Search This Blog

MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI - 3

 





    Simulizi : Mtoto Wa Mchawi Wa Kijiji

    Sehem Ya Tatu (3)



    Niliamua kutoka tena nje kwenda kuangalia uenda labda alijificha pindi mara ya kwanza nilipotoka. Nilifungua mlango wangu taratibu huku macho yangu nikiyatumbua vyema kuhakisha kwamba ninacho kisikia ndio ninachokiona au la! Sikuweza kuona kitu chochote, ila nilihisi kama mtu yupo nyuma yangu. Niligeuka haraka, nilishituka macho yangu yalipokutana ana kwa ana na Mwajabu, aliniogopesha sana. Namna ya ujio wake, mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio kuliko kawaida. Sikutegemea kabisa hali ile kama ingenitokea muda ule

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huku bado nikiwa kimya vile mdomo wangu ulishindwa hata kutamka neno lolote mbele ya Mwajabu, nilishangaa tu mikono ya Mwajabu ikiwa imekamatia kiuno changu vizuri ikiwa ananivuta kuelekea kwenye chumba changu. Hata sikuelewa kinaenda kutokea nini?

    Wakati ule nilijikuta nipo chini huku juu ya mwili wangu tayari ulishakuwa umetawaliwa vyema na wake mwili kama vile anapiga mbizi kwenye swimming pool. Ajabu Mwajabu alininyonya mdomo wangu kwa nguvu, hapo tena akili yangu ilishaanza kupotea nikajikuta nipo dunia nyingine ya mautamu.



    Nilihisi utamu kila alipojaribu kutalii kwenye kila upande wa mwili wangu. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya mchezo ule pengine tangia nilipojitambua. Lakini kwa upande wake Mwajabu alionekana yuko njema tofauti na nilivyo mimi.

    Muda mchache tu kutokana na maufundi aliyonionesha nilijikuta na mimi naenda sawa na mchezo, utamu nilikuwa nikiupata yamkini hata Asali haikuwa ikitia mguu, hata kidogo. Nilitamani kuwa naye muda wote ndani mule tupeane utamu tu mwanzo mwisho. Hakika utamu alionesha Mwajabu sikuwa tayari kumpoteza kabisa kwenye maisha yangu.

    Kila moja upande wake tulikuwa tumeridhika na hali ya mchezo ule, nilimsifia Mwajabu kutokana na mambo aliyonipa kwa siku ile huku nikijiapiza pendo langu halitatoka kwa mtu mwingine zaidi yake.



    Si mimi tu niliyeonekana kukubali ule mchezo, hata yeye Mwajabu alinisifia kuwa nimejariwa fimbo na ama kweli inachapa. Tena si kwa kawaida hata ingekuwa nyoka wa kiasi gani inaweza kupoteza uhai wake muda mfupi tu. Mwajabu alijikuta akiniambia hayo huku akionesha tabasamu lake waziwazi kwangu. Nilijihisi nimekuwa mtu wa bahati sana. Nilishasahau kuwa muda si mrefu Mzee wake anaweza kumwozesha kwa mtu mwingine.

    ______________

    Kigiza cha asubuhi kilishaanza kupotea kuikaribisha siku mpya iliyojaa nuru ndani yake, hakukuwa hata moja kati ya Wanakijiji wa Tangeni aliyeamini kuwa angekuwa hai kutokana na hali ilivyokuwa punde tu ilipokatika Mvua ambayo ilinyesha kwa siku saba mfululizo, na mambo ya kutisha ndani ya usiku wa siku ule hakuna hata mmoja aliyekuwa akiamini kuwa yuko salama.

    Hali ilizidi kuwa ngumu, hakuna hata aliyethubutu kulitaja jina la Mzee Shabani, uchawi wake ulikuwa ni zaidi ya uchawi na Wachawi wote waliowahi kutokea kipindi cha nyuma baada ya matatizo kama yale kuwatokea Wanakijiji, lakini hii ilikuwa ni kiboko kabisa.

    Baada ya wiki kama moja hali ilitulia kidogo, matukio ya ajabu yalipungua, tofauti kabisa na mwanzoni. Kidogo iliwasahulisha Wanakijiji machungu, hata hawakujua kuwa Mzee Shabani alikuwa yu sehemu gani maana mahali ilipo nyumba yake hakukuwa na kitu chochote kilichoonekana zaidi ya shimo tu ilikuwepo siku kadhaa baada ya upotevu wa wale vijana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku kadhaa baada ya matukio ya ajabu kupotea hali ya kijiji ilitulia kabisa, lakini usiku mmoja baada ya siku kumi tu ya yale yote kutokea, vilisikia vitu vya ajabu sana katika kila mahali. Ilikuwa ni hatari tofauti kabisa na mwanzo, hali ilibadilika ghafla na kuwa si ya kawaida. Hali ya kugofya zaidi ilitanda ndani ya kijiji.

    Kelele za kuomba msaada zilisikika kila pande za Nyumba nyingi ndani ya kijiji kile,

    "Mama Mama nakufa, toba. Mungu nisaidie.” Zilisikika huku zikifatiwa na sauti zile za ajabu zikienda sambamba na miungurumo ya radi kana kwamba mvua ilitaka kunyesha tena.



    Ziliendelea kwa muda mrefu kidogo na hatimaye ukimya ukachukua nafasi ndani ya kijiji kabla ya kusikia vilio kila pande. Vilio vile vilivyokuwa vikisika wazi vilikuwa vimejaa uchungu, namna ya waliaji wenyewe walivyokuwa wakilia, ilikuwa ikihuzunisha sana na kuogopesha mno. Vilio vya kwikwi vililindima mno, lakini haikufanya baadhi ya wenye Nyumba zingine ambazo hazikukumbwa na balaa lile kutoka kama ilivyo taratibu za kijiji kile wakiwa wamepata tatizo. Lakini kilichokuwa kikitawala ni ukimya wa sauti za watu upande ule mwingine na kelele za milango iliyokuwa kama ikihimarishwa kukabiliana na lile. Usiku ulikuwa mrefu sana na hata palipokucha ilitumia muda sana watu kutoka ndani ya Nyumba zao kufahamu lile lililokuwa likiendelea kutokana na ile hali ilovyokuwa usiku wa kuamkia siku ile.

    Habari za kusikitisha zilienea haraka ndani ya kijiiji pindi nuru iliporejea tena kuikaribisha siku ile. Habari zilizofanya kuacha simanzi nzito ndani ya kijiji kile huku ikiongeza machungu juu ya Mzee Shabani na familia yake. Lakini cha kufanya hawakuwa nacho kwa muda ule hali ilizidi kuwa tete vifo viliongezeka siku hadi siku huku baadhi ya Wanakijiji wakihama ndani ya kijiji kile kusogea upande wa vijiji vingine. Zoezi lile likiwa la bahati nasibu maana wengi wao walishia kufa njiani kutokana mauzauza njiani, paka mara simba watu basi, ilimladi tu mambo ya ajabu tu kwao yote ni mateso kutoka kwa Mzee Shabani ambaye chanzo hata hakijulikana kwa mara moja.



    Mpaka pale takribani nusu ya wanakijiji walipopoteza maisha hali ile iliwastua sana viongozi wakijiji wakiongozwa na Baba Jack ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kijiji kufanya mipango ya kumleta Mzazu wa Mzazu kwa mara nyingine tena ndani ya kijiji cha Tangeni. Kupambana na hali ile mambo yalifanyika haraka haraka ukiongozwa na waganga wa pale ndani ya kijiji na hatimaye Mzazu alilejea ndani ya kijiji cha Tangeni kupambana na lile ila safari hii aliamua kufanya kazi kwa namna tofauti hakuitaji vijana tena aliwaomba viongozi wote kuhusika kwenye kazi ile ambayo aliipanga kufanyika usiku ule.

    _____________

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa upande wangu namna alivyokuwa akinisifia Mwajabu nilizidi kupagawa wakati nikifahamu ukali wa Mzee wake, ila nilijisemea tu kimoyo kimoyo kama mwanae amenikubali na tunapendana hivi anaweza kurudisha posa ya mwanae kutokana tu jinsi tulivyo.

    Nilivuta pumzi ndefu huku nikimwangalia Mwajabu kwenye kile changu kitanda hali iliyofanya Mwajabu kuniangalia kwa jicho la kunitamani tena, niliona raha sana jicho la Mwajabu nilivyokuwa likiniangalia nilitamani kila siku liwe linaniangalia vile kabla ya kuniswalika swali.

    "Vipi mbona kama unawaza kitu Jack wangu." Swali lile liniingia vizuri nakunitoa kule kwenye fikra dhidi yake nikimwangalia tena halafu nikaanza kumwambia jambo,

    "Unajua Mwajabu jinsi gani ninavyokupenda, si leo upendo wangu sikuzote utabaki kwako. Simjui mwanamke mwingine zaidi yako, na sitamani mwingine, ahhhhhhhhhh." Niligumia kidogo huku nikizungusha macho yangu kumwelekea Mwajabu ambaye alikuwa sasa amenilalia kwenye kifua changu pindi naongea yale. "Lakini Mwajabu suala la wewe kuchumbiwa linaniumiza kichwa utawezaje kumshawishi Mzee Shabani kulikataa ilihali hali tayari amekubali kupokea posa yako na wanasubiri tu muda muafaka wa ndoa yako? Eti.” Nilimaliza kuongea yale huku ikifatiwa na maneno ya Mwajabu akiniambia kuwa atajua yeye nimwachie suala lile. Sikutaka kubisha jambo lile nilimwitikia kwa kichwa kuonesha nimekubali.



    Tuliongea mengi chumbani mule zikifatiwa na ahadi nyingi za mapenzi, kiukweli nilijisikia raha sana namna ya uongeaji wake, sauti iliyojaa visa vya kimahaba, ilinifanya nijisikie nipo dunia nyingine, na hata hapo muda ulizidi kwenda hakuna aliyoonekana kulijali hilo. Maongezi yalinoga kwelikweli, yaani kama lisingekuwa lile jogoo kuwika muda ule, basi kigiza kingetufikia nipo na Mwajabu ndani ya mule. Lakini mara nyingi mimi hupendelea kusikiliza ule uwikaji wa jogoo huwa unanipa taarifa ya muda angalau hapo ulinipa taswira ya muda kwenda, hivyo wakati ule niliona ni sahihi kwa Mwajabu kuwahi kurudi Nyumbani kwao.

    Harakaharaka Mwajabu alivaa nguo zake huku na mimi nikivaa zangu kumaliza kule kuvaa kulienda sambamba na kufungua mlango wa chumbani kwangu, lakini cha ajabu ile tunatoka tu mule ndani kuna kitu kilinistua kwenye mboni zangu.

    Kana kwamba macho yangu yaliingia kitu hivi kwani uzito wa macho yangu kuona mwanga mbele ulininitiza nilifikicha macho lakini bado hali ile ilikuwa bado inaendelea. “Mwajabu,“ Niliita nikifatiwa maneno yale yalikuwa yakitoa kwenye kinywa changu. “Mwajabu macho yangu mazito, mpenzi sioni vizuri baby.”

    “Unasemaje Jack?”

    “Sioni vizuri Mwajabu.”

    “Embu niangalie,”Mwajabu aliniambia haraka nilifanya vile nilishanga akiyafikicha macho yangu na viganja vyake mara nuru ilirejea sawia ndani ya mboni zangu, hali ile ilipotea haraka kama haikunitokea punde tu. “Vipi Jack unaonaje mpenzi?”Aliniuliza Mwajabu huku akiwa amekamatia kiuno changu vizuri kwa mahaba, nilijibu nipo sawa huku ikifatiwa na kicheko cha Mwajabu. Sikujua kwanini ananicheka ila kwa vile nilikuwa sijiwezi kwa mambo aliyenionesha muda mfupi na mimi nilijikuta nacheka tu.

    Taratibu tuliendelea na safari ya kusindikizana njiani mule hadi nilipoona panatosha, nilimuacha Mwajabu. Wakati huo tukipeana ahadi ya kuonana tena siku inayofata nikiwa nafuraha isiyo nakifani maana sikutegemea kama safari yangu ya mapenzi na Mwajabu ingeanza kwa namna ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliendelea kupiga hatua kuelekea kwenye kijumba changu nikiwa nachekacheka hovyo njiani mule, kama ingekuwa napishana na mtu aliyekuwa amenizoea, basi angehisi nimekuwa chizi ghafla. Lakini kwa jinsi nilivyokuwa, nisingejali. Ama kweli penzi linanguvu mno, sikuwahi kuwa na furaha ndani ya moyo wangu kama siku ile na hata pale nilipofika Nyumbani nilielekea chooni kuoga huku nikipiga miluzi kama ndege, miluzi ambayo ilikuwa ikikonga kweli moyo wangu.



    Dakika kadhaa niliweza kumaliza kuoga na kumaliza kule kulienda sambamba na kuvaa na kutoka ndani ya chumba changu huku akili yangu ikiwa inawaza kuelekea uwanjani kwenda kuangalia mazoezi kama siku zote ratiba yangu ilivyo.

    Japo sikuwa na uwezo wa kucheza mpira, ila nilikuwa mpenzi sana wa mchezo ule, kwangu mimi unaweza ukuninyima vitu vyote lakini si kutizama mpira. Nilikuwa nikipenda sana mchezo wa mpira hivyo mida ya jioni ratiba yangu ilikuwa lazima nisogee kwenye kiwanja cha kijiji huku ndio nilikuwa nikipata burudani ya mpira pamoja na porojo porojo za vijana wengi wa kijiji pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog