Search This Blog

MALAIKA WA KUZIMU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Malaika Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    Ilikuwa ni majira ya saa moja za usiku alionekana mtu mmoja akikimbia huku akionekana kuwa na wasiwasi....kumbe alikuwa akikimbizwa na watu waliobeba mawe pamoja na mapanga.....mtu huyo alifumaniwa ugoni akiwa na mke wa mtu kwenye nyumba ya kulala wageni(gest) inasemekana mtu huyo alikuwa na tabia ya kutoka kimapenzi na wake za watu...... ghafla mtu huyo alijikwa na kudondoka chini punde watu waliokuwa wakimkimbiza walianza kumshambulia kwa kumpiga mawe mpaka akafa......walipohakikisha kafa waliindoka zao....punde alitokea mwanamke.

    mwanamke huyo alikuwa mweupe kama mzungu akaisogelea maiti ya mtu yule na kuanza kuinyonya damu kisha akatoweka kimiujiza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***************



    Asubuhi palipokucha ilikuwa ni siku ya jumapili

    ??wewe ndiye tegemezi langu sifa kwako ee bwana..

    zilisikika sauti hizo wakiimba nyimbo na mapambio ya kumsifu Mungu waumini wa kanisa moja lililoitwa MWOKOZI WA DUNIA...kanisa hilo lilikuwa la mchungaji EMMANUEL....punde waliacha kuimba na ibaada ikaanza...siku hiyo mchungaji alisema leo ni siku ya maombi ya kubaliki michango ya pesa waliyoitoa waumini wake kwa ajili ya kuendesha kanisa katika mahitaji mbalimbali...watu walianza kusali....baada ya lisaa limoja ibaada ilikwisha na waumini wote waliondoka kurudi majumbani kwao..

    alibaki mchungaji.. baada ya kuhakikisha waumini wote wameondoka akafunga milango ya kanisa kisha akazipiga hatua kuelekea mbele pale anaposimama kuendesha ibaada....alinyoosha mikono yake juu kwa sekunde kadhaa..ghafla kanisa lile lilibadilika pakaonekana kuwa na mazingira ya kutisha sana punde alitokea mtu wa kutisha akasimama pembeni ya mchungaji....wakaanza kumuabudu SHETANI kwa ishara na matendo...ghafla lilitokea joka kubwa ukutani kisha mchungaji akageku na kulifuata joka hilo....akachukua kikombe alichokitumia kuweka divai akakipeleka mdomonj mwa joka hilo..liliachama mdomo na kutema damu ikajaa ndani ya kikombe hicho....kisha akamwaga damu hiyo kwenye ndoo iliyokuwa pembeni yake....kumbe waumini waliokuwa wakija kwenye ibaada walinyonywa damu pasipo wao kujua kinachoendelea...joka hilo alilitumia mchungaji kwa ajili ya kunyonya damu waumi walipokuja kwenye ibaada ili damu hiyo aipeleke kuzimu kama chakula cha malaika wa shetani..



    ****************



    siku zilisonga sasa yapata mwezi mmoja tangu kanisa hilo lilipofunguliwa saifa zilienea jihi zima watu wengi walikwenda kusali kanisani kwa mchungaji Emmanuel. alijipatia waumini wengi sana......waumini waliokuwa wakisali kanisani humo walijikuta wakimuamini na kumuabudu mchungaji Emmanueli ilifika kipindi wakamuona yeye ndio mungu wao....habari zilienea kila kona

    sikumoja mchungaji Emmanuel akiwa katika ibaada alikuwa kashika fuvu la binadamu lakini waumini waliona kama kashikilia bibilia....haikuwa rahisi wao kuona kuwa kile alichokishika mchungaji sio bibilia ni fuvu la kichwa cha binadamu......baada ya ibaada kuisha mchungaji alitangaza kuwa usiku wa leo kutakuwa na ibaada maalumu ya kujitakasa mwili na roho....waumini walilipokea tangazo hilo kwa moyo mmoja...baada ya dakika kadhaa waumini waliondika na kurudi majumbani kwao....

    ilipofika majira ya saambili za usiku watu walianxa kuja kanisani ilipofika saasita za usiku waumini wote walikuwa wameshafika.....mchungaji alisimama eneo alililosimama kila siku wa ajili ya kuendesha ibaada ghafla alituokea malaika wawili kutoka kuzimu...malaika mmoj alisimama upande wa kushoto na mwingine alisimama upande wa kulia mwa mchungaji.....waumini hawakuweza kuwaona malaika hao wa kuzimu....

    ibaada ikaanza mchungaji alisema """kama kunamtu anamatatizo aje mbele nimuombee watu walijitokeza akawa anawaombea huku akiwashika kichwani.........kila aliyemshika aliingiwa na kitu cha ajabu ndani yake......CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika majira ya saa saba za usiku ibaada ilikwisha kila mmoja alirudi nyumbani kwake....



    ***********



    asubuhi palipokucha kila muumini aliyekuwepo kwenye ile ibaada ya jana usiku...walianza kufa moja baada ya mwingine kila siku zinavyozidi kwenda.......vifo vifo hivyo vya mfululizo vilianza kuwastu na kuwaogopesha baadhi ya waumini...sikumoja waumini wakiwa njiani kutokea kanisani......muumini mmoja aitwae ELASTO aliwaambia waumini wenzake kuwayeye anajitoa kwenyekanisa hilo...wengine walimuunga mko wengine walimpinga.....



    alipofika nyumbani kwake alistahajabu kukuta mke na watoto wake watatu wamekufa katika mazingira ya kutatanisha wakati anastahajabu mara ghafla.



    Mara ghafla joka kubwa likajitokeza....ni lile joka lililokuwa kule kanisani kwa mchungaji Emmanuel..likambana sehemu za mbavu akakosa pumzi mpaka akafa......mambo ya ajabu na kutisha yaliendelea kuwatokea waumini wa kanisa la mchungaji Emmanuel.....ikafika kipindi waumini waliosalia wakaanza kufanya vitendo vya ukatili wa hali ya juu...waumini wanawake walianza kufanya uhasherati kwa kuchukuwa wame za watu kwa kuwashawishi kufanyanao ngono.....na kila mwanaume aliyeshiriki ngono na muumini wa kanisa hilo basi haikupita wiki mtu huyo lazima afe......mambo yaliendelea kuwa magumu kwa taifa........kadri siku zilivyozidi kusonga ndivyo wafuasi wa kanisa hilo walizidi kuongezeka......



    **************



    upande mwingine alionekana mchungaji Emmanuel akiwa nyumbani kwake akimuabudu shetani kwa ishara na vitendo...baada ya dakika kadhaa kupita alijitokeza yule malaika kutoka kuzimu akasema"" kesho ni siku ya kutoa Sadaka kwa Mungu wetu LUSYFAR.....inahitajika damu ya binadamu msichana bikra...baada ya kutoa taarifa hiyo akatoweka kimiujiza.....mchungaji alichukua simu yake na kumpigia mzazi wa binti mmoja aliyekuwa na umri kati ya miaka kumi na saba hadi kumi na tisa... mzazi wa binti huyo alipoipokea simu ya mchungaji alikuwa anasema hivi"""kesho alfajiri ya saa 10 namuhitaji binti yako kanisani kwangu aje kunisaidia kuandaa sakrament takatifu pamoja na kuandaa somo la kesho kabla misa haijaanza..

    mzazi wa binti huyo alilipokea ombi la mchungaji kwa sababu alimuamini kuliko anavyomuamini Mungu muumba wa vyote.....akamuita binti yake na kumwambia alichoambiwa na mchungaji....ilipofika majira ya saa 10 mzazi wa binti huyo alimchukua binti yake na kuliwasha gari wakaelekea kanisani kwa mchungaji Emmanuel.



    wakati huo huo alionekana mchungaji akimalizia kujiandaa kisha akaingia kwenye gari na kuelekea kanisani siku hiyo ilikuwa ni jumapili ni siku ya ibaada kama ilivyo kawaida ya madhehebu ya kikristo......alipofika alifungua mlango na kuingia upande wa ndani....siku hiyo ilikuwa maalumu kwa kutoa kafala la damu ya binadamu......kwa ajili ya sadaka kwa Shetani...



    *************

    baada ya muda kidogo yule mzazi alifika kanisani hapo na kumuacha binti yake kwa mchungaji kisha akaondoka zake kurudi nyumbani.......baada ya mzazi huyo kuondoka mchungaji alizipiga hatua kuufuata mlango kisha akaufunga...akarudi mpaka pale alipokuwa amesimama yule binti..

    mchungaji akasema""fumba macho nikutakase kwa maombi kabla haujagusa sakramenti takatifu....binti yule alifumba macho na mchungaji akaanzisha maombi...wakiwa wanasali mchungaji alitoa kitambaa kilichokuwa na madawa ya kulevya akamziba kwenye pua kwa kutumia kitambaa hicho....baada ya sekunde kadhaa binti huyo alipoteza fahamu..kisha mchungaji akamfunga kamba mikono na miguu na kumziba mdomo kwa kumfunga kitambaa kisha

    akambeba na kumlaza juu ya meza kwa ajili ya kafala.. mchungaji akapifa hatua mbili kurudi nyuma kisha akaaimama kando akimsubiri malaika kutoka kuzimu aje kuifanya kazi yake...



    ************



    muonekano wa ndani ya kanisa ulianza kubadilika pakaonekana ni sehemu ya kutisha sana...kisha akajitokeza yule malaika wa kuzimu...akiwa na mtu wa kutisha sana...mtu huyo mwili wake uliinekana ni mifupa tu. huku akiwa amevalia joho jeusi lililofunika sehemu ya kichwa chake huku ameshikilia rozali ya ajabu iliyokuwa na msaraba usio wa kawaida....wakazipiga hatua mpaka pale alipokuwa kalazwa binti yule....wakamzunguka kisha kazi rasmi ya kumtoa kafala binti huyo ikaanza... walijaribu kwa dakika kadhaa lakini walishindwa...malaika wa kuzimu alistahajabu sana....haijawahi kutokea hata sikumoja yeye kushindwa kuifanya kazi ya shetani...alipomtazama binti yule aligundua kuwa binti huyo si wakawaida inaonesha kunakitu ndani yake.....kinacho mlinda....kumbe binti huyo alizaliwa kwa ajili maalumu....ambayo hakuna hata mmoja aliyetambua ni kitu gani kilichomo ndani ya mwili wa binti huyo....walijitahidi lakini walishindwa kabisa....masaa yalisonga hatimae pakaanza kukucha.....wakati wanamstahaju binti huyo mala ghafla alizinduka....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    binti huyo aliogopa sana baada ya kufumbua macho na kuona yupo katika mazingira ya kutisha sana..palionekana kujaa mafuvu na mifupa ya binadamu...kwa mbali aliona moto mkubwa sana ukiwaka kwa kasi kama unapulizwa na upepo....alipo angaza angaza macho alistahajabu kumuona yule malaika wa kuzimu akiwa na mtu wa kutisha sana.......alipotaka kupiga kelele alimuona mchungaji Emmanuel amesimama mbali akimtazama....binti huyo aitwae..Monica alinyanyuka haraka kutoka pale juu ya meza alipojaribu kukimbia alidondoka chini kwa sababu alikuwa amefungwa kamba miguu na mikono...

    malaika wa kuzimu pamoja na yule mtu wa kutisha walichanganyikiwa.......mchungaji Emmanuel macho yalimtoka.....wakati anatahamaki...Malaika wa kuzimu pamoja na yule mtu wa kutisha walitoweka kimiujiza na kutokomea kusikojulikana......mchungaji Emmanuel alizipiga hatia za haraka haraka kumfuata binti Monica akamfungulia kamba alizokuwa kamfunga........dakika zilizidi kusonga na palizidi kukucha....alipoitazama saa yake ya mkononi ilikuwa ni saa moja kasoro......akakimbia haraka kwenda kule mbele anaposimama kuiendesha ibaada....alipofika alinyanyua mikono yake juu ili muonekano ule wa kutisha utoweke paonekane ni ndani ya kanisa....alijaribu lakini alishindwa....monica aliamua kutimua mbio akaufuata mlango wa kutokakea upande wa nje..

    akaufungua na kutoka haraka akatimua mbio...



    wakati huohuo waliinekata waumini wa kanisa hilo wakiwa njiani kuelekea kanisani kwa ajili ya kumuabudu mungu wao...



    ****************

    kule mdani ya kanisa alioneka Mchungaji Emmanuel akiendelea kuhangaika kurudisha muonekano wa kanisa kutoka katika muonekano wa kuzimu.....jasho lilimtoka mpaka shati alilokuwa kalivaa lililowana.....alijitahidi kufanya miujiza ya nguvu za giza....hatimae alifanikiwa kulirudisha kanisa katika hali ya kawaida...akatimua mbio mpaka mlangoni akaufungua mlango na kuuwacha wazi......baada ya dakika kadhaa kupita waumini walianza kuingia mmoja mmoja mpakakanisa likajaa kisha ibaada ikaanza...



    **************



    upande mwingine alionekana binti monika akitimua mbio kuelekea nyumbani kwao....monica alikuwa peku lakini hakujali kwa sababu ya uwoga alikimbia hatimae alifika nyumbani kwao....lakini hakumkuta mama yake...kumbe kipindi monica anaelekea nyumbani kwao ndio wakati mama yake alikuwa anatoka nyumbani kuelekea kanisana kwa Mchungaji Emmanuel..

    monica aliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake akapanda kitandani akalala.....lakini hakupata usingizi...ile picha ya kule kuzimu ilimuijia mara kwa mara...alijiuliza maswali mengi lakini hakupata jibu....usingizi ulianza kumnyemelea hatimae akasinzia kabisa...



    ***********

    kule kanisani alionekana mcgungaji akiendelea na ibaada lakini akili na mawazo yake yote yalikuwa yakiwaza juu ya binti Monica.....alijiuliza Monica ameshajua siri ya kanisa hili je akieneza habari hizi itakuwaje????wakati akiwaza hivyo malaika wa kuzimu alijitokeza na kusimama pembeni yake...mchungaji aliendelea kuhubiri...yule malaika wa kuzimu alizipiga hatua na kuwagusa baadhi ya waumini waliokuwa wamekaa kwenye viti vya mbele. kisha akarudi kusimama pembeni kwa mchungaji emmanue, mchungaji aliendelea kuhubiri ghafla wale waumini walioguswa na malaika wa kuzimu wakaanza kudondoka chini na kagalagala sakafuni kama wameugua kifafa, mchungaji emmanuel aliendelea kupiga maombi kisha akawafuata waumini wale waliodondoka chini na kuwagusa mapaja yao ya uso huku akiendelea kupiga maombi baada ya dakika kadhaa watu wale walinyanyuka na kurudi katika hali zao za kawaida. baada ya lisaa limoja ibada iliisha na waumini walianza kurudi majumbani kwao

    ***********

    mama monica alionekana akiingia nyumbani kwake alipofika alistaajabu kukuta milango ipo wazi aliingia haraka akapitiliza mpaka chumbani kwa monica, alipofungua mlango wa chumba cha monica;monica alipiga kelele kwa uwoga mama monica akauliza umepatwa na nini mwanangu????? monica alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha alianza kumusimulia mama yake alichokiona kanisani, mama monica alicheka na kusema pole mwanangu hiyo itakua ni ndoto tu umeota usingizini kwani umelala kwa muda gani?? monica hakujibu kitu alibaki kimya, mama yake hakujali aliamua kuondoka kabla hakafika mbali alisikia monica akipiga kelele akarudi haraka chumbani kwa monica, alipofungua mlango hakuanini alichokiona...



    mama monica aliogopa sana baada ya kumuona Monica ametapakaa damu kwenye nguo zake...pia damu zilitapakaa chumba kizima.....akaingia haraka akamvuta monica na kutokanae upande wa nje.....kisha akamuuliza""umepatwa na nini?? mama monica aliuliza huku akimkagua mwili mzima alistahajabu hakuona jeraha lolote....

    monica mwanangu niambie nini kilichotokea???

    monica hakujibu kitu alibaki kimya huku akimtazama mama yake kwa macho ya mshangao..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kume kipindi mama monica alivyotoka na kumuacha monica chumbani....kuna mtu wa kutisha alijitokeza na kutaka kumdhuru monica lakini alipojaribu kumgusa monica ...kuna miale ya mwanga ilichomoza kutoka mwilini kwa monica na kumpiga mtu yule akapasuka kama puto...damu ziliruka na kutapakaa chumba kizima...

    pia ziliruka kwenye nguo alizokuwa amezivaa monica...



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog