Search This Blog

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU - 3

 







    Simulizi : Jinsi Jini Alivyolitesa Penzi Langu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Ule mlio uliwashitua lakini wakaamua kuendelea ila kwa tahadhari kubwa.Waliendelea kupanda ngazi mpaka walipo fika ghorofa ya juu,walipofika huko walikuta kibalaza cha kupumzikia ambapo ukiwa pale unaweza kuona mji wote.Mkewe na kamanda alitoo burungutu la manoti ya elfu kumi na elfu tano kisha kumkabizi mzee John na kumwambia "hizo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/zitakusaidia nauli ukifika chini chukua taxi itakayo kupeleka mpaka bahari huko utaingia boti litakalokupeleka mpaka dar es salaam sawa!!?"sawa asante "alijibu mzee John na kulitia burungutu lile mfukoni.Kwa mara nyingine tena mkewe na kamanda alitoa kamba ndefu kisha akaifunga vizuri kwenye nguzo iliyokuwa karibu na kumwambia mzee John kwamba



    atatumia kamba hiyo kushuka mpaka chini.Basi mzee John alipanda kamba haraka haraka na kuanza kushuka kufuata ile kamba taratibu,ilimchukua dakika kama kumi kufika chini,baada ya kufika chini mzee John alinyanyua mkono juu na kumuaga mkewe na kamanda.Mkewe na kamanda aliivuta ile kamba harakaharaka na kurudi chumbani kwake ambapo



    alimkuta kamanda akiwa bado anakoroma.Huku nako mzee John alisimamisha taxi ambayo ili mchukua mpaka bahari.Mzee John alimpa ujira yule mwenye taxi.kisha kufika bahari alitafuta boti ya kwenda Dar es salaam kwa muda kidogo hatimaye akaipata na kuingia tayari kuelekeaDar es saalam.Safari ilichukua karibu saa moja na nusu ambapo



    waliwalisili Dar es saalam majira ya saa kumi na mbili asubuhi.Mzee John alishuka haraka na kutafuta daladala ya kuelekea kimara.Kwenye lile jumba kamanda aliagiza kwa walinzi wake mzee John alletwe mbele yake na kisha kupigwa risasi na alisema akiwatoroka tu cha moto watakiona.Basi walewalinzi walienda mara chumbani kwa mzee John na kufungua mlango ghafla,wakaangaza huko na huko na kupekua kona zote hawa kumwona mtu wakarudi na kumuarifu kamanda********





    kamanda alibwatuka"pumbavu sana,wajinga nyie poteeni nataka mmlete hapa sasa hivi" kamanda alizunguka zunguka zunguka kwa hasira kali huku akiwaza kwamba kama atakuwa ametoroka basi ndo utakuwa muda wa yeye kuanikwa hasa kwa biashara yake haramu ya madawa ya kulevya.Wale walinzi walipita kila chumba ndani ya jumba lile huku



    wasambarua kila kitu labda pengine watampata mzee John.waliendelea kumtafuta lakini hawakumwona,wakaamua kurudi kwa kamanda na kuripoti kuwa hawaja mwona.Ile kamanda anapokea ile taarifa alichomoa bastola yake na kuwapiga wale walinzi,walinzi wote walianguka chini na kufa papo hapo .Damu ilisambaa chumba kizima.Kamanda aliondoka kwa hasira mpaka chumbani kwake kwa leo la kumuua mkewe lakini alistaajabu kuona kitanda

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kiwazi,aliangalia uvunguni na mlangoni lakini akaambulia patupu hivyo alizidi kupandwa na hasira akaamua kufungua droo yake na kutoa burungutu la pesa pamoja na vitambulisho vyake vya kusafiria ili aweze kutoroka.Alifanya hivyo himahima na kisha kuiweka bastola yake kiunoni,alifungua mlango na kutoka nje kuelekea car park tayari kwa



    kutoroka.Lakini alipokuwa akishuka ngazi kuelekea chini alishitushwa na risasi iliyogonga kioo cha dirisha kubwa lililokuwa mbele yake.Kamanda alibonyea chini kwa ustadi mkubwa kisha kuchomoa bastola yake na kujibu mapigo na huo ukawa ndo mwanzo wa kurushiana rasasi lakini mkewe na kamanda alitumia ustadi mkubwa akamlenga kamanda



    risasi ya bega"paaaa!!!!!" "aaaaghhhhh"kamanda aliguna.Mzee John nae alikaribia mazingira ya nyumbani kwake kimara kisha kubisha hodi"hodiiii""karibu"aliitikia mkewe na mzee John,ile mkewe na mzee John anatoka nje kufungua mlango akakutanisha macho yake na mzee John,ila hakuamini akaamua kuita mzee Johnnn!!!naam mama Lulu .Kuona vile mkewe na mzee John aliruka na kumkumbatia mzee John kwa furaha kubwa hali iliyompelekea kutoa machozi.Kamanda



    alianguka chini"puu" na kutulia kimya huku damu zikiendelea kumtoka,mkewe na kamanda alijihakikishia kwamba amemaliza jazi hivyo alimsogelea kamanda ili aweze kuchukua hela,akiwa anasogea kamanda alinyanyuka ghafla na kumfyatulia risasi mbili za kifua kwa mkewe ****



    Mzee John na mkewe waliingia ndani kisha kumfuata mtoto wao Lulu, mzee John hakuweza kujizuia chozi lilimdondoka hasa kutokana na mapenzi ya kweli kwa mwanae,alimpakata kisha kumbusu.Mzee John alianza kwa kuulizia kama wavuvi wenzake walikuwa hai na ndipo alipopata habari za kuhuzunisha kwamba walikwisha fariki na matanga yao



    yamekwisha fanyanywa,kwa kweli ilimuuma sana akabaki kuwa ombea Mungu.Ule wasaha wa mzee John kuelezea nini kilimpata ukafika ambapo alieleza yote aliyofanyiwa na kumshukuru mkewe kwa maombi yake kwa kipindi chote

    alipokuwa hatari.Kisha mongezi hayo mzee John alichomoa kibunda cha hela alichokuwa amepewa na mkewe na kamanda kisha kuanza kuzihesabu pamoja na mkewe,iliwachukua takribani saa moja kumaliza kuhesabu pesa ambazo



    zilikuwa shilingi millioni mbili na nusu,loo! ilikuwa ni pesa kubwa kwao hivyo wakaamua kukarabati nyumba yao na kununua toyo(pikipiki).Naam zile risasi mbili zilimwingia mkewe na kamanda barabara na kumpeleka chini,alianza kulia na kuhangaika kwa mauvivu makali akijaribu kujiokoa pasipo matumaini Lakini ghafla alisikia milio ya king'ora nje ya nyumba

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akajaribu kujikongoja mpaka dirishani na kuchungulia njeLo!walikuwa ni pollisi ambao walianza kuizingira nyumba huku wengine wakianza kuingia ndani,mkewe na kamanda akajivutavuta toka pale dirishani mpaka chumbani kwake.Akiwa





    ndani alisikia tangazo"yeyote aliyomo ndani ya nyumba hii ajisalimishe" kusikia vile mkewe na kamanda alichukua rundo la nguo na kujifunika ili kujificha.Polisi nao hawakuchelewa waliingia ndani na kukuta maiti ya kamanda na wale walinzi lakini baada ya kuangalia vizuri wakaona michirizi ya damu ikienda mbele wakaamua kuifuatilia 



    Walielekea kule damu ilikokuwa inatokea mpaka walipofika mbele ya mlango wa chumba cha mkewe na kamanda.Polisi walipeana ishara za kijeshi wakiwa na lengo la kujipa tahadhari hasa kwa kutojua ninini kilichopo ndani na ninani



    aliyopo huku,polisi wawili waliingia kwa tahadhari huku bastola zao zikiwa mbele.Mkewe na kamanda aliendelea kutokwa na damu nyingi zilizotokana na majeraha ya risasi,akiwa bado chini ya nguo aliweza kuona polisi wakiingia na bastola zao,akajaribu kujipapasa na kuangalia kama anabastola lakini alikua ameisahau pale sebuleni,akaamua kusubiri



    kitakacho tokea na kitokee,kisha polisi kuingia waliangalia kila kona kisha kuzirudia zile damu na kukuta zimeishia kwenye lundo kubwa la nguo,wakazipangua zile nguo haraka haraka na kukutana uso kwa uso na mke wa kamanda,wakamchukua mkukumkuku na kumpeleka kwenye gari la polisi hukuakiwa ndani ya pingu na kuambia kuwa



    yeye ni muuaji,maneno yaliyoenda sanjari na kipigo.Polisi wengine walianza kuipekua nyumba nzima ya kamanda na kufanikiwa kukuta kilogram mia mbili za madawa ya kulevya,wakayachukua na kwenda nayo kituoni.Jalada la kesi lilifunguliwa kama kesi ya mauaji na ya kukitwa na madawa ya kulevya.Mawakili wa pande zote mbili waliendelea



    kubishana kisheria.Kwa ujumla kesi ilikuwa imebalansi kiasi kwamba hukumu ilikuwa haitabiri .Hatimaye siku ya hukumu iliwadia mkewe na kamanda alipandishwa kizimbani chini ya ulinzi mkali wa askari polisi hukuwakizongwazongwa na waandishi wa habari waliotaka kupamba vyombo vyao vya habari.Punde si punde hakimu aliingia mahakamani ,watu



    wote wakasimama kama ilivyo ada ya mahakamani,kisha hakimu kukalia kiti cha akaanza kutoa maelezo mafupi kuhusu ile kesi huku vifungu vya sheria vikitumika na sasa akaanza kutoa hukumu,watu ndani ya mahakama walitulia tuli kusubiri hiyo hukumu huku mawakili wa pande zote mbili wakionekana kutokuwa na wasiwasi huku kila mmoja akiamini upande wake utashinda*****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Hazikupita dakika tano hakimu akasema"kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizo wekwa mtuhumiwa anahukumiwa kifungo cha maisha na kazi ngumu" kisha kumaliza halpo askari liita "court!!!!"""" watu wakasimama hakimu akatoka nje .Mkewe na kamanda alitokwa na chozi mara baada ya hukumu hasa pale alipokumbuka kwamba maisha aliyokuwa



    akiishi yalisababishwa na mumewe kamanda ambaye kamwe hakuwa chaguo lake la moyoni kwani wazazi wake ndio waliomlazimisha kuolewa nae hasa kutokana na tamaa ya pesa.Alikuwa ameshindwa kutoroka hasa kwa sababu



    alitishwa kuuwawa endapo angejaribu kutoroka,aliwaza pia ni namna gani ataenda kuishi gerezani kwani hali ya maisha hayo alikuwa akiiona kwenye television.Polisi wakamchukua na kumuingiza garini tayari kuelekea gerezani kutumikia adhabu yake.Njiani mkewe kamanda alionena kuweka kichwa dirishani ili awezekuiona dunia kwa mara ya mwisho.Ni



    miaka miwili sasa tangu mkewe na kamanda aanze kutumikia adhabu yake,umbo lake lilionekana kupungua na kuzoofu pia alikuwa mtu mwenye msongo wa mawazo.Mfungwa mmoja aliyekuwa rafiki yake alijaribu kumshauri kwamba ayakubali tu maisha hayo kwani ndio yaliyobaki na kuachana na mawazo,lakini ushauri huo ulikuwa kama upepo haya kupata hata chembe ya nafasi katika kichwa cha mkewe na kamanda chazaidi ni kwamba aliiendelea kujitenga na



    wenzake.Mwaka mmoja baadae hali ya mkewe na kamanda ilizidi kuwa mbaya kwani sasa ikuwa hali tena chakula hivyo mkuu wa gereza akaagiza apelekwe hospitali.Alichukuliwa haraka haraka mpaka hospitali na mara baada ya kuwasili walipokelewa na daktari kisha mgonjwa kulazwa chini ya uangalizi mkali wa askari na ilipofika mjira ya saa nane usiku hali ya mgonjwa ili badilika *****

     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog