Search This Blog

SANDA YA SIWA - 3

 







    Simulizi : Sanda Ya Siwa

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Joeli alionekana kama kupagawishwa na kile kilichotokea,hali iliyompelekea kumtazama mara mbili mbili Naomi na kisha kurudisha macho yake ulipo lala mwili wa Siwa akiwa tayali ameshafariki. "Joeli kipi cha kufanya sasa?.." alihoji Naomi.

    "Daah! Hata sielewi Naomi, yani sijui nikujibu nini kwakweli" alijibu Joeli huku akitetemeka.

    "Mbona sasa unaonekana unahofu? Wakati suala hili tulilipanga wote" aliongeza kusema Naomi. "Lah! Siogopi ila nawaza ni namna gani wa kulimaliza haraka hili suala kabla hakujatokea chochote " Joeli alijibu. Naomi alishusha pumzi kwa nguvu kisha akakaa kimya huku akionekana kutafakari jambo fulani ndani ya kichwa chake. Alinyamanza dakika zisozopungua mbili halafu akasema "Mimi nimepata wazo"

    "Wazo gani? .." Joeli aliuliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Taarifu ndugu jamaa na marafiki,uwapashe habari kwamba umepata msiba ili tukamzike"

    "Anhaa,Sawa kabisa" alisema Joeli na kisha akaanza kutafuta namba za watu wake wa Karibu ili kuwapatia taarifa ya msiba. Taarifa hiyo ilipomfikia Magesa,alishtuka sana. Bila kuchelewa akaomba ruksa kazini kisha akaanza safari ya kuja nyumbani kwa Joeli,ambapo alipofika alikuta tayali umati wa watu umeshakusanyika. Walikuwepo ndugu baadhi wa upande wa marehem Siwa,nao walifika baada kusikia Siwa kafariki. Simanzi ilitanda malangoni kwa Joeli,vilio vya kina mama vilizidi kumfedhehesha Joeli. Kiasi kwamba alishindwa kuyazuia machozi yake,licha ya kwamba yeye ndio muhusika mkuu wa kifo cha Siwa mgumba asiyekuwa na hatia. Lakini mwisho wa yote Siwa alizikwa,mazishi yakamalizika salama kabisa.



    **BAADA YA MIEZI MITANO**

    Mimba ya Naomi ilikuwa kubwa kabisa,Joeli alimtoa kule alipokuwa amempangishia nyumba akamleta kwenye nyumba ambayo hapo awali alikuwa akiishi na Siwa. Siku ya kwanza Naomi kuhamia hapo ilikuwa ni furaha sana kwake kwa maana hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu,ndoto ya kuishi na Joeli kama mke na mume hatimae ndoto hiyo ikawa imetimia. Siku moja jioni Joeli alipotoka kazini,aliketi sebuleni huku akijisomea gazeti. Punde si punde akaja Naomi akitokea chumbani,Naomi aliketi na Joeli kwenye sofa moja akamkisi na kisha akasema "Hivi Mume wangu unajua kweli ujauzito huu unamuda gani?..ama tu upo upo" Joeli kabla hajamjibu Naomi ambaye ndiyo mkewe kwa sasa. Aliangua kicheko kwanza halafu akajibu "Kwanini umeniuliza hivyo? Mimi najua unamiezi mitano, sasa sijui nimepatia? .."

    "Upo sahihi kabisa kabisa mume wangu,aamh Joeli nikwambie kitu?" NAOMI alijibu huku akiacha swali. "Ndio niambie wala usihofu"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nakupenda sana kiukweli,na ndio maana hata Siwa aliponiambia kwamba ananiazima wewe niliona kama anamkabidhi fisi bucha. Kwa kipindi kirefu sana nilikuwa nakutamani,niliwaza nitakupata lini wewe mwanaume. Lakini mungu alivyokuwa wa ajabu eti leo hii mimi nimekupata. Hakika nakuhakikishia hutokuja juta mpaka katika maisha yako" alisema Naomi kwa sauti nyororo huku akijilaza kwenye kifua cha Joeli ambacho muda huo alikivisha kaushi. Joeli alishusha pumzi ndefu mara baada kuyasikia maneno hayo Naomi,akakaa kimya kidogo halafu akajibu "Ahsante sana Naomi,unajua hivyo ulivyokuwa ukiniwaza wewe hata mimi nilikuwa nakuwaza na kukutamani pia. Pia hata nilipogundua kwamba Siwa ni tasa, nilianza kufanya mikakati ya kutafuta mwanamke mwingine wa kuweza kunizalia mtoto ama watoto;sio kumzalisha tu kama mbwa,lahasha nia yangu ni kumuweka ndani awe mke wangu. Sasa basi kama utamumbuka,kuna siku moja Siwa aliniomba nikusindikize nyumbani unapoishi. Sikujua ilikuwa na lengo gani,lakini ukweli ni kwamba nilijikuta nakukubali sana,hadi ikafikia hatua badala kushika kirungu cha gea nikajikuta nagusa paja lako. Yote shauri ya kuvutiwa nawe,na kizuri zaidi Siwa nae akaniomba anichagulie mwanamke nitakae zaa nae bahati nzuri akanichagulia wewe. Ukweli nilifurahi sana kwa sababu alienda na hisia zangu zlipokuwa zinagonga. Kwahiyo naona hakuna jipya, cha zaidi ni sisi kuendelea kupendana ili tujenge familia bora. Maana nilikuwa naona wivu ninapowaona wenzangu wanatoka na familia zao kwenda kuponda raha wakati huo mimi natoka na mke wangu tu kama njiwa" alisema Joeli akieleza kwa kirefu juu ya hisia zake lakini maneno hayo ya mwisho yaliweza kumfanya Naomi kuangua kicheko. Baada kukatisha kicheko chake,nae akasema "Wala usijali,ndiyo maana nimekwambia nakupenda na nitaendelea kukupenda daima" Kimya kidogo kilitawala hapo,ila haikuchukua muda mrefu kimya hicho kutoweka baada Joeli kumwambia Naomi kuwa amamaliza deni alilokuwa anadaiwa. Alikopa pesa bank akamnunulia Naomi gari aina ya Hulux,na ndio gari ile Naomi aliyokuja nayo siku ile baada kuitwa na Siwa. Naomi aliposikia habari hiyo alifurahi sana,akamsogelea zaidi mume wake akamkisi kisha akamwambia "Mungu mkubwa sana mpenzi,Kwahiyo tuna magari matatu sasa. Ukitoa gari hilo la kampuni tunabaki na magari mawili..."

    "Ni kweli mke wangu Naomi, lakini ujue gari hiyo nyingine ni gari la marehem mke mwenza wako!.." Joeli alijibu.

    "Mmh sawa,ila hatakama lilikua lake. Siwa alishakufa,kilicho kuwa chake sasa ni changu haina ubishi mume wangu"

    "Ni kweli sipingani nawe" Joeli alifunga mjadala namna hiyo,baada kukubali kile akisemacho Naomi.

    ****

    Basi maisha ya wapenzi hao yaliendelea kuwa ya furaha kila kukicha,wote kwa pamoja walimsahau Siwa kama aliwahi kuwepo duniani ila gari na baadhi ya nguo alizoacha ndizo ziliweza kuwakumbusha kwamba Siwa aliwahi kuishi hapa duniani. Na hata hivyo hizo nguo za Siwa mwishowe Naomi aliwagawia baadhi ya marafiki zake na nyingine alivaa kwa sababu nguo hizo zilikuwa nzuri za kumfaa mwanamke yoyote mwenye umbile kama la Siwa. Hapo sasa ikabakia gari,ambalo nalo Naomi aliamshawishi Joeli ili waulize. Joeli alikubali kuliuza gari hilo la marehem Siwa, gari ambalo Siwa aliachiwa na wazazi wake ambao tayali wametangulia mbele ya haki. Furaha isiyo kifani iliendelea kutamalaki kwa Joeli na Naomi,furaha iliyowapelekea siku hiyo kula na kunywa huku wakitembelea sehem mbali mbali za starehe. Walienda kutalii mbuga ya wanyama,walifanya kila starehe waliyoimudu. Yote hayo wakiyafanya kwa pesa waliyouzia gari la marehem Siwa.

    Usiku ulipo wadia, walirejea nyumbani wakiwa wamechoka sana pasipo kuwa na mfano kiasi kwamba walipoingia ndani walijitupa kitandani kama mizigo ya kuni adondoshwapo kutoka kichwani.

    "Nafikili umefurahi sana" Alisema Joeli akimwambia Naomi. Naomi alilembua jicho lake na kisha akajibu "Zaidi ya sana mpenzi wangu,istoshe kuuzwa kwa hili gari kutanifanya niwe na amani kabisa"

    "Kwanini?.." Joeli akahoji. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa sababu kila nilipokua nikiliona basi nahisi kama bado Siwa yupo" Alijibu Naomi,Joeli aliangua kicheko kisha akasema. "Hapana ondoa hiyo imani mke wangu,mtu akisha kufa amekufa"

    "Ni kweli ila kwa sasa naona tayali Siwa kafa kiukweli ukweli" Alijibu Naomi,safari hiyo akichezea ndefu ndogo zilizokuwa kwa kwenye kidevu cha Joeli. Joeli alishusha pumzi halafu akaongeza kusema "Lakini gari lenyewe nimeuza kwa bei nafuu ujue?.."

    "Hakuna tabu kwani kuna hasara gani umepata? Nenda kaoge upumzike ili usichelewe kazini" alijibu Naomi. Joeli alinyanyuka akazipiga hatua kuingia bafuni. Naomi nae alifanya hivyo ambapo mara baada wote kumaliza kuoga walianza safari ya kulitafuta lepe la usingizi ambapo kwao haikuwa tabu kulipata yote ikiwa shauri ya uchovu waliokuwa nao. Hivyo ndani ya dakika kadhaa walisinzia,ila ilipotimia saa nane usiku Joeli alizinduka kutoka usingizini baada kuota ndoto ya kutisha. Aliota kwamba anashuhudia mwili wake unapelekwa kuzikwa kaburini ilihali yeye anajiona bado yupo hai,kitendo kilichompelekea kuwapigia kelele wazikaji lakini wazikaji wakawa hawamsikii. Aliogopa sana Joeli,akawa ametoka usingizini huku akihema haraharaka. "Mmh inamaana gani ndoto hii?.." alijiuliza Joeli.



    Alijiuliza Joeli ndoto hiyo inamaana gani,alikosa jibu akaishia kushusha pumzi ndefu huku macho yake yakimtazama Naomi ambaye yeye alikuwa yupo kwenye dimbwi kubwa la usingizi. Joeli alinyanyuka kutoka kitandani akazipiga hatua kuelekea bafuni, alijimwagia maji halafu akarudi kitandani kuendelea na usingi muda huo tayali ilikuwa saa tisa kasoro. Ndani ya dakika sita tu usingizi ukamjia,alilala fo fo fo lakini baadae kidogo alirudia kuzinduka kutoka usingizini. Safari hiyo aliota ndoto ya kutisha zaidi tofauti na ile ya mwanzo,alijiuliza kwa mara nyingine maana ya ndoto hizo lakini hakupata majibu yake. Muda huo huo Naomi alimka,alishngaa kumona Joeli akiwa ameketi kitandani. Naomi akamuuliza Joeli "Mbona umeamka usiku wote huu halafu istoshe unaonekana hauko sawa?" Joeli alishusha pumzi kwanza kisha akajibu "Ni kweli siko sawa mke wangu, yote sababu ya ndoto hizi mbili nilizoota usiku huu.."

    "Ndoto? Unamanisha ndoto ndio zimekufanya uamke ama ukose usingizi?.."Aliuliza Naomi. Joeli akajibu "Ndio, zinatisha sana"

    "Sawa unaweza kunisimbulia japo ndoto moja?.."

    "Inawezekana tu Naomi;Ndoto ya mara ya kwanza nimeota kuwa maiti yangu inakwenda kuzikwa ilihali naishuhudia kwa macho yangu,niliogopa sana haraka nikawafuata wazikaji nikitaka wasiizike maiti yangu waiache kwa sababu bado nipo hai. Lakini wazikaji walionekana kama kutonielewa kile ninacho kisema kwani hakuna hata mmoja aliyenigeukia na kunisikiliza,walizidi kulikaribia kaburi ambalo tayali nilikuwa limeandaliwa kwa ajili ya maiti yangu. Walipolikaribia zaidi kaburi,nilizidi kuogopa nikiamini kuwa endapo kama maiti yangu itafukuwa basi huwenda ukawa ndio mwisho wangu. Hapo ikabidi nipige kelele, ndipo nilipozinduka na kugundua kuwa hiyo ilikuwa ni ndoto." Alisema Joeli wakati huo Naomi alishusha pumzi kwa kasi, akampa pole kwanza Joeli ya kuota ndoto hiyo ya kutisha baada ya pole hiyo alihitaji kufaham na ndoto ya pili aliyoota Joeli.

    "Ndoto ya pili sasa mmmh hatali kweli kweli" Alisema Joeli na kisha akaanza kusimulia. Siku hiyo alichelewa kurudi nyumbani baada kutingwa na shughuli za kiofisi.alirudi nyumbani usiku, wakati akiwa ndani ya gari yake ghafla mbele yake alimuona mwanamama mmoja wa makamo akimpungia mkono haraka haraka. Akili yake Joeli ikamtuma kwamba asimamishe gari huwenda huyo mama akawa anakimbizwa na jopo la wahuni Kwahiyo itafaa kama atampatia msaada,alipo simama akashusha kioo cha gari kisha akamsikiliza yule mama. Mama yule akamwambia Joeli "kaka naomba unisaidie nitakufa mimi kuna watu wananikimbiza wanataka kunifanyia kitendo kibaya nisaidie tafadhali" alisema yule huku akiangua kilio wakati huo anasema maneno hayo punde si punde kwa mbali Joeli aliona tochi zisizopungua nne zikija mahali alipokua amesimama na yule mama. Ndipo mama yule akaongeza kusema"wanakuja kaka wanakuja nisaidie nakuomba" haraka bila kuchelewa Joeli alimfungulia mlango wa gari yule mama akaingia kisha akarudi upande wake akafungua mlango akaingia halafu akaanza safari kutoka mahala hapo. Wakiwa ndani ya gari,Joeli alimuuliza yule mama "Kwani ulikua unatoka wapi usiku huu?.." Yule mama akajibu "Nafanya kazi bar,kwahiyo nilikuwa natoka kazini naelekea nyumbani. Ghafla nikawa nimekumbana na wale vijana"

    "Anhaa Dah! Pole sana. Basi nitakupeleka mpaka nyumbani kwako" Joeli akaongeza kusema. Yule mama akajibu "Sawa nitashuru"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwihiyo kinachotakiwa hapa ni kunielekeza tu,kwamba pita kulia ama pita kushoto" alisema Joeli. Mama yule akacheka kidogo halafu akajibu "Haina shida" kwisha kujibu hivyo,ukimya ulitawala ndani ya gari ya Joeli ila ukimya huo ulikuwa ukivunjwa pindi yule mama alipokuwa akimuelekeza Joeli wapi pakuelekea. Hatimae walifika eneo la Sinza makaburini,wakati huo tayali kiza totoro kilikuwa kimetanda kila mahali huku magari moja moja yakipita kwa kasi ya ajabu. "Kata kushoto" alisikika akisema yule mama. "Huku makaburini? .." Joeli akahoji. "Ndio " alijibu yule mama. Joeli akakata kona kuingia huko alikosema yule mama kisha akasimamisha gari. "Mbona unasimama sasa?.." Yule mama akamuuliza Joeli. Joeli akamgeukia kisha akamjibu "We mama wewe,yani kukutoa kote kule bado tu. Kwanza nahitaji kurudi nyumbani nafikili nyumba unayoishi ni ile pale kwahiyo tembea kwa miguu gari huko hiwezi kufika" alijibu Joeli huku akionekana kufura hasira moyoni mwake. Yule mama aliposikia maneno hayo ya Joeli akarudia kusema "Kwanini isifike? Ukumbuke umeniahidi kunifikisha mpaka nyumbani kwangu.."

    "Hatakama,acha ajinga basi. Kwanza inakuaje mnajenga jirani na makaburi hamuogopi?..nafikili sina muda wa kupoteza, niache niondoke zangu bwana. Yani umekaribishwa sebuleni unataka uingie na chumbani?utakua ujinga huu.." Alisema Joeli kwa hasira kisha akataka kurudi ndani ya gari lakini kabla hajafungua mlango ili aingie ndani mara ghafla yule mama akaanza kuangua kicheko,kicheko ambacho kiliambatana na mvua kubwa huku radi nazo zikiunguruma angani. Joeli alishtuka,akajikuta akiogopa. Punde baada kutokea tukio hilo ilisikika sauti ya yule mama ikisema "Nipelekea mpaka nyumbani kwangu" wakati huyo mama anasema maneno hayo,ile nyumba iliyokuwa ikionekana mbele yao ilipotea na kujikuta wakiona makaburi tu. Muda mchache baadae makaburi hayo yalianza kutikisika, haikuchukua muda Joeli akaona watu wakifufuka kutoka katika makaburi hayo. Aliogopa sana Joeli mtu mzima akijikojolea ilihali wale wafu nao wakionekana kulanda landa huku na kule makaburini hapo. "Nyumba yenyewe ikowapi mama?.." Aliuliza Joeli kwa sauti ya woga,lakini hakujibiwa alipotazama pembeni yake hakumuona yule mama. Haraka sana alirudi ndani ya gari,akawasha kisha akaondoka zake kutoka eneo hilo la makaburi.lakini kipindi yupo ndani ya gari,mara ghafla akaguswa bega. Akapunguza mwendo kisha akawasha taa akageuka nyuma kumtazama mtu aliyemshika bega akamuona yule yule mama,ishtuka Joeli alirudisha macho yake mbele akamuona tena mbele yule mama ambaye yumo ndani ya gari...; Ndoto ya pili ni hiyo mke wangu,hata sielewi zinamaana gani ndoto hizi. Alisema Joeli baada kumaliza kumsimulia Naomi ndoto hizo. "Kiukweli hizo ni ndoto za kutisha mno mmmh.. lakini hizi ndoto tusizipuuzie mume wangu,tajaribu kutafuta mtalam wa kuzitafsiri huwenda zikawa na maana.." alisema Naomi. "Kabisa,wazo zuri sana hilo na nilazima nilifanyie kazi" Joeli alijibu kisha wakalala.

    Kesho yake asubuhi Joeli alikwenda kazini,ila alipofika kazini alijikuta muda mwingi akiutumia kulala kwa maana jana usiku hakupata muda mwingi wa kulala baada kukumbwa na ndoto zile za kutisha zilizomsababishia kutokulala muda mrefu. Hali hiyo iliendelea mwishowe akaona haina haja ya kujibana sana,alitoka ofsini akaelekea mahali ilipo gari yake akaingia na kisha akaanza safari ya kurejea nyumbani kulala. Wakati Joeli anaondoka,upande wa pili ofsini alionekana Magesa akipitia baadhi ya mikataba ya wafanyakazi. Ila ghafla alisitisha zoezi hilo baada simu yake ya mezani kuita. Magesa alipokea,ikasikika sauti ikisema "Bosi kuna mgeni wako"

    "Mruhusu apite" alijibu Magesa kisha akairejesha simu hiyo sehem husika. Punde si punde mlango wa ofisi yake ulifunguliwa,mgeni huyo alifanana na marehem Siwa kila kitu. Magesa alipomuona alishtuka akaogopa sana. Mgeni huyo akamuuliza "mbona unaogopa? " Magesa hakujibu aliishia kumeza mabunda ya mate kila sekunde huku akinyanyuka pole pole kutoka kwenye kiti chake. Mwishowe alinyanyuka na kisha akatimua mbio kutoka humo ofsini mwake. Alipofika mapokezi,alimwambia muhusika wa hapo ambaye alijilikana kwa jina Tecla. "Tecla, ama kweli dunia inamambo. Nadhani uliwahi kusikia kuwa Joeli kafiwa na mkewe" alisema Magesa huku akihema kana kwamba amekimbia umbali mrefu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndio nilisikia" Alijibu Tecla. Magesa akaongeza kusema "Basi bwana ndio huyo uliyeniambia mgeni wangu nikakwambia mruhusu"

    "Mungu wangu..ila sidhani kama atakuwa yeye" alijibu Tecla. Kisha akaongeza kusema "Kama sivyo twende tukamuone vizuri,ondoa woga"

    "Sawa twende" Magesa alikubaliana na Tecla wakazipiga hatua za woga mpaka kwenye ofisi ya yake lakini hawakumkuta yule mwanamke ambaye Magesa alidia kwamba amefanana na marehem Siwa. Alishangaa sana Magesa,akahisi kama ndoto tukio hilo. Lakini wakati hayo yakitokea huko kwa Magesa, upande mwingine alionekana Joeli yupo ndani ya gari akirudi nyumbani.Kabla hajafika mara hafla simu yake ikaita,alipoitazama akaona ni namba mpya ndiyo iliyompigia. Alipokea ikasikika sauti ikisema "Mambo vipi bwana Joeli? Ebwanaee kuna jambo limetokea huku kila mmoja anashangaa..."

    "Jambo gani? Na wewe ni nani?.." Aliuliza Joeli. Jamaa huyo aliyekuwa akiongea kwenye simu alijibu "Huwezi kunijua ila nimeamua kuitafuta namba yako ili nikupatie habari hii,habari yenyewe ni kwamba marehem mkeo tumemuona sokoni akinunua mahitaji kama kawaida" alijibu huyo jamaa. Joeli alishtuka,haraka sana akakanyaga bleki kisha akahoji "unasema?.." Jamaa akarudi kusema

    "Nasema hivi,mkeo yule tuliyemzika miezi kadhaa nyuma. Leo kaonekana sokoni akinunua mahitaji"





    Joeli alikata simu kisha akaliwasha gari lake kwa kasi ya ajabu kuelekea nyumbani kwake, habari hiyo ilionyesha kumshtua sana kiasi kwamba hata usingizi uliokuwa nao ulimpotea. Alipofikia nyumbani alipiga honi mfurulizo ili mlinzi Jerome afungue geti,haraka nae Jerome aliposikia honi hizo alikimbia kwenda kucgungulia ili ajue ni nani aliyepiga honi hizo akaona gari ya bosi wake bila kuchelewa alifungua geti haraka sana uwezekanyo. Ndani ya gari alitelemka Joeli,alipofunga mlango wa gari alimgeukia Jerome na kisha akisema kwa hasira "Jerome,mbona siku hizi unakua mvivu sana kwenye kazi. Umekichoka kibarua?.." "aaah hapana bosi nilikuwa namwagilia maua mara moja,samahani sana" alijibu Jerome. Joeli alitikisa kichwa chake halafu akaongeza kusema "Siku nyingine kuwa shapu we ni kijana bwana" kwisha kusema hivyo alizipiga hatua kuingia ndani. Alipofika sebuleni alimkuta Naomi akiandaa chakula mezani,Naomi alipomuona Joeli alitabasam huku akijongea kumfuata. Alipomkaribia alimkumbatia kisha akamuuliza sababu hasa iliyomfanya siku hiyo arudi nyumbani mapema,Joeli kabla hajamjibu Naomi alishusha pumzi halafu akajibu "Basi tu mke wangu unajua siku huwa hazifanani,kama unavyofaham usiku as jana mimi sijalala sababu ya zile ndoto nilizoota. Kwahiyo imenipelekea kushindwa kufanya kazi,muda wote nalala . Ndio maana nimeona bora nije kupumzika nyumbani" alisema Joeli. Naomi alijitoa kwenye imaya y Joeli,akamshika mkono moja kwa moja wakaingia chumbani ambapo huko Joeli alipoliona kitanda slijitupa chali huku akiambatanisha na kushusha pumzi ndefu ilihali akili yake ikifikilie simu ile aliyopigiwa na kupewa taarifa ambayo iliushtua moyo wake. Aliwaza mengi sana Joeli lakini hakutaka habari hiyo imfikie Naomi, aliiweka moyoni kama siri yake mwenyewe pasipo kumjumuisha Naomi.

    Baada kuwaza mengi mwishowe usingizi ulimpitia, alilala fo fo fo Joeli akaamka jioni wakati huo jua tayali limekwisha zama. Jambo la kwanza alichukua simu yake akaangalia kama kutakuwa na mtu amempigia,alikuta Missed calls nne. Alipofungua aliona Magesa kampigia mara moja,ila Missed call zilizobaki ni zenye namba aliyokuwa akiitumia marehem Siwa. Hapo Joeli alishtuka akaitupa simu kitandani huku akihema haraka haraka,moyoni akijiuliza "Hii mbona shida sasa,Siwa kanipigia? Ama Naomi alinipigia kupitia namba yake aliyokuwa akitumia enzi ya uhai wake?Na kama kanipigia iweje anipigie wakati anajua nipo ndani?.." alijiuliza Joeli bila kupata jawabu la swali hilo alilojiuliza,ndipo alipoamua kumuita Naomi. Naomi alitii wito wa mumewe. Joeli akamuuliza Naomi "Hivi mke wangu line ya marehem Siwa unayo?.." Naomi alitaharuki kusikia swali la Joeli,hali iliyopelekea badala kujibu akajikuta nae akihoji "ili iweje sasa na kwa faida gani? "

    "Nijibu basi mbona unakua hivyo?.."aliongeza kusema Joeli. Naomi akajibu "Sina kwani ulitaka uifanyie nini?.." CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Basi kama huna nikajua unayo siunajua ile kampeni yetu" alisema Joeli.

    "Anhaa ile ya kuhakikisha kwamba kila alichokuwa anatumia Siwa ni kukipoteza?.."

    "Haswaa" Joeli alijibu ingawa kwa sauti ya kusuasua. Naomi aliposikia jibu hilo la aliangua kicheko kisha akaongeza kusema "Hapo nimekuelewa ila katu hizi nguo zinazo nifaa sitoweza kuzipoteza, kwa sababu zimenioendeza sana" Alipokwisha kusema hivyo alimtaka Joeli akaoge ili wale chakula cha jioni. Joeli alielekea bafuni kuoga alipotoka alikula chakula ila hakula kama anavyokula siku zote, siku hiyo alikuwa tofauti sana kwani alikula kidogo kisha akaacha. Naomi alishangaa sana, akamuuliza nini tatizo? Joeli aliishia kusema "Siko sawa mke wangu,ndoto zile bado zinazunguka kichwani mwangu" alisema hivyo Joeli ila siri kuu akiwa nayo moyoni kwani alichomwambiw Naomi na kile kinachomfanya akose amani ni vitu viwili kabisa. "Mmh pole sana mume wangu,lakini hizo ni ndoto tu wala zisikufanye raha sawa? Jaribu kupiga moyo konde acha kufikilia kitu ulichokiota kwenye ndoto,Kula basi hata kidogo ili mkeo nifurahi" alisema Naomi kwa sauti nyembamba nyororo nzuri kuliko hata jina lake.

    "Daah we acha tu,naomba nikapumzike basi nitakula hata baadae" alijibu Joeli. "Sawa,ila sipendi uwe hivyo kwani unapokuwa hivyo roho yangu inaniuma sana" aliongeza kusema Naomi. Joeli alinyanyuka kutoka kwenye sofa huku akisema "Usijali mke wangu nitakuwa sawa tu" Na kwisha kusema hivyo alizipiga hatua kuelekea chumbani kulala ilihali kichwani akiwa na mawazo chunguzima.

    Masaa yalisogea Joeli akiwa bado yupo kwenye dimbwi la mawazo,wakati huo Naomi alikuwa ameshamaliza kazi ya kuweka vyombo sawa. Alipomaliza alienda kuoga kisha akaelekea moja kwa moja chumbani kulala ambapo huko alimkuta Joeli bado yupo tongo macho. Aliketi kitandani akamgusa kisha akasema "Joeli amka kwanza,kuna jambo nataka nikuulize " Alisema Naomi. Joeli kwa kuwa hakutaka kumuonyesha Naomi kile kinacho msumbua sana moyoni mwake, hivyo aliamka akamsikiliza. Hapo Naomi akasema "Joeli mimi ni mkeo,kwa hiyo naomba uniambie ukweli ni nini hasa kinacho kusibu.." Joeli aliposikia maneno hayo ya Naomi aliachia tabasam halafu akajibu "Hayo yalisha kwisha bwana ila kwa sasa nafikilia kumleta yaya atakaye kusaidia kazi mbali mbali za hapa nyumbani " Alidanga Joeli. Naomi alikaa kimya kidogo akashusha pumzi kisha akajibu "Mmh hapana sijafikilia jambo hilo kiukweli,mbona sijaona kazi za kunishinda ? Kwahiyo acha usiumize kichwa juu ya jambo hilo"

    "Lakini ujue kuna dhalula mke wangu, kwa hali hiyo uliyonayo hufai kukaa peke yako. Lazima awepo mtu wa kukuangalia" aliongeza kusema Joeli,ila Naomi alikataa katu katu hali iliyopelekea kuzua ubishi ingawa mwishowe Joeli alikubaliana na mawazo ya Naomi. Baada kufikia muafaka,Naomi alisema "leo nitaka" Joeli akauliza "Unataka nini? " Hapo Naomi hakusema kitu bali alimsogelea Joeli na kisha akaanza kumpapasa, kitendo kilichomfanya Joeli kujua ni nini anachotaka Naomi kwa wakati huo. "Mmh Naomi na hali hii?.." Alihoji Joeli akishangaa Naomi kutaka tendo hali ya kuwa ni mjamzito,lakini Naomi bado aliweka ugumu wa kumjibu Joeli. Aliendelea kufanya alichotaka kufanya, mpaka Joeli akashawishika akafanya kile alichokita Naomi.

    Lakini wakati wawili hao walipokuwa kwenye mambo ya kiutuuzima,mara ghafla simu ya Joeli ikaita. Naomi alikerwa na jambo hilo,ilihali Joeli nae akionekana kusitisha alichokua akikikfanya ili aifuate simu. Naomi alikataa ambapo simu iliendelea kuita mpaka ikakata, na punde si punde ilisikika sauti ya ringtone ya ujumbe mfupi. Baada kumalizika tendo Joeli aliifuata simu yake ili atazame ni nani aliyempigia,wakati huo Naomi akihoji "Inamaana watu wako hawajui kama usiku ni muda wa kupumzika?" Joeli hakujibu chochote licha ya kusikia swali hilo la mkewe kwa sababu mawazo yake yote yalikuwa kwenye simu,akijiuliza ni nani aliyempigia huku fikra zikihisi huwenda ikawa namba ile ile aliyokuwa akiitumia marehem Siwa. Alipouchukua simu yake alitazama kwanza Missed call kabla ya ujumbe,akakuta ni Magesa ndiye aliyekuwa amepiga. Hapo Joeli alishusha pumzi kisha akafungua ujumbe mfupi akakutana na ujumbe aliotuma Magesa ukieleza "Joeli habari yako. Hivi unataarifa kama marehem shemeji CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/yangu yani mkeo wewe leo kanitokea ofsini? Alikuulizia ujue sasa sijui hii imeakaaje kwa upande wako" Ulieleza huo ujumbe ambao ulimshtua kwa mara nyingine Joeli, akakumbuka na maneno yale aliyoambiwa na jamaa mmoja ambaye hakumfaham jina"Nasema hivi,mkeo yule tuliyemzika miezi kadhaa nyuma. Leo kaonekana sokoni akinunua mahitaji" Joeli aliyakumbuka hayo maneno. Ghafla mapigo ya moyo wake yalienda mbio,kijasho kikaanza kumtoka akamtazama Naomi halafu akarudisha uso wake kwenye simu kuutazama ujumbe huo. Alijikuta akichoka kabisa huku akijilaza pole pole kitandani hali ya kuwa upande wa Naomi alikuwa ameshajifunika mpaka shuka, kwahiyo Joeli aliungana nae huku akili yake ikaanza upya kufikilia taarifa hiyo kumuhusu marehem Siwa.Kiukweli lilikua jambo la maajabu sana lililo muacha mdomo wazi Joeli,alijikuta akishindwa kuamua la kufanya,mambo hayo aliyosikia yalimuweka roho juu huku akijiuliza iweje Siwa kamzika miezi kadhaa nyuma halafu leo hii asikie kwamba kaonekana sokoni akinunua mahitaji? Je, hajafa kama ilivyodhihilisha? Na hayo mahitaji aliyokuwa akinunua aliyapeleka wapi? Vile vile ni wapi alipo kama kweli Siwa hajafa? Maswali hayo alijiuliza Joeli ndani ya kichwa chake wakati huo akiwa kitandani kajilaza ambapo mwishowe alishusha pumzi huku moyo wake ukihisi kujawa na hofu,kitendo ambacho kilimfanya kusikia joto mwilini mwake lililompelekea kuamka kutoka kitandani moja kwa moja akazipiga hatua kuelekea bafuni ili akajimwagie maji kisha aanze safari ya kusaka lepe la usingizi usiku huo ambao tayali ulikuwa usiku wapata saa sita na robo,lakini kabla hajafika bafuni alishtuka kuona nyao za damu zikiambaa kuelekea bafuni. Na punde si punde alisikia watu wawili wakiongea pia wakicheka huku kwa mbali ikisikika harufu ya ubani.





    Joeli alishtuka baada kuziona hizo nyayo za damu ambazo ziliambaa kuelekea bafuni,ilihali bafuni ikisikika sauti za watu wakiongea huku wakicheka wakati huo marashi ya ubani nayo yakiwa yameipamba nyumba hiyo. "Mungu wangu" alijikuta akijisema hivyo Joeli ndani ya moyo wake huku akizikodolea macho nyayo zile za damu,ila mara ghafla zilitoweka mbele yake na punde si punde akasikia vishindo vya mtu anayetembea nyuma yake. Haraka sana Joeli akageuka,safari hiyo aliona zile nyayo za damu alizoziona mbele zipo nyuma yake huku nyayo moja baada ya nyingine zikiongezeka kuelekea chumbani kwake. Alishangaa sana Joeli,akaogopa akataka kurudi chumbani lakini aliogopa. Upande wa bafuni,sauti zilisikika zikiongea rugha isiyoeleweka. Jambo ambalo lilizidi kumchanganya Joeli ingawa alipiga moyo konde na kisha kuusogelea mlango wa bafuni halafu akafungua pole pole ili aangalie ndani kuna watu gani. Alipofungua mlango hakuwaona watu wale aliokuwa akiwasikia wakiongea,ilihali wakati huo huo ile harufu ya ubani ilitoweka. Hapo Joeli akajikaza kisabuni akafungulia maji kisha akaanza kuoga,alipomaliza aliyafunga hayo maji halafu akafungua mlango ili arudi chumbani kulala. "Daah hii inamaana gani? Mbona mauzauza sasa!" Alisema Joeli huku akijifuta maji na taulo lake wakati huo tayali ameshaufungua mlango wa bafuni ambapo haikuchukua muda mrefu akazipiga hatua za wasi wasi kurudi chumbani huku nyayo zile za damu zikiwa zimeshatoweka. Alipo ukaribia mlango wa chumbani alisikia tena watu wale wakiongea bafuni,tena safari hiyo ilisikika na sauti ya maji yakichuruzika. Joeli alishtuka kwa mara nyingine, katu hakutaka kulala bila kujua ni watu gani waliomo ndani ya nyumba yake,hivyo alirudi bafuni chap chap ambapo alipofika alisukuma mlango wa bafu kwa nguvu akiamini kwamba huwenda akawabahatisha watu hao. Lakini bado mambo yakawa ni yale yale,hakukuta watu lakini pia sauti ile aliyokuwa akiisikia ilipotea ila alipotoka mle bafuni aliona nyayo za mtu aliyekanyaga miguu ikiwa imelowa maji. Hicho kitendo kikaizidi kumpagawisha Joeli,na hivyo aliziruka nyayo zile za maji haraka haraka kurudi chumbani kwake huku moyoni akiamini kwamba tayali maji yameshazidi unga. Ila kabla hajaukaribia mlango wa chumba,alikutana na Naomi. Joeli akamuuliza "Wapi usiku huu?.." Naomi akajibu "Nimebanwa na haja,lakini pia joto mume wangu ngoja nikajimwagie maji " alijibu Naomi huku akizipiga hatua kuelekea bafuni ilihali muda huo Joeli akiishia kumsindikiza na macho huku moyoni akijiuliza "Inamaana yeye hizo nyayo hazioni? Ama anajua ni nyayo zangu? Na kama anajua ni nyayo zangu mbona zipo hadi mbele yangu wakati sijipakanyaga?.." Alijiuliza Joeli wakati huo akiendelea kumtazama Naomi hadi pale alipoingia bafuni. Baada ya Naomi kuingia bafuni Joeli alirudisha macho yake kutazama kule anapoelekea alizipiga hatua kuingia chumbani ambapo huko alijikuta akipigwa na bumbu wazi baada kumuona Naomi akiwa amelala kitandani ilihali muda mchache uliopita alimuona NaomiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ akielekea bafuni akidai kwamba anakwenda kujisaidia lakini pia kujimwagia maji. Kwa hakika joto lilimpanda Joeli, aliogopa sana alirudi nyuma huku akihema kwa kasi wakati huo asiamini kile kinachoendelea usiku huo. "Kwanini lakini?.." Alijiuliza Joeli. Lakini kabla hajapata jibu la swali alilojiuliza ghafla kitasa cha mlango wa chumbani kilicheza ishara kwamba kunamtu anataka kuufungua mlango. Joeli alishusha pumzi kisha akatazama mlangoni ili aone ni nani anayetaka kuufungua mlango huku moyoni akiashum kwamba itakuwa ni yule Naomi aliyemuona akielekea bafuni, lakini cha ajabu mlango ulipofunguka hakuona mtu. Ila licha ya Joeli kutomuona mtu aliyefungua mlango,bado alikodoa macho kutazama kule mlangoni. Alitazama kwa muda wa dakika kadhaa kisha akajikaza kiume akaenda kuchungulia,alipochungulia nje ya chumba chake bado hakumuona mtu yoyote yule. Aliendelea kuchungulia na punde si punde aliona kitambaa cheupe sakafuni,kitambaa hicho kilionekana kutapakaa damu kwa kiasi kidogo. Joeli alistaajabu sana,akajiuliza "Kile sio kitambaa kweli? Na sio kitambaa cha kawaida itakuwa sanda ile sio bure" aliongeza kusema Joeli baada kujiuliza kuhusu kile kitambaa alichokiona. Na wakati Joeli anaendelea kukishangaa kile kitambaa cheupe,mara ghafla yule Naomi aliyeelekea bafuni kuoga alitokea akachuchumaa kukichukua kitambaa kile cheupe kisha akazipiga hatua kuja mahali aliposimama Joeli. Joeli aliogopa sana akarejea chumbani ambapo huko nako alionekana Naomi mwingine akiwa amelala kuachilia Naomi yule aliyekuwa akimfuata Joeli,hatimae Naomi yule aliingia chumbani. Sasa wakawa wakina Naomi wawili,mmoja akiwa amesimama ilihali mwingine akiwa amelala. Joeli alimeza mate mfurulizo yote ikiwa shauri ya woga wakati huo akishindwa kueleww yupi Naomi wa kweli na yupi Naomi wa uongo. Kitendo hicho kilimfanya kaonekana kana kwamba kuchanganyikiwa,hali iliyompelekea kuanguka chini na kisha kupoteza faham.

    Alizinduka kesho yake alfajiri,na hata hivyo Naomi ndiye aliyemuamsha. Joeli ilipoamka alipika kelele,kelele ambazo zilimshanga Naomi. Akamuuliza "Joeli kulikoni mume wangu? Na mbona umelala chini kwani kitanda hujakiona?.." aliuliza Naomi wakati huo Joeli akinyanyuka kutoka chini alipoangukia baada kupoteza faham. Na alipo simama alijisogeza kitandani akakaa huku akiwa amejiinamia hali yakuwa kichwa nacho kikimgonga,lakini dakika nne mbele kilipoa ambapo kumbumbu zilimjia vizuri. Muda huo Naomi alikuwa sebuleni akiandaa chai,punde akaacha zoezi hilo akazipiga hatua kuelekea chumbani kumuona mumewe. Alipofika aliketi kitandani kisha akamgusa bega Joeli halafu akasema "Joeli mume wangu" Joeli aliposikia sauti ya Naomi alitoka kwenye dimbwi la mawazo,akamgeukia Naomi kumsikiliza. Ghafla akashtuka baada kukumbuka tukio lililomtokea jana,lakini alipiga moyo konde kumsikiliza Naomi anasema nini. Naomi alishusha pumzi kisha akahoji "vipi Joeli mbona leo upo hivi. Je, kuna tatizo mume wangu?.." aliuliza Naomi. Joeli akajibu "Hakuna tatizo mke wangu,usiwe na wasi wasi. Saa ngapi muda?.."

    "Sahizi saa Kumi na mbili kasoro,jiandae nenda kaoge uje unywe chai ili uwahi kazini mume wangu" alisema Naomi kwa sauti ya upole iliyojaa mahaba ndani yake. Joeli alisimama akaelekea bafuni kuoga kichwani chini huku akiwa na mawazo chungunzima,safari hiyo bafuni hali ilikua shwari hapakuwepo na mauzauza yoyote. Joeli alitumia dakika chache kumaliza kuoga,alikwenda mezani kunywa chai kisha akajiandaa na safari ya kwenda kazini.

    Alipofika kazini alipaki gari yake sehem maalum halafu akashuka na kuzipiga hatua kuingia ndani ghorofa ilipo ofisi yake,lakini kabla hajaingia ndani alisikia sauti ikimuita "Joeli Joeli" alikuwa ni Magesa ndiye aliyemuita. Joeli aliposikia Magesa akimuita alisimama kisha akageuka nyuma,ambapo alimuona Magesa wakati huo Magesa nae aliufunga mlango wa gari yake akajiweka sawa kola ya shati yake kisha akajongea kumfuata Joeli ambaye alikuwa amesimama akimsubili. "Joeli mambo vipi?.." Magesa alimsalimu Joeli. Joeli akajibu "safi kwema?.."

    "Daah kwema basi tuongozane swahiba wangu" aliongeza kusema Magesa kisha wawili hao wakapandisha ngazi kuingia mahali zilipo ofisi zao. Kabla hawajaachana kila mmoja kuingia kwenye ofisi yake,walizungumza mambo kadhaa japo kwa ufupi. Mambo hayo yalihusu mwenendo wa kampuni yao,lakini baadae kidogo waligusia na tukio lilitokea jana. Ambapo Mgesa alisema "Joeli achilia mbali utani tulio nao,huu sio utani tena. Kwa macho yangu kabisa nilimshuhudia marehem mkeo akinitokea ofisin kwangu,na cha kushangaza bwana alikuulizia wewe" Aliongea Magesa akimwambia Joeli. Joeli alishusha pumzi halafu akajibu "Doh! Ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya filauni. Sio hilo tu rafiki yangu Magesa,kuna mengine mengi yamezuka siku ya jana mpaka usiku. Yani hapa unaponiona Joeli mimi sijalala" CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Khaah! Kwanini sasa? Ama na wewe alikutokea?.." Alihoji Magesa kwa mshangao wa hali ya juu. Joeli alikaa kimya kidogo na kisha akajibu "we acha tu. Nitakwambia baadae" Joeli kwisha kumjibu hivyo Magesa,kila mmoja aliingia ofisini kwake wakati huo upande wa pili alionekana Naomi akiwa sebuleni ametulia akisoma kitabu cha hadithi kitabu hicho alipenda kukisoma marehem Siwa enzi ya uhai wake,kwahiyo muda huo Naomi nae aliona atulie huku akikipitia kitabu hicho kilichokuwa kimebeba hadithi nzuri ya kusisimua. Lakini wakati Naomi enanogewa na hadithi hiyo ya kusisimua ambayo alianza kuipenda kadili alivyoisoma, mara ghafla alisikia harufu ya ubani. Naomi alishtuka akajiuliza "Harufu hii inatoka wapi?.." Alijiuliza Naomi,na kabla hajapata jibu la swali alilojiuliza,punde si punde akaja Joeli akioneka kuwa na haraka ya kuwahi kazini. Naomi slishtuka alipigwa na butwaa, akaona kama ni ndoto anayoiota. Akakumbuka kuwa Joeli tayali alishakwenda kazi masaa kadhaa yaliyopita,sasa iweje tena muda huo amuone akijiandaa kuelelea kazini?



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog