Search This Blog

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU - 4

 







    Simulizi : Jinsi Jini Alivyolitesa Penzi Langu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Daktari aliitwa haraka na kwenda,alipofika alimkuta mkewe na kamanda akikata roho,akamfunika shuka kisha kuwaambia wale askari waliokuwa karibu kisha akatoka kwenda kuandaa cheti cha kifo,baada ya kumaliza askari waliutwaa mwili wa marehemu na kwenda kuuzika.Miaka mitano ilikuwa imepitaa ambapo Lulu alikuwa mkubwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kidogo,siku moja jioni mkewe na mzee John alimwita mwanae na kumuuliza"mwanangu ungependa kuja kuwa nani ukiwa mkubwa?","kuwa mwanasheria "Lulu aliendelea kwani ninapenda sana kuja kuwa mtetezi wa kinamama na watoto kwani mwalimu alitufundisha kuwa katika jamii zetu watoto na wanawake ndio watu wanaoonewa sana."sasa kazana sana na



    masomo".Maneno hayo yalimfurahisha sana mkewe na mzee John kwa furaha alimkumbatia mwanae.Maisha yaliendelea kwa amani na furaha lakini kwa upande mwingine maisha ya pale kimara yakizidi kuwa magumu,hali iliyomfanya mzee John awe anachelewa kurudi nyumbani sababu ya kusubili wateja katika toyo yake.Jioni ilipofika mzee John alimwita mkewe na mwanae na kuwaambia kuna jambo anataka wazungumze******





    Kwakweli nimeamua kuwaiteni hapa ili kuwa fahamisheni kwamba "hali yangu ya kiafya inazorota''.kauli hiyo ilitoka kwasababu alikuwa amepatwa na uvimbe sehemu yake ya kulia ya tumbo lake,mkewe na mzee John alionekana



    mnyonge na mwenye simanzi kubwa,na akajikuta akitamka"pole baba lulu tumwombe Mungu atatusaidia,maana sisi sote ni watoto wake na ipo siku utapona" kisha kusema hayo Mzee John aliiendelea na wewe mwanangu kipenzi cha



    roho yangu kazana sana kusoma na hakikisha unaongoza darasani"sawaee""ndio baba" Lulu alijibu,mzee aliendelea, maana hiyo elimu ndio ukombozi wako,mimi na mama yako unavyotuona hapa hatukufanikiwa kusoma enzi zetu na ni



    kwasababu wazazi wetu hawakuwa na uwezo wa kutulipia ada,ila wewe mwanetu umebahatika kusoma tumia nafasi hiyo ili uje uwe na maisha mazuri na ya raha, si umenielewa,"ndio baba" Lulu alijibu kwa ujasiri mkubwa kisha kumalizia"baba na mama kamwe sitawaangusha".Kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo Lulu alivyozidi kukua na wakati



    hali ya afya ya mzee John ilikuwa bado haieleweki yaani haijatengamaa na hivyo kupelekea yeye kulazwa katika hospitali ya Lugalo.Madaktari walimpokea na kumfanyia vipimo,vipimo vilipo kamilika familia ya mzee John ilitwa na daktari,baada ya mkewe na mzee John kuketi daktari aliwapa pole kisha kufungua karatasi ya majibu*******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Karatasi ya majibu ilionyesha kwamba mzee John alikuwa anaugua kansa ya tumbo ambayo ni ngumu sana kwa yeye kupona.Taarifa hii ya daktari ili wasononesha sana na kuwastua sana akina Lulu na mama yake,ambao macho yao



    haya kusita kuonyesha hisia kwa kutoka machozi mithili ya mvua nyikani.Siku ile mkewe na mzee John pamoja na mwanae hawakuondoka pale hospitalini.Ilipofika majira ya saa moja usiku hali ya afya ya mzee John ilianza kutia matumaini walau kidogo kwani aliweza kuongea japo kwa shida shida,mzee John akamwita mkewe sanjari na mwanae



    Lulu kisha kuwaambia"mke wangu nakuomba jitahidi sana umsomeshe mwanetu mpendwa,tunza zile mali zetu,wakati haya yote yakiendelea mkewe na mzee John alikuwa amejiinamia pembeni ya mumewe huku akibugujikwa na machozi, mzee John aliendelea "nawe mwanangu Lulu kazana kusoma na ushike sana elimu na usimwache aendezake maana huo



    ndio ufunguo wako wa maisha" kisha kusema hayo aliomba apatiwe maji maana alijihisi kubanwa na kiu,mkewe aliinuka haraka haraka na kuchukua maji na kuanza kumnywesha,akiwa bado anaendelea kumnywesha maji akaona mzee John akishua pumzi kwa haraka na mara akaona maji aliyokuwa akimnywesha yakitoka mdomoni mithili ya udenda,akajiribu kumtikisa huku akiita "mzee John!!"mzee John!!!,hakuna sauti iliyotoa jibu,mkewe alianza kulia kwa sauti huku akimwita



    daktari aje kumpa msaada.Mara baada ya daktari kuchukua vipimo kwa mzee John aliwageukia mkewe na John na mwanae,"kwakweli mzee hatunaye tena" kauli hiyo ilipokelewa kwa vilio vikali.Mwili wa marehu ulifunikwa na kuchukuliwa mpaka mochwari ambako ulihifadhiwa kusubiri taratibu za mazishi.Tarattibu za mazishi zilifanyika na mwili wa marehemu ulipata nyumba ya milele katika makaburi ya kinondoni.Wakati mzee John anafariki dunia Lulu alikuwa na umri upatao miaka saba.Kifo cha mzee John kilimpa majonzi mengi na simanzi kubwa mama lulu hali iliyopelekea afya



    yake kudhoofu kutokana na msongo wa mawazo hali hiyo ilimpelekea kukosa nguvu na kumshawishi ajione mwenye mikosi na balaa tupu hapa duniani kisha kumlilia Mungu wake "kwanini mimi tu".Miaka ilizidi kusonga na hali ya mkewe na mzee John ilirejea katika hali yake ya kawaida hasa baada ya mawazo na kumbukumbu za kifo cha mumewe kuanza kupotea.Siku moja mkewe na mzee John alikuwa akitoka katika kazi yake ya kuuza mboga mboga za majani alijihisi kuumwa na kichwa lakini alifikiri kuwa hali hiyo ilisababishwa na jua kwani siku hiyo alishinda juani.Siku zilisogea hali ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/mkewe na mzee John ilizidi kubadilika na kuwa mbaya,hali ya iliyomlazimu Lulu kumwendea jirani yao ,bwana Masele na kuomba msaada.Taarifa ziliwafikia pia majirani wengine ambao walimchukua na kumpeleka hospitali.walipokuwa njiani mmoja wa majirani aligungua kitu****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog