Search This Blog

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU - 2

 







    Simulizi : Jinsi Jini Alivyolitesa Penzi Langu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Mzee John na wenzake walichukua ndo zilizokuwamo mle kwenye boti kisha kuanza kutoa maji yaliyokuwamo kwenye boti, walijitahidi kutoa maji haraka haraka ili mradi boti yao isizame. Hiyo



    botiwanayoitumia ilikuwa ni boti ya kijiji ambayo hukodishwa kwa vikundi mbalimbali vya wavuvi basi na sasa ilikuwa mikononi mwa kundi la akina mzee John.Waliendelea kutoa maji ambayo sasa yalionekana wazi kuanza kupungua.Upepo mkali uliendelea kuvuma kwa kasi zaidi hali8 iliyowapelekea akina mzee John

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuendelea kuogopa lakini walijipa moyo kwamba hali hiyo ya upepo ni ya muda mfupi tu.Tayari ilikwisha8 timu saa saba usiku wakiwandani ya bahari mzee John na wenzake walijaribu kutega nyavu zao ili waweze



    kuambulia chochote,basi walifanya hivyo haraka haraka hukuwakiogopa isije kufika asubuhi wangali bado hawaja pata kitu.shughuli nzima ilimalizika na wao akina mzee John wakatulia botini huku wakiwa wamewasha taa zao ilikuwavuta samaki.Dakika ishirini mbele hali ya hewa ilianza kubadilika taratibu wingu



    zito lilianza kujikusanya angani.Mzee John alihamaki kuona hali ile lakini wenzake wakamshauri kwamba wasubiri kidogo ili waweze kubahatisha samaki wanakurudi nao nyumbani .Wote wakakatashauri kusubiri kwa muda kidogo.Wakati wakiendelea kusubiri radi nazo zilianza kuunguruma mvululizo hivyo kuzidi



    kuogopesha,mzee John alipepesa macho kulia kushota,kaskazini kusini na mashariki magharibi bila kuona taa yoyote iliyokuwa ikiwa hivyo kuashiria kwa kulikuwa nakuna wavuvi wengine karibu katika bahari kubwa ya Hindi.Kuona hivyo alishauri waondoke mida hiyo lakini wenzake walionekana kulipinga hilo wazo.Huku



    wakiendelea kubishana mara mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ulioshahabiana na radi za kutosha ilanza.Mzee John na wenzake wakaamua kuvuta nyavu zao haraka haraka ilikuangalia kama watakuwa wamepata walau kidogo basi walifanya hivyo na wakahesabu .....moja.....mbili....tatu kisha



    wakavuta nyavu zao kwa haraka.Lo!!!! walikuwa wameambulia samaki kumi tu.Mvua kubwa iliendelea kunyesha huku upepo nao ukizalisha mawimbi makubwa sana.Mzee John na wenzake wakaanza safari ya



    kurudi nchi kavu lakini kiisha kwenda umbali wa mita kumi boti ilianza kujaa maji huku mawimbi yakiisukuma sukuma na kutaka kuipindua.Wakaanza tena shughuli ya kutoa maji nje, wakiwa katikati ya shughuli lilikuja wimbi moja kubwa likaibetua ile boti ambayo sasa ikawa ipo wimawima*********


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ ile wimbi liliibetua ile boti kisha kuipindua kabisa basi mzee John na wenzake wakakupwAhuko na kuiacha boti ikielea peke yake.Basi mzee John na wenzake walijitahidi kilammoja kupiga mbizi ili kuikaribia ile boti,kutokana na upepo mkali ile boti ilizidi kwenda karibu na kilindini.Mzee John
    aliizama na kuibuka huku akijaribu kwenda kwa kasi sana ili awezekulifikia botti,alifanya kuhudi sana na kufanikiwa kulikuta boti ambalo sasa lilikuwa umbali wa mita kama sabini hivi toka pale lilipopindukia basi pasi kukawia mzee John alilikwea lile boti kisha kuliwasha.kila alipojaribu 
    kuliwasha lilikataa kuwaka alijaribu kwa mara ya mwisho huku akirushwa rushwa na mawimbi ya
    baharini,wale wenzake nao wakaifikia boti mara baada ya kupiga mbizi vya kutosha.walipofika tu wakakutana na taarifa kutoka 8 mara ikawaka wote wakashangila y....e...ssssssss.Safari ya kurudi inchi kavu ilianza tena sasa wakikatika mwendo wa tahadhari,wakiwa bado safarini na huku mvua kubwa ikinyesha mara wakaona samaki mkubwa akijichomoza mbele ya boti yao
    kisha kuzama.Hilo halikuwatisha sana akina mzee John kwani ni kitu cha kawaida katika bahari ya hindi .Basi waliendelea na safari yao,wakiwa theluthi moja ya safari alitoke samaki mkubwa 
    akaipindua ile boti na kuwatupa mbali akina mzee John na ilikuwa saa kumi na moja kasorobo.kila
    mmoja alijitahidi kupiga mbizi ili kunusuru maisha yake.Lile boti nalo likazama na huo ndo ukawa mwisho wa boti.Mzee John aliendelea kupiga mbizi huku akijaribu kuangaza huku na huko akijaribu kuomba msaada,Mzee John alianza kuishiwa nguvu huku njaa kali ikiwa imembana,aliendelea kupiga mbizi.Huku nyuma mkewe na mzee John alianza kuingiwa na hofu...
    mara baada ya kuona kwamba mumewe harudi kwani haikuwa mazoea yake kuchelewa kurudi 
    kiasi kile akaamua kuendelea kusubiri zaidi.Ilipofika majira ya saa mbili asubuhi mzee John akiwahoi bin taabani alikatatamaa na kuamua kusubiri kifo huku hisia kali za kumbukumbu ya mwanae Lulu pamoja na mkewe kumjia kwa machungu yote akawa anaona sasa kwamba mwanzo wa maisha magumu kwa mwanae na mkewe umewadia.Akiwa katika dimbwi zito la mawazo Mzee John akasikia sauti kwa mbali alipo nyanyua kichwa aliona boti ikiwa inaelekea upande
    wake***********



    mzee akaamua kunyosha mkono juu ili wale waliopo kwenye lile boti waweze kumwona na kumpa msaada.Kisha kufanya hivyo mzee John alijisemea moyoni "kama ni kufa wacha nikafie mbali" akazama tena majini huku akipiga mbizi kuelekea upande ilikokuwa ile meli,pamoja na jitihada zake nguvu nazo



    hazikuwai tena upande wake kwa kule kutokula chochote kwa muda mrefu na kuogelea umbali mrefu kulimfanya awe mchovu zaidi.Huku kwa wavuvi wenzake na mzee John hali ilikuwanitete kwani wote walikuwa wamekwisha poteza lakini upande walioelekea kulikuwa hakuna msaada wowote ule basi kwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    matumaini hafifu na yenye harufu kali ya kifoi waliendelea kupiga mbizi ili kuitafuta nchi kavu.Wale watu waliokuwemo kwenye ile boti walifanikiwa kuona mkono wa mtu kwa mbali ambaye alikuwa akiomba msaada, wakasemezana wao kwa wao kisha kukubali kwenda kumwokoa yule mtu(mzee



    John).wakaendesha ile boti kwa kasi kubwa kuelekea mahali alipokuwa mzee John walipofika pale mmoja wao,ambaye alikuwa kiongozi wao alitoa amri"zamieni majini haraka kisha mwokoeni huyo" .wale jamaa waliruka haraka na kuingia majini huku wakiangaza huko na kule , baada ya dakika tano hivi kupita mzee



    John alikwisha okolewa, akiwa anahema kwa tabu sana hali iliyowapelekea wao kumpa huduma ya kwanza kisha kufanya hivyo waligeuza boti lao na kurudi kambini kwao.Wale wenzake na mzee John walijaribu kujiokoa lakini wapi nguvu ziliwaishia taratibu walianza kuelemea huku mmoja wao akinywa maji yale kwa



    kasi.Lo! maskini mvuvi yule alianza kuzama vivyo hivyo na mwenzake ambae tayari alikuwa amekwisha zama.Baada ya nusu saa maiti mbili zilionekana kuelea juu ya maji ,samaki nao hawakuwa nyuma kwani walishambulia zile maiti na kuacha mafuvu na mifupi vikishuka chini ya maji.Huku nyuma mkewe na mzee John alikwenda kuripoti polisi juu ya kupotea kwa mumewe,polisi wakaanza upelelezi wao mara baada ya



    kupokea taarifa hizo.Mzee John alipokea huduma ya kwanza iliyomfanya kuanza kujielewa.Baada ya kuangaza macho huku na huko akagundua kuwa yuko kwenye boti huku akiwa amezungukwa na watu asio wajua.Safari ya kuelekea kambini ili endelea hakuna mtu aliyekuwa akiongea chochote hali iliyomfanya mzee John kushituka kidogo akaamua kuuliza"samahani ninyi ni akina nani? akiwa na matumaini ya kupata jibu zuri mara alisikia sauti nzito ilioambatana na ukali"kimya""funga domo lako""






     Mzee John alikaakimya huku kengele ya hatari ikiendelea kulia kichwani mwake lakini kwa upande mwingine nafsi ilimwambia avute subira kidogo ili aone nini kitafuatia.Safari iliendelea kimyakimya na hatimaye wakafika nchi kavu na baada



    ya kufika hapo mzee John aliamuriwa kushuka botini haraka sana naye alifanya hivyo bila kuleta ubishi wa aina yoyote.Mara tu baada ya mzee John kushuka kiongozi wakundi aliyejulikana kama kamanda aliamuru "MFUNGENI KITAMBAA USONI"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitambaa kilifungwa haraka haraka .Baadae kidogo mlio wa gari lililokuwa kasi ulisikika ukikaribia eneo walilokuwepo akina mzee John.Hatimaye gari lilifika eneo walilokuwapo akina mzee John , mzee John alichukuliwa mkukumkuku kisha kutupwa ndani ya gari na kwa kasi gari liliondoshwa.Njiani mzee John alitamani kuuliza ni wapi walikokuwa wanakwenda na kwanini



    wamemfunga kiasi kile ila yote hayo hayakuwezekana kwani tayari alikuwa amekwisha fungwa kitambaa mdomo hali iliyomfanya kushindwa kutoa sauti.Moyoni mwake aliwaza "hawa watakuwa ni majangili basi hapa lazima nitauawa lakini yote na mwachia Mungu".Gari lilisimama ghafla honi kali ilipigwa "piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kisha geti lilisikika likifunguliwa gari



    lilisimama milango ilifunguliwa,mzee John alichukuliwa mpaka kwenye chumba kimoja kisha kuwekwa humo.Alifunguliwa vitambaa vyote .Kabla mzee John hajaongea lolote mlango wa chumba walimokuwamo ulifunguliwa na kufungwa haraka



    ambapo aliingia dada mmoja na kuweka chakula mbele ya mzee John kisha amri ilitolewa"MALIZA CHAKULA CHOTE HARAKA" kisha amri hiyo kutolewa mlango ulifunguliwa na wote wakatoka kumwacha mzee John akila chakula.Huyu kamanda ambaye ndio kiongozi wa kundi ambalo linajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nje na ndani ya



    nchi.Ilimchukua muda kidogo mzee John kuamua kula kile chakula kwani kuna wakati alihisi labda kinaweza kuwa na sumu lakini tena upande mwingine njaa ilikuwa inamuuma sana,akakatashauri kukila kile chakula na alifanya hivyo ila mara baada ya kula kile chakula mzee John alijikuta akiishiwa nguvu na mwili kulegea akataka kupiga kelele kuomba msaada ********




    Haikupita hata dakika mbili mzee John alikuwa amepitiwa na usingizi mzito muda huo ilikuwa ya pata saa kumi na moja jioni .Huku nyuma mkewe na mzee John alibaki akilia kwa uchungu sana huku akimtizama mwanae lulu , aliwaza mengi sana kiasi



    kwamba mochozi ndo yakawa yanatiririka kama maji . Polisi nao waliendelea na upelelezi wao pasi kupata majibu.Familia za wale wavuvi wawili ziliamua kuomboleza msiba kwaajili ya ndugu zao lakini kwa upande wa mkewe na mzee John hali haikua vile aliendelea kumuomba Mungu ili aweze kumwona tena mume wake kipenzi.Mkewe na mzee John aliamua kulima bustani

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ya mboga ili aweze kuuza hiyo mboga kisha kujikimu kimaisha hasa ukizingatia kwamba mtoto wake bado mdogo na anahitaji matunzo.Ilikuwa ni asubuhi nyingine tena ambapo mzee John aliamka kisha kufikicha macho na kujinyoosha akaangalia kushoto na kulia, juu na chini kisha kuachwa na bumbuwazi mara baada ya kujiona yupo kwenye chumba kizuri



    sana cha kifahari chenye malumalu,sofa kubwa la kupumzikia na friji kwa pembeni bila kusahau television akiwa haamini anachokiona mzee John alilinganisha maisha ya nyumbani kwake kimara na pale akaona yuko sehemu ghali sana akiwa bado anawaza mara mlango ulifunguliwa akaingia binti mrembo mithili ya mabinti wa kigogo,akamwambia"habari ya asubuhi"



    "nzuri" "umeamkaje?" "salama" , yule dada aliendelea, naomba unifuate.Basi mzee John aliondoka na yule dada mpaka mbele ya mlango mmoja,walipofika mlango ulijifungua wakaingia ndani.Mlendani walimoingia ilikuwa ni sebule kubwa na ya kisasa .Mzee John alikaribishwa chai nzito kisha kumaliza walitoka nje ya sebule na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu a



    mbapo walikutana na mlango mmoja.Yule dada alibisha hodi na mlango ukafunguliwa kisha dada yule alisema"huyu hapa boss" "sawa waweza kwenda" boss alijibu.Dada alitoka nje.Boss alimkaribisha kiti mzee John kisha kumwuliza"waitwa nani wewe na waishi wapi??! "naitwa mzee John naishi kimara" mzee John alijibu.sawasawa kunajambo nyeti nataka

    kukueleza********




    Kwanza nataka nikufahamishe kwamba sisi tulikuokoa wewe kule baharini ulipokuwa ukikaribia kuzama na tukaamua kukuleta huku kambini maana kuna kazi muhimu tunayotaka wewe ufanye na ukikataa tu mwisho wa maisha yako



    utakuwa umefika.Sisi tunajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ,hivyo sisi tutakupa wewe chochote kile utakacho na utakipata ila sisi tunataka wewe kujaza madawa ya kulevya katika pakiti hafu zitapelekwa kwenye mashine tayari kwa kufungwa hatimaye kusafirishwa,haya tuambie basi uko tayari au la?.Mzee John aliinamisha kichwa



    chini huku akitafakari nimaamuzi gani ayachukue,picha ya mkewe pamoja na mwanae Lulu zilimjia na kumuhimiza kurudi nyumbani kuwasaidia maana wanateseka,Mzee John aliipima kazi aliyokuwa akienda kuifanya akakumbuka jinsi alivyo wahi kujiapiza kwamba hata kaa kujihusisha na madawa ya kulevya lakini upande mwingine bado alihitaji kuiona familia



    yake.Baada ya tafakuri ya muda wa takribani dakika tano,Mzee John alijibu"niko tayari",boss alicheka"ha...ha....ha" safi sana nenda kapumzike tutaanza kazi. Baada ya miaka mitatu kupita pasipo kumwona mumewe mkewe na mzee John alikata tamaa na kuamini kwamba huenda mumewe alikwisha fariki dunia.Mzee John aliendelea na kazi yake ya kujaza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    madawa kwenye pakiti ambapo ilimlazimu kujaza pakiti mia tatu kwa siku ambapo alitakiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi mpaka jioni,kwa muda wote aliokuwa kwenye lile jumba hakuwahi kutoka nje hivyo hakujua ni wapi alipo.Siku moja akiwa anaendelea na kazi aliona mlango ukifunguliwa na dada mmoja mweusi wastani mrefu kidogo aliingia ndani kisha kumsalimu mzee John"shikamoo mzee""marahaba""nikusaidiaje?" nataka kukuuliza jitu sijui ukotayari



    "ulizatu''asante yule dada aliendelea,mimi ni mke wa kamanda kiongozi wa hili kundi ningependa kujua ulifikaje huku maana si eneo zuri hafu nimekuwa nikikuonea huruma sana.Mzee John alieleza kila kitu mpaka yeye kufika pale lakini aliendelea "natamani sana kurudi kuiona familia yangu kwani nilimwacha mke wangu na mtoto mdogo hana hata mwaka



    hafu sijui wako hai au la,machozi yalimtoka mzee John kisha aliendelea nimeambiwa sitatoka humu ndani hafu sijui niko wapi mimi" pole usilie mzee,alijibu mkewe na kamanda,ki ukweli toka uingie humu mume wangu"kamanda" amekuwa akizungumzia juu ya kukuua kwani anaogopa kwamba utatoa siri kwa kweli kesho ndio siku ya kifo chako ila mimi



    nataka nikusaidie.Nitashukuru sana alijibu mzee.Sasa kesho saa nane usiku nitakugongea mlango ili kukutorosha.Baada ya maongezi hayo waliachana.Usiku ulipoingia Mzee John hakulala hamu ya kuiona familia yake ilizidi ,ilipotimu saa nane



    mlango uligongwa,mzee John alifungua haraka na kumwona mkewe na kamanda akiwa amevalia mavazi ya kijeshi,akamwambia nifuate.Safari ya kutoka nje ya jumba ilianza walipandisha ngaz kwa haraka na tahadhari,lakini ghafla wakasikia mlio mkubwa '"paa!!!!!! ********

     
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog