Simulizi : Sanda Ya Siwa
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naomi hofu ilizidi kumtanda moyoni,woga nao ukashamili vile vile. Aliogopa sana kuona mambo hayo yanayotokea ndani usiku huo,wakati huo huo mlango uliendelea kugongwa huku sauti nazo za watu zikiendelea kusikika. Sauti ambazo zilikuwa hazieleweki,kilicho ileweka ni kicheko tu ambacho kiliwakilisha kufurahisha jambo ambalo walikuwa wakilizingumza watu hao. Naomi alihema kwa kasi ya ajabu,kijasho ndembe ndembe kilimtililika alipotaka kumuamsha mume wake aliogopa kwani muda huo Joeli akionekana akiwa maiti. Naomi alichanganyikiwa alishindwa afanye nini usiku huo,ndipo pole pole akaamua kutelemka kutoka kitandani akaisogelea switch ya taa kisha akazima. Ndani pakatawala giza nine,hapo akajisogeza kwenye kona ya chumba halafu akachuchumaa na kujikunyata mfano wa kifaranga kilicho nyeshewa na mvua. Hofu dhofu lihali ikiambatana na woga viliendelea kumganda Naomi,kuzimia alipenda lakini kitendo hicho abadani hakikuweza kumtokea. Wakati akiwa kwenye hali hiyo kunako giza,mara ghafla taa iliwashwa. Hapo Naomi alishtuka, alikodoa macho kutazama kulia na kushoto na punde si punde mlango ulifunguliwa akamuona Siwa akiingia chumbani huku mkononi akiwa na makaratasi yaliyoandikwa mkataba. Naomi alizidi kupigwa na butwaa,asiamini kama kweli huyo ndiyo Siwa. Na kibaya zaidi Siwa alimtokea Naomi akiwa na mavazi yale ambayo aliyavaa wakati wanaandikishiana mkataba. "Mbona unaogopa?.." alihoji Siwa,ambapo sauti yake ilisikika ikijirudia mara mbili. Naomi hakujibu alitetemeka mwili mzima huku akinyoosha mikono ishara ya kukataa jambo fulani. Alicheka Siwa kisha akasema "Simama" Naomi akasimama kwa woga kufumba na kufumbua akajikuta yupo sebuleni. Alihema kwa nguvu wakati huo huo sauti kutoka kwa Siwa ilisikika kwa mara nyingine ikisema"Mkataba huu unaukumbuka? " Naomi akajibu kwa sauti ya uoga "Ndi...o ndio nakumbu... Nakumbuka"
"Sasa kama unaukumbuka kwanini umeuvunja? Kwa taarifa yako nimekuja kukwambia kwamba bado nipo hai na chamoto utakipata msheshi mkubwa wewe" Kwisha kusema hivyo alipotea. Naomi aliogopa akashtuka kutoka usingizini. Ilikuwa ni ndoto ambayo aliiota baada kupitiwa na usingizi,hivyo alipotazama ukutani akaona tayali ni usiku wa saa nane wakati kwenye ndoto aliota kwamba aliamka usiku wa saa sita. Alishusha pumzi akamtazama Joeli ambaye muda huo alikuwa amelala usingizi mzito,akaona yupo kawaida tofauti na alivyomuota ndotoni kwani kwenye ndoto aliota kuwa kuna vicheko na sauti zisizoeleweka zinalindima ndani wakati huo Joeli nae akiwa ni maiti iliyovishwa sanda. Hapo Naomi aliketi kitandani,akaitafakari ndoto hiyo aliyoota huku akikumbuka maneno ya marehem Siwa "Sasa kama unaukumbuka kwanini umeuvunja? Kwa taarifa yako nimekuja kukwambia kwamba bado nipo hai na chamoto utakipata msheshi mkubwa wewe" maneno hayo makali yalijirudia kichwani mwa Naomi. Jambo hilo lilimshtua sana,akajiuliza "Au haya mauzauza yanayotokea ni sababu ya Siwa? Lakini inawezekana vipi mtu aliyekwisha kufa akarudi duniani? Na huu mkataba kwa mara ya kwanza niliuona kwa macho yangu na safari hii umenitokea ndotoni! Hapana kutakuwa na jambo hapa sio bure" alijiukiza na kujiaminisha hivyo Naomi. Baada ya hapo alirudia kulala akajifunika shuka na kuanza safari ya kuutafuta usingizi kwa mara nyingine baada kuamshwa na ndoto ya kutisha.
Kesho yake asubuhi mtu wa kwanza kuamka alikuwa ni Naomi,ambapo alipoamka alimuamsha na Joeli. Joeli akaamka lakini kabla hajashuka kitandani ili akaoge,Naomi akamwambia "Mume wangu,jana usiku mwenzio sijalala hata kidogo?.." Joeli kabla hajamjibu mkewe alipiga mwayo kwanza huku akijinyoosha na kujingunja kulia na kushoto mbele na nyuma. Baada ya kufanya hivyo akamuuliza "Kwanini sasa?.." Naomi alishusha pumzi kisha akajibu "Mmmh nimemuota Siwa kwamba kanitokea, lakini pia istoshe nikawa nasikia sauti za watu wanaongea lugha ambayo haieleweki. Yani kiswahili sio kiswahili kingereza sio kingereza,kilugha sio kilugha. Na kibaya zaidi mlango ukawa unagongwa,kufumba na kufumbua akaingia Siwa. Hivyo sielewi ndoto hii inamaa gani,au inamaana kwamba Siwa yupo duniani? Na ndiyo huyu anae tusababishia mauzauza?.." alisema Naomi. Joeli alisonya akashuka kitandani kisha akamjibu "Naomi hayo sio mambo ya kuzungumzia sasa,kinachotakiwa ni kufikikilia kipi cha kufanya. Unajua hapa ni mjini nyumba zinakila aina ya mambo,kwahiyo huwenda labda ile damu tuliyomwaga humu ndani yawezekana mazindiko ya nyumba yamekasirika na ndio maana yanatokea mauzauza haya,mara ndoto za kutisha. Hivyo basi kinachotakiwa ni sisi kuhama hii nyumba,lakini pia tutakapo hamia nyumba mpya kabla hatujaanza maisha huko tumuite mchungaji aiombee kwanza nyumba hiyo ili kama kuna mazindiko basi yateketee" Alijibu Joeli akijaribu kumuondoa Naomi kuamini kuwa kweli marehem Siwa yupo,alifanya hivyo ili Naomi asiogope zaidi ya anavyoogopa sasa. Lakini Naomi aliguna kidogo kisha akasema "Joeli acha kunichekesha bwana,unanifanya mimi mtoto mdogo sio? Nyumba hii ni nyumba ya kampuni,iweje waweke mazindiko? Ingekuwa nyumba ya mtu binafsi hapo sawa lakini nyumba ya kampuni? CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Aawapi bado hujanishawishi! Na kuhusu suala la kuhama,hapo nakubaliana na wewe ila suala la kuita mchungaji hilo utakuwa unachekesha kiukweli,hivi unafikili mchungaji gani ataitika wito wako wakati hata mara moja hujawahi kuhudhulia kanisani" Alisema Naomi. Joeli alikaa kimya kidogo kisha akasema "Nichemshie chai bwana niwahi kazini,mwanamke unaongea kama mzaramo?.." alipokwisha kusema hivyo alizipiga hatua kuingia bafuni kuoga. Muda mchache baadae alimaliza akanywa chai halafu akaisogelea gari yake kwa tayali ya kuelekea kazini,hivyo Jerome alihitajika kufungua geti. Lakini kabla Jerome hajafungua geti, alimsogelea Joeli kisha akamwambia "Bosi,nimepata taarifa kutoka nyumbani kwetu kwamba nahitajika haraka sana siku ya kesho ama kesho kutwa,hali ya dada yangu sio nzuri" Joeli akajibu "Usijali kuhusu hilo,nikitoka kazini nitakupa pesa yako" mlinzi Jerome alifurahi sana moyoni,haraka sana alisogelea geti akafungua ambapo Joeli alitoka kwa kasi akaelekea kazini. Huku nyuma Naomi nae alikuwa akijiandaa kueleke kwa shangazi yake ili ampeleke kwa mtalam aweze kumsaidia juu ya mauzauza hayo yanayowaandama,Naomi aliamini huko anaweza kupata suluhisho.
Alipofika kwa shangazi yake aliambatana nae hadi kwenye gari kisha safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza,walitumia muda mchache kufika huko. Mganga huyo aliitwa Kalumanzila. "Hodi hodi babu " Alisema shangazi yake Naomi akibisha hodi kwenye kibanda cha mzee Kalumanzila. Muda huo mzee Kalumanzila alikuwa ametoka kidogo,alielekea mahala fulani kuchimba dawa. Hivyo baada shangazi yake Naomi kugundua kuwa mganga hayupo,alimwambia Naomi wakae kumngojea. Walitulia chini ya mti wa mwembe kumsubili Kalumanzila, haikuchukua muda mrefu Kalumanzila alirejea ambapo alipomuona shangazi yake Naomi alimkumbuka. "Karibuni sana" alisema Kalumanzila huku akizipiga hatua kuingia kwenye kibanda chake. Shangazi yake Naomi alimtaka Naomi waingie ndani kumfuata mzee Kalumanzila. Walipofika ndani,Kalumanzila aliwasalimia kwanza kisha akavaa mavazi yake ya kazini. Nyimbo za kilugha aliimba Kalumanzila, na punde si punde akapandisha mizimu yake na kumruhusu Naomi aseme kinachotakiwa kufanyika. Naomi alieleza kila kitu huku akiomba mauzauza yapotee ndani ya nyumba yake. Mizimu ya mzee Kalumanzila iliposikia matakwa hayo ya Naomi ilikohoa kidogo kisha ikaangua kicheko,ilipokatisha kicheko ikasema "Afadhali umekuja mapema, kwani ulibakisha siku kadhaa kuaga dunia. Hivyo tupo tayali kukusaidia lakini kwa sharti moja tu. Je, upotayali? .." Naomi aliposikia swali hilo alimtazama shangazi yake. Shangazi yake nae akamjibu "Kubali"
"Ndi..Ndio nipo tayali" alijibu Naomi huku akiwa na woga. Mizimu ya mganga Kalumanzila iliposikia jibu hilo la Naomi iliangua kicheko kisha ikasema "Mtoto wako huyo aliyopo tumboni ndio tunataka damu yake" maneno hayo yalimshtua Naomi,ambapo alimtazama shangazi yake kwa hasira akanyanyuka kisha akasema "Sipo tayali kama ni upuuzi huo,nitamwambia nini mume wangu? Bora niendelee kuteseka hivi kuliko kuniulia mwanangu" Alisema Naomi. Mizimu ya mganga Kalumanzila iliangua kicheko "Ahahahaaaaa! " kisha ikasema "Lazima ufanye hivyo,lazima ufanye hivyo nasema lazima ufanye ufanye hivyo. La sivyo la sivyo utanitambua" Maneno hayo ya mizimu ilimshtua sana Naomi pamoja na shangazi yake,shangazi mtu alionekana kuogopa zaidi na hivyo alisimama na kumtaka Naomi amsikilize mganga ili asipatwe na matatizo,Ila Naomi alikataa katu katu ilihali muda huo ilisikika sauti kutoka kwa mganga ikihoji "Mkataba huu unaukumbuka? " Naomi alitaharuki kusikia swali hilo,na kibaya zaidi sauti iliyosikika haikuwa ya mganga Kalumanzila tena bali ilikuwa sauti ya marehem Siwa.
Naomi alishangaa kitendo hicho cha mganga kuongea masula ya mkataba,na kibaya zaidi sauti aliyoisikia ni sauti ya marehem Siwa. Haraka sana Naomi aliondoka eneo hilo,wakati huo shangazi yake akishangazwa na uamuzi aliochokua Naomi kwani wakati mganga anaongea suala la kuhusu mkataba,yeye maneno hayo hakuyasikia iliyeyasikia ni Naomi peke yake. Hivyo shangazi mtu alimkimbilia Naomi, alipomfikia alisema "Naomi,unafanya nini sasa? Badala ukae umsikilize mganga ili aone namna gani atakusaidia,wewe unajichukulia maamuzi tu ya kuondoka. Je, unategemea sehem gani tena utakimbilia?.." Naomi aliposikia maneno hayo ya Shangazi yake alishusha pumzi kisha akamjibu "Shangazi yangu mimi namuheshimu sana,lakini katika hili mimi sipo tayali. Yani nimtoeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kafara mtoto wangu? Unafikili Joeli alivyokuwa na shauku ya kutaka mtoto atanielewaje mimi pindi atakapojua kwamba mimi ndio chanzo cha mtoto wake kufa"
"Mmh sawa nakubaliana na mawazo yako,ila naomba usinifuate tena kwa jambo hili sawa?.." Aliongeza kusema shangazi yake Naomi, tena aliongea kwa msisitizo. Baada ya hapo alirudi kibandani kwa mganga Kalumanzila ili amuage,ajabu alipofika kule hakumkuta bali alimuona mwanamke aliyevaa mavazi meupe huku macho yake yakiwa mekundu. Shangazi yake Naomi aliogopa akatimua mbio huku akipiga mayowe ilihali nyuma akisikika sauti ya kicheko kutoka kwa yule mwanamke ambaye si mwingine ni Siwa. "Naomi fungua mlango wa gari tuondoke haraka sana" Alisema shangazi mtu akimtaka Naomi afungue mlango wa gari. Naomi alifanya hivyo kisha nae akaingia "Haraka sana tuondoke hapa,fanya hima Naomi " Aliongeza kusema shangazi yake Naomi huku akihema haraka haraka,Naomi aliwasha gari kisha akaliendesha kwa kasi ya ajabu. Walipofika mbele zaidi alipunguza mwendo,akaendesha mwendo wa kawaida ambapo mazungumzo yakaanza. Naomi alisema "kipi sasa kilichokutoa mbio kule?" "Daah we acha tu,nillirudi ili nikamuage mganga. Nilipofika nyumbani kwake cha kushangaza nikamkuta Siwa" Naomi aliposikia maneno hayo alishtuka kisha akauliza "Siwa huyu huyu ama?"
"Kwanini nikudanganye sasa? Siwa kwa macho yangu nimemuona"
"Loh! Sasa naanza kuelewa maana ya ile ndoto niliyoiota jana usiku,najutia sasa maamuzi yangu" aliwaza Naomi,halafu akashusha pumzi kisha akasema "Shangazi kama kweli uliyemuona ni Siwa basi nimekwisha"
Upande wa pili mlango wa ofisi ya Joeli ulifunguliwa akaingia Magesa. "Habari yako bwana Joeli" Alisema Magesa huku akikaa kwenye kiti,Joeli alishusha pumzi kisha akajibu "Salama tu Magesa nambie"
"Naam nimekuja bwana, namba ya dalali tayali nimeipata " aliongeza kusema Magesa,Joeli alitabasam halafu akajibu "Dah kweli Magesa? Na unamuamini kabisa nyumba nzuri. Maana asije akanipeleka kwenye nyumba mbovu kama kontena"
"Hahahaa Hapana namuamini sana huyu jamaa,nyumba taklibani zote za Dar es salaam anazielewa. Najua hawezi kukupeleka nyumba mbovu kama za Tandale kwa tumbo " Alijibu Magesa, maneno yake hayo yalimfanya Joeli kuangua kicheko huku wakigongeana mikono. Baada ya hapo Joeli akachukua simu yake akampa Magesa kisha akamwambia "Niingizie namba hizo" Magesa alipokea na kuanza kucharaza namba za dalali kwenye simu ya Joeli,alipoamaliza alimrudishia simu yake halafu akasema "Huyo naitwa Tito, unaweza kumtafuta muda wowote ambapo mnaambatana nae kuangalia nyumba unayoitaka. Lakini Joeli, vipi sasa kuhusu ile nyumba ya kampuni? .." Alihoji Magesa. Joeli alimtazama Magesa kisha akamjibu "Kaka! Hivi umenipa namba ya dalali nikishapata nyumba tu,nakabidhi mjengo sehem husika ila uwezekano wa mimi kuendelea kukaa kwenye ile nyumba ni mdogo sana. Siwezi kuishi kama punda,kila siku hili mara lile"
"Unafikili hiyo ndiyo itakuwa njia ya kumkimbia marehem Siwa?.."
"Ndio huwenda ikasaidia " Alijibu Joeli.
"Mmh haya sawa, acha mimi nikaendelee na shughuli yangu. Nilikuja kukupa namba uliyohitaji,kwahiyo najirudisha ofisini kwangu. Mtafute huyo mtu" Alisema Magesa na kisha akaondoka zake. Joeli aliitazama namba hiyo aliyopewa, alitazama kwa muda wa sikunde kadhaa kisha akaiweka simu sehem husika. Baada ya hapo alijisemea "Nitamtafuta nikitoka hapa"
Baadae jioni alipotoka kazini alimpigia simu dalali,ni bwana Tito. Mzee maarufu kwa kutafuta vyumba,nyumba na viwanja pamoja na magari. Ni mzee mpenda kuvaa kanzu na baraka shia, popote pale unapomuona utamkuta na fimbo yake umaridadi kwake ulikuwa jadi.
"Halooh!" Alisema Joeli. Dalali Tito akajibu kwa sauti ya mbali "Halooh nani mwenzangu?.. "
"Unaongea na Joeli, we sindio Tito?.." Aliuliza Joeli.
"Ndio yeye"
"Basi nilikuwa ninashida ya chumba"
"Sawa leo au kesho?.." Alihoji Dalali. Joeli akakaa kimya kidogo kisha akajibu "Hata leo sio mbaya,cha muhimu nikipate chumba yani niwe na uhakika kabisa" alisema Joeli. Dalali Tito akamuuliza "kwani muda huu uko wapi"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Natoka kazini kwangu, ila kama hutojali tukutane magomeni mikumi ili tujue cha kufanya" alijibu Joeli,hapo dalali Tito akajibu "Sawa ukifika niambie"
"Sawa hamna shida mzee wangu" Akakata simu Joeli kisha haraka sana akafungua mlango wa gari akaingia ndani,kwa furaha aliyokuwa nayo baada kuongea na dalali ilimfanya akafungua muziki mnene ndani ya gari na punde si punde akaliendesha gari lake kwa kasi kutoka hapo alipokuwa ameipaki. Alikuwa wa kwanza kufika magomeni mikumi,lakini hakuchukua muda mrefu dalali Tito nae alifika kwa usafili wa daladala. Walisalimiana na wakazungumza mambo mawili matatu kisha wakaingia ndani ya gari wakaelekea huko mahali ilipo nyumba. Walikwenda moja kwa moja mpaka maeneo ya Sinza kwa lemi,hapo dalali alimuelekeza Joeli sehem anayoweza kupaki gari yake kwa ulinzi madhubuti. Joeli aliacha gari eneo hilo na kisha wakazipiga hatua kuelekea mahali ilipo nyumba,wakiwa njia dalali alimuuliza Joeli "Unataka nyumba ama chumba?.." Joeli akajibu "Sio mbaya hata nikipata nyumba,ilimladi iwe na vigezo vyote vinavyotakiwa"
"Sawa twende huku nikakuonyeshe mjengo unaoendana na wewe" aliongeza kusema dalali.
Na hatimae walifika sehem hiyo ilyopo nyumba,hakika ulikuwa mjengo wa maana. Nyumba imekamilika kila idara huku pembeni yakionekana maua mbali mbali yaliyopandwa kwa niaba ya kuipendezesha nyumba,lakini wakati Joeli anaichunguza nyumba hiyo ili ajilidhishe cha ajabu kuna baadhi ya watu wapita njia na majirani na nyumba hiyo walionekana kulitazama tukio hilo huku minong'ono us hapa na pale ikisikika ingawa Joeli na dalali hawakuweza kuisikia. "Watu wamjini bwana umbea kila kona,tazama wanatushangaa shangaa tu. Unajua bwana Joeli asilimia kubwa ya watu wanaoishi maneo haya wanashindwa kupanga humu ndani Kwahiyo ndio maana wanakuona wewe ni bonge la bosi halafu istoshe unaonekana kijana mdogo usiedhaniwa mbele ya uma" Alisema dalali Tito akimwambia Joeli. Joeli alicheka kidogo kisha akasema "Sasa mzee wangu nyumba nimeipenda,nyumba nzuri kweli kweli hivyo kilichobaki ni mimi na wewe tumalizane unikabidhi funguo ili kesho nihamie humu rasmi"
"Wala hakuna shida bwana Joeli,ni wewe tu maliza mambo nikukabidhi funguo yako" Alijibu Tito. Walijadili namna gani ya kupeana pesa hizo,siku hiyo hiyo Joeli akakabidhiwa na mkata wa kuishi ndani ya nyumba hiyo lakini pia alipewa na ufunguo kwa hiyo jukumu likabaki kwake yeye kuchakua siku gani atakayo hamia. "Nitahama kesho" alijisemea Joeli wakati huo tayali yupo ndani ya gari yake akirejea nyumbani. Alipofika alimkuta Naomi sebuleni akiwa amejinamia,Naomi alikuwa akiyafikilia Yale mambo aliyokutana nayo kwa mganga. Hivyo Joeli alipofika alimgusa kitendo ambacho kilimfanya Naomi kukurupuka,Joeli akacheka kisha akasema "Mbona unakuwa muoga sasa? Acha kuogopa wewe utakufa mapema bwana"
"Mmh we acha tu yani safari hii hata panya akipita lazima uogope" alijibu Naomi wakati huo Joeli akikaa kwenye sofa. Alipokaa sawa akaongeza kusema "Usijali mke wangu,nafikili huu ni muda wa kuanza kulifurahia penzi letu kama zamani. Mauzauza haya yote mwisho usiku wa leo,kilichobaki ni kutoa taarifa kazini kwangu ebwanaee nyumba yenu imenishinda nimeamua kuhamia nyumba nyingine full stop. Sitotaka maelezo meeengi kama nabembeleza mwanamke,kwa sababu nimeshindwa kuishi kwenye nyumba isiyo na amani hata chembe" alisema Joeli. Naomi akashusha pumzi kisha akahoji "Enhee na vipi kuhusu kazi ?.." Joeli aliposikia swali hilo aliguna kidogo halafu akajibu "Elewa nimeacha kuishi kwenye nyumba ya kampuni na sio nimeshindwa kufanya kazi ya kampuni"
"Enhee na wewe vipi huko mlikoenda?" Aliongeza kusema Joeli huku akiuliza suala lile la Naomi na shangazi yake. Naomi alisikitika kidogo kisha akamjibu "Mwenzangu mganga akaniambia Oooh! Kama unataka dawa ya kuzuia mauzauza hayo ipo ila itahitajika damu ya mtoto uliyopo tumbuni mwako. Nikasema nyooo kama ni hivyo bora niendelee kuteseka,nitamwambia nini mume wangu pindi atakapo gundua kuwa chanzo cha kifo cha mwanae ni mimi?..haraka sana nikaondoka zangu. Kwahiyo bwana dawa nimekosa kwa style hiyo" Joeli alishangazwa sana na habari hiyo lakini mwisho alichukua kwenye begi lake ndogo akafungua zipu huku akisema"Safi sana,sasa tuachane na hao waganga mke wangu. Makataba huu hapa,kesho nampa Jerome pesa yake lakini pia kesho hiyo hiyo tunaham humu ndani" alisema Joel,mkataba akiwa ameuweka juu ya meza. Lakini cha kustajabisha Naomi alishtuka kwa sababu mkata aliokuwa anauona sio mkataba wa nyumba kama Joeli anavyodai bali mkata aliokuwa anauona ni ule aliosaini na marehem Siwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mbona unashtuka,huamini kama huu ni mkataba wa nyumba?.." Joeli alimuuliza Naomi baada kumuona kashtuka pindi alipomuonyesha mkataba wa nyumba mpya.Naomi kwa kuwa hakuwahi kumwambia Joeli kuhusu ule mkata aliosaini na marehem Siwa,hivyo hakutaka kusema kile alichokiona. Zaidi alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Mmh hapana hakuna tatizo mume wangu,unajua lazima nishtuke kuona umefanikisha jambo hili. Sasa natumaini mauzauza yote tunayaepuka tunaenda kuanza maisha mapya "
"Kwahiyo umefurahi sana?.." Aliongeza kuhoji Joeli. "Ndio kwanini nisifurahi?.." alisema Naomi. Joeli alikusanya karatasi hizo za mkataba akazipiga hatua kuelekea chumbani kwake kuzihifadhi. Baada kufanya hivyo alitoka chumbani akaelekea kwa Jerome,alipomfikia alimuita. Jerome alitii wito,alimkaribia bosi wake na kisha akamsalimu "Ndio bwana habari yako bosi wangu" Alisema mlinzi Jerome. Joeli kaitikia "Ni nzuri" punde si punde akaongeza kusema "Eenhe unakumbuka ni kiasi gani unachodai?.." Mlinzi Jerome aliposikia swali hilo la bosi wake alitazama juu akijaribu kuvuta kumbukumbu ya miezi mingapi aliyofanya kazi,lakini kumbukumbu zilimpota na hivyo akazipiga hatua za haraharaka kuelekea kwenye kibanda chake,huko alitoa sanduku alilohifadhia nguo zake akalitafuta daftari lake la kuhifadhia kumbukumbu alizozijua yeye. Alipolipata hilo daftari alirudi mahali alipo simama Joeli,akafunua kurasa kadhaa akaiona mahali alipohifadhi kumbukumbu kisha akamtajia Joeli pesa anayodai. Bila kupoteza muda, Joeli aliingiza mkono mfukoni akachomoa kitita cha fedha tasilimu za kitanzania akahesabu kiasi kile anachokidai mlinzi Jerome, akampatia. Jerome alipokea pesa hiyo lakini kabla hajaitia mfukoni alitoa ndimi nje akagusisha kidole chake kwenye ulimi kisha akazihesabu,alipohakikisha zimetimia alikohoa kidogo halafu akasema "Shukrani sana bosi wangu,hakika nimefurahi sana kuwa nanyi kwa kipindi chote tangu enzi za marehem Siwa mpaka uwepo wa sasa wa Naomi. Hakika mungu mkubwa,lakini pia kama kuna mambo kadhaa niliyowahi kukukosea basi tusamehene maana sisi sote ni binadam,hakuna binadam aliyekamlika chini ya jua" alisema mlinzi Jerome ikiwa tayali ameshapokea ujira wake. Joeli alipoyasikia hayo maneno alitabasam kidogo. Kisha akamjibu "Hakuna tatizo bwana Jerome, sisi wote ni wanaume. Kwahiyo ni vizuri kuachana kwa wema kwa sababu hakuna ajuae kesho yake,we nenda salama nyumba wasalimie pia"
"Hakuna tatizo bosi wangu,Ahsante sana. Basi ngoja nifue fue nguo zangu ili kesho mapema tu nianze safari" Aliongeza kusema Jerome,hapo walipeana mikono kisha Joeli akarudi ndani ilihali Jerome nae alienda kufanya kazi aliyokuwa akifanya hapo awali kabla hajaitwa na bosi wake.
Usiku ulipoingia ulikuwa usiku wa amani sana, hayakutokea mauzauza yoyote yale wala kati yao hakuna aliyeota ndoto mbaya za kutisha. Kitendo hicho kiliwashangaza sana Joeli na mkewe ambaye ni Naomi,lakini hicho kitendo katu hakikuweza kuwashawishi wao kuendelea kusalia ndani ya nyumba ile. "Mke wangu,naona zindiko la hii nyumba limeamua kutulia ili tuendelee kusalia humu humu. Jambo ambalo haliwezekani hata kidogo hahahahaha! " Alisema Joeli huku akifatisha na kicheko,maneno hayo alikuwa akimwambia Naomi asubuhi alipoamka. Naomi alicheka kidogo halafu akajibu "Fanya haraka bwana uwahi kazini,usichelewe kurudi ili tufanye mkakati wa kuhama"
"Sawa mke wangu hakuna tabu "aliongeza kusema Joeli wakati huo akijifunga kiunoni taulo yake ili aende bafuni kuoga. Hakuchukua muda mrefu sana alimiza, akavaa haraka haraka akachukua funguo ya gari akaanza safari ya kuelekea kazini. Siku hiyo alifunga geti mwenyewe kwa sababu Jerome tayali alikuwa aneshaondoka zake,alipoitoa gari nje alirudi ndani kumuita Naomi ili aje afunge geti. Wakati Naomi anainama kulifunga geti,Joeli aliangua kicheko kisha akamtania kwa kusema "Sasa hapo siunamfinya mtoto tumboni? .." Naomi akajibu "Kwenda zako huko.."
"HAhahahaaa! Sawa bwana,baadae basi mke wangu" aliongeza utani Joeli kwa Naomi,baada ya hapo aliingia ndani ya gari akaondoka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipofika ofisini,aliandika barua ya kukabidhi nyumba ya kampuni. Aliorodhesha na vigezo kadhaa vilivyomfanya ahame,wakati huo alijiwekea msimamo kwamba utasubili majibu akiwa tayali yupo kwenye nyumba nyingine kwani aliamini katu kampuni haitaweza kumkataza.
***********
Jioni ilipowadia Joeli alikodi gari ndogo ya mizigo,akiwa njiani alimpigia Naomi ili aandae baadhi ya vitu. Punde si punde kwa muda wa masaa mawili mchakato mzima wa kuhama ukawa umekamilika. Rasmi Joeli na mkewe wa kuitwa Naomi walihamia kwenye nyumba mpya,hiyo ni baada kuteswa na mauzauza ya hapa na pale kwa kipindi kirefu. Wapenzi hao waliamini kwamba kuhama nyumba ile ya mwanzo inaweza kupelekea kuishi kwa amani,na ukawa ndio mwisho wa kusumbuliwa na mauzauza. Hakika ilionekana ni nyumba nzuri sana ya kuvutia,nyumba ambayo ingemshawishi mtu yoyote kuishi humo. Mwanzo wa maisha mapya baina ya wapenzi ilikuwa raha mstarehe,hakuna kilichotokea chochote ambacho kiliweza kuwafanya kujutia kuingia katika nyumba hiyo. Hali hiyo ilimfanya usiku mmoja Naomi kuvunja ukimya na kisha kusema "Mume wangu Joeli,sasa nimeamini kuwa hii ndio ilikuwa dawa pekee ya kuyaepuka yale mauzauza na sio kwenda kwa mganga" Alisema Naomi. Joeli alikaa kimya kidogo halafu akajibu "Umeonaee,tena kwa uturivu huu wala hakuna haja ya kuleta mchungaji eti aombee nyumba. Nyumba iko powa kabisa" Alicheka Naomi baada kusikia jibu hilo la Joeli,na mara baada kukatisha kicheko chake akaongeza kusema "Kwanza unafikili ni mchungaji gani atakubali kupoteza muda wake kuja kuombea nyumba yako? Wakati we mwenyewe hapo ulipo hata mara moja hujawahi kudhulia kanisani" Alisema Naomi akibenza mtazamo aliotoa Joeli hapo awali.
Siku zilisonga,mambo yakiendelea kuwa shwari ndani ya nyumba hiyo mpya. Hatimae wiki mbili sasa zikakatika, furaha bado ikiendelea kutamalaki katikati yao Joeli na mkewe Naomi. Jambo hilo lilimfurahisha sana Naomi,hivyo akatamani habari hiyo njema amfikishie Shangazi yake. Joeli akiwa ofisini kwake mara ghafla simu yake ikaita, alipoitazama aliona ni Naomi ndiye aliyempigia. Haraka sana alipokea. "Joeli mpenzi pole na kazi" Ilisikika sauti ya Naomi ikisema ikimwambia Joeli. Joeli aliposikia maneno hayo matamu kutoka kwa mkewe,alivuta pumzi ndefu huku akijizungusha kwenye kiti kulia na kushoto kisha akajibu "Oooh! My love. Kazi zinaenda salama kabisa,sijui wewe ulivyoshinda hapo kwenye nyumba ya amani,nyumba ya hadhi ya juu isiyokuwa na papala yoyote " Maneno hayo ya Joeli yalimpelekea Naomi kuangua kicheko, alipokatisha akasema "Nzuri tu,aaamh unajua nini mpenzi? Nimemkumbuka sana shangazi yangu,kwahiyo nakupata taarifa kwamba natoka mara moja nakwenda kumuona"
"Ni vizuri mke wangu wala usiwe na hofu, cha kufurahia gari unayo kwahiyo kazi kwako" Alijibu Joeli. Baada ya hayo waliagana kisha Naomi akakata simu akajiandaa haraharaka akaenda kumtembelea Shangazi yake,wakati huo Joeli nae aliendelea na kazi mbali mbali hapo ofisini. Baadae kidogo alifunga ofisi tayali kwa safari ya kurudi nyumbani kupumzika,hakupita sehem yoyote bali alinyoosha moja kwa moja mpaka nyumbani kwake. Alipofika alimkuta Naomi akiwa sebuleni amekaa kwenye sofa,Joeli akashangaa sana na hivyo akamuuliza "Kulikoni hukwenda kwa shangazi?.." Naomi akatabasam kidogo halafu akajibu "Nimeenda,kwani vipi nimewahi kurudi?.."
"Ndio,lakini yote kwa yote ngoja nikabadilishe nguo nije unipe habari mpya kutoka huko kwa Shangazi " alisema Joeli na kisha akazipiga hatua kuelekea chumbani. Ajabu alipoingia chumbani alimuona tena Naomi,akiwa amekaa kitandani. Joeli alishtuka,akaogopa moyoni akajiuliza "Mbona sielewi? "Lakini hakupata jibu la swali hilo alilojiuliza na hivyo haraka sana alirudi sebuleni ambapo huko napo alimkuta Naomi yule yule akiwa na mavazi yale yale aliyovaa Naomi aliyemkuta chumbani.
Joeli alitaharuki kumuona Naomi mwingine sebuleni achilia mbali yule aliyemkuta chumbani,moyoni akajikuta akajisemea "Loh! Nimekwisha Joeli mimi" wakati huo huo Naomi yule aliyemkuta sebuleni alitabasam kisha akamuuliza "Vipi mbona hujabadilisha nguo?.." Joeli hakujibu. Mapigo yake ya moyo yalimuenda mbio,kijasho chembamba kikaanza kumtoka na punde si punde yule Naomi wa aliyemuona chumbani nae alitoka na kumfuata sebuleni,hivyo Joeli akajikuta yupo katikati ya Naomi wawili. Hofu maradufu ikaendelea kumpanda Joeli,alipiga kelele za kuomba msaada huku akiangalia upenyo pakuweza kupita ili atimue mbio. Alipata upenyo huo,kitendo ambacho kilimfanya akimbie mithili ya digidigi. "Mamaweee maweee Mamaeeee!" Aliita Joeli huku akiwa anakimbia ilihali muda huo Naomi nae alirejea kutoka kwa shamgazi yake, alishangaa kumuona mumewe anakimbia hovyo kana kwamba kapamdwa na wazimu. Naomi alikajaga bleki kisha akatelemka ndani ya gari, haraka sana akamkimbilia Joeli huku akipasa sauti ya kumuita. Joeli aliposikia sauti ikimuita aligeuka nyuma, akamuona Naomi. Akajua ni Naomi yule yule aliyekutana nae ndani hivyo aliongeza kasi ya mbio. "Ooh mungu wangu,Joeli kakutwa na nini jamani?.." alijiuliza Naomi akianza kwa kushusha pumzi. Baada ya hapo alirudi ndani ya gari moja kwa moja akaelekea nyumbani kwake.
"Magesa unajua mimi tayali ni mtu wa kuteseka sasa?.." CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanini ndugu yangu Joeli,kwani bado yale mauzauza bado yanakuandama?.."
"Daah yani we acha tu,ujue mwanzo wakati nahamia ndani ya nyumba ile hari ilikuwa shwari kabisa lakini leo nilichokutana nacho heeeh hata mungu hapendi"
"Umekutana na kitu gani ndugu yangu mpaka useme mungu hapendi "
"Leo wakati nipo job,shemeji yako alinipigia simu akadai kwamba anakwenda kumtembelea shangazi yake. Mimi nikamwambia hakuna shida we nenda tu. Sasa baadae kidogo nilifunga ofisi ili nakapumzike,heeh nilipofika tu nikamkuta shemeji yako kakaa kwenye sofa nikamuuliza kulikoni hujsenda? Akanijibu Nimeenda vipi nimewahi kurudi?. Ah mimi sikutaka kujaji sana ikabidi niingie zangu chumbani nibadilshe nguo, nilipoingia tu nikamuona tena shemeji yako. Nilishtuka kiukweli nikaogopa, haraka sana nikarudi sebuleni. Huko nikamkuta tena shemeji yako, muda mchache baadae yule niliyemuona chumbani nae akaja sebuleni Kwahiyo wakawa wawili wanaofanana. Daah nikasema msinitanie,nikatimua mbio hizo sio mchezo.." Alisema Joeli akimsimulia rafiki yake kile alichokutana nacho nyumbani kwake,kwani Joeli baada kutimua mbio alikimbilia kwa rafiki yake wa karibu kumpasha habari. Magesa alishangaa sana,alishtushwa na taarifa hiyo. Aliinamisha kichwa akitafakari ni kipi cha kufanya ili amsaidie rafiki yake. "Kwani nyumba yenyewe ipo maeneo gani?.." aliuliza Magesa. "Sinza kwa lemi" Alijibu Joeli. "Anhaa sawa,sasa bwana Joeli mpaka hapo nafikili ujanja huna,sikukatishi tamaa hapana. Ila kuna mganga mmoja hivi nafikili anaweza kukusaidia. Mganga mzuri sana ndugu yangu, yani namkubari sana zaidi ya sana. Huyo anaweza kukusaidia na endapo kama atashindwa basi anakwambia bwana jambo hili mimi siliwezi tafuta mtu mwingine akusadie..."
"Daah Magesa ndugu yangu twende hata sasa hivi bwana" aling'aka Joeli. Magesa alicheka kidogo halafu akajibu "Sahizi muda umeenda Joeli tufanye kesho sawa?.."
"Sawa,ila leo siwezi kulala nyumbani acha nikalale hotelini" Alisema Joeli kisha akaondoka zake,alienda mpaka kwenye kituo cha taxi. Hapo alikutana na kundi la vijana ambao kila mmoja alikuwa akimvua kwake "Bro Njoo upande pamba nyepesi,haraka sana nakufikisha uendako"
"Aaa kaka hilo goroka bwana,Njoo kwenye hii mpya full kipupwe"
"Njoo huku brother achana nao hao mimi nitakupunguzia dau "
"Oi kaka hii hapa pruuuumpaka maka" Vijana hao walisikika wakinadi magari yao ilimladi kuweza kumshawishi Joeli aingia kwenye gari nzuri. Lakini kwa kuwa Joeli alikuwa amechoka sana kutokana na balaa alilokutana nalo kulinganisha uchovu wa kazi,hakutaka kulemba mwandiko. Mtu wa kwanza alimfuata akamtaka afungue mlango wa gari,dereva taxi huyo alimfungulia Joeli mlango,-Joeli akaingia kisha nae alifungua upande wake akaingia na kuliwasha gari lake. "Mambo vipi bro! Unafika wapi?.." aliuliza dereva taxi. Joeli alishusha pumzi kidogo kisha akamuelekeza dereva huyo mahala pa kumpeleka. "Ok hapa hadi kule shilingi elfu kumi na tano tu" Aliongeza kusema dereva taxi baada kuifaham sehem hiyo aliyoelekezwa na Joeli. "Sawa twende " alisema Joeli.
Nje ya hoteli iliyoonekana kuwa na maadhali ya kuvutia, Joeli alishushwa hapo akamlipa dereva taxi hela yake kisha akazama ndani mapokezi akatia saini na akalipia chumba akakabidhiwa funguo. Lakini kabla hajaingia chumbani alihisi njaa,hivyo alitoka nje akaanda kujichanganya sehem iliyoonekana imejaza watu huku wakila na kunywa. Hapakuwa mbali na hoteli hiyo aliyochukua chumba Joeli. Alipokaa tu muhudumu alikuja kumsikiliza,ambapo Joeli aliomba manu akachagua chakula anachopendelea kula na punde si punde aliletewa. Kabla hajaanza kula, alichomoa simu yake akatafuta namba ya dalali Tito. Alipoipata akampigia lakini simu ya Tito haikupatikana,hivyo Joeli akaachana nae ndipo akaanza kula. Alipomaliza alirudi hotelini,moja kwa moja akazipiga hatua mpaka kwenye chumba alicholipia. Hakutaka kupoteza muda alilala kitandani huku akiwa amejifunika shuka kuanzia miguuni mpaka kichwani. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ilipofika aliamka ila ghafla alishtuka kujikuta yupo chumbani kwake na sio kwenye chumba cha hoteli aliyolipia usiku wa jana,hakika alishanga sana Joeli moyoni akajiuliza "Hapa si nyumbani kwangu?Nyumbani kwangu? Na je,nimefikaje hapa Nimefikaje hapa?" Alijiluliza huku akinyanyuka kutoka kitandani iliahali akionekana haelewi kilichotokea. Punde si punde Naomi aliingia chumbani, Joeli akashtuka wakati huo huo Naomi alisema "Ndio nilikuwa nimekuja kukuamsha mume wangu,najua leo ni mapumziko kwahiyo tupo wote nyumbani" Joeli hakujibu lolote zaidi alichukua simu yake akampigia Magesa. "Ndio najiaandaa kuja kukupitia hapo" Alisema Magesa baada kupokea simu "sawa" alijibu Joeli kisha akakata simu na punde si punde akanyanyuka akaelekea bafuni kuoga. Alipomaliza kuoga alikumbuka jana alimpigia dalali Tito akawa hapatikani hivyo alirudia tena kumpigia. Safari hiyo simu iliita,muda mchache baadae ilisikika sauti ya Tito ikisema "Hello "
"Ndio mzee wangu habari za siku nyingi" alisema Joeli.
"Salama nani mwenzangu? .."
"Mimi ni Joeli,yule kijana ulinitafutia chumba kipindi cha nyuma kidogo"
"Mimi sikufaham bwana kwanza mimi sio dalali, na siijui kazi hiyo bwege wewe" Alijibiwa Joeli na mtu huyo,Joeli alishangaa sana,lakini mwishowe aliishia kushusha pumzi na kisha akaendelea kujiandaa. Ila wakati anafanya hivyo,alihitaji kujua amefikaje nyumbani kwake ilihali alilala Hotelini,hivyo alimuita Naomi akamualiza "Mke wangu nimefikaje nyumbani? .." swali hilo lilimshtua Naomi ambapo alimtazama Joeli kisha akamjibu "Kwahiyo umesahau kama uliletwa na taxi?.."
"Aah kumbe? haya mke wangu nimekuelewa " alijibu Joeli huku akitabasam kwa mbali. Muda huo ghafla simu yake Joeli ikaita,alipoitazama akaona ni Magesa ndiye aliyempigia haraka sana akapokea "Enhee nielekeze sasa nipite wapi ili nije mpaka nyumbani kwako" Aliuliza Magesa,Joeli akampa maelekez kisha akakata simu. Baadae kidigo simu ya Joeli ikarudia kuita,safari hiyo alitoka ndani akasimama nje ambapo aliiona gari ya Magesa hivyo akapokea kisha akasema "Tazama kulia kwako Magesa kisha njoo " Wakati Joeli anamwambia Magesa maneno hayo,Magesa alitoka ndani ya gari ajabu aliona tu makaburi kulia na kushoto. Alipotazama upande wa kulia kwa mbali zaidi alimuona Joeli akiwa amesimama juu ya kaburi akinyoosha mikono ili Magesa apate kumuona. "Mungu wangu kumbe siku zote Joeli na mkewe wanaishi makaburini bila wao kujua?.." alijiuliza Magesa halafu akasema "Njoo bwana tuwahi muda umeenda" alisema hivyo Magesa kwani aliogopa kujitosa kwenye wigo ule wa makaburi. "Kwahiyo hutaki uje kuona mjengo ninao ishi rafiki yako?.." alihoji Joeli huku akizipiga hatua za pole pole kumfuata Magesa. Bado Magesa alionekana kushangazwa na maneno hayo ya Joeli, hivyo alirudia kujiuliza "Inamaana ni kweli Joeli hatambui kama anaishi makaburini?." Muda huo Joeli alimfikia sasa Magesa,walisalimiana kisha Joeli akamuonyesha Magesa nyumba anayoishi huku akijinadi kuwa mjengo mzuri sana,lakini ukweli ni kwamba Magesa yeye alikuwa haoni nyumba zaidi ya kuona Makaburi tu. Yote kwa yote wawili hao waliingia ndani ya gari,wakaanza safari ya kwenda kwa mganga kwa mara nyingine. Wakati huo huku nyuma,ghafla Naomi alijihisi tumbo kumuuma. Haikuchukua muda mrefu akatokwa na damu sehem ya siri,hapo alipiga mayowe kuomba msaada lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza kwani muda wote walikuwa wakiishi makaburini pasipo wao kujua. Hivyo Naomi aliendelea kusafa, baadae kidogo kilionekana kitambaa kikitoka Kwenye uke wake kikiwa kimelowa damu. Kitambaa hicho kilikuwa ni sanda, ambapo baada kutoka chote kilijivuta mpaka chooni kisha akatokea Siwa akiwa amekivaa. Mbele ya macho yake Naomi akamuona Siwa. "Ni wewe?" alihoji Naomi huku akitetemeka nguo zake zikiwa zimetapakaa damu. Siwa hakujibu zaidi ya kumdondoshea mkataba mbele yake baada ya hapo alisema "Huu ni wakati wa kuvuna ulichokipanda Naomi,huna nafasi ya kuishi tena hapa duniani. Kwani kufanya hivyo ni kuzurumu nafsi yangu. Hembu Tazama wapi ulipo?.." Naomi akainua shingo yake akatazama huku na kule,ghafla alishangaa kujikuta yupo kwenye Makaburi,aliporudisha uso wake chini hakumuona Siwa na wala hakujua mimba yake ilivyotoweka bali alijikuta mkataba anao mkononi,alitaharuki Naomi. "Nitamwambia nini Joeli" alijiuliza Naomi asiamini kilichotokea Hali hiyo ilimuogopesha sana,akatoka makaburini akitambaa mwili ukiwa umekosa nguvu,na punde si punde alichanganyikiwa baada usongo wa mawazo kuzidi kichwani akawa mwenda wazimu, popote utakapo muona utamkuta na mkataba wake. Upande wa pili Joeli na Magesa hawakufanikiwa CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kumkuta Maganga,hali hiyo sasa ilimuogopesha hasa pale baada Magesa kumwambia ule ukweli kwamba anaishi makaburini bila kujijua, Joeli alipokumbuka na majibu ya dalali alipompigia simu akaamini kuchezeshwa mchezo pasipo kujitambua, aliamini maneno ya Magesa ilihali muda huo huo kichaa Naomi alimzukia Joeli huku akicheka na mkononi akiwa na makaratasi,"Mungu wangu Naomi wangu mimi! Alisema Joeli akiwa ameweka mikono kichwani asiamini kama kweli ni Naomi anayemuona Karibu yake,na kibaya zaidi Naomi hakuwa na mimba. Hivyo Jambo hilo lilimshtua sana,muda huo huo kichaa Naomi alimtupia makaratasi Joeli usoni. Joeli alipoyatazama akaona neno mkataba, haraka sana aliyaokota akasoma akawa amebaini marehem mkewe ambae ni Siwa enzi ya uhai wake waliandikishiana mkataba na Naomi juu ya mapenzi yao,lakini mwisho wa yote Naomi akawa ameuvunja. Hakika Joeli aliumia sana,akajikuta akijutia maamuzi yake. Na yote kwa yote hakuona sababu ya kuendelea kuishi duniani,alijinyonga huku akimuacha Naomi duniani akisafa na uwenda wazimu na mkataba wa marehem Siwa. Miaka miwili baadae kichaa Naomi nae alifariki baada kugongwa na gari wakati akivuka barabara.!
Mshahara wa dhambi ni mauti.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment