Search This Blog

MALAIKA WA KUZIMU - 3

 







    Simulizi : Malaika Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakazipiga hatua mpaka kwenye dirisha la chumba cha monica....malaika wa kuzimu alimgeukia mchungaji kisha akamgusa wakatoweka kimiujiza wakajitokeza upande wa ndani ya chumba cha monica.......kisha malaika wa kuzimu akamuaru mchungaji aichukue picha iliyokuwa juu ya kifua cha binti monica......mchungaji alizipiga hatua za taratibu kwa kunyatia....alipomkaribia monica mchungaji alinyoisha mkono wake ili aichukie picha hiyo....ghafla monica alijigeuza na kulala kiubavu ubavu....mchungaji akasita akamgeukia malaika wa kuzimu wakakutanisha macho....malaika wa kuzimu akasema chukua muda unazidi kwenda....kabla haijafika saa sita na dakika moja yatupasa tuwe tumeondoka humu ndani.....jasho lilianza kumtoka mchungaji huku akitetemeka kwa uwoga wa hali ya juu......kwa sababu monica hakuwa binadamu wa kawaida alikuwa na nguvu zilizomzunguka mwilini mwake....mchungaji akaupeleka mkono wake akaigusa ile picha akaivita taratibu....monica akajigeuza tena alalia ubavu mwingine....mchungaji akasita akaiachia picha ile.....



    ***************



    wakati huohuo upande mwingine alionekana muumini mmoja akitimua mbio kuelekea kanisani kwa mchungaji emmanuel....alikwenda kwa ajili ya kumuomba mchungaji aende nyumbani kwake akamfanyie maombi mtoto wake mdogo aliyepooza mwili ghafla......alipofika kanisani aliingia moja kwa moja mpaka ndani ya kanisa kwa sababu mlango ulikuwa wazi....akapaza sauti ""MCHUNGAJIII nisaidie mwanangu anakufa.....aliita kama mara kadhaa lakini aligundua kuwa mchungaji hakuwepo kanisani humo akaamua kuanza kusali mwenyewe kumuombea mtoto wake.......ibaada ya dakika mbili kupita ikatimia saa sita kamili za usiku..muumini huyo aliendelea kusali huki akikemea....ilipotimia saa sita na dakika moja muonekano wa ndani ya kanisa ukaanza kubadilika.....pakaonekana kuwa ni sehemu ya kutisha mafuvu ya vichwa vya binadamu yalikuwa ni mengi sana walionekana watu wawili wameuzunguka moto huku wakiimba kwa lugha isiyoeleweka....wakati huo ye mtu alikuwa anasali huku amefumba macho...alipomaliza alifumbua macho alistahajabu kujikuta yupo sehemu ya kutisha.....aliogopa sana akaanza kutimua mbio huku akipiga kelele ghafla alitokezea kwenye pango lililokuwa na moto uliokuwa ukowaka kwa kasi kama unapulizwa na upepo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****************



    upande mwingine kule nyumbani kwao monica alionekana mchungaji ameichukua picha ile alipogeuka nyuma hakumuona malaika wa kuzimu na malaika wa kabiri...walitoweka mda ule kabla ya saa sita na dakika moja....mchungaji akapagawa kila alipojaribu kutoweka kimiujiza ilishindikana alibakia himo humo ndani ya chumba cha binti monica....akajaribu kufungua mlango ili atimue mbio kuelekea sebuleni..atafute namna ya kutoka uoande wa nje......alipogusa kitasa monica alistuka akaamka......



    monica akastuka kumuona mchungaji yumo chumbani kwake...akauliza""umefikaje humu ndani au ulikuja na mama??? mchungaji aliogopa macho yakamtoka alijua huenda monica alikuwa anaona yote yaliyokuwa yanaendelea..hivyo kamuuliza swali hilo kwa kumtega....

    mchungaji alisita kuongea kisha akajibu kwa kudanganya""mama yako yupo, nimemuacha kule kanisani kwenye maombi maalumu usiku wa leo yupo pamoja na waumini wengine..hivyo ameniagiza nije nikufate kwa sababu nilikuwa nakwenda mtaa wa pili ...ili kumfanyia maombi bibi mzee aliyekuwa amezidiwa kwa ugonjwa...kwa sababu sikukuona kule kanisani nikaona ni vyema nipitie hapa nyumbani kwenu ili tuondoke pamoja kwenda kwenye ibaada ya usiku wa leo.....wakati mchungaji akiongea maneno hayo ya uwongo...monica alikuwa akimtazama kwa umakini....monica hakutambu kilichokuwa kikiendelea akayaamini maneno ya mchungaji...likini monica alisema""sijisikii kutoka humu ndani nyinyi kaendeleeni na ibaada mimi nabaki hapa nyumbani namsubiri mama yangu...

    maneno hayo yalimfanya mchungaji aingiwe na amani moyoni mwake..aliona hiyo ndio nafasi pekee ya kuondoka.....akajibu""basi sawa mimi naondoka zangu narudi kule kanisani....akafungua mlango na kuzipiga hatua....kwa sababu alikuwa hajawahi kuingia kwenye nyumba hiyo hivyo alikuwa akibahatisha mlango wa kutokea upande wa nje..wa sababu nyumba hiyo ilikuwa na korido zenye kona kona nyingi....monica alichungulia kwenye mlango wake amtazame mchungaji....alistuka kumuona mchungaji akifungua kila mlango utadhani anatafuta kitu...akajiuliza """kwani mchungaji kapitia wapi mbona kama nilifunga milango yote""" monica hakujali alihisi huenda alisahau kufunga milango hivyo ilikuwa wazi....akatoka chumbani kwake na kuelekea upande wa sebuleni..alipofika alikita mchungaji tayari katoka upande wa nje....akachungulia dirishani akamuona anatimua mbio.....monika alibaki akijiuliza akamua kurudi chumbani kwake akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi......



    ***************



    asubuhi palipokucha monica alidamka mapeka kama kawaida......akaanza kufanya usafi wa ndani alipomaliza akaenda kuoga.alipomaliza alirudi chumbani kwake akavaa nguo kisha akatoka na kuelekea sebuleni akawasha runinga na kuanza kutazama...baada ya masaa matatu kupita ilikuwa ni saa tano za asubuhi...akaanza kupata wasiwasi alijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu alijiuliza mbona mamayake hajarudi...tangu jana mpaka sasa hivi...aliamua kuifuata simu ya mezani akampigia mama yake...lakini namba ikawa haipatikani!!! akaamua kuzima Runinga akatoka nje akazipiga hatua kuelekea kule kanisani akaangalie huenda mama yake alikuwa kabaki huko kanisani...



    *************



    wakati huo huo alionekana mchungaji Emmanuel akiwa ndani ya kanisa lake....lakini upande wa ndani palionekana tofauti palikuwa panafuka moshi mzito ghafla alijitokeza malaika wa shetani safari hii alikuja na mtu wa kutisha zaidi mtu huyo alikuwa na misuli mingi mikononi mwake alikuwa na mdomo mkubwa sana na meno yake ya mbele yalikuwa marefu yenye ncha kali... wakati huo mchungaji alikuwa kainua mikono yake juu huku ameshikanisha mikono yake......malaika wa kuzimu alimsogelea kisha akasema""bado unawakati mgumu na usipokuwa makini ili kunasa binti monica basi yeye ataondoa uhai wako......macho yalimtoka mchungaji akauliza nitatumia njia ipi ili kumnasa Monica kwa urahisi??CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    malaika wa kizimu alijibu kwa mkato """PICHA..



    **************



    upande mwingime alionekana monica akiwa njiani akizipiga hatua za taratibu kuelekea kanisani.....akiwa njiana wazo lilimjia akaanza kutimua mbio ili awahi kule kanisani....baada ya dakika kadhaa alifika eneo la kanisa akaanza kuzipiga hatua kuufuata mlango wa kanisa.....alipofika alikuta mlango umefungwa kwa ndani akaamini lazima mchungaji atakuwemo ndani...

    wakati huohuo alionekana malaika wa kuzimu akiwa amebadilika sura na uso wake kuonesha kuwa na wasiwasi....akainua shingo yake upande wa juu.....akasema""nasikia sauti pia nahisi harufu chafu sana hii ni hatari....akagundua kuwa monica hayupo mbali na eneo hilo.....

    upande wa nje monica alisukuma mlango ukafunguka kwa urahisi alipotazama ndani ua kanisa hakuamini alichokiona........aliona kanisa linamuonekano wa kutisha sana..akaogopa sana akataka kutimua mbio.....ghafla malaika wa kuzimu akajitokeza mbele yake monica akapiga kelele za uwoga.....malaika wa kuzimu akanyoosha mkono wake ili amshike shingo..



    ghafla akasita, alihisi kama mwili wa monica unawaka moto mkali sana aliponyoosha mkono wake kabla hajamgusa alikuwa kama anaunguzwa na moto , akaIpiga hatua tatu kurudi nyuma huku macho yake yakimtazama monica kwa mshangao......monica alistaajabu alijiuliza kwanini amerudi nyuma!! kasimama kando??wakati monica akijiuliza hivyo malaika wa kuzimu akatoweka kimiujiza na kutokomea kusikojulikana, monica akatimua mbio, alikimbia bila kujua ni wapi anaeleka



    ***********

    wakati huohuo alionekana mchungaji akiwa ndani ya kanisa ghafla ile hali ya mwonekano wa kutisha ilitoweka na kanisa likarudi katika hali yake ya kawaida. mchungaji alizipiga hatua kuufuata mlango wa kutokea nje akaingia ndani ya gari lake na kuondoka zake



    monicaalionekana akikimbia baada ya muda alifika nyumbani kwao aliingia moja kwa moja mpaka chumbani kwake .wakati huohuo alionekana mchungaji akiingia nyumbani kwake akalipaki gari na kuingia ndani kwake ,mchungaji alionekana kuchanganyikiwa akaandaa mpango wa kutafuta ili mtu huyo amunase monica kwasababu hakuwa na uwezo wa kumunasa monica kila alipojarbu kumgusa monica alihic mwili wa monica umezungukwa na moto mkali sana



    ************

    Baada ya siku tatu kupita siku ya leo ilikua ni jumapili, mchungaji aliamka mapema na kuwahi kanisani alipoingia ndani ya kanisa alichukua ile biblia iliyoandikwa kwa maneno ya kugeuzwa juu chini/chini juu akaandaa somo la leo kuwahubiria waumini wake baada ya lisaa limoja kupita waumini wakaanza kuingia kanisani hatimae kanisa lilijaaa na ibada ikaanza-:



    wakati huo huo alionekana monica akiwa nyumbani kwao alijiuliza maswali mengi mama yake yuko wapi leo ni siku ya nne hajaonekana nyumbani akaanza kua na wasiwasi na mchungaji,akaamua kwenda kule kanisani kwa mchungaji ili akamuulize na apate ukweli kuhusu mama yake kaenda wapi? safari hii monica hakuwa na uwoga alikuwa tayari kashazoea kuyaona maajabu ya kutisha....

    akajisemea moyoni""mara ya mwisho mchungaji alisema mama yake yupo kanisani kwenye maombi maalum,

    akaendelea kuzipiga hatua alipolikaribia kanisa aliona mlango upo wazi na waumini wapo ndani wakiendelea na ibaada. monica alizipita hatua akaingia ndani ya kanisa, mchungaji alistuka kumuona monica.....pia monica alistahajabu kuona waumini wameketi juu ya mafuvu ya binadamu.....lakini wenyewe waliona wameketi kwenye viti vya kawaida......monica alipotazama upande wake wa kushoto aliona shimo kubwa lililokuwa na moto ndani yake hakuogopa akaendelea kuzipiga hatua kumfuata mchungaji..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    binadamu wa kawaida waliona kanisa lipo kawaida lakini monica pekee aliona kuwa sio kanisa bali palikuwa ni sehemu ya kutisha (KUZIMU) wakati huo mchungaji macho yalikuwa yamemtoka alijua wazi kuwa monica anauwezo wa kuona kinachoendelea.......monica alipomkaribia .............mchungaji akaanza kupiga hatua kurudi nyuma.....ghafla ile bibilia ilidondoka....alipotaka kuiokota monica alikuwa amefika karibu kabisa..mchungaji akasita kuokota ile bibilia......monica akauliza""mama yangu yuko wapi??? mchungaji alibaki kimya bila kujibu kitu chochote.........monica akauliza tena ""mama yangu yuko wapi???? safari hii monica aliuliza huku uso wake ikionekana kuwa mkakamavu....kisha akainama na kuiokota bibilia ile......alipoitazama alistahajabu kuona maneno uameandikwa juu chini/chini juu

    waumini hawakueza kuona kinachoendelea bali walimuona monica akiwa kule mbele alipokuwa amesimama mchungaji....watu wote wakastahajabu kumuina mchungaji kaacha kuendelea na ibaada akizipiga hatua za uwoga kiridi nyuma.....wakabaki wanajiuliza kwa nini mchungaji anaonesha kumuogopa monica!!!!!!

    monica akasema"" namtaka mama yangu wewe ndiye unajua alipo......mchungaji akapagawa macho yakamtoka ..kisha monica akageuka na kutazama nyuma akapaza sauti""hili sio kanisa bali ni kuzimu...waumini walistahajabu wakaanza kukemea kauli ya monica....monica alipo ona hawamjali aliamua kuindoka zake huku akimwambia mchungaji namtaka mama yangu..

    kabla hajafika mbali alisikia mtu akiita jina lake aliitambua sauti hiyo ilikuwa ni ua mama yake ........



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog