Search This Blog

SANDA YA SIWA - 4

 







    Simulizi : Sanda Ya Siwa

    Sehemu Ya Nne (4)



    Joeli akiwa ofisini kwake punde si punde mlango wa ofisi yake ulifunguliwa,akaingia mfanyakazi mwenzake ambaye muda huo alimletea chai. Mfanyakazi huyo aliitwa Maklina,ambapo Maki alishangaa kumuona Joeli akiwa amejiinamia kwenye meza yake iliyojaa mazaga mbali mbali badala ya kufanya kazi. Lakini Maki hakutaka kujaji sana zaidi alimsogelea akamuamsha,ambapo Joeli aliamka kwa kukurupuka kana kwamba kuna ndoto ya kutisha alikuwa akiiota. "Samahani bosi,ammh chai tayali karibu unywe " alisema Maklina. Joeli alishusha pumzi ndefu halafu akajibu "Doh Ahsante sana Maklina"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa bosi,lakini bosi mbona kama unaonekana haupo sawa. Nini tatizo hasa kwa sababu sijawahi kukuona unalala muda huu" aliuliza Maklina. Joeli hakujibu chochote kwani safari hiyo alikuwa aikiipeleka mdomo wake kwenye kikombe cha chai,aliivuta chai kidogo halafu akasema "Maklina nina mengi yananisibu ila huu sio wakati wa kukusimulia, kafanye kazi. Siku yoyote nitakayo kuwa na nafasi nitakueleza tu wala usijali"

    "Sawa bosi" alijibu Maklina kisha akaondoka zake. Baada Maklina kuondoka ndani ya ofisi ya Joeli,punde si punde simu ikaita. Joeli aliitazama akaona ni Naomi ndiye aliyempigia,haraka sana akapokea. "Hallo Joeli.." alisema Naomi. Joeli akajibu "Naam mke wangu,nakusikiliza" wakati Joeli akisikilizia Naomi anakipi cha kumwambia, ajabu Naomi alikata simu. Joeli alishangaa sana,akawa haelewi alichomanisha Naomi. Lakini akili ya haraka ikamtuma kwamba huwenda labda salio limemuishia,hivyo bila kupoteza muda alimpigia ila simu ya Naomi iliita bila kupokelewa. Hakuishia hapo, alirudia tena kumpigia lakini bado simu haikupokelewa. Joeli alishtushwa na kitendo hicho,alijiuliza maswali mengi kichwani mwake maswali ambayo aliyakosa majibu yake. Nguvu ya kuendelea kufanya kazi sasa ilimtoweka, akajihisi kuchoka mwili mpaka akili. Akajiuliza "mbona kapiga simu na kisha kukata?na kwanini nikimpigia hapokei? Je, kakutwa na tatizo ama?" Alijiuliza Joeli ambapo baada kujiuliza hivyo alishusha pumzi ndefu huku akipiga meza kofi kwa hasira. Wakati huo huo simu ya mezani ikaita,akiwa amjawa na hasira alipokea. Ikasikika sauti ikisema "Bosi kuna mgeni wako" Joeli akajibu "Mruhusu" Muda mchache baadae mlango wa ofisi yake ulifunguliwa akaingia kijana wa makamo,kijana huyo alimsalimu Joeli kisha akajongea mahali kilipo kiti akakaa. Joeli akamgeukia halafu akamuuliza "Ehe nikusaidie nini kijana?.." yule kijana alijiweka sawa kwenye kiti halafu akajibu "samahani kaka mimi naitwa Tito,nimhitim wa chuo mwaka cha..." Kabla kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina Tito hajamaliza kusema lengo lake lililomleta hapo ofisi,Joeli alimkazia macho kisha akamwambia "Kijana embu simama" Tito akajibu "Mbona hivyo bro? Sijamaliza kuelezea, tayali umenibadilikia. Nisikilize kaka nisikilize tafadhali" alijibu Tito huku akiwa amepiga magoti. Lakini Joeli hakuonyesha nia ya kumsikiliza Tito,alizidi kumzia macho na kumtaka ondoke ndani ya ofisi yake. Ajabu Tito badala ya kuondoka alirudi kukaa kwenye kiti,kitendo hicho kilimkera sana Joeli. Alinyanyuka kutoka kwenye kiti chake kisha akasema kwa sauti kali "Bwana Tito unaelewa kiswahili vizuri lakini? Nimekwambia ondoka ndani ya ofisi yangu kakaaa. Zipo kampuni kibao za kuomba kazi sio hapa tu. Au mpaka nikufanyie kitendo kibaya ndiyo uondoke.." Alisema Joeli lakini kufumba na kufumbua Tito alibadilika akawa Siwa kisha kicheko kilisikika. Joeli alishtuka, akarudi nyuma huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio. Muda huo huo Siwa alisema halafu akasema "Joeli mbona unashtuka sasa? Je, hutaki kumpa kazi Tito? Aah Joeli punguza choyo bwana. Hahahaa! HAhaha! " alisema Siwa kisha akamalizia kwa kicheko. Bado Joeli alionyesha kupigwa na bumbuwazi,ni baada kumuona marehem mkewe kwa macho yake kwani jana yake aliambiwa kwa maneno lakini sasa anamshuhudia. "Mungu wangu,kweni Siwa hajafa?" Alijisema Joeli ndani ya moyo wake wakati huo bado Siwa akiendelea kucheka. Punde si punde Joeli akajisogeza mahali ulipo mlango,alipopata upenyo alifungua kisha akatimua mbio mpaka kwenye ofisi ya Magesa. Alipofika kule alimkuta Magesa akiwa yupo kwenye harakati za kuhifadhi vizuri mafaili ya kampeni, hivyo alishtuka baada kuona mlango wa ofisi yake umefunguliwa kwa pupa. Alipogeuka nyuma alimuona CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Joeli,kabla hajamuiliza kinacho msibu. Joeli alisema "Magesa.. Magesa Magesa,nimemuona kwa macho yangu hakya mungu kaja ofisini kwangu" Magesa aliposikia maneno hayo ya Joeli aliyokuwa akiyaongea istoshe kwa tabu, aliacha mara moja zoezi alilokuwa akilifanya,kisha akamsogelea Joeli akamuuliza "umemuona nani?.." Joeli kabla hajamjibu Magesa, alishusha pumzi kwa nguvu akazama mfukoni akachukua leso yake kisha akajifuta jasho halafu akasema "Magesa ndugu yangu mimi nimekwisha. Kwa macho yangu haya mawili, nimemshuhudia Siwa. Ila alikuja kwa style ya mtu mwingine tena kijana mdogo tu akiiihitaji kazi. Ujue mimi nimefurugwa sana,nina mambo mengi sana kichwani yanichangaya. Shemeji yako mjamzito,mara hili mara lile Kwahiyo kichwa changu kizito kama nini yani. Sasa nikaona huyo kijana anayetaka kazi kama anazidi kunichanganya hivi,ikabidi nimfukuze tu ili nipumzishe akili yangu. He! Kufumba na kufumbua yule kijana akageuka Siwa. Daah! Yani sijui nitajificha wapi mimi sielewi Magesa,naomba unisaidie rafiki yangu" alisema Joeli. "Pole sana bwana Joeli,lakini nafikili kifo cha mkeo kitakuwa cha kutatanisha sana. Ila ondoa shaka nipo tayali kukusaidia, kuna mtalam mmoja hivi yuko vizuri sana. Nafikili anaweza kukupatia msaada" Magesa akimwambia Joeli. Joeli akajibu "Magesa embu twende muda huu bwaa,tusipoteze muda"

    "Sawa subili niweke sawa baadhi vitu hapa kisha twende huko" aliongeza kusema Magesa.

    Baada ya dakika ishirini kila kitu kilikaa sawa,Joeli na Magesa walionekana wakitoka ndani ya ghorofa yenye ofisi zao wakazipiga hatua mpaka kwenye magari yao. Walifika kwa mganga wa kienyeji,mganga huyo alimueleza Joeli shida ikiyomleta kabla hata Joeli hajaanza kumuelezea. Kielelezo hicho kilimfanya Joeli kumuamini mganga huyo huku akiamini zaidi kwamba matatizo hayo yansyozuka yanaweza kutoweka.

    Kwingineko,Naomi alizinduka baada kupoteza faham. Hali hiyo ilimtokea pindi alipomuona Joeli anatoka chumbani akiwa na haraka ya kuwahi kazini,hali ya kuwa Joeli ameshakwenda kazini masaa kadhaa nyuma. Jambo hilo lilimshangaza sana Naomi,na ndio maana akaamua kumpigia simu Joeli,ajabu Joeli yule aliyekwenda kazini masaa kadhaa nyuma alipokea simu wakati huo Joeli huyu ambaye yupo nyumbani alionekana akichomekea vizuri shati yake. Kitendo hicho kilimfanya Naomi kuanguka na kupoteza faham,na ndio maana pindi Joeli alipompiga simu ikawa inaita bila kupokelewa. Ila mara baada kuzinduka,alitazama huku na kule,ghafla macho yake yakagonga juu kwenye meza akaona karatasi huku maandishi makubwa yakiwa yameandikwa "Mkataba"

    "Mungu wangu,mkataba? Mkata gani sasa?.." Alijiuliza Naomi.





    "Kijana umefika hapa kwa mzee Zamwela,mimi huwa sishindwi na kitu. Nimesaidia watu wengi sana ndani ya nchi hii na nje pia,Kwahiyo nakuomba kuwa mtulivu tatizo lako limekwisha.AHahahahaha hahahah!" Alisema mganga huyo aliyetimbulisha kwa jina Zamwela,mganga mwenye asili ya mtu wa kigoma. Kwisha kusema hayo aliimba kidogo halafu akaongeza kusema"Kijana,wewe siunaitwa Joeli?." Joeli akajibu "Ndio jina langu wala hujakosea "

    "Basi ondoa shaka Joeli" Aliongeza kusema mganga Zamwela. Kisha akachukua kibuyu kidogo akamkabidhi Joeli,Joeli alipokea kibuyu hicho akakishika kwa mikono miwili. Baada ya Joeli kukipokea hicho kibuyu,ndipo Zamwela akamwambia aongee hutaji lake kipi akifanye ili mauza uza yanayomtokea yatoweke. Akiwa na hofu Joeli aliongea kwa sauti kuu, "Nataka marehem mke wangu asinitokee popote pale, iwe nyumbani ama ofisini. Nisimuone wala yasinitokee mauza uza yoyote ama kuota ndoto za kutisha" Alisema Joeli alipo hakikisha amemaliza matakwa yake ilimrejeshea Zamwela kibuyu chake. Mganga Zamwela alikipokea kibuyu hicho,akaangua kicheko huku akiinyunyuzia dawa ilihali muda huo akaanza kuimba nyimbo zake za jadi. Alipomaliza zoezi hilo alimtazama Joeli kisha akamwambia "Sasa kila kitu kinakwenda kuwa sawa,mizimu imekubali kukusaidia. Leo nakupa dawa hii ikusaidie usiku wa leo usikumbwe na mauzauza yoyote,lakini dawa kamili ya kuyapoteza mauza uza hayo itabidi uje uchukue kesho. Ukija njoo na mbuzi wa kafara,vile vile dawa hii niliyokupa naomba uzingatie kile nitakacho kwambia. Itie kidogo kwenye maji ya kuoga, nyingine inyunyuze kwenye kisingiti cha mlango wa chumbani kwako,na bafunia pia. Itakayo bakia korogea kwenye chai kisha kunywa" alisema Zamwela. Akambidhi Joeli dawa hiyo,Joeli alipokea. Zamwela akaongeza kusema "Sawa mnaweza kwenda ila toa saka yako kwanza " Joeli akazama mfukoni akachomoa kiasi cha pesa shilingi elfu ishirini akatupia kwenye pembe la ng'ombe ambalo ni mahususi kwa kutolea sadaka. Baada ya hapo waliondoka zao. Waakiwa njiani wakizipiga hatua kuzifuata gari zao,Magesa alisikika akisema "Yani Joeli kwa mganga yule,he! Mbona matatizo yako yote yamekwisha?.." CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh kweli lakini Magesa?.." Alihoji Joeli. Magesa akacheka kidogo kisha akajibu. "Nakwambia hivi yule mganga ni Moto wa kuotea mbali,kuna jamaa yangu fulani hivi kasoma mpaka ikifikia hatua ananuka makaratasi. Vyeti vyake vikosawa kila idara,lakini kila alipokwenda kutafuta kazi. Aliambiwa vyeti havijamilika wakati yeye aliona viko sawa. Nikamwambia ndugu yangu hapa mjini,kuna michezo inafanyika. Jaribu kutembelea kwa mtalam ili akuangalizie kilichojificha nyuma ya panzia maana sio bure kutakuwa na kitu,jamaa akaja kwa huyu mtalam. Mtalam alivyoangalia kwenye mambo yake akakuta shangazi mtu ndiye aliyemfanyia huo mchezo ili jamaa asipate kazi. Lakini mwisho wa siku huyu huyu mtalam akamaliza huo mchezo,mpaka sasa jamaa yupo kitengo cha juu kazini kwake. Kwahiyo ondoa shaka Joeli kila kitu kitakaa sawa cha muhimu kesho njoo na huyo mbuzi " alisema Magesa. Muda huo tayali walikuwa wamefika kwenye gari zao. Kila mmoja alipanda gari yake kisha wakaanza safari ya kurudi nyumbani.

    Upande wa pili Naomi bado alionekana kuchachawa,aliyatazama makaratasi yale yaliyoandikwa MKATABA. Alijikuta ikihema haraka haraka huku kijasho kikimtoka. Aliogopa sana,hima alitoka mbio ndani akakimbia nje. Mlinzi Jerome alipomuona Naomi akitoka ndani mbio alisimama akamtazama,wakati huo huo Naomi alifika mahali hapo alipo simama Jerome ambapo alionekana kana kwamba kuna kitu anakiogopa. Jerome alimlaki kisha akamuuliza "Bosi kulikoni mbona mbio mbio?.." Naomi huku akihema kwa kasi alijibu "Jerome nakufa mimi,Jerome nakufa mimi nisaidie" Jerome alimshangaa Naomi. Akarudia kumuuliza "Nikusaidie nini bosi? Na kuna nini ndani?" Kabla Naomi hajaeleza chchote mara ghafla honi ililia nje ya geti. Jerome alijing'atua kwa Naomi kisha akalisogelea geti akafungua. Ni Joeli,ndiye alikuwa amerejea kutoka katika mizunguko yake. Aliisogeza gari yake eneo maalum kisha akatelemka. Alipoufunga mlango wa gari alizipiga hatua kuingia ndani,lakini kabla hajaingia ndani alishangaa kumuona Naomi nje huku uso wake ukionyesha kubena taharuki fulani. Wakati huo Naomi alipomuona Joeli alimkimbilia,alipomfikia alisema "Joeli mpenzi wangu sioni sababu ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hii,nakuomba fanya juu chizi tuhame hapa" Alisema Naomi, Joeli akajua tayali mauza uza yaliyomuandama usiku wa jana sasa yamemtokea na mkewe. Lakini licha ya kuamini jambo hilo,ila hakutaka aendane na mawazo ya Naomi. Hivyo alimtuliza kwa kumwambia "Ngoja basi mke wangu tuliza presha mumeo ndio kwanza nimefika hata ndani bado sijanyagia,twende kwanza ndani kisha hayo mengine tutazungumza. Sawa mamaa" Alisema Joeli,Naomi akashusha pumzi kisha akaambatana na mumewe kuingia ndani. Na kabla wajaingia ndani Joeli aligeuka nyuma akamwita Jerome. Jerome akatii wito haraka sana,Joeli akamwambia "Jerome mambo vipi? "

    "Mambo powa bosi" Alijibu Jerome huku akionyesha haibu fulani machoni mwake. Joeli akaongeza kusema "Uko powa kabisa?..haya kama uko powa basi ni jambo la heri. Nimekuita ili nikwambie kwamba gari yangu tayali imechakaa,Kwahiyo ipige pige maji basi"

    "Anhaa kuhusu hilo wala usijali bosi wangu,yani nitaioosha kiasi kwamba ukija kuitazama ujione sura yako" Alijibu Jerome kisha akafatia na kicheko ambacho kilimfanya Joeli nae kucheka. Na baada kukatisha kicheko Joeli akasema "Halafu Jerome leo nilipanga nikuletee suruali moja nzuri sana na shati ya kufa mtu bila kusahau ndula,watu wa siku hizi wanasema moka ama lakuchumpa. Lakini bahati mbaya kuna sehem nilipita Kwahiyo nikawa nimeshindwa kupita sehem hiyo kukununulia. Ila usihofu bwana kesho nayo ni siku lazima nikununulie ili mwisho wa siku ukirudi kijijini kwenu madem wote wakushibokee. Kama unavyofaham wasichana wa vijijini wanavyoshobokea watu wa mjini,dah kiukweli Jerome utawamaliza wote" Alisema Joeli huku akimalizia na kicheko. Maneno hayo yalimfurahisha Jerome,nae alicheka kidogo kisha akajibu "Sawa nitashukuru bosi wangu acha nianze hii kazi muda huu" kwisha kusema hivyo Jerome aliondoka zake ilihali Joeli nae aliingia ndani ambapo alimkuta mkewe kakaa kwenye sofa huku akiwa amechoka mwili hadi akili. Naomi alijikuta akiwa katika hali hiyo baada kutoukuta ule mkataba pale mezani,aliona tayali mambo yamekuwa si mambo. Kitendo hicho alishindwa hata kumuelezea Joeli kwani enzi ya uhai wa Siwa,Joeli haluambiwa kwamba kuna mkataba kati ya Naomi na Siwa. Siri hiyo ilibakia mioyoni mwao tu hawakuthubutu kumwambia mtu yoyote. Naomi aliwaza sana,alijiuliza maswali mengi mno ndani ya kichwa chake lakini mwishowe aliishia kushusha pumzi tu huku akibadili mikao kwenye sofa kitendo ambacho kilizidi kumshtua Joeli ambapo nae alijikuta akijiuliza "Mbona leo Naomi yupo hivi? Je, Siwa atakua amemtokea na ndicho kinacho mfanya aniambie tuhame nyumba hii ama? Na kama sivyo mbona haniambii kinacho msibu wakati mimi ndiye mumewe. "Hapo Joeli alishusha pumzi kwanza kisha akajisemea "Ngoja nikae kimya kama kuna tatizo basi ataniambia,maana nasikia kwamba kuna baadhi ya mimba huwa zinatabu sana. Itakuwa mimba yake imeanza kunichukia " Joeli ipokwisha kujisema hayo alinyanyuka kutoka kwenye sofa akazipiga hatua kuingia chumbani kupumzika.

    Usiku ulipoingia alifanya vile alivyoambiwa na mganga,kweli usiku huo hakuna mauza uza yoyote yaliyomkumba wala ndoto za kutisha. Joeli alilala usingizi mzuri kabisa. Kesho yske asubuhi alipoamka alifurahi sana,haraka sana alimpigia simu Magesa. Mgesa alishangaa sana kuona Joeli kumpigia simu asubuhi asubuhi kwani haikuwa kawaida yake,alipo pokea Joeli akasikika Joeli akisema "Daah ama kweli yule mzee ni fundi kati ya mafundi hapa chini ya jua " Magesa akajibu "Aah Joeli umeona sasa? Eeh huyo bwana ndio Zamwela. Nadhani jana mambo yalikuwa tofauti kabisa"

    "Magesa rafiki yangu nakwambia usiku nimelala vizuri kabisa bila tabu yoyote"

    "Sawa kaka jitahidi urudi kule ili ayapoteze kabisa" alisema Magesa. Joeli akiwa mtu mwenye furaha akajibu "Basi baadae tutaongea zaidi ngoja nijiandae ili niwahi kazini" Alikata simu Joeli kisha akajiandaa haraka haraka akaelekea kazini huku akimsifu Jerome kwa kumuoshea gari kwa astandadi mzuri. Alipofika kazini alifanya kazi halafu baadae aliamua kutoka akaelekea kwa mganga Zamwela ambapo kabla hajafika alimpigia simu mmoja ya wanakijiji hicho anachoishi Zamwela. "Nimefika mleta sasa huyo mbuzi " alisema Joeli baada huyo mwanakijiji kupokea simu. "Sawa nisubili dakika mbili tu kaka" alijibu mwanakijiji huyo. Punde akafika akiwa na mbuzi mkubwa kiasi,Joeli alimpatia jamaa pesa waliyokubaliana kisha akaanza safari ya kuelekea mahali kilipo kibanda cha mganga Zamwela. Alipofika alikaribishwa,Joeli akakaa. Mganga Zamwela akamuuliza "Nini shida kijana? " swali ambalo lilimshtua Joeli lakini hakutaka kujaji sana zaidi alimkubusha kwa kusema "Nimekuja mtalam kuchukua sasa ile dawa uliyoniambia nije kuchukua leo"

    "Dawa? Dawa gani?.." Alihoji mganga Zamwela,ajabu safari hiyo ilisikika sauti ya Siwa badala ya sauti ya mganga. Joeli alishtuka,na punde si punde mganga huyo akageuka Siwa kisha akaangua kicheko.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Joeli alipoona kitendo hicho alitimua mbio lakini kabla hajafika mbali alikutana na Siwa mbele yake,aliogopa kwenda mbele alirudi kule alikotoka ambapo safari hiyo hakumkuta mbuzi wake ila alimkuta mganga Zamwela. Aliogopa sana Joeli,alihaha mfano wa mwendawazimu akatimua mbio kutoka hapo kwa mganga. Njiani hakukutana na Siwa,hivyo alipoingia ndani ya gari aliwasha na kuondoka kwa kasi ya ajabu huku akitazama nyuma kupitia vioo vya pembeni. Joeli aliemdesha gari kwa kasi ya hali ya juu,lakini wakati yupo kwenye kasi hiyo alitazama nyuma kupitia kioo cha mbele kilichopo juu yake alishtuka kumuona Siwa akiwa amekaa siti ya nyuma. Alipagawa sana Joeli mapigo ya moyo yalimuenda mbio akiogopa,kitendo ambacho kilimfanya kukanyaga bleak haraka kisha akaiweka kando. Baada kufanya hivyo alifungua mlango wa gari ili atimue mbio,lakini akajikuta kwamba kila akifungua mlango mlango haufunguki hali ambayo ilimpekekea Joeli kupiga kelele na punde si punde akapoteza faham.

    Upande wa pili alionekana mlinzi Jerome akipiga zogo mbili tatu na Naomi,kwani Naomi aliogopa kukaa ndani peke yake. Naomi alisema "Jerome unajua kwamba siku hizi nyumba haikaliki?.."

    "Kivipi bosi " aliuliza Jerome. Naomi alishusha pumzi kwanza halafu akajibu "Kila siku mauzauza ya ajabu ajabu,nadhani unamkumbuka Siwa.."

    "Ndio namkumbuka" alisema Joeli. "Enhee unahabari kwanga" kabla Naomi hajasema alichotaka kumwambia Jerome, mara ghafla honi ya gari ililia nje. Jerome akanyanyuka na kwenda kufungua geti,ambapo iliingia gari ya Jerome ikaenda kusimama sehem maalum anapoiweka kila siku. Naomi alipoona mumewe amerejea alinyanyuka kutoka mahali alipokua amekaa akasimama mbele kidogo huku mikono ikiwa kiunoni akisubili Joeli ashuke kwenye gari. Lakini dakika zilizidi kutaladadi Joeli akiwa bado yumo ndani ya gari,jambo ambalo liliwashangaza sana Naomi na Jerome. Ambapo mwisho Naomi aliisogelea gari kisha akafungua mlango,ajabu siti ya mbele haikuwa na mtu ila alipotazama siti za nyuma alimuona Joeli akiwa amelala. Naomi alishtuka, akamuita Jerome. Jerome akatii wito. "Jerome ujue haya ni maajabu sana. Joeli nimemkuta nyuma amelala wakati siti ya mbele haina mtu lakini funguo ipo kwenye uskani. Na kibaya zaidi mlango ulikuwa haujabanwa. Au anatupepesa macho?.." alisema Naomi. Joeli akajibu "Itakuwa" kwisha kujibu hivyo,Jerome alimuomba Naomi funguo ya gari kisha akafungua mlango wa nyuma halafu wakamuamsha Joeli. Joeli hakuamka,bado Naomi alijua ni masihara ya mpenzi wake kwahiyo alimtaka Jerome amletee maji kidogo kwenye kikombe ili amwagie. Jerome alifanya hivyo,ambapo Naomi alipopokea kikombe cha maji alimmwagia kidogo Joeli nae akawa amekurupuka huku akipiga kelele "Nisamehe Siwaaaa nisamehee " kelele hizo za Joeli ziliwashangaza Jerome na Naomi, wote akajikuta wakutazamana. Wakati huo Joeli alitoka ndani ya gari mbio akakimbilia ndani,haraka sana Naomi nae akamfuata. Ilihali huku nyuma wakimuacha Jerome akiwa amepigwa na butwaa asielewe ni senema gani inayoendelea kati ya Joeli na mkewe. "Loh kutakuwa na kitu juu ya kifo cha Siwa sio bure,kiukweli ni bosi niliyetokea kukubali kwa kila idara" alijisemea Jerome huku akiwa amejiinamia. Kumbukumbu yake akivuta maneno ya mwisho aliyowahi kuzungumza na marehem Siwa,ambapo siku hiyo Siwa alimletea chai lakini uso wake ukionyesha kubeba simanzi nzito. Kitendo ambacho kilimshtua Jerome na hivyo alimuita Siwa na kisha akamwambia "Samahani kwa kukusumbua bosi wangu, nia na dhumuni ya kukuita ni kutaka kukushukuru kwa chai yako. Lakini pia kuna jambo nataka nikuulize "

    "Jambo gani? .." alihoji Siwa.

    "Unajua Bosi,kwanza naomba ufaham kwamba jina lako ni kama jina la mama yangu huko kijijini. Ila yeye anaitwa kwa kirefu;yani Siwa wazuri. Sijui lina maana gani lakini nahisi anamanisha binadam ama walimwengu siwazuri,Eeh kwahiyo bibi yangu akaona ni bora ampatie mwanae hilo jina baada kuona walimwengu siwazuri hata kidogo " Alicheka kidogo Jorome mara baada kusema maneno hayo,alipohitimisha kicheko chake aliendelea kusema "Kwahiyo basi,kwa kuwa wewe ni wajina wa mama yangu. Napenda nikuite mama yangu ingawa kiumri tunashabiana japo wanizidi miaka kadhaa. Hivyo mama!? Naomba leo uniambie ni jambo gani hasa linakusumbua kwani kimuonekano sura yako inaonyesha ubebea maswahibu mengi mno, niambie basi huwenda nikakupa hata ushauri. Amaa kwa kuwa mimi ndiyo hivyo tena na siwezi kukushauri?.." alisema Jerome,Hapo Siwa aliachia tabasam kidogo kisha akamjibu "Hapana Jerome ndiyo hivyo nini sasa? We ni binadam unanafasi yako pia na ndiyo maana tukakuamini na kukuweka hapa getini. Aamh tuachane na hayo Jorome,ila ukweli ni kwamba mwenzio napitia maswahibu mengi sana sana tena ya kusikitisha."

    "Enhee mambo yapi hayo,au ni yakifamilia ambayo mimi sipaswi kujua?.." Alihoji Jerome huku akiikunja mikono yake kifuani kana kwamba anasikia baridi. Siwa kabla hajamjibu alishusha kwanza pumzi kwa nguvu kisha akasema akianza kwa kuguna "mmh,Jerome sioni sababu ya kuficha hili jambo. Kwa maana hata wahenga waliwahi kusema kwamba mficha maradhi kifo humuumbua,Kwahiyo mimi ni kama mgonjwa katu siwezi kuyaficha maradhi nitatakwambia kila kitu kwani huwenda ukawa na kitu cha kunishauri " alisema Siwa,mlinzi Jerome aliuendeleza uturivu wake. Wakati huo Siwa akaanza kumueleza kila kitu kuanzia hatua ya ugomvi kuhusu suala la upatikanaji wa mtoto mpaka kufikia ile hatua ya kumtoa sadaka Joeli kwa Naomi akiamini kwamba kufanya hivyo inaweza kumletea amani kati yake na mumewe ambaye ni Joeli,kitendo ambacho kilienda sawa hapo mwanzoni lakini kadili siku zilivyozidi kwenda ndivyo mambo yale yale ya zamani yakanza kujirudia mpaka kukomaa kabisa. Mlinzi Jerome iposikia mkasa huo wa Siwa,aliinamisha uso CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/chini huku akisikitika. Baadae kidogo aliinua uso wake kisha akasema "Daah! Pole sana bosi wangu, kwani ukisikia majaribu ndiyo hayo. Kitu cha kwanza naweza kusema umefanya kitu kimoja cha busara sana ila mumeo ndio fala." Siwa alishtuka kusikia kauli hiyo ya mlinzi Jerome,kwa mshangao akahoji "We Jerome unamaana gani?.." Jerome alicheka kidogo halafu akamjibu "Nina maana kwamba mumeo ni fala,kwani hakujui thamani yako ingawa pia na wewe ulikurupuka kuchukua maamuzi magumu japo ulifanya kitendo cha busara. Bosi una.." kabla Jorome hajaendelea kusema alikiweka kwapani kurungu chake kisha akaendelea kusema, "Bosi unajua siku zote ukizama katika suala nzima la mapenzi, utagundua kuwa sisi wanaume kwenye mapenzi ni kama madume ya mbwa. Hahahaha.." Alisema Jerome huku akimaliza kwa kicheko,wakati huo Siwa akimtazama tu ingawa mwishowe alivunja ukimya na kisha kumuuliza swali

    "Bado sijaluelewa Jerome,hembu nifafanulie hayo maneno yako"

    "Unataka nikufafanulie,juu ya jambo hili nililokwambia kwamba wanaume kwenye mapenzi ni sawa na madume ya mbwa?.. hahahahaaa mbona rahisi sana kujua maana. Basi suburi nikwambie" Alikumbuka Jerome hayo mazungumzo aliyowahi kuzungumza na marehem Siwa. Hakuishia hapo alikimbuka mpaka alipo muuliza swali kuhusu Joeli. Jerome alimuuliza swali Siwa "Hivi unampenda sana mumeo?.."

    "Ndio tena zaidi ya sana kiukweli Jerome" Alijibu Siwa huku akionyesha msisitizo. Jerome safari hiyo alikaa kimya ikiwa uso amainamisha chini,ingawa mwishowe aliuinua na kisha kuongeza kusema "Kwanini usifikilie suala la kuondoka nyumbani hapa, kwani kwa dalili hizo ninazo ziona tayali mumeo hakuhitaji tena ila anashindwa kukwambia. Na pia ukae ukijua moyo huo ulio nao wewe sio alionao rafiki yako,mapenzi mchezo mchafu. Rafiki anaweza kuwa mnafiki,akamshawishi mumeo wakakubaliana kukuua ili wabaki wakiponda raha. Kwahiyo kabla hayajatokea yote haya ni bora uondoke zako,kwa maana siku zote akufukazae hakwambii toka" Kwisha kukumbuka maneno hayo ya marehem Siwa,alishusha pumzi kwa nguvu kisha akasogea eneo lake la lindo. Aliketi huku akiwaza mambo mengi sana Jerome,na moja ya mambo hayo ni kufikia hatua ya kuacha kazi arudi nyumbani kwani tayali iliona mambo yametibuka. Lakini wakati mlinzi Jerome anafikia suala hilo,upande wa pili ndani,Naomi alimsogelea Joeli aliyeonekana kupagawa. Alipomkaribia alimtuliza kisha akamwambia "Joeli mume wangu niambie basi kipi kimekusibu" Joeli alishusha pumzi ndefu kisha akauliza "Nimefikaje kwanza hapa? " Naomi akajibu "Usijali nitakwambia,niambie kwanza kipi kilicho kusibu" Alikaa kimya kidogo Joeli halafu akasema "Mke wangu Naomba nisubili kidogo nikabadilishe nguo zangu kisha nije nikwambie"

    "Sawa mume wangu" Alijibu Naomi kwa sauti ya chini,Joeli alinyanyuka kutoka kwenye sofa,akazipiga hatua kuelekea chumbani. Alipoingia chumbani alivua koti lake akalitunduki kwenye enga kisha akaanza kufungua visikizo vya shati yake ilihali macho yake yakitazama juu kwenye paa,alipomaliza alishusha uso wake akatazama kitandani. Ghafla akamuona kitandani yule mbuzi wa kafara aliyempeleka kwa mganga Zamwela,na punde si punde sauti ya Magesa ikasikika kutoka kwa yule mbuzi. Sauti hiyo ilisema "Vipi umemfanikisha lile jambo kwa mtalam?"



    Joeli alishangaa sana kumuona mbuzi anaongea,istoshe sauti iliyosikika kutoka kwa mbuzi huyo ilikuwa ni sauti ya rafiki yake ambaye ni Magesa. Haraka alitoka chumbani huku akipigawa mayowe,alipofika nje aliingia kwenye kisha akamtaka Jerome afungue geti. Jerome bila kuchelewa alinyanyuka akafungua geti,ambapo Joeli aliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu wakati huo nyuma akionekana Naomi akiwa anashangaa bila kuelewa ni kitu gani kilichompelekea Joeli kutoka chumbani mbio na kisha kuingia ndani ya gari na kuondoka. Kitendo hakikumshangaza Naomi tu bali hata mlinzi Jerome nae alipigwa na bumbuwazi,hali iliyompelekea baadae kushusha pumzi na kisha kumgeukia Naomi kule mlagoni. "Bosi kulikoni,mbona hivi?.." Alihoji Jerome. Naomi hakujibu zaidi alirudi ndani moja kwa moja akapitiliza hadi chumbani kwa dhumuni la kwenda kutazama ni kipi kilichomtoa mbio mume wake. Lakini hakukuta kitu chochote,hapo Naomi akajikuta akiishiwa nguvu alijihisi kuchoka na hivyo alikaa kitandani na kisha kujiuliza maswali mengi sana juu ya mitihani hiyo wanayokumbana nayo. Baadae kidogo alikumbuka kuwa shangazi yake ambaye alikuwa akiishi nae kabla hajaolewa kwa Joeli,aliwahi kupelekwa kwa mganga wa kienyeji na rafiki yake. Shangazi yake huyo kipindi cha nyuma kabisa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kuvimba vile vile kutokwa maji kwenye nyayo. Lakini alipopelekwa kwa huyo mganga,tatizo hilo lilitoweka mara moja. Hivyo Naomi akaona heri CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akazungumze na shangazi yake ikiwezekana ampeleke kwa yule mganga aliyemtibu ili nae amsaidie juu ya mambo yanayotokea kila kukicha,wazo hilo Naomi aliona linafaa sana. Hakutaka kupoteza muda alienda bafuni kuoga,kisha akavaa mavazi mazuri yakiyonendana na mimba yake. Alipomaliza alichukua pochi yake kisha akatoka ndani akamwambia Jerome amfungulie geti,lakini Jerome kabla hajafungua alimfuata kwanza halafu akamwambia "Samahani bosi wangu,nimepigiwa simu nyumbani nimeambiwa kwamba dada yangu anaumwa hali sio nzuri kwa hiyo nahitajika kesho kutwa niwe nimefika" Naomi aliposikia maneno hayo ya Jerome alimtazama kwa jicho ngebe kisha akamsonya na kumwambia "Usiwe kama kichaa Jerome,huoni haya mambo yanayotokea? Unapotuona hapa akili zetu haziko sawa kabisa,Kwahiyo usitake tuendelee kuumiza vichwa kwa sababu ya upuuzi wako" alisema Naomi kwa hasira. Jerome alishusha pumzi kisha akaongeza kusema kwa sauti ya upole "Lakini bosi ukumbuke hili nililo nalo nalo tatizo pia,jaribu kuwa na utu ndugu. Ama ndio msemo ule kwamba mbamba ngoma huvutia kwake?.."

    "Usinichanganye bwana kwani ndio Doctor? Basi kama vipi ondoka. Nimekuzuia mimi?.." alijibu Naomi. Mlinzi Jerome alikaa kimya kidogo halafu akasema "Naomba ujira wangu"

    "Fanyakazi kama hutaki unaweza kwenda" Alijibu Naomi kisha akapanda ndani ya gari akaondoka zake kwa shangazi yake. Kauri hiyo ilimfanya mlinzi Jerome kushusha pumzi ndefu kwa mara nyingine, ukweli aliamua kutumia mbinu hiyo ya uongo akiamini kwamba Naomi ataweza kumuonea huruma ili ampe mshahara wake wa miezi aliyofanya kazi kisha aondoke hapo kwani tayali aliona mambo yamekuwa kizungumkuti. Na mara baada Jerome kushusha pumzi ndefu ijisemea "Na bado mtakoma mlizani mliyokuwa mnamfanyia ni mazuri? Laana hiyo inawajia. Sasa sipati picha siku akiwatokea marehem mwenye. Kheeh nadhani hiyo mimba kama kibuyu itakutoka kama sio kupasuka bwaaaa" alijisema hivyo mlinzi Jerome huku akijisogeza mahali kilipo kiti chake.

    Upande wa pili Naomi alikuwa akiendesha gari kwa kasi kuelekea kwa shangazi yake,alipofika alimkuta shangazi yake akiwa sebuleni akisuka ukili. Shangazi yake Naomialifurahi sana kumuona Naomi kwani ni siku hawajaonana. "Naomi karibu" alisema Shangazi yake Naomi huku akitabasam. Naomi nae akionyesha uso wa furaha akaitikia "Ahsante shangazi" Alikaa kwenye kochi kisha akasema "Enhee Shangazi yangu habari za siku nyingi"

    "Ni nzuri sijui kwako"

    "Kwangu salama ingawa sio sana"

    "Mmh kwanini? Ama ujauzito huo ulio nao?

    "Sio hivyo Shangazi ila mwenzio nina matatizo chungunzima"

    "Sawa kwa kuwa umefika kwa shangazi yako amini kwamba nipo tayali kukusaidia hata kwa mawazo na ushauri, lakini kabla hujaanza kunielezea niambie unatumia kinywaji gani "

    "Ammh kuhusu kinywaji wala usijali shangazi"

    "Hapana Naomi usiogope bwana,niambie unakunywa kinywaji gani"

    "Daah sawa nomba maji tu inatosha. Na vipi Veronique mbona simuoni? "

    "Vero kaniaga anakwenda kusukwa,toka asubuhi mpaka muda huu hajarudi" Naomi alijibiwa na Shangazi yake baada kumuulizia Veronique ambaye ni binamu yake. Wakati huo Naomi anajibiwa hivyo Shangazi yake alikuwa akizipiga hatua kumchukulia maji kwenye friji. Punde alirejea akiwa na jagi pia na grasi. Alipoketi alimimina maji nusu Kwenye grasi kisha akampa nafasi Naomi aweze kuzungumza matatizo hayo yanayomkumba. Naomi alikunywa maji bunda moja halafu akaanza kusema "Basi Shangazi mwenzio maji yamenifika shingoni kiukweli,na kwa hatua hii sioni sababu ya kukuficha nitakueleza kila kitu" Alisema Naomi akanywa tena maji kidogo halafu akaendelea kusema."Marehem rafiki yangu Siwa hakuwa na uwezo wa kuzaa,Kwahiyo akawa anakosa amani yeye na mumewe. Kwa sababu Joeli alihitaji mtoto wakati huo Siwa yeye ni mgumba,hali hiyo ikapelekea wao kuzozana kila siku. Kupitia hilo sasa Siwa akahisi huwenda Joeli akatafuta mwanamke mwingine wa kuzaa nae,kitendo ambacho Siwa aliamini kinaweza kumpelekea kumpoteza Joeli Kwahiyo akaniomba mimi kama rafiki yake nimzalie mumewe mtoto akidai kwamba atanipa pesa na gari. Lakini nitakapo jifungua nimuachie mumewe ila malezi ya mtoto nitasaidiana nae kulea. Hapo tukaandikiana mkataba . Nilikubali shangazi kama unavyojua maisha yangu yalivyokuwa kipindi cha nyuma,leo nipo kwako kesho kwa marafiki zangu yani sieleweki eleweki hali duni. Lakini pia istoshe Joeli nilikuwa nampenda sana tangu awali,Kwahiyo nafasi hiyo nikaamua kuitumia kumteka hisia Joeli na mwisho wa siku shetani mbaya akanipitia nikakubaliana na Joeli tukamuua Siwa.."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa maana hiyo umevunja mkataba?.." Aliulizwa Naomi na shangazi yake. Naomi akajibu ndio kisha akaongeza kusema "Sasa tangu kifo cha Siwa,nyumba imekuwa ya moto. Ndani hapalaliki shangazi yangu yani mpaka najikuta najutia kile nilichomfanyia Siwa" alisema Naomi safari hiyo akiangusha chozi. Shangazi yake alimsogelea kisha akamwambia "Yameshatokea hayo nadhani hupaswi kujilaumu bali nyamanza ili tujue ni kipi cha kufanya ili tulipoteze tatizo hili. Kuna mtalam yule iyenitibia tatizo la miguu kuvimba,yule atakusaidia. Aliweza kutibu ugonjwa nilitegewa kitu njiani? Sembuse hayo mauzauza?.." Alisema hivyo Shangazi yake Naomi.

    *******

    "Acha kunichanganya bwana Joeli, mbuzi ataongeaje sasa?.."

    "Magesa nikudanganye ili iweje?mbuzi kabisa kaniuliza tena sauti yenyewe ilikuwa sauti yako .."

    "Daah basi kama imefikia hatua hiyo ndugu yangu nakushauri tu ile nyumba hama. Utakufa siku si zako" Yalikuwa mazungumzo ya Joeli na Magesa. Kumbe Joeli alipotoka ndani mbio alikimbilia nyumbani kwa Magesa ili akamwambie tukio lingine la ajabu lililojitikeza,lakini Magesa licha ya kuambiwa alionekana kutokuamini na mwisho wa yote alimpa ushauri huo Joeli ili aepukane na mauzauza hayo. Joeli alipopewa ushauri huo kutoka kwa rafiki yake alikaa kimya kidogo kisha akasema "Ni kweli Sinabudi kufanya hivyo,istoshe hata mke wangu mwenyewe ilinishauri nifanye hivyo. Kwahiyo acha nianze kufanya mchakato siku yoyote nahame. Kwahiyo nakuomba rafiki yangu ukipata namba ya dalali basi nipaatie"

    "Usijali kuhusu hilo,kesho tukutane kazini nitakuwa nayo"

    "Sawa acha mimi nirudi nyumbani ndugu yangu"

    "Haya ingawa shemeji yako ndio anaanda mambo"

    "Doh Magesa unafikili hata ham ya kula ninayo? Itoke wapi sasa!.."

    "Pole sana bwana ila ndio ukubwa huo" alimaliza kusema hivyo Magesa,Joeli akajongea mahali ilipo gari yake akingia akawasha kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani hali ya kuwa huku nyuma mkewe Magesa alimwambia mumewe"Kulikoni Joeli kaondoka kabla hajala?.." Magesa akajibu "Kashachanganywa yule laana mkewe inamsumbua"

    Kwingineko Joeli alifika nyumbani, alimkuta Naomi akiwa amekaa kwenye sofa. Naomi alipomuona Joeli alitabasam wakati huo Joeli alikaa kwenye sofa, shusha pumzi ndefu na kisha akasema "Habari yako mke wangu?.." Naomi akajibu "Salama, pole kwa maswahibu yanayotukumba mume wangu"

    "Dah Ahsante pole na wewe "

    "Ahsante pia,lakini muda ule ulipotoka na mimi nilitoka, nilienda kwa shangazi yangu ili anipeleke kwa mtalam wake aliyemtibu ila nia yangu mimi ni kutaka mtalam atusaidie kuondokana na vitisho hivi. Akaniambia kesho nirudi ili anipeleke" alisema Naomi. Joeli akakuna kichwa halafu akajibu "Kajaribu na wewe ingawa mpango uliopo ni kuihama hii nyumba,la sivyo nitakuwa kichaa"

    "Usiseme hivyo mpenzi wangu, tuachane na hayo basi. Leo tena usiku nataka game.."

    "Mmh mimba hiyo bwana itulize kwanza" Alijibu Joeli. Naomi alitabasam halafu akaongeza kusema "Joeli bwana ama hujui mwanamke mjamzito anakuwa na hisia mara kwa mara?.."

    "Aah kumbe? Basi usijali nitakufaa usiku huu"

    Usiku wapata saa mbili wapenzi hao walikula chakula,muda huo pasipo kutokea jambo lolote la kutisha. Walipokwenda kulala wijikuta wakipitiwa na usingizi,lakini baadae Naomi aliamka kisha akaanza kumuasha na Joeli ili amkate kiu. Na kabla Joeli hajaamka mara ghafla Naomi alisikia watu wakiongelea ndani,sauti zilizosikika ilikuwa ya mwanaume na mwanamke. Naomi alishtuka macho yakagonga saa ukutani "saa sita na nusu" Alisema Naomi ndani ya nafsi yake wakati huo sauti hizo zilikuwa zikiangua kicheko,na punde si punde mlango wa chumbani kwao ugagongwa. Hapo Naomi akazidi kuchchawa,kijasho kikaanza kumtoka. Hamu ya tendo ilimpotea haraka sana,na hivyo akamuamsha mumewe ili asikilize yanayo jili lakini wakati anaendelea kumuamsha mara ghafla Joeli akageuka maiti iliyoonekana kuvishwa SANDA huku mwili ukiwa wa baridi na vilevile ukioneakana kukakamaa. Upande mwingine napo mlango uliendelea kugongwa huku vile vicheko navyo vikizidi kushamili humo ndani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog