Search This Blog

MALAIKA WA KUZIMU - 2







    Simulizi : Malaika Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Pili (2)



    mama monica aliendelea kumuuliza mwanae kwa msisitizo ili amwambie nini kimetokea..lakini monica alibaki kimya hakusema jambo lolote..

    mama monica aliendelea kumshangaa monica.

    kisha akasema ""nenda ukaoge.....

    monica akazipiga hatua kuingia ndani akiongozana na mama yake...walipoingia chumbani kwa monica walistahajabu kukuta chumba kisafi hakina hata chembe ya damu...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************



    upande mwingine alionekana mchungaji akiwa ndani ya kanisa lake...akizipiga hatua kuufuata mlango kisha akaufunga.........baada ya dakika kadhaa kupita yule malaika wa kuzimu alijitokeza huku uso wake ukionekana kuwa na hasira....akasema"""wewe ndio chanzo cha yote haya kwa nini ulimleta binti ambaye damu yake imezungukwa na ngivu zisizo za kawaida..ina maana ulikosa binti mwingine tofauti na huyo???

    mchungaji alibaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema"" naomba unisamehe ewe Malaika wa kuzimu......aliomba msamaha uku akifanya ishara ya kusujudu kwa kuinamisha uso wake chini kisha akagusa miguu ua malaika wa kuzimu...

    ""malaika wa kuzimu akazipiga hatua kadhaa huku akisema ili usamehewe nahitaji damu ya watu wasiopungua hamsini (50) siku ya ibaada ya juma pili.....kisha akatoweka kimiujiza

    mchungaji Emmanuel alikasirika sana....alimchukia monica kwa kuvuruga mipango yake...



    *****************



    siku ya juma pili ilipofika mchungaji Emmanuel alidamka alfajiri na kuwahi kanisani....alipofika alinyanyua mikono yake juu ghafla watu wawili walio onekana kama wafu walijitokeza huku miiliyao ikiwa imeoza na kuzungukwa na Funza..

    kisha mchumgaji akawaongoza watu wale mpaka kwenye chumba kidogo kilichokuwa ndani ya kanisa hilo....chumba hicho kilikuwa na siri nzito kuhusu kanisa la mchungaji Emmanuel...kulikuwa na mafuvu mengi ya binadamu...aliwafungia watu wale ndani ya chumba hicho kisha akatoka na kuelekea pale anaposimama kuendesha ibaada

    baada ya lisaa limoja kupita waumini walianza kuja kanisani baada ya muda kanisa lilienea waumini na ibaada ikaanza...



    *************



    upande mwingine alionekana mamaonica akimsisitiza monica ajiandae waende kanisani kwa sababu walichelewa kudamka. monica alikataa kwenda kanisani jumapili hiyo..

    mama monica ilibidi aondoke zake na kumuacha monica nyumbani.....

    mama monica alipofika kanisani alikuta ibaada imeshaanza akaingia na kujumuika na waumini wengine........wakati mchungaji akiendelea kuhubiri

    ghafla milango ilijifunga kisha ukazuka moto mkubwa waaumini walianza kupiga kelele za kuomba msaada...lakini mlango ulikuwa umefungwa moto ulizidi kuwaka ukaanza kuwaumguza baadhi ya waumini walipoteza maisha hata mama yake monica alikuwa ni miongoni mwa waumini waliokufa kwa kuungua moto........ghafla moto ukazimika kimiujiza na mlango ukafunguka......waumini waliobaki hai walitimua mbio kutoka upande wa nje huku wengine wakiwa wanamajeraha ya kuungua kwa moto..

    cha kistahajabisha kanisa halikuungua hata viti vya mbao havikuguswa na moto huo..

    kila muumini aliyetoka hai himo ndani ya kanisa hakuweza kukumbuka chochote kilichotokea...yeye aliona kama ibaada imekwisha.........baada ya lisaa limoja kupita hapakuwepo na mtu hata mmoja nje na ndani ya kanisa hilo isipokuwa mchungaji.....malaika wakuzimu akajitokeza kisha akasema umesamehewa kwa kazi nzuri uliyoifanya kisha akatoweka kimiujiza...mchungaji alizipiga hatua mpaka kwenye kile chumba alichokuwa amewafungia wale watu wawili walio onekana wafu walio hai.....alipofungua mlango mara ghafla

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wale wafu wawili walionekana kupiga kelele za kuomba msaada....huku wakijikujakunja miili yao kama wanaunguzwa na moto mkali....mchungaji alibaki akiwatazama watu hao.....kisha akafunga mlango wa chumba hicho akazipiga hatua kuelekea pale anaposimama kuiendesha ibaada..

    akanyoosha mikono yake juu.....baada ya sekunde kadhaa malaika wa kuzimu alijitokeza akasema""siku ya leo umefanya kazi nzuri sana umemfurahisha MUNGU WA KUZIMU..ameamua kukuongezea nguvu za ziada...aliyasema maneno hayo huku akugusa paji la uso la mchungaji Emmanuel na kumkabidhi kitambaa cheupe....na kusema utatumia kitambaa hiki kila unapoendesha ibaada utakuwa umekishikiria kwa mkono wako wa kushoto...kisha akampa bibilia iliyoandikwa kwa maneno yaliyogeuzwa juu chini""" bibilia hii asiwahi kuigusa binadamu yeyote tofauti na wewe utaitumia kuendesha ibaada.....utakapokuwa unahubiri kwa kutumia bibilia hii utakuwa unamtukuza na kumsifu Mungu wa kuzimu...lakini binadamu wa kawaida wataona kama unahubiri injiri......Mchungaji alipokea kitambaa pamoja na bibilia hiyo..

    Malaika wa kuzimu akazipiga hatua kuufuata ukuta uliokuwa mbele ya kanisa hilo akachora Arama ya nyota yenye pembe sita kisha akachora msaraba uliogeuzwa juu chini/chini juu....akazipiga hatua za taratibu akanyoosha mkono wake kwa sekunde kadhaa likajitokeza beseni lililojaa damu ya maiti waliokufa muda mchache...damu hiyo ilionekana kuwa na rangi nyeusi kwa mbali....kisha akasema utatumia damu hii utakapokuwa unafanya ibaada kwa kuiweka kwenye chupa ya plastiki na kuwanyunyizia waumini kipindi unafanya maombi...binadamu wa kawaida hawataweza kutambua kuwa ni damu ya maiti....bali wataona niaji ya kawaida....

    kisha Malaika wa kuzimu akatoweka kimiujuza....ghafla ulifuka moshi mkubwa ukitokea kwenye kile chumba alichowafungia wale wafu wawili walio hai.....

    akazipiga hatua za haraka kwenda kutazama moshi huo unatokana na nini.



    **************



    Upande mwingine alionekana monica akitoka chumbani kwake na kuelekea sebuleni....alipofika alichukua picha ya marehemu baba yake na kuitazama huku machozi yakimlenga machoni..

    baba monica alifariki miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya damu(kansa) baba monica alikuwa ni mtu mwenye imani kali sana alikuwa akijitahidi kuyafuata yale yanayompendeza Mungu...ingawa alifanya machache ya kidunia pasipokujua kwa sababu hakuna binadamu aliyekamilika....

    miaka kumi na nne(14) iliyopita kabla monica hajazaliwa kipindi hicho mama monica alikuwa na ujauzito upatao wa miezi miwili.....siku hiyo majira ya saa mbili za usiku baada ya kumaliza kula chakula cha usiku baba monica aliingia chumbani na kuanza kusali akimuomba mungu amlinde yeye pamoja na familia yake..alisali kwa masaa matatu mfululizo.....ilipofika saa tano alipanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi...baada ya dakika kadhaa kupita usingizi ulimnyemelea akasinzia kabisa....akiwa usingizini aliota ndoto.....aliota anaongea na mungu...akaambiwa kuwa mtoto aliye tumboni mwa mke wake sio mtoto wa kawaida mtoto huyo atazaliwa kwa ajili ya kupambana na kuangamiza nguvu za giza...

    asubuhi palipokucha baba monica alipoamka alishindwa kunyanyuka kitandani mwiliwake ulikuwa umepararaizi hata hakuweza kuongea neno lolote.....alikuwa ni mtu wa kubebwa na kurudishwa kitandani kwa miaka kumi na nne(14)

    mama monica alihangaika kila hospitali lakini alipofanyiwa vipimo iligundulika kuwa anasaratani ya damu(kansa) monika alipotimiza umri wa miaka kumi na nne(14) baba yake aliiaga dunia...kwa sasa monica anaumri wa miaka kumi na saba(17)ni miaka mitatu tangu baba yake amefariki...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***************

    Monika alifuta machozi akairudisha picha ya baba yake pale juu ya ukuta..kisha akatoka nje akafunga mlango na kuzipiga hatua kutoka nje ya geti....



    **********

    kule kanisani alionekana mchungaji akizipiga hatua kuufuata mlango wa kile chumba cha siri alipofungua mlango alistahajabu sana,,, aliona wale wafu wawili wamebadilika na kuwa mifupamifupa,, vichwa vyao vilionekana kuwa fuvu..akaufunga mlango haraka akazipiga hatua kutokanje ya kanisa....

    wakati huohuo monica alikuwa njiani kuelekea kwenye kanisa hilo baada ya kuona mama yake amechelewa kurudi nyumbani... alipolikaribia kanisa la mchungaji Emmanuel ghafla aliingiwa na roho ya ajabu akawa jasiri sana.....

    mchungaji alipotoka nje alikutana uso kwa uso na Monica......mchungaji alistuka sana kumuona monica....sasahivi monica uso wake ulionekana kuwa mkakamavu mchungaji aliweza kugundua kuwa monica sio binadamu wa kawaida ananguvu za ajabu...mchungaji alitimua mbio kuingia ndani ya kanisa kisha akaufunga mlango.

    monica alishangazwa na kitendi hicho akasukuma mlango ili aingie ndani amuulize mchungaji kama mama yake alifika kanisani hapo....mlango ulifunguka kwa urahisi monica akaingia upande wa ndani....mchungaji alistahajabu kuona monica kaweza kufungua mlango wakati yeye aliufunga kwa ndani kwa makomeo matatu.monica akaanza kuzipiga hatua kuelekea kule mbele alipokuwa amesimama mchungaji



    Mchungaji macho yalimtoka jasho likaanza kumtiririka...akauliza kwa mshangao ""unataka nini??kilikoni?? mbona huu sio muda wa ibaada!!!

    mchungaji aliuliza maswali hayo ya mfululizo huku akimtazama monica kwa macho ya mkazo..

    monica hakujibu kitu alizidi kuzipiga hatua kumsogelea mchungaji....

    mchungaji Emmanuel aliamua kutimua mbio kuufuata mlango wa dharura wa kanisa..akaufungua na kutimua mbio akatokomea kusikojulikana...monica alibaki na mshangao akijiuliza kwa nini mchungaji anakimbia!!! alafu macho yake yakionesha wazi kuwa anamuogopa..monica alijitazama kuanzia miguuni akaangalia mikono yake kisha akajisemea moyoni"kwani mwili wangu umepatwa na nini!!! mbona nipo vilevile!!!! wakati monica akijiuliza maswali hayo,,,,,,,,malaika wa kuzimu alijitokeza nyuma ya monica akawa anamtazama monica akijikagua mwilini....monica akanyanyua shingo yake alipotazama huku na kule aliona kuna kioo kule mbele kwenye ukuta..akazipiga hatua za harakaharaka akajitazame kwenye kioo kwa kidhani huenda sura yake inadosari....wakati huo malaika wa kuzimu alikuwa akitembea nyuma ya monica..

    monica alizipiga hatua huku akiangaza angaza macho yake huku na kule..akageuza shingo yake upande wa nyuma hakuona kitu....lakini malaika wa kuzimu alikuwa akitembea sambamba na monica ingawa monica hakuwa na uwezo wa kumuona ......alipokikaribia kioo akaanza kujitazama kwa kupitia kioo hicho...alistuka kumuona mwanamke mweupe kasimama nyuma yake...alipogeuza shingo yake hakuona kitu chochote....akakitazama tena kioo alimuona malaika huyo akinyanyua mikono kwa kutaka kumgusa bega...monika aliogapa sana akageuka nyuma haraka lakini hakuona kitu......akazipiga hatua kuindika kwenye kioo hicho....ghafla alihisi sauti ya kitu kimedondoka alipotazama aliona kuna mlango umefungwa...akahisi sauti ilitokea ndani ya chumba hicho chenye mlango uliofungwa.....akazipiga hatua kuifuata mlango ..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipoukaribia aligusa kitasa ili akizungushe mlango ufunguke.....

    macha yakamtoka malaika wa kuzimu akataka amguse monica ili asifungue mlango huo..alipoinua mkono wake kumgusa monica kuna miale ya mwanga ikachomoza kutoka mwilini kwa monica...malaika wakuzimu alihisi kuungua akatoweka kimiujiza...

    monica akasita kuufungua mlango ule..akasimama kwa sekunde kadhaa kisha akageuza na kuufuata mlango wa kutoka nje ya kanisa hilo.....



    ***************



    upande mwingine alionekana mchungaji akitimua mbio kuelekea nyumbani kwake.....alioagawa mpaka akalisahau gari lake alilokuwa amelipaki mbele ya kanisa...baada ya muda mchache kupita alifika nyumbani kwake akaingia upande wa ndani..akafunga mlango.....akafungua friji akatoa maji ili anywe.....malaika wa kizimu akajitokeza..

    na kusema""huyu binti ni hatari hawezi kufa kirahisi....nakuamuru ndani ya siku saba hakikisha roho ya binti huyo inatoka na kuacha kiwiliwili. kisha akatoweka...mchungaji aliogopa sana akaingia chumbani kwake akasimama kwenye kona ya chumba akatanua miguu yake na kutengeneza alama ya pembe tatu akaanza kuongea na sheteni kwa kutumia alama za vidole vyake huku akiongea lugha isoyojulikana hapa duniani....alipomaliza alitoka upande wa nje na kurudi kule kanisani...kumbe aliambiwa aende kwenye kile chumba cha siri kilichomo ndani ya kanisa akachimbe shimo kisha amzike binadamu aliye hai...hiyo itakuwa ni zindiko lake hivyo monica hatoweza kufanya lolote akija humo kanisani....kisha akaambiwa usiku wa leo utaongozana na malaika wawili atakuwepo malaika wa kuzimu sambamba na malaika wa kaburi...mtakwenda nyumbani kwao monica kisha mchukue picha ya baba yake iliyopo ukutani picha hiyo ikawekwe juu ya lile shimo alilozikwa binadamu hai..kwa kufanya hivyo monica hatakuwa na nguvu tena.....



    *************



    upande mwingine alionekana monica akizipiga hatua kurudi nyumbani kwao njaa ilianza kumkamata akawa anatembea hatua za kinyonge..

    alipofika alimuita mama yake lakini nyumba ilikuwa kimya hapakuwepo na mtu ndani yake...monica hakujali alikumbuka siku mbili zilizopita mama yake alisema jumapili hii kunasherehe ya chama chetu tunavunja kikoba siku ya jumamosi hivyo tutafanya sherehe siku ya jumapili.......akaingia jikoni akaanza kupika...alipomaliza alikula kisha akaoga akaenda sebuleni kutazama Runinga....ilipofika majira ya saa tano za usiku monica aliona mama yake anachelewa kurudi akaamua kwenda kulala..alipofika chumbani alipanda kitandani.....baada ya sekunde kadhaa alitika chumbani na kurudi sebuleni...akaichukua picha ya baba yake iliyikuwa ukutani...akarudi chumbani kwake akapanda kitandani akalala chali huku ameikumbatia picha ya baba yake..

    wakati huo huo mchungaji alikuwa akiwasubiri wale malaika...malaika wa kuzimu na malaika wa kaburi ili waende nyumbani kwao monica.....baada ya muda wakajitikeza na safari ya kwenda nyumbani kwao monica ikaanza....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Monika aliendelea kuikumbatia picha hiyo...baada ya dakika kadhaa kupita usingizi ulimnyemelea na hatimae akasinzia kabisa.......

    upande wa nje alionekana mchungaji akiwa na malaika wa kuzimu pamoja na malaika wa kaburi..



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog