Search This Blog

MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI - 4

 





    Simulizi : Mtoto Wa Mchawi Wa Kijiji

    Sehem Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Japo sikuwa na uwezo wa kucheza mpira, ila nilikuwa mpenzi sana wa mchezo ule, kwangu mimi unaweza ukuninyima vitu vyote lakini si kutizama mpira. Nilikuwa nikipenda sana mchezo wa mpira hivyo mida ya jioni ratiba yangu ilikuwa lazima nisogee kwenye kiwanja cha kijiji huku ndio nilikuwa nikipata burudani ya mpira pamoja na porojo porojo za vijana wengi wa kijiji pale.

    SURA YA NNE.

    Nilipiga hatua kadhaa baada ya kutoka ndani kwangu hatua ambazo hazikuchukua muda mwingi hatimaye nilikuwa nimefika uwanjani lakini cha ajabu sasa nilishangaa hali niliyokutana nayo pale kiwanjani.

    ____________

    Sasa saba usiku zilisikika sauti ambazo zilikuwa zikiongozwa na mganga Mzazu huku akiwa pamoja na viongozi wa kijiji.

    “Hahahahaha….tulia” Sauti ya Mzazu ilisikika huku akiwa ameshika kitu mithiri ya pembe la ngo’mbe akirizungusha zungusha kwa muda kidogo. Kabla hajanena kitu mbele ya viongozi wa kijiji kile wakiwa wanaongozwa na Mwenyekiti, Baba Jack.



    “Naam! Tatizo lenu nimelitambua, hahahaha! nimelitambua” Sauti ya kutetemesha na kuogofya ilitoka ndani ya kinywa cha Mzazu na kuwaogopesha zaidi viongozi wale.

    Wakati huo kijiji kilikuwa tuli, kimya kilikuwa kimetawala kumwachia Mzazu. Walikuwa wakiona kama mkombozi wao kutokana na kadhabu walizokuwa wakizipata kutoka kwa Mzee Shabani, gwiji la wachawi.

    “Leo ndio mwisho wake, nimeamua kumalizana nae, lakini kabla sijalimaliza ili lazima mtambue kitu kimoja Mwenyekiti,” aliita Mzazu kwa sauti iliyomfanya kumshtua Baba Jack. “Sikia, wewe na Mzee Shabani mlikuwa mna matatizo wa uongozi, kumbuka wakati mnaitisha uchaguzi wewe ukiwa kiongozi ambaye uliamua kugombea tena. Wakati huo Mzee Shabani akiwa na miezi mitatu ndani ya kijiji lakini alikuwa akipendwa sana na hata alipoamua kugombea kwenye uchaguzi ule na kushinda, ila nyinyi kutokana na fitina zenu mliamua kupindisha lile, na hata alipoamua kuwafata kistarabu mlikuwa mkijibu majibu yasiyoridhisha, hahahahaa.” Mzazu aliongea maneno yale yaliyofanya kuwatisha zaidi viongozi wa kijiji.

    “Hahaha… lakini Mzee Shabani ni mtoto mdogo kwangu, leo ndio nataka mtambue kwanini niliitwa kiboko ya Wachawi wote, leo ndio mwisho.” Mzazu aliongea huku akifikicha macho yake kabla ya hali ya eneo lile kubadilika na kuwa sehemu ya ajabu sana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taswira za wale viongozi vilionana ana kwa ana na Mzee Shabani, wakati huo mpambano mkali ulizuka baina ya Mzazu na Mzee shabani, mpambano ulidumu zaidi ya nusu saa. Kabla ya Mzee Shabani kukimbia eneo lile, sekunde kadhaa zilianza kusikika sauti za vilio kutoka kila sehemu ya kijiji cha Tangeni, vilio ambavyo havikuwa vya kawaida huku eneo lile ambalo lililogeuka uwanja wa vita kilisikika kicheko kikali.

    “Hahahahaha.” Kicheko ambacho kilimpagawisha Mzazu kabla ya kukaa sawa na sauti zile za vilio kupenya sawia kwenye masikio ya Mzazu na viongozi wa kijiji. Kazi ilikuwa ngumu sana kwa upande wao maana licha ya jitihada ambazo Mzazu alizifanya usiku kucha bado hakuambulia tena kudhibiti Mzee shabani ambaye asubuhi aliacha vilio na simanzi ndani ya kijiji haswa kwa koo za viongozi walikuwa wamekufa karibia watu wote ndani ya koo zao. Hiyo iliongeza machungu sana haswa kwa Baba Jack ambaye alipoteza ndugu zake wote.

    Ajabu zaidi hakufanikiwa kuona mwili wa mkewe kipenzi Mama Jack jambo ambalo lilizidi kumwongezea machungu dhidi ya Mzee shabani. Wakati huo mchana kutwa Mzazu akitathimini njia gani ya kumthibiti Mzee Shabani.

    ________

    Uwanja ulikuwa umefurika kila sehemu huku shangwe zilikuwa zikisikika sawia ndani ya masikio yangu shangwe ambazo dhahiri zilikuwa kutokana na kile kilichokuwemo uwanjani mule. Ugeni ule ulinishangaza zaidi lakini nilijijibu mwenyewe kutokana na kushindwa kuhudhuria uwanjani pale kwa siku mbili ndio maana nilikuwa sijapata taarifa za mechi ile ambayo ilikuwa ikituhusisha timu yetu ya kijiji na timu ile ya kijiji cha Misongeni.



    Niliendelea kuangalia mechi ile nikiwa nafatilia kila tukio lilikuwa likiendelea pale kwa mbali upande wa pili macho yangu yalionana na Mwajabu. Kiuzuri yeye pia alikuwa ameniona kuonana kule kulienda sambamba miguu yangu kujongea mahali kule alipokuwa amekaa Mwajabu.

    Sikuchukua dakika nyingi nilikuwa nimefika eneo lile na kuanza kuzungumza na Mwajabu huku watu walikuwa karibu yetu walitega vyema masikio yao kusikiliza kile tulichokuwa tunaongea. Mechi nayo ilikuwa ikiendelea na wakati huo bado matokeo yalikuwa vile vile kama nilivyokuwa nimeyakuta. Nilimuuliza Nyumbani vipi akaniambia alimkuta Baba yake anajiandaa kuja kuangalia mechi ile ila akuongea sana hivyo waliongozana wote kuja eneo lile. Maneno yake yalinitisha kumbe muda wote tunaongea

    Mzee shabani alikuwa eneo lile, wakati natafuta neno la kuongea juu ya lile ile nageuka macho yangu yaligongana na ana kwa ana na Mzee Shabani.

    Kwanamna ya uangaliaji alikuwa ananingalia nilijuwa wazi atakuwa anakitu anafikiria juu yangu hivyo neno lilofatia kwenye kinywa changu ni kumuaga tu Mwajabu, wakati huo nikiwa nachepuka kutafuta mahali kwa kukaa sikutaka Mzee shabani anione tena naongea na mwanae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilirudi eneo lile nilipokuwa naangalia mechi ile kwa mara ya kwanza lakini hali haikunipa kabisa, kupenda kwangu mpira kote lakini siku ile ilinishinda kabisa. Nilijikuta tu miguu yangu inanisukuma na kuongoza njia ya kwenda Nyumbani. Muda nao ulikuwa umeenda kijua taratibu kilianza kupotea kuukaribisha usiku wa siku hiyo.

    Nilifika Nyumbani nikafanya taratibu za kula mapema tu, nilipika chakula na kula mpaka pale nilipoona nimetosheka, niliamua kujitupia kitandani kwa muda kidogo. Mambo yale ya mchana yalikuwa yakijirudia rudia ndani ya kichwa changu. Yalicheza kweli kwenye kichwa changu kwa muda hatimaye usingizi ulinichukua.

    “Mwanangu Jack, achana na yule Mwanamke utajisababishia matatizo makubwa sana. Baba yake si mtu mzuri. Najua jinsi gani mnavyopempenda na hata wewe unampenda lakini kuna shida sana ndani ya penzi lenu.”

    “Shida gani Mama wakati tunapendana, najua kuwa amechumbiwa lakini yeye alinimbia mwenyewe kwa kinywa chake kuwa hatakubaliana na hilo Mama.”

    “Nalijua hilo lakini wewe hujui jinsi gani yule Mzee wake alivyosabisha machungu upande wako, yuko wapi Mjomba wako? Yuko wapi Baba yako? Yote kwa jili yake na wewe unataka kuwa kama wao?” Maneno ya Mama yalisikika vyema kwenye masikio yangu wakati nipo usingizini. Yalinistua sana. Niliogopa mno.

    “Ahhhh! Imekuwaje hili?” Nilijikuta nikjisemea mwenyewe wakati huo nikiwa nahema mithili ya saa iliyopoteza majira.

    “Aaaaaa! Kwanini? Inamaana gani?” Hapo hata usingizi haukuja tena.

    Si sauti ya Mama yangu ilikuwa ikiyanena yale maneno wakati nipo usingizini, inawezekana vipi? Nilijiuliza kwa mara nyingine. Hapo ilinikumbusha mbali sana Vifo vya wazazi wangu ambavyo vilitokea kiutata utata na hata mazishi yake sikupata kuhudhuria mimi wala Mjomba. Nilikumbuka kile kilichotokea miaka mitatu nyuma ndani ya kijiji cha Tangeni.

    Vifo vilivyokuwa vikihusishwa na uchawi. Nikiwa kwenye kitanda changu ghafla zilisikika hatua kama za watu zinatembea ndani ya juu ya paa la chumba changu jambo ambalo liliniogopesha sana pale kitandani. Hatua zile zilichukua muda kadhaa kabla ya kupotea masikioni mwangu.



    Nilitulia pale nikitafakari jambo lile. Kufikiria kule hata sikuelewa nilijishangaa tu macho yangu yanafumba na kulazimishwa kuingia kwenye usingizi, usingizi ambao haukuwa wa bure kabisa, ninaweza kusema maana mambo ya ajabu sana niliyoona ndani ya usingizi ule. Alikuwa ni Mzee Shabani kabisa kwenye mboni za macho yangu huku akijitahidi kufanya kitu ambacho wazi niliona akishindwa, kila alipojaribu kunisogelea hakuwa pekee yake alikuwa na gwiji la wachawi ndani ya kijiji chetu Bibi Subira na wachawi wengine wakiwa uchi kama walivyozaliwa. Sura zao zilikuwa kama na masizi hivi lakini mboni zangu ziliweza kutambua lile.

    Walikuwa wakicheza mbele na kurudi nyuma kimgongo mgomgo, nilikuwa nikiogopa mno. Kila nilipokuwa nikiwatazama na mimi kunitazama. Nilisikia vijimaneno vyao ambayo yalinitisha zaidi ya kwamba wazazi wangu aliweza kuwamaliza kiurahisi mimi nimekuwa mgumu eti lazima ale sahani moja na mimi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upepo mkali ulivuma wakati huo bado nikiwa naangalia kile nikiwa kwenye usingizi ule wa kulazimishwa, huku nikijitahidi kufumbua macho na kunyanyua mdomo wangu kupiga yowe la kuomba msaada, lakini ile ilikuwa kama kujisumbua tu mdomo ulikuwa mzito kufanya vile. Mwanga mkali ulinijia ndani ya mboni zangu na kujenga taswira nyingine.

    Je nini kitaendelea? Usikose sehemu inayofata.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog