuchukua maamuzi magumu japo ulifanya kitendo cha busara. Bosi una.." kabla Jorome hajaendelea kusema alichotaka kumwambia Siwa,alikiweka kwapani kurungu chake kisha akaendelea kusema, "Bosi unajua siku zote ukizama katika suala nzima la mapenzi, utagundua kuwa sisi wanaume kwenye mapenzi ni sawa na madume ya mbwa. Hahahaha.." Alisema mlinzi Jerome huku akimaliza kwa kicheko,wakati huo Siwa akimtazama tu ingawa mwishowe alivunja ukimya na kisha kumuuliza swali
"Bado sijakuelewa Jerome,hembu nifafanulie hayo maneno yako"
"Unataka nikufafanulie,juu ya jambo hili nililokwambia kwamba wanaume kwenye mapenzi ni sawa na madume ya mbwa?.. hahahahaaa mbona rahisi sana kujua maana?Basi suburi nikwambie nimemanisha nini"
"Mbwa hata umpe chakula kingi kiasi gani,ila akienda kuzulula akiona mfupa mtaani katu hawezi kuuacha. Nikiwa na maana kwamba mwanaume hata umpe mapenzi ya namna gani,kamwe hashindwi kumtamani mwanamke mwingine. Bali mwanaume asiyekuwa na tamaa ni yule aliyeikamata dini na anayatumikia maandiko vizuri,kwani huyu ni sawa na mbwa aliyefungiwa ndani ya uzio wa geti" Siwa alicheka baada kusikia maelezo ya mlinzi Jerome. Baada ya kicheko hicho alimtazama na kisha akamwambia "Hapo nimekuelewa,Hahaha hahaaa!!! Jerome unavituko wewe? Mmnhmm haya nishauri sasa nifanyeje mimi ili ndoa yangu iweze kuimalika vizuri "
"Hivi unampenda sana mumeo?.." Jerome aliuliza.
"Ndio tena zaidi ya sana kiukweli Jerome "Alijibu Siwa huku akionyesha msisitizo. Jerome safari hiyo alikaa kimya ikiwa uso amainamisha chini,ingawa mwishowe aliuinua na kisha kuongeza kusema "Kwanini usifikilie suala la kuondoka nyumbani hapa, kwani kwa dalili hizo ninazo ziona tayali mumeo hakuhitaji tena ila anashindwa kukwambia. Na pia ukae ukijua moyo huo ulio nao wewe sio alionao rafiki yako,mapenzi mchezo mchafu. Rafiki anaweza kuwa mnafiki,akamshawishi mumeo wakakubaliana kukuua ili wabaki wakiponda raha. Kwahiyo kabla hayajatokea yote haya ni bora uondoke zako,kwa maana siku zote akufukazae hakwambii toka"
"Mmh hapana Jerome, ushauri wako sio mzuri kiukweli. Yani mimi niondoke nimuachie mume rafiki yangu ? Hapana siwezi kiukweli labda useme jambo lingine nitakuelewa" alijibu Siwa.
"Kwa hapo sina jambo lingine zaidi ya kukupa pole,ila ushauri wangu ulikuwa huo tu" alieleza Jerome kisha akazipiga hatua kuelekea mahali kilipokuwa kiti chake,aliketi wakati huo Siwa nae alirudi ndani.
Jioni ilipo wadia,muda wa kutoka kazini. Alionekana Joeli akitoka ofisini huku akiuzungusha ufunguo wa gari akizipiga hatua kuifuta gari yake,alipo ifikia alifungua mlango lakini kabla hajaingia ndani alisikia simu ikiita. Haraka sana aliingiza mkono mfukoni,alipotazama aliona Magesa ndiyo kumpigia. Joeli alipokea "Ndiyo ndugu!.."
"Ukowapi Joeli?.." aliuliza Magesa.
"Nipo nje hapa ndio narudi nyumbani,vipi kwani kuna tatizo?.."
"Hapana,ila nina mazungumzo na wewe Joeli sasa sijui tukutane wapi!.."
"Kwani wewe ukowapi?.."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kuna kazi ndogo sana namalizia hapa"
"Anhaa basi acha mimi nirudi nyumbani utakapo toka unipigie simu"
"Sawa haina tabu Joeli" Joeli alikata simu kisha akaingia ndani ya gari. Aliliwasha gari lake moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Naomi. Alikuta tayali Naomi kapendeza, na kilichokuwa kimesubiliwa ni kutoka na kwenda kuponda raha. Joeli alipomuona Naomi kapendeza alitabasam na kisha akasema "Mmmh mtoto mzuri mzuri,natumai tutajenga familia nzuri pia" alisema Joeli huku akilivua koti lake na moja kwa moja akamkumbatia mpenzi wake. Baada ya hapo alikwenda bafuni kuoga,aliporudi alikuta chakula tayali kipo mezani. Joeli alikula chakula tonge la kwanza akamtazama Naomi ambaye muda huo alikuwa amekaa kiti cha mbele yake "Naomi nikwambie kitu?.." alihoji Joeli. Naomi alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Ndio niambie wala usiogope"
"Kiukweli leo umenikosha sana, yani umepika chakula ambacho sijawahi kula katika maisha yangu. Ulivyo mtam uwanjani na kwenye mapishi ni hivi hivi,mungu akupe umri mrefu bwana Dah!..Na ulivyo jua kucheza na tumbo langu we acha tu,maana siunajua leo tunatoka tunaenda kula nyama choma?.."
"Ndiomaana nikapika chakula laini laini mpenzi" alijibu Naomi. Jibu ambalo liliwafanya wawili hao kutazamana na kisha kuangua kicheko. Muda mchache baadae Joeli alimaliza kula,aliingia chumbani kubadilisha nguo alipendeza mno ambapo walijongea mpaka kwenye gari kwa niaba ya kwenda kwenye kumbi ya starehe. Wakiwa ndani ya gari,mara ghafla simu yake iliita. Ni Magesa ndiye aliyempigia muda huo. Joeli alipokea na kisha akamuelekeza mahala wanapotegemea kwenda kuponda raha. "Anhaa Sawa nakuja huko huko" alijibu Magesa halafu akakata simu. Punde si punde walifika eneo hilo husika,ni ukimbi mzuri sana ulionekana kupendeza kila mahali. Muziki mzuri kutoka mashariki ya mbali uliupamba vilivyo ukumbi huo. Joeli na Naomi walishuka kwenye gari wakaingia ndani ya huo ukumbi,wakayi huo huo Magesa nae alifika na gari yake. Alishuka kisha akaambatana nao kuingia ndani,lakini alipomuona Naomi alishtuka ila hakusema jambo lolote zaidi ya kuishia kusikitika. Wote kwa pamoja waliketi kwenye viti vya meza moja,muhudumu alikuja kuwasikiliza ambapo kila mmoja akaagiza kile akipendacho baada ya hapo zogo lilifiatia huku Joelia akimtambulisha Naomi kwa Magesa,vile vile Magesa alitambulishwa kwa Naomi.
"Hahahaah hahaah!!!! Daah Joeli we kweli kiboko,upo vizuri.." alisema Magesa akianza kwa kuangua kicheko. Joeli alicheka kidogo halafu akajibu "Huu ndio uwanaume Magesa,siwezi kukaa na mwanamke mmoja kwani umsikia mimi mbovu? .." aliuliza Joeli kwa masihara ilihali Naomi nae akiishia kutabasam tu. "Alaah! Kwahiyo kumbe unamanisha wanaume wanye mpenzi, mke mmoja hao ni wabovu? .."
"Ndiyo hivyo Joeli kubali ukatae "
"Doh! Sawa bwana" alikata kauli Magesa kisha mazungumzo mengineyo yakafuatia. Baada kuzungumza mengi,hatimae Magesa alimuita faragha Joeli ili aseme nae jambo hilo lililomsukuma na kutaka wakutane ili amwambie. "Samahani kidogo shem,ila sio muda mrefu namruhusu aje " alisema Magesa akimwambia Naomi. Naomi alicheka kidogo halafu akajibu "walaa! usijali" Walipotoka hapo walijiweka kando sehem ambayo wakizungumza wanasikika vizuri. "Joeli,mbona mkeo ananiletea kesi kwamba wewe siku hizi umebadilika? Humjali,akikuoigia simu unamkalipia mara hili mara lile eeh sikuelewi ujue?.." alisema Magesa.
"Siwa ndiyo kakuambia maneno hayo?.." alihoji Joeli.
"Ndio kwani sindio mkeo?.."
"Sawa,labda nikuulize swali bwana Magesa. Hivi ikitokea shambani mwako kuna mmea usio zaa matunda utauchulia hatua gani?.."
"Sijakuelewa,embu achana na hizo nahau zako bwana nijibu kama ni kweli haya unayomfanyia shemeji ama sio kweli,na endapo kama ni kweli unampango gani kwake? .."
"Magesa,jibu lako utalipata endapo endapo kama utanijibu swali langu! Kwani hajakwambia chanzo ni nini?.."
"Hapana ndio nataka uniambie wewe"
"Ok,Shemeji yako ni kama mmea usio zaa matunda. Na siku zote mkulima akiona mmea usio zaa abadani hawezi kuendelea kuucha shambani,anaungoa na kuutupa. "
"Joeli,unamana kwamba shemeji ni tasa? CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio,na ndio maana nimechukua kifaa kipya ili kinizalie mtoto. Hivi hujui kama naona wivu ninapowaona wenzangu mnatoka na familia zenu?.."
"Daah masikini Siwa,lakini ujue Joeli wewe ndio msababishaji wa tatizo hilo"
"Kivipi sasa? Magesa acha kunipanda kichwani,kwanza niache bwana" alisema Joeli,safari hiyo alikuwa amekasirika sana baada Magesa kumtuhum kuwa yeye ndio chanzo cha tatizo alilonalo Siwa. Jambo hilo lilimkera vilivyo Joeli ambapo aliamua kuondoka zake huku akimtolea Magesa kauli chafu, kauli ambazo Magesa alishindwa kuzivumilia. Nae alimjibu mara mbili zaidi ya zile alizokuwa akizitamka Joeli. Magesa alisema "Kua na tabia za kiume mtu wangu,kumbuka yule mkeo lakini pia alikutoa mbali mpaka kufika hapo ulipo. Lakini jitu unakua na tabia za kimama? Huyo ni malaya kwako na yule ni mkeo hatakama tasa;mshenzi wewe" alisema Magesa,kijana muongeaji ambaye alibarikiwa sauti kubwa. Joeli hakumjibu Magesa,alizipiga hatua mpaka mahali alipokaa Naomi. Alipofika alimtaka Naomi waondoke mahala hapo,haraka sana Naomi alinyanyuka kutoka kwenye kiti alichokuwa amekakalia,hima akatii matakwa ya Joeli. Walipokuwa ndani ya gari wakirudi nyumbani, Joeli alisikika akisema "Siwa? Aah sio wakunitangaza nje mimi?Kanivunjia heshima kabisa,sasa nafikili hanijui ngoja nikamkomeshe" Alijiapiza Joeli, Naomi aliishia kumtazama tu pasipo kujibizana nae. Punde si punde walifika nyumbani,Naomi alitelemka kwenye gari na kisha Joeli akageuza gari kurudi nyumbani alipo Siwa huku moyoni akiwa amefura hasira. "Atanitambua leo" alisema Joeli huku akiongeza kasi gari yake,ilihali kumbukumbu zikimkumbusha kuwa ndani ya wiki hiyo anatakiwa kuchukua maamuzi magumu kwa mgumba Siwa.
Haikuchukua muda mrefu Joeli kufika nyumbani kwake,wakati huo tayali ilikuwa imetimia saa tano usiku. Alikuta mlinzi Jorome amesinzi,hali iliyopelekea Joeli kupiga honi taklibani mara tatu. Jerome alipoisiki honi ya gari alizinduka kutoka usingizini,haraka akakimbilia kwenye tundu maalum la kutazamia nje. Akagundua kuwa ni bosi wake kafika, bila kuchelewa alifungua geti ambapo alijikuta akitupiwa maneno machafu na Joeli. "Jerome unalalaje muda huu? Acha ujinga bwana umekuja kufanya kazi ama umekuja kulala?.." alifoka Joeli huku akikata kona gari yake kuingia mahala pakuipaki. "Daah Samahani bwana bosi, kausingizi kamenipitia hapa nilikuwa nasikiliza karedio" Alijibu Jerome huku akiiweka sawa kofia yake aliyovaa kichwani lakini Joeli hakujali maneno hayo ya Jerome,zaidi alishuka kwenye gari na kisha akazipiga hatua za haraka haraka kuingia ndani. Alipofika sebuleni akamuita Siwa kwa sauti ya ukali. "Siwa Siwa..ukowapi mshenzi mkubwa wewe? .."Aliita Joeli wakati huo Siwa alikuwa yupo chumbani, aliposikia sauti ya mumewe ikimuita alishtuka akanyanyuka kutoka usingizini akakaa kitandani kisha akajiuliza "Kwani nimefanya nini? Mbona leo kakasirika sana? Ama Magesa kamwambia tofauti na kile nilicho mwambia?.." alijiuliza Siwa wakati huo huo Joeli akaingia chumbani huku akiwa bado amefura hasira iliyompelekea kumjia juu na kisha kusema "Siwa kwanini siri za ndani unaweka gadharani"
"Siri za ndani naziweka hadharani? Kivipi yani Joeli sijakuelewa?.." Alihoji Siwa huku akisimama chini kutoka kitandani ilihali akionekana kushtushwa na maneno aliyosema Joeli. "Kwahiyo umeamua kusimama? Unataka tupigane sio?.." Joeli aliuliza. "Sio hivyo Joeli lakini.." "Lakini nini?.." alipigwa kofi Siwa kabla hata hajamaliza alichotaka kusema. Siwa akaangukia kitandani, akajiinamia huku akilia. Wakati huo Joeli aliendelea kusema "Mwanamke mjinga sana wewe, huna akili. Huwezi kunitangazia mabaya inje mimi,ili iweje sasa? Siwa wewe ni mfano wa mmea usio zaa matunda,shambani unangoja nini kama sio kung'olewa na kisha kuutupa mbali? Yani huna faida. Ila mimi kwa fadhila zangu bado unaishi na mimi,kitu ambacho mwanaume mwingine abadani hawezi kuishi na mwanamke asiyezaa" Alisema Joeli maneno hayo. Maneno ambayo yilimchoma Siwa, ambapo aliinua uso wake ambao ulikuwa bado ulikuwa ukibubujika machozi na kisha kusema "Joeli we sio wa kunidhihaki kiasi hicho bwana,umesahau kwamba chanzo cha ugumba wewe ndio umenisababishia? Kumbuka nilinasa mimba mara ya kwanza,ukanishauri nitoe ili niendelee na masomo lakini pia kwa ajili ya kukunusuru wewe. Nilikubali. Nikanasa mara ya pili bado ukanitaka nitoe. Tena safari hiyo kwa kunilazimisha,nilikubali. Je, unafikili mungu alipendezwa na dhambi hiyo? Hakufurahishwa na ndio maana mshahara wetu ni huu" alisema Siwa huku akidondosha machozi. Joeli akajibu "Mshahara wako wewe sio mimi? Usiniletee mambo yako ya kipuuzi"
"Mpuuzi wewe Joeli na sio mimi" Alijibu Siwa,Joeli akashtuka akahoji "Unasemaje? Siwa unaniita mimi mpuuzi?.." Siwa hajajibu alikaa kimya huku akiwa ameinamisha uso wake chini. Hapo hapo Joeli akampiga kofi na kisha akasema "Nakwambia hivi kuanzia kesho nisikuone humu ndani,ondoka la sivyo nitakuua "CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Siondoki,kwa kipi hasa. Na kama unataka kunifukuza basi tugawane kila kitu" Siwa alijibu kwa sauti ya kilio. Joeli alizidi kakasirika mara dufu. Akaongeza kusema "Anhaa labda unatafuta kifo,na sio kugawana mali zangu. Mali hizi ataridhi mwanangu na sio wewe mwanahidha uliyekosa muelekeo" alisema Joeli. Hayo maneno yalimuumiza Siwa,aliendelea kumwaga machozi huku akipandisha kwikwi. Baadae kidogo aliyafuta machozi yake na kisha akajibu "Ujinga huo Joeli,mwanaume gani wewe? Sijawahi kukushtaki ila katika hili lazima nikushtaki kwa makosa yako mawili,moja kutishia uhai wangu. Pili unagoma kunipa talaka na kugawana mali ili niondoke zangu? Kumbuka kuanzia sahani na vitu vingine tulivitafuta wote,sasa iweje niondoke mikono mitu..." Kabla Siwa hajamaliza kusema alichotaka kuongea,Joeli alighazibishwa na maneno hayo yaliyompelekea kumpiga kofi usoni Siwa. Siwa akaanguka kitandani huku akiangua kilio,wakati huo huo Joeli alitoka ndani akaenda nje akaingia kwenye gari akapiga honi kumshtua mlinzi Jerome afungue geti. Jerome aliamka kutoka mahali alipokuwa amekaa, akaenda kufungua geti haraka haraka ilihali muda huo Joeli alikuwa tayali ameshalikalibia geti,ambapo alipopata upenyo aliongeza kasi na kisha kutoweka zake kwenye kiza kinene kilichokuwa tayali kimtamalaki usiku huo.
"Mmmh sio bure kutakuwa na jambo hapa" alijisemea Jerome huku akifunga geti. Na mara baada kuhakikisha komeo ibana vizuri,alizipiga hatua kurudi mahali alipokuwa amekaa mwanzo. Alipofika aliketi kwa muda wa dakika kadhaa,ambapo mwishowe aliamua kujisongeza kwenye kibanda chake aliingia na kisha kuanza safari ya kuutafuta usingizi.
Kesho yake asubuhi Jerome aliamka na kuendelea na majukumu yake, kwani licha ya kuwa mfungua geti ama mlinzi wa getini vile vile alihusika kufanya kazi za hapo nyumbani. Na pia Jerome alizoea kila siku ifikapo saa nne asubuhi pindi amalizapo kazi hizo,huletewa chai na Siwa. Lakini siku hiyo hali ilikuwa tofauti kabisa,kwani mpaka muda huo unafika hakuona dalili yoyote ya kuletewa chai wala hakumuona Siwa. Kitendo hicho kilimshtua Jerome, akajiuliza "Kunani kwa Bosi wangu wa kike! Kuna tatizo ama?Na kama hakuna mbona mpaka muda huu hakuna dalili yoyote ya kupata kifungua kinywa,au mbona simuoni akitoka ndani?" Alijiuliza mlinzi Jerome kisha akaishusha pumzi kwa nguvu. Na mara baada kujiuliza hivyo aliongeza kujisemea "Aalah! Sio bure yawakini Joeli alipoondoka jana usiku kutakuwa na kitu amekifanya kwa Siwa" Alijisemea mlinzi Jerome. Wakati huo upande wa pili Siwa alinyanyuka kutoka kitandani huku akiwa amechoka dhofu ilihali,mwili ukimuuma kila sehem shauri ya kipigo alichokipata kutoka kwa mume wake siku ya jana usiku. Alipo kanyaga sakafu alijihisi kizunguzungu,akajikuta akishindwa kusimama hali iliyompelekea kurudi kukaa kitandani. Hali hiyo iliendelea,na punde si punde alijihisi kichefu chefu ambacho haikuchukua muda mrefu akatapika. Siwa alitapika mpaka akajihisi kukosa nguvu,hali yake ikionekana muda wowote inaweza kuwa mbaya. Hivyo alichukua simu yake akampigia Naomi akamueleza hali harisi anayomkumba,taarifa ambayo ilimfanya Naomi kujifanya kushtuka. Akasema "Dah pole sana rafiki yangu,basi subili nakuja sasa hivi" alisema hivyo Naomi. Kweli ndani ya nusu saa honi ilisikika ikilia nje ya geti,ambapo Jerome alifungua geti ikaingia gari ndogo mpya aina ya Hulux. Ndani ya gari hiyo alishuka Naomi,akampa salamu Jerome kisha akazipiga hatua za haraka haraka kuingia ndani ambapo alipitiliza hadi chumbani. Huko alimkuta Siwa akiwa kajilaza kitandani,akionekana kulegea mwili mzima viungo vya mwili wake vikikosa nguvu. Siwa alipomuona Naomi alimtazama kisha akasema "Naomi,kosa langu nini mimi?Mbona Joeli ananifanyia haya?.." Naomi hakujibu, alikaa kimya huku uso wake akiwa ameuinamisha chini. "Joeli? Anafanya nini sasa? Iweje akupige kwa kosa lipi sasa? Mmh ngoja nimpigie simu kwanza" alisema Naomi baada kuvunja ukimya. Simu ya Joeli iliita, punde si punde akapokea. Naomi akasema "Joeli fanya uwezavyo urudi nyumbani hali ya mkeo sio nzuri"
"Kwani kakutwa na nini?.." akauliza Joeli, Naomi akajibu "we njoo bwana" kwisha kujibu hivyo akakata simu. Joeli alishusha pumzi,akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali kitu fulani. Wakati huo huo ujumbe mfupi wa sms uliingia kwenye simu ya Joeli,Joeli akaitazama simu yake akaichukua akaufungua ujumbe huo akakuta unaeleza "Umesahau tulichopanga?.." Ulisomeka ujumbe huo,hapo Joeli akakumbuka. Akili iligoma ila moyo ulipenda kutimiza jambo hilo walilopanga,na mwisho wa yote Joeli aliamua jambo moja tu. Nalo ni kutekeleza matakwa ya Naomi pasipo kulifikiria kwa jina kina jambo hilo. Haraka sana alitoka ofisini,akaonana na uongozi husika akaomba ruksa kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani. Kabla hajafika nyumbani alipita dukani akanunua kitu fulani halafu akaendelea na safari,alipofika nyumbani alimkuta Naomi akimuogesha Siwa bafuni. Naomi aliposikia Joeli kafika alitoka bafuni akamfuata. Alipomfikia alisema kwa sauti ya chini. "Nafikili kila kitu kipo sawa,Kwahiyo imebaki kazi moja" alisema Naomi. "Ndio, na sumu nimeshanunua" alijibu Joeli. "Sawa umefanya vizuri sana,ndio maana nakupenda. Mmmwaaa aah! ! Mume wangu. Basi fanya haraka andaa chai mezani hapo kisha tia sumu akinywa tu mchezo uwe umekwisha. Acha mimi nikamalizie kumuogesha" CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sawa hakuna shida" alijibu Joeli wakati huo nafsi na moyo vikizozana juu ya kutenda jambo hilo. Safari hiyo nafsi ilimsuta Joeli kufanya hicho kitendo ilihali moyo nao ukilidhia. Lakini mwisho wa yote moyo uliibuka kidedea,alitia sumu kwenye chai Joeli. Siwa alipoinywa chai hiyo,ghafla alihisi tumbo kuuma. Alilalama huku akisema "Joeli..Joeli nakufa mimi" alisema Siwa kwa sauti ya kulalama huku akihaha kwenye kiti mpaka aakunguka chini ,wakati huo huo Naomi akakimbilia chumbani akachukua mto wa kulalia na kisha kuja nao mpaka alipoangukia Siwa. Alipo mkaribia alisimama huku akimtazama. Siwa alipomuona Naomi akiwa aneshika mto alisema "Naomi? Kwanini lakini?.." Naomi hakujibu jibu lolote zaidi ya kumziba Siwa pua na mdomo kwa kutumia mto huo wa kulalia. Siwa alirusha miguu huku na kule,hakutoa sauti yoyote wala kupumua. Kitendo ambacho kilimpelekea kupoteza maisha,alikufa Siwa muda huo huo Joeli alitoka chumbani akakuta tayali Naomi kamalizia mahali alipoishia yeye. Joeli aliitazama maiti ya Siwa pale chini kisha akamtazama Naomi akajikuta akishusha pumzi kwa nguvu huku akihema haraka haraka.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment