Search This Blog

DHAHAMA - 1

 







    IMEANDIKWA NA :HASSAN O MAMBOSASA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Dhahama

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya simanzi ilikuwa imetawala katika eneo zima la kasri la kupendeza la kifalme katika himaya ya Majichungu inayopatikana katika bahari ya hindi, himaya hii ya kijini iliingia katika huzuni baada ya mfalme wao kuwa katika harakati za mwisho za maisha yake. Mfalm huyu aitwaye Zulain mwenye miaka yapata elfu tatu alikuwa katika ugonjwa kwa muda wa miaka kumi sasa leo ndiyo dalili za kufikia mwisho wa uhai wake zilionekana dhahiri kwa majini wote wa hapo kwenye kasri hilo. Akiwa kalala kwenye kitanda chake cha thamani kwa muda wa miaka kumi kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua ambao haujulikani, kwa mara ya kwanza aliinuka kitandani ghafla akakaa kitako kisha akasimama akaelekea kwenye kiti chake cha enzi akiwaacha watumishi wake wakiwa na simanzi sana. Kuugua mfalme kwa muda mrefu kisha kuinuka ghafla ni dalili tosha ya kuwa siku za mwisho za miaka yake zimekaribia, hivyo hata watumishi wa ndani ya kasri hili walitambua kuwa siku za mwisho za uhai wa mfalme wao zimekaribia.

    Hata mfalme mwenyewe alitambua kuwa ana masaa ya kuishi duniani au siku ya kuishi duniani hivyo alitaka kuongea maneno ya mwisho kabla roho yake haijaachana na mwili wake, alipokaa kwenye kiti chake jambo la kwanza kulitamka ilikuwa ni kuitiwa mawaziri wake wote pamoja na viongozi wengine waliopo chini ya utawala wake ili awaambie jambo la muhimu pamoja na kuacha kauli ya mwisho katika himaya yake. Amri ya kuitwa mawaziri na viongozi wa juu katika himaya yake ilitekelezwa mara moja na baragumu maalum likapulizwa kwa haraka sana na mpulizaji wake anayetoka katika himaya hiyo, ndani ya sekunde kadhaa chumba cha mkutano kilijaa mawaziri na viongozi wenye nyadhifa kubwa katika himaya hii ya kijini ambao walikuwa ni majini wa aina mbalimbali.

    "Himaya ya Majichungu inaelekea kukumbwa na simanzi kubwa kwani kiongozi wake niliyetawala kwa muda wa miaka 2500 nakaribia kufa na dalili kuu ya kufa kwangu nadhani imeonekana kabisa dhahiri kwenu na kwa watumishi wangu, sasa basi suala la kutafutwa mrithi wa taji langu na kiti changu cha enzi nawapa nyinyi. Nahitaji mjukuu wangu Zalabain ambaye ndiye mrithi wa kiti changu cha enzi na taji langu apatikane haraka iwezekanavyo kwa namna yoyote na afutwe popote alipo aletwe huku akabidhiwe jukumu lake la ufalme kwani mwanangu Zaif ambaye ndiye baba mzazi wa Zalabain hatunaye na wote mnatambua ni jinsi alivyougua hadi akata roho katika himaya hii. Sasa basi Zaif kabla hajafa alisema duniani yupo mjukuu wangu aitwae Zalabain, sasa inabidi huyo mjukuu wangu atafutwe.kwa hali yoyote hadi apatikane ili aje kuchukua wadhifa wangu kama mrithi pekee aliyebakia. Pia nahitaji mila na desturi za himaya hii zibaki kama nilivyozikuta na zisibadilishwe kwa namna yoyote na wala asitokee kiumbe akabadilisha au akamshawishi kiumbe yoyote abadilishe. Mwisho kabisa nahitaji Sadik bin Zultash baba wa mapacha Saliim na Salmin aachiwe huru kuanzia sasa kwani uzao wake kwa faida moja umetusaidia kwa kutuletea jini mwenye nguvu kuliko wote na anayeifanya himaya yetu isidhuriwe na kiumbe wa aina yoyote, sina la ziada ni hayo tu" Mfalme Zulain alihitimisha na kikao kikamalizika mara moja karibia viongozi wote wakatawanyika wakiwa na simanzi juu ya mfalme wao. Siku iliyofuata ilikuwa ya simanzi zaidi kwa himaya nzima ya Majichungu kutokana na kifo kilichomkumba mfalme wao, himaya nzima iliomboleza kifo hicho kwa muda wa wiki saba na baada ya hapo jeshi la majini watatu ambao ni makomandoo likaundwa kwenda kumtafuta Zalabain popote alipo ili aje kurithishwa ufalme wa babu yake.



    ****



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    WIKI MOJA BAADAYE

    USIKU WA MANANE

    AMBONI

    TANGA

    Eneo la miamba yenye mapango ya kihistoria jijini Tanga jirani kabisa na mto mkubwa Tanga nzima uitwao mto Sigi kulikuwa kuna kundi la vijana kumi waliokuwa wameuzunguka mti mmoja wa mkoko ambao unasadikika kuwa mti wa ajabu kutokana na kuota eneo ambalo lipo mbali na ufukwe wa bahari. Vijana hao walikuwa wameuzunguka mkoko huo ambao ulikuwa umening'inizwa chupa ya ukubwa wa lita moja ambayo ilikuwa ikijibadili rangi kila kukicha, walikuwa wamejifunga kaniki nyeusi kiunoni na vitambaa vyekundu kichwani na kwenye mikono yao. Muda wote walikuwa wapo makini kuitazama chupa hiyo pamoja na mazingira ysnayozunguka mto Sigi pamoja na upande wa mapango ya Amboni, walikuwa wapo kimya sana na umakini wao katika kuangalia mazingira ya hapo ndiyo ulizidi kwani walikuwa wanapambana na wachawi wa kila namna ili kuilinda chupa iliyopo hapo mtini ambayo huonekana usiku kwa wenye uwezo kuiona na mchana haikuonekana kabisa.

    Siku hiyo majira ya saa nane usiku vijana hao walimshuhudia Mamba mmoja mkubwa akitoka ndani ya mto Sigi na akakaka pembezoni mwa mto huo mita chache kutoka pale walipo, wote walimpuuzia mamba huyo kutokana na dawa zao wanazotumia hawezi kuwaona. Walibaki wakimtazama yule Mamba kwa jinsi alivyo mkubwa huku kuliko hata Mamba wote waliowahi kuwashudia katika mto Sigi tangu wakiwa watoto, mmoja kati ya wale vijana alishikwa na shauku ya kwenda kumtazama yule Mamba na akasogea karibu zaidi kwani dawa zao zilikuwa zinawazuia wasionwe na wanyama wakali. Alisogea akamtazama zaidi na akabaini ni mamba wa ajabu mwenye rangi tofauti na Mamba wa pale mtoni, akiwa anashangaa uajabu wa yule mamba ghafla alijikuta akipigwa mkia akatumbukia mtoni na mamba huyo naye akazama mtoni akiwaacha wale vijana waliobakia wakikimbia hadi pembezoni mwa mto wakiacha kuilinda ile chupa. Hilo lilikuwa kosa jingine kwao na hawakupata hata nafasi ya kulirekebisha kwa balaa lililotokea, kimbunga kikali kilivuma kuuzunguka ule kwa muda wa dakika kadhaa na kilipoacha ile chupa wanayoilinda ilikuwa imepasuliwa tayari. Kabla hata hawajatafakari kitu cha kufanya maji ya mto Sigi nayo yalianza kuzunguka kisha yakanyanyuka juu urefu wa mlima huku yakizunguka na yakatengeneza umbo la jitu kubwa ambalo mkono mmoja lilikuwa limemshikilia kijana yule aliyepigwa mkia na Mamba akaingia mtoni. Vijana walipoona hivyo wakajua wameingiliwa na kazi yao imeshaharibika hivyo walitaka kukimbia ili kujiepusha na hatari kwani viumbe waliowavamia sio wa kawaida, walikimbilia upande lilipo pango wakijua ni salama kwao ili wapate sehemu ya kutorokea. Walipokaribia kuingia pangoni walikutana uso kwa uso na nyoka mwenye vichwa kumi na ikawabidi wakimbilie mtoni kwa upande mwingine bila ya kutambua wanajipeleka kwenye eneo la kifo, vijana hao walijitupa mtoni kwenye maji wakiwa wanataka kuokoa maisha yao tu na wala hakukumbuka kuwa dawa waliyojipaka ya kuzuia wasidhuriwe na wanyama wakali inatoka mwilini ikiwa utaingia kwenye maji. Walipokuja kukumbuka tayari walikuwa wamezungukwa na mamba zaidi ya kumi wa mto huo, walikuwa wamejirusha sehemu yenye maskani ya Mamba bila ya kujijua na wakawa kitoweo cha Mamba.



    ****



    Sherehe kubwa ilifanyika katika kasri la kifalme la Majichungu katika kusherekea kupatikana kwa mjukuu anayepaswa kurithi kiti na taji la ufalme wa babu yake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mjukuu huyo mwenye mchanganyiko wa binadamu na jini kufika katika himaya tangu azaliwe. Sherehe ilipoisha ndipo taratibu zote za kimila na desturi za kumpatia ufalme Zalabain zikaandaliwa kama ilivyofanyika kwa wafalme waliopita. Siku iliyofuata sherehe nyingine ya kuvikwa taji la ufalme ilifanyika katika uwanja mkubwa uliopo nje ya kasri la kifalme ambayo ilihudhuriwa na wanahimaya hiyo karibia wote, kiti cha kifalme kilitolewa kikawekwa sehemu yenye jukwaa lililopambwa kwa busati lenye rangi nyeupe. Muda wa kuvikwa taji Zalabain ulipowadia Mkuu wa baraza la sheria la himaya hiyo aliingia akiwa amebeba taji la kifalme liliwekwa kwenye kasha lililopambwa na fito zenye rangi nyekundu, Zalabain akiwa nyuma ya Mkuu huyo wa baraza la sheria pembeni yake akiwa na walinzi wenye miili mikubwa pamoja na sura za ajabu. Zalabain na mkuu huyo walipanda katika jukwaa lenye kiti cha kifalme huku mamia ya wanahimaya ya Majichungu wakishangilia kwa nguvu, aliamriwa aketi kwenye kiti cha ufalme naye akatii akaketi na Mkuu wa baraza la sheria akashika kasha lenye taji la kifalme akasogea kisha akawageukia Wanahimaya ambao wapo hapo kushuhudia tukio hilo.

    "Leo ni siku maalum na ya kihistoria ya kumpata kiongozi wetu aitwae Zalabain bin Zaif atakayeiongoza himaya yetu akirithi utawala wa Babu yake Zulaif, akiwa na miaka 26 tu atakuwa kiongozi mdogo kuwahi kutokea katika Himaya yetu hii hivyo naomba mumpokee" Mkuu wa baraza la sheria aliongea kisha akamgeukia Zalabain ambaye tayari ameshavaa mavazi ya kifalme akawa anatazama nae.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwa mamlaka niliyokabidhiwa ninakukabidhi na kukuvisha taji hili la Kifalme litakalokufanya uwe mfalme, miongoni mwa wafalme, wa ukoo wa kifalme, waliowahi kuwa wafalme, uwe kiongozi wa kasri la kifalme. Zalabain sasa wewe ni mfalme wa himaya ya Majichungu" Mkuu wa baraza la sheria alipomaliza kusema maneno hayo aliliweka taji kichwani mwa Zalabain huku halaiki ya wanahimaya wakishangilia, kushangalia huko kulizimika ghafla mithili ya umeme unavyozimika eneo lenye giza. Wote walibaki wameduwaa baada ya taji la kifalme lililowekwa kichwani mwa Zalabain kuruka kando likaanguka kwenye busati lililotandazwa hapo jukwaani. Mkuu wa baraza la sheria aliona ni jambo la kawaida sana na aliinama akalishika ili alinyanyue lakini taji halikuinuka na lilikuwa zito sana na ikambidi alishike kwa mikono miwili na akashindwa kuliinua vilevile. Aliamua awaite wale walinzi walioingia na Zalabain walinyanyue nao wakashindwa pia kulinyanyua eneo hilo. Wanajeshi wanaoaminika wana nguvu sana nao walishindwa kulinyanyua taji hilo, Zalabain mwenyewe alibaki akiwa anashangaa kwa tukio hilo ambalo hakulielewa limetokana na nini.

    Mnajimu mkuu wa Himaya hiyo aliitwa mara moja na akapewa kazi ya kulitatua tatizo hilo kwani yeye ndiye anayeaminika katika himaya hiyo, mnajimu huyo wa kijini alianza kulizunguka taji hilo la kifalme kisha akajaribu kuliinua lakini alishindwa kabisa na akaanza kubadilisha macho yake yakawa kama ya paka akamtazama Zalabain.

    "Siyo uzawa wa ukoo wa mfalme huyu ndiyo maana taji limemkataa na wala siye mtoto halisi wa Zaif, taji hili linahitaji abadilishwe kiongozi kwani kizazi cha ukoo wa mfalme alibaki Mfalme Zulain tu ambaye amefariki tayari. Ufalme unatakiwa uhamishwe katika koo nyingi.." Mnajimu alishindwa kumalizia kauli yake na akajikuta amepigwa kofi zito hadi akaanguka chini, akiwa hajajua nani aliyempiga akahisi anakabwa shingoni huku akinyanyuliwa juu. Walinzi walipoona hali hiyo walitaka kusogea ili wamdhibiti kiumbe anayemkaba Mnajimu mkuu lakini walisita baadaya kiumbe mwenyewe kujitokeza hadharini, Salmin ambaye anajulikana na wanajamii hiyo kama jini mwenye nguvu kuliko wote ndiye aliyeonekana akimkaba Mnajimu huyo shingo.

    "Kwanini unasema uongo ilihali wewe ni Mnajimu unayeheshimiwa na kuaminiwa katika himaya hii" Salmin alimuuliza Mnajimu huku akizidi kumkaba, Mnajimu aliomba aachiwe ili aongee na alipoachiwa ndipo akamwaga uhalisia wa jambo lenyewe.

    "Wanahimaya na wakuu wote naomba mnisamehe sana kwa kusema uongo juu ya mjukuu wa mfalme, tamaa ya madaraka ndiyo imesababisha niseme uongo. Niliahidiwa kupewa nafasi ya mkuu wa baraza la sheria ikiwa tu nitafanya hila ufalme uhamishiwe katika ukoo wa waziri mkuu ili waziri mkuu awe mfalme wa Himaya hii, narudia tena viongozi wangu na wanahimaya wenzangu naomba mnisamehe kwani mimi nina nafsi na tamaa ni kitu cha kawaida kwa mwenye nafsi" Mnajimu alitoa maelezo hayo akiwa na aibu usoni kutokana na jambo alilolifanya, kuomba kwake msamaha hakukusaidia kitu kwani alikamatwa yeye na Waziri mkuu baada ya mkuu wa baraza la sheria kutoa amri hiyo. Baada ya kukamatwa kwa Waziri mkuu na Mnajimu mkuu Salmin alilitazama taji la kifalme kisha akamtazama Zalabain kwa umakini, macho yake yalianza kutoa nuru mithili ya almasi iliyomulikwa na mwanga mkali.

    "Zalabain.......Zalabain mrithi wa kiti cha mfalme aliyestahiki kuvishwa taji la ufalme wa himaya hii lakini taji limemkataa kutokana na jambo moja tu ambalo mrithi wa kiti hiki hatakiwi kuwa nalo kabisa ambalo wewe unalo, udhaifu.....udhaifu wako ndiyo chanzo cha taji hili kukukataa. Ikiwa unatakiwa kuwa mrithi wa taji hil na kuna ubaya ambao umetendewa unatakiwa ulipe kisasi kwanza na si kusamehe ili upate taji hili, baba yako Zaif ameangamizwa na wanadamu akiwa na miaka 1500 na wanadamu hao ndiyo chanzo cha taji hili kukukataa na pia kuwa zito kuinuka kwa yoyote mwenye wazo la kuliweka kichwani mwako. Kisasi cha ubaya uliofanyiwa ndiyo kinahitajika ili hili taji likae kichwani mwako na hakuna mwingine atakayelivaa isipokuwa wewe, unapaswa utambue kwamba himaya hii yote inahitaji kiongozi na haiwezi kuendelea bila kiongozi na pia kiongozi ni wewe unatakiwa ulipe kisasi ili watu wako uwaongoze na si usamehe wapotee. Je upo tayari kuongoza himaya hii?" Salmin alifafanua chanzo cha kutokea jambo lililotokea kisha akamuuliza Zalabain.

    "Nipo tayari kuongoza, nipo tayari kisasi cha kuuawa kwa baba yangu na nipo tayari kulipa kisasi cha ubaya uliotendwa kwangu" Zalabain aliongea huku macho yakibadilika na kuwa mekundu kabisa na yenye kung'aa, Salmin alimsogelea akamshika mkono kwa sekunde kadhaa kisha akamuachia halafu akamuambua "kazi njema". Salmin aliliokota taji la kifalme akamkabidhi Mkuu wa baraza la sheria kisha akaondoka, sherehe hizo ilivunjwa hapohapo na Zalabain akahitajika atimize kile alichoahidi mbele ya majini wote wa himaya hiyo.



    ****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi ya siku iliyofuata tangu litokee tukio la kutoveshwa Zalabain taji, wafanyakazi wa kampuni ya upangishaji nyumba iitwayo Extoplus walikuwa wanasafiri kuelekea katika kijiji cha Duga Maforoni kwenda kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa nyumba mpya za kupangishwa za ksmpuni hiyo. Siku hiyo wafanyakazi wote waliotakiwa kwenda kwenye sherehe hiyo walijawa na hofu, karibu kila mfanyakazi alikuwa anasita kwenda anasita kwenda kwenye sherehe lakini hawakuwa na uwezo wa kukataa kwani ni idara nzima imeteuliwa kuhudhuria sherehe hiyo. Saa mbili kamili wote walikuwa kwenye basi wakielekea Duga kuhudhuria sherehe hizo, ndani ya basi kimya kilitawala kuanzia mwanzo wa safari na kilikuja kuvunjwa baada ya gari aina ya toyota coaster waliyokuwa wanaitumua kuvuka daraja la Utomfu. Mwanamke mmoja wa makamo alivunja ukimya uliopo ndani ya gari kwa kusema, " jamani mimi jana usiku nimeota ndoto ya ajabu sana".

    "mmh! Hebu tueleze ni ndoto gani hiyo" Mwenzake aliyekuwa pembeni naye alidakia.

    "nimeota nashuka kwenye gari natoka kazini nikakutana na mtoto wa miaka sita hizi akaniamkia kwa uchangamfu na mimi nikaitikia, yule mtoto kaniuliza unaujua mtego wa panya mimi nikamjibu ndiyo. Akaniuliza je kiumbe chochote kikiugusa unamnasa au unanasa panya tu, nikamjibu yoyote akiugusa ananaswa haijalishi kama Panya au siyo panya. Nilipomjibu akatabasamu nikamuuliza mbona umeniambia hivyo, akanijibu safari yako ya kesho Duga ni mtego wa panya ukienda utanasa ingawa wewe sio panya. Nimeshtuka usingizini hapohapo nikawa najiuliza kuhusu ndoto hiyo jamani ina maana gani" Yule mwanamke alieleza ndoto yake na alipomaliza wafanyakazi wote walikuwa wameingiwa na woga hapohapo.

    "jamani hata mimi hii ndoto nimeiota" Mwanamke mwingine akadakia huku akionesha kuogopa.

    "hata mimi" Mwanaume wa makamo ambaye ni mmoja wa wafanyakazi hao naye akadakia na mwishowe wote kwa pamoja wakatamka kwamba wameiota ndoto hiyo na hofu ikawa imetawala nafasi zao huku wengine wakimsihi dereva ageuze gari wasiende. Walikuwa wameshafika Amboni na sasa wapo kwenye daraja la kulia la mto Sigi hivyo dereva alikuwa yupo makini kulimaliza daraja hilo na hakuwasikiliza kabisa, baada ya kulipita daraja ndipo dereva akasema "jamani hata mimi nimeota ndoto ya namna hiyo lakini nimeipuuzia kwani si kila ndoto ni ya kweli".

    "unasemaje wewe hebu simamisha nishuke nipande mabasi yanayotoka Horohoro nirudi mjini" Mwanamke yule aliyeeleza kuhusu ndoto alikuja juu.

    "sawa ngoja tufike Mpirani kwenye kituo ili upate hilo gari" Dereva akimwambia yule mwanamke lakini hakutaka kumuelewa.

    "simamishe gari nakuambia!" Yule mwanamke alizidi kufoka, dereva hakuwa na jinsi ilimbidi akanyage breki lakini gari ilikataa na ndiyo mwendo ulikuwa unazidi na usukani ikawa unajiongoza wenyewe.

    "we mwanaharamu wewe simamisha gari nishuke sio kuongeza mwendo" Yule mwanamke alizidi kufoka baada ya kuona mwendo wa gari unazidi kuwa mkali, dereva hakumjibu yule yeye alitoka kwenye usukani akasimama kisha akawaangalia wafanyakazi wa idara nzima akiwa na hofu.

    "si mimi ninayeendesha jamani gari linaenda lenyewe hili hebu oneni" Dereva aliongea huku akiwaonesha wafanyakazi wote jinsi usukani ulivyokuwa unajiongoza wenyewe, wafanyakazi wote walipoona hicho kioja walijikuta wakijaribu kutoka nje lakini walishindwa kwani milango haikufunguka na vioo vyote vilijifunga ghafla hata vile vilivyokuwa wazi vyote vilijifunga. Wafanyakazi wote walijaribu kupiga vioo ili wavunje lakini walishindwa kwani vioo vilikuwa vigumu sana, gari nayo ilizidi kuongezeka mwendo hadi ikawa kama ipo kwenye mashindano.



    ****



    Makelele ya woga ndiyo yalitawala kwa watu wote kasoro kijana mmoja ambaye ni mmoja kati ya wafanyakazi wa idara hiyo ya kampuni ya Extoplus, yeye alikuwa kauchapa usingizi na wala hakunekana kama anatambua kuna tatizo, mwendo wa gari ulivyozidi kuwa mkali ilibidi wamuamshe huku wakimpigia kelele hadi akaamka. Kijana huyo alipoamka alionekana kukerwa na sauti za watu waliokuwa wanampigia kelele, kisha akalala tena akionekana kazidiwa na usingizi.

    "We Saleh hebu amka si tupo kwenye hatari we unalala,.amka tusaidiane kutoka ndani ya gari hili tutakufa wote" Yule mwanamke aliyekuwa aking'ang'ania kushushwa alipaza sauti kumuambia yule kijana aamke aache kulala wapo hatarini, yule kijana aliinua kichwa mara ya pili akiwa anaonekana kama mtu ambaye alikuwa hajalala na hana dalili ya kusinzia. Saleh alikuwa amejawa na tabasamu alipoinua uso wake hadi wenzake wote wakawa wanamshangaa sana, wenzake walipozidi kumtazama kwa hofu yeye aliangua kicheko kabisa akionekana kufurahishwa na hofu ambayo imevamia nyuso za wenzake. Alipoona wamezidi kumshangaa aliamua kuwaambia, "mtakufa nyinyi ila sio nitakufa mimi". Kauli hiyo ilizidi kuwashangaza sana wenzake waliokuwa wana hofu na kifo, wote walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa kwani si jambo la kawaida kwa mtu mwenye akili timamu kutamka maneno hayo katika eneo la kuelekea kwenye mlango wa kifo.

    "We Saleh ni wewe kweli tunaokujua ni muoga au umechanganyikiwa tayari?" Mwanamke mwingine aliyekaa pembeni yake alimuuliza akionekana kuchanganywa na kauli ya Saleh.

    "ushasema Saleh ni muoga sasa, utaulizaje ni Saleh au siyo wakati unaona kabisa mimi siyo muoga, labda jibu la kukusaidia ni kwamba Saleh yupo nyumbani kwake Mikanjuni amepumzika baada ya kuota ndoto iliyokuwa na onyo juu ya safari hii aliyoizingatia lakini nyinyi mnaojifsnya wapuuzaji wa mambo kisa elimu zenu leo utakuwa mwisho wenu" Yule kijana aliyesadikika kuwa ni Saleh alianza maneno yaliyozidi kuwashangaza wafanyakazi wote pamoja na dereva wa gari. Mwanamke mmoja aliyekaa pembeni yake yule kijana akiwa upande wa dirishani aliamua kumtandika makofi mawili mazito ya mashavu huku akisema, " hebu amke Saleh nahisi umelala bado".

    "Nishaamka tayari ngoja nikulaze wewe sasa ulale milele" Yule kijana aliongea kisha akampiga yule mwanamke ngumi moja ya kichwani juu kidogo ya sikio, ngumi hiyo ilitoboa kichwa cha huyo Mwanamke na ubongo wake uliochanganyika na damu ukaruka hadi kioo cha dirishani na kuibadilisha taswira ya eneo la karibu na hapo kuwa damu na madonge ya ubongo yakiwa yameruka hadi kwa wengine waliopo jirani na endo hilo. Mayowe ya uoga yalizidi ndani ya gari hilo huku watu karibia wote wakitamka majina ya mama zao kutokana na tukio waliloliona, Yule kijana alipoona makelele yamezidi aliamua kunyanyuka akawatazama wafanyakazi huku macho yake yaking'aa kama macho ya paka. Mikono yake ilianza kutoa kucha ndefu kama za Simba na sura yake ikabadilika ikawa ya kutisha, mabegsni alitoa mabawa kama ya popo na kinywaji akawa anatoa cheche za moti pamoja na mngurumo unaoashirua hasira.

    "Kwa jina la yesu pepo mchafu usiyehitajika tokaaaaa!" Mwanaume mmoja ambaye alikaa kiti cha nyuma kabisa alipaza sauti huku akimnyooshea mkono yule kijana ambaye muda huo alikuwa amegeuka kiumbe wa ajabu, Yule kiumbe aliangua kicheko huku akimtazama yule Mwanaume kwa jinsi anavyobabaika kukemea kama Mlokole.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ha! Ha! Ha! Ha! Yaani kila siku unashinda bar ukinywa pombe na unamuasi Mungu kwa kila unachokifanya na Kanisani kwako ni kama kituo cha polisi kwa teja ndiyo utegemee ukikemea nitaondoka. Mungu hasaidii watu kama nyinyi ambao mmeshindwa hata kumtaja mkiwa na tatizo . Mnashuhudia huyu mwenzenu nikimuua na mmekimbilia kuwataja mama zenu kama ndiyo mnaowaabudu. Sasa naanza na wewe unaejifanya kimbelembele sana" Yule kiumbe aliongea kisha akamnyooshea mkono yule Mwanaume aliyekuwa anakemea, yule mwanaume alijikuta akivutwa kuufuata ule mkono kwa kasi ya ajabu na alipoukaribia mkono wa yule kiumbe aliachiwa pigo moja takatifu lililomgawanya vipande viwili mithili ya papai linalotayarishwa kwa ajili ya kutolewa mbegu ili liliwe. Tukio hilo lilishuhudiwa na kila mmoja humo ndani na hadi wanashuhudia vipande vya mwili vya yule mwanaume vikianguka chini tayari mwanamke aliyekaa kitu kilicho jirani na yule kiumbe alikuwa ameshapoteza fahamu papo hapo kutokana na mshtuko wa moyo na akaanguka jirani na miguu ya yule kiumbe akiwa hajitambui, yule kiumbe alimtazama yule mwanamke kisha akaachia pigo la kutumia mguu wake lililoshuka kwemye shingo ya yule mwanamke hadi kichwa kikaruka na damu zikaanza kusambaa ndani ya gari ikiweka taswira isiyopendeza.

    "huyu peke yake ndiyo kafa kifo cha kistarabu akiwa hana fahamu ila nyinyi mtakiona cha mtema kuni" Yule kiumbe aliongea kisha akanyanyua mikono yake juu, watu wote nao walienda juu wakajipigiza kwenye paa la gari hiyo. Yule kiumbe alipoirudisha mikono yake chini watu nao walirudi chini wakijipigiza kwenye sehemu za juu viti ambazo hutengenezwa kwa chuma kilichovikwa godoro gumu. Sauti za kuvunjika kwa viungo vya ilisikika walipojipigiza kwenye viti huku mayowe ya maumivu yskitawala ndani ya gari ambayo yalimfanya yule kiumbe apeleke mikono yake juu na chini kwa haraka na watu walizidi kujibamiza kwenye paa na kwenye viti.

    Waliendelea kubamizwa hivyo kwa mara nyingi hadi wakawa wamevunjika kila viungo vya miili yao na wakawa hawawezi hata kunyanyuka, baadhi ya wafanyakazi walikuwa kwenye hali mbaya kwani mifupa yao mingine iliyovunjika ilikuwa imetoka nje ya miili iliyowaletea maumivu makali yaliyowafanya walie kama watoto wadogo.

    "Sasa nyinyi wa kupuuzia mambo nataka mfe huku mjiona kwa kuungua moto" Yule Kiumbe alisema huku akiwasha moto kwenye kiti cha mbele pembeni ya dereva halafu akatoweka huku gari likizidi mwendo kuliko uwezo wa mwendo wake.

    Gari hiyo aina ya toyota coastar ilikuwa imeshafika maeneo ya Bwaga Macho ambapo mbele kulikuwa na gari kubwa la mafuta likitembea kwa mwendo wa tararibu sana kutokana na uzito uliolielemea, gari iliyobeba wafanyakazi ilienda kugonga gari la mafuta kwa nyuma na kupelekea gari tanki la mafuta litoboke na mafuta yavujie ndani ya gari lililobeba wafanyakazi ambalo tayari moto ulikuwa unaunguza kiti cha mbele.

    Kilichofuata hapo ulikuwa ni mlipuko mkubwa hadi gari zote mbili zikarushwa juu huku zikiteketea, zilipotua chini ziliteketea zote hadi zikabaki mabati tu kutokana na kikosi cha zima moto kuchelewa kufika eneo hilo vikitokea Chumbageni wilaya ya Tanga.



    Ilikuwa kizaazaa kilichozaa vizaazaa vingine kwani wakati tukio hilo linatokea hilo linakaribia kutokea tayari waganga wa jadi wa eneo lote la Bwaga Macho walishaona kwamba kuna kiumbe wa ajabu aliyekuwa anawatesa wanadamu ndani ya gari, walihitaji kuwakomboa wanadamu waliopo ndani ya gari hiyo kwa kupambana na kiumbe hicho. Wakati yule kiumbe anaweka moto kwenye kiti cha ndani ya basi la wafanyakazi halafu anapotea ndani ya gari lile ili aondoke, alikutana na makombora kumi ya kwa pamoja kutoka kwa waganga kumi tofauti ambayo yalimrudisha nyuma hatua kadhaa lakini hayakumdhuru. Alipoangaza vizuri aliona kundi la waganga wapatao kumi wakiwa wanaelea hewani wakiwa waejifunga kaniki nyekundu viunoni na vilembe vyeusi, waganga hao tayari walikuwa wamemzunguka tayari wakitaka kummaliza kwa pamoja. Waganga hawa hawakutambua kuja kwao hapo ni kujiingiza katika vita isiyowahusu, wao walichojali ni kupambana na kiumbe aliyesababisha kuteseka kwa wanadamu wasiowajua. Wakiwa wanapanga kuachia makombora mengine yule kiumbe alijizungusha kama pia na kikatokea kimbunga kikali kilichowazoa wote kwa pamoja, uzito wa kimbuka hicho ukisababisha hata viti vilivyokuwa jirani na hapo kupeperushwa huku waganga wakitoa mayowe ya maumivu wakiwa wapo ndani ya kimbunga hicho. Hadi magari yanalipuka kimbunga hicho bado kilikuwa kipo angani na hadi yanateketea yanaisha bado kilikuwa angani kikizunguka huku sauti za watu wakilia kwa maumivu zikisikika, tukio hilo lilishuhudiwa na kila mtu aliyekuwa eneo hilo ingawa hawakujua hizo kelele ni za kina nani. Kimbunga hicho kilipoanza kupungua ndiyo wakashuhudia lita nyingi za damu iliyokuwa ina vipande vya nyama pamoja na mifupa ya binadamu ikidondoka barabarani na kulifanya eneo zima liwe kama machinjioni na kupelekea baadhi ya watu wasio na uatahimilivu wa kushuhudia vitu kama hivyo kukimbia huku wengine wakuzirai hapohapo baada ya kuona mafuvu ya binadamu yakiwa yametapakaa damu katika hali ambayo si rahisi kutazamika.



    ****



    Jirani na uwanja wa mpira wa miguu uliopo jirani na njia ziendazo katika bwawa maarufu la Duga maforoni linalotumiwa na wananchi wa eneo lote la Maforoni kulikuwa na nyumba za kisasa kama ishirini zilizojengwa na kampuni ya Extoplus ambazo zilikuwa zinazinduliwa katika siku hiyo ambapo sherehe ya uzinduzi ilikuwa inasubiri wafanyakazi kutoka makao makuu wafike ili sherehe hizo zianze. Wageni na waandaaji wa sherehe hiyo walisubiri hadi ilipotimu saa sita adhuhuri lakini hawakuona dalili za kufika wafanyakazi hao, ilipopigwa simu makao makuu ya kampuni ya Extoplus walipewa taarifa ya wafanyakazi hao kuondoka ofisini tangu saa mbili asubuhi. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya sana waandalizi wa sherehe hiyo na ikawabidi watume kikosi cha watu kumi wakiwa ndani ya gari kwenda kufuatilia kilichowapata wafanyakazi hao, gari ya kampuni ya Extoplus nyingine aina ya landcruiser prado iliondoka Duga maforoni kwenda kufuatilia gari ya kampuni iliyokuwa imebeba wafanyakazi wa kampuni yao. Watu waliotumwa kwenda kufuatilia wenzao nao hawakufika mbali kwani walivaana foleni kubwa ya barabarani walipokuwa wapo katika daraja liliopo katika barabara hiyo ya Mombasa ambalo linajulikana kwa vibweka vyake ambavyo vilitokea mwaka 2003 katika ujenzi wa madaraja na uboreshwaji wa madaraja, moja ya vibweka vyake ambavyo vinasemwa na wakazi wa jiji la Tanga vilivyowahi kutokea ni mashine za kupimia wakati wa ujenzi kutofanya kazi na ikapelekea mwaka huo ujenzi wa madaraja ufanyike na daraja hilo kushindikanika kujengwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kikosi cha wafanyakazi kumi kilichotumwa kuangalia wenzao kiliishia hapo darajani ambako kuna lami baada ujenzi wa mara ya pili kufanikiwa kujenga, magari ya hapo darajani yalikuwa hayaendi kabisa.na ikawalazimu washuke waulize kujua kipi kilichosababisha magari hayo yakwame, walipoambiwa chanzo cha kukwama kwa magari hayo walijikuta wakikodi pikipiki kila mmoja wakienda kushuhudia wenyewe kilichotokea huku gari wakimuachia mmoja aliyekuwa dereva ambaye aligeuza akarudi.







    SURA YA PILI

    Utepe mwekundu tayari ulikuwa umezungushwa katika eneo la barabarani lenye damu pamoja na mifupa ya binadamu na barabara yote ilikuwa imefungwa , askari wa jeshi la polisi vikosi vitatu tofauti walikuwa wamefika hapo wakiwa wanafanya kazi yao katika eneo la tukio. Kulikuwa kuna askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakipima kwani inasadikika kuwa chanzo cha tukio hil ni ajali, kulikuwa kuna askari kanzu kutoka kitengo cha CID (criminal investigation department) ambao walikuja kuchunguza juu ya tukio hilo ambalo pia lilihusisha mauaji kutokana na uwepo wa mabaki ya miili ya binadamu. Kikosi cha mwisho cha jeshi la polisi tayari kilikuwa kimechelewa kufanya kazi yao kwani magari yote yalikuwa yameshateketea kwa moto kabisa, kikosi hichi cha jeshi la polisi cha zima moto kilifanya kazi tu ya kutoa miili ya watu waliokutwa katika magari hayo ambayo haikutambulika na kuipakiza kwenye magari ya wagonjwa ya hospitali kuu ya Bombo ambayo tayari yalikuwa yameshafika eneo la tukio. Askari wa CID waliochukua maelezo kwa mashuhuda wa tukio hilo walijikuta wakiwa na walakini mkubwa juu ya maelezo hayo kwani yalikuwa yametawaliwa na imani za kishirikina hasa baada ya kusikia juu ya kimbunga kilichodondosha damu nyingi iliyochanganyika na vipande vya nyama pamoja na mifupa, mashuhuda wengi wa tukio hilo walisema watu waliouliwa katika tukio hilo la kimbunga ni waganga kwasababu ya kuonekana kwa mavazi kiganga kuonekana pamoja na vitu kadhaa vya kiganga. Mashuhuda wengine wa tukio hilo walikuwa ni wasaidizi wa waganga ambao walithibitisha waliokuwa kwenye tukio hilo ni waganga waliokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wapo ndani ya gari iliyoungua moto. Maelezo yao yalionekana kuwa hayana maana mbele ya jeshi la polisi kwani polisi na serikali nzima ilikuwa haiamini uwepo wa wachawi au uchawi hivyo waliyapuuzia maelezo yao.



    ****



    Kundi la vijana kumi ambao sasa wamebaki tisa baada ya mmoja wao kugeuza na kurudi na gari lilifika Bwaga Macho kwa msaada wa pikipiki tisa walizozikodi, kitendo cha kushuka kwenye pikipiki zao mmojawapo aliona kibao cha namba za gari kilichokuwa kipo kwenye majani na ikamlazimu akiokote akiangalie. Alijikuta akishtuka sana baada ya kubaini ni namba ya gari la kubeba wafanyakazi la makao makuu, yule mtu aliwaonesha wenzake akionesha haamini kama ni namba za gari la kampuni au siyo.

    "hizi namba za usajili za staff bus namba 5?" Aliwauliza wenzake huku akionekana kutoamini.

    "eeh! Ndiyo zenyewe kabisa, hebu chekini hii picha niliyopiga mbele ya staff bus namba 5" Mwingine alikiri kuwa namba ya basi hilo kisha akatoa simu yake akawaonesha picha ya mbele ya aliyoiseti kwenye simu yake ambayo hujulikana kama wallpaper kwa lugha ya kigeni, walipoiona hiyo picha waliamua kukimbia kuelekea enro lilipotokea tukio. Waliyaona magari mawili yaliyoungua yakiwa yapo jirani na dimbwi kubwa la damu lililokuwa limeanza kukauka tayari. Dimbwi hilo pamoja na magari yaliyoungua yalikuwa yamezungushiwa utepe ili kuzuia watu wasiingie. Vijana hawa walijikuta wakitaka kuingia katika eneo liloozungushiwa utepe lakini askari hao waliwazuia na kuwaelewesha wapo kazini lakini vijana hawa hawakutaka kabisa tena mmoja wao ndiyo alionekana kutaka kufanya fujo na mwisho wake wote wakawekwa chini ya ulinzi. Walipelekwa hadi upande wenye askari wengi wakawekwa chini ya uangalizi wa askari na mmoja kati ya wale vijana alikuwa muda wote alikuwa akilia huku akiiangalia gari ya abiria ambayo ilikuwa imebeba wale wafanyakazi kutoka idara moja ya makao makuu ya kampuni ya Extoplus.

    "Hebu nyamaza mtoto wa kiume wewe unalialia nini" Mmoja wa maaskari ambao alikuwa akiwangalia hawa vijana wa kampuni ya Extoplus alimwambia yule kijana aliyekuwa analia.

    "mama yangu yupo ndani ya gari lililoungua sasa wewe ulitaka nicheke" Kijana alimjia juu yule askari aliyekuwa anamwambia hivyo.

    "kijana una uhakika gani kama gari lile ndiyo mama yako alikuwemo?" Yule askari aliuliza.

    "uhakika ninao kibao cha namba za gari hiki hapa tumekiokota kule kwenye majani" Aliongea yule kijana kisha akampatia askari kibao chenye namba za usajili wa gari.

    "tena askari gari yenyewe ni hii hapa niliwahi kupiga nayo picha" Kijana yule aliyeiweka picha ya gari la wafanyakazi kwenye simu yake akiwa amepiga nalo picha naye aliongea huku akimuonesha askari picha aliyoipiga na ile gari yenye namba sawa na namba zilizokuwa kibao cha namba za usajili walichokiota. Yule askari aliziangalia kwa umakini kisha akaangalia muundo wa mabaki ya gari la abiria lililoungua halafu akawaambia, "hebu nifuateni mara moja"

    Yule askari aliondoka mara moja akaelekea mahali pengine kwenye kundi kubwa la maaskari waliovaa kiraia na waliovaa sare za polisi, alimfuata askari mmoja aliyevaa kiraia akatoa heshima kisha akamuuma sikio huku akiwaonesha kidole wale vijana. Yule askari aliyevaa kiraia aliwasogelea wale vijana akiwa na yule askari aliyewaleta kisha akawaashiria wamfuate, alielekea kwenye gari ya polisi aina ya toyota land cruiser yenye viti katika sehemu ya kuwekea mizigo kisha akapanda akawamuru nao wapande.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "naitwa ASP John Faustin natokea kito cha polisi Mkwakwani, wenzangu mnaitwa nani majina yenu" Asp John alijitambulisha kwa wale vijana huku akionesha kitambulisho chake cha kazi kisha akawauliza majina yao, wale vijana walitaja majina yao wote.

    "ok James naomba naomba uache kulia unieleze kila kitu" Asp John alimuambia yule kijana aliyekuwa analia baada ya kuona gari lile lililoungua.

    "afande sisi wote ni wafanyakazi wa kampuni ya Extoplus na tulikuwa tupo Duga kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba mpya za kupangishwa za kampuni yetu, tulikuwa tukitarajia ujio wa staff wa idara ya uhasibu kuiwakilisha ofisi ya makao makuu tangu asubuhi lakini hadi inafika saa sita hawakuwa wamefika. Sisi tulitumwa kuwafuatilia na tulifuatilia ndipo tulipokuta hali hii tena tulianza kuanza kuona kibao cha namba za usajili za gari ya kampuni, na tuliifananisha na picha ya gari la kampuni tukaona linafanana kila kitu" James aliongea huku akiwa na uchungu. Asp John aliyanakili maelezo ya James kisha akajiandaa kuuliza swali jingine lakini king'ora cha gari la zima moto kilimkatisha na akajikuta akiangalia lilipo gari la zima moto. Wale vijana nao waliliona lile gari la zimamoto likipita pembezoni mwa eneo la tukio kwa tabu kisha likaingia barabarani kisha likaingia barabarani likawa linaelekea Duga Maforoni kwa mwendo wa kasi sana huku milio ya ving'ora vyake ikiwa imetawala njia nzima. Asp John alipoona hali hiyo alihisi kuna jambo na akawa anataka kujua kuna nini kilichotokea, alinyanyua simu ya upepo akaongea kwa muda kisha akatulia akasikiliza upande wa pili na akajikuta amegwaya.

    "nyumba za kampuni yenu zilizokuwa zinazinduliwa zote zimeungua kwa moto wa hitilafu ya umeme" Asp John aliwaambia wale vijana.

    "eti nini?" James alisema kwa mshangao.



    ****



    "Ndiyo maana yake hizo nyumba mlizotakiwa kuzizindua leo zote zinateketea kwa moto" Asp John alimuambia James ambaye alionekana kutoamini kwa alichomuambia, vijana wote wa kampuni ya Extoplus walichoka kuliko walivyochoka baada ya kusikia mali ya kampuni ikiwa inaungua. Taarifa hizo zilikuwa ni kama kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda ambacho hakijapona kwa James, kilio chake kilichoanza kunyauka usoni mwake mithili ya mche usiopata matunzo kilianza kuchipua tena kwa taratibu mithili ya mti wa muhogo unavyoota majani baada ya kuwa umechimbiwa chini kwa muda wa siku kadhaa. Kilio hicho kilikolea baada muda wa dakika mbili tu mithili ya garimoshi la makaa ya mawe lililosaza mabeleshi kadhaa ya makaa ya mawe, Asp John ilimbidi asitishe kufanya mahojiana na akawa ana kazi ya kumbembeleza James akishirikiana na wenzake ili waendelee na mahojiano. Ilikuwa ni kazi ngumu sana kumtuliza James ambaye alionekana kuna jambo jingine linamuuma ambalo halikujulikana kwa wenzake wala kwa Asp John.

    "nina mkosi gani mimi?" James aliongea akiwa yupo katikati ya kilio chake.

    "ya nini useme hivyo wakati huna dalili ya kuonekana na mkosi katika maisha yako" Asp John alimfariji.

    "we afande hujui hulisemalo na mimi ninajua nilisemalo" James aliongea huku akipangusa michirizi ya machozi iliyokuwa inatiririka mashavuni mwake.

    "James unaongea nini mbona hatukuelewi?" Kijana mmojawapo aliyefika na James aliyefika eneo hilo alimuuliza akionekana kutatizwa sana na kauli zake.

    "Gasper yaani ungejua nilichokutana nacho juzi" James alisema huku akimtazama yule kijana aliyesema hawamwelewi.

    "hebu wengine nyamazeni kwanza, James hebu eleza vizuri nikuelewe" Asp John aliongea akiwa amemahika bega James.

    "Afande juzi nikiwa natoka kazini niliamua kuelekea Makorora jirani na kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani, niliamua kwenda kwa mguu kutokana na eneo lenyewe kutokuwa mbali na ofisi yetu. Wakati navuka reli zilizopo njiani kuelekea kwenye kituo cha basi nilikutana na mwanamke wa kiarabu ambaye alinichangamkia kwa kunisalimia ingawa hatufahamiani. Yule msichana aliniambia kuwa anafikiri kuwa mimi nimepotea njia na alitaka anielekeze njia iliyosahihi kuifuata, nilimwambia mbona sikuelewi na yeye akaniambia hivi punde utanielewa wala usijali. Aliniambia nyenzo yangu kuu ya maisha imegharamiwa kwa kitu kilicholetwa baada ya kuondoka maisha ya mwingine, mzazi wako wa kiume anatambua hili ingawa analificha ndiyo maana ana maslahi mazuri kutokana na kusitiri kisichostahiki kusitiriwa. Sasa basi tambua na wewe unafuata njia ambayo baba yako ndiyo maana nikakuambia umepotea njia sasa basi unatakiwa ubadili muelekeo uende njia nyingine la si hivyo utakuja kuzama shimo moja ukiteketea ambalo wazazi wako watazama wakitekea siku ya sherehe ya nje ya mji. Kusema kweli nilimuona yule msichana ni kachangayikiwa na nilibaki nikiwa nashindwa hata kumuuliza swali, msichana yule nilimuona akivuka barabara kisha akawa anafuata uelekeo wa reli zinazopita pembeni ya shule ya sekondari ya Usagara . Nilibaki namtazama hadi pale lilipopita basi kubwa la abiria ambalo llinikinga nisimuone na basi hilo lilipopita sikumuona tena yule msichana na sikuelewa ameondoka vipi. Nilibaki nilishangaa kwa muda wa dakika kadhaa hadi pale nilipohisi kushikwa bega na nilipogeuka nilimuona mwanamke ambaye kiumri anafaa kunizaa akiniuliza nina tatizo gani, nilipomjibu sina akaniuliza kwanini nilikuwa naongea mwenyewe kwa muda mrefu. Nikamwambia nilikuwa naongea na mtu ambaye tayari ameshavuka barabara ameelekea njia iliyopo relini inayoelekea katika shule ya Usagara, nilpomuambia maneno hayo aliniambia nina matatizo maana yeye alikuwa akinitazama kwa muda mrefu na ameniona nikiongea peke yangu. Niliona huyo mwanamke ananichanganya tu kama alivyonichanganya yule msichana kwa kauli zake" James alieleza akiwa amepunguza kulia kwa muda na alipomaliza aliendelea kulia, maelezo yake yaliwashangaza sana wwnzake hadi ingawa hayakuwa wazi kwao kuelewa kinamchomliza James. Imaniza kishirikina pamoja na uchawi ndiyo uliyotawala maelezo ya James, wenzake wote walimshangaa sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "James unajua maelezo yako hayana tija yoyote katika ushahidi wa kiserikali kwani hakuna kipengele chochote cha sheria za serikali inayosema uchawi unahusika katika ushahidi pia katika maelezo yako hayajaonsha kiini cha wewe kulia uliposikia kuhusu kuungua kwa hizo nyumba" Asp John aliongea kwa upole huku akimtazama James usoni.

    "Afande nimeambiwa wazazi wataketea katika shimo moja siku ya sherehe ya nje ya mji, huoni kama siku ya sherehe yenyewe ndiyo leo na mzazi wangu mmoja ameshateketea kwenye huu mlipuko wa basi la kampuni. Unafikiri moto wa pili atakuwa salama huko hebu jaribu kufikiri, tena ngoja niende hukohuko" James aliongea akionekana amechanganyikiwa kabisa kwa matukio yaliyomtokea hadi muda huo, aliamua kunyanyuka ili aondoke lakini Asp John akamzuia na kupelekea aanze kizazaa kutokana na fujo alizozianzisha James. Wenzake nao walijaribu kumtuliza lakini ilishindikana kabisa na hata walipomzuia alipiga makelele kama kichaa akiwasihi wamuachie.

    "James hebu tulia kwanza huna uhakika wa kifo cha baba yako sasa fujo za nini?" Asp John alimuambia

    "unasemaje wewe? Hivi ingekuwa ndiyo wewe unakutana na mtu anakupa habari za namna hii na siku himi uliyoambiwa unakutana na mabalaa kama hili utakuwa katika hali gani? Hebu fikiri ingekuwa ndiyo mzazi wako na si kufikiri imemtokea mwenzako" James aliendelea kulalamika huku akizidi kuleta utata kwa Asp John na wenzake waliombana ili asiondoke.

    "subiri basi nimalize kukuhoji ndiyo uende James" Asp John alimsihi.

    "hapa hahojiwi mtu ikiwa sijaenda Duga kumuona kama baba yangu yupo hai au la, ukitaka mahojiano nami basi uniache niende na nikitoka huko ndiyo unihoji" James alizidi kuwela utata.

    "ok haina shida ngoja twende wote huko kwa gari....Kostebo ondoa gari usawa wa Duga Maforoni" Asp John alimuambia James kisha akapaza sauti kumuambia askari aliyekuwa amekaa kwenye usukani.

    "afande" Aliitikia yule askari kidha akawasha gari na akaweka gia akaanza kulipitisha gari pembeni ya barabara kuvuka eneo lenye utepe halafu akaongeza mwendo kuelekea Duga maforoni.



    ****



    Muda ambao ajali ya pili ya moto inatokea kwa upande mwingine mkoa wa Tanga katika sehemu ya jiji kulikuwa kuna kikao kizito cha viongozi waiuu wa kampuni ya Extoplus wakiongozwa na mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa kampuni hiyo bwana Hamid Buruhan, kikao hicho kilikuwa kinajadili mambo mbalimbali kwa ajili ya kukuza kampuni hiyo. Mambo mbalimbali ya kimaendeleo yalikuwa yakijadiliwa kuhusu kukuza kampuni ikiwemo suala la kuongeza nyumba za kupangisha katika sehemu zote zenye maendeleo duni ambazo watumishi wa umma hupelekwa ili wapate makazi bora kama waliyoyaacha mjini. Mojawapo ya kutekezwa mpango huo ulikuwa umeshaanza katika kijiji cha Duga na ulitegemea kuendelezwa katika sehemu zingine za Tanga nzima, mameneja hawa wakuu walikuwa, mkurugenzi, pamoja na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo walionekana wana ari ya kuwa na kampuni kubwa yenye maendeleo katika kila kona ya nchi na hata nchi nyingine.

    "Hadi kufikia mwaka 2020 mpango wetu huu utatufikisha mahala tulipojiwekea kufika katika nyanja za kimaendeleo. Extoplus kwa maendeleo" Hamid alihitisha kisha kikao hicho na hapo kikao kikawa kimefikia mwisho kwa siku hiyo, alipeana mikono na wafanyakazi wake wakuu huku akibadilishana nao mawazo kwani walikuwa pia ni marafiki zake. Walionekana na furaha sana wala hawakutambua kama kuna kuzungumkuti kimetokea kinachohusu kampuni yao, walikuwa na furaha sana kutokana na kiasi kikubwa cha fedha wanachokiingiza kutokana miradi yao na hata uzuri wa maisha wanayoishi.

    "GRIIIIII! GRIIIIIIII!" Mlio wa simu ya mezani isiyo na waya ulisikika ukilia ambayo ilikatisha maongezi na Hamid akaipokea kisha akasema, "halloo!".

    "kuna tatizo gani wewe Gasper hebu eleza vizuri nikuelewe" Hamid aliongea

    "etii! Unase.."Hamid alisema kwa mshangao sana akionekana ameshtushwa sana na taarifa aliyopewa na hata maneno aliyoyataka kuyasema hakuyasema kabisa kwani nguvu zote zilimuishia kutokana na taarifa hiyo na akaanguka kama gunia la chumvi akiwa tayari ameiachia simu. Wenzake walipomfikia na kumtazama mapigo yake ya moyo walikuta yanapiga kwa mbali na ikawalazimu wote kwa pamoja wambebe kumuwahisha katika zahanati ya kampuni hiyo iliyopo ghorofa ya pili ya kampuni hiyo, walifanikiwa kufika salama na wakamuingiza kwenye wodi akaanza kuhudumiwa kwa haraka sana. Mameneja wakuu wote walikaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa ili wasubiri majibu ya daktari pamoja na wauguzi ambao walikuwa wanashughulika katika kumtibu mkuu wao wa Kampuni, baada ya kupita dakika kumi na tano tangu waanze kusubiri kaimu mwenyekiti mtendaji wa kampuni na hiyo na rafiki wa karibu wa Hamid anayeitwa Hisan Shelukindo alinyanyuka kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akasema, "jamani mimi nimesahau simu katika chumba cha mkutano floor ya nane wacha niifuate nitarejea maana ni muhimu kuwa nayo kwa ajili ya kupokea taarifa muhimu". Hisan aliposema hivyo wenzake waliitikia kwa kutikisa vichwa kisha akaondoka hadi nje ya mlango wa kuingilia katika zahanati, akitokea kwenye korido kisha akatembea hadi zilipo lifti za jengo la kampuni yao. Alibonyeza kitufe kilichokuwa kipo jirani na lifti kisha akasubiri kwa muda mfupi ambapo lifti ilifunguka akaingia akabonyeza kitufe namba nane, milango ya lifti ilijifunga na lifti ikaanza kupanda kuelekea juu hadi ghorofa ya nane, lifti ilifunguka kisha Hisan akashuka akatembea hadi kwenye mlango wa chumba cha mkutano akaufungua. Alikutana na giza kutokana na taa ya humo kuzimwa na chumba chenyewe huwa hakipitishi mwanga hata mchana kutokana kuwa na vioo visivyoruhusu mwanga kupita.

    "Mmh! Hizi taa za humu kazizima nani tena" Hisan ajisemea huku akiwasha taa na ilipowaka alirudishia mlango wa chumba hicho cha mkutano kisha akatembea kuelekea mezani alipoiacha simu yake, akiwa yupo katikati ya umbali uliopo kati ya meza na mlango taa za humo ndani zilizima tena na giza likarudi kama ilivyokuwa awali kabla hajawasha taa.

    "Shit! Hawa vijana wa chumba cha kuongozea umeme wanafanya upuuzi gani, inamaana wameachia umeme wa Tanesko ndiyo ufanye kazi" Hisan alijisemea kisha akageuka ili aende kufungua mlango ili hata mwangaza wa madirisha yaliyopo kwenye ngazi yamuongoze kuifuata simu yake, alipopiga hatua moja taa zikawaka ten akaghairi kwenda kufungua mlango akarudi kuchukua simu yake. Alianza kutembea kuelekea kwenye meza na alipofika akaichukua simu yake halafu akaanza kuelekea mlango ili atoke nje, alitembea kwa hatua kubwa hadi mlangoni akanyonga kitasa kuufungua lakini haukufunguka na ilionekana ulikuwa umefungwa kwa nje. Hisan alijikuta akiachia tusi zito sana kutokana na kitendo hicho, aligeuka nyuma akaangalia chini akaiona simu iliyoangangushwa na Hamid alipopoteza fahamu.

    Wazo la kuiokota ndiyo lilimjia kichwani mwake na akalitaka kulitekeleza tu kwani hakukuwa na njia nyingine itakayomuwezesha yeye kupata msaada kutoka nje, alipoanza kupiga hatua ili aifuate taa zilizimika tena kisha kofi zito lilitua shavuni mwake lililompeleka hadi chini. Taa zilipowaka hakuona mtu yoyote ndani ya chumba hicho ingawa maumivu ya kofi alilopigwa alikuwa anayasikia, aliposimama miguu yake yote ilizolewa yote kama anapigwa mtama na akajikuta ameenda kusalimiana na sakafu yenye marumaru katika chumba hicho. Taa za chumba hicho zilizima tena safari kipigo kizito kikawa kinamshukia Hisan bila hata kumuona huyo anayempiga, taa zilipowaka tena Hisan hakuwa anaweza hata kuinuka na alikuwa akitokwa na damu usoni sehemu nyingine za mwili wake na mbele yake kulikuwa kuna mtoto wa miaka takribani saba akiwa amekasirika san ambaye sura yake haikuwa ngeni sana kwa Hisan.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Jamadin" Hisan aliita kwa uoga na macho yake yakawa yakimtazama yule mtoto.

    "nipe" Yule mtoto alisema kwa sauti nzito iliyojaa kitetemeshi.

    "nikupe nini?!" Hisan aliuliza kwa uoga.

    "narudia kwa mara ya mwisho nimesema nipe" Yule mtoto aliongea kwa hasira akaanza kumfuata Hisan

    "nikupe nini?!" Hisan aliongea akiwa anatetemeka akijiburuta kusogea nyuma kwa makalio yake, Yule mtoto alizidi kumsogelea na alipomkaribia alipotea kimaajabu akamuacha Hisan akiwa anashangaa lakini mshangao wake haukudumu kwani alijikuta akishikwa kichwa chake kwa nguvu kutokea upande wa nyuma. Kichwa chake kiliminywa kwa nguvu hadi kikapasuka na akawa ameingia katika orodha ya wasio na uhai waliowahi kuwa hai.



    ****



    Gari ya waliyopanda James na wenzake pamoja na Asp John ilikuwa ilienda kilomita kadhaa kutoka pale bwaga macho kwenye ajali wakaikuta ile gari aina ya Landcruiser prado iliyotumiwa na wakina James kuja nayo ikiwa ipo pembeni na mwenzao akiwa yupo pembeni akiwa ameegemea. Gari ya polisi waliyopanda kina James ilienda kuegeshwa mbele ya gari hiyo na kisha wote kwa pamoja wakashuka wakamfuata mwenzao wakiwa na Asp John.

    "Vipi Tom gari mbovu nini?" Gasper alimuuliza yule mwenzao waliyemuachia gari arudi nalo kule Duga kwenye sherehe ya kampuni.

    "aisee hii gari kuiendesha ni kujitakia kifo bora mlivyokuja tuondoke wote mimi siigusi tena na kazi kwenye hii kampuni naacha" Tom aliongea huku akiwafuata.

    "kuna nini kijana?" Asp John alimuuliza.

    " jamani baada ya kuniachia hii gari nimeendesha vizuri ila nilipo fika hapo nyuma nikiwa kwenye mwendo mkali naanza kusikia sauti ya bosi mkuu ikivuma kama mwangwi masikioni mwangu ikisema nataka damu ya vijana wangu kumi. Nikiwa najifikiria juu ya eneo inapotoka sauti hiyo si ndiyo nikashudia kioo cha mbele chote kikiwa kimejaa damu hadi nikawa sioni kabisa ingawa nilijitahidi kusimamisha gari nikafanikiwa na hapo damu hizo zikawa zimetoweka mara moja na kioo kikawa kawaida kama ilivyokuwa awali. Nimeshuka ndani ya gari na sina hamu nalo tena" Tom aliongea akiwa anahema sana kwa uoga, wenzake wote waliposikia kilichomkuta ndiyo walizidi kuingiwa na hofu kasoro tu Asp John alionekana yupo kawaida tu.

    "nyie hebu wacheni uoga wenu, wewe hebu nipe hizo funguo za gari hiyo niendeshe mimi na nyinyi pandeni hiyo ya polisi tuondoke" Asp John aliwaambia akionekana hana hofu kabisa.

    "Afande utakufa usipande" James aliongea.

    "kwani wewe ndiyo utakuwa hufi, kama leo ndiyo nitatakiwa nife nitakufa tu hata nisipoendesha hili gari, hebu nipe ufunguo sasa"Asp John aliongea na Tom akampatia ufunguo wa gari.

    "mambo si hayo bwana sio kuleta uoga wa kike wakati nyinyi ni wanaume" Asp John aliongea akiwa anaelekea kwenye gari ya kampuni ya Extoplus baada ya kukabidhiwa ufunguo na Tom, aliufikia mlango wa gari hiyo akaufungua akawa anaingia ndani ya gari.

    "leo sihitaji damu ya askari jasusi nataka ya hawa hapo mbele sasa ukijipendekeza tu katika jambo lisilo kuhusu utasalimiana na kaburi" Sauti ya mwangwi ilivuma kwenye masikio ya Asp John lakini akaipuuzia na kuamua kuingia ndani ya gari kisha akaiwasha gari hiyo, alinyonga ufunguo na gari ikawaka kisha ikazima. Alinyonga tena ufunguo safari hii gari ikatikisika sehemu ya injini kisha moto mkubwa ukawaka ukawa unakuja kwa kasi mithili ya moto wa nyikani kwenye katika upande aliopo Asp John.

    "Ha! Ha! Ha! Ha! Si mbishi wewe ngoja nikuchome kama kuni" Sauti yenye kuvuma iliendelea kusikika masikioni mwa Asp John na hapo akaona hatar ipo mbele yake na akaamua kujirusha nje akaangukia upande wa pili barabara sehemu yenye majani, moto uliokuwa unawaka ndani ya gari haukuonekana na wala gari halikuonesha kama linalipuka. Asp John alijinyanyua kutoka pale alipojirusha akaenda hadi pale alipowaacha vijana wa kampuni ya Extoplus akawaambia, "pandeni kwenye gari tuondoke".

    "Afande kulikoni mbona umejirusha nje baada ya gari kuwaka si ulisema unaliendesha" Tom alimuambia Asp John kwa kejeli kutokana na tabia yake ya kudharau mambo anayoambiwa.

    "kaa kimya na upande kwenye gari na mwenzako tuondoke" Asp John aliongea huku akipanda kwenye gari la polisi aliyokuja nayo, vijana wa Extoplus nao wakapanda na safari ikaendelea na muda huo ndiyo Gasper alimpigia simu msichana wa mapokezi makao makuu aliyemuunganisha simu na mkuu wao Hamid akamueleza tukio zima. Baada ya dakika kumi na tano walikuwa tayari wameshafika Duga maforoni na wakielekea moja kwa moja hadi kwenye soko kuu la Duga maforoni wakashukia upande huo kutokana na upande wa pili kwenye eneo la tukio kutokuwa na nafasi, walivuka barabara wote kwa pamoja wakaupita uwanja wa mpira wakakuta umati wa watu ukiwa umezunguka nyumba hizo bado zilikuwa zinateketea na moto huo ulishindikana kuzimwa na kikosi cha zima moto kilichofika hapo kwani magari yao yalitumia maji hadi yakaisha lakini moto haukuzimika hata kidogo. Asp John pamoja na wale vijana waliwafuata wale askari wa jeshi la polisi kikosi cha zimamoto ambao walionekana kukata tamaa kabisa katika uzimaji moto, maaskari hao walitoa saluti kwake huku wakisema, "jambo afande".

    "jamboo, nipeni taarifa mmefikia wapi katika kazi yenu kwani naona bado moto unawaka" Asp John aliwaambia.

    "Afande tumefanya juhudi za kuuzima huu moto kwa kutumia kila njia ila imeshindikana hadi maji yanaisha hatukuweza kuuzima na ikatubidi tutumie gesi lakini bado tumeshindwa kuuzima na inasadikika Mkuu wa idara ya sheria makao makuu ya kampuni hizi yupo ndani ya nyumba ya tatu na hajatoka hadi muda huu na hata tulipofika tulikuwa tukisikia kelele za mtu akiomba msaada lakini sasa hazisikiki" Mmoja wa maaskari wa zimamoto aliongea kwa ufupi juu ya tukio hilo la kuungua kwa nyumba hizo, James aliposikia maelezo hayo alipiga kelele huku akiita, "Babaa!". Aliwapita askari wa kikosi cha zimamoto akakimbia kuelekea ulipo moto katika nyumba ya tatu ya kampuni, maaskari wote walianza kumkimbiza ili wamuwahi asiingie ndani ya moto huo kutokana na ukali wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mbio za watu wote waliokuwa wakijaribu kumzuia James asiingie ndani ya nyumba hazikuzaa matunda yoyote katika kumzuia kwani James aliingia ndani ya nyumba hiyo kabla hawajamzuia, wenzake pamoja na maaskari wote walipojaribu kuikaribia mlango wa nyumba aliyoingia James walijikuta wakitupwa nyuma wote baada ya mlipuko mzito kutokea katika nyumba hiyo kisha nyumba nyingine zilizosalia nazo zikapata mlipuko wa aina hiyo hiyo. Asp John, maaskari wa zimamoto pamoja na wenzake James wote walisikitika kwa kitendo cha James kuingia katika nyumba hiyo inayoungua ambayo tayari imeshatoa mlipuko mzito wa moto, bado walikuwa wamelala chini baada ya kutupwa na mlipuko mzito waliposogelea nyumba aliyoingia James ili wamuokoe. Ajabu ya mlipuko huo uliowatupa haukuwaunguza hata kidogo wala hata kunuka harufu ya moshi, walikuwa wameumia tu baadhi ya sehemu za miili yao baada ya kuanguka chini. Wakiwa hawana hata akili ya kunyanyuka pale chini tayari jambo jingine la kustajaabisha lilianza kutokea ambalo liliwafanya wakimbie kuelekea ulipo uwanja wa mpira ili wakae mbali na ardhi ambayo imebeba nyumba hizo, lilikuwa ni tetemeko la ardhi lililoikumba ardhi iliyobeba nyumba hizo huku eneo la jirani na hapo likiwa limetulia bila kupatwa na tetemeko hilo. Matofali ya nyumba hizo ambazo bado zilikuwa zinawaka yaliporomoka katika mpangilio wake uliounda ukuta na yakajazana kama tanuli katika kila nyumba iliyokuwa imejengwa, tukio hilo lilishuhudiwa na halaiki ya watu ambayo tayari ilikuwa imeshajikusanya katika uwanja wa mpira kuangalia maajabu hayo. Waandishi wa habari kituo cha televisheni cha Tanga nao walikuwa wakilirusha tukio hewani, hata waandishi wa habari waliopo mkoa wa Tanga kuwakilisha vituo vyao wakikuwa wameshawasili pia walikuwa kazini.

    Tetemeko hilo la ardhi la maajabu liliendelea kutikisa ardhi hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Extoplus hadi hata matofali yalijijaza vifusi katika kila eneo lililokuwa limejengwa nyumba yakasagika yakawa mchanga mtupu, baada ya tetemeko kutulia ndipo askari wa zimamoto na uokoaji walipopata ujasiri wa kusogelea katika kifusi cha mchanga uliosagika ambao ulikuwa ni wa matofali wa nyumba ile waliyoingia James na Baba yake kwa nyakati tofauti. Walikifukua kifusi hicho kwa kutumia vifaa vyao na kukagua kila sehemu ili waweze kuitoa miili ya baba na mwana lakini hawakuambulia hata kiungo kimoja cha miili ya James na baba yake, askari walizidi kupigwa na mshangao watu tukio hilo kwani ilikuwa ni jambo la ajabu sana.

    "mmh! Sijawahi kukutana na tukio kama hili tangu nianze kufanya kazi katika kikosi cha zimamoto na uokoaji katika jeshi la polisi" Kiongozi wa askari wa zimamoto na uokoaji alimuambia Asp John.

    "hivi jambo kama hili linawezekanaje?" Asp John alijikuta akiuliza swali ambalo halina maana yoyote kwa mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji.

    "hilo swali hata sijui nikujibu vipi unaona kabisa imezekana katika namna isiyokuwa rahisi, mtu aingie ndani ya nyumba halafu ilipuke tu kisha tetemeko liloikumba ardhi ya ukubwa wa ekari kumi na tano litokee liangushe matofali yasagike halafu moto uzime tusipate hata baki la mwili wa binadamu katika sehemu waliyoingia" Yule mkuu wa kikosi cha zimamoto aliongea.

    "ama kweli hii ni dunia ina mambo ambayo usiyoweza kuyadhania" Asp John aliongea huku akisikitika.

    "ndiyo hivyo afande" Mkuu wa kikosi cha zimamoto aliongea.

    "hapa hamna la ziada ngoja nirudi nikaendelee na tukio la kule la Bwaga macho, vijana nina shida na nyinyi hebu nifuateni" Asp John aliongea huku akiondoka na wale marafiki zake James wakamfuata.







    SURA YA TATU



    Hadi jioni inaingia tayari tukio lile la ajabu lilikuwa lishaenea jiji zima la Tanga na kwingineko ndani ya nchi ya Tanzania na hata Afrika ya mashariki, ilitokea kuwa habari iliyoteka vyombo vyote vya habari katika ukanda huu na hata katika kituo BBC idhaa ya Kiswahili ilitangazwa na kupelekea kuwa habari iliyosikika karibia dunia nzima kwa watu wanaongea kiswahili. Taarifa za vibweka vilivyotokea huko Duga zilimfikia mmiliki wa kampuni ya Extoplus Hamid akiwa yupo kitandani katika wodi ya zahanati ya kampuni yake tangu alipoanguka kwenye chumba cha mkutano, aliipata taarifa hiyo kupitia luninga iliyopo katika wodi aliyolazwa akawa amebaki na masikitiko tu kutokana na hasara aliyoipata kuungua kwa nyumba hizo ambazo zilimgharimu pesa nyingi hadi kukamilika kwake. Hadi saa nne usiku anaruhusiwa alikuwa na majonzi kutokana na jambo hilo, alirudi nyumbani kwake kwa msaada wa dereva wake.

    Asubuhi ya siku iliyofuata alitoka mapema nyumbani akaenda ofisini akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake, siku hiyo ilikuwa mbaya kwa Hamid kuliko siku zote za maisha yake kwani alipifika ofisini kwake tu akakumbana na kisanga kingine baada ya mwili wa kaimu mwenyekiti mtendaji wa kampuni yake Hisan kukutwa ukiwa chumba cha mkutano alichokuwemo siku iliyopita akiwa na wafanyakazi wake wakuu wakiongea. Mwili wa Hisan ulikutwa na mfanya usafi wa kampuni hiyo ambaye alichanganyikiwa baada ya kuuona ukiwa hauna uhai upo sakafuni. Tukio hilo lilikuwa ni tukio jingine la aina yake ambalo ilionekana ni kama mkosi umeingia kwenye kampuni hiyo kutokana na kuzaliwa kwa jambo jingine lililozidi kumchanganya Hamid, baada ya polisi kuchukua vipimo vyote pamoja na kuondoka na mwili wa Hisan afisa ajira wa kampuni hiyo aliingia katika ofisi ya Hamid akiwa na faili kubwa aliloweka mezani kisha akaweka barua juu yake.

    "Msuya ndiyo nini hii unaniletea" Hamid aliuliza.

    "Bosi hiyo ni barua ya kuacha kazi katika kampuni hii ili niwe salama na maisha yangu" Msuya ambaye ni afisa ajira katika kampuni hiyo aliongea.

    "unasema nini wewe?!" Hamid aliuliza kwa mshangao.

    "ndiyo hivyo bosi kutokana na ndoto niliyoiota usiku wa leo iliyonipa onyo juu ya maisha nikiendelea kufanya kazi hapa sina budi kuacha kazi, uamuzi huu si wangu peke yangu bali ni wa mameneja wote pamoja na wakuu wa idara wote na barua zao zipo kwenye faili nililokuletea" Msuya aliongea maneno yaliyozidi kumchanganya Hamid.

    "yaani Msuya pamoja na kuwa ni msomi mwenye elimu kubwa bado unaamini ndoto" Hamid aliongea kwa masikitiko.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sina budi kufanya hivyo kwani kila mtu aliyeandika barua hii ameota ndoto kama hii tena ameonywa kuhusu kifo kilichotokana na ubishi wa staff wa idara ya uhasibu waliokufa jana ikiwa atabisha. Nimeamua kuacha kazi mimi na wenzangu na kila mmoja hahitaji marupurupu yoyote tunaondoka kama tulivyokuja" Msuya aliongea kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo akimuacha Hamid akiwa amechanganyika akiwa anakaribia hata kulia, alitulia ofisini kwake kwa muda mfupi kisha akaamua kutoka kupitia idara zote kuangalia kama kile alichoambiwa na Msuya ni kweli au ilikuwa ni utani. Huko ndipo aliposadikisha maneno ya Msuya baada ya kukuta ofisi zote zikiwa zipo tupu hakuna hata mfanyakazi, Hamid alijikuta akianza kulia mwenyewe na akaona hali aliyoikimbia kabla hajawa na familia sasa inaanza kumrudia. Yeye hakutaka hali hiyo imtokee tena na alikuwa yupo tayari kuizuia kwa namna yoyote ile na hapo ndipo alipopata ufumbuzi wa matatizo yake kwa mtaalamu wake maalum.

    "Dokta Bundi atanisaidia niepukane na adha hii ngoja niwahi kwenda kwenda kwake Mwamboni" Hamid alijisemea mwenyewe kisha akaanza kutoka mbio kuelekea nje ya ofisi ambapo alipanda gari yake akaiondoa kwa mwendo wa kasi akiwa na haraka ya kuwahi safari yake. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi akiwa na ari ya kuwahi kufika Mwamboni kwa mganga wake ambaye huwa anamsaidia katika matatizo mbalimbali, akiwa yupo ndani ya gari akiwa anakatiza katika barabara ipitayo Chumbageni alisikia sauti ikimuambia "aisee nishushe hapohapo chumbageni police station nataka kuongea na jamaa yangu".

    Hamid alishtuka sana akatizama nyuma kwa uoga na akijikuta anatamani hata apotee kimiujiza humo ndani ya gari, laiti kama moyo wake ungekuwa na nguvu kama ya vijiko vinavyojenga barabara ya kugusa ukuta tu na kuuangusha basi ungekuwa ushapasua kifua chake kwa jinsi ulivyokuwa unadunda kwa nguvu baada ya kumuona Hisan aliyekutwa akiwa amekufa katika chumba cha mkutano asubuhi ya siku hiyo.

    "unashangaa nini Hamid hebu simamisha gari hapo Chumbageni polics station nikaangalie ripoti ya kifo changu kilichonipata jana kama polisi wamechunguza kiusahihi" Hisan aliongea huku akionekana yupo katika hali ya kawaida tu, Hamid alikuwa tayari ameshaachia mkojo ulimtoka bila hata kujijua.

    "Ona sasa dume zima una miaka arobaini na nane unajikojolea kisa kumuona mtu aliyekufa akiwa anatembea, hebu simamisha gari nishuke wewe nishafika tayari nataka nikaangalie ripoti ya kifo changu nasikia anayo Inspekta Ismail Mdoe. Au hii sura inakuchanganya ngoja niibadilishe basi uoga ukupungue" Hisan aliongea kisha akabadilika kuanzia sura hadi mwili ukawa wa mtoto aliyemtokea Hisan kabla hajafa.

    "Hapo vipi utaniogopa tena?" Aliuliza huku akimtazama Hamid ambaye alizidi kuogopa na akawa anahangaika kufungua mlango ili ajitupe nje kuikimbia sura aliyoiona sasa hivi ikiwa ina macho mekundu, milango ya gari ilikuwa haifunguki na hata alipotoa kifunga mlango bado haikufunguka hata kidogo. Hamid aliendelea kuhangaika na kukivuta kitasa cha ndani cha mlango akiwa haamini kama mlango umejifunga, alibaki akihangaika kuchezea kitasa kutokana na kuchanganywa na tukio hilo.

    "ukimaliza uniambie" Yule mtoto alimuambia huku akikunja miguu yake ikatengeneza umbo la nne akimtazama akiwa na tabasamu lisiloashria furaha hata kidogo.

    Hamid alikuwa ameshasahau kama alikuwa anaendesha gari na alipokuja kukumbuka aliona gari linaenda lenyewe kwa mwendo wa taratibu sana na lilikuwa likipitwa na magari yanayowahi. Alibaki akimtazama yule mtoto huku akitetemeka kiuoga na mikono akiwa ameweka ishara ya kuomba msamaha.

    "halafu unataka kuruka nje huku umejifunga mkanda sasa ndiyo unafanya ujinga gani?" Yule mtoto alimuambia Hamid ambaye hakuwa anatambua hakuwa amefungua mkanda katika harakati za kutaka kuoko nafsi yake, alipotaka kuufungua mkanda yule Mtoto alinyoosha mkono wake na mkanda wa gari ukamzunguka Hamid shingoni mwake kama nyoka na ukaanza kumkaba kwa nguvu hadi mishipa ya damu ya kichwani ikawa inaonekana.

    "Nipe" Yule mtoto alimuambia Hamid huku akimtazama kwa hasira.

    "siii....sinaa" Hamid aliongea kwa tabu kutokana na jinsi mkanda ulivyomkaba.

    "kimoja umenipatia, nataka unipe kilichobakia. Sasa nipe!" Yule mtoto aliongea kwa hasira huku akitokwa na cheche za moto mdomoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sinaa!" Hamid aliongea kwa tabu huku macho yake yakibadilika rangi kutokana na kukabwa, mishipa ya kichwani ilikuwa imemtoka hasa.

    "Ok haya fungua mlango ukimbie" Yule mtoto aliongea na muda huo mkanda ukaacha kumkaba Hamid na mlango ikawa ipo kawaida, Hamid alifungua mkanda akafungua mlango akajitupa nje bila hata kuangalia barabarani. Kitendo cha Hamid kujitupa nje ilsikika

    honi ya gari ya mizigo iliyolia kwa nguvu pamoja na vyuma vya breki kutoa mlio mkali, vishindo viwili vizito vikafuata kwa kupishana sekunde mbili na hapo kila aliyekuwa yupo karibu na eneo hilo akashika kichwa kwa mshangao.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog