Search This Blog

MALAIKA WA KUZIMU - 4

  







    Simulizi : Malaika Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Nne (4)





    alipogeuka nyuma alistahajabu kumuona mama yake akiwa ndani ua lile shimo lililokuwa linawaka moto mkalim..waumini walibaki wakimtazama monica walikuwa hawamuelewi anachokifanya...wakati wakistahajabu mara ghaflaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    walijitokeza watu wengi walioonekana kuungua kwa moto.....kisha wakatoweka kimiujiza monica akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea ule upande lilipokuwepo lile shimo....ghafla akajitokeza MFALME WA KUZIMU akiwa na jicho moja kwenye paji la uso huku kichwa chake kikiwa na mapembe mawili..



    Akazipiga hatua akaingia ndani ya lile shimo lenye moto uliokua ukiwaka kwa kasi kama unapulizwa na upepo ,Monica alistaajabu uwoga ukamwingia yule mfalme wa kuzimu akamnyanyua mama Monica huku moto unawaka mwikini mwake kama jiko la kuni baada ya sekunde kadhaa mfalme wa kuzimu alitoweka kimiujiza ghafla Monica aliona ule muonekano wa kutisha kutoweka na pakaonekana ni ndani ya kanisa ,,Monica alistaajabu sana macho yalimtoka ..... sasa Monica akagundua siri nzito inayoendelea ndani ya kanisa hilo,akapaza sauti""jamani hili sio kanisa ni kuzimu nawasihii sana msisali tena kwenye kanisa hili. Waumini wakahisi huenda Monica amepatwa ugonjwa wa akili .Monica alipoona kua hawamjali alikasrika sanaa ,akazipiga hatua akuelekea kule mbele alipokua mchungaji.

    Mchungaji aliogopa akaanza kutimua mbio baada ya kumuona Monica anamfuata akapitia mlango wa nyuma wa kanisa na kutokomea kusikojulikana, Monica alizipiga hatua za haraka haraka mpaka kwenye meza iliyokuwepo pale mbele ,akaichukua ile biblia iliyoandikwa maneno yaliyokua yamegeuzwa juu chini/chini juu,Monica akarudi mpaka kwenye viti walivyokua wameketi waumini akanyoosha mkono wake juu huku ameishka biblia hiyo na kusema"" ni nani anaeweza kuniambia hii biblia ni ya aina gani??,tazama maneno yaliyoandikwa humu ndani yamegeuzwa juu chini/ chini juu!!! waumini walipoitazama biblia hiyo waliona inafanana na biblia zingine za kawaida, hata maneno yaliyokua yameandikwa kwenye biblia hiyo waliyaona yapo kawaida hayajageuzwa kama alivyosema Monica!!!

    ikasikika sauti ya mzee mmoja aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha katikati akipaza sauti""wewe binti hivi akili zako zipo sawa?? mbona unataka kuidharilisha biblia takakatifu!!!! ulaaniwe....

    waumini wote wakamuunga mkono mzee huyo ....

    Monica alichukia sana akaamua kutoka ndani ya kanisa hilo na kurudi nyumbani kwao.....



    ************

    Alipofika nyumbani Monica alipitiliza mpaka chumbani kwake ,akajilaza lakini hakuweza kupata usingizi kwa wakati huo,akili na fikra zake zote zilikua na mawazo kuhusu mama yake, alijisemea moyoni ""siamini kama mama yangu kapelekwa kuzimu.Monica alinyanyuka kitandani akainama na kuitoa ile picha ya baba yake uvunguni mwa kitanda....akaitazama picha hiyo karibia dakika kumi mfululizo...kisha akaanza kulia.....aliamini hatamuona tena mama yake..wakati huo monica alikuwa hafahamu kuwa ndani ya mwilini kunanguvu za ajabu...zinazoweza kupambana na nguvu za giza......akasita kuendelea kulia akaingia jikoni akaanza kuandaa chakula kwa sababu alihisi njaa kali.......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    upande mwingine alionekana mchungaji akiwa ndani ya nyumba yake.... alionekana kuchanganyikiwa akajisemea moyoni""aisee mbona nitaumbuka!!!!huyu binti ataharibu kila kitu sijui nifanye nini wakati akijiuliza,wazo likamjia akakumbuka kuwa aliisahau ile biblia kule kanisani...akakumbuka siku ile aliambiwa na malaika wa kuzimu kuwa asithubutu binadamu wa kawaida kuishika biblia ile..... akaamua kurudi kule kanisani haraka...



    wakati huo huo,kule kanisani waumini walibaki wakijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu.....walistahajabu mpaka sasa ni lisaa limoja limepita tangu mchungaji alipotimua mbio na kutokomea kusiko julikana.......waumini wakaanza kuondoka mmoja moja mpaka kanisa likabaki tupu hakuna watu ndani yake....

    mbaada ya dakika kadhaa kupita mchungaji alifika kanisani hapo..akapitia mlango wa nyuma kuingia upande wa ndani ya kanisa...alistuka hakukuta mtu hata mmoja....ghafla ukafuka moshi mkubwa akajitokeza malaika wa kizimu....akasema," ni masaa sabini na mbili(72) yamebaki yakipita bila kumuangamiza monica basi yeye ataangamiza maisha yako....pia atasababisha matatizo makubwa sana atawafungulia watu wote waliokuwa kuzimu na watakuwa huru.....huyu si mtu wa kawaida....sasa kazi kwako....baada ya kusema hivyo akatoweka kimiujiza.......mchungaji alichanganyikiwa akazipiga hatua za haraka haraka akaufuata ule mlango wa chumba cha siri...alipoufungua alikuta kisu kilichotengenezwa kwa kutumia madini ya dhahabu...kisu hicho kilikuwa na umbo la usaraba (cross)

    kisha ikasikika sauti ya mfalme wa kuzimu ikisema tumia kisu hicho kumchoma binti huyo katikati ya kifua wakati amelala kitandani....kwa kukidunga mara moja tu, bila kurudia kudunga tena...kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kumuangamiza binti huyo....kwa sababu kisu hiki ni kisu maalumu ninachokitua mimi kwa kukata kitu chochote hapa duniani....mimi ndiye mfalme wa DUNINI NA KUZIMU.....sauti ile ilinyamaza na ukimya ukatawala.... mchungaji alikichukua kisu hicho na kuondoka zake kurudi nyumbani.

    aliandaa mpango wa kwenda nyumbani kwao monica usiku wa leo kwa ajili ya kuifanya kazi hiyo..

    ilipofika majira ya saa saba za usiku mchungaji aliianza safari ya kwenda nyumbani kwo monica...



    wakati huo huo alionekana monica akiwa ndani ya chumba chake akisali kumuomba mungu amlinde usiku huo.....alipomaliza kusali alipanda kitandani na akajilaza chali....akachukuwa ile picha ya baba yake iliyoitoa ukutani sebuleni,,akaikumbatia kifuani kisha akajifunika shuka na kuanza kuutafuta usingizi....baada ya dakika kadhaa usingizi ulimnyemelea hatimae akasinzia kabisa...



    wakati huo huo baada ya monica kupitiwa usingizi,

    mchungaji alikuwa amefika eneo la nyumbani kwao monica...akaingia ndani ya uzio kwa kutumia nguvu za giza ....kisha akafungua milango bila monica kusikia chochote....akaingia mpaka chumbani kwa monica.... akazioiga hatua kumsogelea monica.....alifurahi alipomuona kalala chali.... kisha akanyanyua kile kisu ili amchome katikati ya kifua........



    Akakishusha kisu kile kwa kasi kikadunda juu ya ile picha ya baba yake Monica...aliyokuwa ameiwwka kifuani....mchungaji alistahajabu kwa nini kisu kimedunda!!! hakutambua kuwa monica alikuwa ameiweka picha ile kifiani hakuweza kuiona kwa sababu monica alikuwa amejifunika shuka...kwa sababu picha hiyo ilikuwa imehifadhiwa kwa mbao nyembamba zilizokuwa zimeizunguka pembe zote..na kwa upande wa juu kiliwekwa kioo....hivyo kisu kile hakikuweza kumdunga monica kilidunda juu ya kioo kile...

    mchungaji aliyakumbuka maneno ya mfalme wa dunia na kuzimu...ilimwambia kuwa adunge mara moja tu bila kurudia....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    monica alistuka akakurupuka usingizini...akamuona mchungaji Emanuel akiwa ndani ya chumba chake huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.. monica akastuka akahisi huenda anaota...akauliza kwa mshangao,"Umewezaje kuingia chumnani kwangu!!?? na unataka nini?

    mchungaji alibaki kimya bila kujibu kitu...ghafla akajitokeza malaika wa kuzimu nyuma ya mchungaji....akamgusa begani wakatoweka kimiujiza.....

    monica alinyanyuka haraka kutoka kitandani akasimama kando ya kitanda...akajiuliza,"haya niliyoyaona ni kweli!!au naota??? akafungua mlango kuelekea sebuleni

    wakati huo huo alionekana malaika wa kuzimu kajitokeza sebuleni na kujibadilisha sura yake akaonekana kufanana na mama monica...



    monica aliendelea kuzipiga hatua huku akitazama huku na kule...alipofika sebuleni alistahajabu kuona mama yake akiwa amesimama sebuleni...huku akimsihii monica asogee karibu amwambie jambo fulani..

    monica alistuka akaogopa sana akauliza kwa mshangao!!! wewe ni nani?? hakujibiwa..

    monica akasema,"wewe sio mama yangu niambie wewe ni nani na unataka nini??? wakati huo malaika wa kuzimu ambaye kajibadilisha na kuinekana kama mama monica...alikuwa ameshikilia kile kisu...akazipiga hatua kumsogelea monica ili amchome kifuani kwa sababu mchungaji alishindwa....monica akatimua mbio kurudi chumbani kwake,alipofungua mlango alistuka kumkuta malaika wa kuzimu yumo ndani ya chumba chake...monica akawa ameshajua kuwa huyo sio mama yake!!! ..

    monica akatimua mbio akafungua mlango wa chooni akaingia upande wa ndani na kujifungia humo....jasho lilimtoka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu...macho yalimtoka..ghafla malaika wa kuzimu akajitokeza ndani ya choo monica akapiga kelele...alipotazama atafute upenyo akimbie akamuona malaika wa kizimu kwa kupitia kioo kilichokuwa ukutani humo chooni...akageuza shingo yake ili kumtazama lakini aliona bado yupo katika sura ya mama yake tofauti na anavyoonekana kwenye kioo.....monica alihisi kuchanganyikiwa...ghafla malaika wa kuzimu akatoweka akajitokeza ndani ya chumba cha monica na kuichukua picha ya baba yake monica kisha akatoweka nayo......kumbe ilikuwa imetimia saatisa kamili za usiku.....mda huo ni muda maalumu ambao yeye anatakiwa awe amerudi kuzimu kwa ajili ya kumtukuza mfalme wa dunia na kuzimu kwa kumshika miguu yake..

    hiyo ikawa ponapona ya monica.......akatoka chooni haraka akakimbia mpaka chumbani kwake...alipotazama juu ya kitanda hakuweza kuiona picha ya baba yake...akaanza kuitafuta lakini pia hakufanikiwa kuiona..



    **********



    upande mwingine alionekana mchungaji yumo ndani ya kanisa akichimba shimo ndani ya kile chumba cha siri..ili amtafute mtu aliye hai amzike pamoja na picha ya baba monica kabla ya masaa sabini na mbili (72) hayajatimia.....alipomaliza kuchimba shimo hilo alitoka nje na kufunga mlango.. akajitokeza malaika wa kuzimu na kumkabidhi mchungaji ile picha...kisha akatoweka kuelekea kuzimu....

    mchungaji akaiweka picha ile juu ya meza iliyokuwa ndani ya kanisa na kuondika zake kurudi nyumbani kwake.....



    kule nyumbani kwao monica aliamua kuondoka usiku huohuo kuelekea kule kanisani...aliamini mchungaji ndiye anayo picha ya baba yake....alipofika alisukuma mlango wa kanisa ukafunguka kwa urahisi..akaingia ndani akazipiga hatua kuelekea upande wa mbele yakanisa..akaiona ile picha ikiwa juu ya meza akaichukua..



    wakati huohuo alionekana mchungaji..amesimamisha gari lake wazo lilimjia arudi kanisani akaichukue picha ile...alihisi hajaihifadhi kwa usalama. akirudi kanisani alipofika alistuka kukuta mlango upo wazi..wakati yeye aliacha ameufunga.....wakati huohuo alionekana monica bado yumo ndani ya kanisa...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mchumgaji akazipiga hatua za harakaharaka akaingia ndani ya kanisa....monika aliposikia vishindo vya mtu akitembea...akaamua kujificha..akaingi chini ya kiti akajificha vyema bila kuinekana....huku kaikumbatia picha ya baba yake... mchungaji alizipiga hatua za mwendo wa haraka nusu akimbie...akaangaza macho yake huku na kule hakuweza kumuona mtu aliyeufungua mlango wa kanisa...akaamua kuifuata ile meza ambayo alikuwa kaiweka picha ya baba monica uoande wa juu...alipoikaribia meza hiyo..macho yalimtoka...akashangaa sana kutokuikuta picha ile...akazidi kuchanganyikiwa..akazipiga hatua kuelekea kwenyekile chumba cha siri..akaufungua mlango.....



    ********************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog