Search This Blog

MALAIKA WA KUZIMU - 5

 







    Simulizi : Malaika Wa Kuzimu

    Sehemu Ya Tano (5)



    likawa ni kosa kubwa la usahaulifu alilolifanya....ilikuwa haitakiwi chumba hicho kifunguliwe muda ule..kwa sababu ilikuwa ni muda wa kumuabudu mfalme wa duniani na kuzimu.....hivyo kitendo kile cha kuufungua mlango huo kikasababisha jambo kubwa lililokuwa ni siri ya Mchungaji kufichuka...baada ya mlango huo kufunguka walitokeza watu wengi kupita kiasi...walijitokeza kwa mfululizo kila baada ya sekunde tano...watu hao waolionekana ni wafu walio hai....walitoka ndani ya chumba kile cha siri....mchungaji alipagawa..akakumbuka kuwa amefanya kosa kubwa na ni ngumu uwarudisha kwa sababu muda ulikuwa umekwenda sana..yapata saa tisa na nusu za usiku ....ni muda ambao hairuhusiwi mtu yoyote ambaye anamuabudu mfalme wa duniani na kuzimu..kufanya jambo lolote usiku huo...(N.W.O)

    NEW WORLD ODDER.....



    ****************



    monica aliogopa sanaakaamua kutoka kule chini ya kiti alipokuwa amejificha na kuanza kutimua mbio kuelekea upande wa nje...wakati huo wale wafu walio hai walikuwa wametapakaa ndani ya kanisa hilo....monica alikimbia huku akipita kati kati yao...monica alifanikiwa kutoka nje ya kanisa hilo akatimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea... akafika kwenye barabara kuu...akaamua kukimbia kuelekea nyumbani kwao....



    ****************



    Upande mwingine kule kanisani...walionekana wale wafu walio hai wakizunguka zunguka ndani na nje ya kanisa......mchungaji alifanya jitihada za kufanya jambo ili aweze kuwarudisha ndani ya kile chumba cha siri...ili asije akaumbuka pia kwa upande wake itakuwa ni hatari...kama ikitimia saa kumi na nusu za usiku kabla hajawarudisha ndani ya chumba hicho. akausogelea ukuta uliokuwa mbele ya kanisa akaugusa kwa mikono yake miwili ghafla ulitokea moshi uliokuwa ukifuka taratibu kusambaa ndani ya kanisa hilo.....muda ulizidi kisinga bila mafanikio yoyote...mchungaji akazidi kupagawa..jasho lilimtoka akamua kuufuata mlango ili atoke na kuondoka zake......CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika saa kumi kamili za alflajiri.....watu wale walianza kuhisi kula nyama mbichi na damu mbichi....wakaanza kimfuata mchungaji......huku wakikoroma kwa sauti za kutisha...mchungaji alitimua mbio lakini alikuwa ameshachelewa....walimnasa na kuanza kumshambulia...wakaanza kumla nyama mzimamzima huku anajiona....mpaka akakata roho..ndio ukawa mwisho wa mchungaji Emmanuel.....ilipotimia saa kumi na nusu....alijitokeza malaika wa kuzimu na kuwaamuru wafu walio hai...kurudi kuzimu....wakaanza kuyayuka na kutoweka...kisha na malaika wa kuzimu akatoweka kimiujiza....

    kanisa likabaki tupu pamoja na maiti ya mchungaji ikiwa chini.........



    ************



    baada ya masaa matatu kupita......maiti ya mchungaji Emmanuel ilionrkana kuanza kubadilika....hata vile vidonda vya majeraha aliyong'atwa vikaanza kubadilika rangi..na kuwa na rangi nyeusi ghafla akafumbua macho yake.. yalionekana kuwa meupe bila kuwa na mboni yenye kiini cheusi.....akanyanyuka na kusimama wima huku mate ualiyorendemka yakimtoka mdomoni akazipiga hatua kuifuata mlango na kutoka nje ua kanisa.....alitembe barabarani kwa mwendo wa kikakamavu...ghafla akahisi njaa akawa anatamani kula nyama mbichi pamoja na damu ya mbichi..



    Akazipiga hatua mpaka kwenye nyumba moja iliyokuwa na zizi la mbuzi upande wa nje..akaingia ndani ya zizi na kumkamata mbuzi mmoja akamrarua tumboni akaanza kumla mbichi..alipohisi kashiba akaamua kuondoka akawa anazunguka zunguka mitaani..mpaka pakakucha..



    *****************



    asubuhi palipokucha alionekana Monica akiwa nyumbani kwao..alisikitika sana..aliamini hatomuona tena mama yake...akanyanyuka kitandani akatoka na kuelekea jikoni ili aandae chai.....alipofika akakafua kama kuna chakula cha kupika mchana..akaona hakuna chakula kilikuwa kimekwisha...akazipiga hatua akaingia chumbani kwa mama yake...akafungua droo ndogo ya kwenye kabati...akachukua kadi ya benki ya Mama yake ili akatoe pesa akanunue chakula cha mwezi mzima akiweke ndani......alipoicgukua kadi ile akatoka na kuzipiga hatua kuelekea ATM ya CRDB BANK.....

    alipotoa pesa akaelekea sokoni ili kununua chakula.....alipofika alistahajabu kuona watu wakitimua mbio huku na kule.....alipotazama huku na kule,kwa mbali aliweza kumuina Mtu aliyeonekana kutisha huku tumbo lake likiwa wazi...na mdomoni mwake pametapakaa damu...monica alibaki kasimama huku akimshangaa mtu huyo..watu wengine walimshangaa monica kumuona amesimama badala ya kukimbia....

    monica akamuona mtu huyo akimkamata mtu na kumng'ata shingoni kisha akavuta nyama ya mtu huyo ikang'oka ......baada ya dakika kadhaa watu hao walianza kubadilika na kuwa kama yeye..wakawa wanatamani kula nyama mbichi pamoja na damu mbichi...macho yalimtoka monica akatimua mbio.......

    taarifa hizo zilisambaa Mji mzima.....vyombo vya habari vikatangaza kuwa watu wote wajifungie majumbani mwao......ili jeshi liingie mitaani kuwaanganiza

    viumbe hao midebwedo""hahhahahaha achechee waaanakuuujaaa hatari wanaume...ilisikia sauti hiyo ya Yozz Piano Maya.....huku akitimua mbio na kutokomea kusiko julikana..



    ******************



    upande mwingine alionekana Monica akiingia nyumbani kwao na kufunga geti kwa makomeo akaufuata mlango wa kuingia ndani ya mgumba..akastuka kuukuta upo wazi.....hofu kubwa ikatanda juu yake akapiga hatua za kunyatia huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa akaingia ndani....kisha akapaza sauti,"" wewe nani uliyeingia ndani kwetu...

    hakujibiwa akazipiga hatua kuelekea vyumbani alistahajabu kumkuta paka wake ameraruriwa na utumbo umemwagika chini kwenye korido..akaogopa akageuka ili atimue mbio..ghafla alikutana uso kwa uso na mtu aliyekuwa anajeraha kubwa shingoni huku akizipiga hatua za kizembe (mdebwedo) monica alipiga kelele....alipotaka kukimbia ili aingie kwenye chumba..ghafla akadondoka chini baada ya kutereza alipo ukanyaga utumbo wa yule paka aliyeraruriwa...

    yule mtu wa kutisha akazioiga hatua kumfuata monica....huku akionekana kuitama nyama na damu ya monica......alipomkaribia monica alimkanyaga kwa kumsukuma kwa miguu...lakini cha kushangaza mtu yule alidondoka na kuanza kutoka funza mida huo huo akabadilika na kubaki fuvu pamoja na mifupa....

    hapo ndipo monica akagundua kuwa mwili wake unanguvu za ajabu........akatoka akaelekea upande wa nje....alipofungua geti ili atoke nje ya uzio..alistahajabu kukuta kundi kubwa la watu walio onekana kutisha huku wakiwa na majeraha shingini huku wengine wakionekana utumbo uko nje na kuning'inia....monica akafunga geti haraka akarudi upande wa ndani huku akiomekana kuwa na hofu kubwa....



    ******************



    uoande mwingine walionekana watu wakiwa ndani ya majumba yao huku wakiangalia taarifa ya habari iliyokuwa inarushwa muda huo kuonesha mambo yanayoendelea mitaani....walistahajabu kumuona mchungaji amebadilika na kuwa mtu wa kutisha aking'ata watu na kula nyama zao zikiwa mbichi...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine walionekana waumini waliokuwa wakisali kwenye kanisa la mchungaji Emmanuel wakitimua mbio kuingia kanisani kwa ajili ya usalama zaidi..walikuwa wengi mpaka kanisa likafulika....ghafla kanisa likabadilika na kuonekana ni sehemu ya kutisha (kuzimu)kisha mlango ukajifunga.......ili asitoke mtu..

    waumini wakaogopa sana wakagundua kumbe hilo halikuwa kanisa bali ilikuwa ni dini ya shetani......waumini wakaanza kupiga kelele za hofu......wakiomba msaada..ghafla akajitokeza malaika wa kuzimu pamoja na malaika wa kaburi......sasahivi kila muumini aliweza kuwaona

    kwa macho..



    kila muumini alitamani ardi ipasuke atumbukie ndani....ghafla akajitokeza Mfale wa kuzimu..akaamrisha waumini wote wachukuliwe na kukalishwa sehemu moja....malaika wa kuzimu alifuata amri ya mfalme wa kuzimu akapaza sauti....sauti hiyo ilikuwa kali ikiambatana na mngurumo mkubwa wa kutisha..akasema,,""kila mmoja apite na kusimama mbele ya mfalme wa kuzimu...

    mfalme wa kuzimu akaketi juu ya kiti chake cha kifalme...kiti hicho kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu huku kimepachokwa mavuvu mawili ya binadamu upande wa juu....akasema ""mtasimama mmoja mmoja na nitauliza swali...kwa atakayepinga amri yangu weka katika moto wenye mateso milele....sasa basi atakayee niabudu mimi kwa nafsi yake apite mbele...ataishi maisha mazuri na yenye amani hapa duniani na kuzimu...atapata kila kitu atakacho kihitaji.........

    na anayemuabudu Mungu abaki amesimama hapohapo akisubiri mateso na tabu zikiamba na shida za milele... baada ya kusema hivyo mfalme wa kuzimu na duniania ya wenye kumtukuza..akabaki kimya bila kuongea nene lingine......akasubiri ili aone watakaokuja upande wake...lakini hakujitokeza hata mtu mmoja kati ya wale waumini..waliokuwa wakisali kwenye kanisa la mchungaji Emmanuel wakidhani kuwa ni kanisa takatifu kumbe ni kanisa lililokuwa na siri nzito ya kuzimu.....ili kumuabudu mfalme wa duniani na kuzimu..



    ****************



    upande mwingine alionekana monica akiwa nyumbani kwao akitafuta namna ya kutoka nje ili akajaribu kutafuta chakula kwa sababu alihisi njaa kali sana.....akaamua kuchungulia dirishani ili aone upande wa nje...alistuka baada ya kuona wale watu waliobadilika na kuonekana kutisha huku miili uao ikiwa na majeraha makubwa baada ya kung'atwa na mchungaji Emmanuel....wakilisukuma geti kwa nguvu..hatimae likang'oka na kudondoka,,,kisha wakaingia ndani ya uzio huku wakizipiga hatua za kizembe.....wakiifiata nyumba yao monica....monica akaogopa sana akaamua kupitia mlango wa nyuma ili atimue mbio.......alipofungua mlango alikutana iso kwa uso ma watu wanne wa kutisha(midebwedo) achecheee waanakuuujahatari wanaume....monica akafunga mlango haraka lakini watu wale walizuia mlango usifungwe....wakausukuma na kuingia upande wa ndani......monika akakumbuka kuwa akigusa miili ya watu hao wanapoteza uhai.... akapata ujasiri akamgusa mmojawapo...

    mtu huyo wa kutisha akatetemeka kama kapigwa shoti ya umeme kisha akaanza kubadilika na kuwa mifupa na kubaki fuvu.....akafanya hivyo hivyo kwa wale watatu waliobaki wakayayuka na kubaki mifupa......



    monica akatoka upande wa nje....akawa anapita katikati ya watu hao wakutisha(midebwedo)

    walipojaribu kugusa mwili wa monica waliyayuka na kubakiki mifupa na vichwa vyao kuwa mafuvu.

    alitumia masaa mawili kuwateketeza watu hao wa kutisha....lakini njaa ilimzidia na mwili ukawa dhaifu na kunyong'onyea akawa anazipiga hatua kutafuta chakula.......kimya kiliutawa Mji mitaa ilikuwa haina watu.....bali yalionekana makundi makundi ya watu wakutisha (midebwedo)waliokuwa wakiranda randa mitaani kutafuta nyama mbichi.....na kila walipo mng'ata binadamu au kimbe chochote chenye uhai basi baada ya dakika kadhaa kiumbe hicho kilibadilika na kutoka katika hali ya umauti na kurudi katika uhai na kuanza kutamani kula nyama mbichi....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****************



    monica aliamua kuelekea sokoni alipofika aliparamia matunda akayatafuna kwa uchu wa njaa..alipohisi kashiba aliamua kuchukua matunda mengine na kuyaweka kwenye mfuko kwa ajili ya akiba......akazipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa...kwa mbali alimuona mwanamke mmoja akiwa na mwanae wa miaka miwili wamezungukwa na watu hao wa kutisha..wakitaka kuwala nyama....

    monica akatimua mbio kwenda kumsaidia mwanamke huyo pamoja na mtoto wake.. alipowakaribia monica hakuwa na muda wa kupoteza aliwapiga makofi ya uso watu hao wa kutisha...na kila kofi lilipogusa miili ya watu hao waliyayuka na kubaki mifupa...akawamaza wote kisha akaongozana pamoja na mwanamke yule huku kambeba mtoto wake mdogo....

    wakiwa njiani wazo lilimjia monic,, akakumbuka kuwa chanzo cha yote ni lile kanisa la mchungaji Emmanuel....hivyo aliamua kwenda kutazama kama kutakuwa na watu wa kutisha ndani ya kanisa hilo awaangamize ili wasije wakatoka na kudhuru binadamu wema....akamchukua mwanamke yule na kumuhifadhi ndani ya nyumba moja iliyo onekana kuwa na usalama..kisha monica akaondoka zake kuelekea kanisani kwa Mchungaji Emannuel......na kumuacha mwanamke yule akiwa na mwanae..

    kumbe ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na wanafamilia wawili waliong'atwa na kubadilika kuwa watu wa kutisha(midebwedo) wakatoka upande wa chumbani na kuelekea sebuleni.......huku wakizipiga hatua za kizembe..



    wakati mwanamke yule akiwa hana hili wa lile ghafla alistukia kakamatwa na na watu wale wakam-ng'ata na kung'o vipande vya nyama kwenye mwili wake..mtoto alipo ona damu zikimtoka mama yakw akaanza kulia....

    watu wale wakamkama mtoto huyo na kumtoboa tutombo wakaanza kula utumbo pamoja na maini ya mtoto huyo...



    ***************



    upande mwingine alionekana monica akitimua mbio kuelekea kule kanisani...alipolikaribia kanisa akapunguza kasi ya kukimbia akaanza kutembea....

    wakati huo huo ndani ya kanisani walionekana waumini wakimlilia Mungu awaokoe katika kifo....

    mfalme wa kuzimu alipo ona zimepita dakika nyingi na hajajitokeza hata mtu mmoja kuja upande wake akaamuru malaika wa kuzimu awachukue waumini hao na kuwatumbukiza ndani ya shimo lililokuwa likiwaka moto mkali kama unapulizwa na upepo......ghafla moto ulizimika mfalme wa kuzimu alastahajabu sana alipotazama kushoto kwake alimuona monica akiwa anazipiga hatua kuja kule mbele alipokuwa ameketi.......mfalme wa kuzimu alikasirika sana na uso wake ukabadilika na kuonekana kutisha zaidi akanyanyuka akanyanyuka kwenye kiti chake..



    waumini walibaki wakimshangaa minica kwa nini amejileta yeye mwenyewe kwenye kifo!!!

    monica aliendelea kuzipiga hatua mpaka mbele kabisa kule alipokuwepo mfalme wa kuzimu..



    upande mwingine walionekana wale watu wa kutisha wakirandaranda mitaani....kwa makundi makundi...mji ulikuwa kimya zilisikika sauti za ndege na mivumo ya upepo.. kwa mbali alionekana mchungaji emmanuel akizipiga hatua za kizembe...huku utumbo unaning'inia.....alikuwa anahisi njaa kali akawa anatafuta nyama mbichi au damu mbichi... CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo huo kulikuwa na gari limepaki katikati ya barabara....ndani yake kulikuwa na baba na mwanae wa kike.....mzazi huyo alikuwa tayari ameng'atwa na watu wale wa kutisha...akaanza kubadilika kila baada ya dakika......wakati huo binti yake alikuwa akilia kwa kumuonea huruma baba yake.....pia aliogopa kutoka nje ya gari kwa sababu wale watu wa kutisha ( midebwedo ) walikuwa wamezagaa kila kona za mitaa.....ghafla baba yake akaanza kuhisi kula nyama mbichi....hata sauti yake ikaanza kubadilika akawa anakoroma tu...macho yake yakaanza kubadilika alipotaka kumla nyama mwanae..alishindwa kwa sababu alikuwa kajifunga mkanda wa kiti cha gari hivyo alishindwa kunyanyuka...mwanae alipo ona hivyo akachukua Adjust jeck iliyokuwa upande wa nyuma na kumpiga nayo baba yake kwenye utosi kichwa kikapasuka..kisha akamfungulia mkanda na kumtupa nje...akawasha gari na kutokomea kusiko julikana...



    ********************



    upande mwingine alionekana mkuu wa majeshi akiamuru..jeshi liingie mitaani na kuwaangamiza watu hao wa kutisha(midebwedo)acheche wanakuuja hatari wanaume...

    baada ya dakika kadhaa wanajeshi waliingia mitaani na kutekeleza amri ya mkuu wa majeshi..

    huko mitaani ilisikika milio ya risasi mfululizo,, wanajeshi wakiwauwa wale watu wa kutisha...

    walipofika ule mtaa aliokuwepo mchungaji Emmanuel....ilikuwa ni vita kabambe....kila walipojaribu kumpiga risasi mchungaji ziliingia mwilini mwake na kutokeza upande wa pili lakini hakufa...wakajaribu kulenga kichwa lakini bado alizidi kuzipiga hatua na kuelekea ule upande ambao walikuwepo wanajeshi...achecheee hatari wanaume....wanajeshi wakaanza kutimua mbio kurudi nyuma..walistahajabu kuona mtu huyo hafi kwa risasi....kwa mbali akaonekana mwanajeshi mmoja akichukua bazoka (RPG) siraha hii ni maalumu kwa kutungulia ndege angani.......akaweka shabaha kumlenga mchungaji Emmanuel...kisha akabofya kitufe cha kufyatulia..

    kombora lilikwenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa mchungaji akasabaratika vipande vipande ukawa ndio mwisho wa mchungaji Emmanueli..



    *******************



    upande mwingine kule kanisani...alionekana malaika wa kuzimu akifanya jitihada za kuwauwa waumini wote kabla Monica hajawakomboa...

    Monica alimfuata malaika wa kuzimu alipomkaribia malaika wa kuzimu akatoweka kimiujiza na kujitokeza nyuma ya minica....alipojaribu kugusa mwili wa monica alitetemeshwa kama kagusa nyaya za umeme...akarushwa kando.....macho yalimtoka akakutanisha macho na mfalme wa kuzimu... akamuina mfalme wa kuzimu akitoweka kimiujiza na kumtelekeza hapo....ghafla ule muinekano wa kuzimu ukatoweka kanisa likaonekana katika muonekano wa kawaida......

    malaika wa kuzimu alipo ona mfalme wa kuzimu kashindwa vita....hofu ikamuingia..akajaribu kutoweka kimiujiza lakini akashindwa...kumbe alipogusamwili wa monica...nguvu za giza zikatoweka mwilini mwake.....kisha monica akamfuata mpaka pale alipokuwa amedondoka....akamgusa mwilini,,, malaika wa kuzimu akayayuka na kubaki mifupa na kichwa chake kikawa fuvu....ukawa ndio mwisho wa malaika wa kuzimu.....ghafla walijitokeza wale wale waumini waliopelekwa kuzimu sikuile pamoja na mama yake monica....monica alifurahi kumuona mama yake akiwa hai..akamkimbilia na kumkumbatia mama yake....

    wakati huohuo alionekana mfalme wa kuzimu akiwa ameshafika kuzimu kwenye utawala wake..alikasirika sana kisha akajisemea moyoni,,"Mungu ni mjanja sana lakini hajanikomesha wacha nijipange kwa mara nyingine tena.....aliyasema maneno hayo huku akiongeza adhabu na kuamuru moto wa jehanamu uongezeke ukali mara mia..



    *****************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule ndani ya kanisa waumini walifurahi sana wakamsifu mungu kwa kwa kuwakomboa kupitia monica...ikasikika sauti ya monica ikisema""poleni sana kwa kudhani mkimuabudu mungu kumbe mlikuwa mkiongozwa na shetani kupitia mchungaji Emmanuel. pasipo nyinyi kujua..

    imani zenu zimewaponya.....waumini wakamshukuru monica kwa kuwakomboa kwenye mauti.

    walipotoka upande wa nje ya kanisa hali ilikuwa shwari...huko mitaani wanajeshi waliuwa walw watu wa kutisha(midebwedo) wakaisha wote...

    watu wakawa na amani monica na mama yake wakarudi nyumbani kwao na waumini wakaondoka na kuelekea majumbani kwao...



    ********MWISHO WA HADITHI HII*******

0 comments:

Post a Comment

Blog