Search This Blog

DHAHAMA - 2

 







    Simulizi : Dhahama

    Sehemu Ya Pili (2)



    Gari aina ya Scania ya mizigo ndiyo ilikumbana na kishindo cha kwanza baada ya kumgonga Hamid na kupelekea kichwa chake kupasuka na kutengeneza taswira isiyofaa barabarani kuangaliwa na binadamu wa kawaida kwani haifai binadamu kuona kichwa cha binadamu mwenzako kikiwa kimepasuliwa kama puto liliingia katika kichaka chenye miiba. Kishindo kingine kilikuwa ni cha gari la Hamid baada ya kugonga mti wa mwembe uliopo katika makutano ya barabara inayotoka Kwa minchi, inayoelekea Amboni na hiyi inayopita Chumbageni. Ndani dakika zisizopungua tatu tayari maaskari walishajaa kutokana na kituo cha polisi kutokuwa mbali na hapo ilipotokea tukio hilo, askari hao walikuwa mchanganyiko kati ya askari wa usalama barabarani na wa kawaida ambao walishiriakiana na kuifanya kazi hiyo kwa haraka. Uchunguzi wa magari yote yalipokaguliwa yalizidi kushangaza watu kwani katika gari aina ya Scania hakukuwa na dereva ingawa mashuhuda walisema dereva hakushuka na katika gari aina ya range rover sport aliyokuwa anaitumia Hamid hakukuwa na dereva vilevile. Maaskari wakiwa bado hata hawajasahau tukio la siku iliyopita tayari wanakutana na tukio jingine la kushangaza kama hilo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sasa haya magari yatajiendeshaje yenyewe hebu nyinyi kachunguze vizuri mazingira ya jirani na ule mwembe ilipogonga ile Range tena someni na stika zake tumjue mmiliki nilitaka kusahau hilo" Askari mwenye nyota tatu mabegani mwake aliongea, maaskari walipiga saluti kisha wakaenda kuchunguza walichoambiwa na mkubwa wao kwa haraka. Baada ya dakika moja tu tangu wale askari waondoka simu ya upepo ya yule Inspekta ambaye ndiye mwenye nyota tatu ikakoroma kisha ikasikika sauti ya yule askari mwingine ikimuita kule kwenye gari aina ya Range rover iliyogonga mti wa Mwembe, Inspekta huyu alienda haraka hadi pale kwenye kwenda kuona alichoitiwa. Alipofika alipigiwa saluti kisha akaongozwa na askari mwingine hadi kwenye kioo cha gari hiyo, yule askari aliyemuongoza alimuonesha yule Inspekta stika za gari ile ambazo ziliandikwa jina la mwenye gari.

    "Hamid Buruhan, si mmiliki wa kampuni iliyokumbwa na kadhia isiyoeleweka jana" Inspekta aliongea

    "ndiyo afande" Yule askari aliyemuita aliitikia.

    "Sajenti Shehoza hebu licheki hili gari halafu..." Yule Inspekta aliongea lakinj akasitisha maneno yake baada ya kuona alama za kung'oka majani yaliyoonekana yametokana na kuburuzwa kitu kuelekea katika majani marefu yaliyopo jirani na Mwembe, aliamua kufuatilia alama hizo kuelekea kwenye majani marefu akiwa anatazama chini kwa umakini sana ambapo aliona vitu mbalimbali vya uganga vikiwa vimeanguka njiani kama vile hirizi na vibuyu pamoja na kitambaa chekundu cha kaniki. Inspekta huyo aliendelea kufuatilia hadi mwisho wake ambapo alikutana na mwili wa mzee wa makamo ukiwa umelazwa kwenye majani yaliyoonekana kupunguzwa kwa kitu chenye kali katika sehemu ulipolazwa mwili huo. Mavazi yaliyokuwa yamevaliwa na maiti hiyo ambayo yalionakana aliyavaa mwenyewe kabla hajakumbwa na umauti yalikuwa ni ya kiganga kabisa, kaniki nyekundu aliyojifunga ilitosha kumtambulisha kama mganga ukiachilia mbali hirizi iliyopo begani kwake. Inspekta yule aliwaamrisha maaskari wale wachukua vipimo vyote juu ya mwili kisha wawaite wauguzi maaskari waliofika hapo baada ya kupigiwa simu waje wauchukue mwili ukahifadhiwe, Inspekta huyo aliondoka akarudi alipokuwa awali ambapo barabara ilikuwa inasafishwa baada ya uchukuaji wa vipimo kukamilika alisimamia taratibu zingine. Gari la kuvuta magari mabovu maarufu kama Break down nalo liliitwa likaondoa magari yote yakaenda kuhifadhiwa katika kituo cha polisi cha Chumbageni. Maaskari waliokuwa kule kwenye majani marefu walirejea wakiwa na wauguzi maalum wa jeshi la polisi waliobeba machela yenye mwili wa yule mzee aliyekutwa kwenye majani, wakiwa wanaelekea kwenye gari la wagonjwa la hospitali kuu ya Tanga yaani Bombo. Mwanamke mmoja asiyejulikana ametokea wapi alikimbia hadi pale walipokuwa wale maaskari na wauguzi akaufungua ule mwili kisha akaanza kulia kwa uchungu huku akipiga kelele kwa uchungu.

    "Jamani mume wangu mimi!" Aliropoka yule mwanamke huku akiishika machela iliyobeba mwili.

    "we mama hebu tulia tufanye kazi yetu" Sajenti Shehoza aliongea huku akimzuia yule mwanamke na wale wauguzi wakaendelea na safari.

    "Baba Hadija nilikumbia usisaidie usiowajua umeona sasa, Mayoooo mayooo" Yule mwanamke alizidi kuongea kwa nguvu huku akilia kama mtoto mdogo.



    ****



    Wakati askari wakishughulika katika ajali ya kutatanisha iliyotokea Chumbageni, upende mwingine wa jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone hali ilikuwa shwari kuliko kawaida katika kampuni ya mafuta ya Matro inayosifika kwa kutoa huduma bora za mafuta jijini Tanga na kwingineko. Ndani ya makao makuu ya kampuni hii wafanyakazi walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida ili kuinua kampuni na pia kuendesha maisha yao. Siku hiyo mmiliki wa kampuni hiyo Hussein Buruhan ambaye ni mmojawapo wa matajiri wakubwa nchini alikuwa yupo ofisini kwake ghorofa ya kumi na mbili ya jengo la kampuni hiyo akiendelea na kazi kama kawaida.

    Baada ya nusu saa za uchapaji kazi alianza kuhisi kubanwa na haja ndogo na ikambidi aende msalani kutokana na kushindwa kuvumilia kukaa katika hali hiyo, alifunga ofisi kisha akaingia katika maliwato ambayo ipo jirani na ofisi yako. Aliingia moja kwa moja msalani akajisaidia kisha akatoka akiwa anapiga uruzi wa nyimbo anayoipenda akiwa na tabasamu pana usoni mwake, kama ilivyo kawaida yake huwa akitoka maliwatoni lazima aende kwenye kioo kipana chenye masinki yenye koki kadhaa za maji kwa chini yake ili anawe mikono. Alienda kwenye sinki hilo akafungua maji akanawa mikono kisha akanawa uso akiwa anapiga uruzi wa wimbo anaupenda unaoitwa this i promise you ulioimbwa na kundi la wanamuziki wa kimarekani liitwalo N-sync, akiendelea kupiga uruzi huo ghafla taa za huko kwenye maliwato zikazima na kukawa giza kutokana na madirisha madogo yaliyomo humo kutopitisha mwanga vizuri.



    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "shit! Yaani hawa Tanesco wanakera sana" Hussein alisema kutokana na umeme kuzimika humo maliwatoni, lawama zake zote alizielekeza kwenye kampuni ya usambazaji umeme nchini kutokana na kuzimika kwa taa ya humo ndani. Hakuwa ametambua kama alikuwa anawabebesha lawama kwa wasiohusika na tatizo hilo, hakika hakujua kama kuna ugeni uliokuwa umemfikia na dalili yake ndiyo hiyo ya kuzimika kwa taa humo maliwatoni. Akiwa na uso ulionekana kukerwa kabisa na tatizo hilo taa ziliwaka tena akajikuta akitukana tusi zito halafu akainama ili anawe uso ingawa alisita baada ya kuhisi hayupo peke yake blali kuna mtu mwingine, aligeuza uso pembeni akamuona kijana mwenye asili ys uchotara wa kiarabu na mbantu akiwa ananawa uso wake tararibu bila hata kushughulika kumuangalia Hussein na wala haikujikana aliingia muda gani hapo.

    "wewe umeingia saa ngapi hapa?" Hussein alimuuliza yule kijana, yule kijana aliposikia swali la Hussein aliacha kunawa kisha akajifuta uso wake halafu akamtazama kwa sekunde kadhaa.

    "nimeingia muda si mrefu" Yule kijana alijibu kisha akafungua tena koki ya maji akaendelea kunawa, jibu hilo lilimchanganya zaidi Hussein na akajikuta akimshangaa sana yule kijana hadi akaanza kumuogopa kwani mlango haukuwa umefunguliwa kuashiria kama kuna mtu aliingia.

    "Kwanza wewe ni nani mpaka uingie kwenye sehemu ambayo staff wa kawaida hawafiki?" Hussein alimuuliza yule kijana.

    "mimi ni Zalabain ndiyo maana nimeingia humu na cheo changu ni prince ndiyo maana nipo humu" Yule kijana aliongea huku akitabasamu.

    "unasemaje mbona sikuelewi na sikujui?" Hussein aliongea kutokana na kuchanganywa na maelezo ya yule kijana.

    "utanielewa na utanijua" Yule kijana aliongea na hapo ndani taa zikazimika tena na zikawaka, yule kijana sehemu aliyokuwepo awali hakuonekana kabisa na hapo ndipo Hussein alizidi kuingiwa na uoga. Alipoangalia kwenye kioo ambacho kilimuonesha upande wa nyuma yake ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kwa alichokiona, alitaka kusoma dua ya kujikinga na viumbe waovu lakini mdomo wake ulikuwa mziti na haukufunguka kabisa kama amelishwa mawe. Alipogeuka ili aone vizuri kwa kudhani labda anaona maruweruwe tu ndipo akajikuta akipokea kofi zito lililompeleka hadi chini, alipoinua uso wake alikutana uso kwa uso na yule mtoto ambaye aliwatokea Hisan na Hamid muda mfupi kabla hawajaiaga dunia.

    "Huna akili kweli yaani unataka kusoma dua chooni kisa umeniona mimi, toka lini jina la Muumba likatajwa chooni wewe na hata ungesoma unafikiri angekusaidia wakati muda unaingia chooni hukumkumbuka hata kidogo kwa kumuomba akulinde ukiwa humu" Yule mtoto aliongea huku akisikitika.

    "sio mimi nisamehe" Hussein aliongea huku akitetemeka akiwa amekaa kitako kwenye sakafu ya maliwatoni hapo.

    "Heh! Kwanini siyo wewe, inamaana huitwi Hussein Buruhan mtoto wa tano wa mzee Buruhan" Yule mtoto alimuambia Hussein huku akionekana kushangaa kwa jinsi anavyoongea.

    "ndiyo mimi Hussein" Hussein alijibu huku akitetemeka kwa uoga.

    "basi kama wewe ndiyo Hussein basi ndiyo wewe" Yule Mtoto aliongea kwa hasira kisha akamsogelea Hussein kwa kasi sana na alipomfikia alimkaba kooni hadi akawa hawezi kupumua vizuri, alimnyanyua juu akambamiza kwenye kioo kikubwa kilichokuwa kipo humo ndani juu ya masinki ya kunawia. Hussein alikatwa na vipande vya vioo na akajikuta akipiga kelele za kuomba msaada huku akimtaja mama yake kama ilivyo watu wengi wakiwa katika matatizo, kelele hizo hazikusaidia chochote kwani kipigo kiliendelea kama kawaida na alizidi kumtaja mama yake.

    "Watu kama nyinyi ndiyo mungu hawasaidii hata kidogo, yaani unamkumbuka mama yako kwenye shida halafu unamsahau Mungu wako anayekupa pumzi hizo zinazokutia jeuri. Haya nipe upesi" Yule mtoto alimuambia Hussein.

    "si.....sina" Hussein aliongea kwa tabu kutokana maumivu ya kipigo alichokipata.

    "ohoo! Huna, basi utaenda kuonana na kaka yako Hamid huko roho yake ilipo" Yule mtoto aliongea kisha akajizungusha kama pia hadi kikatokea kimbunga kilichomzoa Hussein akawa yupo katikati, milio ya makofi ndiyo ilifuatia akiwa yupo humo ndani ya kimbunga hicho na makelele ya maumivu yakawa yanasikika. Kimbunga hicho kilipokuja kuisha Hussen alitupwa chini akiwa amevunjika sehemu mbalimbali za mwili wake, Yule mtoto bado alikuwepo na safari hii alikuwa yupo karibu yake zaidi na mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata koo la Hussein.

    "salamu zao kwa waliotangulia kabla yako" Yule mtoto aliongea kisha akalivuta koromeo la Hussein hadi akalitoa nje kiaha akalivunja akautoa mfupa wake akauweka pembeni, Hussein tayari alikuwa amekwisha maliza mkataba wake wa kuishi duniani hadi muda huo akiwa miongoni waaiokuwepo duniani kimwili.



    ****



    KITUO CHA POLISI CHUMBAGENI

    TANGA



    Baada ya yule mama kuvamia mwili wa yule mwanaume aliyekutwa kwenye majani amekufa katika ajali ya gari ya Hamid, yule Inspekta aliamuru yule mama awekwe chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi na alipelekwa kituo cha polisi Chumbageni kusubiri Inspekta arudi ili afanye mahojiano naye. Inspekta yule aliporudi kituoni baada ya kumaliza kusimamia kazi kule barabarani yule mwanamke aliingiza kwenye chumba cha mahojiano, yule inspekta aliingia katika chumba cha mahojiano akiwa na maaskari waliokuwa wadogo kivyeo.

    Naitwa Inspekta Ismail Mdoe, kulia kwangu yupo Sajenti Juma Shehoza na kushoto kwangu kuna Staff sajenti Dickson Mushi, sijui mama unaitwa nani?" Yule Inspekta ambaye ndiye Inspekta Mdoe aliongea huku akitoa utambulisho kwa wenzake.

    "naitwa Mwanamkuu Jumanne" Yule mwanamke alijibu kwa unyonge.

    "Ok Bi Mwanamkuu una umri gani, unafanya kazi gani na unaishi wapi?" Inspekta Mdoe alimuuliza.

    "nina miaka 48 nafanya biashara ndogondogo, ninaishi hapahapa Chumbageni" Bi Mwanamkuu alijibu kwa unyonge, muda huo Sajenti Shehoza alikuwa akiandika kila kilichokuwa kinafanyika kwenye mahojiano hayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wewe na marehemu mna uhusiano gani?" Inspekta Mdoe aliuliza.

    "Marehemu ni mume wangu" Bi Mwanamkuu alijibu.

    "ok, unaweza ukatuambia kilichokufanya utamke yale maneno kwenye eneo la ajali?" Inspekta Mdoe alimuuliza.

    "afande chanzo cha kutamka maneno yale ni kutokana na mume wangu kuingilia mambo yasiyomuhusu na hatimaye akauawa" Bi Mwanamkuu alizidi kuongea na safari machozi yalikuwa yakimtoka.

    "una uhakika gani na hayo unayoyasema? Hebu fafanua kauli yako" Staff sajenti Mushi alimuuliza kwa mara ya kwanza.

    "muda mfupi kabla mume wangu alikuwa akiendelea na kazi zake za uganga, alipandisha maruhani yake akasema kuna mtu yupo hatarini kuuawa hivyo anahitaji kumsaidia. Akichukua vifaa vyake vya uganga akaenda huko, na sikumuona tena hadi niliona mnambeba" Bi Mwanamkuu aliongea huku akilia, maelezo hayo yaliwafanya maaskari hao waliokuwa wanamuhoji watazamane kwa muda wa sekunde kadhaa.

    "Mama usituletee maelezo yasiyokuwa na uthibitisho wowote" Inspekta Mdoe aliongea akionesha kuchanganywa na maelezo aliyoambiwa.

    "Afande hii siyo kiwango chenu naomba muiache na huyu mbaya wangu aliyeniulia mume wangu nitamkomesha" Bi Mwanamkuu aliongea kwa hasira kisha akaanza kuangaza pande zote za humo, alianza kunguruma kama simba akiashiria mashetani yamempanda. Maaskari waliokuwa wanaomuhoji walibaki wakimtazama tu wakionekana kuwa hofu nae, Bi Mwanamkuu aliposimama akionekana ana hasira kimbunga kizito kiliibuka humo ofisini kikamzoa na kilipotoweka naye alitoweka papo hapo.



    ****



    Mfanyakazi wa kampuni ya Matro anayehusika na usafishaji vyoo na korido katika ghorofa la kampuni hiyo alianza kufanya kazi kama ilivyokuwa kawaida yake, alianza kufanyakazi katika ghorofa tofauti na mwishowe akamalizia katika ghorofa ya mwisho ambayo ndiyo inapatikana ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Kijana huyo anayeitwa Niko alianza kusafisha korido mbalimbali za ghorofa hiyo na hatimaye zamu ya kusafisha maliwato za ghorofa hiyo ya mwisho ikaanza, alianza kwa kusafisha maliwato ndogo na hatimaye akahamia kwenye maliwato kubwa ambayo ipo jirani na ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Akiwa na kotoroli chenye vifaa ambacho alikiburuza hadi katika mlango wa maliwato hiyo kisha akaupa mlango mgongo akawa anakiburuza kitoroli ili aingie nacho ndani akiwa ameufungua mlango kwa kuusukuma na mgongo wake. Alifanikiwa kuingiza kitoroli hadi ndani akiwa anaimba kwa kuchangamka akiwa ameungalia mlango na ameipa mgongo sehemu ya ndani ya maliwato hiyo, akichukua fagio lenye nyuzi maalum kwa kufanyia usafi akaanza kufanya usafi kuanzia mlangoni na sehemu za pembeni ya mlango. Baada ya kumaliza kufanya usafi maeneo hayo ndipo alipogeuka nyuma ili aendelee na usafi akakutana na hali isiyopendeza kutazamwa. aliuona mwili wa bosi wake mkuu ukiwa upo chini na koromeo lipo pembeni ya mwili huo. Niko alijikuta akitoa ukelelewa uoga kisha akakimbia kuelekea mlangoni, aliponyeza kitufe cha kengele ya hatari ya ghorofa kisha akakaa kitako akawa kama mtu asiyejielewa kabisa.



    Mlio wa kengele ya hatari katika jengo lote ulisikika na kupelekea kundi kubwa la wafanyakazi litoke nje ili kuchukua tahadhari kama kuna uwepo wa jambo la hatari, walinzi wa kampuni wenye silaha wakaanza kupandisha wakiwa na tahadhari kubwa kwani kengele hiyo ilimaanisha jambo la hatari. Walinzi hao walipita kwenye ghorofa mbalimbali kwa tahadhari na hatimaye wakafika ghorofa ya mwisho, walitembea kwa tahadhari katika ghorofa hiyo hadi walipomuona Niko wakamfuata huku wengine wakiwa wanaangalia usalama. Walipomfikia Niko aliishia kuonesha kidole ndani ya maliwato ndipo maaskari hao walipoingia huku wengine wakimuuliza maswali ambayo hakuyajibu zaidi ya kutetemeka. Walinzi walioingia waliwaita wenzao wakajionea kilichotokea humo ndani ya maliwato, simu ilipigwa haraka kituo cha polisi ambapo polisi walifika ndani ya muda mfupi tu wakajionea hali halisi na wakachukua vipimo mbalimbali pamoja na kuuchukua mwili wa Hussein.



    ****



    Maeneo hayohayo ya Raskazoni kwa upande mwingine kulikuwa kuna mzee wa makamo aliyekuwa akiangalia luninga sebuleni, alikuwa ni mzee wa miaka takribani hamsini na ushee ingawa alionekana kutozeeka sana. Wakati mwili wa Hussein ukiwa umeondolewa kule kazini na ukiwa tayari umeshafikiishwa hospitali ili kuhifadhiwa, mzee huyu aitwae Shafii Buruhan alipigiwa simu na alipoipokea na akasikia alichokisikia alizidi kuchanganyikiwa na akabaki akilia kwa sauti kama mtoto mdogo hadi mkewe akaja sebuleni akamuona mume wake akiwa katika hali hiyo.

    "Baba Zayina kuna nini?" Mke wake aliimuuliza baada ya kumkuta akiwa analia kama mtoto.

    "wadogo zangu Hamid na Hussein mama Zayina" Shafiu alijibu huku akilia kwa kushindwa kustahimili jambo aliloambiwa.

    "wamefanyaje tena?" Mke wake aliuliza akionekana kutoelewa.

    "hatunao tena duniani, wadogo zangu mimi jamaniii" Shafii alijibu huku akilakamika na mke wake akaanza kumbembeleza huku yeye mwenyewe akilia baada ya kusikia mashemeji zake wamefariki. Shafii alilia sana kama mtoto mdogo kutokana na vifo hivyo, mkewe naye alikuwa ana kazi ya kumbembeleza ingawa hata yeye alikuwa akitokwa na machozi.

    "Baba Zayina jikaze wewe ni mwanaume" Mke wake alimwambia huku akimfuta machozi, muda huo mlango wa hapo sebuleni ukafunguliwa na akaingia mwaume alivaa kinadhifu.

    "Ally mdogo wangu" Shafii akimuita yule mwanaume kwa jina lake halisi.

    "Kaka kuna nini mbona unalia" Allu alimuuliza kaka yake.

    "kaka zako Hamid na Hussein hatunao" Shafii aliongea kwa huzuni huku akitokwa na machozi, Ally aliposikia taarifa hiyo alijikuta akikaa chini kisha machozi yakaanza kumtoka ingawa hakutoa sauti kuashiria analia.

    "Ally jikaze twende hospitali tunahitajika" Shafii aliongea akinyanyuka macho yakiwa mekundu kwa kulia, aliingia ndani halafu akarejea akiwa amevaa viatu na miwani ya jua ili kuficha macho yake.

    "Farida sisi tunatoka, wewe baki. Ally twende" Shafii alisema huku akimnyanyua, kisha wakaondoka hadi nje.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***-



    Taarifa ya kifo cha mmiliki wa kampuni ya Matro tayari zilishawafikia waandidhi wa habari na hadi anafikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti tayari waandishi wa habari walikuwa wamejaa nje ya chumba hicho wakisubiri kupata habari kamili. Hadi gari aina ya Cadillac la milango sita linawasili jirani na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti bado waandishi wa habari walikuwa wamejazana eneo hilo, dereva wa cadillac hilo aliposhuka kwenda kufungua mlango waandishi wa habari walikuwa wapo makini kujua anayeshuka katika gari hilo la gharama ni nani. Shafii alipotangulia kushuka kamera mbalimbali za waandishi wa habari zilikuwa zikifanya kazi ya kumpiga picha tu, waandishi wa habari walikimbilia kumuuliza maswali mbalimbali lakini hawakupata ushirikiano.

    Shafii aliingia ndani ya sehemu ya kuhifadhia maiti akiwa na Ally na alipita hadi ofisini ndani ya ofisi hiyo ya chumba cha kuhifadhia maiti alimkuta msimamizi wake akiwa amekaa kwenye kiti akipitia mafaili mbalimbali.

    "karibu mzee" Msimamizi wa hicho chumba alimkaribisha.

    "Asante" Shafii aliitikia huku akivua miwani ya jua akafuta machozi.

    "pole sana mzee wangu kwa masaibu haya" Msimamizi alimpa pole.

    "asante sana, nakusikiliza" Shafii alisema.

    "Ok nifuateni" Msimamizi aliongea kisha akainuka akaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, Shafii na Ally nao walimfuata kwa nyuma. Yule msimamizi alielekea sehemu yenye mitoto mingi kama ya meza au kabati akiwa anatafuta namba maalum hadi akazifikia namba za mitoto ya makabati ya jokofu ya kuhifadhia maiti yanayofuatana, alifungua mojawapo kisha akafungua lailoni lenye zipu akamuonesha Shafii ambapo aliuona mwili wa mdogo Hussein ukiwa hauna koo. Shafii aliutazama mwili ule kwa umakini huku machozi yakimtoka kisha akamuamuru yule msimamizi afungue jingine, jingine lilipofunguliwa aliuona mwili wa mdogo wake Hamid ukiwa umeharibika kutokana na ajali aliyoipata.

    "hapa kuna mkono wa mtu nasema sikubali" Shafii aliongea kwa hasira.

    "ndiyo maana mzee nikakuita uje kujionea mwenyewe ili uwahi kwa babu kule" Msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti alimuambia.

    "ok nashukuru ngoja niende kwa babu yako kabla mambo hayajawa mabaya" Shafii aliongea huku akimpa burunguru la pesa yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti halafu akaondoka huku Ally akiwa anamfuata, walipotoka nje Shafii alimuambia mdogo wake "Ally wewe nenda ukampe taarifa shemeji Hamisi na wengine juu ya vifo hivi, mimi naenda kwa Mtaalamu Sauti ya radi kule Amboni".

    Shafii aliingia ndani ya gari na dereva akaondoa gari, Ally alichukua teksi naye akaondoka.





    ****



    Safari ya Shafii iliishia Amboni kwa mganga wake ambaye ndiye babu yake yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Bombo, gari yake ilisimama kwenye umbali mrefu kutoka pale yalipo makazi ya mganga huyo kwenye pori dogo lililopo karibu sana na mto Zigi. Shafii alishuka akatembea kwa mguu hadi kwenye kibanda cha mganga Sauti ya Radi kisha akabisha hodi huku akivua viatu vyake, alipopewa ukaribisho aliingia ndani akaketi kwenye jamvi kuukuu mbele ya vibuyu vya mganga.

    "Karibu Shafii mwana Buruhan" Mganga Sauti ya radi alimkaribisha Shafii kwa mara ya pili, Shafii aliitikia ukaribisho huo kisha akaeleza kila kitu kwa mganga.

    "hakuna kinachoshindikana hapa mbele ya sauti ya radi nikinguruma natoa miale maadui wanashindwa wenyewe, kuna kiumbe anakuandama na leo ndiyo kiama chake" Mganga Sauti ya radi aliongea kwa msjigambo kisha akanyanyuka akatoka nje, alirejea akiwa na moto kidogo kwenye chombo kinachotumika kuwekea ubani. Alikiweka kile chombo mbele ya Shafii kisha akamwaga dawa zake kwenye moto uliomo kwenye chombo hicho, moshi mzito ulitanda humo ndani na mzee Sauti ya radi akawa anaimba nyimbo zisizoeleweka huku akimzunguka Shafii akicheza kama anacheza ngoma ya kikabila. Moshi huo ulipokuja kupungua Mganga akiendelea kucheza alihisi anashikwa kiuno wakati akicheza, moshi ulipoisha alihisi anashikwa makalio kwa kutomaswa. Alipogeula nyuma kumuangalia anayemshika alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa anatabasamu.

    "Yaani ungekuwa mwanamke ungefaa kucheza Baikoko kwa jinsi inavyojua kukata kiuno" Zalabain aliongea akiwa bado hajatoa mikono kwenye makalio ya Mganga Sauti ya radi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zalabain alizidi kuonesha uso wa dharau kwa kuyaminya makalio ya mganga Sauti ya Radi na kusanabisha mganga huyo apandwe na hasira sana, Mzee Sauti ya Radi alinguruma kwa nguvu kama simba dume aliyejeruhiwa akiashiria mashetani yamempanda tayari kwa ajili ya kukabiliana na kiumbe aliyejitokeza muda huo ambaye hakuonekana na nia nzuri kwake wala kwa Shafii. Alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain aliambulia patupu kwani hakuonekana kabisa, Mganga alipoona anachezewa akili alizidi kupandwa na hasira mara dufu. Aligeuka kila pande za eneo alilopo lakini hakumuona Zalabain na alimuona Shafii akiwa amekaa pale alipokuwepo akionekana hajui chochote kinachoendelea, Mganga hapo alishusha pumzi kisha akasema "ana bahati sana yule".

    "Nina bahati sana kwa kuweza kushika makalio yako sio, sasa nimeyashika tena ili nikujulishe kwamba bahati hiyo ni yangu tu" Sauti ya Zalabain ilisikika kwa mara ya pili na Mganga akahisi kushikwa makalio kwa mara nyingine tena safari hii alijiona kaingia katika mikono ya basha kwa jinsi alivyokuwa anatomaswa, mara hii hata Shafii alimshuhudia Zalabain akiwa yupo nyuma ya Mganga Sauti ya Radi akifanya udhalilishaji wake. Mganga alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain alipigwa kofi moja lenye uzito wa aina yake hadi shavu lake likachanika kabisa, Zalabain alipotea kwa mara ya pili na moshi mzito ukatanda kama ukungu ikifuatiwa na sauti ya Mganga akilia kama mtoto mdogo. Sauti ya mtu akipigwa vibao ndiyo iliyokuwa imetawala ndani ya nyumba hiyo ya Mganga kwa muda wa dakika kadhaa, ilipokuja kuisha moshi uliotanda ghafla uliondoka papo hapo na Zalabain akaonekana amesimama akiwa ameukanyaga mwili ya Mganga ambao haukuwa hata na dalili ya kuwa na uhai. Alama za mikono zilionekana katika mwili wa Mganga zilizoweka kama mhuri karibu kila sehemu katika mwili wa Mganga huyo, Zalabain alikuwa kasimama akiwa na hasira tena akiwa anamtazama Shafii huku akihema kwa nguvu sana.

    Shafii naye alijikuta akitokwa na upepo bila hata kutarajia na jasho lilikuwa likimvuja kama alikuwa amekaa jirani na moto mkali kwa muda mrefu, kila akitazama macho ya Zalabain yalivyo na hasira ndiyo alizidi kusota kwa kurudi nyuma hadi akafika ukutani kabisa akawa pa kwenda hana akabaki akimtazama Zalabain kwa uoga sana.

    "Unafikiri unaweza kunizuia mimi kwa kutumia nguvu za huyu mzee?" Zalabain alimwambia Shafii huku akiukanyaga mwili wa Mganga Sauti ya Radi kwa nguvu hadi viungo vikawa vinavunjika na kuzidi kumtia uoga Shafii.

    "Ujue kila mwizi na arobaini yake na siku ya arobaini yake ndiyo hukamatwa au kuuliwa, sasa wewe utabaki unapumua kwakuwa arobaini yako bado ila ikifika utakufa kifo cha huzuni kuliko hata hiki cha huyu" Zalabain aliongea huku akimtazama Shafii na akamaliza kauli kwa kuikanyaga shingo ya mganga hadi kichwa chake kikaruka upande aliopo Shafii na kupelekea yowe la uoga limtoke kwa uoga kutokana na kuogopa kichwa hicho kikiwa hakina uhai. Zalabain alipotea papo hapo baada ya kichwa kuruka upande aliopo Shafii na hapo ndipo akili ya kukimbia ilipomjia Shafii na akasimama na kuanza kukimbia bila hata kuangalia wala kuangalia mlango upo wapi, alijikuta akipigiza uso ukutani katika ukuta wa nyumba ya mganga baada ya kukimbilia ukutani akijua ni mlango ulipo kutokana na kuchanganyikiwa na balaa aliloliona.

    "Oooow!" Aliachia ukelele wa maumivu kutokana na kuumia pua yake alipojibamiza ukutani hapo, Shafii alinyanyuka akawa anaona mawenge tu na asijue wapi mlango ulipo. Alipoamua kutimua tena mbio alikutana tena na ukuta ulimbamiza puani kisawasawa hadi zikaanza kumchuruzika damu puani, aliumia sana lakini alinyanyuka na kuanza kukimbia tena mbio akiwa amefumba macho kwa maumivu ya puani aliyonayo. Alifanikiwa kutoka nje na akatimua mbio moja kwa moja bila hata kuangalia mbele tena akiwa na mbio kuliko kawaida, laiti angeshindanishwa na mwanariadha Usain Bolt mwenye uwezo wa kukimbia mita 100 kwa sekunde tisa angekuwa mshindi yeye kwa jinsi alivyokuwa ana kasi ya ajabu kukimbia eneo ambalo alishuhudia mauzauza ya kifo cha Mganga wake wa toka siku nyingi.

    Mbio za Shafii zote hakuwa ameangalia mbele na alikuja kufumbua macho na kurudiwa na akili zake za kawaida baada ya kuhisi amekumbwa kikumbo kikubwa na mtu mwenye mwili wenye ubavu kuliko yeye, alianguka chini moja kwa moja lakini alijiinua akiwa na wasiwasi sana moyoni mwake baada ya kumshuhudia mtu aliyechafuka kwa mchanga mweupe akiwa ameshika gunia.

    "hivi we mzed una akili timamu kweli? Huoni kama ulikuwa unakimbilia mtoni tena kwenye Korongo ambalo chini kuna mamba wengi sana?" Yule mtu alimuuliza Shafii huku akimshangaa sana.

    "hapa ni wapi?" Shafii naye alijikuta anamuuliza yule mtu.

    "We mzee umechanganyikiwa nini hebu angalia kushoto kwako" Yule mtu alimuambia Shafii huku akimuonesha upande wa kushoto, Shafii alipogeuza macho upande wa kushoto aliona yupo mita takribani mbili kutoka mwisho wa Korongo refu ambalo chini yake mto Zigi unapita tena sehemu hiyo ya mto huo mkubwa Tanga nzima ulikuwa umejitanua sana na chini mamba walikuwa wanaonekana bila hata kificho wakiwa wapo pembeni.

    "Hiii!" Shafii alisema kwa uoga akaanza kukimbia upande mwingine ili akae mbali na eneo hilo la korongo.

    "Mzee wangu una matatizo sana, yaani isingekuwa mimi kukuona wakati naenda kuchimba mchanga mtoni basi ungekuwa kitoweo cha Mamba sasa hivi" Yule mtu alimuambia Shafii ambaye alikuwa ametulia tayari na akawa anamsikiliza.

    "asante kijana, sasa utaendaje kuchimba mchanga mtoni wakati kuna mamba?" Shafii alimuuliza yule mtu kutokana na kushangazwa na mtu kwenda kuchimba kwenye mto huo wenye mamba wengi sana, yule mtu aliposikia swali la Shafii alimuonesha kamba nyeusi iliyofungwa begani mwake yenye hirizi pamoja na simbi kadhaa.

    "hii ndiyo kinga yangu Mamba hanishiki ila kwa mgeni ukisogea hata pembeni umeisha, mzee umekumbwa na nini mbona una damu puani na usoni umechanika?" Yule mtu alimueleza Shafii kisha akamtazama kwa udadisi na akagundua ameumia, alimuuliza juu ya kilichomuumiza kwani alikuwa anavuja damu nyingi sana.

    "Kijana ni habari nyingine kabisa usijali sana....asante sana hii ni zawadi yako ya kukomboa maisha yangu" Shafii aliongea kisha akatoa pochi yake mfukoni akamkabidhi noti kadhaa yule mtu halafu akamuaga akaondoka. Ilikuwa bahati kwa yule mtu kupata kitita kikubwa cha pesa kama hicho kwa kumuokoa mtu asiyemjua asiingie katika maskani ya mamba wengi wa mto Zigi ingawa kwa Shafii ilikuwa ni jambo dogo sana kutoa kitita kama hicho cha fedha kwani alikuwa ni tajiri sana. Shafii alirudi hadi alipoacha gari lake akaingia akamuamuru dereva aondoe gari kuelekea hospitali.



    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Muda ambao Shafii alikuwa anaona vibweka vya kuuliwa mganga wake aliyeanza kumtumia miaka mingi iliyopita, ndiyo muda huohuo mdogo wake aliwasili nyumbani kwa shemeji yake Shafii yaani kaka wa Bi Farida mke wa Shafii anayeitwa Hamis. Ally aliingia nyumbani kwa Hamis akiwa na huzuni kwa kuwapoteza kaka zake tena machozi yalikuwa yakitaka kumtoka kila akiwakumbuka kaka zake hao, alipokelewa na mfanyakazi wa ndani wa nyumba ya Hamis na akapelekwa hadi ukumbini ambapo alimkuta Hamis akiwa amekaa kwenye jamvi akinywa shurubati ya maembe.

    "Ally vipi kwema?" Hamis alimuuliza Ally kutokana na hali ya huzuni aliyomuona nayo.

    "si kwema shemeji" Ally alijibu na machozi yalianza kumtoka hapo hapo.

    "heeh! Kunani hebu nieleze?" Hamis alimuuliza Ally.

    "Kaka Hamid na Hussein hatunao" Ally akiongea na hapo machozi yakaanza kumtoka kama chemchem.

    "Eti nini?" Hamis aliuliza kwa hasira na hapo akaanza kunguruma na mwili wake ukaanza kutetemeka kama kamwagiwa maji ya baridi, Ally alipoona hali hiyo aliacha kulia hapohapo akatoka mbio kufuata ukumbi mwembamba uliopo katika nyumba hiyo na alirejea akiwa ameshika udi unaowaka akamuwekea Hamis mbele yake jirani na pua zake.

    "Kuna dhahama, kuna dhahama! Linataka kuikumba familia zetu nasema sikubali lazima nililizuie......nasema sikubali! Nasema sikubali! Nasema sikub...Aaaasrgh!" Hamis aliongea akionekana tayari ameshapandisha mashetani kichwani lakini alijikuta akikabwa shingoni hadi akashindwa kuongea akabaki akitoa ukelele wa maumivu huku akishika shingo yake hadi Ally akaanza kuogopa. Hamis alianza kukoroma huku macho yakiwa yamemtoka kwa namna ya kutisha, Ally alipoona hivyo alinyanyuka akataka kukimbia lakini mtama mzito ulimkuta na yeye akaanguka chini huku mpigaji akiwa hamuoni. Alipoanguka alipigwa kofi la nguvu la kwenye shavu akatulia chini kama maji mtungini, baada ya Ally kuanguka ndipo Hamis alipohisi kuachiwa tangu aanze kukabwa. Alikohoa mfululizo akamkimbilia Ally akamtikisa Ally lakini hakuonesha dalili ya kuamka, Hamis alipagawa kabisa hasa alimpotazama Ally aliyetulia tu.

    "Sijatumwa kuua bali nimetumwa kuzuia, Hamis umerithi majini kutoka kwa babu yako lakini ukataka kuyatumia kupambana na usichokiweza sasa nimeyakaba nikayaua na wewe utakiona. Huyo mwenzako pia kapata aliyostahiki kwa kiherehere chake" Sauti ilisikika ikitokea juu ya dari ikawa inavuma kama mwangwi ikapotea.

    "Hamidaa!" Hamis aliita kwa nguvu huku akimnyanyua Ally.

    "Abee Baba!" Sauti ya kike iliitika ikitokea chumbani.

    "leta funguo za gari upesi" Hamis aliongea akielekea mlangoni, binti wa miaka takribani kumi na nane alimfuata kwa nyuma akiwa na ufunguo wa gari. Hamis alienda kwenye gari lake na yule binti akafungua mlango wa gari Ally akawekwa, geti kubwa lilifumguliwa na Hamis akaingia ndani akawasha akaliondoa kwa kasi.



    SURA YA NNE









    Hali ya jiji la Dar es salaam ilikuwa tulivu na muda huo sehemu mbalimbali za jiji kulikuwa kuna watu wakiendelea na pilikapilika zao za kila siku, upande wa chuo kikuu cha Dates salaam wanafunzi walikuwa wakiendelea na masomo yao kama kawaida yao. Ilikuwa ni vipindi vya pili vya masomo baada ya vile vya asubuhi na wanafunzi wote wenye vipindi muda huo walikuwa wapo madarasani wakifundishwa.

    Darasa la wanafunzi wanaosoma shahada ya sheria masomo yaliendelea kama kawaida na muda huo Professa wa chuo hicho alikuwa akifundisha darasani na wanafunzi walikuwa wapo makini sana kumsikiliza, katikati ya kipindi aliingia kaimu mkuu wa chuo darasani akiwa na mgeni ambaye hakufahamika ni nani hadi muda huo. Kaimu mkuu alimfuata Professa aliyekuwa anafundisha akamuuma sikio kwa sekunde kadhaa, Professa alimsikiliza kaimu mkuu wa chuo kisha akaafiki kwa kutikisa kichwa.

    "Zaina Buruhan you are needed (Zaina Buruhan unahitajika)" Professa aliongea na wanafunzi wote wa humo darasani wakamtazama binti aliyenyanyuka katika viti vya katikati ya darasa.

    "Take your things you are not return today, there is an emergence(Chukua vitu vyako hutarudi leo, kuna dharura)" Kaimu mkuu wa chuo aliongea na Zaina akachukua vitabu vyake akamfuata Kaimu mkuu wa chuo akiwa na yule mgeni kisha wakatoka nje.



    Walipofika nje kaimu mkuu wa chuo alimtambulisha yule mgeni kwa Zaina na mgeni akaonesha kitambulisho chake akajieleza kwa Zaina dhumuni lake la kuja hapo chuoni.

    "kuna dharura gani huko nyumbani?" Zaina alimuuliza yule mgeni

    "nimetumwa tu kuja kukufuata mengine utayajulia huko huko nyumbani, Baba yako na mama yako wameniambia nisikueleze chochote" Yule mgeni alijibu, kwakuwa alikuwa ameshakamilisha taratibu zote za hapo chuoni Zaina na yule mgeni waliondoka kwa pamoja hadi kwenye gari la kifahari alilofika nalo yule mgeni wakaingia kwa pamoja na safari ikaaza, baada ya dakika thelathini walifika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakashuka wakaingia ndani ya majengo ya ndani ya uwanja sehemu ya ndege binafsi. Walipanda kwenye ndege ndogo ya kisasa ambayo ilikuwa ikiwasubiri wao na wakafunga mikanda, milango ya ndege ilipofungwa ndege ilianza kutembea taratibu ikielekea kwenye njia za kurukia na hatimaye ikaiacha ardhi ya jiji la Dar es salaam.

    Baada ya dakika ishirini ndege hiyo ilianza kuinama kwa mbele kisha ikashuka chini taratibu, baada ya muda ndege hiyo iligusa ardhi kisha ikasimama papo bila kutembea ardhini kama ilivyozoeleka ndege ikigusa ardhi lazima itembee mitaa kadhaa ndiyo isimame.

    "mbona ikitua hii ndege haitembei kama ndege zingine" Zaina alimuuliza yule mfanyakazi wa baba yake aliyemfuata chuoni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hii ni tofauti na ndege unazozijua, unaweza ukashuka sasa" Yule mgeni aliongea, Zaina alisogea mlangoni akafunguliwa na akakutana na ngazi ya kushuka kwenye ndege zenye rangi ya dhahabu tofauti na zile alizotumia kupanda. Aliposhuka chini kabisa alikutana na mandhari tofauti na ya uwanja wa ndege wa Majani mapana wa jijini Tanga, anga la eneo hilo lilikuwa jekundu kupitiliza na lisilo na wingu hata. Mbele yake kulikuwa kuna kasri kubwa la kifahari lililotandazwa zulia jekundu kuanzia mlangoni hadi pale aliposimama, alipogeuka nyuma kuangalia ndege aliyoitumia ndipo aliposhtuka zaidi baada ya kubaini hakuwa amepanda ndege bali alikuwa yupo kwenye joka kubwa lenye miguu na masharubu kwenye mdomo na mgongoni alikuwa na kitu kama behewa la treni lilipambwa kwa vito mbalimbali na lilikuwa na ngazi ya dhahabu ambayo ndiyo ile aliyoshuka wakati anatoka. Hadi kufika eneo hilo kumbe alikuwa amempanda mnyama anayejulikana kama dragon bila kutambua akijua ni ndege, alipoona yupo katika mazingira asiyoyaelewa aliachia ukelele wa uoga na kupelekea eneo zima pembeni ya zulia kuanzia kwenye ngazi alizoshukia hadi kwenye mlango wa kaari kuonekane kuna viumbe wenye sura za binadamu wakiwa wamekaa mstari mmoja.

    "We mwanadamu hebu wacha kelele" Sauti ya yule mtu aliyemchukua chuoni ndiyo ilisikika ikitokea kisha yule aliyemdhania ametumwa na baba yake akatoka ndani ya behewa lililopo mgongoni mwa dragon akiwa ana mavazi sawa na viumbe waliojipakaza mstari.

    "hapa ni wapi na wewe ni nani?" Zaina aliuliza kwa uoga.

    "sina mamlaka ya kujibu maswali yako msubiri mwenye mamlaka akujibu maswali yako" Aliongea kisha akashuka akapiga hatua kumsogelea Zaina halafu akamwambia "angalia kule mlangoni kama ukijijua wewe ni mgeni, mkuu wa eneo hili mjukuu wa mfalme anaingia".

    Alipomuambia hivyo alipiga goti la kiheshima na viumbe wote nao walipiga goti na mlio kama wa tarumbeta ulisikika na milango ya kwenye kasri ikafunguka, Zalabain alionekana akija hadi pale alipo Zaina huku akitabasamu akiwa na umbile lake la kibinadamu.

    "Karibu sana Zaina nadhani majibu ya maswali yako yote utayapata" Zalabain aliongea akitabasamu.

    "Wewe ni nani na hapa ni wapi?" Zaina aliuliza akiwa na hofu.

    "Naitwa Zalabain mjukuu wa mfalme na hapa ni ndani ya makao ya himaya ya Majichungu" Zalabain alieleza

    "Majichungu?! Ni wapi?" Zaina aliuliza kwa wasiwasi ingawa tabasamu la Zalabain lilimuonesha kwamba hakuna hofu yoyote.

    "chini ya bahari" Zalabain alijibu.

    "unasema?" Zain aliuliza akiwa na mshtuko kisha akaanza kurudi nyima kwa uoga. "Haina haja ya kurudia mara mbili Zaina utanijua zaidi ila inabidi ukae huku kwa ajili ya usalama wako tu na pia kwa ajili ya tahadhari, hutakiwi kuingizwa kwenye mtego wa panya bila kujijua wakati huna hatia, Hallain!" Zalabain alimueleza Zaina kisha akaita kwa sauti na kupelekea viumbe wengine wenye sura za wanawake warembo wenye asili ya bara la Asia wajitokeze mbele ya Zalabain.

    "Kiongozi wetu tumeitika wito wako" Viumbe hao waliongea kwa utiifu wakiwa wamepiga goti moja kiheshima.

    "Mchukueni huyu mmoja wa wanadamu wenye heshima huku kwetu.......Zayina utakaa hapa na usijaribu kuleta ubishi upate matatizo huku binadamu wanachukiwa kwani wao ndiyo chanzo cha kuwa na wingu jekundu kila muda humu kwenye himaya na mwanga wenye nuru haufiki kutokana na kuibiwa kito Dainun cha baba yangu Zaif" Zalabain aliongea na wale viumbe wakamchukua Zaina wakatoweka naye. Baada ya Zaina kuchukuliwa Zalabain aliingia ndani ya kasri akiwa ameongozana na yule kiumbe aliyemleta Zaina hadi katika chumba cha siri cha ndani ya Kasri hilo, huko ndani ya chumba hicho walikutana na Salmin akiwa amekaa kwenye kiti kimojawapo kilichonakshiwa na mapambo ya lulu. Zalabain na yule kiumbe waliketi kwenye viti vya aina hiyohiyo wakawa wanamtazama Salmin.

    "je mmefanikiwa kuipata Dainun?" Salmin alimuuliza Zalabain

    "hapana bado sijafanikiwa kuipata kwani kila anayetakiwa aende na maji nikimuuliza anasema hana" Zalabain alimueleza.

    "Inabidi uipate hiyo ndiyo taji la kifalme litakaa kichwani mwako hata kama ukilipa visasi hadi ukamaliza bila ile hutakuwa mfalme na hata ukiipata hujalipa kisasi bado taji litakukataa vilevile" Salmin alimuambia Zalabain.





    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Sawa nimekuelewa, enhe wewe Kainun niambie kazi niliyokuagiza imeendaje" Zalabain alimuuliza yule kiumbe aliyemchukua Zaina.

    "Mtukufu mjukuu wa mfalme na mfalme wetu mtarajiwa kazi imeenda kama ulivyoniagiza kwa kumzuia yule mwanadamu anayeitwa Hamisi aliyepandisha vijini vyake akataka kuingilia kazi yako ya kurudisha nuru iliyopetea katika himaya yetu" Kainun alitoa maelezo kwa Zalabain.

    "Vizuri kama umemzuia, je niambie ulimzuia vipi?" Zalabain alimpongeza kisha akahitaji kujua aliyoitumia kumzuia Hamisi asiingilie kazi yake.

    "Baada ya yeye kuwapandisha majini wake kwenye kichwa chake niliamua kumkaba shingo yake hadi yakafa yote kisha nikampiga kofi moja yule mwenzake aliyetaka kuchochea kuharibika kwa kazi yako kwa kuleta udi unaowaka" Kainun alieleza kila kitu alichokifanya hadi Zalabain akatabasamu huku akitikisa kichwa kuashiria amependezwa na kazi yake.

    "Vizuri sana kwa kumtandika kibao huyo Ally Buruhan maana anafuata mkumbo tu" Zalabain aliongea.

    "Kainun napenda asipewe kazi nyingine hadi hali itulie maana majini aliowanyonga ni watoto wa mganga Sharkar aliyeuawa na kaka yangu Saliim miaka mia moja na ushee kupita baada ya kristo kuondoka, kwa mujibu wa maono yangu hao vifo hivyo tayari vishagundulika kwa ukoo wa Sharkar sasa huyu kumuachia kazi nyingine itakayomlazimu kutoka nje ya himaya hii ni sawa na kumkaribisha na vita na kifo chake" Salmin aliongea baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tena macho yake yakibadilika rangi yakawa yanawaka kama ya paka, Zalabain aliposikia maelezo hayo akatulia akajifikiria kwani hakuwa na mwingine mwenye kuaminika na kutumwa katika kazi zake miongoni mwa majini wote wa himaya hiyo isipokuwa Kainun na ndiyo huyu ameambiwa asimtumie na jini mwenye nguvu zaidi na mwenye kuona yajayo. Himaya hiyo kuna baadhi ya watumishi walikuwa sio wa kuaminika kutokana na kuwa miongoni mwa wafuasi wa waziri kkuu aliyetaka kupata ufalme kwa hila sana, alipoambiwa asimtumie Kainun kwake lilikuwa ni jambo jingine gumu kwake.

    "Hapo unanipa wakati mgumu sasa, watumishi hawa sio wa kuaminika huenda kuna wengine ni wafuasi wa aliyekuwa waziri mkuu aliyefungwa katika gereza la giza. Sina wa kuaminika atakayekuwa akisaidia kuzuia kazi yangu isiharibike zaidi ya huyu tu" Zalabain aliongea.

    "Usisononeke Zalabain nadhani yupo jini mwingine mwenye msaada mkubwa kwako kama Kainun na naamini atakufaa kuzuia watu na viumbe wasiohusika wasiharibu kazi yako" Salmin alimuambia Zalabain kwa utulivu.

    "unafikiri nani atakayeweza kuwa mbadala wa Kainun?" Zalabain aliuliza.

    "Baada ya mimi na pacha wangu Saluim kuzaliwa katika kasri la mfalme Mukhatar wa bara Arabu kuna jini mmoja alinieleza kuhusu asili na chanzo cha kufanya mambo yasiyofanywa na binadamu wa kawaida. Jini huyu alinieleza kuhusu asili yangu mimi ni jini na niliyezaliwa na mwanamke wa kibinadamu ila baba yangu ni jini huyu Ibin Zultash na sio mfalme Mukhtar kama nilivyoelezwa wakati nikiwa mdogo na mama yangu ambaye alikuwa Malkia wa himaya baada kifo cha mfalme Mukhtar. Jini huyu ndiye aliyemuelekeza kaka yangu akaenda kwa mganga wa kijini Sharkar akaongezewe nguvu, baada ya kaka yangu kuongezewa nguvu alikosea sharti akanywa damu aliyoambiwa asinywe na hapo akawa muangamizi akaangamiza himaya ya mama yetu na akataka kumuangamiza huyu jini ambaye aliamua kujisalimisha nyumbani kwao ambapo ndiyo hapa Majichungu. Nilipopambana na kaka yangu kwa msaada ya mganga Zaid wa bara Arabu nilifanikiwa kumshinda kaka yangu na nikamfungia kwenye sanduku nikaja kulifukia h Afrika kipindi hicho ni pori tu kwani ilikuwa imepita miaka 100 tu tangu Kristo aondoke duniani, baada ya kazi hiyo niliwachukua Zaid na mama yangu tukaja kuishi huku na tukapokelewa na babu yako kipindi hicho bado ni kjana mdogo wa miaka arobaini hivi. Jini huyo alipokuja huku akifungiwa katika gereza la giza na hakuwahi kutoka hadi leo hii ninavyokusimulia habari hii, huyo ndiyo jini pekee kwa mujibu wa maono yangu anaweza akakaimu nafasi ya Kainun" Salmin alisimulia kisa cha MUANGAMIZI kisha akamtajia jini mwingine mwenye kuaminika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NDUGU MSOMAJI NAJUA KISA HICHO KILICHOELEZEWA NA SALMIN WENGI WENU HAMJAKISOMA, HIYO NI RIWAYA YA KWANZA YA 'MUANGAMIZI' AMBAYO INAELEZEA UZAO WA SALIIM NA SALMIN KAMA MAJINI WENYE NGUVU. SALIIIM ALIFUKIWA NA MDOGO WAKE SALMIN BAADA YA KUWA MUANGAMIZI LAKINI ALIFUKULIWA NA WATU WA KAKIN WENYE KUMTUMIKIA SHETANI ILI WAITWALE DUNIA. KWA WASOMAJI WA MWANZO NADHANI WANAKUMBUKA HIYO RIWAYA AMBAYO NI SEHEMU YA MFULULIZO WA KITABU CHA THE FALL OF KAKIN( KUANGUKA KWA KAKIN).



    "je naweza kulijua jina lake huyo kiumbe?" Zalabain aliuliza.

    "usiseme unaweza bali ni wajibu wako kumjua anaitwa Maalun nadhani ukimpa uhuru atakaimu nafasi ya Kainun... Kainun utaendelea kuwa mkuu wa majeshi ya angani kama ilivyokuwa awali" Salmin aliongea kisha akamtazama Zalabain usoni, Zalabain alipotazamwa hivyo alipiga kofi mara na viumbe wa ajabu wakatokea mbele yake wakiwa na mavazi yanayofanana.

    "Ndiyo mtukufu tumeitikia wito wako" Wale viumbe waliongea kwa utiifu wakipiga goti moja mbele ya Zalabain.

    "nahitaji nimuone Maalun hapa akiwa ametolewa gereza la giza ndani ya sekunde tatu tu" Zalabain aliongea na wale viumbe walipotea kisha wakarejea wakiwa wamemkamata Maalun aliyeonekana kuwa mnyonge sana.

    "muwekeni kwenye kiti na nyinyi muondoke haraka sana" Zalabain na wake viumbe wakakuweka Maalun kwenye kiti wakapotea.

    Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Maalun kuwa huru baada ya kufungea gerezani kwa muda wa miaka takribani 2000 kutokana kuisaliti himaya hiyo na kwenda kuishi kwenye ardhi ya wanadamu, alipoona wale majini waliomleta wamepotea alianza kuwatazama wote waliobaki ambapo hakumtambua Zalabain wala Kainun. Yeye alimtambua Salmin tu na hapo akamuangukia miguuni akaanza kuonesha kuomba msamaha.

    "Maalun yaliyopita na pia kuongelewa kwake kumepita, kosa ulilotenda milenia mbili zilizopita nishakusamehe cha msingi inabidi tuangalie liliopo hapa" Salmin aliongea na wote wakaafiki kwa kichwa, kauli hiyo ilimfanya Maalun atabasamu na apotee ghafla alipokuwa ameamuangukia na akatokea kwenye kiti kimojawapo kilichopo hapo walipo wenzake.

    "Oooh! Namshukuru mungu kumbe nguvu bado zipo, haya nawasikiliza" Maalun aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu kisha macho yake yakaweka kituo kwa Zalabain halafu akamwambia " nakusikiliza ewe mtukufu"

    Zalabain alianza kumueleza Maalun kila kitu hadi majukumu aliyotakiwa kuyafanya, maelezo yalipofikia mwisho wote walimtazama Maalun wakisubiri kusikia uamuzi wake.

    "Kwa ajili ya kuokoa himaya hii isiteketee kwa kukosa mfalme anayestahiki nipo tayari kwa kazi yako ewe mtukufu na hata ungeniambia nikusaidie kuwaangamiza nipo tayari" Maalun alikubali na wote wakatabasamu.

    "vizuri Maalun na anza kazi yako kuanzia sasa, yeyote atakayeingilia kazi ya mfalme mtarajiwa wewe mzuie ashindwe kuendelea kabisa na si kuua maana utamuharibia kazi Mfalme wetu mtarajiwa" Salmin aliongezea kisha akasimama akapotea na wote waliosalia wakatoka ndani ya chumba cha siri.



    ****



    Upande wa ardhi ya binadamu kwa muda huo ndiyo muda ambao Shafii alifanikiwa kufika katika hospitali yake akapewa tiba ya majeraha yaliyompata na kushonwa usoni alipopasuka kutokana na kujigonga alipoona tukio la Mganga Sauti ya Radi akiuawa na Zalabain, alipomaliza kutibiwa ndipo alipopokea taarifa ya kulazwa kwa mdogo wake katika hospitali hiyohiyo upande wa wagonjwa mahututi. Taarifa hiyo ilimfanya atoke sehemu aliyokuwa anatibiwa baada ya kumaliza tu kushonwa vidonda vyake akaelekea mahali zilipo wodi za wagonjwa mahututi wa hospitali hiyo iliyopo chini ya kampuni yake, alipokaribia katika mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi alimuona Hamisi akiwa amekaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akiwa amejiinamia. Shafii alimfuata upesi kisha akamuuliza. "Shemeji kuna nini kimemkuta Ally" Shafuu aliuliza huku akimtazama Hamisi ambaye naye aliishia kumshangaa kutokana na plasta alizonazo usoni pamoja na michubuko kadhaa.

    "Aisee! Shemeji we acha tu. Hii ni vita kali na Ally amekumbwa na kadhia ya kupigwa na kiumbe kisichoonekana na mimi majini yangu yote yameuawa " Hamisi aliongea kwa masononeko.

    "Vipi hali yake ipoje huko wodini?% Shafii aliuliza.

    "bado madakatari wanafanya kazi yao, na wewe vipi mbona maplasta mengi usoni? Umepata ajali? Hamisi alimuekeza Shafii kisha akamuuliza kilichomsibu hadi akawa na plasta nyingi usoni.

    "Yaani shemeji ni bora ingekuwa ajali ingekuwa afadhali kuhusu kisanga kilichonikuta huko kwa Sauti ya Radi, yeye mwenyewe ni mfu hadi muda huu" Shafii aliongea akioneksna anakaribia kukata tamaa kabisa

    "hivi huyu anayeiangamiza familia yangu nimemfanya nini? Au uadui wa kibiashara, yaani Ally mdogo wangu hata kuoa hajaoa ndiyo kwanza anajijenga kimaisha yeye aje kumfanyia hivi kweli. Sikubali hata kidogo nitapambana kulipa kisasi cha hawa wadogo zangu" Shafii aliongea huku machozi yakimtoka kwa uchungu alionao.

    "Shemeji nafikiri hii vita tutakuwa wote katika kukomboa familia zetu, waite Hassan, Yusuf na Halid waje watuongezee nguvu" Hamisi alimuambia Shafii, muda huohuo mlango wa wodi ulifunguliwa na daktari akatoka akiwa anaelekea ofisini kwake. Wote walipomuona walimkimbilia wakawa wanamuuliza ju ya hali ya Ally lakini dakari aliwasihi waende naye ofisi, wote walitii wakaelekea hadi katika ofisi ya Daktari huyo na walipofika wakaribishwa katika viti. Shafii na Hamis walikaa wakawa wanaamuangalia Daktari ili wapewe raarifa za Ally kimatibabu.

    "Mgonjwa anaendelea vizuri kwa sasa ingawa bado hajarejewa na fahamu, tatizo kubwa alilolipata mgonjwa wenu ni kuvunjika kwa taya yake kwani inanekana alipigwa na kitu kizito shavuni na kupelekea damu zivuje sikioni pia ikionekana hata sikio lake limepatwa ingawa bado haijathibishwa na E.N.T surgery wa hapa hospitali. Kwa sasa tumempatia matibabu kwa ajili ya taya lake na baadaye mtaalam wa E.N.T atakuja kucheki sikio lake. Ni hayo tu bosi" Daktari aliongea kwa kirefu juu ya tatizo lililomkuta Ally, maelezo hayo yalimsikitisha sana Shafii na akajikuta anapandwa na hasira zaidi hadi machozi yakawa na yanamtoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Na bado tu huo ni mwanzo tu ila kwa sasa naomba utambue binti yako wa pekee yupo katika himaya yangu" Mwangwi wa sauti ya Zalabain ulivuma katika masikio ya Shafii na kumfanya ashtuke sana hadi Hamisi na Daktari wakamshangaa.

    "shemeji kuna nini?" Hamisi alimuuliza Shafii baada ya kumuona alivyoshtuka na sasa alikuwa anaangalia dari la ofisi hiyo ya Daktari kama ndiyo kwanza analiona kutokana na sauti hiyo iliyomjia masikioni mwake ikitokea huko darini.

    "Ohoo! Zaina, Zaina mwanangu" Shafii aliropoka kisha akatoka mbio huko ofisini kwa daktari hadi Hamisi naye ustahimilivu ukamshinda ikabidi amkimbize shemeji yake, Daktari naye alijitahidi kukimbia kwa uwezo wake wote ili amuwahi Shafii. Wote kwa pamoja mbio zao hazikuzaa matunda katika kumkamata Shafii aliyeonekana amechanganyikiwa kwani aliingia kwenye gari yake aina ya Cadillac akaiwasha bila hata kumuambia dereva wake aliyekuwa yupo pembeni katika mti akiwa amepumzika, Shafii aliwaachia vumbi tu kwa mwendo bao aliondoka nao kama jambazi anayefukuzwa na polisi baada ya kupora benki.

    "Beka daka ufunguo huo tumuwahi huyo asipatwe na matatizo" Hamisi alimwambia dereva wa Shafii kisha akamrushia funguo za gari halafu akakimbia kuelekea lilipo gari lake, Beka naye alimfuata akaingia upande wa dereva akawasha gari, Hamisi naye alishaingia kiti cha pembeni ya derwva akafunga mkanda.

    Gari ya Hamisi nayo iliondoka kwa mwendo uleule alioondoka nao Shafii kuingia barabarani, baada ya kukimbiza gari sana waliona moshi mwingi ukiwa umetanda katika reli zilizopo katika njia iendayo Makorora tena kichwa cha treni kikiwa kimesimama mita kadhaa kutoka eneo la lenye moshi mzito. Barabara nzima ilikuwa imefungwa na kundi hilo na ikawalizimu Hamisi na Beka wasimamishe gari lao wafunge milango vizuri waende kuangalja kuna nini kimetokea, waliposogea karibu zaidi ndipo walipoliona Cadillac la Shafii likiwa lipo matairi na wananchi walikuwa wakimtoa Shafii ndani ya gari hiyo baada ya kufanikiwa kuvunja kioo. Hawakutaka kupoteza muda nao walijichanganya katika kundi hilo la watu wakafanikiwa kufika mbele wakamtoa Shafii ndani ya gari hilo ambaye alikuwa hajitambui, walimpakiza kwenye gari wakishirikiana na wasamaria wema wakampeleka wakamkimbiza hospitali kwani alionekana bado anapumua.



    ****



    Zaina alipelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa kina hadhi kubwa kuliko hata chumba alichokuwa akikitumia kule nyumbani kwao, alikuwa akipewa kila huduma aliyokuwa ya muhimu kwa wanadamu kutoka kwa vijakazi wa kasri la kifalme hadi akajihisi yupo ndani ya sehemu salama. Zilipita siku mbili akiwa ni mtu wa kukaa ndani na hana popote pa kwenda zaidi ya kukaa humo, hali hio ilianza kumchosha tu ndani ya siku hizo mbili tu kutokana na mazoea kutokaa ndani aliyokuwa nayo. Siku ya tatu ilipoingia alianza kulalamika kwa kufanywa mateka kwa watumishi hao waliomletea chakula, onyo alilopewa na Zalabain alilipuuzia na akawa anawatolea maneno mabovu vijakazi hao.

    "Kelele wewe mwanadamu la sihivyo nitakiponda kichwa chako kwa ngumi moja tu ukasalimiane mababu zako waliotangulia" Sauti ya ukali ilisikika na kisha Kainun akatokea akiwa na hasira baada ya kusikia maneno ya Zaina.

    "nirudisheni kwetu hamtaki!" Zain alizidi kuongea kwa ukali kama anaongea na binadamu wa kawaida.

    "unasemaje wewe sasa nakutoa utumbo huku unajiona maana nyinyi wanadamu ndiyo chanzo cha matatizo kwenye himaya hii yote yaani nuru hatuijui tangu Mfalme wetu alipokufa kwa ajili ya ubaya wenu mlioufanya" Kainun aliongea kwa hasira akawa anamfuara Zaina kama Mbogo aliyejeruhiwa na sasa hivi akageuka na kuwa umbo la kutisha. Kuonekana kwa Kainun akiwa na umbile lake la kijini kulimfanya Zaina apatwe na mshtuko na azirai hapohapo, Zalabain naye alitokea hapohapo akiwa na hasira kupitiliza hadi macho yakawa mekundu. Alimpiga pigo la nguvu Kainun hadi akaenda chini kama gunia la udongo ulaya, alimuinua Kainun akamkunja akamuinua akamtazama usoni kwa hasira sana.

    "unataka kufanya nini wewe?!" Zalabain alimuuliza halafu akampiga kichwa kizito.

    "Ewe mtukufu hakika unatambua sisi tunavyowachukia binadamu kwa kutusababisha tusiwe na nuru, binti huyu wa kibinadamu ameanza kutoa maneno machafu katika kasri hili takatifu" Kainun aliongea kwa ghadhabu zaidi.

    "hata kama afanye hivi unamjua ni nani huyu na kwanini nimempa hadhi sawa na familia ya kifalme?" Zalabain aliongea kwa hasira hadi mdomo wake ukawa unatoa cheche akamsukuma Kainun akaanguka chini.

    "Mtukufu huyu si binti wa yule mmoja wa wabaya wako tu" Kainun aliongea akiwa amekaa kitako chini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hata kama ni mtoto mtoto wa mbaya wangu lakini elewa mama yake ni mama yangu ila baba yake si baba yangu, huyu ni dada yangu mdogo Kainun. Unafikiri ukimuua nitakuacha wewe ukiwa hai" Zalabain aliongea kwa hasira zaidi hadi akawa anatetemeka, Kainun aliposikia hivyo alibaini kama ametenda kosa akaomba radhi hapohapo akiwa amepiga magoti.

    "Inuka uende na usitie mguu chumba hichi ushamtisha Zaina" Zalabain alimuambia Kainun ambaye aliinuka na kuondoka.



    y****



    SIKU ILIYOFUATA



    Ndani ya nyumba mbovu yenye vumbi pamoja na samani za kizamani katikati ya jiji la Tanga, ndani ya nyumba hiyo Shafii alionekana akiwa amezungukwa na mke wake, mtoto wake na baba yake mzazi wakiwa wanamtazama kwa chuki huku yeye akionesha uso wa majuto akiwa amesimamia magongo mafupi kutokana na kushindwa kutembea.

    "naomba kuanzia leo usiniite baba yako na mimi nasema sikuwahi na mtoto kama wewe!" Mzee Buruhan aliongea kwa hasira huku akimtazama Shafii ambaye alikuwa analia kama mtoto akiomba msamaha.

    "Mke wangu, mwanangu nisameheni ili baba naye anisamehe" Shafii alipiga hadi magoti ingawa alikuwa anasikia maumivu kutokana na kutopona vizuri mguu.

    "Baba yangu aliyepelekea uzao wangu hawezi akafanya hivi, nina wasiwasi nilikuwa nakuita baba kimakosa tu. Sina baba mshirikina na katili kama wewe" Zaina naye alitia msumari wa moto kwenye kidonda cha Shafii kwa maneno aliyoyaongea.

    "We! We! We! Tena komaeh! Usiniite mkeo mimi, nafikiri nilioana na wewe kwasababu uliniloga lakini sikuridhia hivyo mimi siyo mkeo" Bi Farida aliongea kisha akamsindikiza na singi Shafii hadi akadondoka.

    "Tena umuombe msamaha huyo hapo na siyo sisi" Mzee Buruhan aliongea huku akioneaha kidole kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya nyumba hiyo mbovu ya kizamani, Mtu mwenye joho jeusi alionekana akiingia akjwa ameahika sururu lenye mpini mweupe. Mtu huyo alipomkaribia Shafii, Mzee Buruhan, Bi Farida na Zaina walitoka nje wakimuacha Shafii na huyo mti aliyeingia.

    "We shetani unakufa" Yule mtu alimuambia Shafii halaf akampiga sururu la kichwa kwa nguvu.

    "Aaaaaaaaaaaargh!" Shafii aliachia ukelele wa maumivu lakini alipoangaza macho yake alijikuta yupo sehemu yenye kitanda cheupe na shuka jeupe, alipoona mazingira hayo alizidi kupiga kelele kwa nguvu akidhani labda yupo kuzimu.

    "jamani atajitoa dripu yule, muwahini na sindano ya usingizi kabla hajajitonesha na ile shingo yake iliyovunjika" Ilisikika sauti ya kike ikitokea kushoto kwake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****



    Ilikuwa ni sauti ya muuguzi wa kike baada ya kuona dalili za purukushani anayotaka kuileta Shafii baada ya kuzinduka kutokana na ndoto mbaya aliyokuwa anaiota, mandhari ya eneo alilokuwepo ndiyo ilizidi kumchanganya kabisa akajiona ndiyo kama anaandaliwa kwa ajili ya kupigwa sururu na yule mtu aliyemuota ndotoni. Wauguzi waliokuwa wapo ndani ya wodi aliyolazwa walimuwahi kwa sindano ya usingizi ili asije kusababisha madhara mengine zaidi kwa mwili wake. Hadi muda huo tayari mwili wake ulishapata madhara mengi kutokana na ajali ya gari na laiti kama angecheleweshwa basi ingekuwa ni mengine, Shafii tayari alikuwa kashavunjika shingo.na kiuno katika ajali ya gari aliyoipata kutokana na kuchanganyikiwa baada ya sauti kusikika akilini mwake ikimwambia mwanae kipenzi tayari yupo ndani ya mikono ya mtu asiyemjua tena mwenye nia mbaya na yeye.



    ****





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog