Search This Blog

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU - 5

 







    Simulizi : Jinsi Jini Alivyolitesa Penzi Langu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Mwili wa mama Lulu ulikuwa umekauka na hakukuwa na dalili yeyote ya yeye kupumua,akawataarifu wenzake na mara baada ya kumwangalia vizuri waligundua kwamba alikuwa amekwisha fariki dunia.Lulu alishuhudia kifo hicho cha mama yake kipenzi,Lulu alilia sana tena kwa uchungu na majonzi mengi kwani tayari alikuwa ameuanza ukurasa mpya wa 

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kukosa mapenzi na malezi ya baba na mama yaani ukurasa wa uyatima,alikumbuka maisha aliyoishi na mama yake huku akibugujikwa na machozi tele.Taratibu za mazishi zilifanyika na ndugu wa Lulu waliwasili pale kimara na hatimaye mazishi yalifanyika katika makaburi ya kinondoni,mahali pale pale alipozikwa mzee John .Baada ya mazishi kumalizika


    wanandugu wa Lulu walikaa kikao na kuamua kwa pamoja kwamba mjomba ake na Lulu ndiye atakae mlea Lulu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea.Wakati mama yake na Lulu anafariki dunia Lulu alikuwa akisubiri matokeo yake hasa mara baada ya kuhitimu darasa la saba.Hivyo Lulu alilazimika kuhamia Mbagala kwa mjomba ake,ambako alienda


    kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya jitegemee.Lulu alipokelewa vizuri katika familia ile ya mjombaake na maisha yalikuwa mazuri kwani alipewa mahitaji yote aliyoyahitaji.Alipendwa sana na shangazi yake na kila siku alimsisitizia kusoma kwa bidii.Lulu alionyesha kusikia na kushika vizuri yaleyote aliyoambiwa kwani kila mtihani alikuwa anakuwa wa kwanza darasani hali iliyompelekea kupendwa na kila mtu si wanafunzi wenzake tu bali hata


    walimu wake.Lulu aliendelea kujituma zaidi ili aweze kufaulu mitihani yake,pamoja na hayo yote alikutana na Seleman ambaye alikuwa classment wake katika shule ya sekondari jitegemee,walishirikiana vizuri sana katika masomo yao hivyo kuweka ushindani mkubwa sana katika nafasi ya kwanza na ya pili darasani mwao.Siku moja Lulu na Seleman walichaguliwa kwenda kuiwakilisha shule yao katika mashindano ya 'debate' ambapo shule zote za Tanzania zilihudhuria kupitia wawakilishi wao,ambapo katika mashindano hayo kulitokea kitu cha kushangaza********** 






    Wanafunzi wa shule moja waliongoza katika mashindano yale ya debate na hawa si wengine bali ni Lulu na Seleman kutoka shule ya sekondari Jitegemee.Katika mashindano hayo Lulu na Seleman waliweza kuelezea vizuri sana namna

    ukosefu wa demokrasia katika nchi unavyoweza kuchangia kudidimiza maendeleo ya nchi.,kutokana na maelezo yao bora walizawadiwa computer moja kila mmoja.Jambo hilo lilikuwa la furaha sana kwao hivyo walipongezwa na wote waliohudhuria ile debate na wao pia walipongezana.Haya yote yaliendelea kuwatia moyo na kuwapa ari na hamasa


    kubwa ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.Maisha yao ya shule yalikuwa ya kuigwa kwani kila mwanafunzi darasani mwao alipenda kwenda kuuliza maswali pamoja na kuomba ushauri wa kimasomo kwa Seleman na Lulu na hii ilikuwa kwasababu tu walikuwa na uwezo mzurri wa kimasomo.Hali haikuishia hapo waliendelea kupendwa na walimu


    wao kwani siku moja wakiwa darasani wanafunzi wenzao walipanga kumpiga mawe mwalimu wao wa kiingereza sambamba na kuchoma moto nyumba yake kisa alikuwa haingii darasani kufundisha na ifikapo mwisho wa muhula huingia na kutoa mtihani ,wakiwa katikati ya mazungumzo yao Lulu na Seleman walishauriana namna ya kutuliza jazba 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ile na hatimaye kutoa wazo la kumuita mwalimu husika na kumweleza shida yao na kumtaka awe anahudhuria vipindi.Uamuzi huo ulipokelewa na wanafunzi wote ambao walimwita mwalimu na kumweleza yote ,naye mwalimu alikiri akisema "nisameheni wanafunzi nitabadilika" na hii ilisababisha amani kutawala tena pale shuleni kwao.Miaka nayo ilizidi


    kwenda kadhalika pia siku nazo zilikuwa hazigandi Lulu na Seleman walimatiza kidato cha nne.Muda wa matokeo kutoka uliwadia ambapo shule ya sekondari Jitegemee ili faulisha wanafunzi wote kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili,kwa upande wao Lulu na Seleman walipata daraja la kwwanza yaani "division one" na ilikuwa ni bahati sana kwao


    kwani walichaguliwa kujiunga kidato cha tano katika shule moja.Maisha ya "high level" yalikwenda salama na hatimaye siku iliyokuwa ikingojewa iliwadia ambapo Lulu na Seleman walifika ukingoni mwa elimu yao ya sekondari yaani kidato cha sita.Siku ya mahafali yao iliwadia huku kila mmoja akiipokea kwa hamu kubwa na katika hali isiyotegemewa Selemani aliona kitu******






    Alikuwa ni Lulu ambaye alionekana kutokuwa na furaha yoyote ile na hii ilijidhihirisha wazi moja kwa moja toka usoni kwake hali iliyomfanya Sele kumkaribia na kumuuliza "kulikoni rafiki yangu?""niko sawa tu,kwani unaonaje,aliuliza Lulu."niambie ukweli kwani unaonyesha wazi kwamba hauko sawa, tafadhali niambie,Sele alisisitiza.Akiwa anajiweka

    sawa kwa kuelezea yote yanayo msibu alijikuta akitokwa na machozi mengi ,Sele alijaribu kumtuliza.Lulu aliongea kwa kwikwi "nawakumbu.......ka......wa.....za.....zi,alishindwa kuendelea kuzungumza huku kilio cha kwiki nacho kilimbana.Baada ya kutulia kidogo aliendelea"unajua Sele natamani sana kama wazazi wangu wangekuwepo katika


    mahafali haya,ningefurahi sana tena mno""usijali sahau hayo maana hiyo ni kazi ya Mungu na haina makosa ,acha basi kuwa mnyonge tusherekee vizuri,alisema Sele.Kwa shingo upande Lulu alikubali kuendelea na maandalizi ya mahafali yao.Muda wa mahafali uliwadia ,wageni nao walikuwa wamesha wasili,kwa bwembwe nyingi na shamra shamra sana


    wahitumu waliingia ndani ya ukumbi ulio pambwa vizuri na ukapambika haswa,punde si punde kelele zililindima ukumbini «««happy day,happy day»»»».Wazazi wa Selemani waliwasili ukumbini huku wakiwa wamekumbatia zawadi nyingi bila 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    shaka zilikuwa kwa ajili ya mwanao , naye mjomba ake na Lulu sanjari na mkewe walikuwepo ukumbini.Burudani ziliendelea huku watu wakiserebuka na kula na kunywa.Wakati hayo yote yakiendelea Lulu alimwita Sele na kumnong'oneza kitu




    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog