Search This Blog

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS





    *********************************************************************************







    Simulizi : Jinsi Jini Alivyolitesa Penzi Langu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikuwa ni alhamisi tulivu yenye upepo mwanana huku watu wakiendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.Madaktari nao walikuwa bise na taaluma yao ya kuokoa roho za watu.Ndani ya hospitali ya lugalo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/wagonjwa wengi walifurika huku madakaktari nao wakiendelea kutoa huduma, kama ilivyo ada ndugu wa wagonjwa walikaa nje kusubiri taarifa za maendeleo ya wagonjwa wao, basi hali ilikuwa hivyo kwa mzee



    John ambaye alikuwa akimngoja mkewe amletee nuru dunia yaani ameletee mwana atakae kuwa mrithi wake wa baadae. Akiwa amejiinamia mzee John aliwaza sana ni namna gani atampenda huyo mtoto wake



    mpendwa atakae zaliwai ukizingatia kuwa huyo ndie atakae kuwa kifungua mimba chake pasi wazo hilo kuisha jingine la jinsia yai mtoto liliingia la hasha! hilo halikumchanganya sana mzee John kwa alijikuta akisema"yote namwachia Mungu". Ndani ya hospitali ya Lugalo madaktari waliendelea kumhudumia mkewe



    na mzee John, hali haikuwai nzuri sana kwa upande mkewe na mzee John kwani alitokwa na damu nyingi sana wakati wa kujifungua hali iliyomfanya Dr.Martin awaambie madaktari wenzake "doctors her condition is get worse she bleed a lot" baada ya kauli hiyo daktari akamwagiza nesi ampeleke mgonjwa chumba cha



    wagonjwa mahututi( I C U) bila kupoteza wakati mgonjwa alikimbizwa ICU kisha jopo la madaktari watatu kufuata.Juhudi za kunusuru maisha ya mtoto na mama ziliendelea, lakini mara dkt.Martin aligeukia kipimo kilochokuwa kikionyesha mwendo wa mapigo ya moyo ya mgonjwa.oooopssss daktari aliguna kwa mshangao.



    Dkt.Martin aliguna kwa mshangao mara baada ya kuona mapigo ya moyo yakienda kasi yaani presha ilikuwa juu sana,daktari akaamua kuchukua maamuzi ya haraka kwa kumwekea mgonjwa mashine ya kumsaidia



    kupumua.Madaktari wengine waliendelea kuzuia damu zisiendelee kutoka zaidi na hatimaye walifanikiwa,kazi iliyobaki ilikuwa ni kushusha presha(mapigo ya moyo).Dkt. Martin aliangalia tena kile



    kipimo kwa umakinizaidi kisha akasema"dah!! tumshukuru Mungu hali yake imewezakutengamaa" mapigo ya moyo yakienda kwa kasi ya kawaida. Jopo zima la madaktari lilimgeukia kichanga aliyezaliwa na kukikuta kikiwa kinalia,hii ilikuwa ni ishara tosha kwamba kichanga kilikuwa hai.Huku nje wasiwasi ulizidikumtawala

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/mzee John kwani muda ulizidikwenda pasipo yeye kupokea majibu yeyote yanayohusu hali ya mkewe,hali iliyompelekea mzee John kuzungukazunguka kwenye benchi aliliokuwa amekalia.Punde kidogo dkt.Martin alitoka nje na kumpahongera mzee John ,alimshukuru sana daktari kwa kazi nzima ya kumuhudumia mkewe



    na akamwomba aingie kumwona mkewe pamoja na mtoto wake,daktari alimruhusu huku akimsitisizia asikawie kutoka kwani mgonjwa bado anahitaji mapumziko.Pasi kuchelewa mzee John aliingia wodini na kumpahongera mkewe na kukigeukia kichanga chake kwa furaha iliyopitiliza akakibusu "mwaaa".Mzee John



    alianza kufuatilia ruhusa kwa daktari ili waweze kuondoka siku ile ile.Ilikuwa yapata majira ya saa mbili usiku ndipo walipopata ruhusa ya kurudi nyumbani kwao kimara.Majira ya saa tatu kasorobo( na dakika arobaini na tano) usiku safari ya kuelekea kwao9 ilianza hasa baada ya kukodi taxi toka Lugalo



    hospitali.Safari ilianza vizuri huku mzee John na mkewe wakifurahia ujio wa mtoto wao mpendwa.Wakiwa njiani kuelekea nyumbani mzee John alimhimiza dereva aongeze mwendo ili wawahi kufika nyumbani,naye dereva bila ubishi alitii kwani alichokuwa anajali yeye ni pesa yake tu.Basi wakiwa ndani ya mwendokasi huo



    mara taa za mbele za gari zilizimika ghafla na mara dereva alipiga kelele" tunakufaaaaa,kisha mshindo mkubwa ukasikika"paaa" kisha ukimya mkubwa ukatanda****************



    Tayari gari lilikuwa limetumbukia mtaroni na watu wa mitaa ya karibu nao hawakuchelewa kuona vile walisogea chapuchapu ili kujaribu kuokoa.Baada ya dakika mbili hivi kupita tayari watu wengi walikuwa wameshajaa kulizunguka gari ili kutaka kujua nini kinaendelea.Basi raia mmoja akashuka chini na kuukaribia mlango wa dereva kisha kuchungulia



    ndani na kumwona dereva akiwa anavuja damu kwenye paji lake la uso huku akiwa hajitambui.Kuona hivyo akaamua kuita watu wengine ili waweze kumsaidia kumtoa yule dereva kupitia dirisha la lile gari.kisha kumtoa yule dereva yule



    raia alirudi kwenye gari na kuchungulia kwenye mlango wa katikati na kuona watu kwa mbali alipoangalia vizuri alimwona mwanamke mmoja pamoja na mwanaume wakiwa wameshika katoto kadogo.Basi aliwaita wenzake na kuanza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kuwatoa.Mara tu baada ya kutolewa kwenye lile gari mzee John na mkewe waliwashukuru wote kwa kuja kuwaokoa kwani wao walitoka salama , wote wakaongozana mpaka pale alipokuwa amelazwa yule dereva taxi.Wakajaribu kumpima kasi ya mapigo ya moyo wakaona yana piga taratibu sana hivyo ikawalazimu kukodi taxi nyingine ili



    kumuwahisha yule dereva hospitalini.Mzee John na mkewe walipasika kukodi taxi nyingine mpaka nyumbani kwao kimara.Baada ya yule dereva kufikishwa hospitali manesi wa zamu walipokea haraka haraka na kumpeleka ICU



    madaktari walianza kumuhudumia.Baada ya masaa mawili dereva aliweza kuzinduka na kujielewa lakini baada ya dakika kumu dereva alilaanza kulalamika kuwa kifua kinambana sana,nesi kuona vile akakimbia kumwita daktari, daktari



    alipofika alimwona mgonjwa akizidikuishiwa nguvu,daktari akaita « dereva»sauti kwa mbali iljibu«na...a...a..m» daktari akaita tena «dereva»kwa mara hii hakuna sauti iliyosikika ikijibu chochote**********



    Daktari alimsogelea dereva kisha kumgusa sehemu ya moyo na kuinamisha kichwa chake .daktari hakuamini alichokuwa anakishuhudia akaamua kuweka kifaa chake cha kupimia mapigo ya moyo katika sehemu ya



    usawa wai moyo na kukivaa vizuri masikioni mwake.Loo!!!maskini dereva alikuwa amekwisha aga dunia(kwisha fariki) basi daktari akamwagiza nesi kumfunika marehemu kisha kufanya taratibu za



    kumpeleka mochwari ,hati ya kifo iliandaliwa na kila la kitu kilikuwa sawa kusubiri taratibu za mazishi. Mzee John pamoja na mkewe walifika nyumbani kwao salama salimi,basi wote kwa pamoja walimshukuru Mungu kwa kuwaepusha na ajali mbaya sana ya gari. Maisha mapya kwa Mzee John yalianza hasa baada ya



    mwanafamilia mmoja kuongeza.Mzee John alizidisha upendo wake kwa mkewe hata kufikia kumpikia chakula hakika kila mmoja wao alifurahia maisha ya ndoa huku akiomba mwenzake aishi maisha marefu.Baada ya



    miezi mitatu kupita mkewe na mzee John alirejea katika hali yake ya kawaida yaani alikuwa amepona kabisa,tayari walikwisha mpa jina mtoto wao ambaye sasa anaitwa Lulu.Mzee John alirejea katika shughuli yake ya uvuvi katika bahari ya hindi na siku hiyo ilikuwa ni jumatatu ndipo mzee John alikwenda baharinni na



    kukutana na wavuvi wenzake walio mtania wakisema"annhaa mzee John naona nyavu zako zimecheuaa...na sasa ka mwaka haka umepata kabinti"hahaha!!! wote walicheka.Baada ya makaribisho hayo yote mzee John aliuliza,jamani kazi zinaenda????!wakamjibu kwa tabu sana.kisha mazungumzo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    walikubaliana kwamba usiku wataenda kuvua,waliagana na kilammoja akaenda nyumbani kwake kujiandaa na safari ya usiku.Mkewe na mzee John alimsubiri mumewe kwa hamu na mara mzee John alitokea basi



    mkewe alimuwao kisha akamkaribisha chakula nao wote wakajumuika katika chakula hicho.Ilipofika jioni mzee John alimuaga mkewe tayari kwa safari ya baharini.Majira ya saa mbili usiku wavuvi wote waliingia



    ndani ya boti yao kuanza safari.Mara walipokaribia kilindi boti ilianza kuyumba kwa kasi huku maji yakiingia ndani hasa sababu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini**********




    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog